Tunatakiwa kutazama kwa macho ya rohoni! – Kamugisha

kanisa

Wapendwa katika BWANA YESU KRISTO.

Ni neema kubwa kutoa sadaka yangu katika blog ya INJILI HALISI.Binafsi sikujua kama kuna siku nitatoa hii sadaka kwa wale wote wenye DHAMIRA YA KUISHI NDANI YA UNYENYEKEVU HALISI yaani unyeyekevu wa YESU (Wafilipi 2:3-4).

Lakini Mungu aliye hai anayetangaza mwisho kabla ya mwanzo alijua ya kwamba UJUMBE WAKE  UTATUFANYA TUANZE KUISHI NDANI YA UHURU HALISI yaani uhuru wa Roho Mtakatifu(2Wakorintho 3:17).

 Kiini na chanzo cha kutamani na hatimaye kuingia ndani ya mioyo ya wanyenyekevu wote duniani ni mjadala wa mwaka 2012 kuhusu nukuu ya nabii TB JOSHUA ambayo alitabiri ajali ya ndege iliyotokea Kenya na kumuua marehemu George Saitoti.

Katika mjadala huo ambao ulionekana kuwa na mvutano mkubwa huku mioyo ya washiriki ikivua nguo na kubaki uchi kabisa, Roho Mtakatifu amenifunulia mengi makubwa na magumu ambayo sikuyajua (Yeremia 33:3).Kabla ya kueleza kile ambacho ROHO WA MUNGU

ALIYE ameniongoza kusema naomba katika hekima na unyenyekevu wote kutoa shukurani zangu kwa washiriki wote nikiwataja baadhi kwa majina kama ifutavyo: Pelesi,Mwangomo,Amina,Robert.Milinga,Stella,Gwamaka,Haggai,CK Lwembe,Nduta,John Paul, Edwin Seleli,Orbi,Ivan John, Eucalyptos, James, Mabinza LS, Primi Mosile,Daniel J,John Haule,Jerry na Sam. Mungu aliye hai awafiche ndani ya moyo wake.

Maisha ndani ya Kristo ni maisha yenye changamoto katika ulimwengu wa Roho na siyo ulimwengu wa mwili!!Kuna mstari mwembamba mno unaotenganisha kati ya maarifa ya Mungu na maarifa ya shetani. Ni mstari unaotenganisha na kutofautisha upendo ulio kufa na upendo unaoishi.

Ni mstari unaotenganisha na kutofautisha watumishi wa shetani na watumishi wa Mungu,Huo mstari ni NENO LA KRISTO NDANI YA ROHO MTAKATIFU

NA ROHO MTAKATIFU NDANI YA NENO LA KRISTO. Kwa mtazamo mpana wa unyenyekevu ni lazima tukubali kwamba sisi bado ni VIPOFU NA VIZIWI

WA MAISHA YA KIROHO(ISAYA 42:18-20).Tunahitaji kuendelea kunyenyekea sana ili TUWEZE KUTEMBEA NA MACHO SABA YA MUNGU(UFUNUO 5:6,ISAYA 11:2).

Tukiweza kuingia ndani ya Roho (macho) saba za Mungu KILA KITU KITAKUWA WAZI KABISA na yote yaliyokuwa yamefichika yatajifunua yenyewe na zaidi ya yote tutapata UTULIVU WA ROHO MTAKATIFU katika kufikiri, kunena na kutenda(1 Yohana 2:20.27,Luka 12;2).Mambo ya rohoni hujadiliwa rohoni japo yanafundishwa

katika ulimwengu wa mwili.WATUMISHI WOTE WA SHETANI WANAJULIKANA NA WATUMISHI WOTE WA MUNGU WANAJULIKANA NI KANUNI YA MUNGU KWAMBA MBWAMWITU NAO WASAIDIE KUTANGAZA INJILI YA YESU DUNIANI(WAFILIPI 1:15-18).MOTO WA YESU UNANIFANYA NITABASAMU!(LUKA 12:49-51)

Mnyenyekevu anayetafuta unyenyekevu ulio hai,

Dickson Kamugisha

Cape Town, SOUTH AFRICA.

Si dhambi kuoa wake wawili – Magreth

biblia

Japo wengi watanishangaa lakini hakuna aliyepigwa na mawe kwa kuoa wake wawili katika biblia. Lakini ukificha na kufanya kimada walikupiga mawe hadi kufa. Biblia haisemi kuwa ni dhambi ukioa wake wawili, lakini kimada ni dhambi kwa kuwa unazini.

Mapokeo ya kanisa yanaambia watu ni dhambi kuoa wake wawili na sio kweli.

–Magreth

Mtume Augustus Baraza apinga injili ya misukule!!

 • barazaa

  Misukule ni nini? Ni watu ambao hufa wakazikwa lakini sio kifo cha ukweli ni kifo cha kichawi ambapo wachawi wanafumba watu macho. Na mtu aliekufa huwa anapelekwa kulima mashamba. Wachawi wana uwezo wakuwateka watu kuwapeleka musukule ama kuwarudisha kwa nguvu za giza.

  Mimi sipingi kwamba watu wa Mungu hawawezi kurudisha mtu toka msukule.Lakini ninachopinga ni kwamba haiwezi kuwa ni kila siku nenda rudi ni kurudisha misukule

  Misukule ni disco na dansi ya wachwi. Na Mungu hawezi cheza mchezo huu na shetani kila siku kwani Yesu alishinda kifo mara moja wala haitaji kushindana na wachawi wa Misukule kila siku ili kuonyesha ana nguvu juu ya mauti.

  Alishinda mauti mara moja aliposema imekwisha UFUNUO 1-18 Mimi ni Alfa na Omega Mwanzo na Mwisho, nilikuwa nimekufa na sasa Tazama niko mzima hata milele ninazo funguo za Uzima na mauti

  Kumbuka Mungu hafanyi kazi kwa mwelekeo moja. Inapofika mhubiri kubuni Injili ya misukule inageuka na kuwa dini maana Roho wa Mungu ni kama upepo anafanya kazi kwa njia mbalimbali.

  Mtu wa Mungu anaweza kutumiwa kurudisha msukule mara kadhaa lakini hawezi kudai kwamba YEYE NISPECIALIST WAKURUDISHA WAFU WA MISUKULE EVERY DAY, EVERY CRUSADE HIYO NI MCHEZO WA KICHAWI mchezo huu unafanywa kwa wingi nchi ya HAITI ambapo wachawi huwapiga watu kufa kifo cha kimapepo hata siku 20 ambapo mtu anaonekana amekufa anazikwa halafu baada ya siku 10, 20,30,40 wachawi wanakuja kaburini mchana peupe na wanamfufua mfu.

  NAWABIENI KAMA MTUME WA YESU KRISTO.

  MUNGU HAYUMO KWENYE MCHEZO WA MISUKULE KILA SIKU NENDA RUDI HIYO NI DISCO NA NI NGOMA YA SHETANI. NI MCHEZO AMBAPO WACHAWI WANAJARIBU KUONYESHA WANA NGUVU JUU YA KIFO. SISI WAKRISTO TUNAJUA YESU AMESHINDA KIFO MARA MOJA NA WALA HATARUDIA KAMWE.

  Ishara nyingine za manabii wa Uongo hizi hapa:

  Wanauza mafuta, Vitambaa, Funguo, picha, udongo, kofuli, mishumaa, wanapenda pesa, wanaishi maisha a kifahari, wana kiburi tena wanadai wao ndio besy of the best

  Akijibu swali la ndugu Frank Daniel aliloandika kutoka Isaya 42:22 “lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa;wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka wala hapana asemaye, RUDISHA. kumbe kuna watu walioibiwa na kutekwa na hakuna awaokoae wala arudishaye

  Mtume Baraza akajibu “Mashimo na magereza ni mengi ndugu Frank andiko hili liko applicable kwa sehemu nyingi kama kwa mfano kuna gereza na mashimo mbalimbali kama ukahaba, ulevi, uchawi, wizi nakadhalika wala huwezi kulifanya misukule pekee.

  Zaburi 40 Daudi anasema Nalimgoja Bwana kwa subira akanitoa toka shimo la uharibifu. Daudi alikuwa shimoni wa msukule

  Isaya 58 Ukisoma inataja vifungu vya nira na kongwa mbali mbali kwahiyo andiko ulilotoa linazungumza juu ya nira aina nying halizungumzii msukule pekee.

  Amini usiamini nakwambia kama mtume wa Kristo ni makosa kwa mhubiri yeyote kuhubiri misukule mkoa kwa mkoa mkutano kwa mkutano. Hiyo ni confusion na ni upotovu na nimafundisho yasiyo ambatana na Kristo.

  Ikiwa Gwajima anahuduma ya Misukule mbona asiende nchi ya Haiti huko kuna wachawi wanachukua watu misukule mchana sokoni hawajifichi. Huduma yake itapamba moto huko

  Mbona asiende huko kuna watu maelfu misukule hadharani mchana.

  Ikiwa yuko tayari nitamnunulia ticketi ya ndege nimlipie hoteli miezi sita twende naye huko nchini Haiti arudishe misukule, yaani watu wasiokoke lakini kila siku akiamka tunaenda naye sokoni Haiti kupambana na wachawi wanaoteka misukule na Gwajima anarudisha, ikifika jioni tunaenda kulala asubuhi ikifika tunakunywa chai tunaenda sokoni.

  Sijui kama mnaipata point yangu? Je hii ndio Injili Yesu ametutuma tuhubiri kila siku? Kuchalenge wachawi ama tuhubiri watu waokolewe?

  Naomba majibu labda nimechanganyikiwa!!

  –Mtume Augustus Baraza Matibila

Maoni juu ya Mpinga Kristo atakavyokuwa!!

mpingaakristo

WOKOVU WA BAADAYE WA ISRAEL.

KWELI KUU: Kukubalika kwa Kristo kama Masihi kutaleta matokeo ya kupandikizwa tena.

MSTARI WA KUKUMBUKA:
Na hao pia wasipokaa katika kutokuamini kwao watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena (Rumi 11:23)

MAANDIKO YA SOMO: WARUMI 11:1- 36

UTANGULIZI:
Kitovu kikuu cha wokovu wetu ni kuamini kuwaYesu Kristo ni Bwana na kwamba Mungu alimfufua katika wafu. Rumi 10: 9-10, Mdo 4: 12,
Njia pekee ya kumfurahisha Mungu n ikukubali kwa njia ya imani kwamba Yesu pekee ndiye anaweza kutupumzisha na mizigo ya dhambi Math 11: 28-30. Hatuna uwezo wa kumridhisha Mungu kwa njia ya matendo ya sharia lakini tukawa tumemkataaYesu katika maisha yetu.
Matendo yanafaa kama u katika Bwana. Wayahudi walijitahidi kupata haki kwa kufanya matendo yaliyodaiwa na sharia lakini wamekataa kuufuata mpango wa Mungu wa wokovu kwa njia ya imani. Rumi 9:30-32.

Leo hii Wayahudi wengi wamemkataa Yesu Kristo katika maisha yao isipokuwa mabaki waliochaguliwa kwa neema Rumi 11:1-10. Kwa sababu ya kumkataa Yesu Wayahudi wengi wamejiweka wazi kwa Mpinga Kristo atakapokuja awatawale. Kwasababu ya uhusiano uliopo kati ya Mpinga Kristo na Wokovu wa baada ya Israel, tunalazimika pia katika somo hili kuangalia habari za Mpinga Kristo.

HABARI ZA MPINGA KRISTO:
Ufunuo 13:11-18
Mpinga Kristo (Anti – Christ) nimwonekano wa shetani katika hali halisi ya mwili. Katika vitabu vya unabii, kuna Mpinga Kristo, Nabii wa uongo, na Shetani mwenyewe. Huu ni utatu mwingine wa kishetani. Hatuelewi kama Mpinga Kristo ameshazaliwa bado, lakini tunajua kupitia maandiko ya kuwa yuko kazini hata sasa. 1Yoh 4:3

MAONI JUU YA MPINGA KRISTO ATAKAVYOKUWA:
1. Anaweza kuwa kiongozi wa dini: Atajifanya kuwa ni mtu wa dini mwenye uwezo wa hali ya juu sana hasa katika kuongea, kushawishi na kuvuta watu. Atasaidiwa na baadhi ya nchi kupata nguvu za kisiasa. Ufun 16:13. Baada ya kufanikiwa atadhihirisha wazi chuki yake juu ya Wakristo wa kweli na Kristo mwenyewe.
2. Ni kama Yesu: Anaweza kuwa ni Myahudi mwenye kadri ya miaka 30 atakapoanza kuwa mwenye nguvu. Atatangaza dini mpya nakufanya miujiza na ishara nyingi kama Yesu alivyofanya. Ufun 13:13, Math 24:24. Lakini yeye atapigania pia kupata nguvu ya kisiasa na ataipata.
3. Mhubiri mpya: Atakuwa anatabiri na mambo yanatokea. Atakuwa anawasiliana na  watu moja kwa moja. Yeye atatangaza kuwa kila mtu ni Mungu. Atakuwa ni mwanaume asiye na haja ya mwanamke.
4. Ni Philosophy: Ufu 16:14. Hata kuwa ni mtu bali ni wazo fulani, au siasa Fulani inayosisitiza uhuru wa kila mtu kufanya lolote linalompendeza. Siasa hii itazivumilia dini zote kuwa ziko sawa isipo kuwa Ukristo wa kweli.

Na; Mr Ndaki
15 / 06 / 2014

Kupata ujauzito kwa njia za kisayansi!

ujauzito

Kupata mimba kwa njia za kisayansi: je, ni dhambi?

Hana mchumba wala dalili za kuolewa bila shaka ktk mtizamo wa kibinadamu. Ameamua kuzaa kisayansi kwa kupandikizwa mbegu za toka benki ya mbegu za Kiume kama ilivyo tu benki ya Damu Mahospitalini. Je huyu dada atakuwa ametenda dhambi kwa kuzaa kwa njia hii ya kisayansi?

Dah! haya mambo ya kutopata Waume bwana tunayaongea na kujadili msiyachukulie simple kama tunapiga mastory, tuko ktk huduma kabisa na tumeona, kushughulika na mengi na hata kusoma mengi. Notice: Hii si story, huyo mdada anayeenda kupata mimba soon anafahamika na rafiki yangu Kanisani ambaye tuliyetafakari mada hii mahali fulani iliporushwa.

Kama Kiongozi wa Vijana, Wanafunzi, Mchungaji  na Mwalimu au hata Msoma Neno tu na Ufahamu wako huru, unasema nini juu ya hili?

Press on.

Edwin Seleli

Ombea tumbo la uzao wako!!

uzao

Mlio kwenye Familia yaani Mwili mmoja,na Mnaoelekea huko.

Jifunze kuomba kwa ajili ya maisha yako na Familia ya hapo baadae,hili somo linazidi kunikaa kila siku nikikaa kwenye utulivu linanijia, Mke hakikisha unaliombea tumbo lako mara nyingi kadiri unapopata nafasi,hili upate uzao mwema,Mume pia hakikisha unaliombea tumbo la mkeo ili upate uzao Mteule,ndani ya tumbo kuna vitu vya KiMungu na vingine siyo vyake….Ndo maana Mungu anasema,

Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;
Maana ya Kutakaswa ni kutengwa na vitu ambavyo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

Luka 1:15 Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.

Angalia hapa ni raha ilioje Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni,watu wengi hawaelewi Maisha ya Mtoto yanaanza tangu tumboni,usijipe likizo ni vema ukaomba mbele za Mungu.

Nabii Isaya nayeye ananipa siri hapa anaposema, Isaya 49

1 Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. 

Mwanzo 25:22-23 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yapo tumboni mwako, Na kabila mbili za watu zitafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo…

Maisha yanaanza tangu tumboni….jifunze kuomba….usisahau

–Conrad