91 thoughts on “Ni sawa mwanamke kuvaa suruali?

 1. Biblia iliposema mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanaume maana yake kuna nguo za kiume na kike,

 2. terimbere assir, nani ambaye suruali ni mavazi yake sasa. Kwani Yesu alivaa suaruali, babu wa babu wa babu yako alivaa suruali? Mbona tunahangaika na vitu ambavyo hata si vya msingi!!

  Ivi nyinyi mmekuwa wayahudi wa mwili enyi ambao ni mataifa, ni lini Mungu aliingia nanyi agano la hayo mambo, au mnajaribu kudandia meli?

  Na suruali ni vazi la kiume kwa mujibu wa andiko lipi?

  Hebu ifike sehemu tukue.

 3. Suruali mbinti sio mavazi yenu hata kidogo.bali
  Ni malezi tuu mlio pitia kutokana na développement ya kidunia na tabia kutoka
  Inchi za wazungu ikabidi mkafurahiya ivo na kuziridhisha nafsi.
  kwa sababu dunia ya sasa kila binadam hupenda kuonekana
  Kua amependeza mbele y a watu kua ni mrembo amajaliwa.
  Basi wamoja huwa wanakusudia Kuwaonesha watu yale anayohisi mungu kamjalia
  Kuyawonesha na asiye juwa ajuwe

 4. mimi nami nimefurahi kwa mafundisho yenu mpendwa ya kuhusu mavazi, mtazamo wangu ni kwamba yatupasa kusimamia maandiko na sio kuenenda kwa jinsi ya ulimwengu huu kwani neno la Mungu ni taa ya miguu yetu

 5. Dada usiangalie sinema ya Jesus of Nazaleth maana wale ni waigizaji tu kama waigizaji wengine wa muvi nyingine tu na Yale siyo maisha halisi ya YESU kristo
  Nakushauli tujifunze zaidi kupitia NENO LA MUNGU ( BIBLIA TAKATIFU) na sio kupitia muvi ambazo ni maigizo tu

  Japo binafsi kwangu sipendi Dada avae suluari na sketi iliyo fupi ( iliyo juu ya goti) pia sipendi mwanaume kuvaa suluari za kubana (modo).

  That is my reason

 6. Siyi,

  Kimsingi hakuna jambo la kimwili ambalo siyo la kiroho. Labda ungefafanua ulicholenga kukisema hasa katika hilo, kuliko kukomea tu kutoa angalizo.

  Suala la nini cha kuvaa ni la kiutamaduni hasa, ndio maana hata sisi leo hatuvai kama Yesu na mitume walivyovaa.
  Suruali ukifuatilia vema katika nyakati zao ilikuwa ni kaptula ya kuvaa ndani, ambayo leo twaweza kuiita pajama.

  Tusijaribu kulifanyia utamadunisho kanisa, church is a diverse organ culturally.
  Ndio maana biblia inasema kuwa kila kitu kwa asili ni chema, ila matumizi yaweza kukifanya najisi.

 7. Watu wanaotetea dhambi, utawasikia wakisema hivyohivyo, kuwa kuvaa suruali halihusiani na mambo ya kiroho!! Kuvaa sketi kwa wanaume, ni jambo ambalo halihusiani na mambo ya kiroho! Watu wenye mawazo ya namna hiyo hao wooooote ni wafu kiroho!! Waangalieni sana ndugu zangu. Kiujazacho moyo, ndicho kinachojidhihirisha kwa nje! Wasiwadanganye kirahisi hivyo!
  Neema ya Bwana iwafunike.
  Siyi

 8. Well spoken Ziragora!

  Ni aibu sana leo kanisa kupoteza muda likijadili aina ya mavazi ya kuvaa, tulitakiwa kuwa tunashugulika na mambo ya kiwango cha juu ya ufalme wa Mungu.

  Lakini ati unakuta leo mtu anatokwa povu madhabahuni anaongelea suala la wanawake kuvaa suruali, ni aibu sana.

  Kama Yesu angekuwepo kimwili asingepoteza muda kuongelea mavazi.

  Angeongelea zaidi ufalme, ambao kwa sehemu kubwa kanisa tumekosa kuijua mentality yake sawasawa (Yaani Kingdom Mentality)

 9. Tufahamishane wapendwa
  Kwa hiyo hata wanaume leo tunapovaa suruali, tunatembea na nguo za ndani, huenda tumeenda mbali kuasi zaidi ya wanawake tukitembea na nguo za ndani?

 10. KUTOKA 28:42
  “NAWE WAFANYIE SURUALI ZA NGUO YA KITANI….”. Ukisoma kwa lugha nyingine utaona kama suruali inayozungumuziwa hapa siyo suruali kama tunavyoifahamu. Ilikuwa nguo ya ndani (underpants). Nguo ya Kuhani ilikuwa Kanzu, Joho na Kilemba.
  Kwa mfano ukisoma hio shairi katika KJV utaona ni beeches na katika AMP utaona ni undergarments.
  AMP: Exodus 28.42 You shall make for them [white] linen undergarments to cover their bare flesh, reaching from the waist to the thighs.

  Lenda, ingelikuwa heri upachike shairi yote:
  “Kutoka 28: 42 Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;”. Kwani ni suruali ipi tukilinganisha na suruali tunazoziona ambazo huishia tu mapajani? Je kama ni hizo wanawake hawana ruhusa ya kuzivaa kama nguo ya ndani?

  Pia wakati Yesu alipokuwa akifundisha alisema; “Luka 3:11 Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo.”
  Yesu anaonyesha kama nguo ni kanzu ya yeye alivaa Kanzu.
  Na wanawake walivaa kanzu.”Matendo ya Mitume 9:39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.”

  Ukweli ni kama kwa leo wanaume wamezoea vaa suruali lakini sivyo ilikuwa zamani. Pia sijaona mwanaume amefika dukani ashindwe tofautisha suruali ya mwanaume na mwanamuke.

  Ina maana kuna surali ya mwanaume na mwanamuke, viatu vya wanaume na wanawake, shati, …………
  Jameni, tatizi siyo mavazi, ni akili zetu !!!!!!!

  Bwana Yesu awabariki.

 11. BIBLIA INAZUNGUMZA JUU YA WANAUME KUVAA SURUALI. SIJAONA WANAWAKE.

  KUTOKA 28:42
  “NAWE WAFANYIE SURUALI ZA NGUO YA KITANI”

  KUTOKA 39:28
  “….NA HIZO SURUALI NGUO YA KITANI NZURI ILIYOSOKOTWA”

  EZEKIEL 44:18
  WATAKUWA NA VILEMBA VYA KITANI JUU YA VICHWA VYAO NAO WATAKUWA NA SURUALI ZA KITANI VIUNONI MWAO;”

 12. the best way it to think this: As a Christian, I’m compeled to believe that what matters is your heart. If by wearing those pants has nothing negative in your heart, you can do it but again, do not do something that will make others sin because it will be counted against you by God. Just wear loose, decent clothes and follow what the Bible says on the adornment. Vaa mavazi ya kusitiri mwili wako vilivyo na usiwache uchi kwa watu wengine kutazama na kuona uchu wa ngono. Just don’t do it!
  1 Peter 3:3-4
  Do not let your adorning be external—the braiding of hair and the putting on of gold jewelry, or the clothing you wear— but let your adorning be the hidden person of the heart with the imperishable beauty of a gentle and quiet spirit, which in God’s sight is very precious.

  1 Timothy 2:9-10
  Likewise also that women should adorn themselves in respectable apparel, with modesty and self-control, not with braided hair and gold or pearls or costly attire, but with what is proper for women who profess godliness—with good works.

  Deuteronomy 22:5
  “A woman shall not wear a man’s garment, nor shall a man put on a woman’s cloak, for whoever does these things is an abomination to the Lord your God.

  Matthew 6:25-33
  “Therefore I tell you, do not be anxious about your life, what you will eat or what you will drink, nor about your body, what you will put on. Is not life more than food, and the body more than clothing? Look at the birds of the air: they neither sow nor reap nor gather into barns, and yet your heavenly Father feeds them. Are you not of more value than they? And which of you by being anxious can add a single hour to his span of life? And why are you anxious about clothing? Consider the lilies of the field, how they grow: they neither toil nor spin, yet I tell you, even Solomon in all his glory was not arrayed like one of these. …

  1 Peter 3:1-6
  Likewise, wives, be subject to your own husbands, so that even if some do not obey the word, they may be won without a word by the conduct of their wives, when they see your respectful and pure conduct. Do not let your adorning be external—the braiding of hair and the putting on of gold jewelry, or the clothing you wear— but let your adorning be the hidden person of the heart with the imperishable beauty of a gentle and quiet spirit, which in God’s sight is very precious. For this is how the holy women who hoped in God used to adorn themselves, by submitting to their own husbands, …

 13. Hapo nilipochangia katika thread hii nikimjibu dada Regy, nilisema kwamba, “sisi wanaume hiyo ndiyo kazi yetu, kuwatazama wanawake maumbile yao na kuwatamani, ndio maana Kristo hakusema “mwanamke atakayemtazama mwanaume kwa kumtamani, atakuwa amekwisha kuzini naye…” bali alisema mwanaume!”

  Jambo hili naona limewatatiza wapendwa wengine, wakaniona mimi ni mtu ninayewatamani sana wanawake, lakini ninaamini ni kutokana na ufinyi wa uelewa tu. Bali dhana ya maelezo yangu hayo ilikuwa ni kujaribu kuwaleta wapendwa kuyajua yote yanayowazunguka katika jamii tunazoishi, haswa tukiwa ni ule waraka, kwa yale mavazi yetu!

  Basi ktk kuirejea ile amri aliyoitoa Kristo, jambo la uzinzi huwahusisha watu wawili, ndipo katika hilo, mwanamke awe ameokoka au mpagani, akijiwasilisha katika namna ambayo maungo yake, yale yanayopaswa kusitirika badala yake yakawa yanajionesha, basi wanaume wa kawaida, kwa maumbile, “the animal in them!”, huamka katika tamaa. Nayo sheria ile haimuhusu mkristo pekee, bali dunia nzima, kwahiyo ni katka mazingira ya namna hiyo ndipo nimeainisha kuwa mwanamke wa kikristo aweza akajikuta katika tatizo asilowahi kulifikiria wala kulishiriki, bali ni kwa ile jinsi alivyojiwakilisha yamemkuta hayo!

  Kwahiyo ni vizuri tukaelewa kuwa hatuishi katika ma convent, bali katika jamii mchanganyiko, nasi ni sehemu ya jamii hiyo, ndio maana twapaswa kuwa waraka!

 14. Lwembe ikifika kwenye mambo kama haya kusema kweli uwezo wako wa ku-reason huwa nauona uko chini saa. Utanisamehe kwa kukuona hivyo brother.

  Ngoja nikuoneshe vitu vichache hapa:

  Nakunukuu; ”sisi wanaume hiyo ndiyo kazi yetu, kuwatazama wanawake maumbile yao na kuwatamani” haya ni maneno yako kwa dada Regy Edward.

  Na ukaongeza kusema;
  ” ndio maana Kristo hakusema “mwanamke atakayemtazama mwanaume kwa kumtamani, atakuwa amekwisha kuzini naye…” bali alisema mwanaume.

  Hapa Umeongea upuuzi ambao unatia kichefuchefu kusemwa na mtu kama wewe Lwembe.( sorry once more)

  Kristo kaonya tusimtazame mwanamke kwa kumtamani, halafu wewe mkristo Lwembe unasema kazi yetu sisi wanaume ni kuwatazama wanawake maumbile ao na kuwatamani.
  Ivi anayeongea ndani yako ni pepo au kitu gani?

  Halafu kwa nini unasema ”kazi yetu sisi wanaume”, kwa nini unatujumlisha wanaume wote? Sema kazi yako wewe Lwembe ni kutazama wanawake kwa kuwatamani, maana huo ni udhaifu wako wewe.

  Halaf Lwembe kwa umri wako kiufahamu usingesema ati ndio maana Kristo hakuonya kuhusu mwanamke kumtazama mwanaume bali mwanaume kumtazama mwanamke.
  Ktika utamaduni wa kiyahudi mwanamke hakuwa anachukuliwa kama subject ya accountability yoyote. Ndio maana sehemu zote biblia inapoongelea mtu kwa ujumla, hum-refer mwanaume ( sijui hii kama utaielewa maana hata kusoma theolojia mnapinga ninyi akina Lwembe)

  Hebu sasa sema Lwembe kwa mujibu wa andiko hili ;22:5, “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke… Je wanaume wa kiyahudi walikuwa wanavaa vazi la suruali ambalo unataka wanawake wasilivae au hilo andiko Mungu alikuwa wanawaambia wasukuma wa Mwanza na wazaramo wa Pwani?

  Au nikuulize kama wewe unavyopenda kuuliza, kwamba ni wapi biblia imesema kuwa suruali ni vazi la kiume?

 15. Dada yangu Regy, msingi wa kwanza katika mavazi ni kusitirika kwa mwili, haswa mwili wa mwanamke! Kwa nini mt. Paulo anamzungumzia mwanamke kuhusu huko kujisitiri, hilo pia unaweza ukaanzisha mjadala kulihusu, na ninaamini mwisho wa siku utaishia NJE ya Maandiko!

  Lakini, Yeye Mungu ndivyo alivyoliona jambo hilo, na maagizo yake yako hivyo. Licha ya hayo, bado umenifurahisha kwa ule ukiroho wako hapo unaposema, “….na mwanamke akivaa sketi fupi ukaona guu lake la bia na hipsi zake au kifupi ukaona uumbaji wa Mungu mzuri bd mtatamani wanaume…” hilo laonesha kuwa unafahamu fika kwanini mt. Paulo ameongelea mavazi ya kusitiri kwa mwanamke!

  Pia kuhusu utamaduni, napenda nikueleze kuwa UKRISTO ni utamaduni kamili, unaojitosheleza katika kila nyanja. Iwapo utakaa chini na kufunzwa na walimu waliojazwa Roho Mtakatifu, utayaelewa mengi sana kuhusu utamaduni huu mpya, hata hayo ya mavazi yatakuwa wazi sana kwako, lakini ukiwa chini ya walimu waliomix dunia na Mungu, basi ndio hivyo, dini inabakia kuwa ni ile ya kwenda Jumapili kanisani au kama ni msabato, Jumamosi na kutoa sadaka nyingi nk. Bali Mungu anasema ktk Kum 22:5, “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.” Kwahiyo unaweza ukamuelezea Mungu kuhusu utamaduni wenu hapo utakapofika huko na kuonana naye uso kwa uso, huenda atakuelewa!!!

  Ila binafsi ninakuonya kama dada yangu mpendwa, ACHANA NA SURUALI, mwili wako ni wa kutamanisha dada yangu, sisi wanaume hiyo ndiyo kazi yetu, kuwatazama wanawake maumbile yao na kuwatamani, ndio maana Kristo hakusema “mwanamke atakayemtazama mwanaume kwa kumtamani, atakuwa amekwisha kuzini naye…” bali alisema mwanaume! Vazi la suruali halimsitri mwanamke, ni uongo ambao hata ninyi wanawake mnaujua! Wanawake wote wanaovaa suruali, agenda yake wanaijua, na mwisho uliojificha gizani wa ajenda hiyo, ni kuangukia katika kesi ya UZINZI usio ulalia!!!

 16. comment zenu wapendwa ni nzuri sana ila mda mwngine mnatoka kiroho mnaingilia dis mwili…iko hivi neno litabaki kuwa kama neno na maneno yatabaki kunwa kama maneno. Ila katika Timotheo paulo anasema mwanamke na ajipambe na kujisitiri……swala la mavazi halijaandikwa ni suruali au gauni bali ajisitiri, Tukienda nchi nyingine suruali ndo vazi la mwanamke na gauni ndo vazi la mwanaume so tuangalie tamaduni au tuliangalie Neno? mimi ninachofahamu kwa mujibu wa mada zenu hapo juu hata mwanaume ukivaa suruali ikabana bado vishawishi vipo kwetu wanawake….na mwanamke akivaa sketi fupi ukaona guu lake la bia na hipsi zake au kifupi ukaona uumbaji wa Mungu mzuri bd mtatamani wanaume…Alafu nipe andiko lililoandika mwanamke alishonewa sketi na mwanaume suruali tusisikie kwa mapoke kwa wachungaji tuu tusome neno nasisi tulipambanue vema.
  MY VIEWS:
  1.Usimwangalie mwanaume/mwanamke kwa kumtamani ukiona tamaa ya mwili ni bora uwe na wakwako.
  2. Paulo anasema kama hujaoa kuwa kama aliyeoa na kama umeona kuwa kama asiye oa.
  3. Biblia inasema amani ya kristo na iamue mioyoni mwenu………

 17. Dah, unajua Sungura, nimecheka saana baada ya kuyasoma maelezo yako!

  Kwanza, kwa majibu yako, umenihakikishia kuwa umeulewa vizuri sana mfano nilioutoa, shawishi na hukumu zake! Huo ndio ulikuwa ujumbe wangu.

  Pili, nakunukuu: “Halaf kwa nini umwangalie mwanamke kwa kumchunguzachunguza kiasi hicho na kwa mtazamo huo, kama si roho ya tamaa ni nini? Kwani wenye hips na makalio makubwa wakivaa magauni makalio na hips zao huwa zinapungua ukubwa? Vipi kuhusu wanaume wanaoonekana suruali zao zimetuna pale mbele (madhbahuni) eidha kuelekea upande wa kushoto au kulia ulishawauliza wanawake wakakwambia huwa wanajisikiaje wakiona hivyo?”

  Kwa kadiri ya haya unayoyasema, nimegundua jambo moja, aidha ufahamu wako sio imara, au ni mjuzi wa kujifanya, yaani unafanya impersonation! Una impersonate innocence!!! Kama unaweza kumchunguza mwanaume kiasi hicho ulichokisema halafu ukajua na wa kumuuliza, wewe si mjinga kama unavyojaribu kujipresent, unajua staha ya mavazi!!

  Sasa, kwa kawaida, mwanaume akitokea akavaa kama hivyo ulivyosema, kwa kawaida huwa ni jambo la aibu kwa wote wanaomtazama, na kukitokea fursa basi huambiwa, “na wewe, nunua chupi mpya bwana!” Umbile la mwanaume si la kuvutia kama la mwanamke. Watazame wanyama na ndege, madume ndiyo yanayopendeza, ni binadamu tu aliyeumbwa tofauti, sisi, wanawake ndiyo wenye kuvutia Sungura, basi wewe ukijifanya huwaoni, ni utani!!! Mimi nikiwatazama, huwa nina behold the beauty, na kuishinda tamaa ya mwili by simply knowing that she is my sister! Na akivaa hizo suruali, huwa ninawaambia, don’t put up your beautiful body for sale, men will lavish you and you will end up in the same pit with all the whores of the world, despite your physical innocence, spiritually, you done it!!

  Pia, hebu niambie, utamaduni, unacomprise nini? Unaweza kuwa na utamduni bila mavazi? Acha theories, be realistic, boy! Mavazi ndio item na 1 katika utamaduni! Kule Edeni, walipochemka tu, wakaanza na mavazi, Mungu akawakuta Hawa kavaa kisuruali na Adamu kavaa kama ulivyoeleza hapo juu “mzigo” ovyo, ndipo akawatengenezea mavazi ya staha, akawavisha! Lakini sasa hivi walimu akina Sungura wanawarudisha kule kule, lakini subiri wapate Roho Mtakatifu, kama wale wanawake wa Kiswati niliokuambia, watakaa sawa!

  Karibu Sungura tusemezane!

 18. Mr. Lwembe kati aya mimi na wewe nani karudi mwilini kma tukitazama hizi comments zetu kwa makini?

  Hebu ngoja nikunukuu hapa: “kwamba mko kanisani katika ibada, labda watu 4000, baada tumbuizo la kwaya yenu ya vijana, ndipo anaingia mchungaji wenu. Basi mchungaji huyo ni mwanamama, ana makalio makubwa, na hips zilizojitosheleza, kisha amevaa suruali ambayo imemuingia katika msamba na kuyagawa makalio yake, na kiblauzi chake kinachoyaonesha matiti yake kwa chati hapo yalipobanwa pamoja na kutengeneza mfereji wa kupendeza, amekichomekea; kisha akaanza kutamba kwa munkari wa mahubiri akizunguka huku na kule; hebu niambie, ni wanaume wangapi watakaoingia katika hukumu ya UZINZI yenye adhabu ya kifo kwa kumtazama na kumtamani mchungaji wenu huyo? ”

  Mr Lwembe kama wewe uko sawa na mmoja wa waumini uliowatolea huu mfano basi uko kwenye hatari kubwa sana, yaani umesimama kwenye udongo wa utelezi. Kama bado unamtazama mwanamke kwa mtindo huu, a.k.a mtido wa KUVUSHA, basi wewe huwa uko salama tu ule muda mfupi unaokuwa kanisani (ibadani) kwenu, punde unapotoka na kuingia mtaani unaanza kuingia kwenye hiyo uliyoisema hukumu ya uzinzi, maana mtaani zinavaliwa zenye kuonesha zaidi ya ulichokisema.

  Halaf kwa nini umwangalie mwanamke kwa kumchunguzachunguza kiasi hicho na kwa mtazamo huo, kama si roho ya tamaa ni nini? Kwani wenye hips na makalio makubwa wakivaa magauni makalio na hips zao huwa zinapungua ukubwa? Vipi kuhusu wanaume wanaoonekana suruali zao zimetuna pale mbele (madhbahuni) eidha kuelekea upande wa kushoto au kulia ulishawauliza wanawake wakakwambia huwa wanajisikiaje wakiona hivyo?

  Hata hivyo huyo mama mchungaji mwenye kuvaa suruali ya hivyo hatakuwa amafanya jambo jema sawasawa na baba mchungaji ambaye atakuwa amevaa suruali nyepesi bila kujisitiri vizuri mzigo wake wa ndani na kusababisha mzigo huo kutuna na kuvimbisha suruali mpaka kila mshirika akaona.

  Kwa hiyo ishu haiko kwenye suruali mr. Lwembe bali iko kwenye kuvaa mavazi yenye kusitiri. N vazi lenye kustiri laweza kuwa suruali, kikoi, kanzu n.k

  Mwisho; si kweli kwamba ukristo una utamaduni fulani wa jumla katika masuala kama ya mavazi. Ispokuwa kila jamii wanapomfuata krito hutakiwa kufuata yale ambayo ni mema na biblia inayakubali yaliyo katika utamaduni wao. Kwa mfano mmasaai akiokoka ni sawa akiendelea kuvaa lubega zaka ,asilazimishwe kuvaa sketi au suti, na mskotishi mwanaume akiokoka ni sawa akiendelea kuvaa sketi.

 19. Wapendwa Mwalemwa, Sungura na wengineo,

  Kwa kadiri ninavyowaona, inasikitisha saana kwamba mnatembea sana mwilini mpaka Injili inawakimbia! Kwa taarifa yenu Kanisa leo hii liko katika ulimwengu wa roho, lilikwisha ondoka mwilini siku nyingi sana, ndio maana haki yetu inapaswa izidi ile ya Mafarisayo!

  Mnapozungumzia ‘ustaarabu’ au ‘utamaduni’, katika maana halisi ya mambo hayo, kisha mnapotaka kuuchanganya na Ukristo, ni lazima muishie katika “uvuguvugu”!! Ukristo by itself ni utamaduni na ustaarabu unajitosheleza katika mambo yote, kuanzia mavazi mpaka, you name it!! Sasa hayo hayaji kwa sheria, bali hujidhihirisha katika upendo. Maana Roho Mtakatifu anapowajilia, yeye haji mtupu, bali huja na package nzima ya jinsi ya maisha mapya, mwenendo mpya, mavazi mapya, katika namna ambayo humstahilisha huyo aliyenunuliwa kwa Damu ya thamani!

  Adamu na Hawa, kabla ya Mungu kuwashonea hayo mavazi, wao walijitengenezea mavazi, kulingana na hekima mpya waliyoipata baada ya kula lile tunda. Lakini Mungu alipowakuta katika mavazi hayo, aliyaona HAYAFAI, ndipo akawatengenezea mavazi ya mapya, ile DINI safi iliyosafika kwa damu ya mwanakondoo, hiyo ndiyo iliyowafunika huko mwanzo na sasa anapokuja tena leo hii, yeye huja tena na mavazi yanayostahili, akituvua mavazi yetu yasiyostahili. Wanawake wa Kiswati, wakiwa matiti nje katika mkutano wa Injili, Roho Mtakatifu alipowashukia, kila mmoja alitafuta nguo ya kujisitiri; hata hawa mnaowavisha hizo suruali, wakishukiwa na Roho Mtakatifu, watazivua!!!!

  Hebu wazia jambo hili: kwamba mko kanisani katika ibada, labda watu 4000, baada tumbuizo la kwaya yenu ya vijana, ndipo anaingia mchungaji wenu. Basi mchungaji huyo ni mwanamama, ana makalio makubwa, na hips zilizojitosheleza, kisha amevaa suruali ambayo imemuingia katika msamba na kuyagawa makalio yake, na kiblauzi chake kinachoyaonesha matiti yake kwa chati hapo yalipobanwa pamoja na kutengeneza mfereji wa kupendeza, amekichomekea; kisha akaanza kutamba kwa munkari wa mahubiri akizunguka huku na kule; hebu niambie, ni wanaume wangapi watakaoingia katika hukumu ya UZINZI yenye adhabu ya kifo kwa kumtazama na kumtamani mchungaji wenu huyo? Basi wanawake hao wenye kuvaa hizo suruali mnazo zishabikia, mkiwadanganya dada zenu, wanawaingiza kifoni wanaume wangapi kila siku? Hao wanawake wenyewe, licha ya kukiri kwao huo wokovu, Je, wanajua kuwa wamepoteza wokovu wao na sasa wanatumika kama vifaa vya kuulia watu wasio na hatia??

  Muwe makini katika nyendo zenu, maana unapomuona mwanamke ametinga mavazi ya kiume, basi jua kuwa she is perveted, pamoja na mume au mzazi anayeruhusu mambo hayo!!!

 20. Mungu akawatengenezea mavazi Adam na mkewe, akamshonea suruari na shati Adam na akamshonea sketi na blauzi Eva” Unashangaa kwani hujaisoma katika kitabu cha Mwanzo?

  “Unajua wapendwa wanaiga utamaduni wa kigeni”. Ok wewe vipi umeiga utamaduni wa kinini, kienyeji au?

  Mnapenda wanawake wavae sketi ili uendelee kuwachungulia wakijisahau eh? Tunapenda sana kukaa na khanga makanisani ili wanawake wakianguka chini wakati wakifanyiwa huduma tufanye kazi ya kuwafunika eh?

  Mapokeo hayana tofauti na utumwa, inaweza kuchukua vizazi hata kumi kuyaondoa kichwani.

  Anyway, that’s enough. This is such a trivial issue to spend time discussing!!!!!

 21. UKWELI NI KWAMBA ANAETAKA AVAE ILA SURALI SIO VAZI LA KIKE YOTE UTAKAYO SEMA UTAJITETEA TU, KWANI HII YOTE NI KUIGA UTAMADUNI WA KIGENI NA KUTAKA UTANDAWAZI USIWAPITE LAKINI KWA ALIYE OKOKA ASIVAE,,. KWANI SHETANI AKITEKA UFAHAMU WA MTU ANAKUPA NJIA NYINGI NA MIFANO ILI TU AWAPATE. MWANAMKE SURUALI SIO VAZI LAKO!!!!!! IGA TU KWA VILE UNATAKA, KWANINI ULETE MASWALI MENGI UKIVAA SKETI YAKO UNAJISIKIAJE ILI TU TOFAUTIANE, NADHANI HAUTA PUNGUKIWA VAA SKETI ASANTE.

 22. ninavyojua mimi hakuna suruali za wanawake ila ktk kumsaidia kazi shetani watu walibuni vazi wakaliita hivyo lakini mwanamke hastahili kabisa kuvaa.

 23. Enyi mnaosema wanawake hawaruhusiwi kuvaa suruali, ACHENI KUDANGANYA WATU! Tangu lini wokovu ukawa reduced to whether umevaa suruali au sketi?

  Itakufaa nini kama ukivaa sketi na moyoni ukawa hauko sawa? (Mathayo 23:28)

  Wanadamu tunatazama ya nje lakini Bwana hutazama mioyo (1 Samwel 16:7)

  Jamani, hivi kweli lipi lililo muhimu mbele za Bwana, kwamba umevaa suruali au sketi au kuwa sawa na Bwana moyoni? Kwa wale mnaosema suruali haziruhusiwi kwa wanawake, mnamaanisha haiwezekani kwa mwanamke anayevaa suruali kuwa sawa na Bwana moyoni?

  Suala la mavazi ni la kiutamaduni zaidi na lazima tuelewe kuwa utamaduni unabadilika (tradition is dynamic not static). Hivi mnafikiri hata hizi suruali zilikuwa vazi la Kitanzania kabla watu toka tamaduni nyingine hawajaja (kabla ya ukoloni etc)? Au ni kwanini basi leo hii wote tusivae majoho au kanzu kama utamaduni wa kiyahudi enzi zile Yesu allipokuwa duniani? Au ni kwanini tusivae mavazi yetu ya asili kabisa (mgolole kwa wahehe na wabena, rubega kwa wamasai n.k)? Kama utamaduni uliweza kubadilika hapa kwetu, wanaume wakaacha migolole na rubega na kuvaa suruali, ni kwanini utamaduni huu unapobadilika tena na wanawake kuanza kuvaa suruali ZA KIKE inakuwa suala la kubishana tena.

 24. Asante wote kwa michango yenu, nashukuru kwamba mchango wangu unaweza kusaidia wengine, basically kama alivyonotice John Paul ninapenda kuchangia ili niweze kujifunza pia ninapenda sana kujifunza kwa vitendo yaani kushiriki, hivyo popote mnapoona nimekosea msichoke kunijuvya. ni kweli ninashuhuda kubwa lakini Mungu akiniwezesha nitakuwa ninazitoa kwa awamu ili wengine waweze jifunza. Kwenu akina dada ninawapenda na ninaomba sana mfuate maadili ya Kikristo ili kuepuka matatizo mengi kama vile ndoa zinazovunjika au kuleta maradhi kama UKIMWI. Barikiweni

 25. Ndugu Mubelwa,

  Nashukuru kwa jibu la mchango wango.

  Ni kweli ulivyosema kwamba tuna viwango tofauti vya uelewa. Na hii ndiyo inatufanya tuzidi kuhitajiana kwa sababu kila mtu anayesoma hapa anauelewa zaidi wa jambo fulani kuliko mtu mwingine. Ni kweli pia kwamba kila mtu ana background na struggle yake ya maisha tofauti na ya mwingine. Kwangu mimi naona hii ndiyo sababu inayotufanya tunajadiliana hapa kwa kubadilishana ujuzi na uzoefu wa maisha, na hasa, maisha ya Kikristo kwetu sisi ambao tumekubali kumfuata Yesu! Kama tungekuwa na kiwango cha uelewa kinachofanana pia background za maisha nazo ziwe zinafafana, naamini hakuna mtu angehangaika kutembelea blog hii kwa sababu kila ambacho kingekuwa kinaandikwa kingekuwa kinafanana tu na yale aliyonayo. Kule kutegemea kupata mambo mapya, kila mtu anapotembelea hapa, ndiko kunakoongeza uzuri wa blog na kwa wengine, kama kwangu mimi, blog hii imekuwa kama sehemu ya maisha yangu kwa sababu yako mengi ya kujifunza kutoka kwa wengine kila wakati ninapotembelea hapa!

  Katika michango yangu mimi huwa ninazingatia sana ninachoandika nisije nikaropoka. Na kwa kila kitu ninachoandika hapa huwa nina akiba nyingine ya kutosha kukifafanua. Ndiyo maana mara nyingi huwa naandika kwamba niko tayari kujibu kila swali linaloweza kuwa limejitokeza kutokana na mchango wangu. Kama kuna mahali unakumbuka kwamba nilisema tofauti na sasa, kwa maana ya kupingana, ninauhakika kabisa itakuwa ni namna ulivyoelewa wewe. Lakini kama pangehitajika ufafanuzi ningefanya hivyo ili kufafanua kile nilichomaanisha kwa kuandika vile. Lakini kwa kuwa umesema hauna tatizo na jambo hilo, nami pia nasema kwamba sina tatizo nalo. Kwa hiyo tusonge mbele!

  Katika jibu lako nimezingatia haya:

  “Kama nilivyokwambia awali, siko hapa kupingana na neno la Mungu lakini kama nikiuliza nikaonekana hivyo, then ni vema usinijibu kuliko kutaka kuonesha kuwa UNANIFAHAMU KULIKO NILIVYO.
  Kwa hiyo kuna haki ya kuelimishana lakini si haki ya kuelewana hasa unaponielewa tofauti na nilivyo. Ungejua Background yangu na struggle yangu na maisha yangu kwa ujumla ungeweza kuelewa maana na nia ya kuuliza haya. And now that you don’t know it, you wont know it.
  Sina RESPONSE zaidi ya hii kwako na ukitaka kuendelea kuelimishana i’ll be more than happy, if not, then just read and don’t try to be in my personal abilities of understanding.”

  Maneno yangu kutokana na hiki ulichoandika ni haya:

  Ninavyofahamu mimi ni kwamba kinachotusaidia hapa ni kile ambacho mtu unachoweza kushirikiana na wenzako na si status ya maisha binafsi. Hata kama ikitokea uwezekano wa watu kuelewana background ya maisha yao kitakachokuwa na msaada ni kama katika ushuhuda wa maisha hayo kuna mtu mwingine anaweza akajifunza kitu, lakini kama hakuna cha kujifunza basi kuyaelewa maisha ya mtu mwingine itakuwa ni kupoteza wakati. Ndiyo maana tunasoma habari za maisha ya watu wengi kwenye Biblia ambao background na struggles zao za maisha vina ushuhuda ambao ni muhimu kwa wengine kujifunza kitu. Ndiyo maana tunasoma habari nyingi sana kuhusu Mfalme Daudi, Ayubu, Dabiel, Ibrahimu na wengine wengi. Hata hivyo kuna watakatifu wengine wengi ambao walitembea na Mungu katika maisha yao na wakafa katika uchaji Mungu. Lakini si wote ambao habari zao zimeandikwa kwenye Biblia kwa sababu tu katika shuhuda za maisha yao hakuna kitu cha kumsaidia mtu mwingine. Ndiyo maana hakuna habari yoyote, kwa mfano, inayowahusu wale watu 700 ambao hawakumpigia goti Baali wakati wa Eliya, Mtishibi!, japo pia walikuwa mashujaa wa Imani na Mungu anawatambua. Kama background yako inaweza kunifaa kwa namna moja au nyingine ningependa kuifahamu lakini kama hakuna lolote la mimi kujifunza, sina haja nayo!…… Endelea kuishindania imani na kuutafuta kwa bidii utakatifu ambao hapana mtu atakayemuona Mungu asipokuwa nao.

  Kwa hiyo ndugu Mubelwa kama background na struggle yako ya maisha vina kitu cha kuweza kumsaidia mwingine ni vema ukaweka ushuhuda wako. Pengine kwa kufanya hivyo wengi, pamoja na mimi, wanaweza kujifunza kitu na kusaidika katika maisha yao. Na zaidi sana jina la Mungu litatukuzwa!

  Kwa mimi kuifahamu background yako kuna faida si kwangu tu ambapo yawezekana nikajifunza kitu lakini pia itakusaidia wewe katika jitihada zako za kufundisha wengine. Mchango wako hapa ni wa muhimu sana pia. Lakini umuhimu huo utaonekana tu wakati mchango wako unapokuwa umeeleweka kwa wasomaji. Lakini kufundisha huku unakokufanya wewe, bila kuweka wazi maana yake hasa ni nini, kunafanya michango yako mingi, kama si yote, ipate changamoto pingamizi. Na mwisho wa yote utaendeelea kuonekana kama mtu mwenye kutetea mambo mengine tofauti na ukristo. Kinachofanya uonekane hivyo ni huko kutumia staili ambayo bado maana yake haijaeleweka, nawe bado unaificha!

  Kuna watu ambao, japo kwa ufupi sana, walishaweka hapa background zao ambazo ndizo zinafanya wanachochangia kiwe kilivyo. Nakumbuka dada Mary Sabihi alishafanya hivyo, na recently dada Rose kafanya hivyo pia. Ushuhuda wa namna hii unajenga sana na unasaidia kujibu maswali iwapo mtu atakuwa anajiuliza nini maana ya mtu huyo kuchangia vile au kuuliza vile. Na hakuna njia ya kuelewa ushuhuda wa mtu kama si kaamua kuutoa mwenyewe. Ni kwa sababu, kwa mfano, dada Rose aliweka background yake, japo kwa ufupi kama nilivyosema, ndiyo maana siwezi kumuuliza nini maana yake kuchangia kama vile, kwa sababu tayari nimeshamuelewa. Sasa wewe kama unaficha background yako, japo kwa ufupi, kuhusu kinachokusababisha michango yako ‘iwe kama’ ya mtu anayepingana na maadili ya kikristo, tegemea kupata changamoto kwa kila mchango unaouandika ambao haueleweki uko upande gani! Si kutoka kwa John Paul tu bali hata kwa msomaji mwingine yeye yote anayefuatilia kwa makini michango inayotolewa hapa!

  Tuendelee kujifunza!

 26. Hakuna mtu ATAKAYETIMULIWA BILA YA KWANZA KUKETISHWA NA KUAMBIWA/KUFUNDISHWA YOTE(Kweli YOTE).
  HIVI Wewe unafikiri hawa wadada/wamama wanaovaa vinguo vya AIBU HAWAJIJUI NDANI YA MIOYO YAO KUWA WANAVAA HIVYO ILI KUTEGA MITEGO YAO? WENGI SANA WANAVAA HIVYO KWA MALENGO MAALUM YA KUNASA WANAUME na ENDAPO mimi nikawa mchungaji MIMI NITAKUWA NAWAFUKUZA wasiingie kanisani na vinguo vyao vya aibu!

  HATA KWENYE BUNGE LA SERIKALI wewe unafikiri unaweza ukaona wamama wamejivalia tu vinguo vya AIBU? HASHA!
  SASA HAMJUI KANISANI NI MAHALI PA HESHIMA SANA?

  MSIMAMO WANGU: Mwanamke/mwanaume avae ajisitiri kwa HESHIMA NDIPO AINGIE KANISANI(UMATI WA WATU WA MUNGU), kama hataki kuvaa kwa heshima ARUDI NYUMBANI AU AENDE WANAKOKUBALI UCHAFU/UOVU/UKENGEUFU!

  Martin.

 27. Asante saana Ndugu SHOO kwa mistari yako hiyo. Naamini kwa kuisoma na kuielewa naweza kushirikiana na yeyote mwenye mapenzi mema kuielimisha jamii nayo IKAEPUKA kufanya yaikwazayo jamii. Na hili ndilo nililokuwa nikisema kuwa TUKIWAFUNDISHA ILIYO KWELI WATAACHA WENYEWE lakini sio KUWATIMUA BILA KUJUA KWANINI TWAFANYA HIVYO.
  Kwa mara ya tena ASANTE NA NASHUKURU KWA KUFIKIRIA OMBI LANGU NA KUNIELIMISHA

 28. Namshukuru Mungu kwa ajili ya wote mliochangia baada ya swali nililouliza muda mrefu, nilichotamani kujifunza nimejifunza kwa sehemu, MUNGU AWABARIKI SANA WACHANGIAJI WOTE.

  Unajua? Mungu kama muumbaji ni wa ajabu sana sana. Kila kitu alichokiumba Mungu ana makusudi kamili. Kila kiumbe kwa Mungu kina makusudi na umuhimu wake. Kila kiungo cha mwanadamu kina umuhimu na makusudi yake, viungo vingine twaviona muhimu sana kuliko vingine, vingine tunavipa heshima sio Afrika tu bali duniani kote.

  Mwanamke kaumbwa kwa namna ya ajabu sana, vipo viungo vya mwanamke havipaswi kuonekana hivi hivi. Hapa sizungunzi kwa msingi tu wa Neno la Mungu tu bali nature ndivyo inavyobainisha. Ndo maana duniani kote kuna standards za mavazi rasmi katika maeneo fulani fulani na kwa sababu maalum. Tukikataa kuwa mavazi hayazungunzi tutakuwa tunajidanganya.

  Wapendwa wengi tunajidanganya kuwa hata mwanamke akiwa uchi mbele yako hakuna shida, lakini hii sio kweli. Maneno ya Yesu ya kuwa amtazamae mwanamke kwa kumtumani amekwishazini nae nafsini mwake ni muhimu sana kuyazingatia. Kwa namna hii Yesu alivyozungunza wanaume wazinzi leo watakuwa wangapi? Yumkini mwanamke mmoja kwa kuvaa mavazi yasiyo ya adabu, akawafanya wanaume wengi tu kutenda dhambi ya uzinzi nafsini mwao bila yeye binafsi kujua kasha zini nafsini na wanaume kadhaa. Nikukumbushe mbele za Yesu ukizini nafsini, na ukazini kwa mwili hizo zote ni dhambi sawa tu. Itashangaza tutakapofika Mbele ya kiti cha hukumu na binti akaambiwa alishazini na wanaume kadhaa ambao wengine hakuwahi hata kuwaona akashangaa. Lakini jibu la Yesu yumkini likawa ulipovaa nguo isiyokusitiri ulimfanya mwanaume fulani kukutamani na kuzini nawe nafsini mwake. Nadhani tutabaki tunashangaa.

  Wapo wanaume dhaifu, akimwona mwanamke yuko uchi au nusu uchi ni taabu tupu. Sasa wewe mwanamke uliyeokoka kwanini kumsababishia kijana au baba wa watu dhambi kwa ajili ya nguo tu?

  Nimeona maswali kadhaa yakiuliza uongozi wa Neno la Mungu kuhusu mavazi, hapa Neno linatoa rules au guidelines

  1Timotheo 2:9-10 Kadhalika, nataka wanawake wajipambe kwa heshima na kwa busara. Mavazi yao yawe nadhifu, si kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu na mavazi ya gharama kubwa, bali kwa matendo mema kama iwapa savyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.

  1Petro 3:1-5 Kadhalika ninyi wake, jinyenyekezeni chini ya waume zenu, ili kama wako wasioliamini Neno, wapate kuamini kwa kuvutiwa na mwenendo wa wake zao. Hawatahitaji kuambiwa neno, kwa sababu wataona maisha yenu safi na ya kumcha Mungu. Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje, yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. Bali kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu. Maana ndivyo walivyojipamba wanawake wata katifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao.

  1Korintho 8:9,12,13 Lakini hata hivyo tuwe waangalifu jinsi tunavyotumia uhuru wetu tusije tukawakwaza walio dhaifu katika imani……Mnapowatenda dhambi ndugu zenu kwa njia hii na kuharibu dhamiri zao dhaifu, mnamkosea Kristo. Kwa hiyo kama chakula kitamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke.

  Nadhani kwa mistari hii hapo juu haina maana tusivae nguo nzuri na za heshima, bali kabla ya kufikiria mavazi haya ya adabu na heshima, tuwaze kwanza upambaji ndani ya mioyo yetu. Itakuwa vigumu kuni-convice kuwa mwanamke anaevaa mavazi ya aibu ndani ya moyo wake kajivika adabu na heshima.

  Kwa leo nihitimishe kuwa uzuri wa sura ya mwanamke hauletwi na kuvaa na kujipamba kama miss world au mwanamuziki fulani maarufu. Uzuri wa mwanamke anaemcha Mungu upo katika moyo ulipambwa na unyenyekevu, adabu, busara na heshima. Ukiwa na moyo wa namna hii utavaa kwa adabu, busara na heshima pia.

  Tuendelee kufundishana, MUNGU AWABARIKI NYOTE

 29. Amani, Heshima na Upendo kwenu
  Ndg Martin. Kama unahisi haitasaidia that’s fine. Na kwa mimi kuuliza nulizayo si kwamba NAPENDA KUWAFURAHISHA WATU WAOVU, LA HASHA. Huo ni MTAZAMO WAKO kutokana na kushindwa ku-prove namna utakavyo-execute ufukuzaji wako. Again, mimi nipo hapa kujifunza, kama hudhani kuwa unaweza kuelimisha THAT’S FINE.
  Dada Rose, asante kwa mara ya tena. Sina ubishi na ukweli kuwa kuna mavazi yakwazayo, lakini kam mtu anafikia hatua kuwa NTAWAFUKUZA basi ni lazima awe na vigezo atakavyoangalia kulingana na NENO LA MUNGU. Ama kama ilivyokuwa kwako, AWASAIDIE WAOKOKE NA WAYATAMBUE MAVAZI HAYO KWANI KWA KUWAOKOA NAO WATAANZA KWENDA NA TUNE YA WOKOVU NA HATAHITAJI NGUVU ZOZOTE KUWAFUKUZA BALI WAO WENYEWE WATAJIONEA AIBU.
  Kakangu John. Am glad you didn’t go as far as you did the other day. Ni kweli kuwa unaweza kurudiwa na wasiwasi kuwa hakuna nililojifunza ama kuelewa. That’s fine. Tunatofautiana uelewa na unaweza kuwa muelewa kuliko mimi. And i don’t mind and or have problem with that. Nakumbuka ulisema katika makala moja kuwa Neno la Mungu ndilo linaloongoza na tunatakiwa kufuata Biblia isemavyo (sijaweza kuwa na muda wa kusaka uliposema haya) na kuomba mtu ku-refer kwenye Biblia. Lakini sasa unasema vingine. Na sina tatizo na hilo.
  Kama nilivyokwambia awali, siko hapa kupingana na neno la Mungu lakini kama nikiuliza nikaonekana hivyo, then ni vema usinijibu kuliko kutaka kuonesha kuwa UNANIFAHAMU KULIKO NILIVYO.
  Kwa hiyo kuna haki ya kuelimishana lakini si haki ya kuelewana hasa unaponielewa tofauti na nilivyo. Ungejua Background yangu na struggle yangu na maisha yangu kwa ujumla ungeweza kuelewa maana na nia ya kuuliza haya. And now that you don’t know it, you wont know it.
  Sina RESPONSE zaidi ya hii kwako na ukitaka kuendelea kuelimishana i’ll be more than happy, if not, then just read and don’t try to be in my personal abilities of understanding.
  Blessings

 30. Niliposoma yale maneno ya Mubelwa Bandio akisifia uelimishaji bora kabisa kuliko wowote aliowahi kusoma kwenye blog hii nilitaka kumuuliza ameelewa nini na kuelewa huko kumemsaidiaje yeye lakini nikasema ngoja nivute subira, isije ikawa kweli kaelewa kitu halafu mimi nikawa mrukiaji wa mambo! Lakini maneno ambayo Mubelwa bado anaandika na hata kufikia kuhitaji mistari ya Biblia inayotaja kwamba ‘MAVAZI YA WANAUME NI HAYA NA HAYA halafu ya WANAWAKE NI HAYA NA HAYA au WANAWAKE HAWATAKIWI KUVAA SURUALI KANISANI’ yanafanya ule wasi wasi kwamba yawezekana hakuna alichokuwa amejifunza, unirudie! [simaanishi hakuna alichojifunza].

  Kama ni kweli Mubelwa alikuwa ameelewa kitu kutokana na mada hii mimi sikutarajia tena aendelee kudai maandiko specific kwa ajili ya suruali, gauni, blauzi na pengine hadi soksi. No! Biblia si kitabu cha sheria to be so detailed hata kwa mambo ambayo leo lipo na kesho halipo. Suruali unaivaa leo halafu baada ya siku mbili imetatuka is too minor kuchukuwa nafasi katika Biblia. Biblia ni package kwa ajili ya uzima wa milele! Mambo mengi ya kimwili yamejumuishwa katika maandiko ya pamoja kwa kuwa si mambo hayo peke yake yanayomkamilisha mtu katika njia ya utakatifu bali ni Uongozi wa Roho Mtakatifu!

  Biblia si kitabu cha sheria bali ni kitabu ambacho hujenga msingi moyoni mwa mtu ili aweze kuipokea Neema ya Wokovu na kisha Roho wa Mungu akae ndani yake kwa ajili ya live directions! Hiki ndicho ameandika dada Rose katika kipengere chake cha 5. Baada ya kuteseka katika ubishi wa dini hatimaye alipoupokea wokovu, sasa, she flows with the tune kwa sababu moyoni kumebadilika. Hategemei maandiko tena kwenye karatasi bali hujisikia amani au hatia moyoni mwake kutegemea na jambo husika. Ndiyo maana nilimwandikia ndugu aliyekuja kwa jina la Mr. G kwamba maandiko ya Biblia yana kazi zaidi katika kuwaelimisha watu waingie katika wokovu kuliko kuwaongoza watu ambao wameshaokoka tayari! Maana mtu akiokoka dhamiri yake huwa hai! [na hiki ndicho ameandika dada Rose pia]. Wokovu goes far beyond akili! Moyo wa mtu huanza kufurahia uongozi wa roho kwa kuona ubaya au uzuri wa jambo fulani hata kabla akili haijaona maandiko ya jambo hilo. Katika mada ya wanaume kuvaa cheni niliandika kwamba Roho Mtakatifu ana mambo mengi sana ya kutufundisha zaidi ya yale yaliyoandikwa kwenye Biblia. Kilichoandikwa kwenye Biblia ni msingi tu lakini kuna issues nyingi sana ambazo wale wanaoogozwa na Roho hushuhudiwa mioyoni mwao usahihi au kutokuwa sahihi kwayo. Wokovu hauendi hivyo kwamba kila jambo lipate word to word scripture ili kuonekana kwamba ni sahihi au si sahihi!

  Hata hivyo ndugu Martin alikusanya maandiko mengi sana kuhusiana na mambo haya. Dada Rose naye akaandika jinsi ambavyo kuna watu wako makanisani, wanafundishwa kila siku lakini wanang’ang’ania kufanya mambo ambayo hayana tija yoyote. Halafu akaongeza maandiko mengine tarehe 2/10/09! Mimi nilifikiri yalikuwa yanatosha na zaidi, kumbe kwa sababu hakuna palipoandikwa “mwanamke akivaa suruali kanisani afukuzwe” bado hayajafaa??????
  Hata hivyo What is suruali hadi imfanye mtu ang’ang’anie kuvaa tu hata baada ya kuonywa? Kung’ang’ania huko lazima kuwe na nguvu ambayo iko kinyume na ile nguvu inayoonya! Mengi yalishaandikwa kuhusu umbile la mwanamke na jinsi ambavyo anatakiwa ajisitiri. Hata hapo juu dada Rose pia amelirudia suala hilo. Lakini naamini kuna watu walishaelimika kutokana na maelezo ya namna hiyo!

  Kudai maandiko specific kwa kila item siyo ishara nzuri. Hii ina maanisha kwamba tunataka tuongozwe kwa sheria na tuwe tunatembea na vi memo vya maandiko, ukiona jambo fulani unafungua usome, na usipoona maandiko yanayohusu inabidi ukubaliane nalo tu hata kama moyoni unajisikia hatia? [kama alivyoandika dada Rose katika kipengere cha 5]. Katika hali hiyo Roho Mtakatifu hatakuwa na kazi tena kwa kuwa tutakuwa tunaongozwa nasheria. Hali ikiendelea hivi iko siku mtu ataingia na chupi kanisani halafu akikemewa atadai maandiko yanayokataza kuvaa chupi kanisani. Hatuwezi kufika kwa mtindo huu!

  Kuna mahali nilishaandika mfano mmoja kwamba watu wanaovuta sigara si kwamba wanavuta kwa sababu hakuna mahali palipoandikwa kuvuta sigara ni hatari. Sasa kama pamoja na kuandikwa kwenye packet yake kwamba uvutaji wa sigara ni hatari watu wanaendelea kuvuta, unafikiri itawezekanaje mwanamke mpenda kuvaa suruali aache kuvaa kanisani wakati hakuna mstari wowote kwenye Biblia unaosomeka hivi; “Hairusiwi kwa wanawake kuvaa suruali kanisani”???. Mfano huu una-hold pia kwa mwanamke anayependa kuingia na mavazi ambayo hayamsitiri mwanamke kanisani. Hata kama atasomewa maandiko yanayohusu suala hilo 7X70 kwa siku, kama moyo wake haujaelewa onyo analopewa bado ataendelea kuvaa!

  Martin ameandika kuna uwezekano wa kuandika saaana saaaana hapa kuhusiana na mada hii lakini isisaidie! Pia kuna mahali ndugu Mubelwa aliandika hivi:
  “Kwa hiyo nakushukuru kwa maoni yako Dada Rose na nafurahi kuwa licha ya kutokukubaliana, tumeendelea KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA.”
  Ingawa hapa mimi nilishangaa kwamba kwa nini ‘kutokukubaliana’ kuwe ni jambo la kufurahisha kwa watu ambao wote wanajiita ni wakristo, nikataka kuuliza swali lakini nikanyamaza ili nione kama kutokukubaliana huko kweli kutaleta furaha aliyoitaja ndugu Mubelwa!

  Lakini hata sasa, hali inavyoonyesha, naona inaweza ikafikia hatua tukakubaliana kutokukubaliana. Hali ikifika hivyo, kwa upande wangu, si jambo la furaha na wala siwezi kufurahi kwa sababu tumekubaliana kutokukubaliana. Kwangu mimi kinacholeta furaha ni kukubaliana kwa kumaliza tofauti zilizopo ili kweli tuwe wenye nia moja.

  Nasubiri kwa hamu kusoma response ya ndugu Mubelwa hasa baada ya dada Rose na kaka Martin kuandika waliyonayo. Najua mimi niliingilia tu, na kilichonifanya niingilie ni lile suala la UABUDUJI ambalo, kutokana na majibu ya Mubelwa, natumaini tumeshali-close! Nilishaandika mengi sana kuhusiana na mavazi ikiwa ni pamoja na suruali kwa mwanamke, kwa hiyo kwa sasa natamani nisome kutoka kwa wengine.

 31. Ndg Mubelwa, mchango wangu hautofautiani na wa Ndg John Paul na Martin, wamechambua vizuri sana mie naongezea tu kuonyesha kuwa ninaunga mkono hoja zao na najaribu kujibu niwezavyo; ila kwa leo sina muda wa kuichambua hii mistari ina verse namba ngapi:
  1. Mungu alipotuumba tulikuwa hatujui wema na ubaya kwani tulikuwa bado tunamtii (ubaya haukuwepo) kutokutii kwa kula tunda Edeni walifunguliwa macho wakaujua wema na ubaya ni kitu gani cha kwanza walichotambua kuwa si sahihi? NI YA KUWA WAKO UCHI! na Mungu kuonyesha hapendezwi na hali hii wala vile vimajani walivyojifunika aliwavika nguo za KUWASITIRI
  Hivyo baada ya kuondolewa Edeni Mungu alitupa utashi wa kujua mema na mabaya kama hapo juu. Kwa kukujibu tu mtu yeyeto mwenye akili timamu anao utashi wa kujua mema na mabaya.
  2. Katika Biblia pia tunaambiwa kuna mavazi ya Kikahaba (yule mwanamke malaya katika Kitabu cha Methali ametajwa amevaa kikahaba) Hivyo mavazi ya makahaba na wasio kahaba yanatambulika katika jamii.
  3. Mtume Paulo alifundisha tusichanganye mavazi yampasayo mwanaume na mwanamke, KILA MTU AVAE ILIYO STAHILI YAKE. Suruali na vazi la kiume, vivyo kusuka nywele na hereni ni vya kike, sio kwamba wanaonewa ila siku COMEDY wakiingia kanisani na yale mavazi yao na ndevu usoni watarudishiwa mlangoni, wanaume wenye kusuka pia na bukta & vesti hao pia sijui ni utashi gani huo.
  4. Hivyo ndg Mubelwa mtu yeyote awe Mkristo au si Mkristo anao utashi wa kujua kuwa nimevaa vipi, watu wananitazama vipi, hapa ni wapi na panafanyika nini?! more so womens who are naturally very conscious in their appearance! wanaelewa kuwa ninapoenda kusimama mbele za Mkuu fulani ambaye ndiyo ameshikilia uhai wangu na kila kitu changu ninapaswa kuvaa nini? otherwise unaye mwingine ambaye ameshikilia haya maisha yako, na kama ni hivyo basi huna moyo uliopondeka mbele za Mungu wangu nenda kwa huyo Mungu unayemwamini na code of conduct yake! Niambie ukienda ukweni kuchumbia au kuchumbiwa mtu ambaye unajua ni familia ya heshima unaweza vaa vest na bukta au msichana pedal pusher??
  5. Mkristo ambaye ameokoka na anafuata au ana moyo wa kupenda kujifunza ataongozwa na Roho mtakatifu mambo yote katika maisha yake ikiwemo mavazi. Ninasema hivi kwani nami nilikuwa mbishi na dini yangu lakini toka nimeokoka I just flow with the tune yaani ukitaka kupinga mwenyewe utaona hatia
  6. Mtumishi anayeongoza sio dira yangu eg Joyce Meyer, na anachoongea ninachuja pia, ibada yangu na dira yangu ni Mungu kupitia NENO lake, mtumishi anakujenga tu na wewe pia unapaswa kumwombea na kumkemea kama anaanguka mfano Mtume Paulo alimkemea Mt Petro alipokataa kula na wasiotahiriwa kuogopa kutengwa na wayahudi.
  7. Ninamwomba Mungu Baba mwenye rehema atupe wote Roho ya hekima katika kusoma na kuyatambua makusudi yake katika NENO lake. Barikiweni

 32. Hapa naona tunaweza kuendelea sana kuandika ILA HAITASAIDIA.
  Makanisa yapaswa kuwa na taratibu ambazo zitajenga USIKIVU NA UTULIVU ili pawe ni mahali pa kusaidika bila kubughudhiwa kwa wale wenye kuhitaji msaada.Wale wenye kuja kuonyesha SHOW watafukuzwa, waende huko mtaani wakapigiwe makofi na walimwengu!
  MIMI NITAWAFUKUZA KAMA HAWATAKI KUFUATA TARATIBU TULIZOJIWEKEA.WATUMISHI wengi leo hii badala ya kuuleta ulimwengu kwa Yesu, WAMEULETA ULIMWENGU MAKANISANI MWAO halafu UWEPO NA HOFU YA MUNGU vimeondoka makanisani.
  Wewe unataka Kufurahisha watu waovu au unataka kuwalea wanyofu wa moyo hatimaye ufike nao mbinguni?

  MIMI NITAKUWA MKALI KAMA YESU KRISTO ALIVYOWAFUKUZA WAFANYABIASHA KULE HEKALUNI !
  WADADA/WAMAMA WAVAA MASURUALI WOTE WAENDE SEHEMU NYINGINE wanaoridhia uvaaji huo!
  MSIMAMO WANGU NDIYO HUO.

 33. Wow!!!
  Asanteni saaana Kaka zangu John ana Martin. Nimeweka pembeni suala la DINI na sasa wacha tuzungumzie WOKOVU.
  Narejea kwenye swali langu kuwa
  KWA MUJIBU WA BIBLIA INAYOTUONGOZA KUHUSU WOKOVU, NI WAPI PANAPOZUNGUMZIA SUALA LA MAVAZI SAHIHI NA YA KIKRISTO? Hili ningependa kupata jibu kwani ninapenda kujua VIGEZO VYA NENO LA MUNGU ambalo ndugu Martin atatumia kuwafukuza waliovaa masuruali kanisani. Hilo ndilo ninalopenda kujua kwani mimi sipendelei mavazi yawaoneshayo wakiwa nusu uchi, lakini siwezi kusema kuwa wakivaa suruali wafukuzwe kanisani kwani kanisa latakiwa kuongozwa na neno la Mungu na ningependa kujua reference ya mahala hapo.
  Kaka Martin umesema kama sitapinga mavazi basi NIMEPOA, NIMERUDI NYUMA, NI KIPOFU NA NINA WOGA lakini hujaniambia kuwa nipinge mavazi hayo kisha niwashauri yapi kwa mujibu wa andiko lipi?
  Sehemu kubwa ya maelezo yako inaonekana kuwa sahihi, lakini inaonekana ni NADHARIA ZAIDI KWANI SIJAONA ULIPOHUSISHA NA NENO LA MUNGU.
  Ni hilo tu ambalo mkinielimisha mtakuwa mmenipa ZANA ZAIDI ZA KUWAELIMISHA WENGINE.
  Kumbukeni kuwa twaelimishana ili tukawaelimish wengine, lakini kama uelimishaji tuutoao si sahihi, basi TUNAWAPOTOSHA WENGINE.
  Blessings

 34. Ndugu Mubelwa,
  Naamini aliyoandika ndugu John ni ya msaada mkubwa!

  NENO LA MUNGU NDILO LITAKALODUMU MILELE!
  POROJO za wanadamu zitapita!

  Hukumu yangu itaendana na Neno la Mungu.
  Na YESU ndiyo alituletea Wokovu ambao ni NEEMA YA MUNGU KWA WANADAMU WOTE. ILA PIA NENO LA MUNGU limetuonya tusiipokee NEEMA ya Mungu bure au TUSIENDELEE KUTENDA DHAMBI ETI KWA KUWA NEEMA IPO BURE(Soma Rumi 6).
  JAMBO lolote unalolifanya ambalo ni kinyume cha Maandiko na unawakwaza wapendwa( mfano uvaaji mbaya) basi wewe utakuwa hutembei katika UPENDO WA MUNGU.
  Ukishaonywa juu ya uvaaji wako mbaya na ukakataa kubadilika BASI SHARTI UAMBIWE TU NENDA UKATAFUTE SEHEMU NYINGINE WANAYORIDHIA MATENDO MAFU YA DHAMBI UKAJIUNGE NAO; lakini kama utataka kuwa nasi basi ujiweke jinsi tunavyotaka(JINSI TULIVYOPATANA SISI KWA SISI KWA KIGEZO CHA MAADILI YA NENO LA MUNGU).

  WOKOVU HAUNA CHA MAZINGIRA YA JOTO AU BARIDI.Wokovu unajali sana kutunza kuwa TAA na NURU ya ulimwengu.

  WEWE FUATA KILE NENO LIMESEMA USIWAANGALIE WAHUBIRI mashuhuri.Hatupo hapa kuwafuata wahubiri mashuhuri, TUPO HAPA KUMFUATA YESU KRISTO KWA NJIA YA NENO LA LAKE NA ROHO MTAKATIFU.

  Mungu akikukabidhi kanisa ulichunge inabidi uwe VERY VERY SERIOUS MAANA UTAKWENDA TOA HESABU MBELE ZAKE.NA INABIDI USIWAANGALIE WENGINE WANAFANYAJE BALI ANGALIA YESU KRISTO ALIFANYAJE NA ANASEMA NINI KWENYE NENO LAKE.
  KUMBUKA SIKU ILE YA MWISHO YESU ATAWAFUKUZA wahubiri/watenda miujiza wakubwa MAANA WALIKUWA WENYE KUJIFURAHISHA KATIKA DHAMBI!(Mtayo 7:21)
  PIA NENO LINASEMA KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA. NA PIA INASEMA KUMCHA BWANA NI KUUCHUKIA UOVU!

  “KUMCHA BWANA NI KUUCHUKIA UOVU”
  Sasa kama unauchukia UOVU WA UVAAJI VINGUO VYA AIBU si UTAUPIGA VITA KWA NGUVU ZOTE KANISANI KWAKO UKIWA MCHUNGAJI?

  BASI KAMA hautaupiga vita uvaaji mbovu BASI WEWE UMESHARUDI NYUMA, UMEPOA, UMEKUWA KIPOFU, HUONI MAMBO YALIYO MBALI, UMEJAA WOGA MAANA wewe ni mtu wa kidunia hii tu!
  NA INJILI utakayokuwa unaihubiri ni LOVE, PEACE GOSPEL(Ninaposema LOVE, PEACE GOSPEL ni hii injili inayohubiriwa siku hizi ambayo wahubiri wengi hawataki kuwaambia UKWELI wale washirika wao ili tu wasikwazike na kuhama makanisa ILI SADAKA ISIJE IKAPUNGUA).

  LENGO LETU LIWE KUWAHUBIRI WATU NA KUWALEA KATIKA NENO NA KUWAFIKISHA MBINGUNI.Lengo la wahubiri wengi sana leo hii ni kujaza makanisa yao ili WAPATE PESA NA VITU VYA DUNIA HII. MACHO YAO YAMEPOFUKA!
  HAWAONI TENA KUWA YESU YU KARIBU KUJA KUWANYAKUA WATEULE! HAWAONI TENA DHIKI KUU IPO MLANGONI KUUKABILI ULIMWENGU ULIOMKATAA YESU KRISTO!

  TWAPASWA KUWA SERIOUS!
  MUDA WETU WA KUISHI DUNIANI UNAZIDI KUYOYOMA!
  HATA LINI TUTAENDELEA KUFANYA MAKANISA KAMA KLABU ZA POMBE?
  HATA LINI TUTAENDELEA KULALA USINGIZI WA KIROHO NA KUWAHUBIRIA WATU JINSI YA KUPATA VITU vya dunia hii huku wakipoteza roho zao zenye thamani kuu mbele za Mungu?

  MAKANISA YANAPASWA YAWE NA TARATIBU TAKATIFU ZA KIMUNGU ZENYE KUHIMIZA UCHAJI WA MUNGU.
  NA WOTE WANAOKAIDI TARATIBU HIZI LAZIMA WAITWE NA KUONYWA NA ENDAPO WATAKATAA KUBADILIKA BASI WAFUKUZWE!
  JE, HAUJUI SISI WATEULE TUTASIMAMA NA KRISTO KUHUKUMU MATAIFA? BASI YAPASA KUPITISHA HUKUMU YA HAKI KATI YETU SISI WENYEWE ILI TUSIJE TUKAHUKUMIWA PAMOJA NA WASIOAMINI(ulimwengu).

  Martin.

 35. Ndg Mubelwa,

  Ninafuatilia mjadala huu. Nami nimeona nichangie katika suala la UABUDUJI ambalo umesema uliuliza swali na jibu lake likawa hapana.

  Mimi ninavyofahamu uliandika kuhusu namna ya ubuduji katika ile mada ya kuwaombea wapendwa wote wanaoishi Ulaya. Ulichoandika ilikuwa ni jibu kwa mchango wangu na ukaandika hivi, “TUACHE KULAZIMISHA KUWA TUABUDUVYO TANZANIA NI GLOBAL WAY na PIA KUJUA MAENEO YA UABUDUJI VYACHANGIA MAONI YA MITAZAMO TOFAUTI katika mambo mengi yanayowekwa humo!”

  Sijakumbuka kama kuna mahali ambapo uliandika maneno hayo kwa mfumo wa swali. Lakini kama ni hili la kujadili wokovu kwa kulingana na jiografia mimi nilishalijibu. Baadhi ya maneno yalikuwa kwenye jibu langu ni haya:

  “Kabla sijaendelea sana nami nakushauri hivi TUACHE KULAZIMISHA KWAMBA TUNAVYOABUDU ULAYA AU MAREKANI NDIYO KUABUDU KUNAKOLINGANA NA NENO LA MUNGU! Si kuabudu Kitanzania kunakompendeza Mungu wala si kuabudu Kiulaya kunakompendeza Mungu bali ni kuabudu kulingana na mafundisho ya Neno lake takatifu! Nilishasema mara nyingi, na ndivyo ilivyo, kwamba kipimo chetu katika KILA JAMBO ni neno la Mungu. Kitu chochote, hata kama kiwe kinaonekana kinafaa namna gani katika mtazamo wa kibinaadamu lakini kama HAKILINGANI NA MAELEKEZO YA NENO LA MUNGU kitu hicho hakifai katika kumsaidia mtu kuweza kuingia mbinguni.”

  “Katika michango yangu mbali mbali kuna wakati ulijibu mchango wangu mmoja ukaandika kwamba ninapochangia I must consider globally. Mimi katika kujibu niliandika kwamba mimi sichangii mada ki-tanzania, ki-marekani, ki-asia nk bali mchango wangu unatokana na mafundisho ya Neno la Mungu. Kwa sababu HAITASAIDIA KABISA KUCHANGIA MADA KWA KUTUMIA MITAZAMO WA SEHEMU HUKU TUKIIACHA KWELI YA NENO LA MUNGU. Hakuna mbingu ya watanzania, wamarekani, waafrika, wazungu nk. Mbingu iliyopo ni moja tu, ya wale waliosafishwa kwa damu ya Yesu Kristo na kujilinda na mawaa ya ulimwengu huu. [Ufunuo 22:14]”

  Neno ambalo umekuwa ukilitaja mara kwa mara ni DINI. Mimi na wewe tulishajadili suala la dini wakati fulani. Lakini dini ni kitu kimoja na wokovu ni kitu kingine. Na hapa (Strictly Gospel) sijawahi kuona mtu ye yeyoye akijadili mada kutokana na dini yake, bali wote huwa tunajadili kutokana na Neno la Mungu. Yawezekana ndiyo maana maswali uliyouliza kuhusu dini Tanzania hayakuweza kujibiwa. Kwa ufupi mimi nashauri tusiingize mambo ya dini hapa.

  Kuna mfano wa watu ulioutoa hapa kwamba wao wanafanya tu mambo ambayo Tanzania hayatendeki na kwa kuwa hayatendeki Tanzania ndiyo maana yanaweza kuonekana kama si sahihi kwa Wakristo. Lakini inabidi ukumbuke kwamba yako pia yanayotendeka Tanzania ambayo sehemu zingine za dunia wanaweza kuyaona kuwa si sahihi kwa Mkristo. Lakini summary yangu hapa ni kwamba haijalishi suala linatendeka huku halafu kule halitendeki bali kinachojalisha ni yale maelekezo ya Neno la Mungu. Vinginevyo tunaweza kujikuta tunachambuwa maandiko na kusema haya ni kwa ajili ya Afrika, na mengine ni kwa ajili ya Ulaya nk. Watu kama watu wanaweza kufanya jambo lolote. Ninachoona kinatakiwa ni kuchukuwa tahadari kwamba si kila kitu kinachofanywa na watu maarufu kwenye dini zao au makanisa yao ndiyo usahihi wa Mungu mwenyewe. Inatubidi kujifunza zaidi na zaidi kuhusu Neno la Mungu ili kuweza kupata ufahamu kamili.

  Tukiongea jambo lolote katika mtazamo wa dini ni rahisi sana kujiwekea mipaka maana kila dini iko sahihi katika mtazamo wake yenyewe. Hapa ndipo tunaweza kukuta dini zilizoanzishwa kwa mtazamo wa kijiografia, mtazamo wa kielimu, mtazamo wa kiuchumi nk. Na hapa ndipo husababisha utofauti wa mitazamo katika mambo mbali mbali japo wanaotofautiana wanaweza kusema ni wote wakristo! Lakini kama tukijadili mada kulingana na Imani ya Wokovu inawezekana kabisa watu tunaojiita wakristo tukawa na lugha moja juu ya mambo mengi, kama si yote yanayohusu mwenendo wa kiroho,hali ambayo inaweza kusaidia katika kuwaleta watu kwa Yesu, kwa sababu mtazamo wetu utakuwa ni huo huo wa neno la Mungu na kwa ushawishi ule ule wa Roho yule yule wa Mungu yule yule lakini si kwa sababu mmoja yuko Tanzania na mwingine yuko Marekani.

 36. Kaka Martin. Heshima kwako.
  Nashukuru kwa majibu na uelimishaji wako kuhusu mada hii. Nami napenda kuendelea kuuliza na kueleza baadhi ya mambo ili kutuwezesha kufunzana zaidi.
  Niliwahi kuuliza hapa hapa (Strictly Gospel) kuwa JE!! NI SAHIHI KUSEMA KUWA UONGOZAJI WA IBADA NA UABUDUJI WA TANZANIA NDIO SAHIHI KULINGANISHA NA DUNIA NZIMA? Jibu lilikuwa hapana. Kwa hiyo tunapozungumzia mambo haya ya ukristo tuzungumze kama global issue na sio issue kwa kuangalia Tanzania kama role model. Nasema haya kutokana na swali lako ulilouliza (na hapa nanukuu) ” YAANI UNAWEZA KUVAA BUKTA AU PENSI AU VEST HALAFU UKAINGIA KANISANI KUONGOZA WATU WA MUNGU UKIWA NA MAVAZI HAYO TU?” Na jibu langu ni kuwa NDIO. Wanafanya hivyo. Umeshawahi kumuangalia Bishop Eddie Long wa New Birth Missionarry Baptist Church anavyovaa? abda uniambie kuwa KWA MUJIBU WA BIBLIA, YEYE SI ASKOFU (ukinukuu kama utaweza) basi ntaachana na hii point katika kujibu swali. Ama vipi kuhusu Joyce Meyer anayevaa suruali akihubiri? Naye si kiongozi wa dini? Point yangu ni kuwa, kwa kuwa hayatendeki Tanzania (ambako nimegundua kuwa sehemu nyingi kuna uoga kuliko ukweli wa dini), haimaanishi kuwa haitendeki kokote. Nimewahi kuuliza maswali mengi kuhusu dini hasa Tanzania lakini sikujibiwa. Inaonesha fika kuwa Tanzania tunakwenda waaaaaaaay too far kwenye mambo kama haya. Ni kweli kuwa wapo kinadada ambao kama alivyosema Dada Rose pale juu, wanakwenda waaay too far kwenye uvaaji wao. Pengine nikuulize. Mavazi kama avaayo Joyce Meyer ahubiripo, ni kwazo kwako? Unadhani ni asilimia ngapi ya wakristo waishio nchi za baridi wanavaa suruali wakati wa winter? Je! Ni sahihi kwao na si kwa wanawake wakristo wa Tanzania? Sijui kama Biblia imesema kuhusu haki kwa mujibu wa mazingira ya kijiografia. Na ndio maana nilikuuliza kuwa MAVAZI SAHIHI KWA MUJIBU WA BIBLIA NI YAPI? Na hili pia hujalijibu. Ningependa kujua kuwa kama unavyosema kuwa ungekuwa na utakuwa mkali katika mavazi, utafuata neno gani? Napenda kujua UTAFUATA MAANDIKO GANI YA BIBLIA KATIKA KUKEMEA MAVAZI?
  Ninalohisi ni kuwa kama huna unaloweza kusema kuwa VAZI hili si sahihi, hutaweza kutenda iliyo sahihi miongoni mwa waumini wako. Na mwisho niulize kuhusu utaratibu utakaotumia. Je!! UTAWAITA NA KUWAFUNZA KWANZA KISHA UWAONYE NA NDIO UWAFUKUZE AMA UTAFANYAJE? Pengine wako pale kubadilika na hiyo ni moja ya tabia ambayo ungeweza kuwabadili kama ungewapa MAFUNZO YA KIROHO kuhusu mavazi na mienendo yao kabla hujawafukuza.
  DADA ROSE AMEELIMISHA KIUSAHIHI KABISA HAPO JUU KUWA KUSINGIZIA MAJARIBU SI SAHIHI, LAKINI KUWAWEKA WENGINE KWENYE MAJARIBU SI SAHIHI PIA. Hili ndilo unalopaswa kuwafunza. Kuwaonesha pande zote mbili ili watakapokwenda nje ya kanisa na kukutana na wale wasioamini wanaotaka kuwarudisha nyuma, wawasikilize, wawaelewe na kuwaelewesha kuhusu pande zote.
  Kama hutafanya hivyo na kuwafukuza moja kwa moja, basi utakuwa hujatenda kazi uliyotumwa. Kumbuka hata wokovu unaodhani kuwa unao ni NEEMA ambayo Mungu aliitoa kwa Dunia. TAMBUA KUWA WAKATI MUNGU ANAAMUA KUMLETA YESU, DUNIA ILIKUWA KWENYE HALI MBAYA KULIKO UNAVYOWAONA HAO WANAWAKE WAKIVAA SURUALI.
  SASA KAMA MUNGU ALIONA NI VEMA KUIPA DUNIA NAFASI YA PILI, WEWE NI NANI KUTOFANYA HIVYO?
  Ntashukuru kama utanijibu kuhusu maandiko juu ya mavazi na namna utakavyofanya maamuzi yako juu ya mavazi mabaya

 37. Ndugu Mubelwa,
  Kanisa ni chombo kitakatifu cha Mungu hapa duniani na Mungu anataka tutumie AKILI alizotupa.Hatuwezi tukasema kila kitu tunachokifanya lazima tufanye maombi.
  Maombi yana sehemu yake!Na vitendo/action zina sehemu yake!

  Maombi + Vitendo = Matokeo(Desired results)
  If you pray and you don’t take any action, you are wasting your time!

  Yesu alipowafukuza wale waliokuwa wanafanya biashara kule hekaluni kwani ilikuwaje? MBONA HAKUWAACHA WAENDELEE kufanya biashara hekaluni HALAFU AKAFANYE TU MAOMBI? YESU ALIKUWA ANAMZIGO NA KAZI YA MUNGU!
  Nasi sharti tuwe na MZIGO NA KAZI YA MUNGU!

  BORA UBAKIWE NA WATU WACHACHE WENYE KUKUBALI KUFANYA KILE NENO LISEMACHO KULIKO KUWA NA UMATI MKUBWA WA WATU WAASI WA WAZIWAZI WA NENO LA MUNGU!

  KUMBUKA TUNAPOWAFUKUZA WALE WANAOKAIDI KUENENDA SAWASAWA NA NENO LA MUNGU NI KWA MANUFAA YA WALE WAKRISTO WACHANGA NA HATA WALIOIMARIKA WASIINGIWE NA UKENGEUFU WA KUFANYA UASI HARADHANI.

  MAANDIKO KUTOKA KING JAMES BIBLE

  1Cori 5:11-13
  11But now I have written unto you not to keep company, if any man that is called a brother be a fornicator, or covetous, or an idolater, or a railer, or a drunkard, or an extortioner; with such an one no not to eat.
  12For what have I to do to judge them also that are without? do not ye judge them that are within?
  13But them that are without God judgeth. Therefore put away from among yourselves that wicked person.

  “…THEREFORE PUT AWAY FROM AMONG YOURSELVES THAT WICKED PERSON.-1Cor 5:13”

  Romans 16:17-18
  17Now I beseech you, brethren, mark them which cause divisions and offences contrary to the doctrine which ye have learned; and avoid them.
  18For they that are such serve not our Lord Jesus Christ, but their own belly; and by good words and fair speeches deceive the hearts of the simple.

  1Timothy 1:19-20
  19Holding faith, and a good conscience; which some having put away concerning faith have made shipwreck:
  20Of whom is Hymenaeus and Alexander; whom I have delivered unto Satan, that they may learn not to blaspheme.

  “…THEREFORE PUT AWAY FROM AMONG YOURSELVES THAT WICKED PERSON.-1Cor 5:13”

  KWA NINI MUNGU ATUPE MAANDIKO MENGI KIASI HICHO HALAFU TUENDELEE KUWA WAJINGA?
  MAKANISA MENGI SANA LEO HII YAPO KIENYEJI SANA!
  JE, INA MAANA MUNGU HATAKI TUWEKE TARATIBU NZURI KATIKA MAKANISA YETU?
  TARATIBU AMBAZO, NDIYO ZA KIBINADAMU LAKINI ZENYE UCHAJI WA MUNGU NDANI YAKE NA ZENYE KUSAIDIA WALIO DHAIFU WA IMANI!

  HIVI MCHUNGAJI AKIENDA KANISANI KUHUDUMU ANAVAAGA BUKTA AU PENSI AU VEST HALAFU AKASIMAMA MBELE ZA WATU KUHUBIRI?
  HIVI INA MAANA SISI WAKRISTO SI WATU AMBAO TUNAPASWA KUWA NA AKILI KATIKA MAMBO YOTE?
  YAANI UNAWEZA UKAVAA BUKTA AU PENSI AU VEST HALAFU UKAINGIA KANISANI KUONGOZA WATU WA MUNGU UKIWA NA MAVAZI HAYO TU?
  JE, NI SAHIHI WADADA/WAMAMA KUVAA NGUO ZAO WAKAJIONYESHA SEHEMU AMBAZO SI SAHIHI KUONEKANA KWA WATU WOTE?
  KWA NINI TISIWAAMBIE KWA UPENDO kisha kama hawataki kubadilika TUKAWAAMBIA WATAFUTE MAHALI PENGINE PANAPAPORUHUSU MATENDO MAFU YA DHAMBI NA WAHAME HAPO KANISANI KWETU KWA MAANA WANAENENDA KINYUME NA MALENGO YETU!

  VITU VILE TUNAVYOWEZA KUVISHUGHULIKIA BASI TUVISHUGHULIKIE NA VILE VILIVYO NJE YA UWEZO WETU TUMWEKEE MUNGU TUMAINI ASHUGHULIKE NAVYO!

  MIMI MSIMAMO WANGU UTAKUWA MKALI NA WALA SITABADILIKA WALA KUTISHIWA NA MWANADAMU AWAYE YOTE!

  1Cor 14:38
  38But if any man be ignorant, let him be ignorant.

  Matin.

 38. Naomba tu kuwajuza wale wanaowakwaza wenzao kuwa Mtume Paulo alisema ni kutenda DHAMBI, ingawa ameongelea chakula lakini ni mfano wa makwazo yoyote
  Rumi14:
  13Basi, tuache kuhukumiana. Badala yake tuamue kuwa hatutamkwaza ndugu kwa kitu cho chote. 14Ninajua hakika kuwa nikiwa katika Bwana Yesu hakuna kitu cho chote ambacho kwa asili yake ni najisi. Lakini kwa mtu anayeamini kuwa kitu fulani ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 15Kama ndugu yako anahuzunishwa kwa sababu ya kile unachokula(au kuvaa), basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16Usiruhusu kile ambacho unachokiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 17Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki, amani na furaha ndani ya Roho Mtakatifu. 18Kwa maana mtu ye yote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na anakubaliwa na wanadamu.
  19Kwa hiyo basi, tufanye kila juhudi tutimize yale yaletayo amani na kujengana. 20Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Vyakula vyote vinafaa, lakini ni kosa kula kitu ambacho kinamfanya mwenzako kujikwaa. 21Ni afadhali usile nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lo lote litakalomfanyandugu yako aanguke. 22Unavyoamini kuhusu mambo haya, iwe ni siri yako na Mungu. Amebarikiwa mtu ambaye hajisikii kuhukumiwa afanyapo jambo analoamini kuwa ni sawa. 23Lakini mtu mwenye mashaka kuhusu anachokula, amehukumiwa ikiwa atakula, kwa sababu kula kwake hakutokani na imani. Kwa maana jambo lo lote ambalo halitokani na imani, ni dhambi.

 39. Amen, nashukuru sana kaka Mubelwa kama mchango wangu kukusaidia, Sifa na utukufu kwake Yse anayetuwezesha.
  Ni kweli kaka Martin inachosha, unakuta mtu ni mke wa mtumishi, au yeye mwenyewe ni mtendakazi kanisani miaka nenda rudi halafu anapanda na mavazi yasioeleweka madhahabuni kwakweli hii inatia shaka kama wanaye Roho Mtakatifu au? Tuzidi kuomba nakelimishana ili Kanisa liwe kweli mahali ambapo Mungu anaonekana. Barikiweni

 40. Really Martin?
  Na neno hapo ni lipi? LILIVYOANDIKWA KATIKA VERSION GANI YA BIBLIA? KING JAMES AMA YA ZAMANI KABLA YAKE? UNADHANI BIBLIA ZIMEANDIKWA EXACTLY THE SAME? NA KAMA SIO, BASI NI NANI MWENYE MAMLAKA YA KUITAFSIRI NA NI IPI UTAKAYOTUMIA NA VIPI?
  Na utasoma neno kwa neno ama utatafsiri maana? Maana najua hata Yesu aliongea kwa mifano. Ninalohisi ni kuwa unaweza kuja na TAFSIRI YAKO YA BIBLIA na kujikuta umefanya tofauti na maana ya uliyotafsiri.
  Pengine unapozungumzia kiasi uanze kwa kuwa na kiasi wewe mwenyewe. Ni kama vile UMESHAPANGA NINI UTAFANYA KWA NGUVU ZAKO NA SI ZA MUNGU MAANA SIJASOMA POPOTE UKISEMA KUHUSU MAOMBI. KWA HIYO UTATUMIA AKILI ZAKO KUITAFSIRI BIBLIA NA KISHA KUAMUA UKIDHANI UNATENDA IMPENDEZAYO MUNGU kumbe yawezekana unamkwaza kwa kutokuwa na kiasi.
  Labda nimalizie kwa kusema NAOMBA TAFSIRI YAKO YA NGUO ZINAZOFAA KUVALIWA KANISANI KWA MUJIBU WA BIBLIA.
  Kuna haja ya kufikiri kabla ya kuenda kwani KAMA UMEFUMBA MACHO UNAWEZA KUDHANI KUWA HUWAONI, KUMBE NI WEWE USIYEWAONA KWA KUWA UMEFUMBA MACHO.
  Tafakari

 41. Mimi ningekuwa pastor halafu wadada/wamama waje kanisani na mavazi ya aibu BASI NINGEWARUDISHA MAJUMBANI MWAO NA KUWAONYA ENDAPO WATAKUJA TENA KANISANI NA MAVAZI YA AIBU KIASI HICHO NITAWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA.
  Tatizo letu leo ni sisi wapendwa tumekuwa na UPOLE WA KIPUMBAVU.
  Kama watu wanajua kanisani panaenda watu wengi wenye kuhitaji MSAADA,KWANINI wewe UVAE VIBAYA KWENDA KUSUMBUA UTULIVU WA WATU WENGINE?
  Yesu aliwafukuza hekaluni watu waliolifanya hekalu jumba la wanyang’anyi!
  NA MIMI NITAWAFUKUZA!
  LAZIMA TUWE SERIOUS NA KAZI YA MUNGU!
  TUSIPOKUWA SERIOUS TUTAYAJAZA MAGUGU MENGI SANA MAKANISANI NA HATA NGANO INAWEZA IKAPOTEA KABISA!
  Kanisa Bwana atakalonipa NITAKUWA VERY VERY SERIOUS! NA nitakuwa nafanya kazi kwa mikono yangu kama mtume Paulo ILI MTU YEYOTE ASIJEFIKIRIA AKIONDOKA KANISANI NITAKUFA NJAA! MTU akikataa kuishi sawa na NENO ANAAMBIWA TU AONDOKE KANISANI AENDE AKATAFUTE MAHALI PENGINE AMBAPO WANARIDHIA MATENDO MAFU YA DHAMBI!

  Martin.

 42. I have to admit kwamba KAMA TUNGEKUWA TUNAELIMISHANA KWA NAMNA HII (uliyoitumia Dada Rose) BASI WENGI TUNGEWEZA KUELIMIKA. Maandiko haya nimekuwa nikiyafahamu lakini sikuwahi kuyawaza kuyahusisha na mjadala huu. Lakini japo yalionekana kwenda tofauti na ulivyoandika hapo, umeweza kuyatumia kuonesha kile kisemacho tofauti na unavyoamini, lakini pia ukamalizia na kile kisemwacho kwa upande wa uaminivyo na baada ya kuonesha kuwa wazitambua pande zote (na kwa kuwa pande zote zipo) umeendelea kuonesha ni kwanini waamini uaminivyo.
  Uelimishaji mzuri kuliko wowote niliowahi kusoma humu.
  Stay Blessed DADA

 43. Amen na asante kwa kukubaliana huku nami najua kuna andiko la tamaa na majaribu linalofanana na maelezo yako
  Yakobo 1: 12Amebarikiwa mtu ambaye anavumilia majaribu, kwa sababu akisha stahimili atapewa taji ya uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao. 13Mtu akijaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu,” kwa maana Mungu hajaribiwi na uovu na yeye hamjaribu mtu ye yote. 14Lakini kila mtu hujaribiwa anapovutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe. 15Kisha tamaa hiyo ikisha chukua mimba, huzaa dhambi; na dhambi ikisha komaa, huzaa mauti.
  Ndiyo maana nikasema wako “walio dhaifu”, lakini Yesu alitoa onyo kuwa ole wao wale wanaowakwaza wenzao! Hivyo Injili ni upanga una makali kotekote. Ubarikiwe

 44. Heshima kwako Dada Rose.
  Kama ulivyosema kuwa unaomba kutofautiana nami, nami nakubaliana nawe.
  Ninalofahamu ni kuwa siku hizi hakuna mtu anayetaka kubeba msalaba wake katika yale yamtokeayo. Mtu anaweza kuwa na tamaa ya kufanya mapenzi na binti mdogo wa mri wa bintiye lakini hawezi kumtamani bintiye. Siamini kuwa ni nguvu ya Mungu ndani mwake inayomuepusha na tamaa hizo kwa bintiye(kwani naamini Mungu hawezi kumfanya mtu amtamani mtoto mdogo) bali kwa kuwa ameji-tune kuwa huyo ni mwanae na hawezi kufanya uzinzi naye. Tunaona wanaovuka mipaka wanafanya hayo na watoto wao. Lakini haya ni mapungufu ya kuendekeza TAMAA zetu. Walevi wanasingizia kubaka kwa kuwa walikuwa wamelewa lakini hawabaki mbwa wala mbuzi. Kwanini??? Wanajua nini na kipi wanafanya. Kwa hiyo kuna namna ya kuchukulia kila jambo. Kama tutaendelea kudhaifisha mioyo yetu kwa kuangalia wasiotutakia mema, hatutaweza kupingana nao kwani wao nia yao ni kupata “ATTENTION” toka kwetu na kuwapa attention hiyo ndio kujipunguzia msimamo.
  Kwa hiyo nakushukuru kwa maoni yako Dada Rose na nafurahi kuwa licha ya kutokukubaliana, tumeendelea KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA.
  Blessings

 45. Kaka Mubelwa, naomba kutofautiana nawe hapa, mimi nina wokovu na ninapoabudu wanavaa wengine hizo nguo ingawa wanasema ni za heshima lakini ukiangalia wakipita mbele za watu utaona tu kunakuwa na hali ya kutokuwa na utulivu, wengine wanaamua kugeuzia huko macho yao wasiangalie, wale wenye mioyo dhaifu ndo basi anakaza macho kwenye hayo maumbile yanayoanikwa. Sasa unaweza sema sio tatizo lakini si kila mtu amesimama na hata waliosimama unawakosesha amani.Kama ni kitu ulipanda madhabahuni kukitangaza, kushuhudia, kupokea wageni yaani kuna wengine hawatabarikiwa kabisa na wanaweza waamue kutokusogelea ulipo. Sasa sijui hata mwanaume au mvulana angekupenda na akaulizia mtu kama unavaa hivi wanaweza kum discourage kabisa kuwa “hana heshima” Usiwadanganye wasichana dhamira zinawasuta ambaye ndiye Roho aliaye ndani yao. Ubarikiwe

 46. Dada ROSE.
  Hudhani kuwa jibu la kwanza ni fikra potofu za mwanadamu aliyeendekeza uzinzi na kutafuta kila kisingizio katika kila baya afanyalo?
  Kwani wazazi wa kale walivaa nini? Si vipande vya kujisitiri sehemu za siri? Na hakukuwa na UZINZI NA UASHERATI KAMA ULIO SASA mbapo mt anasingizia kuwa msichana kavaa nguo inayom’bana.
  Tuache kumsingizia SHETANI. Nadhani shetani mkuu ni yule anayetuongoza kumtumia shetani kufanya maovu.
  Hiyo sababu ya kwanza naoma nikubaliane kutokubaliana nayo.

 47. Naomba kujibu swali la Shoo GAP:
  Mavazi yasiyompa Mungu utukufu:
  1. unawakwaza wengine kwa kuwafanya watamani ngono na kama ni ibada basi wanakuwa wanashindwa kuabudu vema
  2. unajivunjia heshima kwa kuonyesha maungo yako nyeti kwa kila mtu, na unaliaibisha Kanisa kwa ujumla
  3. unawafanya wasiookoka wasione haja ya wokovu maana wewe mwenye nao hujabadilika
  4. unamhuzunisha Roho mtakatifu anayeishi ndani yako na baadae atakuacha na utapoa kabisa

 48. Shalom wapendwa!!
  Nimebarikiwa sana na michango yenu yenye ukweli na kujenga
  Mimi kama msichana naamini kuwa tunatakiwa kuvaa kiheshima iwe ni sketi , gauni, blouse na hata suruali (inapotokea. Kuna mavazi kadhaa kama T shirts, kanzu e.t.c sometimes huvaliwa na jinsia zote.

  Nakubali kuwa suruali ina nafasi kubwa katika kuchonga maumbile ya mwanamke hasa pale inapobana. Lakini kuna baadhi ya mazingira suruali huwa ni vazi lenye kuleta wepesi na ufanisi mfano,

  1.Aina ya kazi; kwa mfano mimi ni researcher (mtafiti) wa viumbe vinavyoishi katika maji (aquatic environment)so suruali haikwepeki
  2.Katika safari mbalimbali,;huleta wepesi wa kutembea na kuruka.

  Lakini ukweli unabaki pale pale unavaa kwa dhumuni gani? Ni kweli wengi hawavai kwa ajili ya mazingira kama nlivyoainisha bali ni kwa fashion na self interest.

  Wapendwa pia naamini mazoea nayo hutesa sana watu na hata anapookoka hawezi change abruptly na tunahitaji sana Roho Mtakatifu.
  Nakumbuka kabla sijaokoka sikuwa navaa sketi, nlizoea suruali na hivi wanaita vipedo, lakini nlipookoka Bwana Yesu alinisaidia kiasi kikubwa hata sasa naweza kuvaa sketi ndefu, za kati na suruali mara chache kikazi au ktk shughuli lakini na blouse ndefu na pana.

  Ni kweli naweza kuwa sijakamilika lakini angalau sipo pale nlipokuwa zamani na nitaendelea kupokea ushauri na kudhamiria kubadilika kila siku.
  ‘Bwana hututoa nguvu hata nguvu’
  Msichoke kutuonya, kuturekebisha na kutuombea ili tuwe mabalozi wazuri na tisiwakoseshe watu wokovu.Roho Mtakatifu atuongezee usikivu, hekima, busara na uadilifu

  Wadada wenzangu tusikatae kuonywa hata pale tunapokuwa hatujashinda vizuri kutokakatika hilo eneo bali tuwe wasikivu na hakika itakuwa rahisi kuibadili jamii na kuwaepushia vishawishi na mmomonyoko wa maadili.
  Nawapenda wote

 49. ni sawa mwanamke wa kikristo kuvaa suruali lakini suruali iwe ya heshima. suruali zipo aina mbili za kike na kiume na zinatofauti. si dhambi kwa mwanamke aliyeokoka kuvaa suruali lakini iwe ya heshima.

 50. Kwani tatizo liko wapi kuvaa suruali, sio ndio sitakuwa mwanamke. Na mwanaume akivaa gauni hatakuwa mwanamke. Na hata sketi siku hizi wanaume wanavaa. Kwa hiyo nguo ni nguo tu. Ila najua wengi wanasema kimila na desturi suruali ni za akina baba na magauni ni ya akina mama. Binafsi nikiwa TZ sivai kabisa suruali na hata hapa niishipo navaa kwa ajili ya baridi.

 51. Sijasoma maoni yote (na naamini sihitaji kusoma katika hili swali) lakini NATAMBUA kuwa hakna ubaya wa mwanamke kuvaa suruali. Sijui ni wapi panapotofautisha kanzu na gauni ama joho la mchungaji na gauni la kike. Sijui kwanini kunakuwa na tafsiri ya mambo ya dini kulingana na mazingira na si Ulimwengu kwa ujumla. Kunaweza kuwa na tatizo katika jamii fulani lakni haimaanishi kuwa yeyote aliyeokoka hastahili kuvaa.Blessings

 52. Asante sana Mary nimefurahi sana mfano wako. kwakweli hapo kwaza tayari umeifundisha jamii pia kuna mahali imenigusa nywele za bandia na kuingia kwenye draya ni dhambi.
  pia yapo makanisa ya kidunia kama vile mtumishi akikuongoza sala ya toba ukiokoka na ukafanikiwa kifedha anataka umpe fungu la kumi hii ni sawa????moyo wangu unalalama juu ya hilo

 53. Ndugu Shoo, siyo mabinti tu hata wakina mama wapo wanaofanana na mabinti.Ninapenda kutoa mifano yangu mwenyewe , katika kanisa ninaloabudu (silitaji) alihamia mama mmoja akitokea kanisa fulani (silitaji pia) ikatokea akawa rafiki yangu wa karibu sana, katika mazungumzo tulifikia maswala hayo ya mavazi na nywele, alinieleza kuhusu mchungaji wa kanisa lake jinsi alivyochukua hatua ya kufundisha na kusisitiza kwa maandiko, hata akaonekana kama analeta sheria ndani ya kanisa. Msimamo wa yule mchungaji ni kwamba tunaubeba udunia na kuuleta kanisani, badala ya kulileta kanisa duniani yaani watu waone tofauti 1Yoh 2:15-16. Kwa kweli Roho Mtakatifu alisema nami kwa namna nisiyoitegemea, niliguswa mno na hoja hiyo nilipojikagua nikajiona ni mmoja wapo ninayeipeleka dunia kanisani, kwa mavazi na manywele ( sipendi kuvaa suruali)bali kwa nguo zenye mipasuo mikubwa, niliamua kutubu, nguo zote zenye mipasuo nilizishona , minywele ya bandia(ya rangi) nilichoma moto yote na bado ninaomba Roho aendelee kufanya operation ya ndani zaidi, ninataka nimwone Mungu wa matendo.Sipendi nimhukumu mtu, ila najua kila jambo na wakati wake.

  Msimamo wa yule mchungaji ni kupinga na kutokomeza tabia ya kuleta dunia kanisani na kusisitiza msimamo wa NENO LA MUNGU. ALIFAULU.

  MUNGU AWABARIKI.

 54. NAONA HAKUNA MAJIBU.
  MUNGU NA ATUPE MOYO WA UNYENYEKEVU TUNAPOJIFUNZA TOKA KWA HUYU MTUMISHI WA MUNGU SEAT TARIMO

 55. HALELUYA WANDUGU.
  Nilikuwa nataka kuanzisha mjadala huu baada ya kuwaangalia mabinti wengi waliookoka na mavazi yao na nilitamani wa jinsia ya kike wachangie tu. Nilipokuwa nafikiri Mungu kwa neema yake akanipeleka kwenye hii link. Namshukuru Mungu kuwatumia watumishi wote waliochangia hapa, ingawa nilipoanza kusoma niliona kuwa baada ya kusoma mchango wa John Paul wa october 2, 2008 at 3:19 pm nikazani kuwa aliyoandika yalipaswa kuhitimisha. Lakini Mungu akatoa neema ya wengine kuendelea kuchangia. Ila ningewaomba walioendelea kuchangia watulie na wamwombe Roho Mtakatifu awafundishe kisha wasome tena yale maelezo ya John Paul.

  Swali nililokuwa nalo ni hili: Mabinti wakiristo wanajua athari ya kuvaa mavazi yasiyompa Mungu utukufu?

  NOTE: Athari kwa pande hizi:-
  (a) Mungu/ maisha ya kiroho.
  (b) Kwa wanaume.
  (c) Na kwa binti binafsi.

  Baada ya kusoma maelezo ya John Paul naomba mnisaidie kujibu hilo swali sasa. Naomba sana kila mmoja atoe maoni yake ya kile anachokifahamu, KWANI NINATAMANI KUJIFUNZA KITU TOKA MAELEZO YENU.

 56. Bwana Yesu asifiwe!
  Ninaamini si kila anayesoma safu hii ameokoka hivyo ni vyema tukamuomba Mungu uongozi wa Roho Mtakatifu ili tuweze kuandika kitu ambacho kitawajenga wengine na kuwasaidia.
  Suala la vazi la suruali ni kweli haliruhusiwi kwa wanawake na hata katika jamii yetu ya Kitanzania ila ni vema tumsii Roho Mtakatifu ili amani yake iamue ndani ya moiyo yetu.
  Chunga sana amani ya Mungu ndani ya moyo wako isipotee kwa sababu tu ya kupenda kuufurahisha mwili kamwe mwili hautosheki.
  Wenzetu wazungu kwao je, tutalizungumziaje?

  Mungu awabariki nyote mnaomtegemea
  Hakika Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele.

 57. NDUGU JOHN PAUL
  ASANTE SANA MUNGU AZIDI KUKUBARIKI.
  KWAKUWA UMESEMA NISIKUJIBU SIKUJIBU ILA NAONGEA KWA AJILI YA FAIDA YA WENGINE, NANAKUBALIANA NAWE KABISA KWAMBA TUNAPO JADILIANA MIMI NAWE WENGINE PIA HUJIFUNZA.
  INAWEZEKANA HUONI KAMA UNASTAHILI KUNIFUNDISHA, MIMI BADO NAJIFUNZA MENGI KUTOKA KWAKO.
  NIMEKUELEWA NAMANA UNAVYO ELEZEA NENO BALANCE KWA MTIZAMO WAKO NA NAKUBALIANA NAWE ILA SIMAANISHI HIVYO UNAVYO ELEWA,NIELEWE SIJITETEI ILA NATAKA UNIELEWE ILI TUFIKIE HITIMISHO.
  NISAHIHI KABISA KWAMBA SI SAHIHI KUWEKA BALANCE KATI YA DHAMBI NA UTAKATIFU AU KATI YA MUNGU NA SHETANI.
  LAKINI PIA INAHITAJIKA BALANCE NAMNA YAKUENENDA MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU, MFANO WANGU JUU YA DANIEL KU-BALANCE MAMBO YAKE NI NAMNA ALIVYO MJUA MUNGU NA KUITUMIKIA SERIKALI BABEL BILA KUJINAJISI MBELE ZA MUNGU HUKU AKILINDA UTAKATIFU,
  JOHN 22:37 LOVE THE LORD YOUR GOD WITH ALL YOUR HEART AND WITH ALL YOUR SOUL AND WITH ALL YOUR MIND, THIS IS THE FIRST AND GREATEST COMMANDMENT, AND THE SECOND IS LIKE IT LOVE YOUR NEIGHBOUR AS YOU LOVE YOURSELF,
  SASA HAPA UNAWEZA KUONA NAMNA GANI BALANCE INATAKIWA YAANI UKIMPENDA SANA MUNGU KAMA ALIVYO SEMA HAPO KWENYE AMRI YA KWANZA NA USIPO MPENDA JIRANI KAMA UNAVYO JIPENDA WEWE MWENYEWE AU UKIMPENDA JIRANI YAKO KAMA UNAVYO JIPENDA MWENYEWE NA USIMPENDE MUNGU WAKO KAMA ALIVYOSEMA YESU KWENYE AMRI YA KWANZA SIZANI KAMA UTAKUWA UMEBALANCE APPLICATION YA UPENDO KAMA YESU ALIVYO AMURU.,
  ACTS 10:2 HE AND ALL HIS FAMILY WERE DEVOTED AND GOD- FEARING, HE GAVE GENEROUSLY TO THOSE IN NEED AND PRAYED TO GOD REGULARLY,43 ALL THE PROPHETS TESTIFY ABOUT HIM THAT EVERY ONE WHO BELIEVES IN HIM RECEIVES THE FORGIVENESS OF SINS THROUGH HIS NAME.
  HAPA NAPO UNAWEZA KUONA NAMNA KORNELIO ALIVYO KUWA ANAFANYA MATENDO MEMA KWA WATU PAMOJA NA KUMCHA MUNGU LAKINI BALANCE ILIKOSEKANA KWASABABU TU HAKULIAMINI JINA LA YESU MPAKA IKAMGHARIMU MUNGU KUMTUMA MALAIKA ILI KULEKEBISHA MIZANI.
  NAKUBALIANA NAWE KWAMBA KWA MTU WA MUNGU KUSHIRIKI MAOVU NA TABIA AMBAZO ZINA KIUKA MAADILI YA KIMUNGU SI SAHIHI ILA NAONA BADO HAWA WATU WANASTAHILI REHEMA ZA MUNGU,MSAMAHA WA MUNGU, UPENDO WA MUNGU KUTOKA KWETU, INAWEZEKANA MIMI NA WEWE HATUJUI NINI KIFANYIKE ILA MUNGU WETU ANAYO MAJIBU,

  LET US ALWAYS BE ATTENTIVE TO HIS CALLING, HE WILL WORK THROUGH US FOR THEM IN HIS DEVINE TIME AND DEVINE APPOINTMENT IN THE RIGHT PLACE,

  MORE BLESSINGS
  MORE LOVE
  MUNGU ATUSAIDIE
  NAONA NDUGU JOHN PAUL UTAKUWA UMENIELEWA

 58. Ndugu Pona,

  Nashukuru kwa reply yako na ninajisikia amani kwa sababu umenielewa! Ila napenda tu kusema kwamba mimi sina kiwango cha kukufundisha wewe isipokuwa ninachangia kwa kuandika yale niliyonayo mimi moyoni mwangu kwa habari ya safari ya kwenda mbinguni. Katika ku-share ideas kwa namna hii kila mtu anaweza kupata angalau moja ambalo yeye hakuwa nalo, kwa hiyo tunachofanya hapa naamini ni kwa mutual benefits. Na pia nafahamu kwamba tunachojadiliana hapa mimi na wewe si kwa faida yetu tu bali kuna watu wengi wanafuatilia. Kama kuna cha maana katika mjadala wetu nao wanaambulia walau kidogo. Lakini kama katika tunayojadiliana hakuna lolote la maana, basi kujadili kwetu kunakuwa hakuna faida! Na uzuri wa mjadala ni pale unapofikia mwisho. Lakini kama kila jibu la swali hutengenezewa swali jingine, kufikia tamati huwa ni vigumu na kinachobaki ni malumbano ambayo hayafaidishi upande wowote. Kama usingekuwa umeuliza maswali nisingekuwa na lolote la kuandika kuhusu reply yako. Lakini inabidi nikujibu hayo maswali yako kwa kutegemea kwamba majibu yangu hayatasababisha maswali mengine. Lakini kama itatokea baadhi ya majibu yangu kuzaa swali jingine, usisite kuuliza maana ninalo jibu kwa kila swali linalojitokeza kutokana na ninachokiandika hapa.
  JAMBO LA KUZINGATIA ZAIDI NI KWAMBA SISI SOTE NI WANAFUNZI WA BWANA YESU. KAMA NIA YETU WOTE NI KWENDA MBINGUNI KWA NJIA YA YESU BASI WE ARE NOT AGAINST BUT FOR EACH OTHER!

  Here we go!:

  1. MTAZAMO: Kila binaadamu ana mtazamo tofauti na wa mwingine juu ya jambo husika. Ni mara chache sana watu kuweza kuwa na mtazamo unaofanana. Na kwa sababu ya utofauti wa mitazamo ndiyo maana watu hukaa na kujadili kwa pamoja, kila mtu akieleza mtazamo wake na hatimaye wanakubaliana na kufuata mueleko mmoja wenye kuleta manufaa. SASA kwa habari ya Mambo ya Mungu tofauti za mitazamo yetu huwekwa pamoja na Neno la Mungu. Na kama ikitokea kila mtu akawa na tafsiri tofauti kuhusu Neno fulani la Mungu, tafsiri hiyo lazima itakuwa kwenye muelekeo huo huo wenye kumpa faida kila Mwana wa Mungu.

  Umeelezea kwamba, ‘nanukuu’: NADHANI HUKUNIPATA VIZURI NILIKUWA NAMAANISHA NINI KATIKA MTIZAMO WANGU. ‘mwisho wa kunukuu’. Baadaye ukaelezea kwamba kama Yesu alivyoshuka kutoka mbinguni na kuja kuishi duniani pasipo kufanya dhambi ni jambo linaloonyesha jinsi alivyojishusha. Ukamalizia kwa kusema kama nasi tunamfuata Yeye lazima tumuige.
  Ni kweli kabisa ulivyosema. Tuko pamoja!

  2. HAKI YA MKWAZAJI NA ANAYEKWAZIKA
  Ni bahati nzuri sana umetumia maandiko hayo hayo ambayo nami ningeyatumia pia katika kusisitiza jambo ambalo mkristo anatakiwa afanye. Hebu tuangalie:
  Rom 14:13 ”Let us not therefore judge one another any more: but judge this
  rather, that no man put a stumblingblock or an occasion to fall in
  his brother’s way”
  Katika maandiko haya tunapata reference ya jinsi nilivyoandika kwamba Kila Mkristo anatakiwa ajitahidi ili asiwe sababu ya mtu mwingine Kukwazika. Sehemu ya kwanza ya mstari huo hutumika na watu ambao huwa hawataki kubadilika kwa namna moja au nyingine. Watu hawa huwa wameshikilia vitu vya ki-dunia (kama vile mavazi mabovu) na wanapoonywa HUJITETEA KWAMBA BIBLIA IMESEMA TUSIHUKUMIANE! Kwao watu hawa sehemu muhimu ya msitari huu, yaani NOT TO PUT A STUMBLINGBLOCK OR AN OCCATION , kwao si kitu. Kumbe watu hawa walitakiwa kuzingatia sehemu ya pili na muhimu kwamba KILA MTU ASIWE SABABU YA KULETA KWAZO KWA MWINGINE. Kwa mkristo anayetaka kuwa baraka kwa Mkristo mwingine YEYE HUWA TAYARI KUACHANA NA MAMBO ANAYOONYWA NA WANA WA MUNGU KWAMBA HAYALETI USHUHUDA MZURI KWA WAFUASI WA YESU! Hivyo tunachojifunza hapa ni kwamba Mkristo akionywa juu ya jambo fulani ambalo kwa namna moja au nyingine linaleta shida kwenye mwili wa Kristo dawa ni kuachana nalo na wala si kutafuta maandiko yanayomtetea.
  Kwa hiyo kama Wakristo hatutajitahidi kutokuwa sababu ya wengine kukwazika, watu wataendelea kukwazika kwa kiasi hicho hicho!

  3. MAHUSIANO KWA MUNGU NA WANAADAMU
  Hapa umetoa tafsiri yako kutoka katika alama ya pembe nne za msalaba. Kwamba horizontally ni uhusiano na wanadamu wengine na vertically ni uhusiano kwa Mungu. Ni sawa kutokana na tafsiri yako. Na ni vizuri kwamba umesema hii ni tafsiri yako.
  Mimi nasema kwamba tafsiri hiyo imetengenezwa tu na sisi watu kutumia alama ya ‘+’ ya msalaba kuonyesha aina hizo za uhusiano symbolically. Ni tafsiri njema pia. Lakini juu ya namna ya kuhusiana na watu/Mungu hakuna njia tofauti ambayo mtu anaweza kuifanya kwamba sasa ni kwa ajili ya uhusiano na Mungu na kisha kitu tofauti kwa ajili ya kuwa na uhusiano mzuri na watu. Mtu anapofanya matendo mema yanayowapendeza watu kwa namna hiyo hiyo huwa anampendeza Mungu. Hakuna mambo yanayompendeza Mungu halafu yakawa yanawakwaza watu wa Mungu. Mambo yanayompendeza Mungu yanaweza kuharibu uhusiano na watu wasiomcha Mungu lakini ufumbuzi wa hili si kutafuta BALANCE bali ni kuwasaidia watoke huko waliko ili waingie kwenye NURU ili nao waweze kuona wema wa matendo mema yanayompendeza Mungu.

  4. MFANO WA DANIEL
  Tafsiri yako kutoka katika mfano huu ni sawa kwa upande mmoja. Lakini kwa tafsiri ya kwamba Daniel alikuwa na Mahusiano mazuri katika watu wa serikali ya Babel nitatofautiana na wewe. Daniel HAKUWA MTIIFU kabisa kwa amri za serikali ya Babel. Sijaelewa unavyoisoma Biblia. Mstari ulioutolea mfano wenyewe unaonyesha jinsi ambavyo Daniel ALIKUWA KINYUME NA TARATIBU ZA SERIKALI. Katika Dan 6:4-9 inasema Serikali ilitoa AMRI KWAMBA MTU ASIABUDU KWA MUNGU MWINGINE TOFAUTI NA SANAMU ALIYOTENGENEZA MFALME DARIUS. Ndipo ukaja huo mstari wa 10. Kitendo hicho cha Daniel KUPIGA MAGOTI KWA MUNGU ALIYE HAI kulileta vurugu kubwa hadi ikasababisha atupiwe kwenye Pango lililokuwa na Simba. SIJUWI NI KWA NINI WEWE UNASEMA HUU ULIKUWA NI UHUSIANO MZURI wa kuigwa!!. Kwamba hapa kuna BALANCE YA KUIGWA? Hapa nahitaji kufundishwa!

  Ndugu Pona, Unaonaje hapa kama tungetafsiri ifuatavyo: ”Daniel angetaka kuleta BALANCE angesema atapiga magoti tu na kutamka maneno ya kuabudu sanamu kwa mdomo tu lakini moyoni akiwa hamaanishi. Halafu akishamaliza hapo ndipo aende chumbani kwake akamuombe Mungu wa kweli.” Nadhani hii ingefanana na BALANCE ambazo baadhi ya watu wanapokuwa WAMEMPOKEA YESU huendelea na Ibada za Dini zao (ili kuweka ushirikiano mzuri na viongozi wa dini) ambazo nyingine ni pamoja na kupiga magoti mbele ya Sanamu au Picha fulani halafu katika siku fulani za wiki HUHUDHURIA FELLOWSHIP au kwenda kwenye MIKESHA ya WALOLOKE. Ndiyo! Hii ndiyo BALANCE ambayo Daniel aliikataa kabisa. Msimamo wa Daniel ulikuwa either WHITE or BLACK na siyo kutafuta BALANCE. Sheria ya kukataza Kuabudu Mungu ila Sanamu ilipotangazwa NDIPO Daniel akaendelea na Maombi mara tatu kwa siku, wala si kwa kificho. Angekuwa anataka balance ANGEFUNGA MADIRISHA wasimuone. Lakini alifanya waziwazi ili wajuwe kabisa YEYE ALIKUWA KINYUME NAO!

  5. MAJIBU

  a. Ili tusihatarishe safari yetu ya Mbinguni kwa kukumbatia mambo madogo madogo ya hatari inabidi tubadilike kabisa. Maana Mtu akiwa ndani ya Kristo anakuwa kiumbe Kipya, ya kale yote yanaondoka. Vile vile inatakiwa tuitowe Miili Yetu iwe dhabihu safi mbele za Mungu. 2Cor 5:17, Rum 12:1. Kwa ujumla yatupasa tuwe watakatifu katika mwenendo wetu wote. 1Pet 1:15

  b. Mimi na Wewe tumeweza kuokoka kwa sababu YESU ALING’AN’GANIA UTAKATIFU WAKE. (Yesu alipokuwa hapa Duniani alikuwa bado ni MUNGU pamoja na WANADAMU). Kama asingekuwa amebaki na DIGNITY yake kamwe Mpango wa Wokovu usingefanikiwa! Kila mtu aliyekutana na Yesu aliachwa akiwa ni mtu aliyabadilika kabisa. Kazi ya Yesu ilikuwa/ni kuleta Nuru palipo na Giza.
  Nimeeleza Kwamba watu wanaong’ang’ania dunia ni watu ambao wameshaifahamu Neema ya wokovu lakini wanakumbatia mambo mengine kwa tamaa zao za mwili na wala si kwa utukufu wa Mungu. Naomba tutofautishe kati ya mtu asiyemwamini Yesu kabisa na mtu anayeng’ang’ania dunia. Mtu asiyemwamini Yesu huyo si kwamba anang’ang’ania dunia bali hajajuwa kama mtu anaweza kuishi maisha tofauti na hayo anayoishi yeye!

  c. Nilisema hapo juu kwamba HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA KAMA HATUWEZI KUWAAMBIA WATU JUU YA KUWEKA THABITI MSIMAMO WA WOKOVU WAO. Unapomuonya mpendwa mwenzako juu ya jambo fulani si kwamba UNAMNYANYAPAA. Au unapomuambia mtu kwamba inabidi amwamini Yesu na kumfanya awe Bwana na Mwaokozi wake si kwamba Unamnyanyapaa. Kazi ya mtu aliyemwamini Yesu ni kuwasaidia na wengine waweze kumwamini Yesu kama na yeye ambavyo alisaidiwa kuingia kwenye wokovu.

  d. Rafiki yagu Pona, Hakuna Muuguzi yeyote anayetibu mgonjwa pasipo kuchukuwa kinga ya yeye kuambukizwa toka kwa mgonjwa anayemtibu. Niliandika kwamba HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA TUNAUPOINULIWA NA MUNGU HALAFU TUNARUDI CHINI KUWATUMIKIA WATU KWA MAMBO YANAYOHATARISHA KIROHO CHETU. Hii ilitokana na wewe kuandika kwamba TUNATAKIWA KUSHUKA TOKA MADARAJA YA JUU KWENDA KUWAFUTA MIGUU WATU WA CHINI SANA. Lakini kuwafuta miguu watu ni kuwasafisha. Na kuwasafisha si kwa maji na sabuni bali kwa kuwaambia kweli ya NENO LA MUNGU kwa habari ya kutubu dhambi na kumfuata Yesu.

  Kuwatumikia watu kwa mambo yanayohatarisha KIROHO CHETU ni kama vile kutaka kushirikiana nao kwa mambo ambayo hayampi Mungu utukufu na yanayoweza kuharibu ushuhuda wetu na mwisho wake uhusiano wetu na Mungu.
  Fikiria mfano huu: Kama mkaka ameokoka alikuwa na marafiki wavuta bangi na wahuni wahuni, wengine waaovaa suruali wanalegeza hadi nguo zao za ndani zinaonekana, wakikaa mahali kila msichana anayepita wanampigia mluzi na kutamka maneno ya hovyo hovyo, halafu mkaka huyo aliye okoka anakuwa katikati yao, na anavaa kama wao, kwa kisa cha kulinda uhusiano mzuri na kuogopa kuwanyanyapaa wenye dhambi, unadhani wokovu wa namna hii utakuwa na ushuhuda? Utakuwa na matunda? Ninalofahamu ni kwamba kama kaka huyo atakuwa anawaeleweza kweli ya Neno la Mungu na namna ya kuwa na mwenendo mwema kwenye jamii, watu hawa hawawezi kuvumilia awepo kati yao, atakuwa kero maana anawaambia wafanye mambo ambayo yako kinyume na matakwa yao. Na ikifikia hapo watamfukuza atoke kati yao maana ni msumbufu.
  Sasa ndugu yangu Pona, katika hali kama hii utachukuwa jukumu la kuwa nao, ili usionekana umewanyanyapaa? au utawaambia ukweli hata kama ukweli utawafanya wakuone wewe ni adui yao? Pia, kwa sababu huogopi kuhatatarisha kiroho chako utaambatana nao hata kwenye maficho yao wanapovuta bangi? Je katika hali kama hii bado wewe Utakuwa ni Chumvi ya Dunia? (Mat 5:13)
  (Sihitaji unijibu maswali haya bali ni kwa ajili ya wewe kutafakari)

  KUWATUMIKIA WATU PASIPO KUULINDA WOKOVU ni utumishi usio na malengo kwa sababu mwisho wa siku utakuta MTUMISHI na WANAOTUMIKIWA wote wameanguka dhambini. Sasa hapo kuna faida tena ya UTUMISHI WA NAMNA HII???

  Natumaini tuko pamoja!

  Barikiwa!

 59. ASANTE KWA MAFUNDISHO BROTHER JOHN PAUL.
  NIMEKUELEWA SANA ILA NAZANI HUKUNIPATA VIZURI KUHUSU NINI NILIKUWA NAMAANISHA KATIKA MTIZAMO WANGU, SIMAANISHI ILI KUWAPATA WENYE DHAMBI LAZIMA TUSHIRIKANE KATIKA DHAMBI ZAO,MAANA YANGU HAPA NI KWA MFANO.
  BWANA WETU YESU NI MTAKATIFU LAKINI ALIACHA ENZI YAKE MBINGUNI KWA BABA YAKE AKAJA DUNIANI AKAZALIWA NA MWANADAMU NA AKAISHI KAMA MWANADAMU WA KAWAIDA LAKINI HAKUTENDA DHAMBI. KWANGU MIMI HAPO ALIJISHUSHA TENA SANA, NA KAMA TUNA MFUATA YEYE BASI TUMUIGE.

  POINTI YANGU KUHUSU HAKI YA MKWAZAJI NA ANAE KWAZIKA UNAWEZA KUSOMA
  KATIKA WARUMI 14.13 THEREFORE LET US STOP PASSING JUDGMENT ON ONE ANOTHER. INSTEAD MAKE UP YOUR MIND NO TO PUT ANY STUMBLING BLOCK OR OBSTACLE IN YOUR BROTHER’S WAY

  1,KORINTHIANS 8.9 BE CAREFUL ,HOWEVER THAT THE EXERCISE OF YOUR FREEDOM DOESNT BECOME A STUBLING BLOCK TO THE WEAK.
  UMEELEZEA VIZURI KUHUSU MAVAZI ILA TAFSIRI YAKO YA NENO BALACE SIJUI UMEITOA WAPI.

  NINASEMA BALANCE KATIKA MAMBO YA MUNGU NINA MAANISHA HIVI KWA MFANO: MSALABA WA YESU UNAPEMBE NNE, MBILI JUU NA CHINI,MBILI KUSHOTO NA KULIA UKIAMUA KUJIFIKIRISHA UNAWEZA KUPATA TAFSIRI YAKO MWENYEWE ILA YAKWANGU MIMI NI HII. KUTOKA CHINI KWENDA JUU NI MAHUSIANO YA MWANADAMU NA MUNGU AMBAYO YESU AMEYAREJESHA,KUTOKA KULIA KWENDA KUSHOTO NI MAHUSIANO YA MWANADAMU NA WANADAMU,WAKATI MWINGINE HAIHITAJI SANA KUHUBIRI ILI KUWALETA WATU KWA YESU MAISHA YA MTU YANAWEZA KUWA KIELEZO TOSHA.DANIEL 6:10 NOW WHEN DANIEL LEARNED THAT THE DECREE HAD BEEN PUBLISHED,HE WENT HOME TO HIS UPSTAIRS ROOM WHERE THE WINDOWS OPENED TOWARD JERUSALEM, THREE TIME A DAY HE GOT DOWN ON HIS KNEES AND PRAYED, GIVING THANKS TO HIS GOD JUST AS HE HAS DONE BEFRORE,

  MFANO HUU UNAONYESHA NAMNA DANIEL ALIVYOKUWA YUPO COMMITTED KWA MUNGU WAKATI HUO HOU AKIWA NA MAHUSIANO NA WATU KATIKA SERIKALI YA BABLON PIA ALIKUWA NAMSIMAMO JUU YA MUNGU WAKE, HII NDIO BALANCE NINAYO ISEMA PAMOJA NA MISUKOSUKO UHUSIANO WA MTU NA MUNGU MTU NA WATU UNAKUWA HAUTETELEKI SIO KUWA VUGU VUGU. MFANO BINAFSI: NILIANZA KUSOMA BIBLIA KABLA SIJAANZA KWENDA KANISANI AU KUOKOKA.NILICHOKIONA KIKUBWA HUMO KWENYE NENO LA MUNGU NI UPENDO WA MUNGU KWA WANADAMU NA AMRI YA MUNGU KWA WANADAMU JUU YA KUMPENDA YEYE NA WANADAMU KUPENDANA. NILIPO OKOKA MAMBO YALIKUWA TOFAUTI SIMAANISHI KULIKUWA HAKUNA UPENDO KABISA ULIKUWEPO UPO ILA WAKATI MWIGINE KUNAKUWA NA MATABAKA, MFANO WATU WENGINE WANAPEWA VIPA UMBELE SANA KATIKA MICHANGO WENGINE HAWAPEWI,
  KAMA ULISOMA VIZURI HAPO JUU NIMESEMA MUNGU HAWEZI KUKUPA NAFASI YA KUMKARIBIA YEYE SANA, AU KUMJUA YEYE SANA, KUMTAFUTA YEYE SANA HARAFU AKUNYIME HEKIMA YA KUENENDA NA HUO UPAKO MBELE ZA WATU. NINAAMINI HIVI MUNGU ANAPO NIPA NAFASI YA KUMJUA YEYE SANA NI KWA AJILI YAKUNI IMARISHA MIMI NA KUWATUMIKIA WATU.

  NUKUU
  HATUTAWEZA KUWA WATAKATIFU SANA KAMA TUTAKUMBATIA YALE MADOGO MADOGO AMBAYO TUNAYAKUMBATIA KWA TAMAA ZETU WENYEWE WAKATI TUNAHATARISHA MUSTAKABALI WA SAFARI YETU YA KWENDA MBINGUNI.

  SAWA. TUFANYE NINI BWANA ?

  HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA KAMA TUTASHUKA TOKA MADARAJA YA JUU NA KUUACHA UTAKATIFU KWA SABABU YA KUTAFUTA BALANCE NA WATU WANAONG’ANG’ANIA DUNIA

  SAWA. JE WEWE UNGE OKOKAJE KAMA YESU ANGENG’ANG’ANIA UTAKATIFU WAKE NA ENZI YAKE MBINGUNI?

  HATUWEZI KUWA WAKIROHO SANA KAMA TUTASEMA TUNAMPENDA MUNGU NA WAKATI HUO HUO TUNAIPENDA DUNIA

  SAWA. TUFANYE NINI WAKATI BADO TUPO DUNIANI TUNAISHI ILI TUENDE MBINGUNI BILA KUWANYANYAPAA WENYE DHAMBI?

  HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA KAMA MUNGU ANAPOINUA BADO SISI TUNARUDI CHINI ILI KUWATUMIKIA WATU KWA MAMBO YANAYOHATARISHA KIROHO CHETU

  SAWA. TUNA WEZAJE KUWA KONDOO KATIKATI YA MBWA MWITU KAMA TUNAOGOPA KUHATARISHA KIROHO CHETU?

  ENDELEA KUNIFUNDISHA BADO NINA MAPUNGUFU MENGI
  BLESS YOU ALL
  LOVE YOU

 60. Ndugu Pona,

  Nimejitahidi kutafuta ujumbe uliotaka kuufikisha kwa msomaji, katika maelezo yako ya mwanzo na katika majibu kwa ndugu Asheri lakini sijakupata vizuri. Yawezekana ni kiwango changu cha kuelewa au ni namna ambavyo hujaweka wazi msimamo wako. Naomba nami nichangie kutokana na maelezo yako lakini lengo letu wote likiwa ni kuzidi kuitafuta kweli, maana kweli itatuweka huru!

  1. Umeelezea kuhusu mtu anayekwazika hana haki ya kukwazika. Nadhani hapa ulikuwa umesahau yale maneno aliyoyasema Yesu: Mambo ya kukosesha (MAKWAZO) HAYANA BUDI KUJA, lakini ole wake mtu ASABABISHAYE……….(Math 18:6-7). Kwa hiyo hapa mtu hawezi kukwazika hadi amesababishiwa. Makwazo ni FIMBO INAYOTUMIWA NA UFALME WA GIZA kuwapiga watu wa Mungu ili wanapoonana wasiwe na umoja. Kwa maana hiyo jambo la kukosesha (Kwazo) likija lazima litawaumiza ambao limelengwa kwao. Jambo la kutafutia ufumbuzi hapa ni KUONDOA MAMBO YAKWAZAYO na wala si KUWAPA WATU SUGU WASIKWAZIKE YANAPOKUWA YAMEFANYIKA. Dawa hupewa mgonjwa ili ugonjwa uondoke na si mwili wake uwe sugu. Kuufanya mwili sugu siyo tiba maana ugonjwa ukishazidi mgonjwa hukatika ghafla! Kwa hiyo suala hapa si kuwafundisha watu wasikwazike bali kuwafundisha watu wasisababishe makwazo. Haya nayo ni mafundisho ya Yesu kwamba: Basi, yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo TORATI na MANABII (Math 7:12), yaani kwa kiasi kile kile ambacho mtu hutaki ukwazike, basi jitahidi wewe mwenyewe usiwe sababu ya kukwaza mwingine.

  2. Kuondoa makundi kwa kukubali mabadiliko. Hapa ulisema kwamba ”wanaojiona watakatifu sana wanyenyekee mbele za Mungu na wanadamu na wanaojiona wanadhambi sana wafanye bidii kujirekebisha kwa msaada wa Roho mtakatifu ili tufike sehemu ya kuongea kugha moja kwa ajili ya kuujenga mwili wa Yesu”. Mpendwa Pona, kwa habari ya mambo ya Mungu HAKUNA BALANCE (kwa kuwa umetumia neno hili). Hakuna vuguvugu! Kuna baridi au moto peke yake. (Ufunuo 3:16). Balance maana yake ni VUGUVUGU! Kwa Mungu haipo! Ni tatizo sana kwamba kuna watu WANAOJIITA WAMEOKOKA lakini hawataki kufikia viwango vya utimilifu wa wokovu. Wameng’ang’ania mambo ya mwilini ambayo hayana manufaa yoyote kwenye ufalme wa Mungu halafu wanataka kuwateremsha walioko juu (Umewaita wanaojiona watakatifu sana) ili wafikie balance! Hili ni tatizo kubwa kwenye Wana wa Mungu, wanaomtaja Yesu! Umoja wetu binaadamu hauna maana kama si Umoja wa watakatifu. Najuwa kwamba wote tunapambana ili tuweze kuingia mbinguni, hakuna ambaye amemaliza mwendo tayari. Lakini hii si sababu kwamba wale wanaomtafuta Mungu kwa mioyo yao yote, na kwa akili na nguvu zote WALEGEZE MWENDO ili KU-BALANCE na wale wanaopenda mambo fulani ya kidunia, kwa kisingizio cha Umoja. Hii siyo sahihi. Natumaini ulishasoma ile habari ya Wanawali 10. Watano wenye akili na Watano wapumbavu! Isome tena katika Math 25:1-13. Ku-compromise na mambo ya Ki-dunia ni sawa na kumpunguzia mafuta mtu ambaye taa yake haina. Lakini wale wanawali wenye busara hawakufanya hivyo!

  Ninavyofahamu mimi MTU YEYOTE ALIYEOKOKA na ana Roho wa Mungu ndani hawezi ng’ang’ania mambo ya mwili huu ambayo yanaleta mkanganyiko.

  3. Kutokuchangamana kwa sababu ya mavazi na mambo madogo madogo.
  Mpendwa Pona hebu naomba utakafari kidogo juu ya mifano michache hapa chini:
  – Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeweka mpaka wa mavazi yanayotakiwa yavaliwe bungeni. Mtu akikiuka hutolewa nje.
  – Wanafunzi mbalimbali hutakiwa kwenda na sare za shule kama hauna inabidi ukatafute.
  – Watu huvaa sare kwenye mambo mbali mbali. Mtu ambaye hana sare akiingia kwenye kundi hilo huonekana ni kituko na ni tofauti na wenye nazo.
  SWALI: Sasa, Ikiwa katika mambo ya kimwili mavazi yana nafasi kubwa namna hii, Je si zaidi sana katika Mambo ya kuutafuta Uzima wa Milele?

  Najuwa kwamba hakuna sare au mavazi maalumu kwa ajili ya watu waliookoka. Lakini kuna mavazi ambayo hutumika katika maisha ya kawaida ya hapa duniani na makundi mbali mbali ambayo mtu aliyevaa hutambulika kuwa ni wa kundi la watu ambao huvaa hivyo. Mfano Manesi wana mavazi yao ambayo yanatambulika na mtu yeyote atakayeona. Kwa hiyo mtu aliyevaa vile hutambulika moja kwa moja ni Nesi. Na kama siyo Nesi watu watapata tabu sana kueleweshwa kwamba kama si Nesi wa nini avae kama Nesi anavyovaa? Kama si Nesi kwa nini asivae mavazi ya kawaida, mbona yako mengi tu? Kuna mavazi ambayo huvaliwa na watu wenye sifa ya tabia mbaya kwenye jamii. Mtu mwenye tabia njema akivaa hayo naye huonekana ni mwenye tabia mbaya. Na watu watashangaa, Kama wewe si wa tabia hiyo kwa nini Uvae hivyo? Mbona nguo za kawaida ziko nyingi tu? HIVYO MAVAZI YANASEHEMU KUBWA KATIKA TAFSIRI YA MTU!
  Mambo madogo madogo hukuyataja. Lakini udogo wa jambo si tatizo. Tatizo ni effect yake. Jambo hata kama ni dogo kiasi gani lakini KAMA LINASABISHA JUHUDI ZA WATU KUMTAFUTA MUNGU ZIPUNGUWE Jambo hilo ni la kulikimbia kwa nguvu zote! Kwa kuwa hujatoa mfano wa MAMBO MADOGO MADOGO sitaendelea sana hapa.

  5. Mungu kuheshimu umoja
  Ni kweli kabisa Mungu huhesimu umoja. Ndiyo maana imeandikwa: Tazama ilivyo vema na kupendeza; Ndugu wakae pamoja kwa umoja. Zab 133:1. Lakini kumbuka nimesema hapo juu Umoja anaouheshimu Mungu ni Umoja wa watakatifu wenye nia ya kuutafuta Uso wake. Umoja mwingine wowote ambao unalengo kinyume na hilo Mungu hauheshimu bali huubomowa. Umetumia Mfano mzuri wa Wakati wa Ujenzi wa Mnara wa Babeli kwamba Umoja wao ndio ulifanya Mungu awasambaratishe. Vema. Kwa nini? Kwa sababu haukuwa umoja wa kumtafuta Mungu. Ulikuwa ni umoja wa KIBURI. Vivyo hivyo Umoja wetu, hata kama umekusanya wengi kiasi gani, kama si wa Utakatifu na kumtauta Mungu, Mungu ataubomoa!
  Kukubaliana kwa Mambo madogo madogo (yaliyo tofauti na misingi ya Ukristo) hakutaleta Manufaa kwenye Umoja wa mwili wa Kristo. NI LAZIMA TUSIKUBALIANE HATA NA YALE YANAYOONEKANA KAMA NI MADOGO MADOGO lakini ndani yake KUMEJAA HILA ZA UFALME WA GIZA. NI HADI WAKRISTO TUTAKAPOKUWA NA MACHO YA ROHONI YA KUONA HATA YALE AMBAYO KWA MACHO YA NYAMA YANAONEKANA SI TATIZO LAKINI KUMBE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NI MAMBO YA KUFISHA!

  Soma yafuatayo (just the opposite of yours)

  HATUTAWEZA KUWA WATAKATIFU SANA KAMA TUTAKUMBATIA YALE MADOGO MADOGO AMBAYO TUNAYAKUMBATIA KWA TAMAA ZETU WENYEWE WAKATI TUNAHATARISHA MUSTAKABALI WA SAFARI YETU YA KWENDA MBINGUNI.

  HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA KAMA TUTASHUKA TOKA MADARAJA YA JUU NA KUUACHA UTAKATIFU KWA SABABU YA KUTAFUTA BALANCE NA WATU WANAONG’ANG’ANIA DUNIA

  HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA KAMA MUNGU ANAPOINUA BADO SISI TUNARUDI CHINI ILI KUWATUMIKIA WATU KWA MAMBO YANAYOHATARISHA KIROHO CHETU

  HATUWEZI KUWA WAKIROHO SANA KAMA TUTASEMA TUNAMPENDA MUNGU NA WAKATI HUO HUO TUNAIPENDA DUNIA

  HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA KAMA HATUTAWEZA KUWAAMBIA WATU UKWELI JUU YA KUWEKA THABITI MSIMAMO WAO WA WOKOVU
  Kumbuka: Na hao waongozao wengine kutenda Haki watang’aa kama Nyote milele hata milele! Daniel 12:3

  Laiti kila mtu aliyeokoka angekuwa wa Kiroho sana! Hapo ndipo tungekuwa na umoja wa kweli. Umoja wa watakatifu. Hapo ndipo wakati tungelikuwa katika kunena Mungu angesikia na Kabla ya kuomba Mungu angejibu! (Isaya 65:24). Lakini inasikitisha kwa sababu kuna watu wameshaitwa kwenye Neema ya Mungu lakini wao bado wanakumbuka Matango na Nyama za Misri – Hesabu 11:5. Na badala ya kutoka huko wapige hatuwa mbele wanataka kuwavuta mashati walioko mbele yao!

  Kwa wanaotaka kwenda Mbinguni ni wakati wa kubadilika. There must be a Remarkable Change!

  Tuendelee kujifunza.

 61. YESU NI BWANA.
  ASANTE KWA MASWALI MTUMISHI ASHERI.
  1.WALE WANAOJIONA WATAKATIFU SANA , MAANA YANGU NI WATU WANAO SHUGHULIKA NA MAMBO YA KIROHO TU NA WAKO MSTARI WA MBELE KUKOSOA WENGINE WAO MARA ZOTE WANAJIONA WAKO SAHIHI ILA WENGINE WANAKOSEA. MIZANI NI UPENDO

  2.WANAOJIONA WENYE DHAMBI SANA AU MAKOSA, MAANA YANGU NI WATU AMBAO WAMEMKOSEA MUNGU WAKAAMUA KUTAFUTA MSAADA ILI WATUBU NA MARA WANAPOKUTANA NA WATUMISHI ILI WASAIDIWE BADALA YA KUSAIDIWA KWA UPENDO WANAKOSOLEWA KOSOLEWA YAANI WANAKUWA (OVER CORRECTED) NA WATU AMBAO NAO WANGEPATA NAFASI YA KUWAKOSOA KWA MUJIBU WA NENO LA MUNGU, HAO WATUMISHI NAO WAKATI MWINGINE WANALIKOSEA NENO INGAWA WAO NDO MABINGWA WA KUKOSOA. HIVYO KUSABABISHA WATU KUWA MANUNDA AU SUGU KATIKA KUTENDA DHAMBI.

  3. UKIROHO SANA MAANA YANGU NI KUNA WATU WENYEKUSHIKILIA MITIZAMO AU MAPOKEO AMBAYO YANAONEKANA YA KITAUWA INAWEZA KUWA LIFESTYLE NA NAMNA WANAVYOFANYA MAMBO YAO YANAYOKUBALIKA KATIKA NYUMBA ZA IBADA LAKINI UKIYAPIMA SAWA NA NENO LA MUNGU UTAKUTA KUNA KASORO. MIZANI NI UPENDO

  MUNGU HAWEZI KUJICHANGANYA ILA SISI TUNA JICHANGANYA WENYEWE. MUNGU NI ROHO NA WOTE WAMWABUDUO IMEWAPASA KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NAKWELI. MUNGU HAWEZI KUKUPA NAFASI YA KUMKARIBIA YEYE ZAIDI YAANI KUWA KIROHO SANA HARAFU AKAKUNYIMA HEKIMA YA NAMNA YA KUENENDA NA HUO UPAKO MBELE ZA WATU WAKE.

  KUWA KIROHO SANA KWA MAANA YA KUMKARIBIA MUNGU SANA NI JAMBO JEMA NA NI SAHIHI MAANA HUKO NDIKO KUUSHINDA ULIMWENGU.
  HATUWEZI KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA MUNGU KAMA HATUTAKUWA NA MAHUSIANO MAZURI WATU HASA TUSIO WAPENDA,
  HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA MBELE ZA MUNGU KAMA HATUTII NINI MUNGU ANATUAMURU KUWAFANYIA WATU.

  HATUWEZI KUWA WAKIROHO SANA KAMA HATUTAKI KUSHUKA TOKA KWENYE MADARAJA YA JUU NA KWENDA KUWAFUTA MIGUU WATU WA CHINI SANA, HATUWEZI KUWA WA KIROHO SANA KAMA TUNATAKA KUINULIWA NA MUNGU NA TUNAKATAA KUWATUMIKIA WATU.

  HATUWEZI KUWA WAKIROHO SANA KAMA TUTASEMA TUNAMPENDA MUNGU SANA TUSIPO WAPENDA WANADAMU. SIZUNGUMZII UPENDO WA MANENO MATUPU, UPENDO UNAGHARIMU MUDA WAKO,MALI YAKO,AKILI YAKO, HISIA ZAKO, NGUVU ZAKO, TAALUMA YAKO NA MOYO WAKO.

  TAFADHALI NIFUNDISHENI
  ASANTENI

 62. Shalomu!!

  Bwana Yesu asifiwe wapendwa!!!!

  Namshukuru Mungu kwa michango mbalimbali iliyotolewa kuhusu eneo hili.

  Nimesoma mchango wa ndugu Pona (A.K.A DASURVIVOR), nikawa sielewi baadhi ya mambo aliyoyasema nikaona ni vema nimuombe anisaidie kunipa alimaanisha kitu gani. Mambo yenyewe ni kama yafuatayo:-

  Wale wanaojiona watakatifu sana…….

  Wanaojiona wenye dhambi sana au makosa…….

  Ukiroho sana..(pamoja na kuwa hakusema kuhusu Ukiroho kidogo, nitaomba pia anipatie maana yake kwa kuwa ni kinyume cha ukiroho sana…)

  Mungu awabariki na kuwafanikisha.

  Asheri

 63. OK. STAHA NIJAMBO LA MSINGI KATIKA MAVAZI LAKINI SI KATIKA MAVAZI TU BALI KATIKA MAMBO YOTE LAZIMA KUWE NANAMNA AMBAYO TUNAFANYA AU TUNA VAA, KAMA WATU FURANI WANA KWAZIKA BASI TUSIFANYE AU TUSIVAE, LAKINI NAO SIO HAKI YAO KUKWAZIKA TU KILA WANAPO WAONA WATU FURANI WANAFANYA AU WANAVAA MAVAZI FURANI, KINACHO KOSEKANA HAPA NI BALANCE KWA SABABU ANAEKWAZIKA HANA HAKI NA ANAE KWAZA HANA HAKI, KINACHO TAKIWA NI KUWA MAKINI AU KUWA MACHO( CONSCIOUSNESS) ILI KUSIWE NA MAKUNDI AU MGAWANYIKO KATIKA KANISA LA LEO LAZIMA KILA MTU AKUBALI MABADILIKO WALE WANAJIONA WATAKATIFU SANA NA KUWAONA WENGINE WAMEPOTEA WAWE WANYENYEKEVU MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU MAANA NAO WANA DHAMBI PIA, NA WALE WANAO JIONA WANADHAMBI SANA AU WANAMAKOSA SANA BASI WAFANYE BIDII KUREKEBISHA KWA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU ILI TUFIKE SEHEMU TUNAKUTANA NA KUONGEA LUGHA MOJA KWA AJILI YA KUUJENGA MWILI WA YESU.

  KWA SABABU KAMA MAVAZI NA MAMBO MADOGO MADOGO YANA SABABISHA TUSICHANGAMANE TUTAWEZAJE KUKAA PAMOJA NA KUJADILI MAMBO MAKUBWA YANAYOHUSU JAMII NA NCHI YETU KWA UJUMLA????? AU NDO KILA MTU KIVYAKEVYAKE? AU NDO UKIROHO SANA?HAIWEZEKANI MAANA HATA MUNGU ANAHESHIMU UMOJA, KUMBUKA MNARA WA BABELI NI UMOJA WAO ULISABABISHA MUNGU KUWASAMBARATISHA. LEO HII WAKRISTO WAKO WENGI LAKINI HAWAKUBALIANI KATIKA MAMBO MADOGO MADOGO TUJIFUNZENI KWA SIAFU WADUDU AU MCHWA.

  TUACHE KUSHIKILIA MITAZAMO INAYOTUSAMBARATISHA BADALA YAKE TUTAFUTE UFUMBUZI AMBAO UTALETA SURUHISHO LA SISI KUELEWANA NA KUKUBALIANA, HALI ILIVYO SASA LAZIMA TUBADILIKE, SI KILA MABADILIKO LAZIMA TUBADILIKE NAYO LAKINI YALE AMBAYO YANAGUSA HATIMA YA IMANI YETU NA MAISHA YETU YA KILA SIKU HAPO INABIDI TUKAE CHONJO

  .A.K.A DASURVIVOR

 64. Kwa upande wangu naona hili swali linazidi kuwa gumu kutokana na wengi wanaojadili wanajadili kibinadamu na si kiroho napenda kumuunga mkono Ndg Paul kwani amelezea kiroho zaidi.Mtu anayeongozwa na Roho mtakatifu sio rahisi kubabaika kwenye swala la uvaaji.

  Iko haja yakumuomba Mungu azidi kutufunulia na Roho mtakatifu atuongoze katika hili .
  Kwa namna yakibinadamu suruali sio mbaya kwa mwanamke kwani wapo wanawake wanavaa sketi ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kiasi kwamba ni bora mtu huyo angevaa suruali kuliko kuvaa hiyo sketi ambayo tunaita ndio vazi la mwanamke.

  MUNGU AWABARIKI.

 65. Mpendwa Asheri Mungu akubariki sana kwa mchango wako ulio rohoni mno kwa lugha nyepesi kabisa kwa kila mkristo wa leo ambaye ana mapenzi mema na hamu ya kwenda mbinguni bila kumtukanisha Bwana wetu YESU.
  Nashauri wapendwa tujitahidi kuwa na michango halisi kama hii ambayo itasaidia wapendwa wakristo wenzetu waliopoteza mwelekeo kujiona katika mwanga bora wa neno la Mungu wetu.
  Mungu awabariki wote.

 66. Shalomu!!

  Nami naona niseme kidogo sana juu ya jambo hili, mchango wangu ni huu, Ndugu John Paul (sehemu ya kwanza) amefanya tathmini kubwa sana juu ya hali ya kanisa kiroho, hali ambayo imetufanya tuwe tofauti sana na wenzetu waliotutangulia. Baada ya kusoma uchambuzi wake, nilidhani hoja hii ingefikia mwisho kwani sote tunafahamu kuwa kanisa liko katika hali mbaya sana.

  Hivi sasa wokovu umepoteza radha yake na kitu kikubwa kilichotufikisha hapa ni ile hali ya kutopenda kujitenga na dunia, tumeipenda dunia na hivyo tumeacha kumpenda Mungu, nawaomba tusome yale aliyoyasema ndugu John Paul na kuona ni kwa jinsi gani mambo hayo yametukumba, na hapa nasema kwa kila mmoja wetu binafsi.

  Kama wokovu ni kujitenga na dunia? hivi kweli tumejitenga na dunia? Hivi wale wenzetu waliosimama na kufanya mambo makubwa kiroho hawakuwa wanaongozwa na Roho Mtakatifu? Hivi tunamsubiri Roho Mtakatifu atuambie kuwa kuvaa nguo fulani ni vibaya wakati kila mahali jambo hilo linazungumzwa? huko kutakuwa ni kumkosea heshima Roho Mtakatifu!!!! Mimi naona kanisa la leo tunashangaza sana, tunapata shida na nguo gani tuvae? Biblia inasema tumejengwa katika misingi ya Mitume na Manabii, ukiangalia mitume hawakuwa na muda wa kujadili ni mavazi gani wavae, walikuwa wakiangalia kuona kuwa hawalaumiwi kwa jambo lolote katika utumishi wao. Hivi kuna heshima gani mtu aliyeokoka akapita mahali watu wakajiuliza hivi huyu naye ameokoka? au waseme kama wokovu wenyewe ndio huu basi afadhali sisi.

  Ndugu zangu naomba tufahamu kuwa huko Ulaya yanakotokea mambo haya, hali ni mbaya sana, Mungu hatajwi huko, makanisa yamegeuzwa madanguro au majumba ya makumbusho, watu hawana muda na Mungu, ingawa wapo wale wasiompigia magoti baali. Inaonekana hata sisi tunaenda huko huko, kwani kila kinachotoka Ulaya tunakiona cha maana, leo hii tunashindana kwa mavazi wakati Paulo anatuonya tuishindanie Imani, ndugu zangu, hakuna cha kulinganisha na imani, imani ni kitu cha thamani sana, tunapaswa tuwe na dhamiri hiyo na kukaa katika mtazamo huu. Ukiangalia yale yote yanayotutesa siku za leo, utagundua ni mambo ya kimwili, na kawaida mwili hushindana na Roho na hivi viwili haviwezi kukaa pamoja. Mtu akitetea kuvaa suluari, hata kama inaleta shida si tu kwa watakatifu, bali hata miongoni mwa jamii isiyoamini, je huo si mwili?

  Mimi hujisikia vibaya sana pale ambapo ukionekana una maadili unaulizwa kama ni Muislamu, yaani mtu akikuona unatunza maadili anakuuliza are you a muslim? Hivi kweli sisi tunazidiwa maarifa na ufahamu na hao? Hivi sasa uislamu unapata nguvu ulaya na moja ya sababu ni kuwa ukristo hauna radha, hakuna maadili wala wakristo hawana tofauti na watu wengine hivyo mtu aliyechoshwa na hali hiyo akatamani kuona jamii bora basi anaona afadhari awe muislamu maana hao huonekana wana afadhali hasa kwa upande wa maadili na hapa nasema maadili ya nje. Je hatutahukumiwa na Mungu kama mwonekano wetu na maadili yetu yanatufanya tuonekane ovyo kuliko hata waislamu?

  Nawaombeni sana wapendwa, tunayo kazi ya kushughulikia suala la maisha ya utakatifu ili na sisi tusizimie kama wenzetu walivyo hivi sasa, tukumbuke Bwana wetu Yesu anakuja.

  Shalomu!!!

 67. Ahsante sana mr Bernard kwa mchango wako mzuri sana wa kujenga ufalme wa Mbinguni.
  Hata hivyo napenda kukujulisha kuwa kuongozwa na Roho mtakatifu si kama watu wengi wanavyofikiri kuwa ni kuacha mambo yajifanye yenyewe. Biblia inatufundisha kuwa tunapaswa kuenenda kwa roho ili tusizitimize tamaa za mwili.[Gal6] Naomba ujue kuwa kazi ya Roho Mtakatifu ni kututia kwenye kweli yote,kutufundisha,kutufariji na kutufunulia kwa habari ya hukumu,haki na DHAMBI [Soma injili ya Yohana kuanzia sura ile ya 14-15]
  Ni vizuri kuwa Agano jipya limepandwa mioyoni ambako ndiko tunakotakiwa kuhifadhi amri na sheria za Mungu na unaweza kuona Ukiri wa mtume paulo katika barua kwa Rumi “nasema kweli katika kristo DHAMIRI YANGU IKINISHUHUDIA”
  Tunapaswa kufahamu kuwa biblia inafunua kuwa maisha ya kikristo ni ya kuenenda kwa IMANI si kwa kuona [2kor5:7] na si vinginevyo. Sasa kuishi kwa kumtegemea Roho wa kristo ni kuliishia neno la kristo ambalo ni kweli yote anayoifunua kwetu tunaposoma na kuzingatia mafundisho yake na hapo dhamiri zetu zinahuhishwa na utu wetu wa kale zikiwemo akili na mapenzi yetu unachakaa na dhamiri mpya inaundwa ndani yetu ambayo inatufanya tujue hakika nini yaliyo mapenzi ya kristo. Maneno ya Yesu akali katika mwili huu wa nyama alisema ‘Ninyi mkikaa katika neno langu mtaifahamu kweli nayo itawaweka huru kweli kweli” mahali pengine akaagiza kuwa “Mkinipenda mtakaa katika neno langu” tena “Ninyi mkikaa katika neno langu na maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni mtakalo lote nanyi mtapokea” Uhuru aliouweka Yesu kwetu si wa kuzivunja amri za Mungu bali kuona kuwa amri zile ni takatifu na hivyo nguvu mpya ndani yetu inaundwa ndani yetu inayotuwezesha kuchukua hatua ya kuishinda dhambi. Mtume Paulo anaita nguvu hii ni silaha yenye uwezo wa kuangusha ngome na kuangusha kila fikra ipate kumtii kristo na pia kupatiliza maasi.[2kor10:3-4]

 68. Tukisema Roho Mtakatifu mwenyewe atufundishe, inamaanisha kuwa wokovu ni rahisi sana, kitu ambacho si kweli. Wokovu ni mgumu sana, ndiyo maana hata sasa watu wanahubiriwa kwa Roho Mtakatifu juu ya wokovu, lakini bado wanapinga na kueleza kuwa hakuna kuokoka duniani. Shetani anatumia sana dini, anatumia sana viongozi wa dini, watu au washirika katika dini hizo wanawafanya viongozi wa dini kuwa ndiyo miungu wao wadogo. Hilo limefanya hata waliookoka nyakati hizi, wabaki bado kwenye wokovu vuguvugu, kwa kuzidi kuwa katika mapokeo mapya; wameacha mapokeo ya zamani wameingia kwenye mapokeo mengine na kuwafanya viongozi wao wa madhehebu, kuwa ndiyo Roho Mtakatifu.

  Ndugu zangu katika Kristo, kuhusu mavazi ambayo yamezua mjadala mkubwa sana, hata kati ya watumishi na watumishi; swala la kufahamu hapa kwa kila mtu aliyeokolewa na Kristo, ni kwamba mavazi peke yake hayana sehemu kabisa katika wokovu, kinachotakiwa ni wokovu kisha mengine yafuate.

  Hatuwezi tukaokoka halafu tuseme eti tumsubiri Roho Mtakatifu aseme mwenyewe ndani yetu no, hiyo bila shaka ni roho ya kiburi. Mtu anasubiri aambiwe na mchungaji wake, kuwa kitu fulani ni dhambi au la, kwa nini tusubiri mpaka wachungaji wetu watueleze? Kama ni hivyo, hatujakombolewa bado, tungalimo katika dini, tumetoka kwenye dini moja na kuingia kwenye dini nyingine!.

  Jaribu kuwaza, kwa mfano huku Zanzibar niliko mimi, eti mwanamke uliyeokoka unaenda kumhubiria mwislamu umevaa suruali! Sijui utaanzia wapi hata kuhubiri Injili yenyewe, atakushanga na kukuona kafiri kikwelikweli. Yeye (mwislamu) amevaa nguo za kujisitiri, tena hana Roho Mtakatifu, wewe unaenda mabega wazi na suruali yako tena umejaa Roho Mtakatifu na unazidi kumsubiri huyo Roho azidi kukueleza zaidi yapasayo kufanywa, hakika hutaeleweka kabisa. Hivyo mavazi wapendwa, yanasehemu kubwa sana, hasa katika kuhubiri Injili yetu.

  Unapokuwa umevaa kama unavyotaka wewe pamoja na wokovu wako, watu wasioamini hawawezi kukuelewa! Ndiyo maana kuna wengine utakuta wanasema “Nitakapookoka mimi nitaokoka kweli kweli” Kwa nini wanasema maneno hayo? Ni kwa sababu ya tabia zetu, mienendo yetu, mavazi yetu na maisha yetu ya wokovu kwa ujumla yanakuwa siyo mazuri au ya kuridhisha.

  Tukiwa hatutaki kubadilika eti mpaka Roho Mtakatifu atuamlie, tutabaki hatuna nguvu za kiroho wala ujasiri kamili juu ya kuhubiri Injili hatutakuwa nao.

  Nyakati hizi ni nyakati nyingine, maandiko yanasema watakatifu watazidi kutakasika na wachafu watazidi kuwa wachafu; tusiwe miongoni mwa wanaozidi kuwa wachafu, bali tuwe miongoni mwa wanaotakasika. Tusifungiwe nira ya mapokeo; kama viongozi wetu hawataki kuweka msisitizo juu ya hili (yaani mavazi) tuachane nao, kwani wao hawana mbingu za kwako, kila mmoja atahukumiwa sawasawa na Injili ya Kristo!

  Tusitake mambo mteremko, maandiko yanasema ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu, si nguvu za kimwili bali pamoja na kumshirikisha Roho Mtakatifu (Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka).

  Ingekuwa rahisi kiasi hiki, akina Petro wasingeuawa kwa kusulibiwa kichwa chini miguu juu, akina Paulo wasingeuawa kwa kukatwa kichwa, akina Yohana wasingetupwa katika kisiwa cha Patmo. Inabidi tufikie hatua ya kukataliwa na dunia, ndipo Mungu atakapoweza kututhibitisha kuwa tuko katika imani au la! Tukienenda kama ulimwengu uenendavyo, hakika tutajikuta siku ya mwisho tunakataliwa; Mungu atatuambia, tokeni kwangu enyi mtendao maovu, sikuwajua ninyi kamwe!!!. Itakuwa ni kilio na kusaga meno!.

  Mbarikiwe na Bwana,

  Mungu ampe neema kila mmoja wetu, kuzidi kumsikia Roho Mtakatifu katika kweli, badala ya wanadamu, Amina!.

 69. Mpendwa Dar Silva ninakushukuru kwa maoni yako ambayo yanasaidia kuinua kazi ya Mungu.
  Hata hivyo napenda kukujulisha kuwa Paulo hajawahi kusema kuwa mwanamke kuvaa mavazi ya mwanaume ni dhambi.
  Huenda umefananisha na maelekezo ya Torati ambayo yanaagiza mwanamke kutovaa mavazi yampasayo mwanamme na kinyume chake. Ambacho mtume Paulo ameagiza kwa wanawake wakristo ni kuvaa mavazi yenye staha na kujipamba kwa ndani.
  Vile vile napenda kukushauri tu mpendwa kuwa tuwe makini kujadili jambo lolote ambalo hatuna uelewa nayo mzuri. Ni vizuri kufanya utafiti tukiongozwa na Roho mtakatifu ambaye atakupa kuelewa kwa wazi kwani yeye ndiye mwenye jukumu la kututia kwenye kweli yote.
  Suala la mavazi tuwaachie walio katika malumbano sisi tujifunze kwa maandiko na kumsihi Roho wa Mungu atupe ufunuo wake ambao utakupa amani ya kweli.
  Mungu akubariki sana

 70. Naomba tusi iii dilute bible ….Paulo alisema Mwanamke kuvaa mavazi yampasayo mwanaume ni dhambi and vise vesa is true….

 71. Napenda wapendwa tujitahidi sana kuangalia maswali na majibu yetu kwani yapo maswali mengine ambayo hayana ukomo na kwa hakika unaweza kutumia majibu mengi tofauti kuyatafutia ufumbuzi lakini yanabaki yakielea tu.

  Nionavyo mimi ni vyema Roho wa Mungu aamue katika dhamiri yake kuwa anachofanya ni sawa ama la. Mtume Paulo katika barua kwa Wakolosai mwishoni mwa sura ile ya pili ameasa tusijitengenezee sheria zetu(USIGUSE,USISHIKE,USINUSE. MAMBO HAYA YANAONEKANA YANAONEKANA KUWA NA HEKIMA KATIKA IBADA TULIZOJITUNGIA LAKINI HAYAFAI KITU KUZUIA TAMAA YA MWILI) Mahali pengine mtume Paulo amefundisha sana kwa Wakorintho hasa katika barua ile ya kwanza kuhusiana na ibada ya sanamu. Yeye aliwataka Wakristo wa korintho waepuke ibada ya sanamu lakini akawataka wanafunzi watambue kuwa sanamu si kitu mbele yao na kuwa wapo huru kula chakula ama vinywaji vilivyotolewa kama sadaka kwa sanamu lakini si kwa kuadhimisha ibada hiyo lakini ni kama chakula kingine chochote. Lakini si hayo tu aliwakemea Wagalatia juu ya kurudi katika kuabudu kwa mfumo wa sheria [Galatia 3:3-6] akithubutu kuwaita WAGALATIA MSIO NA AKILI. TENA WALIOLOGWA. Si kwamba hakutaka watu wasiji behave kama maandiko yanavyotaka lakini aliwataka watambue kuwa wao ni huru bado wapo na Bwana harusi Yesu hivyo Roho wa Yesu ndani yao ni mkuu kuliko kiu ya mambo ya dunia hivyo waenende kwa jinsi ya Roho tena waenende kwa imani si kwa kwa kuona [Galatia 6:156;2Korintho5:7]
  Tunaweza kusema sana juu ya mambo mbali mbali kama mavazi na kadharika lakini msingi wa mtu aliyeokoka ni kukumbushwa na kufundishwa na Roho mtakatifu. Kukazana kuwashambulia ambao dhamiri zao hazijafundishwa na Roho mtakatifu juu ya mambo hayo ni sawa na mkulima anayetumia trekta kufukia majani kwa udongo wakati wa kiangazi ambapo itaonekana kama yamekufa lakini wakati wa mvua majani haya huchipua kwa nguvu tena kwa upya.
  Niwaombe sasa kwa maombi na mafundisho ya Imani ipatikanayo katika agano jipya tuchukue nafasi yetu kuwasaidia wenzetu kwa upendo yale ambayo tunadhani hawamtendei haki Mkombozi wetu Yesu kristo.

  Ukweli tukubaliane kuwa ukristo wa nyakati hizi umeathiriwa sana na mapokeo ya kimagharibi ambayo mengine yalielemea kwenye mila na desturi za wamisionari wetu walioleta ukristo. Wasomi wetu wa neno la Mungu wanaficha mengi ambayo yangesaidia kuondoa baadhi ya utata uliopo sasa.
  Mungu awabariki wote

 72. Wapendwa,
  Hapa hakuna ubishi kuwa vazi la suruali ni kwa ajili ya mwanaume na kamwe watu wa Mungu hatuwezi kukubaliana na sababu yoyote ile ya kuhalalisha vazi hili kwa wanawake.Biblia ina jibu la kila swali tatizo ni watu hawasomi maandiko na hata wakisoma hawamuombi Roho Mtakatifu awape ufunuo wa wayasomayo.Wanawake kung’ang’ania kuvaa suruali hakika iko roho ya ibilisi nyuma yake,na roho hii iko kuanzia kwa watengenezaji mpaka wavaaji.Watu wa Mungu(waliokoka) tusimame kwenye zamu zetu ili roho huyu mchafu atoweke na wanawake warudi kuvaa mvazi yanayowastahili.
  MUNGU AWABARIKI WOTE.

 73. Habari? sualuali mi naona inategemea ni suluali ipi. Maana zipo zilizotengenezwa kwa ajili ya wanaume na nyingine kwa ajili ya wanawake. Kingine mi nadhani kama ni dhambi itakuwa ni aina ya uvaaji kuna wasichana au wanawake wengine hawastahi miili yao. Wanavaa zimewabana au maungo yao yanaonekana. Lakini pia zipo suruali za heshima ambazo hazimpi mwanaume kishawishi na hata mvaaji naye anakuwa huru kupita sehemu yoyote ile. Ni dhambi kufuatana na nia ya mvaaji.

 74. Mpendwa First,

  Naomba kukushauri tu kwamba kwa masuala ya Rohoni kila mtu anasimama kwa nafsi yake mwenyewe. Ninasema hivyo kwa kuwa nimeona kwenye komenti zako unatumia neno la first person plural yaani ‘sisi’ kila unapohitaji ufafanuzi au kuelezea fikra zako. Sina uhakika kama unawakilisha kundi fulani ambao wanakuambia uandike kwa niaba yao pia. Narudia tena sina uhakika. Ninakushauri sana utumie first person singular ‘mimi’. Hii itakusaidia wewe binafsi kujuwa umesimama wapi.

  Kwa mfano ninanukuu “Mimi nilitegemea tutapewa maandiko yanayoelezea vazi sahihi kuliko mtizamo wa mtu binafsi. Tusaidieni maandiko kutoka kwenye Biblia tubadilike” Mwisho wa kunukuu.
  Kauli kama hii iko too general. Naamini kuna baadhi ya watu wanaosoma hapa ambao wao wanayaelewa maandiko na walisha badilika. Kwa hiyo ukisimama mwenyewe kwa nafsi yako inaweza kuwa rahisi kwako kupata msaada wa kiroho kuliko kujiweka katika kundi.

  Hata hivyo suala la vazi sahihi kwamba wanaume wavae suruali na wanawake wavae gauni au kinyume chake halijaandikwa namna hiyo. Kilichoandikwa kwenye Biblia ni kwamba Mwanamke asivae mavazi yampasayo Mwanaume na Mwanaume asivae mavazi yampasayo Mwamamke. Mavazi yanabadilika na wakati. Na kila wakati unakuja na mavazi ya kiume tofauti na ya kike. Andiko lenyewe ni hili lifuatalo:
  “Deutronomy 22:5 The woman shall not wear that which pertaineth unto a man, neither shall a man put on a woman’s garment: for all that do so are abomination unto the LORD thy God”

  Kwa maelezo zaidi, lakini kwa ufupi, kuhusu mavazi yampasayo mkristo endelea kusoma yafuatayo kutoka kwa Mwalimu Bruce Lackey wa Way Of Life Literature. ( Zaidi ni kutoka http://www.wayoflife.org/fbns/bibleguidelines.htm iliyotambulishwa na Kars):-

  The thing I want to talk to you about tonight is Christian clothing. What do we mean when we say “Christian clothing”? Is that some particular article? No, we can’t hang a particular suit or a particular dress up here tonight and say this is Christian. Rather, there are five questions that you need to ask yourself to answer the question, “What kind of clothing should I wear?” There are five questions, and I am going to support these by God’s Word.

  No. 1 IS IT WORN BY THE OPPOSITE SEX?

  Turn back to Deuteronomy 22:5 for our beginning. Here is our first principle. When I am trying to decide whether or not I should wear a certain thing, my first question is “Is that item worn by the opposite sex?” In other words, I as a man should not wear anything that a woman would wear. And a woman should not wear anything that a man would wear.
  “The woman shall not wear that which pertaineth unto a man, neither shall a man put on a woman’s garment: for all that do so are abomination unto the Lord thy God.”
  I am well aware of the fact that people resent using this verse because it is in the Old Testament. And many times people say we can’t use that verse unless we are going to use the whole chapter. For instance, we wouldn’t want to use verse nine. A lot of people violate that verse by planting two or three different kinds of seeds in the same plot of ground. Similarly, we’ve all violated verse eleven about wearing garments with different kinds of cloth. Nearly everything we have on is made out of a weave of different things. So how can we take verse five and not take verse nine or verse eleven?

  Here is the principle for rightly dividing the Word of Truth: Any principle found in the Old Testament which is repeated in the New Testament is for us today. Let me prove that to you. Keep your place at Deuteronomy and go over to 1 Corinthians 10. In 1 Corinthians 10 we have a book written by a grace preacher. Nobody can deny that the Apostle Paul was a grace preacher. He preached that we’re not under the law but under grace, and he wrote about that time and time again. Without a doubt he is a New Testament preacher. But I want you to notice that in this entire chapter of 1 Corinthians 10 he constantly uses the Old Testament Scripture to prove something. Look at verses one and two: “Moreover, brethren, I would not that ye should be ignorant, how that all our fathers were under the cloud, and all passed through the sea; And were all baptized unto Moses in the cloud and in the sea.” That was taken from Exodus 13 and 14, in which passage we read about the cloud, and about the Red Sea parting, and how they walked across on dry land, which was similar to being baptized. They were covered with the water, even though not a drop of it touched them. Paul is referring to the Old Testament. Look at verse three: “And did all eat the same spiritual meat.” That refers to Exodus 16, when God gave the manna from Heaven. That was called spiritual food. Verse four: “And did all drink the same spiritual drink: for they drank of that spiritual Rock that followed them: and that Rock was Christ.” That refers to Exodus 17, when Moses took his rod and struck the rock, and God gave gushing water out of that flinty rock.

  Notice that he is referring to several Old Testament incidents. Verse five: “But with many of them God was not well pleased: for they were overthrown in the wilderness.” That is referring to Numbers 13 and 14. They refused to go into the land of Israel and inherit it, and they said, “We can’t take it,” and so God overthrew them in the wilderness. Many of them died.

  Now look at verse six. “Now these things were our examples, to the intent we should not lust after evil things, as they also lusted.” You see. It’s not wrong to use the Old Testament to teach New Testament Christians to do something right. Paul did it.

  Let’s keep on going. Verse seven: “Neither be ye idolaters, as were some of them; as it is written, The people sat down to eat and drink, and rose up to play.” Here he refers to Exodus 22:6. The Apostle says, “Don’t you be like that.” Verse eight: “Neither let us commit fornication, as some of them committed, and fell in one day three and twenty thousand.” That is talking about Numbers 25. Verse nine: “Neither let us tempt Christ, as some of them also tempted, and were destroyed of serpents.” That is talking about Exodus 17. You remember about the brazen serpent being raised in the middle of the camp, and so on.

  Look at verse ten: “Neither murmur ye, as some of them also murmured, and were destroyed of the destroyer.” That is found in Exodus 15, 16 and 17, among many other places; they murmured several times.

  Now look at verse eleven: “Now all these things happened unto them for ensamples: and they are written for our admonition, upon whom the ends of the world are come.” Two times in these chapter, in verse six and in verse eleven, he tells us without a doubt that those Old Testament writings were for us today. It is a foolish and fictitious objection when someone says that we can’t use the Old Testament for us today. Here he very clearly outlines verse after verse, experience after experience in the Old Testament, to prove something that Christians ought to do right now. And that’s not the end. In the rest of the chapter he does it again and again.

  We can go by the Old Testament. What is our rule? Any Old Testament principle repeated in the New Testament is for us today. Now you won’t ever find a New Testament verse that says observe the sabbath day. That is the reason we don’t do it. You won’t find any New Testament verse that says we are to kill an animal and have a blood sacrifice. That’s the reason we don’t do it. But anything commanded in the Old Testament and repeated in the New Testament is for us today.

  Do not wear clothing that the opposite sex wears. And if you are in doubt about it, just don’t and you will be safe. Just make sure that what you wear identifies you as a male or as a female, and not in a way that a person would have to look at the tempting zones of the body to tell whether you are a male or female. That is what the Devil wants you to do, and surely you don’t want to cooperate with the Devil on this matter.

  No. 2 WHAT DOES IT MAKE OTHERS THINK OF ME?

  In Proverbs 7:10 the Scripture has a warning to a young man against immorality: “And, behold, there met him a woman with the attire of an harlot, and subtil of heart.” God is warning about a woman dressed like a harlot. Now the question we ask is how is a harlot dressed? Have you ever seen a program on television in which they show a woman posing as a prostitute? If you have watched any of the police shows you see that. All you have to do is look at the way they are dressed. The bad thing about is that some Christian people dress the same way. Now, you don’t want anybody to think that about you. You might wonder if people really think that about you. Yes, they do.

  No.3 PREDOMINATELY, WHAT KIND OF PEOPLE DRESS THAT WAY?

  See, here is the third question. Predominately, what kind of people wear the kind of clothes you are thinking of wearing? If it’s the wrong kind, you surely don’t want to identify yourself with it.

  No.4 MUST I USE THE ARGUMENTS OF THE WORLD TO JUSTIFY IT?

  Here is the fourth question: Must I use the arguments of the world to justify it?
  “Where is the wise? where is the scribe? where is the disputer of this world? hath not God made foolish the wisdom of this world?” I Cor. 1:20
  “That your faith should not stand in the wisdom of men, but in the power of God.” I Cor. 2:5
  “For this cause we also, since the day we heard it, do not cease to pray for you, and to desire that ye might be filled with the knowledge of his will in all wisdom and spiritual understanding.” Col. 1:9

  No.5 WILL IT CAUSE OTHERS TO STUMBLE?

  It is good neither to eat flesh, nor to drink wine, nor any thing whereby thy brother stumbleth, or is offended, or is made weak.” Rom. 14:21
  What you do or what you wear, will it cause somebody to stumble? Now you might say the other fellow has to look out for himself. That is not what the Bible says. The Bible says, “It is good neither to eat flesh, nor to drink wine, nor any thing whereby thy brother stumbleth, or is offended, or is made weak.” We are responsible.

  CONCLUSION
  All of this is a matter of the heart. You might get somebody straightened out on the matter of the clothes they ought to wear and they still be just as lost as they were before you met them. Before I talk to anybody about clothes or anything else, the first thing I want to know is what about the heart? Have you been saved? Acts 15:9. Has your heart been purified by faith? Romans 10:9. Have you believed in your heart that God raised Christ from the dead? The first thing I want to know is about the heart and salvation. All that I said here tonight applies to those who are saved. If you haven’t been saved, it’s not going to help you your soul one way or the other to change your clothes. It’s not going to help at all. If Jesus does not live in your heart, that is your first need. You first have to come to Christ.

  If you are saved it is still a matter of the heart. If I were talking to a Christian about this, the first thing I would want to talk to him about would be the heart. Is your heart right with God? If your heart’s not right with God, you are not going to be able to understand any of this. You’re going to resent every argument, and resent anybody even bringing up this discussion

  Kama nilivyoandika hapo mwanzo, ni vizuri ukafuata link niliyoandika hapo juu. Naamini utapata kuelewa zaidi.

  Barikiwa!

 75. Mwanamke kuvaa mavazi yampasayo mwanamme ni dhambi vivyohivyo kwa mwanamume kuvaa mavazi yampasayo mwanamke! Paulo alisema sijui awaijie kwa fimbo ndio mtaelewa?

 76. Mimi nilitegemea zaidi tutapewa maandiko yanayoelezea vazi sahihi kuliko mtizamo wa mtu bainafsi. Tusaidieni maandiko kutoka kwenye Biblia tubadilike

 77. BWANA YESU ASIFIWE!
  UKWELI NILIKUWA NAJIONDOA KIAINA AINA KWENYE MIJADALA YA MAHALI HAPA KUTOKANA NAMNA AMBAVYO WATU TUNATOFAUTIANA JINSI TUNAVYO YATIZAMA MAMBO.
  NAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YAKO KARS SIJUI NI MDADA UA MKAKA KUIWEKA HIYO ISSUE HAPO JUU SANA SANA HAPO KWENYE FIVE KONKULUTION. KWANGU MIMI HAYA MAMBO SIYO SULULISHO UPANDE WA MAVAZI TU BALI KATIKA MAMBO YOTE TUKI ZUNGATIA HIVYO VIPENGELE TUTAKUWA TUME PONA.
  MUNGU AWABARIKI WOTE!

 78. Shalom!

  Natarajia sana wanawake wachangie zaidi katika mada hii maana wanaume tukisema sana twaweza ambiwa tunaleta mfumo-dume hadi kwenye mambo ya kiroho. . . . (sijuwi hili nalo ni swali jingine?)

  …hata hivyo mchango wangu ni kama ifuatavyo:

  Nakumbuka wanawake walipoanza kuvaa suruali katika sehemu niliyokuwa naishi ilikuwa mwanamke akipita amevaa suruali watu walikuwa wakisimama na kumwangalia kwa mshangao, vinywa wazi, kwamba kitu kama hicho kingewezekanaje! Lakini baada ya muda fulani kupita wanawake wengi wakawa wanavaa suruali na hivyo hakuna tena mtu wa kushangaa…! Watu wakazoea na kikawa kama ni kitu cha kawaida.

  Natumaini utakubaliana nami kwamba kuna wanawake wengi huvaa suruali wakiwa mijini lakini wakisafiri kwenda makwao, hasa vijijini, huficha kabisa suruali zao na wengine huziacha mjini. . . Kwa nini? Nilishawahi kusikia wengi wakisema sababu ya kutokutaka kuvaa suruali kijijini ni kwamba watu (hasa ndugu) watamuona ni muhuni! Wachache ambao huwa hawajali watu watasema nini huvaa hivyo hadi vijijini kwao. Lakini kwa sasa katika vijiji vingi vazi hili linakuwa maarufu ingawa wanawake wanaovaa huonekana kama si wa kawaida kwa namna moja au nyingine!

  Suruali zilipoingia Tanzania, kama unafuatana nami, ilikuwa ni sawa na kuikana imani kwa mwanamke aliyeokoka kuvaa. Mwanamke aliyeokoka alikuwa ‘hapati picha’ kwamba atatembeaje na suruali barabarani? (Nakumbuka hadi kuna nyimbo zilikuwa zikiimbwa kwenye makwaya kwamba watu wanapenda anasa kiasi cha wanawake kuanza kuvaa suruali). Ni nyakati hizi usingeweza kuona wanawake wamepaka midomo kwa rangi tofauti tofauti kanisani; Ni nyakati hizi ambapo usingeweza kuona wanakwaya wakiimba na kucheza kwa mtindo ambao wameiga toka bendi fulani ya muziki wa duniani (secular music); Ni nyakati hizi ambapo watu walikuwa wakikaa hadi sala ya mwisho wa ibada ndipo watoke; nk. nk. nk!………….
  ……..LAKINI ni katika nyakati hizi ambapo mtu mwenye pepo alikuwa havuki mlangoni kuingia kanisani bila kudondoshwa na ‘uwepo’ wa Mungu. Ni katika nyakati hizi watu wengi walikuwa wakitowa unabii na jumbe tofauti tofauti ‘live’ kutoka kwa Mungu kwa kumalizia ..’. . asema Bwana wa majeshi”! Ni katika nyakati hizi ambapo watu walikuwa wakiogopa kutenda maovu maana akiingia tu kanisani alikuwa akitajwa na kuambiwa atubu na kuomba rehema kwa Mungu; Ni katika nyakati hizi watu walikuwa wakiabudu na kububujika hata kama hakuna magitaa na vinanda…..nk, nk,nk!

  Hali iliendelea kubadilika. Wanawake waliookoka wakaanza kuvaa nguo zilizobana na kuingia nazo kanisani. Waliokuwa wakiwaonya walionekana kama wanataka kufuata sheria wakati huu wa neema. Hali ikaendelea hadi wakaanza kuvaa suruali, maofisini, majumbani na sasa hadi kanisani wanaingia nazo! Hakuna anayetambuwa tena kwamba hapo zamani watu walikuwa wakifunga na kuomba ‘roho’ hiyo isiingie kwenye kanisa la Mungu! Mwanzoni wachungaji walikemea lakini mafuriko ya mabadiliko na ‘kwenda na wakati’ vikawazidi. Na wengine wakaona wakikemea sana watafukuza washirika makanisani. Hivyo wakakaa kimya. Makanisa yakageuka kuwa kama sehemu ya kuonyeshana mitindo mipya ya mavazi, mitindo mipya ya utengenezaji wa nywele; huku kila aliyekuja na ‘mpya’ akitarajia neno ‘umependeza sana’ kutoka kwa wenzake…….nk; nk; nk
  ………LAKINI ni katika nyakati hizi ambapo watu wanaojipatia mali kwa udhalimu wamepewa ‘uzee’ wa kanisa (makanisa ya watu waliookoka); Ni katika nyakati hizi waovu wa kila namna ni wanakwaya na waimbaji maarufu wa injili; ni katika nyakati hizi ambapo ndoa za watu wanaojiita wameokoka zinavunjika tu kama vile za watu wasiomwamini Yesu; Ni katika nyakati hizi wachungaji wanagombea sadaka mikutanoni; Ni katika nyakati hizi ‘ujumbe’ toka kwa Mungu “live” umekuwa adimu; Ni katika nyakati hizi waimbaji wanategemea nguvu ya ‘stage shoo’ kuliko upako katika nyimbo zao; Ni katika nyakati hizi wajumbe wa shetani (agents) wanaingia makanisani na kuamuwa kuondoka wenyewe baada ya kutimiza uharibifu waliokusudia nk, nk, nk………!

  Je, ni nini kimetokea hadi mambo yakawa hivi?

  Watu waliookoka wameipenda na kuifuatisha namna ya dunia hii. Watu wa Mungu wanajiona wanyonge wasipoishi vile watu wasiomcha Mungu wanaishi. Watu wanaionea haya injili na kuuficha wokovu ndani ya mioyo na kusema ‘wokovu ni moyoni’ huku wakidhani wao watakuwa salama. Watu waliookoka wanajiona kwamba hawawezi kuupatia ulimwengu kitu chema bali wao ndio wako tayari kupokea na kuiga kila mitindo ya mavazi bila kujuwa mingi wa mitindo hiyo inabuniwa katika ulimwengu wa giza kwa ajili ya kuwanasa walimwengu. Watu waliookoka wanafikiri watawavuta watu kuja kwa Yesu kwa kufuwafuatisha wanavyoishi bila kutambuwa kwamba tofauti iliyopo kati ya ‘giza’ na ‘nuru’ ndiyo itamfanya aliyeko gizani aje kwenye nuru. Watu waliookoka wanataka Yesu akae moyoni na wakati huo huo kimwili waishi maisha ya kidunia asilimia 100…..!

  ….Mioyo yetu imetiwa ganzi. Yaliyokuwa yanatukosesha amani zamani sasa tuna amani nayo. Tumemzimisha Roho aliyekuwa akishuhudia ndani yetu. Hatuwezi kumsikiliza tena na sasa tunataka kusilizana sisi wenyewe. Na bahati mbaya sana si kila asemaye huwa anasema neno kutoka kwa Mungu. Na hata wakati mwingine tunataka watu watuambie tunayotaka kuyasikia.. . . . Kanisa linapoteza muelekeo. Watu wa Mungu tumeifuata ‘dunia’ huko iliko na kuileta kanisani na kwenye mikutano yetu.

  Uhai wa mtu aliyeokoka unategemea sana uhusiano wake na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu ana mambo mengi sana ya kumuonya mtu kujiepusha nayo hata ambayo kibinaadamu hayajafikiriwa hivyo. Kinachotakiwa ni kuisikiliza sauti ya ndani. Tunahitaji msaada wa Mungu ili kuondoa ‘ganzi’ iliyoko mioyoni mwetu. Ganzi hii ikiondoka hatutaweza kufanya chochote ambacho kinasababisha maswali na utata juu ya Imani yetu.

 79. Ni swali zuri linalohitaji maelezo marefu kidogo. Nitaweka baadhi ya changamoto za kufanya tufikiri zaidi na kulipanua zidi swali lenyewe ili watu wachangie zaidi:

  1. Vazi hili lilianza kuvaliwa na Binadamu lini?
  2. Jinsia gani ilivaa vazi hili kwanza kama vazi rasmi la jinsia hii?
  3. Ni lini na kwa nini Binadamu wanavaa mavazi mchanganyiko (cross dressing)
  4. Mungu ana msimamo Gani juu ya mavazi?
  5. Nani anatengeneza haya mavazi?
  6. Wanaotengeneza mavazi haya wana Imani gani?
  7. Wanaotengeneza mavazi hii leo wana ajenda yoyote nyuma yake?
  8. Je kuna hili suala la mavazi limo kwenye ajenda kuu ya kuurudisha ulimwnegu kule babeli ?
  9. Kwa nini uvae suruali na si nguo nyingine ambazo hazina utata?
  10. Kwa nini uvae nguo zisizo na utata wa jinsia na si suruali
  11. Watumishi wa Mungu/walokole wa kike karne zilizopita (Kabla ya mfumuko wa imani potofu mablimbali) walivaa mavazi ya aina Gani
  12. Ukigundua ukweli, upo tayari kuachana na utaratibu wako kama ni kinyume na ukweli?

  Kwa herini kwa sasa

 80. Mimi niliwahi kipindi flani kujiunga na wanamaombi flani (sitawataja). Hawa ndugu wako kiroho sana hivyo sikuwa navaa suruali wala nguo za kunibana. Sasa nkagungua kuwa hata sketi niliyovaa nliambiwa haifai. Wao wanavaa sketi pana za marinda tu! Kwa kweli swala la mavazi inabidi tuelimishane kimaandiko. Mavazi gani mwanamke na mwanamme anapaswa kuvaa? Kwanini tusivae majoho basi ili wote tujisitiri maungo yetu? Pia sisi wanawake tuliookoka kwanini tunajidhalilisha kuvaa vitop, transparent clothing, mipasuo, vimini, tight jeans? Tuchangie hii mada bila kuwa na (conflict of interests).

 81. Ni kweli maandiko yanasema mavazi ya mwanamke yasivaliwe na mwanaume na ya mwanaume yasivaliwe na mwanamke.lakini kuna suruali ambazo zimeshonwa/zimetengenezwa kike na hata mwanaume akivaa watu watashangaa, sasa vp kuhusu hizi zikivaliwa na wanawake? nafikiri hata jeans zipo za kike na za kiume,kwa kifupi nami nahitaji mtu aninasue hapa kwani huwa navaa suruali na nampenda YESU.

  MUNGU AWABARIKI.

 82. Ndg Bernard,
  Kama nimekuelewa vizuri uvaaji unategemea na jamii iliyokuzunguka. Hivyo ukienda katika jamii ambayo wanaume huvaa sketi (England) nawe utaweza kuvaa sketi? Asante kwa mchango wako.

 83. Tatizo hapa nadhani si juu ya dhambi au si dhambi ukivaa, lakini tatizo ni je, jamii kwa ujumla inakuonaje!. Kama jamii nyingine itakuona kuwa u wrong, basi ni dhambi kwa sababu unaifanya jamii ikwazike na kutokukuelewa kwa ajili ya vazi lako! Mwanamke asiyeamini ambaye havai suruali, huwezi kumhubiria akaikubali Injili yako.

  Kwa jamii ya Watanzania, mavazi ya mwanamume ni suruali na shati na mavazi ya mwanamke ni gauni au sketi na blauzi n.k. Unapokuwa mwanamume ukivaa sketi na blauzi, tayari jamii inakuona vingine, hali kadhalika na kwa mwanamke kuvaa mavazi yaliyozoeleka kuvaliwa na mwanamume jamii inakuona tofauti.

  Maandiko pia yanasema, mavazi ya mwanamke yasivaliwe na mwanamume na ya mwanamume hali kadhalika. Hapa haikutajwa iwapo ni vazi la kanzu au gauni. Roho Mtakatifu aliacha hivyo kwa kujua kuwa mavazi yanategemeana na jamii yenyewe!.

  Bwana awabariki, na huo ni mchango wangu, nionavyo mimi.

 84. Mimi nina swali, je mwanamke kuvaa suruali ni dhambi??
  Suruali ni vaji la jinsia gani? Enzi za Bwana Yesu suruali zilikuwepo? Maana naona ile sinema ya Jesus of Nazareth waigizaji wamevaa kanzu na mkanda kiunoni. Binafsi sipendi suruali za kuonyesha maungo ya mwili ila hua navaa suruali za heshima na blouse za heshima.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s