Ushabiki wa Timu ya Mpira na Ukristo

FCB, CHELSEA, SIMBA SPORTS CLUB, MANCHESTER UNITED, LIVERPOOL, ARSENAL, YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB, VALENSIA C.de.F. ACM nk. nk

Siku hizi limezuka wimbi la ushabiki wa mpira wa miguu, kiasi kwamba kuna mifano ya watu waliojinyonga kwa timu zao kufungwa au kuua wenzao kwa hasira ya timu yake kufungwa, wengine kufurahi hadi kusababisha maafa akifurahia timu yake kushinda n.k. Mechi nyingine huchezwa usiku, wapo wana wa Mungu ambao wanakuwa tayari kuangalia mechi hizo hata kama ni mpaka saa 9.00 usiku, lakini ukiwaambia kuna mkesha wa maombi na kujifunza Neno la Mungu hawako tayari. Wengine wanapokutana na wenzao jambo la kwanza ni kuelezea habari za mpira badala ya kushuhudia wema na upendo wa Yesu.

Ni sahihi kwa wana wa Mungu kuwa na ushabiki wa mpira?

Kama ni sahihi; kwa namna gani? Kama sio sahihi; kwa nini?

Kushabikia timu za mpira kuna manufaa gani?

15 Responses to “Ushabiki wa Timu ya Mpira na Ukristo”

  1. Musa Says:

    Kuna starehe nyingi duniani na wapendwa nao wanastahili kushiriki starehe zile zisizowapelekea kwenye dhambi. Ushabiki wa mpira ni mojawapo ya hizo starehe na tukianza kuwekeana sheria kwamba mpira usiangaliwe nadhani tutakuwa tunawapa watu sheria ambazo Mungu hakuzisema. Naona itakuwa kama ufarisayo fulani.Waacheni watu wawe huru, kuokoka ni kuwekwa huru siyo kuingizwa kwenye kambi ya sheria za usiguse hiki, usiangalie hiki au usisikilize hiki. Kwani hao wapendwa waangaliao mpira hawana Roho Mtakata?

  2. MaryWilly Says:

    Musa ni mada nzuri ya kuelimishana,binafsi ni mpenzi wa mpira especially football,nazipenda baadhi ya timu ikiwemo enyimba though am not crazy on it.Lakini napata mashaka kwa mtu kushabikia timu kama Man United wanaojiita Mashetani wekundu! hakika kwa mtu wa Mungu kuwa shabiki wa timu kama hiyo sidhani kama kuna utukufu! Naomba ufafanuzi zaidi juu ya ushabiki wa mpira.
    stay blessed

  3. jon Says:

    mkiongozwa na roho mtajua kipi ni chema na kipi ni kibaya kwa mkristo aliyeokoka kushiriki mpira si dhambi hata kidogo ila kama mlokole inakupasa kuwa na kiasi na kufanya hiyo ni starehe isiyoweza kuharibu ratiba yako kwa kazi za Mungu sio uahirishe hata kwenda kanisani sababu ya mpira Roho mwenyewe akituongoza tutakuwa na kiasi nafsini mwetu hasa kwa mambo ya kidunia MUHIMU KUELEWA NI KWAMBA ULOKOLE SIO MATESO BALI KUISHI MAISHA YANAYOMPENDEZA MUNGU,
    swali langu kwa Mary Willy: umesema hupendi Man U kwa sababu wanaitwa mashetani wekundu je na hiyo Enyimba unajua maana yake?

    nawasilisha!

  4. Shoo GAP Says:

    Ndugu yangu Musa,
    Hapa ni mahali pa kujifunza na wala hatuanzishi sheria mpya hapa hata kidogo. nimeijua SG kwa muda sio mwingi nimesoma post nyingi humu, ila sijaona wachangiaji wakilenga kutunga sheria. Nilichoipendea SG they are God’s word centred, inapotokea mtu akaenda nje ya Neno la Mungu anarudishwa kwenye mjadala kwa kutumia Neno la Mungu. Mada iliyopo hapo juu imekuja kwa namna ya maswali, yanahitaji majibu ambayo ni ya Kibiblia. Upo ushabiki, upenzi na ukeretwa wa michezo mbalimbali. Binafsi nilinyamaza kimya ili nijifunze na nibadilike iwapo nimeenda mkono wa kuume au wa kushoto wa Neno la Mungu. HICHO NDICHO NINATAMANI KWA HAMU HAPA. Katika mjadala wowote unaoendelea hapa ni lazima kuwa tayari kubadilika, na sio lengo letu kubishana au kulumbana au kukashfiana au kumshambulia mtu yeyote.

    Yesu alipotoa mfano wa mpanzi alionyesha zipo mbegu zilizoanguka katika udongo mzuri na zikazaa sana. Udongo mzuri ni moyo wa unyenyekevu uliotayari kujifunza kwa Yesu kwa kulipokea Neno lake. Maandalizi ya moyo wako ni kazi yako bali jibu la ulimi ni kazi ya Mungu.

    Andaa moyo wako Musa, tulia watoto wa Mungu waanze kutufundisha mimi nawe, mimi nami nina upenzi usiorasmi wa timu fulani fulani. Napenda kujua niwe mpenzi namna gani au nisiwe mpenzi kabisa. Nisaidie nawe pia Musa ushabiki wa mpira una umuhimu gani kwa kujibu maswali hayo hapo juu. Mungu akubariki sana. Nakupenda katika Kristo Yesu.

  5. Asheri Says:

    Shalomu,

    Nawasalimu kwa Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

    Sijaja kutoa mchango wangu kwasasa, bado sijapata muda wa kukaa chini na kuangalia kama biblia imezungumza juu ya jambo hili, ila nimekumbuka habari za ndugu yangu mmoja nikaona niitoe hapa ingawa sijapata ridhaa yake.

    Huyu ndugu aliokoka wakati mimi tayari nimeokoka. Baada ya kuokoka, sikumbuki ilipita muda gani lakini ninachokikumbuka alikuja akatushuhudia kuwa hapo kale (kabla ya kuokoka) alikuwa mpenzi mkubwa wa timu fulani ya hapa Tanzania na alikuwa na picha za hiyo timu, lakini kati ya mambo yaliyotokea baada ya kuokoka ni kuongozwa kuachana na mambo ya upenzi wa mpira/timu. Ili kulitii neno hilo alizichoma moto zile picha zote alizokuwa nazo za hiyo timu.

    Nimeona nitoe habari hii kwasababu ilitokea baada ya mtu kuokoka. Inawezekana sijaweza kukielezea kisa chenyewe kwa sahihi sana, hii ni kutokana na muda mrefu kuwa umepita tangu kilipotokea, kama 15 hivi. Wakati huo bado hatukuwa na exposure kubwa ya hii michezo ya kimataifa tuliyonayo leo.

    Mungu akinipa neema nitarudi kutoa mchango wangu pamoja na maswali kadhaa niliyo nayo kichwani mwangu.

    Shalomu

  6. Mary Sabihi Says:

    Mpendwa Shoo, umenena na Mungu wangu akubariki, kweli uwanja huu ni shule , tena zaidi ya shule, hatuna haja ya kuwa na jazba bali tukubali, kujifunza.Kupitia SG kuna mambo mengi mno tunayapata, mimi nimepata kujua mambo mengi, mengine niliyaona mema kwangu kumbe yalikuwa hayampendezi Mungu..Tuendelee KUJIFUNZA.

  7. Baba Raul Says:

    Sidhani kama kuna tatizo mtu kuwa mpenzi wa mpira,unajua kila binadamu ana kitu anachokipenda sana, mwingine kuimba, mwingine kucheza ngoma, na kadhalika. na upenzi wa mpira nao ni hivyo hivyo. mpira una mambo mengi mazuri ya kuburudisha na kufundisha pia, binafsi katika maisha yangu sidhani kama kuna jambo ninalolifanya bila kuwa na analogue yake katika mpira, nikiwa darasani nasoma,au kazini ni lazima nitatafuta motivation inayohusiana na soka, kwa mfano kama mambo yamekuwa magumu basi ninatumia neno ambalo lipo kwenye website ya Real Madrid “impossible is nothing” huo ni motto wa Adidas. pia ninapofanya kazi yangu huwa nasema ni lazima nifike mwisho tena vizuri na huo ni moto wa Real Madrid “it is not enough to win, but we must win by playing better” so nami pia ndio ninavyoishi. na mpira unatufundisha kushinda na pia kupokea tunaposhindwa jambo, lakini tunajipanga ili kufanikiwa katika nafasi ijayo huo ndio mpira ulivyo. pia mpira huo huo unaweza kutumika kuleta amani katika sehemu zenye vita na ujumbe huwa unafika haraka sana. katika wiki chache zijazo kutakuwa na mashindano yanaitwa peace cup kule Hispania, hayo ni mashindano ya kuhamasisha amani katika mashariki ya kati. hivyo kwa mpenda amani yeyote atakuwa na jambo la kujifunza hapo awe ameokoka au hajaokoka. na hivi sasa ninapoandika kuna mchezaji mmoja maarufu toka Hispania yupo nchini Mali akijitahidi kutoa misaada kwa watoto ili waweze kuishi vizuri, hayo ni mambo ambayo hayahitaji kuokoka ili kuona kama ni mazuri.
    linapokuja suala la ratiba za soka na ibada hilo ni jambo la mmoja kuangalia, kwa mfano wengine makanisa tunayosali yana ibada nyingi zinazopishana muda hivyo unaweza kuchagua ibada inayokufaa, ili mradi yote mawili yaende vizuri. binafsi jumamosi usiku na jumapili usiku kunitoa kuiangalia Real Madrid ikicheza unahitaji karandinga.

  8. Steve M. Says:

    Shalom Wana wa Mungu,
    nimefurahi kuona watu wakitoa maoni yao. Nami pia ningependa nitoe maoni yangu kulingana na mada na kwa kupima na Neno la Mungu.

    Kabla ya kuanza, ningependa niweke changamoto moja ambayo wana wa Mungu tunajisahau wakati mwingine. Mara nyingi tunakuwa tunatafuta wapi Mungu amekataza kitu fulani. Mathalani ktk mada ya kama ni halali kwa mkristo kutumia kileo na nyingine nyingi. Changamoto yangu ni hii, badala ya kujiuliza ni wapi Biblia imekataza pekee, ni vema pia tukajiuliza “Ni wapi Biblia imeruhusu?” Ni changamoto!

    Sasa nikirudi kwenye mada husika, kabla ya kuendelea ni vema tukaelewana juu ya maana ya maneno nitakayotumia. Yawezekana maneno haya yakawa na maana zaidi ya hii, lakini mimi katika kuandika hapa nitayatumia kama ifuatavyo:
    Mpenzi wa mpira – Mtu yeyote anayependa mpira. Yaani akikuta mpira ktk Tv au computer au hata watu wanazungumzia, anakuwa anapendelea. lakini yeye si mfuatiliaji sana. Anapenda mpira tu.

    Kwa mtu kama huyu, kwake mpira ni sawa na kunywa soda, au hata kuogelea au michezo mingine isiyo kinyume na Biblia. Biblia iko wazi kuwa mtu kama huyu hakosei na yuko sahihi. Ni mambo ambayo mtu anakuwa anachagua na hayana madhara katika uhusiano wake na Mungu.

    “Let no man therefore judge you in meat, or in drink, or in respect of an holyday, or of the new moon, or of the sabbath days…Wherefore if ye be dead with Christ from the rudiments of the world, why, as though living in the world, are ye subject to ordinances, (Touch not; taste not; handle not; Which all are to perish with the using;) after the commandments and doctrines of men? ” (Colossians 2:16 – 22 )

    Kundi la pili ni la wale “mashabiki”. Nitalitumia neno hili nikimaanisha mtu ambaye hawezi kufanya chochote kama kuna timu anayoipenda inacheza mpaka aone, au ambaye timu yake ikifungwa anapata kiharusi au hata siku hiyo nyumbani hapakaliki. Mkristo hawezi kuwa shabiki wa timu fulani (kwa maana ya hapo juu). Maandiko yanamtaka Mkristo awe “shabiki” wa Kristo, au kwa maana sahihi, “Kristo ndio kila kitu”. Ukifika mahali huwezi fanya chochote kama timu yako ikipoteza au kuonewa au kufanywa chochote, unakuwa kama mwenye msiba au unapata presha na mengineyo, uko hatarini.

    1. Uko hatarini kuufanya au tayari umeufanya mpira ndio Mungu wako. Mtu yuko tayari kufanya chochote anapokuwa chini ya mungu wake. Sasa kama uko tayari kufanya chochote kwa ajili ya timu yako, jichunguze kama mpira haujawa mungu wako.

    “All things are lawful unto me, but all things are not expedient: all things are lawful for me, but I will not be brought under the power of any. Meats for the belly, and the belly for meats: but God shall destroy both it and them. Now the body is not for fornication, but for the Lord; and the Lord for the body” 1Corinthians 6:12-13

    Question: Are you under power of soccer or any THING?

    “All things are lawful for me, but all things are not expedient: all things are lawful for me, but all things edify not.” 1Corinthians 10:23

    Question:Does Soccer or any other game you watch edify you?

    “(For many walk, of whom I have told you often, and now tell you even weeping, that they are the enemies of the cross of Christ: Whose end is destruction, whose God is their belly, and whose glory is in their shame, who mind earthly things.) For our conversation is in heaven; from whence also we look for the Saviour, the Lord Jesus Christ: Who shall change our vile body, that it may be fashioned like unto his glorious body, according to the working whereby he is able even to subdue all things unto himself.” Philippians 3:18-21

    Question: Is soccer your god??

    2. Uko hatarini kupoteza mtazamo wa Kikristo. Nakumbuka nikiwa shabiki wa timu fulani, sikuwa serious na mambo ya Mungu kabisa. Na cha ajabu ni kuwa, nilipokuwa serious na mambo ya Mungu na kuhamisha mtazamo wangu kuelekea mbinguni, nikapoteza ushabiki na kubaki mpenzi tu wa mpira.

    Kama mpira unakuwa chanzo cha kuhamisha mawazo yako, toka kuwaza kwenda mbinguni hata kufikia kuomba muda wako wa kuishi uongezeke ILI TU uzidi kufurahia raha za soka, taa nyekundu inawaka. Mawazo yetu yanapaswa kuwa juu aliko Kristo.

    “For our conversation is in heaven; from whence also we look for the Saviour, the Lord Jesus Christ” Philippians 3:20

    Question: Is all your conversation about soccer or Jesus?

    “For in this we groan, earnestly desiring to be clothed upon with our house which is from heaven” 2Corinthians 5:2

    Question: Have soccer made you WISH to trade heaven and desire earnestly to remain on Earth forever?

    “If ye then be risen with Christ, seek those things which are above, where Christ sitteth on the right hand of God. Set your affection on things above, not on things on the earth. For ye are dead, and your life is hid with Christ in God” Colossians 3:1-3

    Question: where is your affection, above or below? Have soccer make you seek player names, best goals, player histories instead of things of Risen Christ?

    Baada ya hayo, napenda nimalizie kusema kuwa, kuna mambo ambayo katika mpira si sahihi. Hii ni kwa sababu kuna watu wenye imani tofauti katika timu tofauti tofauti. Kwa hiyo kuna hatari kadhaa katika kuangalia mpira ambazo hatuwezi kuzifumbia macho. Staili za ushangiliaji, mwonekano n.k ni baadhi tu. Kwa hiyo basi, siungi mkono mkristo kuwa shabiki, japo aweza kuwa mpenzi wa mpira (cf. definitions hapo juu).

    Badala ya kujitia sana katika mambo ya ulimwengu, sisi kama wakristo tuna majukumu mengi ambayo Mungu anataka tufanye, maana wakati unaelekea ukingoni. Na kama tukiwa waaminifu katika haya, hatutapata muda wa kuwa mashabiki wa mambo mbali mbali ya duni (si soka pekee). Haya ni baadhi tu ya hayo majukumu. Na haya ni maswali ambayo tunatakiwa tujiulize mmoja mmoja:

    1. Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost: Teaching them to observe all things whatsoever I have commanded you: and, lo, I am with you alway, even unto the end of the world. Amen. (Matthew 28:19-20) — Are you doing it??

    2. Study to shew thyself approved unto God, a workman that needeth not to be ashamed, rightly dividing the word of truth. (2Timothy 2:15)

    These were more noble than those in Thessalonica, in that they received the word with all readiness of mind, and searched the scriptures daily, whether those things were so. (Acts 17:11)
    — Do you study the Word of God daily? Do you check what your pastor/minister teaches if it is Biblical or you just swallow a caked poison?

    3. Pray without ceasing. (1Thessalonians 5:17) — Do you pray?

    4. For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men, Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly, in this present world; — Are you saved by Grace of God? What does it teach you? (Titus 2:11-12)

    5. Looking for that blessed hope, and the glorious appearing of the great God and our Saviour Jesus Christ; (Titus 2:13) — Are you desparately waiting for your Great God Jesus?

    6. Who gave himself for us, that he might redeem us from all iniquity, and purify unto himself a peculiar people, zealous of good works.(Titus 2:14) — Are you zealous of Good or evil works?

    7. These things speak, and exhort, and rebuke with all authority. Let no man despise thee. (Titus 2:15)-Do you speak out exhortation and rebuke to edify the body of Jesus? Do you do that with authority of the Word of God or yours?

    Almighty God help us!

  9. Shoo GAP Says:

    Glory to God almighty; Namshukuru Mungu kwa ajili msg yako borther Steve M nimejifunza mengi, Mungu akubariki sana.

    Baba Raul nashukuru kwa mchango wako kwa jinsi ambavyo umekuwa wazi. Lakini naona walakini hapa “binafsi jumamosi usiku na jumapili usiku kunitoa kuiangalia Real Madrid ikicheza unahitaji karandinga.” Soma ushauri wa brother Steve M, hatupaswi kuwa watumwa wa haya mambo. Mungu akubariki sana.

    Mimi huwa nikiwanatazama mpira ninakuwa upande wa wale wanaoonekana ni vibonde au wanyonge, sina timu rasmi. Na sijalewa upenzi kiasi cha kuvuruga ratiba yangu na Mungu au ratiba ya shughuli zangu binafsi.

    NAOMBA WENGINE TUENDELEE KUTOA EXPERIENCE ZETU, KWANI KATIKA HIZO TUNAJIFUNZA PIA.

    MUNGU AWABARIKI NYOTE.

  10. Steve M. Says:

    Nashukuru kwa kuwa umejifunza kitu.
    Utukufu namrudishia yeye Kristo na Roho wake atuongozaye. Tuzidi kuombeana ili tuendelee kujifunza
    Mungu akubariki na SG wote!

  11. jon Says:

    kaka mchezaji tajiri wa real madrid ni mlokole na hata zawadi yake ya uchezaji bora wa dunia aliitoa kwenye kanisa lake huko kwao Brazil na tunamwona kwenye match akifunga goli lazima anainua mikono juu kumshukuru Mungu na kabla ya FIFA kupiga marufuku alikuwa navaa fulana ya ndani yenye ujumbe wa Mungu mf THANK YOU JESUS akifunga goli anafunua anaonyesha yale maneno kwenye kamera kwenye match kama za word cup mamilioni ya watu wanaona ule ujumbe na wasiojua wanajiuliza who is Jesus.

  12. Baba Raul Says:

    Asante sana Shoo GAP kwa ushauri wako. Lakini hapo hakuna walakini hata kidogo, mimi sioni tatizo, kwani Jumamosi usiku na Jumapili usiku nakuwa nyumbani, huo muda sipo kanisani wala wapi na sio muda wa ibada walau kwa kanisa ninakoabudu, hivyo sioni tatizo hapo. Labda kwa taarifa yako tu sikupenda kuandika sana, kama alivyosema ndugu Jon, kuna wachezaji wachamungu sana tu, mfano ndio huo alioutoa hapo juu, Kaka, yeye mlokole, kila akifunga goli anashangilia kwa kuinua mikono juu, kila mechi anavaa fulana ndani yenye ujumbe tofauti tofauti, lakini mara nyingi ujumbe anaopendelea kuubeba ni huu hapa “I BELONG TO JESUS”, kila timu yake ikitwaa ubingwa ni lazima atavua hiyo fulana na watu kuona ujumbe, au kama mechi imeisha anapobadilishana jezi na mchezaji mwingine huo ujumbe waandishi wa habari wanausaka mpaka wauonyeshe, hebu niambie ni mamilioni mangapi ya watu wanapata ujumbe hapo? kwa wanaotumia rozari pia kama moja ya sala zao, kuna mchezaji Christiano Ronaldo kila mara anakuwa kaivaa hiyo hasa wakati wa mazoezi, nayo ni kitu chema labda kama huamini katika hilo.
    kwa kuongezea tu, hiyo mechi kabla haijaanza ni lazima nisali kwanza, na ikiisha ni lazima nisali pia, nasali mwanzo kuombea timu yangu, na mwisho wa mchezo nasali kushukuru Mungu kwa lolote timu ishinde au ifungwe. hivyo kwangu mimi hilo pia huniweka karibu na Mungu.
    nasisitiza tena, kwangu mimi mpira ni sehemu ya maisha yangu, ni kitu kinachonipa burudani.

  13. Shoo GAP Says:

    Jon & Baba Raul ninawashukuru kuwa wazi juu ya kile mnachokishabikia. Naomba kuwaambia kuwa hutalazamishwa hapa SG kuucha ushabiki wako na sina mpango huo. Lakini ninaomba ujue hili, kisiwapo kitu chochote katika maisha yako cha kupunguza ushirika wako na Roho Mtakatifu. Kuna jambo ambalo Wakristo wengi hatujui, nalo ni hili; Roho mtakatifu anatamani kila wakati kuwa na ushirika nasi wakati wowote, sio wakati tukiwa katika nyumba za ibada tu. Binafsi Roho Mtakatifu amenipeleka kujifunza mengi nikiwa katika ratiba zangu binafsi, mfano nikiwa nalima, natembea barabarani, nikiwa kwenye daladala n.k. Unafika wakati mwingine kukiwa kuna kipindi muhimu kwenye redio au TV Roho Mtakatifu anaweza kunipeleka kusoma Neno la Mungu au kwenda kuomba, kwa hiyo inanibidi niache ile ratiba yangu niifuate hii ya Roho Mtakatifu. Nikijua kuwa mwili wangu ni Hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo niko tayari kumwacha aendeleze ibada ndani yangu any time without being interfferered.

    Mfano mnaoutoa wa Kaka sio mara ya kwanza kuusikia, JINA LA BWANA LIBARIKIWE na Mungu aendelee kumsimamisha katika hilo alilomwitia. Ninaomba tuwe makini sana unapoiangalia shilingi angalia pande zote mbili. Unapotoa mfano wa Kaka, angalia pia mifano ya wale wengine wanaomwamini shetani na kuniambia nini unachojifunza kwao(Hawa ni wengi mno), maisha ya wachezaji wengi hayana ushuhuda hata kidogo. Katika vilabu vingine wanafanya ushirikina mtupu au msingi wa uendeshaji wa klabu hizi ni ushirikina mtupu, hapo unasemaje? Kumbuka shetani ana hila nyingi anaweza kukuwekea jambo mbele yako lina uzuri fulani lakini nyuma yake kukawa na uharibifu mwingi. Hatuachi kuzitambua hila za ibilisi anayejigeuza hata kufanana na malaika wa nuru.

    Kuna mambo mengi ya kujiuliza unaposhabikia hizi klabu. Tutafika mahali pengine kushabikia hata bendi za miziki ya duniani humo au hata wacheza shoo walio uchi kwa kuwa eti mamevaa misalaba mikubwa shingoni au wanamtaja Mungu katika miziki yao bila kujiuliza unajengwa vipi?.

    Neno la Mungu linatuambia katika 1Korintho6:12“Kila kitu ni halali kwangu,”lakini si kila kitu kina faida. “Kila kitu ni halali kwangu,”lakini SITATAWALIWA na cho chote. Kwa nini ukubali kutawaliwa na mpira?

    Tunapoendelea kujadiliana ninaomba uniambie unajengwa vipi haswa kwa yale yasiyofaa yanayooneshwa na klabu na wachezaji sio wa mpira wa miguu tu hata michezo mingine mbalimbali?

    Ushabiki kwa maana iliyotolewa na Steve M ni kukubali kutawaliwa na mapenzi ya timu fulani, unakuwa tayari kuisupport, kuitetea, kuishuhudia, kuifuatilia, kujitoa kwa hali na mali, kuiombea(kama alivyosema Baba Raul) n.k. Du! huyu kwa kweli ni bwana mwingine. Kumbuka hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili. Niwaulize jon & Baba Raul, ukakutana na mtu asiyemfahamu Yesu akaanza kutukana kocha, wachezaji na mfumo wa kilabu yako mbele yako au hata kukukashifu wewe mwenyewe unajisikia je? Unafanyaje? Utasema nini? MUNGU ATUSAIDIE. Kinachonishangaza sana ni jinsi mashabiki wengi walivyona uwezo wa ajabu kukariri majina sifa na historia za wachezaji wa kilabu anayoishabikia lakini wengine ukiwauliza akutajie majina tu ya wanafunzi wa Yesu au afungua kitabu cha Yuda kwenye Biblia mpaka akuulize kiko Agano la Kale au Jipya? Tuendelee kutafakari vyema tunajengwa vipi na ushabiki? .

    MUNGU AWABARIKI.

  14. leva Says:

    michezo si mibaya kama mpira, kukimbia .japo kuna mingine ni kweli haitufai kama mieleka na ngumi,ndiyo maana tukaambiwa vitu vyote ni halali ila sio vyote vifaavyo ndani ya michezo kuna michezo mingine haina ubaya na kuna mingine ina ubaya.ila tu kila unapohitajika kushughulika na mambo ya mungu huna budi kuacha na kuendelea na Mungu, na kama Roho amekupa nafasi unaweza tu kuangalia mpira katika Bwana. mimi sio mpenzi kabisa wa mpira lakini kama mtu ataangalia kwa utaratibu bila kuiweka merch namba moja aendelee kuburudika bila hofu kwani hauna ubaya,Muhimu Yesu awe namba (1) akiitwa kwenye kazi ya Mungu hana budi kuacha kuangalia huo mchezo na kutimiza kwanza mambo ya rohoni.mbarikiwe.

  15. Shoo GAP Says:

    Kuna jambo la kutofautisha hapa kati ya ushabiki wa mchezo fulani na uchezaji wa mchezo huo, wapo ambao ni mashabiki tu ila hawajui hata kucheza, wapo pia ambao si mashabiki wa timu fulani bali ni wachezaji haswa, wapo pia ambao ni mashabiki na pia ni wachezaji.

    Nimejaribu kuangalia katika Biblia na kukuta baadhi ya mistari inayozungunza juu ya michezo mbalimbali, ila bado sijapata inayozungunza habari za ushabiki wa michezo. Nayo ni hii hapa:-

    MAZOEZI/ UCHEZAJI
    (1) 1Timotheo.4:7-8 …… Jizoeze kuishi kwa kumcha Mungu. Maana japokuwa mazoezi ya mwili yana faida kiasi, kumcha Mungu kuna faida kwa kila hali, kwa sababu kumcha Mungu kuna faida kwa maisha ya sasa na maisha yajayo.
    (2)2Timotheo 2:5 Hali kadhalika mwanariadha hawezi kupewa tuzo kama hakufuata masharti.
    (3)1Korintho 9:24-27 Mnajua kwamba katika mashindano ya riadha wote wanao shindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu anayepata tuzo. Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa njia itakayowapatia tuzo. Kila mwana-riadha anayeshiriki katika michezo ya mashindano hufanya mazoezi makali. Wanafanya hivyo ili kupokea tuzo ambayo haidumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata tuzo isiyoharibika kamwe. Mimi sikimbii pasipo kuwa na lengo. Sipigani kama mtu anayepiga hewa; lakini nauimarisha mwili wangu na kuutawala, ili baada ya kuwahubiria wengine, mimi mwenyewe nisije nikakataliwa.

    Kwa wana wa Mungu tunaimizwa kulenga mazoezi juu ya utakatifu/ kumcha Mungu ambayo yana FAIDA ya maisha haya na yale yajayo. Hapa anaonesha pia kuwa mazoezi ya mwili yana faida kiasi, kwa uelewa wangu ni vizuri kufanya mazoezi ya mwili. Mazoezi haya yanaweza kufanywa kwa namna mbalimbali mf. mazoezi ya viungo tu(gym), kukimbia, kutembea, mazoezi kwa kutumia michezo mbalimbali mfano Soka, netball, volleyball, basketball, tennis, ngumi n.k.

    TAHADHARI: Yapo mazoezi yanayohusishwa na imani mbalimbali wakati wa ufanyaji mf. yoga, kareti, uchezaji shoo za muziki n.k. kama wana wa Mungu twapaswa kuchukua tahadhari, katika nyumba nyingine za mazoezi(gym) wanafanya mazoezi wakipiga miziki ambayo muktadha wake haueleweki wakati mwingine.
    Hizo faida kidogo za mazoezi ni zipi? Nitataja chache kwa ufahamu wangu:-
    (1) Kuufanya mwili uwe imara/ kuujenga mwili ambao ni hekalu la Roho MTakatifu.
    (2) Kuongeza uwezo wa kufikiri.
    (3) kuungeza uwezo wa kutatua changamoto kwa namna ya haraka zaidi.
    (4) Kujenga utendaji wa pamoja(team working)
    (5) Kujifunza namna ya kuweka malengo na kutafuta mbinu za kuyafikia.
    (6) Kuinua kipato.
    (7) Kuutawala mwili.
    (8)Kujifunza kutii mamlaka na taratibu zilizowekwa.

    NAOMBA MWINGINE ATUPE HASARA ZA MICHEZO AU MAZOEZI YA MWILI.

    Katika zama hizi za teknolojia kazi nyingi zimerahisishwa sana na zinafanywa zaidi na mashine. Unaweza kukuta mtu anaamka asubuhi anaingia tu kwenye gari anaendesha hadi ofisini, anashuka na kuingia ofisini na kukaa kwenye kiti hadi jioni anarudi nyumbani kwa mfumo ule ule, hapa bila mazoezi mwili utalemaa.

    Lakini pia katika uchezaji wa michezo twapaswa kutumia nafasi hiyo kwa malengo mengine ya ziada kwa mfano; kumhubiri Kristo(mf.Kaka wa Real Madrid), kujenga mahusiano mema na wachezaji wenzako ili kuudhihirisha upendo wa Kristo; lakini pia twapaswa kuchukua tahadhari ya michezo au mazoezi hayo yasije kuutawala mioyo yetu na kuchukua nafasi au ratiba ya Mungu.

    USHABIKI WA MICHEZO

    Sikufanikiwa kupata ambapo ushabiki wa mchezo umezungunzwa moja kwa moja katika Biblia. Lakini katika maneno ya Kolosai 2:15 yasemayo And having disarmed the powers and authorities, he made a public spectacle of them, triumphing over them by the cross. Hapa tunaona Yesu baada ya kumshinda Shetani akishabikia na kuushangilia ushindi wake yeye mwenyewe. Ninaamini kuwa nasi pia kila siku tunapaswa kuushangilia huu ushindi na kuendelea kuwa wapenzi, mashabiki, wafurukutwa n.k. wa timu hii ya Yesu.
    Lakini binafsi pamoja na kukosa ushahidi wa moja kwa moja katka Biblia, tuna mambo mengi mema ya kujifunza unapoangalia mchezo wowote. Twende pamoja tuangalie kwa mifano michache hapa:-

    Ukiungalia mchezo wa mpira kwa mfano unaweza kujifunza mambo mengi sana. Ni lazima kuweka magoli, bila magoli katika uwanja huo mpira utakuwa na walakini. Magoli haya ni mfano wa malengo katika maisha ya kila siku. Hata dakika 90 au 120 zikaisha na timu hizi mbili wakawa 0-0 au wasipofanikiwa kuingiza mpira kwenye yale magoli; lakini jambo la msingi walikuwa na lengo hilo. Unaweza kujifunza pia jinsi ambavyo mwili wa Kristo unavyofanya kazi. Ebu fikiri Golikipa akawa mzembe sana na washambuliaji wakawa na bidii sana, timu itafunga magoli mengi sana na pia wanaweza wakashindwa kwa kufungwa magoli mengi sana.

    Fikiria pia timu nyingine wanamabeki imara sana na washambuliaji wavivu sana, hatima yake mabeki watachoka kwani mpira utakuwa upande wao tu. Katika Ufalme wa Mungu tunaweza tukafanya huduma au maombi ya kujilinda tu ambayo hayaleti madhara kwa shetani na ufalme wake. Kumbe tunapaswa kujilinda(kuomba ulinzi wa Mungu, kujiepusha na mafundisho yasiyofaa,kujizuia n.k); pia Kupigana na ufalme wa giza(kushuhudia, kuomba maombi ya vita tukiteka ngome, fikra, hila na mipango yote ya adui n.k.).
    Katika Kanisa kila mmoja anapaswa kusimama katika zamu yake kwa bidii Mwinjilisti&waombaji(washambuliaji), Mchungaji(Kipa), Mwalimu&manabii(Kocha). Mmoja akiwa mzembe timu itashindwa.[HII NI MIFANO YA MAWAZO YANGU TU, INAWEZA ISIWE SAHIHI.
    Pia unapoangalia timu ya mpira mara nyingi wafungaji wanasifiwa sana lakini beki, kipa, kocha, daktari wa timu n.k wanaweza wasikumbukwe kabisa. Wakati mwingine anaweza kukaribia kufunga kabisa akaona mwenzake yuko katika nafasi nzuri zaidi basi anampasia ili amlizie-HUU NI USHIRIKIANO NZURI SANA NA KANISA TWAWEZA KUJIFUNZA KITU HAPO. Unaweza ukamshuhudia mtu na akampa Yesu maisha unapaswa kujua kuwa wewe ni mmaliaziaji tu Roho Mtakatifu amewatumia watu wengi ambao wamefanya kazi kubwa wengine hata kwenye huo mkutano wa injili hawajahudhuria, hupaswi kujivuna mwenyewe tu.

    Huu ni mpira wa miguu tu, lakini katika kila mchezo kuna jambo la kujifunza ukiangalia kwa makini sana. Humo ndani wapo pia ambao wanaonesha tabia mbaya(wanacheza faul) n.k.

Leave a Reply