Kwanini wengine hawapokei uponyaji?

Kati ya mambo aliyoagiza Bwana Yesu ni pamoja na kuombea wagonjwa nao wakapata afya; Mathayo 10:8, Mark 16:18.  Watu wengi wameponywa katika huduma za maombezi mbali mbali na shuhuda ziko nyingi na wengine wanaendelea kuponywa. Lakini katika watu wanaokwenda kuombewa si wote wanapokea uponyaji. Ni hali ya kawaida, kwa mfano, kundi la watu wenye aina fulani ya ugonjwa wakaitwa kwa ajili ya kuombewa lakini katika kundi hilo wengine hupokea uponyaji na wengine hawapokei.

Swali: Je, ni kwa nini wengine hupokea uponyaji halafu wengine wasipokee? Nini sababu za hali hii?

Advertisements

4 thoughts on “Kwanini wengine hawapokei uponyaji?

 1. super natural healing process- inaweza isifanyike mara nyingine kwa mtu anayeombewa, kwa sababu kama zifuatazo:
  -una mafundo tele kwenye moyo wako na watu ambayo hutaki kuwasamehe.( let it go)
  -pia uwe na imani unachokiomba na kukifukuzia kukipata ambacho ni uponyaji is real, na uamini kuwa umepokea.
  – ili kufanikisha hili zoezi lifanikiwe, ndio maana kuna kuwa na counselling kwanza hasa ya kupatana na watu au kutubu.
  -kuna wakati mwingine procees yote ya deliverance ifanyike ibilisi achimbwe na mzizi wake. hii ni pross ambayo inahitaji muda wa kutosha kuhoji na kutafuta ni mlango gani adui aliingilia.
  tusisahau kuwa usiposamehe mfereji unaziba, kwa ajili ya matakataka.

 2. Kwa nini wengine wanapokea uponyaji na wengine hawapokei!.

  Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mtu kutopokea uponyaji wakati wengine wenye shida kama yake wanapokea. Njia za Mungu si njia zetu, njia za Mungu ni za juu sana. Tunaloweza kufikiria sisi kuwa ndilo linaloweza kuwa, Mungu hafikirii hivyo. Kila njia ya Mungu huwa hivyo inavyoweza kuwa ili Mungu mwenyewe atukuzwe. Kwa ujumla kuna njia au sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha mtu kutokupokea uponyaji kutoka kwa Bwana.

  Nikianzia na mtu aliye katika imani kwa uthabiti, sababu mojawapo inayoweza kusababisha mtu wa namna hiyo kutopokea uponyaji mapema, ni ili ajaribiwe. Tunaweza kujifunza jambo kama hili kwa Ayubu, aliyepata mateso makubwa sana katika mwili wake na hata katika mali zake, japo alikuwa katika imani.

  Ayubu alipata majaribu hayo yote baada ya shetani kumshitakia kwa Mungu kuwa Ayubu anamcha Mungu kwa sababu ya hali yake kuwa nzuri katika kila eneo. Tunaona maongezi hayo kati ya Mungu na shetani katika, [Ayubu 1:09-12], Tunasoma, “Ndipo shetani akamjaribu BWANA na kusema, Je Ayubu huyo yu amcha BWANA bure?…..Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. BWANA akamwambia shetani, tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe [maneno yangu, yaani asimwue]. Basi shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.” Kilichoendelea, tukisoma mistari inayofuata tunaona ni mateso ya aina mbalimbali kwa Ayubu. Hapa Ayubu alipata majaribu japo alikuwa katika utakatifu wote. Kumbe tunaona kuwa Mungu huweza kuruhusu majaribu kwetu ya kutokutupa uponyaji tunaouhitaji, ili kutujaribu na kuona iwapo imani zetu ni thabiti au la, yaani kuona iwapo huyo tunayemwendea yaani Mungu kama tunamwamini.

  Dhahabu ili ikubalike kuwa kweli ni dhahabu hupimwa kwa kuchomwa katika moto mkali, iwapo ni madudu basi kwa moto huo madudu yote huungua, lakini iwapo ni dhahabu basi hubaki iking`aa zaidi. Nasi kama watu tuliookolewa tunapoletewa majaribu ya namna mbalimbali na kuyashinda basi ni matarajio ya Mungu kuwa imani yetu hung`aa au hukomaa zaidi. Katika 1Petro 1:6-7 tunasoma, “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima , mmehuzunishwa kwa MAJARIBU YA NAMNA MBALIMBALI, ili kwamba KUJARIBIWA KWA IMANI YENU, ambayo inathamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.” Yanapokuwa yanatokea majaribu kama haya, iwapo kweli tunashuhudiwa kuwa tupo katika imani kwa ukamilifu, basi tuzidi kuishindania imani yetu mwisho wake ni kama Ayubu; tutashinda na zaidi ya kushinda. [Yakobo 1:12], “Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima”

  Sababu nyingine inayoweza kumfanya mtu kutopokea muujiza wake ni yeye mwenyewe kutokuwa katika imani kwa uthabiti bali kuwa katika maovu, [Yakobo 1:13], “Mtu ajaribiwapo asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu,….” Ndiyo maana pia katika, [Isaya 59:1-2], tunasoma, “Tazama mkono, wa Bwana haukupunguka, hata asiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata asiweze kusikia; LAKINI MAOVU YENU yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeificha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Hivyo sababu mojawapo ya kutokujibiwa maombi inaweza kuwa ni maovu ya mtu. Jambo la msingi hapa pia, ni kujichunguza iwapo tupo katika imani kwa thabiti au la, na iwapo tutajiona kuwa tumepungua ni kuchukua hatua za kuhakikisha tunakaa katika kweli yote.

  Sababu nyingine inayoweza kumfanya mtu asipokee uponyaji au muujiza ni kutokutaka kukaa katika Neno. Watu wengi nyakati hizi wanataka Mungu afanye miujiza kwao, lakini hawataki kukaa katika Neno Lake. Wanataka waende tu katika maeneo yanayohubiri miujiza lakini hawataki kukaa huko ili wajifunze Neno na kukaa katika hilo. Mtu wa namna hii asidhani kuwa anaweza kupokea muujizi, wakati mwingine anaweza kupokea muujiza lakini hauwezi kudumu, Mungu ni mtakatifu, hivyo miujiza mbalimbali hudumu kwa walio watakatifu.

  Sababu nyingine inayoweza kusababisha mtu kutokupata muujiza ni, watumishi wa Mungu wenyewe wanaofanya kazi ya kuwapa Neno la imani wahusika. Mtumishi wa Mungu ili aweze kufanya miujiza, kwanza lazima yeye mwenyewe aishi maisha ya utakatifu haswa. Asipokuwa mtakatifu, Mungu mara nyingine huweza kuzuia uponyaji kwa muhusika ili mtumishi huyu ajiulize na ikiwezekana amtafute Mungu kwa bidii ili atumiwe. [Hosea 4:6], Tunasoma, “…..kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”. Hivyo Mungu wakati mwingine huzuia muujiza baada ya kuona muhusika yaani mtumishi haendi sawasawa na jinsi Mungu anavyotaka.

  Tunachoweza kujifunza hapa pia ni kwamba, Mungu hajali sana juu ya miili yetu hii yenye kuharibika na pia hajali sana mambo yetu ya duniani; bali anajali sana sisi kwenda mbinguni aliko yeye. Ndiyo maana hutumia njia mbali mbali ili kuwafanya watu yamkini wamjue Mungu na kuweza kuishi sawasawa na njia apendazo yeye.

  Kifupi, miujiza ni njia tu ya kuwavuta watu wamjue Yeye, lakini si kwamba kila atakayeenda kwake atapata uponyaji wa mwili na miujiza mingine, la hasha,bali kila mmoja atapokea kadiri Muumba wetu anavyopenda. Ndiyo maana wengi wetu tutakuwa mashahidi, unaweza kuona mtu anaweza kwenda leo leo katika maombezi tena kwa mara ya kwanza na anapokea siku hiyo hiyo muujiza wake wakati kuna mwingine mwenye tatizo kama hilo hilo, ambaye pia yupo katika imani katika kanisa hilo hilo, tena yuko siku nyingi, lakini hajapata muujiza kama huo.

  Tunachotakiwa watu wa Mungu tuliopata neema ya kumjua Kristo, ni kukaa katika Neno lake kwa ukamilifu na uaminifu wote kadiri inavyowezekana; kama Ayubu siku tusiyodhani nasi tutapokea muujiza wetu kutoka kwa Bwana. Tosipopokea muujiza, hatuna haja ya kujiumiza vichwa, zaidi sana tuhakikishe tupo katika imani kwa uthabiti ili tusikose yote mawili; duniani na mbinguni.

  Amani ya Kristo.

 3. I only got a few words to say
  kuto kupokea uponyaji inatokana na IMANI ya MGONJWA
  kama nina kumbuka viema Yesu kristo alipotaka kufanya chochote kwa mtu fulani ilitokana na imani yake. Mwana mama yule aliye gusa vazi la Yesu for example: alikua na determination combined together with FAITH na mpaka alipo gusa Yesu akamwambia “NENDA IMANI YAKO IMEKUPONYA”

  I’m not very good at keeping verses but i keep the words in the book or mark capter 6 read the whole verse na utaona jinsi gani Yesu alikosa kufanya miujiza na kuponya wa gonjwa kwasabbu ya ukosaji wa IMANI.

  Mfano mwingine mzuri ni wa kufufuka kwa Lazaro in John chapter 11:26 unaruka mpaka Verse 40 Usikie Jinsi gani IMANI is the ACTIVATION CODE for our miracles (I love to define faith in that way)

  GODBLESS

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s