Ndoto na Maono

Je, Kuna tofauti gani kati ya Ndoto na Maono?

Advertisements

5 thoughts on “Ndoto na Maono

 1. Bwana Yesu asifiwe sana!!

  Tumefundishwa na Mtumishi wa Mungu kuwa ndoto hazitoki kwa shetani ila kwa Mungu. Mimi binafsi nilijua kwamba ndoto zinatoka kwa shetani na wakati mwingine kwa Mungu.
  Kutokana na maelezo ya Mtumishi huyu, eh nikaona pia yawezekana yuko sahihi.

  Kwa maelezo yake alifundisha kuwa; mfano umeota unapandishwa cheo ofisini mara wakati wa maamuzi wakurugenzi wakasema usipandishwe cheo badala yake waajiri mtu mwingine. Hapa ni Mungu anakuonyesha kwamba mbele yako kuna jambo jema lakini kuna watu wanajaribu kukuzuia ni juu yako kupigana na hivyo vipingamizi.

  Labda umeota hali ya ajali mahali fulani. Hapo Mungu anakuonyesha kuna mauti inakuja kwa hiyo ni juu yako kukataa mauti si kwako tu hata kwa wengine. Mfano dhahiri mwaka jana kama sijakosea kuna ajili mbaya ilitokea mto Nduruma Arusha (Kwa Mrefu). Watu kama watatu walishudia kwamba waliota, wengine walifuta ajali wengine hawakufuta. Labda kila aliyeonyeshwa kuna ajali angefuta huenda isingetokea.

  Labda pia umeota unacheza ngoma na wachawi usiku. Mtumishi alituambia ni alert kwamba kuna roho ya kichawi inakufuatia/ au wachawi wanajaribu kukuloga ni juu yako kupambanua.

  Nilitoka na jibu kwamba ndoto iwe nzuri au mbaya ni a kind of alert something is going to happen/ some thing is happening and a Message from God.

  Mimi naomba mwenye ujuzi zaidi juu ya ndoto atafundishe.

  Bwana Yesu asifiwe.

  Tunajifunza

 2. Maono ni ‘kuonyeshwa’ kitu fulani, inaweza kutoka kwa Mungu au Ibilisi. Kwa vile ndoto nikuona kitu katika hali ya usingizi inaweza kuwa ni maono pia.
  Kitabu cha Daniel, Ufunuo, Ezekiel tunaona watumishi hawa wakionyeshwa maombo mengi yajayo katika hali kama usingizi na pengine katika hali ya kawaida wakiwa na wenzao ila hao wengine wasione kitu. Shetani pia anadanganya watu wengi kwa maono na ndoto hivyo neno la maarifa au uongozi wa Roho mtakatifu ni muhimu ili utafsiri ndoto au maono yoyote, mwulize Mungu kwa maombi au kushirikisha wengine. Maana ndoto ni mawazo ya mtu kama moyo wako umejaa mawazo fulani ukiota ndoto usijesema ni maono toka kwa Mungu bila kuuliza na kuomba kwanza.

 3. Nionavyo tofauti siyo kubwa maana ndoto zaweza kuwa na inspiration ya Mungu au hata isiyo ya kimungu lakini maono yanatanguliwa na inspiration ya Mungu iwe ni kwa ndoto au Mungu anaposema na mtu.Ukitaka kuona vizuri angalia Samweli wa Kwanza uone wito wa Samweli au Kitabu cha Yeremia uone maono kwamba Yeremia alioneshwa vitu halisi mfano kikapu chenye tini akaulizwa umeona nini?Mungu alimpa tafsiri ya kila kitu kwa namna ya Roho japo ni vitu vya kawaida .TUYACHUNGUZE MAANDIKO TUTATAMBUA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s