Utu wako wa Ndani! (MOYO)

Je Mungu anaweza kukaa kwenye moyo wako? Je Moyo wako u safi? Yeremia 17:9-10 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake”.

Moyo wako ulivyo ndivyo unavyoishi, Hivyo basi ikiwa wewe ni mzinzi, mlevi, msengenyaji n.k ndivyo moyo wako unavyofanana! Moyo ni mtu wako wa ndani asiyeonekana, ni pacha wako, unavyojiona wewe kwa nje jua kwamba ndivyo na moyo wako unavyofanana kwa ndani! nje wewe ni mwili unaoonekana lakini ndani ni pacha wako, ambaye ni moyo wako!Mwanzo 6:5 “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote”

Kama unavyoujali mwili wako na kuupamba vivyo hivyo na moyo wako lakini huo Utu wako wa ndani (pacha wako) mapambo yake ni yasiyoharibika Galatians 5:22-24 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake

Utu wako wa nje yaani mwili wako unafuata matakwa ya mtu wa ndani! Ndio maana mtu afanyapo dhambi huanza moyoni sio mwilini, mfano mtu anapoamua kuzini huanzia moyoni. Hivyo inakua hatua mpaka mwili unafanya tendo halisi. Imeanzia moyoni!

Utu wako wa ndani (MOYO) ukipona na nje umepona pia, mapepo yote yanakaa moyoni, kiburi nacho vivyo hivyo Ezekiel 28:2 Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu”

Hivyo tunahitaji kufanya upasuaji wa mioyo yetu. , Yeremia 4:4 Jitahirini kwa Bwana, mkaziondoe govi za mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu”.

Muhubiri 10:2Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote”.

Tumwambie Mungu afanye upya mioyo yetu, atufinyange upya tuweze kutoa matunda mazuri katika hali ya uhalisia! Zaburi 51:10-11 “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu, Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee“.

Wakolosai 3:1-2 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi”

Mungu awabariki

–Pastor Rodger Mahanyu–

Advertisements

One thought on “Utu wako wa Ndani! (MOYO)

  1. Bwana asifiwe Pastor Rodgar Mahanu. Mungu akubariki sana. Nimefurahia sana somo. Endelea kumwinua Yesu aliye hai

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s