Mimi nimeokoka January mwaka huu nimekuwa na maswali kuhusu maana ya TOBA, na nini maana ya ubatizo wa TOBA? na pia kuna mstari kwenye Biblia nikisoma siuelewi vizuri kuhusu ubatizo, unatoka Yohana 3:5 ‘Yesu akajibu Amin Amin nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.’
–Hellen Charles

kuzaliwa mara ya pili,ni kuachana na dhambi zote na kumfuata Yesu! bytheway,ni dhambi kuongozwa sala ya toba.mtu akiamua kuokoka,atubu mwenyewe kwa kinywa chake yale aliyomkosea Yesu.Pia,maneno yale yatoke rohoni mwake mwenyewe kama Zachayo.alipoamua kutubu,alikiri makosa yake mbele ya watu na Yesu bila kuongozwa namtu yeyote kutubu.ina maana,walokole wengi,hatujaokoka sawasawa sababu,tumeongozwa kutubu! a challenge-Precious.
Precious,
Mimi nadhani toba ya Kweli haijalishi umeongozwa na mtu….hasa baada ya kulisikia Neno la Mungu na Kusema sasa nifanyeje (Matendo 2:37) Au umeifanya peke yako….La Msingi Toba hiyo itazaa matunda (Matunda yapasayo toba) Kuacha maovu na kuamua kumfuata Kristo……!
Labda tungemsaidia muuliza mada maana ya Toba….na Ubatizo wa toba…..
Precious,
Mafundisho ya’ Ubatizo wa toba” yanafundishwa sana na watu wenye misimamo ya “Oneness Pentecostalism” ambao baada ya kukujia kwa “ubatizo wa toba” watakujia tena na “Ubatizo wa jina la Yesu tu” kwanza huanzia mbali sana kwa kuuleza “Utatu” kwa tafsiri ambao inayalazimisha maandiko yaseme wanachotaka yaseme…….na kutokea hapo utafundishwa mafundisho mengi ambayo ni ya kufuata sheria tu (legalistc) .hivyo labda ningoje wale wanaofundisha “ubatizo wa toba” waje na maelezo yao….tuone kama yanakwenda sambamba na maana ya ubatizo kama ulivyojifunua kwenye maneno ya Mungu……..andiko hilo moja…Yoh 3:5 haliwezi kuwa ndilo la msingi kujenga hoja au fundisho la “ubatizo wa toba” Inabidi uangalie maandiko yote kuhusu ubatizo ndani ya Biblia ndio uje na fundisho….! Mstari mmoja tu haujengi fundisho (Doctrine) Hii ni kanuni ya msingi mno katika kuyaelewa maneno ya Mungu.
UBARIKIWE.
Shalom. kwa uelewa wangu, kwamujibu wa Yohana 3:5, kwanza ubatizo unaotambulika kibiblia (wa maji) ni ule wa maji mengi. na utakapobatizwa kwa maji mengi means utakuwa umetimiza haki yote. na utakapobatizwa kwa maji mengi baada ya kukata shauri la kuokoka, unakuwa umebatizwa kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. maana yake ni kwamba, huwezi kubatizwa kama hujamwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mokozi wako, halafu kisha ukamkiri kwa kinywa chako hadi kuitwa/kusema nimeokoka. baada ya hayo, ndipo inabidi utimize haki yote kwa kubatizwa kwa maji mengi kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. sasa, kama umeokoka na umebatizwa kwa maji mengi, usirubuniwe kubatizwa kwa maji mengi na mtu yoyote. maana utamkufuru Roho Mtakatifu. kwani unapoamini na kuokoka, utabatizwa kwa maji mengi huku Roho mtakatifu akihusika kwa 100%.
KUZALIWA KWA MAJI NA ROHO KUNAMAANISHA: UBATIZO SI MAJI MATUPU TU BALI NI MAJI KATIKA NENO LA KRISTO. NA KUZALIWA MARA YA PILI KUNAMAANISHA KUFANYWA UPYA ROHO YAKO YAANI KUONDOA DHAMBI YA KWANZA AMBAYO KILA BINADAMU HUZALIWA NAYO {DHAMBI YA ADAMU NA EVA KULA TUNDA BUSTANINI EDENI] HIVYO KWA KUBATIZWA TUNAKUA TUMEZALIWA UPYA ROHO ZETU.
asanteni sana na Mungu awabariki wote mlioshiriki kunisaidia kuelewa japo kwa ufupi lakini imenipa changamoto ya kuendelea kuelewa zaidi, lakini nilichokuwa namaanisha zaidi na hichi ndicho kinachonifanya nisielewe utofauti uko wapi, kuna mfanya kazi mwenzangu ameokoka akaniuliza je baada ya kuokoka umebatizwa kwa maji mengi? nikamwambia hapana, kwani haitoshi kuongozwa sala ya toba na kukiri mwenyewe kuwa nimempokea Ykuwa Bwana na Mwokozi wangu na kuenenda sawasawa na mapenzi yake na kufanyika kuwa Mwana wa Mungu hadi nibatizwe kwa maji mengi?, ndipo akaniambia kuwa nisipo batizwa kwa maji mengi nitakuwa bado sijafanya kitu kwenye kuuona ufalme wa Mungu, akanipa baadhi ya mistari ambayo ipo kwenye biblia inasema kuhusu ubatizo, nikaisoma lakini nimeshindwa kuelewa vizuri, Mungu awabariki sana na mzidi kuniombea.
1. sijawahi kuona mstari kwenye bibilia unataja maji “MENGI”. mistari yote ninayoifahamu inataja maji. kama kuna mtu anamstari unaosema neno “MENGI” nauomba tafadhali.
2.kubatizwa kwa maji ni ishara ya nje ambayo inaendana na kukiri. haya yote huwa ni kwa ajili ya muonekano wa nje. Muonekano wa ndani ndio TOBA HALISI. Toba halisi ni kuishi sawasawa na neno la Mungu. JOSHUA 1:8 na wakolosai 2:16.
3. Maji hayajawahi kuondoa dhambi. kama huamini uliza kuna watu wamebatizwa hadi mara kumi lakini dhambi iko pale pale iwe ni kuiba au kusengenya. kama huamini jiulize kwa nini viongozi wetu wakuu wa dini ambao wanatuletea mafundisho ya maji hawapendani? wanatukanana kwenye tv, wanakashfiana wao kwa wao kwa sababu macho yao yamepofuliwa na maji (ambali sio fundisho kuu) badala ya NENO LA MUNGU. ukijali sana mafundisho ya maji utasahau kuhusu neno la Mungu. Mimi nakwambia toba ya kweli na KUSOMA,KUYATAFAKARI NA KUTENDA SAWASAWA NA NENO LA MUNGU. HUU NDIO UBATIZO WA ROHO NA MOTO.
Mungu awabariki wote mliyoshiriki kunisaidia kuelewa na aendelee kuwatia nguvu, Kwa hiy dada Martha mtu ukiokoka na kumkiri Yesu kuwa bwana na mwokozi tayari unakuwa umebatizwa kwa maji na kwa roho mtakatifu, naamini nilivyoelewa ndivyo ulivyoelezea. Asante
Mwanangu,
Nakupa ushauri huu. Mwone Mchungaji wako aliyekubatiza, atakupa mafundisho mazuri kuhusiana na swali uliloliuliza katitika mtandao. Cha muhimu ni pongezikwa uamzi huu mzito kuhusiana na hatua ya usindiya kubatizwa amani ya Bwana iwe nawe.
Makunzo (Songea) 0754060996
kubatizwa kwa maji mengi ni lazima,maandiko yaonyesha waziwazi kwa kubatiza maana yake nikuzikwa na Yesu Wakolosai 2;12 ‘Mkazikwa pamoja nae katika ubatizo’Rumi6;4- Basi tulizikwa pamoja nae kwa njia ya ubatizo neno kuzikwa linaeleweka kwamba tunapozika huwa hatuziki kichwa pekee bali mwili wote, Mdo 8;36 ‘wakafika mahali penye maji’ Rumi 8;38′wakatelemka wote majini’Math 3;6 ‘akawabatiza atika mto jordani’Math 3;16-akapanda kutoka majini’ katikahaya maandiko yanonyesha jinsi ambavyo maji mengi yalitumika ktk kubatiz na ubatizaji wenyewe ulivyokuwa wa kutumbukizwa mtu mzima mzima
Safi sana Noel!.Ubatizo ni lazima!.jamani, tuangalie ‘MIFANO’ Yesu aliyotupa kwa vile alivyofanya,ndipo na sisi tutaishi sawasawa katika wokovu.maana,Yeye ndiye Mungu,Bwana na Mwokozi.tukishaelewa kila ‘step’ ya maisha yake,tutaushinda ulimwengu huu! Ubatizo ni kufa pamoja na kufufuka na Yesu,colossians2:12.ndugu,Mtangoo.ubatizo wa kweli,ni katika jina la YESU wa Nazareth(jina lipitalo majina yote).’Wapentecost’,tumepewa jina lakini hatujui kulitumia.tunabatiza kwa jina la baba,mwana na roho?!
Je,baba yupi?maana,hata shetani ni baba wa dunia hii ya uovu,baba wa uongo! Specify!.
Mwana,ndo nani? Mwili(Kristo)-ndo ulizaliwa na Yusuph na Maria.ila,Yesu;hakuzaliwa.alishuka pale Kristo alipomwendea Yohana mbatizaji,kubatizwa.
Roho,Ipi? Hata shetani ni roho!
Kabla ya Yesu kuleta ufalme wake,ilikuwa hairuhusiwi kutaja jina lake bure.Ila,baada ya Yeye kuja,akatupatia jina lake,tupate kulitumia.ndo hayo mamlaka tuliyopewa.ndo nguvu,ushindi,uzima.jina la Yesu ni kila kitu kwetu.Ubatizo katika jina la Yesu,ndio ubatizo wa kweli,wenye nguvu,mamlaka,ushindi,mafanikio n.k
Hili ni somo kubwa sana na linahitaji muda wa kukaa chini na kufafanua vyema tukitumia Neno la Mungu(Yesu wa Nazareth).
Ila kwa hayo,ningeshauri kila mtu afunue Biblia na kuangalia nini kile mitume walifanya.Jinsi gani walibatiza.
Toba;kuachana na dhambi na kumfuata Yesu maana,Yeye ni mtakatifu pia,hupendezwa sana na watakatifu.Ubatizo wa toba:ubatizo wa ondoleo la dhambi.Huu ndo ule alioutumia Yohana mbatizaji.Kwa mengi zaidi,njoo ‘House of Prayer church’-Boko Magengeni.Mbarikiwe wapendwa!.
Ujumbe:tupende sana kupata changamoto especially,kutoka katika Neno la Mungu,tutakuwa kiroho na kiufahamu zaidi!.
Hellen umeuliza swali ambalo linawatatiza wengi hasa maana ya kuokoka au kuzaliwa mara yapili au kumpokea yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako. Tatizo linatokana na neno hilohilo ambalo Yesu alimwambia mzee Nikodemo. Yesu alipoona Nikodemo haelewi anachomwambia akasema Yohana 3:8 “upepo huvuma upendako na sauti yake waisikia lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Kadhalika na hali yake mtu aliyezaliwa kwa roho (aliyeokoka)”. Na ndivyo ilivyo kwako Hellen maana unaamini tu kuwa umeokoka lakini haieleweki ni nini hasa kimekutokea. Kuokoka sio kuacha dhambi maana wako wapagani hawatendi dhambi wanaishi maisha ya kupendeza tu wakati mwingine kuliko hata waliookoka. Kuacha dhambi kunatakiwa kuwe ni matokeo ya kuokoka. Kwahiyo kuacha dhambi sio kuokoka. Kuokoka ni nini basi? Ni mabadiliko ya kiroho (spiritual transformation) yanayompata mtu anapookoka au kuzaliwa mara ya pili. Nini maana ya neno la Yesu la Yohana 3:5? Kwa lugha nyepesi kabisa (layman’s language) ili mtu auone ufalme wa Mungu sharti azaliwe mara tatu:
(i) Kuzaliwa kwa mwili (mst.wa 6a ) sababu kilichozaliwa kwa mwili ni mwili yaani mtu huzaliwa kwa mwili anapotoka tumboni mwa mama yake;
(ii) Kuzaliwa kwa maji (mst wa 5b) Mtu asipozaliwa kwa Maji na… sasa huo ndio ubatizo wa maji na;
(iii) Kuzaliwa kwa roho (mst wa 6b ) mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho maana kinachozaliwa kwa roho ni roho sio mwili tena.
Hellen wewe ulikwisha kuzaliwa kwa mwili (kutoka tumboni) na hata kwa maji (ubatizo). Lakini unapoongozwa sala ya toba (haijalishi ni mlokole gani aliyekuongoza) ndipo unapozaliwa mara ya pili au unapookoka au unapompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Kwahiyo tunapozungumza juu ya ubatizo ambao utamfanya mtu aingie mbinguni tunazungumza juu ya ubatizo wa kuzailwa mara ya pili yaani kuzaliwa mara ya kwanza kwa maji (ubatizo wa Maji) na kisha wa pili kwa roho (kuokoka). Huo ndio ubatizo unaoongelewa katika mstari wa 5.
Hata hivyo bado si rahisi kuelewa maana ya kuzaliwa mara ya pili au kuokoka. Mzee Nikodemo akamwuliza Yesu “itawezekanaje mtu mzima kuzaliwa mara ya pili? je atarudi tumboni mwa mama yake azaliwe upya? Ni ngumu kuelewa kwa sababu unapookoka saa ile unabakia kuwa yuleyule wa zamani hakuna kinachobadilika sanasana wengine huona furaha sana ndani ya mioyo yao furaha ambayo huwa inafika mahali inatoweka. Kuokoka ni kama Yesu alivyosema katika mstari wa 8 kama vile upepo usivyoeleweka unakotoka wala uendako. Hii ni kwasababu kuokoka ni mchakato wa kiroho (spiritual process) ambao hatuuoni kimwili au hata kihisia. Kwakuwa ni mchakato kuna hatua tano za msingi ili kuokoka.
(i) Kujitambua kuwa wewe ni mwenye dhambi (Warum 3:23) tafakari sana juu ya maisha yako yaliyopita ili uone jinsi ambavyo maisha yako hayakumpendeza Mungu kisha anza kujenga hasira ya kuichukia dhambi maana imekuchelewesha kwa mengi.
(ii) Kutafakari kuwa Yesu alikufa wa ajili ya dhambi zangu hivyo sina sababu ya kuendelea kuishi katika dhambi (Yohana 3:16;Warumi 8:1)
(iii) Kutubu dhambi. Kutubu dhambi nao ni mchakato ambao una hatua tatu kuu.
(a) Kuisikitikia dhambi kama Daudi alivyosema katika Zaburi 38:18 “Kwa maana nitaungama uovu wangu na kuisikitikia dhambi yangu”. Kuisikitikia dhambi vipi? Fikiri umemtukana mama yako je utakuwa na amani moyoni mwako? Si zaidi sana tunapomkosea Mungu ambaye ni mkuu kuliko mama zetu? Tunahitaji tuumbe hasira ya kuchukia na kusikitikia dhambi tulizofanya
(b) Kukiri dhambi zako kwa kinywa chako. Huku ndio kuongozwa sala ya toba. Ni vizuri kukiri dhambi zako mbele za watu kwa sababu dhambi (ambayo pia ni roho) ina tabia ya kuona aibu. Yaani ni lazima kuiaibisha dhambi mbele za miungu (wanadamu) kwa kukiri mbele zao. Kusema kweli hapa ndipo mtu anapopokea wokovu. Warumi 10:9-10 . Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako……..utaokoka. Tunapomwamini tunakuwa na haki ila tunapomkiri kwa vinywa vyetu ndipo tunaokoka.
(c) Kuacha dhambi usirudie tena (theoretical). Maana yake dhamiria moyoni mwako kuacha dhambi yaani kasirikia maisha yako ya zamani ambayo yalikuwa hayampendezi Mungu. Ni kazi kubwa sana maana mwili ni uleule, marafiki na ndugu ni walewale, mazingira unayoishi ni yaleyale, hali ya maisha ni ileile, na hata Tanzania ni ileile nk. Hakuna kinachobadilika ila moyoni.
(iv) Umpokee Yesu ndani ya moyo wako kwa njia ya Roho Mtakatifu. Baada ya kumpokea Yesu moyoni kwa kawaida mtu huwa mwenye furaha ya ajabu sana ndani ya moyo wake sababu Roho Mtakatifu huwa ameingia ndani yake. Mpaka hapo unahesabika kuwa umeokoka na jina lako limeandikwa katika kitabu cha uzima wa milele. Lakini kuna hatua moja bado ya msingi sana ambayo na yenyewe inakuhitaji utumie muda mrefu sana kutembea humo. Ni hii;
(v) Kufanyika kiumbe kipya yaani kuutupa utu wa kale na kufanyika upya. (2Wakorintho 5:17). Huu nao ni mchakato unaohitaji maelezo ya peke yake maana unaeleza namna ya kuukulia wokovu na sio kubweteka. Maana yake sio kwamba kwakuwa mtu ameongozwa sala ya toba tayari amefanyika kiumbe kipya la hasha, kuna hatua zaidi za kuchukua ili mtu awe kiumbe kipya na ya kale yawe yamekwisha kupita. Ya kale yamepita ni yapi hayo? Maana kama mtu alikuwa mwongo sio kwamba uongo umekwisha, mawazo ya kutamani bado yapo, kama alikuwa msengenyaji usengenyaji bado haujatoka na ndiyo maana wapo walokole wasengenyaji maana bado hawajawa viumbe vipya. Soma Wagalata 5:19…. tabia hizo ziko na walokole wengi kwa sababu ni kazi kubwa sana kufanyika kiumbe kipya. Kimsingi toba ni kuokoka kila siku.
John Bethania,
Congratulations!! Very elaborative points, May God Bless you abundantly! Sifa na utukufu zibaki Kwake Yeye awezaye kuwatumia watu kama John katika kuifunua siri hii ya wokovu.
John Mtangoo,kama hujawahi kuona maji mengi ktk biblia,je mbona wapo wanaobatiza watoto wadogo ingawa haionyeshi popote kwamba watoto walibatizwa ila walibarikiwa tu,maana watoto hawahukumiwi adhabu hata wakifa ,maana biblia yasema ‘aaminie na kubatizwa’je mtoto mdogo aweza kuamini?.Unaposema toba ndiyo halisi si toba pekee ila chochote kilichoagizwa ktk biblia ni cha muhimu neno lasema ‘kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao,na kwa kuwaongoza,na kwa kuwaadibisha ktk haki. Wapo waliobatizwa kwa maji mengi pia hukengeuka lakini pia waliotubu toba halisi hukengeuka.Unaposema TOBA HALISI ndio ya msingi,Mungu asingeagiza agiza uwepo ubatizo,na kama hujafundishwa maana ya ubatizo na ukajua faida yake bora usibatizwe kwanza mpaka ujue maana yake na faida yake,ndio maana NINAPINGA VIKALI watoto wadogo kubatizwa,maanaikiwa wakubwa tu hawajui maana na faiday ubatizo sembese watoto wadogo,hata KUOKOKA watu hawapaswi kuokoka ikiwa hawajui maana yake,ili wasije ingia ktk dhambi mara mbili.Kwa kuuona ubatizo si kitu halisi kama TOBA ndiko kuliko sababisha watu wakachukulia kirahisi kwa kubatiza kichwani tu,na wakasema UBATIZO unaondoa dhambi ya asili,ingawa si kweli maana tunaona hata watoto bado hukasirika ingawa inasemwa dhambi ya asili imeondolewa kwa kubatiza,elewa kwamba dhambi inaanza kuhesabiwa mara baada ya mtu kujua mema na mabaya,mtoto kamwe hahesabiwi hukumu.Ndani ya ubatizo tunatimiza haki yote.Elewa kwamba mtu anapobatizwa si jambo la kimwili tu ila na roho yake inapata kitu,ndio maan ukuija ktk ubatizo wa watu wanaoamini ujazo wa Roho Mtakatifu,baadhi ya watu hujazwa Roho mtakatifu{Mathayo 3;16-},wengine huponywa magonjwa,wengine mapepo hulipuka na kukimbia {Yohana 1;26-}Ukiona watu wanabatizwa halafu hakuna ishara hizo basi anza kuwa na mashaka na mahali ulipo.HAPO JUU NIMEONYESHA BAADHI YA MAANDIKO YANAYOONYESHA NI NINI MAANAYA KUBATIZA KWA MAJI MENGI, BIBILIA IMETUMIA NENO “KUZIKWA PAMOJA NA KRISTO KATIKA UBATIZO “RUMI6;4-,WAKOLOSAI 2;12,NA NIKAONYESHA JINSI AMBAVYO WOTE WALIOBATIZWA WALIBATIZWA KWENYE ENEO LILILOKUWA NA MAJI MENGI RUMI 8;38,MATHAYO 3;16. NIPIGIE KWA MAELEZO ZAIDI 0756 038556 na Mungu awabariki nyote.
Thanx a lot john, na mungu akaubariki sana maana umeufanya ubongo wangu kupokea kitu kizuri sana na moyo wangu kufurahi maana hicho kitu kilikuwa kinaniumiza kichwa sana na kinaninyima raha, Litukuzwe jina la bwana maana amekutumia kufungua kifungo cha mawazo yangu, mungu akubariki sana, Amen
Naomba nikujibu kidogo Preciuos,Kubatiza kwa Jina la Baba,na Mwana na Roho Mtakatifu ni agizo tena limetolewa kwa kinywa cha Yesu mwenyewe Mathayo 28;19- hatubatizi kwa jina la Yesu pekee kamwe.Kubaiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu inaonyesha ni jinsi gani unaamini utatu mtakatifu,kwa sababu unapookoka hawa wote UTATU MTAKATIFU unakaa kwako.Kama unatamka baba wa herufi ndogo basi ujue unatamka shetani ila kama unajua unachotamka kwamba ni ‘Baba’ni herufi kubwa unajua unaemtaka kwamba ni MUNGU Muumba mbingu na nchi,lakini zaidi sana maisha unayoishi katikadhamiri yako ndiko kwenye jibu hata kama ukijifanya unatamka Mungu muumba mbingu na nchi,haitasaidia walahaitakuwa kinga kwako kwamba unaamaaniha MUNGU MKUU ORIGINAL GOD,maisha yako yako ndiyo yanayotamka jina kuu wala si kinywa chako pekee,sawa precious na wote ?
Jamani tusiwe wajuzi kuliko Yesu,usiongeze wala kupunguza neno,ni kuzaliwa mara ya pili wala siyo mara tatu,maana hata imani potofu huanza hivyo hivyo.Pia ubatizo ni kwa ajili ya waliotubu tu ila ambao hawawezi kutubu ubatizo kwao ni batili Mathayo 3;11 Nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba,ubatizo wa maji ni ishara kwamba mtu huyu alitubu au alimkiri Yesu kwa kinywa chake.
Kutubu ni kubadili mtazamo ulionao.Ni kuachana na dhambi,Nikujikana na kuubeba msalaba wa Yesu. kutubu ni pamoja na kugeuka na kuachana na dhambi kwasababu, Biblia inasema watendao dhambi hawakufanana na Mungu.Kubatizwa kwa Roho ni kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu ambazo bila hizo huwezi kumpendeza Kristo.Ndiomaana katika matendo ya mitume18,19,Paulo anawauliza,Mlipookoka mliupokea na ubatizo wa Roho Mtakatifu?Hiini kuwajulisha kuwa kila anayeokoka ni lazima apokee na ahadi ya Roho Mtakatifu ili aishi akiwa na uhakika wa kufika kwa Kristo kwasababu waongozwao naRohowa Mungu hao ndio wana wa MUNGU.
Yeyote anayejazwa Roho Mtakatifu lazima matokeo yake huwa ni kunena kwa lugha,asiyenena kwa lugha,jibu ni rahisi tu kwamba hajajazwa Roho mtakatifu na kunena kwa lugha kuna tafsiri mbili kuu nionazo mimi (1)Kuongea lugha yoyote ambayo hukuwahi kujifunza,na hata unapoiongea unakuwa huielewi,lakini pia inaweza kuwa ni lugha ya watu wa kabila au taifa lingine,ila wewe huielewi (Mdo 2;4-13) (2)1 Kor 14;2)Kuongea lugha ambayo,hakuna anayeielewa,ni lugha haieleweki katika nchi yoyo duniani,hata wewe mwenyewe unakuwa huielewi,lakini ni Roho Mtakatifu anapeleka taarifa zako kwa mambo yako ya sirini.
Ndugu Masanjila,
Ni Biblia ipi hiyo inayofundisha kuwa mtu anayejazwa Roho Mtakatifu matokeo yake ni Kunena kwa Lugha….tu?”…? Hata Yesu alisema mtapokea Nguvu………matokeo ya Mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu ni Nguvu anayopata ya kumtetea KRISTO….KUMUHUBIRI KRISTO….KUWA TAYARI KUMFIA KRISTO……Hivyo ndivyo navyoona ndani ya Maandiko……….Je Maandiko haya hayako ndani ya Biblia yako…….
1. Matendo 4:8- 13 Ndipo Petro AKIJAA Roho Mtakatifu Akawaambia……..walipoona UJASIRI WA PETRO……
(Hakuna kunena lugha yoyote hapa……bali Ujasiri wa kutangaza Kristo)
2. Matendo 4:31 Hata walipokwisha Kumwomba Mungu mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”
(Hii inazidi kuthibitisha maneno ya Yesu ya Kupokea Nguvu……sio lugha wala kunena….)
3. Matendo 7:55 ” Lakini yeye (Stephano) AKIJAA ROHO MTAKATIFU AKAKAZA MACHO…….AKASEMA…….
(Stephano alipojazwa Roho Mtakatifu…..alipata Nguvu….Ujasiri….hakuna Lugha au kunena lugha mpya……)
4. Paulo alipojazwa Roho Mtakatifu Magamba yalimtoka ( Matendo 17:39)
Matokea ya Kujazwa Roho Mtakatifu sio Kunena kwa Lugha…..bali ni ujasiri/Nguvu ya kushuhudia Kristo……
5. Kunena Kwa Lugha katika Matendo ya Mitume kuliambata na NGUVU /UJASIRI wa kunena Habari za Mungu na ili kuwafikia kundi la watu waliojazana Yerusalem Roho Mtakatifu aliwawezesha MITUME Kunena kwa Lugha INAYOELEWEKA……..Kila mtu alisikia Matendo ya Mungu kwa Lugha yake Mwenyewe……..!
6. Matendo 2:41- 42 Lile kundi la watu elfu lililopokea Neno la Mungu kwa Mahubiri ya Petro…….lilibatizwa na kuendelea na mafundisho ya Mitume pasipo kunena kwa Lugha…..Je Petro alisahau kuwafanyia ubatizo huo….!
6. Lugha “ISIYOELEWEKA” INAYOONGIZWA na Roho Mtakatifu kama itazungumzwa mahali ambapo pana Kundi la Watu (waumini) Ni LAZIMA IWE NA TAFSRI……..Hivyo ndivyo anavyosema Paulo katika Kitabu cha Corintho…..
7. Paulo anataka TUNENE KWA LUGHA KAKINI HALAZAMISHI Kunena kwa Lugha…….anasema tutake sana Karama za Rohoni…..ambazo ziko nyingi…….
8.Paulo anasema anayehutubu ni MKUU kuliko anenaye Kwa Lugha…..
Nachoshauri ndugu Masanjila jaribu mno kuyapa Maandiko ya pande zote nafasi……
Ndugu Orbi,
Umenibariki saaaana!!!
Mbarikiwe nyote
Heri kumcha Mungu
SHALOM WAPENDWA.
Mungu awabariki sana, kuna vitu tunavipata ni vipya ktk masikio yetu.
PRECIOUS, naomba namba yako ya simu nina jambo nikuulize nakereketwa nalo.
AMEN.