Mwinjilisti anayetibu kwa kutumia tiba asilia!

Dk. Isack Ndodi amekuwa maarufu hapa Tanzania hasa kwa sera yake ya kutibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia tiba mbadala na kwamba magonjwa yote yaliyomo hapa duniani dawa zake zipo hapa hapa duniani.

Akiongea na Strictly Gospel Dokta huyo anatabainisha kwa kusema yeye ni mtumishi wa Mungu pia ameruhusu tutumie dawa za miti shamba “Mganga wa kienyeji nambari wani ni Mungu mwenyewe, alitengeneza miti mimea na kila kitu, nguvu iliyo kwenye miti na mimea hiyo ni Mungu mwenyewe kaiweka. Tunaruhusiwa kutumia dawa za miti shamba” akiendelea kusema “Wapendwa wengi wanamsaidia kazi shetani kumfanya mtawala wa kila kitu, shetani ni mwizi anajua kwamba miti, matunda na mboga ni dawa yeye anaongeza nguvu zake za giza kwa kunyunyuzia maneno yake na kuwavisha watu mahirizi, mradi alionao shetani ni kuwateka watu kwenye ufalme wake ili waingie jehanamu” Alisema

Ndodi Alisoma vifungu kutoka Ezekiel 47:12, Nahumu 1:9, Ufunuo 22:1-3, Kutoka 15:23-26, Yohana 9:6, Isaya 38:21 ambavyo anasema vinathibitisha kwamba ni halali kutumia miti shamba.

Dokta huyo ambaye anapatikana Magomeni mwembechai amesema ni makosa kwenda kwa wachawi, wanajimu na waaguzi kwa maana wao ni watumishi wa shetani. Lakini ni vyema kama watu wakiwaendea watumishi wa Mungu.

–Pichani akiwa akihubiri katika moja ya makanisa yao ya kisabato--

36 thoughts on “Mwinjilisti anayetibu kwa kutumia tiba asilia!

  1. Wapendwa mimi naomba msaada wenu hii mada ni vizuri kila mmoja wetu afundishe kadri ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Mimi sina la kuweka maana hapa sijui ukweli ni upi, mimi tangu niokoke sijatumia dawa ya miti shamba, wapendwa mada hii ni nzuri sana tuijadili itatusaidia sana tujue ukweli ni upi katika hizi dawa za kienyeji.

  2. Praise the Lord,
    Kimaandiko siwezi kuongelea sana kwa sababu sijui andiko hata moja linaloelezea kuhusu miti shamba. Ila ninavyojua kuwa hata dawa hizi za kizungu tunazotumia zinatokana na dawa za mitishamba, ni kwamba zimepelekwa kiwandani kutengenezwa na kuboreshwa ikiwa na kuwekwa kemikali ili ziweze kukaa kwa muda mrefu bila ya kuharibika, kemikali ambazo zina madhara kwa miili yetu.
    Huyu Dr. nimekuwa nikimfuatilia sana toka anaanza ikiwa ni pamoja na kuongea nae pia nimeshawahi kuongea nae.
    Vitu ambavyo kidogo vinanitia wasiwasi, moja nilitaka kufahamu kama yeye amesomea,amesomea wapi na elimu yake ni ya kiwango gani?
    Pili kuna dawa ya Malaria ambao amewahi kuitambulisha, ni ya kujifukiza, kwamba unachemsha maji unachukua shuka halafu unajifunika ili mvuke uingie mwilini,kumbuka kuwa utaacha sehemu ndogo ili uweze kupumua.
    Kwenye hiyo dawa ya pili mimi ndio nina wasiwasi na nilipoanza kupoteza imani na Dr.Ndodi, kwa nini? Kwa sababu madawa ya aina ya kujifukiza ndio ambayo waganga wa kienyeji wanayatumia sana. Yeye akuwahi kufafanua kwa nini waganga wa kienyeji wanatumia na yeye anatumia, anachosema siku zote ni kuwa ‘watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa’.
    Hilo nakubaliana nae, lakini kama anasoma hapa ningependa anijibu maswali yangu hayo mawili.
    Vinginevyo mimi sioni tatizo na Dr.Ndodi.
    MUNGU AWABARIKI SANA.
    Mtanzania,
    tmajaliwa@yahoo.com

  3. Madawa ya hospitalini kweli yanatokana na natural products (vitu asilia) ila kwa jinsi hii mimea inavyochumwa kunakuwa hakuna masharti yoyote ya namna ya kuichuma. Ila inapokuja kwenye maswala yetu sisi kuichuma unakuta kuna masharti ya kufuata km kuabudu, kutoa sadaka n.k. Pia unakuta mtu anahamishia imani kwenye hiyo mimea. Wenzetu wahindi unakuta hadi hayo majani kwenye kuta za nyumba zao! kwanini wasitundike panadol wanaweka mimea wakisema ni dawa!

    Kuna semina moja ya wanawake niliwahi kuudhuria ktk kanisa moja la assemblies na walikuwa wamemwalika mama Teri kama mna mkumbuka. Elimu aliyokuwa anatoa ilizidi mipaka maana alikuwa anafundisha matumizi ya vyakula na kutueleza faida za kula vyakula bila ya kuvipika, mfano njegere, karanga, ngano ambazo unaziacha zianze kuota then unakula mbichi, mbegu za papai unasaga na kunya. Akasema unakunya na mkojo kila siku asubuhi. Mungu ashukuriwe mchungaji wa kanisa hilo aliingilia kati swala la kunywa mkojo akalipinga kwa ukali.

    Sasa hapa wana wa Mungu tujawe na maarifa ya Mungu na hatutadanganywa.
    Mimi namsikilizaga Dr. Ndodi ila sikubaliani nae katika yote anayosema.

  4. Naomba tuendelee kuelimishana hapa asante sana Dada Juliet hata mimi juu ya hizi dawa za kienyeji na jinsi huyu mtumishi anavyotibu ninautata naye na mimi sikubaliani naye Labda wapendwa wenzetu waaje na wao ili tuelimishane tunasubiri michango yao.

  5. Nami nimeona nishirkiane nanyi japo kidogo tu!

    Sijapata muda wa kusoma mistari aliyokuja nayo kuona kama ni kweli inaruhusu, na kama inaruhusu kwa kiwango gani. Mfano Mungu anaruhusu tendo la kujuana, lakini si kila mtu, kila jinsia, kwa kifupi kuna mipaka ya sehemu na jinsia husika. Nitalifuatilia kama Mungu atanipa neema ya kufanya hivyo.

    Nyanya ni tunda, Muhogo ni mzizi, muwa ni shina na kisamvu ni majani. Vyote hivi tunakula na Mungu hana tatizo. Tofauti inakuja wapi? Mfano Dada Levina amekunywa maji ya muhogo wa kuchemsha(Au mzizi fulani) baada ya kupewa na Ndugu Ndondi (Huu ni mfano tu na si halisi) amepona. Mimi nimechukua mzizi huohuo na kuchemsha na kunywa lakini sijapona na ndo kwanza kifua kinabana. Naenda kwa Dkt Ndondi napata dawa hiyohiyo na anaitengeneza vilevile na napona; hakuna kifua kubana. Je ni nani anatibu hapo?

    Kitu kingine, vitu tunavyofanya wakristo, ni vile Biblia inaruhusu tu. Vidole tumepewa na Mungu na tunaweza kukunja tutakavyo, huo ni ukweli. Lakini kutokana na jinsi fulani ya ukunjaji wa vidole kutumiwa kama ishara ya salamu kwa wana wa shetani (Freemasons, satanists, etc); Mungu haturuhusu kukunja vidole vyetu namna hiyo.

    Mwisho lazima ujue tofauti ya mambo wanayoamini wakristo na wasabato. Watu wengi wakuwa too inclusive na kufikiri kuwa kila kitu kinachotaja Yesu ni cha kikristo. Hapa siongelei mtu mmoja mmoja bali naongelea kama taasisi ya kisabato. Nimeshawahi kuona mahojiano ya moja kwa moja ya mkristo mmoja na msabato mmoja wa rank ya juu na katika mahojiano niligundua usabato ni kitu kimoja, na ukristo halisi ni kitu kingine. Nina maana lazima upime anatafsiri hiyo mistari ki-Kristo au ki-sabato?

    Sijafanya uchunguzi wa kutosha kusema conclusion lakini kama kuna mtu anaweza kufanya nimeweka vitu vichache ambavyo ni kama angalizo. Juua ya hilo la dini zinazokuja zikijificha nyuma ya mwavuli wa ukristo si mbaya nikizitaja hata kwa uchache.
    1.Usabato
    2.Mashahidi wa Yehova
    2. Watakatifu wa siku za mwisho
    4.Ukatoliki
    5. Sayansi ya kikristo

    Tuonane muda mwingine jamani.
    Mbarikiwe na wikiendi njema!

  6. Shalom!

    Kuna swali linalonitatiza kama ifuatavyo: Je, ni kipi kinatumika kutagaza kingine kati ya Uganga na Uinjilisti? Jibu linaweza kuwa kati ya haya mawili 1). Uganga unatumika kutangaza uinjilisti au 2): Uinjilisti ndio unatumika kutangaza Uganga!

    Kinachoweza kurahisisha jibu la swali hili ni kutambuwa nini kilianza kabla ya kingine. Yawezekana alianza kuwa Mwinjilisti kwanza halafu ndiyo akawa Mganga; vile vile yawezekana alianza kuwa Mganga kwanza halafu ndiyo akawa Mwinjilisti. Sidhani kama vyote hivi vilianza kwa wakati mmoja. Kilichoanza kwanza ndicho kitakuwa kinatumika kutangaza cha pili. Lakini pia kama alianza kuwa mganga kwanza ndipo akawa mwinjilisti hana sababu yoyote ya kutumia mistari ya Biblia kuhalalisha uganga wake maana alishakuwa mganga pasipo Biblia. Halafu kama alianza kuwa mwinjilisti kwanza kabla ya uganga angeshatambuwa Nguvu iliyoko ndani ya Jina la Yesu na kuwahamasisha watu wamkimbilie Yesu maana Yesu anaponya bure kabisa na hivyo asingekuwa na sababu ya kuwabebesha watu mzigo mkubwa wa gharama za matibabu kwa mfano kumuona tu ni shilingi 10,000/- za Tanzania! Na hapa kutakuwa kuna mgongano mkubwa wa kimaslahi kwamba awaombee watu wapone bure kwa jina la Yesu, kama ni mtumishi wa Mungu kweli, au awatibu kutumia uganga na kuzipata hizo pesa zao. Watumishi wa Mungu ninaowafahamu mimi wanawaombea watu bure kwa jina Yesu nao wanapokea uponyaji (Mark 16:18). Lakini kama anatumia ujuzi wake kuwatibu watu hana sababu yoyote ya kujiita ni mtumishi wa Mungu au kama ndivyo, basi Madaktari wote na Wauguzi mahospitalini watakuwa ni watumishi wa Mungu maana hawatumii nguvu za giza katika kuwatibu wagonjwa!

    Lakini suala muhimu la kuzingatia hapa ni kama huyu Mwinjilisti kaokoka, yaani ameshampokea Yesu moyoni au sivyo. Nasema hivi kwa sababu wako watu wanaoitwa ‘wainjilisti’ kwenye dini zetu lakini wako kinyume kabisa na habari ya wokovu. Hawa hawana tofauti na mtu mwingine yeyote asiyekubali habari za Yesu; ‘uinjilisti’ kwao ni cheo tu cha kikanisa, si lazima wawe ni wainjilisti wa Injili ya Bwana Yesu kweli.

    Kutumia ukuu wa Mungu kuhalalisha ujuzi wetu wa kibinaadamu nadhani siyo vizuri sana maana Mungu ni mkuu mno. Uweza wa Mungu hauna formula. Jemadari Naamani alipoambiwa akajichovye katika mto Yordani na alipojichovya akatakasika ukoma haikuwa na maana kila mtu mwenye ugonjwa huo akijichovya mara saba katika mto Yordani hupona. (2Kings 5:14). Bwana Yesu alipofanya tope kwa mate na kumpaka mwenye upofu na kumwambia akanawe katika birika la Siloam na akapona si kweli kwamba mtu yeyote akitengeneza tope kwa mate na kumpaka mtu mwenye upofu na kwenda kunawa Siloam hupona. (John 9:6-7). Wana wa Manabii walipopika matango-mwitu na kushindwa kuyala kwa sababu ni machungu Nabii Elisha aliweka unga ndani ya sufuria nayo yakawa matamu, hii pia si kweli kwamba kila mtu akiweka unga kwenye matango-mwitu machungu hugeuka kuwa matamu!
    (2Kings 4: 38-41). Kwa hiyo Mungu anapotumia vitu vinavyoonekana huwa ni ishara tu lakini si kweli kwamba ili Mungu afanye uponyaji ni lazima atumie kitu fulani, tena hicho hicho kwa wakati wote, si kweli.

    Uganga wetu binaadamu una mipaka. Umebanwa na kanuni ambazo ni lazima zifuatwe pasipo kukosewa. Kwa mfano mtu wa kwanza anapoambiwa ale machungwa manne (4) kila siku kwa siku 3 mfululizo ili kuponya ugonjwa fulani mtu wa pili naye itabidi ale kiwango hicho hicho cha machungwa na kwa muda ule ule ili kupona ugonjwa huo. Lakini kama angekuwa ni Mungu angeweza kumwambia yule wa pili ale hata embe moja tu na angepona ugonjwa ule ule ambao wengine walipona kwa kula machungwa 12. Kwa hiyo linapokuja suala la Mungu si kanuni zitumikazo bali ni nguvu ya ajabu aliyo nayo Mungu ya kuweza kutumia kitu chochote pasipo kubanwa na kanuni; Ni kama ilivyo sasa kwa kuomba tu kwa jina la Yesu mtu hupokea uponyaji. Hakuna kanuni kwamba lazima kumnyooshea mgonjwa kidole au kumshika kichwani nk. Kwa hiyo mtu anayetibu kwa kutumia kanuni na taratibu ha-qualify kujiita ni mtumishi wa Mungu. Ni vyema akajitambulisha tu kwamba yeye ni mganga, inatosha.

    Kama Dk. Ndodi ana sababu yoyote ya kuitwa ni mtumishi wa Mungu basi iwe ni kwa sababu yeye ni Muinjilisti na si kwa sababu anatibu watu kwa kutumia miti-shamba pasipo kutumia nguvu za giza. (kama hili ni kweli). Na hii inampa sababu moja ya kutambuwa kwamba ni heri kumtumikia Mungu kuliko taaluma maana akiwa mtumishi wa Mungu kweli kweli atawasaidia watu katika kuwaelekeza njia sahihi ya kwenda kwenye uzima wa milele kuliko kuitumikia taaluma ambayo mipaka yake huishia wakati mtu akiwa hai. Kwa kutumia taaluma waweza tibu watu wengi ambao bado wanakuwa hawana guarantee ya kuishi, kwa mfano wengine waweza kufa kwenye ajali wakiwa katika safari ya kutoka kuchukuwa dawa kuelekea makwao. Taaluma ya kibinaadamu haina suluhisho la kudumu kwa matatizo yote yanayomkabili binaadamu!

    Dk. Ndodi, katika kutetea uganga wake, alinukuu mistari ya Biblia katika Kutoka 15:23-26. Sehemu hii inazungumzia wana wa Israel katika safari yao ya kwenda Kaanani walifika sehemu iliyokuwa na maji machungu. Watu walimnung’unikia Musa na Mungu akamwonyesha mti na alipoukata na kuuweka kwenye yale maji uchungu ulikwisha (nimeshaelezea mifano kadhaa hapo juu). Lakini mstari wa 26 unasema hivi: ”And said, If thou will diligently hear the voice of the LORD your God, and will do that which is right in his sight, and will give ear to his commandments, and keep all his statutes, I will put none of these diseases upon thee, which I have brought upon the Egyptians: for I am the LORD that healeth thee”. Bahati mbaya sijaweza kupata tafsiri ya Dk. Ndodi juu ya mstari huu wa 26. Lakini hapa ndipo ulipotokea wimbo maarufu wa muimbaji wa Injili Don Moen: ‘I am the God…., that healeth thee….I am the God your healear….. I send my word and heal your disease…, I am the God your healer! …………..
    Mstari huu wa 26 unaweza kuelezeka kwamba kama watu tungesikia vizuri na kushika maagizo ya Mungu magonjwa yote yasingekuwepo. Maana Mungu ndiye mponyaji wetu. Sielewi kama Dk. Ndodi huwa anawaeleza watu kwamba kama watamfuata Mungu vema kwa kuishi maisha matakatifu hiyo ndiyo kinga na tiba nambari moja ya magonjwa yote yaliyoko duniani. Hii inampa sababu nyingine ya kumtumikia Mungu kwa kuwataarifu watu kwamba Kinga na Uponyaji nambari moja wa Mungu uko katika kumcha yeye. Kwamba kama watu wakiishi maisha matakatifu hawana sababu tena ya kwenda kwa Dk. Ndodi maana Bwana ndiye mponyaji wao. Bwana hulituma Neno lake nalo huwaponya. Ndiyo maana hata hapa kwenye Blog tunaomba kwa pamoja na Mungu anasikia maombi yetu naye anawaponya wengi! Kwa hiyo pesa ambayo tulikuwa tuitumie kwa ajili ya kunulia dawa twaweza kuitumia kwa mambo mengine, kwa utukufu wa Mungu!

    Wingi na aina ya wagonjwa wanaokwenda kwake pia si kigezo kwamba yeye ni mtumishi wa Mungu. Pamoja na kuwa kwa Yesu kuna uponyaji wa bure, huwezi amini kuna wagonjwa wengi ambao wako tayari kufa kuliko kupokea uponyaji, ingawa ni wabure, kutoka kwa Yesu. Wagonjwa wa namna hii wako tayari kuingia kwenye uchochoro wowote (sina maana ya kwa Dk. Ndodi) kusaka uponyaji. Wako tayari kukopa pesa ili wakalipe huko. Kama kungekuwa na uponyaji wa bure mahali pengine popote wangekwenda huko. Lakini ni bahati mbaya kwao kwamba ni Jina La Yesu Peke yake ndilo liponyalo magonjwa bure. Hakuna gharama kwa Yesu. Kuna magonjwa mengi ambayo hayaponi si kwa waganga wa kienyeji wala kwa waganga wa kigeni. Magonjwa haya husababishwa na nguvu za giza. Magonjwa haya ni sababu ya watu wengi kuzunguka huko na huko wakitafuta uponyaji. Sijuwi wagonjwa hawa wakifika kwa Dk. Ndodi huwa anawasaidiaje. Sijuwi kama huwa anawaombea kwa Jina la Yesu na wao kupokea uponyaji. Na kama ndivyo Je, hawa nao hulipia?

    Dk. Ndodi amekuwa akijitangaza pia kwamba yeye ni mwinjilisti. Lakini sifahamu kama uinjilisti huo huendelea hadi kwenye chumba cha daktari, anapokuwa yuko na mgonjwa. Sifahamu kama huwa anapata nafasi ya kumueleza kila mgonjwa anayeingia pale juu ya habari za Yesu; kwamba pamoja nakuwa yeye anatibu magonjwa yote yanayosumbuwa mwili yupo Daktari anayetibu yote yanayosumbuwa mwili, nafsi na roho, yaani Yesu! Yeye mwenyewe (Dk. Ndodi) anajibu sahihi!

    Utaalamu wa Udaktari wa ‘kigeni’ huwa na muda maalumu unaojulikana wa kuusomea (kama vile miaka 4 nk,) na katika chuo kinachojulikana lakini utaalamu wa Udaktari (uganga) wa kienyeji hauna muda wala chuo maalumu. Wengine huamka na kusema wameoteshwa ndoto na hivyo kwa usiku mmoja tu mtu anaweza kuwa mganga wa kienyeji na kisha kuendelea kuongozwa na mashetani kwenda msituni kuchimba dawa na elimu zaidi huendelea huko huko msituni. Dk. Ndodi hajatufunguwa katika hili. Bado amekaa kimya kuhusu alikosomea. Au labda yeye ndiye mwasisi wa taaluma hiyo; lakini hata kama ndivyo ni lazima pia aseme alipataje hayo ‘mafunuo”. Waganga wa kienyeji huwa hawaweki taaluma yao wazi kwa sababu huwa ni ya ki-kishetani na sharti moja wapo ni kuhakikisha mganga anatunza siri kwa jinsi hiyo hiyo atakavyotaka kuendelea kuishi hapa duniani, huwa ni watumwa wa ‘waalimu wao’ . TUnasubiri kutoka kwako Dk. Ndodi!

    Namalizia kwa kusema kwamba mimi sina chuki yoyote kwa Dk. Ndodi. Nampenda. Siwezi kumhukumu kwa lolote. Mungu, aliyemlea tangu akiwa tumboni mwa mama yake hadi sasa anaitwa Dokta, ndiye mwenye uwezo wa kumhukumu. Ninachofanya mimi ni kujilinda ili niweze kujiokoa nafsi yangu kwa kujinyenyekeza kwa Mungu aonaye sirini ili anipe ufahamu wa kuepuka na udanganyifu wowote unaoikumba dunia kwa sasa. Mungu anawafahamu walio ‘wa nuru’ na ‘walio wa giza’. Kwa walio ‘wa nuru’ anawahimiza wazidi kuwa watakatifu na walio ‘wa giza’ anawaita bado kwa upendo ule ule wajisalimishe kwa Yesu kabla giza la milele halijawafunika!

    Watu wa Mungu tumuombe sana Mungu atusaidie ili tuweze kutambuwa hila zote za shetani zinazoweza kujitokeza katika siku zetu hizi!

  7. mimi siyo coment hila nauliza kama huyu Dr anayo dawa ya kuponyesho macho ambayo hayaoni kabisa. anieleze namna ya kumpata yaani contact zake.

  8. jambo moja nalopenda kuchangia juu ya doctor Ndodi,ni kwamba, kwanza watanzania tungependa kufahamu chanzo cha mafundisho yake,na kama chanzo cha hayo ambayo anayazungumza ni salama basi tiba yake inaweza kuwa haina tatizo ,ingawa sisi kama wakristo lazima tumtazame doctor ndodi kwa macho mawili asije kuwa anatumia maandiko kupotosha kweli ya Mungu,tusiwe wakristo tu wa kupokea na kumeza kila tunachoambiwa na kuona kwenye TV na eti kwa sababu mtu anatoa maandiko ya kusuport yale anayoongea,,kumbuka hatupaswi kutafuta maandiko ya kusindikiza hoja zetu, ila hoja tunazotoa ndizo zinazopaswa kufuata kweli ya Mungu, yaani Neno lake,,,tukumbuke hata shetani hutumia maandiko kusuport hoja zake mfano mzuri utauona kwenye mathayo sura ya nne wakati adui alipokuwa anatumia maandiko kumtega yesu,,,kwa upande wangu pia kwa upande mwingine nampongeza doctor kwa kile anachofanya, ingawa napenda kumshauri ajaribu kuujulisha umma wa watanzania kuwa uponyaji wa kweli wapatikana kwa Yesu,tukiziacha njia zetu mbaya, na kumgeukia Mungu na kumcha yeye basi hakika yeye atatuondolea magonjwa yote ya Misri,,,,,,,mbarikiwe wooote. Amina

  9. Kuhubiri kutegemea mitishamba uiite tiba asili ni kujaribu kupunguza nguvu ya msalaaba pale calvary, kama Kristo ndiye dawa, hakuna zeli mahali pengine zaidi yake.
    KUNA DAWA KUNA DAWA – DAWA NI YESU- muimbaji hakukosea

  10. Bwana Yesu asifiwe,tatizo langu ni chunusi mara kwa mara zinanisumbua na nimejaribu dawa nyingi ila zina niponyesha kwa kipindi je nitumie dawa gani?Uso wangu ni wa mafuta.

  11. DADA DORIS kuna LOTION Fulani inaitwa ( Elizabeth Arden ) inauzwa pamoja na pafyum yake na sabuni ya kuogea ni kama sh´elfu hamsini itakusaidia sana hiyo.Usipopata nenda kwenye zile phamacy kubwa zinazoaminika uulize unatakiwa kutumia nini juu ya huo uso wako wanajua, usipakepake vitu, jaribu hata kwenda hata kwa daktari wa masuala ya ngozi, ila hiyo niliyokutajia unaweza kuipata kwenye yale maduka makubwa ya posta posta.

  12. Mimi naomba dokta anisaidie niweze kupona macho yangu yanawasha sana kiasi cha kutamani kulia,nimepewa dawa hospitali lakini bado tu.

  13. KAKA JULIUS NENDA PHAMACY KANUNUE DAWA INAYOITWA HIVI (OPTICROM – NI YA MAJI)KWENYE ZILE PHAMACY KUBWA ZINAZOAMINIKA UNAWEZA KUPATA .KITONE KIMOJAKIMOJA KILA JICHO,ASUBUHI NA JIONI KWA MDA WA SIKU 7 UKIONA YAMEPONA ACHA KUWEKA KAMA BADO ENDELEA MPAKA SIKU YA 21 MWISHO. ILA ONYO HIYO DAWA SIKU YA 21 BAADA YA KUFUNGUA INABIDI UITUPE USIITUMIE TENA. TATIZO NI KUPATA HII DAWA ILA DAWA NO. 1 NI NENO LA MUNGU HAPO NAAMINI KWA NENO NI 100 KWA 100 UTAPONA, KWA SASA BADALA YA KUMTAFUTA HUYU MCHUNGAJI WA MITI SHAMBA WEWE NENDA KANUNUE HII DAWA.

  14. Bwana Yesu asifiwe sana.
    Mimi sina andiko lolote linaloruhusu ama kukataza aina hii ya tiba anayotumia mwinjilisti Ndodi.
    Hivyo ninashauri wale wenye maandiko yanayopinga ama kuunga mkono jambo hili watufunulie kwa wazi bila kuhusisha mgando wa ukoloni kuwa tiba ni mpaka itokane na mitambo ya ulaya na amerika.
    Nina maana tuwe na sababu za msingi zinazomtukuza Kristo si mapokeo yetu.
    Mungu awabariki wote.

  15. OF ALL THE THINGS ZINAZOTUUMIZA KICHWA NI KNOWLEDGE/MAARIAFA HALISI YA MAMBO TUNAYOYABISHIA KUHUSU DR.NDODI.

    KUNA UKWELI,LAKINI HATUPASWI KUAMINI KWA SABABU AMESEMA NDODI. TUNAPASWA KUSOMA PIA SISI WENYEWE. LAKINI KWA SABAB HATUJAUTAFUTA AU KUUSOMA VIZURI TUTABAKI TUNABISHA, TUSOME BIBLIA NA VITABU VINGINE ILI TUUJUE UKWELI KATIKA YOTE.

    SOMA BIBLIA NA VITABU UPATE MAARIFA. UWE MAKINI NA VITABU VISIVYOFAA. TUMIA HEKIMA, BUSARA NA UONGOZI WA MUNGU KUGUNDUA VITABU VIZURI.

    MUNGU ATUBARIKI WOTE.

  16. Dr.Mungu akubaliki sana lakini kumbuka watanzania wengi ni masikini na wanaishi chini ya dola moja hivyo tunaomba bei ya dawa angalau ipungue,me nilikuja magomeni (ITUMBI)nikaambiwa bei ya dawa ni 240000 japo mwezi huu kuna punguzo la bei kwa 20% bado nashindwa kuja MUNGU AKUBALIKI SANA

  17. Bwana Yesu asifiwe!!

    Kaka Julius jaribu tetracyclin ya macho iko kwenye ki-tube kidogo ni nzuri sana.

    Kwenye vipindi vyake sioni kama Yesu anainuliwa pale zaidi ya Dawa zake. Ila wengine wamefuata maelezo yake na wamepona.

    Be careful mtu wa Mungu usijeingia kwenye mtandao fulani bila kujua.

    Jina la Yesu tumeachiwa mataifa tulitumainie Math 12: 21. Lakini haimaanishi usiende hospitali bali takasa dawa zako.

    BwanaYesu apewe sifa!!

  18. Bwana Asifiwe wapendwa!!
    Mimi nimejaribu tiba yake ya ndimu na kusema ukweli inasaidia sana na ndani mwangu ndimu haziishi.
    wiki iliyopita nilikua na flu, dawa nayotumia na inaponya kwa siku 2 tu, juice ya limao, cinnamon,ginger, honey kwenye maji ya moto, unakunywa ikiwa bado ya moto halafu unalala unahakikisha uko na joto.
    nikihisi kikohozi kidogo natumia tangawizi nyingi,

    mimi kwa kweli huwa sipendi dawa wala vidonge, kwa hiyo kama naweza kunywa tangawizi nikapona kikohozi, nikwanywa maji lita 2 kwa siku kichwa kikaacha kuuma n.k kwa nini nisitumie?

  19. Kaka Julius nenda kwa daktari specialist wa macho, inaweza kua ni allergy ni bora ujue, mimi nina tatizo hilo la macho kuwasha toka nikiwa mdogo na niliambiwa ni allergy, kuna dawa tofauti na ni vizuri upewe na daktari aliyekuchunguza.
    Si vizuri kwenda tu phamarcy na kununua dawa, hasa kwenye suala la macho.

  20. Dada Doris, kama unakunywa maziwa acha kama kwa miezi mitatu halafu angalia kama kunatofauti, usitumie chochote kinachotokana na maziwa. Pia nunua dawa inaitwa dalacin T, kuna lotion na solution, nunua solution, inauzwa ghali kidogo kama tshs 20,000 ila inasaidia na usitumie kitu kingine chochote.

    Mimi nimesumbuliwa sana na pimples mpaka nilipoacha maziwa. ukitaka ushauri zaidi nitumie email anna.abela@gmail.com

  21. Mwambieni Dk. Ndodi, asijidanganye, Mungu hadhihakiwi, kila apandacho mtu ndicho atakachovuna. Siku ya mwisho inakuja. Yesu lazima aje kuchukua walio wake. Hata kama watu hawataki kubadilika. Kwa hiyo, kama ameamua kuuza dawa za kienyeji auze kama mganga wa kienyeji, lakini asitumie jina la Yesu kama mwamvuli wa kuuzia dawa zake kwa wakristo. Mungu awabariki sana

  22. Shalom!
    Ukisoma vizuri katika Biblia utangudua kuwa shetani naye anasoma Biblia na anaielewa vizuri ndo maana hutumia Neno la Mungu(Biblia) kuwajaribu wakristo. Mfano Mw 3:1-6, pia Yesu alijaribiwa nyikani kwa kutumia maandiko Math 4. Sasa mie sishangai kuona yanayotendeka. MIe nimefanya uchunguzi na kungundua kuwa Madaktari hawa wa mitishamba kwa asilimia 98 ni wasabato, Na wote wanaitwa watumishi wa Mungu, (wainjilisti, n.k)na wanatumia vyombo vya habari vya Kikristo.
    Mie nahisi kuna ajenda ya siri humo ndani. Tuwe macho.
    Kwanza: Dr huyu yuko kifedha, maana ukikanyaga kwake uweze kuogea naye utoe 10,000. Sasa uinjilist gani wa malipo?
    Pili: hana vifaa vya kupima uli kujua mgonjwa anasumbuliwa na nini? (Je anakibali kweli cha kuwa na hospital, zahanati au klinik?)
    Tatu: ukifanikiwa kumuona hatakufanyia huduma ya maombezi, ataanza kwa kukusikiliza na kukuandikia dozi ambazo ni za gharama kupita kawaida.
    Nne:Sikuhizi ni siku za sayansi na teknolojia, msitegemee mganga wa kienyeji kuwa kama zamani.
    Kuweni macho msilishwe sumu itakayo ondoa uhusiano wako kidogo kidogo na Mungu wa Kweli.
    Sam

  23. Nimejaribu kusoma maoni ya wakristo wengi kuhusu dr.ndodi na inaonesha wengi wanamchukulia kama mganga wa kienyeji anaesingizia kristo! NASEMA BADILIKENI MUWE NA MUONO POSTIVE!
    DR.NDODI ANAJUA ANACHOFANYA NA NI MKWELI KWAKUA MUNGU ALIUMBA DUNIA NA VYOTE VILIVYOMO,AKAUMBA BINADAM NA VIUMBE HAI KWA NAMNA ZAKE PIA AKAUMBA MIMEA ILIYO BORA KWA MATUMIZI YA CHAKULA NA TIBA KWA VIUMBE HAI WOTE, WEWE MKRISTO UNAE AMINI UPONYAJI WA YESU HUKU UKISINDILIA SODA NA VINYWAJI NA VYAKULA VILIVYOSINDIKWA KWA MADAWA YANAYOATHIRI AFYA YAKO UNAMKOSEA YESU NA IMANI YAKO! KUMBUKA WEWE NA MWILI WAKO NI VITU VIWILI TOFAUTI,UJALI MWILI WAKO ILI UPATE KUISHI VEMA MUDA MREFU!

  24. SWALI LANGU LA KWANZA NA KUU KWA WAPENDWA ni kuwa JE!! INGEKUWA NA RESPONSE TOFAUTI KAMA ANGETAJWA KAMA MTABIBU WA TIBA ZA ASILI? Ama kwa kuwa ametajwa kama MGANGA ndio yaleta shida? Na pili ni kuwa ni nini asili ya madawa mnayokunywa?
    SIJAWAHI KUMUONA HUYO DAKTARI LAKINI BAADHI YA MAONI YANANIPA SHAKA NA FIKRA YAKINIFU ZA KILICHO / KINACHOENDELEA.
    Ni kweli kuwa TUNAJIKIMBIA WENYEWE KWA KUAMINI KUWA U-ASILI WETU NI DHAMBI?
    Ni wangapi kati yenu wanaosoma INGREDIENTS za madawa mnayokunywa?
    Ama kwa kuwa yamekuwa PRESCRIBED mnaamini hayatokani na mitishamba?
    Ndugu MTANZANIA (mtoa maoni wa tatu) ameeleza vema kuhusu asili ya yale madawa mnywao. Lakini pia akaonesha wasiwasi wa dawa ya kuvukiza. Ninalowaza ni kama VICKS VAPOR nayo hamuitumii kwa kuwa ni ya kuvukiza (vaporizor)?.
    Tulishazungumza huko nyuma kuwa suala si uasili wa madawa, bali utekelezaji wake. Ndugu Juliet (wa nne) amefafanua ninaloeleza. Tatizo si madawa yenyewe, tatizo si kilichomo humo, bali DHAMIRA YA KUYANYWA.
    Nikiwa sekondari wapo waliokuwa wakitumia PIRITON kuchanganya na mambo mengine kuyafanya kama madawa ya kulevya. Je! Ni sahihi kuichukia piriton kwa kuwa wapo wanaoifanya iwe madawa yadhuruyo akili ya mwanadamu? La Hasha. La kulaumiwa ni MATUMIZI na si dawa yenyewe.
    Lakini pia Ndg Juliet ameonekana kupinga matumizi ya mkojo na elimu nyingine aliyoisikia toka kwa Mama Teri. Nawaza linalofanya watu wasitumie mkojo kama tiba ni nini? Hasa kama ni wako. Kwa wataalamu wa afya wanaweza kueleza kinagaubaga kwanini MKOJO unatumiwa utumikavyo hata kwenye kukata makali ya vitu kama sumu. NAKUBALIANA NA MATUMIZI HAYO UNLESS KUNA ANAYEWEZA KUSEMA NI KINYUME NA NENO LA MUNGU. Na pia wacha nizungumzie suala la VYAKULA kwa kuwa Ndg Juliet amezungumzia. Ulaji wa baadhi ya vitu vibichi ama ambavyo havijaiva saana ni suala la ki-afya kuliko LADHA. Kwa mjuao mapishi mmesoma kuhusu food de-nature na mnajua athari za kula vyakula vilivyopikwa kuliko kiasi ambayo ni sawa na kula makapi. Watu wanachukulia vitu kama UGALI WA DONA kama maisha ya hali ya chini ilhali SEMBE ni kama makapi.
    Ndg STEVE M, nimejifunza mengi kutokana na maoni yako, na MTAZAMO WA MATUMIZI YA VIDOLE UKO SUPERB. Labda msaada ni kwenye kujua kwanini unaamini waSabato na waKatoliki sio waKristo?
    Ndg yangu John Paul ameeleza vema UMUHIMU WA KUJUA NI KIPI KILIANZA. Na labda umuhimu huo tuutumie hapa katika kujibu hoja. Kuangalia kama huwa TUNAANZA KUOMBA TUELEWE KILICHOANDIKWA ama TUNAAMINI TUMEELEWA KILICHOANDIKWA, TUNAKUWA NA MSIMAMO NA KISHA NDIO TUNAOMBA LA KUANDIKA KUHALALISHA MSIMAMO WETU?
    Ndg Denis Kiandika ameweka maonyo mema na ninajifunza kwayo.
    Ndg Larry naamini maoniyo yameeleweka kwa wengi na umemalizia kwa nukuu ya wimbo wa KUNA DAWA ukisema “muimbaji hakukosea”. Ninalowaza ni vipi kama utaambiwa kuwa muimbaji aliamini kuwa “mstari huo na wimbo huo utawezesha albamu yake kuuza zaidi”? Si kwamba ndivyo ilivyo, lakini kama ndivyo (kwa kuwa yawezekana ikawa hivyo) basi hata kumnukuu yeye yaweza kuwa kosa pia.
    Ndg Levana katika kumjibu Ndg Doris umeweka hiyo product ya Elizabeth Arden ambayo inasifika kwa “kurejesha ujana na kuufanya uzee usionekane kwa kasi” na sina hakika kama umeshapitia INGREDIENTS zake, kama hapana basi chungulia hapa ujionee http://www.livestrong.com/article/278963-what-are-the-ingredients-in-elizabeth-arden-ceramide-moisturizer/
    NDUGU AMIN NGULUMA naamini swali lako ndilo hasa nililonalo mimi kuwa TUONDOKANE NA MAWAZO YALIYO NA “MGANDO WA UKOLONI KUWA TIBA NI MPAKA ITOKANE NA MITAMBO YA ULAYA NA AMERIKA”

    Madawa ya asili mimi ni mtumiaji mkuu. Ninayatumia kama yalivyo NA BILA MASHARTI. Ni tiba ya asili tangu miaka na nimekua nikiona ikitumika nyumbani kwetu. Labda yawezekana ninamuabudu shetani bila kujua na ndio maana ninapenda vipengele vya Biblia kuonesha kuwa kufanya nifanyavyo yaweza kuwa mbaya. Ama hata kuonesha kuwa afanyacho Dr Ndondi kutibu kwa mimea na miti ya asili (kama haambatanishi na masharti ya kuabudu vingine) ni makosa.
    Bado naamini katika tiba za asili kwa kuwa mengi ya yatumikayo sasa toka viwandani ni mazao ya asili.
    Mfano mzuri ni mke wangu alipojifungua hapa Washington Hospital aliandikiwa dawa ya kutumia kukandia matiti kutokana na maumivu na complications alizokuwa nazo. Kabla sijanunua nikakutana na nesi mmoja mwenyeji wa visiwani aliyekuwa akituona kama wanawe pale na ambaye amefanya utabibu kwa zaidi ya miaka 30, alipoona ile prescription alienda akatuletea hiyo dawa, akatuonesha ingredients zake ambazo ni asilimia kubwa products za cabbage. Akatushauri kuweka jani la kabeji kwenye joto kisha kukanda. Na tulifanya hivyo. Sio tu tuliokoa pesa, bali hata KEMIKALI ZILIZOAMBATANA NA UTUNZAJI WA DAWA KUU NDANI YA DAWA HIYO
    Kuna madhara mengi ya madawa ya viwandani lakini kuendelea kuyapinga bila kueleza kwanini, ni kuendelea kuathiri KIZAZI CHETU KWA MAKEMIKALI.
    Baraka kwenu

  25. Mimi sina neno maana sijafanya utafiti juu ya huyu docta ila ninachoweza kusema ni kwamba watumishi wa Mungu tuwe waangalifu katika mambo kama haya yanayomtamanisha mtu kwamba yatamwondolea tatizo lake lililoshindikana maana shetani naye huja kwa mtego akitumia pale anapoona kuna udhaifu hasa katika mwili.Hasa magonjwa maana yanakuwa ni usumbufu wa kila siku shetani hupitia sana kuingiza watumishi kwa waganga wa kienyeji na umasikini shetani huutumia kuingiza watumishi kwenye wizi, uongo na hata wengine kukata tamaa na Mungu na kwenda kwa waganga wa kienyeji.

    BARIKIWENI Wapendwa

  26. Kumbukeni maandiko yanavyosema kuwa siku za mwisho maarifa yataongezeka, wengi watakuja kwa jina langu. atakaye vumilia mpaka mwisho huyo ataokoka. hivyo msishangae.

    MBARIKIWE

  27. watu bwana wanashangaza hukataa tiba hii asilia huku nwakikimbilia maombi na miujiza ya nguvu za giza, MUNGU katoa mmea wa kondeni uwe tiba kwa miili yao dhaifu,wao hutaka miujiza .Yesu alisema hakuna muujiza mkubwa kama ule wa Yona. leo wanashangaa miti halali kama tiba huku wakiaminishwa na miujiza feki.Kweli hiki ni kizazi kikuu tangu kuumbwa kwa Dunia.Asiyetaka dawa za Ndodi akanywe vikombe viko tele nchi nzima

  28. Ni kweli mpendwa hakika ya tiba za dawa zako ipo kwa kadri ulivyojaliwa ila shida inakuja pale watu wa hali ya chini wanapokuwa na matatizo ya magonjwa ambayo unayatibu halafu wao hawana uwezo wa kununua dawa zako na wewe unajua hilo, je ni busara watu waumie na magonjwa yao kwa kukosa uwezo wa pesa wakati dawa unazo kama mtumishi wa Mungu? Ndio ulishasema kuwa unatumia gharama nyingi katika kuandaa hizo dawa lakini kweli huwezi kuwahudumia watu kama hao bure? au utapata hasara kwa Mungu?

  29. Ni tiba gani asilia naweza kutumia ili kupunguza uchovu wa mwili,baridi yabisi na kuumwa sana na kichwa?pia dada Levy nifahamishe vzr khs hy lotion ya kuondoa makunyanzi.thnx

  30. bwana Yesu asifiwe wapendwa kwa kweli yesu anaponya tena bila Gharama yoyote ukiomba kwa imani tu unapona mfano mimi nimesumbuliwa na aleji madonda mwili mzima nimepoteza hela mpaka Muhimbil Dor aliniambia nijikubali siwezi kupona lkn mm nilikuwa na imani kama madakitari wa dunia hii wameshindwa Yesu anaweza na kwel nimepona Bwana yesu asiwe lkn sishauri watun waache kutumia dawa hapana watumie lkin wasiende kwa waganga ila tiba asili waende kwani tiba asili ni mimea na matunda aliyoumba mungu mwenyewe

  31. Wapendwa katika Yesu, tumsifu Yesu Kristo. Kama wewe ni mtazamaji wa EATV kila Jumapili saa 7.30 mchana utaamini nikikwambia kwamba Dr. Ndodi anasitahili kuitwa Mtume au Nabii wa Mungu kwa mafundisho yake kwa binadamu na kama ukimsikiliza kwa makini haina haja kwenda ofisini kwake kutoa hela nyingi watu wanazosema ila utatengeneza dawa za vyakula na mimea na utapona bila wasiwasi. Ebu jaribu

  32. Ndugu,

    Dokta Ndodi kazi aifanyayo haina shetani ndani yake. Wapendwa na wachungaji bado wengi wana vichembechembe vya kizungu na kikoloni ambapo wanadhania kwamba miti na mazao yake yamejaa ulozi na uchawi.

    Nyumbani kwangu aliwahi kuja mzee mmoja wa kisukuma kuniomba achimbe mizizi ya mapapi ili akamtibu jirani mwenye matatizo ya magonjwa mbalimbali. Mke wangu alimkatalia kabisa kwa hoja kwamba hiyo ni tiba asili inayotumia mizizi na kwamba haifai kwa mujibu wa Imani yetu ya Kipentekoste. Yule mzee wa Kisukuma alikata rufaa akaamua kunitafuta ili nitoe ruhusa apate mizizi ya mti wa mpapai. Mimi nilimpa ruhusa akachimbe bila matatizo nikamwambia mke wangu kwamba mimi sina tatizo kabisa na tiba yoyote inayotumia mizizi. Mimi nina tatizo na tiba za ulozi, uaguzi, uchawi, ramli na mazindiko ya mizimu na kuuliza mashetani na majini yakupe majibu.

    Kama Dr. Ndodi na wengine wanaotuambia tutumie dawa asili wanafanya hivyo kwa kutuhusisha na Minugu nje ya Mungu Muumba wa ARDHI na MBINGU hatuna budi kuwakataa.

    Katika dunia ya leo, taifa lenye watu wanaoishi miaka mingi sana ni lile ambalo limeondokana na kutumia dawa za kemikali katika kutibu watu. Taifa ambalo watu wake wanatumia mimea asilia, chakula asilia, vinywaji vya asilia (lakini siyo pombe) mfano: uji wa ulezi, soya, maharage, nanasi, machungwa, maembe, nk. taifa hilo lina watu wenye uwezo wa kuishi kwa wastani wa miaka 80 hadi 90. Taifa hilo lina watu wasioumwa umwa hovyo magonjwa kama homa, mafua, TB, Minyoo, mifupa, uchovuuchovu wa hovyo, kukosa nguvu za tendo la ndoa, kushindwa kubeba mimba, nk.

    Wananchi wa China na Malysia kwa mfano wengi kwa sasa wanatumia dawa za asili kabisa. Afya zao na uchumi wao unakua kwa kasi sana. Watu wake ni wenye afya tele. Watoto wana afya ya mwili na akili. Ukiangalia hata Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya, asilimia kubwa wameelewa kwamba “Chemical medicare” siyo tiba salama kwa mwanadam. Wengi wamegeukia EDENI yaani kutumia vdawa za asilia kabisa(SIYO KWAMBA WAMEGEUKIA UCHAWI).

    Ukijaribu kujifunza kwa nini ADAM na EVA na watu wa enzi zile za Adam waliishi miaka zaidi ya 900 utagundua kwamba ni kwa sababu walikula vyakula na matunda ya asili.

    Inashangaza kuona wapendwa wengi wanaosoma maandiko tukishindwa kulielewa swala hili kwa urahisi kabisa bila hata kusoma sana Maandiko. Leo hii mtanzania anayeishi miaka 80 tunamwona kama ajabu sana. Lakini ukifuatilia historia ya ulaji wake haiwezekani kabisa ukakuta alikuwa akila ugali wa SEMBE, JUISI ZA MAKOPO, WALI ULIOLOWEKWA NA KUOSHWA SANA, SODA, BISKUTI, NYAMA CHOMA ZISIZOIVA, nk. Ukifuatilia sana utakuta alikuwa akila ugali wa dona, viazi, mihogo mibichi toka shamba, ukwaju asilia, maembe asilia, ugali wa ulezi au uwele au ngao asili, maharage, karanga, na mbogamboga za asili kabisa.

    Ulaji wa namna hiyo ndiyo dawa zenyewe. Mhubiri yeyote anayepinga tiba itokanayo na mimea na mizizi yake NI MPINGA KRISTO, NAAM HAWAJUI MAANDIKO NA UWEZA WA MUNGU KATIKA MIMEA.

    Natamani watanzania wote turudi EDEN ili tule vyakula vya asilia, mizizi, matunda na mbogamboga za asili kabisa ili tuweze kuishi kwa wastani wa miaka 80 tofauti na SASA WATANZANIA WANAISHI KWA WASTANI WA MIAKA 50.

  33. KUNA KITABU CHA KISABATO CHA HOME REMEDIES NI MUST KUWA NACHO SEMA WATZ WAVIVU KUSOMA NI KIKUBWA SN KINAELEZEA TIBA MBADALA WA MAGONJWA YOTE UYAJUAYO KWA KUTUMIA MIMEA/MATUNDA SO DOKT ANACHOFANYA NI KUAPPLY HUMO TU HANA KIPYA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s