SHUSHO AIBUKA NA TUZO KWA MARA NYINGINE,”LISEME” WA SARAH K, NAO WABEBA TUZO YA MWAKA.


Pastor Uche Agu muongozaji wa sherehe hizo akimuombea maisha marefu na yenye baraka mwimbaji Ruben Kigame.

Christina Shusho mwimbaji nyota wa muziki wa gospel Tanzania jioni ya tarehe 28 ameibuka tena kidedea kwenye tuzo za groove zinazotolewa kila mwaka nchini Kenya kupitia kipengele cha mwanamuziki bora wa mwaka kutoka Tanzania tuzo ambayo alishinda mwaka jana akiwapita waimbaji wenzake waliopendekezwa kwenye kipengele hicho akiwemo Rose Muhando,Bahati Bukuku,Neema Mwaipopo pamoja na Boniface Mwaitege.

Sherehe za utolewaji wa tuzo hizo ziliongozwa na pastor Uche Agu mwimbaji wa Joyous pamoja na mwanadada Kambua ambao walikuwa wakiweka utani wa hapa na pale na kuchangamsha mamia ya wakazi wa Kenya waliojazana katika ukumbi wa kanisa la Baptist jijini Nairobi.wimbo ”LISEME” wa mwanamama Sara Kiarie ama Sarah K umechukua tuzo ya wimbo bora wa kuabudu wa mwaka,huku mwanadada Emmy Kosgei akiondoka na tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na wimbo wake wa Ololo ukimpatia tuzo ya wimbo bora wa mwaka kwa upande wa eneo la Rift Valley.

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa injili nchini Kenya Ruben Kigame alipewa tuzo maalumu kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki wa gospel nchini humo. Mwimbaji huyo hakuwepo kwenye tuzo hizo kwakuwa yupo safarini nchini Marekani, ingawa tuzo yake alikabidhiwa kabla hajaondoka ambapo ilionyeshwa video fupi kutoka kwake akishukuru kwa tuzo hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasifu waandaaji kwa kuzifanya tuzo hizo kuwa bora. Pia alitoa ushuhuda wake mfupi wa maisha yake kabla hajaokoka na hata alipookoka,aliweka bayana kwamba baada ya mkewe kufariki alifikiria kwamba asingeweza kuimba tena lakini Mungu ni mkuu akafanikiwa kutoa album yake ya ”TULIA”.
Baada ya video hiyo pastor Uche aliwanyanyua watu na kuongoza sala fupi juu ya Ruben Kigame akimuombea maisha marefu na baraka.

Mwanadada Neema kulia akiimba na mwenzie wimbo Wema na fadhili wa Ruben Kigame maalumu kwa ajili ya mwimbaji huyo.

Lakini kama kuna tuzo ambayo ilishangaza na kutoa kama surprise si kwa waimbaji pekee bali hata kwa umati uliohudhuria,ni baada ya mwanakaka Ekko Dydda kuibuka mwimbaji bora wa kiume wa mwaka tuzo ambayo watu walio wengi walitegemea Juliani ndiye angeshinda kwani hata mshindi mwenyewe alikiri hilo wakati wa kushukuru.Kwakuwa tuzo hiyo ndiyo ilikuwa ikikamilisha tuzo hizo ikamaanisha kwamba Juliani licha ya kuwemo kwenye category tano hakupata hata moja na kuwaachia majonzi mashabiki wake ambao wameonyesha wazi kutokukubaliana na hilo.

Ekko Dydda akiimba wimbo wake Getto unaompa jina nchini humo.

Tuzo hizo ambazo zilikuwa zikirushwa moja kwa moja na kituo cha KTN pamoja na kwenye mtandao zimesifiwa kwa kuzidisha ubora kila mwaka huku kukiwa hakuna malalamiko ya upendeleo na kuonyesha mfano wa kuigwa kwa tuzo nyinginezo ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa zawadi,pia waimbaji wa nchi hiyo waliweza kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji.pastor Uche alihitimisha ngwe hiyo kwa wimbo wake My God is good.

ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA TUKIO HILO KAMA ZILIVYOTOLEWA NA WAANDAAJI WA TUKIO HILO GROOVE AWARDS 2012.TUTAKULETEA PICHA NYINGINE ZIKIPATIKANA.

Hapa wakati jukwaa likiwekwa sawa siku ya Alhamisi.
Mambo yakiwa sawia eneo la zuria jekundu (red carpet).


Umati wa watu ukiwa eneo la Red carpet kwa viburudisho wakisubiri kuingia ukumbini hii leo.
Jukwaa likiwa sawa na tukio likiendelea.
Mwanadada Kambua akimsifu Mungu.pia alijishindia tuzo ya mtunzi bora wa nyimbo wa mwaka.
Ekko Daydda mwimbaji bora wa kiume wa mwaka akiwa haamini huku waimbaji wenzake wakifurahi pamoja naye.


Kundi la MOG wakiwajibika jukwaani.
Juliani akimsifu Mungu jukwaani.
DK na Jimmy Gait wakicheza style ya furi furi dance ambayo imewapa tuzo.

Habari na Gospel Kitaa

Solomon Mukubwa azindua UTUKUFU KWA MUNGU

Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Christina Shusho wakiingia uwanjani

Katikati muimbaji kutoka Kenya, Emmy Kosgei na Rose Muhando wakiwa uwanjani

Solomon Mukubwa akiwapungia mashabiki

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akiangalia album ya UTUKUFU KWA MUNGU, Kushoto ni John Merere, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, Solomon Mukubwa, Askofu Gamanywa

Pamoja na umaridadi wa kucheza. Rebeka Malope amehaidi kununua nyumba Tanzania na kuhamia kabisa.

Ephrahim Sekeleti kutoka Zambia

Rose Muhando na Utamu wa Yesu

Tumaini John

Mh. Bernald Membe alipata muda wa kutosha kutoa salamu kwa maaskofu, Raisi na waziri Mkuu, na kuongelea msiba wa Kanumba, akawaomba watu wasimame dakika moja kuomba Mungu amlaze pahali pema peponi na Raisi wa Malawi.

TAMASHA LA PASAKA siku ya Jumapili limehudhuriwa na idadi kubwa ya watu, kuliko matamasha yaliyowahi kutokea hapo nyuma, waandaaji wa tamasha hilo MSAMA PROMOTION wamefanikiwa kuwaleta waimbaji wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo kufanya watu wapate mahali pa kwenda kufurahia sikukuu ya kufufuka Bwana Yesu Mwokozi!

Ilikuwa ni Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, ukumbi uliwaka furaha kumuona Rebecca Malope aliyeimba nyimbo zake huku akizunguka uwanjani, pia Rose Muhando na wimbo wake wa Utamu wa Yesu, John Lisu naye alikuwepo akiimba nyimbo zake Live, Ephrahim Sekeleti, Solomon Mukubwa na uzinduzi wa album yake KWA UTUKUFU WA MUNGU, Tumaini John, Mwalyambi kutoka Sumbawanga, Christina Shusho, Upendo Kilahiro na wengine ambapo walichelewa kuanza hivyo kupelekea waimbaji wengine kutopanda jukwaani.

Baada ya Tamasha hili nimewaza, pamoja na watu kuhudhuria kwa wingi, na waimbaji kuimba na kucheza kwa furaha lakini kuna haja ya kufikiria roho zinazotaka kuokoka, waandaaji wa matamasha ya Injili nchini, kuna haja ya kufikiria kuwaleta watu kwa Bwana Yesu!

 –Picha na John Bukuku

Reinhard Bonnke na Huduma ya Africa

Nigeria hivi karibuni!

Mwinjilisti wa kimataifa Reinhard Bonnke amejulikana kwa mikutano mikubwa anayoifanya Afrika. Ni mtoto wa mchungaji, alimpa Yesu maisha yake akiwa na miaka tisa (9) na Mungu alimuita kufanya kazi katika bara la Afrika tangu akiwa kijana mdogo na kuanza na mikutano yake maarufu kama “Fire Conference”

Katika mikutano yake ya Injili watu wengi wamekuwa wakimpa Yesu maisha yao,  Imekuwa ni furaha ndani ya moyo wake kuona watu waliopotea wakija kwa Kristo!

Katika miaka 35 tangu ameanza huduma yake ya kimataifa ijulikanayo kama Christ for all Nations (CfaN) ambayo ina ofisi Marekani, Kanada, Ujerumani, Uingereza, Nigeria, Afrika kusini, Singapore, Austraria na Hong Kong. Pamoja na kuhubiri Injili amekuwa akionesha filamu zenye changamoto kwa kanisa na Uinjilisti wa Roho Mtakatifu.

Bonnke ameweka historia kwenye kazi ya Mungu, Afrika haitamsahau na dunia haitamsahau kwa kazi amefanya, Mungu ambariki baba huyu kwa kukubali wito unaobadilisha maisha ya watu wengi, ni mume wa Anni, watoto wake ni Kai-Uwe, Gabrielle na Susie, pia ni babu wa wajukuu nane.

Malezi kwa Mkristo Mchanga

Kuna mkutano wa Injili ulifanyika katika kitongoji cha Ndala, mkoani  Tabora. Katika watu waliookoka alikuwepo pia kijana mmoja. Siku ya tatu baada ya kuokoka kwake, wakati mkutano huo bado unaendelea, alijiunga katika kucheza wakati wa mapambio ya kusifu.  Yeye alipoanza kucheza alikuwa anataka kucheza na mwanamke/msichana kama wafanyavyo kule disco: wawili wawili!

Wakati anaendelea kulazimisha msichana wa kucheza naye, kuna kiongozi mmoja wa kanisani alimuona kisha akamuita na kumwambia “Umecheza kiasi cha kutosha, hebu njoo huku nikuonyeshe kazi nyingine!”.  Kijana huyo alipewa kazi ya kupanga panga vitu sehemu ya kukaa mhubiri hadi kipindi cha sifa kikaisha.

Je, hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi yake ilikuwa sahihi? Kama ingekuwa ni wewe uliyemuona kijana huyo ungechukua hatua gani?

Mtume Danstun Maboya kufanya Mkutano Mkubwa!

Askofu Mkuu wa kanisa la Calvary Assemblies Of God Tanzania, Mtume Danstan Haule Maboya, anatarajia kufanya mkutano mkubwa wa Neno la Mungu katika Viwanja vya Biafra Jijini Dar es salaam tarehe 27 hadi 30 October 2011. Kuanzia saa 9 Alasiri mpaka 12 jioni. Watahudumu waimbaji mbalimbali wakiwemo Upendo Nkone, CAG Mass Choir pamoja na Rose Mhando.

Walete wagonjwa na wenye mahitaji  mbalimbali wataombewa na kuponywa kwa Jina la Yesu!

Matamasha wiki hii Jijini Dar es salaam!

Wiki hii imekua njema kwa wakazi wa Dar kukiwa na matamasha mengi sehemu mbalimbali, Swali ni kwamba inakuwaje kuna matamasha mengi hivyo kwa siku moja? Je hawafahamishani? nadhani kungekua na haja ya kupeana nafasi ili wengine wengi washiriki baraka za watumishi wa Mungu wanaohudumu!

Juu Pichani, John Lisu katika Tamasha la Yehovah Yu Hai, lililofanyika Diamond Jubilee

Kamera ya SG ilimpata Jackson Benty akiwa na familia yake baada ya Tamasha la John Lisu kumalizika!

Mwalimu Christopher Mwakasege ameanza semina Jumapili 4 hadi tarehe 11, Viwanja vya Biafra, Kinondoni (picha na Kilinyepesi)

Sarah K, pichani akiwasili Dar es salaam international airport kwa ajili ya huduma ya Jumapili, Landmark Hotel, iliyoandaliwa na Utakaso Fellowship ya jijini Dar es salaam! (Picha na Wapo Radio 98.0 Fm)