Tumepewa Mamlaka

Nguvu ya ushindi i katika kukiri kwetu, tumepewa mamlaka ya kumiliki kila tunapokanyaga iwe ofisini, shuleni kwenye biashara zetu sehemu yoyote ile tumepewa mamlaka ya kutawala mahali hapo. Tambua hili, sema na mahali ulipo, shida yako iambie haina nafasi katika maisha yako, haijalishi ina jina kubwa kiasi gani au ni ugonjwa wa aina gani JINA LA YESU ni juu ya majina yote iwe ugonjwa, matatizo katika ndoa yako. Sema kwa kinywa chako, tabiri kwamba mimi ni mshindi kwa jina la YESU, mimi ni mzima kwa JINA LA YESU, Mimi ni mwenye afya na mafanikio, sema kwamba hakuna kitakachonidhuru kwasababu Yesu Yu ndani yangu. Tazama nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachonidhuru. (Luka 10:19-20 )

Na ikiwa bado hujaokoka sali sala hii, Ee Mungu, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi, naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu, natubu mbele zako, naomba Damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa, Nimefungua Moyo wangu. Bwana Yesu nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwangu uwe Bwana na Mwokozi wangu,kuanzia sasa na siku zote. Asante kwa kunisamehe na kuniokoa, shetani hana mamlaka tena juu yangu katika Jina la Yesu Kristo. Amen

Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika Neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.

Advertisements

11 thoughts on “Tumepewa Mamlaka

 1. MAMLAKA YA AJABU YA JINA LA YESU:
  1.KUTOA PEPO
  2.KUSEMA KWA LUGHA MPYA(lugha mpya maana yake ni lugha ucyoielewa)
  3.KUSHIKA NYOKA
  (ucshangae mpokee yesu utweza)
  4.KUNYWA KITU CHA KUFISHA NA KISIKUDHURU(sumu)
  5.KUPONYA
  Marko 16:17-1

 2. AMEN MARY HAKIKA UNANIBARIKI SANA MAANA UNA IMANI KALI SANA SANA !
  NA MIMI NITASIMAMA KTK IMANI HIYO PAMOJA NA KWAMBA NAPITA KTK JARIBU KUBWA SANA KTK HALI YA KIBINADAMU ILA NINA HAKIKA NITASHINDA MAANA ALIYE NDANI YANGU NI MKUU SANA SANA!
  HAJAWAHI KUSHINDWA HATASHINDWA WALA HATAKAA HASHINDWE YEYE NI MSHINDI SIKU ZOTE JINA LA YESU LINA NGUVU NYINGI!
  LIHIMIDIWE JINA LAKE YEYE ALIYE MKUU KULIKO WOTE!
  WAPENDWA TUDUMU KTK IMANI HIYO!

 3. halleluya! nikweli kabisa jina la yesu ndio silaha yangu maana nimeyaona mengi kwa hili jina la ajabu lipitalo majina yooooooooote!

  God loves you!

  The bible says,God so loved the world that he gave his one and only son.that whoever believes in him shall not perish.but have enternal life.

  TUNA MAMLAKA KWELI KWELI KWA JINA LA YESU

  BE BLESSED OF THE NAME OF JESUS AMEN! ILOVE U ALL!!!!!!!!

 4. ameeeeeeeeeeeeeeeeeni!ni kweli tukisema kama hivyo ulivyoandika hapo juu tutaishi kama Paradiso huku tukiwa bado Duniani maana hakuna kitakachotudhuru,barikiwa sana na Bwana na wabarikiwe wote wanaompenda Yesu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s