Aina za mbegu na namna ya kupanda katika roho
a) Mawazo
Jinsi mtu awazavyo (unapowaza unapanda) ndivyo alivyo (avunavyo) Mtu anapowaza, anapanda na kama asipoyabadili anayoyawaza (asipong’oa mbegu/mche huo) atavuna
Kama vile Mungu alivyopanda bustani ya Edeni, ametupandia akili njema (sound mind) ili tuwaze vema na kutoa mavuno sahihi, Mungu aweza kutupa (mavuno) zaidi ya (mbegu tupandazo) tuwazavyo na tuombayo. Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”
b) Kumcha Mungu ni pando ambalo mavuno yake ni tunda la roho Galatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria“. Pamoja na yaliyoelezwa katika agano la Mungu na wanadamu. Yona 12:26 “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu“.
Tupande mambo muhimu matatu WAKATI WOTE (interchangeably)
a) Kufanya bidii katika kujilisha Neno la Mungu
b) Kufanya bidii katika aina zote za maombi
c) Kufanya bidii katika kumsifu na kumwabudu Mungu katika roho na kweli
Kufanya bidii katika hayo yote matatu ni kufanyaje?
Haya yafanywe wakati wote, kwanza wakati tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, pia kuwepo na nyakati za kujitenga na shughuli nyingine ili kufanya hayo matatu au moja au mawili kati ya hayo pekee. Ili kufanya wakati wote.
-E.Kiwia-