Wachungaji ni matingo wa mitume?

Naomba nafasi hii nitoe yangu kuhusu hali tata inayoendelea kulighubika kanisa hapa nchini inayosababishwa na madhehebu mapya au vikundi (ministries) vinavyoongozwa na watu wajiitao mitume na manabii.

Mitume na manabii wamefikia hatua ya kugawa au kuuza upako kwa wawapendao, na kuwapa wake zao uchungaji badala ya kumwachia Mungu aamue ni nani ampe huduma gani na nani apepwe nafasi gani.

Tukiangalia wanaume wengi wanaojiita mitume na manabii (mtume na nabii au nabii na mtume). Jambo linalosumbua akili yangu, ni kwamba, kila anayejiita nabii au mtume, lazima na msaidizi wake (mkewe) naye aitwe mchungaji. Na kama nabii au mtume ni mwanamke, basi mumewe ataitwa mchungaji.

Ninaposoma Biblia yangu Waefeso 4:11. inaonesha wazi kuwa Mungu ndiye anayechagua watu na kuwapa huduma kama apendavyo yeye. Siyo mtume kuamua kumpa mkewe uchungaji au nabii kumpa mumewe upako. Kama kweli hao wake za mitume na manabii ni wachungaji kweli, mbona hawafanyi kazi zote za kichungaji isipokuwa kuhubiri na kukemea pepo? Je wanaruhusiwa kubatiza, kufungisha ndoa na kushiriki meza ya BWANA? au kuna ushahidi kuwa wake wa manabii na mitume wa zamani walikuwa wachungaji?

Siku moja nilimsikia mtume mmoja akiieleza sababu za kumpa mkewe uchungaji. Namnukuu: “Mke wangu nimeamua kumtangaza kuwa mchungaji ili kuwafanya washirika wamtambue na waweze kumpa heshima stahiki. Pia inampa uzoefu wa kutumika, hata kesho nikitwaliwa, hawezi kudhalilika! Hawezi kuuza mchicha! Huduma hii ndio urithi wake. Wewe usipomwandaa mkeo shauri yako!” Mwisho wa kunukuu.

Hapo ndipo nilipofunguka macho, nikasema aaahaa! Kumbe! Mtu kujiita mtume au nabii ni njia ya kukwepa kazi ngumu na kujipatia mapesa kiulaini? Kumbe hii ndio janja ya nyani? Walio wa jinsi hii hawamtumikii BWANA Yesu Krsito ila matumbo yao (Warumi 16:17-18, Wafilipi 3:17-19). Ndiyo sababu hawa wanawake waitwao wachungaji ninawafananisha na matingo walioitwa na ndugu zao ili wawafundishe udereva ili nao kesho wale vichwa barabarani.

——-Vedasto M. Mbatiina, Dar-es-salaam +255 784 706 753——–

Advertisements

3 thoughts on “Wachungaji ni matingo wa mitume?

 1. Kwanza namshukuru Yesu ambaye ametoa uelewa mkubwa kwa watumishi wake,kweli watu waliochangia hapa wanaupeo mkubwa ambao sikuamini kuwa ni watu wengi wana upeo wa neno kama huu.Wabarikiwe.

  Upande wangu,najua kila aliyeitwa na Mungu hutenda kazi kwa Hofu kuu na unyenyekevu akijua kazi si yake bali ya yule aliyemtuma,sioni kama kweli Bosi wako ni Mungu utakuwa na jeuri hata kidogo ikiwa mabosi wetu wa kazi za duniani tunawahofu na kuwahi makazini mapema na kutoa Ripoti kwa umakini. Enye watumishi wanafiki hamjui hata Mungu huzisimamia kazi zake karibu nasi sana,ama kwa kuwa hawamuoni kwa macho ya nyama ndio maana kiburi hupanda? hamsomi habari za akina Abraham walioitwa wakitetemeka hata kumtoa mwanae achinjwe.
  Wito upo ila baadhi ya watumishi hawamjui aliyewaita au hawaujui wito wao vizuri.Wito upo ila HAKUNA TABIA ZA WITO(GOD`S REPUTATION) sisemi udhaifu wa mtu najua kila mtu ana udhaifu wake ila Tabia zisizo za kimungu sio udhaifu ni dhambi.
  Tatizo lingine ni uhuru zidi(over freedom)biblia inazungumza kuhusu kujikinai kwa watumishi na kujaa na kiburi na kujisikia,lazima hofu na mipaka ktk huduma iwepo,na nauliza je tuna Vyuo vya watumishi au au vituo vya mafunzo ya huduma?maana hata nabii Eliya alikuwa na chuo cha kinabii,kwanini watu wasipende kujifunza zaidi kuliko kujitutumua.
  Mbali na wito Biblia inatuhimiza kujifunza na kuchimba(PONDER) kama watu wa Beloya ili tujue je hivi ndivyo ilivyo.Nahisi watu wengi wamejikinai kwa kupenda kuonyesha huduma zao wakati ni wepesi ktk fundisho la Mungu. Mtu anajiita Mtume au Nabii lakini hana funzo(commentauols) za kutosha ukimuuliza maswali ya msingi ya kihuduma anakuwa mkali na anakimbilia kusema anachojua ni aliisikia sauti ya Mungu ikimuita Lakini Mungu anapokuita anataka uendelee kujifunza zaidi na zaidi sio kujimatamfua kila wakati kwa kutaja majina makubwa hiyo ni kujihami (defensive mechanism) ili usimkosoe.
  Anyway,mimi ni Pastor na nafundisha Bible Schools duniani nashauri watumishi wakeshe ktk kusoma na kujifunza neno kimapana,wapate ujuzi na upeo ktk neno na maarifa; haitoshi uumeokoka, kubatizwa na kujaza Roho halafu unabweteka. Hii ni hatari maana wachanga ktk Roho hupotezwa na hawa viongozi vipofu ambao watapata hukumu zaidi hata wao wasiingie ktk malango ya Mbingu. Mwisho; makanisa ya zamani acheni umimi na ufalisayo na kutoamini, pia aminini kazi zake Mungu sio tu kuamini juu ya kutoa mapepo, ila tuzidi kuwashauri wanaokosea ktk wito na kuwaombea. Ndivyo mtume Paulo alivyofanya.

  Blessings

 2. Hii ni mada nzito ambayo muda huu mfupi hautoshi kujibu. Lakini nitajaribu kuelezea na Mungu anisaidie. Ni kweil biblia iko wazi juu ya uvamizi wa mitume wa shetani, manabii wa uongo, wachungaji wa mishahara, waalimu wafundishao mafundisho ya mapepo na wainjilisti wanaohubiri injili nyingine. Jibu rahisi ni kuwapima kibiblia. Mfano kuna toleo moja la nyakati limeweka document juu ya unabii wa uongo aliotoa Geor Davie. Mitume wamekuwa wakijigawia title wanavyotaka lakini kazi za kitume???

  Ninachoona mimi, ni biashara ya upako inaendelea. Injili haihubiriwi bali upako, uponyaji….. Kazi ya mitume, manabii, waalimu, wachungaji, wainjilisti- iko wazi kibiblia. Mfano, sielewi title ya Mtume na Nabii inapotoka. Mtume anaweza kutembea katika karama ya kinabii inapohitajika. Na ni Roho pekeee ajuaye lini inahitajika. Sasa Mtume na Nabii????

  Mwisho niseme hivi, hakuna huduma bora kuliko nyingine. Sote tunahitajiana ili kufanya kazi ya Mungu. Huduma hizi zipo kujenga mwili wa kristo. Tunahitaji Mitume na manabii kwa ajili ya kuliweka kanisa katika msingi sahihi. Tunahitaji Mitume na wainjilisti kwa ajili ya kuwahubiri watu walio nje ya Kristo. Tunahitaji Mitume na waalimu, kufundisha waamini wasimame katika mwamba sahihi. Mwisho tunahitaji Mitume na wachungaji ili kuchunga kundi la Mungu likue kila siku, na lote lifike mbinguni

  Mtume hataendelea kuchunga kondoo akiisha mfundisha na kukabidhi mchungaji (kati ya waamini wapya). Bali ataendelea kuwasiliana naye na kuwatembelea mara kwa mara kulitegemeza kanisa. Pia hataendelea kufundish baada ya mwalimu kusimikwa bali atabaki kutoa sapoti huku akiendelea kuchanja mbuga hadi mbuga kuibeba injili. Kwa ujumla yeye si mtu wa kukaa mahali pamoja na ana uwezo wa kutembea katika karama zote kwa kadri ya neema ya Mungu katika mazingira hayo

  Labda kwa kifupi niache ushuhuda hapa. Nilikuwa nafikiri Mungu ameniita mwinjilisti kwa kuwa kipindi fulani nilipenda mno uinjilisti (Mpaka leo napenda), lakini baada ya muda nikaona karama ya ualimu….mwisho nikagundua baada ya kupata mlo sahihi kuwa Mungu ameniita katika kazi ya utume. Lakini sio lazima mke wangu awe mchungaji, wala wachungaji sio matingo, bali ni viungo katika mwili wa Yesu, watendakazi pamoja nami shambani mwa bwana, sawasawa na mimi mbele za Bwana lakini tukiwa tumepewa majukumu tofauti na karama tofauti na huduma tofauti!

  Cha msingi, ni kuwatambua watumishi wa shetani na kuwatofautisha na watumishi wa Mungu. Nafikiri kifupi nimechangia kitu, karibuni

  Mtume wa Yesu
  Steve

 3. Mimi nadhani, tusilaumu juu wa mitume wanaowafanya WAKE ZAO kuwa wachungaji. Huenda wake zao hao, wanakuwa tayari wamejifunza vya kutosha kutoka kwa waume zao, hata kufikia kuwa mchungaji. Hii ni kwa sababu, kama ni manabii wa kweli, wanauwezo pia wa kuzalisha au kutoa wachungaji wengine miongoni mwa washirika wao.

  Tatizo tunalotakiwa kuliangalia hapa ni je, hao wanaoitwa mitume au manabii, kweli wanafanya kazi hizo za kitume au kinabii? Kweli wametumwa na Yeye?

  Nikisoma biblia yangu, naona mitume na manabii wa nyakati za biblia, walikuwa na viwango vya juu sana vya utumishi. Hawa wa nyakati hizi, kwa kweli bado nina wasiwasi nao kwani hata utakatifu ambao ningetarajia kuwa wangekuwa nao, bado naona wanachanganya masomo, hata wale wanaofundishwa nao, wameshindwa kuwa na viwango vinavyotarajiwa kwa sababu mwanafunzi hamzidi mwalimu wake, na ikiwa atazidi, basi atakuwa kama mwalimu wake.

  Majina haya ni mazito mno, tukilinganisha na huduma zenyewe. Huduma miongoni mwao ni nyepesi mno, japo neno nabii ni kusema au kuhubiri maneno ya Mungu na Mtume ni yule aliyetumwa na Mungu kuzitenda kazi zake. Hivi sasa wanadamu, wanawaangalia sana hawa wanaosema kuwa ni manabii au mitume, ili waone ni wapi wanaposhindwa hatimaye waubeze utume au unabii wao!

  Tuitwe tu watumishi wa Mungu au wainjilisti, yadhuru nini? Kwani tukiitwa manabii, ndiyo tutafanya kazi ya nabii kisawasawa, hata kama wito huo hauko kwetu? Mimi nadhani tukifanya kazi halisi ya kinabii au kitume, bila sisi kujiita tayari watu wanaoziona kazi zetu watatuita manabii au mitume.

  Mungu atubariki, na azidi kutusaidia watu wa Mungu, ili kuzidi kuijua kweli iliyopotea miaka mingi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s