Mahusiano yanapovunjika!

Shalom, Nimekaa na msichana zaidi ya miaka sita ya urafiki na mahusiano yetu yamevunjika wakati tumeanza kujitambulisha kwa wazazi, naomba mtuombee ili tuweze kurudisha mahusiano yetu na tuwe tayari katika utambulisho hadi tuweze kufunga ndoa, tunahitaji kufanya hivyo maana tumekaa Muda mrefu na tulipendana sana kwa hiyo nashangaa imekuwaje hadi tunavunja kitu tulichokijenga kwa miaka mingi.

–Aidan, silk_aidan@yahoo.ca

16 thoughts on “Mahusiano yanapovunjika!

 1. Hero ya,mwaka mpya,tunashangilia siku zote katika kristo Yesu , utukufu una yeye milele na milele

 2. Sam,
  SIYO LAZIMA UFUATE USHAURI HUU LKN UTAKUSAIDIA MARA TU UTAKAPOMALIZA KUSOMA.
  USILAZIMISHE: nakushauli jipange kwa upya anza kwa upya, usiendelee kusubiria kitu ambacho hakipo.
  tumia muda wa kutosha kwa kupata utulivu ili kuruhusu nguvu za Mungu kuiponya nafsi MAPEMA!!!!.
  jiponye nafsi yako kwakutokubali kulazimisha vitu ambavyo avipo; pia usikubali kukumbatia kivuli,
  kuna mtu mmoja aliambiwa na Mungu jiponye nafsi yako.(Ruthu) nami ninakushauli katika hili jiponye nafsi yako kabla ujaruhusu mfumo wa mwili kutibuka na kutengeza presha ya juu au ya chini/ sukari ya juu au ya chini au kupata kichaa cha fikra na kuanza kuchukia kila mtu atakayekushauri tofauti na unavyotaka.
  coz usipokuwa makini ktk hili kichaa cha fikra kitakusukuma kufanya maamuzi usiyo tarajia then baada ya miaka michache utagundua kuwa si wewe uliyeamua bali kichaa furani aliyeota ndani yako ndiye aliyeamua kile ulichokumbatia sasa….

  USITUMIE MUDA MWINGI KUSIKILIZA WALE TU WANAOKUHURUMIA COZ UTACHELEWA KUPONA NAFSI YAKO.
  TOA MUDA KUSIKILIZA HATA WALE WASIOKUHURUMIA AU KUKUUNGA MKONO COZ KUNA KITU FURANI UWA WANAKIONDOA NDANI YAKO PALE WANAPOSEMA HAPANA.

  MWISHO: usipende kuhurumiwa wala kujihurumia. ENDELEA MBELE.

 3. Mungu ndio kila kitu (luka 1:37) Mwambie yeye anaweza! sisi tunaweza kukushauri leo na ushauri huo usikusaidie. halafu wengine tunaweza kukuhukumu tu hapa na kukukatisha tamaa ushauri wangu ni kwamba,rudi magotini ndugu yangu mtafute Mungu ni mwaminifu atakwambia kwa nini mahusiano yako yameyumba hivyo mwishoni. naamini utapata majibu next time utatwambia majibu ya swali lako wewe mwenyewe

  barikiwa!

 4. Shalom, dada Easter,

  Kwanza nashukuru kwa kuupokea ushauri wangu.

  Pili nikutoe wasi wasi kuwa ninachoongelea ninakifahamu kabisa, nimeshawahi kukutana na hiyo hali na kwa sababu Yesu aliniwezesha kushinda basi na ninajua hata hiyo ‘OBLONGATA’ ikitiishwa chini ya Yesu inatii na kutulia sababu imeandikwa.

  Mithali 3;5-6
  Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

  Dada yangu, kuna wakati tunafanya maamuzi ambayo machoni petu tunaona au hisia zetu hutupelekea kudhani kuwa sahihi kumbe mwisho wake huenda ukawa mbaya sababu Mungu ndiye hajua undani na yatakayojitokeza mbele (mazuri au mabaya).

  Mithali 16:25
  ‘Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti’
  Namfahamu Mungu ninayemwamini katika jina la Yesu hakika hakuna neno gumu kwake.

  Kuachwa ni kweli kunaleta maumivu kibinadamu, lakini haimaanishi kuwa yakufanye ung’ang’ane tu hata pale inapogungua mahusiano yenu (ya muda mrefu) mliyoyaanzisha hayana future nzuri kwako, hayapo chini ya mpango wa Mungu na pengine baadaye yanaweza yakakuletea mwiba wa maisha. Na saa nyingine si kwamba utasikia sauti ya Mungu physically bali atainua kikwazo kitakachozuilia ndoa hiyo.

  Pia ujue katika maisha kuna majaribu mengi tu ambayo Mungu ana / ata ruhusu ili kupima imani zetu na pia kutufanya imara zaidi.Na saa nyingine anaruhusu jaribu la muda tu halafu ukimtii anakurudishia mumeo.
  Unafikiri ilikuwa rahisi kwa Ibrahimu kukubali kumtoa Isaka, ‘the only son’ ili akafe? alimpenda sana. Lakini alimpenda Mungu zaidi hata akawa tayari kupoteza mtoto ambaye alikuwa ni wa thamani / faraja /tumaini na furaha kubwa sana kwake.

  Ni kweli tunatakiwa kuwaombea wachumba, japo sijajua unaomba vipi, na katika hatua ipi?

  1) Kwamba kwa kuwa umeona kuwa anakufaa basi unamuombea tu ili asikuache hata kama si mpango wa Mungu ?
  2) Tayari Mungu amekuthibitishia kuwa anakufaa na ametoa kibali cha ndoa kwa hiyo unamuombea ili ulinzi wa Bwana uwe juu yake kwa ajili ya kutimilizwa kwa lile kusudi la ndoa kati yenu,( maisha na kumtumikia Mungu pamoja)?

  Mimi ninachoshauri ni kuwa, katika mchakato jambo lolote katika maisha yetu i.e ndoa, tuwe tayari kusikiliza na kupokea uongozi wa Mungu hata ikionekana kuwa njia tuliyoenenda / chaguo tulilofanya si sahihi na tunahitaji kuanza upya bila kujali umepoteza muda, mali au sifa kwa watu.

  Na katika mahusiano ya mapenzi / uchumba ni muhimu kuzingatia

  1) Kumtafuta Yesu kwa bidii, kuyajua mapenzi yake na kulinda roho yako katika ‘WOKOVU’
  2 ) Kutunza mwili wako (hekalu la Roho Mtakatifu) kwa kutoruhusu ngono kabla ya ndoa

  Miaka 6, 10, 20 e.t.c unayoweza ukawa umepoteza katika chaguo ambalo si sahihi au mkono wa Mungu haukuwa juu yake si kitu cha kuhofia au kukuvunja nguvu na kukusababishia ukate tamaa, uone sasa ndo mwisho wa maisha, hata ukamkosea Mungu, ukakufuru, ukataka kujiua au kuacha kutunza uaminifu wako kwa Mungu.

  Hapana, hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea. Mlango mmoja ukifungwa, Mungu hufungua mwingine.

  Nawapenda wote, tuendelee kujifunza
  Dada Imani.

 5. SHAROM
  DAD IMANI, USHAURI WAKO NI MZURI SAANA, ILA HUJAWAI KUACHWA HATA SIKU MOJA NAZANI.
  SIKU UKIACHWA UTAONA JINSI OBLONGATA INAVYOCHANGANYIKIWA.
  IN SHORT TUSHAURIANE KUWAOMBEA WACHUMBA TULONAO NA SI VINGINEVYO.

 6. Shalom!

  Ni kweli kabisa kama usemavyo dada Lisa, vya Mungu huwa vina upinzani sana.Kitu pekee kinachohitajika ni kuhakikisha pamoja na changamoto zozote tunazopitia ni lazima tuwe na msimamo wa kutunza utakatifu na usafi wa miili na roho zetu. Kama ni jaribu ambalo halijatokana na kujichangaya basi ni lazima Bwana ataongoza na kufanikisha sawa sawa na mapenzi yake na haja za mioyo yetu

  Kuna watu wengi wamapoteza waume / wake zao kwa kuharibu / kuchafua mahusiano yao katika hatua za uchumba.
  Mie nina toa ushauri kwa vijana wenzangu, kama ni kweli unapitia changamoto katika uchumba lakini maadam unasimama katika uaminifu kwa uwezo wa Yesu Kristo Aliyeushinda ulimwengu kwanza basi huna haja ya kuhangaika, jitie nguvu, msifu Bwana kama Paulo na Sila na hakika utashinda.

  Ngoja niwape ushuhuda mmoja;

  Kuna dada mmoja alikuwa ameokoka na kumtumikia Bwana kwa uaminifu. Akawa ameonyeshwa kijana fulani katika kanisa alilokuwa akiabudu, lakini wakatofautiana katika jambo hili, kaka alikuwa hana uvumilivu na alionyesha haraka na tamaa pia.

  Basi kaka akaamua kumchumbia dada mwingine kanisani na ndoa ikatangazwa. Yule dada wa kwanza aliumia sana lakini alivumilia kwa kuwa hakuwa na hatia mbele za Mungu na alijua Mungu atamtengeneza njia.

  Harusi iliandaliwa na siku ya siku kaka akamwoa yule dada wa pili. Maharusi walipokuwa wakitoka kanisani kuelekea nyumbani gari lao likapata ajali na bibi harusi akafariki.

  Kilichotokea yule dada wa kwanza baadaye akaja kuolewa na yule kaka kama alivyoonyeshwa

  Tunachojifunza hapa ni kuwa, mwenye haki siku zote atasimama, usiogope kuachwa, cha msingi upo safi mbele za Mungu ni bora uachwe mara 100 na wachumba ukiwa safi kuliko kumpoteza Yesu.Maumivu yake hayatakuwa makubwa coz Bwana atakuwa upande wako.

  Wengi wanaumia coz anapochumbiwa kwa kuogopa kumuudhi mwenzie yupo tayari afanye naye uzinzi kwa kuwa ana uhakika atamwoa so anapoachwa anabaki na jeraha, anajiona hafai tena, anakata tamaa.

  Nawapenda sana
  Dada Imani

 7. BWANA YESU ASIFIWE SANA!!

  KITOKACHO KWA MUNGU MARA NYINGI KINA UPINZANI.
  SHETANI ANAJUA AKIVAMIA ENEO LA NDOA ATAWAPATA WENGI.
  NDIYO MAANA UCHUMBA HUVUNJIKA SIKU CHACHE KABLA YA NDOA. AU HATA NDOA NYINGINE ZINAKUWA HAZINA MAHUSIANO MAZURI YA NDANI.

  VIJANA WALIOOKOKA WENGI IKISHATOKEA TATIZO KAMA HILI WANAJITAFUTIA JIBU LA “HAIKUWA MAPANGO WA MUNGU TUISHI WOTE”. KUMBE SHETANI NAYE HUWEKA MKONO KWENYE HAYA MAHUSIANO ILI TU KUVURUGA SO LONG AS AKISHAWAVURUGA NDOA HAKUNA TENA. WENGINE HUISHIA KUINGIA KWENYE DHAMBI, AU KUOLEWA/KUOWA MTU AMBAYE HAKUWA AMEPANGA.

  KAMA TUNAVYOJUA KWENYE NDOA NDIO KWENYE UUMBAJI. CAN U IMAGINE MADHARA YANAYOTOKEA SHETANI AKISHIKA ENEO HILI LA UUMBAJI. VERY BAD!!!!!
  SHETANI ANAWEZA KUVURUGA UZAO KWA UJUMLA KAMA WALE WANAOOANA HAWAKUWA KATIKA MPANGO WA MUNGU.
  WENGI WANAOPATA MATATIZO HAYA HUKATA TAMAA, SASA ANAPOKUJA KUOLEWA/KUOA NA MAJERAHA YA KUACHWA ALL IN ALL NDOA HII ITATOA WATOTO WA KIMAJERAHA MAJERAHA IWAPO WANANDOA HAWATASHTUKA MAPEMA NA KUVUNJA HIZO ROHO.
  ENEO LA NDOA NI MUHIMU KULINDWA TANGU KWENYE UCHUMBA MPAKA NDOA. HAPA KUNA UUMBAJI KWA HIYO SHETANI ANADILI SANA NA MAENEO HAYA ILI AKAMATE WENGI.

  TUWE MAKINI KWA KUOMBA ILI TUUSHINDE UPINZANI WA SHETANI WAKATI WA MAHUSIANO YANAYOPELEKEA NDOA.

  TUNAJIFUNZA

 8. Aidan,
  Ni vema ukamtafuta huyo binti mkaa na kuzungumza ili akujulishe wazi kwa upendo sababu za yeye kubadili msimamo wake.
  Nashauri ukae wewe na huyo binti na mchungaji wenu ili mfikie muafaka mzuri.

 9. Nashukuru kwa maswari yenu na nimeyaelewa, katika mausiano yetu tuliishi katika kumtegemea Mungu japo hatukuwa indeep sana, na kama unavyoelewa makosa yalikuwepo mara mimi nimekosa au hata yeye kukosea, lkn ninachoongelea ni pale alliponitambulisha kwa mama yake, na mama yake kumuuliza kuwa yuko tayari kuwa na mimi naye akakubali, nami niliisha mtambulisha kwetu kabla ya hapo, shida ilikuja pale wakati wazee wangu walipoamua kumfata baba yake maana baba yake yuko mikoani, naye baba yake kwa kuwa hakufahamu juu ya mausiano yetu aliamua kuwaeleza kuwa atalishughulikia mean kuwasiliana na mtoto pamoja na mama, alipomuuliza mama akakubali lkn alipomuuliza mtoto akakataa, wote tuna imani moja maana ni wakristo,
  kama mna maswari msisite kuuliza,
  nashukuru sana

 10. Ndugu Aidan,

  Mimi ninaamini ulipoamua kuleta hitaji lako hapa ulimaanisha kabisa ya kwamba kweli unahitaji msaada wa maombi. Na ni jambo la kutia moyo kwamba tayari watu wamejitokeza kukuuliza baadhi ya mambo ili waelewe. Ninaamini kuwa nia ya kuuliza maswali hayo ni njema tu ili kufahamu ni namna gani mtu aombee hitaji lako.

  Kwa hali ya kawaida watu wengi huwa wanahitaji maombi lakini utakuta kumbe anachohitaji si maombi bali ni yeye mwenyewe kuchukuwa hatua katika mambo fulani, au unaweza kukuta, kwa mfano, yeye mwenyewe ndiye sababu ya tatizo. Katika hali ya namna hii hata watu wakiomba namna gani, hakuna kinachoweza kubadilika.

  Katika Biblia tunapata ile habari ya mtu mmoja, tajiri, aliyemuuliza Yesu juu ya nini afanye ili aurithi uzima wa milele. Baada ya kuulizwa hivyo Bwana Yesu hakumjibu moja kwa moja kwamba anatakiwa afanye hivi na vile. Tunaona jinsi ambavyo ilibidi amuulize maswali kadhaa ili mtu huyo aweze kujitambua alivyo na baada ya kujitambua ndipo aambiwe ni nini anachotakiwa kufanya. [Marko 10:17-21].

  Ninavyoona mimi ni kwamba hayo maswali uliyoulizwa tayari ni hatua za wewe kupata msaada unaouhitaji. Kinachotakiwa kwako ni kutambua hilo na kisha kujibu maswali hayo. Kujibu maswali hayo kutasaidia mtu anayeomba aombe vipi au akushauri vipi!

  Kutokujibu maswali uliyoulizwa, mimi naona, hakutakuwa na maana yoyote ya wewe kuleta hitaji lako hapa!

  Ninaamini utajibu maswali hayo ili uweze kupata msaada unaostahili!

 11. Pole sana kaka kwa yaliyokukuta.kwa maoni yangu suala lako linaweza kuwa gumu sana kupatia ushauri kwani hujatoa maelezo ya kujitosheleza, mimi binafsi bado najiuliza maswali yafuatayo:
  1.Umesema mahusiano yenu yamevunjika bila kutaja chanzo
  kilichosababisha mahusiano kuvunjika.
  2.Hatujui imani zenu ninyi wawili, je mna imani moja?
  3.Mulikuwa wawazi katika kuzungumzia hatima ya mahusiano yenu?MAANA YAKE mnaweza kupendana lakini si kigezo cha kufunga ndoa na kuishi kama mme na mke.
  4.Sijui kama katika mahusiano yenu mlitunza usafi wa mioyo yenu i.e uchumba wa kikristu
  5.Nashindwa kufahamu mliwezaje kukaa zaidi ya miaka sita ktk mahusiano pasipo kutambulishana kwa wazazi?
  Nikija kwenye suala lenyewe,mimi naona kama mlifuata taratibu zote zinazohusu uchumba na kuishi ktk imani basi kuna haja ya kuomba na kumlilia Mungu naye atafanya njia kwani yawezekana ni jaribu la shetani kutaka kuyumbisha imani yenu kwa Mungu.Pia ni vizuri mkakaa na mwenzi wako kujichunguza kama kuna sehemu mlimwacha Mungu ili kusimama kwenye lango kuomba toba kwa damu ya Yesu.zaidi ya yote bado Mungu ndiye mwenye maamuzi kama ndoa yenu ilikuwa mpango wake au la,ni vizuri kumsikiliza Mungu anasema nini kuliko kuangalia mapendekezo yetu kwani sisi tunaangalia kwa nje bala Yeye anaangalia moyo.Inawezekana huyo uliye naye ni Yona Mungu ameona akimruhusu kuingia kwenye merikebu atasababisha bahari ichafuke na hatimaye merikebu kuzama na kuwaangamiza.kwa kifupi ni hayo tu niliyonayo kwa maoni yangu,MUNGU AKUBARIKI SANA NA AKUPE JIBU LA TATIZO LAKO!

 12. Mpendwa pole sana, huenda uhusiano wenu una kusudi la Mungu ndio maana adui kajiinua kuvuruga, jambo la msingi simama mahali palipo bomoka na liweke mikononi mwa Mungu, omba rehema iwapo mna jambo mmekengeuka ili Mungu arekebishe. Usikate tamaa, yanapokuja masuala ya uhusiano na hasa inapoelekea kutaka kufunga ndoa ndipo adui anajiinua sana hasa kama ndoa ina kusudi la Mungu, ingia vitani kaka utashinda. Nimeona huruma maana mara nyingi tumezoea wanawake kupitia hali hii hivyo kuliona kama jambo la mazoea lakini unapoona kaka kama wewe unahitaji msaada kiasi binafsi nasikia kuguswa. Ubarikiwe na utashinda

 13. AIDAN,
  Suala lako linahitaji ushauri kabla ya mtu kuliombea.
  Kuna maswali kadhaa ambayo yanapaswa kujibiwa kwanza.
  1. Je kama wewe hujui sababu ya kuvunjika uhusiano, je huyo mchumba wako naye hajui sababu?
  2. Katika uhusiano wenu huo wa miaka sita, je kuna neno lolote la wazi Mungu aliwahikusema nanyi kuhusu mapenzi yake katika uhusiano huo?
  3. Katika muda wote wa uhusiano wenu, je mna uhakika na mnashuhudiwa na roho wa Mungu kuwa mmeishi kwa uaminifu na usafi wa kimahusiano?
  4. Je mlikuwa na mshauri wenu wa karibu kuhusu uhusiano huo kwa miaka yote hiyo?
  5. Je mko kwenye imani moja?
  6. Je mnaye (wewe na huyo msichana) baba wa kiroho?
  7. Je mmeokoka? na huyo msichana je?

  Kama unavyoona kuna maswali mengi mengi ya kujiuliza kabla ya kuanza kuomba uhusiano huo kurudi.

  Naamini kuwa katika uwanja huu (STRICTLY GOSPEL) utapata ushauri wa kutosha.

  Bwana Yesu atusaidie.

  AIDAN,
  Suala lako linahitaji ushauri kabla ya mtu kuliombea.
  Kuna maswali kadhaa ambayo yanapaswa kujibiwa kwanza.
  1. Je kama wewe hujui sababu ya kuvunjika uhusiano, je huyo mchumba wako naye hajui sababu?
  2. Katika uhusiano wenu huo wa miaka sita, je kuna neno lolote la wazi Mungu aliwahikusema nanyi kuhusu mapenzi yake katika uhusiano huo?
  3. Katika muda wote wa uhusiano wenu, je mna uhakika na mnashuhudiwa na roho wa Mungu kuwa mmeishi kwa uaminifu na usafi wa kimahusiano?
  4. Je mlikuwa na mshauri wenu wa karibu kuhusu uhusiano huo kwa miaka yote hiyo?
  5. Je mko kwenye imani moja?
  6. Je mnaye (wewe na huyo msichana) baba wa kiroho?
  7. Je mmeokoka? na huyo msichana je?

  Kama unavyoona kuna maswali mengi mengi ya kujiuliza kabla ya kuanza kuomba uhusiano huo kurudi.

  Naamini kuwa katika uwanja huu (STRICTLY GOSPEL) utapata ushauri wa kutosha.

  Bwana Yesu atusaidie.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s