Kusherekea harusi

Je ni sawa kwa mtu aliyeokoka kusherekea harusi ya ndugu ambaye hajaokoka? kwa mfano mkatoliki, msabato, muislamu n.k?

–Leva–

Advertisements

53 thoughts on “Kusherekea harusi

 1. Bwana asifiwe. Ningependa kumwuliza ndugu yangu swali moja. Ni nini maana ya kuokoka?
  ukamwangalia mtu kwamba ni wa dhehebu fulani ukasema kwamba hajaokoka, kana kwamba ndiwe mwenye kuwaokoa waovu! Mungu hatazami dhehebu ila moyo wa mtu binafsi kulingana na neno na mafundisho yake

 2. kwani kuna shida gani? Mungu tunae mwabudu ni mmoja tatizo madhehebu ni mengi..

 3. Shalom wapendwa,
  mimi ninakubaliana na ndg Mwendam, nadhani kuna baadhi ya vitu ambavyo ni vigumu mtu ulieokoka kuvishiriki kwenye hizi sherehe.
  Mfano mwanzo wa wokovu wangu kuna mdogo wangu alikuwa anaoa, nami nikaona nichangie, kwa vile hatuna wazazi hivyo gharama sie ndo tuligawana kumsaidia. Ndugu zangu hawajaokoka nilichanga sawa nao kwani kuna gharama kubwa hizo harusi zao…
  Sasa nilijitahidi nikawaambia hela yangu itumike kwenye vitu isipokuwa pombe, sikwenda kanisani, nilienda ukumbini kule nilikuta zimekodiwa ngoma ambazo hazina maadili ya Kikristu, pombe tele, kuanzia nimefika hadi nilipoamua kuondoka saa 6 hakuna kuomba ni hotuba, ngoma, kula… baadaye nilikaa muda nikona kama milango ya uchumi imefungwa kabisa… ilibidi nijiulize wapi nimekosea … kwa kifupi ninaona hata kuchangia pesa yangu kule nilifanya vibaya, lakini sasa hivi Roho ananiongoza, nimejua kusema hapana na kuwa wazi kwanini ili kama wanafundishika wajue na kutubu. Baikiweni.

 4. majibu yote ni mazuri sana,TAFSIRI HALISI ya WOKOVU bado ni shida kwa wapendwa

 5. Nawashukuru sana mr Nyandaro na Mwenda kwa kufikia mwisho lkn ninawasiwasi km mmeridhika.Nami nasema kwamba muuliza swali kwanza arekebishe swali lake ndipo 2changie kwa ufasaha kwa kufuata maandiko yanasema nn.Yeye c MUNGU maka awataje kwa mifano kuwa wakatoliki,walutheri n.k kuwa hawaja okoka.pili tafsiri ya kuokoka inayo zungumziwa ktk biblia si ulokole naomba ifahamike hivyo unless km kunamstari unao onyesha hivyo na tatu mwuliza swali aombe msamaha ili kudumisha UPENDO ulio zungumziwa ktk biblia.Baada ya hapo nitaporomosha vilivyo na ikumbukwe kuwa wokovu haupo ktk dhehebu upo………………… MUNGU AWABARIKI NYOTE.

 6. Mungu akubariki ndg. Nyandaro, ni kweli tusiingize mada ambayo siyo mahali pake hasa, uwe na amani ya Bwana.

 7. Kaka Mwenda naona sasa tutatoka nje ya mada,kwani kila mtu anaejiita mkristu amemkiri Yesu kuwa ni bwana na mwokozi wake?kuna hata watu wamejikuta wamezaliwa kwenye familia za kilokole lkn binafsi hawajamkiri Yesu lkn wanajiita wakristu,na hao ndio niliokuwa nawazungumzia.

 8. Ngd. Nyandaro
  Sijakuelewa unaposema unazungumzia NDOA ZA WAKRISTU AMBAO HAWAJAMPOKEA YESU. Hivi, mkistu ni nani? Na tunapozungumzia habari za Wakristo tunamaanisha nini?
  Hivi; kuna Wakristo ambao wanaweza kuwa wa-Kristo lakini bado hawajampokea Kristo? Naomba nijifunze kwako!

 9. Kaka yangu Mwenda
  Nimesema tuna perception tofauti ktk wokovu kwakuwa sioni sababu ya kutokwenda au kutoshiriki kwenye harusi(ndoa) ya ndugu yangu,rafiki yangu kwa kisingizio cha wokovu,naiheshimu ndoa kwakuwa ni tamko la Mungu,pia nafikiri ni vizuri km mlokole(believer)kumwonyesha mtu unampenda na kumjali hata km hajamjua Yesu and thats why nikatoa mfano wa kutembelea wagonjwa mahosptalini bila kujali hata imani zao,kwakuwa mimi tayari nimepata hiyo neema yanipasa niwe mfano,na sidhani km ni dhambi anyway kwakuwa hakuna mstari unaosupport hii mada ni mawazo yetu sisi tu km wanadamu.
  Ndugu zangu hapa naomba nieleweke,nazungumzia ndoa za wakristu ambao hawajampokea Yesu,ndoa za msikitini sizijui kwahiyo siwezi hata kuzizungumzia sana kwakuwa sidhani hata km wanatumia mistari ya bible ktk kufungisha ndoa zao,na ndio maana nikasema nikubali kutokukubaliana,based on what i have shared already.
  shalom

 10. Mpendwa Nyandaro.
  Nadhani hapa labda tatizo liko kwangu ambaye sijaweza kueleweka vizuri katika maelezo yangu. Mimi katika maelezo yangu, nakumbuka sijasema kuwa mtu akifunga ndoa ya kimila au nje ya wokovu kwamba akiokoka atamwacha yule mke/mme aliyemwoa au kuolewa naye kabla ya ndoa hiyo, la hasha, nililolizungumza mimi hapa ni juu ya kuhudhuria hizo sherehe za ndoa za kimila au za kidini nje ya wokovu kwa sisi tuliookolewa.

  Nimejieleza kuwa hatutaweza kuhudhuria kila ndoa eti kwa sababu ni halali hata mbele za Mungu. Kuna ndoa za aina nyingi, kuna ndoa za kimila, kuna ndoa za kidini, kuna ndoa za watu waliookolewa, kuna ndoa za serikali yaani bomani n.k. Mpendwa Nyandaro, iwapo utatafakari na kufahamu maana ya ndoa za kimila nadhani unaweza kunielewa ninamaanisha nini, ndoa za kimila huweza kuambatana na kila namna ya ushirikina na mambo yanayofanana na hayo, ndipo mimi niliposema, je, turudi tena msikitini ili kuhudhuria ndoa? Ninaamini kabisa kuwa ndoa iliyokuwa nje ya wokovu haiwezi kukwepa mambo ya kimila japo itakuwa ni ya kidini kwa sababu nami kabla ya wokovu niliweza kuhudhuria ndoa nyingi za namna hiyo.

  Katika hili, mwenye kuelewa maana ya wokovu sioni kama ataona kuwa kuna perception tofauti ya wokovukati ya mmoja na mwingine. Wokovu ni moja , kwamba hatupaswi kuifuatisha namna ya dunia hii, [Warumi 12:2] “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.

  Ni kweli, mtu aliyeoa au kuolewa kabla ya kuokoka haruhusiwi kuoa au kuolewa tena baada ya kuokoka kwa sababu tendo la kuoa au kuolewa ni la halali hata mbele za Mungu. Ingekuwa sivyo basi tungeweza pia kusema kuwa, watu waliozaliwa bila kuokoka hawastahili kuokoka kitu ambacho kisingewezekana kwa sababu wokovu ni kwa wanaotoka katika dhambi, lakini sasa wanastahili kwa sababu kuzaliwa ni halali kwa kila mwanadamu, tofauti inakuwa tu kwamba wanazaliwa wakiwa katika dhambi.

  Kuzaliwa kwao katika dhambi hatuweza kusema kuwa hawafai, na kuwa kwao katika dhambi sisi tuliookoka hatuwezi kukubaliana nao katika kila jambo. Watu hawa wakisha kuokoka wanakuwa na haki kabisa ya kuwepo katika kanisa bila kupunguza chochote katika maungo yao, japo mwanzo tulikuwa hatushirikiani nao katika kila jambo.

  Vivyo hata katika hizi ndoa, hatusemi kuwa si halali, bali ni halali, na kuwa kwake halali hakutufanyi sisi tuliookolewa kushiriki katika kila mikakati ya maandalizi yake, kwa sababu hazipo katika haki ya Mungu japo baadaye zitapata kibali iwapo wahusika wataokoka. Kupata kibali kwa ndoa hizo baada ya wahusika kuokoka ni sawa na kupata kibali mtu aliyekuwa na dhambi na kwenda zake mbionguni baada ya kuokoka.

  Mambo yanayofanana na hayo ni pamoja na watu wanaozaa watoto kabla ya kuokoka, watoto wanaowazaa bado ni halali mbele za Mungu japo wamezaliwa katika uasherati. Watoto hao wakifa kabla ya kujua mema na mabaya wanakwenda zao mbinguni, na iwapo watakuwa wamejua mema na mabaya kisha wakaokoka bado wanakwenda zao mbinguni japo walizaliwa kwa uasherati! Ninachoweza kutilia mkazo zaidi hapa ni kwamba, tusiituatishe namna ya dunia tuliyoiacha baada ya kutangaza wokovu. Hivyo ndivyo ninavyoshuhudiwa na Roho wa Mungu.

  Amani ya Kristo itufunike!

 11. Shalom
  Wapendwa nafikiri hapa tukubali kutokukubaliana,maana naona hapa kila mtu ana perception yake ya wokovu.
  Maana ndoa iliwekwa na Mungu ndio maana hata ukioa au kuolewa kabla ya kuokoka hufungi ndoa tena unapookoka,si km tunavyoona kwenye mambo mengine km ubatizo nk.hilo ni neno la Mungu.

 12. Ubarikiwe sana kaka Mwenda hii ndiyo kweli yenyewe kaza buti mimi binafsi nimeungana na ulichosema na nimekubaliana.Mungu akuzidishie Hekima na ufahamu uzidi kuitoa Elimu ya kirsto kama ilivyo bila kujali uso wa mtu.amani nakutakia.

 13. Mimi nadhani wote tunakubaliana jinsi tunavyopaswa kuwa na ndugu zetu pale wanapokuwa na matatizo au shughuli zao, lakini lengo la mada hii ilikuwa je ni sawa kwa mtu aliyeokoka kusherehekea arusi ya ndugu ambaye hajaokoka? Hili ndilo tunalojadiliana nalo.

  Ninafahamu kuwa tumeokolewa ili tumtumikie Mungu, na moja ya utumishi wetu ni kuwaleta watu kwa Kristo Yesu. Ili kuwaleta watu kwa Yesu lazima tuwajue wanakoweza kupatikana.

  Hata hivyo hatuwezi kuwatafuta na kuwahubiria katika shughuli zao maalum kama; bar katika ulevi, matambiko, sherehe zao za kimila, sherehe zao za kidini shughuli zao zinazohusiana na mambo ya kidini na sikukuu zao mbalimbali n.k. Hatuwezi pia kushiriki katika maeneo hayo eti ili tuonekana tunawapenda na hatimaye tuwapate! Tukifanya hivyo, wokovu wetu utakuwa hauna ushuhuda wowote, tofauti yetu haitaonekana kabisa na wao. Tutakapokuwa tunasema kuwa tumeokoka watashindwa kutuelewa vizuri kwamba wokovu wenyewe hasa ni nini!

  Kwa vile sisi nasi tutakuwa tunashiriki yale ambayo kimsingi ni Hali hiyo itaweza kudhaniwa kuwa nasi ni walevi kama wao, au tunaweza kudhaniwa kuwa nasi tunashiriki katika matambiko kama wao na hivyo kuonekana kuwa hakuna tofauti kati ya mtu aliyeokoka na mtu asiyeokoka. Hawatakuwa na hukumu wala jitihada za kumtafuta Mungu. Watu tuliookoka lazima tutakuwa na tofauti katika maeneo mengi, na pia hatutaweza kwenda sehemu yoyote eti kwa sababu wokovu hauondoki kwetu!

  Mimi nionavyo, kama watu tuliookolewa bado tunapaswa kuangalia ni wapi panatufaa kwenda na kushiriki masuala mbalimbali na ni wapi hapatufai kwenda. Tunapokuwa tumeokolewa si rahisi kuwapendeza ndugu zetu wote kwa kila jambo, lazima mambo mengine tutaonekana ni vichaa au wendawazimu, ndivyo hata maandiko yanavyotuambia. Hata mtume Paulo alipokuwa katika harakati ya kuihubiri Injili, katika kujitetea kwake alionekana mwendawazimu, Tunaweza kuliona hilo katika, MATENDO 26:24-25 “Festo akasema kwa sauti kuu, Paulo, una WAZIMU, kusoma kwako kwingi kumekugeuza akili. Lakini Paulo akasema, Sina wazimu, Ee Festo mtukufu, bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili”. Unaona! Hivyo hatupaswi kuogopa ndugu zetu hata ifikie kufanya mambo yasiyo na ushuhuda.

  Tunapokuwa tumeokolewa si kwamba tunakuwa tumetengeneza amani na ndugu zetu, la hasha bali tunakuwa tumetengeneza uhasama, hawatatupenda katika mambo mengi. Tunaona pia maandiko yakituambia katika, [Luka 12:51-53], “Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano. 52 Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu. 53 Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu”. Unaona, hii ndiyo hali halisi.

  Kama nilivyosema katika mada yangu ya huko nyuma ni kwamba, ndugu zetu wanapokuwa na matatizo ya namna mbalimbali kama ya misiba, ugonjwa n.k. tunapaswa kuwasaidia kadiri tutakavyoweza ikiwa ni pamoja na kuwaombea pale panapohitaji maombi, n.k. Hatutaweza kuacha kushiriki misiba au ugonjwa kwa ndugu zetu eti kwa sababu sisi tumeokoka, hiyo haitaeleweka hata katika hali halisi ya maisha ya kawaida.

  Hata hivyo, kuna mambo yao mengine ambayo hayahusiani kabisa na matatizo, mambo hayo ni kama arusi n.k. Maswala kama haya, pale wanapotualika au wanapotaka kutushirikisha kuwa tushiriki tunapaswa kuangalia kwamba kuna umuhimu kiasi gani kwetu kuweza kushiriki au kuchangia, na pia la muhimu zaidi ni kuangalia kwamba, je kwetu haitakuwa dhambi, na pia je kwetu haitafanya kiroho chetu kuathirika n.k.

  Kwa vile kuoa si dhambi, yale ambayo tutashuhudiwa na roho wa Mungu kuwa tuyashiriki tutashiriki nadhani hii itakuwa ni pamoja na ushauri, lakini hatutaweza kushiriki kila kitu eti hata ibada zao. Jamani, mnataka tuingie tena misikitini na kushiriki nao? Hayo tuliyakataa baada ya kuokolewa, sasa tupo katika Nuru yaani Kristo, hatupaswi tena kuyaendea hayo hata kama harusi hizo zitakuwa ni za kaka zetu au dada zetu au wadogo zetu wa kuzaliwa tumbo moja. Tumesha jifunza kwamba Yesu Kristo hakuja kuleta amani bali upanga!

  Amani ya Kristo itufunike!

 14. kwenda kwenye hizi sherehe za wasiookoka mimi naona ni kuyajenga yale tuliyoyabomoa,na ni kama kumuunga shetani mkono watu waendelee kuona hakuna ubaya maana hata mwanafunzi wa yesu anafurahia .tunajifunza

 15. Shalom
  Nafikiri ni vizuri kuringa na kumwinua Yesu pia kufanya mambo yanayompendeza Mungu,inaleta maana sana ktk wokovu,pia hakuna anejidanganya kuwa ataingia mbinguni kwa kuwa tu ameokoka mbinguni ni pa watakatifu kwakuwa ni patakatifu,kwahiyo km mtu c mtakatifu apasahau,na wala utakatifu wa mlokole hauondolewi kwa kwenda kwenye harusi au mazishi ya nduguyo or rafiki.

 16. Nukuu
  “””Nafikiri utakua unajidanganya kama unafikiri sababu unasema umeokoka ndio tiketi ya kuingia mbinguni.””””
  Mimi naringa na kumtukuza Mungu as long as nimepiga hatua la Muhimu nisiipoteze tiketi. Huu ni uelewa wangu binafsi. Naelewa ni process that is why i explain what i can do ili nisipoteze tiket in my last paragraph. Lakini kuringa kwa sababu niko ndani ya Yesu kwangu mimi ni important.
  Thank you
  Tumwinue Yesu.

 17. Nakubaliana na Ndg Nyandaro na Ndg Esther na nilishawahi kuandika hapa mara kadhaa kuwa “KWAZO KUU KWA WASIOOKOKA AMA WANAOTAKA KUOKOKA NI BAADHI YA WALOKOLE WENYEWE. AMBAO (baadhi haohao na ambao huwa wapaza sauti zaidi) KWA UFINYU WA ELIMU SAHIHI YA BIBLIA WANAISHIA KUWATENGA NA KUWABAGUA HATA WALE WENYE UHITAJI”
  Wasilojua ni kuwa kwa kuwatenga wahitaji, wanakuwa hawatimizi mpango wa Mungu

 18. shallom
  tatizo c walokole tunacomplication ambazo hazina maana, cjui ni kwasababu ya elimu duni au ni nini, mana most of us education kidogo inakuwa ndogo sana, hadi tunacomplicate mambo ya Mungu.
  mie ni muumini mzuri sana wa kanisa fulani la kilokole ila unakuta ubaguzi wa makanisa mengine ni waajabu espacialy ukiwa mgeni, watakuchunguza hadi basi utazani wenyewe ni malaika, wakati ukiwaangalia kwa makini wanaskendo kibao.
  ubaguzi c mzuri kama ni hivyo Mungu tunaemuabudu angekuwa anatoa neema zake kiubaguzi. ila anawanyeshea wema na wabaya.
  Walokole tuamke, mambo mengine tuache.
  warumi 12:15
  damu ya Yesu iwafunike.

 19. Bw asifiwe wapendwa,
  Wajameni tunapookoka tunaokoa roho zetu,haya mambo ya duniani ni yakupita na yataisha,naona walokole wa nyumbani mna mtazamo wa kiconsertive hata ndio maana watu wanakuwa wanaogopa kuokoka kwa kuona km ni mzigo,harusi au mazishi ya ndugu yako utaacha kwenda kwa kisingizio cha ulokole?hata machoni kwa Mungu haitampendeza,ukiokoka unatakiwa uwe na upendo wa kweli na ndio maana hata watu wanatembelea wagonjwa mahospitalini bila kujali wameokoka au lah.
  Na sidhani km eti kwenye harusi kukiwa na ngoma za kienyeji km ndio wokovu umepotea,wajameni inasikitisha sana kuona watu wanauchanganya wokovu hivyo.

 20. dada Lisa,

  naomba nitumie kiingereza. Salvation is a life time process and not a one time time thing! Till the day you die thats when the salvation process end.
  THERE IS NOTHING YOU CAN DO TO EARN OR DESERVE A SALVATION. It’s only by grace of God that you will enter heaven. Nafikiri utakua unajidanganya kama unafikiri sababu unasema umeokoka ndio tiketi ya kuingia mbinguni. na huwezi ukaringa ukasema unaingia mbinguni, inabidi umshukuru Mungu ya kukuokoa wewe na sio mwingine, inabidi umtukuze Mungu kila wakati. Read Titus 3:5 na zaburi 130:3-4

  And Jesus didn’t come to the world so that we all go to heaven, otherwise we have died once we get born again. he want us to have relationship with our Heavenly Father, He wants us to be like Him in everything. God want us to us love Him with all our heart and soul. He wants our heart, He want us to love Him because He loved us first.

 21. Bwana Yesu asifiwe!!!

  Wakati mwingine si kufanya kazi na wasiookoka tu bali hata wale wanaolipa mishahara/waajiri wetu nao si kwamba hawajaokoka tu bali wengine hushiriki hata nguvu za giza kupata fedha. Wengi sana wa matajiri wakubwa hasa wa TZ wanashiriki nguvu za giza, so long as Tz kwa sasa ni nchi ya pili kwa uchawi Afrika. Hata mashirika mengine yako Tz ila nyuma ya pazia/machimbuko ni huko huko kuzimu. Watu hawa tunalipwa nao mishahara, tunafanya nao kazi, tunasherehekea kufunga na kufunga mwaka na mambo mengi mengine.
  La Muhimu tusicheze mbali na Uso wa Mungu, tuutafute kwa bidii kwa kusoma neno lake na kujifunza zaidi kuhusu neno lake bila kujali mazingira tuliyopo.Tuombe Roho wa Mungu atuongoze zaidi, tuwe na ujasiri kama Musa alivyokataa kuitwa mwana wa binti farao na kujiunga na Hebrews. Kama mtu wa karibu yako atafanya chochote kwa kukushirikisha, fanya kwa mipaka.

  Kwako Peter; kwa jinsi ninavyoelewa mimi kuokoka ni kukata tiketi ya kwenda mbinguni. Ni sawa na kukata tiketi kwenda Mwanza, lakini basi linaweza kupata ajali na usifike huko Mwanza.
  Kwa hiyo ukishakata tiketi yako kwenda mbinguni(kuokoka)dereva ni Yesu na mafuta ni maombi yako;usukani ni neno la Mungu; kiongozi wa msafara ni Roho Mtakatifu; na mafundi (in case kama basi lako litaharibika/pancha etc) ni watumishi mnaosaidiana kufundishana na kusoma neno la Mungu. So mtu aliyeokoka kama ameamua kutoka katika moyo wake amepiga hatua kubwa sana kwenye hii safari ya kwenda mbinguni wakati wengine hata nauli hawajapata. Tuna kila sababu ya kuringa ndani ya Yesu.
  Tunajifunza.

 22. thanx alot Imani.
  iam sorry nilikosea nikaandika kaka imani and na wewe umeniita dada carol ,my name is karoli and ni kaka.yote heri mpendwa.
  uzidi kubarikiwa sana na Roho wa Mungu azidi kukuongoza.
  Kuhusu kuchangamana na watu wasiookoka ninao ushuhuda fulani.Miaka 3 iliyopita alikuja kwangu usiku rafiki yangu akiwa amelewa na ana chupa ya bia,nilijisikia vibaya sana na nikataka kumfukuza lakin nikasikia kama sauti inaniambia moyoni mwangu usimfukuze ila mkarimu na uongee naye.kabla ya kuongea naye akaomba msamaha kwangu kwani anajua ni kosa.nikamjibu nimekusamehe ila unapata faida gani ?akaniambia anapenda sana kuokoka ila anashindwa,nikaomba naye ktk hali yake hiyo akaondoka.baada ya muda mfupi akaokoka.nilijawa furaha sana na amesimama kweli ktk wokovu.
  sisemi watu waendee mazingira mabaya kwa kisingizio cha kuhubiri ila tumuachie roho atuongoze na watu wanakutana na Mungu ktk njia mbalimbali zaidi ya kwenda kanisani tu.
  stay blessed.Amen

 23. Big sana Elisante Yonah nakubaliana na wewe yesu hakuacha dhehebu hapa duniani kikubwa alichokisema ni kumwamini yeye kuwa ndiye mwokozi.Mengine haya yote ni utashi wa kibinadamu.DINI NA DHEHEBU LAKO HALITAKUPELEKA MBINGUNI na kuwa mlokole si tiketi ya kwenda mbinguni.

 24. Wapendwa,

  Hakuna tatizo lolote, nikuonyesha upendo ambao Mungu anaonyesha kwako, upendo ambao hauna kipimo. Nani aniambie Mungu akiamua kuhesabu makosa yetu leo hii, atasimama na kusema yeye ni safi?? Ni kwa neema tu, neema ambayo ni bure kwa wote.
  kwenye sherehe kama hizo usijihusishe tu na vitu ambavyo vitakukwaza kiroho. Kitu nacho shangaa, mbona hao wanaosema haifai kusherehekea wanafanya kazi na wasiookoka?? na kushirikiana nao?
  Yesu alikua rafiki wa watoza ushuru, malaya, alihudhuria harusi ya cana, watu walimfuata Yesu sababu alikua anajali na alikua na upendo wa hali ya juu kupita yote.
  Mchungaji anayewaambia waaumini wake watengane na mke au mume sababu si mlokole, huyo amepotea kabisa na mkimbie. Na wake waliookoka watiini waume zenu ambao hawajaokoka, ndivyo biblia inavyosema!!
  Upendo wa Mungu haubagui, na anawapenda watu wote sawa sawa kabisa, hata kupenda zaidi ukiokoka au kukupenda kidogo sababu sio mlokole.

  nashauri watu wasome biblia zao na kuacha kusikiliza ushauri wa watu, wengine ni wapotovu. Mahubiri yeyote uyasikiayo nenda angalia kwenye biblia, kama hayaendani tupilia mbali.

 25. Shalom,

  Nashukuru sana dada Carol kwa baraka, utukufu kwake Mungu, sababu amempa kila mmoja jambo la tofauti kwa lengo la kusaidiana katika safari hii ya wokovu.

  Dada Imani

 26. Kaka Imani asante sana na ubarikiwe.
  yaani umetukumbusha kuwa yatupasa tuongozwe na roho mtakatifu katika kuamua sio akili za kibinadamu.
  iwapo roho wa Mungu anatuzuia kwaniini twende?akiruhusu waweza kwenda.

 27. Wokovu ni nini hasa?

  Kuna nadharia nayoifikiri kuwa si sahihi, kuna kufananisha ustaarabu wa kimagharibi na ukristo, kuwa makini hii si sahihi…

  Kumbuka ukristo ulipoingia sehemu yoyote ulikuta tamaduni za sehemu zile na kuna baadhi ziliheshimiwa na kuendelezwa… Moja wapo ni taratibu za uendeshaji wa sherehe kama za harusi nakadhalika…

  Ukienda china, japan, afrika ya kusini, bara la amerika ya kusini, kule kuna ukristo pia na wanataratibu ambao umeingizwa katika taratibu za kikristo pia.

  Ifahamike kuwa sisi wakatoliki tuna utaratibu wa kutamadunisha taratibu za kanisa kwa jinsi na mahala kanisa lilipoenda na ndio njia pekee ya kuwapata wakristo wengi.

  Hapa naona watu wanasema ngoma za jadi zinaharibu wokovu wa mtu? sidhani kilichomo ndani ya zile nyimbo za ngomani ndio huenda kitaleta mambo ambayo si sahihi…

  Sidhani miziki ya duniani ina tatizo kwenye sherehe kama imebeba ujumbe wa kuwaasa maharusi juu ya maisha bora ya ndoa…

  Anyway ni mtazamo tu…

 28. Nashukuru mpendwa BW, nadhani tuko pamoja. Ndg Imani kama ulivyosema, amefafanua vizuri zaidi. Mimi sipo tofauti na mtazamo uliouonesha hapo juu, labda mwanzo sikukuelewa vizuri. Tuendelee kuwa pamoja!

 29. Amani iwe nanyi,

  Ndugu Mwenda,

  Ahsante kwa mchango wako ,kuna mahali umeandika ” Hivyo ni wajibu wetu kujilinda, hatupaswi huwaonea huruma ndugu zetu katika jambo ambalo ni la hatari kwetu. Kutokwenda katika arusi za wasioamini si kwa lengo la kuwadharau, bali ni kwa ajili ya kujilinda na roho za upotevu”
  Nafikiri nimepitia mchango wangu na sijaona mahali nimesema tunapaswa kuhidhuria sherehe hizo kwa sababu tunawaonea Huruma,ila nilichomaanisha ni kama inafaa tushirikiane nao kwa njia inayofaa kama ilivyoandikwa katika 2 Wakorintho 6:14 na si kuwakimbia kabisa hata pale inapotubidi kuwa nao
  Ni kweli kabisa inafaa tujilinde nafsi zetu kama ilivyoandikwa katika 2 Petro 3:17 ila je kujilinda huku ni kukimbia kushirikiana na hao mataifa na kujitenga nao kabisa? Hili linawezekana kweli?

  Neno la Mungu linasema katika 1 Wakorintho 5:9-13 “9Niliwaandikia katika barua yangu kuwa msishirikiane na waasherati. 10Sikuwa na maana kwamba msishirikiane na watu wa dunia walio waasherati, au wenye tamaa mbaya, wanyang’anyi au waabudu sanamu. Kufanya hivyo ingewabidi mtoke duniani. 11Lakini nilikuwa namaanisha kwamba msishirikiane na mtu ye yote anayejiita ndugu lakini ni mwasherati, mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu, mtukanaji, mlevi na laghai. Wala msile na mtu kama huyo. 12Si kazi yangu kuhukumu watu walio nje ya kanisa. Je, si hao walio ndani ya kanisa mnaopaswa kuwahukumu? 13Mungu anawa hukumu walio nje ya kanisa. “Mfukuzeni mtu mwovu atoke kutoka katika ushirika wenu.”
  Ndg Imani amesema vyema inatupasa tushiriki kwa mipaka,tuchangie pale inapofaa na pasipofaa tukae kimnya kadri tutakavyoongozwa na Roho mtakatifu

  Amani ya Bwana Yesu iwe pamoja nayi nyote

  BW

 30. Namnukuu Ndg IMANI
  “Unaweza ukapata kibali kuwapa habari za Yesu(kama Bwana ataridhia usilazimishe usije ukaleta malumbano), na hata wanapokushirikisha taratibu fulani za kufuatisha, mambo ya arobaini, matambiko e.t.c basi utawapa msimamo wako wa kutoshiriki ukiwaelimisha kupitia neno na kama Bwana ametoa kibali watapokea maana kuna wengine wanaiga tu hawajui kama ni sawa au siyo sawa so unaweza ukawa umewasaidia..

  -Kuna walokole wengine ni waoga sijui, utakuta analetewa taarifa ya kuhusu matambiko / ibada za wafu/ mila na desturi na kwa sababu yupo mjini na anajua ni machukizo kuhudhuria lakini kwa kuwa anahofu kuwakwaza nduguze basi atatuma pesa na yeye atatafuta excuse. Hapana, hii ni sawa na umeshiriki tu.

  Imani yako iwe wazi kabisa na mipaka yako ijulikane. Ikitokea kuna kikao cha kupanga mikakati fulani kinyume na imani yako, nenda usiogope, na kwa kuwa utakuwa umejikabidhi kwa Roho Mt basi atakupa ujasiri na maneno ya kuongea kudhibitisha imani yako kwa neno la Mungu, wakikuelewa nao kubadilika sawa, wakikufukuza na kukupinga wewe achana nao bila ugomvi.”

  Nadhani mengi ya nilyokuwa nataka kuchangia yamejumuishwa humu
  SHUKRANI KWAKO NDG IMANI
  Naamini twajifunza zaidi na zaidi

 31. Bwana Yesu asifiwe sana!!
  Nashukuru kwa mchango wako najua wengi wamefaidika. La muhimu ni kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu.
  Tunajifunza

 32. Shalom
  Dada Lisa uliyeuliza swali hapo juu

  Nanukuu
  ‘Nauliza hivi; Wengi tunaochangia hapa tuko mijini sasa kwa mfano mimi niko hapa mjini lakini ndugu wa karibu kabisa yuko kijijini na hajaokoka sasa mfano Mungu akimchukua mimi siruhusiwi kwenda kwenye mazishi??. Ukizingatia most of our villagers bado wako na mtazamo wa dini. Kama harusi zao sishiriki na je how about mazishi???.’

  Mimi ningependa kusaidiana nawe kidogo,
  Ni kweli kuna baadhi ya vitu Roho wa Mungu ANAWEZA KUTUKATAZA KABISA tusihudhurie wala TUSIPINGANE NAYE,’LAKINI SI VYOTE’, . Tunaona kwenye Biblia tuna mifano ya watu walioomba ushauri kuhusu mambo mbali mbali.

  Hesabu 22; 18- 19
  ‘Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza. Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua Bwana atakaloniambia zaid’

  Hesabu 20
  ‘MUNGU AKAMJIA BALAAMU USIKU, AKAMWAMBIA, KWA KUWA WATU HAWA WAMEKUJA KUKUITA, ENENDA PAMOJA NAO; LAKINI NENO LILE NITAKALOKUAMBIA NDILO UTAKALOLITENDA’

  Balaam alijua Balaki alikuwa wanataka ashirikiane ktk jambo ambalo lisilompendeza Mungu lakini Mungu akampa kibali aende kwa sharti la kusema sawa na mapenzi yake na kukiri tu kile alichoambiwa na Mungu, ndio maana alibariki na si kulaani kama ambavyo Balaki alimtaka afanye. Na ndio maana Balaki anamlaumu na ndipo alipokuwa jasiri kusimama katika neno la Mungu.

  Hesabu 23:11-12
  Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa. Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile Bwana atialo kinywani mwangu?

  Mtazamo wetu ukiwa ni kumpendeza na kutegemea uongozi wa Mungu ktk kila jambo kwa kweli ni rahisi sana kutembea katika mapenzi yake, kwa kuwa ana njia tofauti na tulizozizoea na tonazoweza kufikiri.

  Michango / ushauri ni sehemu tu ya msaada tunaoweza kusaidiana ukilinganisha na uwezo mkubwa mno wa Roho mwenyewe kutuongoza, sisi tuna mipaka, lakini Yeye anaweza akafanya jambo la ajabu na lisilotegemewa na likasaidia kutatua maswali na mkanganyiko ambao tunaweza kukutana nao. Maarifa yake ipo juu sana

  Sasa naomba nichangie kwa uchache;

  MISIBA
  Eg; Tuna wazazi wetu hawajaokoka na ndugu wengi tu na inapotokea wamefariki hatuwezi kukataa kwenda kuwazika. Tulichoshauri ni kuomba uongozi wa Roho Mt akuongoze kuenenda kwa hekima sawa na mapenzi ya Mungu kwa kutoshiriki yale mambo, ibada zisizofaa na taratibu zilizo kinyume na mapenzi yake.

  – Kuna baadhi ya dini baada ya kuzika siku ya pili huenda kufanya matambiko, sadaka na ibada; so wewe huwezi kweda.

  -Kuna sala / nyimbo zilizo kinyume; kuwaombea marehemu, kuwaomba wafu, wewe usiwafuatishe kaa kimya sema na Mungu wako kimyakimya tena ukiomba afungue fahamu zao waweze kumpokea Yesu

  Unaweza ukapata kibali kuwapa habari za Yesu(kama Bwana ataridhia usilazimishe usije ukaleta malumbano), na hata wanapokushirikisha taratibu fulani za kufuatisha, mambo ya arobaini, matambiko e.t.c basi utawapa msimamo wako wa kutoshiriki ukiwaelimisha kupitia neno na kama Bwana ametoa kibali watapokea maana kuna wengine wanaiga tu hawajui kama ni sawa au siyo sawa so unaweza ukawa umewasaidia..

  -Kuna walokole wengine ni waoga sijui, utakuta analetewa taarifa ya kuhusu matambiko / ibada za wafu/ mila na desturi na kwa sababu yupo mjini na anajua ni machukizo kuhudhuria lakini kwa kuwa anahofu kuwakwaza nduguze basi atatuma pesa na yeye atatafuta excuse. Hapana, hii ni sawa na umeshiriki tu.

  Imani yako iwe wazi kabisa na mipaka yako ijulikane. Ikitokea kuna kikao cha kupanga mikakati fulani kinyume na imani yako, nenda usiogope, na kwa kuwa utakuwa umejikabidhi kwa Roho Mt basi atakupa ujasiri na maneno ya kuongea kudhibitisha imani yako kwa neno la Mungu, wakikuelewa nao kubadilika sawa, wakikufukuza na kukupinga wewe achana nao bila ugomvi.

  SHEREHE
  Kuhusu mambo ya sherehe kama harusi, birthday, graduations e.t.c. Pia utahitaji uongozi wake Roho Mt.

  Ikiwa ni lazima kabisa kusupport financially au kwa mawazo basi Roho akusaidie, ushauri wako mzuri unaweza ukakubalika au usikubalike ‘usilazimishe’

  Kuna wengine huamua kununua vitu kabisa km mchele, ng’ombe ili pesa yao isije kutumiwa kununua vileo e.t.c (sijasema tufanye hivyo) ni kadiri roho anavyoongoza.

  Suala la ushiriki physically ni lazima liwa na mipaka, hapo usitafute kufurahisha watu, yasiyokuhusu kaa kimya pembeni na si lazima ukae mpaka mwisho usije ukakwazika au kujinajisi kwa kuona, kusikia na kushiriki maana kuna muda watu wakishalewa, hakuna ustaarabu bali ni uchafu tu.

  Naweza kuwa sijajibu ipasavyo lakini nina imani utakuwa umepata picha, changamoto fulani itakusaidia

 33. Bwana Yesu asifiwe sana!!!
  Mr. Bernard umeongea kwa ushuda, nimejifunza kitu.
  Nami naomba nitoe ushuhuda lakini haikuwa katika harusi. Dada yangu ameokoka kabla yangu, kuna wakati tulikuwa tunaadhimisha kumbukumbu ya mwisho ya bibi( ni makosa). Dada yangu huyu yeye aliingia katika maombi ili asihudhurie. Sisi tulilaumu sana lakini baadaye alikuja kunishudia kwamba taarifa aliipata baada ya tukio hilo kupita kabisa kwa hiyo hakushiriki. Mungu alijibu maombi yake.
  Tunaweza kufanya hivyo kwani sherehe za harusi zinachukuwa maandalizi hata mwaka.
  Tunajifunza.

 34. Bwana Yesu asifiwe!!!
  Kama wengi walivyoandika japo si moja kwa moja wanashauri tusishiriki kwenye hizi harusi.
  Nauliza hivi; Wengi tunaochangia hapa tuko mijini sasa kwa mfano mimi niko hapa mjini lakini ndugu wa karibu kabisa yuko kijijini na hajaokoka sasa mfano Mungu akimchukua mimi siruhusiwi kwenda kwenye mazishi??. Ukizingatia most of our villagers bado wako na mtazamo wa dini. Kama harusi zao sishiriki na je how about mazishi???.
  Nisaidieni
  Tunajifunza.

 35. Ni sahihi kabisa maana kuokoka sio dini bali ni kujikabidhi mbele za Mungu na kumwambia Mungu bila wewe mimi siwezi kabisa naitaji msaada wako katika maisha yangu na ukijua hivi utashirikiana na watu wote maana hata Yesu alikuja kwa wenye dhambi sio wenye haki.mbarikiwe sana

 36. Nd.BW
  Nimesoma maelezo yako na nimekuelewa kuwa unaunga mkono kuwa, kushiriki Arusi za wasioamini si vibaya kwa sisi waamini. Mimi nami nimependa kutoa maoni yangu kwako na kwa wanaosoma hapa kama ifuatavyo:-

  Si kwamba, sisi tuliookolewa hatupaswi kushiriki katika majukumu mbalimbali, kama Arusi za wasioamini n.k. eti kwa sababu ya kuwachukia au kuwadharau, hapana, bali ni zaidi ya hapo. Hatushiriki ibada zao kwa sababu tunampenda Mungu kuliko kuupenda ulimwengu.

  Umezungumzia kuhusu Arusi ya Kana mji wa Galilaya; ni kweli Yesu alialikwa katika arusi hiyo na alikwenda. Lakini tunaona kwenda kwake hakukuwa kwenda tu kwa kawaida, bali alikuwa na kazi maalumu aliyokwenda kuifanya. Kazi aliyokwenda kuifanya ni kugeuza maji kuwa divai iliyokuwa njema kuliko ile ya kwanza waliyoimaliza. Kugeuza maji hayo kuwa divai, kunaonesha kuwa ndiyo kazi aliyodhamiria kwenda kuifanya ili watu wamwamini kuwa yeye ni nani.Tunaona hata wanafunzi wake ambao labda walikuwa na mashaka mashaka juu yake walimwamini [Yohana 2:11].

  Kwa mtazamo huo, tunaona kuwa kumbe Yesu alienda kule akiwa na lengo maalum la kuhubiri Neno lake. Sisi tutakapokuwa tunakwenda tunakoalikwa na wasioamini tutakuwa tunakwenda huko kwa lengo lipi; lengo la kumuhubiri Kristo au kufurahisha ndugu? Kama tutakuwa tumekwenda kwa lengo la kumhubiri Kristo nadhani itakuwa kazi njema kabisa, na hakuna atakayeweza kupinga juu ya hilo.

  Kama nilivyoelezea katika mada yangu ya huko nyuma, ni kwamba iwapo mtu ameokoka kweli na anakaa katika viwango vya maombi muda mwingi, nakwambia akienda katika maeneo kama hayo, yaani ya watu wasioamini eti kushiriki sherehe, hatakuwa na amani kabisa ya kuendelea kuwepo eneo hilo.

  Mimi kwa neema ya Mungu sijisifu, niliokoka katika viwango vya juu sana, na kwa neema ya Mungu nilikuwa nipo tayari kufuata kila Neno ninalofundishwa na mchungaji wangu au kila Neno linalotoka kwa yeyote ambaye Roho alinishuhudia kuwa anafundisha kweli.

  Nakumbuka katika hali hiyo, siku zile katika uchanga wangu kabisa, kuna shemeji yangu mmoja wa kiume, mdogo wa mke wangu alikuwa anaoa. Dini aliyokuwa nayo na ambayo aliitumia kufunga ndoa yake ndiyo dini niliyokuwa nayo kabla ya wokovu wangu. Nilialikwa katika Arusi hiyo, na kwa kutokufahamu nilienda kushiriki, tena mimi nilianzia mbali zaidi, nilishiriki kuanzia ibada.

  Kwa kutokufahamu, wakati ibada inaendelea nilijiona ni kama mtu anayetaka kuchanganyikiwa, nilitoka nje ya jengo la ibada. Hali ikawa bado mbaya zaidi, ikabidi nitoroke ibada na kutangulia sehemu ya sherehe ilikopangiwa kufanyikia; nilipofika huko bado nikawa sioni furaha wala amani kabisa katika mazingira yaliyokuwepo. Maana kulikuwepo na ngoma za kienyeji, miziki ya kidunia, na mambo yanayofanana na hayo.

  Mpaka hapo nilikuwa sina chuki kabisa na shemeji yangu huyo, nilikuwa na nia thabiti kabisa kutoka moyoni, kuwa shemeji yangu afanikiwe katika arusi yake. Lakini napenda kuelezea kwa unayefuatilia habari hii, ni kwamba kutwa nzima ya siku ile nilikuwa kama mgongwa; sikuwa na raha wala amani kabisa. Sisemi uwongo, mimi nimeokoka, uwongo ni dhambi, na mshahara wa dhambi ni mauti [Warumi 6:23],

  Sikulala katika eneo la tukio la arusi ile; hali iliniwia ngumu, jioni ile ile nilipanda gari kurudi nyumbani kwangu. Shemeji zangu na ndugu wengine upande wa yule shemeji walinilaumu sana, kwamba nimeidharau ibada na Arusi ya shemeji yangu kwa vile mimi “najifanya mlokole”.

  Kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu siku hiyo. Baada ya kufika nyumbani, niliwaeleza wapendwa wenzangu yaliyonikuta, nadhani kwa sababu ya uchanga wangu hawakutaka kuniambia ni kwa nini nimepatwa na madhara hayo, labda walidhani ningekwazika, waliniombea na kukemea kila roho chafu iliyokuwa juu yangu, nikajikuta napata afueni.

  Sasa mimi kama mimi, ninapozungumzia suala kama hili, si kwamba nazungumza kwa chuki za kidini, au najiinua la hasha, bali nazungumzia kitu ambacho nime-experience.

  Hivyo kutokana na hayo yaliyonipata, nashuhudiwa kabisa kuwa arusi hiyo ilikuwa ni miongoni mwa mambo ambayo Mungu anatukataza katika kitabu chake cha, [2Wakorinto 6:14-18]. Kujitenga katika mambo kama hayo nadhani si kujikweza bali ni kujilinda. Maandiko yanasema katika, [2Petro 3:17] “Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, JILINDENI NAFSI ZENU, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu”. Pia tunasoma katika, [1Yohana 5:18] “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; BALI YEYE ALIYEZALIWA NA MUNGU HUJILINDA, wala yule mwovu hamgusi”.

  Hivyo ni wajibu wetu kujilinda, hatupaswi huwaonea huruma ndugu zetu katika jambo ambalo ni la hatari kwetu. Kutokwenda katika arusi za wasioamini si kwa lengo la kuwadharau, bali ni kwa ajili ya kujilinda na roho za upotevu. Katika ulimwengu wa Roho, unaposhiriki jambo lolote la ibada maana yake unalikubali kuwa ndivyo ilivyo na ndivyo inavyofaa. Unapokuwa na roho pingamizi ndani yako, lile eneo unalotaka kushiriki hutakuwa na amani nalo kwa sababu ndani yako kunakuwa na vita, baina ya kile unachokiamini na kile usichokiamini. Vita hivyo vitakufanya wewe mwenyewe, ambaye ni nyumba ya hizo roho upate shida.

  Kama nilivyoelezea katika mada yangu ya nyuma kidogo, ni kwamba, siku hizi wokovu umekuwa fasheni, karibu kila mtu anaukubali wokovu na anasema kuwa ameokoka. Ukimwuliza anajitofautishaje na mwanzo kabla ya wokovu wake, hawezi kukuelezea maana haoni tofauti yoyote, zaidi sana ataeleza kuwa ameokoka kwa sababu ameona maandiko yanazungumzia wokovu. Pia tatizo jingine ni uchanga wa kiroho ambao upo kwa wengi waliookoka. Uchanga huu umeanzia kwa watumishi wenyewe, bado kuna watumishi ambao wanaona si lazima kufuatisha kila Neno la Mungu lililoko katika maandiko, hapo ndipo hatari inapoanzia.

  Wokovu ni zaidi ya kuona maandiko katika biblia, wokovu ni halisi; hata kama mtu hajui kusoma na kuandika akiokoka atajua kuwa ameokoka. Lakini hii itategemeana na mwalimu wa kwanza anavyokuwa amemfundisha huyo aliyeokolewa. Tuzidi kutafuta Neno la Mungu kwa bidii.

  Shalom!

 37. Ndugu Elisante YONA unataka kunambia kwa Mtumishi Mwakasege kanisani hakuna jina? nijuavyo mimi kuna jina na linajulikana kuwa ni kanisa la kiroho.tujifunze

 38. Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
  SAMAHANI KWA MARA YA TENA NITAKAA UCHANJONI MWA MADA ILI KUMUULIZA Ndg Elisante Yona.
  Kwanza nashukuru kwa mchango wako pia. Na nimesoma na kuelewa baadhi. Pia kuna ambayo sijaelewa (na hii yaweza kuwa ni kutokana na ufupi wa fikra changanuzi kwangu). Umesema (na hapa nanukuu) “Ndugu wokovu upo kila mahali kwa yeye aminiye jina la Yesu,na Neno la biblia halijawahi kutaja kuwa Wokovu uko TAG,Full Gospel,Lutheran,Roma au Sabato,bali biblia yangu ninanionyesha wokovu unapatikana kwa kumuamini YESU KRISTO peke yake,hawa jamaa wanao hubiri madhehemu na Dini waogope kama ukoma,ni wasanii wanatafuta hela na waumini kwa faida zao wenyewe”
  Ina maana unaamini kuwa unaweza kuwa katika dhehebu lolote na kuwa UMEOKOA as long as UNAMWAMINI YESU? Linalonifanya niulize hivi ni kwa kuwa wapo watu wengi walio katika madhehebu na licha ya kwamba hawatangazi wala kuonekana kushabikia madhehebu hayo, wanashiriki ibada ndani mwao na wanaMWAMINI YESU. Na hawa pia si wameokoka (kwa mujibu wa nukuu yako hapo juu)?
  Kuna dhehebu ambalo ushiriki wake unakufanya uwe / ama unaenda tofauti KIMATENDO NA MTU ANAYEMWAMINI KRISTO?
  Kwenye ile topic ya Padre Kalugendo, nilisoma maoni meengi yenye mtazamo hasi juu ya ibada na imani ya waKatoliki. Unazungumziaje hili?

 39. Bwana Asifiwe Mpendwa,

  Ni sahihi kushiriki kama wewe unawaona hao uliowataja hawajaokoka ni bora ukawasaidia wakaja kwa Yesu kuliko kuwahukumu.

  Ndugu wokovu upo kila mahali kwa yeye aminiye jina la Yesu,na Neno la biblia halijawahi kutaja kuwa Wokovu uko TAG,Full Gospel,Lutheran,Roma au Sabato,bali biblia yangu ninanionyesha wokovu unapatikana kwa kumuamini YESU KRISTO peke yake,hawa jamaa wanao hubiri madhehemu na Dini waogope kama ukoma,ni wasanii wanatafuta hela na waumini kwa faida zao wenyewe,Kila neno litapimwa na kila ulimi utakiri kuwa Yesu ni Bwana,Yesu alitufundisha kuhusu umoja na upendo,Labda nikuulize ili sherehe ya Kana ambayo Yesu alihuzuria ilikuwa ni ya Dini au dhehebu gani?
  Kama ukiijua kweli na kweli itakuweka huru,

  Bwana asifiwe

  E.Y.Mjema,Karibu kwenye Semina ya Mwakasege -Biafra upigwe shule ya bible.Asante

 40. Kaka Bernard.
  Kwanza sijaona sababu ya wewe kuomba msamaha ama kusema samahani kabla ya kunijibu.
  Nashukuru kwa ufafanuzi na ntaurejea tena na tena kupata kuuelewa zaidi.
  Lakini shukrani kwa kutumia muda na busara zako kujibu maswali yangu.
  Ntaendelea kuyasoma na kama kuna aliye na cha kuongeza nitashukuru kusoma zaidi na zaidi.
  Na nikishasoma na kutafakari basi ntauliza lolote lihusianalo na haya uliyojibu (kama nitakuwa nalo)
  Baraka kwako Kaka

 41. Watu wa Mungu Bwana Yesu Apewe Sifa,

  Nilipoona swali hili sikupata msukumo wowote wa kuchangia ila baada ya kusoma michango ya wapendwa hapa nimejisikia kuandika kidogo,

  Mimi nafikiri ni sawa kabisa kwa watu waliookoka kushirikiana na hao mataifa katika sherehe hiyo kwa sababu sehemu kama hiyo ndipo haswa kama mlokole unatakiwa uonyeshe imani yako ilivyo dhabiti.Yesu alipohudhuria harusi ya Galilaya si kwamba watu wote pale walikuwa watatakatifu ila alitumia nafasi ile kufanya muujiza wake wa kwanza!(Soma Zaidi Yohana 2)
  Je sisi tunajifunza nini katika neno hili?Yatufaa sana kujitenga na ulimwengu katika kila tunalofanya kwa kuwa tunafikiri sisi ni watakatifu au tunajua zaidi ya wengine?Warumi 8:16 “Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu”
  Nionavyo mimi Matendo yangu,maneno yangu ,muonekano wangu mbele ya watu unatosha kabisa kuhubiri habari njema za Yesu kristo.Petro alivyomkana Yesu wakati bado watu hawakuamini kutokana na muonekano wake(soma Marko 14) Ndio ni kweli tunakatwaza kushirikiana na wasio haki Lakini ikiwa tu ni kwa jinsi isiyo sawa
  2 Wakorintho 6:14 “Msifungwe nira pamoja na wasio amini kwa jinsi isivyo sawasawa kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?.” Sasa je katika jambo takatifu kama ndoa tumeambiwa pia tusishirikiane na hao wasio haki?Katika maisha yangu ya kiroho naogopa sana tena sana kujikweza na Roho mtakatifu anisaidie maana Biblia inaniambia Hatujafika bali tunakaza mwendo ili kuifikia ile Taji

  Mbarikiwe sana
  BW

 42. Nd. Mubelwa T Bandio
  Samahani, naomba nijibu maswali yako kadiri ninavyofahamu, kuhusu mtu aliyeokoka na asiyeokoka kushirikiana katika mambo mbalimbali, iwe ya kiimani au ya kidunia.

  1. Ninavyofahamu mimi, mtu aliyeokoka hana uhusiano wowote na dhebu lolote lile. Mtu aliyeokoka anakuwa ameokoka tu, na dhehebu kama dhehebu linabaki kuwa dhehebu. Dhehebu ni sehemu ya kuwahubiria au kuwashawishia watu imani iliyopo katika dhehebu hilo. Iwapo linahubiri wokovu vema, iwapo halihubiri wokovu bado ni dhehebu tu.

  2. Ni kweli, kuna baadhi ya madhehebu, mtu akiwepo huko katika madhehebu hayo itatafririwa kuwa bado hujaokoka. Kwa sababu gani; kwa sababu mtu aliyeokoka anatarajiwa kuwa katika ibada ambazo kiongozi wake naye atakuwa ameokoka pia. Iwapo kiongozi wake atakuwa bado hajaokoka, ni wazi kabisa mshiriki wa eneo hilo ataweza kuaminika kuwa hajaokoka. Katika hali ya kawaida, haitarajiwi mtu kuwa chuo kikuu lakini mwalimu anayemfundisha akawa wa Elimu ya shule ya msingi! Au haitarajiwi kuona mtu anasoma masomo ya chuo kikuu, wakati huo huo anaendelea kusoma na masomo ya shule ya msingi.Mtu huyo tutajua anahangaika tu, hajui nini anataka.

  3. Ulokole siyo dhehebu kama nilivyoeleza hapo awali, lakini mtu aliyeokoka inampasa ajiulize kwanza kwamba huo wokovu ameupata kutoka kwa nani! Au kwa lugha nyingine amehubiriwa na nani hata akaamini! Iwapo atakuwa amehubiriwa na kiongozi wake yule yule wa awali, basi anaweza kuendelea hapo kwa sababu huenda siku za nyuma alikuwa anahubiriwa lakini bado alikuwa hajafunguka au hajaamini, na sasa ameamini ameokoka. Lakini iwapo amehubiriwa na mtu wa nje ya hapo anapoabudia, kuna sababu gani ya kuendelea na ibada za hapo? Na kama ataendelea kweli atakuwa anaimarika au atakuwa amezaliwa na kufa?

  Dhehebu ambalo huwezi kuwa ndani yake na ukahesabika kuwa umeokoka ni dhehebu ambalo halimhubiri Yesu wazi wazi kuwa anaokoa. Ni dhehebu ambalo watu ambao hawajaokoka hawahubiriwi waokoke na pia hawaongozwi sala ya toba kuwa watubu dhambi zao kwa kumaanisha kuziacha. Huo ndio mtazamo wa kiroho.

  4. Makanisa yasiyo na uambatanisho na udhehebu [kama nimekuelewa kwamba yanakusanya watu wa madhehebu yote, iwapo kiongozi wake anahubiri wokovu kwamba watu waokoke basi huo ndio mpango wa Mungu hasa, kwa sababu yeye hahubiri dini bali Kristo anayeokoa.

  Kwa ujumla tangu zamani dini zilikuwepo, hata nyakati za biblia dini zilikuwepo pia ambazo zilikuwa hazihubiri wokovu. Pia katika nyakati za agano jipya, kulikuwepo watu ambao walikuwa wanaokolewa kutoka makanisa yanayohubiri wokovu lakini baada ya kuokoka kurudi tena katika dini zao. Ndipo Paulo kwa uchungu sana akaandika katika kitabu cha [2Wakorinto 6:14-18] “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, TOKENI KATI YAO, MKATENGWE NAO, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
  18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi”.

  Pia hata katika Isaya tunaona maandiko yanayofanana na hayo; [Isaya 52:11], tunasoma, “Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana”,unaona!

  Bahati mbaya sijui tuseme, makanisa mengi siku hizi hata yale yaliyokuwa bora zamani, siku hizi yanazidi kupunguza viwango vya ubora na kufanya wanaookoka katika mikutano au kwa njia mbalimbali washindwe kutofautisha kati ya washirika wa dhehebu lao na washirika wengine waliookoka katika makanisa yanayosemwa kuwa ya kiroho. Hakuna tofauti! Mtu aliyeokoka na mtu asiyeokoka hawawezi kutofautishwa, lakini zamani haikuwa hivi, Mungu atusaidia. Maandiko yanatuambia kuwa Mungu atawapatia haki wale wote wanaomlilia mchana na usiku, lakini anayo mashaka iwapo atakapokuja ataiona imani duniani, [Luka 18:7-8].
  Jambo la msingi ni kwamba kila mmoja anapojijua kuwa ameokolewa, afanye hima kutafuta mahali ambapo atashiba Neno, aking`ang`ania na dhehebu lake, siku ya mwisho atajikuta anaachwa na asijue ni kwa nini! Kumbe ataachwa kwa sababu hakuyafuata maagizo yote ya Mungu kama maandiko yasemavyo [Zaburi 119:6]. Kuyafuata maagizo yote ya Mungu haitakuwa rahisi iwapo mtu baada ya kuokoka bado ataendelea anang`ang`ania dini au dhehebu lake ambalo halihubiri kweli yote.

  Amani ya Bwana!

 43. Levana Katana,
  Ni swali zuri lenye kumtaka anayelijibu ajitosheleze kwa hoja kwa kufuata nini neno la Mungu linasema au kutaka.Kwa sasa sitasema chochote kwanza mpaka hapo baadaye ila tu nataka kuwakumbusha wachangiaji wengine wasiandike tu kutokana na utashi wao binafsi bali hoja zote ziangalizwe kwenye dira yetu kuu ambayo ni neno la Mungu yaani biblia.Pia naomba tutofautishe kati ya harusi(ndoa) ambayo ni ibada kamili kulingana na mahali inapofungiwa na sherehe za harusi ambazo kikawaida huwa hazina taratibu za kiibada(ingawa baadhi zinazo).Kuanzia hapo tunaweza sasa kuanza kuchangia.Nimesema hivyo kwa sababu nimeona wengine wanasema ndoa na ziheshimiwe na watu wote, lakini hapa muuliza swali ameomba tu kujua kuwa ni halali kwako wewe/kwetu sisi tuliokoka kushiriki sherehe ya harusi ya mtu ambaye hajaokoka.Wengine wamefikia kusema alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe,kwani kushiriki au kutokushiriki sherehe ya harusi kunahusika vipi na kutengaisha wanandoa?
  Mpendwa Mary Sabihi nimesoma kama ulivyotuomba wote tusome Rumi 12:15 na maneno ya Mungu yanasema hivi “Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wenye kulia”(nukuu kutoka biblia mpya ya NENO iliyotafsiri toka NIV).Ni kweli neno la Mungu linatutaka tufanye hivyo lakini nikajiuliza ndg yangu Mary ukimkuta jambazi aliyefanikiwa kuiba fadha nyingi benki anafurahia ‘mafanikio’ hayo je utafurahi pamoja naye? Au ukimkuta kiongozi mla rushwa anafurahia mapato au ‘mafanikio’ yake je nawe uliyeokoka utaendelea kufurahi pamoja naye? Hii ni mifano michache tu ambayo nilitaka kukuangaliza kuwa sio kila kitu tunaweza kufurahia pamoja na wafurahio.Shetani naye hufurahi sana anapoona kundi kubwa la watu wanamfuata, sasa lile kundi dogo lililobaki haliwezi kufurahi pamoja naye.
  Naomba tuendelee kujifunza kwa upole na unyenyekevu mkubwa.

 44. Mimi nadhani, sisi kama watu tuliookoka, iwapo ndugu zetu wa kimwili wataoa au kuolewa, tutawaunga mkono kuwa jambo walifanyalo ni jema. Lakini bado hatutaweza kushiriki kikamilifu katika shamra shamra zao za arusi. Tutashiriki katika kupata taarifa za kujua anaolewa na nani au anamwoa nani na siku ipi wanahitimisha ndoa yao. Zaidi ya hapo tuwaache wapange mipango yao wenyewe japo ndoa hiyo itakuwa ni halali,lakini kwetu sisi tuliookoka ndoa hiyo si ya watu walio katika haki. Kwa sababu gani, kwa sababu watu hao hawajamjua Mungu tunayemwamini sisi, ambaye ni Kristo Yesu. Hivyo hata taratibu zao za sherehe zitakuwa kinyume na mpango wa Mungu. Maandiko yanatuagiza kuwa tusifuatishe namna ya dunia hii, “Warumi 12:2”. Kutokana na hilo, iwapo sisi tutashiriki kikamilifu, tunaweza kujikuta tunashiriki ngoma za mashetani.

  Mimi katika mtazamo wangu ni kwanba, tuwaache waoane lakini la msingi kwetu ni kuwahubiria injili ili waokoke, kwa sababu kuoa au kuolewa siyo njia ya kwenda mbinguni japo tutasema kuwa ndoa yao ilikuwa ya halali. Tusipoenda katika sherehe zao siyo dhambi, na kama tutakwenda, iwapo kweli tumeokoka, tutakapokuwepo katika sherehe hizo hatutakuwa na amani kutokana na yale yatakayokuwa yanaendelea hapo!

  Kama ilivyo vyema kwetu tuliookoka kwa mtu ambaye hajaokoka kupata mtoto, ndivyo inavyokuwa vyema pia kwetu kwa mtu ambaye hajaokoka kuoa; mambo hayo siyo dhambi ni halali.

  Note: Arusi zao zitakuwa ni halali hawataruhusiwa tena kuachana hata kama watakuja kuokoka.

  Amani ya Kristo.

 45. Shalom,

  Wapendwa, mimi naomba nichangie kwa mtazamo tofauti kidogo,
  Nimepata swali, naona wengi mnajibu ni sawa; ni sawa kusherekea nini? Inawezekana ni sawa au si sawa vilevile unless kama unajua nini ni sahihi na kipi si sahii.

  KatikA harusi, sherehe za kuzaliwa na misiba kuna mambo mengi yanayofanyika kulingana na mila, desturi, kawaida za ulimwengu ambazo nyingi haziendani kabisa na maadili ya ki-Kristo. Tunahitaji kufanya kila jambo kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Ukijiuliza
  Kwa nini naenda, kwa faida gani na Ili iwe nini?

  Warumi 12;2
  Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

  Si kila sherehe lazima uhudhurie, inategemea. Kuna mazingira ambayo yanaweza kukulazimu, kama misiba, japo hatushiriki kila kitu e.g kuna aina ya sala, mila, desturi na taratibu hazituhusu. Pia kuna baadhi ya sherehe inaweza ikakulazimu, tuna ndugu, majirani, wafanyakazi wenzetu wengi tu ambao hawajaokoka; lakini hatushiriki kila kitu e.g, aina ya usherekeaji, miziki, vileo e.t.c . Lakini ni muhimu kujua hatuishi ili kuifurahisha jamii au kujitahidi kuwaridhisha watu bali kuyatimiza mapenzi ya Mungu, kwa hiyo Roho Mt awe mshauri wako mkuu

  Nia na dhamira ya Kristo ilioumbika ndani yetu, siku zote inatakiwa kuwa ndani ya mapenzi ya Mungu ndiyo kitu cha msingi. Lazima upate uongozi wa Roho Mtakatifu, hata mitume walipokuwa wakieneza injili walihitaji uongozi japo injili ilikuwa ni muhimu kwa kila mtu aipate lakini bado kuna mahali hakuwaruhusu, maana alijua mbele kuna nini sasa sembuse sherehe tu za kidunia ambazo ni kwa ajili ya kuufurahisha mwili tu na nyingi ndani yake kumejaa uharibifu tele. Kuna wakati unaweza kuwa na nia njema ya kufanya jambo fulani lakini yatakayotokea huko hatuyajui na inaweza ikawa hasara kwetu, ila ni ngumu kwetu kujua sababu hatujaruhusu masikio, macho ya rohoni kusikia sauti ya Roho Mt kutuongoza, kutushauri katika KILA jambo na kutufunulia yaliyo sirini..

  Wapendwa wengi hatujui mipaka yetu na wala hatuna muda kumshirikisha Roho atongoze. Kuna wengi tu wanajichanganya eti waende kitchen party hii mara ile, wakati ndani ya hizo kitchen party watu wasiomjua Mungu wanaruhusu mashoga kumfunda bibi harusi, wengine wanawasindikiza rafiki zao bar, disko eti kwani itanidhuru nini? Je tunajifunza nini?
  Kuna sherehe au makusanyiko mengine yaweza kukuchafua, kukukwaza na kukuingiza katika mitego isiyofaa. Tusipende kuifurahisha sana dunia kuliko Mungu, kuna wakati ni bora lawama au kuhukumiwa na ulimwengu, kwa mambo ambayo hayana utukufu kwa Mungu otherwise tutayumba , tutatetereka.

  Na ndo maana siku hizi kuna harusi za kilokole utashangaa, hazina tofauti na za watu wa dunia.
  Juzi juzi katika kipindi cha chereko chereko kinachorushwa na TBC 1 kuna harusi ya walokole maarufu kabisa ilinishangaza mno, sikujua kwa urahisi lakini nlishangaa kusikia njimbo za injili zikipigwa kwa wingi lakini the whole sherehe imejaa mfumo, theme zile zile za kidunia, show off, sifa ushindani e.t.c.

  Wakorintho 2;12-13
  Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
  Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

  Tupo pamoja kujifunza.

 46. jamani hakuna ubaya wowote . pia mungu hapendi tujikweze. sasa dada/kaka uliyeuliza swali umekosea , maana umesema ni vizuri kwa mtu aliyeokoka kwenda kwenye harusi za wasiookoka, kama wasabato, waroma nk. lakini ukumbuke dhehebu ni jina tuu na dini tutaviacha hapa hapa . wapo wasabatato na waruteli wameokoka sana, na labda kuliko wapendekoste . maana wapendekoste tunapenda kujikweza mno . kila mara tunawambia wenzetu wameng’ang’ania dini . lakini sisi pia tunafanya yale yale tunaweka ukuta mkubwa kwamba sisi tuu ndio tuliookoka na wengine bado.MUNGU HAPENDI MAANA AJINYENYEKEZAE ATAKWEZWA NA AJIKWEZAE ATASHUSHWA.

 47. Swali la Ndg Levana lauliza “Je ni sawa kwa mtu aliyeokoka kusherekea harusi ya ndugu ambaye hajaokoka? kwa mfano mkatoliki, msabato, muislamu n.k?”
  Swali hili limenifanya kujiuliza maswali mengine ambayo nina imani kwa nikipata majibu yake itanisaidia kuchangia vema hapa.
  1: Kwanza NAOMBA TAFSIRI YA mtu aliyeokoka na uhusiano wake na dhehebu lolote lile.
  2: Na ndg Levana amemalizia kwa kusema “n.k” ambayo naamini kuwa yamaanisha NA KADHALIKA. Neno hili kuja baada ya kutaja madhehebu yaonesha kuna madhehebu mengine ambayo kuwemo ndani mwake kwakufanya uonekane HUJAOKOKA.
  3: Ina maana mtu hawezi kuwa ndani ya uSabato ama uLutheri ama uAnglikana ama dhehebu jingine na kuwa AMEOKOKA?
  4: Ina maana ULOKOLE NI DHEHEBU? Na kwamba ukishaokoka yakupasa ujiunge na dhehebu hili na kulikana ulilokuwemo? Ama ni madhehebu gani ambayo hauwezi kuwa ndani mwake na kuhesaka (kwa mtazamo wenu wa kibinadamu) kuwa umeokoka?
  5: Vipi kuhusu makanisa yasiyo na uambatanisho na mahehebu na ambayo yanaongozwa na watumishi (kama ya kina Joyce Meyer, Joel Osteen, T.D Jakes na wengine). Hawa nao watakuwa wapi kwenye swali hili?
  NTAULIZA MASWALI MENGINE KADRI YAJAVYO NA NAENDELEA KUSUBIRI MAJIBU TOKA KWA YEYOTE AJUAYE MAJIBU YA MASWALI HAYA

 48. Sherehe ya harusi ni ya kifamilia.Hushirikisha ndugu wote waliokoka, wapagani , waislamu nk. Na hufanyika kwenye kumbi, na si kanisani. Ni mahali ambapo kila mmoja hufurahi , hata ndugu walookosana siku nyingi huweza kupatana. Kuna sherehe kuu tatu ambazo mtu hufanyiwa katika maisha yake:
  1. kuzaliwa
  2.sherehe ya ndoa
  3.Kuzikwa.

  Hizi sherehe hazina ubaguzi wowote. Watu wote hushiriki pasipo kujali dini.

 49. Why not!Ni sahihi kabisa sio kusherekea tu bali na kutoa ushirikiano kwani ndoa ni Mungu ndiye anayeunganisha na ni sharti iheshimiwe na watu wote waamini na wasioamini pia.Ndoa ni takatifu.Je ni kanisa gani la waliookoka tu? Hata yesu hakufanya hivyo alishirikiana na wote LUKA 19, 15:1-2).Siku hizi kuna makanisa ambayo wachungaji wao huwalazimisha watu wakiokoka wawaache wenzi wao wasiookoka na waoe wapendwa wenzao, hayo ni mafundisho ya kishetani na yatatupeleka motoni,kani aliyounganisha Mungu mwanadam asitenganishe.GOD BLESS YOU ALL!

 50. why not ? i mean why shouldnt he/she ? kama anaweza kufanya kazi na watu wa mataifa definetly anaweza kusheherekea

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s