Pasaka Njema!

Kufufuka kwa Yesu Kristo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa ni chanzo cha mjadala dunia nzima. Dini nyingine zimedai kuwa Yesu hakufa na hivyo kumaanisha hakufufuka. Wanazuoni wengine wamejaribu kuhusianisha kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo kama mwendelezo wa imani za kipagani zilizokuwapo kabla ya ukristo, na mengine mengi, kadha wa kadha.

Kwetu sisi wakristo, imani Yetu inasimama au kuanguka katika kufufuka kwa Yesu Kristo. Kwa kufufuka kwake, aliushuhudia ulimwengu kuwa Yeye ndiye Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele na mfalme wa amani kama Ilivyotabiriwa na manabii (Isaya 9:6). Kushambulia kufufuka kwa Kristo Yesu, ni kushambulia kiini cha ukristo kama mtume Paulo alivyoandika “Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. Na hapo wao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tumemtumainia Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote” (1Wakorintho 15:17-19)

Maneno ya Paulo yana maana kubwa wapendwa. Kama Kristo hakufufuka, tumepoteza muda bure, kuomba kwa Mungu mfu, tumejinyima bure kwa ajili ya mtu aliyekufa miaka 2000 na zaidi iliyopita, na tumaini letu kuwa Yesu anatuandalia makao na yakuwa atakuja kutuchukua tena ni bure! Je waona sasa ni jinsi gani imani yetu inasimama au kuanguka katika kufufuka kwa Kristo? Naam, kama Kristo hakufufuka, ni heri tuishi na kuponda mali maana kufa kwaja!

Kristo Yesu alifufuka katika wafu! Historia inashuhudia hivyo, na neno la Mungu linashuhudia hivyo. Wanahistoria kama Luka, Mathayo, Yohana, Josephus, Tacitus na wengine wengi wameandika mambo mbalimbali kuhusu kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo. Lakini hii ina maana gani kwetu? Kwa nini Yesu alikufa? Ni kwa ajili ya dhambi zetu! Unaweza sema utakwenda mbinguni kwa kuwa u mwema. Ndio, inawezekana u mwema ukilinganisha na Adolf Hitler. Lakini je Mungu anakuonaje? Mwema? Kama jibu ni ndio, hili ni jaribio waweza kufanya ili kujiona u mwema kiasi gani!

Viwango vya Mungu viko juu sana, na wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23). Sote tumehukumiwa kwenda katika ziwa la moto, maana baada ya kifo hukumu (Waebrania 9:27). Mbele za Mungu Baba, aliye Mtakatifu sana, hatufai na haki yetu itokanayo na matendo yetu ni kama takataka mbele za Mungu (Isaya 64:6). Mbele ya hakimu wa haki, hatuna la kujitetea. Tumetenda dhambi hali tukijua maana Mungu ameandika sheria yake katika mioyo yetu (Warumi 2:14-16). Kwa hiyo, kwa binadamu wote, ziwa la moto haliepukiki!

Habari njema ni kuwa, Yesu Kristo alikuja kulipa deni hili. Aliishi maisha Matakatifu ambayo mimi na wewe hatuwezi kuishi. Lakini pia alikufa, katika sehemu yetu. Kwa hiyo wote wanaokubali kazi yake msalabani na kufufuka kwake, wanahesabiwa haki, si kwa wema wao, bali kwa haki iliyo ndani ya Kristo Yesu (1Petro 3:18).

Mfano unaofanana kidogo ni huu, mko mbele ya mahakama, mnadaiwa deni kubwa sana ambalo hamwezi kulilipa. Hukumu imetolewa, mlipe deni au mwende kifungoni maisha na viboko kila siku. Hamna uwezo wa kulipa na mnasubiri mpelekwe kifungoni. Ghafla hakimu anasema, hizi hapa ni pesa toka mfukoni kwangu, nimelipa deni lote. Ila ili uhesabiwe umelipiwa sharti ukiri kwa kinywa na kuamini kwa moyo kuwa mimi hakimu nimekulipia deni lote.

Muhammad, Buddha, Confucius na wengine wengi, walioanzisha dini mbalimbali hawakulipa deni la dhambi. Ni Yesu pekee alilipa. Mwamini Yesu Kristo leo upate kulipiwa deni lako na kuhesabiwa haki wewe ambaye bado hujampokea Yesu. Ni rahisi na haihitaji gharama. Ni lazima udhamirie moyoni kuacha dhambi na kuishi kwa ajili ya Kristo (Utubu). Biblia inasema ukimkiri Yesu kwa kinywa chako NA kuamini katika moyo wako kuwa Mungu alimfufua toka wafu UTAOKOKA. Chaguo ni lako! Na wewe mpendwa ambaye umempokea Yesu Kristo, hili ndilo tumaini pekee ulilo nalo, ya kwamba Yesu alifufuka na anaandaa makao na atakuja kutuchukua(Yohana 14:2)

Neema ya Kristo na amani kutoka kwa NIKO iwe nanyi, Amina!

Advertisements

4 thoughts on “Pasaka Njema!

 1. Mpendwa msomaji,
  Bwana yesu asifiwe!!!!
  Tangu dhambi ilipo ingia duniani kwa mara ya kwanza ndipo dunia ilipo ingia katika uharibifu, ndio maana hakuna kilicho kamili mpaka leo, sisi sote hatupo kamili,hali ya hewa si kamili,miili yetu haifanyi kazi kwa ukamilifu, uchumi haupo kamili,mpaka DNA hazipo kamili hii ni kwasababu ya dhambi.
  Warumi 3;23,Maana yake ni nini?ili vyote hivyo viwe kamili Dunia(wanadamu)wamugeukie Mungu wa Mbinguni.Pasaka njema.Habari ndiyo hiyo!
  Karibu Kigoma.

 2. Bwana Yesu Asifiwe Sana!!!
  Wapendwa tunayo sababu ya kumshukuru sana Mungu Kwani anatupenda Upeo ( Injili ya Yohana Mtakatifu 3:16). Nataka kumcheka shetani, kwa kusema kwamba angejua alichokuwa anakifanya msalabani asingemsulubisha Mwana wa Adamu (Yesu Kisto). Kwani kwa kifo chake sisi Msalabani sisi tumekombolewa (1 Wakorintho1:18). Amina

  MUNGU ATUBARIKI WOTE, MUNGU ATUFANIKISHE WOTE, MUNGU ATUINUE WOTE, MUNGU ATUFANYE KUWA VICHWA NA WALA SI MIKIA (KUMBUKUMBU 28:13).ADUI AKIINGIA KWETU KWA NJIA MOJA ATAWANYWE KWA NJIA SABA(KUMBUKUMBU 28:7) KWANI NENO LAKE LAKE LA MSALABA NI UKOMBOZI KWETU NA NI NGUVU YETU ( 1 WAKORINTHO 1:18), KWANI KATIKA HUO TUNATEMBEA NDANI YA KIWANGO KIKUBWA SANA CHA UPAKO WAKE. NINAWAPENDA WOTE, AMINA

 3. Mungu atukuzwe mimi naamini ya kua hii ni nafasi ya pekee kumtangaza Yesu kristo hasa wakati huu wa pasaka ili watu wapate kujua ni nini maana ya pasaka. Kwani watu wengi huamini maana ya pasaka ni kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu lakini hawajui undani kwa nini Yesu alikufa na kwanini alifufuka, hivyo ni nafasi yetu ya pekee kupitia njia hii kuwataarifu watu sababu na maana ya pasaka.kwa kifupi tuu, maana ya kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu ni kutuletea sisi tulio kwenye dhambi ukombozi yaani tupate kuurithi uzima wa milele.

 4. Heri ya Pasaka wapendwa wote.
  Nina shawishika kushirikiana nanyi mafundisho haya kama nilivyopokea toka kwa Mtumishi wake naam naamini Roho wa kristo yu pamoja nami katika kuifunua siri ya historia (THE MYSTERY OF HOSTORY) Katika hii siri ya historia tuta angalia matendo matano makuu(five acts) ambayo Mungu ameyatenda anatenda na ata yatamiza.
  Waefeso 3;2-6

  Mungu alinipa jukumu la kuileta neema yake kwenu, ameruhusu nifahamu SIRI ya mpango wake kupitia ufunuo, na siri kuhusu Kristo.katika kizazi kilicho pita siri hii haikufunuliwa kwa watu.Lakini sasa Roho wa Mungu amefunua mpango wake kupitia manabii na mitume. siri hii ni kwamba kupitia Habari njema, watu ambao si wayahudi(WAMATAIFA)Washiriki baraka za Mungu pamoja na wayahudi!nao ni sehemu ya mwili mmoja na washiriki sawasawa ahadiza Mungu ambazo ameziweka kwa Kristo Yesu.

  SIRI YA HISTORIA KATIKA MATENDO 5( THE MYSTERY OF HISTORY)

  1.MUNGU ALIUMBA VYOTE
  Hakuna jambo lolote amabalo mwanadamu ameongeza tangu Mungu aumbe Dunia na vyote viujazavyo ulimwengu, kadli wanasayansi wanavyo fanya utafiti ndivyo inavyo tusaidia sisi wengine kuona ninamnagani Mungu alivyo Mkuu na si kwamba wana sayansi wanakuja na jambo jipya isipokuwa wanazidi kugundua yale ambayo tayari Mungu amekwisha yafanya.
  MUNGU ALIUMBA VYOTE ILI KUFUNUA UPENDO WAKE.
  Warumi 11;36

  Kila kitu kinatokana na Mungu, kila kitu kimekuwepo kwa uwezo wake na kila kitu kilikusudia utukufu wake.
  ili KUDHIHISHA UTUKUFU WAKE.
  Zaburi 145;9

  Wema wake unatuunganisha na vitu vyote afanyavyo.
  Ndiyo maana Mungu anapendezwa na ndugu kukaa pamaoja kwa umoja kwa maneno mengine tungesema kusudi la Mungu kuumba vyote ilikuwa ni kuunda FAMILIA.
  Yakobo 1;18

  Kwa ukarimu wake Mungu alichagua KUTUFANYA WATOTO WAKE kwa kutupa neno la kweli.nasi katika uumbaji wote tumekuwa chaguo la miliki yake.
  Waefeso 3;14-15

  Ninapo fikiri juu ya hekima na uwezo wa Mungu katika mpango wake, ninaanguka katika magoti yangu na kuomba kwa baba Mungu mwenye familia kuu ambao baadhi yao tayari wako mbinguni na wengine hapa duniani.

  2.KUKOSEA KWA ADAMU
  Mungu alipo umba kila kitu alisema tazama kila kitu kina pendeza na alipo muumba Adamu alimpa mamlaka ya kutawala kila kitu na kula kila aina ya matunda katika bustani ya Edeni, hapa maisha yalikuwa kamili hakuna kifo, hakuna njaa, hakuna sunami, hakuna vita NK. Na walikuwa mtu mume na mke uchi katika bustani wakishi maisha makamilifu ambayo Mungu aliwapa.
  katika hali ya kawaida tunapo zungumzia upendo lazima mtu achague kupenda au akatae,pendo lolote linalo tokana na kulazimisha hilo si pendo ndiyo maana hata Mungu hakumuumba Adamu kama roboti ili afanye kila kitu kwa lazima, hivyo akampa uchaguzi wa kumpenda Mungu au kumkana kwa kumkataza kula tunda la mti mmoja tu katika miti yote iliyokuwemo bustanini hapa tuna ona Adamu alichagua kutomtii Mungu na kula tunda la mti alilo katazwa,na hapa ndipo kwenye asili ya mwanadamu mara nyingi huwa tuna fanya vitu tunavyo katazwa na mungu. Warumi 5;12
  Dhambi iliingia ulimwenguni kwasababu ya kile kilichofanywa na mtu mmoja, na kwa hiyo dhambi ikaja mauti.

  Tangu dhambi ilipo ingia duniani ndipo dunia ilipo ingia katika uharibifu, ndio maana hakuna kilicho kamili mpka leo sisi sote hatupo kamili,hali ya hewa si kamili,miili yetu haifanyi kazi kwa ukamilifu, uchumi haupo kamili,mpaka DNA hazipo kamili hii ni kwasababu ya dhambi.
  Warumi 3;23

  Sisi sote tumetenda dhambi na imethibitishwa kwamba hatuwezi kuishi maisha yenye utukufu kama impendezavyo Mungu.
  Hapa tunaweza kuona inakuwa ni vigumu kwetu mara tu tunapokuwa tupo Duniani kufahamu makusudi ya uwepo wetu katika ulimwengu kwasababu tangu dhambi iingie duniani mwanadamu alipoteza kusudi.
  Warumi 8;20

  kwakuwa binadamu alihukumiwa kwakupoteza kusudi, hata hivyo BADO KUNA TUMAINI;Kwamba kila kiumbe sikumoja kitawekwa huru mbali na utumwa, upotevu na kushiriki utukufu na uhuru wa wana wa Mungu.

  3.YESU ALIKUJA KUTUREJESHA SISI
  Warumi 4;25
  Yesu alitolewa ili AFE KWA AJILI YA DHAMBI ZETU na ALIFUFUKA toka wafu ILI KUTUWEKA SAWA AU KUTUPATANISHA NA MUNGU.
  Warumi 5;6

  Tulipokuwa HATUWEZI KUJISAIDIA WENYEWE katika kipindi cha uhitaji wetu, Kristo alikufa kwa ajili yetu ingawa tulikuwa tukiishi kinyume na mapenzi ya Mungu.
  Wapendwa ninachotaka kusema hapa hatuwezi kuwa wakamilifu kwa nguvu zetu wenyewe hata kama tuta weka sheria nyingi makanisani haita wezekana kwasababu biblia inathibitisha kwamba sheria haziwezi kutusaidia ndiomaana mpaka leo sheria zipo na bado watu wanazivunja kama alivyo fanya ADAMU.
  Warumi 8;3

  Sheria za Musa hazikuweza kutuokoa kwasababu ya dhambi ya asili.lakini Mungu aliweka madhala TOFAUTI KATIKA MPANGO WA KUTOKOA.alimtuma mwanae wwa pekee katika mwili wa mwanadamu kama tulivyo,isipokuwa miili yetu ni midhambifu, Mungu aliiharibu dhambi inayo tawala juu yetu kwa kumtuma mwanae kama sadakakwa ajiliya dhambi zetu

  4.MUNGU HUTUPA UCHAGUZI
  Kama nilivyosema hapo awali kwamba pendo ili liwe pendo lazima uamue kwa hiari yako kupenda kumbuka unapo amua kuto amua unakuwa umeamua (DECIDING NOT TO DECIDE IS TO DECIDE)

  Unauchaguzi wa kufanya maamuzi yeyote ya kumkubali Kristo Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako au kumkana kumbuka una uhuru wa kufanya uamuziwa uchaguzi wowote lakini huna maamuzi ya kuchagua matokeo ya uchaguzi wa maamuziunayo ufanya sasa.

  1Wafalme 18;21
  Hata lini utaendelea kusita sita katika chaguzi mbili? kama Bwana ni MUNGU mfuate.
  Yohana 7;17
  Kama mtu yeyote atachagua kutenda mapenzi ya Mungu atafahamu kwamba mafundisho yangu yatoka kwa Mungu au la,

  2wakorintho 5;15
  Kristo alikufa kwa ajili ya wote ili kwamba wote wanao ishi WASIENDELEE KUISHI KWA AJILI YAO WENYEWE.alikufa kwa ajili yao na ALIFUFUKA TOKA KWA WAFU ili kwa waishi kwa ajili yake.
  Kumbukumbu la torati 30;15

  Leo NAKUPA UCHAGUZI kati ya mema na uovu, na kati ya uzima na kifo

  5, FAMILIA YA MUNGU ITADUMU MILELE
  Waefeso 1;10
  Huu ndio mpango wake, kwa wakati wake Mungu atavileta vitu vyote pamoja chini ya mamlaka ya Kristo kila kitu mbinguni na duniani
  Ufunuo 21;3-4

  Kisha makazi ya Mungu yatakuwa pamoja na watu wake, ataishi pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye atayafuta machozi yote toka katika macho yao na hakutakuwa na kifo tena,hakutakuwa na mateso,hakutakuwa na kilio wala maumivu.
  haya mambo ya wakati ulopita hayatakuwepo milele.
  Warumi 8;19,21

  ULIMWENGU NA VYOTE VIUJAZAVYO UNA SUBIRI KWASHAUKU KUBWA HIYO SIKU IJAYO WAKATI MUNGU ATAKAPO WADHIHILISHA WATOTO WAKE HALISI JINSI WALIVYO.ULIMWENGU NA VYOTE VILVYOMO UNATARAJIA SIKU ITAKA WAUNGANISHA WANA WA MUNGU KATIKA UTUKUFU WA UHURU MBALI NA KIFO NA UPOTEVU.

  Mpendwa msomaji hujasoma mafunuo haya kwa bahati mbaya ni Mungu anafunua mpango alio nao katika maisha yako ili baadaye ukafurahie uchaguzi wako leo.
  kama umeamua kumpa Yesu maisha yako sema YESU NIPOKEE JINSI NILIVYO KISHA NENDA UKAPATE MAFUNDISHO NAMNA YA KUENDELEA NA UAMUZI ULIO UFANYA KATIKA KANISA LA WATU WALIO OKOKA
  UBARIKIWE

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s