Nisaidieni Ushauri

Mimi Mungu alinibariki nikapata mtoto ingawa katika njia isiyo sahihi lakini Mungu amenibariki, amenisamehe na sasa nimesimama katika wokovu nikimtazama Yehova. Kwa kweli sikupenda lakini nilijikuta nikizaa na mtu ambaye alishawahi kuoa. Huyu baba wa mtoto wangu na mkewe hawako katika maelewano, lakini mimi nimelijua Neno sitaki tena kuanguka dhambini. Amekuwa akinihudumia mimi na mtoto wangu lakini kwa imani yangu bado sio kibali cha yeye kuniona mimi kama mke wake.

Jambo jema zaidi ametokea mtu ambaye anataka kunioa, nami nimemshukuru Mungu kwa sababu naamini Mungu pia atatengeneza ndoa ya baba wa mtoto wangu ingawa mwenyewe hataki anasema mimi ndio mkewe. Naamini mimi pia nina haki ya kuwa na mume wangu, bila kugombana ama kuingilia nyumba ya mtu mwingine.

Naamini mawazo na maoni ya watu yatanisaidia kupata ujasiri wa kumueleza baba wa mtoto wangu na akanielewa bila kukorofishana ili nisiendelee kusababisha mwanangu kukosa kupata huduma kutoka kwa baba yake kwa sababu ya sisi wazazi wake kutofautiana.

Asante, mbarikiwe

–A.S–

Dar  es salaam

Advertisements

8 thoughts on “Nisaidieni Ushauri

 1. Manka Mtoto,

  Ushauri wako ulioandika kwa A.S ninakubaliana nao kwa sehemu kubwa isipokuwa kipengere cha IMANI. Ulichoandika kwenye mchango wako ni kwamba A.S asijali kuhusu kuokoka au kutokuokoka kwa huyo anayetaka kumuoa. Ninaheshimu kwamba nao ni ushauri lakini sidhani kama ni ushauri wenye kumtakia mema katika imani yake ya wokovu. Kwa sababu hiyo mimi siafiki kwamba asijali hali ya kiimani ya huyo mtu anayetaka kumuoa, kwa sababu si Kikristo na hata Neno la Mungu halitushauri kutokulizingatia jambo la Imani.

  Pamoja na kuwa anahitaji ushauri lakini mimi naona ni vema akapewa ushauri utakaomsaidia kumuongoza katika kweli na haki yote ya Mungu.

  Asante.

 2. A.S
  Mimi nadhani wewe ni jasiri sana, and i salute you for that, regarding the first commentator, sidhani ni haki wewe uache kuwasiliana na baba wa mtoto wako kwa vile u tegemezi, kwa sheria za nchi na kwa haki za mtoto, ni vema mkawasiliana kwa mipaka, ni vyema mtoto akajua huyo ni baba yake na hata ukiwa na kazi nzuri bado ana jukumu la kuchangia malezi kama baba usimnyime hilo kabisa, ninashukuru una mpango wa kuolewa na hata kama huyo kijana hajaokoka au ameokoka, ninadhani kwa nuru uliyo nayo mpaka akakupenda basi atafuata njia iliyo njema, mradi hujaanguka kwenye dhambi ya kuzini na mume wa mtu tena, kuonana kwa ajili ya matunzo ni kitu muhimu na kinamjenga mtoto kuwa hakuachwa , pia wanaokuuliza maswali kuwa ulikuwa unajua kama kaoa au la, hata kama ulijua yameshatokea sidhani kama ni jambo la kujadili, jambo la kujadili ni matunzo ya mtoto going forward na mipango yako ya ndoa kwa mwenzi wako, Mungu akutie nguvu sana, napenda sana ujasiri wako.

 3. Kama ndo hivyo dada yangu napenda kusema mambo mawili.Kwanza soma vizuri ushauri wa dada Rose hasa pale anapoongelea juu ya maisha tegemezi kwa huyo baba wa mtoto wako.Kama huna kitu cha kufanya ni vizuri ukatafuta ili ikusaidie kujifungua kidogokidogo toka kwa huyo mume wa mtu maana kwa kadri unavomtegemea ndivyo anavyozidi kupata nguvu.

  Pili,kabla haujaingia kwenye ndoa nyingine hakikisha mambo yote yanayokuhusu wewe na huyo mume wa mtu yametafutiwa ufumbuzi wa kudumu.Pia nilikuuliza kama huyu anaetaka kukuoa sasa ameokoka lakini hujasema kama ndio au la maana kama ameokoka na amekusudia kukuoa atakusaidia sana katika hili.Kwa hiyo ni muhimu kuyazungumza haya yote pamoja ili muwe huru na yote yatakayofuata baada ya ninyi kuchukua hatua ya kuoana.

  Mwisho,maamuzi yoyote yale utakayoyafanya kumbuka yana gharama zake.Usisahau kuwa huyo mkewe kama unavyosema mwenyewe bado ni mkewe na ana haki zote na hata akifanya jambo lolote ni ndani ya hiyo haki yake,hivyo namuomba Mungu baba akupe hekima ya namna utakavyopata suluhisho hasa kwa sababu utapata mashauri mengi juu ya hili.Sauti ya ndani isikilize sana.

 4. Sasa dada yetu mpendwa hujatueleza mchumba uliyempata ameokoka kama hajaokoka mueleze maana ya wokovu ili ampokee Yesu ili muishi katika ndoa ya amani. Lingine je unafanya shughuli gani?

 5. Napenda kujibu maswali mliouliza. Kaka Petro na Raphael. Wakati tuna uhusiano na baba wa mtoto wangu sikufahamu kama ameoa nilikuwa sifahamu hadi nilipopata ujauzito. Mimi siku zote baada ya hapo nimekuwa nikipinga tena kuwa na uhusiano naye, kwa sababu hata kama hawaelewani na mkewe bado ni mkewe na sina kibali cha kuingilia ndoa ya mtu mwingine. Pili huyo anayetaka kunioa, anafahamu nina mtoto.

 6. Mpendwa pole kwa yaliyokupata,bado hata katika hayo Mungu anakuwazia mema.Usikate tamaa.Nina maswali machache yatakayoweza kunisaidia kutoa ushauri wangu juu ya hili.

  Kwanza,kabla hujazaa na huyo mume wa mtu ulijua au alikwambia kuwa ana mke au alikuficha?

  Kama ulijua kuwa ana mke,je mlikubaliana juu ya nini kitafuata baada ya kupata mtoto? kwa mfano,mlikubaliana mipaka ya uhusiano wenu ilihali yeye ana mke?

  pia huyu kaka anaetaka kukuoa anajua kuwa wewe una mtoto wa mtu mwingine na kuwa huyo mtu mwingine anakusema wewe kuwa ndo mkewe?

  Kama anavyosema ndugu yangu Petro,kama huyu anaetaka kukuoa hajaokoka usikubali bali zaidi ya kuto kukubali ni muhimu ukajua na kutafakari tukio la kwanza lilitokeaje kabla hujazama katika huyu wa pili.Kumbuka siku zote za maisha yako kuwa ni rahisi kupanda juu ya mti kuliko kushuka.

 7. Ushauri wangu ni kuwa huyo uleizaa naye bado ana mke hata kama hawaelewani. Ukimkubalia ujue unazini. Huyo mwingine ambaye yuko tayari kukuoa na hana mke, huyo ni sawa akikuoa.Lakini je ameokoka? Kama hajaokoka usikubali.

 8. Shalom mpendwa, pole na matatizo kama unavyoyaita.
  Namshukuru Mungu kwamba umeweza kuokoka na kuondoka kwenye huo uhusiano na mme wa mtu. Kinachokufanya wewe uendelee kuitwa mke ni hayo matunzo unayopokea, je una kazi? au hata biashara? Kama huna jaribu kumwomba Mungu akupe wazo la kujitegemea ili usihitaji kabisa kuwa na mahusiano na huyo mtu. Ukipata wazo hilo jaribu taratibu kuanza kutomtegemea huyo baba mtoto, pia mjulishe hali ilivyo huyo mwenza mpya akushauri jinsi ya wewe kumlea huyo mtoto bila kuwa na contact kila siku na huyo mume wa zamani. hakikisha umemaliza kabisa hayo matatizo ya kuitwa mke wa mtu mwingine kwa kumtegemea matunzo kabla hujaolewa la sivyo huko uendako unapeleka balaa kubwa kwani mumeo hawezi mvumilia mtu anayekuja kwenu na kukuita mke kisa analeta matunzo. Mungu ni Baba wa yatima na wajane amini kuwa ataweza kumtunza huyu mtoto wako pia, kumtegemea huyu mtu ni njia ya shetani kukushikilia wewe hapo. Ubarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s