Mtume na Nabii Josephat Mwingira

mwingira.jpg

Huyu ndiye mwanzilishi wa huduma ya EFATHA, Mtume na nabii Josephat Mwingira wa jijini Dar-es-salaam.

Advertisements

150 thoughts on “Mtume na Nabii Josephat Mwingira

 1. Mtumishi Mungu akubariki sana kwa huduma yako nzuri iliyolenga kuwaleta watu kwa Yesu. Ila tu ningeomba urekebishe kidogo kwenye fundisho linalosema ndoto zote zinatoka kwa Mungu maana Bilblia imeweka wazi kuwa si zote hutoka kwa Mungu. Na sahihisho hili litaifanya huduma hii iliyoaminika kuendelea vizuri bila ya swali katika mafundisho yake. Evence G. Mfungameza kutoka Bukoba

 2. KATAKA KUSOMA MAANDIKO SIJAONA KABISA ALIYEKUWA MTUME NA NABII, KAMA ALIKUWA NABII NI NABII,NA KAMA ALIKUWA MTUME NI MTUME. SASA HAWA WA SASA MTU MMOJA HUYO HUYO MTUME NA NABII INAKUWAJE? NAOMBA KUELEWESHWA. JAMBO LA PILI HAWA MITUME NA MANABII WA SASA HAWAELEWANI WALA KUSHIRIKIANA WAO KWA WAO, NA KILA MMOJA ANA UFUNUO TOFAUTI NA MWINGINE, HIZI FUNUO WANAZIPATA WAPI? KWANI BWANA YESU KASEMA WOTE WAWE N A UMOJA KAMA YEYE ALIVYO NA BABA Yoh 17:20-22. NATAMANI SANA KUYAFAHAMU HAYA WAPENWA,

 3. Baba yangu wa kiroho Apostle Mwingira ntakupenda milele, kwa wenye macho wameona, wenye masikio wamesikia matendo makuu ya Bwana kupitia apostle Mwingira, Mungu hawezi kushuka yeye kama yeye ilia roho wake huja ndo maana amewatuma wajumbe wake. kwa wachanga wa kiroho ndio wana mabishano kwa kua hawajui wanachobisha wanafuata mkumbo tu. penda kumja Yesu na sio kuwa jaji watumishi wa Mungu utabeba dhambi bure. na ndo mana kipindi cha wana wa israel alikuwepo Musa kama wana wa israeli wangeweza kumwendea Mungu direct si wangeenda kwanini Mungu alimchagu Musa kuwa kiongozi wao? ukijua hilo haina haja ya kubishana au kuwa jaji watumishi wa Mungu. Hata hivyo walio wengi wanamzungumzia Mwingira Hawajui kazi anayoifanya kwa undani zaidi.Mwingira ni mkalimani wangu na ntampenda milele ndo kwanza mvomsema vibaya mnaongeza kumpenda zaidi.
  lov uuuuuuuu dady mwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

 4. Mimi nina wasiwasi sana huyo jamaa yenu mnayemwita mtume na nabii Mwingira!! Huwa namwangalia sana kwenye huduma zake kupitia TV yake. Mambo mengi anayoyafanya huwa ni UNBIBLICAL!! Siku nikipata fursa, nitaeleza haya halafu watu wajaribu kuyaangalia kwa jicho pevu kama kweli yanalingana na BIBLIa. Bwana awabariki sana.

 5. What a blessing to have a Father and a leader who knows where he is going.I Love you My Dad.May the LORD GOD who lives up high in Heaven bless u abundantly and exceedingly your my mental

 6. I accept Apostal Josephat Mwingira as a real Prophet through his Prophetic words when he Prophesize it hapens Amen!

 7. we , member christians of Efatha Ministry, Rwanda love our leader and founder Josephat Elias Mwingira and our mother Eliakunda Mwingira. May God bless you. Welcome to Rwanda

 8. mimi, mke wangu ,watoto wangu na kituo/kanisa la KIGALi, baado tuna mpenda mtume na nabii Josephat E. MWINGIRA na familia yake na Juduma yake na baado tuna mtambua kiongozi wetu . Tunamkaribisha Rwanda atembereye kanisa lake. Mungu ambariki.

 9. Nina wasiwasi kuwa kuna idadi kubwa ya wakristo wanamkiri tu Yesu lakini hawamwamini!!!!

 10. rey, mstari mmoja wa maombi unatosha maana Mungu ni yule yule! kwa hiyo kama umejiwakilisha kwa maombi kwa ‘your father Mwingila’, ukiwapo hapo kusubiri tohara, mimi nadhani inatosha, kuliko kuleta tena maombi SG! Kusimama kwenye zaidi ya mstari mmoja wa maombi, ni dalili ya kutokuamini, yaani ukizigeuza huduma kama uganga wa kienyeji! Amini tu kuwa Mungu alikusikia katika siku yako ya kwanza ulipomuomba na ukae usubiri jibu, hata likikukuta umo kaburini, basi hilo ndilo jibu stahili kwa jambo uliloliomba; maana waweza kubadili waombeaji kama soksi na isikusaidie kitu, Mungu hufikiwa kwa Imani tu!!

 11. baba mwingila mimi penda sana wewe najua siku roho atasema ki2 juu yangu nakuamina mbaka unipake mafuta au nifanyiwe tohara bila ivyo efatha siiachi chezea yesu anafanya naajua atafanya makubwa kwangu kupitia mwingila ndo maandalio yangu jawabu kwa mnazalet

  mwingila is my father jesus is mesiya devol kafuli

 12. nimesoma maelezo ya orbi nikaelewa ni mtu wa aina gani. kwa kifupi angalia sana unayoongea yasije yakakurudia maana nimeona wengi wakifikwa na hayo. usiwe na kiburi cha uzima. ni usiku nitakupa maelezo yanayokufaa siku nyingine nikiona uko sawa

 13. Sasa Mtume kaja na Tohara ya moyo………waumini wake inabidi wafanyiwe tohara hii……….kweli iko kazi…

 14. Habari Ndugu Daniel Seni,

  tambua kwamba kuna karama na huduma

  kuna karama 9 unabii ukiwemo ndani na kuna huduma tano nabii akiwemo ndani

  mkristo yeyote aweza kutoa unabii kama karama lakini watu wachache wanaweza kutembea

  katika huduma ama office ya nabii. NAOMBA USICHANGANYE MAMBO

 15. najivunia kua na mtume na nabii katika nchi yangu ya Tanzania ambaye ananipa ujasli na kujiamini pale napokua nimesongwa na matatizo mawazo kila ninapo msikiliza mtume na nabii josephat mwingila najikuta ndo nazariwa leo wala sina tatizo lolote Mungu wa efatha akuinue zaidi na kukupa nguvu za kusonga mbele siku zote usirudi nyuma tupo pamoja kwa umoja BABA NAKUPENDA SANAAAAAAAAAAAAA…..KAMA UNAVYOSEMAGA SAMA YEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE….NAMI NA SEMA YEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEESU…HALELUYA
  !!

 16. Mungu akubariki Mtumishi na azidi kukuinua kwa kazi unayoifanya, hakika nimeiona kazi ya Mungu kupitia kwako Mtumishi, natiwa moyo kila ninapoona miujiza inayotendeka Efatha na sasahivi ninaiona kupitia TRENET na nimemshangaa sana Mungu jinsi hao wamama wavyopata unguchu na kwenda kujifungua. Mungu azidi kukuinua na kukutia nguvu katika huduma yako pia nasi tuombee tulioko mikoani ili nasi tupate kupokea miujiza kupitia kwako Mtumishi wa Mungu, Mungu akubariki.

 17. baba mwingila mimi kanza nipo tayari unifundishe unipake mafuta nami nikatumike dunia itanichelewesha kwenye kongamano uliita wenye elim ya juu niliumia sana ila najua Mungu atakwambia napenda kuwa mwanao maandalio ni yangu jawabu kwa Bwana mi nakupenda Yesu alisha kuchagua utusaidie amina

 18. Mungu azidi kumbariki Baba yetu wa Kiriho Mtume na Nabii Josephat Mwingira na Mama Eliakunda.. Amen..

 19. Ndg Pius na Gabriel,
  Shalom!
  Naomba mnisaidie, Niliwahi kumuona mtumishi apostle Mwingira, akimbatiza mama wa kimasai ktk mkutano wake huko kibaha kwa “kumwagia ndoo ya maji” na kulowesha chapwa chapwa!!!
  Je, jambo hili ni la ki Maandiko??

  Mbarikiwe!

 20. TUNAKUSHUKURU KWA HUDUMA YAKO MTUMISHI.ENDELEA KUTULISHA CHAKULA CHA ROHO.TUNAKUTAMANI SANA UFIKE BUKOBA TUKUONE

 21. Ubarikiwe kaka John Paul,

  Mungu atusaidie, kutafuta kumjua sana Yeye na kutafuta kufanana na Yesu. Tujifunze kuwaombea watumishi zaidi na si kukazana kuwasifia au kuwaponda……

  Tuwaheshimu watumishi lakini tusiache kuwaombea nguvu na hekima ya Roho Mtakatifu iwaongoze siku zote wakaseme na kutenda sawa na mapenzi ya Mungu na wakawe wanyenyekevu kadiri wanavyoinuliwa. Penye mafanikio ni rahisi sana roho ya kiburi na kujitwalia utukufu kupata nafasi.
  Yakobo 4;16
  ‘‘Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema

  Mungu awabariki sana watumishi wake na azidi kuwalinda. Akaachilie rehema na msamaha wake hata pale wanapoteleza.

  Mbarikiwe sana

 22. Binafsi nabarikiwa na mafundisho mbali mbali ya mtume na nabii wake E.Mwingira, wakati mwingine pia namshangaa Roho Mtakatifu huwa ananisukuma kwa jinsi ya ajabu ili nimwombee mtumishi huyu nami napenda kuwa mtii kwa Roho wa Mungu, mimi siabudu kanisani kwake ila nafanya kile Roho anachoniongoza. Mungu Mbariki mtumishi huyu bariki kila mipango anayoifanya ili asitoke nje ya mstali wako, pia tumkumbuke katika maombi yetu binafsi sio huyu tu na watumishi wengine wanaomtumikia Mungu wetu wa kweli. Na wale waomtumikia Mungu kwa udanganyifu huduma zao zidumae. Mungu wangu AWABARIKI NYOOTE

 23. siku zote mti wenye matunda ndio unapigwa mawe, baba hata wakupake matope kuanzia juu hadi kwenye unyayo we songa mbele EFATHA sisi ni jeshi la BWANA hatuna mashaka coz tunajua wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaenda. BE BLESSED WAKUNYUMBA!

 24. WOW!,napenda sana kukupongeza kwa kazi kubwa unyoifanya.Yesu akubariki! unatetea watanzania.
  Ujumbe:usijali kwa criticism,unazopata.Yesu na akupiganie milele.usife moyo.ziba masikio,kaza mwendo katika wokovu.Vumilia mtumishi,your ministry is a big blessing to us.Keep up! never be down.akina Yuda wengi sana ila.mwangalie Yesu tu..uu..u..!
  From:Precious.

 25. Hatari iliyopo katika makanisa, hasa haya ambayo hayajawa Taasisi, bali yanaongozwa chini ya MAELEKEZO ya Mwanzilishi wake ni ile hali ya KUMWAMINI Zaidi mtumishi na kumuona kuwa yeye ndiye mlango wa wengine kuingia mbinguni. Yaani kuna watu wanakuwa wakimuona kuwa bila yeye WAO SI KITU! Huko ni kudanganyika. Mungu anamtambua mtu mmoja mmoja. Hakuna KK, yaani “Kupitia kwa…”. Hakuna!!

  Kuna wimbo maarufu unaosema “Kila mtu atauchukua…mzigo wake mwenyewe. Na kila mtu atatoa….hesabu yake mwenyewe…..Mbele za Mungu….Siku hiyo inakujaa”

  Maneno ya wimbo huo ni machache lakini ni HALISI. Ye yote anayeitwa MTU au Binadamu, atatoa hesabu yake mwenyewe. Mungu hana upendeleo. Mungu haangalii cheo, makanisa gani ulianzisha, una wafuasi kiasi gani nk. Yeye ni wa HAKI.

  Sasa kwa suala la watumishi, najua kila mmoja kuna mahali anaposhiriki kama sehemu ya kanisa husika. Na hapo alipo ndipo anaamini kuwa ni sahihi kutokana na upeo wake wa kulifahamu Neno la Mungu na pia ushuhuda wake juu ya kukutana kibinafsi na Yesu Kristo. Lakini ninanaloshauri mimi ni kuwa, SI vibaya kuwaamini watumishi hawa na kuwafuata wanavyofanya. LAKINI tusiwaamini KUPITA KIASI na kuwaona wao ni KAMA MUNGU. Hapana! Maana kuna wakati Mungu akiona TUNAWAHESHIMU zaidi YAKE, na yeye ni Mungu mwenye Wivu, anaweza kuruhusu SHIDA katika Kanisa husika, juu ya mtumishi huyo ili KURUDISHA MAWAZO YA WATU Kuwa huyo wanayemuona kama MUNGU naye ni Binadamau tu, hivyo anaweza kukosea. Hiyo inaweza kuwa na lengo la kumyenyekeza mtumishi husika ili ASIJIINUE kupita kiasi WALA WATU WASIMWAMINI MNO na KUANZA KUMUABUDU na wakamsahau Mungu!!!

  Linapokuja la mabishano ya NANI ZAIDI kati ya Mtumishi na Mungu basi Mungu HULAZIMIKA KUJITAMBULISHA KUWA YEYE NDIYE ZAIDI!!! Na anaweza kulifanya kwa namna anayoona mwenyewe kuwa Itafaa!!

  Kwa hiyo, katika yote, Twatakiwa kuwa watu wa rohoni, tukitathmini katika, mtazamo wa rohoni na wa msisimko tu wa Kimwili!

  Tuzidi kuomba neema ya Mungu kwa watumishi wote, kwa ujumla wao! Yale yanayonenwa juu yao, na ya kweli, Mungu awasaidie moyo wa unyenyekevu watubu na kubadilika na yale yasiyo ya kweli, basi hayo yatapotea mara!!!

  Jina la Bwana Mungu na Litukuzwe!

 26. Ndugu Baraka,

  Ni wapi Mtume Mwingira alipotukanwa? Kwa mtazamo wa mawazo kama hayo mnakosa kuwa msaada kwa Ephata na mwili wa Kristo kwa ujumla……! Biblia iko wazi muumini aliyekosa hurejeshwa kwa upendo…..!Na Dhambi yoyote dawa yake ni toba tu…..! Sio kujaribu kuikwepa na kuitolea sababu mbali mbali….!

  Na labda kwa kukusaidia tu….kama unataka kuonana na mimi omba anwani yangu Strictly Gospel watawasiliana na mimi ili kukupatia…..wala usisite

  Tuzidi kuombea Kanisa la Tanzania kwa ujumla…..na kipindi kigumu wanachopita wana Ephata.

  Ubarikiwe.

 27. Shalom wapendwa
  ni kweli tuzidi kuomba, hasa Roho wa Mungu atembee ktkt yetu. Afungue macho na masikio yetu ya rohoni, asante ndg Orbi kwa neno nitalipitia, zidi kuomba kwa ajili ya kanisa Mungu anasikia
  Kwako ndg Baraka kamwe sintakaa kimya kama namuona mtu anapotea au anapotezwa
  huko ndio kusimama kwa zamu, mtatuita maadui, mtatupiga mawe lakini neno litasimama mambo yote yatapita lakini neno litasimama na hicho pekee ndicho kigezo cha ukristo. Mtume Petro alipokemewa na Paulo kuhusu unafiki wa kujitenga na wakristo wasio wayahudi wakati Mungu alimwonyesha wazi ktk ndoto kuwa kwake hakuna aliye haramu ambaye amemtakasa hakuwa anamuhukumu, hakuwa anamtukana bali alimwambia wazi ili atubu na kanisa lisonge mbele leo hii sijui kama angeishia wapi bila ya kushituliwa kuwa huo ni unafiki na woga wa kuogopa kutengwa na wayahudi.
  Sisi ni mwili wa Kristo tunapaswa kuombeana, tunapaswa pia kuonyana ili kanisa lisonge mbele, najua inaumiza lakini ni lazima ili kulinusuru kanisa
  tuzidi sana kuombeana na kuliombea kanisa, barikiweni

 28. wapendwa katika kristo, tunatakiwa kusoma alama za nyakati, siku hizi idadi za madhehebu ya kikristu yanakaribia kuzidi idadi za watu,makanisa mengi yamekuwa yakifunguliwa kwa sababu binafsi na ukiangalia usipokuwa makini utajikuta ukiabudu kanisa, mtume, nabii, askofu, kuhani n.k kuliko kumuabudu MUNGU WA KWELI NA YESU KRISTO na utajikuta unahama na kubadili madhehebu kwa kutafuta miujiza n.k.
  Ukiwa ni mkristo unayemwamini YESU KRISTO mlilie MUNGU kwa sala, kuwa na amani na furaha moyoni, fanya matendo matakatifu…soma biblia kila siku, hakika utapata SULUHISHO. kwa upeo wangu nazani ndio maana hata katika biblia hakuna sehemu ilipotajwa kuwa kanisa furani ndio njia, au la Yesu. nazani makanisa yapo hapa duniani tu, tena yameandikwa kwenye nyaraka za serikali tu!

  kwa maoni yangu nazani kila mtu ashike imani yake, kwa kusoma neno la Mungu na kumuomba Roho mtakatifu amfundishe zaidi na kumuongoza kuishi na kushinda dhambi mambo ya yanayolikumba kanisa la leo.

  tujiangalie tujihadhari tusikumbwe na mhubiri, nabii au kitabu kingine kinachopotosha; pia kutokuwa wepesi wa kurukia ukweli mdogo au mitindo ya kisasa ya uhubiriji injili. tuchunguze kwa makini mambo yanayojitokeza hivi sasa katika miambali; sali na mwombe Mungu na roho wake ili upate mwanga….katika hili usifanye haraka kuamua, bali uwe mtulivu, fikiri na tafakari ukiona magumu omba ushauri, jadiliana na wenzako wanaotafuta ukweli kwa uaminifu.

  kusema tu kwamba nimeokoka na naabudu kwenye kanisa la mtume,nabii, kuhani nk halafu ukabweteka ni mbaya sana kwani waweza kuwa msukule wa huyo nabii/kuhani wa unayemwamini eti kupitia yeye umemuona Mungu na Roho wake… jamani siku hizi hawa watumishi wanaozuka wanatumia nguvu za giza kuvuta waamini na kujipatia kipato… ukitaka kupima wengi huhubiri kuhusu kutoa sana, kupanda mbegu na kuwa watii wa makuhani/ nabii; cha ajabu yule anayetoa sana ndio huonekana mfuasi safi na wakati mwingine hupewa nafasi nyeti katika uongozi wa kanisa, bila kujali tabia yake na chanzo cha mapato…

  sasa naomba niwashirikishe ndugu zangu sifa 10 za nabii wa kweli na sifa kumi za nabii wa uongo

  NABII WA KWELI

  1. HADAI CHOCHOTE TOKA KWA WENZAKE(yohana 5,41)

  2.ANALETA MABADILIKO AKIWA KATIKA KANISA ( yoh: 10,16; 17,21)

  3.ANATAFSIRI NA KUELEWA MAANDIKO MATAKATIFU KATIKA MWANGA WA MAPOKEO YA KANISA ( mt.18,18; lk 10,16)

  4. ANAWAPENDA NA KUWAHESHIMU WATU WA DINI NA MADHEHEBU MENGINE (lk 10.29 -37)

  5. ANATAFUTA WONGOFU WA ROHO ZA WATU (MK. 1.15)

  6. YEYE NI MNYENYEKEVU NA HAANGALII UBINAFSI WAKE (wafil. 2.3 – 4)

  7. ANAMHUBIRI KRISTU MFUFUKA ( I Kor 1:22 – 24; mk8.34)

  8. ANAOMBA NEEMA YA mUNGU NA hURUMA YAKE ( mt. 6:7-13)

  9.ANAWASAIDIA WATU WATAFUTE NA WATRENDE MAPENZI YA MUNGU ( mk. 3:35)

  10. ANAFUNDISHA NA ANATENDA NA KUSHIKA AMRI ZA MUNGU ( Yoh:14.15; 15:10)

  NABII WA UONGO

  1. ANATAFUTA MALI NA HESHIMA (2 PetrO 2:1-3; I KOR 1: 10 -12)

  2. ANAANZISHA KIKUNDI CHAKE AU DHEHEBU LAKE NJE YA KANISA
  .
  3. ANATUMIA HERUFI ZA MAANDIKO MATAKATIFU KWA KUZUSHA MAWAZO YAKE NA NDOTO ZAKE (2 pETRO 2:1)

  4. ANAWADHARAU NA KUWACHAMBA WOTE WASIO WA KUNDI NA MADHEHEBU YAKE NA KUWAONA NI WENYE DHAMBI (LK. 18: 9 – 14)

  5. ANAPENDA KUWASISIMUA WATU KWA MAMBO YA YA NJE YANAYOVUTIA MACHONI ( Mt. 7:21)

  6. HUPENDA KUJIONYESHA NA KUJITUTUMUA (YOH. 7:18)

  7. ANAJISHUGHULIKA NA MIUJIZA NA MAMBO YA AJABU AJABU ( 7: 22 – 23)

  8. ASALI ILI APATE UTAJIRI, HESHIMA, UMATI WA WATU NA KUFAULU KIDUNIA (Lk 6: 22 – 23)

  9. ANATOA UNABII KWA KUTAJA TAREHE ZA MWISHO WA ULIMWENGU KINYUME CHA INJILI ( MT. 24:36)

  10. ANAFUNDISHA IMANI ISIYO NA MAADILI YA KIKRISTU NA UTU ( YAK. 2: 18 – 22)

  wapendwa wokovu unataka kazi, uvumilivu na unyenyekevu katika imani na umoja wa MUNGU, si miujiza kutoka kwa kila anayejiita mtume na nabii kwani hata SHETANI hufanya miujiza angalia MAT. 7:21 -23; 24,24. sina ubishi kuwa nabii ni mjumbe wa MUNGU, na ni yule anayezungumza badala ya MUNGU, anatahadharisha ubaya na uovu uliopo, anaona mbele, anakleta matumaini kwa wenye kuacha uovu, anatahadhalisha juu ya adhabu kali kwa wale wagumu wa mioyo

 29. Jamani, jamani hata watiwa mafuta wanafanya haya nabado mnaendelea kuwahamini kwamba wametiwa mafuta? Kuweni makini nyie watu

 30. Dada yangu Rosemary,

  Kila napoliangalia kanisa la Tanzania na mambo yanayotendeka mimbarini unaomba rehema ya Mungu itutembelee upya…….Kanisa linatoa picha kamili ya jamii ya Tanzania leo…….tutakemeaje ufisadi wakati ufisadi umeweka makao mimbarini? Tutakemeaje uroho wa mali na madaraka wakati hayo yote yamejikita mimbarini? Utakemeaje Unafiki katika siasa….wakati unafiki unaanzia mimbarini na kutambaa kuwagusa mashemashi….hadi waamini…… Uoga wa kusimama katika Kweli ya aina yoyote ile….iwe ya Mungu au yoyote ile umekuwa sehemu ya Waumini…. na yale yanayowasukuma watu wasiomjua Mungu kutafuta mali na utajiri….na sisi ndio yanayotukimbiza mbio mbio…..kwa kivuli cha baraka! Na Mitume na Manabii wamegundua siri hiii….na sasa wanahubiri kile watu wanachotaka kukisikia! Chukua baraka yako…..! Chukua muujiza wako…..! Hakuna tena ujumbe wa utakatifu….! Hakuna tena kuhusu hukumu ijayo…wala kuna siku tutakutana na MUNGU ALIYE HAI KWA HUKUMU……..haya yamekuwa mafundisho manyonge!

  Imani ya Kristo imekuwa ni mtaji wa kujipatia mali na utajiri……..waumini wanahama toka kanisa moja hadi jingine……toka kwa Nabii huyu kwenda yule……toka kwa Mtume nadhani muda si mrefu…..tutasikia huduma ya Makuhani…..!Kisa wanatafuta chakula cha kiroho…….bila kujua chakula cha kiroho kiko katika maneno ya Mungu ambayo hawataka kuyapa nafasi kila siku katika maisha yao…..! Biblia zinangoja tafsri ya mtume na nabii………Kila siku kuna jipa toka mimbarini….mara wenye Biblia zenye jalada yenye rangi nyeusi wanazuia baraka…….na ili tupate baraka lazima wenye BIBLIA nyeusi wavue “magamba” ya Biblia hizo ili upenyo wa baraka ushuke….. Mara hakuna neno “Biblia” ndani ya maneno ya MUNGU….neno Biblia lilitoka kuzimu…..!

  Lakini dada Rose hakuna jipya chini ya jua……Petro aliisha tuonya haya……” LAKINI KULIONDOKEA MANABII WA UONGO KATI YA WATU KAMA VILE KWENU KUTAKAVYOKUWEPO….WAALIMU WA UONGO WATAKAOINGIZA UZUSHI WA KUPOTEZA…….NA KWA HAO NJIA YA KWELI ITATUKANWA……..NA KATIKA KUTAMANI WATAJIPATIA FAIDA KWENU KWA MANENO YALIYOTUNGWA (2 Peter 2:1-3)

  Lakini dadangu unapojaribu kukaa na waumini na kuwaomba angalau watafakari kidogo basi yanayotoka midomoni mwa manabii….mitume….na waalimu kama mafundisho hayo ni sambamba na maneno ya Mungu….unatafuta kupigwa mawe…! Maadamu miujiza inatendeka….maadamu watu “wanafunguliwa” hata kama wanafungwa katika ufahamu wa kiroho hiyo haijalishi! Sauti ya Nabii….Mtume…imegeuka na kuwa sauti ya Mungu….! Hapo ndipo panaponiumiza mno ukiliangalia kanisa la Leo……..

  Mungu akubariki….ukipata nafasi soma 2 Peter:2 (sura yote ya pili)

  Tuzidi kuliombea kanisa la Tanzania…….

 31. Shalom wapendwa
  kutokana na haya yanayotokea na mengine mengi tu tunayoyaona kila kukicha kwa hawa watumishi hasa wanaojiita manabii, tunapaswa kumuomba sana Mungu kwa ajili ya kanisa.
  Kuna mada moja nilichangia hapa nikasema hiki sio cheo kwa maana kuwa daily mtu anatoa unabii enzi hizo ziliishapita!…. matokeo yake kwa sababu ni kitu wamejivika wenyewe ni kutokuwa na uongozi wa Roho mt, au kwa maana nyingine wameisha mhuzunisha na amewaacha, hii ni mbaya sana kwa kiongozi wa huduma kutotii uongozi wa Roho mt….unakuwa kipofu huna dira na wala hutaweza kuzisoma nyakati….
  Kama mkristo nimesikitishwa sana kuanikwa kwa kesi hii tena kati ya waumini kwa waumini, na kibaya zaidi ni kuwa ushahidi wa mshirika wa uzinzi huo na mke wa mtumishi kukiri kuwa ni kweli wakati mtumishi akikataa kutubu,…..
  Kwa hali hii asemayo kaka Orbi ni sawa kabisa, kwani nini hatima ya mtu anayefanya shingo yake ngumu? badala ya kuendelea kutishwa na nabii nyingine za uwongo nadhani tunapaswa kumsihi Mungu atakase kanisa lake tukianzia na wenzetu mlio chini ya huduma hii, sio muda wa kujibishana na kupinga hebu turudi ktk neno na tutubu kwa ajili yetu, kanisa na taifa kwa ujumla. Pili tusibweteke kwa kuamini kila roho tuzichunguze na tuombe sana Mungu atupe macho ya rohoni tuweze kutambua yaliyo mapenzi yake.
  Tusimame ktk zamu kila mmoja wetu tuombe kwa ajili ya watumishi wetu, hakika jambo kama hili ni aibu na alama ya kushindwa kama kanisa na ni kikwazo kikubwa kwa wasiomjua Mungu wa kweli kuokoka. Kanisa tuamke kila mtu ktk zamu yake! Mbarikiwe sana na nawapenda wote

 32. Ndugu yangu Gaston,

  Niliandika awali nikiwa na haraka……..Kama Kanisa la Prophet Mwingira lingekuwa hai kiroho, siku nyingi Mtume angelikuwa amekalishwa kitu cha nyuma hadi tuhuma zimalizike mahakamani rasmi…….kwani fununu ya tuhuma hizo hazikuanza siku zilipoandikwa magazetini…..!Huu Ndio utaratibu katika makanisa mengi yenye msimamo wa utakatifu…..Huwezi kuhudumu ukiwa ndani ya tuhuma……! Na hata kama kanisa lisingemketisha bench….yeye mwenyewe kama angelikuwa na dhamira iliyo hai angelikaa kando kuhudumu ili kanisa lisinajisike kwa tuhuma.

  Lakini makanisa mengi leo Utakatifu sio kitu….kitu “Power” ………..Wokovu sio kitu…….Kitu ni “power” Na kwa wengine maadam pepo na purukushani nyingi za miujiza zipo hiyo ni dalili tosha Mungu yu pamoja nasi! Hakika huyu si Mungu wa Biblia ambaye wito wa msingi aliotuitia ni wautakatifu!

  Narudia tena njia ya Toba na msamaha iko wazi kwa kila mtu hata kwa Mtume na Nabii…….na dhambi haiwezi kuweka uvunguni….kuna siku itatokeza hadharani hii ni kanuni isiyokimbilika ………Hivyo wana Ephata tumieni wakati huu kumsaidia Mtume kwa kumlilia Mwenyezi Mungu….wengi hatupendi kuona huduma hii ikiporomoka….na Wakristo wakiumbuana Mahakamani ni aibu katika mwili wa Kristo…..Paulo katukataza kufanya hivyo………tunaamini kabisa Ephana kuna baadhi ya watu waliokuwa wakimtafuta Bwana katika Roho na kweli ….itakuwa ni uchungu wakipotea…..!

 33. Ndugu Gaston,

  Sasa ni busara kutamka yapi? Dhambi ikitendwa inabidi itubiwe…..iwe nimefanya mimi au wewe au Mwingira au mtumishi mwingine yoyote yule….Je kuna kigezo tofauti kati yangu au wewe na Mwingira mbele za Mungu….? Nikituhumiwa kwa uzinzi……au kudhulumu mali ya mtu au hata kuichukua kiulaghai kwa kumtumia Mungu……kama ikibainika ni kweli sina jinsi….ni toba tu….maana Mungu hadhihakiwi….au kuna dawa nyingine ya dhambi licha ya toba? Tueleze ndugu yangu Gaston kama ipo…..

  UBARIKIWE

 34. orb and rosemary,
  sipingani nanyi bali nimeogopeshwa na kauli ya orb kuwa bila ya mwingira kuomba msamaha wa dhati kwa Mungu na kwa waumini huo ndo utakua mwanzo wa huduma hiyo kufa…. na ukaendelea kuwa mungu hadhihakiwi……………………
  Kwa upande wangu sidhani ni busara kutamka hayo jua kuwa hata wewe ni mtumishi wa Mungu na Mungu anakupenda. ISAYA 42:18-

 35. Shalom nakubaliana kabisa na ndg Orbi,
  hawa manabii waache kujiinua mno nasi tuache kuwatukuza, matokeo yake hata kushuka ktk matukio kama haya na ushahidi wote bado inakuwa ngumu.
  kweli tunapaswa kuombea na kuliombea sana kanisa
  barikiweni

 36. Ndugu Gaston,

  Kama wafuasi wa Nabii na Mtume Mwingira watatambua kuwa Mtume na Nabii wao ni kama binadamu wengine walioitwa na Mungu tu hiyo itakuwa vyema…..Lakini kama baadhi yao wanavyooandika na kuonyesha kuwa ni yeye amelibeba Kanisa La Tanzania mabegani mwake….na ndiye aliyeinuliwa katika majira haya….sidhani wanaweza kuamini kuwa yeye ni kama binadamu wengine tu walioitwa na Mungu kumtumikia kama wewe usemavyo………hivyo anaweza kuanguka katika dhambi iwe ya tamaa ya mali au uzinzi kama waumini wengine tu asipochukua tahadhari…..!

  Kwa watu kama mimi licha ya kumuombea Mtume Mwingira kupita salama katika haya yanayomkabili, lakini naamini itampa muda wa yeye kutulia, kutafakari na kuungalia wito wake upya na kujifunza! Labda kwa watu kama Mtume Mwingira mafundisho ambayo wanaweza kuyaelewa ni kama haya yanayokuja kwa njia ya matukio……..Na labda tuhuma hizi zinazomkabili zitampa nafasi ya Kunyenyekea mbele ya Mungu na mbele ya waumini anaowaongoza na kuomba msamaha na kufanya toba halisi kuwa yeye ni binadamu anaweza kumkosea Mungu…kama waumini wengine wanapojikwaa njiani wanapotembea katika njia hii……Naamini kabisa akifanya hivi si kwamba ataponya maisha yake kiroho….bali ataponya huduma yake…..na ataponya roho nyingi za waumini ambazo zimeumizwa na kujeruhiwa……naamini ni kwa njia hii tu Mwingira anaweza kusonga mbele…….naogopa kusema kwamba kinyume cha hapa ndio mwanzo wa kuanguka kwa huduma hii…kwani Mungu hadhihakiwi…na kila kosa hupata ujira wa haki.

  Naamini pia itakuwa somo kwa wengi kuwa hakuna binadamu anayeweza kuchukua nafasi ya Kristo! Imani yetu LAZIMA ijengwe kwa Kristo tu sio mtume wala na nabii…..si ukubwa wa huduma….na wala si miujiza….! Si wingi wa watu….wala “mafanikio” ya huduma…! Somo ambalo naona ni gumu mno kwa waumini wa leo……!

  Mungu na Atubariki.

 37. Ninachojua mimi na kuamini ni kwamba mtume na nabii J.E. Mwingira ni mwanadamu kama wanadamu wengine, na katika utumishi wake amekumbana na mambo mengi ya kutisha kuliko hili linaloendelea magazetini.
  Ushauri wangu kwa watu wote wanaomjua kristo ni kumuombea mtumishi huyu ili Mungu amtie nguvu na ampe busara katika kupambana na suala hili ili asiende kimwili bali amsikilize roho anachomuelekeza.
  Binafsi sina shaka na utumishi wake namuombea Mungu apite salama katika suala hili.

 38. Nimerudi ndani ya Blog na kuikuta nukuu yangu ya August 11/2010

  “Kwa watu wanaomjua Mungu,wanafahamu wazi kuwa hata mtu atumiwe na Mungu kiasi gani, anabakia kuwa binadamu!hawabadiliki hali ya kuwa kati Binadamu na Malaika, au kati ya Malaika na Mungu!Tumeona kwa Musa, Daudi,Suleimani na pia Tumeona kwa Petro maana hata akiwa ni Mtume ayejazwa na Roho Mtakatifu, bado Paulo alimkemea alipoenda kinyume cha Injili! Na hata pia Paulo Mwenyewe kuna mafundisho ya Imani yalikuwa yakimtatiza ilibidi arudi Jerusalemu kupata ufafanuzi! na hata kusema anaogopa akisha hubiri Injili asije kataliwa!

  Kwa kifupi we do more harm tunapomwaga sifa badala ya kuzitoa kwa Yesu! Na yeye ni binadamu Je sifa hizo zikimwingia akajiona yeye ndio yeye itakuwaje? Unajua ni dhambi gani ambayo ndugu Mwingira anashindana nayo? Jifunzeni kumwombea! sio kumwaga sifa ambazo hatujaona mtumishi wa Mungu katika agano Jipya akimwagiwa.”

  Mungu Awabariki Wana Efatha mnapopitia kipindi hiki Kigumu….Labda ni wakati mzuri wa Kutafakari……ili kumsaidia “Mtume” katika mapito yanayomkabili…….

 39. Wapendwa,

  Nadhani nimewahi kuandika wakati fulani katika blog hii kuwa hizi sifa za ziada ambazo tunawabebesha watumishi zinaweza kuwa ni kitanzi kwao…….wao ni binadamu tu……..ni vyombo vya udongo kama muumini yoyote yule…….yeye (MTUME/NABII) na waumini wengine tumenyeshwa Roho yule yule mmoja…………Nadhan sasa i itabidi ifanyike kazi ya ziada na maombi kumsaidia Ndugu Mwingira na hizi shutuma mpya zilizojitokeza magazetini hivi karibuni……..kwani ni huzuni katika mwili wa Kristo………Na itawatatiza wale walio wachanga katika Kristo……………Na kama “Mtume” Mwingira angelikuwa amewajenga wafuasi wake kusimama katika Misingi ya Maneno ya Mungu shutuma hizi toka kwa mmoja wa wafuasi wake wa Karibu zingelitatuliwa ndani ya Kanisa……..sio kuzianika magezetini…….hii ni kanuni ya iliyoko ndani ya Biblia……..Wakristo hatutatui mambo yetu kwa kupitia Magezetini……..na pia kwa Viongozi wetu wawe Mitume/Manabii/Maaskofu/Wachungaji……Mimbari si mahali pa Mipasho/Kutumiana Lawama/Kubeza Waumini wenzio hata kama una tofauti gani…….Mimbari ni Mahali pa Kutangaza UJUMBE WA KRISTO! na tukitumia Mimbari kwa misukumo yetu matokeo yake ndio haya tunayaona magezetini…….Mungu na Aturehemu! Poleni Waumini Wenzetu wa Efatha……..

 40. Ndugu Daniel Seni na wengine,
  Maneno niliyokuwa nimeweka hapo kwenye post yangu ya mwisho ni toka kwenye biblia takatifu, hivyo waweza kusoma tu mistari hiyo toka kwenye biblia yako ya kiswahili na kurudi ili kujadili. Mistari yote nimeonyesha nilipoinukuu/itoa.
  1WAKORINTHO 2:4-5, 12:27-31 na 4:19-20.

 41. Mimi pia mtoto wako wa kiroho nipo pamoja nawe katika kukuombea ili kuendeleza kusudi ulilopewa.Nina imani baada ya kumaliza masomo yangu ya kidato cha nne nita jaribu kutengeneza website ya wana wa EFATHA ili kuweza kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe ndani ya EFATHA.BWANA MUNGU na akubariki katika utumishi wako.AMEN

 42. WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA….

  Mungu atusaidie sana tuijue kweli yake na tuwe na neema ya kupima na kuuelewa kila unabii. Tuachane na uchanga na umbumbumbu wa kiroho.

 43. i love you baba Mwingira
  the way you sacrify yourself for Tanzania that the
  Lord may use you to touch all Tanzanians
  GOD BLESS YOU….!

 44. shalomu! ningependa kwanza kumsalimu mtume na nabii Josephat Mwingira, na kumpongeza. na Mungu wa Bwana wetu Yesu kristo amtunze na kumlinda maana hata ktk maisha yangu nimemuona YESU akitenda kazi kupitia yeye na nimtu ambaye namuona wa muhimu ktk maisha yangu kwa sababu ya mafundisho yake na Mungu anavyo mtumia. nakuwa nasha ngazwa na walokole ambao kazi yao ni kulumbana kuhusu watumishi wa Mungu amesahau neno la Mungu alilisema ktk isaya agusaye mtumishi wangu amegusa mboni la jicho langu kama unaona huelewi kazi ya huyo mtumishi rudi kwenye biblia soma tena kisha piga magoti omba Mungu akufunulie sio mnakaa na kulumbana maana malumbano ni yawapumbavu maana hawana muelekeo na kule wanakoeleke na Mungu anakuwa kawaficha siri yake na wanakuwa wamepotoshwa. hivyo rudini kwenye mandiko Mtakatifu na kumuomba Roho Mtakatifu awasaidie. ni mtumishi wa kwanza Tanzania kukusanya maelfu ya watu nakuwaweka sehemu moja ndani ya wiki nzima kuwalisha na kuwalaza pasipo kuangalia elu zao minamshukuru Mungu kwa sababu ya kutupa mtume na nabii

 45. Ndugu, nataka sana kujadiliana juu ya jambo hili! nakuomba nukuu zote uzitafasiri kwa kiswahili na ndipo tuendelee, maana umenipa kazi kweli ya kutafuta maneno kwenye kamusi. napenda sana tuendelee na ninaahidi kuzama kwa ndani ili kueleweshana!

 46. Hahahaha! Nimecheka sana baada ya “kuambiwa” tumuite ndugu Daniel John Seni kama mtume na nabii.

  Kwako “Mtume na nabii Daniel John Seni” naomaba nikuhoji pamoja na wengine juu ya ulilosema kuwa “Bwana YESU ametutuma wote kwenda ulimwenguni, je na wewe unataka sasa uitwe mtume? pia kuhusu unabii: tunayo biblia ambayo imefunua unabii wote, kwa hiyo kila anayesoma biblia kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ni nabii…”
  Kwanza mimi sijakuelewa kama unasema wote wanaosoma biblia ni manabii au sivyo.
  Pili sijaelewa maneno yako umeyatoa kwenye NENO au kwenye “maneno”.

  Biblia inasema hivi “And my speech and my preaching was not with enticing words of man’s wisdom, but in demonstration of the Spirit and of power:
  That your faith should not stand in the wisdom of men, but in the power of God.” -1Cor 2:4-5.
  Swali la kwanza hayo “maneno” kwamba wote wanaosoma biblia ni au si manabii ni ya nani? Mungu au hekima za kibinadamu?

  Swali la pili; Biblia inasema “Now ye are the body of Christ, and members in particular.
  28 And God hath set some in the church, first apostles, secondarily prophets, thirdly teachers, after that miracles, then gifts of healings, helps, governments, diversities of tongues.
  29 Are all apostles? are all prophets? are all teachers? are all workers of miracles?
  30 Have all the gifts of healing? do all speak with tongues? do all interpret?
  31 But covet earnestly the best gifts: and yet show I unto you a more excellent way.”-1 Cor 12:27-31.
  Ningeomba tujadiliane kwa undani juu ya maneno hayo na mengineyo ili kujua kama hao mitume walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo au ni “maneno ya hekima za kibinadamu”?

  PLEASE NOTE: “But I will come to you shortly, if the Lord will, and will know, not the speech of them which are puffed up, but the power.
  20 For the kingdom of God is not in word, but in power.” -1Cor 4:20

 47. shalom! msimamo wangu ni ule ule kuwa kipindi hiki HAKUNA MTU MWENYE TITLE YA MTUME NA NABII bali kuna huduma yake tu. hii inatokana na kwamba Bwana YESU ametutuma wote kwenda ulimwenguni, je na wewe unataka sasa uitwe mtume? pia kuhusu unabii: tunayo biblia ambayo imefunua unabii wote, kwa hiyo kila anayesoma biblia kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ni nabii, kwa maana anafunua siri za Mungu kupitia Biblia kwa wale wasiojua! mwanadamu mwenye tabia ya rohoni anaweza kujua mafumbo ya Mungu,je na huyu sasa tumwite nabii? jibu nadhani utasema hapana! kama ni hapana kwa nini sasa leo unataka kusema kwamba Mtumishi wa Mungu, mpakwa mafuta wa Bwana Mwingira ni mtume na nabii? labda kitu ambacho wengi hawajui ni ile hali ya KUONYESHWA MAONO (Vision/trance) juu ya jambo fulani! inawezekana mtu akawa na karama hiyo kabisaaa! hapo nakubali, lakini kuwa na karama hii hakumfanyi mtu huyu kuwa na title ya nabii! kama ni hivyo HATA MIMI KUANZIA LEO WATU WANIITE MTUME NA NABII. ahsante!

 48. SHALOM. MUNGU AKUBARIKI SANA MTUMISHI, NI MAMBO MAKUBWA SANA EFATHA IMENITENDEA KATIKA MAISHA YANGU. TANGU MUNGU ALIPONIFUNGUA KUTOKA KATIKA VIFUNGO VYA KIPEPO NA MAAGANO YA MABABU NIMEUONA NA NAENDELEA KUUONA MKONO WA BWANA KATIKA MAISHA YANGU.

  NIKIWA NDANI YA EFATHA NIMEFANIKIWA KUPATA YALE AMBAYO NILIYATAMANI SANA KATIKA MAISHA YANGU, NILIYOKUWA NADHANI SIWEZI KUYAPATA. KWA SASA MIMI NI MWANAFUNZI, NASOMA MASTERS DEGREE AMBAYO NIMEIPATA BAADA YA MTUME NA NABII KUTAMKA NENO JUU YANGU. NILIPATA VYUO ZAIDI YA KIMOJA NA SPONSOR ZAIDI YA MMOJA HIVYO ILIKUWA NI JUKUMU LANGU KUCHAGUA NISOME CHUO KIPI NA NIAMUE NANI AGHARAMIE MASOMO YANGU.

  KWA KWELI ALIYONITENDEA HUYU YESU WA EFATHA HAYAISHI MIDOMONI MWANGU, JAMII YOTE INAYONIFAHAMU INASHANGAA JINSI NAVYOZIDI KUSTAWI KATIKA MAISHA YANGU NA KWA KUPITIA USHUHUDA WANGU WANAFUNGUKA UFAHAMU NA KUAMINI KUWA YUPO AWEZAE MAMBO YOTE.

  SWALA LINGINE NI KWAMBA KATIKA UTOAJI MUNGU AMENIINUA SANA, NA KILA NINAPOJITOLEA ILI KUENDELEZA KAZI YA MUNGU NDIVYO NINAVYOSONGA MBELE NA KUYAACHA MAISHA YASIYO YA UTOSHELEVU.

  NAKUOMBEA SANA MTUME NA NABII ENDELEA KUTULETEA UJUMBE KAMA MUNGU ATAKAVYOKUAGIZA. WEWE NDIYE BABAYANGU WA KIROHO. UBARIKIWE SANA BABA.

 49. Mtumishi mungu wetu akupe nguvu na kukufunulia yale ambayo anataka uyafanye. Hata Bwana Yesu hakukubalika kwa watu hivyo maneno yao ya kukukatisha tamaa yashindwe na kuharibikiwa kabisa kwa jina la Yesu Kristo wa nazareti

 50. nimekuwa nukiangalia TV ya EFATHA siku za hivi karibuni, kuna matukio mawili ambayo niliyaona na kwakweli naweza kusema ningependa sana kuelimika katika haya ili niweze kukua na kuelewa zaidi neno la Mungu wetu. Moja ni lile ambalo watu waliambiwa wakimwagiwa maji watapata nguvu kupitia maji hayo na kweli walipowamwagiwa tu umati wa watu woote uliokuwa pale mbele walianguka chini wote kabisa kwa wakati mmoja, sasa kwa wale waelewa naomba mnielimisha juu ya hili jee inawezekana watu wote wale walikuwa na mapepo? Tukio la pili ni la mtoto mmoja ambaye nafikiri alisema ana tatizo kwenye mapafu na aliletwa kuombewa akiwa na mfuko wake wa haja ndogo, ningependa niseme hapa si kwamba sina imani ya uponyaji wa Bwana Yesu kwani Bwana Yesu ameshaifanyia mambo mengi sana makuu katika maisha yangu, ila ningependa pia kujifunza jee katika hali kama ile ya yule mtoto (kwa wale watakaokuwa wameona watapata picha kamili), je hakukuwa na haja ya kumwacha hukohuko hospitali na kumfanyia maombi huko huko, kuliko kumtoa huko na mfuko wa kuhifadhi haja ndogo na kumwonyesha kwenye TV akitembea nao. Naamini kwamba uponyaji unapatikana popote pale ambapo Mungu mwenyewe atakugusa.Sipingani na haya yote ila najua kuna waelewa wazuri zaidi yangu ambao kwa maelezo yao yatanisaidia zaidi kukua na kusimama katika imani

  Mbarikiwe.

 51. Ndugu Robert, naomba uniwie radhi kwa kutojibu maswali yako, hii ni kwa sababu nilikuwa sijatembelea hii blog kwa muda kidogo, hivyo hata hayo maswali sikupata nafasi ya kuyaona. Lakini kama unaona kuna umuhimu wa kuuliza tena niulize tu maana nguvu ya mtu iko katika kujua, ndiyo sababu na Mungu wetu ana nguvu nyingi sana kwa sababu anajua sana hata ya miaka mingi mbele. Naomba uniwie radhi sana. Mungu akubariki.

 52. Ndugu Orbi, niliposema kayaulize mapepo sikuwa na maana ya kuku “confuse” ila nilikuwa na maana ya kuwa, kama vile Yesu alivyowaambia wale wasiomwamini, “kama hamniamini mimi basi ziaminini kazi” (miujiza aliyokuwa akifanya). Na wewe kama huwaamini akina Mwingira ziamini kazi wazifanyazo maana wagonjwa wanapona na wenye vifungo wanafunguliwa na wanapata kumtukuza Mungu na Mungu anazidi kujitwalia utukufu.

 53. huduma imeanzishwa na mwanadamu….

  ROHO Mtakatifu anahusika vipi katika huduma hii?

 54. Ndugu John Bethania,

  Kwa kifupi watu kama ninyi ndio mnaoichafua kazi ya huyo mtumishi mnayejaribu kumtetea, hebu angalia nukuu yako hii;

  ” Ukitaka kumjua Josephat Eliasi Mwingira nenda kayaulize mapepo yatakuambia vizuri sana.”

  Hivyo nikataka kujua kazi ya Mwingira inabidi niwasiliane na Mapepo? Na wala sio nirudi kwenye Maneno ya Mungu? Wapi katika Biblia tunayauliza Mapepo kuhusu kazi ya Mtumishi wa Mungu? Je Mapepo yakinifanyia kama yalivyomfanyia Paulo katika Matendo 16: 16-18 Niamini? Paulo hakuamini! Hivyo hata Mapepo yakiniambia Mwingira ni mtumishi wa Mungu aliye juu sitaamini! Kazi ya Mwingira na mtumishi yoyote ile tutaingalia katika wigo wa Neno la Mungu tu! Na wala hatutaenda kuyauliza Mapepo!

  Nakushauri mpendwa fanya homework ya ziada ya kusoma maneno ya Mungu kabla hujaandika! Naogopa sana Ushauri wako usije chukuliwa na wengine kwamba tukitaka kuthibitisha kazi ya Watumishi tunauliza Mapepo! Hiyo ni Injili Ngeni! Huo ni ukengeufu!

 55. Ndugu John Bethania,

  Kwa kifupi baadhi yetu hatuongozwi na “Mitume” “Manabii” na kumeza kila kitu kinachotoka mimbarini! bali tunaongozwa na NENO LA MUNGU! Na Biblia yangu nayoisoma inaniambia wazi kuwa sitasimama mbele ya kitI cha Hukumu na kuulizwa ulifanya nini Kwa Mwingira ! Ndengi! Lwekatare, Mzee wa Upako,Ngurumo…..radi nk! ILA NITAHUKUMIWA MBELE YA KITI CHA HUKUMU KWA KUTOSIMAMA KATIKA KWELI YAKE ILIYOFUNULIWA NA NENO LAKE TU! NA ROHO WAKE TU!Na NAAMINI MUNGU ATANIHUKUMU KWA KUTOITETEA KWELI YAKE DHIDI YOYOTE YULE NJE YA KANISA AU HATA WALE WALIO NDANI YA KANISA NA KUVAA MAVAZI YA KONDOO KUMBE NI MBWA MWITU WAKALI…….!

  Na hivyo ndugu yangu Bethania…..naamini Mungu atanipiga UTASA na mapigo mengi uliyoyasema NISIPOSIMAMA KATIKA KUISEMA KWELI YA INJILI NA KUITETEA!……..Ila Ole na yule anayewapoteza wana wa Mungu……kwani najua maana ya kufungiwa jiwe la kusagia na kutupwa baharini…….!

  Mungu na akupe macho ya kuuona ukuu wa Neema hii ya Wokovu aliowafunulia wampendao! UBARIKIWE!

 56. Ndugu John Bethania,
  Bwana Yesu asifiwe,
  Nafurahi kukuona katika mjadala huu,leo sitazungumzia hiki ulichokisema hapa isipokuwa nawaachia wachangiaji wengine.Mimi niliwahi kusoma mafundisho yako na ushauri wako kwa dada aliyekuwa akiomba ushauri kuhusu maisha yake ya kiroho. Pale ulipochangia kwa kutoa vifungu fulani toka kwenye biblia,lakini nilipofuatilia ndipo niliona kuwa mafundisho yako mengi yalikuwa kinyume na neno la Mungu yaani a total confusion. Nilikuomba unijibu kwa kutoa ufafanuzi kwa faida ya wote wanatembelea SG.Nilinukuu baadhi ya maandiko yako lakini hukujibu. Naamini, uliona isipokuwa uliamua kukaa kimya.Mimi bado nakumbushia majibu toka kwako. Tukiachilia hali hii iendelee wale ambao bado ni wachanga kiroho tutawachanganya sana!Mungu akubariki.

 57. Ndugu Orbi (na wengine wenye mawazo kama hayo), yaelekea wewe humjui Mwingira ni nani, Ukitaka kumjua Josephat Eliasi Mwingira nenda kayaulize mapepo yatakuambia vizuri sana. Acha kumnena vibaya mtumishi wa Mungu, je? waweza kustahimili hukumu ya Mungu juu ya kuwanenea vibaya watumishi wa Mungu? Unajua madhara yake? Soma Hesabu 12:1-15 Unaweza ukapata ukoma ndugu yangu!!; 2Samweli 6:16-23, Angalia Mungu aweza kukupiga utasa wa kiroho, kwa magonjwa nk !! Ukiona kazi anayofanya Mwingira inakukwaza usiinene ila nyamaza maana ukisema unawashawishi na wengine kuikana kazi hiyo na hivyo hukumu yako itakuwa kubwa zaidi kwa kuwa kama ni kazi ya kweli utakuwa umewapoteza wengi sana.Tena ndg. Orbi angalia usije ukawa unapigana na Mungu soma Matendo ya Mitume 5:34-39. Watu hujifunza kwa kuuliza maswali (kama watu wa Beroya Matendo 17:10-11) na si kuwanena vibaya watumishi.

  Hata wewe Orbi ni mtumishi wa Mungu (Zaburi 119:91 “Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo…na Orbi pia amesimama imara… Maana vitu vyote ni watumishi wa Mungu). Umetumwa duniani na Mungu kwa ajili ya kusudi fulani, je? umetumwa kufanya nini? Huoni kama unashughulika na kusudi (mraba) la Mwingira ukaacha la kwako? Utajibu nini siku ya kutoa hesabu? Na iweje wewe uliye mtumishi wa Mungu uwanene vibaya watumishi wenzio? Tena kumbuka maneno aliyosema nabii Eli kwa watoto wake ktk 1Samweli 2:25 “…Mtu akimkosa mwenzake Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea?” Ukiwanena vibaya watumishi wa Mungu unamkosa Mungu, je ni nani atakutetea wakati umemkosea mtetezi wako? Jifunze sana kutoka kwa manabii wa kale kama akina Daudi. Siku moja Mungu alitamka kuwa amemwacha mfalme Sauli 1Samweli 15:10; 16:1,14. Siku moja Sauli akaazimu kumwua Daudi 1Samweli 19:11; 23:14. Siku moja Daudi akiwa nyikani wakitafutana na Sauli akamkuta Sauli amelala usingizi mzito. Biblia inasema usingizi huo ulitoka kwa Bwana. Wenzie wakasema sasa adui yako amepatikana na tumwue 1Samweli 24:1-4. Daudi akajibu kwa unyenyekevu mkuu katika1Samweli 24:5-7. Fikiri Sauli ni adui wa Daudi, maana anataka kumwua, lakini Daudi, pamoja na Sauli kuachwa na Mungu, anamwona ni Masihi (mpakwa mafuta wa Mungu kama akina Mwingira na wenzie akina Ndegi, Rwakatare, Kakobe…..nk) Huoni kwa kuwanena vibaya watumishi wa Mungu unatafuta hukumu iliyo kubwa? “hukumuni ninyi wenyewe”. Mungu awasaidie kuujua ukweli huu.

 58. Bwana awe nanyi siku zote za maisha yenu.ni kweli tukiacha dhambi. tutafanana naye kwa kila kitu kwa maana kama alivyo BABA ndivyo alivyo mtoto.Hivyo dhambi ni kikwazo kikubwa sana cha sisi kutojua mambo tunayopaswa kujua kutoka kwa MUNGU BABA,lakini inatupasa kuzishinda dhambi zote zinazotuzunguka ili tupate neema ya kujua siri hizo za MUNGU BABA. Tukumbuke kuomba TOBA kila muda tunaopata kwa ajili ya maombi kwa maana mwili wakati wote hushawishi kufanya dhambi yaani hushindana na ROHO,Maisha ya wokovu tusiyachukulie kuwa ni mazoea ila yawe ni maisha mapya kila wakati ili tuweze kuwa shirika na ROHO Mtakatifu ambaye hutuongoza na kutufundisha jinsi ya kuenenda katika kweli ya MUNGU; AMEN.

 59. Tumsifu Yesu Kristu

  Biblia inasema ukiijua kweli nayo kweli itakuweka kuwa huru.Nadhani kifo cha Bwana wetu Yesu Kristu kilitupa uwezo wa kuhesabika watoto wa Mungu,kwa hiyo kila mmoja anao uwezo wa kuongea na Mungu,kinachotulimit ni dhambi zetu,tukiacha dhambi hakuna tutakaloomba tukanyimwa na hakuna tutakaloshindwa,kwa kupitia bwana wetu Yesu Kristu. Jamani watu wa Mungu Efatha!(funguka).KEKUUUUUUUUUUUNDU.
  Mungu wetu ni mwema muombe awafungue macho ya roho. MNAWAFANYA WATU WAANZE KUMDHARAU BWANA KWANI IMEKUWA KAMA VYAMA VYA SIASA NA BIASHARA.

 60. Ndugu, nasikitika sana kwamba nimeshindwa kabisa kuielewa huduma hii ya efatha. Juzi nimesikiliza kwa mara nyingine mahubiri ya huyo mtume na nabii mwingira nikastushwa ni pale alipodai, eti wahubiri wote wa dar es salaam hawamfikii yeye upako wake. Tena hukimbilia kwenye tv kusikiliza anachofundisha kisha wao nao hupata cha kuhubiri makanisani mwao. Niliogopa sana na nikatetemeka pale waumini wake walipoitikia mipasho hiyo kwa shangwe kuu.

 61. Aise mwenye macho hambiwi ona namshukuru mungu kwajili yake, watu kama mtume wanaotumiwa na mungu kwa nguvu zote ni wachache sana tena anajali ata uwe mbali wapi anakuona tu.Asante mungu kwani tuna baba wa ukweli.Usichokijua yeye ameshajua kama loliondo.

 62. msiongee msilo lijua,Huyo ni mtimishi wa Mungu,msifanye mioyo yenu kuwa migumu,kubalin n muamini tu.

 63. i’m looking for efatha contact contact number i need to speak to church membar.thank you

 64. mkuu jitahidi kujua hata wewe maandiko sio ku-condem wenzio wakiwa wanafanya kazi ya mungu na mungu

 65. Nimeshangaa na nukuu hiyo!

  “Mimi mwenyewe niliwahi kumsikia Mwingira akisema kuwa siku ya mwisho Yeye atashirikiana na Yesu kuwavika watu (washirika wake) taji. Alitoa mfano wa namna marais wanavyowatunuku wanajeshi nishani ambapo wanaweza kumtunuku mmoja kwa niaba ya wengine na kisha wengine wakaendelea kuvishana wenyewe. Kutokana na mfano huo akasema kuwa siku ya mwisho Yesu atawavika taji wao (akina Mwingira) na wao watawavika watu walioko chini yao, nikashangaa sana!?”

  Yesu aliwaambiaje wana wa Zebedayo ( Marko 10:35-38)walipotaka wapewe nafasi ya kukaa mkono wa kuume na kushoto katika ufalme wa Mungu, alisema “HAMJUI MNALOLIOMBA”

  Kwa kifupi Mtume Mwingira hajui analo lizungumza!

 66. Pingback: Mtume na Nabii Josephat Mwingira

 67. i love efatha because is the place designed where there is JESUS that is why i have SAVED!!!

 68. Wapendwa, tusiendelee kuwa watoto wachanga kama walivyokuwa Wakorintho, waliokuwa wakisema mimi ni wa Paulo na mimi ni Apolo badala ya kujua kuwa Mtendaji Mkuu katika wokovu wao alikuwa ni Mungu!
  Hatuna sababu ya kumsifu mtumishi yeyote maana si mtumishi afanyaye kazi bali ni Roho wa Mungu, mtumishi ni chombo tu kitumiwacho na Roho kama apendavyo!
  Tukiwasifu watumishi tunawajengea kitu kibaya sana kinachoweza waangusha.Tuzidi kuwapenda na kuwaombea ili wasipatwe na kiburi cha uzima cha kujiona wao ndio bora kuliko wengine.
  TUNATAKIWA TUFIKE MAHALI PAKUWEZA KUCHALLENGE mambo yote yanayosemwa na hawa watumishi wa Mungu maana kama hatuwezi kufanya hivyo basi tutadanganywa kirahisi sana katka siku hizi za mwisho.Mimi nimeokoka siku nyingi na huwa kila kitu mtumishi yeyote anachokiongea LAZIMA NAKIWEKA KATIKA MIZANI YA MAANDIKO YA BIBLIA, kama hakiendani na Neno mimi sikiamini hata kama huyo mtumishi ni mashuhuri duniani kote!
  FUATA KANUNI HIZI:
  1.Kuwa na muda wako mwenyewe wa kujisomea na kujifunza Biblia KILA SIKU.
  2.Kuwa na muda wako mwenyewe wa kumwabudu, kumsifu na Kumwomba Mungu KILA SIKU.
  3.Kuwa na ushirika na waamini wenye kumpenda MUNGU kama wewe(Yaani kanisa lenye kufundisha Neno lisemavyo)

  Ukifanya hivyo utakuwa na msingi mzuri ambapo hata kama kiongozi wako wa kanisa atakengeuka siku moja yaani akaiacha imani ya wokovu WEWE HUTATETEREKA MAANA UTAKUWA UMEMJUA MUNGU KIBINAFSI maana God is a personal GOD! Mungu anataka tumjue kibinafsi si kufuata mkumbo!Watu wengi sana siku hizi wanataka vitu vya chapu chapu(shortcuts), SORRY, Mimi nijuavyo KWA MUNGU HAKUNA SHORTCUT! Wewe angalia watu wa Mungu katika Bible- Yusufu, Yesu Kristo, Mitume wa Yesu angalia maisha yao, walijenga uhusiano wao na Mungu ndipo wakawezeshwa kuvuka magumu yote.Sasa leo hii kama hatutafuata nyayo zao na kujizoesha kumtafuta Mungu kibinafsi basi tutakuja danganywa na mpinga Kristo na watumishi wa Shetani kirahisi!

 69. Kaka Orbi!

  If everybody could get hold of Hebrew 06:1 -3. ingetusaidia sana. kimsingi Mungu anatarajia tusonge mbele na kukua kiroho, the only way we can do that ni kwa kutafuta kujua maandiko, si kwa kusubiri yale tunayofundishwa na watumishi tu, bali ni kwa kuwa na maisha ya kujitoa kutafuta kumjua Mungu kwa kusoma na kutafakari maandiko, Roho mtakatifu ndiye mwalimu wa kweli, na tunao uhakika kwa kuwa he is the Author of the word of God. Kuwasikiliza watumishi ni Muhimu, But muhimu zaidi ni sisi kuwa na Muda binafsi wa kutafakari maandiko, na kumwomba Mungu.
  Mungu anatarajia tupige hatua na kukua kiroho, tukizidi kumjua zaidi ili naye adhihirike zaidi katika maisha yetu.

  Mungu awabariki.

 70. Nathan,

  Nashukuru kwa ujumbe wako, na ujumbe wako unakuwa na maana zaidi hasa kwa heshima yako uliyo nayo kwa Mtumishi wa Mungu Mwingira, kwa kifupi ulichosema ni kuwa heshima kwa mtumishi wa Mungu inapokuwa ni ushabiki inatisha! Hasa mtumishi wa Mungu anapokweza nje ya mipaka ya maandiko! Mtumishi wa Mungu yoyote yule huwejenga waumini wake wazidi kujenga imani kwa Bwana Yesu na neno lake! na wala si kwake yeye! Sidhani mtumishi wa Mungu Mwingira anafanya hivyo, ila baadhi ya waumini wake wanataka tuamini hivyo! Kadri mtumishi wa Mungu anavyotumiwa na Bwana yeye mtumishi huzidi kupungua katika macho ya watu na Yesu huzidi kukuzwa! na kuonekana!
  Kama ulivyosema, Biblia inatufundisha kuwaheshimu watumishi wake, lakini sio kuwashabikia! Watumishi wa Mungu ni binadamu tu! na wala si malaika! Paulo alitumika lakini vile vile aliogopa asije akakataliwa! Musa alitumika, lakini akakataliwa kuingia Caanan.Ieleweke kwamba kila Mkristo aliyeokoka ana uwezo na Kibali sawa cha kuingia Patakatifu pa patakatifu kwa njia aliyotuanzishia Mwenyewe! Hiyo Ndio Biblia! na ndio agano Jipya!

  Naogopa sana kiwango cha baadhi ya waumini ambayo Wachungaji, Manabii, Mitume wamekuwa kama daraja la kuwapeleka mbele za Mungu! Waumini wengi hawana personal devotional life! hawasimami katika imani kwa miguu yao wenyewe! bali kwa miguu ya watumishi! Na jambo la kusikitisha kabisa kuona kuwa kuna watumishi ambao wamewajenga waumini kuwa ni tegemezi katika maisha yao ya Kiroho! Ni kweli wanamkiri Yesu au wokovu, lakini katika mgongo wa Mtume, nabii au mchungaji!Mtume au Nabii anakuwa quoted kuliko hata Yesu na Neno lake! Mungu na Aturehemu.

 71. Kaka Orbi!

  I have so Much respect for the servants of God. Kimsingi Mtume na nabii Josephat Elias Mwingira ni baba yangu, and I know God is using in amazing ways. Ninachohofia ni hii imani ambayo baadhi ya wachangiaji wanaionesha kwa kufikia kiwango cha kutamka maneno yasiyotamkika, najiuliza je, ni kweli ndani yao ndivyo wanavyoshuhudiwa na Roho wa Mungu? au wanaongea kwa ushabiki. Mtumishi mmoja katika mafundisho yake anasema “Commitment without Reflection is fanaticism in action, and Reflection without commitment is the paralysis of all action” kwa kifupi ni muhimu kwetu kuwaheshimu na kuwathamini na kuwatii watumishi wa Mungu, lakini hatupaswi kufika mahali pa kumsubstitute Yesu na watumishi waliopo. Ni kweli tunawapenda na ni kweli tunao wajibu wa kuwaheshimu na biblia inatutaka tufanye hivyo. but heshima hii ni lazima iendane na kile tunachofundishwa kwenye neno la Mungu. si vinginevyo. Baadhi ya maneno yaliyowekwa kwenye comments zilizomo humu yanaogopesha sana, na kama ni mtu unayejua vema maandiko, itakupa tabu kuyaelewa pia.
  Mwisho wa yote, ni vema tukatambua kuwa Mungu anawaheshimu watumishi wake na sisi tunao wajibu wa kuwaheshimu, lakini tunaye Bwana mmoja tu wa kumwabudu. ANAITWA YESU KRISTO, YEYE NI MUNGU NA ATABAKI KUWA MUNGU MILELE YOTE.

  Mbarikiwe na YESU.

 72. ooh! jina la Bwana lihimidiwe mtumishi wa Mungu endelea kumtukuza Mungu kwanjia hiyo lakini usisahau kuliombea Taifa hili Tanzania

 73. Nathan,

  Wakristo wa leo hatutaki kufanya homework! Na kwa nini tufanye homework wakati kuna njia ya mkato wa kupitia kwa mchungaji wako au Nabii au Mtume! Ambaye anaweza “kutuangalizia” kwa Mungu! Ni mtume na Nabii kwa sasa hivi wanaweza kutufunulia “kweli yote” Kwa wengi inachukua muda mrefu kumsubiri Roho Mtakatifu! Inachukua muda mrefu kukaa magotini au kukaa kwenye Neno lake! we want instant things! we want quick results! kama Bwana amemfunulia “mtumishi wake” kwa nini sisi tuhangaike tena! we want to hear wonders and mysteries! ambazo Mtume na nabii kaonyeshwa leo! We are ready to die for the man God rather than truth revealed in holy scripture!

 74. katika miaka michache iliyopita tangu nimeokoka, nimejifunza kwamba HAKUNA MWALIMU BORA NA WA KWELI KULIKO ROHO MTAKATIFU. ukijiachia kwake na kumruhusu akufundishe, utaona mambo ya ajabu kuliko unavyoweza kufikiri. JINSI TUNAVYOTAZAMA MAMBO SI MUNGU ANAVYOYATAZAMA, NA TUNAPOANZA KUYAZUNGUMZA Pasipo uongozi thabiti wa Roho tunakosa sana. thats why jesus said MANENO YENU YAWE MACHACHE, kimsingi ndiyo iwe NDIYO, na siyo iwe SIYO.
  NA MAHALI PENGINE TUNAAMBIWA MTU ATAHUKUMIWA KWA KILA NENO LILILOTOKA KINYWANI MWAKE.
  Tufahamu kwamba kama si lazima ku comment, hupungukiwi kitu kwa kukaa kimya, badala yake unajilinda dhidi ya hukumu.
  Lets JUST SEEK TO KNOW GOD, I THINK THIS IS THE ONLY THING THAT WILL HELP US, USITAFUTE KUMJUA MUNGU KUPITIA WATU, DO YOUR HOMEWORK KWA KUWA NA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU NAYE ATAMDHIHIRISHA MUNGU KWA NAMNA YA TOFAUTI KWAKO.
  NOTE: MCHUNGAJI WAKO, NABII WAKO, AU MTUME SI MUNGU.
  JEHOVAH GOD WILL ALWAYS REMAIN GOD

 75. I AM AN EFATHA MEMBER KENYA, I THANK GOD FOR APOSTLE MWINGIRA, A GREAT MAN OF GOD I TRUST HIM AND I KNOW EFATHA IS FROM GOD AND WE LOVE U DAD AS KENYANS UNDER YOUR MINISTRY. BLESSED BE TO MAMA ELIAKUNDA A REAL TEACHER AND SERVANT, STAND FIRM GOD WILL NEVER LEAVE YOU.
  FLORENCE -KENYA

 76. Inols,

  Hofu yangu kubwa kwa baadhi ya waumini Tanzania leo ni ile hali ya “KUWAKWEZA” Watumishi wa Mungu kuliko hata mipaka iliyoko katika maandiko! Hatujaona katika Matendo ya Mitume Paulo, Petro na hata mitume wengine wakifanyiwa hivyo! Haimsadii mtumishi wa Mungu na kwa waumini inakuwa ni mbaya zaidi wanapoanza kujenga imani yao juu ya mtumishi wa Mungu kuliko Mungu wa huyo mtumishi! Kwa kifupi tu Watumishi wengi wanavyotukuzwa LEO hakuna tofauti na Papa anavyotukuzwa katika Ukatoliki! Maandiko yako wazi ” OLE WAKE AMTEGEMEAE MWANADAMU” Hata akiwa mtumishi wa Bwana! BWANA NA ATUREHEMU NA KUTUFUNGUA MACHO YA ROHONI!

 77. Praise the Lord!

  Guys you have praised and said a lot about Apostle and Prophet Mwingira. It’s good that we all appreciate what Prophet Mwingira is doing for Tanzanian Church for Jesus Christ’s sake, but let us be good imitator of works of Apostle Paul. Apostle Paul dared to rebuke, reproach openly to believers about some of the leaders of the church by that time, we all know his misunderstanding with Peter whom he rebuked him for not being clear about the issue of position of circumcised and uncircumcised people in the work done of our Lord Jesus Christ. So this be the case then let us not turn the deaf ears to what is being speculated/said about Apostle and Prophet Mwingira. This is the only way we can heal Tanzanian church by uncovering and rebuking what we know beyond reasonable doubts about the conduct of the leaders of the church.

 78. Nakushukuru YESU kwa kumpa mtumishi wake sikiolakusikia iliatusikizishe. UTUKUFU KWA BWANA.

 79. Yesu kristo ni Bwana na pekeyake anaweza na zaidi ya kuweza,nachukua nafasi hii kumtunza Mungu kwa kuihamisha Tanzania kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyigine kwa kutumia watumishi wake aliowachagua, inakuwaje sasa baadhi ya watu wengi kuanza kulumbana kwa mambo yasiyo eleweka haina utukufu na wala haipendezi,Tuko shambani mwa Bwana tuendele kutenda kazi ili na wengine ambao bado hawajampokea Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao waitambue hii siri ya ajabu,siyo napinga mijadala ila iwe inampa Mungu utukufu.
  MBALIKIWE WATUMISHI.

  KIDUMU CHAMA CHA WALOKOLE, SERA NI ILEILE KWENDA MBINGUNI,Amen!

 80. NI UKWELI AMBAO USIOFICHIKA HUDUMA YA EFATHA UKOMBOZI KWA TANZANIA NA DUNIA NZIMA WENGI WAMEFUNGULIWA KUPITIA HUDUMA HII NAMSHUKURU NABII KWA KUTII SAUTI YA MUNGU NA KUANZISHA HUDUMA

 81. I don’t doubt about the success of EFATHA MINISTRY in Dar es Salaam and Tanzania at large. It brought salvation to me and millions of other people worldwide through the people of efatha and TRINITY television.

 82. Mpendwa Mwakambako,

  Labda kuliendeleza some letu hapo, na labda nikianzia na nukuu yako mwenyewe “Nizidi kuwa wa rohoni” Ni kweli kabisa, sisi tuliompokea Yesu, Kumwalika aingie moyoni mwetu, kumpokea Roho wake na kumhurusu atuongoze, kwa maana neno lake limesema “Kwa kuwa wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu” (Roma 8:14) Kwa kufanya hivyo tunakua tumeingia katika ulimwengu mwingine kabisa! Na Biblia inasema baada ya kuokoka “AKATUKETISHA NAYE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO” Hivyo kwa kuketishwa na Yeye (YESU) Katika Ulimwengu wa Roho Tunaayaangalia mambo kwa macho mengine kabisa! yaani Macho ya Kiroho! na ndio maana Paulo anasema “MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU”(Ephe COL 1:18)

  Hivyo macho hayo ya kiroho ndiyo yanatakiwa kuchukua nafasi kwa sababu sasa tumekuwa wa Rohoni! na wala si kuviangalia vitu kwa macho ya mwilini tu!

  Labda nikirudi nyuma kidogo,maana somo la kuyaangalia mambo kwa jinsi ya Rohoni ni pana sana!sidhani kabisa tunaweza kujadiliana hapa, mimi nitakupa utangulizi tu, na waalimu wengine ndani na nje ya blog hii na wewe kwa kusoma maandiko utaendelea kujifunza, na ili tuwe pamoja, lazima uelewe binadamu ameumbwa katika nafsi tatu (Triune in nature)Heb 4:12) (Kiswahili huwa kinachanganya sana maneno pia ya kiingerez) hivyo Ni lazima uelewe binadamu wa asili kabla ya anguko yukoje, na baada ya kumpokea Yesu nini kinatokea ndani yake, labda dhana yangu ya kutumia vigezo gani kupima jambo lolote lile, liwe la kazi ya Mungu au la! kwani futi kamba unayotumia kuangalia mambo ikiwa mbaya, basi hutakuwa na matokeo mazuri ya kitu unachokipima!

  Hivyo utatu wa binadamu (triune nature of man) lazima uwe ni kigezo cha kumwangalia binadamu, kabla na baada ya kuokoka, nini kinatokea hasa, nikiwa na maana;

  1.Body
  2.Soul (Where is self dwell”
  3.Spirit (Where God dwell)

  Na sehemu yetu inayoongalia mambo ndani ya mwanadamu ni Soul (Nafsi hai) ambayo nayo ina

  1. Man’s emotions
  2.Man’s intellect
  3. Man’s volition, or will.

  Lakini kama nilivyosema Tunapookoka, haya yote ndani ya mwanadamu yanatakiwa yabadilike! Kwa kifupi kabisa mwanadamu sio mwili ILA ni “NAFSI HAI” Iliyouvaa mwili! Na Biblia inaposema tulikufa Kiroho ina maana ni hii nafsi hai!Na ni hii ndio inayowasiliana na Mungu! Ndio yenye UHAI WA MUNGU! na wazazi wetu walipomtenda Mungu, na aliposema HAKIKA MTAKUFA, hakuwa na maana ya mwili tu, kwani baada ya kumwasi Mungu Adam na HAWA waliishi miaka kama 900! Lakini “NAFSI HAI” yenye Uhai wa Mungu ilikufa! Disconnected with God! Yaani kama nilivyoonyesha hapo juu “Man’s emotions, man’s intellect, and man’s will ilikufa! Haikuweza kuwasiliana na Mungu!

  Na labda nisema hapa kwamba licha ya nafsi hiyo kufa- yaani kutokuwa na uhusiano na Mungu, yaani katika kufa kwake huko binadamu, nafsi hiyo inafanya au binadamu huyo bado anafanya mambo mengi sana, uvumbuzi wa sayansi, kufikiri, philosophy etc Lakini HAIWEZI KABISA KUYAFAHAMU MAMBO YA ROHONI! na tatizo kubwa kwamba wengi wetu baada ya Nafsi kuwa hai, au kuhuiswa baada ya kuokoka, bado kwa kutozidi kumjua Bwana Yesu siku kwa siku, tunaendelea kuyaangali mambo kwa jinsi ile ile ya awali!Tunasahau kuwa Biblia inasema “TAZAMA MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA” Akiwa na maana sio sura zetu au maumbo yetu! Ni mabadiliko makubwa katika mtu wa ndani!

  Inabadilisha kabisa jinsi tunavyooyaangali na kuyapima mambo!Binadamu wa asili (asiyeokoka) anavigezo vyake vya kupima mafanikio! au kitu chochote anachokiona lakini Kwa mtu wa Mungu anaangalia mambo kwa macho ya Rohoni na kutumia “parameters” mbali mbali za neno la Mungu! hebu soma 1COR 1- 1COR2:1-16) Kwani kwa kutumia macho ya mioyo yetu, na Hekima ya Rohoni kunabadili mtazamo wetu kabisa wa MAMBO! A new paradigm shift! Kama nilivyosema katika post ya mwanzo kabisa, wingi wa watu au mali na vitu sio lazima kabisa uashirie ni mafanikio toka kwa Mungu!Na ndio maana kwa watu wa Rohoni mambo mengi tunayoyaona ni ya maana, mbele ya wasiomjua Mungu inakuwa ni UPUUZI, na hata watu wengi wa Mungu Leo Baraka za vitu, afya,au kukubalika katika jamii inaweza kuwa ni ishara ya kutembea na Mungu kwa ukamilifu! Lakini hii ni kwa kutumia macho ya nje tu! yaani macho ya mwilini!Na hata watu wasiomjua Mungu wanatumia vigezo hivyo! Kumbuka Eliya kwa kutumia macho ya mwilini aliona ni “ministry” yake tu ndio imebaki kumtumikia Mungu aliye hai, lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje” Nimejisaidia watu elfu saba wasiopiga magoti mbele za Baali”!Kwa macho ya Eliya kuwa hakumuona mtu mwingine akishusha moto kuchoma madhehebu ya Baali, alidhani yuko pekee aliyebarikiwa hivyo! kumbe sivyo kwa kutumia macho ya Rohoni! Hivyo basi ndugu yangu Mwakambako hebu maombi haya ya Paulo kwa Waefeso nayo yawe kwetu pia; ” …..NIKIWAKUMBUKA KATIKA SALA ZANGU,MUNGU WA BWANA WETU KRISTO, BABA WA UTUKUFU, AWAPE NINYI ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE,MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU…….! UBARIKIWE!

 83. Ndugu yangu Mwakambako,

  Hapana ndugu yangu,Si kwa kwamba napinga mafanikio ya Watumishi wa Mungu! La hasha, kwani vipimo vyetu vingi vinakuwa ni kwa macho ya binadamu! Na macho yetu ni ya kimwili tu! Yanaweza kabisa kutupoteza!kwani ni Mwanamke mjane na yule tajiri hekaluni! Yesu alionyesha kuwa ni Mwanamke mjane ndiye thawabu yake ilipokelewa!Tunapofunga je! inatakiwa iwe sirini! Daudi alipochaguliwa kuwa mfalme! Macho ya nje ya kupima mafanikio yalienda kwa watoto wengine wa Yese! Na ndio maana Yesu mwenyewe aliyetuambia Tutafanya miujiza mingi kwa jina lake na ndiye yeye pia aliyesema atatukataa licha ya kuitenda miujiza hiyo kwa jina lake!Je atatumia nini kupima? Anajua yeye mwenyewe kwetu ni vigumu!

  Nachotaka kusema ni kuwa tu waangalifu mno kutoa performance assessment/evaluation kwa vigezo vya macho ya binadamu! Ambavyo mara nyingi huwa ni;

  SUCCESS = ACCOMPLISHMENT!

  Na mpendwa mmoja alisema na mnukuu alisema;

  Accomplishment ” Include both visible accomplishments people can see invisible accomplishments only God sees. People considers someone’s visible (known) accomplishments. ( but God’s equation include variable factors we sometimes overlook.)

  Kwa kifupi tu Mungu anajua amemwita kila mtu kwa kusudi lipi! na amempa nini (Talents) au talanta zipi kutimiza kusudi lake! Na amemfungulia mlango upi! Mlango wa Paulo haukuwa sawa kama wa Philipo au Petro na mitume wengine!

  Inawezekana kabisa kwa macho ya kibinadamu huduma ambayo mimi na wewe tunaona kubwa sana, mbele za macho ya Mungu alitakiwa afanye zaidi! Hakutumia talanta na milango ambayo Mungu alimpatia au kumfungulia! Na pia zile huduma ambazo kwa macho ya kibinadamu zinaonekana
  hazina mafanikio, labda ni kanisa la mchungaji lenye watu 20 kijijini, au mwinjilisi anakaa na kupiga Injili barabarani akawa kabisa anatimiza kusudi sahihi la Mungu na kufanya kile ambacho ameitiwa!

  Ni nini Mungu amekuitia (wito wako) Ni talanta ngapi amekupa (umezitumiaje) na mlango upi Bwana aliokufungulia ( Umeutumiaje)? Na la mwisho kabisa ni motive! Ni nini kinachokusuma ufanye kazi ya Bwana! Ni sifa, ni tumbo nk! Haya yote ni Mungu anajua kuwa kazi hiyo imefanikiwa au la! Anyway tuzidi kujadiliana!

 84. Bwana Yesu asifiwe

  Ndugu Orbi kama kwenye huduma ya Efatha watu wanaokoka, wanapona, na wameweza kupeleka Injili vijijini na watu wakalisikia na kulipokea neno; hayo si mafanikio???

  Tuangalie vigezo vipi basi ambavyo twaweza kusema huduma hii imefanikiwa au la!!!!

  Au ndugu Orbi tuseme wana wa Mungu wanafanya nothing???

  nisaidie na vigezo unavyotumia wewe ili nizidi kuwa wa rohoni zaidi.
  Tunajifunza

 85. Mpendwa Dada Fatuma,

  Pole kwa dhoruba unayopitia, Naamini kabisa Mungu kwa kupitia Mwanawe Yesu Kristo, na kwa uweza wa Roho wake Mtakatifu atakupitisha dhoruba hii, kwani hakuna Dhoruba isiyo mshinda,na ni wengi tumepitia dharuba sawa na wewe!

  Labda nikupe msaada wangu wa mawazo, na hasa kwa kulitumia tu Neno lake.

  1.Kitu cha msingi kabisa cha kuzingatia ni Mungu anakuitaje wewe! au anakutambuaje! Ni wewe tu unaweza kuhakikisha hilo! Dada Fatuma, kama umeokoka,umeoshwa dhambi na Bwana Yesu, yaani umepokea wokovu wa Mungu, Biblia inasema “UMEKUWA MTOTO WA MUNGU” (Yoh1:12)! Na wewe kwa imani umefanya hivyo, yaani umefanyika kiumbe kipya (2Cor 2:15) Huna haja ya kujali binadamu anakuita nani!Wakristo ni wafuasi wa Bwana Yesu, mwana wa Mungu aliye hai! anaishi kwa Roho wake miyoni mwetu! Hivyo hatujali binadamu wanatuitaje!Watuite kwa majina mazuri au mabaya, maadamu tunatembea katika NURU yake ( Maisha yetu ni ya utakatifu) na tunaishi kumpendeza Yeye, Hatuogopi “lebel”yoyote tutakayopewa! Jina letu haliwezi kuchafuliwa mbele ya watu! Labda tujichafue wenyewe kwa kutomtii Yesu na kuishi maisha ya dhambi! Hivyo Basi Nenda tena au rudi kwenye maneno ya Mungu, muombe akufunulie wewe ni nani Katika Kristo Yesu!Hilo litakufungua kuliko kitu chochote kile!Si vibaya kwenda kupata ushauri wa nini cha kufanya kutoka kwa watumishi wa Mungu,lakini hili la kuitwa mchawi na wewe unajua si mchawi linahitaji msaada tu wa kujitambua wewe ni nani katika Bwana Yesu! Ni wanaokuita wewe Mchawi ndio wanahitaji kufunguliwa na mtu wa Mungu kujua kilichoko ndani yako!Na wala sio wewe!

  2. Jambo jingine dada Fatuma kama umeamua kumuishia Mungu, yaani kuokoka, na kutembea naye, ni kuwa na NIA ya makusudi kabisa ya kutaka kumpenda Mungu tu! Huwezi kabisa kuwapendeza wanadamu,Na wala katika maisha yako ya kila siku hilo lisiwe linalokusukuma!kwani binadamu ni wengi! Na kila binadamu ana kigezo chake cha kibinadamu cha kumpima binadamu mwenzie! na kila binadamu atakuangalia kwa macho ya nje tu, haujui moyo wako!La msingi ni kukua katika Yeye,( kuishi kwa ajili ya Bwana Yesu) Kwani BWANA MUNGU ANAANGALIA MOYO! HAANGALII KAMA BINADAMU AANGALIAVYO! SOMA NENO LAKE LITAKUFUNGUA!

  3.Jipe moyo! wewe si wa kwanza kuitwa mchawi!Nimeona watu wengi waliookoka wakiitwa wachawi!Wengine ni kwa vile wachawi au nguvu za giza dhidi yao zilishindwa kufanya kazi! kwa sababu ulinzi wa Mungu uko juu yao!Na wengi wameitwa wachawi kwa ajili ya chuki za kibinadamu tu! Wivu kwa sababu Bwana Amekubariki na kukupigania!nk.

  Dada Fatuma kama umeokoka, unaishi maisha ya kumpendeza Mungu, Ulinzi wa Mungu uko juu yako! Hebu kasome tena Yohana sura ya 14, 15, 16 na hata 17! Ina maneno ya Faraja, kwani sisi ni tawi katika mzabibu ( ambao ni Bwana Yesu! Ukiguswa wewe ambaye ni tawi katika mzabibu, wamemgusa Bwana Yesu! Hebu nakusihi jenga hamu ya kusoma Neno la Mungu toka Agano la Kale uone Mungu alivyokuwa akitembea na Watu wake, na jinsi utisho wake ulivyokimbiza maadui wa watu wa Mungu!

  JIPE MOYO, NITAKUOMBEA, NA BWANA ATAZIDI KUKUBARIKI!

 86. Bwana Yesu asifiwe, naleta maombi yangu kwako baba kwa kunisaidia kuomba. Labda niseme tu nawe kupitia barua hii, naimani mungu atanifungua. Katika maisha yangu yote sijawahi kukutana na dhoruba kali kama hii.

  Baba nimekutana na jaribu la kuitwa mchawi familia moja imeamua kunitenga kisa mimi mchawi. Niliwahi kuja kutaka kukuona lakini nilielezwa siwezi kukuona labda nionane na watumishi wa chini yako. Baba kutokana na tatizo langu mimi nakuomba kupitia barua hii ndogo niweze kuwasiliana na wewe ana kwa ana ili nipate ukombozi kutoka kwako. Baba ni jaribu kubwa sana nililonalo mpaka nakosa amani ya moyo. Naomba nafasi ya kukuona baba na pia maombi yako yaanze sasa nina imani nitafunguliwa. namba yangu ya simu ni 0786 882976 ni imani utanisaidia baba.

 87. Mpendwa ndugu MWAKAMBAKO,

  Ni kipi kinachokufanya usema “pamoja na kufanikiwa kwa huduma hiyo” Ni kipimo gani unachopima mafanikio ya huduma hiyo ya Efatha?

  Je ni wingi wa watu? Je ni uwezo wa kifedha? Kuwa na mitambo ya kurusha matangazo kwa TV? au kujulikana nchi nzima kwa “mtume” na “nabii” Je ni kwa watu kufunguliwa? Kuwa na majengo makubwa! Ni kipi hasa umetumia kama kipimo cha mafanikio ya huduma hiyo?

  Sidhani kabisa hivyo ndivyo vigezo vya Neno la Mungu, kwani siku zote Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo! Si kwa umbo la nje! Si kwa kwa wingi wa magari wala farasi! Sidhani kabisa vigezo unavyoweza kumwangalia Eliya na hata Elisha unaweza kuvitumia kwa “mtume” na “nabii” huyo wa Efatha!

  Kwa vigezo vya nje tu huduma ya Yesu haikufanikiwa! alikufa kijana tu! akiwa na nguo moja tu! hakuwa na mahali pa kulaza kichwa chake! aliingia Yerusalemu kwa mwana punda wa kuazima!

  Tuseme nini juu ya Yohana mbatizaji! au Stephano! au hata Paulo, wakati wa kufa kwake kulikuwa na makanisa machache tu yaliyotapakaa pembezoni mwa Mediterraniani dhidi ya Dola yenye Nguvu ya Rumi! Kwa macho na vigezo vya mafanikio ya kibinadamu usingeweza kabisa kuona chochote cha mafanikio katika huduma hizo! lakini si kwa vipimo vya Mungu!

  Hivyo hebu tuwe na macho ya Rohoni na waangalifu tunapoangalia huduma au kitu chochote ambacho kinafanyika katika Jina la Bwana, kwani mafanikio katika macho ya kibinadamu huweza kuwa tofauti kabisa na mafanikio katika vigezo anavyotumia Mwenyezi Mungu!

 88. Ben bela na Ruge,

  Nadhani sihitaji “KUFUNGUKA” ili nijue siri ya Efatha! Bwana alinifungua nikajua “SIRI” kuu ya Mungu yaani Yesu Kristo! Ambaye alikuja katika mwili, akadhihirisha matendo makuu ya Mungu, akafa kwa ajili ya dhambi zangu! Akafufuka, na sasa amekaa mkono wa Kuume wa Mungu Baba akiniombea! Na alimtuma Roho wake mtakatifu ambaye anatuweka kwenye Kweli Yote! Sihitaji “kufunguliwa” na “Mtume” au “Nabii” Aliyenifungua alikiondoa kiambaza cha kati kinachonitenga na Mungu!Akanihamisha kutoka katika nguzu za giza na kuingia ufalme wa pendo lake! amenipa uwezo na ujasiri wa kukiendea kiti cha rehema, na kupangia patakatifu pa patakatifu pake kwa njia ya damu yake iliyonitakasa!Na ameniambia mimi ni Hekalu lake, ambapo Roho wa Mungu anakaa ndani yangu! Amenipa NENO lake ambalo ni Upanga wa Roho! Na kila silaha ya kuweza kuziangusha ngome! Ameniambia wazi Hakuna hukumu juu ya walio katika Kristo Yesu! Na ameniambia wazi kuwa hii ndio KWELI YAKE! Wala nisisikilize Injili Nyingine! Roho Nyingine, au Yesu Mwingine! Na hata akija malaika akahubiri kinyume cha hayo na alaniwe!

  Sasa ndugu zangu kweli nahitaji tena huduma ya “EFATHA” Nyingine katika maisha yangu! Sihitaji msingi mwingine ujengwe katika maisha yangu zaidi ya ule alioujenga Mwenyewe Bwana! Ni kwa Yeye nitasimama, yeye ndie Mwamba na salama! Si “ministry” wala “mtume” au “nabii” atakayesimama kati yangu na KRISTO! Mbarikiwe!

  Naomba Bwana awafungue macho kuliona hili!

 89. Bwana Yesu apewe sifa

  Kila mahali pana mapungufu. Pamoja na kufanikiwa kwaa huduma hiyo, wengine tumeshuhudia mapungufu pia kwenye huduma hiyo hiyo. Bora tumwiniue Yesu kwani kwa kumsifia sana Mtumishi wa Mungu watu wachanga ndani ya wokovu wanapata shida. Na hata wakati mwingine wanashindwa kwenda mbele za Mungu pale wanapokuwa na tatizo badala yake wanapeleka tatizo kwa Mtumishi. Vitu vingine vina madhara vinapozidishwa miongoni mwa wanadamu tukizingatia katika kukulia wokovu tuko madaraja tofauti.

  Tumwinue Yesu!!!!

 90. Ruge nipo pamojana wewe, asante kwa kumjibu Orbi, kwani hilo jibu linajitosheleza.
  Mimi mwenyewe ni shahidi wa kile nilichokipata efatha na ndio maana nasema hivyo. Orbi funguka uweze kujua siri ya efatha kuhusu huduma yake. Bwana yesu akusaidie, Ameni.

 91. Mungu akubariki baba yangu wa kiroho mtume na nabii Josephat Mwingira……… Mungu akutunze kwaajili ya kazi yake.

 92. mimi nipo ndani ya huduma ya Efatha na nampenda Yesu na baba Mtume Mungu ameniinua kupitia yeye!

 93. Muheshimiwa na nabii,

  Amani ya Bwana wetu yesu iwe pamoja nanyi
  Mukubwa nimependelea tujadiliane mara kwa mara
  sisi tuna patikana congo/GOMA ila tumekuwa sehemu nyingi sana utusaidie baba

  Mtumishi Michael AKILI BONGANWA( 00 243 99 77 15 419,
  00243 53 42 446)

 94. Muheshimiwa prophète na nabii josaphat mwingia, sisi watu wa Congo tunayo furaha ya kuweza kujadiliana pamoja nawe kupitia barua ndogo hii,
  Kama vile Mungu anavyo kutumikisha tumeomba Mungu sana ilisikumoja tuweze kujaliwa neema ya kuonaana pamoja nawe,mutumishi wamungu Aviateur anapatikana arusha ndiye ametuzungumzia kupitia wewe na hata aka tupatia ma vitabu vyenu na tayari tume visoma sana hata usiku kama vile mchana tuna lia kwa Mungu atusikilie huruma sikumoja tusaidiwe na wewe.
  Tunakuwa na kanisa nyingi congo tena zinaendelea sana ila tunayo shahuku tusaidiwe nanyi

  kaniaba ya kanisa zote tumesema aksante
  Mtumishi MICHAEL AKILI

 95. 1Nyakati 20:20…mwamini nabii ndipo utakapofanikiwa…hakuna budi kukisifia na kukitukuza kile unachokiamini…kwa kuwa kama unaamini Mungu ndiyr atendaye kazi ndani ya mtu na wewe humuoni Mungu, utashangilia huyo mtu, maana iwapo ni kwa neema lakini walioitwa ni wengi na waliochaguliwa ni wachache…ni kuchaguliwa inahitaji mtu ajikane mwenyewe na ajinyenyekeshe ili kutumiwa na Bwana Yesu…hivyo kama ni kumsifu mtu katika Bwana Yesu Mtume Paulo anasema hakuna tatizo, alimradi Kiongozi si kipofu na watu si vipofu kuweza kutumbukia shimoni.
  Hata watu walipokufa siku ile mbele ya Musa ardhi ilipopasuka, hawakusema Mungu ameua watu, walisema Musa ameua watu. Walipopita katika bahari Nyaraka za Injili zinatafsiri kuwa Musa akabatizwa na watu wake.
  Kazi iliyo kubwa ni kumwamini yeye aliyetumwa na Yeye(Bwana Yesu) maana kwa uelewa wangu wa kibiblia katika nyakati zote za Mitume na Manabii iwapo walikuwa wengine lakini kuna aliyetembea na Neno la Mungu kipekee..kumbuka Mikaya na wale manabii 450, Eliya na wale manabii 400,…Miriam na Haruni walikuwa manabii wa Bwana lakini soma vizuri Hesabu 12 kwanini |Miriam aliondoka na ukoma mbele za Bwana.

  Ijapokuwa kuna waalimu elfu, hakuna mababa elfu, ni mmoja tu kwa kila wakati! Tutakapotambuana katika Mungu, tutakuwa tumepona, maana tutaelewa ni nani anabeba Neno la Mungu kwa wakati huo na tutamshinda shetani maana tutatambua Mungu anataka tufanye nini wakati huo kama kanisa ambalo ni mwili mmoja.

  Nabii Mwingira hatukuzwi, lakini kinatukuzwa kilicho ndani yake ambacho ni Roho wa Mungu.

  Acha mashaka na Neno la Mungu, mtawatambua kwa matunda yao…anachosema, kikiwa ndicho anachotenda, mashaka ya nini? Hata zamani, akiinuka nabii, kisitokee kile alichotabiri wanampiga kwa mawe, kikitukia, ni kweli ametumwa na Bwana.

  Nabii Mwingira, ninaheshimu ulicho nacho na ninakuheshimu nawe. Fanya kazi, usituangalie mashabiki.

 96. Msimamo wangu kwako Ben-Bella na watu wengine ni ule ele tu, Kuwe waangalifu kwa sifa mnazomwaga kwa watumishi!Haziwajenge!zaidi zinaweza kuwabomoa!Na pia angalieni msije jikuta “MNAMTEGEMEA YESU KWA KUPITIA MWANADAMU” kwani biblia imesema ole!Hivyo Angalieni siku moja msije kawa “disappointed” Kwani ni Yesu anayestahili sifa na Heshima kuu, Hatuombi hayo, ile nawatahadharisha tu!

  Mbarikiwe.

 97. Nawaombea watumishi wa Mungu wa Efatha wakiongozwa na Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira kwa kujitoa kwa ajili ya kazi Mungu Baba, Kwani hii kazi ni ngumu sana lakini wamekua wakitoa kuwafundisha watu mafundisho ya kukulia wokovu kwa kujitoa sana. Hivyo Mwenyezi Mungu awabariki sana awape nguvu za kufanya kazi hii hata lile kusudi alilotumwa Mtume na Nabii likapate kutimia kama alivyoagizwa na Bwana Yesu. AMENI.

 98. Furaha, Tuli Mkayula na wengineo……

  Si vibaya mnavyofanya kumpongeza na kumuenzi ndugu Mwingira…… Lakini kwa Mkristo anayesoma Biblia anabidi awe mwangalifu mno! Hali hii ilitokea katika kanisa la Wakorintho na Paulo akawaona ni watoto wachanga…… na bado hawajamjua Mungu……kwa kifupi ni dalili ya utoto uchanga kiroho unapomuenzi binadamu hata atumiwe na Mungu kiasi gani! Nadhani ni PAULO alipofanya muujiza kwa kumponya mtu kule Greece,Wayunani walikuja na kutaka kumtukuza na kumwabudu,Nini alichokifanya……alichana chana mavazi yake na kuwazuia! na hata Petro alifanya hivyo.

  Kwa watu wanaomjua Mungu,wanafahamu wazi kuwa hata mtu atumiwe na Mungu kiasi gani, anabakia kuwa binadamu!hawabadiliki hali ya kuwa kati Binadamu na Malaika, au kati ya Malaika na Mungu!Tumeona kwa Musa, Daudi,Suleimani na pia Tumeona kwa Petro maana hata akiwa ni Mtume ayejazwa na Roho Mtakatifu, bado Paulo alimkemea alipoenda kinyume cha Injili! Na hata pia Paulo Mwenyewe kuna mafundisho ya Imani yalikuwa yakimtatiza ilibidi arudi Jerusalemu kupata ufafanuzi! na hata kusema anaogopa akisha hubiri Injili asije kataliwa!

  Kwa kifupi we do more harm tunapomwaga sifa badala ya kuzitoa kwa Yesu! Na yeye ni binadamu Je sifa hizo zikimwingia akajiona yeye ndio yeye itakuwaje? Unajua ni dhambi gani ambayo ndugu Mwingira anashindana nayo? Jifunzeni kumwombea! sio kumwaga sifa ambazo hatujaona mtumishi wa Mungu katika agano Jipya akimwagiwa.

  Walikokoka Tanzania miaka ya nyuma wanajua ni sifa gani walizokuwa wakimwagiwa akina Mzee Kulola, Lazaro na wengineo, Kila mtu anaweza kutafsiri historia anavyoona, lakini ushabiki, majigambo kwa waumini juu ya viongozi wao na hata juu ya Dhehebu lao,na kuwa huyu mtumishi anatumiwa na Mungu kuliko huyu, huyu ndiye aliyetupa Bwana nk uliligawa kanisa! ikawa ni doa katika historia ya wokovu Tanzania! kama hatuwezi kujifunza toka kwenye Biblia basi hata tujifunze kwenye matukio ya kila siku!

  Mbarikiwe

 99. I LOVE YOU APOSTLE AND PROPHET JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
  MAY GOD BLESS AND INCREASE YOU IN UPPER AND LOWER CASES!

 100. mtumishi wa mungu kwanza nikupongeze kwakua mtumishi mwenye nguvu ya mungu pili nauliza mbona bukoba umeisahau?

 101. John Paul, Mungu akubariki sana, Asante sana kwa maswali uliyomuuliza ndugu Andongwisye Mwasakapwela, mimi binafsi napenda kumshauri ndugu Andongwisye ni vizuri sana kusoma na kuyaelewa maandiko, ili isije ikamletea shida kwa sababu watu walio wengi wanaingia kwenye mambo ambayo hawayajui, neema bado ingalipo, Jaribu kujua imani yako unayoisimamia, mwanadamu anatakiwa kujua kweli nayo kweli itamweka huru, achana na mambo ya kurithi dini hayo hayatakupeleka popote,Kwa mtazamo wa haraka haraka hapa kulingana na maswali yako inaonekana kabisa kama unayumbishwa na imani zaidi ya moja,kaa kwenye msitari ndugu yangu,
  Karibu tunajifunza.

 102. shaloom mtumishi,mungu akubariki sana mtumishi.kusudi ulilo pewa na Mungu litimie,maana nasi twasema TUMEPATA URITHI MWEMA.

 103. GODBLESS YOU THE MAN OF GOD.LET THE LORD JESUS CHRIST BE WITH YOU TO THE REST OF YOUR LIFE AND MAY YOU ACCOMPLISH THY PLAN OF GOD TO THE EXCELLENCE. AMEN.

 104. i agree with you Charles that Apostle Josephat Mwingira should be placed in Youtube Technology so that people around the world could hear the good news of the gospel of Jesus and be saved!

 105. mungu aendelee kukulinda mtumish wake ili uzid kutuponya wana wake bwana akubaliki sana pasiwepo na ibilisi wa kukujalibu maana shetani anakuwinda nasi tunasema tutazidi kukuombea maana neno la mungu linasema msiache hata kondoo mmoja akapotea ukipotea wewe je! sisi kondoo wa mungu tutakuwaje

 106. Shalom!
  I would like to congratulate and thank our Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira for his dedication towards the work of the Lord.
  Had it been it was somebody he could have left the ministry on the way because he is carrying a very heavy load for us his children.

 107. I know Bishop Elias Mwingira is a big blessing to any that is devout to the truth. I am in Kenya. Ni Ombi nafanya.
  Ninaomba Mtume awezekuwekwa kwa Youtube techonology. The world will behold God’s Great anointing at work.

  Amen.

 108. shalomu mtume na nabii Josephat Mwingira.Nakushukuru kwa kutufikishia kusudi ulilopewa na MUNGU,Taveta KENYA.Nimengi yanatendeka kwa jina la YESU KRISTO

 109. Hallelujah wapendwa!!

  Nimevutika kurudi tena katika huu mjadala.
  Kuna tatizo kubwa sana kwa ‘WAKRISTO WA DINI’ wengi hawana muda wa kutafuta ukweli kuhusu kusudi la Yesu, wengi wanaamini viongozi wao kuliko kutafuta ukweli katika neno. Kwa kweli maombi yanahitajika wafunguliwe.

  Hivi kweli mkristo anadhubutu kusema

  1.Masister, Mapadre , Maimamu na Masheikh ndiyo waliowekwa kwa msingi wa Maandiko, Yapi?

  Hajasoma Waefeso 4;11
  ‘Naye alitoa wengine kuwa Mitume, na wengine Manabii, na wengine kuwa Wainjilisti,na wengine kuwa Wachungaji na Waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke na mwili wa Kristo ujengwe’

  Swali
  -Masheikh, maimamu na hao wengine wanaujenga mwili wa nani na kwa kusudi lipi?
  -Anapingana na mamlaka / huduma ambazo Mungu aliziteua? kwa kupenda kusikiliza maneno na madaraka ambazo watu wamejitungia?

  2.Anadhubutu kuamini uwezo wa shetani (waganga, wapiga ramli) na kutilia shaka uwezo wa nguvu za Yesu katika kutenda kazi (miujiza).Hii ni hatari hata kuendelea kujiita mkristo wakati humwamini na unamdharau na hutaki kufuatilia kwa umakini habari zake.

  Hajasoma;
  Marko 16;17
  ‘Kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya…….. wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya’

  Kwa kweli ibilisi anapofusha sana watu anawafanya wawe watumwa wa taratibu za dunia hii, Mungu si mjinga hata aseme jambo halafu apingane nalo. Tukitaka kupata ukweli kuhusu mambo ya Mungu ni kumtafuta kwa bidii na kupitia neno.
  Huwezi pata ukweli kuhusu nguvu za Mungu kwa watu ambao hawamwamini wala kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao.

  Yohana 12;37-
  ‘Walakini ijapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini ili litimie lile andiko la nabii Isaya alilosema , Bwana ni nani atakayesadiki habari zetu. Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Ndiyo sababu hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema, Amewapofusha macho, amaifanya migumu mioyo yao’

  3. Tena anasikitika watu wanapungua misikitini na makanisani; wakati hilo ndilo kusudi la injili ya Yesu iletayo wokovu ‘kuja kurudisha kilichopotea na kuwapa watu uzima kisha wawe nao tele’

  ‘INJILI YA KWELI ITAENDELEA KUHUBIRIWA, MUNGU ATAZIDI KUINUA WATUMISHI WAKE NA WENGI WATAZIDI KUOKOLEWA’
  Bwana Apewe sifa

 110. Mpendwa Oswine,

  Sifa utukufu na Heshima ni Mungu anayesitahili. Nashukuru kusikia kuwa kuna kitu umejifunza, hili limenitia moyo maana toka nilipochangia mada hii sikuwahi kupata mwitikio wa aina yoyote ile, hata pale nilipoomba ufafanuzi pia sikujibiwa, lakini kuandika kwako kunanifanya nimshukuru Mungu kwa kutambua kuwa watu wanausoma mchango wangu na wengine kujifunza kitu.

  Mungu akubariki, tuzidi kujifunza.

  Shalomu

 111. Hallelujah!!

  Napenda kumtukuza Mungu kwa namna ya kipekee Apostle Mwingira na C. Mwakasege kwa kweli ni miongoni mwa watumishi wenye uchungu na ujasiri wako kupambana dhidi ya kazi za Ibilisi kama unyonge, hofu ,dhuluma, ujinga na umaskini kwa watanzania wanatutia nguvu sana, hakika mnatufungua wengi siku hadi siku

  Kwa macho yangu na maskio yangu nimewahi kusikia akitoa UNABII kadhaa ambao umekuwa UNATIMIA kwa nchi yetu jambo hata mimi mwanzo nilikuwa siamini, ujasiri wake ni wa ajabu, pia wote hawana ubaguzi.

  Mwalimu Mwakasege ni zaidi ya mwalimu, hakika nimekuwa nikiimarika kiroho kwa mafundisho yako, moyo wako na kiu yako kulisha kondoo wa Yesu ni ya kipekee mno.

  Msichoke watumishi wa Mungu ambao kweli mmekubali kutumika kuihubiri Injili ‘WAKATI UNAOFAA na USIOFAA kuhakikisha watu wanakombolewa kiroho na kiakili.

  Tunazidi kuwaombea na ninawasihi wapendwa kila siku hata kwa dakika moja muwe mnawaombea watumishi wa Mungu. Kweli kuna watumishi wa Mungu kweli wamejitoa kufa na kupona bila kujali hatari na vita wanayopambana nao, tuwainue mbele za Bwana naamini nchi yetu inaweza kupona.

  Mbarikiwe mno

 112. Mr.Asheri
  Mungu akubariki sana maneno yako
  yalinijenga sana!!!hakika nimejifunza mengi.

 113. MUNGU AKUBARIKI SANA BABA APOSTLE AND PROPHET JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
  NAKUPENDA SANA.
  MUNGU AKUTIE NGUVU KILA SIKU.
  SONGA MBELE BABA,NIPO NAWE.

  EFATHA – FUNGUKA

 114. Neno la Mungu linatuambia ya kwamba tunapoliamini Neno la Bwana kupitia vinywa vya Manabii wake,hakika tufanikiwa. Hongera Mtumishi wa Bwana, Mtume na Nabii Mwingira, kwa kukubali kuwa kinywa cha Bwana, kwani kupitia Huduma uliyopewa, wengi wamefunguliwa, wanafunguliwa na wataendelea kufunguliwa. Mungu akutie nguvu baba, ufanye kazi yako kwa Uaminifu na uadilifu pasipo kuchoka.

 115. mimi naomba kwanza niwatie moyo wapendwa mliomwelewesha ndugu Andongwisye. mimi kidogo napata mashaka kwake maana sielewi yuko upande gani, wa kristo au au ule mwingine? maana anajikanyaga kanyaga tu. ninawaombea ili roho wa kristo aendelee kuwapa hekima ya kuendelea kumsaidia pia nayeye pia ufahamu wake ufunguke ili aijue na kuijia injili ya kweli,

 116. Mimi Pia ningependa kujua machache juu ya maelezo yako Ndugu Andongwisye Mwasakapwela. Umetaja kuwa

  “Ni kupitia utaratibu huo huo, hivi sasa tuna Masheikh, maimamu, ma-Ustaadh na kadhalika. Ni katika mfumo huo huo ambapo tuna Wachungaji, Mapadre, ‘Masister’, ‘Mafather’ na wengineo wengi kulingana na imani ya watu fulani katika jamii husika.

  Hawa ndio ambao kwa mujibu wa maandiko matakatifu, walitakiwa kuwa watetezi wa nguzo kuu za imani, wasimamizi wakuu wa kuhakikisha maamrisho ya Mungu yanatekelezwa, viongozi wa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wanairekebisha jamii pale inapoonyesha kuanza kupotoka, wanaharakati wakubwa wa kupenyeza imani za kidini katika mioyo ya watu, ili kuwafanya wahusika kuishi na imani hizo na kumshinda shetani.”

  Ningependa kufahamu vitu hivi:
  1. Hayo maandiko matakatifu unayosema hapa ni yapi?
  2. Una maana Masheikh, wachungaji, mapadre, masister, mafather n.k wanafanya kazi ya Mungu yuleyule?

  Natumaini utanijibu maswali haya, jumlisha yale aliyokwisha uliza ndugu John hapo Juu!

 117. Ndugu Andongwisye Mwasakapwela,

  Umeandika mambo mengi mazuri sana katika maelezo yako hapo juu. Lakini katika kuelezea baadhi ya mambo mimi sijakuelewa na kuna maswali mengine ambayo umeyauliza yanakuwa kama yanaulizwa na mtu ambaye ama haamini au hafahamu kikamilifu habari za utendaji kazi wa jina la Yesu Kristo.

  Kwamba unaamini au huamini katika utendaji kazi wa jina la Yesu Kristo, kwamba unafahamu au hufahamu kukamilifu habari za Yesu Kristo siyo lazima kusema kwa sasa, litajulikana wakati tunaedelea kujadili hapa. Kwa kuwa hapani darazani, ni mahali pakujifunza habari za Ufalme wa Mbinguni. Ninachotaka kukuuliza kwa sasa ni maswali yaliyojitokeza katika maelezo yako, ambayo mimi nayaona kama ni ya mtu asiyemwamini au hafahamu kwa ukamilifu habari za Yesu Kristo.

  Maswali yenyewe ni haya hapa:

  1.Kuna mahali umeandika hivi “….kinyume na maandiko wanayoyatumia katika kutuhubiria makanisani na misikitini, na kwa hakika kinyume hata na jinsi nafsi zao zilivyotakiwa kufanya.”
  Swali: Je, unadhani mahubiri ya makanisani yanafanana na ya misikitini hata ukaamua kuyaweka katika mada moja?

  2.Umeandika mahali fulani hivi: “Nadiriki kusema kuwa ndio maana hata idadi ya watu wanaohudhuria makanisani au misikitini imepungua kwasababu ndani ya majumba hayo naamini bila ya Yesu, miujiza haiwezi kutokea.”
  Swali: i). Misikitini huwa kuna Yesu pia?
  ii). Misikitini pia hutokea miujiza? (kama jibu ni ndiyo, miujiza hiyo hutokea kwa nguvu ipi?)

  3.Umeandika: “Wala sio jambo la kushangaza kabisa, kusikia wahubiri hao hao baadhi yao wakihanikiza kuwa wana uwezo wa kuponya hata UKIMWI, lakini hakuna ambaye anaweza kutuonyesha takwimu halisi za kisayansi kuwa ameshawahi kuwaponya watu wangapi ugonjwa huo, na uthibitisho juu ya hilo.”
  Swali: Tofauti na uthibitisho wa vipimo kwamba mtu aliyekuwa na HIV na baada ya maombezi akapimwa na HIV kutokuonekana tena ni takwimu gani zingine halisi za kisayansi na uthibitisho juu ya ya hilo unaouhitaji?

  4.Umeandika pia hivi: “Ndio huku huku katika makongamano hayo ambako watu hutolewa majini, hutolewa mashetani, hutolewa mapepo wabaya, huponywa kwa miujiza ya kuombewa dua ambazo hata hao wanaozitoa, ukiwaambia wazirejee tena wanashindwa maana hazijulikani kuwa ziko katika lugha gani. Ndio wapo hawa, ambao inafkia hatua ambapo lugha wanayoongea inakuwa haieleweki nadhani hata kwao binafsi.”
  Swali: Unaamini juu ishara alizozisema Bwana Yesu kwamba pamoja na kutoa pepo na kuweka mikono juu ya wagonjwa nao wakapona Wamwaminio Yesu pia WATANENA KWA LUGHA MPYA? [Mark 16:17]

  5. Pia umeuliza hivi: “Hivi ni nani anaweza kututhibitishia kisayansi kuwa hayo madudu wakati yanatoka tendo hilo linaambatana na maumivu ya mtu kutaka kulia machozi ya damu?”

  Mimi najibu swali hili kwa kutumia swali jingine kwamba: Hivi ni nani awezaye kututhibitishia kisayansi juu ya uwepo wa Ulimwengu wa roho?

  Ukweli ni huu: Vitu vyote vilivyo katika ulimwengu wa roho pamoja na Mungu Jehova mwenyewe, Malaika, Mbinguni,, nk, haviwezi kuthibitishwa kisayansi kwamba vitu hivi vipo. Lakini kama una mtu unayemfahamu anayeweza kuthibitisha KISAYANSI kwanba kuna viumbe vinaitwa MAJINI natumaini ukimuona huyo atakuthibitishia pia kwamba wakati pepo mchafu anapomtoka mtu tukio hilo huambatana na maumivu ya aina mbali mbali.

  6.Mahali pengine umeandika hivi: “wanachokifanya ni kitu ambacho hata wao wenyewe hawawezi kukithibitisha kisayansi, isipokuwa kwa nguvu za ki-giza giza tu. Ndio, kuna tofauti gani kati ya watu hawa?”
  Swali: i).Kwa kutambuwa uwepo wa nguvu za ki-giza giza Je, unatambuwa pia kwamba kuna nguvu za ki-nuru nuru?
  ii). Kama unatambuwa kuwepo kwa nguvu za nuru, Je, unaamini pia kwamba kuna miujiza inayofanywa na nguvu za nuru isiyoweza kuthibitishwa kisayansi?

  7.Umeandika tena hivi:
  “Lakini haiyumkiniki kuwa katika baadhi ya nyakati, watu wamekuwa wakifanyiwa hivyo na kisha baadae wakakutwa tena wako katika hali yao ile ile iliyokuwa ikiwakabili na kisha mkimuuliza aliyemfanyia maombezi atawajibu “HUYO HAKUAMINI KATIKA JINA LA BWANA”. Sasa swali la kujiuliza hapa ni kuwa, je, kilitakiwa kwanza kipi kati ya haya mawili? Kumpandikiza imani ya kumwamini Mungu, au kumpandikiza miujiza ya muda ambayo naamini ni kwa ajili ya kumuogofya na hali fulani?”

  Yawezekana ni kwa kutoelewa au kutoelewa, watu wengi wamekuwa wakihitaji uponyaji tu kutoka kwa Yesu lakini wakiwa hawako tayari kumpokea Yesu ili akae moyoni na hivyo kuwa na kinga ya kudumu juu ya mashambulizi ya mapepo na majini. Hawa ndio watu ambao baada ya kuombewa na mapepo kutoka kurudia mwenendo wao mbaya wa maisha ya gizani, pasipo Nuru ya Neno la Mungu. Ni kwa sababu ya watu wa namna hii Bwana Yesu alisema katika Mathayo 12:43-45 kwamba: Pepo mchafu amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka, hata akija, aiona tupu, imefagiwa na kupambwa. Mara huenda akachukuwa pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo, na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.

  Mtu akishaombewa na pepo kutoka anatakiwa amkaribishe Yesu Kristo moyoni mwake ili pepo akirudi akute moyo hauko tupu bali Yesu amejaa. Kitakachofuatia hapo ni pepo kugeuza na mtu huyo huendelea kuwa salama pamoja na Yesu Kristo!

  Vile vila suala la Imani ni kwamba Mtu hawezi kupandikizwa Imani bali huamua mwenyewe baada ya kulisikia Neno la Kristo na kulikubali. [Rum 10:17]. Hakuna imani ya kupandikizwa! Na kama unaifahamu kuwepo mahali fulani hiyo si imani tena bali ni KUTEKWA FAHAMU.

  8. Ninamalizia katika mahali ulipoandika hivi: “Je, hivi Mungu ndio aliagiza kuwa watu wawe wanatengwa kwa makundi fulani fulani? Mbona alisema kuwa tupendane daima na tuwapende hata maadui zetu? Mbona nyie mnawakataza hata waumini wenu kuwatembelea waumini wa madhehebu mengine?”

  Ndugu Andongwisye, Neno la Mungu linasema katika 2Korintho 6:17 kwamba: ‘Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana. Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu”. Haya ni maneno ya Mungu mwenyewe akiwaambia watu wamchao. Wanadamu wamegawanyika katika makundi mengi tofauti tofauti. Yapo makundi ya watu wanaomcha Mungu na yapo makundi ya watu waovu. Kwa hiyo kama kuna kundi linalifahamika kabisa kuwa ni la watu waovu, kujitenga na kundi hilo ni suala la kibiblia kabisa. Ni maagizo ya Mungu mwenyewe. Siku hizi kuna madhehebu mengi ambayo wanajiita tu kuwa ni waumini wa Yesu lakini maisha yao na matendo yao yanapingana na maneno yao. Hawa nao wamo katika kundi la watu ambao mtu mcha Mungu ni lazima kujitenga nao.

  Kumpenda adui si lazima ushirikiane naye. Upendo kwa aduwi ni kitu kitakachoweza kukupa msukumo wa kumuombea kama alivyoagiza Bwana Yesu katika Mathayo 5:44 akisema ” Lakini mimi nawaambia, Wapendeniadui zenu, waombeeni wanaowaudhi,”.

  Pia katika 2Korintho 6:14 tunaambiwa kwamba: “….Tena pana ushirika gani kati ya nuru na giza?” Kwa hiyo kama tofauti iliyopo kati ya makundi hayo [fulani fulani] ambayo watu wanatengwa ni kama tofauti iliyopo kati ya nuru na giza basi kutengana huko hakuwezi kuepukika.

  Ninaishia hapa kwa sasa. Kuna maswali amabayo nimekuuliza, kwa upole na unyenyekevu, na ningependa sana kama utayajibu ili kwa pamoja tuendelee kujifunza.

 118. SINA uhakika kama marehemu Vivian Tillya, aliwaona hawa wakati alipokuwa akitunga wimbo wake wa SIWAELEWI, kwasababu hawa nao hivi sasa wamekuwa katika kundi hili hili la hawa wasioeleweka. Nawazungumzia watumishi wa Mungu, wa madhehebu mbalimbali, nchini Tanzania na bilashaka duniani kwa ujumla.

  Nakumbuka zama zile wakati naanza kujifunza masuala ya dini, nilikuwa naambiwa kuwa, zamani za kale, kulikuwa na watu alikuwa wakiitwa Manabii na Mitume. Kwamba hawa walikuwa wateule wa Mungu, katika kuufikishia umma wa Wana-dunia, ujumbe, maamrisho, malekezo na utashi wa Mungu, katika wajawake.

  Kwamba, walikuwa watu ambao waliagizwa kuja duniani kutupatia na kutuelkekeza namna ya kuyafuatisha maandiko matakatifu, ambayo yalikuwa ni maagizo au malekezo ya kutoka kwa Mungu, kwenda kwa kiumbe alichokiumba, akikiusia namna bora ya kuishi humu duniani. Kwamba walikuwa wakizunguka sehemu mbalimbali duniani kutoa maelekezo hayo kwa kadiri Mungu, huyo huyo alivyowajaalia.

  Kwamba watu hawa ambao walikuwa katika baadhi ya nyakati wakiwasiliana na Mungu, kwa namna moja ama nyingine, akiwapa miongozo na ujumbe wa kuwaletea waja wake. Kwamba katika baadhi ya nyakati walikuwa wakikumbana na majaribu mbalimbali kiasi cha kumwomba Mungu, awaepushe na majaribu ya namna hiyo.

  Kwamba katika baadhi ya nyakati walikuwa wakikutana na waja wa Mwenyezi Mungu, wenye matatizo na kisha wakamwomba Mungu awashushie baraka zake na hakika hali ikawa hivyo kwa walioshushiwa baraka hizo wakapona, au kuondokana na matatizo yaliyokuwa yakiwakabili kwa namna moja ama nyingine.
  Sikumbuki kama niliwahi kuambiwa kuwa watu hawa walikuwa na uwezo wa kutenda miujiza, sikumbuki kama niliwahi kufundishwa au kuelezwa kuwa walikuwa wameletwa duniani ili wawe matabibu, wapiga ramli, waganga wa kienyeji au madaktari wa miujiza.

  Hawa ndio waliokuwa Mitume au Manabii, wa enzi hizo, ambao walitumwa na Mungu, na ambao kwa kuwa kanuni ya Mungu ni kuwa binadamu hatoishi milele humu duniani, kila ilipokuwa inakaribia wakati wao wa kurejea kwa udongo, basi walijitahidi kuona wanaacha watu ambao watakuwa viongozi katika mwendelezo wa yale waliyokuwa wametumwa na Mungu kuja kuyafanya duniani.

  Ni katika utaratibu huo huo, ambapo viongozi mbalimbali wa kidini walikuwa wakipatikana, lengo likiwa ni kwa watu hao kuja kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa maandiko, maamrisho na miongozo mbalimbali ambayo Mungu alitaka iwe, inakuwa hivyo kama alivyotaka yeye.
  Ni kupitia utaratibu huo huo, hivi sasa tuna Masheikh, maimamu, ma-Ustaadh na kadhalika. Ni katika mfumo huo huo ambapo tuna Wachungaji, Mapadre, ‘Masister’, ‘Mafather’ na wengineo wengi kulingana na imani ya watu fulani katika jamii husika.

  Hawa ndio ambao kwa mujibu wa maandiko matakatifu, walitakiwa kuwa watetezi wa nguzo kuu za imani, wasimamizi wakuu wa kuhakikisha maamrisho ya Mungu yanatekelezwa, viongozi wa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wanairekebisha jamii pale inapoonyesha kuanza kupotoka, wanaharakati wakubwa wa kupenyeza imani za kidini katika mioyo ya watu, ili kuwafanya wahusika kuishi na imani hizo na kumshinda shetani.
  Hata hivyo, licha ya ukweli huo (kwa mtazamo wangu lakini), hali imekuwa kinyume na hivyo, kinyume na inavyotakiwa, kinyume na Mungu alivyotaka, kinyume na walivyokuwa wakifanya Mitume na Manabii, kinyume na maandiko wanayoyatumia katika kutuhubiria makanisani na misikitini, na kwa hakika kinyume hata na jinsi nafsi zao zilivyotakiwa kufanya.
  Katika miaka ya karibuni, dunia ikiwa inashuhudia mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, hasa katika upande wa mawasiliano, wafuatiliaji wa masuala mbalimbali ya kijamii katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano, watakubaliana nami kuwa masuala ya dini ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakipewa uzito wa aina yake katika vyombo mbalimbali vya habari, bila kujali kuwa ni kwa ubaya au uzuri wake.
  Ni kupitia njia hii hii ambako nami nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu makongamano mbalimbali ya kidini, ingawa nimekuwa nikiona baadhi ya mambo yanayofanyika huko ni kinyume kabisa na maandiko yale yale ambayo sote tunajua kuwa yametoka kwa Mungu.

  Limekuwa ni jambo la kawaida kabisa hivi sasa, na kimsingi hata wengi wanaoyahudhuria ndio wanalokuwa wakilitarajia, kuwa makongamano mengi yamekuwa makongamano ambayo sio kwa ajili ya mafundisho ya neno la Mungu, bali makongamano kwa ajili ya mchungaji au mhubiri fulani kuonyesha miujiza ya uponyaji wa watu wenye matatizo lukuki.
  Nadiriki kusema kuwa ndio maana hata idadi ya watu wanaohudhuria makanisani au misikitini imepungua kwasababu ndani ya majumba hayo naamini bila ya Yesu, miujiza haiwezi kutokea. Bila ya usafi wa nafsi ya mhubiri hakuna muujiza unaoweza kutokea, bila ya imani ya kweli kwa anayemjua na kumjali Muumba wake, hakuna miujiza inayoweza kutokea.
  Kinyume chake, makongamano ndio ambayo yamekuwa yakijaza watu kupita kiwango, bilashaka kutokana na ukweli tu kuwa ni katika makongamano hayo tu ndio miujiza huweza kufanywa na wahusika ambao hata katika mabango ya matangazo kuhusu semina, makongamano au warsha zao za neno la Bwana, huhanikizwa kwa ukubwa wa maajabu na miujiza itakayojiri.

  Si jambo la kushangaza hivi sasa, kumwona mtu ameandaa kongamano la neno la Bwana, lakini akifika pale, hata kabla ya kusalimia waliohudhuria katika jina la anayemwamini, anaanza kwa kuwahitaji wale wote wenye matatizo kujitokeza mbele. Cha ajabu unaweza kukuta waliojitokeza wote ni watu ambao hata hapo mtaani kwenu hamuwajui, na hata ukifuatilia mitaa ya jirani inayowazunguka pia hamna aliye mkazi wa eneo hilo.
  Wala sio jambo la kushangaza kabisa, kusikia wahubiri hao hao baadhi yao wakihanikiza kuwa wana uwezo wa kuponya hata UKIMWI, lakini hakuna ambaye anaweza kutuonyesha takwimu halisi za kisayansi kuwa ameshawahi kuwaponya watu wangapi ugonjwa huo, na uthibitisho juu ya hilo.

  Ndio huku huku katika makongamano hayo ambako watu hutolewa majini, hutolewa mashetani, hutolewa mapepo wabaya, huponywa kwa miujiza ya kuombewa dua ambazo hata hao wanaozitoa, ukiwaambia wazirejee tena wanashindwa maana hazijulikani kuwa ziko katika lugha gani. Ndio wapo hawa, ambao inafkia hatua ambapo lugha wanayoongea inakuwa haieleweki nadhani hata kwao binafsi.

  Hivi bila kuongea kilatino, kijerumani, kizungu, kiholanzi au hata kimarekani kama kipo, dua haliwezi kusikilizwa? Hivi ni nani alisema kuwa maombezi ya Kiswahili hayawezi kusikilizwa na Mungu? Na Kwanini basi watumie lugha ambayo hata wenyewe baadhi ya nyakati wanakuwa hawawezi kuyarudia maneno hayo kuyatamka ikiwa utawataka wafanye hivyo? Katika hilo nani anayehitaji kuombewa kati ya wawili wa aina hiyo?

  Na kizuri zaidi ni kuwa siku hizi imeshakuwa kanuni. Kwamba siku hizi maombezi, warsha, semina na makongamano yote ya dini hayawezi kuitwa hivyo ikiwa hayatakuwa na kipengele cha miujiza, kipengele cha watu kuitwa na kugaragara kwenye mavumbi kama hawana akili nzuri vile (ingawa baadhi ya nyakati naamini kweli hawanazo), wakililia maumivu wanayoyapata wakati mapepo mabaya yakiwatoka. Hivi ni nani anaweza kututhibitishia kisayansi kuwa hayo madudu wakati yanatoka tendo hilo linaambatana na maumivu ya mtu kutaka kulia machozi ya damu?

  Wahubiri mbalimbali siku hizi wamegeuka waganga wa kienyeji, na ninasema kwa makusudi kabisa kuwa ni waganga wa kienyeji kwasababu ni vitu vya kienyeji tu ambavyo huwa haviwezi kuwa na uthibitisho wa kueleweka wa kitaalamu, wanachokifanya ni kitu ambacho hata wao wenyewe hawawezi kukithibitisha kisayansi, isipokuwa kwa nguvu za ki-giza giza tu. Ndio, kuna tofauti gani kati ya watu hawa?

  Lakini haiyumkiniki kuwa katika baadhi ya nyakati, watu wamekuwa wakifanyiwa hivyo na kisha baadae wakakutwa tena wako katika hali yao ile ile iliyokuwa ikiwakabili na kisha mkimuuliza aliyemfanyia maombezi atawajibu “HUYO HAKUAMINI KATIKA JINA LA BWANA”. Sasa swali la kujiuliza hapa ni kuwa, je, kilitakiwa kwanza kipi kati ya haya mawili? Kumpandikiza imani ya kumwamini Mungu, au kumpandikiza miujiza ya muda ambayo naamini ni kwa ajili ya kumuogofya na hali fulani?
  Wengi wamekuwa wakitumia nguvu za giza katika kutenda haya, nadhani wengi wetu tungali tunakumbuka suala la yule mchungaji mkenya kule Uingereza na nyingine kama hizo ambazo sizikumbuki mimi. Wengi wamekuwa ni watu ambao wanajenga mazingira ya kuwafanya wanaowasilikiza kuwa waoga dhidi yao na sio dhidi ya Mungu wao, matokeo yake ni kuwa kila wanalowaamrisha ndilo wanalifanya…..ndio si wameshapandikizwa mazingira hayo?

  Kila kukicha wamekuwa wakizidi kujenga hofu mpya dhidi ya wanaowapandikiza woga huo, na kujijengea majeshi yao ambayo hatimaye huanza malumbano kuwa mimi ni bora zaidi kuliko fulani. Ndio, tumeyaona haya na wala hawawezi kutubishia. Je, hivi Mungu ndio aliagiza kuwa watu wawe wanatengwa kwa makundi fulani fulani? Mbona alisema kuwa tupendane daima na tuwapende hata maadui zetu? Mbona nyie mnawakataza hata waumini wenu kuwatembelea waumini wa madhehebu mengine?
  Katika masuala ya Muziki, hasa nchini Tanzania, kuna kitu wanakiita MUZIKI WA KIZAZI KIPYA. Na bilashaka kuwa hata katika upande huu wa masuala ya dini, muda si mrefu tutaanza kusikia kuwa kuna DINI YA KIZAZI KIPYA. Dini ya watenda miujiza, dini ya waponyaji, wajenga hofu, wasambaratishaji wa umoja wa mwanadamu. Naam, dini ya MATABIBU WA MIUJIZA, dini ya MASHAHIDI WA SHETANI NA MIUJIZA

 119. Dear Apostle and Prophet Mwingira,
  MUNGU AKUBARI SANA, AKULINDE NA KUKUTUNZA,
  AMEKUINUA KWA TANZANIA ILI TANZANIA YETU IPONE.
  UBARIKIWE.

 120. Shalomu!
  Wapendwa nawasalimu katika Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Kwanza niombe samahani kwa kutokukamilisha kile nilichoanza kwa muda muafaka. Tatizo kubwa nililokumbana nalo ni ufinyu wa muda, hata hivyo namshukuru Mungu kuwa leo nimepata fursa kidogo ndipo nikaona niendelee na mchango wangu ili kuruhusu wengine nao waendelee na hoja hii kama itakuwepo haja ya kufanya hivyo:

  Katika mchango wangu uliopita niliishia sehemu ya KUBADILISHA MAJIRA YA KANISA.

  Nimekuwa nikijiuliza maana ya neno majira kama lilivyotumika kwenye ujumbe huu bila mafanikio. Hata hivyo, nadhani hapa anamaanisha kubadilisha hali au kiwango cha kiroho ndani ya kanisa (kwa maana ya kuleta UAMSHO kwa Kanisa la Tanzania, Afrika na Ulimwenguni mwote)

  Kama nitakuwa nimekosea katika kuangalia neno majira nitaomba kusaidiwa kwa kupatiwa maana halisi. Pamoja na kutokufahamu maana halisi ya neno majira, bado ujumbe mzima unanipa matatizo makubwa sana hasa tunapomzungumzia mwanadamu. Tatizo langu ni juu ya huu unabii kutamka kuwa ametumwa kubadilisha majira ya kanisa, swali ninalOjiuliza ni kuwa nani mwenye kanisa? Je huyo mwenye kanisa anaweza akampa mwingine kazi ya kulitengeneza kanisa? Ni kweli kuwa Mungu amewaweka watumishi wanadamu kwa ajili ya kulijenga kanisa na kuliimarisha, lakini katika mambo yote ni YEYE Mungu ambaye hutenda kazi hizo zote. Biblia inatuonyesha kuwa Kanisa ni mali ya Mungu 1Korintho 1:2 (a), 2Korintho 1:1 na mengineyo mengi. Biblia inasema pia kuwa Yesu ndiye Bwana wa Kanisa na kichwa cha hilo kanisa, Efeso 5:23,25-27. Kristo Yesu ndiye anayewaita watumishi mbalimbali kwa ajili ya utumishi na lengo ni kulijenga kanisa, Efeso 4:11-13, hapa tunaona Biblia inasema kuwa alitoa wengine kuwa mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, waalimu hawa wote wakiwa na jukumu moja la kuhakikisha kuwa kanisa linajengwa. Hapa tunaona kuwa si mtu mmoja au huduma moja inayoweza kulijenga kanisa bali huduma mbalimbali zinahitajika kufanya pamoja.

  Hata hivyo, bado mamlaka ya kanisa ipo mikononi mwa Kristo. Tunaona katika Ufunuo 1:12-20 ambapo Yohana alimwona Kristo akiwa katikati ya vinara saba vya dhahabu ambavyo vilimaanisha makanisa saba na katika Ufunuo 2:1 anasema Yeye aendaye katikati ya vinara saba vya dhahabu, maana yake aendaye katikati ya kanisa jambo linalotuonyesha kuwa Kristo Yesu ndiye mwenye kuliongoza kanisa na kulijenga. Kwa maana hiyo na kwa maoni yangu, haiwezekani mwanadamu kutangazwa kuwa ndiye anayebadilisha majira ya kanisa, hii ni kazi ya mwenye kanisa mwenyewe ambaye ni Mungu katika Kristo Yesu. Ni kweli kuwa YEYE huwatumia wanadamu lakini wanadamu wajapo tumiwa bado wao ni watumwa wasiyo na faida wakitenda yale wayapasayo kuyatenda. Tokea zamani za Agano Jipya haijawahi kutokea Mungu akamtaja mwanadamu kuwa ndiye mwenye majira ya Kanisa. Pamoja na kuwa Mtume Petro alipewa jukumu la kulisha kondoo wa Yesu Yohana 21:15-17 (LISHA KONDOO WANGU) bado hakuwahi kutajwa kuwa yeye Petro ndiye mwenye majira kwa ajili ya Kanisa.

  AMEBEBA MAJIRA MAPYA BEGANI MWAKE…
  Maneno haya ndiyo yanayonipa shida zaidi. Hivi ni nani hubeba majira ya Kanisa? Tunaposema mtu amebeba begani tuna maanisha kitu gani?

  Inapozungumzwa mabega ina maana mamlaka, sote tunafahamu askari huwa na alama mabegani mwao yenye kuonyesha vyeo vyao ambavyo ndiyo mamlaka waliyonayo ndani ya majeshi. Biblia inapotoa unabii juu ya Kuzaliwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo inaonyesha kuwa uweza wa kifalme utakuwa begani mwake (Isaya 9:6). Kwa kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na Mfalme wa Wafalme ni sahihi sana kwake kuwa na uweza mabegani mwake, na hata mamlaka juu ya Kanisa iko mabegani mwake.

  Lakini ujumbe huu unatuonyesha kuwa ndugu Mwingira AMEBEBA MAJIRA MAPYA BEGANI MWAKE, hali inatuonyesha kuwa ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya hayo majira mapya ya kanisa. Hili linaoana sana na yale aliyoyasema kuwa ametumwa kubadilisha majira ya kanisa na kuwa MSIKIENI YEYE. Kama nilivyochangia hapo juu, Kanisa ni mali ya Mungu na anayehusika kulitengeneza kanisa ni Mungu mwenyewe ingawa mara nyingi huwatumia wanadamu, na mwenye mamlaka juu ya kanisa na nyakati za kanisa ni Mungu mwenyewe, ndiyo maana Yesu aliwaambia wanafunzi kuwa si kazi yao kujua Nyakati wala Majira ambayo Baba (Mungu) ameyaweka katika mamlaka yake mwenyewe (Matendo 1:7). Kusema kuwa Mwingira amebeba majira mapya kwa ajili ya Kanisa si sahihi kwani mwanadamu hawezi kubeba mamlaka juu ya kanisa, mamlaka hiyo inabakia kwa Mungu mwenye wivu ambaye hawezi kumpa mwingine utukufu wake.

  Sote tunafahamu kuwa Kanisa limejengwa juu ya msingi wa Mitume na Manabii na Yesu mwenyewe akiwa ndiye jiwe kuu la pembeni (corner stone). Biblia inaposema msingi hainaanishi mitume na manabii wa kizazi chetu cha leo, ni wale waliokuwepo kabla ya kuja kwake Yesu na Mitume ambao Yesu mwenyewe aliwachagua na kukaa nao akiwafundisha. Sisi wa leo tunapaswa kuliangalia neno la Mungu na kulifuata hilo na ndiyo maana hata unabii unaotolewa siku za leo ni lazima ufanane na neno la Mungu lililopo.

  Napenda niseme tena kuwa kusema Mwingira amebeba mabegani mwake mambo kuhusu kanisa ni kumwinua mwanadamu na kumfanya aonekane kuwa sawa na Yesu Kristo, maana Yesu Kristo ndiye mwenye mamlaka juu ya Kanisa. Haya ninayoyasema yanathibitishwa na sehemu ya ujumbe huu inayomalizia kwa kusema MSIKIENI YEYE!!

  MSIKIENI YEYE!!
  Tangia mwanzo wa Agano Jipya, hakuna mwanadamu ambaye Mungu aliagiza kuwa asikilizwe. Mtu pekee ambaye Biblia imemsema asikilizwe ni mwanadamu Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu. Haya tunayaona katika Luka 9:35 asemapo huyu ni mwanangu mteule wangu, msikieni yeye.

  Yesu Kristo anapozungumza juu ya Roho Mtakatifu (Yohana 16:13-15) anatuambia kuwa Roho Mtakatifu hatanena kwa shauri lake mwenyewe bali atanena yale atakayoyasikia na kuwa atachukua yaliyo katika Yesu Kristo na kutupasha habari. Hapa inaonyesha kuwa kwa habari ya Kanisa, Yesu Kristo alikwisha maliza.

  Ndugu zangu wapendwa, hivi kweli tukubali kuwa maneno ya Mtumishi Aron ni unabii kwa ajili yetu na kuwa umetoka kwa Mungu kama alivyohitimisha kwa kusema ASEMA BWANA; ALIYE WA KWANZA NA WAMWISHO; ALIYEKO ALIYEKUWAKO NA ATAKAYE KUJA? Hivi kweli huu unaodaiwa kuwa unabii unatimiza vigezo vya neno la Mungu?

  Imekuwaje hivi leo Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu waamue kuwa Kanisa la Tanzania, Afrika na Ulimwenguni mwote limsikilize Mwingira? Katika Ufunuo wa Yohana (1:4-20; 2:1-29 na 3:1-22), tunamwona Mtumishi wa Mungu Yohana akisema yale aliyoambiwa ayaandike kwa ajili ya makanisa ya Asia ndogo na kamwe hakujitwalia utukufu bali alisisitiza kusema kuwa haya ndiyo anenayo yeye akimaanisha Yesu.

  Binafsi nilishtuka sana nilipoyaona maneno ya Mtumishi Aron, hasa anaposema msikieni Mwingira. Si kwamba singependa kumsikiliza Mwingira, lakini unabii ukisema asikilizwe fulani maana yake nini?

  Sote tunafahamu kuwa mwanadamu yeyote aliyeokoka anaendelea kuwa mwanafunzi wa Yesu bila kujalisha ana huduma gani ndani ya kanisa na Mungu anaendelea kumtengeneza siku baada ya siku na wengi wetu tunakuwa na madhaifu fulani ambayo Mungu anaendelea kutusaidia na kututakasa, sasa inakuwaje Mungu atuagize tumsikilize mwanadamu mwenzetu? Kwa nini asiseme tulisome na kuliishi neno lake pamoja na kumsikiliza sana Roho Mtakatifu? Hivi katika ujumbe wa ndugu Mtumishi Aron, nafasi ya Roho Mtakatifu ni ipi? Ndugu zangu naomba tuwe makini sana na matamko kama haya.

  Nimekuwa nikijiuliza sana, hivi Mtumishi Aron ameyasema haya yeye kwa kupenda kwake tu au ni kutokana na aina ya mafundisho anayoyapata kwa Ndugu Mwingira? Napenda kuzungumzia mambo mawili (moja niliambiwa na mtu ninayemwamini sana na lingine nililisikia mwenyewe kuhusiana na mafundisho au maneno ya Ndugu Mwingira):

  Niliambiwa na rafiki yangu kuwa aliwahi kumsikia Mwingira akisema Yeye Mwingira alichukuliwa mpaka mbinguni na Mungu akamtambulisha kwa Yesu kuwa yule mtu tuliyekuwa tukimtafuta kwa ajili ya Tanzania amepatikana, yaani inaonekana kuwa Mbingu ilikuwa ikimtafuta mtu kwa ajili ya Tanzania na ndipo Mungu akamuona Mwingira na akachukua hatua ya kumpeleka Mwingira juu ili akamtambulishe kwa Yesu kuwa ndiye aliyepatikana kwa ajili ya Tanzania. Hili nalo linaleta shida sana na maswali mengi, hata hivyo linafanana sana na maneno ya Mtumishi Aron.

  Mimi mwenyewe niliwahi kumsikia Mwingira akisema kuwa siku ya mwisho Yeye atashirikiana na Yesu kuwavika watu (washirika wake) taji. Alitoa mfano wa namna marais wanavyowatunuku wanajeshi nishani ambapo wanaweza kumtunuku mmoja kwa niaba ya wengine na kisha wengine wakaendelea kuvishana wenyewe. Kutokana na mfano huo akasema kuwa siku ya mwisho Yesu atawavika taji wao (akina Mwingira) na wao watawavika watu walioko chini yao, nikashangaa sana!?

  Nimesema mifano hiyo miwili ili kuonyesha pengine ni kwa nini Mtumishi Aron alisema maneno ya aina hii. Kumekuwepo aina ya mafundisho ambayo Mwingira anayafundisha yenye lengo la kumfanya yeye Mwingira kuonekana kuwa ni mtu wa pekee sana (special servant of God) ambapo wakati mwingine hufika mbali, jambo ambalo ni hatari kwake na kwa washirika walioko chini yake na matokeo yake ni haya maneno ya Mtumishi Aron.

  Binafsi naamini kuwa Mungu anampenda Mwingira pamoja na kundi lote analoliongoza, ndiyo maana nikaona vema nitoe mchango wangu juu ya kauli hii. Hata hivyo, ni vema kuangalia ni mafundisho gani yanatolewa ili watu waweze kumjua Mungu na si kumjua mwanadamu.

  Kama nilivyosema awali nimeandika maneno haya kwa lengo la kuona kama ninaweza kusaidia wengine na mimi mwenyewe kusaidiwa kutoka na ninavyodhani ninafahamu.

  Mungu awabariki na kuwafanikisha sana

 121. Shalomu!

  Nichukue nafasi hii kuwapa pole wote kwa msiba mkubwa uliotupata wa kuondokewa na ndugu yetu mpendwa Fanueli Sedekia. Jina la Bwana Libarikiwe.

  Ni muda mrefu kidogo nilichangia katika ukurasa huu nikiomba ufafanuzi wa maelezo yaliyotolewa na Mtumishi Aron lakini sijajua nini kimempata ndugu Aron maana amekuwa kimya.

  Kutokana na kuto kupata maelezo, nimeona nitoe kile ninachokiwaza juu ya maneno hayo ili wasomaji wengine waweze kuchangia ili tupate ufafanuzi au tuwekane sawa. Hata hivyo, kutokana na kubanwa na mambo mengi, sitaweza kupitia maeneo yote kwa leo, bali nitazungumzia machache, halafu siku nyingine nikipata tena nafasi nitamalizia.

  Kwanza naomba niseme kuwa kwa kawaida yangu sipendi kusema jambo juu ya watumishi wa Mungu. Hata hivyo nimeona nitoe dukuduku langu juu ya maelezo hayo yaliyotolewa kwa maana ya ama kusaidia na/au kusaidiwa.

  Mtumishi Aron aliandika hivi:
  SIKIA EE TANZANIA HUYU SI MTUMISHI MWINGINE TU AMBAYE AMEPAKWA MAFUTA…

  Kulingana na maudhui ya maneno hayo pamoja na mengine kwenye maelezo ya ndugu Mtumishi Aron, huu ni unabii, na unabii huu unalengwa kwa watanzania na kisha waafrika na hatimaye ulimwengu wote.

  Kwa kuwa mimi ni mtanzania, ninapaswa kuuelewa unabii huu. Katika maneno yake anasema huyu si mtumishi mwingine tu ambaye amepakwa mafuta…. Hapa anatufahamisha kuwa huyo mtumishi ni wa tofauti, hayuko kama watumishi wengine ambao tunawafahamu, anajaribu kutufafanulia kuwa pamoja na hao watumishi wengine kupakwa mafuta, lakini huyu si kama hao, ina maana huyu ni tofauti.

  Katika utambulisho huo naomba nami nitoe mawazo yangu kidogo. Kwanza kila mtumishi wa Mungu ni tofauti na mwingine na kila mmoja hupewa namna yake ya kutumika na eneo lake la kufanya huduma, lakini mwisho wa yote, Mungu anapewa utukufu. Tunamwona Paulo akiwaambia Wakorintho kuwa Paulo hakusulibiwa kwa ajili yao, wala Kefa, wala Apolo (1Korintho 1:12,13) anaendelea kusema kuwa yeye apandaye si kitu wala atiaye maji si kitu ila Mungu (1Korintho 3:3-9). Katika eneo hili Paulo anaonya kuwa watu wanaowaangalia watumishi wa Mungu kwa mtizamo waliokuwa nao Wakorintho ni watu wa tabia ya mwilini. (Watoto wachanga wanaokunywa maziwa).

  Nimejaribu kuangalia Mungu anapowaita watumishi wake inakuwaje! kwa kawaida Mungu huwa hawatambulishi watumishi hao kwa wanadamu, bali Yeye husema na watumishi wake. Mfano alipomwita Musa Kutoka 3:1-22), hapa tunamwona Musa akimuuliza Mungu juu ya uwezekano wa kutokukubaliwa kwake, lakini hatuoni Mungu akisema nitakutambulisha kwa wana wa Israeli bali anamwambia akawaambie MIMI NIKO AMENITUMA. Alipomwita Yoshua pia hatuoni akimtambulisha kwa makutano bali anamwambia Yoshua yampasayo kutenda (Yoshua 1:1-9). Tunaona hivyo hivyo alipokuwa akiwaita manabii mbalimbali hakuwahi kuwatambulisha kwa wanadamu bali alijitambulisha kwao akawapa ujumbe wa lile analotaka wakalifanye.

  Paulo alipoitwa pia hakutambulishwa kwa wanadamu kuwa sasa nimemwita Paulo bali Yesu alisema na Paulo mwenyewe juu ya wito wake, Matendo 26:12-18), Mitume wengine pia walipoitwa hawakutambulishwa kwa wanadamu bali Mungu aliwatuma wao na ujumbe wa neno lake.

  Biblia inatuonyesha watu kadha wa kadha ambao Mungu aliwasifia, mfano Musa, Ayubu, Danieli, Nuhu (Ezekieli 14:20), lakini hawa nao hawakutambulishwa bali aliwasifia kwa uaminifu wao.

  Ninaposema kutambulisha, maana yangu ni kuwa kwa kawaida Mungu huwa hamtambulishi mtu anayemtuma kwa wale anaowaendea. Kwa maoni yangu, naona Mungu hafanyi hivyo kwasababu anataka ajitukuze mwenyewe akiwatumia hao watumishi pale ambapo Ukuu na Utendaji wa Mungu utakapoonekana kwao.

  Mwanadamu pekee aliyetambulishwa na Mungu alikuwa ni Mwanadamu Kristo Yesu ambaye Mungu alimtambulisha kuwa huyu ni mwanangu mpendwa ninayependezwa naye msikieni yeye (Mathayo 3:17; 17:7), pia Biblia inaonyesha kuwa Yohana alitabiriwa kuwa atakuja kabla ya Kristo, mtangulizi (Isaya 40:3-11, Luka 7:26). Pamoja na kuwa Yohana alikuwa mtangulizi bado alipoanza huduma yake hakutambulishwa kwa wayahudi kuwa huyu ndiye mtangulizi ya Yesu, na baadhi ya wayahudi walishindwa kumkubali Yesu kuwa ni Masihi kwa sababu walijua kuwa kabla ya Masihi kuja atakuja kwanza Eliya wasijue kuwa Yohana alikuja katika roho ya Eliya.

  Yesu pekee yake ndiye ambaye Mungu alimtambulisha. Ndiyo maana nikaomba ufafanuzi kwa sababu maudhui ya unabii huu ni kumtambulisha Mwingira kwa watanzania, waafrika na walimwengu kuwa huyu si mtumishi tu aliyepakwa mafuta.

  Nimekuwa najiuliza, Mungu akianza kutaja CV za watumishi wake wakiwa hapa duniani si itakuwa shida? Mungu akisema Paulo si kama wengine, kwanza huyu nilimtokea mwenyewe wakati akienda Dameski, halafu anasema Yohana si kama wengine, maana huyu ni mwanafunzi niliyempenda kuliko wengine na alikuwepo wakati nikiwa msalabani, nini kitatokea? Katika ile Wakorintho niliyoionyesha hapo juu, Paulo anasema kila mmoja atalipwa sawasawa na taabu yake.

  Kwa maoni yangu, kusema kuwa huyu si mtumishi mwingine tu ni hali ya kumwinua mtu kuliko vile ambavyo tunapaswa kufanya. Hivi ni lini Mungu amewaambia wanadamu juu ya ubora wa mtumishi fulani? Kama mtu ni mtumishi ina maana anatumika kulingana na matakwa ya Bwana wake. Sasa kama ndugu Aron angetufafanulia tungeweza kuelewa hasa maana ya maneno hayo.

  HUYU NI MTU ALIYETUMWA NA MUNGU NA YESU KRISTO KWA ROHO MTAKATIFU KUBADILISHA MAJIRA KATIKA KANISA TANZANIA AFRIKA NA ULIMWENGU
  Nadhani ule utambulisho ambao tumeuona hapo juu ulikusudia kutufahamisha juu ya ujumbe huu, wa kuwa Mwingira ametumwa na Mungu na Yesu Kristo kwa Roho Mtakatifu.

  Tukisoma mwanzo wa Nyaraka za Paulo, tunaona jinsi alivyoanza kwa kuuelezea utume wake ambapo mara nyingi amesema alitumwa na Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu. Mimi naamini kuwa kila mtu anayemtumikia Mungu hutumwa na Mungu maana huwezi kuwa mtumishi wa Mungu bila kutumwa.

  Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasiondoke mjini mpaka wavikwe uweza kutoka juu (wapokee Roho Mtakatifu) Luka 24:49. Roho Mtakatifu ndiye anayewapa watu uwezo na nguvu za kumtumikia Mungu, bila Roho Mtakatifu hakuna anayeweza kumtumikia Mungu, maana biblia inasema wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndiyo wana wa Mungu.

  Sina tatizo sana na maelezo haya kwani kila mtumishi ni lazima atumwe na Mungu na hupewa Roho Mtakatifu kwa ajili ya huduma anayoitiwa. Kuhusu ubora wa huduma, Mungu ndiye anayejua, lakini kama Paulo alivyosema, kila mmoja atalipwa kulingana na taabu yake. Yesu alipomwona mwanamke mjane anatoa senti mbili alisema huyo ametoa kuliko wengine wote, hivyo ndivyo Mungu anavyoangalia na kuhukumu.

  Kinachonipa shida zaidi ni sehemu ya pili ya maneno haya kuwa “ametumwa kubadilisha majira katika kanisa”. Ninachojiuliza mimi ni kuwa hivi kanisa ni mali ya nani? na nani anayelibadilisha kanisa? Je mwanadamu anaweza kulibadilisha Kanisa? Kama ametumwa kwa ajili ya huduma fulani kwa ajili ya Kanisa, Je Mungu atamtangaza kuwa ndiye anayebadilisha jambo ndani ya Kanisa? Je majira ya kanisa ni kitu gani? na Je tunajifunza nini tunaposoma juu ya yale makanisa saba ya Ufunuo wa Yohana?

  Naomba kwa leo niishie hapa, nikipata muda wiki ijayo nitajaribu kuendelea kuchangia ninavyoona juu ya maneno haya. Kama nilivyosema lengo langu ni kusaidiwa na/au kusaidia.

  Shalomu

 122. Shalomu wapendwa!

  Bado nasubiria majibu ya maswali yangu kwa ndugu Mtumishi Aron ambayo nimeyauliza hapo juu. Nitafurahi sana kama atanisaidia majibu ya maswali haya.

  Shalomu

 123. Ndugu Mtumishi Aron

  Shalomu!!!

  Wapendwa wote nawasalimu kwa Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, ambaye ni Alfa na Omega, wa KWANZA na wa MWISHO.

  Nimesoma maelezo ya ndugu Mtumishi Aron kwa kuyarudia lakini niseme kweli sijamulewa ana maana gani. Sijui ni mimi ambaye sifahamu anachosema au ni yeye (Mtumishi Aron) ambaye hajui ukubwa wa kile alichokisema. Nitaomba sana Mtumishi Aron atufafanulie ameandika maneno hayo akiwa na maana gani na ni nini maudhui ya ujumbe anaoutoa katika malezo yake.

  Shida niliyo nayo juu ya maelezo yake ni kama ifuatavyo:-

  1. Anasema “Sikia ee Tanzania, huyu si mtumishi mwingine tu ambaye amepakwa mafuta…. (Ndugu Mtumishi Aron una maana gani na sentensi hii?)

  2. Ni mtu aliyetumwa na Mungu na Yesu Kristo kwa Roho Mtakatifu kubadilisha majira katika kanisa, la Tz, Afrika na ulimwenguni… (hapa napo Ndugu Mtumishi Aron una maanisha nini?)

  3. Amebeba majira mapya begani mwake… (hapa napo pia ndugu Mtumishi Aron unatuma ujumbe gani?)

  4. Msikieni yeye!!! Asema Bwana; (Ndugu Mtumishi Aron naomba ufafanuzi tena, unaposema MSIKIENI yeye unamaanisha Mwingira au Yesu?)

  Naamini yale maneno ya mwisho “Aliye kwa Kwanza na wa Mwisho; Aliyeko Aliyekuwako na Atakaye Kuja” umeyasema ukimaanisha Yesu Kristo na si Mwingira (kama nimekosea naomba unisahihishe pia katika hili).

  Nimejaribu kuyagawa katika vifungu maneno aliyoyasema ndugu Mtumishi Aron ili atakapo nipatia majibu akienda hatua kwa hatua nitaweza kumuelewa zaidi na pengine kwa ufasaha.

  Nitashukuru sana kupata ufafanuzi wa kina ukiambatana na maandiko ili kuniondolea shida niliyo nayo kutokana na ujumbe alioutoa ndugu Mtumishi Aron

  Mungu awabariki

 124. SIKIA EE TANZANIA HUYU SI MTUMISHI MWINGINE TU AMBAYE AMEPAKWA MAFUTA… HUYU NI MTU ALIYETUMWA NA MUNGU NA YESU KRISTO KWA ROHO MTAKATIFU KUBADILISHA MAJIRA KATIKA KANISA TANZANIA, AFRIKA NA ULIMWENGU… AMEBEBA MAJIRA MAPYA BEGANI MWAKE… MSIKIENI YEYE!!! ASEMA BWANA; ALIYE WA KWANZA NA WAMWISHO; ALIYEKO ALIYEKUWAKO NA ATAKAYE KUJA.

 125. HALELUYAAA MTUME NA NABII MWINGILA,
  POKEA SHUKRANI TOKA KWANGU NA NAPENDA KUSEMA HUDUMA YAKO INATEGEMEWA NA MAISHA YA WATANZANIA WENGI NCHINI. TUTAENDELEA KUWA MSTARI WA MBELE KUICHANGIA TRENET TELEVISION ILI WATU WAENDELEE KUKAA KARIBU NA MUNGU NA KUINGIA KATIKA WOKOVU KAMA MUNGU ALIVYOAGIZA “ANITAFUTAYE BILA KUCHOKA ATANIONA”
  ASANTE BABA MTUMISHI.

  NB; NDOTO ZANGU KUTUMIWA NA EFATHA KATIKA NGAZI KAMA YA MTUMISHI PETER. NAJUA NDOTO ZANGU KWAKUWA NINA ROHO MTAKATIFU ZITATIMIA.

 126. Nimehudhuria huduma zako mtumishi wa Mungu, nabarikiwa mno kuona namna Mungu anavyofanya kazi ndani yako kwa ajili ya wengi waliokatika mahitaji mbalimbali ya kiroho na kijamii!

 127. binafsi hawa mitume huwa siwaelewielewi wadau mnaweza mukanielewesha jinsi ya huduma ya kitume inavyofanya kazi. ili niweze kuitofautisha na zingine ninazozijua kama uchungaji,waalimu n.k

 128. Mungu amekupa upako wa ajabu sana. endelea kumwita mungu aokoe hii nchi yetu iliyojaa wizi na kila aina ya uchawi na rushwa,mungu akusaidie

 129. umependeza sana ndani ya yesu na yesu anakufurahia .mungu akushike mkono katika huduma yake ya kuwahudumia kondoo zake.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s