Mambo hayajileti Yenyewe…….

vinaundwa

MAMBO HAYAJILETI YENYEWE -  MAMBO YANASABABISHWA KUTOKEA.

5Naamna kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu,katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa….(2Petro 1:5)

Bwana akufunulie akili zako ili uelewe hiki tunachojifunza lakini pia akusaidie kuyaweka kwenye matendo haya unayojifunza. Sasa hivi tunaishi kwenye nyakati ambazo kumezuka mafundisho yenye msisitizo mkubwa sana kwenye upande mmoja wa miujiza kiasi kwamba watu wengi sana wamejikuta wanaishi maisha ya kimiujiza miujiza,naamanisha watu wamekuwa wanaishi wakitegemea kufanikiwa katika maisha kwa miujiza tu unakuta mtu hataki kufanya kazi anategemea akienda kuwekewa mikono na watumishi basi mambo yatajileta yenyewe tu! Kwa sababu ya watu wengi kutaka kuishi kimiujiza wamejikuta kila kitu wanaita muujiza, unakuta mtu kafanikiwa kununua gari eti anaita muujiza au mtu kwenda ulaya anaita muujiza, mama kanunuliwa kanga na mumewe anaita muujiza. Sijui kwa nini nimeanza kwa style hii lakini ninamini kuna kitu Mungu anataka tujifunze hapa na nianze kuelezea  kuhusu muujiza. Ukisoma katika kamusi ya Kiswahili sanifu inafafanua neno muujiza kama jambo lisilokuwa la kawaida. Kwa maana  nyingine muujiza ni matendo yanayofanyika kinyume na maumbile ya asili ni mambo ambayo hata ukimwambia mwanasayansi afafanue hawezi kuyafafanua yametokeaje, lakini utakuta mtumishi wa  Mungu anamuombea mtu anasema ,”pokea muujiza wa kwenda ulaya! Pokea muujiza wa gari pokea muujiza wa nyumba! Na maombi mengine mengi ambayo ninaamini msomaji unayafahamu au umeshawahi kuombewa. Nisikilize nikwambie kama hayo maombi unayoombewa yangekuwa yanatokea, mfano unaambiwa pokea muujiza wa gari halafu gari inatokea from no where au ukienda nyumbani unaikuta gari imepark hujui ilikotoka haina mwenyewe basi huo ndo muujiza lakini ukichukua hela ukaenda mwenyewe kununua gari hapo kuna muujiza gani ndugu? Au unaombewa pokea muujiza wa kwenda ulaya halafu ghafla unajikuta uko ulaya hujui umefikaje huo nao ni muujiza. Kitu gani nataka ujifunze hapa? Uache kuishi maisha ya kimiujiza kwa sababu mambo hayajileti yenyewe yanasababishwa kutokea,utanielewa tu huko mbele! Angalia Biblia yako nikuonyeshe mifano michache kuhusu miujiza halafu tuendelee, kutoka  7:10-12 inasema,

10………Haruni akabwaga fimbo yake chini mbele ya farao,mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka.

11Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi;na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo Kwa uganga wao. 12Wakabwaga kila mtu fimbo yake,nazo zikawa nyoka;lakini fimbo ya Haruni Ikazimeza fimbo zao”.

Sikia! hata ungewaita wanasayansi hapo hakuna ambaye angekueleza ile fimbo ya Musa na za wachawi ziligeuka vipi zikawa nyoka! Huo ulikuwa muujiza lakini nataka ujifunze mambo machache hapa, kwanza fahamu Mungu anatenda miujiza lakini pia kama hufahamu shetani naye anatenda miujiza! Umeona hapo fimbo ya Musa ilipotupwa chini iligeuka nyoka na wachawi wa farao wakatupa zao nazo zikawa nyoka lakini (naupenda sana huu mstari) fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zile za wachawi! Unajua maana yake? Ni hivi, kile kitendo cha fimbo ya Haruni kumeza fimbo za wachawi Mungu alikuwa anamaanisha kwamba yeye ni mkubwa kuliko shetani,alikuwa anamaanisha muujiza wake ni mkubwa na unadumu kuliko wa shetani!

Ngoja niishie hapo Mungu akitoa nafasi nitakuja na somo linalohusiana na miujiza na Baraka maana hivi ni vitu vinavyowasumbua sana watu kiasi cha kuwafanya waishi maisha ya kutanga tanga kwa kuhama kanisa hili kwenda kanisa jingine. Sasa angalia maneno anayosema Mtume Petro wakati analiandikia kanisa waraka wake wa kwanza na ninachotaka uone hapo ni yale maneno anayosema “mkijitahidi kwa UPANDE WENU”!  Sijui kama umeshawahi kutafakari mstari huu kwa makini na ukangundua yaliyojificha hapo; Petro anaposema kwa upande wenu ina maanisha kuna sehemu yako wewe kufanya kwa upande wako na kama kuna upande wako kufanya kitu basi  pia kuna sehemu ya Mungu kufanya kwa upande wake na  ndio maana kichwa cha somo kinasema mambo hayajileti  yenyewe kwa sababu kuna kitu unatakiwa kufanya kwa upande wako ambapo ukikiunganisha na upande anaofanya Mungu unapata jibu lako! Ngoja twende na mifano, angalia yeremia  29:12 – 14 inasema hivi:-

12 Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza.13 Nanyi mtanitafuta,na kuniona,mtakaponitafuta Kwa moyo wenu wote.14 Nami nitaonekana,asema BWANA,nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa……………….”.

Kwa tafsiri rahisi ni kama Mungu anasema,kwa upande wenu mnachotakiwa kufanya ni kuniita,mnachotakiwa kufanya ni kuniomba na kwa upande wangu ninachotakiwa ni kuwasikiliza,na kujionyesha kwenu! Maana yake ni nini? Kama huiti Mungu hawezi kuitika! Ndiyo! Ataitikaje wakati hajaitwa? Mpendwa unakumbuka ule mstari ambao hata ukimuuliza mtu asiye na tabia ya kusoma biblia atakutajia mstari huo? Ni ule wa mathayo 7:7, hebu uangalie kwa namna hii nilivyofanya ili kukurahisishia kuelewa!

Upande wako kufanya kitu                                                  upande wa Mungu kufanya kitu

Ombeni nanyi (kuomba)                                                       mtapewa  (kukupa unachoomba)

Tafuteni nanyi (kutafuta)                                                      mtaona (kukuonyesha unachotafuta)

Bisheni nanyi   (kubisha/kupiga hodi)                                 mtafunguliwa (kukufungulia malango)

Kumbuka mambo hayajileti yenyewe bali yanasababishwa kutokea na kwasababu hiyo hauwezi kufanikiwa katika jambo lolote kama utakuwa ni mtu wa kukaa na kusubiri Mungu afanye kitu na hata kama Mungu akifanya kitu amefanya kwa upande wake kama wewe hujafanya  kwa upande wako hauwezi kupata matokeo! Angalia mfano huu nikuonyeshe kitu, fungua Yohana 9:6-7 inasema hivi,

6 Alipokwisha kusema hayo,alitema mate chini,akafanya tope kwa yale mate.

Akampaka kipofu tope za macho,7 akamwambia,nenda kanawe katika birika ya Siloamu,

(maana yake aliyetumwa).Basi akaenda na kunawa;akarudi anaona”.

Hii ni habari ya mtu mmoja aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa  na kwa bahati akakutana na Yesu lakini katika kuponywa kwake kuna kitu alitakiwa afanye kwa upande wake ili kukamilisha uponyaji wake na kilikuwa ni kwenda kunawa kwenye birika ya siloamu na biblia inasema akaenda na kunawa akarudi anaona! Kama yule kipofu angeamua kudharau akapitiliza na kuendelea na mambo yake mengine asiende kunawa ninakwambia angebaki kipofu hivyo hivyo lakini si kwa sababu Mungu hakufanya kitu,hapana, Mungu alishafanya kwa upande wake na ilibaki sehemu yake yule kipofu kufanaya ili kukamilisha uponyaji wake!

Okey! Angalia mfano wa mtu mmoja aliyekuwa na ukoma jina lake Naamani, huyu alimwendea mtumishi wa Mungu Elisha baada ya kusikia kuwa anaweza kumponya. Alipofika kwa Elisha,alitumiwa ujumbe wa mtu kumwambia kuwa aende katika mto Yordani akajichovye mara saba na ngozi ya mwili wake itarudi kuwa kawaida kabisa. Naamani aliposikia hivyo alikasirika na kusema,”Tazama,nilidhania,bila shaka atatoka kwangu, na kusimama na kuomba kwa jina la BWANA,Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa na kuniponya mimi mwenye ukoma. Je abana na farpari,mito ya Dameski si bora kuliko mito yote ya Israel? Siwezi kujiosha ndani yake na kuwa safi? Akageuka akaondoka kwa hasira”.

(soma habari hii katika kitabu cha 2wafalme 5:9-14) Haya ndiyo mwazo waliyonayo watu wengi sana wanapokwenda kanisani au kwenye semina na mikutano ya neno la Mungu au wanapofanyiwa maombezi. Unakuta mtu haamini mpaka awekewe mikono na mtumishi, lakini nataka nikwambie kitu kimoja ambacho watu wengi wamekuwa wanakosea ambacho ni kutokuafuata maagizo wanayopewa na watumishi au kutofuata vile neno linavyosema. Sikia! Kama umeambiwa kanawe katika birika ya siloamu nenda kanawe! Kama umeambiwa kajioshe kwenye mto yordani, nenda kajioshe! Kama umeambiwa endelea mbele hata kama mbele yako kuna bahari, wewe endelea mbele!!! JUST DO IT! Upande wa Naamani ulikuwa ni kujiosha kwenye mto Yordani tu na hakuna kingine na ndio maana wale watumishi walimwambia maneno haya,”Baba yangu kama yule nabii angelikuambia kutenda jambo kubwa,usingalilitenda? Je si zaidi basi akikuambia,Jioshe uwe safi?” nachotaka kukuambia hapa ni wewe kufuata maagizo ya neno la Mungu linavyosema. Kwa hiyo nabii Elisha alifanya kwa upande wake na ulibakia upande wa muhitaji ambaye ni naamani, na lipokubalikufuata maagizo alipona kabisa!(haleluya!) Petro anasema mkijitahidi kwa upande wenu, (kumbuka hilo). Uko upande wako ambao unatakiwa kufanya kitu, sasa kwa sababu ya kutoelewa hili watu wamehangaika huku na huku katika makanisa wakiombewa lakini hawaoni mafanikio na hii ni kwa sababu wanafikiri mambo yatajileta  yenyewe tu baada ya kuwekewa mikono na watumishi! Umeshawahi kukutana na wanafunzi waliookoka? Fuatilia maendeleo yao na utakuta wengi maendeleo yao si mazuri sana au wengine ni mabaya kwa sababu wamekuwa wakiamini kuwa ile kuokoka tu ni tiketi ya kufaulu, na kwa sababu hiyo unakuta hataki kusoma, yeye na biblia na maombi tena ukifika wakati wa mitihani wanajifariji kwa kusema Mungu amesema tutakuwa kichwa wala si mikia!(hii ni ajabu kabisa). Huku ni kushindwa kucheza au kufanya kwa upande wako na mtokeo yake ni kufeli na kuanza kulaumu Mungu, sikia mwanafunzi unayesoma ujumbe huu,jitahidi kwa upande wako kusoma kwa bidii na upande wa Mungu ni kukufunulia akili zako uelewe unachosoma na ukielewa unachosoma mitihani inapokuja ni lazima, narudia tena ni lazima lile neno la kuwa kichwa litimie!( Amen?)

Kitu ni kilekile hata katika maisha ya kila siku tunayoishi, watu wamekuwa wakitaka kubarikiwa na Mungu bila ya kuwa na hata na vyombo vya kukingia Baraka hizo! Angalia kanuni alizotoa Mungu juu ya Baraka halafu linganisha na wewe unavyoenda ni sawa? Fungua kumbukumbu la torati 28:1-8 inasema:-

1 Itakuwa(shika hilo neno) utakapoisikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo,ndipo BWANA, Mungu wako atakapokutukuza juu ya mataifa yote duniani; 2 na Baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. 3 utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako,na uzao wa wanyama wako wa mifugo,maongeo ya ng’ombe wako,na wadogo wa kondoo zako.       5 litabarikiwa KAPU lako, na CHOMBO chako cha kukandia unga…………..8 BWANA ataiamuru Baraka ije juu yako katika GHALA zako, na mambo yote unayotia mkono; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA Mungu wako.”

Hapo juu nimekuandikia kwenye mabano shika hilo neno nikimaanisha lile neno “itakuwa”. Itakuwa nini? Itakuwa Baraka za Mungu zitakujilia utakapoiskia sauti ya BWANA Mungu wako kwa bidii………………..! Siyo utakapowekewa mikono na kuombewa maombi ya kupokea muujiza wa kwenda ulaya au utakapowekewa mikono na kuombewa maombi ya kupokea muujiza wa gari, hapana! Bali  itakuwa utakapoiskiliza sauti ya BWANA  Mungu wako kwa bidii! Huo ni upande wako wewe kufanya kitu na upande wa Mungu ni  kuiamuru Baraka ije juu yako lakini angalia kwa makini hiyo mistari ambayo nimeamua kuiandika kwa urefu badala ya kukupa kazi ya kwenda kusoma biblia na ninajua wengi ni wavivu kusoma biblia ndio maana napenda sana ninapoandika masomo yangu mistari yote niwe naiandika kama ilivyoandikwa kwenye biblia. Sasa Baraka ya Mungu inapoachiliwa juu yako itategemea na chombo ulicho nacho kwa ajili ya kukingia Baraka, pale juu nimeandika kuwa watu wengi wanataka kubarikiwa na Mungu lakini wakati huo huo hawana vyombo  kwa ajili ya kukingia Baraka. Sikiliza! Wakati mwingine hupokei Baraka za Mungu si kwasababu umekosea au shetani amezuia bali ni kwa sababu huna chombo cha kukingia Baraka za Mungu zinapoachiliwa! Sijakosea, nasema hivi wakati mwingine hupokei Baraka za Mungu si kwa sababu umekosea au shetani amezuia bali ni kwa sababu huna chombo cha kukingia Baraka za Mungu zinapoachiliwa! Ngoja nikuulize swali hili, unaelewa nini pale biblia inaposema litabarikiwa KAPU lako? Au inaposema na CHOMBO chako cha kuakandia unga? Au anaposema utabarikiwa mjini utabarikiwa na mashambani? Au unafikiri Mungu aliposema utabarikiwa mjini ni kwa kuwa unazurura mjini au kukaa kwenye vijiwe vya kahawa na kuongelea habari za siasa tangu asubuhi hata jioni? Hii ikusaidie uamke sasa tunapokwenda kufunuliwa hiki na Bwana Yesu. Sasa unisikilize nikwambie! Kazi uliyo nayo ni kapu la kukingia Baraka za Mungu, duka ulilo nalo ni kapu la kukingia Baraka za mungu biashara uliyo nayo (nazungumzia biashara halali) ni kapu la kukingia Baraka za Mungu na kama ulikuwa hujui hata kipaji ulichonacho kiwe ni cha kucheza mpira au kuchekesha au kuimba au kukimbia au basket ball au kucheza tenis au kuigiza au kuchora ni kapu la kukingia Baraka za Mungu! Itakuwa utakapoisikiliza sauti ya Bwana Mungu wako kwa bidii Baraka zitamiminwa kwenye kapu lako haijalishi uko mjini au shambani, oooh! Itakuwa! Akiimimina kweye duka wateja watajaa (si lazima uende kwa waganga ndo duka lako lijae wateja)! Akiimimina kwenye kazi unayofanya mshahara lazima uongezwe pamoja na cheo! Akiimimina kwenye kapu lako la football kama wewe ni kipa magoli hayaingii hovyohovyo na kama wewe ni mshambuliaji hakuna beki atasimama mbele yako, kama ni beki hakuna mshambuliaji atapita kwako nafasi yoyote utang’aa tu! (sema amen!) akiimimina shambani hata kama mvua zitakuwa kidogo utavuna wakati wengine wakishangaa( soma habari ya Isaka utaelewa ninachosema)! Hapa niongee na wale mnaokimbilia mijini mkifikiri ndo kuna Baraka, inawezekana kabisa Mungu alikuwa anataka akubariki ukiwa shambani lakini wewe umekimbilia mjini na huko mambo yako ni magumu unaishi kimiujiza-miujiza lakini bado unajipa moyo kwa kusema kuishi mjini  tu ni form six, hebu kaa na hiyo form six yako ya town na uone kama itakusaidia! Wewe umeacha kapu lako shambani  umekimbilia mjini,halafu unata Mungu akubariki,sasa hata akijaza Baraka kwenye kapu lako utajuaje wakati kapu umeacha shambani? Jipange!    Akiimimina kwenye mifugo ……..kasome habari ya Yakobo alipokwenda kuchunga mifugo ya mjomba wake Labani utaona nini kilitokea! Akiimimina kwenye kapu la kuigiza unapata kibali na kazi zako zinapendwa na unaanza kutengeneza hela kupitia kapu hilo la kuigiza! Ningeweza kusema mengi hapo lakini nataka nikuulize swali wewe unayesoma ujumbe huu, unataka Mungu akubarki ni sawa lakini unalo kapu la kukingia Baraka za Mungu zitakapomiminwa? Wengine wameacha makapu yao mashambani wamekimbilia mjini, aisee ninakwambia mambo hayajileti yenyewe bali yanasababishwa kutokea! Ni lazima ufanye kwa upande wako ili kuleta matokeo ya kile unachotaka kutoka kwa Mungu! Kumbuka Mtume Petro anasema,”Mkijitahidi kwa upande wenu”. Tulia kidogo utafakari kabla hatujaenda hatua nyingine, mwambie Mungu akusaidie ili tuweze kwenda sambamba na tukimaliza hapa usiwe kama ulivyokuwa!

Umemaliza kutafakari? Haya tuendelee, fungua kitabu cha 2falme 4:1-7 biblia inasema hivi:-

1 Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema,Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemwia Amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. 2 Elisha akamwambia,nikufanyie nini? Niambie una kitu gani nyumbani? Akasema mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani ila chupa ya mafuta. 3 Akasema, Nenda, ukatake VYOMBO huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu;

wala usitake vichache. 4 Kisha uingie ndani,ujifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge. 5 Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea  vile vyombo, na yeye akamimina. 6 Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. 7 Ndipo akaja akamwambia mtu wa Mungu, Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako” .

Hii ni habari inayomuhusu mama mjane aliyekuwa anadaiwa na kutokana na yeye kushindwa kulipa deni ilitakiwa awatoe watoto wake waende kutumikia deni hilo mpaka litakapokwisha. Lakini mama huyu hakuwa anataka watoto wake wakawe watumwa, kama ningekuwa nakufundisha kuhusu mwanamke jasiri basi pengine huu ungekuwa ni mojawapo ya mistari ambayo ningeitumia kwa kuwa huyu mama aliamua kupigana ili watoto wake wasijekwenda utumwani kwa sababu ya deni! Mama huyu alimwendea nabii Elisha na kumwambia shida yake lakini sikiliza Elisha anamjibu nini huyu mama, unajua anamwambia nikufanyie nini? Niambie unakitu gani nyumbani?  Elisha kwa upande wake alikuwa na kitu ambacho anataka kumfanyia yule mama lakini kitu kile hakiwezi kukamilika mpaka kuna kitu yule mama amefanya kwa upande wake! Kumbuka hapo nyuma nimekwambia mambo hayajileti yenyewe, mambo yanasababishwa kutokea na Mtume Petro anasema mkijitahidi kwa upande wenu….!

Nataka nikufundishe mambo machache hapa na jambo la kwanza ni hili:-

1: Matatizo hayatatuliwi kwa wewe kuendelea kukaa kwenye tatizo na kulalamika juu ya hilo tatizo! Kama yule mama angekaa tu nyumbani pasipo kutafuta msaada alikuwa anawapoteza watoto wake kwa kuwa hakukuwa na jinsi yoyote ile wasiende utumwani! Kwa hiyo ni lazima uchukuke hatua badala ya kukaa kwenye tatizo na kulalamika. 2: Angalia mistari hii kutoka Luka 8:18 inasema, 18 Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye Kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile kitu               ambacho anadhaniwa kuwa nacho”.

Sasa rudi kwenye maswali ambayo Elisha alimuuliza yule mama na angalia lile swali la pili alilomuuliza,alimuuliza hivi, “niambie una KITU (shika hilo neno)gani nyumbani? Sikiliza! Ili Mungu aweze kukutumia au kukusaidia ni lazima uwe na kitu ambacho kitamvuta Mungu kukutumia au kukusaidia! (tupo pamoja?) kasome biblia yako utaona hiki nachosema, wakati Mungu anamuita Musa alimkuta na fimbo alipomuuliza umeshika nini mkononi mwako Musa alisema fimbo, akamwambia itupe chini na alipoitupa ikageuka nyoka Musa akaogopa lakini Mungu akamwambia mshike mkiani, akamshika ikawa fimbo na tangu siku hiyo ile fimbo ikaitwa fimbo ya Mungu na miujiza mingi sana ilifanywa na Mungu kupitia ile fimbo! Siyo hicho tu kabla ya hapo Musa aliwahi kuua mmisri aliyekuwa anagombana na muisrael na hii ilikuwa sababu iliyomfanya akimbie misri na kwenda kuishi midiani, ndani mwake alikuwa na kitu cha tofauti cha kiuongozi na kiutumishi, hiki ndo Mungu alikiona ndani yake ila Musa alikitumia vibaya kwa kuua akifikiri ndo atakuwa amewasaidia waisrael. Wewe una kitu gani? Mungu anataka kukitumia hicho kitu kukusaidia au kukitumia katika kazi yake na ndo maana Elisha alimuuliza yule mama, una kitu gani nyumbani? Unamkumbuka Saul ambaye kabla ya kuitwa na Bwana alilitesa sana kanisa na kuwaua watumishi wa Mungu? Sikiliza! Kilichokuwa kinamsumbua Paul hata kufikia hatua ya kuwatesa watumishi wa Mungu kilikuwa ni wito na yeye alikuwa anajua kwa kufanya hivyo(kukamata watumishi na kuwaua au kuwaweka vifungoni) anamtumikia Mungu, na Mungu alikiona kitu kilichokuwa ndani ya Paul akaamua kumgeuza na kumtumia katika kazi yake! Kama unabisha rudi kwenye biblia kaangalie kazi aliyofaya Paul utakubaliana na mimi.Sasa wewe jaribu kusumbua watu wa Mungu na kuwaudhi wakati unajua kabisa unafanya makusudi na kwa chuki zako binafsi uone Mungu atakufanya nini!  Angalia wito wa Daudi wengi sana hawajui nini kilimvutia  Mungu kwa Daudi hata  akamweka atawale watu wake Israeli. Daudi alikuwa na moyo wa tofauti na wakati akichunga kondoo wa baba yake huko porini alitokea simba akataka kula kondoo, Daudi alipambana na simba   akamwua vile vile wakati mwingine alitokea dubu akataka kula kondoo lakini Daudi alipambana naye na kumuua. Sasa nisikilize! Kile alichofanya Daudi ndicho kitu kilichomvuta Mungu amtumie Daudi kuchunga watu wake maana Mungu aliangalia jinsi alivyojitoa kwa kondoo akajua huyu kama amefanya hivi kwa kondoo ambao ni wanyama atanifaa kwa ajili ya kondoo zangu(watu wake). Nenda katafute kwenye biblia yako kama kuna mahali Daudi aliwahi kushindwa vita au kama kuna mfalme katika Israel alikuwa mpiganaji kama Daudi! Biblia imesema katika mistari tuliyosoma hapo juu kwamba mwenye kitu atapewa na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile kitu ambacho anadhaniwa kuwa anacho. Ni hivi, kila mtu aliyeumbwa na Mungu ana KITU amabacho Mungu amempa ambacho kwa hicho Mungu atakitumia kupitishia Baraka zake  katika maisha yake na katika kazi yake, sasa hicho kitu ukikitumia unaongezewa na kama hujakitumia kwa kujua au kutokujua utanyag’anywa! Ngoja nikwambie kitu kingine naona Napata mstari mwingine hapa,hebu angalia maneno haya kutoka kitabu cha 1Falme 17:12-16. Yanasema hivi, 12 Naye akasema,kama BWANA, Mungu wako aishivyo,sina mkate ila konzi ya unga katika pipa,na mafuta kidogo katika chupa;nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu,tuule tukafe. 13Eliya akamwambia,usiogope;enenda ukafanye kama ulivyosema;lakini unifanyie kwanza mkate mdogo uniletee;kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.           14 kwa kuwa BWANA,Mungu wa Israel,asema hivi,lile pipa la unga halitapunguka wala ile chupa ya mafuta haitaisha hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi. 15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya;na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 16 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya”.

Huu ni wakati ambao nabii Eliya alitangaza kutokuwepo kwa mvua kwa kipindi cha miaka mitatu na miezi sita na katika kipindi hicho kulikuwa na njaa ya kutisha na Mungu alimwambia Eliya aende akajifiche  karibu na kijito cha kerithi na akawatuma kunguru wamlishe kwa kipindi mpaka kijito kile kilipokauka. Baada ya kukauka kwa kijito kile Mungu akamwambia Eliya aende katika nyumba ya mjane mmoja aliyeishi Sarepta. Eliya akafika kwa mama yule na akamkuta nje ya lango akiokota kuni; akamwambia, niletee maji na alipokuwa anakwenda kumletea maji akamwambia nakuomba uniletee kipande cha mkate mkononi mwako na hapa unaona akimjibu maneno tuliyosoma hapo juu. Sasa mimi sifundishi habari ya utoaji hapa ila nachotaka uone hapo ni kitu kile ambacho nimekuwa ninakufundisha hapo nyuma, kwamba ni lazima uwe na kitu ambacho Mungu akija kwako atakitumia kupitishia baraka  zake kwa ajili yako na kwa ajili ya kazi yake. Yule mama alikuwa na konzi moja ya unga ambayo ilitosha kwa mlo mmoja tu wa yeye na mwanaye pamoja na mafuta kidogo kwenye chupa ambayo yangetosha kutumika kupikia mkate ule na matumini yao yalikuwa baada ya mlo ule wangesubiri kufa tu maana hawakuwa na jinsi nyingine ya kuishi. Lakini hakujua anyezungumza naye amekuja na nini, ooooh! Alikuwa amekuja na Baraka zisizokwisha, zilikuwa zinatafuta mtu mwenye kitu na kwa kutumia kile alichokuwa nacho yule mama yaani konzi moja ya unga na mafuta kidogo kwenye chupa Baraka zikamiminika kwenye ile nyumba ya mama mjane! Hapakuwa na njaa kwenye ile nyumba mpaka mvua iliponyesha maana pipa la unga lilikuwa haliishi unga wala chupa ya mafuta haikwisha! Unga ukiisha kwenye pipa Mungu anajaza mafuta yakiisha kwenye chupa  Mungu anajaza! Ndiyo!! Kama vyombo vya kukingia Baraka vipo,Baraka zinamiminika tu wala hakuna mtu wa kuzuia! Wewe jipange tu! Ni kitu gani nataka uone hapo? Ni hiki, “mwenye kitu atapewa; na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile anadhaniwa kuwa nacho”.

Ngoja nikuambie mifano ya huku duniani kwa kukujengea ufahamu zaidi. Ni hivi, kwa wale wanaofahamu jinsi ya kupata mkopo kutoka bank au taasisi zinazohusika na ukopeshaji wanafahamu kuwa huwezi kwenda kwenye taasisi hizi kuomba mkopo mpaka uwe na kitu ambacho kwa hicho hawa jamaa watakuamini na kukupatia mkopo. Inawezekana ikawa ni nyumba, gari,kiwanja au mdhamini ambaye ana KITU ambacho kitawafanya hawa jamaa wakuamini na kukupatia mkopo. Nafikiri utakuwa umeelewa nini maana ya huo mstari unaosema “Mwenye kitu atapewa;na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile anachodhaniwa kuwa nacho”Ndiyo maana matajiri wanaendelea kuwa matajiri na masikini wamebaki kuwa masikini! Sasa angalia nukuu hii ambayo inatoka kwa mmoja wa watu ninaowakubali kwa kazi zao nzuri na huyu si mwingine bali ni Charles Kimei ambae ni mkurugenzi wa moja ya benki zenye mafanikio makubwa hapa nchini,naizungumzia benki ya CRDB na hapa nitoe shukrani kwa mtandao wa GK (gospel kitaa) ambao ndo nimeipata nukuu hii ambayo ndugu kimei aliitoa wakati wa misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Askofu wa dayosisi ya kaskazini ndugu Thomas Laizer. Kwa mujibu wa mtandao huo wa GK ndugu Kimei alisema hivi,” Askofu Laizer alikuwa ni mmoja wa wale watu, ambao sifa mojawapo ambayo mimi niliipenda na nimeiadmire, na ambayo ndio ilikuwa inaongoza sana dayosisi hii ni ya kuthubutu.

Alipokutana na mimi mara ya kwanza aliniambia kwamba, unafikiri nitafanya nini ili tuweza kukuza, kwanza kukuza ajira kwenye mkoa wetu na kwenye dayosisi yangu, na pili niweze kupata kitega uchumi ambacho kitasaidia dayosisi hii iweze kuwasaidia watu ambao wanahitaji, na zaidi ya hapo iweze pia kutekeleza shughuli za kimissioni ya dayosisi.

Nikamwambia Baba Askofu una nini? akasema usiniulize nina nini, mi nakuuliza wewe, utaweza kutusaidia? Nikamwambia, “lakini, unafirikiri mtu ukiwa na milioni moja, anaweza kuomba bilioni kumi?” Akaniambia anaweza, nikafurahi sana, nikajua huyu ni mtu ambaye ana think big.(mwisho wa kunukuu)

Sasa rudi kwenye somo ninalokufundisha,ndugu Kimei anasema mojawapo ya sifa aliyokuwa nayo Askofu Laizer ambayo yeye(Kimei) alikuwa anaipenda ni ile tabia yake ya kuthubutu. Nataka  nikuambie kwamba Mungu anapenda watu wanaothubutu,nitakuonyesha huko mbele habari ya Petro na utaelewa hapo anaposema kuthubutu. Lakini kitu kingine anasema alipokutana kwa mara ya kwanza na Baba Askofu na kisha Askofu alipomuuliza kuwa afanye nini kukuza ajira katika mkoa wake na katika dayosisi yake na pili aweze kupata kitega uchumi kitakachoweza kuwasaidia wahitaji na kusaidia huduma ya injili? Sasa angalia kitu ambacho ndugu Kimei alimjibu Askofu, anasema hivi,”Nikamwambia Baba Askofu UNA NINI? Linganisha jibu la ndugu Kimei na jibu la Nabii Elisha alilomjibu yule mama mjane aliyekuwa akihitaji msaada kwake(tumeshasoma mistari huko nyuma). Alimwambia yule mama hivi,” nikufanyie nini?  Niambie una kitu gani nyumbani?  Nimekwambia nakufundisha mifano rahisi ya huku duniani ili kukujengea ufahamu kuhusu hiki tunachojifunza. Kitu kingine anasema ,nikamwambia,”Lakini unafikiri mtu akiwa na milioni moja anaweza kuomba bilioni kumi?” kabla sijaeleza kwenye majibu ya Baba Askofu nataka tena utafakari hilo swali ambalo ndugu Kimei alimuuliza Baba Askofu.(rudia tena kutafakari,kwamba mtu akiwa na milioni moja anweza kuomba bilioni kumi?) unapata kitu hapo? Ni hivi, Yeyote mwenye KITU(milioni moja) atapewa………..(bilioni kumi)……..” (Mungu msaidie huyu tu aelewe hapa). Nasema hivi, ukiwa na chupa ya mafuta(milioni moja) halafu ukaitumia kumimina kwenye vyombo vingine vikajaa vyote utakuwa umetengeneza zaidi…….(bilioni kumi). Tukirudi kwenye majibu ya Askofu unaona akijibu swali la ndugu Kimei kwa kusema,”Anaweza”. Sasa mwisho ndugu Kimei baada ya kujibiwa na Baba askofu kwamba inawezekana mtu akiwa na milioni moja akaomba bilioni kumi,alisema,’ nikafurahi sana, nikajua huyu ni mtu ambaye ana think big.” Nini maana maana ya ku-think big? Ni kuona ufito wa mlozi ninamaanisha  kuona vema! Mungu alimuuliza Yeremia unaona nini? Yerermia akajibu naona ufito wa mlozi. Mungu akasema umeona vema.(soma Yeremia1:11-12). Huku ndiko ku-think big. Mungu anafurahi sana kuona watu wake wana-think big! ku-think big ni kuona nchi ya ahadi wakati mbele kuna bahari! Ku-think big ni kuona nchi ya ahadi hata kama mbele yako kuna majitu! Niishie hapo angalia jambo la tatu,

  3: Mwombe Mungu akufundishe kujua na kutumia kitu alichokiweka ndani mwako ili kikusaidie katika maisha yako lakini pia katika kazi yake (Mungu). Yule mama alikuwa na chupa ya mafuta lakini alikuwa hajui thamani yake mpaka alipokwenda kwa mtumishi wa Mungu na kusaidiwa. Muda wote alikuwa anaona ni kitu cha kawaida tu kisicho na thamani yoyote kumbe hakujua kuwa hicho ndicho kitakacho mkomboa. Kitu ni kilekile tukirudi kwa upande wako unayesoma ujumbe huu, una chupa ya mafuta (kipaji) lakini aidha hujui thamani yake au hujui kuitumia ili ikusaidie katika maisha yako! Ujumbe huu umekuja kwa makusudi ya kukufahamisha na kukusaidia ili uweze kujua!

4: Ukijua kitu ulichonacho na ukajua kukitumia kinachofuata ni Baraka kumiminika kupitia hicho kitu. Sasa angalia kilichotokea kwa yule mama, Baraka zilikuwa zinataka vyombo ili zimiminike humo lakini mama hakuwa navyo akaenda kuazima kwa majirani na pamoja na kukusanya vyombo vingi(maana aliambiwa asitake vichache) bado Baraka zilikuwa ni nyingi kuliko vyombo alivyokusanya, maandiko yanasema vyombo vilipokwisha mafuta (baraka) yakakoma! Unajua maana yake? Ukiwa na kitu na Mungu akakitumia hicho kitu kupitishia Baraka zake uwe na uhakika hizo Baraka zitakuwa ni nyingi mno na kwa hiyo ni lazima uwe na vyombo vingi kwa ajili ya kukingia Baraka hizo! (amen?) nimesha kufundisha juu ya vyombo au kapu huko nyuma na ninaamini unaelewa ninaposema vyombo ninamaanisha nini!

Angalia mfano mwingine katika kitabu cha 2 Wafalme 7:3-6

3 Basi walikuwapo watu wane wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, mbona tunakaa hapa hata tufe? 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vilevile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko,ili waende mpaka kituo cha washami; na walipofika mwanzo wa kituo cha Washami, kumbe! hapana mtu. 6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, tazama mfalme wa Israel amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. 7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao,na punda zao,  na kituo chao vilevile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao”. 

Hiki ndicho kitu alichokiongelea ndugu Kimei akimuelezea baba askofu Laizer kwamba katika sifa ambayo yeye alipenda kwa baba askofu ni kile kitendo cha kuthubutu. Hii ni habari inayohusu mji wa Samaria amabao ulikuwa umezungukwa na majeshi ya Shamu(Syria) na hapakuwa na nafasi tena ya kufanya kazi ya kutafuta riziki wala shughuli zozote za kimaendeleo zilizofanyika! Hapa naomba nizungumze na ndugu zangu watanzania mnaosoma ujumbe huu, nazungumzia amani ya nchi yetu ambayo kuna daalili za watu wachache kwa maslahi yao binafsi wanataka kuivuruga amani hii amabayo Mungu ametujalia. Ndugu zangu hii amani tuliyo nayo kuna mataifa wanaitamani sana, kuna nchi ambazo kila kukicha wanapigana na tunaona wakimbizi wakikimbilia kwetu kwa sababu kuna amani. Hivyo ni wajibu wetu kulinda amani hii isitoweke maana ikitoweka mambo yatakuwa kama kwenye habari hii ninayokwenda kuielezea hapa chini. Sikiliza! Amani ikitoweka huo uhuru wa kuabudu ulionao hautaupata tena, amani ikitoweka huo uhuru wa kuamka asubuhi na kwenda kwenye shughuli za kujitafutia riziki hautaupata, hiyo nafasi ya kukaa kijiweni na rafiki zako hutaipata! Nafasi ya kwenda shule mwanafunzi hutaipata, nafasi ya kwenda saloon dada hutaipata! Nafasi ya kwenda shambani ewe mkulima hutaipata! Matokeo yake tutakuwa watumwa katika nchi yetu maana tutapoteza uhuru huu tulio nao. Inawezekana kwa bahati ujumbe huu umekufikia ndugu yangu muislam, hapo ulipo nakuomba kumbuka jinsi tulivyokuwa tukiishi pamoja na kwa amani tangu nchi yetu imepata uhuru, hebu tusiiruhusu hali yoyote ile itutenge na kutufanya maadui! Tusiruhusu kutumiwa na watu wachache wanaotaka kututumia ili kwa maslahi yao sisi tuuane na wao watuuzie silaha! Usikubali kutumiwa na mtu yeyote, mtumikie Mungu wako! Ndugu zangu nikirudi kwenye huo ujumbe hapo juu ni kwamba baada ya majeshi ya Shamu kuuzunguka mji wa Samaria ilifuata dhiki ambayo ilisababisha watu kukosa chakula hata kufikia kula nyama ya punda na biblia inasema hata kibaba cha mavi ya njiwa kikapata kuuzwa kwa vipande vitano vya fedha, sikiliza hapo sijakosea kuandika inasema kibaba cha mavi ya njiwa siyo nyama ya njiwa! Haikutosha ilifika wakati vyakula vilikosekana watu wakaanza kula watoto wao waliowazaa (inasikitisha sana!). tuombe Mungu tusijefikia mahali hapa. Katikati ya dhiki waliyokuwa nayo watu wa Samaria Mtu wa mungu Elisha akatangaza habari njema kwamba, “kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli,na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. Sasa angalia hiyo mistari tuliyosoma hapo juu kuhusu wale watu wanne wenye ukoma, nilikwambia pale nyuma kuwa matatizo hayatatuliwi kwa wewe kuendelea kukaa kwenye tatizo na kulalamika juu ya hayo matatizo, bali matatizo yanatatuliwa kwa wewe kuamua kuchukua hatua ya kutatua tatizo. Ngoja nikwambie kitu hiki labda utanielewa, ni hivi Mungu anapenda watu wanaojaribu mambo!(wanaothubutu) Usichanganyikiwe!! Maana naona unajiuliza kivipi? Soma mistari hii ifuatayo utaelewa:- 28 Petro akamjibu akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.

29 Akasema njoo. Petro akashuka chomboni akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe………” (Mathayo 14:28-31)

Hii ni habari ya Bwana Yesu alipomaliza kufanya muujiza wa kulisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili na baada ya kumaliza aliwaamuru wanafunzi wake wapande mashuani watangulie kuvuka ng’ambo wakati yeye anaagana na watu. Baada ya kuagana na watu alikwenda mlimani kuomba na wakati huo wanafunzi wake walikuwa wameshafika katikati ya bahari. Biblia inasema wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea akienda kwa miguu juu ya bahari na wanafunzi walipomuona wakaogopa wakidhani wanaona kivuli (mzimu). Yesu akawaambia jipeni moyo ni mimi msiogope, na hapa sasa ndio tunakutana na  maneno ya Petro akimwambia Yesu, Bwana IKIWA NI WEWE niamuru nije kwako juu ya maji!(huu ni ujasiri wa ajabu) Unajua kwa maneno mengine Petro alikuwa anasema Bwana mimi siamini kama ni wewe na nitaamini kuwa ni wewe pale utakaponiamuru nije kwako nikitembea juu ya maji! Wengine mkiambiwa kitu hata bila kupima mnakubali tu kwa sababu aliyesema ni mheshimiwa nabii au dk. Mchungaji na majina mengine mengi unayajua wanavyojiita. Sasa bila ya kupima unameza tu matokeo yake wengine wamejikuta wamemeza mawe! (pole sana). Sikiliza petro hakukubali kirahisi wale wanafunzi wengine walikubali kirahisi lakini yeye akasema  ikiwa ni wewe…..! Bwana alimwambia petro njoo! Ninakwambia petro hakusubiri ushauri wowote ingawa hakuwahi kuona mtu anatembea juu ya maji hata siku moja haikumsumbua akashuka akaanza kutembea juu ya maji! Nilikwambia hapo nyuma kuwa ili uweze kutumiwa na Mungu ni lazima uwe na kitu ambacho kitamvuta Mungu kukusaidia au kukutumia na sasa nataka nikwambie kuwa mojawapo ya vitu vilivyofanya petro akafanywa kuwa jiwe (mwamba) ni hiki tulichokisoma hapa(kuthubutu). Kaangalie kwenye maandiko kama kulikuwa na mwanafunzi mdadisi na mwenye maswali mengi kama petro. Walipoulizwa wao wanamuona yesu kama nani wenzake walikaa kimya lakini yeye akasema wewe ni masihi mwana wa Mungu aliye hai! Mahali pengine aliwahi kumuuliza bwana sisi tumeacha vyote tukakufuata, tutapata nini? Wakati Yesu amekaa nao kwenye chakula cha mwisho aliwaambia juu ya mtu atakayemsaliti lakini Petro yeye alisimama akasema yeye yupo tayari kufungwa na hata kuuawa pamoja na Bwana na kama haitoshi ni yeye alimkata mtu sikio wakati yesu alipokuja kukamatwa! Kwa nini asifanywe mwamba? Ngoja nirudi kwenye somo letu, nimekwambia kuwa Mungu anapenda watu wanaojaribu mambo kwa hiyo ingawa Petro hakutembea sana kwenye maji kwa kuogopa kuzama lakini kitendo cha kuthubutu kuchukua hatua na kumwendea Bwana juu ya maji kilikuwa kitendo cha kijasiri ambacho wenzake hawakuthubutu kujaribu! Sasa ukirudi kwa wale wakoma wanne kama nilivyokwambia matatizo hayatatuliwi kwa mtu kuendelea kukaa kwenye hilo tatizo bali yanatatuliwa kwa mtu kuchukua(kuthubutu) hatua za kushughulika na hilo tatizo, wale jamaa wakaanza kuambiana,Mbona tunakaa hapa hata tufe? Wakasema tukikaa hapa tutakufa na tukisema tuingie mjini, mjini mna njaa huko nako tutakufa! Napenda sana jinsi hawa jamaa walivyojadiliana na ninataka nikwambie kitu wewe unaesoma ujumbe huu kwamba inawezekana plan A imekataa isikupe shida na kukukatisha tamaa tafuta plan B, wale jamaa wakasema ni bora tuakaliendee jeshi la washami kama wakituua na watuue lakini haiwezekani tukakaa hapa na kufa na njaa huku tunaona ,ooooh! Ninakwambia kumbe Mungu alikuwa anasubiri wafanye KWA UPANDE WAO kisha na yeye afanye kwa upande wake,alikuwa anasubiri wathubutu na ninakwambia wale jamaa walipoanza tu kuchukua(kuthubutu) hatua za kuondoka mahali pale (kwenye tatizo) biblia inasema, “Bwana aliwasikizisha washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa wakaanza kukimbia ili wajiponye nafsi zao”. (haleluyaaaaa!!) kumbe wakati wale wakoma wanatembea kuondoka zile hatua zao Mungu akazifanya zisikike kama kishindo cha jeshi kubwa kiasi majeshi ya adui yakaogopa na kukimbia!!( unaweza   kumpigia bwana makofi hapo ulipo!). Wewe uliyekaa kwenye tatizo kwa muda mrefu na kubaki unalalmika Bwana amekuona na ameleta ujumbe huu kwako inuka kama walivyofanya wakoma wale wanne, chukua hatua kwa upande wako na Mungu atafanya kwa upande wake!!

Ni upande wa Yesu kumfufua Lazaro lakini kazi ya kuondoa jiwe na kumfungua sanda aende zake ni upande wetu sisi kufanya! KWASABABU MAMBO HAYAJILETI YENYEWE BALI YANASABABISHWA KUTOKEA!

Tafakari tunapomaliza kujifunza somo hili, BWANA na akuongeze zaidi unapoendelea kujifunza! Mungu akubariki kumbuka kuniombea ili niweze kutumika sawasawa na wito alioweka Mungu ndani yangu!         Na usisahau kwamba,       50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni,kwamba mtu  Akile asife”

–Mwal. Alfred T. Katuma.

                           

Tugeuzwe nia Zetu!

nia

Kugeuzwa nia ni jambo endelevu na la kujizoeza; lakini haliwezekani bila mhusika kuamua kwa dhati. Ni jambo linalotaka maamuzi sahihi na thabiti. Kugeuzwa nia; A) ni utakaso wa mwili mbali na uchafu (makosa, hila, ila, maovu) na tamaa mbaya zote, B) ni kutakaswa mawazo na utu/nia wa/ya ndani ili kuwa na dhamiri njema siku zote mbele za Mungu na wanadamu  C) ni kujidhiri ili Mungu akukweze, (fanya yaliyo kinyume na elimu na uchumi wako kwa ajili ya Kristo) D) ni kutengeneza njia na kauli zako ili uyale mema ambayo ni tunda la ulimi wako, E) ni kumwamini Mungu pacpo mashaka wala hofu hata km akili/hali/mazingira havikubali. F) ni kujisimamia na kukisimamia kile ulichoamini na kuendelea kukiri moyoni na hadharani pacpo mashaka maana hofu na mashaka vina adhabu na kutokumwamini Mungu kuna adhabu pia tena kubwa.

Kwa ujumla kugeuzwa upya nia ya roho sio njia rahisi, ina maumivu na mateso. Lakini kwa kuwa aliyetuita hakutuitia raha za dunia ambazo ni za muda mfupi bali za milele ambazo zimehifadhiwa juu ambako nondo wala kutu havigusi, na wala hakusema kuwa hatutateswa ni vema kuamua kumfuata ipasavyo. Nia ya roho ya mtu isipogeuzwa, wokovu wake ni sawa na ubatili na kujilisha upepo. kwanini? jibu lake ni rahisi…“itakufaa nini kuupata ulimwengu wote na kupoteza nafsi yako milele? Kumpokea Yesu ni hiari (mtu halazimishwi) lakini ukishakuwa wake huna hiyari tena ila kufuata nyayo zake kikamilifu. Iko NEEMA ya kukuwezesha, haiji yenyewe bali yampasa mtu kukiendea kiti cha rehema cha Kristo ili akupe NEEMA hiyo. Geuzwa Nia!

Mtu asipogeuzwa nia ya roho yake ni hakika kuyatenda mapenzi ya Mungu kwa mtu huyu ni ngumu sababu dunia na mambo yake na tamaa zake vinaimba wimbo wa kutoitii sheria ya Mungu ndani ya mtu huyu bila kutaka atautii wimbo huo, kwa hiyo si rahisi kuwatumikia mabwana wawili. Lazima mtu huyu ataambatana zaidi na yule anayemuona (dunia, anasa, tamaa ya mali na mwili, kiburi cha uzima, majivuno, dharau, masengenyo, masimango, wivu, husuda, mizaha, kejeri, uzinifu na uasherati, uongo, uchoyo, uuaji wa mwili na roho, mawazo na nia mbaya, unafiki, kutosamehe, kutoachilia, uchungu, hila na ndugu zao) kuliko Yesu ambaye anaonekana kwa Imani.

Namshauri kila mmoja wetu, pamoja na u-busy ulio nao, popote ulipo na kila ufanyalo,
jizoeshe kumwambia Mungu hivi;
1. UKINIGEUZA NITAGEUKA. (na ndani yako iwepo nia ya kugeuka ugeuzwapo/ukunjwapo na Neno)
2.NIVUTE KWAKO NIWE WAKO MILELE(sababu dunia nayo inavuta sana kuelekea kwake so lazima ukubali kumilikiwa na BWANA Yesu)
3. NICHUNGUZE EE BWANA NA UNITAKASE MOYO, MWILI NA NAFSI YANGU.
4. NILINDE NA NJIA MBAYA NA NIEPUSHE NA MARAFIKI WAOVU KWA GHARAMA  YOYOTE
( na uwe tayari hayo yanapokujia kwani maranyingi hatuko tayari kutengwa na rafiki zetu ht km ni waovu so stm Mungu hutumia vituko km dhuluma, magomvi etc kututenga nao) Maombi haya ni ya kila mtu lakini yana matokeo ya wazi kwa mtu aliyeamua kugeuzwa nia ya roho yake kwa kumaanisha.

Kwa jinsi hii, kuna kila sababu ya kukubali binafsi kugeuzwa roho za nia zetu ili tuvikwe utu mpya na kwa ujumla wake ni kujifunza kwa bidii na gharama kubwa (km Yesu wetu) kuwa WANYENYEKEVU na WATIIFU bila kujali gharama hizo.
 

NAWAPENDA KWA KUWA KRISTO ALIAGIZA UPENDO.

Gladys!

Sio miaka yako bali siku zako!!

hesabu

Wapendwa SG,Nina neno nanyi ,nalo ni hili

SIO MIAKA YAKO BALI NI SIKU ZAKO

“Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima”. Zaburi 90:12

Kumbe kuna kupata hekima katika kuzihesabu siku zako. Unapenda kupata hekima hiyo hebu fuatana nami ktk maneno haya.

Wengi wetu kwenye group hii tumekwisha ishi siku elfu kumi na.. na tumebakiza siku elfu kumi na… Mungu anataka uhesabu siku zako, sio miaka yako!!

Kwanini? Kwa sababu ukihesabu miaka unaweza kuona miiingi kumbe ukiibadilisha kuwa siku …… ni kidogo tu. Hebu mchukulie mpendwa aliyeokoka/zaliwa miaka 40 iliyopita, anaweza kujiona kuwa ni wa zamaaani, kumbe hata siku elfu kumi na tano hana (ana siku 14,600 tuu). Kumbuka hata Mungu mwenyewe

anatambulishwa kama Mzee wa siku (Daniel 7:9,13&22).

Zaburi 90:10 inaonyesha wastani wa miaka ya mtu ni 80 sawa na siku elfu 29,200 (tufanye siku 30,000). Sasa hebu chukua miaka 80 toa miaka uliyoishi, umebaki na miaka mingapi? Je, 45, 50, 55 au 60? Mpendwa hiyo miaka iliyobaki unajua ni siku elfu kumi naa ..tu, ikizidi sana siku elfu ishirini?

Now, here comes the crucial question – Je, huoni kuwa hizo siku elfu kumi naa….zilizobaki ni chache? Shetani anafahamu muda aliyo nao ni mchache,

I guess huwa anahesabu siku! Wewe je, uko tayari kubadilisha mtazamo wako, hesabu siku zako how serious you are with the elfu kumi naaa days left? Jana imepita,

leo nayo hiyooo inapita ivi hivi tu?

How many days from your elfu kumi naa days left utakuwa –effective ktk utumishi wako. Biblia inaziita kabla hazijaja siku zilizo mbaya (Mhubiri 12:1).

Please take heed, kila siku ni ya maana sana, itumie vema usiiche iende zake hasa ukizingatia foleni za mjini zilivyo na ubize wake hapo napo ni mtihani wa visingizio.

Mpendwa Zipange, don’t lose easily any day, do something, say something worth it, significant  - NANUKUU “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.” – EFESO 5:15-16.     GET IT?

Stay Protected,

Mathew.

 

 

Jiweke sawa katika utumishi wako 2013!!

pastor

MUNGU ANAPOKUMBUKA

Naomba sasa tufunguwe kwa pamoja katika kitabu cha Isaya 43:26, Biblia inasema “Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako”.

Mstari tuliousoma unaonyesha kana kwamba kuna tatizo katika kumbukumbu ya Mungu ndiyo maana anahitaji akumbushwe. Labda utaniuliza kwani huyo anayesema unikumbushe ni Mungu? Je, unaweza kuthibitisha kuwa ni Mungu? Ukisoma kuanzia mstari wa kumi na tano wa sura hii utaona kuwa anayesema maneno haya ni Mungu mwenyewe.

Kabla sijaendelea na kuuchambua mstari huu, naomba turudi kwenye ujumbe wa somo letu; MUNGU ANAPOKUMBUKA. Mpendwa, Mungu anapokumbuka ni lazima kitu cha tofauti kitokee, jambo la tofauti litokee, matumaini yarejeshwe, Baraka zimiminike, ushindi upatikane ….. kwa sababu Mungu amekumbuka. Wakati huu ulionao tamani sana Mungu akukumbuke, maana mambo hubadilika sana Mungu anapomkumbuka mtu, maombi hujibiwa na muujiza hutokea.

Hebu utuangalie baadhi ya mifano katika Biblia inayoonesha Mungu alipokumbuka nini kilitokea……. Alipomkumbuka Nuhu (nyakati zile za gharika – Mwanzo 8:1) alivumisha upepo na Nuhu, mkewe, wanawe na wakwe zake pamoja na kila chenye uhai wakatoka katika safina. KUTOKA KWA NUHU KATIKA SAFINA KULIHITAJI MUNGU AKUMBUKE!

Alipomkumbumbuka Ibrahimu (wakati wa Sodoma na Gomora), Mungu alimtoa Lutu asiangamie katika miji ile (Mwazo 19:29). Kumbe Lutu aliepuka kuangamia baada ya Mungu kumkumbuka Ibrahimu.

Alipolikumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu, Isaka na Yakobo, aliwatoa wana wa Israel katika utumwa wa Msri (Kutoka 2:24 na 6:5).  Bwana alipomkumbuka Hanna, mwanamke huyu aliyeonekana hawezi kuzaa alichukuwa mimba akamzaa mwana akamwita Samwel (1Samwel 1:11, 19-20).

Mungu alipokumbuka sadaka na maombi ya Kornelio alimtuma Petro ili kupeleka wokovu kwa Mataifa. Kumbuka kuwa Petro alikuwa ni  muumini mkubwa wa uyahudi asiyetaka kuchamana na mataifa (Matendo 10:4), Dorkasi anafufuliwa kwa sababu ya kumbukumbu ya kuwahudumia wajane (Matendo 9:36-39) na kupitia kufufuliwa huko watu wengi wakamwamini Yesu katika mji wa Yafa.

Najua kuna watu wengi sana ambao Mungu aliwakumbuka kisha jambo la tofauti likatokea katika maisha yao. Lakini naomba nimalizie ujumbe wangu kwa kuwaelezea watu wawili ambao Mungu aliwakumbuka. Pia nitakuwa najibu swali nililoulizwa mwanzo mwa ujumbe wangu,

Hata hivyo napenda uzingatie hiki KUMBE MUNGU AKIKUMBUKA KUNA KITU CHA TOFAUTI HUTOKEA. Haijalishi uko katika hali gani inayokatisha tamaa, usihangaike mpendwa mfanye Mungu akukumbuke. Hebu tuangalie mifano ya watu hao wawili. Mmoja kutoka Agano la Kale na wa pili kutoka Agano jipya.

Ukisoma katika Kitabu cha Isaya 48:1 – 8, utaona habari ya mfalme Hezekia, ambaye muda wake wa kuishi katika dunia hii ulikuwa umefikia mwisho. Nabii wa wakati huo, Isaya alitumwa kupeleka habari kuwaatengeneze mambo ya nyumba yake maana HAKIKA ATAKUFA – Mstari wa 1. Hezekia hakuanza kupishana na Nabii Isaya. Badala yake aligeukia ukutani  akamwomba Mungu.

Hebu angalia vizuri mstari ule wa 3, “akasema, Ee Bwana, KUMBUKA HAYA, nakusihi,,,,,,,,,,”, Hezekia hakulalamika bali alimkumbusha Mungu yale aliyoyatenda katika kipindi cha ufalme wake. Kama ungependa kujua alichokifanya mfalme Hezekia,  kwa wakati wako soma 2Wafalme 18:1 – 7. Kwa sababu alijua amemfanyia nini Bwana alikuwa na ujasiri wa kumwambia Bwana KUMBUKA.

Sote tunajua kuwa unabii ambao ulinenwa kwa Hezekia kuwa HAKIKA ATAKUFA ulibatilishwa, Hezekia akaongezea miaka 15 na ishara ikafanywa, kwa sabu Mungu amemkumbuka mtumishi wake Hezekia.

KUUUMBE, Mambo tunayoyafanya kwa ajili ya Bwana ni hazina!!! Na kwa hayo unaweza kuyatumia Kumkumbusha Bwana! Kumbe Mungu hana tatizo la kumbukumbu isipokuwa anataka uhojiane naye (u-present case yako) umweleze mambo uliyoyafanya kwa ajili ya utukufu wa jina lake, utoe sababu ya kupata/kuongezewa hicho unachokitaka … Mpendwa hebu jihoji mwenye, je, unacho cha kumwambia Mungu akumbuke ambacho umekifanya kwa ajili yake na kwa utukufu wake? Ulikifanyaje?

Mpendwa naomba uliangalie tukio la Hezekia kwa utazamo huu, Hezekia alipokuwa mfalme,,, Mungu alimtarajia afanye mambo kadha wa kadha, Hezekia katika nafasi yake alifanya mambo mengi kwa ajili ya Mungu. Tatizo lilipokuja katika maisha yake na likaonekana kuwa ni lazima aondoke na mjumbe akatumwa kwake, Hezekia ali-appeal kwa kutumia mambo aliyomfanyia Bwana. Hakupeleka hoja kuwa Mungu give me another chance, this time ninaahidi nitafanya moja mbili tatu. Bali yeye alimtaka Mungu wake akumbuke yale aliyoyafanya.

Sasa naomba ujihoji mpendwa katika nafasi uliyopo/uliyonayo kuna mambo yo yote unayoyafanya kwa ajili ya Bwana ili jina lake litukuzwe. Ama unasubiri ukibanwa na shida/adha/majaribu ya kutisha ndipo umuahidi Mungu utakayoyafanya.katika mwili wa Kristo je umefanya nini kwa ajili ya Bwana?

Mtu wa pili ambaye ningependa tuangalie habari zake ni yule mwizi msalabani ambaye alisulubiwa pamoja na Bwana wetu Yesu (Luka 23:39 – 43). Biblia inaonyesha kuwa Bwana Yesu aliposulubiwa wezi wawili walisulubiwa pamoja naye. Mwizi aliyekuwa upande mmoja alianza kumdhihaki Bwana Yesu. Ndipo yule mwizi aliyekuwa upande mwinge akamkemea na kumdhibiti kabisa mwizi mwenzie. Ni rahisi kwa mwizi kumdhibiti mwizi mwenzie.  Baada ya kuhakikisha kuwa umemdhibiti mwizi mwenzake alimgeukia Bwana Yesu na kumwambia ….”Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako”. (mstari wa  42).

Mwizi huyu alipofanya kazi ya kumkemea na kumnyamazisha mwizi mwenziwe, alipata kisemeo  mbele za Bwana na kuleta hoja ya kukumbukwa. Alipomfanyia Mungu kazi aliomba akumbukwe. Na bila kuchelewa Yesu alimwambia hivi …….“leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”. (mstari 43).

Watu wote niliyowataja hapo juu wanafanana kwa kitu kimoja walikifanya jambo kwa ajili ya Mungu ndipo Mungu akawakumbuka. Hata (mfalme Hezekia na mwizi msalabani)  mmoja katika nafasi ya mfalme na mwingine akiwa msalabani, walifanya kitu mbele za Mungu na kuomba Mungu awakumbuke. ELEWA HIVI hali uliyonayo (iwe ikulu au msalabani) sio kigezo cha kushindwa kufanya kazi ya Mungu ili jina lake litukuzwe!!!

Sasa naomba nimalizie ujumbe huu kwa kusema maneno haya; lengo la ujumbe huu nilitaka kumtia moyo mtu ambaye anamfanyia Mungu kazi katika eneo lo lote alipo, kuwa kazi yako si bure. Biblia inasema “………mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.” – 1Korintho 15:58.

Kama taabu yetu si bure basi ina malipo/ujira. Bwana wetu anasema … “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” – Ufunuo 22:12. Swali ni kwamba, Je, kazi unayoifanya inastahili malipo, inakidhi viwango vya mbinguni? Mungu akikuangalia anaona unafanya kazi yake kwa ajili yake? Hebu angalia unapofanya kazi ya Mungu unafanyaje. Je, unatimiza wajibu, unafanya kwa mazoea, kwa manung’uniko, malalamiko, kwanini nyingi  na masikitiko kadha wa kadha. BASI WAPENDWA TUJIANGALIE SANA TUNAVYOFANYA UTUMISHI WETU MBELE ZAKE……………. MUNGU YUPO TAYARI KUTUKUMBUKA.

Hivyo unapojiandaa kuupokea mwaka 2013, jiweke sawa katika utumishi wako, ili uwe ni mwaka wa kuweka akiba/hazina ya utumishi mbele za Mungu aliye tayari kukumbuka yote uliyoyafanya kwa ajili yake na kubadilisha hali yako. Kazi kwako mtumishi wa Mungu.

Mshirika mpya SG.

Mathew.

Huruma isiyo ya kawaida, Wema unaopita akili zetu, Rehema na Neema za ajabu, Vyote ni vya Mungu wetu!!

seleli

Jamani Mungu ana huruma, wema,neema,rehema,upendo sana,sana..rest assured, ukitafakari unaweza anza kulia tu hata kama ni mwanaume na haijalishi uwe ofisini,maombini, unaendesha gari,umelala,unatembea, unapika,unasoma, unalima huko village, uko bafuni unakoga, unaweza piga magoti huko huko hata haisumbui, maji ya mvua uyayokoga yanapoendelea kukumiminikia, unaweza anza kububujika na machozi ya furaha na kunena mara tu ukumbukapo wema na huruma za Mungu wetu , oooh! hata niandikapo sasa, nasikia mambo yanabadilika hapa, raha,furaha,uwepo na Roho Mt mwingi, nasikia vitu vinatekenya-tekenya kuleeee ndaniii… chumba cha ndani, allleluya… I love u so much Jesus my master, thank you so much God..my lovely dad jamani..love u dad and I worship u amen.

Maandiko:

Mwanzo. 19:12-25…..Malaika wa Bwana wanamsaidia hata kumshika mkono Lutu na wanae na mkewe ili kuwachangamsha watoroke haraka kabla ya moto kuangamiza,walimwambia afanye haraka haraka tena awatoe nje ya mji yeyote anayehusiana lakini ikawa kama anazubaaa ivi ikabidi malaika wawasaidie kufanya fasta kuchanja mbuga, jamani Mungu anahuruma..

Isaya 49:14-16…Mwanamke aliyezaa mwana inafahamika duniani kua ndiye mwenye huruma na upendo kuliko wote kwa mtoto hata inafahamika uchungu wa mwana aujua mzazi, mwanamke anaweza fanya lolote ili tu kumtetea mwana wa tumbo lake,atalala njaa,atauza vitumbua,matembele,atafukuzwa na mume, ataambiwa atoe mimba ili mapenzi yaendelee but yuko tayari kukosa yote kwa ajli ya mwanae,anaweza ingia ndani ya nyumba inawaka moto usio na ajizi kumuokoa mwanae kisha akatoka nae mtoto amemkumbatia akiwa mzima but yeye sura imeharibika beyond repair kwa kuunguzwa yet Mungu anasema kuna wakati mama huyo mzuri aweza kusahau huruma kwa mtoto wake mwenyewe na kutupilia mbali kule care yake kwa mwanae but si Mungu wetu…oooh my God, our God is indeed very unique jamani

Yona 4:1-11Mungu anahurumia mpaka ng’ombe,punda,pusi,farasi,kondoo,mbuzi, mbali na watu…jamani… can u imagine Mungu ana-care mpaka idadi kubwa ya mifugo na dog,kuku wakiwemo? angalia mstari wa 11.. Acheni Mungu aitwe Mungu

Yohana 13:1 na 15:13-14 Napenda tafsiri ya New King James ktk 13: 1 inasema ”He loved them to the end. wow!  yaani aliwapenda mpaka mwisho hahahaha alleluya..iyo tamu na ina nguvu sana na pia ktk 15:13….mtu anakupenda mpaka anayatoa maisha yake for u…sasa mtu akishakupenda mpaka mwisho na akakupenda mpaka kuhesabu uhai wake si kitu ili wewe na wewe tupone..jamani amebakiza nini sasa? nasikia machozi…anastahili mwokozi kupewa sifa na adhama na utukufu na hesima na kuabududiwa na shukurani...i love u so much Jesus

Mdo 9: 1-16 Mtu siku za nyuma kadhaa alikua anaua watu, sumbua kanisa,chinja wapendwa, vuruga-vuruga watu.kosesha raha wana wa Mungu eti ghafla mtu huyo huyo ambaye  ningekua mie ningeagiza malaika mmoja tu very junior kule juu aje kumchilia mbali kule msumbufu wa kanisa yule but ndio kwanza Yesu mzima zima anamtokea na kumpa  special task na title njema sana..tena anamu-address lovely positive..angalia mstari wa 15...da! Mungu huyu acheni tu…jamaa korofi ivyo na limetusumbua juzi tu Mdo 8:3 ndilo hilo  Mungu anali-pick na kulipa big huduma. yaani sina la kusema Mungu wetu bali uishi milele mfalme wetu mkuu.

Mdo 8:26-40 na 10: 1-48  Mungu mpaka ana-create plan ya kumuokoa/kumrehemu mtu, inabidi malaika atumwe kuongea na Philipo, then Roho Mt ana-direct step by step raketi..mdo. 8:29  then Philipo anakua nae  shap pia mstari wa 30-35, na pia Kornelio  akiwa hajaookoka but utoaji na maombi yake yalifanyika kumbukumbu mbinguniImagine Philipo baada ya mission kua accomplished akapata lift ya mbinguni mstari wa 39-40..imagine Kornelio is not saved but alikua mtoaji na muomba Mungu kila siku yaani raketi zote izi Mungu anaangaika ili awarehemu Kornelio na Mwafrika from Ethiopia

Wafilipi 2:5-11  Mtu yu namna ya Mungu,aliyekuwepo toka mwanzo, mwenye utukufu wa kutisha, mwenye mamlaka na enzi but yote hayo unayaweka kando kwanza then unakubali kuwa kama viumbe ulivyoviumba mwenyewe,kiushi nao miaka 30 ukiuza mpaka viti na meza za baba yako duniani, eti yote hayo ya kujishusha, kutojali spiritual personality yako unayafanya kwa ajli yetu tena tukiwa hatuna habari tunadunda tu na dhambi zetu huko mpaka baadae ndio tena Mungu akatuvuta tukaja kwako tukaokoka..taabu yote hiyo ya nini? kuacha enzi na mamlaka na kuja kudhalilishwa na viumbe hawa hawana adabu duniani!!!!!!!! jamani Yesu nakupenda sana,sana sijui nifanyeje mie ujue nakupenda mpenzi wa roho yangu?

Je unalo andiko/maandiko mengine ya kuonyesha huruma, rehema,neema,wema wa MUNGU, karibu utupie hapa,amen.

Amani ya Bwana Mungu iwe nanyi nyote amen.

Edwin Seleli

Neema ya Mungu inavyo okoa

ushuhuda

Bwana Yesu asifiwe wapendwa,

Napenda kuwashirikisha ushuhuda huu ambao dada mmoja aliutoa Kanisani leo Jumapili tarehe 9/9/2012 wakati akimshukuru Mungu kwa mtoto wake wa kiume kutimiza miaka mitano ya kuzaliwa.

Mama huyu alipata ujauzito wa mtoto huyu wakati akiwa katika maisha ya ukahaba na ulevi wa kutisha sana. Mama mkwe, yaani mama wa bwana aliyempa ujauzito alipofahamu ya kuwa dada huyu alikuwa na mimba ya kijana wake alimkabili na kumwambia alikuwa hataki kabisa kijana wake azae na yeye. Hakutaka kabisa awe na mjukuu ambaye mama yake anaishi maisha machafu na ya ulevi wa hali ya juu. Hivyo akamtaka aitoe ile mimba.

Dada huyu baada ya kuambiwa hivyo na mkwewe hakuona sababu ya kuendelea kutunza mimba isiyotakiwa na wenyewe, akakubaliana nafsini mwake kwenda kuitoa mimba ile. Lakini kabla hajaenda kuitoa, nafsini mwake ikazuka hoja ya pili. Akatafakari umri wake ulikuwa ni miaka 28, akawaza iwapo ataitoa ile mimba ni lini atakuja kuzaa? Au aishi bila mtoto maisha yake yote? Akaona hapana, hata kama mtoto huyo kwao hatakiwi, lakini yeye anamhitaji.

Hivyo akaitunza ile mimba na hatimaye akajifungua mtoto wa kiume.

Yule mtoto alipozaliwa akaanza kusumbuliwa na magonjwa yasiyoisha, ya mfululizo. Hata alipofika miezi tisa hali yake ilishakuwa mbaya sana, akiwa ni mdhaifu na aliyenyongea, hafanani hata kidogo na umri aliokuwa nao. Mama huyu akasimulia jinsi ambavyo alipokuwa akimnyonyesha mtoto wake anapaliwa, maziwa yanaingia njia ya hewa, hali mabayo inatengeneza nimonia na kumfanya awe katika hali kama ya kuelekea kupoteza uhai. Alipokuwa akifikishwa wodini mama huyu analia kwa kuomboleza katika hali ya kukata tamaa. Nimonia, malaria na magonjwa mengi mengine yakawa yameufanya mwili wa mtoto yule kuwa ndio nyumbani kwao.

Hali hii ilikuwa ikijirudia kwa namna nyingi mbalimbali, huku mama huyu akizunguka huku na huku kutafuta tiba, ikiwemo kwa waganga na kila hospitali ambayo aliimudu, hatimaye akagundua hakuna sehemu iliyobakia ya  kuweza kumsaidia. Ndipo alipoamua kumpeleka mtoto wake kwenye Kanisa linaloamini wokovu ili aombewe pengine angepata nafuu.

Siku ya kwanza alipompeleka mtoto huyu Kanisani alikwenda hali akiwa amekunywa pombe nyingi na kulewa. Mchungaji wa Kanisa lile alipomwona na kumsikiliza mara moja alitambua kuwa yule dada alikuwa katika ulevi mwingi. Hakufanya maombi kwa mtoto yule, bali alimshauri huyu dada siku akiamua kumleta tena mwanae ilio aombewe basi ahakikishe hanywi pombe kabisa siku hiyo. Aende kanisani pale bila kuwa amelewa. Yule dada akaondoka na mtoto wake.

Baada ye siku chache huku hali ya yule mtoto ikiendelea kuzorota, dada yule akampeleka tena pale Kanisani huku safari hii akiwa hajanywa pombe. Alipofika yule Mchungaji akampokea vizuri na kuanza kumwombea mtoto wake ili afunguliwe na kifungo kile cha magonjwa. Wakati maombi yakiendelea, mtoto yule wa miezi tisa alipiga ukelele mkali sana, huku akirusha haja ndogo kwa kasi. Baada ya muda alinyamaza, Mchungaji akamaliza maombi yake na kumruhusu yule mama kuondoka na mtoto wake.

Tangu siku hiyo hali ya mtoto ile ikaanza kuimarika. Yale magonjwa ambayo hayakuwahi kukoma tangu alipozaliwa yakakoma na kumwacha yule mtoto. Akaanza kupata afya na kukua kama watoto wengine wazima wanavyokuwa.

Dada huyu baada ya kuona mambo ambayo Bwana Yesu amemtendea mtoto wake akaamua kubadilika. Akaamua kuendelea kusali katika Kanisa lile ili awe karibu na Mchungaji aliyemwombea mtoto wake ili azidi kumwombea. Taratibu hali ya ulevi ikamtoka dada huyu kutokana na mafundisho aliyokuwa akipata pale Kanisani, na hatimaye akaamua kuokoka na kumpokea Yesu Kristo ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yake.

Tangu hapo hali ya maisha ya wokovu ya dada huyu imeimarika sana sana, na leo hii yapata mwaka wa nne katika wokovu, anamtumikia Mungu kwa namna ya pekee na ya kujitoa kwa hali ya juu sana kwa ajili ya kumtumikia Mungu, huku akiwa ni mwombaji mkubwa. Hamu yake kubwa ni kufika mbinguni baada ya maisha ya ushindi hapa duniani.

Hakika ushuhuda huu umenigusa sana. Inaonyesha ni jinsi gani kanisa la Mungu linapaswa kujiandaa kutoa majibu ambayo wanadamu hawawezi kuyapata mahali pengine popote, ili Bwana Yesu atukuzwe na ajulikane ndiye Mungu wa pekee wa kweli. Iwapo mama huyu asingepata majibu ya shida za mtoto wake asingebaki Kanisani pale na hatimaye kuokolewa. Ni dhahiri angerudi kuendelea kuhangaika wa waganga, na pengine maisha yangezidi kuharibika na kumpelekea kuangamia.

Hii ni mojawapo kati ya njia nyingi sana ambazo Bwana Yesu huzitumia ili kuwaokoa watu wengi, hasa wale walioshindikana kwa njia za mahubiri ya kawaida.

Ombi langu na ujumbe wangu kwa Kanisa la Mungu ni kuwa tuendelee kufanya juhudi kubwa kuutafuta uso wa Mungu.Kanisa liwe ni mahali pa makimbilio. Watu wote wafahamu ya kuwa hakuna uzima, usalama wala amani nje ya Kanisa la Mungu.

Wanapokimbilia kwetu watukute tupo tayari kuwapatia majibu, kuwahubiria, kuwafundisha na kuwaelekeza. Kanisa la Bwana litaongezeka, roho nyingi sana zitaokolewa, na wokovu wa watu hawa utajengwa katika misingi imara sana ya shuhuda za jinsi Mungu alivyowatoa katika hali mbaya, yaani wao wenyewe wanakuwa ni mashahidi wa nafsi zao ya kwamba Bwana Yesu anaishi milele, na anahusika moja kwa moja na maisha yao.

Bwana Yesu anatufundisha kupitia neno lake ya kuwa, mtu anayesamehewa sana hupenda sana, anayesamehewa kidogo, hupenda kidogo.

Tutafakari Adiko hili:

Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi? Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki. Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.

-Luka 7:41-47.

Mungu awabariki.

Rev. Deo Mbona

Creating your character

Could creating your character be likened to an artist creating a sculpture? In my opinion, I believe that character is not something that just happens by itself, any more than a chisel can create a work of art without the hand of an artist guiding it. In both instances, a conscious decision for a specific outcome has been made. A conscious process is at work. Character is the result of hundreds and hundreds of choices you make that gradually turn who you are, at any given moment, into who you want to be. If that decision-making process is not present, you will still be somebody. You will still be alive, but may have a personality rather than a character.

Character is not something you were born with and can’t change, like your fingerprints. In fact, because you weren’t born with it, it is something that you must take responsibility for creating. I don’t believe that adversity by itself builds character and I certainly don’t think that success erodes it. Character is built by how you respond to what happens in your life. Whether it’s winning every game or losing every game. Getting rich or dealing with hard times. You build character out of certain qualities that you must create and diligently nurture within yourself. Just like you would plant and water a seed or gather wood and build a campfire. You’ve got to look for those things in your heart and in your gut. You’ve got to chisel away in order to find them. Just like chiseling away the rock
in order to create the sculpture that has previously existed only in your imagination.

But do you want to know the really amazing thing about character? If you are sincerely committed to making yourself into the person you want to be, you’ll not only create those qualities, but you’ll continually strengthen them. And you will recreate them in abundance even as you are drawing on them every day of your life. Just like the burning bush in the biblical book of Exodus, the bush burned but the flames did not consume it. Character sustains itself and nurtures itself even as it is being put to work, tested, and challenged. And once character is formed, it will serve as a solid, lasting foundation upon which to build the life you desire.

Jim Rohn

Learning to Follow the Holy Spirit

Fresh Manna
by Pastor Tim Burt

When my children were small, there would be many times I would announce a family outing. “Come on kids, we are all going to Taylor’s Falls (a beautiful river and mountainous hiking area) for a picnic and hiking. You have a half hour to get ready to go.” With four children, there were always different ideas about what they wanted to do. “Oh dad, do we have to go there again, we just went last year?” “I don’t want to go hiking, can’t we just hang out around the house?” and so on.

I really didn’t pay a whole lot of attention to their whining. I knew they would grow out of it over time. Continuing to remind them of having a good and honoring attitude was just a part of their ongoing speech they would hear from Renee and I as we left on outings like this.

Planning these kinds of days took some work and preparation, so I was at times, tempted to get a little upset with their attitude. Renee was great to remind me of our approach to situations like this. “Don’t worry,” she’d say. “I just tell them, this isn’t a democracy or something that’s up for a vote.” “I get this from them all the time whether it’s hauling them to a grocery store or wherever. I just try to make it fun and they are usually glad.” I agreed with her. I had seen exactly that happen, time and time again. We’d usually have a great time and the kids would end up thrilled that we went. I’d ask them on the way home, “Well are you guys glad we went today?” With a sheepish look they’d say, ”Yes dad. You were right and we were wrong. Thank you for taking us – it was really fun!”

Galatians 5:16 says, “…live according to your new life in the Holy Spirit. Then you won’t be doing what your sinful nature craves.”There are many times where our flesh and our soulish man (our mind and emotions) want to do the wrong thing or are lazy and don’t want to do anything. Our flesh and soul seldom like discipline, or moderation, or doing things that we know are good for us. How many times have you thought about getting up and exercising, or reading your Bible and praying, or beginning a diet, only to abandon those thoughts in a very short time?

Most mornings I will go through an exercise routine. Very seldom as I drag my body out of bed, is it excited about jumping into an exercise routine. Yet I know I will be glad once I’m done. If there were 20 things I should do to start out my day, flossing my teeth would be the last on the list yet I know it’s important and so I do it.

When I will pay attention and listen, the Holy Spirit will always speak to me or impress me to do the right thing. When I obey that leading, then I won’t be doing what my lazy or lustful flesh and mind might cry for. God wants you to yield to the Holy Spirit and have your spirit lead your mind, emotions, and flesh. When it does, you will be walking in the will of God. When we learn to consistently do what our spirit is impressing us to do, then we are learning“..to live according to your new life in the Holy Spirit.”

Over the years there have been many areas in my life where I needed to learn to make changes that the Holy Spirit was showing me to make. Those little changes yielded huge results – a happier wife, happier kids, and godly disciplines instead of lazy attitudes. These changes literally changed my character and made me a better man over time.

As adults, we don’t outgrow the things that come at us that we don’t want to do  and that we have to do. We can whine or complain, or we can grow up. We can develop a good attitude or we can bellyache. We want our kids to develop a good attitude. What about us? 2 Cor 7:1 says, “… let us purify ourselves from everything that contaminates body and spirit, perfecting holiness out of reverence for God.”

For many people, life can be one big pain in the rear end. It doesn’t have to be. If we will let our minds and emotions be purified by trusting in God’s ways and

the leading of His Spirit, the Lord blessing can make every path and process that we go through so much more enjoyable and peaceful.

Galatians 5:16 “So I advise you to live according to your new life in the Holy Spirit. Then you won’t be doing what your sinful nature craves.”

In His Love,
Pastor Tim Burt

 

I AM BORN AGAIN!

By default, I was born spiritually dead.  I am saying this because; if you can trace back my genealogy you will find out I came from Adam.  So, I am born of the first Adam who willingly chose to DISOBEY GOD and agreed with the Devil, an act that led him to die spiritually, loose his position as a son of God and became subjected to the one he obeyed, the Devil.

In the book of Genesis, we can see that God told Adam that the day he will eat of the tree of knowledge of good and evil, he will die.

Genesis 2: 15-17 King James Version

“And the LORD God took the man, and put him into the garden of Eden to dress it and to keep it.  And the LORD God commanded the man, saying, Of every tree of the garden thou mayest freely eat:  But of the tree of the knowledge of good and evil, thou shalt not eat of it: for in the day that thou eatest thereof thou shalt surely die.”

Also see Genesis 3:1-6, 7-19 for more insights.

Now, Not I alone that was born spiritually dead, but, all human race, who are born as a result of a woman and a man relationship, are sons and daughters of the first Adam, they also are, spiritually dead and inside them is a spirit that is under the Devil’s lordship! Capable of all sorts of sin and evil and has no place near God.

(Romans 5:12) 

“Wherefore, as by one man sin entered into the world, and death by sin; and so death passed upon all men, for that all have sinned:”

Sin reigned through spiritual death from that time onwards. This is because all who were born after Adam had a sin nature inside them and couldn’t help themselves not to sin; the nature they carried inside can be equaled to a sin generator. Just like how Paul explains it in the book of Romans.

Romans 7:18

“I know that nothing good lives in me, that is, in my sinful nature. For I have the desire to do what is good, but I cannot carry it out.”

You can read for more insights    Romans 7:7-24

If you have followed me closely, it is clear that, every spiritually dead man is capable of sin; he literally craves to sin, it is just a matter of where he was raised.  The only way God has revealed to us, that to some extent, could govern spiritually dead man is putting in place the Law of Moses. The Law was given us to prove that we are spiritually dead, and are all sinners at our core both Jews and Gentiles,

Romans 3:9-11

What then? are we better than they? No, in no wise: for we have before proved both Jews and Gentiles, that they are all under sin; As it is written, There is none righteous, no, not one: There is none that understandeth, there is none that seeketh after God.”

This is why the Jews had to continually offer sacrifices for the remittance of their sins and we also observe several cases where people were stoned to death because they committed sins that had death penalty.

In fact, on the gentiles’ side, the governments everywhere have put in place Laws, to try to control human behavior, in Tanzania for example, rape cases had to be minimized by rising high the penalty of committing such offence, and everywhere in the world the Laws are developed everyday to try to slow down the disasters spiritually dead men are causing.

Nevertheless, the law is not an ultimate solution, because we all agree that throughout the age’s people kept breaking laws even those with terrible penalties.  Fun enough those who are supposed to enforce the law, break the law themselves.  The problem is not the law the problem is our nature.

To this juncture, we are agreeing with “Romans 8:3,

New Living Translation   

“The law of Moses was unable to save us because of the weakness of our sinful nature. So God did what the law could not do. He sent his own Son in a body like the bodies we sinners have. And in that body God declared an end to sin’s control over us by giving his Son as a sacrifice for our sins.”

Also, Hebrews 7:19

(for the law made nothing perfect), and a better hope is introduced, by which we draw near to God.” 

JESUS CHRIST is the only solution! The BETTER HOPE!

If we can go back to Genesis, we can see that God told Adam that the day he will eat of the tree of the knowledge good and evil, he will die.

Genesis 2: 15-17

“And the LORD God took the man, and put him into the garden of Eden to dress it and to keep it.  And the LORD God commanded the man, saying, Of every tree of the garden thou mayest freely eat:  But of the tree of the knowledge of good and evil, thou shalt not eat of it: for in the day that thou eatest thereof thou shalt surely die.”

Also in,

Romans 6:23 (King James Version):

“For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord.”

The question which remains is, is there any hope? Who can remove this corrupt sinful nature from me so that I live?  How do I quicken my dead spirit? How do I get born again and escape the wages of sin?

The answer is, by accepting Jesus Christ LORDSHIP.  For God through His wisdom thought it fit to reverse all that the first Adam caused through one clean person who will trade His righteousness with our Sins.

John 3:16

“For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth in him should not perish, but have everlasting life.”

Ephesians 1:7 

In whom we have redemption through his blood, the forgiveness of sins, according to the riches of his grace;

Colossians 1:14  

In whom we have redemption through his blood, even the forgiveness of sins:

God has explicitly put it clear that it is only through Jesus Christ our Lord we can receive eternal life. Our sins can be washed away only through Jesus Christ who has paid a terrible price on our behalf by His own blood.

Jesus Christ willingly chose to OBEY GOD and paid the price for our redemption, by giving His own life.

But why JESUS?

JESUS CHRIST is the only individual that was born spiritually alive since the Adam’s fall, we are learning from the bible that He was born without a father, this freed Him from inheriting the sinful nature and made Him able to fulfill every single jot of the law, JESUS never committed sin.  Jesus is able to deliver us from the curse of the law because He is the only man who could keep the law and after He fulfilled the requirements of the Law He chose to trade His righteousness for our Sins and died on our place to pay the wages of our sins. In Him alone one can attain the good qualities of righteousness that God requires.

Jesus in His manhood was tempted as we are tempted today, actually He went through the worst, but he didn’t yield to those temptations and that was possible because He didn’t bare a sinful nature. He stands as a living example that a born again man is completely able to live without sinning, this also, teaches us that, Adam had a capacity not to yield to the devil’s deception. You can read about Jesus being tempted in the book of Luke chapter four.

Luke 4:13 

“And when the devil had ended all the temptation, he departed from him for a season.” 

Being BORN AGAIN!

Romans 10:9-11

That if thou shalt confess with thy mouth the Lord Jesus, and shalt believe in thine heart that God hath raised him from the dead, thou shalt be saved.  For with the heart man believeth unto righteousness; and with the mouth confession is made unto salvation.  For the scripture saith, Whosoever believeth on him shall not be ashamed.”

The believing part is very important, because, we are taught that we can only please GOD by believing all HE says. He is the only faithful dependable person ever!!!

He has called us to live a life of faith. The righteousness of God comes only by faith.

(Hebrews 11:6)

“But without faith it is impossible to please Him, for he who comes to God must believe that He is, and that He is a rewarder of those who diligently seek Him.”

Habakkuk 2:4

“… but the just shall live by his faith.”

Romans 1:17

“For therein is the righteousness of God revealed from faith to faith: as it is written, The just shall live by faith.”

If you believe that GOD raised JESUS from the dead it means you are also able to believe that he can quicken your dead spirit.  Like our Father Abraham who believed GOD is faithful and able to quicken dead spirit and gave his son only son Isaac when He was asked by GOD to do so.

Immediately after understanding the truth and believing, one needs to confess JESUS as his Personal LORD and SAVIOR, and by doing so He is denying the lordship of the Devil. Done!

You are now born unto God’s kingdom and you have become a child of God.

John 1:12

“But as many as received him, to them gave he power to become the sons of God, even to them that believe on his name:”

Romans 8:14-16

“For as many as are led by the Spirit of God, they are the sons of God. For ye have not received the spirit of bondage again to fear; but ye have received the Spirit of adoption, whereby we cry, Abba, Father. The Spirit itself beareth witness with our spirit, that we are the children of God:”

Galatians 2:20

“I am crucified with Christ: nevertheless I live; yet not I, but Christ liveth in me: and the life which I now live in the flesh I live by the faith of the Son of God, who loved me, and gave himself for me”

2Cor 5:17

“Therefore if any man be in Christ, he is a new creature: old things are passed away; behold, all things are become new.”

I now have Christ like spirit, sin no longer have dominion over me. My brand new spirit possesses a righteous nature.  I now reign through the righteous nature inside of me.

1Cor 15:22           

“For as in Adam all die, even so in Christ shall all be made alive.”

I am dead to the spiritually dead nature, the nature I inherited from the first Adam and I am spiritually alive in Christ! The old me was crucified with Christ, SO, the old evil me has passed away, yet I live, the one you see now has the spirit of Christ, I am a brand new creature.

I have become a child of GOD; my reborn new spirit is Jesus Christ like spirit, can be equaled to a righteousness generator, I am a righteousness of God in Christ.

I am accepted, I am God’s beloved, and I can boldly go before GOD.  I am His son as Jesus Christ was His Son and God can now relate with me just like He did with Jesus Christ when He walked in this earth or as Adam before the fall.  God is not just God to me, but HE is now my FATHER, and He loves to Father me. I have all the rights of a legal child. I am an heir with Christ.

A point to remember, it is all GOD’s work that I am in Christ Jesus. GOD made JESUS CHRIST my wisdom, my righteousness, my sanctification and my redemption. I had no part to play in my salvation. I have nothing to boast about. I only have the right to be thankful and to boast in the Lord.

King James Version

1Cor 1:30-31

“But of him are ye in Christ Jesus, who of God is made unto us wisdom, and righteousness, and sanctification, and redemption: That, according as it is written, He that glorieth, let him glory in the Lord.”

Philip 3:9

“And be found in him, not having mine own righteousness, which is of the law, but that which is through the faith of Christ, the righteousness which is of God by faith:

Rom 3:24

“Being justified freely by his grace through the redemption that is in Christ Jesus”

2Tim 1:9

“Who hath saved us, and called us with an holy calling, not according to our works, but according to his own purpose and grace, which was given us in Christ Jesus before the world began”

The born again experience comes not by fulfilling the Law, it does not come because I merited it, and I couldn’t attain the righteous qualities God needs.  I failed completely, but by GOD’s mercies through His one and only begotten Son full of grace freely made me righteous.

I, Mercy Yeshua, can testify that, being Born Again is the most fulfilling experience ever! I praise God whenever I ponder about being born again. Born again experience is the rest that God meant when He talked about Sabbath. He has ceased us from works, meaning, we are no longer trying to please Him by trying to fulfill the Law and be counted worthy.  We are counted righteous by having faith in all He says. I am thankful to God for choosing me. GLORY IN HIM ALONE! I BLESS THE DAY I WAS BORN AGAIN!

After you have read this note, I believe you now understand what do we mean by being Born Again, and if you are not born again I wish to ask you the following questions; Do you believe that JESUS actually died for our sins and rose again to give you a new life?  Would you like to receive Him as your Lord and Savior right now? If so pray the following prayer from your heart.

Dear Lord,

Please come to my heart and forgive me of my Sins, I want to receive you as my Lord and Savior. I want to be born again.

I receive you now as my Lord and Savior. I receive God as my Father.

Thank You for saving me.  Amen!

If you have prayed the prayer above from your heart, YOU ARE BORN AGAIN!

Welcome to the family of God!

I pray that this note will be helpful to many, in JESUS CHRIST NAME! AMEN!

–Mercy Msoka

Kwa namna gani mtu anaweza kumzimisha Roho Mtakatifu?

Na: Patrick Sanga

Roho Mtakatifu ni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye pia anayo nafsi na kwa hiari yake ameamua kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu kwa kuzingatia mgawanyo wa majukumu waliyokubaliana yaani nafsi ya    Mungu Baba, Mungu Mwana(Yesu) na Mungu Roho Mtakatifu. Kazi/lengo kubwa la ujio wake ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu kwenye ulimwengu huu wa mwili, ili kumsaidia kuishi katika mapenzi ya Mungu.

Mungu hana namna ya  kutawala kwenye ulimwengu wa kimwili bila kuwa na mwili wa damu na nyama, kwa kuwa yeye ni Roho (Yohana 4:24). Hivyo hana budi kuingia kwenye mwili wa mtu na kufanya makao yake hapo, ili kutawala na kumuongoza mwanadamu katika mapenzi yake (Yohana14:18, 23, 1Wakorinto 3:16-17, 6:19). Kwa sababu hii ni muhimu sana kwetu kutunza mahusiano yetu na Roho Mtakatifu ili tusimzimishe katika maisha yetu.

Paulo akizungumza na ndugu wa Thesalonike alisema ‘Msimzimishe Roho’ (1Wthesalonike 5:19). Paulo alitoa maonyo haya kwa kuwa alijua, Kumzimisha Roho Mtakatifu, kuna athari mbaya sana kwenye maisha ya mwamini katika kulitumikia kusudi la Mungu na hata maisha yake ya kawaida hapa duniani. Swali la msingi ni, kwa namna gani mtu anaweza kumzimisha Roho Mtakatifu? Ukisoma tafsiri za kiingereza, Biblia ya toleo la GNB katika mstari huu inasema Do not restrain the Holy Spirit’ na toleo la KJV linasema ‘Quench not the Spirit’ (1Th 5:19).

Tafsiri hizi mbili zinapanua zaidi tafsiri ya kumzimisha Roho, katika dhana mbili zifuatazo; moja kumzimisha Roho ina maana ya kumzuia Roho Mtakatifu asitawale na kuongoza maisha yako kwa kukataa msaada wake maishani mwako. Pili, kumzimisha Roho Mtakatifu ina maana ya kuishi katika mazingira ambayo yanamfanya Roho Mtakatifu ashindwe kukusaidia.

Mazingira ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuzimishwa;

 • Kutokumpa nafasi akusaidie

Kwa mujibu wa Matahayo 14:16, Roho Mtakatifu ameletwa kwetu kama Msaidizi. Kwa tafsiri, Msaidizi ni yule atoaye msaada pale anapohitajika na kupewa nafasi ya kufanya hivyo. Vivyo hivyo na Roho Mtakatifu kama hujampa nafasi ya kukusaidia (ingawa yupo ndani yako), hawezi kufanya hivyo na kwa hiyo taratibu utakuwa unamfungia/unamzuia kukusaidia maishani mwako.

 • Kukosa upendo

Ukisoma kitabu cha 1Wakorinto sura ya 13 na 14, utagundua kwamba suala la upendo limepewa msisitizo wa kipekee kwa mtu ambaye anataka kuona utendaji wa kazi wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yake na kwa ajili ya wengine pia. Upendo kwa mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu ni moja ya vigezo muhimu sana kwa Roho Mtakatifu kusema/kujifunua na kufanya kazi ndani yako. Hivyo kukosa upendo ni dalili ya kumzimisha Roho Mtakatifu ndani yako. Ndiyo maana Paulo anasema hata kama angekuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, pia kuwa na imani timilifu kiasi cha kuhamisha milima, kama hana upendo si kitu yeye, naam ni bure tena ni ubatili (1Wakorinto 13:1-3).

 • Kuongozwa au kuenenda kwa mwili

Paulo aliwaambia hivi wandugu wa Galatia ‘Basi nasema, Enendeni kwa kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili’ (Wagalatia 5:16). Maneno haya alikuwa akiwaambia watu waliokoka na si wasiomjua Mungu. Kanisa la Galatia lilikuwa limeacha kuenenda kwa Roho likaanza kuenenda kwa mwili. Paulo akajua jambo hili litamzimisha Roho wa Bwana ndani yao, na kwa sababu hii hawataweza kuishi maisha ya ushindi hapa duniani na kisha kuurithi uzima wa milele, ndipo akawaonya akisema enendeni kwa Roho ili msizitimize tama za mwili.

 • Kutokutii maelekezo yake

Roho Mtakatifu kuitwa Msaidizi haina maana tunapaswa kumpamngia cha kufanya. Yeye ndiye mwenye kutuongoza katika njia itupasayo kuiendea (Zaburi 32:8). Kinachotakiwa ni mtu kuwa mtiifu kwa yale ambayo Roho Mtakatifu anakuagiza. Kukosa utiifu mara kwa mara kila anapokusemesha/kukuagiza ni kumjengea mazingira ya kutoendelea kusema na wewe na hivyo kuondoka kwako na kutafuta mtu mwingine amtumie kwa kusudi lake.

 • Kukosa ufahamu wa utendaji wake

Mara nyingi watu wamemzimisha Roho kwa kutokujua utendaji wake ulivyo. Kuna nyakati Roho Mtakatifu anaweza akaleta msukumo ndani ya mtu wa kumtaka aombe, atulie kusoma neno n.k. Lakini kwa kutokujua namna anavyosema, wengi hujikuta badala ya kutulia na kufanya kile alichopaswa kufanya, wao hufanya mambo mengine.

Pia kuna nyakati katika ibada (sifa, maombi nk), Roho Mtakatifu anaweza akashuka juu ya mtu au watu na akataka kusema jambo, lakini viongozi wa makanisa au vikundi husika wakawazuia hao watu. Kufanya hivyo bila uongozi wa Mungu ni kumzimisha Roho. Mandiko yako wazi kabisa kwamba hatupaswi kutweza unabii (1 Wathesalonike 5:20) na wala hatupaswi kuzuia watu kunena kwa lugha (1Wakorinto 14:39). Zaidi tumeagizwa kujaribu mambo yote, na tulishike lililo jema (1 Wathesalonike 4:21).

Je tutajaribuje mambo yote ikiwa tunawazuia watu Kunena na pia tunatweza unabii? Hofu yangu ni kwamba kwa kuzuia watu kunena na pia kutweza unabii tunaweza tukajikuta tunamzimisha Roho Mtakatifu na kukataa uongozi wake kwenye maisha yetu. Ni vema tukakumbuka kile ambacho Paulo aliwaambia Wakorinto juu ya mambo haya kwamba ‘mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu’ (1 Wakorinto 14:40). Naam na hili lina maana ni vema kwanza ujue utendaji wa Roho Mtakatifu ukoje, ili kuepuka kumzimisha kwa kutokujua utendaji wake.

Pengine yapo mazingira mengine ambayo mtu anaweza akajikuta anamzimisha Roho Mtakatifu. Kumbuka jambo hili kwamba kumzimisha Roho Mtakatifu ni kumzuia asikusaidie, jambo ambalo tafsiri yake ni kukataa uongozi wake kwenye maisha yako. Biblia inasema katika Warumi 8:9 ‘Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake’. Usifanye mchezo na Roho Mungu hakikisha unatunza sana mahusiano mazuri kati yako na yeye kwa kutokumzimisha.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nawe

IMANI – 2

 Ndugu mpendwa nakukaribisha sana katika mfululizo huu wa makala ya Imani;naamini unazidi kubarikiwa na somo hili.Ni mimi Docta Lightness William Ng’unda karibu tuendelee.

       Makala yaliyopita tulizungumza juu ya imani inayoambatana na matendo, na leo nitaendeleza hapohapo ili nisikuache.Imani ya matendo inaenda pia sambamba na ukiri wetu na ni muhimu kuchunguza sana ukiri wetu sio kwa kinywa tu bali katika matendo pia.Ukiri wa matendo huwa una nguvu hata kuliko ukiri wa maneno.Namaanisha usiishie kusema tu bali weka hayo maneno kwa matendo pia.Ni muhimu ukiri wa maneno uende sambamba na ukiri wa matendo.

      Mfano mzuri ni huu watoto wengi wa Mungu wamekuwa wanaishi maisha ya kutozingatia kazi,na wanapendelea maisha ya mteremko kwa watu wengine huku wakidai wanaishi kwa IMANI.Mungu anashindwa kuwabariki kwa sababu hakuna wanachokifanya,wanaishia kumlaumu Mungu na kumwona Mungu kama muongo na kumbe sivyo ilivyo.Mungu ameweka wazi katika (2Wathesalonike3:10) Asiyefanya kazi na asile.Lazima uweke mikakati yako kiroho,kinafsi,kiakili na kimwili kupitia ahadi za Mungu ili afanikishe mipango yako. Ukiomba pesa fanya kazi fulani ili Mungu atumie huo mlango kukubariki huku ukiamini.

IMANI NI MKONO WA KUPOKEA MAJIBU

     Watoto wengi wa Mungu ni waombaji wazuri lakini sio wapokeaji wazuri.Namaanisha mtu anaweza funga hata siku 21 akiomba tu lakini upande wa upokeaji hayupo wala haelewi.Maombi ni mazuri sana ila usiwe unajitesa bure lazima ujue kupokea pia.Inawezekana mambo unayopitia Mungu alishayajibu siku nyingi lakini hukujua jinsi ya kupokea na ndio maana biblia inasema  (Hosea 4:6) watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa).Nguvu ile ile uliyoitumia kuomba itumie nguvu hiyohiyo kupokea.Namaanisha ukijua umeomba jambo lolote sawasawa na mapenzi ya Mungu hilo ni lako tayari, na kujua kwamba ni mapenzi ya Mungu utaangalia neno lake linasema nini juu ya hilo jambo unaloliomba na hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.Na huu ndio ujasiri tulio nao  kwake,ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,  atatusikia.Na kama tukijua kwamba atusikia,tuombacho chote,twajua kwamba TUNAZO zile haja tulizomwomba.’(1 Yohana 5:14) Hapa inamaanisha nini? tunajua tunazo zile haja, kwa hiyo ukiomba uwe na ujasiri kuwa tayari unazo haja unazoziomba kwa njia ya imani.

USHUHUDA WANGU

    Rafiki najua shuhuda zinajenga sana na zinainua sana imani ya mtu,mimi nina shuhuda nyingi sana ila ni kwa nia ya kukujenga ili ujenge shauku ndani yako na Mungu atafanya zaidi.Nilikuwa natamani sana kuwa lecture/mwalimu wa chuo kikuu.Na nilipomaliza elimu yangu ya udactari ya chuo kikuu niliomba nafasi ya kuwa mwalimu katika chuo nilichosomea.Tulifanya interview na nilikosa ile nafasi, binafsi iliniuma sana  lakini kwa sababu sikuwahi kuwa na uzoefu wa kufundisha,na katika interview wenye uzoefu walikuwepo hivyo wakachukuwa wenye uzoefu mimi nikakosa.Nikamuuliza Mungu akaniambia umeomba sana anza kuamini kuwa wewe ni lecture nikaanza kukiri ingawa ilikuwa ngumu sababu Tanzania kuna chuo kimoja tu cha kazi niliyosomea ya walemavu,ikabidi nitafute kazi nchi za ulaya na Asia kwa vile walitangaza ajira pia.Siku moja baada ya kuendelea kuamini niliitwa chuo hichohicho nikaambiwa wiki inayofwata nije kazini na nilikuwa napenda sana kuanza kufaya kazi Tanzania na Mungu akanijibu haja ya moyo wangu, na sasa ni lectuere.Usiogope hata wewe mpendwa Mungu aliyetenda kwangu namsii atende na kwako pia ili aufariji moyo wako.Usiogope Mungu anajua kilichobora kwa ajili yako maadamu Bwana ni mchungaji wetu hatutapungukiwa na kitu (ZABURI 23:1) halleluya.Mungu ametuumba tutawale dunia nchi na vyote vijazavyo ni mali ya bwana dunia na wote wakaao ndani yake (Zaburi 24:1),inamaanisha kazi zote pia ni mali yake na anajua wapi atakuweka na kwa wakati gani rafiki.

       Nimesema tena imani ni mikono ya kupokea mahitaji na haja zetu tunazoomba.Tunapokea kwa kadiri ya nguvu itendayokazi ndani yetu yaani imani yetu.Inamaanisha imani yako ikiwa na viwango fulani unapokea haraka zaidi kinachotofautisha majibu mengi ya wana wa Mungu ni imani waliyonayo kwa Mungu juu ya hilo jambo.Kila mtu alipookoka alipewa kiwango cha imani sawa na mwenzake lakini huwa imani inakuwa kulingana na unavyoifanyiza mazoezi ya kuiweka kwa matendo, na hapo ndipo tunapotofautiana sisi kwa sisi.Na imani yako ikikaa bila matendo kuna mda itakufa kama bibilia inavyosema (Yakobo 2:18) lakini mtu akisema, wewe unayo imani ,nami ninayo matendo.Nionyeshe imani yako pasipo matendo,nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo.Mstari wa 26 maana kama vile mwili pasipo roho umekufa,hivyohivyo na imani pasipo matendo imekufa.

        Ni kwa kadiri ya uhakika wa neno la Mungu uliondani yako yaani imani yako ndiyo utapokea na ndiyo maana huwa nasisitizia sana watu wawe wasomaji wa neno ili waongeze uhakika wa mambo yao katika kuzijua ahadi zao na shetani hatakuweza kwa jana la Yesu.Embu fikiria  kuhusu hali unayopta ni kweli hauna uhakia wa neno la Mungu juu ya hali hiyo? Kuna nini Mungu amesema juu ya hali hiyo kwenye neno lake? Anasema (1Petro 5:7) Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. Dai haki yako kwa baba yako maana wewe ni mwana wake na si mtumwa tena.Mungu si mwnadamu hata aseme uwongo ahadi zae zinasimamaa hata nyota zingezimika ahadi zake zadumu hata milele Haleluya.

          Imani ni kuwa na uhakika /ujasiri na udhibitisho moyoni ukisoma tafsiri mbalimbali za kiyunani.Unapoomba ule uhakika wa haja zako kwamba Mungu atakujibu na ujasiri ndio mikono ya kupokea.Ninamaanisha unapokuwa na imani mambo yatarajiwayo yanakuwa wazi au halisi kwako na ndani yako kabla hayajathihirika, nikimaanisha unaanza kuona majibu yako kwa macho ya imani.

         Hivyo imani kama mikono inaambatana na ujasi ili upokee nitafafanua zaidi hapa na kwa mifano ili uelewe zaidi.Kuna kipindi nilikutana na hali fulani nilipoanza kazi,Mungu aliambia nikianza kazi nimpatie mshahara wangu wa kwanza kama malimbuko.Na hata wazazi wangu na marafii walikuwa wananiambia kumbuka mshahara wa kwanza sio wako Lightness.Nilipokuwa nawaza nitaishi vipi mwezi mzima Mungu akanipa wazo la kuanzisha biashara kwa mtaji wa sh alfu 10 tu.Nilikuwaga muoga sana wa kufanya biashara nikawa nikitoka kazini nauza hereni,  mikufu na bangili za wanawake kwa rafiki zangu maofisini na kanisani.Nikaanza kupata hela nyingi sana  hadi mtaji ukafika laki moja na kuendelea, na mpaka sasa najisikia raha sana kufanya biashara na nimeweza hadi kuajiri watu wasiokuwa na kazi nafanya nao na nawalipa.Nitumia ujasiri na Mungu ananibariki sana na sijawahi kupungukiwa au kujuta naipenda kazi yangu na mshahara sasa ni kama mtaji wangu.

         Mpendwa nataka nikwambie unapoomba pesa Mungu hakupi pesa bali anakupa wazo la kitu cha kufanya ili upate pesa, sababu pesa hazipo mbinguni zipo kwa mikono ya watu.Na uwe jasiri na mbunifu kwa kila wazo Mungu analokupa.Watanzania wengi sio majasiri wala wabunifu, ni waoga sana mtu anawaza nikifanya biashara Fulani atanionaje? Huo ni ujinga na uzembe (Hosea 4:6) Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Usidharau mwanzo wa mambo madogo nitazungumzia hili kwa makala nyingine na ujasiliamali kwa wana wa Mungu.Ukitaka kuishi maisha ya imani kuwa jasiri biblia inasema wenye haki ni majasiri kama samba.Kwa leo nitaisha hapo naamini Mungu kasema na wewe nakutakia maisha mema ya kuishi kwa imani.Ni mimi

 Docta LIGHTNESS WILLIAM NG’UNDA kutoka Moshi KCMC

Kuishi maisha ya Imani, Katika Ulimwengu Usioamini!!

Kuishi maisha ya imani maana yake ni kuwa kwa kipindi chote cha maisha yetu hapa duniani, kwa kipindi chote cha uhai wetu, na kwa namna yoyote ile inayoashiria maisha kama kuongea kwetu, kutenda kwetu, kuwaza kwetu, kuenenda kwetu, kuvaa kwetu, kula kwetu, kuona kwetu, kukiri kwetu, kutoa na kupokea kwetu, kufanya kazi kwetu, lupigana kwetu, kushinda kwetu, kuomba kwetu na hata namna yote ile ya kuwajibika kwetu kwa watu wengine tunayafanya haya yote kwa imani.

Tunayafanya haya yote kwa uhakika kabisa, kwa kutokuwa na mashaka wala hofu, tunayafanya kama vile tumejua mwisho wake hata kama hatujayaona kwa macho yetu bado. Kama kuna mambo tunatarajia katika kuishi kwetu, basi kuishi kwa imani katika hayo tunayoyatarajia ni kuishi tukiwa na uhakika na udhihirisho ya kuwa hayo mambo yatatokea na kufanyika halisi maishani mwetu bila kujali changamoto zitokanazo na imani yetu katika mambo hayo.

Katika tafsiri ya kitabu cha Waebrania 11:1, Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”. Kwa lugha nyingine naweza kusema, imani ni udhihirisho wa mambo ninayoyatarajia kuyapata, mambo ninayotumaini kuyapata, mambo ninayotamani na kuwa na shauku nayo katika maisha yangu. Kwa hiyo naishi kwa namna inayodhihirisha na kuthibitisha kabisa kuwa kuna mambo ninayoyangojea hapo mbele.

Kama imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, hii inamaanisha kuwa ni muhimu sana kuyajua hayo mambo yatarajiwayo ni mambo gani kwasababu siwezi kuwa na imani na kitu nisichokijua. Kwa mfano, siwezi kuwa na imani kama Yesu Kristo atarudi tena wakati simjui Yesu mwenyewe wala jambo lolote kuhusu yeye, siwezi kusema nina imani Yesu ataniponya wakati hata sijawahi kusikia habari za Yesu na kwamba yeye ana uwezo wa kuponya. Hivyo ni lazima niwe nimesikia habari za jambo Fulani, ni lazima niwe nimeyajua hayo mambo ninayoyatarajia ili niseme sasa nina imani nayo kwamba yatatokea kwangu.

Ninachosema hapa ni hiki, kwa sababu imani chanzo chake ni kusikia, ni muhimu sana kujua unasikia juu ya nini. Kila mtu hujenga imani ya kile anachokisikia na zaidi sana kile achokifahamu na kukijua. Ukisikia sana habari za waganga basi utajenga imani yako kwa waganga lakini kitu cha kujua hapa ni kuwa kama wewe ni raia wa ufalme wa Mungu basi ni lazima imani yako iwe katika mambo yatokanayo na ufalme huo.

Neno la Kristo ndio msingi wa kujenga imani ya kweli kwa kila aaminiye kwa moyo wake na kukiri kwa kinywa chake kwamba Yesu ni Bwana. Kwa hiyo kama nimeamua kuishi maisha ya imani ndani ya Yesu, ni lazima nizidi kumsikia sana Yesu ili nizidi sana kujenga imani yangu kwake kwenye mambo ninayotarajia.

Kabla sijajua kuwa Yesu ni mwokozi nilimdharau na kuwakejeli wote walionambia habari zake, kwa hiyo nisingeweza kuishi maisha ya imani wakati huo.

Nilipomjua Yesu ni nani, kwa kusikia, nikajenga imani yangu na kuanza kutarajia mambo kadha wa kadha yaliyondani yake yeye. Kwa hiyo hakika ya mambo yatarajiwayo inakuja kwa kuzidi sana kuongeza ufahamu katika kuyajua hayo mambo yaliyofungwa ndani yake yeye ninayemwamini.

Mambo yatarajiwayo, kwa tafsiri niliyoiweka hapo juu, inamaanisha mambo ninayotumainia ndani ya imani yangu katika Kristo na haya mambo ni kama:

 • Uzima

 • Uponyaji

 • Baraka za mwilini na za rohoni

 • Mafanikio na maendeleo

 • Maisha ya ushindi

 • Ulinzi

 • Uzima wa milele

 • Masomo

 • Chakula

 • Mavazi

 • Nguvu

Kwa kuchukua mfano mmoja hapo juu, mimi nimeokoka ingawa nimekuwa naishi maisha ya hali ya chini kiasi kwamba hata mahitaji ya msingi kama chakula, mavazi na hata mahali pa kulala sina, kuishi maisha ya imani katika hali hii ni kuwa na hakika juu ya hayo mambo ninayoyahitaji kuwa nitayapata kutegemeana na imani yangu katika yeye ninayeamini, yaani Kristo, kuwa anaweza kunipa hayo yote sawa sawa nay ale ninayoyafahamu na kuyajua, yale niliyoyasikia amesema kuwa atanifanyia.

Ingawa mwili wangu utaonekana kuchakaa lakini imani yangu inanipa nguvu na tumanini kwani ninajua kabisa kuwa ipo siku Yule ninayemwamini atayabadilisha maisha yangu kwa kadri ya imani yangu, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yangu na zaidi sana kwa kadri ya utajiri wa utukufu wake.

Kwa upande mwingine, kuna mambo yasioonekana ambayo nayo tunatakiwa tuishi kana kwamba tumeyaona na hapa Neno la Mungu linasema, Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Neno bayana ni sawa na kusema halisia, imani ni uhalisia, waziwazi au inayooneka kabisa kwa macho ya nyama na damu. Umesubiria mtoto kwa muda mrefu, imani inakupa nguvu na tumaini la kuendelea kuishi maisha yako kila siku kama mama aliyepata mtoto tayari. Bayana.

Halisia. Inayoonekana. Kama kuna jambo lolote lile ninalolingojea na bado sijaliona, ninatakiwa niwe nalingojea kama vile nimeshaliona kama vile Babu Ibrahimu, habari zake zinasema alitarajia yasiyoweza kutarajia, alitarajia mambo yasiyoonekana kana kwamba yameonekana, alimtarajia Isaka wakati hali yake na ya Bibi Sara haikuwa na uwezo wa kuwapa motto.Lakini yeye alisubiri katika kutarajia kwake mambo yasiyoweza kutarajiwa kabisa. Nguvu ya imani yake aliipata kwa kumjua anayemwamini.

“Mjue sana Mungu, ili uwe na amani na ndivyo mema yatakavokujia”, ndivyo utakavyozidi kupata ushindi maishani mwako, ndivyo utakavyozidi kushinda vita na makwazo ya duniani hapa na ndivyo utakavyozidi kuishi maisha yenye utulivu na usalama kwa maana unamjua yeye akupaye nguvu za hata kupata utajiri.

Kwa hiyo kuishi maisha ya imani ni katika hali zote kwa maana pasipo hiyo imani haiwezekani kabisa kumpendeza Mungu kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima, sio ombi, lazima aamini (awe na hakika wa mambo anayotarajia toka kwake) kwamba yeye Mungu yuko na zaidi ya hayo huwapa thawabu, huwapa Baraka, huwapa mambo mema, huwapa mafanikio, huwapa hazina njema wale wote wanaomtafuta. Katika hali zote, kufanikiwa au kutokufanikiwa, kupata au kukosa, raha au mateso.

Imani inahitajika na hivyo wakati wa Furaha wewe furahi kwa imani na wakati wa majaribu ya imani yako usiseme hii sio imani kwani ni vema

kuhesabu ya kuwa ni Furaha tupu tunapoingia katika majaribu mbali mbali tukijua kuwa kujaribiwa kwa imani yetu huleta saburi maishani mwetu. Kwa hiyo neno imani lina maneno matano ambayo ni:

 1. Hakika-kutokuwa na shaka wala hafu, thabiti

 2. Mambo-ahadi za Mungu unazozijua kama Neno lake linavyosema

 3. Yatarajiwayo-tumaini la kungojea na kusubiri

 4. Bayana-halisia, inayoonekana

 5. Yasiyoonekana-kwa macho ya nyama na damu

Kwa hiyo, ninapomalizia ukurasa huu, napenda kusema kuwa kuishi maisha ya imani ni kuishi maisha tegemezi katika kile anachokisema Mungu. Ni kuishi maisha ya mtu wa haki, mwenye haki anaishi kwa imani, anaishi kwa kuwa na ujasiri na uhakika wa mambo yote anayoyatarajia hata kama hajayaona kwa macho yake. Tunawaza kwa imani, tunaongea kwa imani, tunakula kwa imani, tunatembea kwa imani, tunafanya kazi kwa imani, tunaomba kwa imani, tunaangalia kwa imani, tunaenenda kwa imani na kwa ujumla wake yote tunayoyafanya iwe ni kwa neno au kwa tendo tunayafanya yote kwa imani katika jina la Yesu tukizidi sana kumshukuru Mungu Baba.

Kwa maana tunajua ya kuwa pasipo imani, haiwezekani kumpendeza Mungu kwani sisi kama wenye haki imetupasa kuishi kwa imani. Kuna uhusiano kati ya kuwa mwenye haki na kuishi maisha ya imani. Haiwezekani mtu akaishi kwa imani bila kuhesabiwa haki katika Yesu Kristo aliye mwanzilishi wa imani yetu. Na huu uhusiano ndio tutakao uchambua na kujifunza juu ya kwa nini mwenye haki aishi kwa imani. Umebarikiwa katika jina la Yesu Kristo!

–Sehemu ya kitabu cha Mtumishi wa Mungu, Mwinjilisti Raphael Joachim Lyela

Mawasiliano zaidi kuhusu kitabu chake wasiliana nae

Email: annointedkaka@yahoo.com

Simu: 0787 110 003

IMANI – 1

                       

MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI (HABAKUKI 2:4)

Mimi ni mtumishi wa Mungu namtumikia Mungu kwa njia  ya uimbaji nina albam 3 na ni mhubiri wa neno la Mungu sehemu mbalimbali.Pia ni dakitari katika hospitali ya KCMC Moshi na ninafundisha chuo cha kutengeneza viungo sanifu viungo bandia vya wanadamu hapa KCMC.

Napenda kukukaribisha rafiki uliyeamua kusoma makala haya nina hakika Mungu atasema na moyo wako na utauona utukufu wa Bwana.

Imani ni nguvu inayoishi,kama tunavyosoma katika (Ebrania 11:1) imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana.Rafiki yangu katika maisha ya mtu aliyeokoka swala la imani ni la msingi sana.Imani yetu inatoka kwa Mugu na Mungu tunamuelewa kwa kulisoma neno lake, hivyo imani yetu ikichaganyika na neno la Mungu inakuwa na uwezo wa kuzalisha nguvu.(Ebrania 4:2) lakini neno  lile lililosikiwa halikuwafaa hao,kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.Hapa tunoona ni jambo moja kuwa na neno na ni jambo lingine kuchanganya neno na imani.Watu wengi wameshika sana neno ila matokeo ya utendaji kazi wa neno hayaonekani  kwa sababu nguvu ya kuamini  lile neno haipo .Mazingira yanakuwa na nguvu kuliko Mungu anachokisema juu ya mazingira na hili  limesababisha watoto wengi wa Mungu kuwa waitaji na kuendelea kuonewa na shetani.

Biblia inasema pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6).Unaweza ukajitahidi kutenda kama Mungu anavyotaka ila kama hauna imani bado haujampendeza Mungu.Kama nilivyosema mwanzoni mwenye haki wa Mungu ataishi kwa imani inamaanisha bila imani huwezi kushinda changamoto za duniani.Katika makala mengine nitazungumza juu ya viwango mbalimbali vya imani usikose makala hiyo rafiki.Imani tuliyonayo ndiyo inayofanya jambo litokee naye heri aliyesadiki;kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na bwana (luka 1:45).Najua rafiki yangu bwana amesema na wewe mambo mengi sana juu ya maisha yako na huduma yako,unachopaswa kufanya ni kuendelea kusadiki ili umpe njia ya kutimiza alichokiahidi kwako.Ngoja nikupe ushuda huu wangu binafsi ili uendelee kumwamini Mungu

Mimi nilikutana na changamoto kubwa nilipomaliza kidato cha sita.Kidato cha nne nilifaulu vizuri sana nilipata daraja la kwanza (div 1.11)  nikafaulu kwenda shule ya vipaji maalumu Kilakala secondary masomo ya physics,chemistry na biology.Nilijaliwa akili sana ila nilipoanza kidato cha tano niliuguwa sana hadi kupelekea matokeo yangu ya kidato cha sita kuwa mabaya . Nilipata daraja la tatu na nililia sana nikijua ndoto zangu za kwenda chuo kikuu zimekufa,ila kwa sababu nilikuwa mwombaji na mcha Mungu niliamua kutumia ulimwengu wa imani wa kuyataja yasiyokuwepo kana kwamba yamekuwapo na Mungu akasema na mimi kuwa yeye ndiye awapae watu vyuo vikuu na hatimaye nilipata chuo kikuu cha private na serikali ikajitolea kulipa ada yangu kwa miaka yote ya masomo na leo ni mwalimu wa madactari hapa kcmc hospitali.Na Mungu kanipa kazi nzuri nikiwa na umri mdogo sana. Huyo ndiye Mungu ninayemsema na isitoshe kanipa karama ya kuimba na hadi sasa nina albam 3.  Nina shuhuda nyingi za kukujenga msomaji wangu kadri Roho atakavyokuwa ananiongoza nitakuwa nakupa pia kwa sababu shuhuda zinajenga sana.

UTAJUAJE IMANI INAFANYA KAZI?

MATENDO YAKO

Yakobo 2:18 lakini mtu akisema, wewe unayo imani ,nami ninayo matendo.Nionyeshe imani yako pasipo matendo,nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo.Mstari wa 26 maana kama vile mwili pasipo roho umekufa,hivyohivyo na imani pasipo matendo imekufa.Imani sio maneno matupu ni kile  unachokifanya baada ya kukutana na changamoto fulani.Rafiki jitahidi kadri uwezavyo uweke imani yako kwa matendo.Namwomba Roho mtakatifu afungue ufahamu wako na kila roho inayokuzuiya ikuachie kwa jina la Yesu.

Tukimwangalia Abrahimu baba yetu wa imani alikuwa mtu wa kuweka imani kwa matendo,kila Mungu alichomwamuru afanye alifanya.Mwanzo 12:1 Bwana akamwambia Abrahamu,Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako,uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.Hapa tunaona Abrahamu alikuwa na imani akaondoka,pia bwana alimwambia mwanzo22:2 Akasema umchukue mwanao,mwana wako wa pekee,umpendae Isaka,ukaende zako mpaka nchi ya Moria,ukamtoe sadaka ya kuteketezwahuko juuya mlima mmojawapo nitakaokwambia.Tunaona Abarahamu alifanya kama bwana alivyomwambia na akahesabiwa kama baba wa imani.Mungu anapima matendo yako kuidhibitisha imani yako na matendo yako yanaweza kukana ua kukubaliana na imani.Matendo yako yakiwa kinyume yanakukana mbele za Mungu.Kama nilivyosema imani ina uhakika na uhakika unaonekana kwenye matendo yako

Nataka ufahamu kwamba vitu vyote vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu dhahiri (Ebrania11:3) Mungu alitumia imani  kuumba ulimwengu. Na sisi ni miungu lazima tutumie imani kwa matendo kuumba vitu tunavyoviitaji maishani.Rafiki nakutia moyo endelea kuchochea karama yako ya imani siku hadi siku ili umpendeze Mungu na atajibu mahitaji yako.Wewe ni mtu wa thamani na Mungu anatanani ufanane na yeye iliuwe balozi mwema wa Kristo. Nakupenda sana, tutaendelea na makala haya katika kipindi kijacho na somo letu la imani.Kama unahitaji msaada zaidi wasiliana nami kwa njia hizi.

Doca LIGHTNESS WILLIAM NG’UNDA , 14 June 2012

Bible Study:“The lust of the flesh, The lust of the eyes, and The pride of life.”

Temptation enters man  through three doors: “The lust of the flesh, the lust of the eyes, and the pride of life.” That’s how it entered the Garden of Eden. “When the woman saw that the tree was good for food (the lust of the flesh), that it was pleasant to the eyes (the lust of the eyes), and a tree desirable to make one wise (the pride of life), she took of its fruit” (Ge 3:6 NKJV). Satan has no new tricks, he just dresses up the same old temptations in new attire.

“The lust of the flesh” is anything you recklessly go into debt for, manipulate for, or violate your integrity for. “The lust of the eyes” has to do with your perception. By the time you start seeing clearly, you’ve lost a great relationship or walked away from an opportunity, only to look back and say, “I was foolish. If only I’d waited.” “The pride of life” is the most subtle, therefore the most dangerous. You need a certain amount of pride to succeed in life. So when does pride cross the line? When you start exalting yourself; when you neglect God and think your success is the result of your own effort; when you can’t admit you’re wrong; when you’re willing to go all the way to the bottom, fighting and blaming others. Someone who cannot repent cannot be restored. After his affair with Bathsheba, David wrote, “The sacrifices of God are a broken spirit; a broken and contrite heart, O God, you will not despise” (Ps 51:17 NIV).

Source:Word for you today!

Yuda alipata pesa lakini alijinyonga. TUBU UISHI

Je wajua ya kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vyanzo vya mapato yako na maisha unayoishi au utakayoishi wewe, watoto wako na vizazi baada yako?

Je wajua usafi wa pesa yako utajidhihirisha kwenye maisha yako na hata kwa watoto wako?

Neno la Mungu linasema “Baraka ya Bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo” (Mithali 10:22). Maana yake ni kwamba pesa yako ikiwa safi utaona raha yake lakini ikiwa ya damu au itakayosababisha mateso kwa binadamu wengine uchungu wake hautaukwepa. Hi nisheria ya mwenendo wa dunia iliyo hai na isiyobadilika.

Katika injili ya Matayo 27:3-5 tunapata habari ya Yuda aliyejinyonga baada ya kumsaliti Yesu. Wale makuhani wakuu na wazee waliifahamu hii sheria. Pamoja na kwamba alijuta na kuwaambia “Nimetenda dhambi kwa maana nimemsaliti mtu asiye na hatia” na kuzirudisha zile fedha, walizikata wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”

Kwa kuwa hakutubu alikwenda kujinyonga.

Waiona sheria ilivyo sio? Hata waliozitoa pesa walifahamu hatari ya ile pesa.
Je ulishawahi kuiona hii sheria ikiwa kazini?
Ukiziangalia mali zako unaona nini?
Ukiziangalia mali zako unakumbuka nini?
Je wafahamu ya kwamba hii sheria haibagui?
Je unapenda uzao wako uishi kwa amani?

Je wajua ya kwamba Mungu “si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe?; Je wajua ya kwamba “huwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne” (Kutoka 34: 7).

Je wajua ya kwamba mzazi wako akilamba pesa serikali hatari ya ile pesa haikuachi? Je wafahamu pesa za wizi zimejenga nyumba? zimepeleka watu shule? Zimelisha na zinalisha familia?

Hata hivyo, Je wajua ya kwamba Mungu ni “mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi? (Kutoka 34: 6).

Yuda alijuta lakini hakutubu. Matokeo yake alijinyonga.

Je wajua ya kwamba Neno la Mungu katika Kitabu cha Isaya 1:18 linasema “Haya, njoni tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”?

Je wafahamu ya kwamba “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga”? (Isaya 1: 19-20)

Katika Injili ya Yohana 8:11 Yesu alimwambia Yule mwanamke “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”

Je UMEAMUA NINI?
Katika Injili ya Matayo 4:17 Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”

Na katika Injili hihi ya Matayo 6:33 Yesu alifundisha na kusema “Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa”.

UMEAMUAJE???

Emmanuel Kwayu

UPONYAJI WA NDOA

—Sharti wanawake wasimame kwenye nafasi zao ndipo wataona uponyaji kwenye ndoa zao. 

Hili lilikuwa jambo la kwanza Bwana kunijulisha, ili niwakumbushe tena akina mama. Nimeshaandika kuhusu nafasi za Mwanamke huko nyuma, Kwa kifupi niseme uponyaji wa wa ndoa yako upo kwa wewe kuwa kwenye nafasi yako. Mungu hana namna ya kukusaidia kama hauko kwenye nafasi yako.

Ni lazima uzijue nafasi ambazo Mungu amekupa na kisha kusimama vema ukiwajibika kwenye hizo nafasi. Kinamama wengi leo wanalia sana Mungu aponye ndoa zao na matokeo yake yanakuwa tofauti na matarajio yao. Endapo kama na ndoa yako ipo kwenye eneo kama hili, angalia kama umekaa vizuri kwenye nafsi ambazo Mungu amkupa katika ulimwengu wa roho. Nina uhakika unaweza ukawa kuna maeneo ulijisahau hivyo tengeneza, maana uponyaji na uharibifu wa ndoa yako kimaandiko upo katika uwezo wako mama.

Ni maombi yangu kwamba Roho Mtakatifu akujulishe jambo hili, uponyaji wa ndoa yako haupo kwa Mungu, bali Mungu ameweka uwezo huo ndani yako. Ili uwezo huo uweze kufanya kazi sawasawa ni jukumu lako kuwa kwenye nafasi zako.

Unahitaji hekima ya Mungu ili kujenga ndoa yako 

Ukisoma kitabu cha Mithali 14:1 Biblia inasema “Kila mwanamke aliye na hekima huijenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe”. Biblia imeshaweka wazi kwamba wewe unaweza kuijenga au kuibomoa nyumba yako. Uwezo wa kufanya jambo hili unategemea kiwango cha hekima ya Mungu ambayo ipo ndani yako na juu yako pia. Hekima ya kuponya ndoa yako ambayo sasa unajua iko mashakani, ipo kwenye neno la Mungu na si kwa waganga wa kienyeji.

Unaipataje hekima ya Mungu?

Katika Mithali 8:1 Biblia inasema ‘Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake?’ mstari wa 10 unasema ‘Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi’. Ule mstari wa 14 unasema ‘Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi ni nguvu’. Na ule wa 16 unasema ‘Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia’.

Siku zote kama unataka hekima ya Mungu ya kukusaidia kwenye eneo lolote la maisha yako utaipata kwenye neno la Mungu au kwa Mungu. Imeandikwa katika Mithali 12:1a “Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa’. Hekima ya Mungu kwa mtu ni matokeo ya kiwango cha neno la Mungu ambalo mtu ameliweka na kulitafakari kwa wingi moyoni mwake. Kwa hiyo kwa Watawala, hekima ya Mungu kwa Mtawala inategemea kiwango cha neno la Mungu kuhusu utawala ambalo Mtawala amekiweka ndani yake. Naam hekima ya Mungu kwa Mwanamke itategema kiwango cha neno la Mungu kuhusu nafasi zako ambacho umekiweka ndani yao nk.

Sharti neno la Mungu kuhusu nafasi zako, wajibu wako nk liwe kwa wingi ndani yako ndipo hekima ya Mungu ya kujenga nyumba/ndoa/familia yako itakapokaa ndani yako na juu yako. Na kwa kuwa hekima ni ufahamu, maarifa, shauri na nguvu, itakusaidia katika kuijenga ndoa yako, kama inavyowasaidia watawala, waung’wana na waamuzi katika majukumu yao (Mithali 8:16). Naam hekima hiyo itaongoza kinywa chako kuleta uponyaji wa ndoa na nyumba yako, kama Biblia inavyosema katika Mithali 31:26 “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake”.

Mithali 8:17 inasema ‘nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona’. Naam siku zote, hekima inawasiaidia wale wanaoitafuta na wakaipata’. Na njia kubwa ya kupata hekima hiyo ni kwa njia ya kusoma na kuatafakari neno la Mungu kila siku na kuomba kama nilivyokufundisha hapo juu.

Uwe makini kufuatilia maisha ya mume wako/watu wa nyumbani mwako 

Mithali 31: 27 “Huangalaia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu”. Tafsiri ya kiingereza ya BBE inasema “She gives attention to the ways of her family; she does not take her food without working for it”. Moja ya nafasi za mwanamke ambayo nilishaandika huko nyuma ni kuwa mlinzi wa mwanaume, hii ikiwa ni pamoja na mume wake.

Naam jukumu la ulinzi ni kubwa sana ambalo Mwanamke umepewa, siku zote mlinzi ana wajibu wa kufuatilia kwa karibu sana maisha/nyendo za yule anayemlinda. Kwa dhana ya ndoa yako, ni jukumu lako kama mlinzi kufuatilia maisha ya mume wako na kujua kama anaishi katika mapenzi ya Mungu. Naam ukijua anaishi nje ya mapenzi ya  Mungu unanafasi kubwa kumsaidia kwa kusuguwa goti lako kwa maombi.

Patrick Sanga

Who Is The Jew?

With all the different ideas floating around out there, one of them is bound to make us happy.  But I am not interested in an idea that is not founded and based upon truth which is the word of God.  There is a prevalent idea among us that states the natural Jew has a foot up and is God chosen apart from the rest of us and furthermore they do not have to receive Jesus as their Lord and Savior because they are Gods chosen.  I am in no way anti-sematic and love every race of people regardless of their natural origin.  My point here is not to divide but to bring to light the full weight and scope of what Jesus did for ALL of mankind not just a select group of people.

If the natural Jew is God’s only chosen then is that the Russian Jew, the Asian Jew, the African Jew…..just which one is it?  I believe the Jew is God’s chosen people and so is every other race on the face of the earth.  He chose all of mankind regardless of race creed or color to be sons of God.  He chose all of us based on one thing and that is the blood of Jesus Christ.   He made His choice now we must in turn choose Him by receiving the very life of Christ.  It is this life that makes man the man He was created to be….the new man in Christ Jesus.

John 14:6 makes a very clear statement:  no man cometh unto the Father, but by me.  There is no natural birth that births you into the Kingdom except first you go through Jesus and His blood.  All men are the recipients of the grace of God.  As all men fell in adam so all men were justified  by Christ.   Romans 5:18 Therefore as by the offence of one judgment came upon all men to condemnation; even so by the righteousness of one the free gift came upon all men unto justification of life.

Who then is the true Jew?  Romans 2:28-29 For he is not a Jew, which is one outwardly; neither [is that] circumcision, which is outward in the flesh: But he is a Jew, which is one inwardly; and circumcision [is that] of the heart, in the spirit, and not in the letter; whose praise is not of men, but of God.  If you are born from above the Jew is you!

It is not your natural birth that makes you a new creation it is the spiritual birth that makes you a son of God.  The bible is not a natural book it is a spiritual book and when we try to naturalize the contents it leaves us with a fall short mentality.  Jesus is not a respecter of persons He gave His life for all men.  He said in John 12:32 if I be lifted up from the earth, will draw all men unto me.  He did not leave out the Jew in the lifting up on the cross, He included everyman.  Redemption for all of mankind.  The heart of every man was intended to be the dwelling place of the Most High God.  His desire is to live in man as God.  By the sacrifice of Jesus and the blood He shed that is now a living reality that can be yours by simply acknowledging Him as your Savior, King and Lord…..Jesus Christ.

–Cathy Walker

Maarifa ya Msingi baada ya Kuokoka

Mpendwa, ubarikiwe! Bwana Asifiwe! Itika, ”Amen“, neno lenye maana, ”Na iwe hivyo“.Mpendwa, umepata neema kubwa kusoma somo hili kwenye tovuti hii. Katika somo hili utapata mafundisho muhimu sana, yatakayokufanya uchote baraka zote za rohoni ambazo Mungu amekusudia kukupa.

Hata hivyo, ili ufuatilie vizuri mafundisho haya, itakuwa vema uwe na Biblia yako karibu, ili ufungue na kusoma mistari inayotajwa, ili upate kuelewa vizuri.

Kwanza kabisa, hongera sana kwa kuokoka. Je, ninajuaje, au wewe utajuaje kwamba kweli umeokoka? Jibu, ni kwamba, kweli tumeokoka, kutokana na jinsi Neno la Mungu linavyotuambia. Wakati ulipotubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, kwa dhahiri Yesu Kristo alikusamehe dhambi zako, maana Neno la Mungu linasema katika

YOHANA 6:37, “……Wala yeyote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe.“ Hakuna mtu yeyote anayekwenda kwa Yesu na kutubu dhambi zake, akiwa anamaanisha kuziacha kisha Yesu akamtupa nje na  kuacha kumsamehe. Hivyo, ni dhahiri kwamba ulipotubu dhambi zako ulisamehewa dhambi . Dhambi zako zote zimesamehewa  na Mungu hazikumbuki tena (ZABURI 103:12; Isaya 43:25). Sasa baada ya kujua kwamba umesamehewa dhambi zako, ni muhimu kufahamu pia kwamba kupewa msamaha  kunaambatana na kupewa wokovu, maana Biblia inasema katika LUKA 1:77, “Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao”.

Hivyo basi, kwa hakika umeokoka, na jina lako limefutwa katika kitabu cha hukumu na kuandikwa katika kitabu cha uzima wa milele mbinguni. Kuna furaha na shangwe kubwa mbele za Mungu na malaika zake, kutokana na uamuzi wako (LUKA 15:7,10). Hivyo tangu leo huna budi kuwa na  hakika ya wokovu wako, ili Shetani asikudanganye kwamba hujaokoka. Shetani huweza kutudanganya kwamba hatujaokoka kwa kutumia hisia zetu, na wakati wote tukawa ni watu wa kufuatisha tu sala ya toba na kutaka kuokoka, tena na tena. Hatupaswi kuwa hivyo. Hatuenendi kwa kuona, bali kwa imani (2 WAKORINTHO 5:7). Na imani ni kuliamini Neno la Mungu, na  kulichukua kama lilivyo.

Sasa je, ina maana kwamba huwezi kabisa kufanya dhambi yoyote kuanzia pale ulipookoka? Na kama je, ukifanya dhambi moja baada ya kuokoka, ndiyo wokovu wako umeishia hapo? Ni muhimu sana kufahamu majibu ya maswali haya au siyo ni rahisi kudanganywa na Shetani na kujikuta tumeacha wokovu. Mara tunapookoka halafu tukajikuta tumekasirika au tumesema uongo n.k., Shetani upesi hutudanganya na kutuambia, ”Wewe bado hujaokoka. Kama umeokoka, mbona  asubuhi hii umekasirika na kufanya jambo baya?“ Inatupasa kuwa na maarifa haya tusiangamizwe (HOSEA 4:6).

Ni kweli, ni mapenzi ya Mungu kabisa baada ya kuokoka tusitende dhambi tena. Hata hivyo tunapokuwa bado watoto wachanga kiroho, bado tunaweza tukajikuta tunafanya dhambi hapa na pale. La msingi ni kwamba, mara unapojikuta umetenda dhambi, unatakiwa kutubu mara moja kwa nia ya kuacha dhambi  hiyo na utasamehewa palepale, na wokovu wako unaendelea nao. Biblia inasema katika 1YOHANA 2:1-2, ”Watoto wangu wadogo nawaandikia haya ili kwanba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote“. Hata hivyo, mtu aliyeokoka hawezi kutenda dhambi kwa kukusudia, yaani anajua kwamba kufanya hili ni dhambi, halafu yeye analifanya  kwa kusudi kabisa eti atatubu! Mtu anayetenda dhambi kwa kukusudia hivyo, huyo bado hajaokoka maana kufanya hivyo, Biblia inasema ni kumtukana Mungu (HESABU 15:30-31). Mtu aliyeokoka anaweza kujikuta amefanya dhambi bila kukusudia na hilo litamkosesha amani sana, na vilevile anaweza kufanya dhambi fulani kwa sababu ni mtoto mchanga kiroho, hivyo hajajua sana nenola haki; yaani hajajifunza sana Neno la Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu kuhusu janbo hilo (WAEBRANIA 5:12-13).

Baada ya kupata maarifa haya, sasa tupige hatua zaidi katika mafundisho yetu. Baada ya kuwa umeokoka sasa, hupaswi kuona haya au aibu kuwaambia ndugu na marafiki zako kwamba umeokoka. Ukiona haya, Yesu Kristo atakuonea haya katika utukufu wa Baba yake (MARKO 8:38). Yaani hatakubali uingie mbinguni. Mtu anayemuonea haya mtu mwingine anakuwa kama hamjui kabisa, na anakuwa hataki hata kumtazama, ili asije kushawishika kumwonyesha upendo au huruma.

Vivyo hivyo, sisi nasi kama tunaona haya kuwaeleza wengine kwamba tumeokoka, siku ya mwisho Yesu atakuwa kama hatujui kabisa. Tukumbuke kwamba tunapookoka na kuwahi kuwaeleza watu wanaotufahamu kwamba tumeokoka, hilo linatupunguzia hatari ya kuvutwa dhambini. Mapema kabisa, mwanzoni tu mwa mazungumzo yetu, na marafiki wa kiume au wa kike wa zamani katika uasherati na uzinzi, ulevi, dansi, ushirikina n.k.; hatuna budi kusema, ”Mimi nimeokoka, hivyo siwezi tena kufanya mambo yale tuliyokuwa tunayafanya pamoja“. Vilevile hatuna budi kuvunja urafiki wa pete na kidole na watu wale tuliokuwa tunafanya dhambi pamoja, maana kama tutaambatana nao kwa karibu sana, kama mwanzo; wataturudisha tena dhambini. Ni vema sasa kuwa na urafiki wa pete na kidole na wenzetu waliookoka (ZABURI 119:63; MITHALI 22:24-25). Hata hivyo hatupaswi kuwachukia au kuwadharau watu ambao hawajaokoka, bali tunapaswa kuwapenda, kuwaombea na kuwaalika kusikia mahubiri, ili wao nao waokoke kama sisi. Bado tutashirikiana nao vizuri ofisini n.k. Ila, wale tuliokuwa tunafanya nao uasherati au uzinzi, tujiepushe nao kabisa maana ni rahisi sana kurudia uchafu wa mwanzo.

Ni muhimu pia kukumbuka kwamba tukiwaambia ndugu na marafiki kwamba tumeokoka, upesi watasema kwamba tumepotea. Tusijali maneno hayo. Hawajui walisemalo. Kabla ya kuokoka, ndiyo tulikuwa tumepotea, lakini sasa tumepatikana, maana Yesu alikuja kutafuta na kuokoa  kile kilichokuwa kimepotea (LUKA 19:10). Furaha na shangwe zilifanyika  baada ya mwana mpotevu kurudi kwa babaye, na inatajwa kwamba alikuwa amepotea, lakini sasa ameonekana (LUKA 15:32). Hivyo waliopotea yaani wana wapotevu, ni watu ambao hawajaokoka, siyo sisi tuliookoka!

Tuendelee tena sasa. Ni muhimu tena wakati huu wa mapema, baada ya kuokoka, kufahamu jinsi ya kuukulia wokovu. Maneno mengine yanayotumika badala ya kuokoka, ni kuzaliwa mara ya pili (YOHANA3:3). Hivyo kwa maneno mengine, umezaliwa mara ya pili, kwa Roho. Ulizaliwa mara ya kwanza, pale ulipozaliwa kwa njia ya kawaida ya kimwili. Wakati huo ulizaliwa kwa mwili, lakini sasa umezaliwa kwa Roho, kama Yesu alivyozaliwa, kutokana na mimba iliyopatikana kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (YOHANA 3:6-7; MATHAYO 1:20-21). Wewe sasa ni mtoto mchanga wa kiroho. Sasa basi, hebu tafakari jambo hili. Je mtoto mchanga anapozaliwa katika hali ya kawaida ya kimwili, anaweza kuendelea kuishi bila kunyonya maziwa? Jibu ni kwamba atakufa baada ya muda mfupi kwa  sababu ya kukosa chakula. Vivyo hivyo hakuna mtoto mchanga wa kiroho anayeweza kuendelea katika wokovu kama hapati maziwa yasiyoghoshiwa yaani yasiyochanganywa na maji. Tunasoma katika 1PETRO 2:2,” Kama watoto wachanga waliozaliwa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu“. Maziwa haya yasiyoghoshiwa ni nini? Ni mafundisho ya Neno la Mungu yanayofundishwa kwa kuzingatia Biblia inavyosema, bila kuchanganywa na taratibu tu za kibinadamu. Neno la Mungu ni chakula cha roho zetu (MATHAYO 4:4; KUMBUKUMBU LA TORATI 8:3; YEREMIA 15:16).

Baada ya kuokoka, haikupasi kuzungukazunguka huko na huko kwenye mahubiri yanayozungumzia tu kutubu dhambi na kuokoka. Hayo pamoja na jinsi yalivyo mazuri, umekwisha yasikia, na tayari umekwisha okoka. Unachokihitaji sasa ni mafundisho ya kina ya Neno la Mungu ya kukuwezesha kufahamu yanayokupasa kufanya na yale yasiyokupasa kufanya, na hatimaye wewe nawe uwe mwalimu wa wengine (MITHALI 12:1 ; HOSEA 4:6; MAMBO YA WALAWI 5:17: MATHAYO 22:29; WAEBRANIA 5:11-14). Kabla ya kuokoka, tulikuwa katika mafundisho manyonge yenye upungufu, ndiyo maana hayakutufanya tuokoke. Baada ya kuokoka, Neno la Mungu linatuonya  kutoyarejea mafundisho hayo manyonge, kama tunataka kuukulia wokovu. Tuwe tayari hata kuwaacha ndugu zetu huko na kutafuta Kanisa lenye watu wenye imani moja na sisi yaani waliookoka kama sisi, ambapo mafundisho yote ni ya wokovu (Soma WAGALATIA 4:9; HOSEA 4:17; 2 PETRO 1:1). Vilevile, kama tunataka kuukulia wokovu, tusitosheke na ibada moja tu ya Jumapili kwa wiki, au kwa mwezi. Miili yetu inakula mara mbiliau tatu kwa siku. Roho zetu ni za thamani zaidi, hivyo hatuna budi kuhudhuria ibada zote za Kanisa kwa gharama yoyote, ili tuukulie wokovu, hata kama Kanisa tuliloliona linatufaa, liko mbali kiasi gani! (Soma MATHAYO 12:42; MITHALI 2:3-5; AYUBU 23:12; ZABURI 119: 72).

Tukiwa ukingoni sasa mwa somo letu, hatuna budi pia kufahamu juu ya Shetani. Neno ”Shetani“, kwa lugha ya asili, maana yake Adui, Mshindani, Mpinzani, na pia Yeye aletaye vizuizi kwa watu wa Mungu au watu waliookoka katika hali ya uadui kabisa, ili ikiwezekana, waiache njia ya kweli ya wokovu ya kumfikisha mtu mbinguni. Shetani anaweza kutumia mawazo yako mwenyewe au ndugu zako wa kimwili, kukuvunja moyo na  kukukatisha tamaa kuendelea na kweli yote ya wokovu uliyoipokea. Utashangaa siku ya ibada ndiyo magonjwa yanaanza, ndiyo wageni wanakuja kukutembelea n.k., ujue vyote hivyo ni vizuizi vya Shetani, mpinge kwa kutokuruhusu lolote lile kukutoa katika ibada (YAKOBO 4:7). Mateso na maudhi mbalimbali kwa mume, wazazi, ndugu n.k; yanaweza kuja kwako baada ya kuokoka. Hii si ajabu, ni kazi za upinzani za Shetani. Yalimpata Yesu. Wewe songa mbele tu bila kujali yatakayokupata (WAFILIPI 1:29-30; 1 WATHESALONIKE 3:3; 1 PETRO 3:14; MATHAYO 5:11-12; YOHANA 5:16; 7:19-20; 8 :48 ; 15 :24-25 ; MARKO 3:21; 2 TIMOTHEO 3:12; WAGALATIA 4:29; 1 PETRO 4:12-16). Kwa vyovyote vile, usigeuke nyuma na kuacha wokovu. Vipige vita vizuri vya imani, imani uilinde (WAEBRANIA 3:14; 2 PETRO 2:20-22; 2 TIMOTHEO 4:7). MUNGU AKUBARIKI!!!

Kwa msaada zaidi muone Mchungaji wa Kanisa linalohubiri wokovu.

*****************

–Askofu Zakaria Kakobe

Zijue Karama za Roho Mtakatifu

I Wakorintho 14:12. Inasema ‘vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. Mungu hafanyi kitu bila kusudi, na kusudi la semina hii ni:-

 • Kuna jambo Mungu anataka kufundisha katikati yetu ambalo litahusisha sana utendaji wa karama za Roho Mtakatifu.

 •  Kurahisisha ujenzi wa kanisa lake na kazi zake. Mfano, kuna urahisi wa kujenga kwa kutumia mashine za kujengea na kubeba matofali kuliko kutumia mkono, ni sawa na kufanya kazi ya Mungu kwa kutumia karama za Roho Mtakatifu.
  I Wakorintho 12:4; anasema pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Karama si za mtu ni za Roho Mtakatifu na kazi yake ni kulijenga kanisa.

  Yesu alisema katika kitabu cha Mathayo 16:18; ”nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitaliweza”. Karama zinatokea mahali kama apendavyo Roho. Katika kitabu cha Yohana 14:16, Yesu alizungumza habari za kutuletea msaidizi mwingine, yaani Roho atakapokuja atachukua nafasi ya Yesu katika kulijenga kanisa lake.
  Roho Mtakatifu sio karama bali anazo karama, pia Roho Mtakatifu sio nguvu bali anazo nguvu. Tunda la Roho linapofunuliwa ndani ya mtu tabia ya Mungu hujitokeza kwake.

  Katika kutafuta vitu vya Mungu, ili kufahamu karama za Roho Mtakatifu na kazi zake, kuna gharama. Mfano, kwenye ndege kuna first class, business class na third class. Ukitaka kupata huduma nzuri zaidi lazima uongeze pesa (gharama) ili upande business class au first class. Lakini dereva wa ndege (captain) ni yule yule. Vivyo hivyo katika maswala ya Mungu wako wanaokaa first, business au third class, lakini wote tunakwenda mbinguni. Hivyo tunahitaji kuingia gharama ili tukae first class ndani ya Yesu. Gharama hizo ni kama:-
  i) kusoma neno la Mungu kwa bidii kwa kadri inavyowezekana ili neno hilo likae ndani yako kwa wingi, maan kujua karama za Roho Mtakatifu bila kuwa an maneno ya Mungu ni vigumu.
  ii) Maombi n.k.

  I Wakorintho 12:1 inasema ‘basi ndugu zangu kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu’. Tunahitaji kuwa na hamu ya kuona kwamba karama za Roho Mtakatifu zinafanya kazi na zinafahamika. Hamu hiyo imepotea katika kanisa la Mungu na hivyo kufanya kazi ya ujenzi wa kanisa la Mungu kutofanyika kama Mungu anavyokusudia.

  I Wakorintho 14:12; ”Vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.UTENDAJI KAZI WA KARAMA. Mambo muhimu (ya msingi) kufahamu ili karama ziweze kufanya kazi. Mambo hayo ni:-1.) kubali kuwa karama za Roho zinaweza kufanya kazi kwako pia. I Wakorintho 12:4.11; ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule, lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye”. Roho Mtakatifu ndani ya mtu anazo karama zote bali anamgawia kila mtu kama apendavyo yeye. Rumi 12:3-6; inasema ”kwa maana kwa neema niliyopewa na mwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyo mpasa kunia ……….., basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali …………..”.2.) Uwe na hamu (haja) kubwa ya msaada wa Mungu. I Wakorintho:1,12; ”ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu, vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.Angalizo: karama siku zote zina mvuto.3.) Tembea katika wito (nafasi) yako. Warumi 12:6, ”……… kwa kadri ya neema tuliyopewa…”, yaani wito (kiwango) ulichopewa. Ndani ya wito kuwa nafasi ambayo Mungu amekupa. Kuna ngazi, kuna mahali na muda unaotakiwa kuufanyia huo wito. Galatia 2:6-7 ”……walipokwisha kujua neema niliyopewa…….. walinipa mimi mkono wa kuume wa shirika”.Mfano: kuna tofauti ya karama ya unabii na huduma ya unabii, yaani kila mtu aliyeokoka anaweza kutoa unabii bali si kila mtu ana karama ya unabii.4.) karama kutenda kazi vizuri ndani ya mtu inategemea kiwango cha Imani alichonacho. Rumi 12:6; ”basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali …….. ikiwa unabii tutoe unabii kwa kadri ya imani”. Sio zaidi ya hapo. Rumi 10:17; ”imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo” yaani kiwango cha imani ulichonacho hakiwezi kuzidi hapo. Imani huja tu kwa neno la Kristo. Biblia haituruhusu kutembea kwenye karama zaidi ya imani tuliyo nayo.Angalizo: kufahamu neno la Kristo kwa wingi ni muhimu. Tembea katika karama za roho kwa kadri ya imani.

  Karama zitumike kwa kadri ya Imani yaani utendaji kazi wa karama za Roho Mtakatifu ndani ya mtu utategemea kiwango cha neno la kristo kilichoko ndani yake. Hii ni kwa sababu Mungu alikusudia kuwa karama katikati ya kanisa zifanye kazi kwa ufanisi na usalama ili kulijenga kanisa.Mfano: Mungu hakuweka unabii ili uongoze kanisa; ila ni kwa ajili ya kuthibitisha neno ambalo Mungu amekwisha kulisema ndani ya mtu.Kwa sababu karama si zako ni za Roho Mtakatifu, kama huna neno la kutosha ndani yako karama inaweza ikaletwa ndani yako ukaikataa.I Wakorintho 12:8 ”maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa apendavyo Roho yeye yule”. I Petro 4:10; ”kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana….”. Kuna kupewa na kupokea- karama. Unaweza kukataa kwa kutokuja au hofu n.k.5.) Jifunze jinsi Roho anavyowasiliana na roho yako, nafsi yako na mwili wako. I Wakorintho 3:16; ”hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?” Mtu ni roho anayo nafsi na anaishi katika mwili. Roho Mtakatifu pia yuko ndani ya mwili. Hesabu 30:2 ”Mtu atakapo mwekea Bwana nadhiri, ……. Asitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake”. Unaposema maneno yanafunga nafsi yako. Mwili unatawaliwa na nafsi, nafsi kazi yake ni kutafsiri kile ambacho mwili unasema ili roho ielewe na kile ambacho roho inasema ili mwili uelewe. Kwa hiyo nafsi inasaidiwa pale, unaposoma neno ili iweze kutafsiri mambo ya rohoni sawasawa na neno. Marko 2:5-8, ”naye Yesu, alipoiona imani yao, …….. wakifikiri mioyoni mwao ….. Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao …..”. Galatia 6:17; ”tangu sasa mtu asinitaabishe kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.6.) Ujazo wa Roho Mtakatifu. Sio wa siku moja ambao unatosheleza. I Petro 4:9-11 ”mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika, kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama,……….. mtu akihudumu na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu, …….”. yaani kila wakati kuna nguvu fresh, mtu asihudumu kwa nguvu alizojaliwa bali anazojaliwa kila wakati na Mungu. Hivyo tunahitaji kurudi kwa Mungu kila wakati kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu.Kuna kiwango cha nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu ambacho hakiwezi (kwa kuwa ni kidogo) kusukuma karama fulani ili ziweze kuhudumu au kufanya kazi; ndio maana tunahitaji kujazwa kila wakati.

  Karama ya neno la Maarifa: I Wakorintho 12:4,8; ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima, na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule”.Kama tulivyo jifunza huko nyuma kazi ya karama ni kulijenga kanisa.Kazi ya karama ya neno la maarifa.

 •  Kukupa habari ya mambo yaliyopo na/au yaliyopita ili kukurahisishia kufanya maamuzi na kutambua hila zilizojificha ili kukwamisha utumishi wako.

 • Wakati mwingine karama hii itakupa kujua maswali waliyonayo watu kabla hawajauliza au kujua mahitaji waliyonayo kabla hawajakwambia.Njia nne ambazo karama ya neno la maarifa inafanya kazi:i. kwa kutumia mawazoii. kwa kutumia ndotoiii. kwa kutumia maono, maono yamegawanyika katika sehemu zifatazo:

 •  Maono ya ndani

 •  Maono ya wazi

 •  Maono yanayotokea wakati akili zako hazina matunda.(suspended)
  iv.  kwa kutumia njia ya kuweka mwilini mwako maumivu au hali aliyo nayo mtu mwenye kuhitaji.

  Karama zinafanya kazi kwa kutegemeana/kushirikiana.
  Mfano. Unaweza kupewa swali na jibu. Kulijua swali ni neno la maarifa na kujua jibu la swali hilo ni neno la hekima.

  i. Njia ya kutumia MAWAZO / WAZO
  Hii ndio njia kuu ambayo inatumika mara nyingi zaidi. Marko 2:6-8 inasema ”……. Mara (ghafla) Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao…..”. Maana yake ghafla wazo tofauti, na lile alilokuwa akiwaza saa hiyo lililetwa na Roho Mtakatifu ndani yake.
  Ukisoma Luka 3:15-16; inasema ”……….Yohana alijibu akawaambia wote,…………”. Yaani alijibu swali ambalo lililetwa ndani yake na Roho Mtakatifu; sio kwamba aliulizwa na mtu yeyote yule.
  Luka 20:18-26; inasema ”……….wakamvizia-vizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali. Wakamwuliza wakisema,………………. Lakini yeye alitambua hila yao akawaambia ……………. Wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa”.

  Mambo ya kukuwezesha kufanya kazi na njia hii ya mawazo:
  a. Jizoeze kukabidhi roho yako, nafsi yako na mwili wako kila siku upya mbele za Mungu.
  b. Omba maombi ya vitu vifuatavyo:

 •  Usikivu (sensitivity)

 •  Utulivu

 •  Kufundishwa na Mungu namna ya kutembea katika hiyo karama.Hii inasaidia kwa mfano, Mungu akisema jenga safina wakati sio msimu wa mvua. Yaani kutii sauti ya Mungu bila kuangalia dalili za nje.

  Karama ya neno la hekima

  I Wakorintho 12:4,8; inasema ” Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima…….”.
  I Wakorintho 14:12 ” ……takeni sana mzidi kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.
  Karama ya neno la maarifa na neno la hekima zinafanya kazi kwa karibu sana.

  Kazi ya karama ya neno la hekima na inavyofanya kazi:
  1. kukupa jibu la swali unaloulizwa lakini hasa swali lenye hila, mtego, ushindani au mashtaka ndani yake.
  Luka 21:12-15 inasema ”lakini, kabla hayo yote hayajatokea watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi…….. basi kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza, mtakavyojibu, kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga”.
  Luka 20:19-26; ”…lakini yeye alitambua hila yao …..”
  Marko 3:1-6; inasema ”……….akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza simama katikati ……….nyosha mkono wako. Naye akaunyosha mkono wake ukawa mzima tena”.
  Hapa tunaona neno la maarifa (kutambua hila ya wale waliotaka kumkamata) ilianza kufanya kazi, neno la hekima pia likafanya kazi baadaye pale Yesu alipomwambia yule mwenye kupooza ”simama katikati” na tunasoma akaanza kuzungumza na wale watu.

  2. inakupa uwezo wa kutatua tatizo lililoko mbele yako.
  Mathayo sura ya 1 na ya 2: Habari ya Yusufu na Mariamu. Katika sura hizi karama ya neno la maarifa na la hekima ilifanya kazi kwa kutumia ndoto. Si ndoto zote zinatoka kwa Mungu lakini kama ukiwa na neno la Mungu utatambua ndoto ya Mungu na isiyo ya Mungu.

  3. kukupa uhuru wa kushirikiana na watu usiowajua kwa kazi ya Mungu.
  Matendo ya mitume 10:1-20; Habari za Petro na Kornelio. Habari hii inaeleza jinsi Petro alivyoona maono wakati amezimia roho (akili zake zilikuwa hazina matunda).
  Maono ya aina nyingine, kama tulivyokwishaona hapo nyuma ni ya wazi, ambapo akili zako zinaona na zinaelewa na bado unaweza kuona katika ulimwengu wa roho.
  Aina nyingine ni maono ya ndani kwa mfano: unapoomba halafu ghafla ndani yako inakuja picha.
  Sasa karama ya neno la maarifa na la hekima itakusaidia kukuwezesha kushirikiana na watu usiowajua.

  4. inakurahisishia kuamua kwa haki katika nafasi ya uongozi Mungu aliyokupa au mahali unapohitajika kutoa maamuzi
  I Wafalme 3:4-28; habari za mfalme Sulemani, jinsi alivyoomba hekima kwa Mungu na akapewa. Vilevile tunaona jinsi ambavyo aliweza kutoa uamuzi wa haki juu ya kesi ya wanawake wawili waliokuwa wakigombea mtoto. Uamuzi wa haki unahitaji msaada wa Mungu.

  Karama ya unabii

  I Wakorintho 12:4,10 ”Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule. na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii, na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha.I Wakorintho 14:12; inasema ”…….takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa”.Mambo ya msingi kuhusu huduma ya Nabii na karama ya unabii:-1. kuna tofauti kati ya huduma ya nabii na karama ya unabii.Efeso 4:11 ”Naye alitoa wengine kuwa Mitume; na wengine kuwa manabii….”. Hapa anazungumza habari ya nabii (ofisi) ya nabii. Huduma ni ofisi na karama ni vitendea kazi katika ofisi. Kazi za nabii (kama huduma)

 • kufundisha mafundisho ya msingi / ya kuweka msingi wa kiroho ndani yako. Efeso 2:19-20 inasema, ”Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, ……..mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”. Hii haimaanishi kwamba kila nabii amepewa kufundisha.

 •  Nabii pia anaweza kupewa kufanya kazi ya kubomoa na kuharibu kazi za shetani na kupanda pando la Mungu ndani ya mioyo ya watu, kama kuna mahali panahitajika kufanya hivyo. Tunaweza kusoma haya katika kitabu cha Yeremia 1:4,5,10; inasema ” …..kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa …………. Ili kung’oa na kubomoa na kuharibu na kuangamiza; ili kujenga na kupanda”.

 • Kazi nyingine ni kuonya. Tunaweza kuona haya katika kitabu cha Ezekieli 2:3-5; ”akaniambia mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israel, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi wao na baba zao wamekosa juu yangu…..”

 • Kazi nyingine ni mwonaji. I Samweli 9:9 ”(Hapo zamani katika Israel, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa mwonaji)”.

 •  Kutabiri (kusema mambo yajayo). Yeremia 23:21; inasema ”mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri.

  Kazi ya karama ya unabii. (kama kitendea kazi):
  Ni kujenga, kufariji, kutia moyo na kujirunza, pia huthibitisha kile ambacho Mungu amekwisha kusema na wewe. Katika kitabu cha I Wakorintho 14:3,4,24,25,31; tunasoma ”Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo. Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa. Lakini wote wakihutubu, kisha akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, abainishwa na wote, ahukumiwa na wote; siri za moyo wake huwa wazi, na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudi-fudi, na kukiri ya kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka. Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe”.

  2. manabii wapo hata leo ila nafasi zao ni tofauti na za wale wa agano la kale.
  Efeso 4:11,14; ”naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamisisha watakatifu; hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa Imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu…………. Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja tukizifuata njia za udanganyifu”.
  Pia katika kitabu cha Matendo ya Mitume 13:1; tunasoma ”……. Palikuwako manabii na waalimu …..”. hii inaonyesha kuwa manabii wapo hata leo.
  Tofauti iko hivi: kwamba manabii hapo zamani (katika agano la kale) walikuwa viongozi wakiongoza watu, yaani walipewa kuongoza watu, lakini katika agano jipya huduma ya nabii ipo ndani ya Kanisa na nabii hakupewa kuongoza kanisa- kila mmoja wakati huu amepewa Roho Mtakatifu ambaye anamwongoza. Hivyo nabii anayesema kwa mausia ya Mungu ni yule anayesema sawasawa na neno la Mungu.

  Kanisa linajengwa juu ya misingi miwili ambayo ni:
  a. Yesu Kristo
  b. Mafundisho ya mitume na manabii ambao wanafundisha mafundisho ya msingi ambayo yanamfanya mtu awe mkristo. (foundation series). Ukisoma kitabu cha Waebrania 6:1; inasema ”kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundishao ya kwanza ya Kristo; tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na Imani kwa Mungu na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu na hukumu ya milele”.

  Manabii wa sasa wanatofauti na akina Paulo na akina Petro ambapo hao wa zamani walipewa mafundisho ya msingi na hawa wa sasa wanapewa wito (hekima au special revelation) wanaposoma Biblia wanafungua siri za mafundisho ya msingi, ambayo akina Paulo walifundisha, na kutufunulia sisi.

  Mambo ya msingi kuhusu huduma ya Nabii na karama ya Unabii, 

  I Wakorintho 12:4,103. Karama ya Unabii (kinachosemwa na Nabii) lazima kipimwe.Kwa nini kupima?

 •  Si wote wametumwa na Mungu.
  Ukisoma kitabu cha Yeremia 23:21,22; anasema ”mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao lakini walitabiri. Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya,…..”. Maana yake ni manabii wa kweli ila tatizo ni kwamba walienda pasipo kutumwa, hawakukaa barazani pa Mungu na kusikiliza kile ambacho Mungu alitaka kisemwe.

 •  Kuna manabii wa uongo waliojiingiza katika makundi ya Mungu.Ukisoma Mathayo 7:15; anasema ”Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

 • Kuna manabii wa uongo ambao wanafanya kazi kwa kutumia Ishara na miujiza, ili kuwavuta watu wawafuate lakini Mungu hakuwatuma. Ukisoma Mathayo 24:24,25 ”kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa Ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata waliowateule. Tazama nimekwisha kuwaonya mbele”.

 •  Kwa sababu ya matumizi yasiyo na utaratibu wa ki-Mungu juu ya huduma ya Nabii na karama ya unabii.
  I Wakorintho 14:29,33,39,40; ”Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, vile-vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. Kwa ajili ya hayo ndugu, takeni sana kuhutubu wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na utaratibu”.

 •  Ni agizo.
  Ukisoma I Yohana 4:1; anasema ” Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”. Pia katika kitabu cha 2 Petro 1:20,21; ”mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukutolewa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”.

  Unapimaje?
  Katika kupima kwa ajili yako wewe kutoa karama ya Unabii au kwa kusikia kutoka mtu mwingine, jiulize maswali yafuatayo:-
  a. Je roho inayokutumia kutoa unabii inakutawala au unaitawala? Ukisoma kitabu cha I Wakorintho 14:32,33 anasema ”Na roho za manabii huwatii manabii….” Roho Mtakatifu hakuleta karama zake zikufanye mtumwa. Ukiona hali hii kaa kwenye maombi tena.
  b. Je hayo yaliyosemwa kwa njia ya unabii ni sawasawa na neno? Ukisoma Warumi 12:6 inasema; ”……tutoe unabii kwa kadri ya imani”. Maana yake kwa kadri ya kiwango cha neno ulichonacho ndani yako. Pia kitabu cha Hesabu 22:18; inasema ”…..siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, alilosema ndani yangu Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.
  c. Je unapotumika katika unabii au kama nabii unajionaje ndani yako? Unaona kama hiyo karama ni kipimo cha kiroho kwamba uko mbali sana? Kitabu cha I Wakorintho 13:9 ” kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu”. Maana yake hakuna mtu ambaye anajua kila kitu hivyo ni muhimu kuwa mnyenyekevu na kuwa tayari kujifunza kwa wengine.
  Pia katika kitabu cha I Petro 4:9-10; inasema ”…….. kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu”. Maana yake uwe tayari kupokea karama ambayo inatenda kazi ndani ya mtu mwingine. Vile-vile kitabu cha I Wakorintho 13:2; anasema ” tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, ….. kama sina upendo si kitu mimi”.
  d. Je Kristo anainuliwa au la? Kitabu cha Kumbukumbu la torati 13:1-4. ”kukizuka katikati yako nabii au mwotaji wa ndoto… akisema, na tuifuate miungu mingine ya nabii yule ………… tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu, ……..”. Kuna hatari pale ambapo karama zinafanya kazi halafu utukufu wanapewa watu badala ya kumwinua Yesu.
  e. Je unabii / kilichosemwa na nabii au unabii ulioletwa kwako unakuweka huru au la? Maana palipo Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru.
  f. Je unabii huo unatimia au la? Ukisoma Kumbukumbu la Torati 18:20-22 anasema ”Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au takayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa…… atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana;………”.
  g. Je tabia za hao manabii zikoje? Ukisoma Mathayo 7:15-23; anasema ” ……..mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri………. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua…………..”
  Mara nyingi tunda huwa linachukua muda kutokea lakini baada ya muda huo litatokea tu.
  h. Je huo ujumbe aliotoa nabii unajenga au unabomoa? Ukisoma I Wakorintho 14:3-5,31 ” Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo……….. bali ahutubuye hulijenga kanisa ………… kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe”.

  Karama ya unabii inavyofanya kazi

 •  Kusema chini ya upako. 2 Petro 1:20-22 anasema ” ……….., wakongozwa na Roho Mtakatifu

 •  Ujumbe unaoambatana na Matendo. Matendo ya mitume 21:9-14; inasema ”….. alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, hivyo ndivyo wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu nao watamtia katika mikono………..”.

 •  Unabii mwingine unatimia kwa maombi. Yakobo 5:17-18; anasema ” Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia pamoja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinye na mvua haikunya juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua nayo nchi ikazaa matunda yake”.

  Karama ya masaidiano.

  I Wakorintho 12:28; inasema ” Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, na tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano na maongozi na aina za lugha”.

  Kuna huduma ya masaidiano na karama ya masaidiano. Karama ya masaidiano inafanya kazi kwa karibu sana na karama ya neno la maarifa ili upate kujua kuna mahali panahitaji msaada. Pia inafanya kazi kwa karibu sana na karama ya neno la hekima kujua ni msaada gani unatakiwa, vilevile inafanya kazi kwa karibu sana na karama ya Imani kwa sababu mahali pengine unahitaji kufanya vitu kwa imani pasipo kuona ishara ya nje.
  Tumekwisha kujifunza kwamba kazi ya karama za Roho Mtakatifu ni kulijenga kanisa kwa hiyo kazi ya karama ya masaidiano pia ni kulijenga kanisa.

  Maeneo manne ya kukusaidia kuifahamu zaidi karama ya masaidiano.

  1. Inasaidia viungo vingine vifanye kazi yake katika kulijenga kanisa. Efeso 4:15-16; ” lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo”. Maana yake kila kiungo katika kanisa kina kazi yake. Karama ya masaidiano huwa haionekani kwa nje lakini ni karama ya muhimu sana.

  2. Inamsaidia mtu avuke kipindi chake cha mahangaiko asije akaacha kazi ya kulijenga kanisa. Matendo ya Mitume 9:1-19; anaeleza habari za Sauli (Paulo) akielekea Dameski. Katika mstari wa 8-9 anasema ” Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali wala hanywi. Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi ……..”
  Hapa tunaona Paulo (Sauli) alikuwa katika mahangaiko ndio maanahakula wala kunywa kwa siku tatu.
  Anania aliwekewa mzingo wa kwenda kumsaidia Paulo katika mahangaiko hayo na tunasoma kwamba baada ya kumsaidi aliondoka. Hii inatokea mara nyingi sana pale ambapo watu wanapata mahangaiko ya wito na hapa ndipo karama ya masaidiano inahitajika.

  3. Inamsaidia mtu mwingine afanikiwe katika wito alioitiwa na Mungu. Yohana 19:38-42; ”Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu (lakini kwa siri kwa hofu ya wayahudi) alimwomba pilato fuhusa ili auondoe mwili wa Bwana Yesu. Na pilato akampa ruhusa………..”.
  Hapa tunaona wanafunzi wa Yesu, baada ya Yesu kufa, hawakuonekana kumsaidia Yesu kwenda kuuhifadhi mwili wake. Lakini msaada wa aina ya pekee ulitolewa na watu wengine ambao hawakuwa wanafunzi wa karibu sana na Bwana Yesu wakati wa maisha yake. Hii ni karama ya masaidiano ilishuka ndani yao kwa ajili ya kukamilisha wito wa Bwana Yesu.
  Mfano: katika eneo kama hili ndipo watu wengine wanapewa mzigo kwa ajili ya utoaji (very specific giving) ili kusaidia kazi ya Mungu isilale, na hii inafanyika bila kujadiliana na yule anayesaidiwa. Hii inatokea hata kwa waombaji ambao wakati mwingine Roho Mtakatifu anaweka mzigo ndani yao ili kuombea tukio (event) fulani tu.

4. Inamsaidia mtu mwingine akubalike katika wito wake. Ukisoma Matendo ya Mitume 9:26-29; anazungumza habari za Sauli alipofika Yerusalemu, tunasoma kwamba alijaribu kujiunga na wanafunzi lakini walimwogopa. Lakini Barnaba, ambaye aliinuliwa na Mungu ili kusaidia, alimtwaa akampeleka kwa mitume na kumtambulisha.

Karama ya aina za lugha

Ili karama zifanye kazi kwa haraka weka ndani yako kiu ya kuona Yesu anatukuzwa. Mambo muhimu kuhusu karama ya aina za lugha:-a. Hizi lugha zinazosemwa ni za aina gani? Ukisoma I Wakorintho 13:1; anasema ” nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao”. Maana yake Roho Mtakatifu anaweza akakuletea lugha ya wanadamu lakini siyo ile ambayo umejifunza. Na pia anaweza akakuletea lugha za Malaika.b. kuna tofauti ya kunena kwa lugha kwa kila aaminiye na kunena kwa lugha kama karama. I Wakorintho 12:29,30 anasema ”Je wote ni Mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?”Maana yake si kila mtu anapewa kufanya haya yote yaliyotajwa, si kila mtu hii karama ya kunena kwa lugha, inatokea kwake kila wakati, ila ni pale ambapo Mungu anaona panahitajika karama hiyo.Mfano: karama hii inaweza kukusaidia pale ambapo hufahamu lugha fulani na unahitajika kupeleka ujumbe kwa lugha hiyo.Kwa upande mwingine kuna kuna kunena kwa lugha kama ishara. Marko 16:17; ” na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watesema kwa lugha mpya”. Hapa anazungumza kunena kwa lugha kwa kila aaminiye na sio karama.I Wakorintho 14:5; anasema ”nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha …….”. Maana yake kunena kwa lugha kama ishara kwa kila aaminiye na siyo karama kwa sababu anenaye kwa lugha anahuisha nafsi yake.

___________________________________________________

Mwl Christopher Mwakasege

DHAHABU

NAPENDA DHAHABU!

Nikifikiria kuhusu Mbinguni, naona Dhahabu. Kwa kweli napenda sana dhahabu na hata nilichagua rangi ya dhahabu kuwa rangi ya mavazi na mapambo yaliyotumika katika harusi yangu. Ni rangi nzuri sana nami ndiyo ambayo huwa naipendelea. Rangi hii hunikumbusha kuhusu Mungu!

 JE!, UNAJUA?

Ili dhahabu isafishwe, ni lazima ipitishwe kwenye moto mkali. Moto huu ndio husafisha dhahabu, kwa sababu hutenganisha uchafu wote kutoka katika dhahabu hiyo. Uchafu wote ukiungua, hubaki dhahabu iliyosafishwa. Msafisha dhahabu huweza kujua kuwa dhahabu imeshakuwa safi ikiwa ataangalia katika dhahabu iliyosafishwa naye akajiona uso wake, kama vile katika kioo. Njia hii ya kusafisha dhahabu kwa kutumia moto ndiyo njia pakee ya kusafisha dhahabu na hakuna mbadala wala njia ya  mkato.

Kama vile msafisha dhahabu anavyoweza kujua kuwa dhahabu yake sasa iko safi kwa kujiangalia ili ajione uso wake, nasi twaweza kujua kuwa tunaelekea kufanana na Mungu wakati mtu anayetuangalia tunapopitia katika majaribu na mateso atajiona kupitia maisha yetu.

Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako.  Zaburi 26:2-3

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza na ukamilifu. Warumi 12:2

Unajua kuwa unafanana na Mungu wakati unapokutana na majaribu na kukimbilia upande wa pili. Unapoweza kujizuia kufanana na dunia, halafu ukachagua kumruhusu Roho mtakatifu afanye upya fikra zako. Unapoweka mbali kila kipingamizi cha fikra kinachokuzuia katika kutekeleza wito wako, na wakati unapokuwa umetumia nguvu zako zote katika kuitikia wito wa Mungu kwako. Unapokuwa una hofu ya yajayo, lakini bado unaweza kuruhusu Mungu aongoze mipango yako. Wakati hofu inapokuwa imekuzunguka lakini ukakataa kuiruhusu iteke fahamu zako. Wakati kila mmoja yuko kinyume nawe lakini una amani kwa kuwa unajua Mungu yuko upande wako, hapo ndipo UNAPOWEZA KUJUA , kuwa unasafishwa ili utoke ukiwa DHAHABU!

Ni wangapi wetu ambao wamewahi kupitia katika hali ngumu, na hatimaye kugundua kuwa hali ya kumtegemea Mungu inaongezeka zaidi na pia uhusiano baina yetu na yeye unakuwa bora? Mungu huwa hatuachi, Yeye yuko nasi kwa ajili yetu! Nafikiria wakati Shadraki, Meshaki na Abednego walivyotupwa kwenye tanuru la moto. Hawakuwa peke yao. Mungu alikuwa humo humo kwenye moto, pamoja nao.

Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara, na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu. Daniel 3:25

Ni jinsi gani ni jambo la kufariji kujua kuwa Bwana yule yule aliyekuwa na hawa watu watatu yuko hapo hapo kwa kila mmoja wetu alipo! Kilicho cha kushangaza sana kwangu ni kuwa hata katika nyakati za majaribu makubwa zaidi katika maisha yetu, ingawa ni lazima tupite hapo, hatupo peke yetu!

Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, Yeye aliyekuumba, Ee Israel, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa, nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe, na katika mito, haitakugharikisha, uendapo katkia moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Isaya 43:1-2

Fikiri kuhusu jambo hilo. Mungu hufanya nini tunapoingia katika kipindi cha kujaribiwa nasi tukapaza sauti kumlilia kwa ajili ya msaada? Kwa njia moja au nyingine, Yeye huwaokoa watoto wake.

Wenye haki hulia na BWANA husikia, naye huwaponya na tabu zao zote. Zaburi 34:17

Nilitaka kuwashirikisha kidogo mahali moyo wangu ulipokuwa nilipokuwa naandika wimbo huu (tutakaousoma huko mwishoni). Nilipata maono asubuhi moja ya wingu kubwa la kijivu lililokuwa likiingia na kutoka katika madirisha ya nyumba na majengo…….Nililiona liingia katika chumba cha mama mmoja aliyekuwa amekaa katika dawati akifanya kazi, huku akionekana amechoka na kulemewa na mawazo; halafu katika nyumba ambayo nilimuona mama aliyelemewa na kukata tamaa na hali ngumu ya maisha;  Nililiona likiingia katika darasa ambalo mwalimu alikuwa amechoka  na wanafunzi waliokuwemo darasani humo wakiwa wenye tabia mbaya kabisa; katika hospitali zilizojaa kukosa matumaini; na makanisa ambayo wachungaji wake walikuwa dhaifu, wameishiwa nguvu na wako tayari kukata tamaa! Yalikuwa ni maono ya kuogofya!

Nilianza kuomba katika roho, na kisha nikamuuliza Mungu, Kwa nini? Kwa nini alikuwa ananionyesha yote haya? Yalikuwa maombi yasiyo na matumaini lakini nilijua tumaini lipo. Ghafla nilijisikia Uhitaji wa kushirikisha watu kwa neno rahisi “USIKATE TAMAA!”

Kwa ye yote anayesoma ujumbe huu, na amekuwa akibeba uzito wa  majaribu na mateso ya maisha; hata kama ni ugonjwa, kupotelewa na wapendwa, kupoteza kazi, matatizo ya kifamilia na ndoa, ndoto zilizoyeyuka, au pengine unajisikia kukosa matumaini na kukata tama, una huzuni, unajisikia kukandamizwa na kushindwa: USIKATE TAMAA! USIKATE TAMAA! Kuna TUMAINI!

Ziangalie mbingu! Itafute Kweli! Ufahamu Ushindi wenyewe ulivyo! Majaribu haya, moto huu ni kwa ajili ya kujenga tabia ya ki-Mungu ndani yetu ili kuleta maishani mwetu Subira, Uvumilivu, Kudumu na Kuendelea katika Mungu. Yote hayo yakiwa na lengo la Kusafisha Imani yetu na kuondoa au kusahihisha udhafu ndani yetu!

Majaribu haya yanadhihirisha kuwa Imani yako ni halisi. Hapo Imani inasafisha kama vile moto usafishavyo dhahabu – ingawa Imani yako ni ya thamani sana ikilinganishwa na dhahabu. Kwa hiyo Imani yako ikiendelea kuwa imara hata baada ya majaribu mengi, itakuletea sifa nyingi na utukufu na heshima katika siku ile Bwana wetu Yesu Kristo atakayodhihirishwa kwa ulimwengu wote. 1Pet 1:7

Utapita katika katika majaribu, maumivu, kukataliwa, uchungu, kudhihakiwa, kuzomewa, kunyanyaswa, kuchekwa, kuchukiwa, kuumizwa na hata kuwa na utayari wa kuuawa kwa ajili ya Kristo. Huku ndiko kunakoitwa “ Dhahabu inasafishwa kwa Moto”.

Lakini yeye aijua njia niendeayo, Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.  Ayubu 23:10

Katika miaka michache iliyopita nimepitia hali hiyo ya “kupita kwenye moto” katika baadhi ya majaribu yangu magumu kabisa, yaliyohusu mashambulizi katika familia yangu, tabia yangu na Huduma. Nilijisikia kutendewa isivyostahili, Kuwakilishwa isivyostahili na Kueleweka vibaya. Nilijisikia kuvunjika moyo na kukatishwa tama, kuchukiwa na kukataliwa. Katika yote hayo nikajifunza kuwa kusimama kwa ajili ya Kweli kuna gharama. Kuna watu watasikia na kushangilia, wengine watachukia na kuogopa. Wakati Mungu anaanza kukuinua juu, wapo wale ambao husubiri kukurudisha chini, kwa kiburi chao, wivu na ubinafsi. Kama unafanya jambo ambalo linaleta changamoto kwa wengine, hali kadhalika tegemea kupatwa na changamoto. Mungu anapokuwa amekutenga (amekuweka maalumu kwa ajili yake), dunia haiwezi kufurahia nafasi hiyo uliyowekwa kwa kuwa inasababisha hatia kwao. Ilinibidi pia kupitia hali hiyo ya kujisikia hatiani na ukweli unaouma, jambo ambalo lilinielekeza katika hali ya kuumiza lakini nzuri sana na halisi kabisa ya Kutubu. Ilinibidi kukubali kuwa mimi pia ni binadamu na najisikia kuchoka, na kupungukiwa nguvu. Nilijisikia kukandamizwa kunanijia lakini nilishinda. Nimejifunza kupiga vita ndani yangu kwa kutumia Upanga wa Roho, nikikataa kukatishwa tama ili nisonge mbele kuelekea thawabu yangu. Mungu ameendelea kuwa Mwamba na Ngome yangu, Amekuwa Mkombozi wangu na Bwana wa Majeshi, Mshindaji. Amebaki kuwa mwaminifu na kunipitisha katika nyakati za udhaifu wangu, Hakuniacha nikimbie wala kukata tama. Kwa kweli amekuwa akinivuta juu zaidi. Amenitembeza katika Bahari ya Shamu na kunilinda na adui zangu. Nimeona miujiza, ishara na maajabu! Nimeshuhudia maongezeko Yake, Wema na Baraka. Ninaamini nina nguvu zaidi! Nimekuwa mpiganaji bora! Naweza nikachukuliana na mengi zaidi. Naweza kupigwa ngumi! Naweza nikasukumwa chini, lakini nikainuka wima tena! Sikati tamaa kwa kuwa Siko peke yangu! Nina lengo! Nina ushindi uliohakikishwa, bila kujali utagharimu kiasi gani!

Nakaza mwendo, niifikilie mede ya dhahabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. Filp 3:14

Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu. Mdo 20:24.

Tena tusichoke katika kutenda mema, maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Gal 6:9

Matunda ya kujaribiwa kwetu yataongeza zaidi na zaidi thamani yetu katika ufalme wa Mungu. Hivyo, basi, na tuwe na ujasiri kuwa matatizo yetu ya sasa yatakwisha, na mwisho wake utakuwa mzuri. Amebarikiwa mtu yule astahimiliye majaribu. Kwa sababu akishakukubaliwa, ataipokea taji ya uzima ambayo Bwana amewaahidi wale wampendao. Yakobo 1:12

Mashairi ya Wimbo wa DHAHABU:

 ****Kisichoweza kukuua hicho kinaweza kufanya uwe na nguvu zaidi!

Nimepigwa mara kadhaa, lakini ni mzima, na unajua ninasomga mbele!

Nimeshaangushwa chini, lakini nikasimama tena, na wala sikimbii!

Kwa hiyo ninachukua muda kushukuru, kwa namna ambavyo nimeongezewa nguvu!

Kwa kupita katika moto, lakini nikatoka nikiwa DHAHABU!

Na ninaendelea juu zaidi, miguu yangu ikiwa bado imesimama sakafuni.

Nilisukumwa nyuma, Nikasukumwa chini, Nikasukumiliwa mbali,

Lakini ni sawa tu maana ninazidi kuendelea mbele!

Kupigwa kwa maneno, kila neno baya walilonisemea,

Hiyo hainifanyi nifikirie. Hapana!

Kwa hiyo ninachukua muda kushukuru, kwa namna ambavyo nimeongezewa nguvu!

Kwa sababu naweza kuchukua maumivu, ambayo hata hivyo ni kwa faida yangu,

Kwa sababu sitavunjika, Upendo umenikamatisha.

Moto huu unanifanyba bora zaidi, nimesafishwa bila kujali kama,

Naonekama kama aliyeshindwa, kwa sababu nitawaonyesha kuwa mimi ni mshindi!

Mnaweza kuchukua vyote kwa sababu mimi ni mtoaji,

Lakini sikati tama wala sikimbii!

Kwa hiyo ni heri mkajua, Nitatoka nikiwa DHAHABU!****

Dunia inahitaji kutuona, mimi na wewe, tukisimama imara wakati wa kusafishwa na moto, kisha tutoke tukiwa DHAHABU.

USIKATE TAMAA!

Nawapenda,

—Beckah Shae–

Tazama kwa jicho la Imani!

Tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele ( 2 wakorintho 4:18 )

Imani ni ya roho, siyo ya hisia. Kama wakristo tunatawala na kushinda katika maisha katika kanuni za imani. Tunafikia mafanikio yetu, ushindi, maendeleo katika maisha kwa kuchochea kanuni fulani za kiroho ambazo tunapata katika Neno la Mungu. Moja ya kanuni hizo ni kuona kwa ”jicho la Imani” kuuona muujiza wako kwanza ndani; hiyo inaitwa ”KUONA VISIVYOONEKANA!”

kabla ya kufunuliwa kimwili kwa Utukufu na Nguvu ya Mungu katika maisha yako, unapashwa kuona kwanza ndani yako. Mara tu unapoweza kuona katika roho yako kwa macho ya imani, basi kitu hicho tayari ni chako.

Huwezi kuwanacho nje kama hujawa nacho kwanza ndani. Hapa ndipo baadhi wamekosa, wanataka kuona kwanza kwa macho yao ya kimwili kabla ya kuita halisi kile ambacho. Mungu ameahidi. Hiyo siyo imani

Imani ni kuita halisi kile ambacho hisia za mwili haziwezi kutambua.

Ni kama mwanamke mjamzito; itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kusema, ” Mimi simuoni mtoto; hiyo inamaana kwamba hakuna kitu katika tumbo lake.” Mtoto yupo ndani hata kama hakuna mtu anayeweza kumuona. hata kabla ya tumbo kuwa kubwa, mtoto alikuwepo ndani wakati wote.Tumbo limekuwa kubwa tu kwa sababu mtoto ambaye yupo ndani tayari  anakuwa mkubwa. Wakati wa mwisho wa kipindi cha ujauzito mtoto atazaliwa.

Katika njia hiyo hiyo, huo ujauzito wa muujiza ulionao hiyo baraka ambayo umekwishaona na kuchukua milki yake katika roho itakuwa wazi na  kutukia kama ukikataa kusita na kuyumba katika imani yako. Kwa macho yako ya imani, ona hiyo kazi mpya unayoitaka, ona mafanikio yako, afya, amani na maendeleo,wokovu wa marafiki na wapedwa.

Anza kutangaza kwa kinywa chako hayo ambayo umeshayaona ndani; siyo ili yatokee, bali kwa sababu unajua  kwamba katika  ulimwengu wa Imani tayari yapo!

Malkia Pamela

Maana ya Wokovu – CASFETA

Utangulizi
Wokovu unahusisha hali ya usalama, uhifadhi, uponyaji au kutoa kitu kutoka katika hali isiyo na usalama, nzuri na kupeleka katika hali iliyo nzuri au bora zaidi. Katika maisha ya Mkristo wokovu ni muhimili wa maisha yake kwa sababu ya historia ya mwanadamu.

Inafahamika kuwa mwanadamu aliumbwa katika hali ya ukamilifu, na isiyokuwa na dhambi, Mwanzo1:26. Mungu alimkusudia mwanadamu aishi maisha yaliyojaa hali ya utawala ndani yake. Alimtaka mwanadamu awe shirika naye katika tabia ya Mungu. Mwanadamu huyo alikusudiwa aishi sawasawa na neno la Mungu. Kwasababu neno la Mungu ni kile alichokisema/anachokisema Mungu juu yako. Wanadamu wa kwanza Adam na Eva wakalisikiliza neno la Shetani na kulihalifu neno la Bwana. Kosa walilolifanya Adam na Eva ndilo linaloendelea kutendwa siku za leo kwa wanadamu kushindwa kuisikiliza sauti ya Mungu wao.

Anguko la mwanadamu lilileta kifo cha kiroho na kimwili. (maana ya kifo ni kutengana) Mwili na roho vikitengana ni kifo cha kimwili, Roho na Mungu vikitengana ni kifo cha kirohoMwanzo 3:15 Mungu anatoa unabii wa wokovu kwa mwanadamu aliyepotea. Ifahamike kuwa baada ya mwanadamu kuanguka alianza kutafuta njia mbalimbali za kumrudia Mungu ambazo hazikuzaa matunda. Jambo ambalo lilizaa dini mbalimbali.

Dini – Ni mpango wa wanadamu kumtafuta Mungu
Wokovu- Ni mpango wa Mungu kuwatafuta wanadamu Yoh 3:16

Wokovu ni tukio linalohusisha mwanadamu kutambua kuwa amemwacha Mungu na kutubia uasi huo kwa toba ya kweli, ambayo itazaa badiliko ndani yake, litakalosababisha asirudi tena katika maisha ya kale na kumwezesha kufikia kilele cha nia ya Mungu, yaani kuishi na Mungu milele. Yoh. 3:8a Kutokumtii Mungu huzaa kitu kinachoitwa dhambi, na dhambi ni uasi dhidi ya Mungu. Ni kushambulia sehemu ya utakatifu na heshima ya Mungu, dhambi inapozoeleka huitwa uovu. Uovu unapomfikia Mungu huzaa ghadhabu ya Mungu, na ghadhabu ya Mungu huondolewa kwa malipizi.

Wanadamu wengi hujiuliza kwanini Mungu asingetangaza msamaha bure kwa watu wote, bila hata kazi ya msalaba? au kwanini Yesu amekuja na watu watubu? Mungu ana sifa nyingi lakini katika hili ana sifa za kipekee tatu zinazomfanya asishawishike kumwesabia mtu mwenye hatia kuwa hana hatia Kutoka 34:6-7 Rumi 2:4-16

(1) Mungu ni Mtakatifu
Kwa asili anapingana na kila kitu kinachoitwa dhambi, Dhambi ni kushambulia utakatifu wa Mungu na heshima yake, Kwahiyo mtu yeyote anapofanya dhambi anajihusisha na kutengeneza silaha ya kupambana na uungu wa Mungu.Pia wanadamu wanapofanya dhambi wanakuwa ni waamuzi wa nafsi zao wenyewe. Kwasababu hiyo ni miungu/ bwana wa nafsi zao. Kwa maana nyingine dhambi ni kukomesha utawala wa Mungu katika maisha ya mtu. Kwa hiyo kuwaachilia wanadamu wote kuendelea kufanya dhambi ni Mungu kujitangaza kuwa yeye si Mungu kati ya wanadamu. Na Mungu ana wivu na kila kitu kinachojiinua kutaka kuchukua nafasi yake. Kwahiyo lazima uovu ukichipua kwa wakati wake uadhibiwe. Ili Mungu abaki kuwa yote katika yote (Absolute controller)

II. Mungu ni mwenye haki
Haki ya Mungu inamadai mbele za Mungu kumtaka atimize Neno lake sawasawa na alivyosema. Inakumbusha Mungu kutoa Malipo kwa kadri ya matendo. Zab 34:15-16. Kutokutimiza neno lake ni kumfanya kuwa muongo na kigeugeu. Na kamwe hatakuwa hivyo. Ikiwa amesema mshahara wa dhambi mauti. akiwatangazia Adamu na Eva kuwa siku mtakayo kula matunda ya mti wa katikati kufa mtakufa hakika. Haki ya Mungu inasimama kudai kutimizwa. “Ogopa sana Mungu anaposimama kwenye haki yake” Hakikisha muda huo upo upande wake maana ni hatari.

III. Mungu ni mwenye rehema
Laiti Mungu asingelikuwa na rehema maisha ya mwanadamu yangaliishia bustani ya Edeni. Kwa mujibu wa aya mbili zilizotangulia mwanaamu hakustahili kuishi, lakini ajabu ni kuwa rehema za Mungu zinafanya kazi ya kumshikilia Mungu asiachilie ghadhabu yake kwa upesi, Hapa ndipo tunapoongezewa muda wa sisi kutubu Zab 100:5.

N:B. Rehema za Mungu zinakikomo. ili kuruhusu Mungu kujilipizia kisasi (Usichezee kipindi cha rehema).

Sababu hizi zinatufanya tuone kuwa kumbe asili na umbile la dhambi ya mwanadamu ilikuwa inatangaza mauti yake. Ndipo tunapopata Yoh 3:16 upendo wa Mungu wa agape. Aliupenda ulimwengu hali ukiwa umejaa dhambi na uovu. Akaandaa mipango mwenyewe udhubuti wa wokovu.

Kosa la Adamu na Eva lilizaa kizazi kilichoanza kuwa na asili ya dhambi (mtaji wa dhambi) yaani mtu akiwekwa katika mazingira ya dhambi anaweza akafanya dhambi. Yesu anakuja ndani ya mtu kuleta dawa ya kuondoa asili ya kuasi/ kipingana na Mungu ndani ya Mwanadamu.

NB Kuna imani zinasema tunazaliwa na dhambi ya asili lakini imani yetu ya kipentekoste inasema tunazaliwa na asili ya dhambi. Yaani dhambi haijafanywa na sisi. Ila tumepokea asili ya dhambi ambayo kwahiyo inatoa mtaji wa kufanya dhambi popote panaporuhusu.

Sasa: Yesu ni mdhamini wa agano jipya

Sifa za mwokozi
(I) Alitakiwa kuwa mtu wa karibu na mwanadamu, mwenye kuwajua na kuwaelewa wanadamu (Yesu akazaliwa kama mtu, akachukua mwili)
(II) Alitakiwa awe na uwezo wa kulipa gharama. (Alitoa damu isiyo na hatia)
(III) Alitakiwa kujitoa kwa hiari (nitume mimi Bwana)
Wokovu ulianzishwa na Mungu Baba ukaletwa kwetu na Mungu mwana na unapokelewa kwa Roho.

Ni neema ambayo inapatikana pasipo mtu kuitaabikia, Kwa hali ambayo mwanadamu alikuwa nayo haiwezekani kujiokoa mwenyewe kwa jinsi yoyote. Fikiri hivi
(i) Mwanadamu mwenye Mungu
- Moyo umejaa Mungu
- Anatembea nuruni
- Sauti ya Mungu ikisemwa, ndani yake yumo Mungu (kunatengeneza mazingira ya makubaliano)

(ii) Mwanadamu Mwenye dhambi
- Moyo umekaliwa na shetani
- Anatembea gizani
- Sauti ya Mungu ikisema, ndani yake yumo shetani. Hakuna mzingira ya makubaliano kati ya Sauti ya Mungu na moyo wake. Ndiyo Maana inahitajika aliyejuu ya yote mwenyewe aingilie nyumba hii amkamate mwenye umiliki amtoe nje, aweke makazi yake (Mungu) ndipo mwanadamu huyu aanze kusikiliza Mungu anasema nini kwa ajili ya maisha yake.

Tukio hili linatupa kuamini tumeokolewa bure kwa neema hakuna kazi tuliyoifanya. Ila deni yetu yote Yesu aliilipa Msalabani Isaya 53. La muhimu kwetu ni maamuzi ya kuamua ama kuokoka au kutookoka ila huruma na rehema za Mungu ni tele.

NB: huu ni ufupisho, inahitaji maelezo mapana kujua nini kmefanyika unapookoka ili usirudi tena ulikotoka. Wokovu unapokelewa kwa toba inayohusisha

- Kumwamini Yesu ya kuwa ndiye njia pekee ya Mungu kuwakomboa wanadamu Rumi 10:9
- Toba- ni huzuni ya kweli juu ya dhambi na juhudi za makusudi ya kutokutenda dhambi hiyo tena.
- Ni kuichukia dhambi kiasi cha kuiacha
- Ukiona mtu ametubu kisha anarudi rudia yale ya zamani, anakuwa hajazaa matunda yapatanayo na toba.
- Wokovu pia unahusisha kutambua nini kimefanyika katika maisha ya mtu (kuzijua haki zake ili asiishi tena kama mtumwa kwenye nchi yake mwenyewe.
- Wokovu unahusisha kuhamishwa kutoka kwenye ulimwengu wa giza kuingia kwenye ulimwengu wa nuru
- Kanuni za ulimwengu huu ni kila mtu kuishi chini ya utawala wa Bwana wake (Utawala wa Nuru ni neno la Mungu, utawala wa giza ni neno la Ibilisi (uovu)
- Asije mtu akafanya dhambi na kuhisi kuwa ufalme wa Mungu utamhifadhi (It will never happen) Efeso 2:1
Tunapookoka roho zetu zinarudishiwa uhusiano zilioupoteza mbele za Mungu
Lakini nafsi zetu kwakuwa ziliharibiwa na utu wa kale tunazigeuza kwa neno la Mungu. kweli inatufungua kila iitwapo leo.

Lakini miili yetu tuaitoa dhabihu na kuisulibisha ikubaliane na kweli. Maana mara zote mwili hautatupa ushirikiano sana lakini tunaisulubisha imfuate Kristo. Nafsi ni kiungo kati ya roho na mwili ila inategemea sana nguvu iliyopo katika roho au mwili ili nafsi ifanye kazi.nafsi inaendeswa na Maamuzi yanayofanyika ama ktk mwili au roho Baada ya kukiri wokovu anahusisha yale yote tunayoyafanya mpaka tunaingia mbinguni

- Hivyo basi tunaweza tukagawanya wokovu katika makundi ya wakati (yaani nyakati tatu) za misingi katika maisha yako.uliopita, uliopo, ujao.

Yaani – ulifanya nini (ulikiri)
- Unafanya nini (unaishi maisha matakatifu)
- Utapata nini (Nitakwenda kukaa na Bwana milele)
Inashauriwa: Ni vyema sana ukasoma vizuri kitabu cha Yohana na kisha warumi, Vitabu hivi vinamjengo mzuri wa kimafundisho ya kukua katika wokovu

Daudi katika roho anayoona hayo katika Zab 32 na kukiri “Heri aliyesamehewa makosa yake ……..” Luka 1:73, 2kor 5:17 yakale yote yemepita.
Baada ya kuokoka tunaambiwa kuwa ya kale yote yemepita
- Hakuna nguvu ya dhambi juu yetu tena
- Magonjwa hayana nafasi
- Laana haziwezi kutufuatilia kabisa

NB: Kunabaadhi ya imani zinazosema umeokoka lakini hauja kombolewa. Hivyo kujihusisha na kuvunja laana.
Elewa Hivi – Kazi ya msalaba ilitosha kutufanyia matukio yote mawili
Laana ililetwa na dhambi
Magonjwa yaliletwa na dhambi.

Alichokifanya Yesu ni hiki
(i) Kulipa Deni – Ndiko kukombolewa
(ii) Kutuhamisha – Ndiko kuokoka
Kwa hiyo haya ni matukio mawili yanayofanyika mara moja
Kumwambia mtu umeokoka bali huja kombolewa ni kusema tumekutoa jela lakini bado unadaiwa madeni laazima uyalipe.
Sisi tunaamini deni ya dhambi ilimalizikia msalabani Yesu akitangaza imekwisha kazi ya kumuokoa mwanadamu
- Kinachobaki baada ya kuokoka ni mtu kuifahamu kweli, na Yesu akatuhakikishia ya kuwa mtaijua kweli na hiyo kweli itawaweka huru.
Kwahiyo basi.

Maeneo matano muhimu ya nguvu za mwamini, Ni muhimu mkristo akayajua haya kwasababu ndipo hasa chemchem za nguvu na uhai wa kiroho na hapa ndipo watu wanapopaharibu na ghafla kuonekana hawapo kiroho.

I: MAOMBI
Ni mazungumzo baina ya mwanadamu na Mungu. Ni sehemu ya ibada ambapo mwanadamu anatulia chini ya uwepo wa Mungu na kuzungumza naye.
NB kunatatizo kubwa hapa katika nyakati zetu ambapo maombi yamekuwa ni one way traffic. Ni tukio la watu kumweleza Mungu bila kujua Mungu ananena nini. Zingatia yafuatayo (What are the demands for effective prayer)
- Maombi yanahitaji utakatifu
- Maombi yanahitaji muda
- Maombi yanahitaji kujitoa (Devotion)
- Maombi yanahitaji muendelezo (hayana cut is a continuation)
- Maombi yanahitaji utulivu (Uhusika wako)
- Maombi yanahitaji umakini
- Maombi yanahitaji ulijue neno la Mungu vizuri
- Maombi yanahitaji imani
- Maombi yanahitaji uhakika juu ya uwepo wa Mungu (kuna watu wanaomba kama watu wapiga kelele tu maana uwepo wa Mungu haupo hapo). Yaani hawajatengeneza mazingira ya kukutana na Mungu. Maana Mungu hashuki popote, hashawishiwi ila anaguswa.
Jumla ya hayo na mengine mengi yamezaa maneno mengi lakini matokeo hafifu.

(NB somo hili la maombi ni somo pana linahitaji nafasi yake). Lakini tunaweza kuyagawa katika maeneo mengi
Prayer at first level – Maombi ya kusikizisha dua, matatizo maombezi na kila aina ya kitu kilichopo katika fahamu.
Prayer at the second level –Maombi ya mtu aliyekomaa kiroho ya kutafuta kukaa na Bwana. Kujenga fellowship, kuutafakari ukuu wa Mungu uwepo na nguvu zake (Kumbuka Mungu ………… kwenye maombi primarily objective sio, kusikiliza shida zetu maana anazijua zaidi kuliko sisi.

II. NENO
Neno ndilo kiongozi wa maisha ya mkristo
- Utaomba sawasawa na neno
- Utafunguliwa kadri unavyolijua neno
- Utaishi neno
- Utasema neno ili ufanikiwe
Popote Mungu anapotaka kufanya kazi atalituma Neno.Alipotaka kuwakomboa wanadamu alilituma neno kutoka mbinguni likafanyika mwili, na Neno ni Yesu mwenyewe na ndiyo maana maandiko yanasema yeye aliyemwamini mwana anao uzima.Refer maelezo ya mwanzo.

III.ROHO MTAKATIFU
Mdo 1;8
Kama tulivyoona wokovu ukiandaliwa na Baba ukiletwa kwetu na Mwana ukipokelewa kwetu kwa Roho. Na ni vyema mkristo akaielewa personality(Unafsi Wa Roho Mt) ya Roho mt ili asipate shida wakati wa kuomba ujazo wa Roho Mt na namna ya kuishi naye.Wengi wamemchukulia Roho mt kama kitu cha namna Fulani ambacho baada ya kuomba kitakuja na kuingia kwa kushtukiza au nguvu Fulani. Lakini msingi ni kuwa Roho mt ni Mungu, ni zaidi ya nguvu, si kitu bali ni Mungu mwenyewe na uwepo wake akitembea na mtu.Kujua personality yaRoho mt kutakusaidia kuelewa kuwa Roho Mtakatifu anahisia, akihitajiwa, akipendwa anajua. Na pia akitendewa jeuri ana mwitikio. Hivyo Mungu hawezi kukuacha utaabike anaitaji tuu uelewa wako ili utembee vizuri na Roho mt.
Nani anampokea
-Aliyeokoka,
-Mwenye imani
-kiu
-Shauku
-Uvumilivu na utulivu
Ukimjua vizuri tamaa yako itakuwa sio aingie kwa kiwango gani bali ujitoe kwake kwa kiwango gani ili akumiliki.

IV.USHUHUDIAJI
Ushuhudiaji ni hali ya kuwaeleza wengine kile Mungu alichokifanya ktk maisha. Angalia mfano wa mwanamke msamaria alizunguka kijiji kizima akisema yale aliyeyaona.Hakuna mtu aliyetendewa jambo na Mungu ambaye aliweza kunyamaza kimya.Lakini zaidi ushuhudiaji ni agizo kuu math 28;19 Marko 16;15
Kutoshuhudia ni dhambi kama zilivyonyingine.
Umuhimu wa kushuhudia
-Ni changamoto ya kuishi maisha matakatifu
-Ni kuendelea kushiriki kazi ya upatanishi kati ya Mungu na wanadamu, huduma ambayo tumepewa 2kor 5;19
-ni kuendelea kuujenga ufalme wa Mungu duniani

V.SADAKA NA MAFUNGU YA KUMI
Katika kukamilisha ibada, sadaka ni jambo la Muhimu na ni agizo la Mungu mwenyewe kuwa tusiingie nyumbani mwake mikono mitupu, tunaheshimu kuwa Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata mali na tupo tayari kumtumikia Mungu kwa nguvu zetu zote, akili zetu zote lakini pia kwa mioyo yetu.Hatumpi Mungu kwasababu anahitaji, au kama tusipotoa tutakwamisha kazi yake.Huo ni mtizamo mbaya ambao ndani yake hauna Baraka.
Nitoe namna gani
-Kwa moyo wa uhiari na kupenda
-Kutoa kitu kisicho kidhaifu kulingana na uwezo wako
-Kutoa kwa nia njema na safi
-Kutoa kitu ambacho kitaugusa moyo wa Mungu
-Kutotoa kwasababu ni kawaida kutoa katika muda na sehemu hiyo lakini kwasababu ni ibada.
Fungu la kumi
Ni sehemu ya kumi ya kila tunachokipata, Ni agizo la Mungu kuwa sehemu hiyo ni takatifu kwaajili yake.Hii ni laazima kuwa makini nayo kwasababu tangu zamani hakuna mtu aliyekula kitu kitakatifu akabaki salama.Na sehemu hii inatolewa ktk kanisa lako linalokulea (local church)

Nb
Kifupi wokovu unasura ya nje na ndani
Nje – Ni namna unavyoenenda
Watu wanavyokusoma/ au unavyosomeka (kumbuka sisi ni Barua ya kusomwa na watu wote)
Ndani – Ni namna ya wokovu kiuhusiano na Mungu
Namna Mungu anavyokusoma/ unavyosomeka. (Maana yeye huichunguza mioyo na kuvipima ..)
Sasa kuna kanuni moja ya kufanikiwa kiroho kama tunataka kuendelea kiroho. Nje yetu ya kiroho lazima ifanane sana na ndani yetu ya kiroho. Namna tunavyojihudhurisha mbele za Mungu sawasawa na tunavyoonekana nje. Mfano. Mafarisayo waliikosea kanuni hii wakasubstitute external outlook na viwango vya kiroho vya ndani
Wakaingiza maisha mema nje lakini ndani yao hawana Mungu.
Wokovu ni kuishi maisha halisi sio kuigiza uhalisi
Wokovu ni kufanya kwelikweli sio usanii
Mungu anatuchunguza pande zote mbili yaani undani wetu na unje wetu
Ndani yetu anatakiwa kuumbika kristo ambaye atachonua na kuonekana nje

Wokovu unaharibiwaje
Kwa mtu kuanza kuonyesha tabia zisizokuwa na uzima /za kimungu
(i) Kutokuitii kweli kwa bidii
(ii) Kuanza kuvutiwa na mambo ya dunia
(iii) Kuona mambo ya kimungu ni mzigo mzito
(iv) Kuanza kufuatisha aina ya maisha ya watu wa dunia hii
(v) Kushindwa kulinda fahamu zake na kuruhusu uchafu ambapo unamnyima Mungu kutembea naye
(vi) Kutokuwa na bidii katika yale anayofahamu kuhusu Mungu
(vii) Kuanza kupata uwezo wa kutetea mambo ya kipagani na kutaka kuyahalalisha kuwa ni ya Kimungu kwa sababu yeye anayafanya.
(viii) Kuigiza wokovu – nguvu za Mungu, utakatifu etc.

Uhusiano wa wokovu/ karama za rohoni na kukua kiroho
Baada ya mtu kuokoka anaweza kupokea karama za rohoni na kuanza kutumika kwa nguvu pengine kuliko hata waliomtangulia kwa kadri ya kiu, shauku kuu na kujitoa. Lakini haimaanishi kuwa amekua kiroho. Kukua kiroho kunahusisha tabia za kristo kuanza kuonekana katika maisha ya mwamini.

Tunda la Roho Galatia 5 kujifunua katikati ya watu. Unaweza ukatumiwa kwa karama nyingi lakini nyenyekea chini ufundishwe yaani ukubali kufundishika ili uukulie wokovu vyema na kuwa chombo kinachofaa kwa kila kazi njema.
Wengi wamezolewa katika eneo hili kwa kuinuka kinyume na watu walio walea kiroho.
Kanisa la Wakoritho lilikuwa na tatizo hilo. Walisisitiza sana karama za rohoni kuliko tunda la roho. Walikuwa ni watu waliokiroho kwa utendaji wa kazi za Mungu lakini waajabu katika maisha yao ya kawaida.
Paulo hakuwakataza kuwa na karama za rohoni lakini anawaonya kuwa mambo haya yanafanyika kwa utaratibu.

KILELE CHA WOKOVU
Baada ya kukiri na kuishi maisha safi tunatarajia siku moja Bwana wetu atakuja kutuchukua ile Yeye alipo sisi nasi tuwe hapo.Biblia inasema kila aliye na matumaini haya ktk yeye hujitakasa.uf 22;20

Heri Yule aliyealikwa katika karamu ya harusi ya Mwana kondoo.

source: CASFETA-TAYOMI MLIMANI BRANCH –DOCTRINE COMMITTEE

Preserving Lives

The Essence of Your Chariot
God told Isaac not to go to Egypt, but to stay in the land of the Philistines where he was, irrespective of the famine in the land. And the Bible says in that same year of famine, Isaac reaped a hundred-fold (Genesis 26). When you discover that your office or the company where you work is having financial difficulties, pray for its prosperity, for in its prosperity, you will also prosper. This is the same thing God told the children of Israel when they were exiled in a strange land (Jeremiah 29:7).

Can God trust you to preserve the lives of those you come in contact with in your chariot of life? Look at the man Joseph; he had dreams as a kid, he saw the sun, the moon and eleven stars bow down before him and he told his family about it. The Bible says that Jacob his father thought about those things and kept them in his heart. Then one day, he asked Joseph, “Do you really mean that your mother, your eleven brothers and I will bow down before you?”

His brothers hated him because of his dreams and the preference their father had for him. Then one day, his father sent him to inquire of the welfare of his brothers in the field. When he found them, they seized him and wanted to kill him but later changed their minds and sold him to a band of travellers. These travellers then sold him to an Egyptian named Potiphar. Joseph became Potiphar’s slave, but God was with him (Genesis 37-39).

This is why you must not be anxious about what happens to you in this world. God is a master strategist and He is with you. After they sold Joseph, things went really bad for him. He was sold to Potiphar, who made him the governor of his own house. One day Potiphar’s wife attempted to sleep with Joseph but he fled for his life. Potiphar’s wife, being grieved, lied against Joseph, accusing him of attempted rape and this landed Joseph in prison. And though he spent thirteen long years in the dark, he held on to God.

Don’t worry if someone lies against you, God is still in charge and He will ensure that everything works out for your good. Joseph trusted in the God of Abraham, Isaac and Jacob. And in that dark place God gave him a supernatural gift of understanding and interpretation of dreams. The king’s baker and butler were thrown in jail, and soon enough God knocked them out with dreams and gave the interpretation to Joseph, and he interpreted their dreams.

The events that followed confirmed his interpretations. Afterwards the butler was released and Joseph told the butler to remember him. Though the butler promised to, he promptly forgot about him when he got out. The same may apply to you today. But when you’re forgotten, count it all joy as you go through divers trials and tests. God is planning to do you good!

At the end of the second year after the butler’s release, God stepped into Pharaoh’s palace one night and gave him a dream. When all his magicians could not interpret it, the butler remembered Joseph that day. And because of the witness the butler gave about Joseph’s ability to interpret dreams, the king sent for Joseph from the prison house.

I believe when Joseph heard the sound of the padlocks, he knew he was coming out of the prison that day, because the Bible says he shaved himself. Shaving was a very wise step for Joseph, because by doing so he linked up with the culture, hence the top brass in Egypt —- the Hebrews shaved when mourning, while the Egyptians shaved for dressing.

When Joseph came out, he told Pharaoh his dream and the interpretation, and that very day he became the prime minister of Egypt; the next in command to Pharaoh!

Soon there was famine in Canaan and all the countries round about, but because of Joseph, Egypt was well prepared. Then came the sons of Jacob to Egypt to buy corn, but they did not recognize Joseph. They said to him, “Sir we have come to buy bread”, and they all bowed down and Joseph remembered his dream. He asked after their daddy, and they told him he was still alive. He then requested them to bring their youngest brother who was at home, as evidence that their words were true. When they brought Benjamin, he tricked them and seized him, refusing to let him go. Then they all fell to the ground, begging him and confessing the wrong they had done to their brother (Joseph) a long time ago. But all this while, Joseph’s heart was breaking.

“Then Joseph could not refrain himself before all them that stood by him; and he cried, cause every man to go out from me. And there stood no man with him, while Joseph made himself known unto his brethren. And he wept aloud: and the Egyptians and the house of Pharaoh heard. And Joseph said unto his brethren, I am Joseph; doth my father yet live? And his brethren could not answer him; for they were troubled at his presence. And Joseph said unto his brethren, come near to me I pray you. And they came near. And he said, I am Joseph your brother, whom ye sold into Egypt. Now therefore be not grieved, nor angry with yourselves, that ye sold me hither: for God did send me before you to preserve life.” (Genesis 45:1-5).

Observe Joseph’s understanding. He knew the purpose of his coming to Egypt, so he told his brothers thus, “God sent me before you to preserve life, that’s why I was sold to that Egyptian. That’s why when I was sold to Potiphar’s house, I didn’t give up hope. From Potiphar’s house, I landed in prison; though things were bad, I still didn’t give up hope. From the prison, God restored my wasted years.”

With this at the back of his mind, he didn’t need to seek revenge. He recognized that he was in the hands of God. Do you see yourself in the hands of God or do you think your life is run by men? What do you think about yourself? Do you attribute your success today only to the help of men? Or do you realize it is the hand of God working for you? Have you entrusted your life to God so much that you can believe that He is the One leading you? How much did you mean it when you gave your life to Christ? Is He the Lord of your life? If He is the Lord of your life, then rest assured He will take care of you.

–Pastor Fideli Irengo—