THE DANGER OF GOOD IDEAS CONTRARY TO GOD IDEAS


We all have our own ideas when it comes to life and ministry. But we should remember that we are not of our own as Apostle Paul said it in 1 Corinthians 6:9-20 ’What? know ye not that your body is the temple of the Holy Ghost which is in you, which ye have of God, and ye are not your own? For ye are bought with a price: therefore glorify God in your body, and in your spirit, which are God’s.

When it comes to your purpose in life and ministry do not confer with flesh and blood (Galatians 1:16, 17) but always consult your Creator. With an open heart, seek the counsel of godly men and women of deep commitment to prayer; these are the men and women of God who can give you true spiritual counsel. But ultimately, you need to be sensitive to the inward witness in your personal life; you must be personally led by the Holy Spirit. Do not just rely on good ideas from your own mind or from other people, good ideas are not always God ideas and if they don’t align with God’s plan and purpose for your life, they are doomed to failure.

SPIRITUAL VITAMIN FOR YOUR SOUL

There is a way that seems right unto a man, but the end thereof are the ways of death.Proverbs 16:25

There are many devices in a man’s heart; nevertheless the counsel of the LORD, that shall stand. 
Proverbs 19:21

Now when he had left speaking, he said unto Simon, Launch out into the deep, and let down your nets for a draught. And Simon answering said unto him, Master, we have toiled all the night, and have taken nothing: nevertheless at thy word I will let down the net. Luke 5:4 -5

For my thoughts are not your thoughts, neither are your ways my ways, saith the LORD. For as the heavens are higher than the earth, so are my ways higher than your ways, and my thoughts than your thoughts. Isaiah 55:8 -9

Utayari Wa Kupokea Mabadiliko Yaletayo Mafanikio

Watu wanaokubali mabadiliko huwa tofauti na watu wanaopinga mabadiliko.

Dunia inabadilika kwa kasi na kwa namna mbalimbali, imefikia kipindi mabadiliko yamekuwa ni kitu kisichoepukika, mtu aweza kubadilika na kuwa mzuri zaidi au mbaya zaidi ya alivyokuwa mwanzo. Lengo la somo hili ni kuhamasiha mabadiliko yanayomfanya mtu awe mzuri zaidi na kupinga mabadiliko yanayomfanya mtu awe mbaya. Kwa sababu lengo ni kuleta mabadiliko katika maisha ya watu, ndo maana sura hii ya kwanza inazungumzia mabadiliko. Kuna watu wahabadiliki kwa sababu tu rahisi ya kutokujua umuhimu wa mabadiliko na jinsi ya kuchukua hatua zinazoweza kuleta mabadiliko katika maisha yao. Ni maombi yangu na dua kwamba Mungu atumie somo hili kubadilisha maisha ya watu wengi.

Tunapozungumzia mabadiliko tunamaanisha kukua, kuongezeka, kuendelea kutoka hali moja kwenda nyingine, kiwango kimoja kwenda kingine, kuacha kufanya kitu kimoja na kuanza kufanya kitu kingine, kuendelea kufanya kitu kile kile lakini kwa ubora zaidi. Inaweza kumaanisha pia kuondoa kitu kimoja mahali fulani na kuleta kitu kingine mfano kuacha tabia fulani isiyo na manufaa na kujenga tabia nyingine yenye manufaa. Neno lenye nguvu zaidi ni mageuzi, mtu unageuzwa na kuwa mtu mwingine kiroho na kitabia, kifamilia, kiuchumi na katika mambo mengine yote yahusuyo maisha kwa ujumla.

Neno la Mungu limezungumzia sana kuhusu mabadiliko na lengo hasa la Mungu ni kubadilisha maisha ya watu. Nami kama mshirika au mdau mkuu wa ufalme wa Mungu sina budi kushiriki kikamilifu katika mpango wa Mungu wa kubadilisha maisha ya watu. Hakika baada ya kusoma utakuwa mtu mwingine kabisa.

Biblia inasema habari za Yesu Kristo katika Luka 2:52 Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Neno la Mungu linasema katikaYohana 14 Mbegu ikikaa hivyo hivyo huwa haizai, lakini ikifa huzaa sana. Ukiendelea kufanya mamyo yaleyale kwa jinsi ileile utapa matokeo yaleyale, kitendo cha mbegu kufa ni kwamba inabadilika kutoka hali moja kwenda nyingine na ndipo inapoaanza kuzaa sana, wengi wetu hatuzai sana kama Yesu alivyosema katika Yohana 15:2 kwa sababu tuko katika hali ileile tumekaa vivyo hivyo.

Ukitaka vitu ambavyo hujawahi kuwa navyo, lazima ufanye mambo ambayo hujawahi kuyafanya. Ni wale tu wenye hekima kupita kiasi na wajinga kupita kiasi hubaki vile vile wakipinga mabadiliko ya kila namna.

Kuvua tabia zisizofaa na kuvaa tabia zinazofaa

Warumi 12:2 Mgeuzwe nia (mawazo, mitazamo, fikra) zenu kwa kufanywa upya

Wakolosai 3:5 – 10, (5) Kwa hiyo, kiueni kabisa cho chote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: Yaani, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na kutamani, ambayo ndiyo ibada ya sanamu. (6) Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. ( 7) Ninyi pia zamani mlienenda katika mambo haya mlipoishi maisha hayo. (8 ) Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote, yaani : Hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu. (9)Msiambiane uongo kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake (10)nanyi mmevaa utu mpya unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Mwumba wake.

Waefeso 4: 21-24, (21) Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. 22Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu. 23Mfanywe upya roho ya nia zenu, 24mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawa sawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.

Hapa mtumishi wa Mungu Paulo anazungumza kwa habari ya kuvua na kuvaa. Unavua tabia zisizofaa na unavaa tabia zinazofaa. Unavua mitazamo isiyofaa na unavaa mitazamo inyofaa. Kuvua hapa anamaanisha kuacha jambo fulani na kuvaa anamaanisha kuanza kufanya jambo jingine. Mfano una tabia ya kutokuweka akiba ya kutosha unavua tabia hiyo na unavaa tabia ya kuweka akiba au kuwekeza ili upate zaidi, unaangalie mbele zaidi ya hapo ulipo na matokea yake kubadilika na kuwa mtu tofauti na ulivyokuwa mwanzo. Lengo hasa la kila mtu halina sababu ya kuwa kitu kingine kinyume na mapenzi ya Mungu, ni muhimu sana kuhakikiksha kuwa tunayajua mapenzi ya Mungu kwetu na mabadiliko yoyote sharti yalenge kuwa kama Mungu anavyotaka tuwe, kwani kuwa tofaouti na Mungu anavyotaka hakuna furaha na utoshelevu wa maisha hata kama utakuwa na mali nyingi kiasi gani. Mtume Paulo anasema katika Waefeso 5: 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini yaliyo mapenzi ya Bwana. Huu ni mstari wa msingi sana katika somo hili. Lengo hasa ni kukuwezesha wewe uyafahamu mapenzi ya Mungu na uenende na kuishi katika hayo.

Kutimiza makusudi ya Mungu katika maisha yako siyo kitu kinachotokea tu hivi hivi, unachokiusubiri ukiwa umebweteka, inahitaji uamuzi, kuchukua hatua ambazo wakati mwingine hujawahi kuzichukua kabisa, kubadilisha tabia fulani fulani zinazokukandamiza, kubadilisha usemi wako, maombi yako, matumizi ya muda, marafiki zako na wakati mwingine hata watu unaoambatana nao mara kwa mara kwani wana nguvu ya kukuambukiza tabia njema au mbaya. Mtu mwenye hekima aliyeamua kutembea na kuishi katika mapenzi ya Mungu huchagua marafiki kwa uangalifu mkubwa.

Mabadiliko ya kweli hutokea pale ambapo kanuni za mafanikio zinafanyika kuwa tabia za watu na si misemo ya kufikirika na kuzungumzika tu. Uadilifu, uaminifu, uvimilivu, uotaji, nk. Vinakuwa ni tabia yako, ni sehemu ya maisha yako.

Cosmas Kisela