Strictly Gospel ni familia kubwa!

Strictly Gospel

Bwana Yesu Asifiwe Wapendwa,

Tunapenda Kumshukuru MUNGU kwa kila anayesoma au kuchangia lolote kwenye uwanja huu, ni heshima, sio jambo dogo kwetu. Tunapenda ifahamike kwamba S.G ni kwa ajili ya watu wote sio dhehebu, hatufungamani na upande wowote, hatutoi wala kupokea pesa yoyote kutangaza lolote.

Tunaomba mtusamehe kwa baadhi ya jumbe au nukuu mbalimbali, hii ni kazi yetu na tunafanya hivi ijulikane kanisa limefika wapi, hatulumbani bali tuna NIA ya kufundishana na kueleweshana, haya yote ni kwa ajili ya UTUKUFU WA MUNGU WETU.

Baadhi ya wapendwa hutumia lugha zisizoujenga mwili wa Kristo, hatujaziweka na hatutaziweka, Nia na lengo kubwa ni kulijenga kanisa na sio kulibomoa, dhumuni hasa ni kuwafikia watu kwa njia hii ya website watu wamjue MUNGU, wabadilike na waone matendo makuu MUNGU anafanya kwa watu wake, pia kwa vijana wasitekwe katika mafundisho yasiyofaa katika mitandao mbali mbali bali kwa kupitia blog hii wakakutane na habari njema za wokovu na HOFU ya MUNGU iwe juu yao.

S.G ni familia kubwa, tunawapenda watu wote, anayetembelea kwetu ni mwanafamilia pia. Karibuni na mzidi kubarikiwa.

StrictlyGospel Team.

Advertisements

2 thoughts on “Strictly Gospel ni familia kubwa!

  1. Asante sana S.G. kwa ufafanuzi wa kuhusu hii blog.
    Ninakutakia kila la heri, Na Mungu katika Jina la Yesu akubariki sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s