Ndoa Takatifu

Hii dhana (concept) ya ndoa takatifu ina maanisha nini? Kuingia kwa undani zaidi, naomba tujadili dhana hii kwa kuzingatia maswali yafuatayo:

1. Je ndoa takatifu ni ipi, na Maandiko yapi yanaunga mkono hoja hiyo?

2. Je mahali ilipofungishwa ndoa panapelekea hiyo ndoa kuwa takatifu au kinyume chake? Mfano, kama ndoa imefungwa bomani au kimila, haiwi takatifu hadi iwe imefungwa kanisani, tena katika kanisa linaloamini wokovu?

3. Je, kama wanandoa wakati wanaoana walikuwa hawajaokoka ndoa yao itahesabiwa kuwa ‘takatifu’ au la?

4. Na vipi kuhusu mwanamume na mwanamke ambao wameishi kwa miaka mingi, na pengine kupata watoto, lakini hawajawahi “kufungishwa ndoa” mahali popote – bomani, kimila, msikitini, au kanisani – je ndoa yao itahesabika kuwa takatifu au la?

5. Hii dhana ya “ndoa takatifu” kihistoria ilianza lini?

Ahsante.

Joel
Advertisements

8 thoughts on “Ndoa Takatifu

 1. BWANA YESU ASIFIWE WOTE
  NAMI NAOMBA NICHANGIE KAMA IFUATAVYO
  ILI NDOA IWE TAKATIFU YAFUATAYO LAZIMA YATIME
  1.KWANZA WENZI WAWILI LAZIMA WAWE WATAKATIFU KWA MAANA YA KUMWAMINI YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU (1PETRO 1:15)
  2.WOTE WAWE TAYALI KUWAACHA WAZAZI WAO NA KUKUBALIANA KUSHI KAMA MME NA MKE NA KULIDHIWA NA WAZAZI WA PANDE ZOTE NA KUTAMBULIWA HIVYO KATIKA JAMII (MWANZO 2:24)
  3.KUFUNGISHWA NDOA NA MTU AMBAYE NI MTAKATIFU KATIKA MWENENDO WAKE WOTE YAANI ANAYE MPENDA YESU KWA MAANA YEYE MWENYEWE AMEOKOKA NA WALA HAPINGI WOKOVU,NA ANAHESHIMIWA NA MUNGU
  UKWELI WA MAMBO NDOA NYINGI ZINAFUNGWA MAKANISANI HAZIWI TAKATIFU LICHA YA KUFUNGWA KWENYE MAKANISA MAKUBWA
  (a)KWANZA MAKANISA MENGI YANAPINGA WOKOVU WANAPINGANA NA MUNGU ANAYESEMA KUWA ANAPENDEZWA NA WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI NA ANAPENDEZWA NAO SOMA (ZABURI 16:3) SASA UNAKUTA MAKANISA MENGI WANAPINGA WOKOVU WANASEMA HUWEZI KUOKOKA UKIWA DUNIANI WANALUSU WATU KUNYWA KIDOGO,KUZINI,NA KILA JUMAPILI NI WATU WA KUTUBU KWA VIONGOZI WAO WA DINI,KWENYE MAKANISA HAYO WATU WAONJA NA KUPEANA MIMBA NDIO NDOA ZINAFUNGWA HUKO NI KUMCHEZEA MUNGU

  BALIKIWA KWA MCHANGO WANGU

 2. Bwana Asifiwe wapendwa katika Bwana! naomba tujadili kidogo hii mada. Niliipenda sana japo haikupata michango mingi kutoka kwa wadau

 3. Shalom!

  Mimi ninaomba kuchangia kuanzia pale kaka Benard alipoishia. Utakatifu katika ndoa una sura mbili tofauti. unaweza ukautazama kwa kuangalia utakatifu wahusika yaani wanandoa, na utakatifu wa ndoa kama taasisi.
  Ndoa inaitwa takatifu kwa kuwa ni taasisi iliyoundwa na Mungu Mwenyewe kwa kusudi la kuendeleza uumbaji wake. kwa sababu hiyo Mungu aliumba ndoa ikiwa ni sehemu ya kusudi lake la kuijaza dunia yaani kuendeleza uumbaji. kama jinsi aliyeiumba taasisi hiyo alivyo mtakatifu ndivyo ilivyo takatifu.

  upande wa pili ni kwamba, utakatifu wa ndoa unaweza ukatazamwa kwa kuwaangalia wanandoa, katika upande huu napenda kuweka wazi kwamba kama kuna wakati ambapo mtu anahitaji zaidi kuokoka, ni pale anapotaka kuingia katika ndoa. sababu ya msingi hapa ni kwamba ndoa ikiwa ni taasisi iliyoumbwa kuendeleza kusudi la mungu inafanikiwa ndani ya kusudi la mungu tu. kwa kuwa nia ya shetani ni kuzuia makusudi ya mungu yasifanikiwe, target ya kwanza anayochagua kuishambulia ni ndoa.kwa sababu hii, ili wanandoa waweze kupambana vita hii ya kiroho wanahitaji wao kwaza kuokoka na ndipo watakapokuwa katika nafasi ya kupambana na shetani na kuhakikisha ndoa yao inakuwa chombo alichokusudia mungu kuendeleza makusudi yake katika kutengeneza uzao wa ufalme.
  Mungu awabariki.

 4. Nakubaliana moja kwa moja na Bernard Mwenda. Mungu akubariki sana. Endelea kumwinua Yesu aliye hai

 5. Ndoa ni kati ya watu wawili wanaopendana ki kweli na kama walioana kipindi hawajaokoka wakiokoka kila kitu kinakuwa kitakatifu mpaka hiyo ndoa ya bomani,unapotubu dhambi zako maana yako unatubu mpaka tendo la kufunga ndoa bomani unahama gizani na kuingia nuruni na vyote ulivyonavyo,pia ndoa takatifu ni ile ambayo watu waliomwamini yesu yaani wameokoka ndiyo wanandoa takatifu inayofungwa mbele za Yesu Kristo kupitia mpakwa mafuta wake kama wataenda kurumbana nyumbani ni wao na ni hira za shetani tu,bila yesu kuanzisha ndoa hakuna utakatifu katika ndoa hiyo nionavyo mimi.

 6. Na je wale ambao wameoana wakiwa wameokoka vizuri na kufunga ndoa ktk kanisa linaloamini wokovu na baadae wakaanza kulumbana ndani ya ndoa na ugomvi,je itaendelea kuitwa ndoa takatifu?.

 7. Utakatifu wa ndoa hauwezi kuonwa machoni pa wanadamu, bali ni mbele za Mungu tu, maana kuna usiri sana wa kibinadamu katika matendo na maisha yanayozunguka mazingira ya ndoa.

  Kwa mtazamo wangu pindi ndoa yoyote inayofungwa madhabahuni huwa inakuwa takatifu kwa wakati ule. Sasa muendelezo wake ndiyo tatizo, ama iendelee kuwa takatifu au ibatilike kutokana na matendo yanayozunguka maisha ya ndoa.

  Kuna baadhi ya watu wanapenda kuhalalisha baadhi ya matendo hata kama kimsingi ni makosa, kama vile kutokuwa na ukaribu na familia kwa ajili ya kutekeleza majukumu mengine ya kibinadamu.

 8. Shalom wapendwa!
  Mimi katika mtazamo wangu kuhusu ndoa, tunaposema ndoa takatifu, kwa kifupi, ni ndoa au maisha ya watu wawili, mme na mke, wanaoishi katika maisha ya utakatifu yaani maisha ya wokovu. Watu hao wawili, wawe wametimiza vigezo vyote vya kuwa mme na mke. Hiyo ndiyo ndoa takatifu.

  Mwanzo wa ndoa takatifu unaweza usiwe mzuri. Wahusika wanaweza kuidhinishiwa ndoa yao na wanadamu wakiwa katika sehemu tofauti tofauti, mfano: bomani, katika mila, madhehebu ya kidini, wakati mwingine hata katika makanisa yanayohubiri wokovu. Lakini pamoja na kuidhinishwa katika maeneo haya, bado ndoa hizo zinaweza kuwa siyo ndoa takatifu.

  Utakatifu wa ndoa unaanzia pale wahusika wanapokuwa katika kweli ya Neno la Mungu pasipo lawama yoyote, mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Utakatifu huu kama nilivyoanza kusema hapo mwanzo, upo katika wokovu katika Yesu Kristo. Kwa kifupi zaidi ni kwamba, bila wokovu katika Yesu Kristo, ndoa inaweza kuwa halali lakini ikawa siyo takatifu.

  Kwa sasa nasimama hapa, na wengine tuendelee kuchangia.

  Amani ya Kristo itufunike.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s