Ikulu haikupokea mapendekezo ya majina kutoka PCT – Dr. Turuka

ikulu picha

OFISI ya Rais, Ikulu, imesema uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, haukuwa na nia ya kulibagua Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania.Imesema kuna kila sababu ya kuamini kuwa mapendekezo ya wajumbe kutoka baraza hilo hayakuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi kama sheria ilivyohitaji.

Pia, imesema pamoja na baraza hilo kutowasilisha mapendekezo yao kama ilivyotakiwa, litawakilishwa vyema na wajumbe walioteuliwa ambao wanajumuisha mjumbe aliyeteuliwa kutoka moja ya madhehebu yanayounda baraza hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ikulu mjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florence Turuka, alisema tamko la Baraza la Maaskofu kuwa linabaguliwa na serikali halina ukweli wowote.

Dk. Turuka alitoa ufafanuzi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, na kuongeza kuwa kama mapendekezo ya baraza hilo yengewasilishwa kwa mujibu wa sheria, yasingeachwa.

Alisema uchunguzi uliofanywa na Ikulu, haujathibitisha kuwa baraza hilo liliwasilisha mapendekezo yake na kwamba ni vyema baraza likajiuliza kwanini kama kulikuwa na mapendekezo hayakufikishwa kwa wakati kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar.

Dk. Turuka, alisema iwapo mapendekezo ya baraza hilo yangefikishwa kwa makatibu wakuu hao, Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohammed Sheni, wangechagua mwakilishi kutokana na mapendekezo hayo.

Alisema uchambuzi wa majina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba umebaini kati ya wajumbe 13 kutoka taasisi za kidini wa Tanzania Bara walioteuliwa, Respa Adam, ameteuliwa kutoka Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Patmos Vission, Kigamboni, ni moja ya madhehebu ambayo maaskofu wake wakuu wanaunda baraza hilo.

Kwa mujibu wa Dk. Turuka, Februari 11, mwaka huu, baraza hilo lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa limebaguliwa na serikali wanayoiheshimu, kuiombea na kuipenda katika uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.

Alisema anawahakikishia Watanzania hususan waliolengwa na taarifa ya baraza hilo kwamba serikali haikupuuzia kundi lolote lililoanishwa kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba.
Dk. Turuka alisema serikali inaliheshimu baraza na inalishukuru katika juhudi inazozifanya kwa kushirikina na serikali katika kuwaendeleza Watanzania.

Alisema makundi 850 yaliwasilisha mapendekezo ya majina 3,636, ambapo makundi ya kidini yalipendekeza majina 429.

Katibu Mkuu huyo, alisema uchambuzi wa mapendekezo 52 yaliyowasilishwa nje ya muda, haukubaini kuwepo kwa mapendekezo kutoka baraza la maaskofu wa Kipentekoste Tanzania.
Katika hatua nyingine, Dk. Turuka alisema hana uhakika kuwa wajumbe waliochaguliwa kutoka Chama cha NLD ni mtu na mke wake.

–Magazetini

Serikali imewatenga wapentekoste?

Watumishi wakiongoza maombi na watu mbali mbali wakiombea Taifa. Picha kwa hisani ya Gospel Kitaa

Hivi karibuni Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste nchini (PCT) Chini ya Uenyekiti wa Askofu David Batenzi Na uratibu mkuu wa Jopo la Maaskofu likiongozwa Na Askofu Josephat Gwajima, Askofu Zakaria Kakobe Na wengineo wakiongozwa Na Askofu Dkt. Paul Shemsanga walitoa TAMKO Kwa Serikali juu ya Kupuuzwa Kwa wapentekoste nchini katika mchakato wa Uundaji Wa Bunge la KATIBA. Katika TAMKO Hilo lililohudhuriwa kwa wingi na wanahabari, Maaskofu hao waliilaumu Serikali Kwa kutochagua wajumbe Kwenye Bunge Hilo la katiba kutoka Kwenye chombo hicho muhimu katika ukristo nchini.

Katibu Mkuu wa PCT, David Mwasota, alisema waliamua kutoa tamko hilo ili kuonyesha namna ambavyo wamesikitishwa na kitendo hicho.

“Tumewaita ili mtusaidie kufikisha masikitiko yetu kwa viongozi, Watanzania na waamini wa Kipentekoste kutokana na kitendo cha serikali yetu tunayoiheshimu, kuipenda na kuiombea, kwa kutubagua na kututenga katika bunge maalum la Katiba, huku tukiwa ni miongoni mwa taasisi kubwa za kidini na makundi mengine ya kijamii,” alisema na kuongeza:

“Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais aliagiza makundi mbalimbali ya kijamii na taasisi za kidini kupendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la Katiba na kwa kuzingatia wingi wa wanachama wetu tulipendekeza majina tisa ya watu tulioona wanafaa kutuwakilisha, lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyeteuliwa.”

Wakati hali hiyo ikiendelea Jopo Hilo la maaskofu tarehe 15 February 2014 limeitisha Maombi makubwa Kwenye Ukumbi wa PTA SABASABA. Maelfu ya Waumini kutoka kila dhehebu la kipentecoste walimiminika Na kufurika Kwenye Ukumbi huo.

Kulikuwa mwamko wa nguvu na umoja katika kusanyiko hilo Kwenye Kanisa la Kristo. Maaskofu Na Maelfu ya Wapentekoste wameiombea Kwa Uchungu nchi ya Tanzania huku wakimkumbusha Mungu kuhusu Maziwa,Mito, Madini ya kila aina Na Sasa Gesi Na Mafuta Lakini kwanini Taifa Hili Ni Maskini!!?.  Lazima Kuomba ili kama Kuna Kiongozi anayesabanisha haya Mungu amtupilie Mbali. Hakuna aliye shindana Na Taifa la Mungu akabaki Salama.

Wapentekoste ambao Kwa sensa ya Haraka wanakimbilia Milioni 11. Idadi hii inayozidi kukua siku hata siku inaleta changamoto chanya Kwenye uhai Wa Taifa.  Maaskofu walitanabaisha Kwamba kuna watu wanasema makanisa ya Kilokole Ni Mengi, kimsingi hata haya yaliyopo Ni machache mno, Mpaka yazidi wingi wa baa zote, grocery zote Na vilabu vyote vya starehe.

–Habari kutoka sehemu mbalimbali

Hongereni John Lisu kwa baraka ya watoto watatu!

lisus

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania John Lisu na mkewe Nelly Kaisi, wamepata mapacha watatu siku ya tarehe 7 January 2014. Akiongea na blogs mbali mbali anasema “Mungu amenibariki kwa watoto watatu mapacha wawili wa kiume na mmoja wa kike”

Mama na watoto wanaendelea vema.

Hongereni sana familia ya John Lisu, Utukufu ni kwa Bwana.

Vijana msiwape uongozi watu mafisadi – Sitta

sitta

Mgeni rasmi Samuel Sitta (katikati) akiwa na Dr Harrison Mwakyembe na Askofu Godfrey Malase

Dar es Salaam. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amesema vijana watafanya makosa endapo tu wataikabidhi nchi mikononi mwa wahuni ambao wanapenda kutumikia matumbo yao kwa nguvu ya pesa kitu kitakachowacheleweshea maendeleo yao.

Sitta anayetajwa kuwa miongoni mwa wawania urais 2015, aliyasema hayo  kwenye mkesha wa Mwaka Mpya uliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo alikuwa akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete.

“Mtafanya makosa kuwapa nchi watu wa jinsi hii ambao badala ya kuwatumikia wananchi wenye hali ngumu  kila kukicha, wanazidi kuteseka kunakosababishwa na mafisadi wachache.

“Endapo vijana wataendelea kupima viongozi kwa nguvu na uwezo wa pesa, tutaendelea kuchelewesha maendeleo ya nchi,” alisema Sitta.

Mbali na hayo, Waziri Sitta alibainisha kuwa kuna baadhi ya viongozi yeye akiwa mmojawao wanaweza kuibadilisha nchi, kwani maono yao ni kufuata tochi ya Mwalimu Julius Nyerere.

Mkesha huo ulioandaliwa na Umoja wa Makanisa Tanzania, ulihudhuriwa viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi.

–Mwananchi

Nelson Mandela dies at 95

mandela2

South African President Jacob Zuma announced late Thursday that revered former South African President Nelson Mandela has died. He was 95.

“This is the moment of our deepest sorrow. Our nation has lost its greatest son, yet what made Nelson Mandela great was precisely what made him human,” said Zuma in an address on CNN.

“We saw in him what we seek in ourselves and in him we saw so much of ourselves. Fellow South Africans, Nelson Mandela brought us together and it is together that we will bid him farewell,” he added.

Mandela emerged from 27 years of imprisonment on Feb. 11, 1990, to eventually lead that country out of decades of apartheid-scarred existence and has been celebrated as an icon worldwide for racial equality.

Zuma explained that Mandela will be accorded a state funeral and noted that he had ordered all flags in South Africa to be flown at half-mast from Dec. 6 until Mandela is officially laid to rest.

According to CNN, Mandela had battled several bouts of illness associated with his advancing age and had returned to his boyhood home in Eastern Cape Province where he explained that he was most at peace.
Reactions to his death have been pouring in from around the world since Zuma’s announcement.

“It is with the deepest regret that we have learned of the passing of our founder, Nelson Rolihlahla Mandela – Madiba,” the Nelson Mandela Foundation noted in a statement posted on its website.

“We want to express our sadness at this time. No words can adequately describe this enormous loss to our nation and to the world,” the statement continued. “We give thanks for his life, his leadership, his devotion to humanity and humanitarian causes. We salute our friend, colleague and comrade and thank him for his sacrifices for our freedom. The three charitable organisations that he created dedicate ourselves to continue promoting his extraordinary legacy.”

–Leonard Brair