Watu wengi wanaenda na UPAKO, wenye akili wanaenda na AGANO, Mungu wetu sio Mungu wa UPAKO ni Mungu wa MAAGANO. Upako Huja hutoweka, Lakini Agano halitoweki linadumu milele.
Wengi wanaotafuta Upako wanahangaika, wengine wanaenda Italia, wengine Israeli, Nigeria n.k yote hayo ni kupata UPAKO, Upako hupotea ndio maana pia inatokea kwa wahubiri wengi kuna kipindi kikifika wanahubiri Mafanikio, kipindi kingine wanahubiri Umoja, wengine Mwaka wa Toba Na vipindi hivi huja Hupotea! Kwa sasa wengi huubiri kuhusu habari za Siku Ya mwisho!
Wawepo Wahubiri Wengi Nchini Sio Tatizo, Tatizo ni Ufahamu walinao Kuhusu Neno La Mungu (Agano) Sio Upako Maana wengine huutumuia Upako huu kwa kupata Mapato ya aibu!.
Wewe Unayefanya biashara hauhitaji Upako, Unahitaji NENO LA MUNGU, Unayeumwa, Wenye Ndoa, Hamuhitaji Upako, Bali NENO. Sio Mtu unakuta ameokoka anahangaika kama mnganga wa kienyeji, akisikia upako wa kupata watoto anaenda, akisikia upako wa kupata pesa anaenda, akisikia mahali Fulani wanapaka mafuta anaenda. Haitakusaidia Kama Hauna Neno La Mungu Ndani Yako, Maana Biblia inasema “Neno la Kristo Likae Ndani Yenu” Utaielewa Kweli (NENO) Nayo Kweli Itakuweka Huru.
Ukiwa Huru Biashara Yako inafunguka, ndoa yako inakuwa na amani, kazi yako inakuwa huru kweli kweli, Maana Umelifahamu na Kulielewa.
–Bishop. Dastun Maboya–

Amen Askofu. Bila kulifahamu vyema Neno la Mungu itakuwa vigumu sana kuishi maisha ya ushindi. Hata upako wanaohangaika kuutafuata hauji kwa njia hiyo. Upako huja kwa kadri Unavyomtumikia Mungu kwa Moyo mmmoja, roho moja, nguvu zote na akili zote.
Mungu awabariki.
Bishop Dustan Maboya,
Kama ningelikuwa na uwezo basi kwa gharama zote ningekuzungusha Tanzania,ili uuhubiri ujumbe huu!! Na kama ujumbe huu ungeliuweka katika kanda basi kwa gharama zangu ningewapatia watumishi na wakristo wengi! Lakini kwa vile umesemama wewe unayefahamika na wengi naamini ujumbe huo umefika, ndio ujumbe ambao kanisa la leo na waumini wa leo wanauhitaji!
Kanisa limesahanu NENO! Wakristo wengi pasipo kujua wameanza taratibu kuishi kwa vitu ambavyo vinaoneka ni vya “Kimungu” lakini sio! Wakristo wa leo tunataka experience! Tunataka tuone ndio tuamini! Tunataka tusikie sauti nyingine zaidi ya Neno!Pengine Penye wingi wa watu ndio pana Mungu! Penye Miujiza Mingi ndio penye Mungu!
Mungu wa leo tunayemtafuta ni LAZIMA ATENDE PENDA ASIPENDE! AMA ZAKE AMA ZETU! lAZIMA ASIKIE, LAZIMA ABARIKI! LAZIMA AONEKANE! Na kama hatendi basi tuna Laana! Na lazima tukaivunja hiyo laana!hata kwa kutapishwa! hata kwa kutafuta kaburi la mababu!Laana ya Adamu ilitoka, lakini ya mababu hapana! Iwe ya laana kutokuwa na pesa! iwe kutopata visa ya Marekani! Iwe ya kutopata Mchumba! Hii lazima iwe ni “nira” iliyotufunga! Na upako wako utavunja hizo Nira!Kama kanisa langu haliwezi nitahamia jingine! kama haliwezi, nitaenda kwa nabii! Hii Nira lazima itafutiwe Upako!
Hatutakia kusikia alichukua laana zetu! Mbona kama hivyo sisi si matajiri wa mali za dunia hii ya kitambo! Hatutaki kusikia NEEMA YANGU YAKUTOSHA!Hiyo ilikuwa Injili ya Paulo ati! Siyo yetu! Sisi tumesikia NENO LA WAKOVU LIMETUCHOSHA! SASA TUNATAKA UPAKO! SASA TUNATAKA POWER!
Hatutaki kusikia maneno haya ya Paulo ” KATIKA DHIKI, KATIKA MISIBA,KATIKA SHIDA,KATIKA MAPIGO,KATIKA VIFUNGO,KATIKA FITINA, KATIKA TABU,KATIKA KUKESHA,KATIKA KUFUNGA,…..BALI SIKU ZOTE TU WENYE FURAHA, KAMA MASKINI TUKITAJIRISHA WENGI,KAMA WASIO NAKITU BALI TUNA VITU VYOTE!Huyu alikuwa Paulo, tujuaje kama alikuwa mchanga Kiroho!NENO TUNALOLITAKA SISI NI LA BARAKA, MAFANIKIO !
Bishop Maboya sisi tunataka upako! hatutakia Agano! Ni kweli hii ndio Injili ya Leo! Neno ni “by the way’ Mungu akubariki kwa ujumbe wako! Na akutie nguvu.Umenibariki MNO!
Amen mtumishi wa Mungu, ubarikiwe sana, inafika kipindi inabidi mtu atuamshe maana watu wanahangaika mno jamani. Umenibariki sana.
mtumishi ulichoongea hata mm naunga mkono maana bila kumjua Mungu wa kweli utahangaika. maana amesema ktk neno lake kuwa. lisikieni,ni pendo la namna ngani alilotupa baba,tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo.maana bila kusimama na neno huwezi kufika mm na wapa pole wanaotafuta upako. tunashindwa kusimama imara kwa Mungu wetu pia kijisimamia wenyewe.na ktk wokovu ukifuata hivyo utabaki kuwa mtoto mchanga kila siku
Yesu akasema mimi ni njia ya ukweli na uzima mtu hawezi kufika kwa baba bila kupitia kwangu. Kanisa kusimama ni Yesu, si upako
Ni ujumbe mfupi, lakini umejaa busara za Kimungu. Mungu Muumba wa mbingu na nchi akubariki.
Askofu Maboya wewe ni baba wa wengi. Umefanyika baraka kwa watoto wako wa kiroho wengi sana. Sisi wa ughaibuni tunatamani kukupata online na kukusikiliza kwenye you tube bila mafanikio. Kuna namna yoyote ya kupata mafundisho yako kupitia internet?Bwana azidi kukubariki.
Lisbon,Portugal.
hili ni Neno la wakati tulionao, natamani kila mmoja angepata ujumbe huu, watu wasitafute upako bali wamtafute Mungu. MUNGU AZIDI KUKUTUMIA!
Na ukweli ni kwamba ukimtafuta Mungu kwa bidii huo upako utakuja wenyewe si mpaka uwekewe mikono..Ubarikiwe Mtumishi.
Amen Bishop, that’s right!
HAKIKA UJUMBE HUU MUNGU ALIUANDAA MAHUSUSI KWA KIPINDI HICHI NA UTOKE KUPITIA KWAKO,MAANA WATU WENGI SASA HIVI WANAPOTEA KUTAFUTA UPAKO HAWAJUI KUWA IMEANDIKWA MWISHO WA DUNIA WATAKUJA MANABII WA UONGO WENGI WAKIONYESHA ISHARA MBALIMBALI ZA UONGO.
well spoken,powerful sermon!!!
kweli askofu
Neno hili limekuja kwa wakati ” a word in season” .Wakristo wengi leo wanahitaji kusikia Neno Hili.Nimeipenda sana.
Orbi,
Umenigusa,
Ubarikiwe!