Sifa Za Mke Mwema

Kitabu cha mithali 31 kuanzia msitari wa 10 hadi 31 kimeelezea sifa mbalimbali za mke mwema, tuangalie kwa uchache sifa hizo kwa kuzichambua katika maeneo tofauti.

 1. Imani

Mithali 31:26, 29, 30

Mke mwema anayashika na kuyafanyia kazi maneno ya Mungu na ni mtu ambaye anamtumikia Mungu kwa moyo wake wote na akili yake yote. Anatafuta makusudi ya Mungu katika maisha yake na kuyafuata. Zaburi 119;15

 2. Ndoa

Mithali 31:11-12, 23, 28

Mke mwema humuheshimu mume wake na anahakikisha anamtendea mambo mema siku zote za maisha yake. Ni wa kuaminika na msaidizi kwa mume wake. Efeso 5:22-24, 1Petro 3

 3. Malezi

Mithali 31: 26, 28

Mke mwema anawafundisha watoto wake njia za Mungu na pia anawatunza kwa upendo. Huwafundisha kwa hekima na kuwaelekeza njia iwapasayo kuiendea. Mithali 22:6

 4. Huduma

Mithali 31:12-15, 17, 20

Mke mwema anamhudumia mume wake na familia yake yote kwa ukarimu na upendo. Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora na chenye afya. Ni mtu mwenye huruma na ukarimu.

 5. Mali

Mithali 31:14, 16, 18

Mke mwema anatafuta kwanza ushauri wa mumewe kabla ya kutumia fedha na pia anafanya manunuzi kwa hekima. Ni muangalifu kununua bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji ya familia yake.Efeso 5:23

 6. Nyumba

Mithali 31:15, 20-22, 27

Mke mwema ni mtu anayeifanya nyumba iwe mahali pa kuishi. Anatengeneza mazingira ya kuvutia kwa familia yake na wageni wote na anawahudumia watu wake wote kwa ukarimu. 1pet 4:9, Ebrania 13:2

 7. Muda

Mithali 31:13, 19, 27

Hutumia muda wake vizuri na kuhakikisha anakamilisha kazi zake za kila siku. Kamwe hapotezi muda katika kufanya mambo ambayo hayampendezi Mungu na yasiyo na faida.

 8. Uzuri / Urembo

Mithali 31:10, 21-22, 24

Ni mrembo na mwenye thamani, ana uzuri wa ndani unatoka kwa Yesu Kristo. Anatumia ubunifu wake na utanashati wake kuleta uzuri katika maisha yake na ya watu wake.

Mungu atusaidie ili maisha yetu yaonyeshe kweli tunamjua na kumwamini yeye.

 Ubarikiwe na Bwana Yesu!

Kutoka www.womenofchrist.wordpress.com

Advertisements

12 thoughts on “Sifa Za Mke Mwema

 1. Niombeeni wapendwa nimpate Mume mwema mweye hofu ya mungu umri unazidi kusonga mbele.
  pia baabda ya kuokoka nimeota nimevikwa sura ya kondoo ina maanisha nini. Nahitaji maombi yenu. Amen Mungu awabariki

 2. Ithank God for being alive! forme ithink we should allow God to be our decider,and let us follow his comandment-Amen Eph 5:1…

 3. wapendwa wa Mungu maoni yenu its so nice & help much to build a strong chistristianity family, na tumuombe sana Mungu wetu anayeishi atupe hekima yake kuu katika kufanya decisions wakati wa kutafute wenzi maana sio kaz rahisi kama watu tunavyochukulia. Mungu atusaidie

 4. I would love being one in the team of this website to equip myself in knowing God more and more

 5. jamani mimi nina kitendawili kikubwa, kuhusu kupata mke mwema. maana nikiangalia wenzangu sipati picha wanavyo juta kuoa/kuolewa. sasa nina umri wa kutosha kuoa lkn mpka nakata tamaa nahisi naweza kufa mapema naonba niombeeni nipate mke mwema si mchumba
  leons aron
  leonsaron@yahoo.com

 6. Mpendwa Faith ubarikiwe , mafundisho haya yanafaa sana kwenye kitchen party za mabinti sayuni.

  Mpendwa Exaud; Usife moyo , Yohana 15:16 Yesu anasema ” si ninyi mlionichagua mimi,bali ni mimi niliewachagua ninyi…..”na Yohana 6:44 Yesu anasema “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba aliyenipeleka…..” tayari Yesu amekuchagua,chukua hatua kwanza mwambie Yesu aondoe huo uzito wa moyo,kisha uwe na ujasiri kwenda kwa mtumishi/mtu wa Mungu yeyote aliye karibu nawe kwa hatua inaoyofuata .MUNGU AKUTIE NGUVU.

 7. Ndg. Exaud,

  Inatia moyo kukusikia kwamba unapenda sana kuokoka! Hili ni jambo muhimu sana unalolihitaji sasa ktk maisha yako kuliko kitu kingine!(utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa). Pia Biblia ktk Ebrania 4:7 inasema ..leo kama mtasikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.

  Moyo wako kuwa mzito ni kwasababu umekuwa ukiishi maisha ya mwilini (nje ya uwepo wa Mungu) na sasa unatamani kuishi maisha ya kiroho, ndio maana kuna mvutano huo, Gal 5;16-17 .. kwasababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili, kwa maana hizi zimepingana hata hamwezi kufanya mnayotaka.

  Hata hivyo NEEMA YA MUNGU INATOSHA kukutoa ktk hali hiyo!

  Pia elewa kuwa ufunguapo moyo wako kwake yeye ataingia na kukubadilisha, na hapo ndipo unapata uwezo wa kuushinda mwili kwani unageuzwa kwa kufanywa upya nia zako. Ninachokusihi ni kuitii sauti inayokutaka umrudie Mungu, ujitoe kabisa na kumkabidhi Bwana Yesu maisha yako ili yeye ndiye ayatawale. Rum 12:1-2

  kumbuka wakati uliokubalika ndio huu na saa ya Wokovu ni sasa!
  Mungu akusaidie kufikia uamuzi mzuri na muhimu utakao kuweka mahali salama, Mungu akubariki.

 8. Mungu wetu apewe sifa mimi nina mchumba na nimezaa naye nje ya ndoa, naomba maombi yenu ili nifunge naye ndoa lakini sijaokoka ila napenda sana kuokoka sijui kwanini moyo wangu unakuwa mzito.

 9. Hellow Watakatifu wa Mungu!!

  Nimebarikiwa sana na Mith 31 Jinsi inavyotupa sifa za kiMungu katika kutengeneza familia nzuri. Kwa kweli sisi akina dada ambao tumeokolewa kabla hatujaolewa tuna bahati sana kuwa tuna nafasi ya kuweza kuzitengeneza ndoa zetu katika misingi imara yenye uongozi wa Mungu.

  Lazima tujitahidi kuwa tofauti na wale wa dunia, hakika ndoa na familia zetu zikajae upendo,heshima, uaminifu, usafi, lugha nzuri, subifa na ucha Mungu.

  Mimi namtukuza Mungu kunipa hii bahati, hakika Roho Mtakatifu atanisaidia, jamani mwanamke asipokuwa na hekima na busara nyumba haivleti fu hata kama baba atajitahidi vipi.

  Kuna tabia ambayo imezuka sasa nawasihi wapendwa wenzangu tujiepushe, hii hali ya kudai haki sawa inayoongozwa na akina mama ambao wao ndoa zao zimevunjika ni hatari sana.
  Tena utakuta akina dada ambao hawajaolewa nao wanavutwa na kuanza kuwa na viburi na kuogopesha wanaume sababu wanaanza kusema ‘sibabaishwi na mwanaume mimi,kama pesa ninazo’, halafu wakiona hawaolewi wanaanza kuvizia ndoa za wenzao ili waziharibu. Jamani ndoa ni jambo muhimu, ni sifa njema na baraka kwa mwanamke na ndiyo maana Mungu alilibariki. Akina dada tusioolewa ni bora tusidanganywe na walioshindwa bali tujifunze kwa waliofanikiwa na kupitia neno la Mungu.

  Hatuwezi kuwa juu ya wanaume hata kama tumejaliwa elimu zaidi, pesa au vyeo, hivyo vyote havikupi mamlaka ya kumtawala mume.Tusiongozwe na influence ambazo si za ki-Mungu, neno la Mungu ni package kamili katika kutuongoza.

  Tujikumbushe
  Waefeso 5;22
  ‘Enyi wake watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe……’

  Pia lazima tutambue hayo yote hayaji hivi hivi, tunatakiwa kulitendea kazi hilo neno kwa maombi ili hizo sifa zidhihirike kwetu. Tuwe wakarimu, wacheshi, wakweli wawazi na wasafi kiroho,kimazingira pia kimwili, sababu inaongeza mvuto na heshima.

  Mie kuna ndoa za kipendwa huwa zinanibariki, kina mama wakijibidisha katika kumcha Mungu na kuwajibika ipasavyo kwa waume, familia na jamii kwa ujumla, naamini na sisi pia tutaweza.

  Tuwe wanyenyekevu, wastahimilivu na kuchunga ndimi zetu, kuna wapendwa wanapenda kusimulia madhaifu ya waume zao na matatizo mengine kwa watu wa nje, hii tabia si nzuri kabisa, unamuaibisha na unaharibu sifa ya nyumba. Yesu ni rafiki yetu ni bora tumshirikisha ili azibe nyufa na kurekebisha pindi tatizo linapotokea.

  Mith 14
  ‘Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake mwenywe na mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe’

  Naamini kwa wale ambao tunatarajia kuolewa, tunaweza kuanza kuexercise hizo tabia kwa nguvu za Roho Mtakatifu na hata wale tunawatarajia watabarikiwa nasi na kwa uhakika tutaolewa na kowa na ndoa zenye furaha daima.
  Mungu awabariki

 10. mpendwa mtumishi wa Mungu john paul Mungu akubariki sana sana majibu yako katika maada nyingi yamekuwa msaada mkubwa wa majibu kwangu ubarikiwe sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s