Ujumbe kutoka kwa mwl Christopher Mwakasege

Je! Umewahi kujiuliza kwa nini wakati mwingine nguvu za Mungu zinakushukia kwa uwingi halafu baada ya muda zinapungua au zinaondoka – unabaki hali kama vile hujawahi kushukiwa hata siku moja? Inawezakana umewahi kujiuliza swali hili na inawezekana hujawahi kujiuliza. Na pia inawezekana hali hii tunayoiuliza hapa juu haijawahi kukutokea. Kumbuka kuwa nguvu za Mungu zinaweza kupungua ndani yako – kwa sababu mbalimbali – ambazo ni pamoja na kutozitumia kwa kiwango kilichokusudiwa. Unakumbuka Yesu alipoulilia mji wa Yerusalemu? Alisema; “Laiti ungalijua, hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani!” (Luka 19:42). Alichokuwa anataka wajue ni kwamba ndani yake kulikuwa na nguvu au upako wa Roho Mtakatifu uletao amani. Lakini tunaona wazi ya kuwa Yerusalemu hawakutumia upako huu na amani ya Mungu ikaondoka pia. Tatizo la Yerusalemu lilikuwa ni kwa sababu hakutambua majira ya ‘kujiliwa’ kwake. Kwa lugha nyingine Yerusalemu ‘ulijiliwa’ au ulitembelewa na nguvu za Mungu ziletazo amani – lakini hawakutambua! Na kwa sababu hawakutambua hilo, kwa hiyo hata nguvu za Mungu hawakuzitambua wala kuzitumia. – Kilichotokea ni kwamba nguvu hizo (1Wakorintho 1:18,24) ziliondoka wasiweze kuzitumia.

Tunaona pia katika Yohana 1:11 ya kuwa “ Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” Yesu anaweza kuja kwako. Nguvu zake (ambazo ndizo nguvu za Roho Mtakatifu) zinaweza kuja kwako – usipozipokea itakuwa vigumu kuzitumia kwa kiwango kinachotakiwa. Maana katika mstari unaofuata wa 12, Yohana anaendelea kusema hivi: “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika …..” Ili uweze kuzipokea na kuzitumia nguvu za Mungu ipasavyo ni vizuri ujue Mungu amezituma nguvu zake kwetu kwa ajili ya nini. Zipo sababu nyingi katika biblia, lakini sisi tunataka tukupe angalau chache wakati huu ili ziwe changamoto kwako.

Sababu ya Kwanza: TUWE MASHAHIDI WAKE

Ili tuonekane na kujulikana ya kuwa sisi tu wanafunzi wa Yesu – tunachohitajika kufanya ni kupendana (Yohana 13:35). Huu ni upendo ambao watu wasiomjua huyu Mungu wetu  wanatakiwa wauone kwetu. Wakiona tunavyopendana, basi watajua ya kuwa sisi tu wanafunzi wa Yesu. Unapofanya sala ya toba na kumkaribisha Yesu katika maisha yako – unaokoka. Unaweza ukawa umeokoka lakini usiwe ‘mwanafunzi’ wa Kristo – kwa tafsiri ya Yesu juu ya nani ni mwanafunzi wake. Ikiwa umeokoka na huonyeshi upendo wa Kristo kwa waliookoka wenzako unapoteza hadhi ya kuwa mwanafunzi wa Kristo. Inapofika hali ya kuwa ‘shahidi’ inabidi upokee nguvu za Roho Mtakatifu. Yesu alisema katika kitabu cha Matendo ya Mitume 1:8 ya kuwa: “ Lakini mtapokea nguvu,; akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” Kazi ya shahidi ni kusimama upande wa anayeshitaki au anayeshitakiwa kumtetea huyo ambaye ameamua kuwa shahidi upande wake – akisema na kwa kuonyesha vithibitisho ili kusisitiza kuwa anachokitetea ndicho sahihi. Katika mazingira ya Bwana Yesu, sisi tunakuwa mashahidi kwa kusema na kuonyesha au kuthibisha kwa vitendo ya kuwa yote ambayo Yesu Kristo amesema na yamefanyika juu yake ndivyo yalivyo, na ndiyo kweli inayotakiwa kufuatwa na kila anayemtafuta Mungu wa kweli. Nguvu za Roho Mtakatifu zinatufanya tuweze kusimama katika nafasi ya kuwa mashahidi wa Kristo.

Sababu ya Pili: Kushinda Dhambi

Ndiyo! Kushinda dhambi. Unaweza kuishinda dhambi. Katika Mwanzo 4:7 tunaambiwa inatupasa au ni lazima tuishinde dhambi. Mungu hawezi kusema tuishinde dhambi kama hakuna mbinu ya sisi kuishinda dhambi. Pia, katika Warumi tunaambiwa ya kuwa dhambi haitatutawala. Lakini ni lazima tujue ya kuwa hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuishinda dhambi kwa nguvu zake mwenyewe. Kila mtu lazima ajue kuzitumainia nguvu za Mungu tunazozipata katika Roho Mtakatifu kwa sababu ya Kristo kufa msalabani kwa ajili yetu. Ndiyo maana imeandikwa hivi katika 1 Wakorintho 1:18,23,24: “ Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookokolewa ni nguvu ya Mungu …… sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.” Hiki ndicho kinachotokea unapookoka; Kristo anaingia ndani yako kwa uwezo wa Roho Mtakatifu- anakuwa nguvu ya Mungu inayokuwezesha kushinda dhambi. Kwa hiyo kama iko dhambi inayokusumbua – tubu, halafu omba Mungu akuongezee nguvu za Roho wake ili upate kushinda dhambi.

Sababu ya Tatu: Kuwa Tajiri

Jambo mojawapo lililotokea kwa mwanadamu dhambi ilipoingia ni kuishi maisha ya umaskini na kupungukiwa. Dhambi pia iliweka matabaka ya matajiri na maskini. Toka mwanzo na hata sasa na siku zote Mungu hapendi watu wake wawe maskini (kwa jinsi ya mwili) Katika 2 Wakorintho 8:9 tunasoma ya kuwa: “ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” Kwa hiyo ni mapenzi ya Mungu tuwe matajiri. Njia ambayo Mungu anatumia kutuwezesha tuwe matajiri ni kwa kutupa nguvu zake. Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu ya Torati 8:18 ya kuwa: “Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” Tunasoma hapa ya kuwa tunaweza kuomba tupate msaada wa nguvu za Mungu ili tupate utajiri halali ndani ya Kristo.

Sababu ya Nne: Kushinda hila za shetani

Tunasoma katika kitabu cha Waefeso 6:10,11 ya kuwa: “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani” Haitoshi kupokea nguvu za Roho Mtakatifu bila kuwa hodari katika kuzitumia ili upate “kuweza kuzipinga hila za shetani” Ili uwe hodari katika mchezo fulani lazima ufanye mazoezi ya kutosha ili kujifunza mbinu za kukusaidia kushinda upinzani katika mashindano. Pia, katika mambo ya rohoni ni vivyo hivyo. Ili uwe hodari katika uweza wa nguvu za Mungu – haitoshi tu kuzipokea kwa kujazwa Roho Mtakatifu. Bali ni muhimu kufanya ‘mazoezi’ sawa na neno la Mungu ili uwe hodari. Hii ndiyo maana unaweza ukajawa nguvu za Mungu na bado shetani akakushinda na hila zake. Kwa nini? Kwa sababu hujazwa hodari katika kuzitumia. Hii ni sawa na mtu kuwa na silaha yenye nguvu vitani lakini kwa sababu hajui kuitumia ipasavyo anajikuta ameshindwa vita! Nguvu za Roho Mtakatifu zipo pia kwa ajili ya kutusaidia kumshinda shetani na hila zake dhidi ya maisha yetu. Lakini ni muhimu tujue kuzitumia sawa na neno la Mungu – tuwe hodari katika uweza wa nguvu zake. La sivyo tutakuwa tunashindwa na shetani wakati tunazo nguvu za kumshinda ndani yetu.

Sababu ya Tano: Kudumu katika maombi

Kila mtu aliyeokoka ndani yake anahamu ya kufanya maombi – kuzungumza na Mungu. Lakini karibu kila mtu anajua ya kuwa kila akiomba anatamani angeweza kuomba vizuri zaidi, kuliko anavyoomba wakati huo.

Jambo hili la kuwa na upungufu katika maombi lisikushangaze. Biblia inatuambia; “…. Hatujui kuomba jinsi itupasavyo ….” (Warumi 8:26). Kazi ya Roho Mtakatifu ni kutusaidia udhaifu huu tulionao wa kuomba – ili kwa nguvu zake tuweze kuomba utupasavyo, na pia tuweze kuwaombea “watakatifu kama apendavyo Mungu” (Warumi 8:27). uzuri wa maombi si tu kwamba ni sababu ya Mungu kutupa Roho wake ili kwa msaada wa nguvu zake tuweze kuomba itupasavyo; bali maombi pia ni njia au mlango wa nguvu za Mungu kuongezeka katika maisha yetu. Ndiyo maana mara nyingi ukikaa katika maombi muda mrefu zaidi – nguvu za Mungu zinaongezeka. Lengo la nguvu hizi kuongezeka ni ili uendelee kuomba kama impendezavyo Mungu hadi upate unachoomba. Kwa mfano, kama nguvu za Mungu ni kidogo ndani yako – hasa wakati umo taabuni au katika majaribu – ni rahisi sana ‘kuzimia’ au kukata tamaa. Imeandikwa hivi: “Ukizimia siku ya taabu, nguvu zako ni chache” (Mithali 24:10) “Bali vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka, bali waowamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia” (Isaya 40:30,31) Nguvu za Mungu ndani yako zitakusaidia usizimie wala usichoke wala usikate tamaa iwe ni wakati wa raha au wakati wa taabu. Ukiona unachoka au unakata tamaa maana yake una nguvu kidogo au zimepungua – kwa hiyo omba Mungu akuongezee nguvu zake ili usichoke wala kuzimia wala kukata tamaa.

Sababu ya Sita: Kuondoa woga

Mtume Paulo aliwahi kumwandikia Timotheo maneno muhimu sana ambayo yanasema na watu wengi hata sasa aliposema; “ Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi” (2 Timotheo 1:7) Timotheo asingeandikiwa maneno haya kama hakuwa mwoga! Inaonyesha alikuwa mwoga kuichochea ‘karama ya Mungu’ iliyokuwa ndani yake! (2 Timotheo 1:6) Kama alikuwa mwoga basi hali hii ilifanya utumishi wake ulegee. Hii inawezekana ilitokea kwa sababu aliona na kushuhudia mateso aliyopata Mtume Paulo alipochochea karama ya Mungu iliyokuwa ndani yake. Kwa kuogopa kuteswa na yeye kama Mtume Paulo, aliamua kuacha kuchochea karama ya Mungu iliyokuwa ndani yake. Ndiyo maana Mtume Paulo  alimhimiza aichochee hiyo karama “….maana Mungu hakutupa roho ya woga bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi” Kama unasikia woga wa kumtumikia Mungu kwa sababu moja au nyingine hauko peke yako. Dawa yake ni nguvu za Mungu ziongezeke ndani yake- na woga huo utaondoka! Timotheo alibanwa na woga. Lakini pia Yoshua alipokuwa anakabidhiwa wajibu wa kuongoza wana wa Israeli baada ya Musa kufa – alishikwa na woga! La sivyo Mungu asingemwambia awe na moyo wa ushujaa mara tatu! (Yoshua 1:6,7,9). Yeremia naye alipokuwa anapewa wajibu wa kumtumikia Mungu akiwa bado mtoto – aliingiwa na woga! Lakini Mungu akamwambia – “Usiogope” (Yeremia 1:4-10). Kwa hiyo kama unasikia woga katika kumtumikia Mungu – omba ili Mungu akupe nguvu zake zaidi ili ziondoe woga. Jambo hili liliwahi kumtokea Mtume Petro. Pamoja na kwamba alimpenda Yesu sana na kuahidi kuwa naye kila mahali – bado woga ulimwingia alipoulizwa kama alimjua Yesu wakati Yesu amekamatwa. Lakini  baada ya kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste hatuoni tena woga ukijitokeza ndani yake – bali tunaona ujasiri mwingi.

Advertisements

206 thoughts on “Ujumbe kutoka kwa mwl Christopher Mwakasege

 1. Pingback: KUENDESHA IBADA ZENYE NGUVU | SALVATION AND LIFE EVANGELICAL MINISTRY TANZANIA-SALEMTANZANIA

 2. Mungu azidi kumwinua mtumishi wake ila ipo siku nami nitamhubiri/mtangaza kwa mataifa yote kuzidi yeye! natamani xana Amen!!

 3. nashukuru kwa somo zuri nimebarikiwa! nimeokoka nataka kumutumikia mungu lakin nitaijuaje huduma yangu?

 4. jamanie mwacheni Mungu aitwe Mungu kwakweli namshukuru Mungu kwa ajili ya mtumishi wake Christopher na Diana Mwakasege aendelee kuwatia nguvu na imani amen

 5. mtumishi wa MUNGU ubarikiwe kwa huduma uifanyayo ningependa kujua ratiba ya semina kama ipo kwa wakati huu nifahamishwe.

 6. Kwa mafundisho haya nimefunguliwa na maswali mengi pia yamejibiwa na mafundisho haya. Mungu akubariki sana.

 7. Mwl. nina swali naomba unisaidie, Ni kwa nini Mungu alianzisha biashara humu duniani?

 8. Bwana Yesu asifiwe mtumishi, napenda sana huduma zako ninaomba uniombee ili niweze kusimama imara katika wokovu wangu pia Mungu anisaidie niweze kukua katika uchumi wangu na kufanya vizuri katika masomo yangu.

 9. Shalom watumishi ninawezaje kuwa msomaji na kuweza kuwa hodari wa maandiko na jinsi ya kuyatumia?

 10. Kristo Bwana apewe sifa mwalimu…… nia yangu kuu ni kukuombea Mungu akutie nguvu katika huduma na nguvu za Mungu ziwe juu yako ili kila ukifanyacho kikapate utukufu kwa Mungu…………,

 11. Bwana Yesu asifiwe,hakika kupitia semina yenu ya Mwanza nimemuona Mungu kwa namna ya ajabu sana,hasa juu ya ujazo wa roho mtakatifu.MBARIKIWE SANA.

 12. Bwana wetu Yesu Kristo asifiwe Mwl, Christopher + Diana Mwakasege, hakika nyie ni wapakwa mafuta wa Mungu kwani huduma yenu ingekuwa imetengenezwa kwa akili na ubunifu wa kibinadamu ingeshakufa siku nyingi, ninasema hivi kwasababau nilikufahamu ningali mtoto mdogo sana miaka ya 90 na nilikuwa nikihudhuria katika semina yako usharika wa Mara Mtaa wa Moshono kwa kipindi hicho. Kwa jinsi nilivyoendelea kukua na kukusikia na kukuona pia huduma yako inazidi kuinuliwa siku hadi siku mpaka sasa ningali ni mama wa watoto wawili.

  Ninabarikiwa sana na mafundisho yako na nimemuona Mungu akinitoa sehemu
  nilipokuwapo hadi nilipo sasa kiroho na kimwili pia, hasa semini ya Juzi hapa Arusha ya kichwa kinachosema KUMCHA MUNGU KUNAVYOFUNGUA NJIA YA MAJIBU YA MAOMBI YETU, sijui kama niko sawasawa sana na hicho kichwa cha habari ila kwa somo hilo nilimuelewa vizuri na kujifunza kitu kipya japo nilipata nafasi ya kuhudhuria siku moja tu.

  Mungu wa mbinguni awape maisha marefu, akiendelea kuwafununulia maono makubwa ya shamba lako alilokukabidhi Mungu mwenyewe.

 13. Mungu atujalie kuwa washindi siku zote,kushinda dhambi,kuwa tajiri,kushinda hila za shetani,kudumu ktk maombi na kuondoa woga!!

 14. LORD OUR PEACE! MWL. MWAKASEGE NA DIANA. SINA LUGHA NZURI YA KUELEZEA HUDUMA YENU ZAIDI YA KUSEMA YESU AWATUNZE. KUTAKUA NA SEMINA LINI ARUSHA? NAFSI YANGU USIINAME KWA BWANA.

 15. Wapendwa Christopher na Diana!
  Haleluya, Mungu wetu ni mwema. Nawaombea afya njema na baraka za Bwana katika mwaka huu wa 2013, ‘Muwe hodari zaidi kupiga injili ya Kristo Yesu maana yu karibu kurudi’.Nayapenda mafundisho yenu na jinsi ambavyo Mungu anawatumia.Karibu sana Dar es salaam tunakupenda. Tell us your annual time table (Dar) please!

 16. kaza mwendo na ile nia ya kristo YESU BWANA na mwokozi wetu iliyondani yako kwani anasema duniani kuna shida nyingi jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu nanyi mtaushinda na msizimie mioyo kwani tutalipwa kwa wakati.TULITANGAZE JINA LA YESU LIVUME KWA MATAIFA KWANI KILA ULIMI UTAKIRI YA KWAMBA YESU NI BWANAAAAAAAAA! HALELUYA

 17. Mwalimu nina hofu kubwa sanaa na vita ya kidini inayoendelea . Mwalimu hawa wenzetu wanataka TZ iweje ombea hayo mapepo yao yawatoke watuachie amani yetu.

 18. Jina la bwana liinuliwe. Mchungaji nabarikiwa sana na mafundisho yako tatizo hatupati kanda zako zote ukishaondoka tunaomba utuelekeze tunapata wapi maana tunazunguka maduka yote ya kanda hawana . Tupo Moshi

 19. kweli ndugu hayo yote ambayo wasema nikweli sana kwani kushinda zambi ni nguvu ya Mungutu. Mubarikiwe sana

 20. Nimatumaini yangu kuwa hujambo wewe pamoja na familiya yako utakapo kujuwa hali yangu mimi sijambo tena wa afya njema sana.Ndugu mchungaji ninahamu kubwasana ya kuweza kufuatilia sana mafundisho yako kwanjia ya enternet.Asanteni sana Mungu awabaliki sana

 21. May the Almighty Lord give you Strength and wisdom in your Ministry,you really bless me a lot.

 22. Mungu akuzidishe,nimeweka hitaji langu Arusha tarehe 16/09/2012 niliota njozi za kuwa mtumishi wa Mungu (mhubiri)kwa zaidi ya mara 4 kwa namna tofauti nikasema Mungu sawa na yeremia 33:3 nami niko tayari.naomba mniweke mikonononi mwa Mungu na atende kwa mapenzi yake

 23. Mtumish Mungu abariki kazi za mikono yako!niombee niwe na nguvu ya maombi ndani yangu

 24. Asante Kwa Ujumbe wa Mungu Kwangu. Napenda zaidi kupata neno la Mungu, nliokoka nmerudi nyuma ila kwa uweza wa Mungu naomba aniinue tena, napenda kutembelea web yenu. Naomba maombezi yenu nifunguliwe ktk Mungu ntumike sawa na mapenz ya Mungu. Heri ktk utumishi. AMINA.

 25. Mungu asifiwe mtumishi cd za mahubiri ya mzaliwa wa kwanza nitazipata wapi jamani nazitaffuta sana naomba mnisaidie nizipate.

 26. nime penda mafundisho mungu anisaidie nifike mahali alipo kusudia mimi nifike, nawapenda wote

 27. Mungu akubariki sana kwa mafundisho. Songa mbele mtumishi wa Mungu ili Watanzania wapone, na Nchi ipone, na adui ashindwe hata kupumua.

  Mungu awabariki sana

 28. BWANA YESU ASIFIWE NAOMBA KUULIZA HUDUMA YA MANA ITAKUWEPO ARUSHA LINI NAOMBA JIBU

 29. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu namshukuru Mungu kwa kunisaidia katika maisha yangu naomba mniombee Mungu anipe upako wa kutoa sadaka.

 30. mwalimu Mwakasege niombee ili niitende vyema kazi ya Mungu aliyeziumba Mbingu na nchi niwe mtumishi mwema atakayesaidia kuueneza ufalme wa Mungu kwangu kwanza na dunia nzima naitwa Yusuph

 31. Hi binafsi namshukuru Mungu sana kipitia huduma hii kiukweli nimejengeka Mungu awabariki

 32. Mwalimu mwakasege mungu akulinde na azidi kukubariki na kukutumia kwa ajili ya kufunguliwa watu wake kwenye vifungo vya shetani na kupokea uponyaji, nakupenda sana maana nikisikia jinsi mungu anakutumia ukiwa unahubiri nabarikiwa sana, Natamani ningekuwa naenda na ww kila unapokwenda kwa ajili ya semina na mikutano ya Neno la Mungu ili nisikose kila kitu unachopewa na mungu lakini nashindwa kwa ajili ya uwingi wa mambo, Lakini nakuombea sana MUNGU AKUBARIKI WW MKEO NA FAMILIA YAKO KWA UJUMLA NA WOTE WANAO SHIRIKIAN NA WW KWA AJILI YA KUTANGAZA INJILI YA YESU, AMEN.

 33. Jina la Bwana Yesu liinuliwe juu,Mungu akupe afya njema Mwl Mwakasege pamoja na mke wako,ninapata faraja sana ninapo ingia kwenye hii website.

 34. Remain blessed as through the word of God people are changing their evil deeds. karibu Dodoma.

 35. Nashukuru sana mtumishi wa Mungu Mwalimu Mwakasege namouomba mwenyezi Mungu aendelee kukujaalia na akupe nguvu ktk maisha yako yote

 36. MUNGU AWABARIKI WATUMISHI WANAOTUMIKA PAMOJA NA MWL MWAKASEGE KWA KWELI NABARIKIWA SANA NAWAOMBEA MZIDI KUSONGA MBELE

 37. Ni kweli watumishi wa Mungu KTK NCHI HII TUNAHITAJI NGUVU ZA MUNGU SANA, KWASABABU SHETANI NATUMIANGUVUNYNGI SANA KURIHARIBU KANISA. MWALIMU! MUNGU NA UKUTIE NGUVU KATK KUUJENGA MWILI WA KRISTO.

 38. DOTTO MALIMA.
  Mungu abariki huduma yenu na kuwalinda na kuwapa siku nyingi ili neno la Bwana lisambae duniani kote amen.

 39. Somo zuri sana ila naomba Mwl Mwakasege atufundishe juu ya ubatizo maana mambo mengi sana yananenwa juu yake juu ya ubatizo wa maji,sasa ingekuwa vema tungesikia kutoka kwake.

 40. Nimebarikiwa sana na semina ya diamond Jubilee jana tarehe 29th January 2012, sadaka inavyompa nafasi Mungu ya kuhusikia na maisha yako ya baadaye, ninamshukuru Mungu kunipa nafasi ya kuhudhuria na kupata kile alichoweka ndani ya mtumishi wake kwa ajili ya watu wake. Mungu alikuwa alisema nami hivi vitu lakini nilikuwa sielewi na kuingia katika mashaka na kusitasita, Nilipewa wazo la ubunifu katika biashara sekta ya fedha mwaka 2009 ambalo nilitakiwa kuliendeleza mpaka kufika kuwa Kammuni ya bima za kiuchumi, kifedha na kibiashara, na ndani yangu nikasikia msukumo wa kutoa sadaka na Roho mtakatifu alinisemesha kiwango cha sadaka, lakini sikufanya hivyo, mwaka 2011 Mungu alikuwa akinionyesha future yangu ya baadaye na familia yangu na ndani yangu nikasikia msukumo mkubwa wa kutoa sadaka, na nikiambiwa niachile sadaka kwa ajili ya wayahudi, taifa la Israel au jews walioko katika taifa la India na Ethiopia hasa katika taasisi ya Kiisrael zinazohusika nao, lakini sikufanya hivyo, kwa kweli ninalia na kuomba toba kwasababu moyo wangu ulikuwa mgumu,

 41. ATUKUZWE MUNGU JUU MBUNGUNI YEYE AWEZAE KUTENDA MAMBO MAKUU KULIKO HAYA TUYAOMBAYO NA TUYAWAZAYO NANI KAMAYESU NAULIZA MIMI
  MAY THE ALL MIGHT GOD IN HEAVEN BLESS HIS SERVANT MWL MWAKASEGE WE REAL LOVE HIM AND HIS WIFE GOD BLESS YOU YOU ARE HELPING US TO SEE THE WAY OUT IN THE NAME OF JESUS MAY GOD REMEMBER YOU IN HIS KINGDOM NOW AND THEN

 42. Nimesoma ujumbe wa mtumishi wa MUNGU,nimejifunza jambo,hakika wana wa Mungu wengi hawajui kuzitumia nguvu za Roho Mtakatifu kikamilifu!kupitia ujumbe huu napiga hatua sasa,na wengine nitawajulisha huu upendo Yesu kwetu.

 43. BWANA YESU ASIFIWE MWALIMU! Nasisitiza kuhusu kujua ratiba ya Mwl kwa mwaka 2012,huku Dodoma tuna kiu sana ya neno.Mungu akubariki

 44. BWANA YESU ASIFIWE? MWALIMU TUNA KIU YA NENO LA MUNGU HIVO TWAWEZE PATA RATIBA YAKO YA MWAKA 2012? HERI YA MWAKA MPYA SIFA NA UTUKUFU APEWE MUNGU PEKE YAKE YEYE ALIYETUWEZESHA KUFIKA LEO,.

 45. Blessed are the people who devote themselves to preach the gospel of living jesus.mwl Christopher Mwakasege and his beloved wife Diana are excellent spiritual teachers,their messeges are evalasting,non-contradictory to world religious,and people of different religions get attracted to your teaching.The reason for this is obvious-because Jesus is with you.Work tiredless,God bless you.

 46. Bwana Yesu Asifiwe mtumishi, nimebarikiwa sana na somo la nguvu za Mungu, hasa kwenye kipengele cha maombi. Mungu mwenyezi, aliyekufunulia haya yote, azidi kukufunulia na mengine, ili tuzidi kupona. Amen.

 47. thank you too, kwa nini tunatoa fungu la kumi? naomba msaada wako ili nipate kuelewa zaidi juu ya jambo hili. I from sokine university of agriculture mororgoro Tanzania.

 48. ninabarikiwa sana na NENO LA MUNGU kwa kupitia kwa mtumishi wake Mwl.Christopher Mwakasege.But katika suala la mahusiano ya kijana kujiandaa kupata mwenzi wa maisha,au uchumba na ndoa ndipo ambapo nasubiria kwa shauku kubwa Mwl. aweze kutulisha.

 49. Bwana Yesu asifiwe sana Mwalimu. Tunamwomba Mungu azidi kukupa uhai siku zote ili na watu wa Manyara tukumbukwe siku moja kwa wewe kuja hapa kutufundisha nNeno la Mungu. Mungu akubariki sana mwalimu

 50. Mungu akubariki sana mtumishi wa mungu maana nabarikiwa sana na mahubiri yako.

 51. Namshukuru MUNGU Baba wa mbinguni kwa kumpa neno MWAL CHRISTOPHER kuhusu malango NENO hili nililipata ktk baadhi ya vitabu vyake lakini ninhitaji vido yake. MUNGU AENDELEA KUMPA NENO ZAIDI.

 52. Tudumu katika kuwaombea watumishi wapendwa. Mwl Mwakasege ubarikiwe sana unatumika kama chombo na sisi tumepokea yenye kutujenga. Ubarikiwe kwa somo nzuri la Umuhimu wa kuomba kwa muda mrefu na faida zake.

 53. Mtumishi Mwakasege hongera sana kwa kazi hii nzito unayoifanya.
  mimi ninaomba maombi yako kwani familia ya mume wangu wanasumbuliwa na ugonjwa wa sukari. Mume wangu ni mmoja kati yao ambaye ansumbuliwa na ugonjwa huu wa sukari. nimeomba ni muda mrefu sasa lakini bado hajapona. naamini Mungu atamponya siku moja ni lini sijui ila naomba maombi yako ili apone kwani kila kikicha ni dawa kama mme wangu naumia sana rohoni. NAOMBA MAOMBI YAKO. AMEN.

 54. Bwana apewe sifa.Huduma ya mwl.Mwakasenge, inafundisha , inabariki na inaponya. Lakini pia ni vizuri kuwapima watumishi wengine. Wapo ambao ni Freemasons ambao wamejiingiza makanisani kuuharibu ukristo.
  Wapo ambao wanafanana na Kibwetere aliyewatapeli waumini wake wakauza kila kitu na kupeleka kwake, akiwadanganya kuwa mwisho wa dunia umefika. Baadaye aliwahamasisha wakaja kanisani. aliwachoma moto wote akiwa amewafungia kanisani, wote waliteketea, yeye alikimbia hadi leo hajulikani alipo.
  Karibu kwa Yesu wa kweli, acha kutangatanga. Acha kukimbilia tiba ya vikombe ambazo hujui siri yake.
  Pata Kitabu changu ” KIKOMBE CHA BABU na Freemasons” kitakufungua macho na kuijua Freemasons na tiba za vikombe.
  Asante

 55. Bwana Yesu apewe sifa. Huduma ya mwl. Mwakasege nina ikubali, ni huduma njema. Inabariki, inaponya na inaokoa. Tuwapime na watumishi wengine kwani kuna watumishi makanisani ni wafuasi wa Freemasons. Wamejiingiza kwa hila kutaka kuiharibu huduma ya Mungu.
  Mfano ni Kibwetere wa Uganda, aliwadanganya waumini wake kuwa mwisho wa dunia umekaribia, hivyo wauze magari, nyumba, mashamba na vitu vingine vyote na hela zote wampelekee yeye kwani mbinguni hakuna kwenda na mali. Waumini kwa uaminifu wakafanya hivyo, baadaye Kibwetere akijua kuwa ni uomgo aliwaalika kwenye mkesha. Walipokuwa wakimngojea Yesu alifunga milango yote akawamiminia mafuta ya petroli akidai ni mafuta ya baraka, baadaye akatoka nje na kufunga mlango kwa nje. Alichukua kiberiti na kuwasha, akawarushia moto, wote waliteketea.
  Kibwetere akakimbia hadi leo hajulikani aliko, hivyo tuwapime watumishi wetu kama ni kweli wameitwa au ni kwa ajili ya matumbo yao na fedha za aibu.
  Nakuomba, pata kitabu changu cha KIKOMBE CHA BABU na Freemasons, utapokea mafundisho ya kiroho. Usiufuate mwili, mfuate Yesu. Epuka pia Tiba za vikombe, huko ni kutapeliwa kwa fedha kwa imani.

 56. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa MUngu namshukuru Mungu kwa ajili sio tu kwasababu umekua baraka kwangu ila umekua mlango mkubwa sana kwa watanzania na Afrika mashariki nzima maneno yako kutoka madhabahuni kwa Mungu yamekua barakka sana na msaada kwetu tangu nilipopata kibali cha kusikia na kuelewa maneno yako mwaka 2007 sijaacha hata leo nilisha qahi kusikia ushuhuda kwa masikio yangu kwa mtu morogoro aliye kutana a Mungu kupitia wewe hakua na mpango wa kuja katika semina yako lakini alitumwa na mama yake mjini kwa bahati nzuri akapita hapo kwenye semina yako akajisikia kukaa kidogo ndipo ulipoanza kutoa unabii wa mambo yake mpaka akashuhudia nguvu za Mungu zkimshukia kwa nguvu sana usiku sa tatu alikua ni mtu mbishi sana kwa habari za Mungu lakini sasa hivi ni tofauti sana, Mungu akuzidishie nguvu zake ili mizigo uliyo beba kwa ajili ya Tanzania ikazaliwe na Mungu akatukuzwe kupitia kazi yako…. ubarikiwe pamoja na watu wa mlango wako ..karibu sana IRINGA tar 2

 57. BWANA YESU APEWE SIFA:…………… NAPENDA KWELI MAHUBIRI YA MWL. MWAKASEGE, NAOMBA KUULIZA ATAKUJA LINI TENA DAR. HALELUYA………

 58. Bwana asifiwe
  Nashukuru kwa kwa neno limenitia nguvu na kunisogeza karibu na Mungu

  Ubarikiwe

 59. OH HALLELUJAH man of God
  I real thank God for the miraculous power that Holly Spirit perform through your ministry may God cause you to move in a very higher level in Jesus Name
  Amen

 60. ANNA EMMANUEL / Sunday, October 9, 2011
  Praise the LORD Man of the Most highest GOD
  Namshukuru sana Mungu kwa ajili yako kuwa tayari kuleta ujumbe wa Mungu katika majira yake, binafsi nimebarikiwa sana na haya masomo ambayo ni muhimu sana kwa mkristo kuyajua
  Yesu akufunike kwa nguvu zake na kukuinua kiwango kile atakacho yeye Roho Mtakatifu kikifikia

  Nabarikiwa sana na nimekuwa katika kiwango kingine na si kama nilivyo kuwa
  Ubarikiwe sana Mtumishi, mwalimu, kocha Mwakasege

 61. Wapendwa ktk Bwana Tumuombe MUNGU atusaidie tuwe waatendaji wa neno la Mungu kwa sababu mafundisho ya neno ka Mungu tunayofundishwa na mtumishi wa mungu mwakasege hayatatusaidia iwapo hatutayafanyia kazi.Mungu awabariki.

 62. .Mwl mwakasege MUNGU Akubarik kazi yako ni njema.na zaidi ya yote akusaidie ROHO YAKO IISHI MILELE.

 63. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu, mwalimu tuliyepewa katika wakati na majira haya. Naomba Roho Mfariji awe pamoja nawe katika kipindi hiki ambapo anahitaji kuendelea kukutumia na habari ya baba yako mpendwa kulala katika uzee wake katika Jina la Yesu Amina.
  Ni mara ya kwanza ninasoma website hii na nimebarikiwa sana, na asante Mungu wetu aliye hai imetupa kibali cha semina hii inayoendelea biafra-DSM iliyoanza tarehe 04/Sep/2011. Bila mashaka Mungu ametupendelea sana kwa sababu sioni kama tulistahili hii neema.
  Kwa kile ambacho nimejifunza ni kwamba kutumika ndani ya Agano la Mungu ni zaidi ya Wokovu ingawa Wokovu imekuwa ni karama ya kwanza kuipata, ninachoona ni kwamba unaweza ukaokoka (kupata wokovu) na hapohapo ukatumika hapa ulimwenguni nje ya Agano la Mungu na ikawa ni hasara kubwa kwa ufalme wa Mungu. Nasema hivyo kwa sababu sioni kwamba Adamu hakuwa Mpakwa mafuta wa Bwana kama wengi wanavyoweza kufikiria hata kukiri, vivyo hivyo kwa Ibrahim, Yusufu na wengine wote unaoweza kuwaona ndani ya Biblia Takatifu maana huko ndiko tunakopata hazina hii. ( NB: kumbuka hata leo wapakwa mafuta wapo.)
  Tunahitaji kumtafuta sana Mungu kwa Neno lake Takatifu maana ndimo anapooneka / anaposhuhudiwa Yohana 5:37,39. Yeye atatugemeza na kuhakikisha ya kwamba tunafika kwake tukiwa tumetimiza yale aliyokusudia tuyafanye tukiwa hapa duniani sawa sawa na Madhabahu yake Takatifu ya Mbinguni.
  Ndugu unayesoma naomba tuelewe ya kwamba Mungu ana makusudi ya kutuleta hapa duniani,na anataka makusudi haya yatimie na hatimaye aachilie tuzo kwa yule atakayekuwa tayari. Na kumbuka amesema tawi la mzabibu lisilozaa(lisilotimiza mapenzi yake) atalikata.
  Maana yake ni nini basi? ni kwamba makusudi ya Bwana Mungu ni lazima yatimizwe. Na kama hautatimiza atakukata na kuinua tawi jingine litakalokaa katika nafasi. HALELLUYA

  Mungu akubariki sana Mtumishi wa MUNGU.

 64. Ujumbe mzuri sana nimebarikiwa, Mungu akulinde na akuzidishie busara

 65. MUNGU NA AKUBARIKI SANA KWA KAZI YA MUNGU. KILA SILAHA ITAKAYOINUKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA.

 66. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu, ubarikiwe na Bwana, mafundisho yako yananibariki sana.by c.ernest

 67. Bwana yesu asifiwe mwalimu mwakasege pole sana kwa kufiwa na baba yako mungu akutie nguvu uwe na amani

 68. Mungu ambariki mtumishi wake mwalimu Mwakasege aishi miaka mingi duniani. Nimebarikiwa na hii website na blog kwa ujumla. Amen

 69. Bwana Yesu asifiwe Mwl Christopher !Nabarikiwa sana kwa huduma zako naomba kujua ni lini utakuja dar kwa mwaka huu.

 70. Ninabarikiwa sana na huduma aliyoiweka Bwana wetu Yesu Kristo ndani yako, Bwana azidi kukutumia, akulinde wewe na familia yako, kuwe na amani na mafanikio mema, na aliyoyaanza Bwana ayakamilishe na kukupa taji ya uzima wa milele. ninaomba mafundisho zaidi kwa njia ya email. stay blessed.

 71. Bwana Yesu Asifiwe sana mtumishi wa Mungu,
  Nimebarikiwa sana na mafundisho yako na jinsi Roho mtakatifu anavyozidi kukutumia ili utupatie ujumbe wa neno la Mungu.
  Please email me your official website so that i may be able to learn more the word of God and share with others.May the Lord continue to use you mighty.
  Judith

 72. Jamani Mwalimu Mwakasege nimesikia mwaka huu utakuja Shinyanga pia baada ya kutoka Mwanza. Kindly and Kindly we need upako na huku tunaomba uje please!!

  Dolorosa

 73. Mwakasege na Diana,Mungu awalinde katika huduma yenu.Nabarikiwa sana na mafundisho yenu.Namshukuru Mungu kwaajili yenu,Na ya barikiwe matumbo yaliyo wazaa.Na wabarikiwe wanaosikiliza na kutenda neno la Mungu mfundishalo!

 74. Mtumishi Mwakasege hongera kwa kazi ya Bwana unayoifanya. Kwa umeshuhudia Watanzania na walimwengu wanavyotabika kimwili na kiroho kazi yako ni njema sana. Wanaofikiri unajiinua au kujikweza pengine wana mawazo ya juu juu hawafahamu kwa undani juu ya utumishi wako. Lakini mtumishi mimi leo nina swali moja kwamba kwa nini Tanzania yetu inapita katika kipindi hiki cha watu kutuhumiwa mambo mbali mbali ya ufisadi na rushwa wakati watumishi wa Bwana mkikesha kuiombea na kuitakia mema mchi yetu. Ni nini maana ya mambo haya yanayotokea Tanzania?

 75. Tumsifu Yesu Kristu,huduma y a Mwal.Mwakasege inanibariki na kunijenga katika kuishi maisha ya ushindi ndani ya KRISTU! MUNGU aendelee kukutumia katika kueneza habari njema kwa watu wote wapate kuokoka.Amin

 76. Ni dhahiri kuwa Mwl Christophe Mwakasege ndiye mwalimu halisi wa kanisa hai la Tanzania na Afrika ya mashariki.
  Mungu akuinue kwa ziada ili maono uliyonayo yalisaidie kanisa hai la Mungu kuimarika na kumtukuza yeye katika kicho cha Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wetu sote.
  Amin

 77. Bwana Yesu asifiwe Mwl Christopher !Nabarikiwa sana kwa huduma zako naomba Mungu aendelee kukutia nguvu Ubarikiwe mtumishi

 78. Bwana Yesu asifiwe, Amani iwe nasi. Mwl Mwakasege naomba utombee katika familia yetu kuna pepo linaitikisa familia yetu umoja, upendo na ushirikiano unaregarega. Pia niombee mimi na mme wangu na mtoto wetu tufunuliwe neema ya bwana ili tuuone utukufu wa Bwana. Kwa Yesu kuna raha. Amen

 79. Nawashukuru kwa wote mliotangulia kwenye maoni haya mimi naomba kwa yeyote atakayesoma maoni haya aniombee niweze kupona ugonjwa wa kisukari kwa kweli unanitesa muno kila siku naukataa kwa Jina la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazaleth na naamini Mungu aliponiumba sikuwa na ugonjwa huo hivyo ninavyoishi sitaki niwe nao.

 80. asante Yesu kwa neema uliyotupa through mwl mwakasege.ila mwl naomba msaada wako wa maombi nimemaliza chuo since 2006 Accounts but realy sifanikiwi kazi.napata tu kazi za shida shida tu.and now since last year sept sina kazi till now.mtumishi naomba maombi yako nipate neema ya kazi nateseka.

  also mwl hivi is it possible kupata mafundisho through mails? bce nisamehe ila nina ugonjwa wa kusahau now nakuta nabarikiwa mno with your mafundisho ila ninasahau even if i wrote down.bye baba,Mungu azidi kukutumia tupate neema.

 81. Shalom
  Napenda kuwasalimu kwajina la bwana Yesu aliye Hai
  mimi ni mwanafunzi wa chuo cha biashara Dodoma nina mshukuru mungu kwa kuniongoza katika masomo yangu na maisha yangu kwa ujumla. Naomba mniombee ninaingia kwenye kipindi cha mitihani ya kumaliza semister.amina

 82. Bwana yesu asiwe.mwalimu naomba uniombee mimi na familia maana katika familia yetu tuko watano na dada yangu alimaliza form four na akafelizi na alirisiti na akafeli na mimi pia nimemaliza form mwaka 2010 na nikapata division 3 ya ishirini na tano na sikuweza kupata credit zote tatu hata ningeenda shule za private nikasome.kwani nilipata credit mbili.kwa mwalimu mimi ninarisiti mwaka huu hili nipate credit moja hili na mimi niendelee na form five na pia namuomba Mungu anitimizie malengo yangu.Mwalimu naomba uniombe jambo hili lisitokee katika familia yangu tena na maisha yangu ya baadaye na pia nina mdogo wangu ambaye yuko form 3 Katika shule ya arusha sec

 83. Namshukuru Mungu kwa ajili yako baba na mama mwakassege nawapenda sana kwani mafundisho yenu yamenisogeza hatua,nawatakia maisha marefu mno katika mapenzi ya mungu

 84. Ubarikiwe mwalimu mwakasege kwa mafundisho mazuri hakika yamenifungua kwa kiasi kikubwa.naamini mungu anapitia kila hitaji la moyo wangu na wakati ukifika atanijibu

 85. Bwana Yesu asifiwe!mtumishi,mungu azdi kukubariki&kukutia nguvu,kuptia mafundisho&maombi yako tangu nikiwa mkoani Tabora{Milambo High School}2008.nimezdi kuuona uweza&baraka za mungu juu ya maisha yngu.Kwa sasa npo UDSM na nnazid kukuombea mungu akutie nguvu katika kuitenda kaz yake,aaamen!

 86. Tunamshukuru Mungu kwa kukupa kibali kufungua ofisi Dar es salaam,naamini itakuwa msaada kwa wengi watakaohitaji vitabu cd au ushari,kuliko ilivyokuwa kabla kusubiri mpaka wakati wa semina,Mungu azidi kukutia nguvu.

 87. Tunaomba mwalimu Mwakasege atoe tamko kuhusu uponyaji wa Kikombe cha Mchungaji Ambilikile! Kama mwalimu wa Maandiko anaweza kusaidia wengi baada ya wapendwa kuwekwa njia panda! Hasa Manabii na mitume wa Bwana walioko Tanzania kutofautiana!Kuhusu huyu “mtumishi wa Bwana” aliyesimama kwa zamu yake Tanzania, Nakufanya kila mwamini kusema kama aonavyo vyema machoni pake!We need guidance at this critical hour!

 88. Bwana Yesu asifiwe, mm ni msichana mwenye umri wa miaka 30 sijaolewa bado nahitaji kuolewa but kila nikipata mchumba itatokea sababu tuachane nilipofanya research nikaambiwa kwamba kwetu shangazi yangu ana mzimu huwa kama hataki mtu aolewe akikupa hutoolewa mpaka maisha yako yote nilipogundua hivyo nikawa najiombea na nikawa nawashirikisha watumishi wengine but nakosa muda wa kuuzuria kwenye vipindi vya deliverence coz muda mwingi nakuwa kazini. naomba mtumishi wa Mungu Mwakasege unisaidie kuniweka katika maombi wakati unaombea watu wengine kusudi nguvu za giza hizi zinitoke.

 89. Bw.Yesu asifiwe,mwalimu nahitaji maombi nimemaliza chuo mwaka 2009 mpaka leo sijapata kazi.

 90. Bwana Yesu asifiwe sana wapendwa naomba unifanyie maombi juu ya watoto wangu ili wafanye vizuri katika masomo yao. nina watoto wawili wa kike na wakiume lkn katika mitihaniyao hawafanyi vizuri kwa sasa wanasubiri majibu ya mitihani yao mmoja kitado cha nne na mwingine kitado cha 2 kwenda cha tatu.
  mimi mwenyewe nahitaji maombi kwa ajili ya kuwalea watoto hao na riziki kwa aj il ya familia nzima

 91. Bwana Yesu asifiwe, naomba nikujibu ndugu Dickson kwamba mimi naamini ratiba ya mtumishi kwamba aende wapi inaongozwa na roho mtakatifu na si kama apendavyo yeye.Hivyo kama unataka aje huko mikoa ya kusini inabidi mkae kwenye maombi kumsihi mwenye kutoa kibali ili amwongoze kuja huko.amen

 92. NAOMBA UNISAIDIE, KWA NINI MWALIMU MWAKASEGE HAJI MIKOA YA KUSINI KAMA HUKU KWETU MTWARA?

 93. MUNGU akujalie nguvu za kusonga mbele ili kulikomboa taifa la Tanzania liweze kutoka katika mfumo wa maisha ambao shetani amelipangia Kazi yenu si bure watumishi wa MUNGU,Kila mmoja akikaa kwenye nafasi yake ANAWEZA KUWA KAMA MUNGU ATAKVYO AWE!!

 94. naomba kuombewa kwa sababu nimekuwa mvivu wa kuomba
  tuna muomba mwl aongeze vipidi kwenye redio sauti ya injili

 95. Bwana Yesu asifiwe, Mwl. naomba niweke katika maombi yako ipate neema zake yeye aliye Mtakatifu na mwaminifu.

 96. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI WA MUNGU ,na mshukuru yesu jinsi alivyonionekea katika masomo yangu ya form six na sasa nipo chuo kikuu sua na nazidi kumwona mungu alivyo jibu mahitaji yangu katika semina ya arusha kwani ktk semina ile nilimwomba mungu atupe umeme nyumbani na baada ya semina mungu alifanya.MUNGU AZIDI KUKUTIA NGUVU KATIKA HUDUMA

 97. BWANA YESU ASIFIWE,
  Asante Mwl Mwakasege kwa mahubiri yako mazuri MWANA AKUBARIKI SANA NA JINA LA BWANA LITUKUZWE MILELE.

 98. Shalom mtumishi wa Mungu!Mungu akubariki sana kwa kazi unayoifanya ya kuwahubiria watu kweli ya Mungu. Hivi mtumishi wa Mungu nikitaka kunena kwa lugha nifanyaje?

 99. Bwana asifiwe nimebarikiwa sana na mafundisho haya ya mwalim mwakasege ni mmoja waalim naopenda sana kuwasikiliza ingawa niko mbali na tanzania ila nayapata kwa net huku india Bwana asifiwe sana

 100. for real God has create something unique in your servises
  still we are praying for you so that God give u strength ot spread his holly name whole over the world
  be blessed the servant of GOD

 101. the way nilivyoelewa mimi!!

  ni kwamba waweza kuwa umeokoka lakini ukawa nje ya agano. kwamba unamtumikia Mungu lakini si kama alivyopanga yeye. kwa mfano mtumishi ameitwa kuwa mwalimu wa neno lakini akajipa uaskofu na kufungua makanisa, watu wataokoka, watafunguliwa, lakini askofu huyo atakuwa nje ya agano kwani Mungu amemwita kuwa Mwalimu.KUWA NJE YA AGANO SI KWAMBA HUJAOKOKA WAWEZA KUWA UMEOKOKA LAKINI STILL UKO NJE YA AGANO. hata Israel walimwabudu Mungu wao wakati wako Misri wa lakini nje ya agano.

 102. Ndg Paul Holella,

  Nashukuru kwa maoni yako juu ya kile nilichoandika nikimshauri dada Salome.

  Jambo mojawapo nililosikia kwenye mafundisho hayo kuhusiana na AGANO ni kwamba kuna uwezekano mtu ALIYEOKOKA akawa anatumika NJE YA AGANO. Sasa sifahamu kama mtu aliyeokoka anapotumika nje ya Agano anaweza kupata matatizo/mapito sawa sawa na ya mtu ambaye hajaokoka!

  Dada Salome alipoandika ameandika pasipo kuweka wazi kwamba ndugu zake hao nao wameokoka. Kwa hiyo mimi nilipoandika nimeandika kuanzia katika msingi, kwa kuwa pia naamni baraka na mfanikio yoyote ya ki-Mungu msingi wake ni WOKOVU. Vile vile nilisema kwamba kama ‘wote wameokoka’ wanaweza kukaa chini wakazungumza kwa pamoja katika mtazamo wa Wokovu, kama watoto wa Mungu. Ninaamini katika kuzungumza huko wanaweza kupata mengi zaidi kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi matatizo yanayowakabili.

  Hata hivyo nilichoandika nimeandika kutokana na kile ninachojua katika kumshauri dada yetu aliyeomba msaada. Kwa hiyo kama kuna ZAIDI ya niliyoandika au kama kuna marekebisho USISITE kufanya hivyo, ili dada yetu Salome na wengine wenye uhitaji kama wa kwake wapate KITU CHA KUWASAIDIA!

  Baraka kwako!

 103. Shalom,
  ndg John nadhani Mwalim Mwakasege alivyokua akiongelea agano aliamaanisha zaidi ya wokovu….. jaribu kurudia hilo somo lakini tafakari sana juu ya “AGANO” …..
  Ubarikiwe

 104. Dada Salome,

  Nami pia nimebahatika kulisikia somo hilo la Mzaliwa wa Kwanza, ingawa si lote.

  Mimi nina haya yafuatayo kuhusiana na kile unachoomba msaada/ushauri

  Kipengere muhimu katika somo hilo, Kutokana na Mwalimu Mwakasege, ni kile kinachosema KUTUMIKA NDANI NA NJE YA AGANO. Nilivyoelewa mimi hapo ndipo pamebeba ujumbe wote wa somo hilo. Kwa kufupisha niseme moja kwa moja kwamba Kutumika nje ya Agano ni pale mtu anapoishi lakini ni nje ya Kusudi la Mungu. Kuwa nje ya kusudi la Mungu ni kuwa nje ya Wokovu. Mtu ambaye hajaokoka hawezi kumtumikia Mungu, kwa kuwa yupo chini ya uongozi mwingine. Anatumikia miungu wengine. Ndiyo maana mtu huyu akija kwa Mungu, Yehova, ni lazima ku-reset mambo yote. Mambo yote aliyokuwa anafanya kule, yote yanafutika. Anaanza moja!

  Katika kuelezea hili Mwalimu Mwakasege alitoa mfano wa Wana wa Israel kule Misri. Baada ya kukaa kule kwa miaka 430, siku Mungu anawatoa kule, aliwaambia kwamba Mwezi huo [walioondoka Misri] ndiyo utakuwa mwezi wa kwanza wa Mwaka kwao. [Kutoka 12:2]. Yaani miaka ile 430 ilikuwa imefutika na hivyo wakaanza hesabu upya. Sababu yenyewe ni kwamba wakiwa kule Misri walikuwa wanamtumikia Farao na si Mungu Yehova. WALIKUWA WANATUMIKA NJE YA AGANO.

  Kutumika nje ya agano, kama Waisrael kule Misri, kuna tabu na shida za aina mbali mbali. Waliteswa, walitumikishwa na wala haikuwa kwa faida yao, bali kwa faida ya waliowatumikia. Kutumika nje ya Agano la Mungu hakuna faida kwa anayetumikishwa. Bali kutumika ndani ya Agano la Mungu kuna faida kubwa, toka kwa Mungu mwenyewe,kwa kuwa Mungu ndiye Baba Yetu.

  Sasa, mtu ambaye hajaokoka, huyo hayuko ndani ya Agano la Mungu. Huyo yuko nje ya Agano la Mungu. Huyo hutumikia miungu wengine, ambao hawawezi kumlipa faida yoyoye yeye wanayemtumikisha. Kumtumikia shetani hakuna faida yoyote. Ni hasara tu. Maana yeye hana Uzima. Hana Amani. Hana Furaha. Yeye ni mkuu wa Mauti. Wako watu wanaoonekana kama wana FAIDIKA sana kwa kule kuwepo nje ya Wokovu. Lakini kumbe kadri wanavyoendelea kukaa nje ya Wokovu ndivyo wanavyoendelea kukijaza kikombe cha mateso.

  Lakini pia kutumika nje ya Wokovu hakuna furaha ya kweli. Hakuna Amani. Hakuna pumziko moyoni. Mtu aliye nje ya wokovu, japo anaweza akaonekana hana mzigo mabegani lakini moyoni mwake kuna mzigo Mzito.

  Hivyo, hao ndugu zako ambao unaona wana tatizo linalohusiana na mzaliwa wa kwanza, ni vema sana ukaangalia kama tatizo hilo linatokana na sababu gani. Je, wako Ndani ya Agano [wameokoka] au Wako nje ya Agano [hawajaokoka]? Kama wako ndani ya Agano hilo ni suala jingine linalohitaji maelezo yake kuhusiana na tatizo walilonalo. Lakini kama Wako nje ya Agano, kinachotakiwa ni KUINGIA NDANI YA AGANO. Waingie ndani ya Agano ili waanze kutumika na kumuishia Mungu.

  Kuingia ndani ya Agano siyo lazima kwa mtu. Mtu halazimishwi kuokoka. Lakini mtu hushauriwa, huelezwa faida za kuokoka na hasara za kutokuokoka. Kwa hali ya kawaida hakuna hasara ya kuokoka, bali mwenye kuona hasara ya kuokoka ni shetani maana yeye ndiye huwa anapoteza watumishi. Lakini mtu kama mtu kibinafsi hana hasara ya kuokoka. Ndiyo maana mtu akiokoka hawezi kamwe kujutia wokovu. La msingi ni kujifunza Neno la Mungu kikamilifu ili kutambua nafasi yake, kama mtoto wa Mungu.

  Kwa hiyo ninachokushauri mimi ni kwamba kwanza jiangalie wewe mwenyewe. Kama uko ndani ya Wokovu huo ndiyo mtaji wako. Halafu angalia na ndugu zako. Kama Wako kwenye wokovu, kaeni chini mjadiliane katika mtazamo wa Wokovu, kama watoto wa Mungu. Lakini kama hawako ndani ya wokovu unachotakiwa kufanya ni kuwaelewesha jinsi wanavyotumika nje ya Agano- yaani nje ya kusudi la Mungu. Sasa tatizo linaloweza kuwepo ni KAMA WEWE MWENYEWE HAUKO NDANI YA AGANO. Lakini ufumbuzi wa tatizo hilo [ambalo linaweza kuwepo kama wewe mwenyewe hujaokoka] ni wewe mwenyewe KUINGIA NDANI YA AGANO NA MUNGU – Ni kuokoka!

  Mtu aliye nje ya wokovu anaweza akaombewa na tatizo lililopo likaondoka. Lakini huyu hawezi kuwa salama kama hajaingia kwenye wokovu. Ni rahisi sana kwa matatizo kurudi, tena pengine makubwa kuliko yaliyokuwepo mwanzo. [Yohana 5:14].

  Kwa hiyo dada Salome, pamoja na somo zuri la Mzaliwa wa Kwanza, Jambo kuu kuliko yote ni KUKAA NDANI YA AGANO na Agano letu kwa sasa ni KUOKOKA.

  Mungu wa Mbinguni atusaidie.

 105. Tumsifu Yesu kristo, Namshukuru mungu sana alieniwezesha kuangalia kipindi cha mwalimu mwakasege, nimefunguka kuhusu mzaliwa wa kwanza bado sijafahamu vizuri jinsi ya kufanya kusaidia ndugu zangu walionatatizo ambalo kutokana na mafundisho nimeona yanahusiana na mzaliwa wa kwanza. Naomba msaada wenu mungu awabariki sana.

 106. Nimebarikiwa sana na hii semina ya neno la Mungu inayohusu namna ya kutathmini hali ya mzaliwa wa kwanza na kuiombea inayoendelea hapa Arusha,Nimeweka kwenye matendo uliyofundisha ndugu zangu wamefunguka nami naona mabadiliko makubwa rohoni,kazini kwangu na nyumbani kwangu.Ni maombi yangu kwa Mungu azidi kulinda hilo lango ili tuendelee kula mana.

 107. Naomba muniombee nguvu za wokovu zimenipungukia sasa mpaka nasikia mwili wangu kuwa mkavu kabisa kama mtu anayeumwa na familia imeparangayika kiasi cha kukosa amani

 108. Bwana Yesu asifiwe,

  Namshukuru Mungu ambaye amenifungua macho ya rohoni kwa sehemu kupitia mafundisho ambayo huyatoa ukiongozwa na Roho Mtakafitu, Jina la Bwana Yesu lihimidiwe milele yote.

  Kazi yenu si bure na Mungu atazidi kuwatia nguvu.

 109. Dada Secilia, kupitia neno hili unayo nafasi ya kumsinda shetani maana ni kweli Dhambi ina nguvu lakini nguvu ya Mungu ni zaidi. Ni wakristo wengi sana wanaosumbuliwa na hali uliyo nayo na wanafikiri wakioa au kuolewa mambo yatakuwa shwari matokeo yake hali inazidi kuwa mbaya na kwa sababu ni jambo la aibu hawadiriki kulisema. Mithali anasema, ” Afichaye dhambi hatafanikiwa”.

  1. Ujue Yesu alicho kifanya msalabani kwa ajili yako.
  Warumi 6: 6 maandiko yanasema, “mkijua neno hili…”
  sijui kama wewe unajua neno hili
  2. Angalia ni vitu gani unavyoilisha nafsi yako kwa KUONA na
  kUISKIA maana nafsi yako inakula kwa namna hiyo.
  3. Amua kushinda maana wewe unaitwa Mshindi ukiwa umezaliwa
  mara ya pili. 1Yohana 5:4,5
  4. Soma neno la Mungu na kulitafakari, kulitii na kufanya
  maombi
  5. Omba Damu ya Yesu ikufunika wewe na nafsi yako
  ikuunganishe na nafsi ya Yesu.
  6. Omba Mungu akupe nguvu ya kuishinda dhambi inayokusumbua.

  Mungu akubariki

 110. Bwana yesu asifiwe sana,tunazidi kuombea huduma mnao itoa ili Mungu aweze kuwainua zaidi.Mimi nimemaliza chuo kikuu leo hivvo naomba mnisaidie maombi niweze kufaulu vema na kuhimili vishindo vya ujana.

 111. MUNGU Awabariki, mtumishi kazi mnayoifanya sio bure kwa kweli mnatusaidia Watanzania na watu wote kwa ujumla kuendelea kumjua MUNGU Kwa kupitia kweli mnayoifundisha mzidi kupanua wigo ili watu wengi zaidi waweze kufikiwa na hasa wa vijijini ambako imekua ngumu kufikika.GOD BLESS YOU ALL

 112. Praise the Lord,I badly need a prayer for my children to get a breakthrough from difficult time they are going through now and prosper in their studies and in their life,For our Good Lord Jesus Christ embrace them

  A M E N

 113. Mungu wetu apewe sifa hongereni kwa kazi ya Bwana, nimeikubali. Huduma yenu nzuri sana ila kuna sehemu inaitwa Kilwa Masoko je, mumewahi kufika au mna mpango wa kuja?
  Mungu awabariki sana.

 114. Bwana yesu asifiwe mtumish mwl mwakasege.
  ninayofuraha kubwa kukushukuru kwa mafundisho uliyoyatoa hapa tabora july 2010 kwa kweli kazi umeifanya nasi unetufumbua kwa kiasi kikubwa hivo binafsi ninakuombea huduma njema.pia ninawashukuru waimbaji walitubariki sana kwa uimbaji mungu awabariki sana.binafsi napenda kiwashukuru na ninawatakia huduma njema.

 115. mungu asifiwe mtumishi
  nimebarikiwa sana na semina iliyofanyika katika mkoa wa tabora.
  mungu akubariki na akuzidishie siku za kuishi ili hata wale ambao hawajapata kusikia huduma yako waweze kubarikiwa.

 116. Bwana Yesu Asifiwe mchungaji, Mimi Edward nimeanzisha shule ndogo ya english medium school, inhitaji kiwanja kikubwa ili kupata usajili na pia nimekumbana na matatizo mengi juu ya shule na familia. Naomba unisaidie kuomba kwa ajili ya shule hii.
  Shule ni Great Vision English Medium School

 117. Bwana Yesu asifiwe mtumishi pole na hongera kwa huduma Mteule namtukuza Bwana kwa matendo yake makuu kupitia wewe kwaajili ya nchi yangu Tanzania kiu yangu mimi ni kulifikia kusudi la Mungu ktk maisha yangu,nina utata sana jinsi Mungu anavyo mtumia kila mtu ili kutimiza kusudi alilomleta alitimize sababu yeye si wa refference natamani sana kutembea ktk kusudi lake kwamaana pasipo yeye kwangu mimi hakuna maisha nakosa ushauri kila ninapotafuta nashindwa kwa kusimamia naliamini sana neno lakini mda mwingine mtoto si huachiwa housgel amlishe?

 118. NAMSHUKURU MUNGU KWA MAMBO MENGI ALIYONITENDEA NA ANAYOZIDI KUNITENDEA,MAMA YANGU ALIKUWA ANAUMWA SANA NA ALIFANYIWA UPASUAJI,NILIKUANDIKIA MESSAGE NIKIOMBA USHIRIKIANE NAMI KATIKA MAOMBI, KUOMBA KWA AJILI YA UPONAJI,NAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA SASA HIVI NI MZIMA NAAMINI MUNGU ATAZIDI KUMPA AFYA,MTUMISHI UBARIKIWE NA MUNGU AKUTIE NGUVU KATIKA HUDUMA UNAYOIFANYA

 119. christo apewe sifa mtumishi wa mungu

  Naomba ufafanuzi juu ya hawa watu wanaoitwa FREE MASSON kwani wakristu wange hatujajua kuhusu jambo hili,naomba mtumishi ikiwezekana uandae somo utufundishe.ubarikiwe sana ktk huduma yako ya mana.AMEN

 120. Bwana yesu asifiwe mtumishi wa Mungu. Namshukuru sana Mungu kwa ulinzi wake na upendo wake kwangu. Mchungaji Mwakasege ninaomba ufafanuzi/maelezo kuhusu nchi ya palestina kisiasa na kiroho. Vilevile napenda kufahamu kibiblia kuhusu taifa la Palestina na Israel. Pili mchungaji naomba maombi yako kwani nina tatizo kubwa sana la ada. Nasoma chuo kikuu cha Kairuki. Nilikuwa nafanya kazi. Baada ya kujiunga na chuo kikuu nimefukuzwa kazi na nilitegemea kuwa ningeweza kujisomesha kwa mshahara wangu. Mungu akubariki mtumishi wa Mungu.

 121. Bwana yesu asifiwe sisi vijana wa arusha tunahitaji semina angalau wiki moja ya Mwl.Chistopher Mwakasege je inawezekana?
  Mungu aibariki Huduma yako daima.

  Laizer.

 122. bwana yesu asifiwe, nimemwona mungu kupitia ujumbe wa neno ambao kwanza niliusikia kwa njia ya redio, tape toka niko kidato cha pili mpaka sasa niko chuo kikuu ARDHI.asante kwa mafundisho ya kunijenga.

 123. Pray the Lord,Am a graduate from the UDSM majoring in Engineering,God has helped and enabled to properly finish my Studies and i thank my Almighty God for am now working and helping my family to some extent,So my problem is am spending much of my time to imagine how will i be able to know the right girl!Am now 28yrs of age and i think is the right age for me to have wife!So i do not have peace of mind as i think its risk to only approach girls whom are around me as i know they will just agreed because of who am i,So advice me pastor and pray for me that i have the right girl
  Thanks and May God keep you safe that you proceed helping use

 124. Bwana Yesu asifiwe mchungaji,Mimi ni Engineer wa umeme,Electrical Engineer nimemaliza chuo kikuu mwaka jana Mlimani-COET,nipo kazini lakini kazi inanibana sana na ninashindwa hata kuishi maisha ya furaha na ndugu zangu,Wananilaumu sipatikani ktk simu na kwa kweli sina furaha na kazi yangu,Nakoumba mchungaji wa Mungu Uniombee Niweze kuwa na furaha na Munga anitangulie ktk shughuli yangu niwe na amani na jamii yangu
  Ahsante

 125. Hawa watumishi mungu awatie nguvu maana bila YESU kuwa ndani yao wasingesimama mpaka leo na watu wanazidi kumwamini yesu kupitia wao wanapomhubiri mfalme wa amani yesu,Maana wanasikia mengi yakukatisha tamaa na bado wanasonga mbele ama nimeamini hakika yesu ni mtetezi wao na wa wote wanaomtegemea ,MUNGU AWABARIKI SANA NAWAPENDA SANA.

 126. Ndg Mussa
  Ahsante kwa kuweka bayana upande uliopo.Lakini kwa upande wangu naona ujumbe uliotaka umfikie Mwl Mwakasege haujaeleweka vizuri.Nasema hivyo kwa kuwa ujumbe huo upo kijumla sana kwamba Mwakasege anajiinua yeye kuliko kumwinua Yesu.Na kwa vile umeuweka ujumbe huo kwenye blog hii nadhani ulikuwa na lengo pia ujumbe huo utufikie na sisi sote tunaosoma na kuchangia mada mbalimbali ndani ya blog hii.Nilichokuomba ukifanye ni kueleza bayana bila kificho Mwl Mwakasege anajiinua yeye kwenye eneo gani au anajiinua kwenye huduma yake nzima?
  Biblia ninayoisoma inasema msingi wa huduma yoyote ya Mungu ukijengwa kwa kumtazama mtu au kumtegemea mtu lazima huduma hiyo itakufa haitaenda mbali, lakini ukijengwa kwa Mungu mwenyewe hata nani asimame kuipinga lazima itasonga mbele.Sasa kama Mwakasege ajiinua yeye badala ya Bwana wetu Yesu Kristo huduma hiyo haitadumu.Sasa ninachokuomba ndg yangu Mussa hebu onyesha maeneo kadha wa kadha ambayo wewe umeona Mwakasege amejiinua yeye.Hili litamsaidia Mwakasege mwenyewe pamoja na sisi tunaosoma hapa ili tujue kwamba kwa kufanya hili na lile tunajiinua sisi badala ya Bwana mwenye shamba aliyetuita tufanye kazi shambani mwake.
  Ahsante na nategemea utatueleza maeneo hayo ambayo Mwakasege ameacha kumwinua Kristo badala yake amejiinua mwenyewe ili sasa sisi(mimi na wewe na wengine wote) tuingie kwenye maombi ya kuugeuza moyo wa Mwakasege aache kujiinua yeye maana kwa kufanya hivyo ataangamia sio yeye tu bali pamoja na wote wanaolishwa mana na mtumishi huyu.
  Mungu wangu akubariki sana

 127. Ndugu yangu mussa, mimi nafikiri mimi pia nimekuelewa vizuri, lakini suala liko palepale kwamba kama umeona mapungufu katika huduma ya mtumishi yeyote ili mradi unaamini kuwa anamtumikia mungu wa kweli, basi huwezi kukwepa, ni lazima sisi tumuombee mimi na wewe, lakini huwezi kusema ujumbe umefika akitaka aufanyie kazi aul la! hayo ni mambo ya duniani, mwakasege ni mwanadamu kama wengine, ingekuwa rahisi kila mtu akiambiwa wewe una mapungufu haya halafu akakubali basi kusinge kuwa na kukosea, katika biblia mitume karibu wote walikosea , tafadhari ndugu yangu mussa naomba tumuombee kama kuna tatizo,hizo ndio taratibu ktk mwili wa kristo,
  Tunajifunza, ubarikiwe..!

 128. Ndg Kinyau, Haggai;
  Naomba nikutoe wasiwasi, mimi sio wa ile kambi nyingine. Mwl. Mwakasege namjua vizuri sana ndio maana sijasita kumnyoshea kidole. Hata hivyo, siwezi kuwalazimisha watu kuamini kila ninachosema, maana kuna wakati fulani hata Yesu alipingwa sana kutokana na kile alichokuwa anakisema juu ya mambo fulani ambayo watu waliyaamini vinginevyo. Tena watu walipoomba ishara aliwapa ile ya Yona. Kwa kifupi, hakuna ishara ninayoweza kukupa ili kuthibitisha hili lakini ninachofurahia ujumbe umefika kwa mhusika. Kufanyia au kutofanyia kazi ni juu yake, lakini mimi nimefanya kazi yangu. Ubarikiwe sana!!!

 129. Ndg Mussa,
  Comment yako ya tarehe 30 March imeniacha hewani kwa maana kwamba hujatoa hujasema ni kwa namna ipi au kwa namna gani Mwl Mwakasege amejiinua yeye badala ya Yesu anayemhubiri. Ninasema kwa dhati kabisa kwamba pengine humjui Mwl Mwakasege kwa undani, laiti kama ungekuwa unamfahamu sawasawa sidhani kama ungetoa comment kama ya kiwango hicho.Wasiwasi nilionao ni kwamba comment hizi zinaweza zikawa zinatoka kwenye ile kambi nyingine, yote katika yote wajibu wetu ni kumuombea Mwl Mwakasege asije akajiinua yeye badala ya Yesu Kristo anayemhubiri.

 130. MUSSA ASANTE SANA KWA UJUMBE WAKO , LAKINI MIMI NINAFIKIRI, TUNAPOONA MAPUNGUFU YOYOTE JUU YA WATUMISHI WA MUNGU SISI WAJIBU WETU NI KUWAOMBEA, HILO HATUWEZI KUKWEPA, KWA HIYO KAMA UMEONA MAPUNGUFU YOYOTE NDANI YAKE NI KWA SABABU HUKUMUOMBEA,MWL.MWAKASEGE NAE NI MWANADAMU TU, ASANTE MUSSA UBARIKIWE SANA.

 131. Huo ujumbe hapo juu wa mussa umeonekana umetumwa na DR.AHMAD, Ni kwa makosa samahani sana wana blog, kulitokea kidogo makosa ya kiufundi

 132. MUSSA ASANTE KWA USHAURI WAKO LAKINI MIMI NAFIKIRI SISI TUNAPOONA KUNA MAPUNGUF YOYOTE JUU YA MTUMISHI YOYOTE NI WAJIBU WETU KUWAOMBEA, BILA HATA KUWAAMBIA SISI HATUWEZI KUKWEPA NI LAZIMA TUWAOMBEE TU, NAO NI WANADAMU TU. UBARIKIWE MUSSA.

 133. nimekuwa nikibalikiwa na mafundisho yako.somo lako la jifunze maombi ya kiulinzi ili umiliki na kutawala lilinibariki sana.naomba unieleze jinsi ambavyo naweza kupata notice masomo yako.Mung azidi kukuinua.

 134. Watumishi wa Mungu naomba mniwie radhi kidogo kwa haya nitakayoyasema. Huu ni ushauri wangu wa bure kwa Mwakasege. Ukweli ni kwamba Mungu amemwinua kidogo sana lakini yeye anajiinua sana. Kwa hiyo mwambieni kama anataka kuinuliwa zaidi anatakiwa ashuke

 135. Bwana Yesu asifiwe Mungu akubariki sana baba yetu mpendwa Mwakasege kwa kazi yako ya kurudisha kondoo zizi!

 136. MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI WA BWANA ! UMEKUWA MSAADA MKUBWA SANA KWENYE MAISHA YANGU TANGU KIPINDI NILIANZA KUHUDHURIA SEMINA ZAKO MWAKA 2008 MPAKA LEO NIMEVUKA HATUA NYINGINE KUPITIA SEMINA ZAKO PALE BIAFRA . MUNGU AKUBARIKI SANA NA HUDUMA ILIYONDANI YAKO ISIKOME .MUNGU AKUPANDISHE UTUKUFU NA UTUKUFU ILI UWEZE KUVUTA WENGI KWAKE . MUNGU AIBARIKI FAMILIA YAKO SIKU ZOTE ZA MAISHA YENU >NA MUNGU WA ISRAEL AWE NAWE ! NAOMBA USOME ZABURI YA 20 . UBARIKIWE

 137. Shalom mtumishi!mungu wetu azidi kukuinua katika kazi yake.nabarikiwa sana na masomo yako.natamani kupata vitabu vyako.je nitapataje?barikiwa mno

 138. Bwana Yesu Asifiwe mimi naitwa Bona nimegusiwa na maombi yako ya toba Mungu akubariki akuzidishie nguvu katika kazi ya kufundisha Neno la Bwana amen

 139. nashukuru sana kwa mafundisho mazuri yenye munatowa kwa ajili ya wokovu ya wanadamu, Mungu awabariki na mutukumbuke kwa maombi juu ya wokovu wetu.
  NIKO congo DRC, Bukavu, Commune Ibanda, Avenue FIZI.

 140. Nasema asante na ninashukuru mungu wakati wote ambapo ninapata mda wa kusikiya mahubiri ya mtumishi mwakasege.
  mimi ni mukongomani,na kaa pa uvira na bukavu.
  Nimepata neema ya kufuata mahubiri haya kwenyi radio free africa.mahoni yangu ni kwamba ingelikuwa vema wakuu wa programu kwenyi radio waongeze mda kwa kipindi icho.asante;
  nikumbukeni wakati wa maombi yenu.

 141. Bwana Yesu Asifiwe watumishi,
  Poleni na kazi ya kuhudumia kondoo wa Bwana. nahitaji maombi yenu kwa ajili ya mama yangu mzazi anasumbuliwa na miguu inamuuma sana inafikia hatua anashindwa hata kutembea. Mama yangu yupo Iringa na Mimi nipo DSM naamini kuwa uponyaji unamfikia mtu mahali popote pale alipo haijalishi yupo umbali gani. Naamini atapokea uponyaji kwa njia yeyote ile iwe ya redio au television au simu. Mbarikiwe katika huduma yenu.

 142. Mungu ni mwema kwa watu wote.
  Mungu wetu awatie nguvu zaidi ndugu mnaowasaidia wenzetu.
  Tuwaombee sana wachungaji wetu Mungu awape uimara zaidi katika kazi ya wokovu. Amina.

 143. bwana yesu apewe sifa mwal mwakasege, namshukuru , namshukuru mungu sana kwa ajili yako kwani masomo ya maombi ya toba kwa ajili ya aridhi na maombi a toba ya muda mrefu yamenifungua sana, bwana azidi kukubariki akuinue na roho mtakatifu azidi kukufundisha.Amen

 144. Mungu akubariki mwakasege neno linatufikia,Mungu akupe maono mengine zaidi na wavijijini wapate huduma ya neno kama sisi wa ofisini

 145. Bwana afisifiwe sana.

  Nimefurahi sana kusoma habari hizi kwani ndio mara yangu ya kwanza kufungua website hii. Napenda sana kumpokea Yesu katika maisha yangu. Naomba mniombee katika hili kwani hali ngumu ya maisha inanifanya nianguke katika dhambi kila siku.

  Najua palipo na Yesu hapaharibiki chochote.

  Mbarikiwe sana

 146. Naitwa Rose nimeolewa mimi Naomba mniombee nipate mtoto nimekunywa dawa sana lakini sijafanikiwa. Mungu awabariki naamini kwa Yesu kuna wototo wengi.

 147. Mimi namshukuru mungu kwa njia hii ya neno la Mungu kwa njia ya internate kwani naishi marekani lakini bado naweza kusoma neno kwa lugha yangu ya asili kiswahili BWANA ASIFIWE SANA

 148. Dada Secilia,
  Neno la Mungu lasema, “Bali wote waliompokea Yesu ALIWAPA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU”-Yohana 1:12
  Pia Neno la Mungu linasema UTOSHELEVU WETU WATOKA KWA MUNGU!
  Mume hatakufanya usifanye UZINZI.Uzinzi ni kongwa la shetani ambalo Yesu alikuja kulivunja 1Yohan 3:8.
  Uzinzi unaanzia MOYONI.
  Dhambi zote zinaanzia moyoni.
  Vita vinatakiwa vipiganwe na ushindi uanzie moyoni.
  BADILISHA MTAZAMO WAKO.
  Je, USIPOPATA MUME wa kukuoa INA MAANA UTAKUBALI kufanya uzinzi maana unataka kutosheleza tamaa za mwili?
  YESU ALISEMA NJIA YA KWENDA MBINGUNI NI NYEMBAMBA NA INABIDI KUJIKANA/KUJIKATAA NA KUBEBA MSALABA WAKO KILA SIKU!
  PIA SOMA WARUMI 13:11-14.
  TUMEAMBIWA TUSIUNGALIE MWILI HATA KUWASHA TAMAA ZAKE!
  Tamaa zipo ILA TUSIZIANGALIE WALA KUTAKA KUZITOSHELEZA!Wagalatia 5:16
  USIPOJIZOEZA KUISHI BILA KUFANYA NGONO WAKATI HUU AMBAO WEWE NI MSICHANA nakuambia HATA UKIJAOLEWA UTAANGUKA KATIKA UZINZI maana SHETANI ANAJUA ENEO LA UDHAIFU WAKO!
  HATA WATU WA DUNIA WANASEMA NJIA MOJAWAPO YA KUSHINDA UKIMWI NI KUJIZUIA BILA KUFANYA NGONO HADI KUOLEWA AU KUOA.
  MUNGU AMEWAPA WANADAMU WOTE UWEZO WA KUKATAA MABAYA ila INABIDI UJUE KWAMBA UNAWEZA KUTOFANYA NGONO HADI UOLEWE.

  SASA KWA KUWA WEWE UMESHAKUBALI KUOKOKA basi JUA KUWA UKIKAA VIZURI KATIKA BWANA UTAPATA USHINDI.

  MIMI NAKUSHAURI UTAFUTE WADADA WALIOOKOKA VIZURI YAANI WENYE USHUHUDA MWEMA AU WAMAMA WALIOIMARIKA KATIKA WOKOVU nenda fanya URAFIKI NAO na waeleze udhaifu wako huu ILI MUOMBE NAO NA WAENDELEE KUKUJENGA KIROHO KATIKA MAFUNDISHO YA NENO.
  PIA TAFUTA USHIRIKA WA WAPENDWA WALIOMAANISHA KWENDA MBINGUNI nenda sali nao, kaa chini yao na JIFUNZE NENO KWA BIDII NA HUDHURIA MAOMBI na vipindi vingine muhimu.

  UKIKAA MWENYEWE HUTAWEZA KUSHINDA DHAMBI.UNAHITAJI USHIRIKA WA WATAKATIFU.

  PIA SOMA NENO KILA SIKU ; SOMA NENO ASUBUHI PIA SOMA NENO JIONI.SOMA MILANGO MIWILI AU MITATU KILA SIKU NA JITENGEE MUDA WA KUOMBA MWENYEWE KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI UNAPOENDA KULALA.

  JUA KUWA KUMFUATA MUNGU katika dunia hii LAZIMA TUTATESEKA. MIILI YETU LAZIMA TUITESE NA KUITUMIKISHA.1Kor 9:25-27.PIA 2Timotheo 3:12

  USIPODHAMIRIA KUCHUKUA HATUA MAHUSISI YA KUJIZAMISHA KATIKA NENO NA MAOMBI hata watu wakikuombea itakuwa kazi bure.CHUKUA HATUA.FANYA UPANDE WAKO NA MUNGU AMEKWISHA FANYA UPANDE WAKE KWA KUMTOA KRISTO NA KUTUPA ROHO WAKE MTAKATIFU.

  Mungu akubariki.

 149. LIINULIWE JINA LA BWANA YESU.Namshukuru Mungu kwa kutuinulia Mtumishi wake alishe kondoo wake.Kikubwa arudishe kondoo walopotea zizini mwa Yesu Kristo.

  Katika huduma yako, naomba unikumbuke ktk maombi kwani nampenda Mungu lakini nakuwa napotea katika dhambi.Nasumbuliwa na dhambi ya uzinzi.Nahitaji mume mwema ili nitulie niweze kuishinda dhambi hii.Hata neno limesema ‘Upendo hupunguza wingi wa dhambi’ Naamini Mungu akinipa mume wangu,sitaweza kufanya uzinzi maana nitampenda mume wangu tu.

  Eeee Yesu uliyekufa msalabani, ukasema yamekwisha, naomba hata kwangu mahangaiko ya kidunia yaishe sasa niwe mtoto mwema daima.

  Asante mwokozi wangu.

  Luv you JESUS CHRIST.

 150. BWANA YESU ASIFIWE! nabarikiwa na semina zako mtumishi wa Mungu.Naomba Mungu azidi kukuinua na kukutumia jinsi apendavyo. ubarikiwa sana

 151. mtumishi wa Mungu Bwana azidi kukutumia kwa viwango vya juu zaidi. ninakuombea….

 152. BWANA YESU Asifiwe,asanten kwa kipindi hiki ambacho kimeweza kufungua mioyo ya watu waliokata tamaa. mm nilikuwa na shida binafisi nawezaje kumpata mtumishi? naomba mnisaidie contact zake kama inawezekana. mbarikiwe

 153. Napenda nikusalimu ktk jina la Yesu aliye hai, mtumishi wa Mungu. Mwenyezi Mungu amekupa upako uje uwaokoe kondoo wake waliopotea, na kulieneza jina lake takatifu. Napenda kukuombea kila siku iendayo kwa Mungu uzidishiwe rehema na baraka tele zenye upendo na amani kwa kwa kupitia wewe wengi wamepona.
  Mtumishi naomba uniombee kwani nina kipindi kigumu cha uhusiano na mume mtarajiwa niweke katika maombi please Mungu akubariki

 154. Bwana Yesu asifiwe,nabarikiwa sana na huduma yako Mtumishi wa Bwana, Mungu akubariki sana na azidi kukufunulia hazina za gizani (zilizofichika) kwa ajili yetu.Mafundisho yako yamekuwa msaada kwangu ktk mtandao na Redioni pia.You are real model to me.

  Nakuombea Mungu azidi kukuinua,pia naomba maombi yako kwani somo la Nguvu za Mungu limenigusa sana hasa ktk kipengele cha maombi.Ndani yangu nguvu za Mungu zimepungua,nakosa mwelekeo kutokana na majaribu ambayo yamekuwa yakinisonga

  Nina mwaka mmoja ktk ndoa sijapata mtoto,naomba Mungu anipe mtoto na pia

  Mimi nipo Dar nafanya kazi Serikalini lakini mume wangu yupo kisiwani anafanya kazi, tangu tulipoanza kuomba uhamisho hatujafanikiwa mpaka leo,naomba maombi ili Mungu amlete hapa tuwe pamoja (kuambatana)

  God is my friend natamani kumtumikia for the rest of life

  Somo la Nguvu za Mungu limenigusa sana ndio maana nimeaguswa kuandika msg hii.

 155. Bwana apewe sifa mimi ninamahitaji yangu ninaomba kuombewa.
  1.Kuhusu familia yangu Mungu aipe Amani hasa mama yangu apate amani na kupokea uponyaji wake kwani anasumbuliwa na Presha na majaribu ya shetani .
  2.Naomba pia tuweze kumaliza nyumba yetu Mungu afungue milango tuweze kufanikiwa pia tuweze kupata na ajira ili tuweze kuendesha familia yetu.
  3.Ninaomba mniombe nipate mume mwema kwani wakati umesha fika wa mimi kuhitaji kuwa na familia yangu ,pia niweze kuondokana na laana ya midomo ya watu kwa maneno wanayo tunenea .

 156. Bwana Yesu Asifiwe ninaomba kuombewa kwani ninasumbuliwa nakifua kinanibana hasa wakati wa vumbi ninapata shida na omba maombi yenu.Pia naomba kuombewa kwani nipo kwenye wakati mgumu sana kuna majaribu mengi ila na fahamu kuwa majaribu ni mtaji, hivyo naomba maombi ili niweze kuyashinda Amen

 157. halelujah mtumishi wa mungu? “Na mshukuru Mungu kwa kuniokoa nikiwa bado kijana mdogo na kumjua kristo nikiwa bado kijana.Nimebarikiwa sana na semina za mafundisho yako mwalimu.Mungu akufunulie zaidi na zaidi.Mimi ninamsukumo ndani yangu kumuona Mungu akitenda mambo makubwa kwa njia yangu sisemi haya tuu! bali nimuombaji pia!natamani roho wa Mungu anijulishe mengi kyt roho juu nafasi yangu ktk kumtumikia yeye.Ninasoma chuo kikuu sasa.I need to see God lifting me higher and higher.

 158. Bwana yesu ainuliwe, Namshukuru mungu kwa ajili ya utumishi wenu na Mungu azidi kuwafunulia. nimebarikiwa sana na mafundisho haya ya nguvu za Mungu kwani niko ktk matatizo makubwa na hii ni kwa sababu hofu ilinitesa sana nikajikuta nikiokoka na kuanguka zaidi ya mara tano lakini somo hili limenifungua na nitang’ang’ana na Mungu kwani yote yanawezekana kwake aaminiye naamini sasa nitaweza kusimama nitayaweza mambo yote kwa yeye anitiaye nguvu. amen

 159. Peter wewe huumwi,kuanzia leo naanza kukuombea usiwe na hofu sasa utajisikia sawa kwa jina la yesu. ningependa unieleze kwa kirefu unajisikiaje.Leo anza kukiri sana damu iliyomwagika ubavuni pa Yesu ikuondolee magonjwa yote.uwe mzima kwa jina la yesu.

 160. Bwana Yesu asifiwe wapendwa! naomba mniombee kwani afya yangu siyo zuri huwa nahisi kama kuumwa lakini kilani kienda Hospital kupima naambiwa hakuna kitu yaani siumwi lakini bado hujisikia vibaya. Nakuombeni mniombee AFYA yangu iwe nzuri na pia MASOMO yangu kwani niko katika Chuo miongoni mwa vyuo vikuu hapa nchini. MUNGU awabariki.

 161. Bwana YESU Apewe sifa Mtumishi naomba Mungu azidi kukuinua katika huduma yako maana masomo yako kwa kweli yamenipa kutimilika sana katika uhodari wa kuubeba msalaba na JINA LA YESU pia katika uweza wa nguvu zake na mishale ya ibilsi ni vigumu sana kupenya sasa maana maarifa ya MUNGU yananivalisha silaha kali sana kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia kwamba MUNGU anafungua ghala zake za silaha mpya.Niombee katika utumishi wangu ukinikumbuka katika sala zako maana mimi ni kijana niayejitahidi kulisimamisha kusudi la MUNGU katika kizazi hiki,nakusihi usisahau.
  UBARIKIWE KATIKA JINA LA YESU!!!!

 162. am extremely in need of an English bible.
  They told me that it is very easy to get it from you at low price. NOW HOW CAN I GET IT.Am at Ardhi University.How much will it cost me.

 163. bwana asifiwe mtumish naomba uniombee mungu anisaidie
  katika familia yanyu ninamatatinzo makubwa naniko
  katika inch yaugenini canada hakuna mutu anaya nifaham
  lakini nina amini mungu a nani faham a nawenza kunitea
  watoto waungu wamechukuliwa nawatu nisojua
  nataka mungu asem nao warundishe watoto mimi naishi
  canada mungu akubaliki god bless you

 164. Bwana asifiwe Mtumishi,naomba uniombee Mungu anisaidie na aniongoze katika sala.Pia aisaidie familia yangu na aingoze katika sala.Naomba pia umwombee Mama yangu Mungu amsaidie aweze kumalizia nyumba yake na ampe uponyaji presha itoweke kwenye mwili wake na ugonjwa wa baridi.Asante sana naamini ile nyumba itakamilika na kabla ya nyumba Mama atapona kabisa.Amen

 165. BWANA YESU ASIFIWE.Mtumishi wa MUNGU ninaomba uniombe nipate kazi.Nimemaliza chuo kikuu cha ushirika mjini moshi mwezi wa 6 mwaka 2008 mpaka sasa sijapata kazi,naamini MUNGU ni mwema kwangu iko siku nitapata kazi ila tu ni kwa mapenzi yake yeye aliye juu.NAOMBA SANA UNIKUMBUKE KWENYE MAOMBI YAKO DAIMA.WASALIMIE FAMILIA YAKO.MUNGU AWABARIKI SANA.

 166. may God bless your ministry and family.umukuwa baraka ktk maisha yangu ya kiroho,nimejifunza mengi kupitia mafundisho yako.ingawa sasa ninapitia mambo magumu kwasababu ya kutokuisikia sauti ya Mungu,mm na familia yangu, naamini kwa semina yako ya Toba kwente viwanja vya Biafra,Dar itanifungua na kunifungua kwenye vifungo.
  Mungu akubariki sana na aendelee kukutumia. Hata haya maneno ya nguvu za Mungu ni mazuri.Be blessed much!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 167. Hallelujah! kuna kitabu nina nimekisoma kinaitwa the purpose driven life. kimeandikwa na Pastor Rick Warren USA, na naweza kukuazima mladi usizamie nacho ila kitabu nikizuri sana unaweza cheki kwenye mambo yetu ukitype hilo jina la kitabu hapo juu na madukani vinapatikana, Mungu akubariki Rapha.

 168. mimi naomba yeyote mwenye mapenzi mema aniangalizie vitabu gani anavyo halafu nijue lakufanya ili nivipate! asante na mbarikiwe na bwana, U S

 169. Bwana Yesu Asifiwe Naomi, semina yake itaanza kuanzia tarehe 12 hadi 19 Otober, 2008 viwanjani Biafra! Wajulishe na wengine waje wale MANNA! Mungu akutunze

 170. hello!Shalom,
  naomba nifahamishwe je mwl mwakasege ameshaanza semina yake Biafra?
  naomba nijibiwe sitaki kuikosa ht kidogo.
  Be blessed.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s