Category Archives: MICHEZO
Sisi ni washindi!

“Mungu wetu anatushindia, ukimuamini hata wewe utakuwa mshindi daima, Bwana Yesu ameniwezesha nimeshinda tena, nimekuwa wa kwanza kati ya washiriki 5231 tu. Jina la Bwana litukuzwe” – Phaustine Baha
Maigizo ya Kikristo
Wasanii ambao hawajaokoka wamekuwa wakiigiza maigizo ya Kikristo na wengine wanaigiza hadi mambo ya ndani kabisa kama vile kuongoza watu sala ya toba, kunena kwa lugha na kukemea mapepo!

Je, wasanii ambao hawajaokoka kuigiza mambo ya Ukristo kuna athari chanya au hasi kwa Ukristo?

Kundi maarufu la Orijinol Komedi walialikwa na kuigiza kwenye tamasha la uzinduzi wa albam ya nyimbo za injili na kwaya ya Haleluya ya kanisa la EAGT Morogoro katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro hivi karibuni.
Kundi lajipanga kupeleka Injili

Viongozi JEWAWI wakisoma Risala na kutabainisha mikakati yao ya kuhubiri Injili mkoa wa Dar-es-salaam na kuombea Umoja kati yao wamama waliookoka na walio nje na kanisa, ili wamama ambao hawajaokoka wavutwe na mwenendo wa kinamama waliookoka, waje kwa Yesu!
Flora Mbasha kwenye tamasha la Mseto wa WAHAPAHAPA
Muimbaji wa Injili Tanzania mwenye album za JIPE MOYO, UNIFICHE, FURAHA YAKO kwa sasa anasikika na wimbo wa WANAWAKE wenye mahadhi ya mchiriku. Atatumbuiza kwenye tamasha la uzinduzi wa album ya MSETO WA WAHAPAHAPA litakalofanyika 7 June 2009 viwanja vya Coco Beach, mbali na yeye kushiriki Tamasha hilo, waimbaji wa muziki mchanganyiko kama Mzee Yusuph (Muimbaji wa Taarabu) Banana Zoro, Enika (Muziki wa kizazi kipya) Calora Kinasha na Wahapahapa Band wataimba.
Pia WAHAPAHAPA ni tamthilia ya mchezo unaosikiwa kila jumatatu kwenye Radio Free Africa (RFA) na Radio One, lengo lao ni kuangalia athari za VVU/UKIMWI kwa vijana. Mbasha ni muimbaji pekee wa Muziki wa Injili atakayetumbuiza.
Kama Siyo Yesu sijui ningekuwa wapi! – Pona

Muimbaji wa nyimbo za injili za kufoka-foka Pona, kama anavyojulikana na wengi kwa jina hilo, amealikwa nchini Marekani kufanya maonesho mawili. Anasema anaipenda sana Hip Hop maana ametoka Mbali, Kama siye Yesu asingekua hapo alipo na atazidi kumuimbia yeye aliye mkombozi wake!
Pichani akiwa Saddleback Church, lake Forest California.

Kijitonyama Upendo Group Ladies
Uzinduzi wa Christina Shusho na mavazi yake!

Christina Shusho akiwa na Mbunge wa kuteuliwa Mh. Alishamaa Kwegir
Tarehe 30 November 2008 Christina Shusho alizindua album yake ya UNIKUMBUKE walikuwepo waimbaji mbalimbali walioalikwa kuimba. Katika tukio la tofauti siku ile alionesha mavazi aliyoyabuni mwenyewe, anasema mavazi hayo ni kwa ajili ya wakristo.
PICHA ZA TUKIO HILI KWA HISANI YA ANDREW NGAI

Upendo Nkone, Christina Shusho na Bahati Bukuku.



Kaka aanza maandalizi ya kumtumikia Mungu!
Mchezaji maarufu wa Brazil Kaka ametangaza Jumapili nia yake ya kurudi kuchezea team yake ya nyumbani Sao Paulo. Mchezaji huyo anategemea kustaafu soka baada ya hapo kabla hajarudi kwenye kanisa la Christ Evangelical Church na kuwa mchungaji.
“Mchezaji anapokaribia kumaliza kazi yake, inabidi afikirie nini afanya katika maisha yake ya baadae” alisema Kaka
“Life changes dramatically. When you are 20 years old, you think about one thing. When you are 30, you change your mind. For this reason, it is important for me to begin to think about what I want to do with the rest of my life. I am going to begin my preparations to one day become a priest,” said the star of the Brazilian national soccer team.
Kaka ni mfuasi wa kanisa la wokovu la Christ Evangelical church.
-chinaview-
Faustine Baha ashinda mbio za marathon!
Faustine Baha ameshinda mbio za marathon tarehe 19-10-2008 Ujerumani. “Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa mshindi wa kwanza kwa kukimbia 2:13:03 km 42 kati ya watu 160,000. kwakweli nilimtanguliza Mungu kabla ya mbio namshukuru ameniwezesha kuwa mshindi”
Kwa wasiomfahamu Faustine aliwahi kupata pesa nyingi kwa njia za giza hapo kabla hajamjua Yesu, alizunguka kwa waganga kutafuta utajiri na anawafahamu waganga wengi hapa Tanzania. Lakini sasa yeye ni mtumishi wa Mungu, ni mwanariadha na ni mwenyeji wa Arusha.
Angela katika hafla ya kupongezwa!
Askofu na mama Askofu Deo Lubala kwa pamoja wakimpongeza binti yao Angela Luballa kwa kushinda ubalozi wa bia ya redds tarehe 6 August katika hotel ya New Africa hotel, yawezekana wana lengo la kumsaidia binti yao kwa vile amefanikiwa kushinda ataweza kuitumia nafasi yake kuonyesha nini alikusudia.
Angela awa balozi wa Redds!
Faustine Baha, Mlokole anayeiwakilisha Tanzania
Ni jambo la kumshukuru Mungu kuona vijana waliookoka kufanya vyema katika fani mbalimbali hii huonesha wazi Mungu wanayemtumaini ndiye anayewawezesha. Faustine Baha mwanariadha mtanzania mwenyeji wa Arusha ameshindana nchini ujerumani hivi karibuni katika riadha ya kimataifa amekua mshindi wa pili kati ya wanariadha 12,500. Utukufu na Sifa ni kwa Bwana wa Majeshi.
Akiwapita wenzake
Faustine katika mashindano
KAKA – Mcheza soka anayependa kuwa Mchungaji
Wapenzi wa mpira wa miguu bila shaka KAKA sio jina geni kwao. KAKA ni kijana ambaye ameokoka na siku zote katika mechi anazocheza na kushinda anamtukuza Mungu na anapenda kusema mara nyingi “I don’t win alone, I want to thank God for all the victories and achievements I had this year as a player.”
Mtumishi wa Mungu KAKA ambaye ni balozi wa Yesu katika soka la kimataifa alisema pia katika vyombo vya habari “I bring here two awards – one is my son, who is coming soon. The other is this FIFA trophy. I want to give it to God and place it in this church, in Lord’s house, so that everyone can see it,”
Kaka hupenda kuongelea imani yake ya Yesu Kristo hadharani na kuzungumzia upendo wa Mungu, anapofunga goli huinua mikono yake juu na kumshukuru Mungu, katika moja ya mechi ya World Cup aliposhinda alionesha T-shirt iliyoandikwa “I belong to Christ” baadae alilimpa rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva.
Ni kijana mwenye miaka 26 anayempenda Yesu na anasema anapenda kuwa mchungaji akiacha kucheza mpira.














