Category Archives: SINGERS
BUBELE&DIANA MINISTRIES Kuleta Uamsho wa Kusifu na kuabudu Afrika
Inapendeza kuona watumishi wanaoenda nje ya Nchi yao kuendelea na huduma na kuzidi kuwa na kiu katika kumtumikia Bwana. Pichani ni dada anayefahamika kama Diana Madida, alisikika sana na album ya MIMI NAJUA KWAMBA YESU ANANIPENDA. Ilikuwa ni baraka kwa wakazi wa kanda ya ziwa kumsikia na kuona nyimbo zake zikisambazwa sokoni mwaka 2003! Strictly Gospel ilipata nafasi ya kuzungumza naye na akaeleza safari yake kwa ufupi na maono aliyonayo kwa sasa. Utaweza kusikiliza na kuona video ya wimbo mpya AFRIKA alioufanya na mumewe Bubele E Kiyaile. Fuatilia chini habari kamili
VIDEO YA WIMBO AFRIKA YETU
Diana Madida au Diana M Kihayile,ni jina jipya baada ya kuolewa mwaka 2006 na Mr.Bubele E Kihayile. kabla ya hapo au kwa watu wengi nimekuwa nikijulikana kwa jina la Diana Madida. Nimezaliwa na kukulia Mwanza Tanzania,kwasasa naishi Birmigham uk,mimi,Mr.Bubele na tuna watoto wawili wa kike,Rina Jodiah(2.4yrs) na Jaina Sasha(5.3mths)
Niliokoka june 1997, kupitia mikutano ya Moses Kulola na nikaamua kujiunga na kanisa la E.AG.T Imani kwa mchungaji Juliana Nyanda, hapo ndipo safari yangu ya huduma ilianza rasmi,1998 nilijiunga kwaya ya kanisa FAITH AMBASSADORS CHOIR, na baada ya muda Mungu alinisaidia nikaanza kuimbisha baadhi ya nyimbo,1999 niliendelea kukua kiroho na kihuduma nikaanza kuongoza ibada za kusifu na kuabudu ndani ya kanisa hilo na 2000 nilijiunga Kihayile band huduma hii Mungu alizidi kuizidisha na kuipaka mafuta na kupata nafasi ya kuhudumu ndani na nje ya kanisa.
2003 nilitoa solo album(MIMI NAJUA KWAMBA YESU ANANIPENDA)iliingia sokoni Tanzania kupitia Mamus distributors, ila hawakuweza kuendelea kuisambaza kwani niliondoka nchini mara baada ya kutoa album hiyo, 2004 Mungu alinifungulia njia nikaja masomoni Birmingham UK. ambapo niliendelea na huduma ya kusifu na kuabudu katika kanisa la Lighthouse chapel, 2008 kwa msaada wa Mr. Bubele niliweza tena kutoa album ingine ya pili (MILELE)ambayo niliingiza sokoni hapa UK na niliweza kuituma nyumbani kwenye baadhi za redio, nyimbo ambazo zilipendwa na waliosikia ni Uwe karibu nami, Tumeahidiwa ufalme mwema na milele. Baada ya hapo kwasababu siko peke yangu, nimeweza kuunganisha plan zangu kihuduma na mume wangu ambapo ni jambo la kumshukuru Mungu kwani naamini mmoja anaweza ua elfu ila wawili makumi elfu. Mr Bubele Kihayile is the perfect match from heaven to me, ni mentor wangu, mwalimu wangu, mtunzi wa nyimbo na muziki wote wa nyimbo zetu na mtumishi mwenzangu katika huduma. kwahiyo kwasasa tuna project mpya kama BUBELE & DIANA MINISTRIES ambapo tunatengeza album mpya au ya kwanza kama ministry, katika abum hii tunatajia kurekodi nyimbo 12 (kumi na mbili) ambapo zitakuwa out hivi karibuni(kufikia wakati wa summer) kwa msaada wa Mungu mpaka sasa tumesharekodi nyimbo nne na tumefanya video moja ya wimbo unaitwa Africa yetu.
Maono katika huduma.
Matarajio yetu ni kuona ufalme wa Mungu umetukuka duniani,we are created to worship and to usher his people into his presence. Ni matarajio yetu kuongeza uamsho wa kusifu na kuabubu kwanza nyumbani kwetu/Tanzania, Africa na duniani kote kwa ujumla, pia kwa kutumia muziki wa Africa kuleta uamsho ndani na nje ya afrika yetu. Tunaamini Mungu ametupa maono katika kuwafikia wengi kwanjia ya uimbaji kwahiyo in future tunategemea kuwa na Music organisation ambayo itakuwa ni kamili nikimaanisha kujumlisha mambo na nyenzo zote ambazo zinaweza kuinua, kupromote na kutangaza habari za Yesu kupitia muziki wa injili.
Mengineyo
Mungu ni mwaminifu siku zote hawezi kumwacha mtu wala kumsahau, hivyo tuendelee kuamini ya kuwa ni baba na rafiki wa ajabu, kama mtu ni mkristo/amezaliwa mara ya pili, asikate tamaa anapopita katika hali ngumu na asimwache Mungu anapopitia furaha tele. Pia kama mtu si mwamini ni vizuri aje kwa Mungu kwa kumwamini Yesu kwasababu Yesu ndiye njia kweli na uzima, pia asijione kuwa hastaili kuitwa mwana wa Mungu kwani Mungu mwenyewe amesema hapendi mtu hata mmoja apotee na hafurahii kifo cha mwenye dhambi hata mmoja!
Pia kama wakristo tuna wajibu wa kutubu na kuiombea ardhi(nchi) ambayo Mungu anakuwa ametuweka tuwe resident wa hapo,tutamke mema na tutabiri mema kwa nchi tukijua ya kuwa haki uinua taifa,na Mungu anatuangalia sisi kama gates/milango ya kuleta Baraka na neema juu ya nchi tunayoishi, hivyo tutamke mema siku zote na tusilalamike na kulaani na walaanio,pia tukumbuke kuwa vinywa vyetu vinaumba kwa hiyo kila tusemayo katika ulimwengu wa roho yanakuwa na hatimaye hudhiirika katika halisi/ulimwengu wa mwili.
Africa Praise Night – Ottawa
Upendo Kilahiro amealikwa nchini Canada kwa ziara ya mwezi mmoja ambapo jumamosi wiki hii atafanya huduma kwenye kanisa la Christ Chapel Bible Church jiji la Ottawa. Huduma atakayoifanya ina lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya Watoto Yatima wa Morogoro.
Amechaguliwa kuwa muimbaji kutoka Tanzania ambapo siku zote atakuwa Canada atafanya huduma ya uimbaji sehemu mbali mbali alizoalikwa na atakazoalikwa.
SIFA EBENEZER FOUNDATION kuzinduliwa Biafra!
Mwimbaji wa Injili kutoka Tanzania Sifa John anatarajia kufanya Tamasha kubwa la uimbaji ambapo atazindua album yake USILILIE MOYONI na huduma yake SIFA EBENEZER FOUNDATION siku ya tarehe 29/4/2012 viwanja vya Biafra.
Akiongea na Strictly Gospel dada Sifa anaielezea SIFA EBENEZER FOUNDATION “nina mzigo wa kusaidia watoto, vijana na mabinti wasiojiweza, kuwasaidia waondoke kwenye mazingira magumu, kutoshawishika kufanya vitendo viovu, kufundishwa ujuzi mbalimbali, kuinua vipaji vyao pia na kupatiwa semina mbali mbali za kiroho”.
“Mgeni rasmi atakuwa Emmanuel Nchimbi, pia ninawakaribisha wadau wote kuhudhuria siku hiyo waimbaji wengi wataimba na kumtukuza Bwana” alimalizia kusema dada Sifa.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na dada Sifa kwa email, sifajohn@ymail.com
Hongera dada Kambua
Jumamosi iliyopita tarehe 7/4/2012 ilikuwa siku ya furaha kwa dada Kambua Manundu. Ambapo alifunga harusi yake na mfanyabiashara na mchungaji Jackson Mathu kwenye bustani Windsor Golf Hotel.
Walihudhuria waalikwa kadhaa na baadhi yao ni pamoja na Esther Wahome, Mercy Masika, Marsha Mapenzi, Alice Kamande. Ambapo Esther Wahome alimshauri “Najua inawezekana kuolewa na kuwa mwenye furaha, Nina ndoa yenye furaha kwa miaka 16 na nina watoto watatu”
Watanzania tunakutakia heri dada Kambua!
Nani Mshamba – Stara Thomas
Muimbaji wa Injili nchini Tanzania, Stara Thomas. Ameachia wimbo wake wa Nani mshamba unaopigwa kwenye vituo vya redio za injili nchini. Wimbo huo una maneno yafuatayo
“Aliye kwa Yesu ni mjanja,
Aliye kwa Yesu si mshamba,
Yuko kwenye mwanga, mwanga wa milele”
Stara akiongea na moja ya redio ya Injili amesema baada ya yeye kumpa Yesu maisha yake “wengi walinitenga na wengine kunidharau lakini mimi sijali maana mtu anayekuwa kwa shetani ni mshamba”
Album ya dada Stara NANI NI MSHAMBA iko tayari na itasambazwa mwezi wa nne.
Habari nyingine zinazosikika ni kuhusu Beatrice William aliyepata umaarufu kupitia Bongo Star Search naye ameokoka tarehe 7/3/2012 kwenye kanisa la Mikocheni B Assemblies of God (Mlima wa moto)
Alipoongea akiwa madhabahuni tarehe 9 Machi kwenye mkesha kuhusu uamuzi wake wa kumpokea Bwana Yesu alisema “Ni uamuzi wangu wa dhati kuokoka na akili zangu timamu. Mara nyingi nilipenda sana kuokoka lakini niliogopa kumbipu Mungu kama wengine wanavyofanya”
Kufahamu mengine kuhusu Stara Thomas fuatilia link hii
http://strictlygospel.wordpress.com/2011/02/21/stara-thomas-ameokoka/
Karibu Roho – Neema Cizungu
Neema ni muimbaji wa nyimbo za Injili mwenye asili ya Congo, anafanya muziki wake nchini Kenya. Amejulikana Tanzania na album yake ya Karibu Roho iliyofanya vyema Afrika Mashariki, unaweza kusikiliza nyimbo zake kama HAKUNA MUNGU KAMA WEWE, KARIBU ROHO, SADAKA ZA SIFA, TUMRUDIE MUNGU, CONNECTION, MSAADA, NI NANI KAMA WEWE na MABOTA.
Akiongea na Strictly Gospel, Neema alisema alianza kuimba kwaya akiwa na miaka sita (6) “Nilipofikisha miaka 12 nikabatizwa kwa maji mengi na kujiunga kwenye kwaya ya watu wazima, nilikuja nchini Kenya nikiwa na miaka 22 na kurekodi album yangu ya kwanza mwaka 2009. Mungu alinisaidia kunipa ujumbe na ilinichukua mwaka mmoja kumaliza kurekodi”
Kwasasa dada Neema anaandaa album yake ya pili tayari amerekodi wimbo mmoja unaitwa JINA LAKO.
Bahati Bukuku asema ni MWAKA WA KIBALI
Muimbaji wa Injili Tanzania Bahati Bukuku baada ya kuwa kimya kwa miaka minne tayari ana album mpya yenye jina MWAKA WA KIBALI, hii ni album yake ya nne ambapo nyimbo mpya kama WEWE NI BABA na UNATISHA zimeanza kusikika redioni.
Bukuku amekuwa akiimba nyimbo za faraja na amekuwa akisisitiza nyimbo zake ni maisha yake na jinsi Mungu anavyo muongoza ili afanyike msaada kwa wengine, kwa Utukufu wa Mungu. Karibu tena Dada Bahati ni siku nyingi tumesubiria!
Glorious Celebration Band
Band nzuri inayovuma kwa sasa nchini Tanzania, kwa uchezaji wao wa staha na sauti zenye kusikika vyema. Kiongozi wa Glorious Celebration Band Emmanuel Mabisa, aliongea nasi machache kuhusu kazi yao na malengo waliyonayo katika kuujenga mwili wa Kristo.
“Maono yetu ni kufanya huduma mashuleni na vyuoni kwa ajili ya kuwahubiria Vijana Habari njema za Kristo, na pia kufanya matamasha makubwa mbali mbali”
Alkadhalika kundi hili linaundwa na waimbaji mahiri wanaosikika kwenye soko la muziki wa injili na wengine chipukizi wanasikika. Band hii inalelewa na msimamizi mkuu Bishop Mwakang’ata wa Full victory Gospel Church ya Chang’ombe Temeke, Dar es salaam.
Waimbaji wengine wanaounda kundi hilo ni Angel Bernard ambaye ndiye mweka hazima, Chaka Mtunguja Katibu wao, Jesca Honore, Nice Marandu, Davina, Risper, Ima Malisa, Emmanuel Materu, Emmanuel Gripa, Daniel Kibambe, Arone Botto, David Silomba, Ester Peter, Paul Mwakanyamale na Mercy Denis.
Kwa sasa wanajiandaa kurekodi Live Dvd mapema mwezi wa sita mwaka 2012! Hapo awali wamerekodi video ya album yao ya kwanza NIGUSE, unaweza kufarijika kwa kusikia wimbo huu wa NIGUSE,
Mpaka sasa wametimiza mwaka mmoja tangu wameanzisha bendi yao na wametoka na album ya NIGUSE….hata hivyo kama watu walivyozoea kila Ijumaa kuwaona THE ATRIUMS HOTEL, kwa sasa itakuwa wanamtukuza Mungu kila ijumaa ya mwisho wa mwezi, viwanja vile vile.
Tanzania tunajivunia kuwa na waimbaji kama hawa!
Umetenda Mema – Kambua
![]() |
| Kambua |
Kambua ni muimbaji wa nyimbo za Injili mwenye jina kubwa nchini Kenya, alianza kuimba na kupenda nyimbo za Injili alipokuwa mdogo na watu wengi waliona kilichokuwa ndani yake, baadaye mwaka 2005 akaenda kusomea Muziki nchini Canada chuo cha Kikristo, Calgary. Na katika maisha yake chuoni, alijiunga na band ya chuo Legacy Youth Conference (LYC). Anasema alipokuwa Canada, hawezi kusahau alipochaguliwa kuimba na Angelique Kidjo kwenye tamasha moja.
Kambua ambaye mama yake ni mchungaji, mbali na nyimbo zake kupigwa redioni na kuonekana kwenye TV pia na tuzo alizopokea haachi kusema kwamba maisha yake ameyatoka kwa Bwana Yesu na kusoma Neno lake mara nyingi.
Muimbaji huyu amekuwa akifanya huduma aliyonayo kwa kushirikiana na waimbaji wengine na kuuinua muziki wa Injili kwa kuiwakilisha nchi ya Kenya na hata Afrika mashariki.
Ametamani kuwa sauti ya wanawake na watoto katika kujenga maendeleo ya nchi zinazoendelea, mbali na shughuli za jamii na uimbaji Kambua pia ni mtangazaji wa Citizen TV, kipindi cha Rauka.
Moja ya wimbo wake unaochezwa kwenye redio na TV za Afrika mashariki
Mtu aponywa UKIMWI kwa kusikiliza Album ya nyimbo za kuabudu!
Mungu apewe sifa kwa matendo makuu anayotenda kwa kupitia mtumishi wake Mwinjilisti Milca Katete anayefanya kazi ya uimbaji nchini Canada. Muimbaji huyu mzaliwa wa Arusha Tanzania, amesikika sana na nyimbo kama NATAMANI SOGEA na KABLA SIJAKUUMBA ambazo zote zinapatikana kwenye album ya YESU NIKO MBELE ZAKO.
Akiongea jinsi Mungu alivyotenda kupitia album yake, anasema anamuheshimu na siku zote kumtii anachosema ili yeye ndiye afanye kazi na maisha ya watu, akielezea jinsi alivyorekodi album yake ya YESU NIKO MBELE ZAKO Anasema ” Nilisikia Mungu akisema nami nitoe album hiyo, katika hatua ya kumsikiliza Bwana, Nikaingia kwenye maombi na kupata hakika wa kuendelea na hatua hiyo ndipo nilipoingia studio na kusikia nguvu ya Mungu ikisimamia album ile hata ilipokamilika.
(Chini ni moja ya wimbo ulio kwenye album ya YESU NIKO MBELE ZAKO, NATAMANI SOGEA)
Anaendelea kutoa ushuhuda baada ya album yake kutoka alipata ujumbe kwa ndugu aliyekua amejawa furaha na shukrani akieleza mambo ambayo Mungu ametenda kupitia album hiyo, Alikua kwenye maombi ya siku mbili akimsihi Mungu amponye, akiwa ndani ya maombi Mungu alisema naye kuuwa atulie asikilize kanda hiyo ya kuabudu yenye jina YESU NIKO MBELE ZAKO.
Akiwa katika kuabudu alikuwa katika hali kama ya kupoteza fahamu kama nusu saa kisha akaamka akasikia sauti ikisema mshukuru Mungu maana umepona.
Alienda hospitali kupima alikua na UKIMWI, akakutwa hana tena. Ndipo nikakumbushwa kwanini niliambiwa niitoe hiyo album, ni kwa Utukufu wa Mungu, sio Burudani tu. Namtukuza Mungu kwa ajili ya Utumishi aliouweka ndani yangu.
–Milka Katete
Ujana ndio muda wa kumtumikia Mungu na pia KUMJUA MUNGU – ELANDRE
Jina halisi anaitwa Emmanuel Andrew Mkumbwa, Anajulikana na marafiki zake kwa jina la ELANDRE. Kwa wanaofahamu muziki wa Gospel Hip Hop, sio jina geni kwao kutokana na radha ya sauti yake na ujumbe wa maneno anavyopangilia. Kwa sasa anasikika na wimbo wa ‘I am what I am’ aliyoifanya, Dreamers Park recording studios chini ya usimamizi wa Sam Mwangati wa CCC. Ambapo wimbo huu uliingizwa kwenye albam ya APRaW, mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za waimbaji wa Injili.
ELANDRE, amekua akishirikishwa na waimbaji wengine wa miondoko hiyo kama Pona Hurst kwenye nyimbo ‘Justice Reign’ na ‘Watch Out’ pia Gee&Seth wimbo wa “This is my Year”, Nicky Urio au NABII nyimbo kama ‘Gospel Party’ na ‘Chapa Snare’ zilizo katika albam yake iitwayo Ladha ya Kinabii, Baltazari kwenye wimbo wa ‘Popote Yupo’ na Mac Elvis wa Uganda amemshirikisha kwenye wimbo wa ‘Church Boy’ wimbo uliomuinua katika chati za muziki wa Injili, nchini Uganda.
“Nilianza christian rap mwaka 2004 kutokana na kikundi cha maombi nlichokua nashiriki kilikua kinaitwa Youth Life Prayers (YLP); pia kutokana na profecy za watu juu yangu na jinsi Mungu atakavonitumia. Single yangu ya kwanza iliitwa ‘Praise the Lord’ inspired by the book of Psalms 150. Ilibamba sana kipindi kile. 2007 nikatoa single ya pili ambayo niliirekodi AM Records ndugu yanu mmoja anaitwa Casy ndo aliiproduce hii track iitwayo ‘KEEP MOVING’. Nayo ilifanya vizuri maana ilifungua milango mpaka ya airplay katika radio ya Praise Power. Hii track ndo ilisababisha mpaka international doors kufunguka. Mchungaji wangu Fred Okello alikuja na kikundi cha waGanda wanaitwa Soul 5..wakarudinayo Kampala. Baada ya hapo nikajulikana huko Uganda” anasema Elandre
Elandre yuko Lusaka, Zambia akirekodi albam ya yake ya kwanza ‘Goemmi Records’ chini ya producer TAZ, ambapo amepata mkataba wa kurekodi kutoka R.I.O.T “Namshukuru sana Pastor Isaac wa Tehillah, Mungu amfungulie milango zaidi”
Anaendelea kusema “Ujana ndo muda wa kumtumikia Mungu na pia KUMJUA MUNGU. Unaweza ukawa unamtumikia lakini humjui na wala hakujui wewe, ndo maana mwisho wa dunia atawaambia wengi sikujui na wala sikuwahi kukujua na wataishia motoni. Mungu anakupenda sana, kaa nae, keti nae mchonge mambo ya maana na sio kupoteza mda na unnecessary business. Nimeokoka, na passion yangu iko kwa vijana, maana wanakua na ni nani ataelekeza the right direction kama sio sisi tulioijua kweli. Blessings, peace and love to you all”
…..Tunakutakia kila la heri na Mungu akuinue katika utumishi aliokuitia…..
Take The Victory ya J Sisters, yawafanya wafikirie Makubwa zaidi!
Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, J Sisiters wakifanya Mahojiano na Dada Mary Damian wa Strictly Gospel
Ni ndugu wa familia moja Juliana Mshamma, Jacqueline Mshamma, Jessica Mshamma na Jennifer Mshamma kwa pamoja wameunda kundi lao wanajiita J SISTERS kwasababu herufi za majina yao ya kwanza zinaanza na J. Wanajulikana sana kwa umahiri wao wa kucheza na utunzi wa nyimbo za kipekee zinazowatambulisha kama J SISTERS, Album yao ya kwanza BADO KIDOGO ndiyo iliyowatambulisha vyema kwenye muziki wa Injili Tanzania na nje ya nchi! Album ya Pili SHUKA BWANA ilifanya vyema na wakafikiria kutoka kimataifa na album ya tatu TAKE THE VICTORY imewafanya wafikirie kufika mbali kimuziki na katika utumishi Mungu aliowaitia.
Pichani Juu: Julie, Jacqueline na Jennifer wakiwa maeneo ya Chuo wanachosoma Liberty, USA. Nyimbo zao zinapatikana sokoni na walio nje ya Tanzania hususan USA wanaweza kupata nyimbo zao kwa kuwasiliana nao kwa simu +434 426 2267
MAHOJIANO ZAIDI SIKILIZA HAPA!
USILE VYA BURE ya Askofu Jangalason!
Askofu Charles Jangalason na mkewe Holipa Jangala wakiwekwa wakfu kwa ajili ya huduma na Bishop Kitonga wa nchini Kenya
Askofu Jangalason, ametoa jumla ya album 11 ambazo ni 1. USIWE KAMA POPO. Vol.2 DUNGWA SINDANO. Vol. 3 VAA KIATU. Vol.4 TIBU MASIKIO. Vol.5 SUGUA MENO. Vol 6 USIMUIGE MBUZI. Vol 7 JIFUNZE KWA KUKU. Vol. 8 FUA NGUO. Vol. 9 JAZA TUMBO. Vol. 10 USILE VYA BURE. Pia kuna album ya Christmas ambayo hakuipa namba, nayo iko Hewani, inaitwa FUKUZA MPANGAJI.
Mbali na uimbaji Askofu Jangala ni mwangalizi mkuu wa huduma ya HOPE FOR ALL NATIONS huduma yake inapatikana Goba, Jijini Dar es salaam, anawakaribisha watu wote kumtembelea ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo zaidi kuhusu Bwana Yesu tu. Albam ya USILE VYA BURE inapatikana Mwananchi Store Kariakoo.
Hongera zako Catherine Kyambiki
Muimbaji wa Injili wa siku nyingi Catherine Kyambiki, tarehe 21 Aug 2011 ilikua ni siku yake ya furaha alipofunga harusi na Mr. Samuel mtumishi wa Mungu kutoka Angola kwenye kanisa la Dorcus Christian Ministries lililoko Kunduchi Dar es salaam. Mahudhurio yalikua ya kutosha waimbaji wengi wa nyimbo za Injili walihudhuria huku wakiongozwa na Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania CHAMUITA Mh. Addo November. Sherehe nzima iliongozwa na MC John Shabani maarufu kama Touching Voice aliyevuma na album ya Marufuku kukata tamaa.
Catherine Samuel ameweka historia Tanzania kwa uimbaji wa nyimbo za Injili pia na kuchunga kondoo wa Bwana. Strictly Gospel inakutakia kila la heri huko Angola!
K-Bazil, kuzindua Yesu ananipenda mwezi huu!
Muimbaji wa Injili wa zamani wa bongo fleva K’Basil ambaye jina lake kamili ni Kashumba Basil ambaye hapo awali aliripotiwa kuokoka ameonyesha kukomaa katika Imani hiyo na kuamua kuachana kabisa na uimbaji wa muziki wa Bongo fleva na kugeukia kumuimbia Mungu.Hivi sassa K’Basil amekamilisha album yake ya kwanza ya muziki wa Injili YESU ANANIPENDA ambayo ataizindua, May 2011.
Randson Saab – Nikupe Nini Jehova?
Ni Mdogo wake muimbaji wa Injili, Marehemu Emachichi ametoa album ya NIKUPE NINI JEHOVA? inayosikika vyema nchini Kenya.
Pia mtumishi wa Mungu Randalson anatoa shukrani za pekee kwa familia ya Askofu Kadodo iliyoko Dar es salaam kwa faraja kipindi kaka yake Emachichi alipoondoka duniani. Mwaka 2007 Randalson aliimba nyimbo za kaka yake na kutoa video ya IENDE MBELE INJILI.
Album ya Randalson inapatikana!
“Ni asubuhi” ya Miriam Lukindo inapatikana
Anasikia – Miriam L Mauki!
‘Tembelea Nchi Zetu” ya Pastor Willy Mshila
Mchungaji Willy Mshila amerekodi video ya nyimbo ijulikanayo kwa jina “Tembelea Nchi Zetu” ambayo kwa sasa iko madukani. Video hii ina nyimbo nane ukiwemo wimbo wa kuabudu ujulinakanao na wengi uitwao “Ni Nani Kama Wewe Bwana..”. Mchungaji huyu ndiye mtunzi wa wimbo huu na alisema maneno ya mwanzo ya wimbo huo ni:
Ni nani kama wewe Bwana – Nani kama wewe x4
Ooh Hakuna – Hakuna mwingine kama wewe Bwana,
Ooh Hakuna – Hakuna mwingine kando yako wewe Bwana x2
Akiongea na SG, mchungaji Willy alisema kuwa yeye alianza Huduma ya kusifu na kuabudu tangu mwaka 1994 na kuanza kuongoza sifa na kuabudu mwaka 1996 akiwa mjini Mombasa, nchini Kenya. Tangu aingie katika huduma ya kuongoza Kusifu na Kuabudu maono yake ni kutumika na kushiriki kuendeleza huduma hii ya Kusifu na Kuabudu hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo hadi sasa anaendelea ndani ya maono hayo.
Alipoulizwa huwa anajisikiaje anaposikia wimbo wake ukiimbwa makanisani na hata kurekodiwa kwenye kanda za nyimbo na za video za waimbaji wengine, yeye alijibu kwamba huwa inamfariji ya kuwa kumbe anaweza kuandika nyimbo na zikubalika kwa ajili ya kumuabudu Mungu. Lakini alisema kuna watu ambao wamekuwa wakiuimba kwa kuubadilisha maneno na hata sauti tofauti na vile alivyoutunga mwanzo. Kutokana na hali hiyo yeye alishauri ni vizuri nyimbo zikaimbwa kama zilivyotungwa. Kama mtu anataka kubadilisha ni vema akamtafuta mtunzi na kuomba kibali cha kufanya hivyo. Labda kwa nyimbo ambazo ni za zamani sana ambazo watunzi wake hawapo tena duniani ndipo mtu anaweza kubadilisha tu. Lakini alishauri sana mtu akiimba wimbo ambao si yeye aliyeutunga ni vizuri akauimba kama ulivyo ili kuendeleza ujumbe na mguso wa asili wa wimbo husika.
Pamoja na kuongoza Kusifu na Kuabudu, kwa sasa mchungaji Willy Mshila anatumika akiwa mchungaji mmisionari, mjini Arusha, nchini Tanzania.
Kwa mawasiliano Mchungaji Willy Mshila anapatikana kwa simu namba +255 754 622963 na +254 726 485545.
MWINUE YESU – Emmy Lubala
Emmy Lubala ni muimbaji wa siku nyingi kutokea jiji la Mwanza, ametoa album yake ya nyimbo za sifa na kuabudu MWINUE YESU yenye jumla ya nyimbo nane (8)
Akiongea na SG anasema “Namshukuru Mungu sana ambae ameniwezesha kufika katika hatua hii. Nilimpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu kupitia nyimbo za Injili tu. Hivyo kiu ya kumtumikia Mungu katika njia ya Uimbaji iliwaka ndani yangu hatiame mwaka 2008 mwezi wa tatu (March), nilifanikiwa kurekodi Albam yangu ya kwanza ya Mwinue Yesu. Japokuwa uimbaji ulianza tangu nikiwa na umri wa miaka saba (7)”
Aliendelea kusema “napenda kumrudishia Mungu sifa na utukufu kwa vile anavyonitumia katika huduma hii ya kumsifu Mungu. Pamoja na uimbaji, pia mimi kama Mama nina shughuli nyingine ya Ushonaji, kupika katika hafla mbali mbali kama vile; harusi, sendoff party, kitchen party na warsha mbalimbali. Pia nina Garment ambayo tunashona nguo za aina zote zikiwemo shela, nguo za harusi pamoja na pazia za kisasa”
Kupata nyimbo za dada Emmy Lema wasiliana naye kwa simu namba 0713317145
Dar es salaam – Kanisa la World Alive, Sinza Mori
Mwanza – Mwanza pharmacy kona ya kuelekea Bugando Hospital
“Kamanda wa Yesu” Ilizinduliwa Arusha bila kiingilio
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili wa jijini Arusha, Samwel Nungwana, maarufu kama “Kamanda wa Yesu”, Jumapili iliyopita, Septemba 12 aliweka wakfu albamu yake ya pili iitwayo “Nasikia Kuitwa”. Tukio hilo lilifanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, kiingilio kilikua bure.
Habari za kuwekwa wakfu kwa album hiyo ziliratibiwa na Kampuni inayobobea katika habari na matukio ya Kikristo ya Living Media ya jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Jackson Malugu, tukio hilo lilienda sanjari na maombi kwa Mwenyezi Mungu ili awezeshe Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba 31, mwaka huu ufanyike kwa amani. Pia maombi hayo yalilenga kumlilia Mungu azipe utulivu nchi zote zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Malugu ameiambia blog ya Strictlygospel kuwa, mnenaji mkuu wa tukio hilo alikuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), dayosisi ya Mkoani-Arusha, Thomas Laiser. Aidha, amesema walikuwepo pia viongozi mbalimbali wa dini za Kikristo na Kiislam wakiwemo Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Simon Makundi, Mtume Dastun Maboya, Nasson Ngoy ngoy, ‘Father’ Mangwangi na wengine wengi.
Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera na Uratibu), Philip Marmo. Pia Walikuwepo viongozi wengine wa serikali , vyama vya siasa na asasi za kijamii.
Kamanda wa Yesu aliweka wakfu albamu yake ya kwanza iitwayo “Mgeukie Mungu Wako” Machi mwaka jana, na ilipokelewa vizuri na wapenda amani wote kwani ujumbe uliomo katika albamu hiyo unaiasa jamii kuondokana na maovu. Albamu ya “Nasikia Kuitwa” nayo inatarajiwa kukonga nyoyo za wengi kutokana na kusheheni ujumbe murua.
Kwaya mbalimbali pamoja na waimbaji binafsi walimsindikiza Kamanda wa Yesu katika tukio hilo. Kwa mujibu wa Malugu, watu waliohudhuria walienda na vitambaa vyeupe ili kuashiria amani.
–Na Norah Lema wa Living Media–
Upendo Nkone Kufunga Ndoa Tarehe 17 October 2010
Muimbaji wa Injili Upendo Nkone atategemea Kufunga ndoa tarehe 17 October 2010 na Mchungaji John Mbeyela ambaye pia ni mjane mwenye watoto watatu, ndoa hiyo itafungwa katika kanisa la Naioth kwa Mchungaji Mwasota.
Akiongea na Strictly Gospel Upendo Anasema “Ninafurahi sana na ninaomba Mungu akamfute machozi kila mjane, haijalishi umekaa miaka mingapi. Mungu yupo atakukumbuka”
Bi. Nkone ambaye ameishi maisha ya ujane kwa miaka 9, ana jumla ya album tatu ambazo ni Mungu Baba, Hapa Nilipo na Zipo faida.
Tunamtakia kila la heri katika maandalizi yote mpaka arusi!
Msaada Wangu – Marion Shako
Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya, Marion Shako ambaye pia anajulikana sana na wimbo wa AHADI ZAKE uliotokea kupendwa sana Afrika mashariki na kati.
Marion pia ni muigizaji na mwandishi wa nyimbo, nyimbo zake zimekua faraja na msaada kwa wengi, pia amekua akisema amepokea shuhuda nyingi ambazo zinamfanya azidi kumtafuta Mungu kwenye uimbaji wake, ili aweze kuimba nyimbo zenye Utukufu na unabii kwenye maisha ya watu.


























