MKESHA WA KUSIFU NA KUABUDU KESHO MAY 4, 2012, KIINGILIO NI BURE

Wachungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jiji Dar es Salaam  (kutoka kushoto) Abel Orgenes na Paul Safari wakiwa na muimbaji wa nyimbo za injili John Lisu wakioongea na waandishi wa habari juu ya mkesha mkubwa wa uimbaji wa kusifu na kuabudu pamoja na maombi kwa ajili ya Tanzania na Bara la Afrika ujulikanao kwa jina la (AFLEWO) ambao unatarajiwa kufanyika 4 May, 2012 ndani ya kanisa la City Christian Centre (CCC)- Upanga jijini Dar es Salaam.

Mchungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jijini Dar es Salaam  Paul Safari (katika) alisema kuwa mkesha kama huwa unafanyika pia katika nchi nyingi za Afrika, kama vile Kenya, Rwanda. Kauli Mbiu ya mwaka 2012 ni kutoka zaburi ya 68:1 ‘Lets God Arise’. Mkesha huu unaundwa na waimbaji zaidi ya 50 kwa kutengeneza timu moja yaani “Praise Team” na hakutakuwa na waimbaji binafsi. 

Mchungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) la jiji Dar es Salaam Abel (katikati) akionyesha kauli mbiu ya mkesha huo ambao unasema,  ’Lets God Arise’. Pembeni yake anayeshuhudia ni mchungaji Paul Safari (kulia) na Samuel Mwangati (kulia) ambaye ni Music Director wa Aflewo.

Kwa upande wake Samuel Mwangati ambaye ni Music Director wa Aflewo alisema kuwa madhumuni ya Mkesha huu ni kama ifuatavyo.

1. Kuwaungaisha Wakristo Kutoka madhehebu yote katika Kusifu na Kuabudu.

2. Kuwaleta Pamoja wakrtisto Kuomba kwa ajili ya Kuliombea Taifa la Tanzania na Bara la Africa kwa ujumla.

3. Kuleta Umoja wa Mwili wa Kristo. Pia aliongeza kuwa kamati ya maandalizi imeandaa utaratibu wa mabasi kuanzia Akiba, Palm Beach na Muhimbili ambapo yatafanya kazi kuanzia saa 1-3 usiku.

Kajuna Blog

Pastor Faustin Munishi atamani kuanika wachungaji waovu

Apostle James Ng’ang’a Gets Very Drunk And Noisy

Apostle James Maina Ng’ang’a of the Neno Evangelism Ministry is said to have had one too many drinks before displaying his other side. The apostle known for his ‘demon removal’, is reported by Ghetto Radio to have had a heavy drinking before getting into a fight with his fiancee. A security officer who happened to be on the wrong side of the argument also encountered the apostle’s wrath.

The cause of argument between the Ng’ang’a and the fiancee is not clear but is thought to be his drinking habits. The story became more interesting when the security guard, who the apostle harassed, was arrested by police. Apparently, Ng’ang’a called the authorities and manufactured a few lies and with money and ‘name’, the ‘soldier’ stood no chance.

Kenyan apostles have not shied away from controversy. The first was Margaret Wanjiru, who, despite the tight political news schedule, managed to book her slot on prime time TV every day, for a whole week, when she declared she was getting married, dressed in a 3 metre veil. That was not helped by the emergence of Kamangu.

Then came the good pastor from Helicopter of Christ Ministry. We have all heard the story, but in a nut shell, he divorced his wife who is demanding several hundreds of thousands every month. She claims the husband is filthy rich and she is part of the reason he got rich. Now comes the good pastor, who claims he can only afford to give her only Sh 5000, every month. The fact that he owns several top of the range vehicles, and controls one of the largest congregation in the city does not help his argument.

Now, James Nga’ng’a Maina has joined the list of ‘drama queen’ pastors. If the rumours are true, the image of the very respected apostle will drop to an all time low.

© nairobiwire.com

BAADA YA HABARI HII KUANDIKWA, MCHUNGAJI FAUSTIN MUNISHI AKAANDIKA YAFUATAYO


Tufunike mizoga KANISANI Kisha tujifanye kila kitu shwari. Twende kwa ‘PUBLIC’ Tuwaalike Kanisani. Ujumbe tuwaambie YESU ANASAMEHE NA KUDUMISHA. TENA UKIMWAMINI UTAFANYIKA KIUMBE KIPYA YA KALE YATAPITA TIZAMA YATAKUWA MAPYA. Halafu baada ya siku kidogo wasikie harufu ya mizoga ya dhambi mliyofunika KANISANI. Which one is more damaging?

Kosa likikosolewa na mtu awezaye kukosa na hajakosa si kosa Kama kuogopa kukosoa kosa na uje ukose kosa sawa na uliloogopa kukosoa. Hilo ndiyo kosa. Au wasemaje?

Somo geni kwa kizazi kinachopenda Injili ya mafanikio ya kuufurahisha mwili kwa muda. Ila kwa kizazi cha wale tuliozaliwa mara ya pili, Injili ya kuwezeshwa kushinda dhambi ndio msingi wa imani yetu. Tukikosa shabaha hiyo, tutakuwa na washirika wanaoishi maisha ya kushindwa na kuwezwa na dhambi, ambao hawaoni ajabu yeyote kwa wapakwa mafuta kufanya maovu, kwani ndiyo mtindo. Je wasemaje?

Mama aliyefumaniwa usinzi kukakosekana wa kutupa jiwe la kwanza ilimaanisha Dhambi ilitawala na itaendelea kutawala hata sasa? Wakati huo Yesu alikuwa hajamaliza kazi ya kuishinda dhambi msalabani ili tukimwamini tuwe zaidi ya washindi. Injili ya kushinda dhambi ni yetu wakati huu au ni ya Mitume?

Dhambi Hazipaswi kututawala. Mtume Paulo alikutana na kesi ya aina hii kwa wandugu wa kanisa la Galatia. Moja ya ufumbuzi juu ya suala hili aliwataka waenende kwa Roho ili wasisitimize kamwe tamaa za mwili. Wagalatia 5:16 ‘ Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili’ . Kuenenda kwa Roho ndio kukoje? Ni kuishi/kuenenda kwa kufuata utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu maishani mwako.

Tuseme kanisani mwako Pastor Amebeba sadaka yote akaweka kwenye gari akaishia nayo. Kumbe Simu yako ya rununu Imemnasa akifanya uovu huo. Ukiposti picha ya Pastor Tapeli hapa na uandike story kidogo kwamba Badala pesa ziwekwe hazina ya kanisa Mchungaji Aweka Zote Kibindoni. Hapo utakuwa umesaidia wengi wajue pesa za kanisa zinapaswa kuwekwa hazina ya kanisa. Wengine watakuita MDAKU usijali.

Munishi Faustin DailyNews

Rebecca Malope Kupamba Tamasha La Pasaka

Na Mwandishi Wetu

MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Alex Msama, alisema Rebecca amethibitisha kushiriki tamasha hilo.

Msama alisema Rebecca ataungana na waimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchi jirani za Zambia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia na Congo (DRC), Rwanda na Uganda.

Malope atakuwa mmoja kati waimbaji siku hiyo wakiwemo Rose Muhando, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Ephraim Sekeleti, Anastazia Mukabwa, Atosha Kissava na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival inayotamba na albamu yao mpya ya Mtu wa Nne, inatarajia kutumbuiza katika tamasha la Pasaka na Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka DRC.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

“Katika tamasha la Pasaka mwaka huu, Rebecca Malope atapata fursa ya kuimba nyimbo mbalimbali zilizomo kwenye albamu zake,” alisema Msama.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

“Bado tunaendelea na mazungumzo na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Rebecca atakuwepo akishirikiana na wengine mahiri kama Rose Muhando, Solomon Mukubwa na wengineo,” alisema Msama.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Rebecca Malope ni mwimbaji nguli wa Afrika Kusini aliyetamba zaidi kimataifa mwishoni mwa miaka ya 90.

Malope alizaliwa katika shamba la tumbaku Afrika Kusini. Akiwa mtoto, yeye na dada zake walikuwa wakiimba kwaya kanisani.

Alijiunga na kundi la muziki wa injili akiwa binti mwenye umri mdogo, jijini Johannesburg, chini ya mtozi, Zizwe Zakho.

Alianza kutoa albamu yake ya kwanza aliyoipeleka Marekani mwaka 1996 na mwaka uliofuata alisaini mkataba na EMI kisha akatoa albamu ya Free At Last.

Wa mabondeni warudishwe kijijini – Mchungaji

MCHUNGAJI wa Anglikana jijini Dar es Salaam, Obedi Ntigogozwa, amesema Serikali inapaswa kuwasafirisha kwa mabasi waathirika wa mafuriko waliojenga mabondeni na kuwapeleka vijijini kwao kama ilivyofanya kwa ombaomba wakati Mkuu wa Mkoa akiwa Yusuf Makamba.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Ntigogozwa alisema huruma ya Serikali imepitiliza kwa kuwa mara kadhaa wamepigiwa kelele ya kuhama katika maeneo hayo lakini wamekaidi amri hiyo.

Mchungaji huyo ambaye ni Msimamizi wa Makanisa ya Anglikana ya mapokeo ya Low Church (Waanglikana Wakiinjilisti), alisema kwa ukaidi wao, suluhisho pekee ni kuwarejesha vijijini mwao kuendeleza shughuli za kilimo walizozitelekeza na si kung’ang’ania mjini.

Aliishauri Serikali kutengeneza miundombinu bora na kuhakikisha vitendea kazi vinapatikana huko vijijini ili watu hao watekeleze azma ya Kilimo Kwanza kwa vitendo na kuongeza uhakika wa usalama wa chakula nchini kuliko kuendelea kuhatarisha maisha yao mabondeni.

“Fursa zipo vijijini walikokimbia na kuja mjini na kujenga katika maeneo ya hatari kama ilivyoelezwa na wataalamu.

“Serikali miaka kadhaa iliyopita wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa Makamba, ilivalia njuga suala la ombaomba wakarejeshwa vijijini mwao na wengi walikuwa wakitoka Dodoma, inashindwaje kwa hawa?” Alihoji Mchungaji huyo.

Alishauri waliogoma kuhama licha ya kupewa maeneo bure huko Mabwepande, wilayani Kinondoni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam waondolewe kwa lazima kwa kupandishwa kwenye magari yatakayokodiwa na Serikali hadi vijiji wanakotoka kwa kuwa hata kupewa
viwanja ni huruma iliyopitiliza.

“Wapelekwe vijijini kuendeleza kilimo, sasa Serikali ina dhana ya ‘Kilimo Kwanza’ wakaitekeleze kwa vitendo huko, wawekewe tu miundombinu sambamba na vifaa vya kilimo na kuimarisha masoko.

“Wakalime tuepuke njaa badala ya kung’ang’ania mahali ambako si salama kwa maisha yao, Mungu kasema kwa njia hii (mafuriko), wanataka nini tena,” alihoji Mchungaji Ntigogozwa.

Aliyataja maeneo yenye rutuba nzuri kwa kilimo ambako alidai baadhi ya waathirika wanatoka huko ni pamoja na maeneo ya Kusini mwa nchi, Kanda ya Ziwa na mikoa ya Kaskazini na kuongeza kuwa mashamba mengi yametelekezwa huku watu wenye uwezo wa kulima, waking’ang’ania mabondeni na baadhi wakijihusisha na utapeli.

Alisema ikiwa Serikali itaona gharama kubwa kukodi mabasi, ifanye harambee kama ilivyofanyika kwa vyakula na mahema sambamba na huduma za maji kwenye makambi ya dharura kwa kuwa anaamini kwamba baadhi ya waathirika waliopewa maeneo hayo mapya, watauza siku si nyingi na kurejea mabondeni.

Hata hivyo Serikali ilishatoa msimamo kuhusu suala hilo kuwa, watakaorudi au kugoma kuhamia Mabwepande, haitahusika na jambo lolote litakalowapata na kwa wanaoishi eneo la Bonde la Msimbazi, watalazimika kuhama kupisha ujenzi wa mradi wa eneo la kisasa la mapumziko.

Ujenzi huo uliwahi kuelezwa bungeni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ingawa alipingwa vikali na baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam wakigoma wapiga kura wao kuhamishwa.

Hata hivyo msimamo huo wa wabunge ilikuwa kabla hawajashuhudia gharika hiyo ya mafuriko ya mwishoni mwa mwaka 2011 iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 40 na wengine zaidi ya 5,000 kukosa makazi.

–Habari Leo

Mchungaji atembezwa uchi, saba wakimbia nyumba

WACHUNGAJI wanane wa makanisa ya Kipentekoste wanaotoka jamii ya wafugaji wa Kimasai wilayani Arumeru wamezihama nyumba zao na kwenda mafichoni wakihofia kukamatwa, kuvuliwa nguo, kutembezwa mitaani na kutozwa faini dume la ng’ombe baada ya kudaiwa kwenda kinyume na mila, desturi na taratibu za jamii hiyo kuhusu sherehe za tohara kwa wanaume.

Waliokimbia nyumba zao kwa hofu hiyo ni pamoja na Mchungaji Edward Supeeti, Simon Sivai, Joel Hamisi na Loi Langasi huku wengine wakiwa ni Loishinde Mollel, Jonas Lebulu na Geofrey Jacob.

Hofu hiyo imewakumba wachungaji hao kutokana na vitisho dhidi yao baada ya mmoja wao, Julius Lukumay (34) kukamatwa na vijana wanaojiita jeshi la mila na kumtembeza mitaani kwa siku mbili akiwa uchi akidaiwa kukataa kuhudhuria kikao cha mila cha rika la Korianga.

Lukumay, baba wa watoto wanne alikamatwa Novemba 17 mwaka huu na kutembezwa katika vijiji vinne tofauti baada ya kukataa kutoa faini ya ng’ombe au Sh500,000 kwa kosa la kuwashitaki wazee wa mila kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Siwandate, Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru, ambao waliagiza vijana wakamate tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 100 lililokuwa nyumbani kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuokolewa na askari polisi waliofika eneo la tukio, siku ya pili tangu alipokamatwa na jeshi la mila, Lukumay alisema licha ya kuvuliwa nguo zote, watekaji wake walimvalisha bati iliyotobolewa sehemu ya kichwa pamoja na mfuko aina na kiroba ulioishia tumboni na kumwacha sehemu zake za siri zikiwa wazi.

“Mimi nimeokoka, ndiyo maana sihudhurii vikao vinavyohusiana na matambiko ya kimila. Cha ajabu, nilishangaa watu wanaoujua ukweli huo kufika nyumbani kwangu na kuchukua tanki langu eti kwa nini sikuhudhuria kikao cha rika na nilipofuatilia wakanikamata, kunivua nguo na kunitembeza uchi mitaani,” alilalamika Lukumay.

Alisema watekaji hao walimtembeza katika vijiji vya Ngaramtoni, Mringaringa, Kenyaki, Olevelosi, Kiranyi na Elerai huku wakimwimbia nyimbo za kumkejeli hadi saa sita usiku walipomrudisha kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Olchoki .

Mwathirika huyo wa sheria za mila alizungumza akiwa Hospitali ya Seliani, eneo la Ngaramtoni alikokimbizwa baada ya kuokolewa na polisi ambapo daktari aliyemchunguza aligundua kuwa alipigwa na kupata majeraha yaliyomsababishia maumivu makali.

Daktari aliyemtibu na kusaini PF3 iliyotolewa Kituo cha polisi Ngaramtoni ambaye alitambuliwa kwa jina moja tu Swai alibainisha kupitia maelezo yake kuwa majeraha na maumivu aliyoyapata Mchungaji Lukumay yalisababishwa na kupigwa kwa fimbo na rungu.

Katibu wa Umoja wa Wachungaji wa Madhehebu ya Kipentekoste mkoani Arusha, Joseph Kaondo alilitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kuwahakikishia usalama, wao na waumini wao dhidi ya vitisho na manyanyaso wanayopata kutoka kwa wazee wa mila na vijana wa jeshi la mila akitolea mfano tukio la kukamatwa kwa Lukumay ambaye aliokolewa zaidi ya saa 22 tangu tukio hilo liliporipotiwa polisi.

Mbele ya wachungaji wenzake, katibu huyo alisema jeshi la polisi linasuasua kuchukua hatua kwa maelezo kuwa hayo ni mambo ya mila yanayostahili kumalizwa na vikao vya mila, licha ya ukweli kwamba wao hawaishi kwa kufuata mila na desturi baada ya kuokoka.

Alisema hata mtendaji wa kijiji aliyepokea malalamiko ya Lukumay kukamatiwa tanki lake maji , Rafael Laizer alikataa kutatua mgogoro huo akidai kuhofia usalama wake na kuwataka wahusika wakayazungumze mambo hayo kwenye vikao na wazee ambao waliagiza Lukumay atembezwa uchi akiimbiwa nyimbo za kejeli au alipe dume la ng’ombe kwa ajili ya
chakula cha jeshi la mila kwa kosa la kuwashtaki ofisi ya Mtendaji.

Baada ya kutembezwa, Lukumay alipelekwa mto Ngarenaro ambako aliogeshwa Saa 11 asubuhi kabla ya kupelekwa nyumbani kwake ili akatoe ng’ombe lakini ikashindikana baada ya mkewe Happines kuhamisha mifugo iliyokuwepo nyumbani kwake, jambo lililowaudhi jeshi la mila waliamua kumchukua mkewe na kuvisha salfeti na kumuunganisha na mumewe huku wakimtelekeza nyumbani mtoto wao, Bezaleli mwenye umri wa miezi saba.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alikiri kufahamu tatizo hilo alilodai linatokea mara kwa mara  kipindi cha tohara za mila kwa jamii ya Wamasai.

Alisema baada ya kumuuokoa kijana huyo walikubaliana Mkuu wa Wilaya ya Arumeru , Mercy Silla kuwa vifanyike vikao vya mapatano kati ya viongozi wa mila na wale wa madhahebu ya dini.

Mkuu huyo wa wilaya pia alikiri kuwepo jambo hilo, lakini amekana kupata taarifa za wachungaji hao kukimbia nyumba zao kwa kuhofia usalama wao baada ya mmoja wao kutekwa na jeshi la mila.

Hata hivyo, alisema baada ya mchungaji aliyetekwa kuokolewa, walikubaliana na viongozi wa mila kuheshimu imani ya wengine wasiokubaliana na matambiko yao.

Alisema wamewaagiza viongozi wa pande zote mbili kuheshimu makubaliano yao ya Februari 22 mwaka jana yaliyofikiwa mbele ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha , Isdory Shirima ikiagiza viongozi wa dini na mila kutoingiliana katika utekelezaji wa shughuli zao .

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa dini akiwemo askofu Leonard Mwizarubi ambaye ni mwenyekiti wa makanisa ya kipentekesto mkoani hapa, Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer, kiongozi wa mila wa kimasai Amani Lukumay, mkuu wa wilaya ya Arusha , Raymond Mushi , mkuu wa wilaya ya Siha , Silla , maaafisa
kutoka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani hapa.

MWANANCHI

Dk. Malasusa: Acheni migogoro, tafuteni Utakatifu

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Dk. Alex Malasusa, amewaasa Wakristo nchini kuelewa kwamba, kanisa liko kwa ajili ya wale wanaomwamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu na si sehemu ya kuanzisha na kupalilia migogoro kwa lengo la kujipatia mkate wa kila siku.

Dk. Malasusa ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya ibada ya ushirika wa Kawe, ambayo imegharimu zaidi ya shilingi billioni moja hadi sasa.

Dk. Malasusa alisema inashangaza kuona baadhi ya Wakristo ndani ya kanisa wakitafuta nafasi mbalimbali za uongozi si kwa lengo la kutafuta utakatifu, bali wakiwa na lengo la kuanzisha vurugu na migongano, tendo ambalo ni kinyume cha kuwepo kwa kanisa.

“Watu wanajumuika kanisani lakini hawautafuti utakatifu.Watu wanasukumwa kudai wawe watumishi wa kanisa, wazee wa kanisa, wainjilisti, wachungaji na wakati mwingine maaskofu ili waweze kupata sifa fulani. Sehemu zingine, watu hawa wamekuwa na ujasiri wa kuzuia hata kufanyika kwa ibada kwa nia tu ya kupata ridhiki yao ya kimaisha na si kwa lengo la kumtumikia Mwenyezi Mungu,” alisema.

Alifafanua kwamba wapo wazee waliochaguliwa katika kanisa kwa nia ya kuwa wapinzani, ambao husubiri kitu kinachofanywa na mchungaji au askofu, ili wapate la kusema na akawaasa kuelewa kuwa, kanisa ni kundi la waamini ambao Kristo amelipata kwa gharama ya msalaba na hivyo akawataka kuyafanya makanisa kuwa pahali pa msamaha na watu wanaoutafuta utakatifu.

Aidha, aliwataka wananchi na jamii kwa ujumla kuenenda katika mwenendo wenye maadili na unaompendeza Mungu kama wanavyokumbushwa kila wanapofika kwenye ibada.

“Tunapokuwa na maeneo ya kutosha ya ibada, ndivyo tutakavyozidi kuwakumbusha wananchi yale yanayoelekezwa na Mwenyezi Mungu kutoka kwa watoto wake. Yeyote mwenye hofu ya Mungu, atampenda mwanadamu mwenzake na kwa hiyo atafanya kazi yake vizuri mahali popote atakapokuwa, na hivyo kuleta maendeleo yanayohitajika,” alisema.

Wakati huo huo, Dk. Malasusa alihitimisha harambee ya ujenzi wa kanisa la usharika huo ulioanza mwezi Julai mwaka huu, ambapo zilipatikana jumla ya shilingi milioni 90 zikiwa ni fedha taslimu na ahadi. Hadi anahitimisha harambee hiyo, fedha taslimu zilikuwa shilingi milioni 50, huku milioni 40 zikiwa ni ahadi.

IPP

Papa ashitakiwa The Hague

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedikto XVI, ameshitakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyoko The Hague, Uholanzi.

Papa anashitakiwa na kundi waathirika wa manyanyaso ya kingono waliyofanyiwa na viongozi wa kanisa hilo, wakiwamo makasisi na viongozi wengine waandamizi. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, mashitaka hayo yalifunguliwa juzi Jumanne katika ICC.Mbali na Papa, wengine wanaoshitakiwa ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, na maofisa wengine wawili wa ngazi ya juu Vatican.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka yanayokiuka haki za binadamu kwa kushindwa kuzuia au kutowaadhibu wahalifu wa makosa hayo ya ubakaji, ngono kinyume cha maumbile, na kwa kuficha kimkakati matendo hayo mabaya yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wa kanisa dunia nzima.

Kituo cha Haki za Kikatiba za Marekani (CCR) kinachowakilisha waathirika hao, kinasema zipo nyaraka zinazoonyesha kuwa maofisa kadhaa wa Vatican na wengine waliwanyima ushirikiano watekelezaji wa sheria kutoka taasisi kadhaa za kimataifa waliokuwa wanafuatilia uhalifu huo kwa nia ya kuwatia hatiani watuhumiwa.

Mwanasheria wa CCR, Pam Spees, amenukuliwa akisema,” Kwa kukataa kutoa ushirikiano, Kanisa limewalinda mapadri waliotenda uovu huu, na limekataa kuwafukuza kazi, huku watoto hawa wakiendelea kubakwa na kushambuliwa kingono. Si kwamba wanashitakiwa kwa matukio au vitendo hivi vya ubakaji, bali pia kwa jinsi kanisa lilivyoshiriki kuzamisha maumivu haya.”

Kwa mujibu wa waraka uliowasilishwa na CCR, Papa, kwa nafasi aliyonayo katika kanisa, ndiye anawajibika kwa matendo maovu ambayo mapadri wake waliwatendea watoto wadogo, na kwa kuficha matendo hayo.

Wengine wanaoshitakiwa ni Kiongozi wa Makardinali, Angelo Sodano, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Cardinal Tarcissio Bertone, ambaye awali, alikuwa anasimamia Idara ya Mafundisho ya Imani.

Megan Petersen, mkazi wa Minnesota, ni mmoja wa waathirika wawili wa Kimarekani waliotajwa, ambao kesi zao zimeunganishwa katika mashitaka yaliyopelekwa ICC.

Wiki iliyopita, Petersen alishinda kesi dhidi ya Jimbo Katoliki la Crookston, na mahakama ikaamuru alipwe Dola za Kimarekani $750,000 (Tsh 1230000000), baada ya kubainika kuwa alipokuwa mtoto alibakwa mfululizo na Padri Joseph Jeyapaul.

Alisema, “Alikuwa mtu wa Mungu, name nilikuwa mtu wa imani, nikitamani kuwa mtawa. Nilimwamini. Kwa sehemu fulani, nipo hapa kuwalinda watoto na watu wazima walio katika mazingira ya kudhurika. Ratzinger (Papa Benedict XVI) ndiye kiongozi wa taasisi hii, na hawa ni kondoo wake. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha jambo hili halimtokei mtoto mwingine.”

Katika ripoti mpya ya Shirika la Amnesty International, linalojishughulisha na haki za binadamu, Vatican ilitajwa kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka zaidi ya 2000, kwa maofisa wake kujihusisha na matendo hayo.

Ripoti hiyo ilisema kwamba ushahidi juu ya matendo haya ulikuwa umesambaa mno, na kanisa limeshindwa kuyatafutia ufumbuzi.

Tanzania Daima

Vichwa vya viongozi vimejaa viroboto – Lusekelo

MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo Kibangu, Antony Lusekelo, amesema kuwa serikali imejaa viroboto, ndiyo maana wameweza kuruhusu usafirishaji wa wanyama nje ya nchi bila kujua kuwa hatua hiyo ni kuliangamiza taifa.

Kauli hiyo, inaweza kufananishwa na ile ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, aliyedai kuwa baadhi ya wabunge wa mkoa huu wanaomwandama kuhusu sakata kwa uuzwaji wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) wanawaza kwa kutumia makalio badala ya ubongo.

Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya kumaliza ibada ya Jumapili iliyofanyika kanisani hapo, Mchungaji Lusekelo alisema kuwa jambo hilo ni kashfa kubwa kwa serikali kuliko zile zilizowahi kutokea za Richmond pamoja na Fedha za Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Alisema hatua ya ndege ya kijeshi kuingia nchini na kisha kuchukua wanyama zaidi ya 160 na kuondoka nao huku vyombo vya dola vikiwa havifahamu, ni hatari kwa taifa.

Mchungaji Lusekelo aliwataka watumishi wa Mungu kuhakikisha wanafanya maombi kwa ajili ya taifa kutokana na kuonekana kama limelogwa; kwamba ndiyo maana viongozi wanakosa maarifa.

“Hivi tunaweza kusema tuna viongozi kweli katika nchi hii…uko wapi usalama wa taifa, serikali, uhamiaji na mawaziri wenye dhamana wa utalii hadi hawajui juu ya kuingia kwa ndege na kubeba wanyama kisha kutoweka nao,” alihoji Mchungaji Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako.

Alisema kuwa kutokana na kashfa hiyo kubwa, Watanzania hawatasahau kwa miaka yote, jambo ambalo linazidisha chuki kwa serikali.

“Tunapozungumzia nchi ni lazima tuzungumzie na vizazi vijavyo, hivi tufikirie kama leo wazee wetu wangeuza wanyama je sisi tungeikuta hiyo rasilimali ya utalii ambayo tunaitegemea?” alihoji.

Akizungumzia kuhusu ajali ya meli ya Spice Slanders iliyoua zaidi ya watu 200, alisema jambo hilo linatokana na nchi kugumbikwa na rushwa ndiyo maana hata wasimamizi wa bandari walishindwa kudhibiti tukio la kujazwa kwa abiria na mizigo.

Alisema serikali imekuwa ikifanya vitu vya kujenga ukuta hasa pale yanapotokea matatizo kama ambavyo imeamua kuunda tume katika suala la ajali hiyo jambo ambalo haliwezi kusaidia kitu chochote.

“Serikali yenye akili timamu haiwezi kuacha tatizo litokee ndiyo ije kuunda tume, kufanya hivyo hakuwezi kufuta machungu ya waliofiwa na wala haitaweza kufufua wale waliokufa,” alisisitiza.

Alisema kuwa kama serikali ingekuwa imejijenga katika mfumo wa kuwajibika basi mpaka sasa wasimamizi wa mamlaka za bandari wangewajibika kutokana na kuguswa na suala hilo na kwa heshima kwani huo ndiyo uadilifu.

Mch. Lusekelo alisema kuwa viongozi wa mamlaka hizo wakubali kubeba dhambi hiyo kutokana na kuzembea kuchukua hatua na kusababisha vifo vya mamia ya watu wasio na hatia.

“Nimeamua kusema ukweli sijutii suala hili hata kama itatokea urafiki wangu na Chama cha Mapinduzi (CCM) utaisha kwa ajili ya kusema ukweli basi katika hilo niko tayari…siwezi kumuona kiongozi wa nchi hajachana nywele nikaacha kumwambia kwa vile atakasirika!” alisema.

Tanzania daima

Bi harusi ajifungua kanisani

BIBI harusi aliyefahamika kwa jina la Mariam Shabani, ameshikwa na uchungu wa kujifungua kanisani wakati akifungishwa ndoa na mchumba wake, aliyefahamika kwa jina la Deo Massawe.Tukio hilo lilitokea juzi Kanisa Katoliki lililopo maeneo ya Majengo Shimoni, wilayani Muheza, huku umati wa watu ukiwa umejaa ndani ya kanisa hilo ukiisubiri kufungwa kwa ndoa hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa hilo, wakati Padri Martin Kihiyo, akiendelea na misa ya kufungisha ndoa hiyo, ghafla bibi harusi akiwa amevaa vazi rasmi la harusi, alianza kupiga kelele akidai anasikia uchungu wa kujifungua.

Hata hivyo, baada ya bibi harusi huyo kupiga kelele, Padri Kihiyo alisitisha misa hiyo  na Mariamu kuchukuliwa haraka na kuwekwa kwenye gari huku akiwa hajiwezi hadi Hospitali Teule Muheza.Pia, Mariamu anafahamika kwa jina la Sada Shabani, baada ya kufikishwa hospitali alipelekwa chumba cha kujifungulia huku akiwa na vazi lake la harusi.

Baada ya kuhudumiwa Mariamu, alijifungua mtoto wa kike na kulazwa wodi ya Azimio wanakolazwa wazazi.Mmoja wa muuguzi hospitalini hapo aliyeomba asitajwe, alisema bibi harusi huyo alijifungua njiti akiwa na miezi saba.Kwa upande mwingine, kwenye ukumbi ambao ulikuwa umeandaliwa kwa sherehe ya  harusi hiyo, watu walikuwa wamekaa ndani wakisubiri maharusi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo bwana harusi alilazimika kufunga ndoa na msichana mwingine wa pembeni kwa niaba ya bibi harusi, ili kuhalalisha sherehe hiyo huku bibi harusi mwenyewe akiwa hospitali analea.

Inasemekana Mariamu alianza kusikia uchungu akiwa saluni na aliwaeleza baadhi ya watu, lakini walimjibu kuwa huo ni woga wa harusi.Katika hatua nyingine, mbuzi wa ndafu aliyekuwa ameandaliwa alianguka chini kwenye mchanga.

Baadhi ya Wakristo walisikitishwa na tabia ya viongozi wa dini kuendelea kuwafungisha ndoa watu ambao wake zao wana mimba kwamba, ni aibu

Source: Gazeti la Mwanachi August 11, 2011.

Lowassa asipokua rais 2015, mniue – Askofu

Kiongozi mkuu wa kanisa la Last Glory Church la hapa nchini Basileus Ezekiel Mabumba, amesema amepokea ujumbe kutoka kwa Mungu unaoeleza kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Ngoyay Lowassa, atakua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Katika mahojiano na gazeti hili (Nyakati), Mabumba alieleza kuwa atawajibika iwapo unabii wake hautatimia. Kwa mujibu wa Torati kile ambacho kilikuja kubainika baadaye kuwa unabii wa uongo, adhabu kwa mtoaji unabii ilikua ni kupigwa mawe hadi afe.

Jumatano iliyopita, Mabumba alitinga katika ofisi za gazeti hili na kueleza kuwa, kwa muda mrefu sasa amekua akipokea ujumbe kutoka kwa Mungu ukieleza kuwa Lowassa ndiye atakuwa rais wa nchi hii ya awamu ya tano.

Sehemu ya mahojiano ya gazeti hili na Askofu Mabumba, ambaye hujulikana pia kama Mtume, ilikua kama ifuatavyo:

Mwandishi: Umesema kwa muda mrefu umekuwa ukiletewa huo ujumbe. Tuambie ni tangu lini? Tuambie pia mtu wa kawaida kabisa anaelewa nini kuhusu unabii?

Mabumba: Tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kwa uhakika unabii huu nimepata kuwaeleza waumini pale kanisani. Sasa nimeona niufikishe kwa watu wengi zaidi.

Unabii ni tofauti na kutabiri. Kuna unabii wa aina mbili. Kwanza, ni ule unabii ambao Mungu anakuruhusu kuona mambo yajayo. Ni pale Mungu anapokuonyesha kutakua na nini siku zijazo. Ni karama za ufunuo. Aina ya pili ya unabii ni pale mtu aliyekusudiwa kufikisha unabii huo anaweza kutamka jambo kwa msukumo wa Roho Mtakatifu. Sasa hapo ndio ujue kwamba kuna msukumo wa kibinadamu, wazo la mwanadamu mwenyewe, msukumo wa shetani na msukumo wa Mungu.

Mwandishi: Sasa Mtu anaweza kutofautisha vipi kama jambo fulani lina msukumo wa mwanadamu, kwa Shetani au wa Mungu?

Mabumba: Unajua kama ni la Mungu kuna msukumo unaolazimisha kulitafakari kila mara kabla hujalikubali. Unakua kama una mzigo fulani ukikubaliana na Mungu ndipo utapata amani ya kulisema.

Mwandishi: Lakini kuna nabii nyingi zimetolewa na watumishi hazikutimia. Kuna mtumishi aliwahi kusema angesigina Biblia iwapo unabii wake usingetimia. Haukutimia na hakusigina, leo yuko kimya. Mwingine akasema kutakua na vita…ziko nabii nyingi tu.

Mabumba: Unabii wangu lazima utimie nimekua nikioneshwa mambo mengi lakini siyatamki. Kuna vitu vidogo  vidogo nimeoneshwa na ikawa kweli. Yako na mambo makubwa labda kwa sababu sikuwa ninayasema kama ninavyofanya leo kwa hili. Hili ninasukumwa sana kulitamka.

Mwandishi: Usipotimia?

Mabumba: Niko tayari kuwajibika. Manabii waliwajibika kwa unabii wao. Hata nisipopondwa mawe, watu hawataniamini tena, hayo tayari ni ‘mawe’

Mwandishi: Kwa mazingira ya sasa ambayo watu wamepunguza imani wapo ambao wanaweza kufikiri kuwa umetumwa na unatumia nafasi yako ya utumishi wa Mungu kutumikia wanasiasa? Wengine wanaweza kufikiria kuwa unatafuta umaarufu.

Mabumba: Kwanza kabisa sitaki kuwa karibu na wanasiasa, hata chama sina, sijishughulishi kabisa na wanasiasa. Sifahamiani na Lowassa. Na ninafikiri kama ni hivyo Lowassa mwenyewe angeenda kwa wahubiri wakubwa. Mimi ninasema nilicholetewa.

Kama kuna watakaofikiria ninatafuta umaarufu, watakuwa wamekosea. Sihitaji umaarufu zaidi ya hapa. Naandika vitabu watu wengi wananifahamu kupitia huduma hiyo. Ninaandika vitabu na vinapendwa, inatosha. Siwezi kutumia unabii feki kujijenga.

Mwandishi: Unaweza kuzungumza chochote kuhusu dhana ya kujivua gamba ndani ya CCM ambacho Lowassa ni mwanachama na kiongozi?

Mabumba: Sifuatilii mambo ya vyama. Kwa habari ya unabii Mungu anakuonesha kidogo tu. Hayo mengine siyajui bwana. Kama kuna kuna kuvuana gamba mi sijui.

Lowassa Waziri Mkuu aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya Kampuni ya umeme ya Richmond hajapata kutangaza hadharani kuwa ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, lakini harakati za kisiasa ndani na nje ya chama chake cha CCM zinaashiria kuwa ni mmoja wa wanasiasa walioko katika ‘vita’ ya urais.

Hivi karibuni Lowassa alionekana katika televisheni akishiriki kwenye ibada katika kanisa linaloongozwa na mhubiri maarufu wa nchini Nigeria, TB Joshua.

Kushiriki kwa Lowassa katika ibada hiyo kulizua minong’ono, wengine wakihusisha na harakati za urais 2015 na kwamba alienda kuombewa ili ‘nyota yake ing’ae’.

Hata hivyo baadhi ya watumishi wa Mungu walikerwa na kitendo cha baadhi ya watu kushangazwa na uwepo wa Lowassa katika Ibada hiyo, wakisema ni kuingilia uamuzi binafsi wa mtu anayemtafuta Mungu wake.

Source: NYAKATI, Julai 10-16, 2011

Mwingira amtangazia kifo Babu wa Loliondo

- Adai siku zake za kuishi zinahesabika

Kiongozi mkuu wa huduma ya Efatha, Mtume na Nabii Josephat Mwingira amemtangazia kifo Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapila, maarufu kama Babu wa Loliondo, huku akisema siku za babu huyo kuishi sasa zinahesabika.

Akitoa tangazo hilo mbele ya waumini katika makao makuu ya huduma hiyo Mwenge, jijini Dar es salaam, Jumapili iliyopita, Mwingira alisema babu Mwasapila atakufa kwa kuwa amemtukana Mungu wa mwingira kwa kuzidi kutamka kuwa tiba anayoitoa imetoka kwa Mungu.

Mwingira ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu tangu atangaze rasmi vita dhidi ya Babu Mwasapila. Akitangaza vita  hiyo, Mwingira aliilaani tiba ya Babu huku akisema; “itoweke na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti”

Katika tukio la Jumapili iliyopita, mwingira alisoma andiko kutoka Waebrania 1:1-2, kisha akasema Mungu haongei na miti huongea na wanadamu ambao ni watumishi wake. Aliendelea kusema kuwa, babu wa Loliondo amemkasirisha sana kwa kuwa amemtukana Mungu kwa kusema kwamba Mungu ameongea na miti na badala ya watumishi wake.

“Mungu haongei na miti, anaongea na watumishi wake, hata katika kuponya Mungu ameagiza tuweke mikono kwa wagonjwa, Marko 16:15-18 inafafanua hili. Sasa kwa sababu babu wa Loliondo amemtukana Mungu, naye siku zake zinahesabika, kwani Biblia inasema usimwache mchawi kuishi” alisema Mwingira.

Wakati akiendelea na mahubiri yake huku akipita kuombea wenye shida mbalimbali, ghafla alifuatwa na mtumishi mmoja wa kanisa hilo na kumweleza kuwa, ndani ya kanisa hilo amekamatwa msichana ambaye ametumwa kuloga ili kuharibu kazi ya Mungu.

Hata hivyo, Mwingira hakuonesha kushtushwa na taarifa hiyo badala yake aliendelea kuombea watu huku akisema; “mimi sitishwi na wachawi” baadaye wakati akiendelea kuombea watu waliofika eneo ambalo msichana huyo alikuwa ameanguka na kuamuru ainuliwe ili amhoji.

Miongoni mwa maswali aliyoulizwa msichana huyo ni wapi alikotokea na alikuwa ametumwa na nani. Katika majibu yake msichana huy0 alieleza kuwa ametokea Ngorongoro na ametumwa na mtu aliyedai amechoshwa na maombi ya Mwingira yanayokwamisha kazi zake za kichawi. Msichana huyo alitaja jina la aliyemtuma ambaye hatuwezi kuandika jina lake.

Msichana huyo alikutwa na pete yenye picha ya mtu aliyetajwa na msichana huyo kuwa ndiye kamtuma, pamoja na chuma kilichochongwa mfano wa fuvu lililobebwa na ndege pamoja na bangili kubwa ya shaba.

Baadaye Mwingira alimuuliza; “sasa nikufanye nini”? yule msichana akajibu; “naomba unisamehe sitarudia tena ufanya uchawi na sitarudi kule nilikotoka” Mwingira akamuuliza tena; “Unakubali kumpokea Yesu”? yeye akajibu; “ndiyo” Baadaye msichana huyo aliongozwa sala ya toba.

Mwingira ni mmoja wa viongozi wa dini ya kipentekoste ambao walikuwa wa kwanza kabisa kutangaza kuipingatiba ya Babu wa Loliondo.

NYAKATI

Makamba juu ya ufahamu wa Biblia

KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, amesema kuwa na uelewa finyu wa biblia si jambo la ajabu kwake kwa sababu yeye siyo askofu.

Makamba aliliambia Mwananchi jana kwa simu, kuwa  licha ya uelewa finyu wa biblia, lakini amekuwa akitoa vifungu hivyo kwenye biblia. Makamba alisema hayo kufuatia, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Thomas Laizer kusema Makamba ana uelewa finyu wa biblia.

Laizer alisema hayo juzi mjini Arusha wakati wa kuwaaga watu wawili waliofariki kwa kupigwa risasi na polisi katika maandamano na Chadema yaliyofanyika Januari 5 mwaka huu.

“Ni kweli ninauelewa finyu wa biblia kwa sababu mimi siyo askofu, hata Qurani naweza kuwa siifahamu vizuri kwa sababu mimi siyo Sheikh, ndiyo maana kila ninachozungumza kuhusu dini hizo nakariri vifungu kutoka katika vitabu hivyo,” alisema. Makamba alisema alimweleza Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutoandamana kwa sababu serikali ilipiga marufuku maandamano hayo, wao wakapuuza.

Alimtaka Laizer kutoa tafsiri ya kitabu cha Warumi 13 sehemu ya kwanza hadi ya saba, inayosema  kuwa kila mtu hana budi kutii  serikali inayotawala kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.
Alisema kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala anapinga chombo kilichowekwa na Mungu na watu wanaoasi hujiletea hukumu.

“ Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu, kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka  basi tenda mema naye atakusifu,” alisema.

“ Laizer anieleze ufinyu wangu katika uelewa wa biblia  upo wapi ikilinganisha na tukio lililotokea mkoani Arusha,”  alisema

Source: Gazeti la Mwananchi

Kakobe Akemea Rushwa Kwa Dakika 56

Fidelis Butahe na Elias Msuya

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amekemea vitendo vya utoaji rushwa na kusema kuwa vinaweza  kuharibu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Amewataka watu  kutokubali kununulika katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuwa fedha haina thamani mbele ya utu wa mtu huku akionya kuwa vyombo vya usalama, mawakala, maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) pamoja na wapiga kura wanaweza kuingia katika mtego wa rushwa.

Akizungumza katika ibada ya pili  iliyofanyika jana makao makuu ya kanisa hilo Mwenge jijini Dar  es Salaam,  Kakobe alisema kutoa na kupokea rushwa  ni dhambi ambayo isipokemewa inaweza kuondoa Baraka za mungu kwa taifa.

Kakobe ambaye hivi karibuni alisema kuwa siku ya uchaguzi mkuu hakutakuwa na ibada yoyote katika kanisa hilo alitumia dakika 56 kuzungumzia rushwa huku akitoa mifano mbalimbali ya ubaya wa rushwa kwa kutumia Biblia takataifu.

Bila kutaja jina la chama, Kakobe alisema kuwa miaka ya zamani  kulikuwa na chama cha siasa ambacho ndani ya Katiba yake kulikuwa na ahadi za wanachama wa chama hicho kukataa kutoa wala kupokea rushwa.

“Miongoni mwa vyama vya siasa nchini kulikuwa na chama ambacho ndani yake kulikuwa na ahadi za wanachama. Kabla ya mtu kuwa mwanachama ilimbidi ale kiapo. Kati ya ahadi hizo, ahadi ya nne ilisema kuwa sitatoa wala kupokea rushwa,” alisema Kakobe,

Aliongeza, “Zamani  wanachama walilazimika  kuyazingatia  haya kwa maneno na kwa vitendo, Rushwa maana yake ni fedha au vitu ambavyo mtu anapewa ili aweze kufanya kile ambacho  aliyempa anataka amfanyie,”.

Alisema kuwa ili kiongozi awe na utu ni lazima ajitenge na vitendo vya kutoa au kupokea rushwa na kuongeza kuwa kushamiri kwa rushwa kunasababisha watu wachache kupambwa na kutukuzwa na wale waliowapa rushwa.

“Rushwa huondoa Baraka za mungu kwa familia na kwa taifa zima, ukijenga nyumba nzuri kwa mgongo wa rushwa dhamira yako itakusuta tu,  ni sawa na kuhifadhi fedha katika mfuko uliotoboka,”alisema Kakobe.

Aliongeza, “Msikubali kupewa khanga na fedha, mwanadamu una thamani kubwa, sasa iweje ukubali kununuliwa kwa khanga au fedha, mtu anayejiheshimu hawezi kukubali kugeuzwa bidhaa, kukubali rushwa ni sawa na kujifananisha na bidhaa, je wewe una thamani ya fulana au khanga?,”.

Kakobe ambaye hivi karibuni alizua mvutano mkubwa na serikali baada ya kupinga nguzo za umeme wa megawati 132  kupitishwa nje ya kanisa hilo,  mara kwa mara alikuwa akimtaja Mwalimu Julius Nyerere kama  mfano wa viongozi wanaojali utu,  akisema kuwa alikuwa kiongozi maskini jeuri, na jasiri asiyetegemea misaada ya wahisani.

“Mwalimu  Nyerere alijulikana kama maskini jeuri, alikuwa akisimama katika misingi ya haki. Alikuwa tayari kwa lolote, alikuwa radhi  madini yasichimbwe yabaki ardhini kwa kuwa yasingeweza kuoza kama nyanya,” alisema Kakobe.

Kakobe alisema kuwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere mgodi wa Mwadui ndio ulikuwa ukifahamika na kusisitiza kuwa kiongozi huyo aliwahi kutamka kuwa kuliko madini kuchimbwa bila manufaa kwa Watanzania ni bora yabaki ardhini.

Kakobe alisema kama kuna mtu yoyote ambaye ameshapokea rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi anatakiwa kutubu na kukubali kuikataa rushwa.

–SOURCE–MWANANCHI

Raisi Kikwete Alivyoanguka Ghafla!

GHAFLA uwanja unazizima, kila aliye katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam anashindwa kuamini kinachotokea, hotuba ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia CCM, Rais Jakaya Kikwete inakatika.

Hali hiyo inajitokeza baada ya kuanza kuzungumzia suala la Utawala Bora katika hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni za Chama hicho jana.

Kutokana na mshituko huo, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba anasimama na kuchukua kipaza sauti na kuwatuliza wanachama, wafuasi na wapenzi wa CCM waliofurika uwanjani hapo kushuhudia uzinduzi huo.

Baada ya muda inabainika kuwa Rais Kikwete amepata matatizo, ameishiwa nguvu na kusaidiwa na wasaidizi wake na kupelekwa kwenye zahanati ya muda nyuma ya jukwaa.

Walinzi walimbeba na kumpeleka kwenye zahanati ya muda iliyokuwa katika uwanja huo, lakini walipoikaribia, Rais alisimama na kuingia kwenye zahanati hiyo akitembea mwenyewe.

Baada ya dakika takriban 15 hivi alirejea kuendelea na hotuba huku akishangiliwa na umati huo. “Jamani nimefungulia,” alisema Rais huku akishangiliwa, akimaanisha kukatiza swaumu.

Hata hivyo, hakuweza kuimaliza hotuba hiyo iliyoonekana kuwa ndefu, pale aliposema tu kwamba Serikali yake iliweza kupandisha mshahara wa wafanyakazi ingawa kwa tofauti kidogo na kiwango kilichokuwa kikitakiwa na Tucta.

Lakini wakati anaanza kuzungumzia yaliyofanywa na Serikali yake katika sekta ya miundombinu, aliomba Watanzania waichague CCM na kumaliza hotuba hiyo.

Hali hiyo ilisababisha mshtuko na hofu ambapo baadhi ya wana-CCM walizirai na baadhi kuonekana wakilia kwa uchungu.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, waliwahimiza waliohudhuria kutulia.

Wakati huo huo, katika hali isiyotarajiwa, mkewe Mama Salma naye alijisikia vibaya uwanjani hapo na kusaidiwa na kupelekwa kwenye zahanati hiyo, kupewa huduma ya kwanza.

Mama Salma wakati akielekea kwenye zahanati hiyo kumjulia mumewe hali, alipokaribia alidondoka na kudakwa na walinzi wake na wakati anaingizwa kwenye zahanati hiyo, alipishana na mumewe mlangoni akitoka.

Hili ni tukio la tatu kwa Rais Kikwete kudondoka mbele ya hadhara wakati akihutubia wananchi.

Oktoba 2005 alipatwa na matatizo kama hayo wakati akifunga kampeni ya kuwania urais kupitia CCM.

Katika tukio hilo, Rais Kikwete alilazimika kukatisha hotuba yake na kuondolewa uwanjani hapo.

Baadaye akazungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake akisema hali hiyo ilisababishwa na uchovu wa kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi akifanya kampeni huku pia akiwa amefunga.

Oktoba mwaka jana, alijisikia pia vibaya na kuishiwa nguvu ghafla wakati akihutubia mamia ya watu katika maadhimisho ya miaka 100 ya Kanisa la African Inland (AIC) kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, hali iliyosababishwa na uchovu wa safari ndefu.

Madaktari wake walishasema hali yake kiafya ni nzuri na matatizo yaliyomkuta ni mabadiliko ya kawaida kiafya. Leo atakuwa Mwanza kuendelea na kampeni.

–HABARI LEO–Gazeti

Kakobe aitikisa serikali

Washirika wa Kakobe wakiwa wamepiga kambi masaa 24

RAIS Jakaya Kikwete ameingilia kati mvutano uliopo kati ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhusu upitishwaji wa nyaya za umeme wa kilovolti 132.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata zinasema kuwa Rais Kikwete ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kuandaa kikao kitakachowakutanisha wadau mbalimbali ili kutatua tatizo hilo.

Hatua ya Rais Kikwete kuingilia kati suala hilo imekuja baada ya juhudi za kikao cha awali kati ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zachary Kakobe kutofikia makubaliano.

Kwa mujibu wa habari hizo, kikao kati ya viongozi wa kanisa hilo na serikali kinatarajiwa kufanyika kesho.

Barua ambayo gazeti hili imeipata yenye kumb. Na. CBD 88/286/01 iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini na kusainiwa na Katibu wa Wizara hiyo, S.M.B. Massola, iliziagiza wizara na wadau wengine kuwapo kwenye kikao hicho kwa lengo la kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Wizara nyingine itakayohusishwa kwenye kikao hicho kitakachofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini kuanzia saa nne asubuhi ni Wizara ya Miundombinu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kakobe.

Wadau wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Wiki chache zilizopita TANESCO ilitoa taarifa ikiwatoa hofu wakazi wa eneo hilo kwamba hawataathiriwa na upitishaji wa umeme wa msongo wa kilovolti 132.

TANESCO ilisema ilihitaji kuyaondoa mabango ya kanisa hilo yenye urefu wa mita 13 ili kuwezesha nguzo zilizobeba umeme huo, zenye urefu wa mita 23 ambao unafuata viwango vya ujenzi wa msongo wa 132 KV kwa maeneo ya mijini kupita katika eneo hilo na kuhakikisha usalama wa eneo hilo.

Hata hivyo uongozi wa kanisa hilo haukukubaliana na maelezo hayo na kutokuwa tayari kuona nyaya hizo zikipitishwa katika eneo la kanisa lao.

Waumini hao, waliamua kupiga kambi saa 24 katika eneo la kanisa hilo, huku wakiwa wamevalia fulana maalum zilizoandikwa kwa mbele ‘TANESCO Muogopeni Mungu’ na nyuma ‘Baada ya Richmond Mmegeukia Kanisa’.

Kuchelewesha mradi huo kunaweza kusababisha Serikali ya Japan ambayo ndiyo inayofadhili mpango huo, kuondoa msaada wake jambo ambalo litafanya Jiji la Dar es Salaam kuendelea kukabiliwa na tatizo la umeme mdogo linalosababishwa na uchakavu wa miundombinu.

TANZANIA DAIMA, 13 Januari 2010

Mchungaji ampa Sheikh Yahaya masharti matatu

Siku chache baada ya mtabiri mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussein wa Dar es Salaam kutangaza katika vyombo vya habari kuwa mwana CCM atakayejitokeza kuchuana na Rais Jakaya Kikwete katika kinyang’anyiro cha kugombea urais mwaka huu, atakufa ghafla, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ Ubungo ametoa masharti matatu kwa mtabiri huyo vinginevyo naye atakufa ghafla.

Katika mahubiri kanisani hapo jana, Mchungaji Kiongozi, Gwajima alisema demokrasia ya Tanzania imo hatarini endapo mtu mmoja ataachiwa kuamua hatma ya taifa kinyume na mapenzi ya Mungu asiyekuwa na upendeleo kwa mtu yeyote.

“Baada ya kuendelea kutenda kazi zake zikiwa ni chukizo machoni mwa Mungu, leo ninatoa hukumu kutoka kwa Bwana, nanyi nyote mtachuja kuwa ni upi utabiri wa kweli kati ya Sheikh Yahaya na Mungu. Ninamwagiza Sheikh Yahaya afanye mambo matatu la sivyo naye atakufa ghafla kama alivyowatishia Watanzania wenzake,” alisema.

Sharti la kwanza alisema ni Sheikh Yahaya kwenda katika kanisa hilo la Glory of Christ na kuonana na mchungaji Gwajima yeye mwenyewe ili amwongoze kwa sala ya toba, kisha ampokee Yesu katika maisha yake.

Sharti la pili, Sheikh Yahaya ameamriwa kuanzia sasa aachane na utabiri wake ambao kwa miaka mingi alisema umewaumiza watu wengine wasiokuwa na hatia na kuwafaidisha wengine wachache kwa njia za giza.

Na sharti la tatu, Sheikh Yahaya ametakiwa, baada ya kuokoka, arudi katika vyombo vya habari kwa nguvu ileile aliyoitumia kutangaza utabiri wake wa mtu kufa ghafla na sasa awatangazie Watanzania mabaya yake yote aliyokwishayafanya kwa watu wa taifa hili hadi siku ya mwisho alipolazimika kuokoka.

Akifafanua juu ya masharti hayo, Mchungaji Gwajima alisema kimsingi yeye anamkubali Rais Jakaya Kikwete kuwa kiongozi wa taifa hili ila kinachomkera ni Sheikh Yahaya kuwatisha watu wengine wasitumie haki yao ya msingi katika kuikuza demokrasia hapa nchini.

Alipohojiwa kwa njia ya simu, Sheikh Yahaya ambaye alisema yuko nje ya jiji la Dar es Salaam kwa siku ya jana, alisema katika kipindi cha miaka 40 ya utabiri wake umekuwa sahihi siku zote na umaarufu wake ni wa kimataifa.

“Kamwe sitakwenda katika kanisa hilo, pia siko tayari kufuata sharti hata moja kutoka kwa mchungaji huyo.

Nimeanza utabiri kabla ya yeye kuwa shemasi wa kanisa hivyo endapo nitakufa najua ni siku zangu zimefikia mwisho wala si vinginevyo,” Sheikh Yahaya alisema.

Akitoa mifano ya utabiri wake ambao aliosisitiza kuwa sahihi mara zote, alitabiri msiba wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa kwa maelezo kwamba taifa litapata msiba mkubwa. Pia alisema aliwahi kutabiri kifo cha kiongozi mashuhuri ambaye kifo chake kingewakutanisha watu wa mataifa mbalimbali, dini, rangi na vyama mbalimbali vya siasa na kwamba kiongozi huyo alikuwa hayati Mwalimu Nyerere.

“Je, sikutabiri kuwa ndani ya CCM utazuka mtafaruku na kusababisha ufa ndani ya chama hicho kitu ambacho ninyi waandishi mmekishuhudia hivi karibuni?

Mimi siwezi kuongea kashfa yoyote dhidi ya mchungaji huyo bali ninachosema akipenda apeleke malalamiko yake Ikulu, kwani nako huko wapo watu wa kumjibu waliozishuhudia kazi zangu kwa miaka yote,” alitamba Sheikh Yahaya.

Alisema alitarajia kiongozi huyo wa kanisa aempe mwaliko rasmi waonane mahali popote siyo hapo kanisani ili waelezane masula ya nyota kwa undani badala ya ‘kumtisha’.

CHANZO: NIPASHE

Mwingira afunuliwa ubatizo mpya

mtume

Kiongozi wa Kanisa la Efatha Mtume na Nabii Josephat Mwingira amesema amepata mafunuo kutoka mbinguni kuhusu kuwabatiza watu kwa kuwamwagia maji kutoka kwenye ndoo. Alisema hivi karibuni alipokuwa katika kambi ya Kibaha mkoa wa Pwani.

Source: NYAKATI

Samahani hatupokei maoni kuhusu mada hii,  ukitaka kujifunza/kuwafundisha wengine kuhusu Ubatizo karibu hapa

http://strictlygospel.wordpress.com/2008/07/16/swali-8/#comment-5030

Wanawake watakaoingia ‘uchi’ kanisani kuvalishwa khanga

-Lengo ni kudhibiti tamaa mbaya ibadani

Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Kigango cha Mtakatifu Vicent wa Paulo, kilichoko Kibamba jijini Dar es salaam, umeanzisha mkakati wa kudhibiti tabia ya baadhi ya wanawake wanaovaa nguo za kumtukuza ibilisi wanapoingia kanisani.

Akizungumza Jumapili iliyopita kwa niaba ya wanawake kanisani hapo. Bi. Mary Bruno alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanawake wanaovaa nguo zisizo na heshima wanapokwenda kanisani, hali inayosababisha kukosekana kwa utulivu kwa waumuni wengine wawapo ibadani.

Alisema kutokana na hali hiyo, umoja wa wanawake kigangoni hapo, umeamua kulivalia njuga suala hilo, kwa kuwavalisha khanga wale wote watakaobainika kuendeleza jambo hilo, ili kukomesha tabia hiyo ambayo imekithiri kwa baadhi ya wanawake. Katika zoezi hilo lililoanza rasmi Jumapili, Bi. Bruno alisema kuwa waumini watakaokumbwa nalo ni wale wanaovaa nguo za kuonesha mgongo (mgongo wazi), nguo fupi, nguo za kubana na nguo zenye mipasuo mirefu.

Alisema umoja huo wa wanawake, endapo utabaini mtu aliyevalia mavazi hayo ya kumtukuza ibilisi, atachukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwemo kumvalisha khanga na hatua nyingine za kiroho.

Aidha, Padre aliyekuwa akiongoza misa katika siku hiyo, Amandus Chitumbi, alipohojiwa kuhusiana na hatua hiyo alisema kuwa ni nzuri, kwani itajenga msingi imara hususan kwa watoto wanaoendelea kukua.

Adriana Mwigani

Chidumule, Dk. Remmy waponda dansi ya sasa

Cosmas Chudumule na Dk. Remmy Ongala, waliotamba zamani katika muziki wa dansi la kidunia kabla ya kugeukia muziki wa Injili, wameponda dansi la sasa, kwa maelezo kuwa limepoteza mwelekeo. Wanamuziki hao, walikuwa sehemu ya wadau wa muziki huo, waliojitokeza jana katika mkutano ulioitishwa na Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) ili kujadili masuala mbalimbali ya muziki huo.

“Nimekuja hapa kusema ukweli. Dansi la sasa liko duni mno, inasikitisha sana, si kama enzi nilipokuwa mimi”, Chidumule alisema. Naye Dk Remmy alisema, Ubunifu katika tungo na mpangilio wa ala nao ni dhaifu hata redio za FM, nazo zimechangia kuua dansi.

–Mtanzania July 23, 2009