Category Archives: FILAMU
“Masanja Mkandamizaji” anaitangaza Injili!
Mchekeshaji maarufu kama Masanja Mkandamizaji, majina halisi Emmanuel Mgaya wa kundi la Ze Komedi Orijino ya TBC 1 inayorusha vichekesho vyao kila alhamis kuanzia saa moja usiku, amempa Yesu maisha yake na tayari muda mrefu ameonekana sehemu mbalimbali akiendeleza kipaji chake huku akihubiri na kuimba nyimbo za Injili na wengi wakimpa Yesu maisha yao.
Hivi karibuni alisikika kwenye kipindi cha redio moja maarufu kinachokuwa hewani kila jumapili kuanzia saa 12.30 alfajiri hadi saa 3.00 kikiongozwa na Mtangazaji, Mchungaji Harris Kapiga, Masanja alisema “Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Ze Komedy, kupitia hilo nina washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu, naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti” alisikika kwa msisitizo!
Kwa sasa, Masanja anaabudu kanisa la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari album yake ya HAKUNA JIPYA iko mitaani!
Pichani Juu: Masanja kushoto akiwa na Apostle Ndegi wa Living Water na Emmanuel Myamba, Anayevuma na Filamu ya Temptation inayopatikana sokoni!
Masanja akiwa kwenye moja ya mikutano ya Injili, Hapa ni Nzega Tabora, Mtumishi wa Mungu, Daniel Kulola alipofanya mkutano wa Injili
Akiwa kwenye kwaya yao ya New Jerusalem kutoka Mito ya baraka
Chini ni moja kati ya video iliyosambazwa, ikimuonesha Masanja akihubiri Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo!
—Picha: Masanja Mkandamizaji na Filamu Central
‘Yesu’ Atua Dar!
Mwigizaji wa sinema za Yesu Randy Brooks ametua nchini kwa ajili ya kuonesha maigizo mawili katika kanisa la City Christian Centre lililopo Upanga jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Brooks alisema atakuwa na maonesho mawili yatakayooneshwa kwa siku mbili katika kanisa hilo.
“Onyesho moja tutaonesha leo na jingine litakua kesho katika kanisa hilo na maonesho hayo pia kutakua na huduma nyingine za uponyaji na maombezi” alisema Brooks.
Akizungumzia sababu ya kuamua kuigiza maisha ya Yesu Kristo alisema haikua rahisi ulimwengu kukubaliana na maandiko juu ya maisha ya Yesu, tangu kuzaliwa kwake hadi kufa kwake:
“baada ya kutafakari kwa kina juu ya suala hilo ndipo nilipoamua kuigiza maisha ya Yesu, ili kuuweka ulimwengu pamoja na kutafakari upya juu ya binadamu kuishi maisha yanayompendeza Mungu, wanayopaswa kuishi hapa duniani”
Msanii huyu wa Kimarekani, maarufu kama Yesu, ameambatana na kikundi chake chote huku kivutio kwa watu wengi katika kikundi hicho akiwa ni kijana aliyeigiza kama shetani.
Akiwa na msafara wa watu 120 ambao wote wanashiriki katika kuigiza maisha ya Bwana Yesu kama ambavyo waumini wa dini ya Kikristo wanavyomtambua, Brooks alisema kuwa ameamua kuzunguka dunia nzima akiwa na kundi lake hilo ili kujitambulisha moja kwa moja kwa watu wasio mfahamu.
SOURCE: Mwananchi, Jumanne Julai 12, 2011.
—————————————————————————
More than 100 actors from US performing live in Tanzania
Dates
July 14th – 7:00 pm
July 15th – 3:00 pm and 7:00 pm
July 16th – 3:00 pm and 7:00 pm
July 17th – 7:00 pm
Venue: City Christian Center
Olympio Street, Dar es Salaam
(Opp Mzumbe University Dar es Salaam Campus)
Entrance Fee: FREE
Get your Free ticket today at City Christian Center or Ubungo TAG.
Or call 0655 100 200
Yesu nakupenda – Mgendi
Waliokuwa wakisubiri video ya YESU NAKUPENDA kutoka kwa mwanamama Jenniffer Mgendi inapatikana madukani, akiongea na Strictly Gospel anasema pia filamu ya TEKE LA MAMA iko sokoni, anasema utapata mafundisho mazuri yatakayokufanya usonge mbele.
Jennifer Mgendi na filamu ya TEKE LA MAMA
Muimbaji wa Injili Jennifer Mgendi anamalizia Filamu yake ya TEKE LA MAMA yenye mafundisho kwa ajili ya watu wa rika zote. Filamu hiyo iko katika hatua ya mwisho sambamba na shooting ya album yake ya YESU NAKUPENDA aliyoiimba mwaka 2004. Tutategemea kusikia hivi karibuni kuhusu nia na Lengo lake kuhusu filamu na muziki wa Injili.
Harris Kapiga naye kutamba katika filamu
Mtangazaji maarufu wa Praise Power Radio, Harris Kapiga au mzee wa nyota njema anatarajiwa kuonekana katika filamu ya NADHIRI, itakayoanza kurushwa na kituo cha television ya kikristo cha ATN kilichopo jijini Dar-es-salaam, Harris ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu huria cha Open mwaka wa pili akichukua masomo ya Political Science and Public Admninistration ameoa na wana watoto wawili.
Niliteseka sana na Mapepo – Sarah Mvungi
Kwa wapenzi wa maigizo hapa Tanzania Sara Mvungi alipata kuvuma sana KAOLE, kwa sasa ni muimbaji wa Injili na anao ushuhuda anaopenda kuwashirikisha watu kwamba “niliokoka tarehe 20/6/2004 siku hii sitaweza kuisahau katika maisha yangu, nilikuwa nateseka sana na mapepo na vidonda vya tumbo lakini Yesu wangu akaniponya” Alisema, 2007 alijikita katika uimbaji na kufanikiwa kutoka na Album ya ASANTE YESU yenye jumla ya nyimbo kumi, mbali na kuimba muziki wa Injili, anaendeleza fani yake, ni mtunzi na mwalimu wa tamthilia ambapo sasa ametunga tamthilia ya NADHIRI inayotarajiwa kutesa katika Television ya ATN hivi karibuni.
Siri ya Mafanikio – Bahati Bukuku
ALBUM YA TATU ya – Bahati Bukuku
Kwa utofauti wa uimbaji na upangaji wa mashairi, kutokana na uimbaji wake wa kipekee amefanyika kuwa baraka kwa wasikilizaji wa nyimbo. Huwezi kuwataja wanamuziki wa Injili ukaacha kumtaja Bahati Bukuku. Tayari ana album tatu mpaka sasa ya kwanza ni Mapito, Nani aitikise Dunia na ya tatu inayotamba sasa nimesamehewa dhambi sio majaribu. Bukuku yuko mbioni kufungua studio yake hivi karibuni. Mbali na uimbaji pia ni muigizaji mzuri wa filamu ambapo amekuwa akishirikiana na rafiki yake ambaye pia ni muimbaji Jennifer Mgendi.
Jennifer Mgendi muimbaji na mcheza filamu

Katika historia ya muziki wa Injili Tanzania, Jennifer Mgendi ni muimbaji wa kwanza aliyevuma na kufanikiwa kama muimbaji binafsi. Mbali na kuwa muimbaji pia ni mtunzi, mwandishi wa filamu na muigizaji anatamba na filamu mbili mpaka sasa PIGO LA FARAJA na JOTO LA ROHO aliyomshirikisha muimbaji mwenzake Bahati Bukuku pamoja na kundi la KAOLE “Lengo kubwa kwanza ni kueneza Injili kwa njia ya uimbaji na uigizaji” alisema, Mgendi alianza rasmi kazi ya muziki mwaka 1995 na albam yake ya kwanza ilikuwa ni ‘Nini?’, albam hiyo ilifuatiwa na ‘Ukarimu wake’, ‘Yesu nakupenda’ na ‘Nikiona fahari’ na ya sasa tayari iko sokoni MCHIMBA MASHIMO.







