Majina ya Malaika na ya Majini/Mapepo

Watumishi  wengi wa Mungu kama vile waalimu,  wahubiri, waombaji husikika wakiyataja MAJINA ya Mapepo, ambayo hayakuandikwa katika Biblia, na kazi zao mbali mbali. Lakini sisi kama wana wa Mungu tunajua majina machache sana ya malaika wa Ufalme wa Mungu, mfano Mikaeli, Gabrieli:

1. Inakuwaje wana wa Mungu wanafahamu majina ya malaika wachache sana kwenye  ufalme Nuru huku wakiwa na orodha ndefu ya majina ya majini/mapepo walio katika ufalme wa Giza, yaani upande wa adui?

2. Wanaoyataja majina hayo ya mapepo/majini Elimu hiyo wameipata wapi?

3. Je, Ni sahihi kutafuta majina ya majini/mapepo na ya malaika wa Nuru toka chanzo chochote?

–Shoo–

Advertisements

24 thoughts on “Majina ya Malaika na ya Majini/Mapepo

 1. Bwana Yesu asifiwe. yamkini nipo katika watu walio chelewa kuwa pamoja na nyie tangu siku ya kwanza katika hii mada ila ningependa kuweka japo neno na linaweza kuwa msaada kwetu wote. bliblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maalifa ni mpango wa Mungu tujuwe siri za mbinguni na tuzitendee kazi pia ni mpango wa Mungu tujuwe siri za shetani na tuzi bomoe ukisoma efeso 6:12 tunaona maana kushindana kwetu sisi si ju ya damu na nyama. MOJA YA MBINU YA KIVITA NI 1KUTUMA WAPELELEZI ILI UKAJUWE HADUI ZAKO WANAKUWAZIAJE. 2 JUA SILAA ZA ADUI ZAKO ATAKAZO KUSHAMBULIA ukimjuwa unaye pambana nae na nguvu zake na uwezo wake vita haiwi kali. ndio maana Elia alimfungua macho msaidizi wake macho ya rohoni pale alipo ona jeshi la maadui wame wazunguka na tunaona akasema walio upande wetu niwengi kuliko walio upande wao. asanteni sana na mbarikiwe

 2. Ikiwa hawa wapendwa wanafanya kazi ya Mungu na matunda yao inaonekana wazi kuwa ni nzuri. kwa nini tuonge vibaya juu yao? Je hii mazungumzo au mafundisho jinsi inavyoitwa ni ya kujenga au kubomoa ama ni ya kujionyesha ya kwamba sisi ndiyo tunajua Biblia? Wakristo tujifunze kuwapenda wenzetu wanaofanya kazi ya Mungu. Tuko na vipawa tofauti na kila mmoja ajifunze kukimbia katika leni yake.

 3. Ni vizuri kwasababu hata YESU alimwuliza yule pepo wa Wagerasi kuwa anaitwa nani naye akasema kuwa yeye na jeshi.

 4. Yeremia 33:3
  Mtoto anapomwita Baba yake kuwa hatari imetokea si lazima ataje hatari ile jina lake bali kama mtoto anajuwa hatari akiitaja itamfanya baba echukuwe hatuwa inayofanana na hitaji la Mtoto wake
  Yeremia 6:12

  kwa kuwa vita vyetu ni juu ya mamlaka ya nguvu za giza hivyo kila pepo hataliwe na jina zuri kiasi gani tunazijumlasha pamoja kama mamlaka ya nguvu za giza,

  Isaya 44:26
  Mungu analiangalia Neno la mtumishi wake apatekulitimiza
  Yeremia 12:1 analiangalia neno apate kulitimiza na siyo jina la malaika wala jini wala la anayekema bali analiangalia neno lake, tena Neno lake, baada ya kuchangia kidogo kile nilichokikuta mezani Basi,

  Amani iwe pamoja nanyi Ndugu zangu na mimi ninatanguliza shukrani zangu hapa mahali, zaidi tujaribu kuwaalika wengi waweze kujifuza kila inapoitwa leo, mimi ni mgeni ni mara yangu ya pili kufika hapa mahali na nimepapende sana kupitia watu wastarabu kama ninyi,nawashukru wote wale wenye nia njema na mapenzi mema na blog hii na hata wasiyona mapenzi mema pia nawashukuru kwakuwa kupitia wao tunaweza kujifuza jisi ibilisi anawatumia watu bila ya wao kupenda
  yote yaliyo ongelewa hapa juu ni elimu kwanamna moja au nyingine kwakuwa hata anayepinga jambo flani basi analo jibu tofauti ni vema tukalisikia jibu lake,

  Nisemekuwa kujuwa majina ya malaika ni jambo zuri bala na majini nao walikuwa malaika walio muasi Mumgu japo kuna mengine niyakutengeneza,
  sasa basi unapopambana vita ni vizuri ukamjuwa adui yako, anaitwa nani au amekaa maeneo gani, kukurahisishia wewe siyo Bwana Yesu kwakuwa bwana Yesu yeye kupitia wewe umetaja jina hujataja wewe ukiwa na uhalali wakulitumia jina la Yesu Pepo la aina yeyote linatoka, uhalali ninaouongelea hapa ni kwanza 1 mwamini Yesu kristo kwa Moyo wako wote 2 mkuri kwa kinywa chako,
  ukubali kubatiza kwa maji mengi na kwa Roho mtakatifu,
  ndipo utumie jina la Yesu kristo kukemea pepo,

 5. “Nakuamuru pepo mtoke mtu huyu” haya ni maneno ya Yesu akikemea pepo. Ni wazi Yesu alifahamu majina,tabia na kazi za majini lakini hakuona haja ya kutaja kwa majina. Hivyo wanadamu leo tunapofanya kazi kama kristo alivyofanya tutapata baraka. Na isitoshe kujua jina na kazi ya shetani haina mchango kiroho kwani hatuongezewi heri kwa kuwa na elimu ya majini. Ni heri tumfahamu Mungu aliyepo upande wetu,BWANA na mkombozi wetu.
  Kwa hiyo wale wanaonufaika na shetani ni lazima wajifunze na kuwafahamu majini na majina yake ili kurahisisha upatikanaji wao pindi wanahitaji kusaidiwa.
  Ombi letu daima liwe ” utuokoe na yule Mwovu”.

 6. lazima upate kumtambua pepo kwa jina vinginevyo unaweza kukesha naye.

  YESU alipokutana na yule kijana aliyekuwa amepagawa na pepo kwa muda mrefu, aliuliza jina lako ni nani?

  mapepo yakasema mimi ni jeshi maana tu wengi.

  mr shoo naomba utambua hilo iliupate kumpinga shetani na malaika wake.

 7. Shalomu,

  Katika mchango wangu wa tarehe 18/06 niliuliza maswali kadhaa kwa dada Josephine, ningefurahi sana kama dada Josephine au mwingine mwenye ujuzi wa hayo mambo angenijibu maswali hayo ili mimi pamoja na wasomaji wengine tuweze kupata ufafanuzi.

  Shalomu

 8. Shalom,Levina nashukuru kwa kujitahidi kunielewesha,kutokana na maelezo yako nakubaliana na wewe kuwa unaweza kukemea kwa kutaja aina ya pepo au spirit yoyote inayomsumbua mtu.Lakini yote kwa yote JINA LA YESU linatosha hata tusipotaja aina ya pepo ingawa ukilitambua na kulitaja ni vema pia.Asante,barikiwa

 9. Binafsi mimi nimemuelewa Josephine, ni kweli watu tumejaliwa neema tofauti tofauti, kuna wengine kwa kumuangalia mtu Roho Mtakatifu hukufunilia jinsi gani alivyo. Kuna wenye Karama mbali mbali za Rohoni kama Neno la Maarifa nk nk. Mungu anawapa watu tofauti tofauti kama apendevya yeye!

  Kuhusu suala la mapepo, pia, kuna wengine wanafahamu siri za wachawi na waganga,kwa neema! lakini wengi wa namna hii waliteswa na shetani kabla ya kuja kwa Yesu! baada ya kuokolewa anatambua huyu aliye ndani ya mtu huyo ni pepo fulani! hukemea kwa Jina la Yesu na huyo mtu husema yote kwamba yeye ni nani na kusema siri zote kwa maana nguvu za giza huogopa na kutetemeka wasikiapo Jina la Yesu. Kama ilivyotokea kwa yule mwenye pepo mchafu Yesu aliyemtoa ng’ambo ya bahari Marko 5:1-18. Yesu alimuuliza Jina lako nani? Akamjibu. jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi!

  Wengi wanaofahamu majina ya mapepo sio kwamba wamejifunza chuo au shetani kawafundisha, pepo wenyewe hujisema. Pia jaribu kumtafuta aliyeokoka lakini aliteswa zamani na nguvu za giza alipokua kwenye ufalme wa giza, Mungu amewapa neema hii kwenye ufalme wa Nuru! au tujaribu kumuuliza dada Josephine yawezekana ana ushuhuda juu ya nguvu za giza! na sitashangaa ndio maana anasema hayo! SHALOM

 10. Shalomu,

  Tusalimiane kwa Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

  Nimesoma hoja za dada Josephine, zimeniacha na maswali mengi sana. Swali kubwa nililo nalo ni kuwa dada yangu hakutumia maandiko katika michango yote mitatu, na hii ndiyo inayonipa shida mimi kiasi cha kutaka kupata ufahamu zaidi.

  Dada Josephine katika mchango wake wa awali amezungumzia kupata siri kutoka kwa wachawi wanaookoka na ndipo kupata ufahamu juu ya elimu ya mapepo na majina yao. Aidha amezungumzia ulemavu kuwa nayo ni mapepo.

  Kwa mtizamo wangu ningefurahi sana Dada Josephine akitupatia maandiko yenye kukaza hoja ya kujifunza na kupata maarifa kutokana na wachawi na shetani. Binafsi niliwahi kusikiliza shuhuda za wachawi miaka ya nyuma kidogo na baada ya hapo nikazichukia. Mfano kila aliyekuwa mchawi atakwambia mimi nilikuwa mchawi namba moja Tanzania, sasa namba mbili alikuwa nani? Nikagundua hiyo nayo ni hila lakini pia biblia imesema wazi kuwa shetani ni mwongo na si mwongo tu bali ni baba wa huo. Vilevile, neno halijanipa fursa ya kumsikiliza shetani, bali kumsikiliza Mungu na kumkaribia Yeye. (Yakobo 4:7,8)

  Kuhusiana na ulemavu, mimi nadhani si sahihi kusema kila kiziwi, kiwete, kipofu, bubu n.k. ni pepo. Inawezekana mtu akawa na ulemavu kwa sababu ya nguvu za giza (pepo), lakini si ulemavu wote ni pepo. Yohana 9 mistari ya mwanzo kabisa inaeleza kuwa wengine wanakuwa walemavu ili tu kusudi la Mungu litimie. Napenda tukumbuke kuwa kuna watu hawapati watoto kwa sababu ya pepo na kuna wengine ni mapenzi ya Mungu kama ilivyokuwa kwa Sara, Leya, Mama yake Yohana n.k. Musa alikuwa na ulimi mzito (tunaweza kusema alikuwa na kigugumizi (Kutoka 4:10) lakini haikuwa pepo. Katika Kutoka hiyo 4:11 Mungu anamwuliza Musa kuwa ni nani afanyaye mtu kuwa bubu, kiziwi, kipofu? Naomba dada yangu Josephine, kama bado unasisitiza hoja yako basi utupe maandiko kuwa ulemavu ni pepo nasi tutajifunza na kufunguka.

  Katika mchango wako wa pili na watatu umezungumzia Yohana 14:12 kuhusu kufanya kazi kubwa kuliko zile alizozifanya Yesu, ninajiuliza, hivi kujua jina la pepo ndiyo kazi kubwa kuliko aliyoifanya Yesu? Hivi tunataka kusema kuwa Yesu hakuwa anajua majina ya mapepo?

  Katika mchango wako wa tatu umezungumzia pia mambo yafuatayo:-

  Shetani hawezi kukudanganya kwasababu una Yesu, Ni kweli shetani hawezi lakini kwa nini utake kujifunza kwa shetani, kusikiliza aliyekuwa mchawi akielezea namna wanavyofanya uchawi inakusadia nini wakati wewe ni mtu wa nuruni na si wa gizani. Kama tunataka kujifunza jinsi mchawi alivyokuwa anaroga kabla ya kuokoka, je itakuwa sahihi kujifunza na mwizi alivyokuwa anaiba, mzinzi alivyokuwa anazini, tapeli alivyokuwa anatapeli….? Haya tukishajifunza hayo yote ili iweje? Huoni kuwa watu wanapenda kusikiliza uchawi kwa sababu ni kama mazingaombwe?

  Hivi neno la Mungu linasema nini juu ya sisi watu tuliookoka kupata maarifa? Nadhani sisi tunapata maarifa kwa kujifunza neno la Mungu na kumsikiliza Roho Mtakatifu. Hivi huo muda wa kusikiliza uchawi kwa nini tusiutumie kujifunza neno la Mungu? Namkumbuka mtu mmoja alisema kuwa sisi watu tuliookoka tumeathiriwa na kukaa na shetani muda mrefu kabla ya kuokoka ndiyo maana tunapenda kuendelea kusikiliza habari zake hata baada ya kuokoka kuliko kutafuta habari za Mungu.

  Umesema Yesu alisema kuwa dunia itajazwa maarifa, inawezekana kweli alisema, lakini maarifa hayo ni ya kujua jina la pepo? na je dunia kujaa maarifa kuna tafsiri gani kwa kanisa la leo?

  Umesema mtu anakuwa kihatua mpaka pazia la macho linaondolewa anaweza kuona kwa macho ya nyama vile visivyoonekana kwa macho ya nyama, naomba kujua kama katika maelezo haya ulikuwa unamaanisha karama ya kupambanua roho kama ilivyoandikwa kwenye 1Wakorintho 12:11.

  Umezungumzia jambo jingine kuwa unaweza kumuamuru Malaika kwa Jina la Yesu aje kwako na akaja, nitaomba pia unisaidie maandiko yanayompa mwana wa Mungu mamlaka ya kuamuru malaika kufanya kama huyo mtu wanavyotaka.

  Pia umezungumzia juu ya kuungana na malaika Mikaeli kuvunja kazi za Ibilisi, hili nalo nitafurahi kama utatusaidia kwa maandiko. Ila ninavyofahamu mimi, aliyeweza kuzivunja kazi ya shetani ni Yesu pekee yake (1Yohana 3:8), hata hivyo nitafurahi kupata ujuzi wa jambo hili.

  Kitu kingine umezungumzia kuwa hatua ya kujua shetani jina ni hatua kubwa kiroho, inawezekana, lakini Waefeso 4: 13 inapozungumzia mtu kukua kiwango cha kiroho inasema ni kwa kumfahamu sana mwana wa Mungu ndiko kunatupa kupanda cheo. Kama una maandiko yenye kuonyesha kuwa tunaongezeka viwango kwa kuyajua majina ya mashetani, basi nitaomba unisaidie.

  Dada Josephine labda nieleze kwa nini nimehitaji maandiko. Kila kitu tunachokijifunza kuhusu elimu ya Mungu ni lazima kitokane na neno la Mungu ambalo ni Biblia. Hivyo ili tuweze kujifunza na kupata ufahamu wa kutosha ni lazima tuwe na neno la Mungu linalotuongoza.

  Mungu akubariki Dada Josephine na tuendelee kujifunza.

  Shalomu!

 11. Mimi nakuunga mkono Dada Josephin .namsaidia kujibu swali aliloulizwa na MARY.kama upo na Yesu hakuna gumu unaweza kujua tu ila kila mtu ananafasi yake kwa Yesu inategemea unavyojitoa.kukemea pepo ikiwa umejaliwa kulijua au watu wanateswa sana na pepo mahaba waweza unapoombea hasa wanapokuwa wengi labda kanisani waweza kutamka maana hapa kwetu tz kuna aina ya mapepo hayo na yanajulika na .sasa basi unaweza tu kuamru pepo makata,pepo subiani pepo maimuna pepo kiziwi pepo bubu pepo masikini pepo la uwongo na kadhalika kwa jina la Yesu.bye bye.muhimu:KWA YESU HAKUNA KUBAHATISHA HATA KIDOGO .kama ni pepo la ushoga utalijua tu likiwa kwa mvulana anaanza kusuka nywele utalitambua tu huku ndani kuna pepo la aina hiyo.unaliumbua tu pepo la ushoga na kujichubua ngozi toka kwa jina la Yesu maana ukisema pepo tu na tabia zake limekuonyesha linafikili hujalijua unaliumbua mpaka linasema siwezi kujificha kumbe nimetambulikana.amani wapendwa mada nzito kidogo.

 12. Mimi naona niache maana hatupo kubishana bali kufundishana ,ninachojua kila mtu anasehemu yake katika mwili wa kristo cha muhimu maadamu pepo amtoke mtu awe inje ya mwana wa Mungu. maadamu kila tunapotamka jiwe letu la kuvunja liwe ni jina la Yesu sioni vibaya kukemea pepo mahaba toka kwa jina la Yesu ikiwa huyo mpendwa amesema nasumbuliwa na zinaa, au sioni vibaya kwa mtu aliyekuwa mganga ninapomhudumia ili afunguliwe anaporipuka mwingine anasema mimi paka ninamuamuru pepo uliyejivisha sura ya paka toka. ila muwe na amani tele mimi inatosha.na juwa safari yetu wote ni kwenda mbinguni ,na katika mwili kuna kila kiungo kikibwa kwa kidogo.vikiungana vyote vinakuwa mwili moja tu.kila mmoja amepewa huduma yake kwa kristo.

 13. Josephine nimevutiwa unavyojitahidi kuurgue,lakini napata wasiwasi juu ya kukemea pepo kwa kutaja majina,tutapataje uhakika kuwa sasa napambana na makata or maimuna?mimi naungana na Shoo na Steve kuwa ni vema tukakemea pepo kwa kulitaja Jina la Yesu kwani lenyewe tukilitaja kwa kumaanisha na kuzingatia maandiko linatosha kutoa pepo bila kujali ni aina gani ya pepo au linatajwa kwa jina gani.stay blessed

 14. Swali sasa mkibana hapo yako wapi yale mambo makubwa mnayofanya zaidi ya Yesuuuuuuuuuuuuuuuuuuu? Yesu alisema mtafanya mambo makubwa na mbona hamvuki zaidi? na Yesu anasema dunia hii itajazwa maarifa? sasa maarifa yamezidi mpaka tunatambua hata aina ya pepo linalouwa tumejua mpaka jina lake.ndio maana tunaweza kutamka pepo makata muache mtu huyu kwa jina la Yesu macho ya rohoni yamefunguka kiasi kwamba hata mgojwa akija unaweza kumwambia wewe unasumbuliwa na kitu fulani sasa ikiwapazia la macho limetoka umeanza kuona visivyoonekana kwa macho ya rohoni umevuka kuona kwa macho ya nyama utaanza kutamka pepo uliyeka mguuni toka kwa jina la yesu umeona na macho ya ndani si utashangaa? ndio pale unapoanza kushugulikia tatizo bila kukemea tu.Yesu anaouweza juu ya viumbe vyote kutaja jina la pepo sio elimu mpya,saa nyingine Mungu anakuonyesha adui mpaka jina lake si ajabu,kujua majina unaweza sio kuwa ndio umefundishwa na shetani shetani ni muongo kweli lakini unafikiri kama una Yesu anaishi ndani yako atathubutu kukudanganya? labda uwe huna Yesu atakupata.tulikuwa hatujaokoka tabia za zamani tumeziacha lakini mtu akiwa na hizi tabia tunaweza kumuombea kwa jina la Yesu uwongo ng’oka,sio pepo inategemea roho anavyokufundisha saa hiyo kuomba.si wote tuna Roho Mtakatifu anayetufundisha kuomba?

  Kaka Shoo si vibaya naweza kuamuru malaika mlinzi njoo katika jina la Yesu au malaika wa vita katika jina la Yesu ninaamuru kila kilichopagwa maishani mwangu kivunjwe kwa jina la Yesu.vile vile naweza kutamka katika jina la Yesu naungana na malaika mikaeli kuvunja kazi za shetani sio vibaya inategemea Roho atakavyoniongoza kutamka.

 15. Ahsante dada Josephine.
  Lakini haya unayosema siyo majina bali ni sifa au tabia za huyom pepo mwenye jina fulani. Naomba nikupe mfano kwa upande wa Ufalme wa Nuru. Malaika Mikaeli ana sifa, kazi au tabia ya kupigana vita na kulinda wana wa Mungu. Soma Ufunuo 12:7, Daniel 12:1 na Daniel 10. JINA ni Mikaeli sifa zake ni Malaika wa vita na ulinzi. Nikuulize dada Josephine ni sahihi kusema huyu malaika jina lake ni Malaika wa Vita au Malaika wa ulinzi. Pia, mtoto mmoja ana tabia ya wizi lakini ana jina lake, labda anaitwa ‘Ruka’, huwezi kusema huyu mtoto jina lake ni Mwizi.

  Kukemea malaika kwa kutaja sifa yake mfano kama Yesu alivyosema “Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, usimwingie tena!” Marko.9:25, kwangu sina shida nako, tatizo linalonisumbua ni majina kama yaliyotajwa na ndugu Steve M hapo juu. Tuendelee kufundishana katika PENDO LA KRISTO. YESU AKUBARIKI

 16. Dada Josephine,
  Nina swali napenda kujua.
  Yesu alisema shetani ni baba wa uongo, na hamna kweli ndani yake. Sasa basi, utajuaje kuwa pepo lilio ndani ya mtu huyo ni Makata, au maimuna? Pili una hakika gani kama kuna Pepo linaitwa Makata, maana hata hayo majina yametoka kwa shetani mwenyewe.

  Kwa hiyo,Mimi naona ni vema tukaiga mfano wa Yesu mwenyewe. Pepo kiziwi huja na uziwi na Pepo kichaa huja na kichaa. Basi ni vema tukafanya kama Yesu alivyofanya. Hakutumia Elimu ya waMisri au Warumi au Wapagani wa kipindi hicho. Kwa nini tutumie mavumbuzi yetu na neno liko wazi? Tunaishi nyakati za madanganyo mengi na salama yetu ni neno la Mungu tu!

 17. Nakushukuru kaka SHOO. Ila nikwambie kweli shetani ni muongo na tunajua isipo kuwa sisi tuliookolewa ambao tunae YESu ndani Tumejaliwa kuzijua siri zote zote ndio maana shetani hana lake ametekwa ukiwa na yesu utashuhudiwa kuwa huyu alilolisema anataka tu kupotosha lakini kama kweli Yesu yupo ndani yako ki sawa sawa hakika wewe utafanya mambo makubwa ambayo watu wanaosikia watawashwa utatumika si kawaida.ila kukemea pepo kwa kulitaja jina la hilo pepo si vibaya,Narudia tena kipofu ni jina ,bubu ni jina kiziwi ni jina maimuna ni jina kiwete ni jina makata ni jina hatuliabudu bali tunayang’oa yamtoke mtu huyo aliyepagawa kwa jina la Yesu.tunapotambua aina la pepo lililopo unaweza tu kuliamuru kwa jina lake toka ikiwa tu umelijua.kuna pepo la kutokuamini au la kukata tamaa unaweza kusema pepo la kukataa tamaa mtoke mtu huyu au pepo wakutoamini mtoke mtu huyu inategemea Roho Mtakatifu atakavyokuhakikishia tatizo alilonalo mtu.sio kuwa tunajifunza mafundisho ya mashetani ila ni yule anayeishi ndani yetu ndie anayejua yote maana yeye ndie muumbaji.ila kama wewe bado hujafikia hatua flani ndani ya Yesu huwezi kuamuru kwa majina maana bado yawezekana hujatambua aina ya pepo aliyeko ndani ya mtu .yote ni hatua hadi hatua.

 18. Josephine ahsante sana kwa mchango wako. Ila nina swali hili, Shetani ni baba wa uongo na ana hila nyingi, sio kila anachokisema ni kweli na akisema kweli yumkini huo ukweli una lengo la hila ya kudhoofisha wana wa Mungu. Kwa hiyo hata kama mtu ameokoka hapaswi kuyakumbuka mambo ya ufalme wa giza na kuyatumia katika ufalme wa NURU na haswa kwa kuwa kipindi hicho cha giza Neno la Mungu linasema alikuwa amekufa, sasa analetaje mambo ya ufu kwenye ufalme wa uzima? Nimeona mahojiano na mapepo yakileta shida nyingi katika Kanisa na jamii, pia wengi wanaoenda kwa wachawi wanaweza kukuchonganishwa na wazazi au ndugu zako wa karibu kwa kukuambia ndiyo chanzo cha matatizo yao, limeibuka wimbi la mafundisho juu ya uflme na idara zake unavyofanya kazi,ambayo ninakuwa na maswali juu yake Je! utajuaje hiki alichokisema pepo au mchawi ni ukweli, au ikiwa ni ukweli ana agenda gani ya hila ya kuteka fahamu au kupotosha wana wa Mungu?

  Katika kuangalia Neno la Mungu nimekutana na mistri hii Ufunuo.2:24, 1Timotheo 4:7 na 1Timotheo 4:1. Naomba tuitazame wote kupata uhakika wa nini Neno la Mungu linachozungunza.

  Ufunuo.2:24-25 Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo wengine wanayoyaita mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wo wote juu yenu): Lakini shikeni sana mlicho nacho, mpaka nitakapokuja.

  1Timotheo 4:11Roho anasema wazi wazi kwamba katika siku za mwisho watu wengine wataiacha imani yao na kusikiliza roho za udanganyifu na mafundisho ya mashetani.

  1Timotheo4:7 Usijishughulishe kamwe na hadithi za kipagani na masimulizi ya uongo ya wanawake wazee, badala yake, jizoeze kuwa mtauwa.

  NIMEJIFUNZA PIA KUWA MAFUNDISHO YAMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU TATU, AMBAZO NI

  1) MAFUNDISHO YA KIRISTO (2Yoh.1:9)
  Yanaitwa pia Mafundisho ya Kweli(1Tim.1:10); Mema
  (1Tim. 4:6); Sahihi(Tit.2:1); ya Bwana(Efe.6:4).

  2)MAFUNDISHO YA WANADAMU (Kol. 2:22)
  Yanaitwa pia Mafundisho ya dunia(Kol.2:8)

  3) MAFUNDISHO YA MASHETANI(1Tim.4:1)
  Yanaitwa pia Mafundisho ya kigeni(Ebr. 13:9); ya
  upotuvu(2Pet.2:1)

  HAYA NI KATIKA MCHAKATO WA KUTAMANI ROHO MTAKATIFU ANIFUNDISHE NA ATUFUNDISHE UKWELI WA NENO LA KRISTO JUU YA HOJA HII. AMANI YA KRISTO NA UNYENYEKEVU WA ROHO MTAKATIFU UTUSAIDIE SOTE KUJIFUNZA NA KUBADILIKA. AMINA

 19. kwanza kabisa mchawi anapookoka lazima atatoa hasara au siri za uchawi na atasema mbinu walizokuwa wanatumia,kama amesema mbinu aliyokuwa anatumia na akasema pepo linalotumika kuvuruga ndoa sioni ubaya kulitaja pepo fulani toka kwa jina la yesu.

  na tujue kuwa Yesu angali anafanya kazi maana yake mchawi au mfuga majini anapookoka na kusema zile siri na aina ya majina na kazi za hao mapepo na ukakumbana na mtu ambaye anataka kufa na unajua jini makata ndiyo bosi wa kuuwa si vibaya kumuamuru pepo makata toka kwa jina la Yesu,muache mtu huyu.maana hata kiziwi nia jina la pepo aliyeko ndani ya mtu,hata kipofu ni jina la pepo aliyeko ndani,hata kiwete ni jina la pepo lililoko ndani,sasa tunapopambana na wale waliojishughulisha na uchawi na wakasema kuwa wanatumia jini fulani kuvuruga ndoa au kuua au kumfanya mtu aachishwe kazi tayari wewe kwa sababu Yesu ameamua kuwaumbua wachawi tunajua hata majina ya mapepo wanayotumia bila shaka ukikumbana na mtu mwenye shida ya aina hiyo waweza kumwamuru pepo mahaba toka kwa jina la Yesu maana umeshajua ana pepo mahaba ndio lipo ndani ya yule mgojwa hata hivyo Roho Mtakatifu atakushuhudia pepo lililopo ndani kama ni ukahaba au mzimu na nk..tujuwe hii dunia itajazwa maarifa kupita kiasi na shetani hatakuwa na nafasi tena maana kila siri yake itakuwa dhahili.sio kwamba wana wa Mungu wanajifunza majina ya majini ila shetani anasema mwenyewe maana ameshatekwa tayari, Ninawapenda wote hakuna anayejifunza majina ya majini ila shetani na mbinu zake ametekwa mambo yake yapo wazi.

 20. 1. Inakuwaje wana wa Mungu wanafahamu majina ya malaika wachache sana kwenye ufalme Nuru huku wakiwa na orodha ndefu ya majina ya majini/mapepo walio katika ufalme wa Giza, yaani upande wa adui?

  Huo ni uvivu wa kufanya assignment zao za kujifunza neno la Mungu. Kama mtu akiwa anafahamu kuwa ana mamlaka juu ya nguvu za giza, hatahitaji kujua majina ya mapepo. Mimi binafsi kwa mfano, huwa na shauku ya Kujua majina ya Malaika na viumbe mbalimbali wa Mbinguni kama Maserafi, Makerubi, wazee 24, Wenye uhai 4, Utendaji wa malaika mbalimbali, Mikaeli, Gabrieli, Yule Malaika wa Bwana (The angel of the Lord) n.k

  Kujua majina ya mapepo sio tatizo. Mfano, kwa kuishi na watu wa imani mbalimbali nafahamu kuwa wanaamini majini kama Makata, Maimuna n.k. Lakini siwezi kujifunza kutoka kwao. Katika maisha yangu sijawahi kukemea pepo kwa Jina (Kama Makata au Maimuna), maana hata sijui Maiuna likoje au Makata liko vipi. Mimi ninachojua yote ni mapepo, na ninapoamuru “pepo mtoke fulani kwa jina la Yesu” Lazima litii.

  2. Wanaoyataja majina hayo ya mapepo/majini Elimu hiyo wameipata wapi?
  Jibu la moja kwa moja ni kwa Kambi ya adui! Jini Makata, Maimuna nk yanapatikana kwa waislamu. Huwezi sema umejifunza kwa Biblia, NO! Ni kwa adui tu!

  3. Je, Ni sahihi kutafuta majina ya majini/mapepo na ya malaika wa Nuru toka chanzo chochote? O yeah, ni sahihi kabisa. LAKINI chanzo hicho ni kimoja tu, Neno la Mungu na si vinginevyo! Kama kwenye Biblia kuna Makata, fine, kemea kwa jina hilo.

  Unajua wapendwa, Lazima ifike mahali tufuate mfano wa Kristo, na huo ndio Ukristo. yesu hakusema Jini Makata nakuamuru mtoke huyu, bali alisema “Pepo Bubu na Kiziwi” na maneno yafananayo na haya.

  Siku zote napenda usemi huu “Tuifanye kazi ya Bwana, kwa namna ya Bwana atakavyo” (Do God’s work in God’s way)

 21. Nashukuru kwa mchango wako wako Isaack.

  1) Quotation uliyofanya Yesu alipojaribiwa na akanukuu Bible unataka kuniambia kuwa nasi tunapaswa kujifunza elimu za kishetani au kusoma mafundisho ya mashetani ili tunukuu tunapopambana na shetani? Nieleweshe zaidi p’se.

  2) Nisaidie pia hapa; ikiwa mtu alikuwa mchawi na kisha akakutana na Yesu akaokoka, anaweza kutumia sehemu ya elimu au mbinu alizokuwa nazo kabla hajaokoka kupambana na mapepo? Naomba unisaidie kwani binafsi ninapata shida na kujiuliza maswali mengi ninapokutana na mafundisho yenye msingi wa yale waliyokuwa wakiamini kabla hawajaokoka juu ya mapepo na ufalme wa giza. I need to be free, but let our center of discussion be the Word of God. Naomba ujibu pia maswali mengine yaliyoulizwa ukijaribu kuonyesha positive impact and negative impact of these teachings.

  Thank you for your contribution.

 22. kuomba kwakukemea mapepo kwa majina mimi sioni shida yoyote and I can’t really critise that

  cauz even the devil when he came to tempt Jesus he referred back to what is written in the book of psalms
  saying ….”IT IS WRITTEN” that He shall sent His Angel to come to your rescue so that you don’t hit your foot on the rock. that was to assure Jesus what he was saying was right.(I’m just trying to make a point here)

  Of course this does not surprise coz who knows, maybe before knowing Jesus the person might have been partners with demons and so knowing their names and knowing what they do, i’m sure even it’s you, you’d like to curse them by names

  hope u’ve got my point.
  be blessed all of you

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s