Biblia hamsini zilichomwa moto Zanzibar – Askofu Kaganga

VIONGOZI wa makanisa wa Zanzibar wametoa malalamiko yao ya vitendo vya uchomaji na uharibifu wa makanisa kisiwani humo na kutaja vitendo 23 huku wakiitaka Serikali kuingilia kati, Katibu wa umoja wa Wachungaji wa Zanzibar Jeremiah Kobero alisema kuwa licha ya makanisa matatu yaliyochomwa na kubomolewa katika vurugu za sasa, kuna matukio 23 ya uchomaji moto makanisa yametokea tangu mwaka 2001.

Aliyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na uchomwaji moto wa makanisa ya The Church of God na Siloam yaliyofanyika mwaka 2011, makanisa mawili yaliyoko Masunguni yote mwaka huo huo, Kanisa la EAGT la Fuoni mwaka huo, kanisa la Pefa mwaka 2009, kanisa la Mwera mwaka 2012, kanisa la Redeemed lililiopo Dilikane mwaka 2001 yote ya mkoa wa Mjini Magharibi.

Alitaja pia makanisa yaliyochomwa katika mkoa wa Kaskazini kuwa kanisa la Tunguu, Unguja Ukuu, kanisa la CMF, Chukwani na Manyanya. Alitaja pia kuwepo kwa tabia hiyo kisiwani Pemba akisema kuwa imekuwa ni tabia kwa wakristo kusumbuliwa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la TAG Kariakoo Zanzibar Dickson Kaganga aliwataka Viongozi wa serikali kuchukua tahadhari mapema kabla vurugu hazijatokea.

“Wakristo tumewafundisha kuvumilia…juzi walipovamia hapa walichoma moto biblia 50, ingekuwaje sisi tungechoma japo kitabu kimoja cha Kurani? Hayo makanisa yote yaliyochomwa, taarifa ziko polisi, lakini ukienda kutoa taarifa unaulizwa, una kibali? Yaani wanakutafutia tena kosa” alisema Askofu Kaganga.

Kaganga ambaye wakati wote alikuwa akibubujikwa na machozi aliwataka Wazanzibar kutambua umuhimu wa muungano kuwa ni pamoja na kuenezwa kwa dini. “Unapoona makanisa yanaenea hapa, ujue na kule bara misikiti inaenezwa na Wapemba ambao ni wajasiri wa biashara. Hiyo ndiyo faida ya muungano ndiyo faida ya kuoleana” alisema.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa askofu wa TAG kitaifa Askofu Magnus Mhiche alihoji kitendo cha wahuni kuvamia makanisa ilihali Serikali ikiwepo madarakani, “Mimi siamini kama ni Waislamu wamefanya haya, ila najiuliza, kama siyo wao basi ni wahuni. Hivi kweli wahuni wanatawala Zanzibar?” alihoji.

Naye Askofu wa kanisa kuu la Anglican Michael Hafidhi aliiomba Serikali kudhibiti mahubiri yanayotukana dini ya kikristo kwa njia ya kaseti akidai kuwa yanachochea vurugu.

“Zipo Kaseti zinazotukana ukristo, zinachochea vurugu, tunaomba serikali idhibiti. Hata ile kamati yetu ya ushirikiano wa dinio nayo imekufa inabidi ifufuliwe.

Kwa upande wake mwakilishi wa ofisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Jongo aliwataka Waislamu kuchukuliwana na Wakristo akisema kuwa hata Mtume (SAW) alifanya hivyo wakati akiitetea dini yake. “Hata Mtume wetu alipopata taabu alipokuwa Madina alikimbilia kwa Wakristo. Mpaka uislamu ulipoenea Makka yote. Hata alipotoka Medina na kwenda Mecca aliyempeleka hakuwa muislamu. Nashangaa leo ninaposikia eti Waislam wanachoma makanisa” alisema Jongo na kuongeza, “Hawa ni waislamu gani, mbona wamechoma hata bendera ya CCM, wamechoma bar na kunywa bia. Nini hasa malengo yao?

WAZIRI wa nchi katika Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohamed Aboud amepiga marufuku mihadhara na maandamano yanayofanywa na vikundi vinavyopinga muungano akisema kuwa watawachukulia hatua kali za kisheria.

Waziri Aboud aliyasema jana hayo baada ya kutembelea kanisa la Assemblies Of God lililopo eneo la Karikoo mjini Zanzibar lililochomwa moto na kubomolewa kutokana na vurugu zilizozuka kufuatia kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa kundi la Jumuiya za mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho). Katika ziara hiyo ambayo aliongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, Waziri Aboud alisema baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi yanayosabaisha vurugu.

“Baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi, yanachochea vurugu zote hizi…. Maneno ni sumu, ndiyo tumeiingiza nchi katika machafuko yote haya” alisema Waziri Aboud na kuongeza, “Sisi kama Serikali tumewaita wenye makundi hayo na kuzungumza. Tumewaambia, kama mtu hataki dini aje kwenye majukwaa ya siasa. Tumekosea kuwaachia watu waanzishe vyama na vimesajiliwa kisheria kwa lengo la kueneza dini, lakini sasa wanaleta uchochezi.

“Kuanzia sasa ni marufuku kufanya maandamano na mikusanyiko yoyote ya aina hiyo” alisisitiza Waziri Aboud. Naye IGP Said Mwema alisema kuwa jeshi hilo limeongeza ulizni katika maeneo maalum yenye usalama mdogo hasa makanisa.

“Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa tunadhibiti maeneo maalum ili yasiendelee kuvamiwa. Tunafanya uchunguzi, ili kuhakikisha nani, kwa nini na wako wapi” alisema IGP Mwema. Alisema jeshi hilo kwa sasa lina kikosi maalum kwaajili ya kuongeza nguvu ya kudhibiti machafuko kisiwani humo na kwamba hadi jana jeshi hilo lilikuwa limekamata watu 46 na kati yao 43 wamefikishwa mahakamani huku wengine watattu wakifanyiwa uchuguzi.

Aidha IGP Mwema alikiri kwamba jeshi hilo limecghelewa kuzuia uhalifu huo na kwamba hatua iliyopo sasa ni kudhibiti usiendelee.

“Kuna mifumo mitatu ya ulinzi, kwanza ni kuzuia kabla mambo hayajatokea, kwa hapo sisi tumeshachelewa. Tuko hatua ya kudhibiti yasiendelee na baada ya hapo tutajenga amani iwe endelevu” alisema. Wakati huo huo Chama Cha Mapinduzi CCM kimesikitishwa na vurugu zilizotokea ambazo wanaamini kuwa zimeandaliwa na Jumuiya za Uamsho na kuitaka serikali kuchukua tahadhari kubwa katika suala hilo kwani kama hatua hizio hazijachukuliwa huenda likaleta maafa makubwa.

“Cham cha Mapinduzi kinaalani vitendo hivyo na kuzitaka serikali zote kudhibiti hali ya amani na utulivu tulioizowea na kuwachukulia hatua kali wote waliosababisha vurugu hizi” alisema taarifa yake kwa vyombo vya habari. Kwa upande wake chama cha Chadema kimelaani vurugu hizo zilizofanywa kwa makusudi na vijana ambao wanaonekana wameshapata mafunzo maalumu kwa kusaidiwa na chama kimoja cha kisiasa kinachounda serikali ya umoja wa kitaifa.

“Chadema tunavitaka vyama vya siasa kuandaa makundi ya vijana ambayo mwisho wake wanakosa kuwapatia kazi na hatima yake kuwa vikundi vya kihalifu nchini” ilisema taaifa hiyo iliyotiwa saini na Hamad Yussuf Naibu Katibu Mkuu.
Chama Cha Wananchi CUF kimelaani vurugu hizo na kusema zimesababishwa na chuki binfasi, ukosefu wa hekima, matumizi ya nguvu za dola na uchochezi wa makusudi kwa wale wasiopendeleaq maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar.

“Vitendo vya watu wachache na kuharibu mali za watu ni uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa kizanzibari, uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua bila ya uonevu wala upendele” imesema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Salim Bimani

sosi: zanzibaryetu

Nassari Atoa Shukrani Kanisani

Mbunge Joshua Nasari na Kangi Lugora wakitoa shukurani zake kanisani.
 

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari  jana tarehe 20 May 2012, alitoa sadaka ya shukrani katika kanisa la FPCT Kilinga Wilayani Meru mara baada ya kuchaguliwa kama Mbunge wa jimbo hilo.  

Akiongea na Mamia ya wananchi wa jimbo hilo katika kanisa hilo Bw Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalum ya kushukuru Mungu mara baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa salama tofauti na wengi walivyodhania.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa vyama vingine kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi na kuachana na tofauti za kivyama ambazo kama zitaendelezwa basi zitachangia kwa kiwango kikubwa sana umaskini wa Meru.

Akiongea katika kanisa hilo kwenye ibada hiyo mchungaji Langaeli  Kahaya  naye alisema kuwa wananchi wanapaswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa rushwa  ndio wanaosababisha hata umaskini na umwagaji damu ndani ya  nchi.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki kujihusisha na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka sasa Rushwa imeshaacha madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia Rushwa ni dhambi kubwa sana.

Gladness Mushi wa Full shwangwe -Arusha

Tumuombe Mungu atupe Raisi anayetufaa watanzania!

Kusema ukweli kuhusu uraisi wa 2015 ni kigugumizi ambacho hata mimi kimenichanganya akili nashindwa kuwaelewa watanzania! Wengine wanasema Mcha Mungu ndiye atakuwa raisi wa nchi ya Tz mwaka 2015 na tunaona Lowasa saizi kampokea Mungu kuwa ndiye mkombozi wa maisha yake na kutoa misaada kanisani, Vipi kuhusu tuhuma za ufisadi wake na wengine wanaotajwa?

Fedha ambazo zilitakiwa kwa ajili ya umeme wa Tz, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, mafao ya wafanyakazi, kurekebishia miundo mbinu ya Tanzania n.k , fedha zote hizo kachukua mtu 1 na wenzie wachache alafu anaenda kucheza harambee makanisani anaambiwa amebarikiwa!

Mi ninachoamini ni kwamba swala la uongozi hasa uraisi anayepanga ni Mungu, ijapokuwa tutafurahi sana endapo atakaye kuwa raisi wa 2015 ni Mcha Mungu kwa sababu atajitahidi kuirekebisha nchi kimwili na kiroho.

Alex E. Mwaibambe


Kujiengua kwa James Millya, Mungu amejibu maombi ya Godbless Lema?

MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, kwa miaka mitano, James Millya,ametangaza kujiuzuru nafasi zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai kuwa CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania. Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini Arusha. Alisema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe. Alitaja nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.

Wakazi wa Arusha hawajaamini ukweli huu, kutokana na Ndugu James Millya alivyokuwa mchapa kazi na mwenye mapenzi na Chama cha CCM kabla ya kukihama chama hicho.

Leo Jumatatu, Tarehe 16 April 2012 ni siku ya saba ya maombi ya kufunga kwa Mbunge aliyevuliwa madaraka Arusha kupitia chama cha CHADEMA, Godbless Lema, alipotangaza mfungo wa siku saba tangu  jumanne iliyopita.

Tumeanza na Mungu, tutamaliza na Mungu – Joshua Nasari

“Cha kwanza kabisa namshukuru sana Mungu ambaye alinipa maono ya kuwa mbunge wa Arumeru mashariki, nimekuwa nikiyasema kwa muda mrefu watu walifikiri natania, lakini vilevile nikishukuru chama changu cha CHADEMA ambacho kilinipa ridhaa ya kusimama kuwakilisha kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki, kwakweli niwashukuru sana watu wa Arumeru mashariki ambao hawakujali umri wangu, hawakujali uwezo wangu kifedha, hawakujali historia ya familia yangu katika siasa, hawakujali kila mapungufu ambayo nilikuwa nayo, lakini wakaamua kunichagua…..napenda niseme  na kama nilivyosema tangu mwanzo kwamba tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu na siyo kwenye kupata kura peke yake, tutaendelea kumtumikia Mungu na kumuweka Mungu mbele, tutamtanguliza yeye na tutaongozwa na yeye siku zote”

Haya ni maneno ya mbunge wa CHADEMA mtumishi wa Mungu, Joshua Nasari (26) aliyeshinda Jimbo la Arumeru mashariki kwa kura 32972 ambazo ni sawa na asilimia 54 na kufuatiwa na mgombea wa chama cha mapinduzi, Sioi Sumari aliyepata kura 26,757 sawa na asilimia 42.

Dini ya Obama bado ni gumzo Marekani

Hivi karibuni mzozo kuhusu dini ya Rais wa Marekani Barack Obama umeibuka tena, ambapo wapinzani wake wakimhusisha na dini ya kiislamu.

Mtumishi wa Mungu Franklin Graham, mtoto wa Mwinjilisti Billy Graham  alipohojiwa na kituo cha MSNBC kuhusu dini ya Obama, Alijibu ” Muulizeni yeye, siwezi kumjibia mtu swali hilo, Ninachojua mimi ni mwenye dhambi, na Mungu amesamehe dhambi zangu, Graham akasema “inabidi kumuuliza yeye, amesema yeye ni Mkristo, hivyo nami nadhani ni Mkristo”

Na alipoulizwa kama Obama ni Mwislamu, akasema “hapana”

Hata hivyo Raisi Obama amekuwa akisema yeye ni Mkristo kwa msisitizo.

TB Joshua atabiri kifo cha Rais Afrika?

Nabii maarufu kutoka Afrika TB Joshua amezua gumzo katika nchi za Africa baada ya utabiri wake alioutoa kanisani kwake mwanzoni mwezi huu, akiongea sehemu ya utabiri huo alisema “God loves us, you should pray for one African head of state, when I say President… again the sickness that is likely to take life; sudden death, it could be sickness being in the body for a long time but God showed me the country and the place but I’m not here to say anything like that.”

“When it’s too close and there is nothing I can do about it, I’ll mention it clear; the place, the country and the person so that they can see what they can do to rescue him. Okay, it is very close. Jesus loves us. Wave your hand, wave your hand,” 

TB Joshua amekuwa akitabiri mambo mengi na kutokea ikiwemo, Ushindi wa Raisi wa Ghana John Atta Mills, Michael Jackson, utabiri wa mpira wa miguu, matetemeko ya ardhi nk pia wana siasa maarufu wamefika kanisani kwake akiwemo mke wa zamani wa afrika kusini Winnie Mandela na Waziri mkuu Tanzania aliyejiuzuru, Edward Lowassa.

Dk. Mwakyembe atoa ushuhuda kanisani!

Mwakyembe akiwa na Askofu Gwajima

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu atoke India kwa ajili ya matibabu. Dk. Mwakyembe alionekana jana kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa muujiza wa kupona ugonjwa uliokuwa unamsumbua na kusema nguvu za mafisadi zimeshindwa kummaliza.

Alisema kuwa hivi sasa anatarajia kuzunguka kwenye makanisa mbalimbali nchini kutangaza shetani alivyopanga kummaliza lakini Mungu akamsaidia.

Nimepanga kuzunguka kwenye makanisa kumzomea shetani kwamba ameshindwa na kuwashukuru watu wa Mungu kwa maombi yao,” alisema.

Picha na Kapingaz Blog

Dk. Mwakyembe alisindikizwa na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; mbunge wa Kahama James Lembeli (CCM); na Aloyce Kimaro, aliyekuwa mbunge wa Vunjo.

Wabunge hao wote waliongea kuhusu utumishi wao na kuongeza juhudi katika kupambana na kuitetea nchi ya Tanzania pasipo kuogopa.

Lowassa; “Mungu Yupo Na Mimi Nitayashinda Majaribu”

Askofu Mkuu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kati Mch, Eliufoo Sima akitoa mahubiri katika kanisa hilo usharika wa Amani Sabasaba mjini Singida wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ulioendeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa.

Askofu wa KKKT Mchungaji Eliufoo Sima akipokea kiasi cha shilingi milioni 10 taslimu kutoka kwa Mhe.Lowasa kama mchango wake katika kufanikisha harambee ya ujenzi wa kanisa hilo.

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe.Edward Lowasa amesema kuwa pamoja na kusemwa maneno mengi sana kwenye vyombo vya habari juu yake lakini anamwamini Mungu kuwa anampigania kila kukicha.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoani Singida Hillary Shoo anaripoti kuwa Lowasa ameyasema hayo leo mjini Singida wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT usharika wa Amani sabasaba mjini Singida. “Wale wanaofuatilia siasa za nchi yetu kuna maneno mengi saana lakini bwana ni mwema na mwaminifu hatimae tumeshinda”.Alisema. Alisema mara baada ya taarifa hizo siku moja akiwa nyumbani kwake na mkewe huku wakiangalia TV na kutaka kujua magazeti yanasemaje asubuhi kulikuwa na maneno mengi yaliyosemwa ya hovyo hovyo juu yake mengine walishindwa kuyasoma.

“Lakini mke wangu alienda chumba cha pili na kuchukua biblia na kunifungulia maneno ya bibilia kitabu cha Isaya 41:10, usiogope kwa maana mimi niko pamoja nawe tusifadhaike kwa maana mimi ni mungu wako nitakutia nguvu naam nitakusaidia, naam nitakushika mkono wa kuume wa haki yangu.” Alisema na kuongeza kwa maneno hayo niliendelea sana lakini baba askofu nisamehe nichukue hadhara hii kuwashukuru watu wengi sana walioniombea na hatimae kufika hapa nilipo. “Wapo waislamu na mashekhe walifanya dua kwa niaba yangu, nawashukuru sana, pia wapo wakristo walioniombea nao nawashukuru sana, mapadri, mashemasi na watawa, wachungaji na wainjilisti wa madhehebu yote, kwaya mbalimbali na waimbaji wa nyimbo za injili, wanamaombi wote, wanamtandao wao wa ajabu una nguvu kweli kweli na maaskofu wa makanisa yote ya kikristo pia nawashukuru sana.” Alisema Lowasa.

Aidha Mhe Lowasa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli alisema kuwa maneno mengi ya kisiasa yalisemwa juu yake lakini kimsingi hayakuwa ya kweli ya ukweli na siasa zinazoendelea kwa sasa ni za kuchafuana. Pia Lowasa alinukuu maandiko mengine ambayo aliyasoma kutoka kitabu kitakatifu cha Warumi ambayo aliyasoma mwenyewe. “ Lakini ikiwa roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu hataihuisha miili yenu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake anakaa ndani yenu” alinukuu Lowasa.Aidha alisema kutokana na misukosuko ya kisiasa ambayo amekumbana nayo amekuwa akimwona Mungu akimtetea na utetezi huo ameupata kutoka kwa Mungu, kutokana na maombi ya watakatifu kutoka dini mbalimbali ambao wako pamoja.

Wale wote ambao wanaamini kuwa nafanya kazi kwa kusimamia haki ya Mungu na kazi zote kwa ujumla waliniombea usiku na mchana na kwa hilo Mungu kawasikia na kanifanya kuendelea tofauti na uchafu ambao mimekuwa nikibambikizwa na siasa za kuchafuana. Hata hivyo Lowasa alidai kuwa kama kiongozi hana Mungu ndani yake hawezi kuhimili mikiki ya kisiasa kwani kinachotakiwa ni kumwomba Mungu ili aweze kutetea kazi zinazofanywa na mtu mwenye haki. “Nimekuja kwenye harambee sio kupiga maneno ya kisiasa, nilimwambia baba askofu tuna utamaduni wa kualikwa haramabee nyingi sana, lakini kabla ya kukubali unauliza kwamba hao unaoshiriki nao wamefanya nini, nyie mmefanya kazi kubwa sana nawashukuru na nafurahi kwenye harambee hii.” Alisistiza na kuongeza.

“Kwa sababu ni njia mojawapo ya kuthibitisha kwamba wananchi wanaweza kufanya mambo yao kwani kanisa kama hili miaka ya nyuma lingeweza kujengwa na wafadhili wa nje lakini leo limejengwa na wananchi wenyewe. Mapema askofu mkuu wa KKKT Dayosisi ya kati Mchungaji,Eliufoo Sima anaamini utulivu wa viongozi wa nchi hii ni dhahiri kwamba Taifa hili kwa jinsi ya utamaduni na mapokeo yake , na mambo magumu yanayotokea siku hadi siku, litafanikiwa kutengeneza njia thabiti ya mafanikio ya watu wake. Askofu Sima alisema kumekuwepo na madai mengi kuwa nchi yetu ni maskini lakini angependa viongozi kuyashughulikia kwa umakini mkubwa ili kuondoa manung’uniko miongoni mwao ili yasiharibu tabia njema ya baadhi yao. Hataa hivyo Askofu Sima alimwagia sifa Mhe.Lowasa na kusema kuwa ni tofauti na viongozi wengine ambao unaweza kuwatafuta kwenye simu kwa muda mwingi na wakawa hawapatikani.

“Kwa kweli wewe ni kiongozi wa pekee,tofauti na wengine,unaweza ukamtafuta kwenye simu hata mara tano na hapatikani, lakini wewe kila ninapokupigia unapokea simu yangu,na hata katika harembee hii nilipokupigia nikakuomba uje Singida ukasema upo njiani unaenda Dodoma,”. “Lakini na mimi nikakwambia nipo njiani naenda Morogoro,ukasema basi tukutane njiani,mtu mkubwa kama wewe kukutana njiani hiyo ni ajabu.”alisema Askofu. Katika harambee hiyo Mhe.Lowasa amechangia kiasi cha shilingi milioni kumi ambapo makusanyo yote yaliyopatikana katika ujenzi wa kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Amani zilipatikana zaidi ya shilingi milioni 138. Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini liliko Kanisa hilo Mohammed Dewji (MO) alichangia shilingi milioni 10, Mfanya biashara maarufu hapa nchini aliyemtaja kwa jina moja tu la Patel amechangia mabati ya kuezekea kanisa hilo yenye thamani ya shilingi milioni 50. Kanisa hilo la usharika wa amani linatarajiwa kukamilika mapema hapo mwakani kwa gharama ya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 480.

–MJENGWA BLOG—

POLITICS IN THE CHURCH

‘Politics’ is the science of government. It has to do with the behavior and activity of those who possess governmental power.  It refers to the methods and tactics used to formulate policy and the principles adopted to apply that policy.

Because inherent in the flesh of human kind is a desire for self exaltation, any kind of power tends to corrupt.  Very few politicians have a selfless desire to improve government if there is nothing in it for them.  They want to increase their positions, further their careers and climb to the top.  They are driven by a desire for power, not because they believe they have the answer, but for powers sake.  Politics therefore becomes a degenerate profession which engages deception and lies as acceptable tools.

Politics is man’s government, using man’s methods, for the exaltation of man.

As such, politics has no part in the Kingdom of God.  There is no room for people who want to be in charge, enjoy position and power and by the ingenuity of the human mind, control the work of God.  God does not give spiritual authority into the hands of men and committees.  He has His ‘sent ones’ who are His servants and He expects them to listen to Him and do as they are told.  In other words He expects them to operate by faith.  We do not need the methods and tactics of men, which originate in logical minds and feed the human ego.  We need Holy Ghost instruction.  We need men and women who are as weak and base and foolish as was Abraham, when he went out not knowing where he was going.

Politicians are everywhere in the modern church, because politics is much easier and much more comfortable.  Politics promise power, possible popularity and recognition by people and, if the methods are clever enough, apparent success.

Politicians are threatened by men and women of faith.  Their kingdom is jeopardized by those who move with the Spirit.  They hear the sound of them, but know not whence they come, or where they go.  But as more humble servants of Jesus, moved by God, are deployed by the Master Strategist into His harvest fields, attested by the power of the Holy Spirit, the politicians will be forced to stand aside as He who governs like no other, imposes His will upon the church He died to produce.

John Hibbert

Lowassa asipokua rais 2015, mniue – Askofu

Kiongozi mkuu wa kanisa la Last Glory Church la hapa nchini Basileus Ezekiel Mabumba, amesema amepokea ujumbe kutoka kwa Mungu unaoeleza kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Ngoyay Lowassa, atakua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Katika mahojiano na gazeti hili (Nyakati), Mabumba alieleza kuwa atawajibika iwapo unabii wake hautatimia. Kwa mujibu wa Torati kile ambacho kilikuja kubainika baadaye kuwa unabii wa uongo, adhabu kwa mtoaji unabii ilikua ni kupigwa mawe hadi afe.

Jumatano iliyopita, Mabumba alitinga katika ofisi za gazeti hili na kueleza kuwa, kwa muda mrefu sasa amekua akipokea ujumbe kutoka kwa Mungu ukieleza kuwa Lowassa ndiye atakuwa rais wa nchi hii ya awamu ya tano.

Sehemu ya mahojiano ya gazeti hili na Askofu Mabumba, ambaye hujulikana pia kama Mtume, ilikua kama ifuatavyo:

Mwandishi: Umesema kwa muda mrefu umekuwa ukiletewa huo ujumbe. Tuambie ni tangu lini? Tuambie pia mtu wa kawaida kabisa anaelewa nini kuhusu unabii?

Mabumba: Tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kwa uhakika unabii huu nimepata kuwaeleza waumini pale kanisani. Sasa nimeona niufikishe kwa watu wengi zaidi.

Unabii ni tofauti na kutabiri. Kuna unabii wa aina mbili. Kwanza, ni ule unabii ambao Mungu anakuruhusu kuona mambo yajayo. Ni pale Mungu anapokuonyesha kutakua na nini siku zijazo. Ni karama za ufunuo. Aina ya pili ya unabii ni pale mtu aliyekusudiwa kufikisha unabii huo anaweza kutamka jambo kwa msukumo wa Roho Mtakatifu. Sasa hapo ndio ujue kwamba kuna msukumo wa kibinadamu, wazo la mwanadamu mwenyewe, msukumo wa shetani na msukumo wa Mungu.

Mwandishi: Sasa Mtu anaweza kutofautisha vipi kama jambo fulani lina msukumo wa mwanadamu, kwa Shetani au wa Mungu?

Mabumba: Unajua kama ni la Mungu kuna msukumo unaolazimisha kulitafakari kila mara kabla hujalikubali. Unakua kama una mzigo fulani ukikubaliana na Mungu ndipo utapata amani ya kulisema.

Mwandishi: Lakini kuna nabii nyingi zimetolewa na watumishi hazikutimia. Kuna mtumishi aliwahi kusema angesigina Biblia iwapo unabii wake usingetimia. Haukutimia na hakusigina, leo yuko kimya. Mwingine akasema kutakua na vita…ziko nabii nyingi tu.

Mabumba: Unabii wangu lazima utimie nimekua nikioneshwa mambo mengi lakini siyatamki. Kuna vitu vidogo  vidogo nimeoneshwa na ikawa kweli. Yako na mambo makubwa labda kwa sababu sikuwa ninayasema kama ninavyofanya leo kwa hili. Hili ninasukumwa sana kulitamka.

Mwandishi: Usipotimia?

Mabumba: Niko tayari kuwajibika. Manabii waliwajibika kwa unabii wao. Hata nisipopondwa mawe, watu hawataniamini tena, hayo tayari ni ‘mawe’

Mwandishi: Kwa mazingira ya sasa ambayo watu wamepunguza imani wapo ambao wanaweza kufikiri kuwa umetumwa na unatumia nafasi yako ya utumishi wa Mungu kutumikia wanasiasa? Wengine wanaweza kufikiria kuwa unatafuta umaarufu.

Mabumba: Kwanza kabisa sitaki kuwa karibu na wanasiasa, hata chama sina, sijishughulishi kabisa na wanasiasa. Sifahamiani na Lowassa. Na ninafikiri kama ni hivyo Lowassa mwenyewe angeenda kwa wahubiri wakubwa. Mimi ninasema nilicholetewa.

Kama kuna watakaofikiria ninatafuta umaarufu, watakuwa wamekosea. Sihitaji umaarufu zaidi ya hapa. Naandika vitabu watu wengi wananifahamu kupitia huduma hiyo. Ninaandika vitabu na vinapendwa, inatosha. Siwezi kutumia unabii feki kujijenga.

Mwandishi: Unaweza kuzungumza chochote kuhusu dhana ya kujivua gamba ndani ya CCM ambacho Lowassa ni mwanachama na kiongozi?

Mabumba: Sifuatilii mambo ya vyama. Kwa habari ya unabii Mungu anakuonesha kidogo tu. Hayo mengine siyajui bwana. Kama kuna kuna kuvuana gamba mi sijui.

Lowassa Waziri Mkuu aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya Kampuni ya umeme ya Richmond hajapata kutangaza hadharani kuwa ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, lakini harakati za kisiasa ndani na nje ya chama chake cha CCM zinaashiria kuwa ni mmoja wa wanasiasa walioko katika ‘vita’ ya urais.

Hivi karibuni Lowassa alionekana katika televisheni akishiriki kwenye ibada katika kanisa linaloongozwa na mhubiri maarufu wa nchini Nigeria, TB Joshua.

Kushiriki kwa Lowassa katika ibada hiyo kulizua minong’ono, wengine wakihusisha na harakati za urais 2015 na kwamba alienda kuombewa ili ‘nyota yake ing’ae’.

Hata hivyo baadhi ya watumishi wa Mungu walikerwa na kitendo cha baadhi ya watu kushangazwa na uwepo wa Lowassa katika Ibada hiyo, wakisema ni kuingilia uamuzi binafsi wa mtu anayemtafuta Mungu wake.

Source: NYAKATI, Julai 10-16, 2011

Edward Lowasa, atabiriwa na TB Joshua?

Pichani Lowasa akiwa kanisani kwa TB Joshua kama anavyoonekana kwenye Emmanuel TV, 12 June 2011

MBINU za Edward Lowassa kutaka kurejea kileleni katika ulingo wa kisiasa zimemnasa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo, imefahamika.

Beatrice ambaye alikuwa akijitambulisha kuwa mmoja wa “wapambanaji dhidi ya ufisadi,” waliopachikwa jina la “Mitume kumi na miwili,” sasa anatajwa kuhamia rasmi mtandao wa Lowassa.

Gazeti hili limepata ushahidi wa maandishi ya mkono wa Beatrice mwenyewe yanayoonyesha kuwa amekuwa mfuasi muhimu wa Lowassa kiasi cha kushawishi wengine kujiunga katika mtandao wake.

Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alieleza mambo matatu katika ujumbe wake kwa Chana.

Kwanza, kumshukuru Chana kwa kukubali kulinda kura zake. Pili,  kumshawishi kumuunga mkono Lowassa. Tatu, kumweleza juu ya ulokole wake na “mtumishi aliyepakwa mafuta” kutoka Nigeria.

Beatrice anamwambia Chana kuwa Lowassa ndiye kampeni meneja wake. Hii ilikuwa katika uchaguzi wa makamishina wa Bunge; nafasi aliyogombea na kushinda.

“Mungu ni wa ajabu, (Lowassa) ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Ana njia za ajabu za kufanya mambo. Ahsante kwa kukubali kuhesabu kura,” inasema sehemu ya ujumbe huo.

Chana, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, ndiye alihesabu kura za Beatrice kwenye uchaguzi wa kutafuta makamishina wa Bunge.

Ni kwenye ujumbe huo ambamo Beatrice anatoboa kuwa siri ya ushindi wake ni Lowassa aliyekuwa kampeni meneja wake.

Katika kusisitiza hoja yake, Beatrice anasema, “Nimezungumza na TB Joshua wa Emmanuel TV Nigeria aliyenipa unabii kuwa rais ajaye Tanzania ni Edward Lowassa, nikamuambia haiwezekani kwani amechafuka sana.”

Anasema Joshua alimjibu, “…alikuwa amechafuka sasa amesafishwa kwani katubu. Akaniambia his past is over (maisha yake ya nyuma si kitu). Akaongeza kwa kusema, wewe Beatrice ningeangalia your past (maisha yako ya nyuma) pengine nisingekuombea kabisa. Akasema my past is over (hajali maisha yangu ya nyuma),” inasema sehemu ya ujumbe huo wa Beatrice.

Hata hivyo, Beatrice hakueleza katika waraka wake kwa Chana maisha yake ya nyuma yalikuwa vipi. Wala hajaeleza alifanya nini, hadi kuamini kuwa kama Nabii Emmanuel angeyatazama, basi asingemuombea.

Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki tatu baada ya Lowassa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje.

Mume wa Beatrice, William Shelukindo alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo iliongoza harakati za kuundwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond.

Ni taarifa ya kamati hiyo iliyosababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu, Februari 2008.

Kwa mujibu wa watu waliokaribu na Beatrice na kwa ushuhuda wake mwenyewe, mwanasiasa huyo ameamua kujisalimisha kwa Lowassa kwa kile kinachoelezwa kuwa “Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania.”

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Lowassa na kundi lake kutaka kujisafisha kwa lengo la kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015.

Miongoni mwa mikakati aliyojiwekea Lowassa na kundi lake ni kujitokeza katika maeneo yote muhimu na kutoa kauli ambazo zitafanya wananchi waanze kumkubali kuwa ni kiongozi anayefaa.

Katika kutekeleza mkakati huo, Januari mwaka huu, Lowassa alijitokeza kuzungumzia vurugu zilizotokea mkoani Arusha zilizotokana na mvutano katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo kati ya CCM na CHADEMA.

Katika mnyukano huo, watu watatu walipigwa risasi na polisi na kufariki dunia baada ya polisi kutumia nguvu isiyo ya kawaida kuzima maandamano ya CHADEMA.

Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa tofauti na msimamo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtaka kuwasilisha maoni yake katika vikao vya chama badala ya kutumia vyombo vya habari.

Kauli nyingine ya Lowassa ilihusu nyongeza ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi, kutokana na kile alichoita mfumuko wa bei kuwa mkubwa.

Bali wiki moja iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mganya alimtuhumu Lowassa kwa kutoa kauli hiyo akisema ana ajenda ya siri nyuma yake.

Mgaya alisema TUCTA haihitaji msaada wa Lowassa katika kusimamia madai yao. Alisema “mbunge huyo wa Monduli inaonekana ana ajenda yake mgongoni.”

Hatua nyingine ya Lowassa katika kujikarabati kisiasa ni kugombea na kupata nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Lowassa amekuwa pia akihudhuria hafla nyingi, hasa za madhehebu ya Kikiristo (KKKT) ambao anaonekana akitoa maoni mbalimbali kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita ukumbi wa Dimaond Jubilee kwenye uzinduzi wea albamu ya moja ya kwaya za injili.

Kwenye kusanyiko hilo, Beatrice naye alikuwepo. Lowassa alimtaka asome maoni ya gazeti la The Citizen juu ya ushirikina uliokithiri nchini; jambo ambalo Lowassa alizungumzia kwa urefu.

MwanaHALISI lilipowasiliana na Beatrice ili kupata maoni yake juu ya ushwahiba wake mpya na Lowassa, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwandishi: Tusaidie maelezo kidogo juu ya ujumbe uliomwandikia Mheshimiwa Pindi Chana kumjulisha kuwa uliambiwa Edward Lowassa atakuwa rais. Ni kweli?

Beatrice: Barua ameandika nani na umeipata wapi?

Mwandishi: Hii barua fupi – memo ndani ya Bunge, uliposema Mheshimiwa Lowassa ambaye amesimamia vizuri kura zako za ukamishna wa Bunge.

Beatrice: Sina taarifa hiyo. Wala siikumbuki. Unajua ndani ya Bunge tunaandikiana mambo mengi, tena mengine ya utani tu. Na mimi na Mheshimiwa Chana sote ni “walokole,” tunafanyiana utani sana.

Mwandishi: Kwani mheshimiwa Shelukindo, mkiwa ndani ya bunge kuna utani mwingi, kwamba huwa mnaandikiana utani sana?

Beatrice: Kabisa, unajua tunaandika mambo mengi. Na kama unaandika kwa utani kwa mwenzako inabaki hivyo ni utani tu. Sasa tatizo hao wanaowaletea mambo haya wanatumia mambo haya kutafuta mipango yao ya kufikia mwaka 2015.

Alisema, “Mimi najua hakuna anayenibeba ndugu yangu. Mimi ni very solid (ngangari), sibebeki. Nakwambia, mbona mimi nina nguvu nyingi mimi mwenyewe; sihitaji kubebwa. Najua wanajaribu kuonyesha tunabebwa, lakini huo ni ujinga wao wa kufikiri.

Mwandishi: Mheshimiwa Shelukindo, kwani nyie waheshimiwa huwa mnatafutana (kufitiniana)?

Beatrice: Hiyo inafanyika sana, watu wakishakuwa na mambo yao wanatumia wengine kutimiza dhamira zao. Lakini mimi ninafikiria wananchi. Nimeshaamua kwamba Beatrice nashughulikia shida za wananchi jimboni. Ninatafuta njia za kuwaondolea umasikini, njaa na mambo kama hayo. Sasa wengine wanatafuta tu pa kunishika.

Mwandishi: Kwa hiyo Mh. Lowassa ndiye alikuwa kampeni meneja wako katika kutafuta ukamishna pale bungeni, au siyo Mheshimiwa?

Beatrice: Lakini kama anafanya kazi ya kampeni vizuri; ni vizuri tu. Isipokuwa kila mtu anajichukulia mwenyewe alivyo. Mimi ni mtu wa kazi sihitaji kusimamiwa hivyo. Na hebu tujadili hili; unajua kaka nyinyi mnafanya kazi kubwa. Sasa hii kusikia, sijui MwanaHALISI hivi, sijui hivi, pengine kuna watu wanachomekea vitu vyao. Tunapenda kazi yenu.

Mwandishi: Mheshimiwa nakushukuru sana.

Beatrice: Karibu sana tutafanya kazi pamoja.

Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, mume wa Beatrice, William Shellukindo, alikuwa na msimamo mkali dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini na hiyo ndiyo inayoelezwa kuwa sababu ya kushindwa kwake ubunge katika mchakato wa ndani ya CCM.

Shellukindo alikuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kwa zaidi ya miaka 20, alishindwa katika kura za maoni na January Makamba, mtoto wa katibu mkuu wa CCM anayetajwa kuwa mfuasi wa mtandao wa Lowassa.

S0urce by Mwanahalisi – 9 March 2011

Watumishi wa Mungu kutuhumiwa

Wapendwa,

Nawasalimu ktk Jina la Yesu Kristo.Naamini kila mmoja wetu ameanza mwezi June kwa furaha, amani, ushindi na Upenyo. Nimesikia na kusoma ktk vyombo vya habari kuwa Rais wetu anawatuhumu watumishi wa Mungu kuhusika na madawa ya kulevya. Kwangu mimi limenishitua na siamini kama kweli wapo wanaofanya hiyo biashara, na kama wapo basi wanamtumikia shetani ambaye ndiye baba yao.

Nami natoa wito kwa Rais wetu kama kweli wapo basi majina yawekwe hadharani ili tuwajue na sheria ichukue mkondo wake. Hakuna kitu kibaya kama kusimama madhabahuni na kukemea wengine wakati ndani kunakusuta, hawa kondoo wa Yesu tunawapeleka wapi

–Pastor JCC

Nyerere was very courageous

President Yoweri Museveni has described the late Mwalimu Nyerere as a person of extra-ordinary courage who sacrificed his life for the freedom of the people of Africa.

The President, accompanied by his wife, Mrs. Janet Museveni, was today among thousands of pilgrims who attended prayers at Namugongo Martyrs’ Shrine for the process of the canonization of the late Mwalimu Julius Nyerere, former President of Tanzania. The prayers were also intended to honour and pay homage to the Uganda Martyrs as well as for peace in the country.

The pilgrims comprised Christians from Tanzania, Kenya, Rwanda and Uganda.

The special Mass that was led by the Archbishop of Kampala Archdiocese, the Most Rev. Dr. Cyprian Kizito Lwanga, was also attended by former President of Tanzania, Mr. Benjamin Mkapa, the widow Mama Maria Nyerere and family members.

President Museveni, who welcomed all pilgrims to Uganda, said that the late Nyerere was very compassionate to human beings, especially the oppressed.

The President added that the late Nyerere was a fearless freedom fighter and united his country through the promotion and use of the Kiswahili language that went a long way in fostering unity among the people of Tanzania, making that country one of the most peaceful in Africa.

President Museveni pointed out that standing up against imperialists and racists in South Africa, Ian Smith in Rhodesia, the Portuguese in Angola and Amin in Uganda, needed an extra-ordinary courage, a quality the late Nyerere had.

The President told the attentive pilgrims that Mwalimu Nyerere was also extra-ordinary because unlike Kwame Nkrumah of Ghana and Patrice Lumumba the DRC who  paid the price for the similar struggle, Mwalimu also supported freedom movements in Mozambique, Zimbabwe, South Africa, Angola and Namibia. He noted with happiness that those countries that comprise one third of Africa are today free.

President Museveni further told the congregation that it was Mwalimu’s selfless sacrifice and support, together with that of Dr. Kenneth Kaunda of Zambia and Samora Machel of Mozambique that helped the people of Uganda get rid of the Amin regime.

On the peace now enjoyed by the people of Burundi, President Museveni said that it was the late Mwalimu Nyerere’s initiative that resolved the seemingly unsolvable problem in that country.

The President said that the late Mwalimu Nyerere involved the principle of democracy in Burundi and security for all, a formula that has brought about tranquility in that country.

He told Namugongo pilgrims that Burundi is today participating in the peace-keeping mission in Somalia.

President Museveni informed the congregation that Mwalimu Nyerere also worked tirelessly for the political federation of East Africa, a process that is currently ongoing.

The President, therefore, compared the late Mwalimu Nyerere to the Uganda Martyrs, who stood for the truth even at the expense of their lives.

President Museveni said he had joined the pilgrims in prayer for the process of the beatification and eventual canonization of the Servant of God (the late Julius Kambarage Nyerere) who was not only a freedom fighter but also a religious person.

The former President of Tanzania, Mr. Benjamin Mkapa, said that the late Mwalimu Nyerere was a great leader who abhorred being worshipped.

The High Commissioner of Tanzania to Uganda, Ambassador Rajab said the late Nyerere dedicated most of his life to the campaign for justice, freedom and peace not only in the region but also in the whole world.

Archbishop Dr. Cyprian Kizito Lwanga of Kampala Archdiocese, in his homily, commended President Museveni and the government for the peace now prevailing in the country.

Other speakers included the representative of the family of the late Mwalimu Nyerere, Mr. Charles Lwanga Nyerere and the Rector of Namugongo Martyrs’ Shrine, Rev. Fr. Deogratius Ssonko, who praised the late Mwalimu Nyerere for being an exemplary leader.

Mkristo Kufanya Kampeni!

Je, ni sahihi au si sahihi kwa Mkristo kumfanyia kampeni mgombea fulani ili achaguliwe?

MAONI: Kudharau kupiga kura ni tatizo kubwa kuliko unavyodhani, usiache kupiga kura na kumchagua anayefaa kuleta maendeleo kwa ajili yako na vizazi vijavyo ni pamoja na Kila Kitu Mungu Alichokiumba na Kukiweka Tanzania!

Je ni viongozi wangapi Tanzania ya leo ambao wako safi?

Ndugu zangu siku za karibuni wamekuwepo baadhi ya wanasiasa na hata Watanzania wenzetu wakiwalaumu wale wote waufanyao ufisadi. Kiasi kwamba unapata picha kuwa hao watu wanaowalaumu wenzao ni  wasafi kuliko.  Ninakumbuka Yesu alipopelekewa yule mwanamke mzinzi na mafarisayo wakitaka apigwe mawe, Yesu akawauliza kama na wao walikuwa hawana hatia ya dhambi ya uzinzi. Maajabu ni kuwa walishindwa kumtupia mawe kwa sababu na wao hawakuwa safi. Naye Mtakatifu Paulo kwenye Warumi 2:1 anasema…”kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia (kwa nini?) kwa sababu wewe uhukumuye wayafanya yale yale”. Hao hawatajiepusha na hukumu ya Mungu(2:3).

Wabunge hao wanaowasakama wenzao kuwa ni mafisadi bila ya kuwaeleza Watanzania ufisadi wao ni nini na ni upi, wao wenyewe ukifuatilia jinsi walivyopata ubunge utagundua wote walitumia njia za ufisadi kupata nafasi hizo. Wanafiki wakubwa hao hawana agenda nyingine zaidi ya kuiingiza nchi kwenye machafuko.

Halafu kama hiyo haitoshi. Hata viongozi wa makanisa na dini nyingine wanapata kigugumizi na wao waseme nini, kwa sababu wao pia wana sehemu yao kwenye ufisadi huo.

Labda niulize. Hivi wewe kama baba kwenye nyumba yako na mtoto wako ni mnywaji mzuri wa pombe, unapogundua kuwa na mtoto wako naye anakunywa kama wewe utafanyaje? Utamwonya au utamwachia huku ukijua kuwa unywaji kwa kawaida una madhara au utaogopa kwa sababu huna moral authority kwenye jambo hilo? Baba wa Taifa Nyerere alikuwa anaweza kukemea ufisadi kwa sababu yeye hakuwa fisadi. Sasa je ni viongozi wangapi Tanzania ya leo ambao wako safi?

Petro Konkoli

Mungiki sect head freed in Kenya

By Moses Njagih

Mungiki leader Maina Njenga is a free man. The State dropped 29 counts of murder against him after spending more than two years in jail. The High Court in Nyeri acquitted Njenga of murder charges in the Mathira massacre where 29 people were hacked to death. He has been in custody for 29 months. The surprise move came barely three days after he threatened to provide what his lawyers termed ‘damning information’ against top State officials who he claimed orchestrated his arrest and detention.

maina

Maina Njenga enters Jesus is Alive Ministries Church, Nairobi.

On Tuesday, his lawyers led by Paul Muite said Njenga would swear an affidavit in which he would give the damning evidence against State officials.

Muite said Njenga was demanding protection as a witness, but the AG was yet to respond to the request.

He said Njenga had given the lawyers the go-ahead to prepare the evidence.

It was also just a day after the court ordered him to take a plea to the charges after six months of cat-and-mouse legal games with the State.

On Friday, Central Province Senior Principal State Counsel Charles Orinda told Justice Joseph Sergon he had instructions from the Attorney General Amos Wako to terminate the case.

He said the instructions were given through the Director of Public Prosecution Mr Keriako Tobiko.

Also enjoying the reprieve through the nolle prosequi entered by AG were 18 other youths separately charged with the same offence.

Njenga had five lawyers ; Mr Robert Asembo, Muite, Mr Kibe Mungai, Mr Mbiyu Kamau and Mr Evans Ondiek.

He was arraigned in court on May 11 to face 29 counts of murder, but for the six months that he was in remand at King’ong’o Prison in Nyeri, he declined to take pleas, as he had filed a constitutional reference case in Nairobi to challenge the legality of his trial.

In his constitutional case, he insisted that on the night of April 21 and 22, when he allegedly committed the offences, he was still serving time in Manyani.

Tight security

On Thursday, when Justice Sergon ordered him to take a plea, Njenga declined to answer to the charges read to him, prompting the judge to enter a plea of ‘not guilty’ as the law requires.

The judge consequently ruled hearing of the case against Njenga and three others be heard on December 10. On April 29, Njenga was freed after serving barely half of a jail term slapped for possessing a gun and drugs. He was however re-arrested soon after. The security at the court was tight. Central Provincial Police boss, John Mbijjiwe sat barely two metres from the dock from where Njenga followed proceedings.

Bishop Margaret Wanjiru with Njenga at the church. He said he has ditched the sect for Christianity. Photos: Collins Kweyu/Standard

Outside security was tight and when Njenga walked out free, a cordon was formed around him as he boarded a prison van back to King’ong’o for clearance.

Next plan

His supporters demanded he addresses them. But he opted to address a press conference saying he had no grudge against his tormentors.

Hii ni hali ya maisha,” he said as he struggled to contain the surging crowd that competed to shake his hand. Mr Njuguna Gitau, the leader of Mungiki’s political wing, was among those present.

He said his priority would be to bury his wife who died more than a year ago.

The other goal, he said, was to be baptised. He then left with a convoy of 20 cars to Nairobi and headed to Jesus is Alive Ministries where he was recieved by Bishop Margaret Wanjiru.

Njenga said he had ‘seen the light’ and urged other sect members to also denounce the sect’s activities.

Wanjiru said she would soon baptise him to signify a ‘rebirth’ and also invited other sect’s followers.

The Standard

Kakobe: Upole wa JK hatari.

kakobe

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, amesema ameshtushwa na ukimya wa Rais Jakaya Kikwete kushindwa kukemea nyaraka zinazotolewa na madhehebu ya dini, hali ambayo inaweza kusababisha machafuko kama haitadhibitiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Askofu Kakobe alisema tamko la Rais Kikwete lina uzito kuliko kiongozi yeyote nchini.

Alimtaka Rais Kikwete asikae kimya, kwani kufanya hivyo kutaonekana kama ni kutaka kumfurahisha kila mtu.

Alisema kama hali hiyo ikiendelea, inaweza kuligawa taifa ambalo limekuwa na misingi ya amani, umoja na utulivu tangu wakati wa Mwalimu Nyerere.

“Rais Kikwete anapaswa kutoa tamko juu ya viongozi wa dini, ambao sasa wanatoa nyaraka mbalimbali… tunaamini kauli yake itakuwa nzito kuliko kiongozi yeyote,” alisema Askofu Kakobe.

Alisema Rais Kikwete ni mpole, lakini anapaswa kuonyesha ujasiri wake ili taifa lisipoteze amani iliyojengeka muda mrefu isitoweke.

Akionekana dhahiri kutoridhishwa na nyaraka hizo za kidini, alisema umefika wakati uhuru wa kutoa maoni utumiwe kwa mipaka, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa maoni yanayotolewa hayasababishi kwa namna yoyote ile taifa kugawanyika.

Alisema moja ya jukumu kubwa la viongozi wa dini, ni kuilinda serikali kwa manufaa ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya dini fulani.

“Mtu kama anataka kutoa maoni yake atoe kama yeye na si kushirikisha dhehebu zima, na aangalie kitu gani anachozungumza si kama walivyofanya Wakatoliki na Waislamu kwa kusema kuwa ‘huu ni waraka wa Wakirsto’ na ‘huu ni muongozo wa Waislamu’,” alisema Askofu Kakobe.

Sababu kubwa ya viongozi wa madhehebu ya dini kutoa waraka na mwongozo, ni kuwataka wafuasi wa dini hizo na Watanzania kwa ujumla kuchagua viongozi wanaofaa.

Alisema viongozi wa dini hawatakiwi kutoa waraka unaohusu siasa na kuwahimiza waumini wao kuchagua viongozi wa dini zao kwani katika uchaguzi mkuu wa mwakani watatakiwa kuchagua viongozi wa serikali na wala si wa dini.

“Kiongozi akienda kuomba kura, haendi kama muumini wa dhehebu fulani, bali anaenda kama mfuasi wa chama fulani. Sijawahi kusikia mbunge wa dini fulani, ila ni mbunge wa Watanzania wote. Kinachotuunganisha ni Utanzania si dini wala ukabila,” alisema Askofu Kakobe.

Alisema nyaraka zilizotolewa na Wakristu na Waislamu, zimejaa maneno ya kichochezi ambayo yanatumika kama miongozo kwa waumini wa dini hizo na Watanzania kwa ujumla.

“Waislamu walipozindua waraka wao, walisema; ‘Wakatoliki wamemwaga ugali na sisi tunamwaga mboga. Kama Wakatoliki wangezingatia ushauri huenda tusingefika huku sisi Waislamu’. Kauli hizi ni za hatari, zinaweza kuleta vita,” alisema Kakobe.

Kuhusu waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki, Askofu Kakobe alisema hali hii inaonyesha mpasuko kwani kila dhehebu linataka mfuasi achague kiongozi kutoka kwenye dini husika.

Akitoa mfano wa maneno yanayoashiria mpasuko katika waraka wa Kanisa Katoliki, Kakobe alinukuu kifungu kinachosema; “wagombea wanavyotawaliwa na dini yao ni muhimu kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuanzia ngazi za vijiji hadi taifa kwa jumuia za kanisa ili tunu za Kikirsto zionekane katika sera na uongozi.”

Katika hatua nyingine, Kakobe alikemea kauli iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Antony Mayalla, kwamba wanasiasa hawana haki ya kuwafundisha viongozi wa dini kama walivyofanya mara baada ya kanisa hilo kutoa waraka wake.

Alisema, Pengo alionyesha jeuri na utovu mkubwa wa nidhamu kwa kiongozi wa nchi, kwa kutoa kauli hiyo mbele ya Rais Jakaya Kikwete.

“Nikemee vikali tamko la kiongozi mmoja wa dini aliyesema ‘wanasiasa wasitufundishe’. Kauli ile aliitoa mbele ya rais, ule ulikuwa ni utovu wa nidhamu. Ilionyesha jinsi alivyo jeuri na asivyotaka kushaurika. Sisi kama viongozi wa dini, tunapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda amani na utulivu,” alisema Kakobe huku akiepuka kutaja jina la Pengo ingawa baadaye alijisahau na kumtaja.

Alisema kawaida waraka hutolewa na viongozi wa vyama vya siasa wakati wa kampeni kwa ajili ya kujinadi mbele ya wananchi.

“Dini inapotoa waraka, inamaanisha inataka kushika madaraka kama vyama vya siasa… wote tunaamini kwamba dini inafanya kazi kama ilivyosajiliwa,” alisema Askofu Kakobe.

“Unajua kama DECI ilisajiliwa na kufanya shughuli zake, lakini ilivyogundulika kwenda kinyume cha sheria, ilifungiwa na kushuhudia inafikishwa mahakamani. Hivyo dini hizi zinapaswa kufunguliwa mashitaka kwa kwenda kunyume na usajili,” alisema Askofu Kakobe.

Alisema anawashangaa viongozi wa dini na watu wanaoshabikia waraka huo wa Kanisa Katoliki, kwamba unapinga viongozi mafisadi wasichaguliwe, ilhali chanzo kikuu cha kuwepo kwa mafisadi ni viongozi wa dini kushindwa kuwajibika na kuwaelimisha waumini wao hadi wakajiingiza kwenye ufisadi.

“Mafisadi wana dini na wamelelewa katika dini hizi hizi, sasa iweje wao wawasemee mafisadi? Ina maana wamekuwa wazembe katika kukemea na kujenga maadili. Kwa hiyo wao ndio wanaotengeneza mafisadi,” alisema Askofu Kakobe.

Aliwataka wananchi kutoshabikia nyaraka zinazotolewa na viongozi wa dini na waziogope kama ukoma kwani vita ikitokea, hakuna fidia watakayopata wananchi kama walivyopata wahanga wa matukio ya milipuko ya mabomu Mbagala.

Alishauri viongozi wa madhehebu ya dini, wanasiasa na viongozi wa kiserikali wakutane na kujadili mustakabali wa umoja na amani ya taifa, ikiwa ni pamoja na athari za dini au dhehebu kutoa waraka unaowaandaa wananchi kwa ajili ya chaguzi za kisiasa.

Source: Tanzania Daima Newspaper

Mtume na Nabii Josephat Mwingira asaidia maendeleo mkoa wa Rukwa

Mwingira

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Uzinduzi wa MANUKATO ya Fanuel Sedekia ulifanikiwa

mrata

Tamasha hili la uzinduzi lilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar-es-salaam, tarehe 8/2/2009 ambapo watu walijitokeza kwa wingi. Pichani ni mbunge wa viti maalumu Martha Mlata  akiinadi CD ya MANUKATO ya marehemu Sedekia, pamoja na kuinadi CD hiyo aliimba nyimbo zake na alisisitiza japo amekufa lakini anaishi kutokana na kazi aliyoiacha. Tamasha liliandaliwa na Waimbaji wa Nyimbo za Injili.

Pia waliuza Cd’s, Tshirts na vitabu vinavyomhusu Sedekia. Mke wa marehemu hakuweza kuhudhuria lakini walikuwepo wadogo wa marehemu. Pesa iliyochangwa ni kwa ajili ya kuisaidia familia ya Sedekia.

Mungu azidi kuifariji familia yake na akasimame kuwatetea.

Waziri mkuu aonya viongozi kwenda kwa waganga wa kienyeji!

pinda1

Waziri mkuu, Mizengo Pinda, ametema cheche kwa kuwaonya viongozi wa serikali, vyama vya siasa na askari wa jeshi la nchini kuacha mara moja tabia ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kutafuta dawa za kupandishwa vyeo.

Alisema kuwa hali hiyo ya kuamini waganga wa kienyeji wana uwezo wa kuwapa dawa ya kupanda cheo, imekuwa ikiwafanya wengi kutowajibika.

Kuhusu mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na mauaji ya Albino na vikongwe alisema hayatawezekana ikiwa viongozi wenyewe hawatakuwa mstari wa mbele katika kuwadhibiti waganga wanaochangia kwa kiasi kikubwa mauaji hayo.

NIPASHE

Tuzidi kuomba Mungu aliponye Taifa letu!

by

Wapendwa katika Bwana, vikundi mbalimbali vinavyoomba kwa ajili ya Tanzania, tuzidi kulifuta suala la mahakama ya Kadhi, OIC na mauaji ya maalbino. Tuombe kwa ajili ya viongozi wa Serikali, Mungu awape uwezo wa kuiongoza nchi katika katika hekima ya Mungu.  Pia tuombe wapendwa nao wajitokeze kuwania nafasi mbalimbali mfano:- Siasa, Maofisini, Vyuoni nk. Ili pakawe na hofu ya Mungu kila mahali.

Kwa sasa Tanzania imegubikwa na masuala ya ufisadi ambapo imepelekea mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona wanashitakiwa kwa kutumia vibaya madaraka waliyokuwa nayo ya uwaziri  na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7, kati ya mwaka 2003 na 2007.

Hello Brethrens!

I urge you to pray for our country. As events are unfolding, you might think things are going well, but nope! Our top leaders are passing in hard times. Let us call for our God’s intervention and preservation of our leaders and make them brave enough to do what God have for Tanzania. It is our duty and let’s do it.

“I exhort therefore, that, first of all, supplications, prayers, intercessions, and giving of thanks, be made for all men; For kings, and for all that are in authority; that we may lead a quiet and peaceable life in all godliness and honesty. For this is good and acceptable in the sight of God our Saviour;  Who will have all men to be saved, and to come unto the knowledge of the truth ” (1Tim 2:1 – 4) 

 

—-App. Stephen—