Maombi kwa ajili ya kanisa la Tanzania 1 June, 2012

Kuanzia tarehe 1 June 2012 tunaanza maombi maalumu kwa ajili ya toba, amani, upendo na ustawi na kukua kwa kanisa Tanzania. Tunamkaribisha yeyote atakayeweza kushiriki nasi popote pale ulipo, atakayeweza kufunga atafunga, ni maombi ya mwezi mzima!

Mistari ya kusimamia
2 Wafalme 5: 16-17
2 Nyakati 7: 14-18
Nehemia 1: 4-6
Nehemia 2: 4 na Nehemia 2: 7-8
Nehemia 4: 7-8 na 1Timotheo 2: 1-6

Mjipe moyo ndugu zetu wa Zanzibar, aliye ndani yetu ni mkuu kuliko wote!

Mungu Ibariki na kuilinda Tanzania!

–Rose Lusinde

Nani ni mume wangu?

Naomba maombi kwa ajili ya ufunuo juu ya nani ni Mume wangu, niliolewa na kijana mmoja wakati huo mimi nilikua nimezaa na mtu mwingine miaka ya nyuma. Nimeishi na huyu kijana sasa ni mwaka wa 8 sijabahatika kupata mtoto naye, akaamua kuzaa na mtu mwingine ila bado anaishi na mimi, sasa tatizo linakuja kuwa mimi nikaanza uhusiano na kijana mwingine na anataka anioe ila huyu mwingine ninayeishi naye hatuongei wala nini, ni mwezi sasa umepita.

Naomba maombezi yenu nipate mtoto na nitambue mume wangu ni yupi, niombeeni kwa jina la Yesu nipate mapacha hata watatu ili huyu baba asininyanyase. Asanteni

Teckla

Tumsifu Yesu Kristo!

Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Mimi ni mama mwenye Familia ya watoto wawili ninaomba mnisaide kuniombea familia yangu imeingiwa na mfadhaiko mkubwa mtoto wa kwanza kati ya hawa wawili anakunywa sana pombe hata siku nyingine kushindwa kwenda kazini. hajaoa bado. na anavuta sigara sana, vilevile hawa wote wawili hawana mwammko kabisa wa kumfuata Yesu, hawaendi kanisani siku za jumapili, nimelazimisha hawaelewi inaniuma sana; jamani mwenyewe sina mume, ninatamani sana ningepata mume ili niweze kufunga ndoa niishi maisha ya kumpendeza Mungu badala ya kuhangaika na waume za watu hili linanisikitisha sana na kuniudhi mno lakini sina bahati hiyo ya kumpata mume wa kwangu mwenyewe.

Mimi ni mtumishi ninafanya kazi ya kuajiriwa; lakini ofisi ninayofanyia kazi,ina majungu kupita kiasi watu ni waongo sana, wasengenyaji, wana wivu kupindukia washirikina pia wamo, wengi wao hawapendani, kwa kweli; yote haya yanahitaji msaada wa Mungu tu, watu wameonywa lakini hawakubali kujirekebisha, tafadhalini wakristo wenzangu wanamaombi tusaidieni, tunahitaji msaada wa maombi. ninaomba maombi yenu ili kuweza kuokoa familia yangu na kazi yangu.

Stella

Ninateseka, niombeeni!

Shalom wapendwa wa blog hii! Ninaomba ye yote atakayesoma ujumbe huu aungane nani katika maombi. Nimeolewa na sasa ni mwaka wa sita sijafanikiwa kupata mtoto. Pia shetani amefunga mafanikio yangu katika nyanja zote, ninateseka sana lakini namtumainia Mungu kupitia Yesu Kristo atanitendea muujiza. Sasa ninaomba mniombee kunihamisha kutoka kwenye nguvu za giza. Shetani anataka nimtumikie nami sitaki kabisa kufanya kazi ya mizimu. Nahitaji kuwa mtumishi wa Yesu. Naomba sana mniommbee nami naamini yote yana mwisho.

Magda

Nasumbuliwa na magonjwa; Nahitaji Maombi

Bwana Yesu asifiwe!

Mimi ninaishi Ubungo Dar es salaam. Nimekuwa nikisumbuliwa sana na magonjwa kwa miaka mingi. Magonjwa ambayo yananisumbua ni: Vidonda vya tumbo; Vidonda vya koo; Vidonda vya ulimi; Vidonda kichwani; Kuhema kwa shida; Maumivu ya kifua; Allergy za mayai,manukato na kudhoofu kwa mwili. Nimeshaonana na madaktari wengi bila mafanikio.

Nahitaji maombi ili Mungu aweze kuniponya! Pia naomba Neno la kusimamia na kutunza uponyaji wangu na namna ya kuliatamia ili hadi uponyaji udhihirike.  Natanguliza shukurani zangu.

Mungu awabariki na kuwafanikisha.

Lucas L. Maro

Wazazi wangu wanataka kuachana, Nifanyeje?

Bwana Yesu asifiwe ndugu ktk Yesu! Nafurahi sana kuona hii website.

Naomba ndugu muniombee niko kwenye majaribu makubwa hadi inafika wakati najisikia sina hata nguvu ya kuomba. Mara kwa mara huwa najiuliza kama kweli Mungu yuko karibu nami. Lakini naamini siku moja Mungu atanikumbuka.

Cha kwanza naomba muniombee, wazazi wangu wanataka ku-divorce, yaani baba yangu alishatuacha nyumbani mimi na wadogo zangu na mama yangu. Sasa wazazi hawasikilizani na wanataka ku-divorce. Mimi nimejaribu kuwaombea muda mrefu na kuwashauri lakini hawanisikii, nami kwa hivyo nimeshachoka na sijui nifanye nini.

Kingine mnaonaje nikiwashauri wazazi wangu kuachana, kweli nitakuwa nimefanya dhambi? Sijui cha kufanya, lakini neno la Mungu linasema kama kilicho tenganishwa na Mungu mwanadamu asikitenganishe. Naomba mnisaidie hapo!

Cha tatu naomba mnisaidie kuomba ili nipate mume mwema kutoka kwa Mungu kwa sababu mara nyingi naogopaga nasema labda sitakuja kuolewa. Sababu ni kuwa mambo ninayoyaona kwa wazazi wangu yananiogopesha sana hadi nakata tamaa,  najiuliza hivi nikipata mume ambaye hatusikilizani hali itakuwa ya namna gani?.

Jamani nawaombeni mnisadie sana kwa maombi na ushauri.
Naitwa Neema Gashu na nina miaka 25.

Mungu awabariki sana!

Miguu inavimba, tatizo halionekani!

Bwana Yesu asifiwe sana,wapendwa naomba mniombee kwani hakika nahitaji maombi na msaada wa Roho Mtakatifu ili niweze kupona, nimekuwa nikiumwa miguu kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita, imekuwa ikivimba tu, nimehangaika sana bila mafanikio, nimepima vipimo vyote lakini sijaonekana na ugonjwa wowote, kwa hiyo hospital hata dawa hawanipi maana hawajui wanipe dawa gani,imekuwa ikinininya raha sana au kama kuna mtu anayeweza kunishauri nituumie dawa gani nitafurahi sana. Mungu awabariki sana.

Nderingio

Israel, Israel, Israel mimi nikikuacha na Mungu anisahau!

Wapendwa napenda tena kuwaita toka ndani ya moyo wangu, mje msimame na taifa la Israeli wakati huu, nina mengi sana ya kusema juu ya taifa la Israeli, watu wake, na jiji la Jerusalem, Si kwamba nimepewa mzigo tu wa kusimama kwa ajili ya taifa la Israeli, lakini nina connection na bond isiyovunjika na taifa la Israeli, kwangu Israeli ni taifa rafiki, pia ni taifa ndugu kwangu, nimeunganishwa na hili taifa, liko ndani ya moyo wangu, upendo nilionao kwa ajili ya hili taifa ni upendo usioelezeka, nimelikumbatia hili taifa, hata kama adui anataka kurusha mishale juu ya Israeli na wayahudi, inipate mimi kwanza, lakini isiifikie taifa la Israeli wala watu wake ambao Mungu amenipa na nina wapenda sana.

I do real have a special connection with Israel, Israeli inapoingia kwenye shida, na mimi huwa ninapata mahangaiko sana ndani yangu, ni kama vile ndugu zangu wako kwenye shida, huwa kuna wakati namuuliza Mungu ni kitu gani hiki?

kwa watu wanaofahamu wanajua Israeli ipo karibu sana kuingia katika vita, iko kwenye hali ya kivita.

Mpango wa Palestina wa kudai taifa huru la palestina katika mipaka kabla ya vita ile ya mwaka 1967 Israel iliposhinda na kuliunganisha tena jiji la Jerusalem ni mpango hatari sana kwa uhai wa taifa la Israeli,

katika Muda wa siku chache zijazo, macho ya ulimwengu wote yataelekea mashariki ya kati, kuna mambo ambayo kwa kweli ukiyaangalia kwa macho ya Rohoni, yanasukuma kutimilika kwa nabii muhimu sana katika Biblia, wale student of Bible prophecy na wale wanaofuatilia habari ya Taifa la Israeli kwa karibu wanajua kitu ninachosema.

Vile vile natoa wito kwa serikali au taifa la Tanzania, Rais, na wizara ya mambo ya nje, na washauri wake wa mambo ya nje, taifa la Tanzania lisiingie katika muunganiko wa mataifa ambayo yatapiga kura kulitambua taifa la Palestine katika mipaka kabla ya vita ile ya mwaka 1967. Taifa la Tanzania lisipigie kura wala kushiriki kui endorse makubaliono yoyote ambayo yanalitambua taifa la palestine na kuugawa mji wa Jerusalem na nchi ya Israeli.

Taifa la Tanzania kama mwanachama huru wa Umoja wa Mataifa, huwa linapiga kura pamoja na mataifa mengine ambayo yako katika baraza kuu la umoja wa matiafa  na pia ni wanachama wa umoja wa mataifa.

Maandiko ninayosoma yananiambia hasira kali ya Mungu ipo kwa ajili ya mataifa ambayo yamekusanyika au yanakusanyika kwa ajili ya kuukandamiza na kuionea sayuni, kuionea Jerusalem, na taifa la Israeli.

Kwa watu wanaotaka kuungana nami kwa maombi, hebu kwa walau masaa machache au dakika chache tu, soma Isaya 62:1-7 pata muda wa kumwambia Mungu kitu juu ya Israeli. Mimi sitaki kuona Israeli inaingia katika matatizo, kwahiyo nina jukumu la Kuomba sana kwa ajili yake, na kulitia moyo taifa la Israeli, lisifadhaike, wala kupoteza tumaini, eh Israeli, sema unazo nguvu, kwa maana Mungu wako yupo karibu sana nawe apate kukutetea na kukupigania, yeye aliye mlinzi wako hatalala wala kusinzia.

Inuka eh Bwana uitetee Israeli mataifa yaliyo ulimwenguni na watu wa kabila zote, dini zote, na watu wote wapate kuona ya kwamba wewe hujaiacha sayuni bali upo karibu sana na sayuni, eh, Mungu wangu majira na Nyakati za wewe kuonekana sayuni zimetimia, inuka eh Bwana mataifa waone ya kwamba wewe Ndiye Mungu wa Israeli. Na Israeli ni mtumishi wako.

Lwitiko Katule

Nishaurini watu wa Mungu!

Shalom, Ninaomba miniombee niyajue mapenzi ya Mungu katika kufanya maamuzi yafuatayo :- Mume wangu yupo Moshi kimasomo kwa miaka mitano na huu ndio mwaka wa kwanza, na mimi nipo Arusha. Tuliona kama tunaweza kuishi hivyo lakini bado hatuna mtoto na ni miaka miwili tangu tumefunga ndoa. Kwahiyo nikaanza kuwaza kuhamia Moshi, na nimeahidiwa kazi na kampuni moja ya waarabu. At the same time kuna nyumba ya kupanga tuliitegemea kwani hapo tunapokaa kwa sasa Arusha, si mazingira mazuri na pia wiki iliyopita nimempelekea jirani yangu (Ambaye ni rafiki) kitu fulani ambacho hakua nacho ( nikamwambia naona mmeishiwa hiki kitu) msichana wake akapokea.

Lakini kesho yake mchana nikakikuta mlangoni kwangu, nilipouliza wakaniamia walichukia nimewaambia wameishiwa. Kweli nimeumia na mpaka sasa ninahitaji rehema za Mungu, kwani nimekua mkimbizi nyumbani kwangu ambapo nimepanga kwa gharama kubwa mno. Kwa sasa nipo kwa mama yangu wa kiroho kwa kuwa mume wangu yupo Moshi. Ninajua sio sawa lakini moyo wangu umeumia sana kwa kile walichokifanya kwanza ukiangalia nimekua nikiwasaidia kila wanapokwama na kunishirikisha.Na niliposema wameishiwa sikua na maana ya pesa au kitu kingine chochote zaidi ya vibanio vya nguo.

Jamani hapa nilipo nasikia kama hili eneo la kifua linapasuka kwa maumivu na uchungu, NIOMBEENI JAMANI WAPENDWA.

Faith

Nifanyeje katika haya?

Mimi ninatamani kusimama kwenye wokovu ila nashindwa nifanyeje? sababu ninaishi na mume wangu hatujafunga ndoa sababu bado hatujaweza kutekeleza yale yanayotakiwa kwa wazazi. Japo wao hawajatuzuia lakini sisi na mume wangu tunahitaji kufanya kitu kwa wazazi ili tutakapofunga ndoa tupate baraka zao.Kinachotuzuia kwenda kwa wazazi hatuna uwezo kwani mume wangu amesoma lakini hajapata kazi toka 2009. Naomba mniombee Mungu ampe kazi mume wangu na pia tuweze kufunga ndoa tuwe na amani. Mungu awabariki sana.

Beatrice Mollel

Je, Umeijaribu Njia

Ya Kristo?

Yaliyopita Yamepita, usiangalie nyuma ifuate njia mbele yako! Mungu ametupa uwezo wa kushinda kila kinachoingilia njia yetu, Unayo nguvu kwa kinywa chako kumwambia shetani akupishe njiani.Usirundike matatizo yako ya zamani ukaendelea nayo hata sasa, yaondoe njiani kwako ili ukutane na njia ya Mungu.. aliyokutengenezea!… Ni uamuzi wak o! Ikiwa ungependaBwana Yesu akutengenezee njia yako au ujirundikie mizigo na ukae njia yako!!

 

—Yohana 16:4a—

Nahitaji Msaada

Bwana Yesu Asifiwe.

Nina mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja. Tuna kama miezi sita toka tumeanza. Hivi karibuni rafiki yangu huyu amekuwa haeleweki. Kabla ya huyo kijana kuja kwangu alikuwa na binti mwingine ambaye wanasema ameenda kwa mganga na ndiye anayekuwa akisambaratisha uhusiano wetu ndio maana kwa sasa hatuelewani. Nifanyeje? Niachane na huyo kijana? Nitajuaje kama ni nguvu za giza ndio zinamsumbua au yeye mwenye ndio kaamua anataka kuniacha? wapendwa naomba mnisaidie.

–Rose

Wazazi wanapiga chenga kufanya mazungumzo.

Bwana yesu asifiwe wapendwa! Nina rafiki wa kike ambaye kwa dhamiri yangu nahisi ndio mwenzi wa maisha yangu.  Tarehe  kumi mwezi wa kumi na mbili mwaka jana nilienda kwao kujitambulisha na kwa jinsi nilivyopokelewa nikaona kama kuna mashaka fulani wanakuwa nayo, wakaahirisha mazungumzo mpaka wakati mwingine. Ukweli ni kwamba tunatofautiana madhehebu yeye Mlutheri mie TAG lakini wote tumeokoka. Sisi binafsi hakuna kikwazo kati yetu isipokuwa kwa wazazi wake, na hapa nilipo nataka nioe maana nahisi nimechelewa sana na kwao kila nikiomba tufanye mazungumzo wanapiga chenga. Nahisi nafsi yangu kuchoka mpaka natamani nimtafute mtu mwingine. Niko njia panda wapendwa naomba ushauri na maombi pia juu ya hili.

David

Prayer of Salvation

Rom 10:9 “if you confess with your mouth the Lord Jesus and believe in your heart that God has raised Him from the dead, you will be saved.NKJV”

Asking Jesus to come in to your life is as simple as making the request, but is not to be taken lightly! Jesus said “Repent” and to consider the cost.

John 15:12-14 “This is My commandment, that you love one another as I have loved you. 13 Greater love has no one than this, than to lay down one’s life for his friends. 14 You are My friends if you do whatever I command you. NKJV

Jesus made it pretty simple to inherit salvation. The two greatest commands are to Love the Lord your God with all your heart, soul and strength. The other is to Love your neighbor. The Bible teaches what Love is. And if we obey him he calls us his friend. Make it your desire to honor God by learning what that means, then, live it.

1 Peter 1:15 “..but as He who called you is holy, you also be holy in all your conduct,NKJV”

We are also called to live Holy lives when we follow Jesus. We may not wake up the next morning in all perfection, but now we have a goal. And you wont be alone in your walk. When we confess Jesus as Lord, the Holy Spirit starts doing his work in us, and we become a “Work in Progress”! So we don’t have to worry if it takes a while to figure out this walk. Just so the EFFORT is there. So If you want to invite the Holy Spirit in for the first time, or if you have fallen and want to re-commit your life to him, pray this prayer.

Lord, I realize that I am a sinner, and it is only by your blood that you shed on the cross that can cleanse me. I believe that you are the Son of God, and died on the Cross for me; Then God raised you on the third day and now sit at the right hand of the Father with all authority. I want you and need you in my life. And right now I am asking you to be Lord and Savior of my life. Thank you Jesus. Amen

Nisaidieni Wapendwa!

Bwana Yesu Asifiwe, Mimi ni mama wa watoto wawili wa kiume, nimeishi na mume wangu miaka 15. Lakini mume wangu amekuwa na uhusiano na mwanamke mwingine wa kiislam, tangu wiki 2 zilizopita amekuwa ananipiga sana akinitaka niondoke kwake hataki kuniona, kitu ambacho kinaniumiza sana, amefikia kuniambia nisipoondoka ataniua. Mimi bado ninampenda sana, ninamwita Yesu katika hili jaribu na imani atanipigania. Naomba uniweke katika maombi.

Grace B--

Nani wa Kumuoa?

Wapendwa wangu katika Kristo naombeni msaada wa majibu ya swali langu la 10/7/2010 ambalo niliomba ushauri kwenu kuhusu muda halisi kibiblia wa kuoa au kuolewa.Binafsi nimekuwa ktkt wakati tete sana haswa inapofikia hapo.Nahitaji kuwa na mke na kikwazo kikubwa kwangu,imekuwa ni Nimuoe Nani? Hii ni kwa sababu ya aina ya maisha ambayo nimeiona kwa mabinti wengi wa sasa, hata baadhi yao wakisema wameokoka. Imenivunja moyo, ninajua MUNGU hashindwi na jambo lolote.

Maombi yenu ni ya thamani sana kwangu.Nimeona watu wakirudi nyuma mara baada ya kuingia kwenye ndoa.MUNGU AWABARIKI SANA.

Aggrey Charles

Maombi Ni Silaha!

Bwana Yesu Asifiwe! Naomba mniombee nimekuwa nikinenwa mabaya kila baya ni mimi nimefanya naambiwa nimeathirika natembea na waume za watu kitu ambacho si chakweli kila anaenipenda akiambiwa anavunja mawasiliano nisaidie naamini Mungu anauwezo wa kuvunja hii roho.

–Mat

————————————————————————————–

Bwana yesu asifiwe wapendwa, napenda kuwashirikisha ugonjwa wa mtoto wa rafiki yangu anayeitwa Rehema Shabani alianza kuumwa akiwa na miaka 4 kama degedege ikawa haiponi akaenda kwa wataalamu wa vichwa akapimwa ikaonekana anakovo kwenye kichwa akaanza dozi akaambiwa akitumia dawa miaka 2 atapona lakini mpaka sasa ni miaka 6 hali ndo inazidi kuwa tete haieleweki kama ni kifafa au ni ugonjwa gani naomba watu wa mungu tushirikiane kwenye maombi kwa sababu huyo mama ni mjane na huyo mtoto ndie binti pekee mama anaitwa Halima

–Rose

————————————————————————————–

Bwana ASIFIWE, Naomba maombie yenu, mniombee kuhusu ndoa yangu imeingiliwa na dada mmoja mwenye imani za kishirikinana mimi na mwamini Mungu najua siku moja atanitoa katika jaribu hilo la maisha yangu hivyo naomba maombi yenu wapendwa pamoja na afya yangu pia sio nzuri nina sumbuliwa sana na tumbo

–ANNET

————————————————————————————–

Wapendwa Bwana Yesu asifiwe. Mungu wabariki sana katika huduma yenu mzidi kutiwa nguvu kwani mnatusaidia sana. Mimi ninahitaji ninaishi ndani ya ndoa sasa ni miaka miwili sijapata mtoto naomba mnisaidie kuomba Mungu anijalie haja ya moyo wangu kwani nimepita kwenye hali mbaya ila Mungu ananipigania nimeumwa tumbo wakati wote nikienda hospitali madaktari wanasema sina tatizo lolote na sijui ninashida gani ila naamini Mungu anaweza yote kwake yeye aminiye.

Mungu awabariki sana watumishi

Celina J

Unapoomba wakumbuke pia na hawa…

GM, ana mahitaji yafuatayo:

1.Ninafanya kazi kwa contract, imeisha tangu mwanzo wa mwezi huu wa nane, lakini sijajibiwa kitu tangu nimeomba ku-renew ninafanya kazi hii kila baada ya miaka 3 nina-renew, lakini hii contract ilikuwa ina utata kuambiwa sifanyi kazi ya kuridhisha ukizingatia huu ni mwaka wa kumi ninafanya kazi hapa kwenye hii organisation. Ninaombeni maombi yenu ya nguvu nikapate majibu yenye habari njema. Msaada wangu unatoka kwa Mungu.

2.Pia yapata miezi 7 sasa muda mwingine ninaota kwamba ninakula nyama nikiwa nimelala au chakula, nimesikia kwenye mahubiri ni jambo la kishetani, matambiko niliyofanyiwa zamani pasipo kujua au kujua nilishafanyiwa deliverance yote niliyakataa, nimekuwa naomba kwa ajili ya jambo hili lakini linapotea na kurudi mara kwa mara. Ninaomba maomba yenu pia.

3.Nina kaka yangu mkubwa hapatani na familia anamsumbua sana mama yetu. ninaomba maombi yenu pia akarudishe moyo ana kiburi na pia visasi. Hana upendo kabisa na sisi dada zake anasema tunapendelewa na mama baada ya baba kufariki. Amekuwa ni mgomvi sana sana, anaitwa (Tadei) ninaomba maombi yenu amani ikarudi tena nyumbani kwetu na tuweze kupatana watoto wote wa familia.

Lucy, Anahitaji lifuatalo:

Bwana yesu asifiwe,wapendwa nahitaji maombi maisha yangu ya shule yamekuwa magumu niko katika wakati mgumu kimaisha na kimasomo.

Justine Mwadimwe, ana mahitaji yafuatayo:

Mimi nimeombewa uokovu muda mfupi umepita. Mahali nilipo ni pagumu kusimama katika uokovu hasa kwa mtu kama mimi kijana.Naomba mnisaidie kwa maombi ili niweze kusimama ni mtukuze Mungu kwa hali na mali kwa ajili ya utukufu wake.Napenda kumtumikia Mungu.

Kuelekea uchaguzi mkuu October 2010

Wateule,
Tuombee Taifa la Tanzania, Uchaguzi umekaribia na kila mwanasiasa anatafuta; wapo wanaotafuta udiwani, wapo wa ubunge na wengine uraisi. Tuombe Mungu ili uchaguzi uwe wa amani na salama bila machafuko yoyote yale.

Tuombe na kukemea nguvu za giza kwa baadhi ya wanasiasa, zisifanye kazi, pia tuwaombee wakristo wote waliojiandikisha kugombea nyadhifa mbalimbali za siasa ili Neema ya Mungu iwafunike.

Tunahitaji Injili isonge mbele watu wakombolewe kutoka kwenye mitego ya shetani.

Jerome Kaera

Kumekua na mitego ya shetani kwenye familia yangu!

Mungu apewe sifa Watumishi wake. Mimi kwanza namshukuru Mungu kwa uzima wake, pili ninaomba tujumuike pamoja katika kuiombea familia ya kwetu. Kumekuwa na mitego ya shetani yakiwemo magonjwa, Kama vile: Baba mzazi ana kisukari karibu miaka 10 na zaidi sasa. Baadhi ya ndugu zangu wamekuwa hawapati watoto, wengine mimba zinatoka bila mpangilio. Wazazi wanasema ni laana za ukoo. Ninaomba tuvunje hizi laana kwa jina la Yesu ili waweze kufunguliwa. Amen

Omega Kessy

Maombi ya Hana kwa Mungu – 1 Samwel 2:1-10

2:1 Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;

2:2 Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.

2:3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.

2:4 Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.

2:5 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.

2:6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.

2:7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.

2:8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.

2:9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;

2:10 Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

Maombezi

Naomba mniombee nina tatizo la kuchukia bila sababu,  jamani kitu hiki kinanikwaza sana pale ninapokaa peke yangu na kujiuliza kinachonifanya nichukie ni nini saelewi. na saa nyingine nikikaa napata maumivu ya mgongo sana na kifua. pia naamini mungu anaweza nina imani kwa maombi yenu Mungu ataniponya.

pia ninawaomba mumuombee mume wangu anaumwa sana kiuno kila siku, ametumia kila dawa na ameonana na madaktari wakubwa wamempima lakini hawaoni kitu. naombeni mtusaidie kwa maombi. Pia naomba muwaombee watoto wangu wawili ambao wa kwanza ana miaka 7 na huyu mdogo ana miaka 4. natamani wawe na hofu ya mungu na mungu awafunike kwa damu ya yesu wasipate magonjwa, wawe na heshima kwa watu wote na wafaulu vizuri ktk masomo yao.

mungu wetu mwenye nguvu na awabariki wote na awape sawa na mahitaji ya mioyo yenu.
mungu awabariki sana.

Maria Abed

_______________________________________________

Bwana Yesu Kristo asifiwe. Naomba maombi Mungu anisaidie nisimame kiroho, nisiwe na hofu popote linapotokea jaribu nguvu za Roho Mtakatifu ziwe juu yangu kunishindia. Pia naomba mniombee nipate kazi, nimemaliza chuo tangu 2008 sijapata kazi ya kudumu.Mwisho ninaomba Mungu anisaidie niweze kushinda kesi ya nyumba ambayo hukumu imepangwa tarehe 14 mwezi wa sita.

Rache Moiso

__________________________________________________

Bwana yesu apewe sifa,naomba maombi juu ya maisha yangu ya wokovu yangu mashambulizi mazito sana, sina hamu ya kuomba, Bwana amenipa huduma na ninaipenda sana but nina mapito yanayoharibu kazi na wokovu wangu. Mungu ananiona na kunifahamu hivo naomba mnitie moyo katika hili sana sana eneo la kumpata mwenzi.

Moses makalanga

_________________________________________________

Shalom watumishi wa Mungu naomba maombi yenu kaka yangu ni mlevi sana anakunywa anashindwa hata kuendesha maisha ya familia yake watoto wamekuwa kama hawana baba hadi mke kamkimbia tuombe rehema za Mungu zimfungue katika hilo.

Grace Anthony

__________________________________________________

 

Tuwakumbuke kwa maombi

Bwana asifiwe sana watumishi wa Mungu.Kuna mtu anannisumbua sana,ananitaka kimapenzi mimi nakataa kwa jina la Yesu hataki kukubali ukweli.Nimeolewa na nina mtoto na nimeokoka pia mimi na mume wangu tunapendana.Naomba maombi yenu mawazo yake kwangu yafutike milele kwani sitaki kumkosea Mungu wangu. Jina la Bwana lihimidiwe, Amina
–Yusta
____________________________________________
Mniombee mtoto wangu James aache tabia mbaya za ujana Mungu amfungue amweke huru toka kifungo cha shetani, Pia tuwaombee watoto wanaovuta bangi waache kuvuta hapa Musoma wapende masomo katika jina la Yesu
–Jane
____________________________________________
Bwana Yesu asifiwe! Naomba kuomba pamoja nanyi ili Yesu ambadilishe mke wangu katika mawazo ya kutaka talaka. Mungu awape pia awape hekima na busara wote wanaomshauri na kumpa nguvu katika jitihada za kuvunja ndoa. Mungu ameshawadhihirisha kwangu tayari.
–Damas
____________________________________________
Nashukuru kwa wote ambao mtajumuika katika maombezi na Mungu awape neema na baraka. Naomba mniombee nipate kazi na pia rafiki yangu hajafanikiwa kupata mtoto kwenye ndoa kwa muda wa miaka saba. Asanteni kwa upendo wenu na Mungu awape nguvu.
–Aunty Nyamizi

_____________________________________________________________