Kesha na Praise Power Radio, kila siku! – Erick Brighton

Kama wewe ni mpenzi wa Praise Power Radio. Erick sio jina geni masikioni kwako hasa usiku, na kila Jumamosi kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 10:00 Jioni kwenye Gospel Annointing.

Erick amekuwa ni mtangazaji mwenye bidii na kazi yake huku akionesha upendo kwa wasikilizaji wake wanaompigia simu wakati wa mkesha na kuomba nao pamoja.

Mbali na utangazaji ni mchoraji mzuri sana, na ni fundi wa kutengeneza transmeter na street Airway. Mara nyingi amekuwa akiwakumbusha wasikilizaji wake kuwa wakati wa kuokoka ni sasa kwa kuwa hatujui siku wala saa na kwamba mtu asitegemee kumuona Mungu kwa kusihi maisha yasiyompendeza.

Kanisa likumbuke kuombea Taifa la Israel – Robin Ulikaye

Kwa wakazi wa Mbeya,Rukwa, Songea, Iringa, Malawi, Zambia, Tabora, Iramba na Singida Jina la Robin Ulikaye sio geni masikioni mwao hasa kwa wale wapenzi wa Radio za Injili, ambapo Ulikaye anasikika siku za juma katika vipindi vya asubuhi na jioni pia Jumamosi mchana.

Ni Mtumishi wa Mungu na mtangazaji wa vipindi vya redio masafa ya 98.6 Ushindi Fm Radio iliyopo Mbeya, Tanzania!

    • Katika kuitangaza Injili miji hiyo na kuboresha vipindi vyake vya redio amekuwa mwenye mapenzi makubwa na nchi ya Israel na katika kipindi chake anachotangaza kila Jumamosi saa 12:00 Jioni, Anaielezea Israel na habari zake pamoja na mgogoro mashariki ya kati lakini pia vinahusiana vipi na unabii wa Biblia. Katika maelezo yake hayo mara nyingi anasisitiza kanisa kuliombea Taifa la Israel ili mapenzi ya Mungu yatimizwe sawasawa na Neno lake.

      Pia kanisa lisisahau kuombea Neema ya Wokovu kwa jamii ya wayahudi kwani pamoja na Neema kuanzia Kule bado jamii haijaijua kweli ya Wokovu unaopatikana katika Yesu Kristo Bwana Wetu.

      Mbali na Ijue Israel pia kaka Robin anafanya Praise and Worship Experience Kila siku za Juma saa 11 Jioni pia na Kurunzi la Matukio na Habari kila siku za Juma saa 3:00 Usiku.

Hongera Joseph na Adella!

Joseph na Adella Msami, tarehe 4 Septemba 2011 imekua siku ya kumbukumbu kwao kwa kufunga ndoa. Joseph Msami aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio ya kikristo WAPO radio 98.0 Fm, kwa sasa ni mtangazaji wa TBC 1 Taifa.

Pichani Martha Mwaipaja akiimba wimbo wake “Kwa msaada wa Mungu tutashinda ya dunia” ambapo Joseph Msami na mkewe Adella wakicheza!

………Tunawatakia kila la heri, kwa msaada wa Mungu, mkafanikiwe na kuzidishwa!…..

PATA PATA – Silas Mbise

Si Jina geni masikioni kwa wasikilizaji wa Redio za Injili Tanzania, Anaitwa Silas Mbise Mtangazaji wa WAPO Radio 98.oFM, Anatangaza  Kipindi cha Gospel Celebration ambapo anafanya mahojiano na waimbaji mbalimbali na kutangaza kazi zao.

Pia Kipindi cha PATA PATA ambacho ni maarufu kwa wakazi wa Dar es salaam kwa  kuhabarisha habari za matukio mbalimbali kila asubuhi. Mbise Anatangaza kila Jumatatu, alhamis na Jumamosi. Pia Ndiye anatangaza kipindi cha zilizotufikia na nyimbo mpya mpya zinazotoka.

Silas Mbise, kazi yako ni njema. Tunaamini Mungu Atazidi kutukuzwa kwa kupitia kazi yako!

Haujaanza wewe – Victor Haroun

victorh

David Robert, Victor Harun, Bahati Bukuku, Ado November na Ambwene Mwasongwe

Muimbaji wa Injili na mtangazaji wa Redio,Victor Haroun (wa pili kushoto) anatarajia kupeleka nyimbo zake sokoni mapema mwezi huu! Victor amesema nyimbo zake zitapatikana katika CD’s na jina la album yake ni HAUJAANZA WEWE, ambapo matayarisho ya video yake yako katika hatua ya mwisho na kukamilika July. Nyimbo zake ni za kufariji na kutia moyo.

Ikupa Ngao na Ana Nelson

ikuai

Watangazaji wa Televisheni ya TRENET jijini Dar-es-salaam, Ikupa Ngao anayetangaza kipindi cha TUTAFAKARI PAMOJA, FAMILIA TUZUNGUMZE na MATENDO MAKUU naye Ana Nelson Mwakasege hapo kabla alikua mtangazaji wa Praise Power Radio alikua akitangaza kipindi cha SOUL FOOD kwa sasa TRENET Tv, anatangaza kipindi cha SIFA.

Pia dada Ikupa anatangaza WAPO radio kila Jumamosi habari kutoka magazetini!

Watangazaji wa Radio za Injili!

Pichani ni watangazaji wa radio za injili jiji la Dar-es-salaam, kutoka kushoto ni Victor Haroun, Anthony Luvanda wote kutoka Praise Power Radio na Ritha Chuwalo kutoka WAPO radio. Watangazaji hawa mbali na kutangaza pia ni washerekeshaji maarufu.

Hivi karibuni kumekuwepo na minong’ono baina ya wapendwa kwamba sio wote wanaotangaza radio za Injili wanakwenda sawasawa na hayo wanayoyatangaza. (kuokoka)

Mnamkumbuka James Mwang’amba!

Litakuwa sio jina geni kwa waliokuwa wasikilizaji wa kipindi chake cha Praise and Worship kutoka katika studio za Praise Power Radio mnamo miaka ya 2005, alikuwa akikiendesha vyema kipindi hicho kwa uwezo wa Mungu, Kwa sasa ni mchungaji, pichani akiwa kanisani kwake Faith, kanisa lililoko Mwenge pia anatangaza WAPO fm, jijini Dar-es-salaam.

Promotion Time na Laura Boniventure

Ikiwa wewe ni mpenzi wa WAPO radio 98.0 fm, utakubaliana na ukweli kuhusu kipindi cha Promotion time kinachoongozwa na Laura Boniventure kila siku kuanzia saa tatu mpaka nne jumatatu mpaka ijumaa ni kizuri. Kinatangaza muziki wa Injili na kutambulisha waimbaji wapya. Bi. Laura ambaye pia ni mke wa Alex Msama au Mkurugenzi wa MSAMA Group anakiendesha vyema kipindi hicho. Songa mbele dada

Muisrael nambari one wa Arusha!

Dar yupo muisrael nambari wani kutoka WAPO radio Fm Elibariki Minja, pia yupo muisrael nambari wani mwingine kutoka jiji la Arusha, Studio za Radio ya Safina 92.6 Fm, Bw. Philemon Rupia au kwa jina lingine “FATHER” au muisraeli nambari wani, yeye hutangaza kipindi cha Israel Leo, mara nyingi katika kipindi hiki amekuwa akisisitiza ni vizuri kuliombea Taifa la Israel na kulifahamu kihistoria tu. Kuna umuhimu wa kuwafundisha watoto wetu pia hata kama una uwezo wa kuombea mambo mengine jaribu kuliombea na kulibariki Taifa la Israel. Mbali na Israel Leo anatangaza kipindi cha WANA WA ASAFU kinachohusu waimbaji na uimbaji. ATAKAYELIBARIKI TAIFA LA ISRAEL ATABARIKIWA NA ATAKAYELILAANI ATALAANIWA

Jovin Abel ndani ya Safina Radio Fm – Arusha

Mtangazaji maarufu aliyepata kuvuma ndani ya Studio za Praise Power Radio miaka miwili iliyopita Jovin Abel Msuya, kwa sasa anatangaza Safina Radio 92.6 Fm inayopatikana Kaloleni, Jijini Arusha, Abel anatangaza vipindi vya Yatokayo Makanisani, Njia ya Kijana, Safari ya Msafiri na Tuitembelee Biblia. Safina Radio ni kituo kikubwa kinachorusha matangazo ya Injili jijini Arusha kinamilikiwa na Dk. Danel Lema.

Tunahitaji mabadiliko! – George Mpela

gm2.jpg

George Mpela ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Gospel Fleva na Sifa moto kinachorushwa katika studio za Praise Power Radio Jijini Dar-es-salaam, mbali na kuwa mtangazaji pia ni producer wa vipindi mbalimbali vya radio, Mpela amekuwa akipenda kuwaasa vijana kupenda kubadilika nakuwa na msimamo wa maisha yao na sio kutaka kupata mafanikio kwa njia za mkato. Amewaasa vijana popote walipo wapende kufanya kazi na kutumia vipaji au karama ambazo Mungu amewapa kwa ajili ya kujiendeleza.