10 Responses to “Mapenzi ya Mungu yatimizwe!”
Leave a Reply Cancel reply
Injili Sio Hadithi, Ni Halisi!!
Tunapenda Kuwakaribisha Watu Wote Kwenye Blog Ya Injili Ya Strictly Gospel. Bwana Yesu anakupenda!
YALIYOMO KWENYE BLOG
Top Posts
- Je tunajua nini kuhusu Freemasonry?
- Rose Muhando Autambulisha UTAMU WA YESU
- TB Joshua atabiri kifo cha Rais Afrika?
- Mtume na Nabii Josephat Mwingira
- Ujumbe kutoka kwa mwl Christopher Mwakasege
- NAMNA YA KUOMBA
- Kwaresma njema
- Edward Lowasa, atabiriwa na TB Joshua?
- ALBUM YA TATU ya - Bahati Bukuku
- Fanuel Sedekia ni marehemu!
- Tumsifu Yesu Kristo!
- Dini ya Obama bado ni gumzo Marekani
CONTACT US
Email:
strictlygospel@yahoo.co.uk
SMS 24 Hours:
TANZANIA
+255 714 915 424
Recent Comments
| ruth on Mtume na Nabii Josephat M… | |
| Eucalyptos on Zijue Karama za Roho Mtak… | |
| Rugomora on Mtume na Nabii Josephat M… | |
| Rugomora on Kwaresma njema | |
| John Bethania on TB Joshua atabiri kifo cha Rai… | |
| Rugomora on Je tunajua nini kuhusu Fr… | |
| Edwin Seleli on TB Joshua atabiri kifo cha Rai… | |
| Ck Lwembe on TB Joshua atabiri kifo cha Rai… | |
| Baraka on Mtume na Nabii Josephat M… | |
| Noel Msanjila Arusha on Je tunajua nini kuhusu Fr… | |
| Meinrald on Usitafute Upako, Tafuta Agano… | |
| Orbi on Mtume na Nabii Josephat M… | |
| mabinza LS, on Utatu Mtakatifu! | |
| Primi P Mosile on Tumsifu Yesu Kristo! | |
| christopher on TB Joshua atabiri kifo cha Rai… |
Fahamu Zaidi!
OTHER WEBSITES
- Ambwene Michael
- Christopher Mwakasege
- Emmanuel Sowane
- Enjoying His Presence
- Ev. Moses Mayila
- Hosanna Inc
- Massaba
- Mgisa Mtebe
- Mr&Mrs. George Kayala
- Mtumishi Lema
- National Network of Prayer
- Nyimbo za Dini
- Patrick Sanga Ministries
- Rhema Outreach Ministries
- Ruma Africa
- Sam Sasali "PAPAA"
- The Daniel Initiative
- Uncle Jimmy
- Women Of Christ
Featured Posts
-
Dini ya Obama bado ni gumzo Marekani
Hivi karibuni mzozo kuhusu dini ya Rais wa Marekani Barack Obama umeibuka tena, ambapo wapinzani wake wakimhusisha na dini ya kiislamu. Mtumishi wa Mungu Franklin Graham, mtoto wa Mwinjilisti Billy Graham alipohojiwa na kituo cha MSNBC kuhusu dini ya Obama, Alijibu ” Muulizeni yeye, siwezi kumjibia mtu swali hilo, Ninachojua mimi ni mwenye dhambi, na [...]
-
Tumsifu Yesu Kristo!
Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Mimi ni mama mwenye Familia ya watoto wawili ninaomba mnisaide kuniombea familia yangu imeingiwa na mfadhaiko mkubwa mtoto wa kwanza kati ya hawa wawili anakunywa sana pombe hata siku nyingine kushindwa kwenda kazini. hajaoa bado. na anavuta sigara sana, vilevile hawa wote wawili hawana mwammko kabisa wa kumfuata Yesu, [...]
-
Umetenda Mema – Kambua
Kambua Kambua ni muimbaji wa nyimbo za Injili mwenye jina kubwa nchini Kenya, alianza kuimba na kupenda nyimbo za Injili alipokuwa mdogo na watu wengi waliona kilichokuwa ndani yake, baadaye mwaka 2005 akaenda kusomea Muziki nchini Canada chuo cha Kikristo, Calgary. Na katika maisha yake chuoni, alijiunga na band ya chuo Legacy Youth Conference (LYC). [...]
-
Zijue Karama za Roho Mtakatifu
I Wakorintho 14:12. Inasema ‘vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. Mungu hafanyi kitu bila kusudi, na kusudi la semina hii ni:- Kuna jambo Mungu anataka kufundisha katikati yetu ambalo litahusisha sana utendaji wa karama za Roho Mtakatifu. Kurahisisha [...]
-
Tembea na Bwana Yesu Wakati wote.
Kama wewe ni mkristo elewa uko duniani kwa kusudi la Mungu, Naamini kwamba Mungu amempa kila mmoja wetu kusudi amempa vipawa au karama na huduma mbalimbali, Naamini kama una uhusiano mzuri na Mungu, kama utatembea naye kila siku kwenye maombi yako na mazungumzo yako uko naye. Unaweza kujua mwisho wako utakapokaribia baada ya kumaliza kile [...]

Shalom,
…………Kila wakati, katika kila maamuzi na katika kila jambo tunaloliendea.
Hatujakatazwa kuomba mahitaji au ‘desires’ (matamanio ya mioyo yetu), lakini Yeye anaona ‘beyond’ ya kuona kwetu, anajua ni kwa namna gani, wakati gani na mahali gani . Anajua hatari na faida zilizopo mbele ya yale tunayoyaomba. Anaweza kujibu sawa sawa na tunavyoomba au tofauti lakini wakati wote ‘NI KWA FAIDA YETU WENYEWE’
Mithali 3; 5-6
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,wala usizitegemee akili zako mwenyewe,
katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako
Kuna wakati tunaomba lkn tunakuwa hatujui future ya yale tuyaombayo. Ukiamini Mungu anakupenda basi utahofu kumwamini kuwa atatenda kwa namna ambayo itakuletea furaha ya kudumu.
Watu wengi wanadhani kuwa Mungu anaweza kukukomoa ukimwachia Yeye atende, tunaanza kutumia akili, hisia na mazingira na mwisho wake tunaishia kulia, kujilaumu na kujuta.
Waebrania 10; 35-36
Kwa hiyo msilitupe tumaini lenu, kwa maana lina thawabu kubwa mno. Inawapasa kuvumilia ili mkiisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi.
IMANI inayoambatana na SUBIRA;ni jambo la msingi sana katika kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie katika maeneo mbali mbali ya maisha yetu.
Mbarikiwe
Ni wakati wote ule au “katika maombi yetu yote”.
Kwanini nasema hivi?
Yesu alisema; “…nanyi msalipo…MAPENZI YAKO YATIMIZWE…”. Japokuwa
mapenzi ya Mungu yaweza kuwa ni kutupitisha mahali fulani tusipotaka
ni lazima tung’amue kuwa YEYE ANATUWAZIA YALIYO MEMA NA MAWAZO YAKE
YAKO JUU SANA YA YALE TUWAZAYO.
Barikiwa!
Shalom!
Tunapaswa kuomba mapenzi ya Mungu yatimizwe kila wakati na kwa kila jambo, coz hayo ndiyo mapenzi yenyewe ya Mungu. It is written in isaiah 46:9-10 …for I am God, and there is no one else; I am God, and there is none like Me,Declaring the end and the result from the beginning, and from ancient times the things that are not yet done, saying, My counsel shall stand, and I will do all My pleasure and purpose,” Psalms 33:11 “The counsel of the Lord stands forever, the thoughts of His heart through all generations.” tena mhubiri anasema katika Ecclesiastes 3:14 “I know that whatever God does, it endures forever; nothing can be added to it nor anything taken from it. And God does it so that men will [reverently] fear Him [revere and worship Him, knowing that He is]
‘
Kimsingi anything less than the perfect will of God leads into Gods Judgment. kama ukiomba chochote ambacho kiko tofauti na mapenzi matimilifu ya Mungu uwe na uhakika unaweza ukakipata, lakini matokeo yake ni hukumu ya Mungu inayoambatana nacho. so to stay safe; Omba mapeni ya Mungu yatimizwe kwa kila jambo, kila wakati.
mbarikiwe.
Swali hili limeleta changamoto sana, hasa kwangu! Maana mara nyingi, kama siyo mara zote, ninaposikia watu wakituma maombi ya kuombea mgonjwa, kila anayehitaji husema kuwa anaamini Mungu atamponya, au anaamini katika Mungu atashinda. Sijawahi kusikia au kusoma mahali popote mtu akiombea mgonjwa kisha akasema kuwa pamoja na maombi hayo lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe!
Nyakati zote, tunapolia kwa Mungu katika jambo fulani, huwa tunahitaji Mungu atuepushie au atue mzigo fulani uliokok moyoni au mwilini.
Ngoja nisikilize niendelee kujifunza kwa wachangiaji!
Kwa kweli biblia kila wakati huonekana nijibu sahihi katika maisha ya mwanadamu, kwa kila anayeiamini nakujifunza kwa bidii.
Kila wakati tunapaswa kutamani kuona mapenzi ya Mungu yakitimia. Huo ni mtazamo mzuri, ambao Mungu anapendezwa nao anapouona mioyoni mwetu.
Nionavyo mimi,
kauli kwamba “Mapenzi yako yatimizwe” inaweza kutumika pale ambapo kuna uamuzi ambao uko mbele ya mtu na kuna ugumu kwa namna ulivyo kuutekeleza,pale ambapo mtu anajaribu “ku-bargain” na Mungu kama kunaweza kukawa na njia mbadala ya kufikia mwisho unaotakiwa (kama vile alivyofanya samweli wakati alipoambiwa aende kumpaka mafuta daudi,Samweli aliogopa kwamba Sauli akisikia atamuua na ndipo Mungu akampa njia ya kufanya 1:samweli 16:1-2).
Kwenye Biblia tunaona sehemu ambayo Yesu alitamka maneno hayo ni pale ambapo jambo alilokuwa analiendea lilikuwa ni gumu kwa mwili ingawa roho yake ilikuwa tayari,
na tunaona Yesu hakupata majibu ya maombi yake kwani yalikuwa nje ya “kusudi la Mungu la kuja kwake(Yesu) duniani”, kwa sababu hakukuwa na njia mbadala ya kumkomboa mwanadamu isipokuwa njia ya msalaba..
Biblia haijatupa jibu alilopewa Yesu aliposema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke
ila mwandishi wa Luka anatuambia kilichotokea baada ya Yesu kukubali kuuendea
ni namna fulani ya mahangaiko yanayokuwa ndani ya mtu hasa kama lile lililo mbele yake kama kusudi la Mungu linaonekana gumu kwa namna ya Mwili kiutekelezaji kama lilivyo..
Wapendwa,
mapenzi ya Mungu=Neno la Mungu..1Yoh 5: 14-15…so ukiomba kitu sawasawa na Neno la Mungu manake unaomba sawasawa na mapenzi ya Mungu..Mukiweza pata kitabu cha Haggin on Prayer Bible study case mtajifunza mambo mengi sana. Ili uombe sawa sawa na mapenzi ya Mungu, ni lazima ulijue Neno la Mungu linasemaje kuhusu hicho unachotaka kukiomba. Kwa wale ambao mmepata neema ya kusikiliza somo la Mwakasege la jinsi ya kusukuma maombi pia mtaweza kusaidia wengine hapa.
Maombi ya Bwana Yesu pale getsemane akisema ‘ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke……ni aina mojawapo ya maombi na hayakuwa maombi yake ya kila siku (This one was a consecrational prayer kind of ).
Mubarikiwe
Kwa ndugu Amani Musomba
Biblia inatupa jibu juu ya maombi ya Yesu aliyoomba akisema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke. Jibu alilopewa na Mungu ni -Malaika alitumwa kwenda kumtia nguvu-(encouragement, neema, nguvu, uwezo ) ya kupitia mateso yaliyokuwa mbele yake Soma Biblia yako vizuri Luka 22:43
Ubarikiwe
Kwako Glady,
nimekuelewa mpendwa,
naona maandishi yangu yalikuwa “trimmed”,ila nilichokuwa nataka kuonyesha ni kwamba;
kwa mujibu wa mathayo,Yesu aliomba ombi hilo moja mara tatu(Mathayo 26:38-44), haituambii jibu alilopewa(kwa mara zote tatu hakukuwa na jibu)
Lakini Luka anatuambia kilichotokea(jibu alilopewa) baada ya yeye kukubali kuuendea msalaba.(luka 22:43).”Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu”..
Nimekupata kabisa mpendwa..
Ubarikiwe..