Kuvaa msalaba na kupamba picha za Yesu!

cross

Kuvaa msalaba wenye picha ya Yesu au alama yoyote ya msalaba, imekuwa ni kitu cha kawaida. Pia makanisani hata majumbani tunapamba picha zenye taswira ya Yesu. Lakini mnasemaje kuhusu hili? maana wengi wana maoni tofauti kuhusu uvaaji wa misalaba hiyo na upambaji wa picha hizo!

Advertisements

9 thoughts on “Kuvaa msalaba na kupamba picha za Yesu!

 1. Kwa kweli mna uelewa mdogo sana kuhusu maandiko na ufalme wa Mbinguni, Naomba Roho Mtakatifu awafungue macho yenu muweze kumwelewa MUNGU zaidi, haimaanishi mimi namjua sana MUNGU, lakini ninyi bado ni watoto wachanga kiimani na kimaandiko.

 2. Ndugu yangu John Paul,
  Nimesoma comments zako kuhusiana kuvaa au kutundika msalaba. Kwa kweli, nimegundua kitu hapo. Ni kwamba, wakristo wengi (nadhani na wewe ukiwemo) hawajaelewa tofauti kati ya msalaba wa enzi za uajemi na utawala wa kirumi na msalaba wa Yesu. Enzi za utawala wa kirumi walitundikwa watu wengi kabla na baada ya Yesu. Lakini msalaba wa Yesu ulipindua ulimwengu kiasi cha kubadili maana ya awali ya msalaba (chombo cha kuulia) na kuufanya msalaba kuwa “Uweza wa Mungu uletao Wokovu” 1Kor. 1:18. Kila aliyeokoka kupitia kifo cha Yesu anauona msalaba wa Yesu kuwa ndio kiini cha wokovu wake. Tafadhali soma vizuri Isaya 53. Kwa hiyo, kutundika alama ya Msalaba makanisani ni kuonyesha kuwa “hapa upo “Uweza wa Mungu uletao Wokovu”. Kuvaa alama ya msalaba au kujichongea msalaba na kuuweka juu ya kitanda kama wanavyofanya wengine kwa kutaka ulinzi ni ibada ya sanamu kwa kuwa msalaba wa Yesu tunauona na kutegemea ulinzi na ushindi kutoka huo “ki-imani”. Yapo maelezo mengi kuhusiana na hilo lakini hatuna muda wa kutosha. Ubarikiwe.

 3. Ah, Masangu (MMN), ulipanga?

  Wapendwa, mimi nilikuwa sijalifikilia sana hilo, mara kadhaa nimeona Msalaba katika majengo, hata mimi nilipokuwa kijana sana, nilipenda kuvaa sana misalaba, mwanzoni sikupata kujua ni kwanini nilivaa na kwa sasa mbona sivai tena! Mawazo yangu hayakuzingatia lolote juu ya uvaaji shingoni au uwekaji Misalaba juu ya majengo nk,nilifikilia ni ‘Logo’ au Nembo ya ukristo,Lakini pia sijui kama uwekaji wa Nyimbo za kwaya za injili katika simu kuna maana tofauti na kuvaa msalaba au kuweka picha zinanazozaniwa ni za Yesu katika majengo.

  Sasa naomba kujua kunaubaya wowote katika kuvaa au kutundika msalaba katika majengo ya kuishi au ya kuabudia?

  Uwekaji wa nyimbo za Injili katika simu ndiyo ucha Mungu au ni Ushabiki na upenzi wa Ukristo?

 4. Ukristo pasipo msalaba hauja kamilika kwa kuwa ndio njia aliyoichagua Mungu atumie kutuokoa. Hata ukisimlia maisha ya Yesu hapa duniani, ukiondoa kipengele cha msalaba hapo hujamaliza hiyo hadithi.
  LAKINI katika yote, tujali maisha yetu ya Kikristo – tabia, maneno tunayosema, myenendo yetu, upendo wetu kwa Mungu na uumbaji nk kuliko tamaduni na mambo yasiochangia utakatifu wtu mbele za Mungu.
  Msalaba wa kuvaa hauongezi utakatifu wako wala kukupunguzia usipovaa.
  Kwa hiyo ni kosa kubwa mkristo ye yote kuweka imaani yake katika msalaba aliyouvaa kuliko kwa Mungu aliyemuokoa kupitia Yesu Kristo aliyekufa pale Msalabani.
  PIA imani ni suala la mtu binafsi, kwa hiyo kama ni roho wa Mungu amekusukuma kuutumia msalaba KWA IMANI, sioni shida kabisa, ukiutumia utaona maajabu ya Mungu kama manabbi waliyotumia vitu kama kijiti kupandisha juu shoka iliyokuwa imezama majini (sasa hapa kijiti tu ni nini? nguvu zake zinatoka wapi kama sio kwa Mungu anayemtumia huyo nabbi?)
  Sasa hapo tusifanye kimazoea au kwa kuiga wengine au kidini tu kwa sababu kwa namna hiyo si imani tena bali ni kuiga (kucopy na kupaste).
  Mbarikiwe sana.

 5. Nimesikia wapo wengine wanavaa misalaba hii ili kujikinga na mapepo, mikosi na mambo mabaya katika maisha yao. Hili nalo mnalionaje?

  Hapa Marekani kuna hata “watumishi wa Mungu” wanaouza hii misalaba yenye kutoa ulinzi. Na ukitazama matangazo yao kwenye runinga utaona jinsi watu wanavyoshuhudia jinsi uvaaji wa misalaba hii ulivyowasaidia katika maisha yao na kuwaepusha na misukosuko ya kila aina!

  Kama alivyosema John Paul hapo juu, ukweli ni kwamba hakuna hata anayeijua sura halisi ya Yesu. Niliwahi kutazama uchunguzi wa kina wa wanasayansi kuhusu suala hili katika History Channel na sura ya Yesu wanayoipendekeza ni tofauti kabisa na hizi tulizozizoea ambazo mara nyingi zinatokana na mapokeo ya Waroma. Uchunguzi wa wanasayansi hawa unapatikana hapa:

  http://nyimbozadini.blogspot.com/2009/02/hii-ndiyo-sura-halisi-ya-yesu.html

 6. Bwana Yesu Asifiwe!
  Ni kweli kabisa watu wengi wamekuwa wanatumia msalaba au picha kinyume na ukristo wetu, kwani neno msalaba lina maana kubwa sana na siyo jambo la mzaha kwani msalaba kwa maana nyingine ni Ukombozi hivyo tutumie kwa kumaanisha kuwa ndio uliotukomboa katika dhambi mpaka sasa na siyo kana kwamba ile picha inawekwa kiunyonge bali ndivyo ilivyokuwa mpaka tukapata ukombozi hivyo tunatakiwa kuwa wanyenyekevu kama Yesu mwenyewe. Mungu wa Mbinguni na awabariki wote walioandaa mada hii Amen.

 7. na mimi pia nigependa kuongeza kwamba kwa maoni yangu tuu suala la kutumia msalaba kama uthibitisho wa ukristo linanipa utata kweli na binafsi sikubaliani nalo kwa sababu hizi:

  kwanza msalaba ulikuwa unatumika nyakati zile kama chombo cha kuulia yaani tool of execution ambapo kwa sasa jamii zetu mtu akihukumiwa kufa basi watatumia bunduki, kiti cha umeme au sindano za sumu maalum nk
  hivyo ni chombo cha mauaji kilichotumika wakati ule wa Yesu kwa mtu aliyehukumiwa kifo basi walimwua kwa kumtundika msalabani

  kwa mfano huo basi wa chombo cha mauaji au kunyongea wakosefu sioni maana yoyote kwa wakristo wa zama hizi zetu kutundika misalaba kwenye majengo ya kanisa ati kama uthibitisho wa ukristo wetu
  Ebu fikiria mfano huu kama leo hii mtoto wako akiuwawa kwa kuchomwa kisu. utasema ni nini chombo kilichotumika kumwua mtoto wako ? jibu ni simple kwamba ni kisu! ina maana chombo cha mauaji au kilichotumka kumyongea mtoto wako ni kisu .sasa itakuwa na mantiki au maana gani leo hii ukaamua kutundika kisu juu ya nyumba yako eti kama alama ya identification yako? au unapouimbia msalaba je unaweza kukiimbia kisu kilichomwua mwanao na kudai eti ndio kitakachokuleteta wokovu?

  pia sidhani kama Yesu alituagiza kusema kwamba msalaba (silaha iliyotumika kumwua yeye ) ndio itakuwa alama yetu ya imani yetu na ufuasi wetu kwake kama jibu hapa ni ndio naomba huyo mtu anionyeshe ni maandiko gani hayo yesu alituambia tutundike misalaba kwenye majengo ya kanisa kuonyesha imani yetu kwake

  pia inasadikika na baadhi ya wanahistoria kwamba Yesu hakuuliwa kwenye msalaba bali aliteswa kwenye STAKE NA SIYO CROSS.
  STAKE maana yake ni mti mmoja na siyo cross kama msalaba
  asanteni
  kwaheri

 8. Kwangu mimi jambo la kuvaa msalaba sioni kama lina maana yoyote ya kikristo. Huwa naona linapotosha kwa sababu hakuna kilicho sahihi. Maana utakuta msalaba wenyewe umerembwa, na pengine kuwa gold-coated, halafu unakuta kuna hicho kijitu ambacho kinasemekana kuwa ndiye Yesu kimekaa katika hali ya kusikitisha. Naamini msalaba was not such beatiful na wala Yesu si myonge vile sasa. Hali ya Yesu kuwa msalabani ilidumu kwa masaa machache tu na wala siyo ndiyo ujumbe kwa Ulimwengu…kwamba maana YESU HAYUKO MSALABANI sasa. Yesu alikufa na akafufuka so kwa nini kubaki na taswira kwamba yuko malabani bado? Huwa nachukulia huo kama udanganyifu wa shetani, kuwafunga macho watu wasielewe Yesu Nguvu na Uweza alionao Yesu!

  Suala la mapicha vilele mimi huwa sikubaliani nao. Picha nyingi ni za kuchora na kama kuna picha halisi (photo) basi itakuwa ni ya mtu aliyeigiza kwenye nafasi ya Yesu kwenye filamu fulani. Na hali sasa imekwenda mbali zaidi, siku hizi huwa naona Waimbaji wa Injili wanaweka kwenye video zao clips za picha kutoka katika filamu za Yesu. Kusema ukweli huyo siye Yesu, ni watu waliigiza tu. Sasa kunyenyekea picha hizo ni kinyume kabisa na ukweli. Ni sawa kwamba waliigiza ili kufikisha ujumbe kwa watu lakini sidhani kama inastahili kutumia picha hizo kama ndicho kielelezo cha Yesu. Yesu hayuko vile!

 9. I would hope that the way we live our lives would be the way someone would know/or suspect we are Christians rather than the wearing of a cross. It could actually be seen as hypocrisy if you were in the middle of committing sin while the person seeing it noticed the cross around your neck.

  Unfortunately non-Christians expect perfect behavior from Christians and when they see one bad thing many times walk away shaking their head.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s