Kwanini bado mtu anakua kwenye vifungo?

Bwana Yesu asifiwe! naomba kuuliza jambo ambalo bado linanitatiza kuelewa katika maisha yangu ya Wokovu. Nilipompokea Bwana Yesu, niliamini kuwa nimekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita na sasa ni mapya. Niliamini pia kutokana na mafundisho niliyopewa kuwa, nimeokolewa /nimekombolewa kutoka katika vifungo vyote vya ibilisi “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa Pendo lake” (Kol 1:13).

Hivyo basi 1.inakuwaje kuwa mtu unaokoka na unaendeea kuwa katika vifungo vya ibilisi, unaendelea kubeba laana za mababu, unarithi magonjwa ya ukoo nk.

2. Ni mpaka ufanyiwe huduma nyingine ya delivarence ndo ufunguliwe? Katika hili pia kuna baadhi ya imani za kipentekoste hazikubaliani na mambo ya delivarence. naombeni msaada.

Benedicta

Advertisements

118 thoughts on “Kwanini bado mtu anakua kwenye vifungo?

 1. Hili swala lipo kweli ukishaokoka uwe karibu na Roho Mtakatifu yeye ndiye msaidizi

 2. Wapendwa John Paulo, Orbi, Kinyau, na wote mimi nipo pamoja nanyi tena.

  Kama ulivyosema John Paulo hujakosea nilimaanisha hivyo.”Mtu akiokoka halafu akashindwa kukaa katika Neema ya Mungu, akikosa roho ya kuomba msamaha, akaficha dhambi zake huyo atajikuta YUKO CHINI YA LAANA TENA kwa kuwa amekuwa nje ya mpango wa Mungu”. Na ”mtu akiokoka halafu akashindwa kukaa katika Neema ya Mungu, akikosa roho ya kuomba msamaha, akaficha dhambi zake huyo atajikuta YUKO CHINI YA LAANA TENA kwa kuwa amekuwa nje ya mpango wa Mungu”.

  Kwa sababu ya mda wangu mdogo, msimamo wangu ni kwamba kama hiyo deliverence inatokana na neno la Mungu nakubaliana nayo na si vinginevyo. lakini napendelea zaidi counceling na intercession naona iko kibiblia zaidi kuliko deliverance au nikitu kimoja? anayejua naomba maelekezo.

  Tupo Pamoja watumishi, Michango yenu naikubali sana.
  Barikiwa

 3. asante! sana Paulo na wote, kwa michango yenu nimejifunza kitu! Mungu awabariki sana

 4. Wapendwa John na Orbi,
  Mlichokiandika juu ya hii huduma ya deliverance ni kweli iliyoko ndani ya Neno la Mungu, na hicho ndicho ambacho kila aliyekombolewa na damu ya Yesu pale msalabani anatakiwa kukijua na kukishikilia.

  Mimi napata taabu sana kwa watu wengine kuona kama deliverance inayoendeshwa sasa ni muhimu kuliko neno la Mungu ambalo linaeleza wazi kuwa ni uzima wetu, ni chakula cha roho zetu, ni taa na mwanga wa njia zetu, ni silaha kali dhidi ya mwovu shetani, ni upanga wa Roho, ni fedha safi iliyosafishwa mara saba (Zab.12:6), linatuonyesha hila na mitego yote ya shetani ili tusitende dhambi (Zab.119:11), lina hekimisha na kumpa mwanadamu maarifa yote anayohitaji katika kuishi kwake hapa duniani, neno la Mungu ni kweli na sheria zake ni za haki, linaongoza hatua zetu ili tusitawaliwe na dhambi yoyote (Zab 119:133,160). Tukitaka kuweka list hii ni ndefu mno, itoshe tu kusema kwamba neno la Mungu ni kila kitu katika maisha yetu katika ulimwengu huu wa mwili.

  Nilikuwa nasoma article moja ya Ben Hinn yenye heading inayosema “Delivered from Death”, pamoja na mambo mengi yaliyoandikwa kwenye article hiyo, nilifurahishwa sana na vifungu vifuatavyo;
  “You have been redeemed from all iniquity. No sin can dominate your life because you are purchased………….. Satan cannot have you, nor can he touch you. The Bible gives us these mighty promises, yet it is up to us as believers to LIVE IN IT, WALK IN IT, AND FILL OUR LIVES WITH GOD’S WORD”. Nimeweka msisitizo kwenye maneno niliyoyaandika kwa herufi kubwa ili kuonyesha kwamba neno la Mungu ni fundamental kuliko hii deliverance inayoendeshwa sasa. Ben Hinn anasema ni juu yetu kuliishi neno, kutembea katika neno na kulijaza kwa wingi ndani mwetu (Kolosai 3:16).

  Najua wengi tunaifahamu sana mistari hii ya Zaburi ya 103:3, Isaya 53:3-10, 1 Petro 2:24 n.k. Baada ya kumpokea Huyu aliyefanyika laana kwa ajili yetu, laana gani nyingine tunahitaji kukombolewa nayo? Biblia inasema baada ya kusamehewa dhambi, Mungu anatuponya na magonjwa yote, je ni deliverance gani nyingine tunatakiwa kuipata ili kupona magonjwa? Damu ya Yesu iliyomwagika msalabani inatosha kuutoa mzizi wa laana zote ambao ni DHAMBI, sasa deliverance gani nyingine inahitajika zaidi ya hiyo ili tuondokane na laana mbali mbali?

  Shida kubwa ya wakristo wa leo hawana muda wa kusoma na kulitafakari neno la Mungu kama walivyoagizwa kwenye Yoshua 1:8 na Mathayo 7:24-27; badala yake wanataka short cuts ambazo mara nyingi zinaishia kuwapeleka kwenye maangamizo.

  Kama John na Orbi walivyosema, huduma ya deliverance imesimama kwenye msingi wa mafanikio ya kimwili zaidi kuliko kkiroho. Kumbuka Yesu alishatuonya kuwa itatufaidia nini tukipata kila kitu cha ulimwengu huu halafu tukazipoteza roho zetu? Mara umpokeapo Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, tayari hiyo ndiyo deliverance halisi, kazi inabaki kwako kung’ang’ana na huo wokovu ili dhambi isikutawale tena.

  Mungu awabariki.

 5. Paul Ubarikiwe………unapoona watu wanapelekewa” kasha” la “delivarance” lakini hawapewi UJUMBE WA WOKOVU WA KUWATOA DHAMBINI NA KUFANYA WAMJUE YESU KWA KUMFUATA NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU hiyo ni ishara wazi kuwa hii ni injili nyingine kabisa…….na ambayo Paulo amesema na ALANIWE ANAYEHUBIRI INJILI HIYO….!

 6. Mpendwa Orbi,

  Ni kweli tumepoteana, naona ni kwa sababu tu ya majukumu. Lakini ni jambo la kushukuru Mungu, kwa neema yake bado tunaendelea katika kumtafuta Bwana na Nguvu zake pamoja na kuliita jina lake!

  Nami nashukuru sana pia kwa maoni yako kuhusu suala hili tata. Na utata huu umesbabishwa na watumishi wenyewe kwa kupindishwa kweli fulani ili mambo mengine yawe rahisi kufanyika kwa matakwa ya kibinadamu tu na si kwa KUMSIKILIZA Mungu!

  Kuna mambo huwa yanasikitisha sana kuhusu suala hili la deliverance. Nimeshawashi kusikia kwa masikio yangu mwenyewe mtu AKISIFIA kituo cha deliverance kuwa PALE HAWAFUATI FUATI MTU KUMUULIZA KAMA AMEOKOKA AU BADO. Mtu huyo, mdada, alisema kuwa ukifika pale unaombewa mahitaji yako kisha unaondoka, unakwenda zako kuendelea na shughuli zako.

  Katika kutafakari hilo nikagundua kuwa ndiyo maana watu hujaa kwa haraka sana katika vituo vya huduma za deliverance kuliko katika makanisa wanapohuhiri Injili, wanaookoka wakalelewa hadi wakuwe kiroho na kuweza kujisimamia wenyewe katika safari hii ya mbinguni. Kwa nini? Kwa sababu Si watu wengi wanatambua kuwa THAMANI YA ROHO ni kubwa mno ikililnganishwa na THAMANI YA MWILI!

  Wengi huenda katika huduma za deliverance ili waondolewe mikosi na balaa, wapate kazi, wapate kibali cha kupendwa, wapate scholarships, biashara zao zisitawi nk. Sijasikia na sijui kama ipo, kuwa kuna DELIVERANCE ya kumfanya mtu ASHINDE DHAMBI! Maana deliverance ime-base sana kwenye LAANA. Na kipimo cha laana ni KUKOSEKANA KWA MAFANIKIO YA KIMWILI, kama nilivyoandika mifano michache katika paragraph hii hii.

  Kwa hiyo deliverance inashughulikia MATOKEO YA DHAMBI ambayo ni LAANA na wala haishughulikii SABABU YA KUWEPO KWA LAANA HIZO. Ni sawa na kukata matawi lakini shina likabaki. Ni dhahiri kuwa shina litachipua tena na kutoa matawi mengine. Hiki ndicho niliandika kuwa wengi sana ni “wateja” wa deliverance, yaani kila akipata nafasi anahudhuria ‘deliverance’ , hata kama ni mara 3 kwa wiki. Sasa hapo ni lazima kuwe na tatizo:

  Kwamba leo mtu anafanyiwa deliverance ya kupata kibali kwa watu; kesho anakuja anafanyiwa deliverance ya kufanikisha biashara yake; siku inayofuata anafanyiwa deliverance ya kupata kazi. Yaani kila wakiita watu wanaohitaji aina fulani ya deliverance na yeye yumo. Hapana! HAPA INABIDI WATU KAMA NDUGU ANTHONY WALIWEKE SAWA JAMBO HILI: Ni nini maana yake mtu kufanyiwa deliverance moja moja kwa mahitaji aliyonayo? Halafu akitoka hapo hashauriwi lolote namna ya KUISHI KATIKA KRISTO?

  Ndugu zangu, hebu tusaidiane katika hili. Mimi najua kweli kuwa mtu anayeishi maisha matakatifu, baraka tayari ziko juu yake. Ndiyo maana kuna maandiko kama lile la Zaburi 1:1-3 lisemalo:

  “Amebarikiwa mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki,
  Wala hakusimama katika njia ya wakosaji, ….”

  “Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, naye huitafakari usiku na mchana…..”

  Na mwishoni mwa mstari ule wa 3 andiko linasema:

  “Na kila alitendalo litafanikiwa”. Sikiliza “KILA ALITENDALO LITAFANIKIWA”

  Hiyo ndiyo Biblia! Baraka, ambacho ni inyume cha LAANA inapatikana katika kumuishia Mungu.

  Na mtu asiyefanya hayo maandiko yanasema hivi katika Yeremia 17:5-6:
  “BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwandamu kuwa kinga yake,
  Na moyoni amemwacha BWANA.

  Maana atakuwa kama fukara nyikani,
  Hataona yatakapotokea mema…..”

  Sasa, kwenye Biblia yapo maandiko mengi sana yanayoonyesha namna ya KUPATA BARAKA ZA MUNGU kutokana na kulitii Neno la Mungu na kufanya mambo yampendezayo Mungu. Vile vile yapo maandiko mengi sana yanayoonyesha ni kwa jinsi gani mtu anapata LAANA.

  Mimi nafikiri kuwa ni rahisi zaidi kujifunza Neno la Mungu, ahadi zilizo katika Neno na jinsi gani mtu afanye ili aishi katika Neno litakaloweka UZIMA na BARAKA ndani yake kwa ajili ya kuepuka DHAMI iletayo MAUTI na LAANA kuliko KUFANYIWA HUDUMA YA DELIVERANCE, mbayo haina sehemu yoyote pa kuichomeka katika Biblia. Dawa ya kuondoa LAANA si kuivunja bali ni Kuifukuza DHAMBI inayoandaa makao ya Laana. Kama vile tu kuwa Njia bora zaidi ya kufukuza Nzi ni KUONDOA UCHAFU UNAOWAVUTIA na si kuwapuliza kwa Ngao au Rungu, maana wakifa watakuja wengine tena! Ukiondoa UCHAFU umewaondoa na Nzi. Hivyo ukiondoa DHAMBI umeondoa na LAANA! Mungu atusadie ili tuweze kuondoa dhambi maishani mwetu. Maana tukishaondoa dhambi LAANA itaondoka na BARAKA itaingia. Amina!

  Kujifunza Neno la Mungu kunaleta maarifa. Na maarifa ya Neno la Mungu ndiyo hufanya WATU WA MUNGU WASIANGAMIZWE. [Hosea 4:6]

  Siku hizi watu wengi sana, hata wanaopinga Uungu wa Yesu na wengine kupinga KUOKOKA ni mafundi sana wa KUKEMEA KWA JINA LA YESU wanapokutana na tatizo lakini wakishakemea huendelea na maisha yao ya gizani. Hii imetokea kwa sababu katika huduma nyingi za deliverance watu hufundishwa KUVUNJA TU LAANA lakini hawaelezwei WAISHI VIPI ILI ZISIJE TENA. Bali hutiwa moyo kuwa mtu akikutana na shida nyingine arudi tena akafanyiwe deliverance!

  Mimi nafikiri watu wakifundishwa nao WAKALIISHI Neno na kuliweka moyoni ili waseme kama Daudi aliposema kuwa “Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako, nisije nikakutenda dhambi [Zab 119:1] mimi naamini kabisa VITUO VYA DELIVERANCE VITAKUFA na VITABAKIA MAHALI WATU WANAJIFUNZA NENO LA MUNGU.

  Na hii inaweza kufanikiwa kwa kuwa Neno la Mungu LI HAI, lina Nguvu na Uweza, lina makali kulipo upanga uwao wote ukatao kuwili…., yaani lina sifa zote za kumfanya mtu aishi maisha yasiyo na LAANA!

  Kwa kifupi ni kuwa NENO la Mungu ndiyo Kila kitu. Kulitii na Kuliishi Neno ndiyo deliverance kubwa na sahihi kulizo zote!

  Naona nijizuwie tu niishie hapa kwa sasa! ili nisubiri kusoma kutoka kwa mwingine!

  Itakuwa vizuri sana kama ndugu Anthony utarejea kujibu maswali mawili matatu yaliyojitokeza, hasa katika mchango wangu uliopita!

 7. John Paul,

  Habari za masiku ndugu yangu……naona tumepoteana….nimeneemeka kwa kusoma mchango wako baada ya siku nyingi…..

  Kwangu mimi mafundisho ya “Deliverance” hasa yale yanayohusiana na kumfungua mtu toka dhambini au kumpatia mtu ushindi katika kutembea katika Neema ya Wokovu hayana mahali pa kusimama katika maneno ya Mungu! Maisha ya Ushindi yako wazi kama tutasimama katika kanuni za Neno la Mungu….na dawa ya dhambi kama Muuimini atajiingiza Dhambini ni Toba tu na Kumrudia Mungu na UTII Katika Neno lake! Hakuna njia ya Mkato ya “Deliverance” ya kumfanya muumini atoke dhambini (Nikiwa na maana ya mtu aliyeokoka) Kwani tendo la Wokovu – KUOKOKA ndio “Delivarance” Wanaokimbilia “Delivarance” ya Kuondolewa katika maisha ya Dhambi warudi tena wakasome sura ya sita hadi nane ya Kitabu cha Warumi na hata Nyaraka za Waefeso/Wakolosai! Hivyo hiyo mikiki mikiki ya Huduma za “Deliverance” ni wale watu wanaotaka Wakristo walioanza kwa Imani wamalize kwa matendo! Na hii sio Injili ya Paulo na Mitume! Ni Injili ya kuwatia Waumini katika Kongwa lisilo na nguvu yoyote ya Uweza wa Mungu! Kwani Uweza wa Kututoa Dhambini uko katika kuliamini NENO LAKE TU! Je tumesahau kuwa tuna Silaha ya Kuangusha Ngome? Je tumesahau kuwa tukiwa na Roho Mtakatatifu KAMWE Hatuwezi kuzitimiza tamaa za Mwili? Kama Kanisa la Corintho halikufanyiwa “Delivarance” na Paulo Hawa “mitume” na “watenda kazi” wa Leo wanasimama wapi katika Biblia na haya Mafundisho? Makanisa Saba katika kitabu cha Ufunuo yalikuwa yamekwama katika kutembea na Bwana katika njia mbali mbali, Na Yohana anayaambia TUBUNI! Na wala sio “Kafanyiweni delivarance”

  Tusitafute njia ya Mkato ya kuuishia Wokovu….”Tukae ndani ya Mzabibu”….”Neno la Mungu lijae moyoni mwetu”……”Tudumu katika Maombi”……..”Tuzivae silaha tulizopewa na Bwana”………”.Mpingeni Shetani”………”.Neno la Mungu ni Upanga”……….”.Hii haiwezekani isipokuwa kwa kufunga na kuomba”……..Jena mbona kuna mengi ya kutusaidia kuuishia Neema hii toka Gombo la Chuo?…..! Huu ufunuo mpya wa “Delivarence” Unatoka wapi? Na kama hauna mahali pa kusimama katika Neno lake haya ni mafunuo ya Wapi?

  UBARIKIWE!

 8. Ndg Anthony,

  Bibafsi nashukuru kwa uchambuzi wako kuhusu suala hili la kwa nini mtu aliyeokoka anaweza kuwa tena chini ya vifungo pamoja na suala la deliverance. Umeongeza upana wa mjadala ili tuzidi kujifunza zaidi.

  Kutokana na maelezo yako ni kwamba, Mtu aliyeokoka na akasimama katika kulitii Neno la Mungu hawezi tena KUPATWA NA LAANA kwa kuwa Kristo alikufa ili tusiwe na laana tena. Kama si sahihi utanisahihisha!

  Lakini mtu akiokoka halafu akashindwa kukaa katika Neema ya Mungu, akikosa roho ya kuomba msamaha, akaficha dhambi zake huyo atajikuta YUKO CHINI YA LAANA TENA kwa kuwa amekuwa nje ya mpango wa Mungu. Hili pia kama si sahihi utanisahihisha.

  Sasa, ninavyofahamu mimi [na ambavyo nawe umeandika] ni kuwa mtu akishindwa kulitii Neno la Mungu, hata kama alikuwa ameokoka, DHAMBI itafanya makao tena ndani yake. Na uwepo huo wa dhambi ndio utasababisha LAANA ipate mahali pa kuishi! Kwa hiyo kinachotokea mtu anaposhindwa kulitii Neno la Mungu si LAANA tu bali na DHAMBI hutawala tena ndani yake. Hivyo kukipatikana dawa ya kusafisha ile dhambi iliyoko ndani yake, yaani mtu huyo AFANYWE UPYA tena, Dhambi itaondoka na NURU ya Yesu Kristo itaingia tena ndani yake!

  Kama maelezo hapo juu ni sahihi, tunaweza kusema kuwa mtu ambaye alitenda dhambi na akashindwa kuitubia, dhambi hiyo itafanya makao kwake nayo italeta laana. Lakini Dhambi ikiondoka na LAANA zilizosababishwa na dhambi ile iliyokuwa ndani yake nazo zitaondoka.

  Na kwa maana hiyo mtu akitubu dhambi zake na kuurejesha utakatifu aliokuwa nao HANA HAJA TENA YA DELIVERANCE maana TOBA YA KWELI inatosha kurudisha uwepo wa Mungu na Mungu akiingia kwenye maisha ya mtu LAANA haziwezi kukaa tena ndani yake kwa kuwa giza na nuru haviwezi kukaa pamoja.

  Jumla ya hayo ni kuwa Kama watu wataishi maisha matakatifu hakuna sababu ya Deliverance. Na kama deliverance ni lazima, basi inabidi ifanyike kwa mtu huyo kuungama dhambi zake ilii zifutwe na Nguvu ya Yesu Kristo itawale tena ndani yake! Na si kama hivi ambavyo inafanyika sehemu nyingi [kama si zote panapofanyika huduma hizo] kuwa mtu HUFANYIWA DELIVERANCE pasipo hata KUSAIDIWA ILI ATUBU DHAMBI ZAKE, awe mtakatifu!

  Watu wanafanyiwa deliverance pasipo kuulizwa wala kushauriwa kuhusu kiroho chao. Wengine baada ya kufanyiwa ‘deliverance” HUSHAURIWA KURUDI HUKO HUKO WALIKOTOKA; wengine kwenye uislamu, upagani na katika dini hata ambazo zinapinga dhana ya KUOKOKA.

  1.Je, katika hali ya namna hii LAANA hizo hazitawarudia tena watu, kwa sababu DHAMBI bado iko ndani yao?

  2. Je, kusudi la deliverance ni kuwaondolea watu LAANA zinazoathiri mwili tu pasipo KUWATUBISHA DHAMBI ZAO ili na roho zao ZIPONE?

  3. Je, twaweza kutenganisha LAANA na DHAMBI kwamba mtu anaweza kuwa na LAANA tu ya kutokulitii Neno la Mungu lakini akawa hana DHAMBI?

  4. Je, kama ni kweli kuwa DHAMBI ndiyo husababisha LAANA kwa nini tusiseme tukiondoa DHAMBI kwa DAMU YA YESU tutakuwa tumeondoa na LAANA PIA?

  Na kama DAMU YA YESU inatosha kusafisha DHAMBI na hatimaye kuondoa LAANA basi KUFANYA DELIVERANCE hata kwa mtu ASIYE NA DHAMBI ni KUIKANA NGUVU YA DAMU YA YESU ya kuondoa dhambi kuwa haitoshi hadi pafanyike huduma nyingine ya Deliverance. Na kufanya deliverance kwa mtu MWENYE DHAMVIi nako hakuna maana kwa kuwa dhambi iliyoko ndani itaendelea kuleta LAANA zingine. Ndiyo maana kuna watu kila leo wanafanyiwa deliverance, wakihama toka huduma hadi huduma na mtumishi hadi mtumishi! lakini maisha yao yakiwa bado yako pale pale. Kwa nini? Kwa sababu DHAMBI haijaondoka ndani mwao!

  Lakini kama Damu ya Yesu inatosha kuondoa DHAMBI na hatimaye LAANA basi, mtu akitubu dhambi zake [na kuishi maisha matakatifu] hakuna haja tena ya Deliverance. Hivyo Badala ya kufanya huduma ya Deliverance kinachotakiwa ni KUWAFUNDISHA WATU WAISHI MAISHA MATAKATIFU maana kwa kufanya hivyo watakuwa mbali na LAANA. Na wale walioanguka katika dhambi na kujikuta wamefungwa tena na laana wanatakiwa wafundishwe WAFANYE TOBA YA KWELI ili Nguvu ya Kristo irudi ndani yao!

  Na kama hiyo ni kweli, basi huduma ya Deliverance HAISTAHILI KUWEPO!

 9. Siku ulipookoka ulipokea stahili yote, ukafanyika kiumbe kipya, laana, dhambi na machukizo yote yaliisha pale kalvari, YESU aliiondoa laana pale kalvari, Maana imendikwa amelaaniwa aangikwaye msalabani, Lakini Bwana aliangikwa ili mimi na wewe tusiwe na laana tena

  Hizi mbadala za deliverance ni kwa sababu waamini wengi wamekuwa wanajidanganya nafsi zao na Mungu, hivyo laana zinawakuta wakiwa wameokoka, ni kwa sababu hawakuifuata kweli inayostahili, mfano siku hizi watu wengi wanashiriki meza ya Bwana hata kama ana dhambi ati anaogopa mchg, wazee watamwonaje?, watu wanaanguka ktk uzinzi na hawafanyi toba inavyostahili, Yapo mengi sana yameharibu kanisa la leo. Hivyo kuzalisha huduma ya Deliverence ili mioyo ya binadamu wa leo ipate faraja tokana na dhambi alizojitendea mwenyewe kwa hiari.

  wiki mbili zilizopita nimesikia ati wapendwa ktk kanisa la linaloitwa la kiroho na kubwa sana wamefukuzwa/kutengwa kanisani lakini walitarajia kufunga ndoa wiki iliyofuata, kisa eti Matroni aliona binti anatapika nakusikia kichefuchefu, akamwuliza binti akakakubali kwamba walianguka na mwanamume ati alikataa walipopima wakakutwa anamimba miezi 3, . Sasa kama walianguka kwa nini hawakufuata procedure za kutubu kanisani, wakapritendi wafunge ndoa huku wajawazito, JE LAANA ZITAKUKOSA HAPO?

  WE MUST KEEP THE STANDARD(TBS) AMBAYO MUNGU ANAAGIZA. KUANGUKA KTK DHAMBI SI AJABU, TATIZO KUFICHA DHAMBI NDANI YAKO MWENYEWE NA MUNGU, Anania na safira hawakuamrishwa wakalete sehemu ya mauzo yao, bali walisema wenyewe mioyoni mwao kwamba watatoa sehemu ya mauzo yao, baadae wakageuka kwa kuona ni nyingi wakatoa kidogo, mnaona jinsi WALIVYOADHIBIWA, kumbe wasingesema naona Mungu asiwaadhibu, hapa Mungu hakulazimisha watoe.

  HIVYO DELIVERENCE IMETOKEA KWA SABABU YA NIRA ZILIZOFUNGWA kidogokidogo mpaka mtu anakuwa ndani ya yoke. KWA WAAMINI WENGI KTK KANISA LA LEO, KWA KUTOKUTII NENO LA MUNGU wamepata laana, Deliverence haikustahili kwepo.

 10. mtu anawezaje kusema amekuwa huru na bado ahesabike kuwa yuko katika kifungo? nashindwa kuelewa. Na je ukishaamini kwamba Yesu ni yote katika yote inakuwaje tena kuwe na ukombozi mwingine mbadala? au kuna aina ngapi za kufunguliwa kutokanako na Damu ya Yesu? na je? mtu asipofanyiwa hiyo deliverance baada ya kuokoka hataingia mbinguni? naomba mnisaidie kwa hili maana naona sasa nachanganyikiwa na haya mafundisho.

 11. Shalom, Mimi niseme tu jambo moja kuwa , mtu anapo okoka anafanyika kuwa kiumbe kipya na anapokea ahadi zote za neema ya wokove , but kol.1:13 this is another part

 12. Ninaomba kuwasilisha jambo ambalo naona hapa panaweza kuwa mahali pake:

  Nimesikia tangazo fulani katika redio juu ya kuwepo kwa mkesha wa KUVUNJA LAANA YA UZAZI WA TUMBO LA MWANAMKE. Sasa baada ya kusikia tangazo hilo nilipatwa na maswali mengi, mengi sana. Na nimeona kama vile nikilileta kwenye mada hii linaweza kuwa linahusiana.

  Ninaomba anayefahamu uwepo wa laana ya namna hiyo, au kinyume chake, achangie maoni yake. Nina shauku sana ya kufahamu kuhusu laana ya namna hiyo kwa mwanamke.

  Asanteni.

 13. Ndugu Paul Hollela,

  Katika kuzipitia post zangu kwenye Blog hii,hasa nikujua pengine sitakuweko katika uwanja huu kwa muda,Kwani sijui Bwana atataka nipige kambi wapi tena hasa kwa ajili ya kujifunza,kushirikiana ufahamu tulionao katika Neema hii, nik walioniuliza, ili nisiacha yanaelea!

  Ndugu Hollela ulinuliza;

  “Jaribu kutafakari unaweza ukapata kitu cha kukusaidia Obi ….Kama ungemuuliza Mungu kwa nini mkeo aote ananyonyesha nafikiri Mungu angekwambia ni nini?”

  Nukuu yako hiyo imejengwa kwenye mifano yangu kuwa,kuna kipindi mke wangu aliota ananyonyesha, na kumbe katika familia yangu tunaamini kazi ya kuijaza dunia kwa sehemu yetu tumeisha ikamilisha, na mke wangu alipokutana na “waonaji” wakamwambia laba katika ulimwengu wa “roho” ana mtoto lazima afunguliwe!!

  Nachotaka kusema ndugu Holela, ndoto ni ufunuo ulio nje ya wigo wa maneno ya Mungu, (Extra Biblical Revelation” Siamini kabisa Mungu atanihukumu kwa kutosikiliza kitu nje ya Biblia! Ila kwa hakika nitahukumiwa kwa kutosilikiza anavyosema katika Neno Lake!

  Lakini pia, kama nilivyokueleza awali, naamini Mungu anaweza kuamua kusema nasi kwa Ndoto,amefanya hivyo katika Neno, Agano la zamani na Jipya hufanya hivyo kwa makusudi maalumu! Sio kanuni,hivyo inataka tahadhari sana! Hebu tusimame kwenye safe ground! Neno lake!

  Mungu Na Akubariki!

 14. Imani haba, udhaifu wa kibinadamu (kukosa uvumilivu, tamaa), mawasiliano na watu wengine wasiojali, kufifisha sala na mengineyo ya kibinadamu ndio sababu ya watu kubaki vifungoni.

  IMANI ni jambo la msingi. Na kufahamu ya kuwa MUNGU hujibu sala kwa namna yake MUNGU, na si kwa namna za kibinadamu au tarajio zihusishazo namna za kibinadamu ni jambo la msingi sana.

  Wapendwa wanapaswa kufahamu ya kuwa sala zao hujibiwa na MUNGU kwa namna ya kipekee sana, na hivyo kukubali, kushukuru na kuzidi kusali, hii itawaepusha na vifungo na kurudiarudia kwa vifungo.

  Pia yawapasa wapendwa kujiepusha na mizizi ya dhambi, itokanayo na dhaifu za kibinadamu, kwa kuwa humfanya mtu abaki katika vifungo na kukatisha tamaa. Mtu anapoanguka katika mizizi ya dhambi, shetani humng’ang’aniza huko na kumrudisha vifungoni. SALA NI JAMBO LA MSINGI SANA WAKATI WOTE.

  Mizizi ya dhambi ya kuepukana nayo ni uzinzi, ulevi, ulafi, wizi, uongo, uchafu, tamaa, na ufisadi.

  Iepuke hiyo mizizi,na kisha utubu, Usali mara zote, ushukuru, utoe sadaka, na kuwapenda wengine, vifungo utaondokana navyo daima.

  AMINA.

 15. Shalom,
  Ndg makambako ahsante kwa kujaribu kuumsaidia huyu ndugu yetu obi kwenye hili eneo la ndoto….yapo maandiko mengi sana ambayo yanathibitisha Mungu anaweza akampa mtu maelekezo kwa njia ya ndoto…. ndugu kabla ya kubisha au kupinga jifunze kumuuliza Mungu kwanza .. biblia inasema tunafahamu kwa sehemu we usifikiri kwa sababu aina fulani ya mafundisho haya make sense kwenye fahamu zako basi sio kweli……jizoeze kumuuliza Mungu ….Biblia inasema wanaoongozwa na Roho wa Mungu ndo wana wa Mungu….Roho wa Mungu hulitumia neno kutuongoza na sio neno kumtumia Roho wa Mungu kutuongoza…jitahidi kuyangalia maandiko ktk Roho Mtakatifu…..
  Soma na uyatafakari haya maandiko yote yanaonesha Ndoto ila kubwa zaidi ni hili la Joel 2:28……..Vijana wenu wataona maono na wazee wataota ndoto …..lini? Roho Mtakatifu atakapokuja….

  Mwanzo 20:3,6 mw 28:12 mw 31:10 Mw 37:5-10
  Mw 40:5-9,16 Mw 41:11-17 Dan 2:3,4-24 Dan4:4-18, Joel 2:28 Mat 1:20 Mat2:12,13,19,22
  Math 27:19….Acts 2:17
  Jaribu kutafakari unaweza ukapata kitu cha kukusaidia Obi ….Kama ungemuuliza Mungu kwa nini mkeo aote ananyonyesha nafikiri Mungu angekwambia ni nini?
  Ili ufundishwe na Mungu ni lazima unyenyekee maana wanyenyekevu hupewa neema na neema inafundisha…..
  Mungu akutunze

 16. NDUGU ORBI!!!

  HEBU NIKUPE SHUHUDA MOJA YA MTUMISHI MMOJA.

  MTUMISHI HUYU NI MTU MZIMA KABISA KWA SASA. LAKINI NA UTU UZIMA HUO ALIOTA SANA ANA UMRI WA MIAKA SABA HUKA AMEVAA BUKTA. KATIKA NDOTO HIYO ALIJIKUTA AMEKAA MAENEO FULANI YA NYMBANI KWAO. ALIMWULIZA MUNGU KULIKONI???

  MUNGU LIMWONYESHA KWENYE MAONO KWAMBA WAKATI YUKO NA UMRI WA MIAKA SABA BABA YAKE MZAZI ALIKUFA NAYE ALIMPENDA SANA. KWA HIYO KWA MUDA MREFU BAADA YA MAZISHI YA BABA YAKE KILA ASUBUHI YEYE ALIPENDA KUCHEZA MAENEO YALE KARIBU NA NYUMBA NA ALIKWENDA MBIO BILA MTU KUJUA MAKABURINI ALIKOZIKWA BABA YAKE ILI AONE KAMA AMEFUFUKA. ZOEZI HILO ALILIENDELEZA KWA MUDA MREFU SANA KWA HIYO SHETANI NAYE ALIHIFADHI KAMA KUMBUKUMBU YAKE. BAADA YA HAPO ALIOMBA MSAADA WA MUNGU NINI CHA KUFANYA NA AKAPEWA CHA KUFANYA.

  MPAKA HAPO MIMI NAAMINI MUNGU ANAWEZA KUSEMA NAWE KATIKA NDOTO.

  KAMA MKEO AMEOTA ANANYONYESHA MTOTO, YAWEZEKANA ANAONGEZEWA UTUMISHI SI LAZIMA AWE MTOTO KAMA TUNAVYOTAFSIRI SISI.

  TUNAJIFUNZA

 17. Uweza na Mamlaka ya Jina la Yesu ni Kuu mno. Haiwezi kufungwa ndani ya kile walichofanya au wanachofanya watumishi fulani fulani wa Mungu. Kuna zaidi ya hapo!

  Hakuna mtume, nabii wala mtumishi yeyote anayeweza kufikia ukomo wa mamlaka ya Jina la Yesu. Na ndiyo maana Yesu mwenyewe alisema kuwa atakayemwamini ataweza kufanya makubwa kuliko hata aliyoyafanya Yesu mwenyewe akiwa hapa duniani!

  Tusiliwekee mpaka Jina la Yesu katika Uwezo na Mamlaka liliyo nayo!

 18. Paul Holela,

  Siku nitakapoelewa hizo “Deliverance” ambazo hazina msingi katika neno la Mungu, basi Biblia haitakuwa na maana kwangu! Kwa maana haitakuwa inasema ukweli! Na nitakapoanza kufuata “Experience” zangu au za mtu yoyote kuwa ndio msingi wa utendaji wa Mungu nitafungulia mlango wa kuamini kila kitu! Neno la Mungu limenifundisha wazi “DONT GO BEYOND THE SCRIPTURE” Na huyo ndio msimamo wa Wakristo wa Biblia! Naamini na wewe ndugu Holela Mungu atakufungua macho uone kuwa mmbo mengi katika hizo deliverance ministry (ukiacha labda magonjwa” ni short cut au quick fixes za kutotaka kukua kiroho! Siwezi kufanya kitu ambacho Paul hakufanya! Petro hakufanya! Yohana hakufanya! I cannot move beyond the scripture! Mungu na anisadie!

 19. Shalom,
  Nimekupata ndg Obi maana umetoa “msimamo wako”……
  na siku moja utaelewa na kukubali unavyovipinga leo….
  Mungu akutunze.

 20. PAUL HOLELA: Nitajibu swali ulililoniuliza, na pia nitaoa msimamo wangu kuhusu ndoto

  1. SWALI: Shida yako ni deliverance au deliverance inavyofanywa na mitume na manabii?

  Shida yangu ni vyote viwili.Na ukisoma articles zangu hapo juu unajua msimamo wangu.Kibiblia hatujaona mahali popote pale ambapo Watu waliokombolewa, walofanywa viumbe vipya, waliofanywa watoto wa Mungu, waliojazwa Roho Mtakatifu, wanaongozwa na Roho Mtakatifu wakifanyiwa huduma hiyo! Na hata katika makanisa yaliyokuwa katika hali mbaya kiroho kama kanisa la Korintho ambalo lilikuwa na uzinzi, ugomvi nk halikufanyiwa huduma hii.

  Je Biblia inasemaje? Kama deliverance ipo kama inavyofundishwa leo, basi Biblia haisemi ukweli! Kitabu cha Warumi hasa ukianza sura ya tano hadi ya nane inaonyesha ni kipi Yesu ametufanyia! na Sura ya sita inavunja dhana nzima ya Deliverance kwa muumini, na haya baadaye yamethibitishwa na vitabu vingine vya Paulo, hasa Wakolosai, Waefeso, Wagalatia nk! Kama ipo basi tulipookoka hatukupata Wakovu!

  2.Msimamo wako kuhusu ndoto: Huo haujasimama katika msingi wa neno la Mungu kabisa,Namfahamu mtu aiyeokoka na akaota mara nyingi yeye ni rais wa Tanzania! mpaka leo hajawahi kuwa katibu kata! Nimewahi kuota natuhumiwa kwa kesi ya uuaji na natafutwa na Polisi! Polisi nimekwenda kuwalipia watu dhamana na minor traffic offences! mke wangu mara nyingi ameota ana mtoto mdogo na ananyoshesha, hatuna mpango wa kuwa na mtoto kwa sasa hivi, na alipomsimuliwa wifi yake, na ambaye yuko kwenye “ministry” za wanaoona ndoto, aliambiwa inawezekana ameolewa kuzimu, na amepata mtoto huko! hivyo inabidi afanyiwe “deliverance” kumkomboa toka hiyo ndoa ya kuzimu! In short hiyo ministry ya ndoto inaleta maangazamizi kwa watu wengi wa Mungu!
  NAAMINI BWANA AMETUPA NJIA BORA NA RAHISI NA SAHIHI YA KUSEMA NA SISI- NENO LAKE!

 21. Benedicta, Nashukuru kwa kunielewe hata kama labda mawazo yangu labda yalikosa kufikisha nilichomaanisha.

  Kwanza Benedicta siwezi ku- “undo” kitu ambacho Bwana amekutendea! Nikiwa na maana Yeye aliyekuokoa au kwa kukuokoa amefanya haya “amekuhamisha na kukutoa katika nguvu za giza na kukuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake” “Amekufanya wewe mzao mteule wa Kikuhani” “Amekujaza na Roho WAKE” ” Amesema wewe ni tawi katika mzabibu ulio hai” “Amesema wewe umekuwa mwanaye katika Kristo Yesu” ” Amesema umekaa ndani yake na yeye Amekaa ndani yako” “Amesema alikujua toka misingi ya Ulimwengu” “Amesema amekununua kwa damu ya thamani” “Amesema ukienenda Kwa ROHO KAMWE hutazitimiza tamaa za Mwili” “Amesema uzivae Silaha zake ili uweze kuzishinda nguvu za giza”

  Je Benedicta mimi kweli naweza ku -“undo” Bwana alichokifanya kwako? Au kuna “mtume” au “Nabii” au “mtenda kazi” anaweza kufanya “Delivarance” juu ya hayo Bwana aliyokutendea? Kama kweli ulipompokea Yesu na kama kweli amekuokoa na amefanya yale niliyokueleza hapo juu huhutaji kuongeza kitu! Ila tumeona katika maisha haya kuwa kuna watu ambao inawezekana waliokoka wakawa au hawajui Bwana alivyowanyia walipookoka, au wameshinda kutembea katika maisha yao wakiwa wamezivaa silaha tulizipewa na Bwana, au kwa makusudi kabisa au bahati mbaya wameshindwa kabisa kulipa nafasi neno la Mungu lijae katika maisha yao, Hawapendi kupitia “painful process” ya kukua kiroho, na mara wanaposhindwa wanataka kitu kingine cha mkato!quick fixes Na cha kusikitisha sana wako watu ambao kweli ni wa Mungu nao pia kwa kujua au kutojua mafundisho sahihi ya Biblia wanadhani kuna njia mbadala au kuna kitu kingine kinaweza kuongezwa katika kile alichokifanya Yesu Msabalani! Na kwa kutumia nafasi hiyo pia Shetani ameingiza mafundisho ambayo hayapo kabisa katika Biblia! Ambayo Kina Paulo, Petro, na hata mitume wengine hawakukifanya! na ambacho hata katika Nyaraka zote alizoziandika Paulo kwa kanisa hakikufanyika! Wanajenga msingi mwingine kabisa ambayo sio Bwana aliyewafanyia watu wake! Kwa hiyo Benedicta angalia mtu asi “undo” kitu ambacho Yesu alikufanyia pale calvary! Nimeona watu wakihama hata yale basi tunayoita madhehebu ya “Kiroho” ingawa hakuna dhehebu la kiroho bali watu wa kiroho walizaliwa na ROHO wa Mungu, wakihamia makanisa mengine ya “rohoni” zaidi! waioisha hata batizwa ubatizo wa maji mengi wakibatizwa tena! Hatuwezi kuyaingia maisha ya ROHO WA KRISTO mara mbili, tatu, nne kadri ya “mitume” na “manabii” wa leo wanavyofuliwa! angalia tena mtu asi “undo” Bwana alichokufanyia!
  Asante

 22. Nakushukuru sana ndg yangu Orbi kwa kunipa pole. Ubarikiwe na Mungu aliye hai. Asante pia kwa kunipa home work, najua nia yako ni njema kabisa kunisaidia. Nitajibu kwa kifupi sana, km sivyo utanifundisha maana km walivyotangulia kusema wengine, name nipo kwa ajili ya kujifunza. kifupi, hii neema a wokovu niliipata baada ya kuambiwa habari njema, nikajua mimi ni mwenye dhambi nahitaji msaada wa Mungu, nikatubu na kumpokea Yesu sawa sawa na inavyosema Rum. 10:9-10, na kwa andiko hilohilo nilithibitishiwa kuwa nmeokoka. Kilichofanyika baada ya kuokoka kwangu umeshanisaidia kujibu. Baada ya hapo Mungu anatarajia niishi maisha matakatifu, ili nimwone yeye, sina bible hapa ila rejea ktk kitabu cha Ebrania 12 anaposema tutafute kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hapana atakayemwona Mungu asipokuwa nao. Agizo moja tu alilonipa ni kwenda kuwaambia watu habari hii njema duniani kote, ili atakayeamini na kubatizwa awe na uzima wa milele (Math 28:18-). Hapa pia, ktk matendo ya mitume ameniagiza nikishapokea nguvu ya Roho Mt. Nikawe shahidi kuanzia Yerusalem mpaka mwisho wan chi. Adui yangu mimi ni Shetani , na mna ya kumshinda tumepewa silaha katika efeso 6:10, na pia ktk ufunuo kuna ushindi upatikanao kwa damu ya Yesu na neon la ushuhuda. Baada ya maisha haya naingoja Yerusalemu mpya ambayo BWANA wetu Yesu anaandaa.
  Sasa nikuulize swali ndugu yangu, mimi kupata msaada wa Mungu ndio imekupa shida wewe? Mimi nimeokoka, na nina uhakika hili lisingenizuia kumwona Mungu maana yeye MUNGU mwenyewe amekuwa shahidi wa maisha yangu. Tatizo hapa ni nini? Kufanyiwa maombezi na kupewa ushauri ni dhambi ndugu yangu? Au unataka ku-‘undo’ nilichokipokea? Ubarikiwe na Mungu aliye hai!

 23. Shalom,
  Ndugu obi,
  ndg yetu obi tunakuomba labda usome michango yetu kuanzia mwanzo ili ikusaidie kujua tulipotoka mpaka tulipofika … nionavyo mimi ni kama umedandia gari kwa mbele….. mwanzo niliwahi kusema kuna mafundisho yaliyopitiliza kuhusu deliverance(EXTREME) sawa na mafundisho mengine kama imani, ubatizo, mafanikio ktk kristo nk pia kuna kupitiliza kwenye maeneo hayo….
  …Shida yako ni deliverance au deliverance kwa namna inavyofanywa na mitume na manabii?…..

  Katika mchango wangu wa mwisho kuhusu ndoto…. sikuwai kusema tunaongozwa na ndoto au tabia yoyote nilicho kiongea ni viashiria vichache tu hata sikumaliza ambavyo vinatokana uzoefu wa kwangu mimi na ndo maana niliweka angalizo hili HII SIO DREAM CODE… na mwisho nilisema ili kuwa na uhakika ni nini shida kwa asilimia mia moja ni lazima uumulize Roho Mtakatifu akwambie……ndg Obi usikurupuke siku zote kupinga fundisho bila kutafakari kwa kina labda kwa sababu doesnt make sense in ur mind…….

  Kuhusu ndoto… Zipo ndoto za aina 3, za kibidamu( zinatokana na shughuli nyingi-au mazingira yako) , ndoto za mapepo( zinaletwa na ulimwengu waroho wa mapepo), na mwisho za kutoka kwa Mungu….

  Mtu ambaye anaota ndoto za mapepo kwa mfano labda anazini na watu asio wajua kwenye ndoto ni wazi kuna tatizo la kushughulikia hapo……

  Mtu anayepata ndoto kutoka kwa Mungu ni lazima aihakikishe kwa neno sawa sawa na neno la Mungu linavyotufundisha kuhakikisha mambo…. njia mojawapo ambayo Roho Mtakatifu hutumia kutufikishia ujumbe ni NDOTO…. ila si kiblia kutafuta ndoto ila ni kiblia kufuta uongozi wa Roho Mtakatifu kwa njia yoyote itakayompendeza yeye kuitumia…..

  nikupe mfano niliowahi kukutana na binti mmoja katika huduma moja ya maombezi… aliniambia anashida na huwa anaota analala na nyoka mkubwa kitandani kwake… nikamuuliza je umeokoka akajibu ndio… tukaanza kuomba Mapepo yakalipuka yule binti akafunguka… aliponisimulia ile ndoto nilijua kuna nguvu za giza zinamfuatilia…
  Leo niishie Hapa maana sina muda wa kutosha …
  Mungu awabariki sana

 24. Kwa kifupi Biblia inafundisha Delivarance……..lakini si kama inavyofundishwa na hawa “Mitume” na “Manabii” wa leo, maana kila mmoja ana formula yake, kuna “Mtume” (transformation classes) ni lazima uingie katika madarasa maalumu, hata kama katika kanisa ulitoka uliiokoka, ulibatizwa au ulijazwa Roho Mtakatifu ni lazima uingie katika madarasa hayo! Na mara nyingi siku za mwisho ni maalumu, wanatafuta mahali maalumu na kwa siku tatu au nne kuhitimisha…..na “Delivarance” lazima ikutoe kitu, huwa lazima i-dismantle unachokiamini na kukufanya uanze upya kabisa, na nimewaona wengi baada ya hapa wakishia kubatizwa upya, hata kama walikuwa wameokoka, wamejazwa Roho mtakatifu hubatizwa upya na kuingia katika daraja la “Watenda Kazi” Siku huwa ni sherehe maalumu kwa huwa sasa huwa wamefanyika “wana wa Mungu” kwani kwa mafundisho ya mtume huyo “kufanyika wana wa Mungu” ni process sio kitu rahisi, kwa maana nyingine “Mtume” huyo ndio anafanya wakristo kuwa “Wana wa Mungu” Kama sio kulifukuru neno la Mungu sijui manake ni nini. Na wengi baada ya hizo “Tranformation Classes” wanakuwa na zeal ya muda tu, baada ya muda wanakuwa na mahangaiko yale yale ya maisha ya mkristo wa kawaida, “upenyo wa pesa” hauonekani, wako wanaosumbuliwa tena na magonjwa kama kawaida, yale mafundisho ya kuwa wao ni “super Christian” yanaendelea kuwafanya disoriented na frustrated, mkristo mmoja alieenda katika madarasa na baada ya kuona kuwa hata wakristo wanaodai wamefanyiwa delivarance wanafanya yale yale kama wakristo walio na tabia za mwili alisema hii kabisa anachokiona sio transformation bali dis transformation!

  Jambo kubwa ambalo wakristo lazima tukubali ni kuwa wengi tunashindwa kuishi maisha ya ushindi, maisha matakatifu, tumejaa tabia za mwilini swali ni Je tutazishindaje tabia za mwilini? Mtume Paulo alisema wazi ” Lakini ndugu zangu sikuweza kusema nanyi kama watu wa tabia ya rohoni, bali kama watu wa tabia ya mwilini, na kama watoto wachanga katika Kristo” Nadhani wote tunajua tabia ya mtoto mchanga……kazi ni kunyonya tu, kulala, kulia anapotaka kitu, kujisaidia hapo hapo, na wote hatushangai anapofanya hivyo, tatizo ni pale muda unapoendelea anapozidi kufanya hivyo! Paulo anaendelea kusema Naliwenyeshwa maziwa na wala sikuwalisha chakula, kwa maana mlikuwa hamjakiweza!, Naam na sasa hamkiwezi!kwa maana hata SASA NI WATU WA TABIA YA MWILINI!” na anaendelea kusema ikiwa kwenu kuna husuda, fitina ninyi ni wa tabia za mwilini! Kwa kifupi wanaofanyia wakristo “Delivarance” wanadhani watawafanya watu kutoka katika hali ya utoto uchanga na kuwafanya watu wazima ghafla! wanaikimbia painful process ya kukua kiroho! Wanataka njia ya mkato! Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ameweka wazi ” Ambaye tuna maneno mengi ya kunena habari zake na ni shida kuyaeleza;KWA KUWA MMEKUWA WAVIVU WA KUSIKIA …….maana wakati mwingi umepita ( yaani mmedumaa) mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu;nanyi mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu……kwa maana atumiae maziwa hajui SANA NENO LA HAKI….KWA KUWA NI MTOTO MCHANGA LAKINI CHAKULA KIGUMU NI CHA WATU WAZIMA, AMBAO AKILI ZAO KWA KUTUMIWA ZIMEZOEZWA KUPAMBANUA MEMA NA MABAYA (Heb5:11-14)
  Wakristo wengi ni wavivu…….bado hawajaweza kupambanua hata lipi ni jema kwa mkristo na lipi baya, bado wanalialia tu, biashara zinaponenda kombo, magonjwa, nk wanadhani au ni vifungo na vinatakiwa vifanyiwe “Delivarance” Ni lini watakaposema kama Paulo ” Ni nani atakayetutenga na Upendo wa Kristo, Je dhiki, au shida, au adha,au njaa, au uchi, au hatari, au upanga” Rumi 8:33.

  Nakala nyingine nitawaletea Delivarance kama inavyofundishwa na Biblia, ningeshauri sana wakristo wasome kitabu cha Warumi. Mungu na Wabariki

 25. Ndugu Paul Holela……Nimeshtushwa na na post yako kuhusu ndoto……na hasa ulipoanza kwa kusema haya.

  ….”angalia ndoto unazoota, kuna aina fulani za ndoto ukiona zinakutokea mara kwa mara ujue kuna eneo kwenye maisha yako haiko sawa….”

  Naamini Strictly Gospel ni Web site ya Kikristo, naamini ni kutuwezesha kuwasiliana, kufundisha katika imani ya Kikristo iliyojengwa katika msingi wa Neno la Mungu, naamini utofauti wetu mdogo mdogo ambao hautavunja ule msingi wa kusimama katika neno la Mungu……na naamini kila hoja lazima iwe imeshiba na imejaa nukuu au ambacho kiko wazi na dhahiri katika maneno yaliyowazi na yaliyofuunuliwa yaani neno la Mungu kwa ajili ya kujengana.
  Kwa kusema hivyo basi…….utasemaje ndugu yangu kuwa ndoto ndio zinakuwa kigezo cha kutuonyesha maeneo ambayo hatuko sawa katika maisha yetu.Tangu lini ndoto zikachukua nafasi ya Neno la Mungu? Tangu lini ndoto zikachukua nafasi ya Roho Mtakatifu? Na huyo anayetafsri ndoto amepewe mamlaka hiyo na nani? Ni mafundisho mapya unayoyapost kwenye web……na si mazuri kwa wakristo hasa wale wachanga,Ndoto haikuwa chombo cha msingi cha kupeleka ujumbe katika agano la kale wala jipya, Narudia tena, Ndoto haikuwa chombo cha msingi cha kuupelea ujumbe wa Mungu kwa binadamu katika kuupeleka ujumbe wake, ni kweli Mungu alitumia Ndoto katika vipindi fulani fulani lakini it was not a pattern…..na wala haikuwa kuwaonya watu katika mwenendo wa maisha yao……na wala hazikuwa ndoto zinazojirudia mara kwa mara kama usemavyo wewe.Maisha ya binadamu ni mapana sana yenye utofauti mkubwa ( Diversity of experiences) Hivyo ni kichekesho sana kutufunga na tafsiri zako chache, Ni neno la Mungu….ambalo ni upanga ukatao kuwili unaweza kuzichunguza nafsi…..” ndio zinaweza kutuonyesha maisha yetu yako sawa au si sawa mbele za Mwenyezi Mungu, na wala sio ndoto zinazojirudia rudia. Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ameweka wazi, kuwa hapo zamani Mungu alizungumza nasi kwa ya manabii na njia mbali mbali, lakini sasa anazungumza kwa kupitia Mwanaye ( Yesu Kristo)
  Tatizo lililoko leo ni Wakristo kulidunisha neno la Mungu na kutafufa njia mbadala ambayo inaonekana ina nguvu zaidi, ndio maana kwa mawazo yangu kuna mfumuko wa Manabii, Mitume, nk ambayo wanaaminika kuliko hata neno la Mungu linavyosema! Manabii, Mitume, Watenda miujiza lazima wawe katika wigo wa maneno dhahiri ya Biblia.Hatutaongozwa na ndoto, maono, experiences zetu hata ziwe za ajabu kiasi gani, na zitakapokuja tutazipima kwa vigezo vya neno la Mungu, Kwetu sisi siku zote na iwe Je maandiko yanasemaje, hatuwezi kukuwa Kiroho tukayapita maneno ya Mungu, na Mungu hawezi kusema na sisi kwa njia itakayoyadunisha maneno yake!

 26. Mpendwa Benedicta pole sana! Labda nianze nanukuu yako ya kwanza
  ” Inakuwaje kuwa mtu unaokoka unaendelea katika vifungo katika vifungu vya ibilisi, unaendelea kubeba laana za mababu unarithi magonjwa ya ukoo nk”

  Benedicta napenda kukuuliza maswali yafuatayo kwanza;
  1.Ulijuaje kwamba umeokoka?
  2.Ni nini kilichokuthibitishia kuwa umeokoka
  3.Ni nini ulichoambiwa kwako kimefanyika baada ya wewe kuokoka
  4.Ni nini Mungu anarajiwa wewe ufanye ukiwa hapa ulimwenguni katika maisha yako mapya ya wokovu.
  5.Ni vitu gani ambavyo nia adui yako katika maisha haya ya wokovu, na utafanyaje kuvishinda ili uweze kuendelea katika maisha yako ya kuokoka.
  6.Je baada ya maisha haya ya sasa yaani ya kitambo kifupi mno, kuna maisha gani mapya katika ulimwengu ujao kwa mtu aliyeokoka, kwa nini kunamaisha hayo, ni kipi ambacho leo tukiwa wana Mungu tumekikosa tutapewa katika maisha yajayo?

  Kwa kifupi Benedicta haya ni maswali yanayoonekana ni ya kitoto katika ukristo……lakini wengi wamekwama hapo, na ukianza na msingi mbaya katika Imani hii, au Paulo anasema ukijenga kwa vitu vibovu juu ya msingi aliouweka yaani Kristo mwenyewe…..kila kitu baadaye kitapotea, na kinaweza kuwa ni usumbufu katika kusimama katika Neema hii!
  Benedicta, Swali la kwanza sijui utalijibuje, Kwa kifupi tumejua tumeokoka kwa sababu Neno la Mungu limesema hivyo ( Sitaki kabisa kunukuu maandiko) ningependwa wewe mwenyewe ufanye homework hiyo! Sidhani uliambiwa na mtu umeokoka, na kama kuna watu….yaani wachungaji, mitume, manabii, watenda kazi walikuambia maneno yao hayana nguvu, lazima upate uthibitisho wewe mwenyewe kama umeokoka, na ni Lazima Neno la Mungu likuthibitishe hivyo SI KITU KINGINE.
  Je Maandiko yanasemaje kuhusu nini kilitokea/kimetokea baada ya wewe kuokoka,Kwa kifupi Biblia inasema umekuwa kiumbe kipya, umekuwa mwana wa Mungu, umefanyika mzao mtakatifu, umetolewa katika nguvu za giza ukaingizwa katika ufalme wa pendo lake, umepata uzima wa milele, sasa basi hakuna hukumu kwako ( kwa walio katika Kristo Yesu) Yesu amefanyika laana kwa ajili yako, yaani kwa kukubali dhambi zako. Je ni nani huyo anayekuambia umeendelea katika laana za mababu, Je ni mtume, ni nabii, ni mtenda kazi! Je ana uwezo wa kubadilisha maneno ya Mungu? ana nguvu ya kutangua kweli hii, usijali hata kama ana uweza wa kuwekea mikono watu wakaanguka chini, usijali hata kama ana kanisa kubwa lenye wafuasi wengi! hawezi kuubadili ukweli huu, Neno la Mungu ni Kweli!
  Unaweza ukaniuliza sasa rafiki Orbi, mbona bado mambo ya zamani (iwe tamaa za dhambi mbali mbali ) zinavuta, na hata kuna wakati naona kama zinanishinda, Ndio nakubali na wewe, lakini Hii aifanye wewe usiwe kiumbe kipya, wala usiwe umetolewa na kuhamishwa kutoka nguvu za giza, kitendo cha kutoifurahia hali hiyo na kuandika kati website hii nikuwa hujaifurahia hali hiyo, na wewe ni hai kiroho! na wala hauko katika vifungo vya ibilisi! Je Biblia inasemaje katika hali hiyo unayoipitia? Tuko katika mashindano ya Kiroho miili yetu hii ya dhambi inataka kuikataa hali yetu mpya iliyoumbwa ndani yetu, miili yetu inaukataa uhai mpya wa Kiroho, tumefanyiwa spirit transfussion, na kadri tutakavyoishi duniani miili yetu itakuwa inajaribu kuikataa hali mpya iliyoko ndani yetu, huyu ni adui yetu wa kwanza kabisa tangu tulipookoka…..na wengi kwa kushindwa kujua hilo, na Yesu amefanya nini kuikabili hilo wamekuja na mafundisho mengi….mengi sana…….miaka ya nyuma katika historia ya ukristo wengine waliamua kuwa watawa na kukaa peke yao……wengine walijitesa na kujivisha duni…..wengine hata kujaribu kujisulibisha kuufisha mwili na tamaa zake ili kuupata ukamilifu……na leo kwa kutojua hilo baadhi yetu wamekuja na mafundisho ya delivarance…….! ambayo ningesema is Just reinventing the Gospel……….ni Injili mpya, injili ya kujikamilisha kwa bidii……NITAENDELEA SIKU NYINGINE TAFADHALI JIBU MASWALI HAYO KWA KUTUMIA BIBLIA TU…….!

 27. Mpendwa A.S, nikinukuu usemi wako ambao umesema hivi ” Delivarance ni muhimu kwa sababu tumepita katika mambo mengi na lazima tufunguliwe kwa Delivarance…” Je ni unaweza kuthibitisha kwa Maandiko? Je ni mambo gani hayo ambayo kifo cha Yesu msalabani kilishindwa kuyamaliza ambayo inabidi yamalize kwa Delivarance? Je hata Roho mtakatifu hana nguvu dhidi ya Delivarance? Manake neno la Mungu linasema wazi TUKIENENDA KWA ROHO HATUTAZITIMIZA KAMWE TAMAA ZA MWILI……Je ni kweli Delivarance ina nguvu kuliko hata Roho wa Mungu? Naogopa sana mafundisho hayo, manake kwanza inabidi tumpokee Yesu ambaye hatamaliza yote, halafu pia inabidi tumpokee Roho mtakatifu, ambaye pia hataweza kutupa uweza kamili, na pia inabidi tuzivae silaha za Mungu ambazo pia hazina uweza wa kutosha kuzishinda nguvu za yule mwovu, isipokuwa mpaka tufunguliwe kwa “Delivarence” Kweli hii ni Injili nyingine, na Yesu Mwingine na Roho mwingine anayehubiriwa, maana yule wa kwanza aliyetuokoa hana nguvu, anahitaji usaidizi wa “Delivarance”!

 28. Ayub Nkya: Unasema kwamba “Delivarance” ni muhimu kwa sababu ya mikataba tuliyoingia na shetani kabla ya hatujaokoka, ni wapi unayapata hayo katika neno la Mungu? Je damu ya Yesu haitoshi kutusafisha kama yasemavyo maandiko, Je nguvu na Uweza wa Roho Mtakatifu unashindwa kututoa katika nguvu za giza mpaka Nabii, mtume, mtumishi au mtenda kazi atufanyie “Delivarance”?
  Mkataba wa kutuingiza kwenye dhambi au nguvu za dhambi ulifanywa na Adamu…….na Kwa njia ya Yesu yeye asiyejua dhambi, lakini alifanywa dhambi kwa ajili yetu ndiye anayeweza kututoa katika nguvu za giza ( Dhambi) na kazi hii ilifanyika miaka 2000 iliyopita! ambapo hati ya mashtaka ya hukumu iliyondolewa kwa wale wanaomwamini Yesu, Sina haja ya kutafuta kaburi la mababu zangu, wala ukoo wangu, kwani aliyeningiiza katika laana ya dhambi ni Adamu na aiyenitoa ni Mwana wa Mungu! Aliyeketi mkono wa kuume wa Mungu baba!na akamwaga Roho wake ndani yangu na kufanya makao yake katika maisha ya yangu na ya kila mwamini! Babu yangu yuko kaburi amelala hana nguvu nami!Na hata ukoo wangu! Babu yangu Anasuburi hukumu…..kama alisikia Injili akaikubali atapata uzima wa milele…..! hana nguvu kamwe na maisha yangu yaliyofichwa katika Kristo Yesu…….hivyo neno la Mungu lisemavyo!

 29. Watu wa Mungu msimamo wetu kwenye jambo lolote lazima uwe katika maneno ya Mungu, wala sio mafundisho ya mtu yoyote, experience zetu zisitulazimishe tutengeneze doctrines ambazo haziko kwenye Neno la Mungu.
  Sijaona mahali popote ndani ya Biblia ( Agano Jipya) Huduma ya “Delivarence” ikifanyika, na kama kweli huduma ya ” Delivarence” inatakiwa kwa mtu aliyeokoka, basi kanisa la Wakorintho huduma hii ingefanyika, kanisa hilo lilijaa uzinzi ndani ya nyumba ya Mungu usiokuwepo hata katika mataifa! Kanisa hilo lilijaa ugomvi na hata kuwaita watu walio nje ya wakovu kuja kuamua! Lakini Paulo hakufanya “Delivarence” Na kama kama “Delivarence” ipo basi yale makanisa saba ya Asia kwenye kitabu cha ufunuo yasingeliambiwa “Tubu” “Tubu” “Tubu” Kanisa la Wagalatia ambalo Paulo alithubutu kuwaambia wamelogwa halikufanyia “Delivarance”…….Kwa kifupi kuanzia kitabu cha matendo ya mitume hadi ufunuo humuoni Petro, Yohana, Paulo, Luka akiwafanyiwa wakristo waliookoka “Delivarence” hata kuwafundisha tu!
  Nini tunachoona katika makanisa yote ndani ya Agano jipya, Ni wakristo ( Watu wenye Dhambi) wakipokea msamaha wa Mungu katika Kristo Yesu, wakizaliwa upya katika roho, na kujazwa na Roho Mtakatifu……wakihamishwa kutoka nguvu za giza na kuingia katika ufalme wa Mungu, Wakilindwa na nguvu za Mungu, wakiambia tazama yote yamekuwa mapya, wakiambia walikufa pamoja na Kristo na na wamefufuliwa pamoja naye na sasa wanatakiwa waenende katika upya wa uzima, na uhai wao umefichwa katika kristo Yesu, na pia wemekirimiwa tabia ya kiungu na mzao mtakatifu wa Kikuhani, na wanakumbushwa kuwa hapo awali walikuwa wazinzi, waaasharati, wachawi, watukanaji, wafiraji…..lakini SASA wamesafanishwa na kufanywa wapya!!! na wanaambia wakienenda Kwa ROHO KAMWE HAWATAZITIMIZA TAMAA ZA MWILI!……Hatuoni kabisa huduma ya “Delivarence” ! Isipokuwa Wakristo waliokoka wanaambia wakue wasiwe tena watoto wachanga, ili wamfikie Yeye ( Kristo) katika yote……na wanambia kushindana kwetu sisi ni dhidi ya pepo wabaya na nguvu za giza katika ulimwengu wa roho……na tuzivae silaha zote za Mungu ili tupate kushinda! Sio kufanyiwa ” Delivarence” na hata tukishindwa tunakumbushwa Kutubu na kumrejea Mungu….kama vile makanisa saba ya Asia yalivyofanyiwa……!!!
  Hivyo ndugu yangu ni Imani ile ile iliyotuokoa, na ile ile iliyotufanya tumpokee Roho wake ndio itakayo tusimamisha! Tulianza kwa Roho je tunataka tumalize kwa”Delivarance” ? Tumelogwa kiasi hicho…..! Mungu na atubariki na kutufungualia neema yake tujue uweza waka kwetu sisi tuaminio, kwani Injili ni Uweza wa Mungu uletao Delivarence kwa kila aaminiye!

 30. Ndg Paul Holela,

  Nashukuru kwa kunitakia baraka za Mungu. Tuzidi kombeana ili mwili wa Kristo upate kujengwa pia kutokana na tunachoshirikishana hapa.

  Mimi binafsi nimejifunza mengi sana kutokana na michango ya maoni unayoandika hapa. Na ninatumaini utaendelea kuandika mengi kadri neema ya Mungu itakavyotujalia kuwepo hapa. Katika mchango wako wa mwisho hapo juu umeandika vidokezo/dalili ambazo zinaweza kuashiria kwamba kuna tatizo mahali fulani. Nimejifunza mengi pia hapo. Jambo la muhimu pia nililopata hapo ni ile tahadhari kwamba hiyo siyo DREAM CODE, ili kwa namna yoyote ile isije ikatafsiriwa vibaya na hivyo kupotoshwa kwa kusudi ulilolikudusia kwa kuandika hayo.

  Ni shauku na maombi yangu kwamba Mungu wa mbinguni akuzidishe katika maarifa ili uendelee kuandika kilichoko moyoni mwako kwa ajili ya watu kuongeza maarifa na ufahamu wa elimu ya Mungu Aliye Hai.

  Neema ya Mungu izidi kukaa nasi!

 31. Shalom,
  Asante sana sana ndugu yetu John Paul kwa ufafanuzi wako Mungu akubariki sana ….

  Niongelee kitu kimoja leo Na NI DALILI ZA KUWEPO KWA VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA KWENYE MWILI/NAFSI YA MTU…. sasa hii inatokana na expirience ya kudeal na aina hii ya maombi kwa watu tofauti tofauti…… ili kujua kama kuna hivi vifungo kwenye maisha yako kuna vitu unaweza kuviona…. YUDA 1:8..Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, ………
  1. Angalia aina za NDOTO unazoota…… kuna aina fulani za ndoto ukioona zinakutokea mara kwa mara uje kuna eneo kwenye maisha yako haliko sawa….
  i) ukiota unazini na watu usiowajua/wakati mwingine unawajua katika ndoto…. hapa ujue kuna shida ipo hasa roho za uasherati
  ii) ukiota upo makaburi na hasa upo na watu usiowajua.. kuna vifungo vya kichawi au nguvu za kichawi zinakufuatilia…..
  iii) ukiota unalishwa vyakula kwenye ndoto….nguvu za kichawi au miungu ya koo ulizotoka zinakufuatilia
  iv) kuota unafukuzwa na manyoka,wanyama nk
  v) kuota unatumbukia kwenye shimo refu…
  vi)kuota upo kwenye maeneo unafanyakazi…au biashara au unabeba mizigo wakati wewe haufanyi hizi kazi…
  vii) kuota unanyonyesha watoto wakati wewe huna mume ….

  2.Angalia nyakati fulani fulani kuna vitu unasikia vinatembea kwenye mwili wako au kichwani….

  3.Tabia za kupenda kula vitu kama udongo wa pemba…. Mkaa….unga……
  4.Kutokufanikiwa wakati umefuata taratibu sahihi…
  5. kubanwa mbavu, kifua au kooo wakati ukiwa ukiomba….
  6.Aina fulani ya majivuno/hasira…. mfano watu wanaotokea kwenye koo za kichifu wana hivi wengi hata kama wameokoka…
  Naomba leo niishie hapa wakati mwingine nitaendelea ila hii sio DREAM CODE…. inatoka na uzoefu tu kuna vifungo vingine unaweza usione hata moja ya hizi dalili….. Kwa uhakika wa asilimia mia moja ni lazima umuulize Mungu akuambie nini kipo hapo…..

  Tuendelee kujadili na kujifunza…..
  Mungu awatunze..

 32. Dada Happy Nashukuru kwa kunitakia baraka. Sifa na utukufu wote ni kwa Mungu. Tuendelee kuombeana katika safari hii ya mbinguni.

 33. Shalom!

  Katika maswali 17 yaliyoulizwa na ndg yetu Eng. Paul Holela kuna swali la 16 naona halijapatiwa jibu hadi sasa. Swali hilo liko hivi:

  16.naomba mnisaidie kuilewa warumi 7:14-25.

  Swali hili ninalijibu kama ifuatavyo:

  Warumi 7:14-25 imeandikwa hivi,

  “Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi bali lile nilichukialo ndilo nalitenda. Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema, kwa kuwa kutaka nataka bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililoj ema, lipo lilipo baya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka wa ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, masikini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”

  Maneno haya ya mtume Paulo yanaonyesha mgongano ulioko ndani ya mtu ambaye anaishi kwa kufuata sheria ya torati wakati huu wa sheria ya Roho. Wakati wa torati mtu alikuwa anahesabiwa haki au hatia kwa kutenda au kutokutenda jambo fulani. Kwa sababu hiyo kulikuwa na uwezekano wa mtu kutenda jambo fulani la torati kwa sababu ya kulazimika kufanya, hata kama ndani yake hajisikii kufanya hivyo. Vile vile kulikuwa na uwezekano wa kutokufanya jambo fulani ili aitii amri ya torati hata kama ndani yake anajisikia kulifanya.

  Baada ya anguko la Adamu asili ya dhambi ilitawala mwili na mwanadamu akajikuta ndani ya mwili wake kunatoka tamaa ya kutenda matendo ambayo torati iliyakataza. Yale matendo yaliyokatazwa na torati yalihesabiwa kuwa ni dhambi. Na kwa sababu ndani ya mtu kulikuwa na tamaa ya kuyatenda hayo, basi dhambi ilianza kutenda kazi ndani ya mtu na kuzaa mtunda ya mauti yaliyoonekana kwa nje.

  Sasa katika hii sura ya 7 kuanzia mstari ule wa 14 anaeleza juu ya mtu anayefahamu agizo la Mungu katika akili yake lakini mwili wake unataka kutenda matendo yaliyo tofauti na kile ambacho akili inakifahamu kuwa ni chema. Ndiyo maana akasema kama anatenda anachoona hakifai basi, si yeye, bali ni ile dhambi iliyo ndani. Kwa sababu ni mapenzi yake kutenda ambacho katika akili yake anakiona kinafaa. Lakini badala ya kutenda hicho anajikuta anatenda kingine. Kwa hiyo ni lazima kuwe na nguvu nyingine inayomsukuma kutenda asichopenda: ndiyo ile dhambi iliyoko ndani yake.

  Ndiyo maana akamalizia ufafanuzi huo katika mstari ule wa 25 kwamba: KWA AKILI ANAITUMIKIA SHERIA YA MUNGU BALI KWA MWILI SHERIA YA DHAMBI.

  Ni ukweli kwamba Mungu anatuhitaji tumtumikie si katika akili zetu tu bali katika miili yetu pia. Lakini tutawezaje kumtumikia katika mwili wakati mwili ndio huo unatumikia sheria ya dhambi?

  Mtu akisoma na kumalizia katika mstari wa 25 wa sura ya 7 inawezekana kabisa akaibuka na hoja kwamba: haiwezekani kumtumikia Mungu katika mwili kwa maana mwili unaitumikia sheria ya dhambi. Kwa hiyo inawezekana tu kumtumikia Mungu katika akili. Hivyo hata kama mtu anaweza kuonekana anatenda matendo mabaya [dhambi], lakini inawezekana katika akili yake mtu huyo anamtumikia Mungu. Ndiyo! Mtu anaweza kuja na hoja hii, kwa sababu ndivyo ilivyoandikwa kwenye Biblia katika Warumi 7:25.

  Lakini ili kuelewa kusudi kamili la ujumbe huu ni lazima kuendelea kusoma Biblia katika sura ile ya 8. Ni muhimu kusoma zaidi kwa sababu Wakati Biblia ilipoandikwa haikuwa inaandikwa kwa sura na mistari. Hivi viliwekwa ili kurahisisha usomaji na uwekaji kumbukumbu. Kwa hiyo si lazima ujumbe fulani wote ukamilike kwenye sura au mstari mmoja tu.

  Katika Warumi 8:1-2 tunapata maandiko haya,
  “Basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru mbali na sheria ya dhambi na mauti”

  Warumi 8:3-4, “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili,ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho”

  Maana ya maneno hayo ni hii: mtu aliye ndani ya Kristo Yesu huyo yuko chini ya sheria ya Roho wa uzima ulio katika Kristo Yesu. Kwa kufa pale msalabani Yesu aliihukumu na kuiondoa dhambi ile iliyokuwa ndani ya mwili. Mtu akimpokea Yesu dhambi inahukumiwa na kuondolewa ndani yake. Baada ya ile dhambi kuondoka ndani yale maagizo ya torati yanaanza kutimizwa kuanzia ndani, ambapo mwanzoni ni dhambi ndiyo ilikuwa inafanya kazi. Kwa hiyo badala ya mtu kuongozwa na dhambi kutenda matendo yaliyo kinyume cha maagizo ya torati, saa maagizo ya torati yanaanza kutekelezwa ndani yake.

  Hali hii ninaifananisha na simu ambavyo baada ya kuharibika kwa program iliyoko ndani yake, ii kuirejesha katika hali nzuri ni lazima kui-flush. Au kompyuta ikiharibiwa na virusi ili kuitibu inabidi kui-format. [au neno lolote ambalo humaanisha kuweka program upya ili irudi katika hali nzuri]. Mtu anapookoka utu wake wa ndani husafishwa. Ile dhambi iliyokuwa ndani huondolewa na nguvu mpya ya Roho ambayo huwezesha magizo ya torati kutekelewa kuanzia ndani huingia. Kwa hiyo huyo automatically hawezi kujisikia vizuri kutenda maagizo ya Mungu.

  Hapa ndipo tunapata maneno haya katika Ebrania 8:10,
  “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israel baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao. Na katika mioyo yao nitaziandika. Nami nitakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu wangu”

  Tukiendelea katika ile Warumi 8:5-7 tunasoma hivi, “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa mana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii”

  Hicho ndicho tulichosoma katika Warumi 7:25 kwamba mwili hutumikia sheria ya dhambi na ambayo ndiyo uadui juu ya Mungu. Ndiyo maana inaendelea kusema katika Warumi 8:8, “Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu” Kwa nini? ….kwa kuwa mwili hutumikia sheria ya dhambi!

  Tukiendelea tena katika Warumi 8:9-11 tunasoma hivi:
  “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu,ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliye mfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu”

  Roho mtakatifu akiingia ndani ya mtu mwili wa mtu huyo huhuishwa ili uweze kutenda matendo mema. Mwili kama mwili hauwezi kutenda mema. Inatakiwa nguvu nyingine ya ziada kuuendesha mwili ili utende mema. Ndiyo maana mtu ambaye hajaokoka hana uwezo wa kujizuia asitende mabaya. Maana mwili unatenda kazi kwa nguvu yake ya asili ambayo inatumikia sheria ya dhambi. Na wakati mwingine hali huwa mbaya zaidi inapotokea mwili wa mtu huyo unaongozwa na nguvu nyingine ya mapepo. Hapo ndiyo kabisaaaa, mtu wa namna hiyo hawezi kuepuka kutenda maovu. Ndiyo maana utakuta watu wengi wanatumikia kwa mfano uasherati kumbe ndani yao kuna mapepo yanayowaendesha. Mtu huyo akiookoka na mapepo yakiondoka hushangaa kuona ile tamaa iliyokuwa inamsumbua haipo tena. Kwa nini?…kwa sababu ndani yake imeingia nguvu mpya – nguvu ya Roho ambayo huusafisha na kuuhuisha mwili huo.

  Kwa hiyo…..

  Warumi 8:12-14,
  Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili; kwa maana mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu”

  Mtu akiishi kwa kufuata mambo ya mwili huyo anataka kufa kwa kuwa mwili hauwezi kuitii sheria ya Mungu. Kinachotakiwa ni kuyafisha matendo ya mwili kwa Roho wa Mungu. Lakini matendo ya mwili yanawezaje kufishwa? Yanawezwa kufishwa kwa kuwa imo nguvu ndani ya Roho wa Mungu yenye uwezo wa kuyafisha. Na yanayofishwa ni matendo ya dhambi, ambayo yanapatikana katika Wagalatia 5:19-21 na baadhi yake ni uasherati,uchafu, usifadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, ulevi, chuki, fitina, faraka, hasira. Maana watendao haya hawataurithi ufalme wa Mungu. Hayo yakishafishwa, badala yake yanawekwa mengine mapya ambayo yanapatika katika Wagalatia 5:22-23, ambayo baadhi yake ni upendo, furahaha, amani, utu wema, fadhili, uaminifu, upole.

  Kama mtu anasema ameokoka lakini bado ni mgomvi, ni mwenye fitina, ni mwenye chuki, nk basi lazima bado kuna tatizo mahali fulani kwa kuwa palipo na Roho wa Mungu hakuna mambo hayo. Na kuna uwezekano mkubwa sana wa mtu wa namna hii kuwa chini ya vifungo vya shetani. Mtu ambaye hajampokea Yesu hana namna yoyote ya kuweza kuitii sheria ya Mungu kwa kuwa bado anaongozwa na nguvu ya asili ya mwili. Katika asili hiyo ndipo kunakotoka matunda ya mwili ambayo nimeyataja katika Wagalatia 5:19-21.

  Njia pekee ya kuufanya mwili uitii sheria ya Mungu ni kwa kuuhuisha kwa nguvu ya Roho mtakatifu. Nguvu ya Roho ikiuhuisha mwili mtu huyo anaweza sasa kuenenda kwa Roho, maana ni kwa kuenenda kwa Roho peke yake ndiko kunakomfanya mtu asitimize tamaa za mwili ambazo matunda yake hupingana na zile tabia njema za Roho.

  Jibu langu limeishia hapa. Kama nimefafanua isivyo sahihi nitafurahi kusahihishwa ili tuendelee kujifunza.

 34. Shalom,
  Tunamshukuru Mungu sana kwa Benedikta kupata kitu cha kukusaidia na kuvuka mahali ulipokuwa umekwama Jina la Yesu litukuzwe….., Hii deliverance tuliyoizungumzia humu ni kipande kidogo sana kulingana na uelewa wa watu wengi ila ni pana sana hasa kwenye eneo la ardhi …. ni muhimu sana kujifunza mafundisho ya namna hiii…. na aina ya mafundisho ambayo shetani huwa hapendi wapendwa wajue maana ndipo mahali hasa ambapo huwa anajificha na kuwakandamiza wana Mungu….. kujua mbinu na mikakati wanayotumia nguvu za giza kushambulia Wana wa Mungu ni kitu muhimu ingawa inahitajika balance hapa usije ukawa EXTREME halafu ukaleta shida kwenye mwili wa Kristo…….Nawaombea Kwa MUNGU wote waliosikia na kuelewa michango tuliochangia kwa nia ya kuwasaidia ndugu zetu tunaowapenda muweze kutendea kazi hakika maisha yako hayatakuwa kama yalivyo……

  Mimi napatikana UDSM…. na pia huwa tunafanya maombi kila mwezi kwa siku 5 mfululizo kwa ajili ya Taifa,Kanisa na pia watu wenye shida mbali mbali …… Tunafanyia Kimara Rombo katika kanisa la KKKT-GIDE sio maombi ya kidini ni ya kitaifa na madhehebu yote mnakaribishwa tuombee nchi Yetu….
  Mungu awatunze Wasomaji wote,

  SG mbarikiwe sana

 35. Bwana Yesu asifiwe. Namshukuru Mungu kwa ajili ya kila mmoja aliyetoa mchango wake katika mada hii.kwa kuwa huwa napenda kujifunza zaidi kutoka kwa wana wa Mungu, Nimepata vitu vingi vya kunisaidia,yale yote niliyoona kwamba yatanisaidia niliyafanyia kazi. Namshukuru Mungu, nawashukuru wachangiaji wote, kwani sasa its almost 2 months sija-experience tena hali ilokuwa ikinisumbua.Huu ni muujiza mkubwa sana kwangu, SIFA NA UTUKUFU KWA JEHOVA!
  Nimejifunza pia mengi, tofauti na msimamo nilokuwa nao, Lakini ukweli sio wote tulopata neema ya kuzaliwa ktk familia za kikristo, wengie tumepitishwa ktk mengi toka tukiwa watoto,bila kuwekewa mkono tungeendelea kuteseka, lakini ashukuriwe BWANA YESU niko huru sasa! Natamani kujifunza zaidi hata hiyo ya ukombozi wa ardhi. nimeisikia ikitajwa nilipohudhuria maombi ya kuombea nchi mahali flani.Naamini kuwa watumishi wote hawajapewa mafunuo yanayofanana, tuendelee kufundishana kwa kadri BWANA alivyomjalia kila mmoja
  Shalom Shalom!

 36. Shalom,
  Tunashukuru kwa ndg yetu John Paul kwa kujibu mpaka swali la 15, tumebakiwa na swali moja la 16 maana swali la 17 ndg yetu Haggai alishalijibu… ila kama kuna mtu ana maelezo mengine zaidi ya haya yaliyotolewa tunakaribisha ili tuendelee kujifunza…

  Ndugu Yetu BENEDICTA je mpaka hapa umepata vitu vya kukusaidia?

  Mungu awabariki Tuendelee kujifunza…

 37. Bwana Yesu asifiwe!

  Ninajibu maswali ya ndugu Eng Paul Holela ambayo yamebakia.

  11.Je Mtu ambaye hajui TRUTH ya mamlaka na privileges ktk Kristo na kuzitumia (exercising authority) hawezi kukandamizwa na nguvu za giza?

  Jibu: Mtu ambaye hajuwi TRUTH ya mamlaka na privileges katika Kristo na kuzitumia (exercing authority)anaweza kukandamizwa na nguvu za giza. Kinachosababisha akandamizwe ni hicho kwamba hana ufahamu wa kutosha juu ya mamlaka na uwezo katika Kristo. Kwa mameno mengine hana ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu.

  Kutokulifahamu neno la Mungu ipasavyo ndiyo sababu kubwa ya kufanya mtu aendelee kukaa katika vifungo hata baada ya kuwa ameokoka. Kutokulifahamu Neno huku hakuhatarishi uhuru wake tu bali huhatarisha hata hatima ya maisha yake ya kiroho na uhusiano na Mungu kwa ujumla. Kadri kiwango cha ufahamu wa Neno kinapokuwa kidogo vivyo hivyo kiwango cha utakatifu huwa kidogo. Na kadri kiwango cha utakatifu kinapokuwa kidogo ndivyo ulinzi wa nguvu za Mungu na mamlaka ya Jina la Yesu unavyokuwa mdogo. Ulinzi mdogo wa nguvu za Mungu ndio hupelekea mtu huyo akandamizwe na nguvu za giza.

  12.Mtu ambaye hajui kuitumia imani kama ngao dhidi ya mishale ya adui efeso 6:16… je mashetani wakipiga mishale haitampata kwa sababu ameokoka? na ikimpata tukamwombea akalipuka pepo atakuwa hajaokoka?

  Jibu: Mtu ambaye hajuwi kuitumia imani kama ngao dhidi ya mishale ya adui ni dhahiri kwamba hawezi kuizuia mishale ya mashetani. Katika kitabu kile cha Waebrania 11 tunasoma juu ya imani. Na katika ule mstari wa 6 imeandikwa jinsi ambavyo pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Na katika Ebr 10:38 imeandikwa jinsi mwenye haki anavyotakiwa kuishi kwa imani pasipo kusitasita maana kusitasita hakumfurahishi Mungu. Kwa hiyo basi ukosefu wa imani na kushindwa kuitumia imani ipasavyo humweka mtu,japo anasema ameokoka, katika mazingira ambayo Mungu hafurahishwi naye. Mazingira haya ndiyo yanaweza kufungua milango kwa mapepo na nguvu za giza kwa ujumla kuweza kumvamia mtu. Kutokuwa na imani na kushindwa kuitumia si hali nzuri kwa mtu anayesema ameokoka. Ni tatizo!

  Kutokana na Efeso 6:10-18 Mkristo, mtu anayesema ameokoka, anatakiwa kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake (Bwana). Na namna ya kuwa hodari katika Bwana ni kwa kuvaa silaha zote za Mungu zilizoorodheshwa hapa. Yaani mtu ambaye hana silaha zote hizo hawezi kuwa hodari kwa maana vita itamshinda tu. Kwa hiyo ukosefu wa imani ni upungufu, ni udhaifu. Hivyo japo mtu anaweza kusema ameokoka lakini akawa hana imani huyo hawezi kuwa hodari. Na ndiyo sababu anaweza kupatwa na mishale ya mapepo.

  Wapo watu wengi ambao pamoja na kuwa wanasema wameokoka lakini wamevamiwa na kukaliwa na mapepo kwa sababu tu wamepungukiwa na moja ya silaha za Mungu ambazo mkristo anatakiwa kuwa nazo. Kuokoka kwa namna hii ni kuokoka ambako hakuwezi kuzaa matunda yoyote kiroho kwa kuwa mtu wa namna hawezi kumpinga shetani kwa kuwa ndani yake tayari kuna shetani.

  Ninachokiona mimi kuwa sababu ya tatizo hili ni kwamba watu wanapookoka si wengi wanaopata mafundisho ya msingi ya wokovu. Siku hizi mtu anaweza kuwa ameokoka lakini akawa hana kituo amacholelewa kiroho. Yaani hana mahali specific ambapo anatambulika na anahudhuria kwa ajili ya kula chakula sahihi cha kiroho. Wapo watu ambao alitolewa mapepo baada ya kuhuduria mkutano fulani wa injili na akaombewa sala ya toba lakini hakwenda mahali popote kujifunza neno la Mungu. Yeye husubiri hadi mkutano mwingine ndipo ahudhurie kwa ajili ya kuchukua mafundisho atakayoyakuta pale. Tatizo lililopo ni kuwa si mafundiso yote yanayotolewa kwenye mikutano na semina yanafaa kwa mkristo mchanga.

  Kutokupata mafundisho ya msingi kwa mtu aliyeamua kuokoka ni moja ya sababu inayofanya mtu huyo awe na vitu baadhi tu vinavyohitajika kwa mkristo lakini vingine asiwe navyo. Mfano mmoja ni kama hivi kwamba sasa hivi mafundiso ya kuvunja laana ni mengi mno. Sasa unaweza kuona mtu kaokokaa leo na leo hii hii anaanza kufundishwa namna ya kuvunja laana! Siamini kama huu ndio utaratibu sahihi wa kumfanya mtu alifahamu vema Neno.

  13. Je Mtu ambaye ni mjivuni( hawezi ku-appreciate kazi, vitu , mafanikio ya wengine ila yeye tu ndio bora na vya kwake tu ndio bora) mfano labda umejipinda ukajenga nyumba ya 80 Million anakuja kwako anaongea hivi aaah sio mbaya kwa kuanzia yaani hawezi kusema hongera… wakati yeye hana hiyo nyumba…Je mtu wa tabia ya namna hii kaokoka? na kama ameokoka je kazi ya msalabani haikutosha kuondoa hii tabia maana yote yamekuwa mapya?

  Jibu: Mtu mwenye tabia ya namna hii, hata kama akisema ameokoka, wokovu wake utakuwa ni wa maneno tu na wokovu usio wa matendo ni sawa na kutokuokoka. Majivuno, chuki, ubinafsi, kujiona kuwa ni bora kuliko wengine, kiburi na yanayofanana na hayo si tabia za mtu aliyeokoka. Mtu akishaokoka nafsi yake inabadilika; majivuno yanaondoka, chuki inatoweka, anaanza kuwatanguliza wengine na kumuona mwenzake kuwa bora kuliko yeye, kiburi kinaondoka halafu unyenyekezu unaingia. Hivi ndivyo mtu aliyeokoka anavyotakiwa kuwa.

  Kazi ya Yesu pale msalabani inatosha kabisa kubadilisha tabia ya mtu kutoka tabia mbaya kuwa nzuri. Na hapa ndipo ya kale huwa yamepita halafu yote yanakuwa mapya. Lakini ili yawe mapya yote ni pale mtu anapoamua kweli kweli kuwa ndani ya Kristo Yesu. Ndani ya Kristo hakuna chuki, hakuna majivuno, hakuna dharau, hakuna kiburi nk. Mtu anaposema ameokoka lakini ana dharau, ana chuki, ana kiburi… ni lazima kuwe na tatizo mahali fulani. Na tatizo hilo si kwa sababu kazi ya Yesu msalabani haikutosha bali ni kwa sababu mtu huyo hajaamu mzima mzima kukaa ndani ya Kristo. Yesu halazimishi na wala utakaso si lazima. Mtu ana hiari ya kupokea. Na kwa sababu ana hiari anaweza kuamua kuchagua nini achukuwe kutoka kwa kazi ya msalaba. Ndiyo maana, kwa mfano, kuna mtu anasema ameokoka lakini hayuko tayari kuacha dini yake. Na mwingine anasema ameokoka lakini hayuko tayari kuacha biashara yake ya magendo. Na mwingine anasema ameokoka lakini hayuko tayari kuacha mila za kabila lake. Katika hali ya namna hii siyo rahisi kupata ukamilifu unaotakiwa.

  Kuendelea kushikilia baadhi ya mambo hata baada ya mtu kuamua kuokoka ni lazima madhara ya mambo aliyoyang’ang’ania yajitokeze katika maeneo mengine ya maisha yake. Na haya yanaweza kujitokeza kama tabia ambazo si sahihi kwa mtu aliyeokoka, mfano wa hayo yaliyotajwa kwenye swali hili. Kuwepo kwa tabia namna hii kwa mtu siyo dalili njema. Hata kama ameokoka lakini wokovu wa namna hii ni ule ulio katika hatari ya kupotea.

  14. Je wapendwa ambao ni wasengenyaji Wameokoka? je hawawezi kuingiwa na pepo wachafu kwa kuwa waliongozwa sala za kuokoka?

  Jibu: Kama nilivyojibu katika maswali yaliyotangulia, usengenyaji si tabia ya mtu aliyeokoka. Usengenyaji ni uchonganishi kwa hiyo ni kazi ya shetani. Mtu aliyeokoka hapaswi kuwa msengenyaji. Mtu msenganyaji anaweza kuingiwa na mapepo kwa sababu ni mtumishi wa shetani.

  Sala za kuokoka hufanya kazi tu kama ziliongozwa inavyopasa na ziliongozwa na mtu anayestahili. Pamoja na kuongozwa sala za toba inavyopasa na na mtu anayestahili ni sharti mtu anayepokea au kukiri sala hizo akubali kupokea badiliko moyoni mwake. Mtu akisali sala za kuokoka kwa imani, mtu huyo hubadilika na moyo wake huwa unajiandaa kwa ajili ya kupokea mafundisho yanayopasa kwa watu waliooka. Hata hivyo watu wengi walisali sala za kuokoka lakini hazikuleta matunda yoyote moyoni, na wanaendelea na maisha yao kama zamani. Tatizo hapa zi kwamba sala za kuokoka hazifanyi kazi bali ni kwamba hawakusali sala hizo kwa imani na hawakuwa tayari kubadilika.

  Lakini pia katika mfano wa Mpanzi uliofafanuliwa na Bwana Yesu Marko 4:14-20 tunapata aina za watu hao ambao pamoja na kuipokea injili na kusali zala za kuokoka si wote husonga mbele. Wapo ambao hukubali kutubu lakini mizizi ya neno la Mungu ikakosekana ndani yao. Hawa hujikwaa kwa urahisi sana na hivyo kuachana na wokovu mapema. Mizizi ya neno la Mungu hupatika kwa kujifunza neno la Mungu. Wapo ambao huipokea injili na kukubali kuokoka lakini kwa sababu ya shughuli za dunia na udanganyifu wa mali [nilitoa mfano wa mtu kuokoka lakini akaendelea na biashara yake ya magendo] hudumaa na hivyo kuwa wakristo wasio zaa. Mkristo aliyedumaa ni rahisi kuingia katika tabia chafu ikiwa ni pamoja na usengenyaji. Na mwisho kuna wale ambao huisikia injili na wakakubali kutubu na kusali sala za kuokoka halafu wakawa watu wenye kuzaa matunda. Hawa ndio ambao husali zala ya toba kutoka ndani ya moyo, kwa imani, na kujitoa kikamilifu kwa Yesu. Kujitoa kikamilifu huko ndiko hufanya ile kazi ya Msalaba ikamilishe kazi yake moyoni mwao kwa kuwasafisha na kuondoa mabaya yote ya kale na kufanya wapya pamoja na kujengewa uwezo wa kinga ya kukabiliana na nguvu za giza.

  15. Je ni sawa kibiblia mpendwa kuharibu mimba au mtoto kufia tumboni? je hizi sio kazi za mapepo? je watu ambao wamewahi kuharibu mimba au watoto kufia tumboni Wameokoka?

  Jibu: Ninavyofahamu mimi hata kwa maisha ya kawaida, kwa watu ambao hawajaokoka, kuharibika kwa mimba ni tatizo. Si sawa.

  Tukija kwa upande wa kibiblia, kubaribika kwa mimba ni tatizo. Lakini ninahofahamu ziko sababu mbali mbali zinazoweza kusababisha kuharibika kwa mimba. [Kama tu nilivyojibu katika sababu za magonjwa nilipojibu swali la 5.] Sababu hizi zipo za kiroho na za kimwili. Za kiroho kwa sababu ziko nje ya uwezo wa kufikiri wa binaadamu na zile za kimwili kwa sababu ziko ndani ya uwezo wa akili ya binaadamu. Yaani anaweza akatafiti na kutambua na kuona ni kwa sababu fulani.

  Kama ilivyo katika magonjwa, si kila kuharibika kwa mimba ni kazi ya mapepo. Kuna mimba zinaharibika kwa sababu ya mjamzito kuugua mfano malaria au ungonjwa ambao chanzo na sababu zake zinafahamika kibinadamu, na kisha ugonjwa huo ukasababisha kuharibika kwa mimba. Kama mtu aliyeokoka anaweza kupata ugonjwa ambao hausababishwi na nguvu za giza vivyo hivyo anaweza kupata tatizo la kuharibika kwa mimba kunakosababishwa na ujinga – ukosefu wa elimu ya kibinaadamu juu ya chanzo hicho. Kwa hiyo nafikiri siyo sahihi kusema mtu ambaye anaharibu mimba ni lazima awe hajaokoka.

  Lakini kupo kuharibu mimba kunakosababishwa na kazi za ma mapepo. Lakini maelezo yake yanarudi kule kule kwamba ni lazima kuwe na uhalali fulani unaotumika kuharibu mimba hiyo. Uhalali huo unaweza kuwa kutokukulifahamu vizuri Neno la Mungu [ambapo hasara zake zimeshaelezewa] na/au maagano fulani katika ulimwengu wa roho ambayo hayajavunjwa. Kutokulifahamu vizuri neno la Mungu hupunguza nguvu za mtu huyo kukabiliana na nguvu za giza. Hii inaweza ikasababisha mapepo kutumia mwanya huo kuharibu uzao. Maagano yasiyovunja, kama ambavyo pia imeelezewa, huweka uhalali wa nguvu za giza kumtesa mtu. Kwa kuwa neno ni taa na mwangaza katika njia ya wokovu, mtu akijifunza neno kikamilifu neno hilo humulika na kudhihirisha kila kikwazo kilichofichika ili kiweze kuharibiwa. Kulifahamu neno kikamilifu ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuisikia sauti ya Roho mtakatifu ambaye ndiye director mkuu.

  Kwa hiyo akina mama ambao walishaharibu mimba au watoto wao kufia tumboni wanatakiwa kujichunguza. Kama ameokoka ni vema kuangalia sababu ya tatizo hilo. Kama sababu ni nguvu za giza ni lazima kuangalia ni uhalali gani uliotumika. Uhalali huo ukigundulika ni vema kuushughulikia mara moja maana si sawa kwa mtu aliyeokoka kuendelea kuwa na muunganiko wa nguvu za giza, kwa namna yoyoye ile. Yawezekana sababu ya mimba kuharibika ikawa iko ndani ya uwezo wa binaadamu. Wapo akina mama wengi ambao mimba ziliharibika kwa sababu ya labda kazi ngumu kupita kiwango kinachotakiwa. Sababu kama hizi zikijulikana ni vema kuepukwa.

  Hivi ndivyo nilivyoweza kujibu kwa sasa. Natumaini kujifunza zaidi mahali ambapo nitakuwa nimejibu isivyo sahihi.

  Kuna mahali ambapo ndugu Paul Holela ulitoa ufafanuzi wa swali la 3 na ukasema kwamba umeona halikujibiwa ulivyouliza. Ulieleza ambavyo linapasa kusomeka kuwa hivi:

  “Je wapendwa waliookoka…(SIO WAZINZI) hawazini, sio waongo…hawanywi pombe….wala hawaibi….maisha yao ni ale nini? avae nini? akae wapi? Nia zao zimemwelekea Kristo? mtazamo wao ni(maisha ya kawaida- natural realm) Je wameokoka?…..”

  Kwa swali hilo mimi nahitaji kusaidiwa kwa sababu sifahamu kama kuna tofauti kwamba mtu anayesema ameokoka akiiba iwe si kuiba kunakofanywa na mtu ambaye hajaokoka. Au mtu akasema ameokoka halafu akadanyanya na kudanganya huko kuwe tofauti na kwa mtu ambaye hajaokoka. Au mtu akasema ameokoka halafu akazini lakini akawa si mzinzi.

  Hapa nahitaji msaada.

 38. Ubarikiwe sana ndg yangu John Paul kwa kuwa kuna kitu kimepatikana toka kwenye majibu yangu.Sifa na utukufu ni kwa Mungu tu wala si kwa mwanadamu awaye yote.Natumaini tutaendelea kujibu na kujadili kwa undani maswali yaliyobakia yaliyoulizwa na ndg yetu Paul Holela.
  Amani ya Kristo iwe nasi sote.

 39. Ndugu Mwalemwa,
  Shalom,
  naomba nijibu swali lako…Mwanadamu si mwili,nafsi na roho, ila ni roho yenye nafsi inayoishi kwenye nyumba inayoitwa mwili…. kwa sababu umeuliza maandiko ngoja nikupe maandiko …. soma kwa makini ukitafakari… Mwanzo 1:26… Mwanzo 2:7… Yohana 4:24…1thes5:23…Heb 4:12……1pet 1:22….efeso 4:23..2cor 5:1,2,4…2Cor 4:16….1pet 3:3,4..Philippians 1:23,24… luka 16, Yoh5:24….Ndugu yangu Mwalemwa hayamaandiko yanaweza kukusaidia kuelewa ……
  Mtu sio mwili ni roho shida watu tuliokoka bado tupo mwilini karibu asilimia 100 ndo maana ni shida kuelewa vitu vya rohoni….
  Mwili wako ukiwa na tatizo haimaanishi wewe unatatizo ni sawa na nyumba yako unaishi ikiwa na panya haimanishi wewe unayekaa ndani ya hiyo nyumba una panya…. Inabidi uiambie nafsi yako ielewe wewe sio mwili ni roho na huu ukweli utakuwa halisi kwako…. amka asubui sema mimi ni roho na sio mwili…
  ndugu hagai nimeupenda ufafanuzi wako uliutoa kujibu swali la John Paul….
  Huko tuendapo nafikiri tutaongea kwa upana zaidi…
  TUSUBIRI MAJIBU YA MWASWALI YALIYOBAKI
  Mungu awatunze Tunaendelea kujifunza.

 40. Ndg Hagai Kinyau,

  Nashukuru kwa majibu ya maswali niliyouliza. Nilipouliza maswali hayo sikuwa na majibu mbadala bali nilitaka kufahamu kitu ambacho sikuwa nakifahamu kuhusiana na suala hilo.

  Ninaendelea kujifunza kwa kuwa tunazidi kupata sababu za kwa nini mtu anaweza kuwa ameokoka lakini akaendelea kuwa chini ya vifungo.

  Mungu azidi kututunza!

 41. Ndugu yangu John Paul, Bwana Yesu asifiwe.
  Kwanza nashukuru kwa nyongeza au ufafanuzi wako wa faida ya kujifunza kwa bidii neno la Mungu kwa mtu aliyeokoka inayompelekea kujua nguvu na uweza unaopatikana toka kwenye neno la Kristo(Mungu),Jina na Damu ya Yesu katika kumfanya aishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi na nguvu za giza.
  Sasa nianze kujibu maswali yako matatu kama ifuatavyo;
  1.Hakika uwezekano kwa rafiki yangu wa kukaa na kutafakari kuhusu mfarakano wao ulikuwepo kabisa.Shida inakuja pale ambapo wanadamu wameumbwa wakiwa na ulinganifu tofauti wa busara na hekima ya kutatua migogoro inayowakuta katika maisha yao.Hasira na mifarakano kwa watu wengine huondoa kabisa busara ya kutatua tatizo alilonalo mtu.Busara hiyo ikiondoka(hata kwa mtu aliyeokoka) hawezi tena kutafuta uongozi wa Roho Mtakatifu, ndipo sasa huanza kutegemea akili yake mwenyewe.Ukisoma Methali 10:12 utakutana na maneno ya Mungu yanayosema ‘Chuki huchochea faraka,lakini upendo husitiri mabaya yote’ Tena ukisoma Methali hiyo hiyo 17:14 inasema ‘Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji, kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza’ Soma pia 1Petro 4:8-upendo husitiri wingi wa dhambi.
  Lingine kubwa ni kule kutokuwa na neno la Mungu kwa wingi ndani ya mtu linalomwezesha kuwa na misuli ya imani ya kuweza kuachilia nguvu za Mungu kwa ajili ya jambo linalomsumbua.Msuli huu wa imani ndio humpelekea mtu kutaka signal ya Roho Mtakatifu kwa kila jambo ili kupata maarifa na ufunuo wa ki-Mungu wa kulitatua jambo hilo.Pia tukumbuke kuwa palipo na mtafaruku au mfarakano panamhuzunisha na hatimaye kumzimisha kabisa Roho Mtakatofu ndani ya mtu.Huyu rafiki yangu na mkewe walifikia kiwango hicho ndo sababu ya kushindwa kukaa chini na kutafakari kwa nini hali hiyo iliwapata.Lingine ni hili la wapendwa wengi kuwa na usiri sana kwa matatizo yanayowapata.Mpaka pale huyu rafiki yetu alipotushirikisha tatizo alilokuwa nalo, ndipo tulipoingia kwenye maombi kwa ajili ya kupata signal ya Roho Mtakatifu, vilevile tulianza kwa kumuuliza ni lini hasa tatizo hilo lilianza.
  Jambo lingine muhimu ni kwamba wapendwa wengi pamoja na kuokoka hawajui au hawana mafundisho thabiti juu ya umuhimu wa toba ya ardhi ya maeneo mbalimbali yanayogusa maisha yao ya kila siku kama vile ardhi ya nyumba wanazoishi(ziwe za kupanga au kujenga wenyewe),maeneo ya mahali wanapofanyia kazi ziwe za biashara au za kuajiriwa,maeneo ya wazazi wao n.k.
  2. Huyu rafiki yangu angekaa chini na kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu lazima angeweza kugundua tatizo walilonalo limetokana na nini kwa sababu Roho Mtakatifu hana upendeleo kwamba atusikie sisi asimsikie yeye kama angekuwa ametubu kwa kugombana na mke wake na kunyenyekea chini ya mkono wa Bwana kwa ajili ya kutaka uongozi wa Roho Mt. katika kutatua tatizo lake(1Petro 5:6-7).Kwa hiyo kama angefanya hivyo bila shaka yoyote angeweza kugundua shida iliyokuwa inawakabili, lakini yeye akaamua kuchukua njia ndefu kidogo ya kutushirikisha sisi na hatimaye Mungu akatatua tatizo lao maana kwake hakuna lisilowezekana.
  3.Wakati tukifanya toba ya ardhi ya eneo hilo tuliwashirikisha/walishiriki wote wawili yaani huyo rafiki yangu na mkewe na baada ya kuwaeleza kuwa shida iko kwenye mapepo yaliyopata uhalali wa kumiliki ardhi ya eneo hilo kutokana na mambo yaliyofanywa na mwenye nyumba hiyo au wapangaji waliowahi kukaa kwenye nyumba hiyo kabla yao, ndipo walipofunguka akili na kukiri kuwa tatizo lao lilianza mara baada ya kuhamia kwenye nyumba hiyo.Kwa hiyo hawakuwa wahanga(victim) tu wa tukio hilo na kutuangalia sisi tukifanya maombi ya toba ya eneo hilo, bali walishiriki kikamilifu baada ya kuelimishwa ni vipi mapepo mengine yanavyoweza kusambaratisha ndoa za watu.Mahali hapa hapatoshi kueleza kila kitu, lakini itoshe tu kusema kuwa wapendwa wanapaswa kufanya toba ya ardhi ya maeneo yao hata kama hawana mafarakanao kati yao.Ardhi inabeba mambo mengi sana ya kambi ya shetani yanayoweza kuachiliwa ili kuleta madhara mbalimbali kwa wanadamu.Nimejitahidi kueleza kadri nilivyoyaelewa maswali yako,kama ndivyo sivyo ulivyokuwa unataka yajibiwe, basi nifafanulie nitajitahidi kueleza zaidi, tupo kwa ajili ya kujifunza kwa utukufu wa Mungu Baba.
  Mbarikiwe na Bwana Yesu.

 42. Bwana Yesu asifiwe

  Tusome pia Matendo Sura ya nane hasa Mdo 8: 23. Mtu anaweza kuamini na bado akawa kwenye kifungo. Hii ni habari ya |Simon Mchawi.

  KWa upande wangu naona ni ngumu kidogo mtu kufikia hatua ya kuongozwa na Roho kwa kila jambo lakini its possible. Sasa kwa mtu mchanga kabisa kwenye wokovu na labda bado yuko kwenye vifungo ni bora aombewe kama vile Simon pale Mdo 8:23.
  Tunajifunza.

 43. Ndugu Haggai Kinyau,

  Wakati tukiendelea kujadili na kujibu kuhusu maswali yaliyoulizwa na ndg Paul Holela, naomba kuuliza jambo kuhusiana na mfano ulioutoa wa rafiki yako aliyehamia kwenye nyumba iliyosababisha mafarakano.

  Kabla ya kuuliza nina machache yafuatayo:

  Katika jibu lako kwa swali la 16 umeandika jinsi ilivyo muhimu kwa mtu aliyeokoka kuendelea kujifunza kwa bidii na kujua mamlaka yaliyoko ndani ya neno la Kristo na uweza wa damu/jina la Yesu katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu. Kwa maneno mengine, ya kwangu, ni kwamba mtu akiamua kuokoka halafu asiwe na bidii katika kujifunza Neno la Mungu kwa ukamilifu hawezi kuwa na maisha ya ushindi. Kwa hiyo kukosa ufahamu wa kutosha wa Neno la Mungu, ikiwa ni pamoja na mamlaka yaliyoko ndani ya Kristo na uweza wa damu/jina la Yesu, husababisha udhaifu wa kiroho na kunaweza kufungua milango kwa mapepo kuweza kumvamia na/au kumfunga mtu. Na hii ndiyo sababu ya msingi inayoweza kumfanya mtu aliyeokoka aendelea kukaa kwenye vifungo – Kutokulifahamu vizuri Neno la Mungu na Nguvu ya Mamlaka ya Jina na Damu ya Yesu Kristo! Mtu mwenye bidii katika Mungu, kwa maombi na kujifunza Neno, huyu huwa amejaa nguvu za Mungu na hawezi kuathiriwa na mashambulizi kutoka kwa nguvu za giza!, yaani hawezi kukaa chini ya vifungo. Na ni bidii hii ndiyo itamfanya mtu aliyeokoka aingine mbinguni.

  Maswali yangu ni haya yafuatayo:

  -Je, kulikuwa na uwezekano wowote kwa rafiki yako kukaa chini na kutafakari kwa nini walipatwa na mfarakano huo?

  -Je, huyo rafiki angekaa chini na kuomba kwa uongozi wa Roho mtakatifu, asingeweza yeye mwenyewe kugundua sababu ya hali hiyo? (ili aondoe uhalali wa mapepo kutawala eneno hilo)

  -Wakati mkifanya toba ya ardhi ya eneo hilo na yeye mlimshirikisha? au yeye alikaa tu kama victim akisubiri kusaidiwa?

  …..mjadala unaendelea!

 44. Hivi mafundisho ya kwamba mtu ni mwili nafsi na Roho yapo wapi katika maandiko?

 45. Shalom, Ndugu yangu kinyau nashukuru sana kwa majibu uliyotoa kwa swali la kumi(10) Mungu akubariki naamini wasomaji wanajifunza na kupata msaada…. pia umegusia swala la ukombozi wa ardhi… ambao mliufanya kwa huyo rafiki yako niliwaitaka kuongelea hili siku moja ila nikaona muda bado…. nilichoelewa hapo kwenye huo mfano ni kwamba ile ardhi ilikuwa inamilikiwa na mapepo kihalali kwa hiyo yeyote aliyeokoka na asiyeokoka wote walipata shida walipokaa juu ya hiyo ardhi…mpaka mlipofanya toba… mkaondoa uhalali wa mapepo…. halafu mkayafukuza pakawa shwali JINA LA YESU LITUKUZWE…tutaongelea hili pia baadae… NGOJA TUJIBIWE MASWALI YALIYOBAKIA..
  Mungu awatunze Wapendwa.

 46. Wapendwa wote,Bwana Yesu asifiwe.
  Naomba tuendelee kujibu au kujadili yale maswali 16 ya Ndg yetu Mhandisi Paul Holela, na leo naomba niendelee kulijibu swali la kumi lililouliza;
  Mtu anayedai ameokoka halafu wanagombana na mumewe(mkewe) na wasiongee siku tatu wakiwa kitanda kimoja;je mtu kama huyo ameokoka? Je hawezi kuingiwa na mapepo?
  Awali ya yote niseme kwamba ni kweli inaweza ikatokea mume na mke waliookoka kutokuelewana kati yao wawili kwa sababu mbalimbali.Na huku kutokuelewana kuna level tofauti tofauti, lakini kutokuelewana huko kukifikia level ya kugombana yaani ugomvi unaoleta kutokuongea kwa siku kadhaa huku wanalala kitanda kimoja, hapo ndipo watu tutakapoanza kujiuliza huo wokovu wao una maana kweli kwenye maisha yao ya ndoa? Nasema hivyo kwa sababu tija ya wokovu wao itadhihirika pale wote wawili watakapokuwa tayari kupendana kuliko wanavyojipenda wao binafsi.Wokovu unaachilia au unatengeneza tabia ya upendo ambao haujali umekosewa au umekosea lazima uwe tayari kusamehe na kusahau.
  Biblia kwenye Efeso 4:26-27 inasema’Mkikasirika,msitende dhambi,wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika,wala msimpe ibilisi nafasi'(Nukuu toka Biblia ya Neno biblia Takatifu).Kwenye biblia ya Bible societies of Tanzania and Kenya toleo la 1997, maneno ya vifungu hivyo yanasomeka hivi ‘Mwe na hasira, ila msitende dhambi;jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka, wala msimpe ibilisi nafasi’ Maneno hayo yanatuelekeza kumaliza tofauti zetu(ziwe za kutokuelewana kama mke na mume au jamii ya waliokoka n.k)kwa upole bila magomvi/kugombana maana ugomvi huleta machungu moyoni na hatimaye ibilisi hupata nafasi ya kuingiza mambo yake.Mtu akiweka uchungu ndani ya moyo wake kwa muda mrefu,panatoa upenyo kwa shetani kuwasha moto zaidi.
  Ukisoma Zaburi 4:4 neno la Mungu linasema ‘Katika hasira yako usitende dhambi,mkiwa vitandani mwenu mtulie kimya mkitafakari mioyoni mwenu’, kwenye biblia zingine neno hasira limeandikwa kama hofu.Je kwa nini biblia inasisitiza kutokutenda dhambi pindi upatwapo na hasira? Kwa maneno mengine ni kwamba kila mtu(hata aliyeokoka)kuna wakati anaweza kupatwa na hasira,lakini wewe uliyeokoka hata ukipatwa na hasira isikupeleke katika kugombana kiasi cha kukaa siku tatu na mwenzi wako bila kuongea wala kupeana jambo.Mtu aliyeokoka siku zote akipatwa na hasira jambo la kwanza la kufanya ni kujitiisha chini ya uwepo wa Mungu na kutubu kwa kuingiwa na hasira na kumuomba Mungu akupe hekima ya kutatua hilo lililoletekeza ukapata hiyo hasira.Hasira isiyodhibitiwa ni mlango wa ibilisi kuleta mafarakano mengi ndani ya familia na jamii kwa ujumla. Kama ni mke au mume au mtu yeyote amesababisha ukakasirika, basi toba yako ianze kwa kumsamehe(Mathayo 6:14-15) huyo mtu ili upate uhalali wa wewe kupata hekima na maongozi ya Roho Mtakatifu katika kufikia muafaka wa jambo hilo.
  Kolosai 3:12-14 inasema “Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi(mliookoka)mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa huruma, utu wema,unyenyekevu,upole na uvumilivu.Vumilieni na kusameheana.Mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake,sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi.Zaidi ya maadili haya yote jivikeni UPENDO ambao ndio unafunga kila kitu pamoja katika amani kamilifu”.Unaweza kuona jinsi wokovu wa kweli unavyoachilia ndani ya mtu vitu hivi:utakatifu,moyo wa huruma,utu wema,unyenyekevu, upole, uvumilivu,kusamehe hata kama hujaombwa msamaha; na haya yote yapo ndani ya neno moja tu-UPENDO.Kama mtu ameokoka halafu anafikia kugombana na mwenziwe na kukaa siku tatu hawaongei,basi wokovu wake unatia mashaka.Inawezekana yuko hivyo kwa sababu neno la Mungu halijakaa kwa wingi ndani yake(Kolosai 3:16) kiasi cha kutokujua kweli ya neno la Mungu.
  Kimsingi ugomvi si tabia ya wana wa nuru yaani watu waliookoka, kwa hiyo kama mtu anagombana na kufikia hatua ya kulala kitanda kimoja na mume au mke bila kumaliza ugomvi huo(bila kusameheana)kwangu mimi watu hao hawajaokoka na ni rahisi sana kwao kutoa mwanya kwa mapepo kuwaingia.Ugomvi na mafarakano ni tabia ya shetani maana hilo ndilo kusudi lake toka awali.Kwa maana hiyo basi kama mtu ameokoka na asibadilike tabia ya ugomvi n.k anahitajika kujichunguza upya kwa kuwa tabia hiyo haimpendezi Mungu wala jumuiya ya waliookoka(ndugu katika kristo-kanisa)na kwa tabia hiyo anafungua mlango wa nguvu za giza kuingia kwake.Hivyo kile kifungu ulichosema je hawezi kuingiwa na mapepo? Jibu ni rahisi kabisa kuwa mtu wa namna hiyo anaweza ingiwa na mapepo maana kuna mapepo ya aina nyingi, mojawapo ni mapepo yaletayo mafarakanao/ugomvi.
  Ni muhimu sana mtu anapookoka kuendelea kujifunza kwa bidii na kujua mamlaka yaliyoko ndani ya neno la Kristo na uweza wa damu/jina la Yesu katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu.Hii inanikumbusha kisa kimoja cha rafiki yetu mmoja ambaye kweli walikuwa wameokoka yeye na mke wake.Kama tunavyojua huku mijini tunaishi nyumba za kupanga, huyu rafiki yangu na familia yake walihamia kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa na shida kubwa ya mapepo ambayo yalikuwa yanaleta ugomvi/kutokuelewana kwa kila mwenye ndoa aliyekuwa anahamia(anaishi) kwenye nyumba hiyo.Huyu rafiki yangu kabla ya kuhamia kwenye nyumba hiyo walikuwa na maisha mazuri ya maelewano ya hali ya juu sana na mkewe, lakini mara baada ya kingia kwenye nyumba hiyo palizuka kutokuelewana kwa kiwango cha kutisha.Vitu vidogo tu vilizusha ugomvi wa ajabu kati yao.Kwa kifupi mpaka wapendwa tulipokaa na kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya tatizo la wapendwa wale ndipo tulipogundua kuwa kwenye ardhi ya eneo hilo yapo mapepo ya kufarakanisha ndoa.Kwa kifupi mpaka tulipofanya toba ya ardhi ya eneo hilo, ndipo amani na furaha ya ndoa ndani ya familia hiyo ikarejea tena.
  Nawatakieni baraka za Bwana.

 47. Shalom,
  Nashukuru ndugu zangu hagai na john kwa kujibu mpaka swali la tisa, Mungu awabariki sana sana ….
  Swali la 3 halikueleweka vizuri ilipasa lisomeke …3. Je wapendwa waliookoka…(SIO WAZINZI) hawazini, sio waongo…hawanywi pombe….wala hawaibi….maisha yao ni ale nini? avae nini? akae wapi? Nia zao zimemwelekea Kristo? mtazamo wao ni(maisha ya kawaida- natural realm) Je wameokoka?….. Naona halikujibiwa nilivyouliza….
  Mpendwa Hagai Swalim la 9.Kama magonjwa si haki yetu ktk Kristo Yesu….Wanaoumwa hawajaokoka?…. Hapa nilimaanisha wanaoumwa huku wameokoka…..
  Swali la 7. …..Mtu ambaye anarekebishwa(Na MUNGU..HUYU MTU NI MLOKOLE Tayari ) mfano kutoka kwenye tabia labda ya majivuno na anakubali anaiacha… kabla ya hapo alikuwa hakuokoka? maana majivuno ni kuwa nje ya upendo kwa mujibu wa 1kor13:4-7…… Kwa jinsi ulivyolijilibu naona kama ulielewa!

  Tusubiri majibu ya Swali la 10-16 ili tuendelee kujifunza……
  Mungu awabariki Wasomaji wote….

 48. Shalom wapendwa wote.
  Kutokana na majukumu ya kazi, imepita muda sasa bila kuchangia chochote hasa mada hii ambayo imekuwa nzuri sana na imetoa uwanja mpana sana wa majadiliano.Nianze na kuwashukuru wapendwa wote waliochangia humu kuanzia ule mchango wa Furaha wa tarehe 10/6/10.Mungu aendelee kututia nguvu na kutupa ufahamu zaidi ili tuendelee kushirikishana neema hii kubwa ya wokovu.

  Kuna kitu kimoja ambacho napenda kuanza nacho leo kwamba wapendwa wengi wanaishi maisha ya kumwogopa zaidi shetani kuliko Mungu, hivyo wamefunikwa na hofu ya kipepo(shetani) badala ya hofu ya Mungu inayomjengea mtu tabia(character) ya kutokutenda dhambi hata kama yupo kwenye mazingira ya watenda dhambi.Ukisoma Methali 8:13 inasema kumcha Bwana ni kuchukia uovu(neno kumcha Bwana kwenye biblia zilizoandikwa kwa lugha ya kiingereza linasema fear of the Lord-kwa kiswahili naweza kusema hofu ya Mungu sio kwenda kanisani). Pia Zab.130:1-4 inasema Mungu anasamehe dhambi ili aogopwe, maana yake ili aachilie roho ya hofu kwa watu wake nayo hofu ikiwafunika iwajengee tabia ya kumheshimu na kumuogopa Mungu kiasi cha kutokutenda dhambi.

  Kuhusu maswali ya ndg yetu Paul Holela, John Paul ameyajibu vizuri sana toka swali la kwanza mpaka la nne. Nami nataka leo niendelee na swali la tano mpaka hapo nitakapoishia. Kabla sijaanza kujibu swali la tano naomba niongezee maelezo kidogo tu kwenye swali la tatu lililouliza, Je waliokoka hawazini…hawasemi uongo…hawanywi pombe wala hawaibi?..n.k. Galatia 5:19-20 na 1Kor 6:9-10 na sehemu zingine kwenye biblia zinaeleza wazi kuwa watendao mambo hayo hawataurithi ufalme wa Mungu. Kama kuna mtu ni mlevi,mwongo, mzinzi n.k na bado anajiita ameokoka, basi mtu huyo ameikataa KWELI ambayo ilitakiwa imuweke mbali na vitu hivyo, na kwa kuikataa hiyo kweli maana yake amelikataa neno la Mungu ambalo ni Yesu mwenyewe(Yoh.1:1-5), hivyo mtu huyo moja kwa moja hajaokolewa kwa sababu hajaliamini jina pekee la Mwana wa Mungu. Inawezekana kabisa analitaja jina hilo lakini amesahau biblia inasema kwenye 2 Timotheo 2:19b kuwa kila alitajaye jina la Bwana na auche uovu. Pia 2 Timotheo 3:16-17 kila andiko lenye pumzi ya Mungu linamuadibisha mtu katika haki ili mtu huyo awe kamili apate kutenda kila tendo jema. Wokovu ni mfumo wa maisha ndani ya Yesu Kristo unaokataa uovu wote, hivyo yeyote anaishi kinyume cha hayo ni wa ufalme mwingine kwa sababu katika mifumo hii miwili yaani giza na nuru hakuna free zone inayoweza kumfanya mtu akakaa katikati ya mifumo hii. Huyo anayejiita ameokoka halafu anazini n.k HAJAOKOKA anatakiwa aamue kama ilivyoandikwa kwenye Yoshua 24:14-15. Huwezi kuitumikia miungu ya uzinzi,ulevi,fitina uchawi n.k halafu ujiite au watu wakuite mwongofu(umeokoka).

  SWALI LA TANO.Je ni sawa/haki kulingana na neno la Mungu watu waliokoka kuwa na magonjwa(kwa chanzo chochote kile-demonic/natural).

  Kimsingi mwanadamu hakuumbwa na magonjwa au hakuumbwa ili aumwe, aliumbwa ili aishi milele bila magonjwa wala kufa. Magonjwa ni matokeo(results,products) ya mwanadamu kumkataa Mungu na kuambatana na shetani kama mtawala wake. Mwanzo 3:17-19, utaoona jinsi Mungu alivyotoa adhabu kwa kosa la mwanadamu. ‘…..michongoma na miiba itakuzalia’ hapa mimi natafsiri kwamba mwanadamu aliumbwa kwa udongo hivyo mwili wake ni udongo na michongoma na miiba itaota juu yake yaani magonjwa na taabu mbalimbali. Hii haikuwa michongama ‘miti’. Kumbuka michongoma hii haijatokana na Mungu bali na shetani, hivyo hili neno natural linanipa ugumu kidogo kulitumia kwa maana ya kwamba Mungu hakuumba magonjwa.
  Kwa mantiki hiyo basi si haki wala sawa kwa mtu aliyeokoka, anayelindwa na nguvu za Mungu kuwa na magonjwa. Hii ni sawa na kusema kuwa ni haki kwa mtu aliyokoka kwenda jehenamu. Nasema hivyo kwa sababu biblia inasema wokovu hutengeneza ukuta wa ulinzi katika ulimwengu wa roho(Isaya 60:18). Shetani mwenyewe analijua hili kwamba mtu anapookoka, yeye mwenyewe ana ulinzi wa ukigo(ukuta) pamoja na mali zake. Hebu soma Ayubu 1:7-10 inasema hivi hasa mstari wa 10…..wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake na vitu vyote alivyonavyo? Kazi za mikono yake umezibarikia,nayo mali yake imeongezeka ktk nchi’. Hapa ina maana tayari shetani alijaribu kwa uwezo wake wote wa kumharibu Ayubu(kwa magonjwa au kwa namna yoyote ile), lakini alishindwa kwa sababu ya ulinzi wa Mungu.

  Ukweli huu unadhihirishwa hata leo hii tunaposikia shuhuda mbalimbali za watu waliokuwa wachawi wanaposema jinsi ambavyo hukutana na ukuta wa moto wanapojaribu kwenda kuroga au kuwanga kwenye nyumba za watu waliokoka kweli. Kwa habari ya Ayubu wote tunajua vyema yaliyomkuta baada ya Mungu kutoa ule ukigo uliokuwa unamlinda, jinsi miiba na michongoma ilivyoota juu ya mwili wake mpaka kwenye mali yake na watoto pia. Siku zote mtu akiwa upande wa shetani lazima tu ipo michongoma imeota juu yake hata kama sisi wanadamu wenzake hatuioni,lazima mhusika anaiona. Shetani kazi yake ni kuharibu na kuua hana uzima ndani yake.Labda la kukumbuka tu ni kwamba magonjwa yote anayoruhusu Mungu kwa ajili ya kujipatia utukufu huwa hayamuui mtu e.g. Ayubu, Paulo,Timotheo n.k

  SWALI LA SITA. Je asili ya magonjwa ni nguvu za giza direct or indirect? Kwa mtiririko wa maswali haya nafikiri nitakuwa pia nimejibu swali hili kutoka kwenye majibu ya swali la tano. Wapendwa tusiwe na mtizamo au uelewa finyu wa hili neno nguvu za giza. Imeonekana kwa wengi wanaposikia nguvu za giza,mawazo yao yote yanaenda kwenye mapepo,uchawi,majini na vitu kama hivyo. Nguvu za giza ni roho zote chafu zilizo kinyume na Mungu zinazoachiliwa na shetani toka kwenye ufalme wake kuja kwenye ulimwengu wa kimwili. Kwa hiyo kwangu mimi nguvu za giza ni jumla ya mambo yote yanayoachiliwa na shetani kuja duniani, iwe ni roho ya uzinzi, roho ya ulevi, roho ya kumtaka mwanamume au mwanamke mwenzio kwa nia ya kutenda tendo la ndoa(ushoga na usagaji), roho ya chuki, roho ya mauti(mauaji), roho ya kujipenda wewe zaidi ya jirani yako, roho ya kutosamehe na kusahau n.k. It is an endless list. Yote hayo na mengine mengi sana sana ni NGUVU ZA GIZA. Kwa swali hilo la sita kwa mfano, mtu ametawaliwa na roho ya ulevi, kanywa gongo mpaka ini lake likashindwa kufanya kazi akapata ugonjwa uitwao cirrhosis, je asili ya ugonjwa huo utaita nini? Definitely ni nguvu za giza zilizo direct kwa huyo mtu. Lakini mtu huyohuyo ameshikwa na liroho la ulevi anatumia hela zake zote kwenye huo ulevi kiasi kwamba ameshindwa hata kutunza familia yake na watoto wameshikwa na magonjwa ya utapia mlo kwa kukosa lishe bora, basi asili ya ugonjwa kwa hao watoto ni nguvu za giza ingawa ni indirectly. Ndg yangu John Paul na wengine pia wamejibu vizuri tu juu ya asili ya magonjwa.

  SWALI LA SABA. Kwangu mimi swali la saba halieleweki labda lifafanuliwe maana umesema akiaacha majivuno, je kabla ya hapo alikuwa hajaokoka?. Huyu unayemzungumzia ni kwamba alikuwa ameokoka lakini akaendeleza tabia ya majivuno au alikuwa hajaokoka na pia alikuwa na tabia ya majivuno lakini ameacha majivuno baada ya kuhubiriwa habari njema ya wokovu nayo ikamchoma akaona majivuno si tabia ya watu waliokoka, naye sasa akaamua kuacha majivuno.

  Kama ulivyosema kuwa majivuno ni kuwa nje ya upendo, hivyo sitegemei mpendwa aliyeokoka kweli kweli akaendeleza tabia ya majivuno. Kama ambavyo nimekuwa nikisema siku zote kuwa wokovu wa kweli siku zote huachilia au hutengeneza au hubadilisha tabia mbaya ya mtu na kumuwezesha mtu kuwa na tabia nzuri zinazoendana na wokovu huo. Ufalme wa nuru lazima uachilie nuru na ufalme wa giza lazima uachilie giza. Hivyo hivyo hata kwa mtu aliyeokoka hatutegemei awe na tabia za watu wasiokoka ambao kwao mtu akifurahi anaangusha tusi akichukia anaangusha tusi hilohilo. Aliyeokoka na asiyeokoka wako kwenye utawala(falme)tofauti, lazima tabia zao ziwe tofauti pia.

  SWALI LA NANE. Kama magonjwa ni haki yetu, kazi ya Kristo ni bure? Swali hili ni zuri sana. Kwa vile mimi toka awali nimeshasema kwamba magonjwa si haki yetu, basi Yesu Kristo kupigwa kwake kwa ajili yetu haikuwa na haitakuwa kazi bure kwake yeye amwaminiye, lakini itakuwa kazi bure kwa wale wote wanaoendelea kumkataa na kumkumbatia shetani kwa matendo na mienendo yao.
  Kwa Yesu kupigwa pale msalabani, alijua fika(hakika) kuwa watu wake wamebebeshwa magonjwa na mwovu shetani(sio haki yetu kuchukua mizigo hiyo), hivyo alikubali kupigwa sana ili tupate haki ya kupona(Isaya 53:4-5).kwa maana hiyo Yesu alipigwa ili sisi tupate haki ya kutokuwa na magonjwa(naitafsiri haki kama uhalali wa…). Lakini haki hiyo tutaipata tu pale tutakapoamua wenyewe, Yeye(Yesu) awe mtawala wa maisha. 1 Petro 2:24 inasema hivi ‘Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti,tukiwa wafu kwa MAMBO ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya HAKI, na kwa kupigwa kwake mliponywa’ Je umejiuliza mambo ya dhambi ni mambo gani hayo? magonjwa n.k, na mambo ya haki je? ni uzima, kutokuwa na magonjwa ambalo ndilo lilikuwa kusudi la Mungu toka awali na kusudi hilo halijabadilika mpaka leo mtu akimkubali na kumwamini Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yake.

  SWALI LA TISA. Kama magonjwa si haki yetu katika Kristo Yesu wanaoumwa hawajaokoka?. Pamoja na swali hili kuwa too general, lakini naomba nijaribu kulijibu kama ifuatvyo. Wapo wanaoumwa kwa sababu hawajaokoka; wanaumwa kutokana na tabia na mienendo yao ya kimaisha kwamba bado mfalme wao yaani shetani anaachilia roho za ulevi,uzinzi, uasherati n.k. Nafikiri nimeeleza kwa kirefu hapo juu. Wapo wengine wamesababishiwa magonjwa pamoja na kwamba wao wameokoka, kwa mfano mtu aliyeokoka anapanda basi linaloendeshwa na dereva mlevi au mzembe asiyefuata maadili na sheria za uendeshaji magari na kisha basi hilo likapata ajali na mpendwa huyu akavunjika mguu au mkono au akapata majeraha mbalimbali kwenye mwili wake, huu ni ugonjwa uliosababishwa na mtu ambaye hajaokoka kwa mtu aliyeokoka. kumbuka sio kwamba Mungu hawezi kumtoa mpendwa huyu salama kwenye ajali hiyo.

  Kwa kifupi ni kwamba sio wote wanaoumwa hawajaokoka na tena sio wote ambao hawaumwi wameokoka. Siku zote huwa namwangalia Ayubu(wa kwenye biblia) kwa jicho la kutaka kujua hata yale ambayo yamekaa nyuma ya pazia. Kwa hiyo siku zote napenda sana kumtolea mfano kwa nia ya kuelewa zaidi. Biblia inasema Mungu alimuona Ayubu kama mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye hofu ya Mungu na anayeepukana na uovu kuliko watu wote duniani. Lakini bado aliumwa sana na kupata mateso mengi si kwa sababu alikuwa hajaokoka/ongoka(hajamtii Mungu), bali ulikuwa ni mpango kamili wa Mungu kumuonyesha shetani kwamba mtu akiwa na uchaji(hofu ya Mungu), hata akipata mateso na majaribu(magonjwa, watoto wakifa n.k) bado hawezi kuacha huo utaji/uchaji/hofu ya Mungu kwa sababu kuwa na huo uchaji unamwezesha mtu asitende dhambi, asimkosee Mungu. Kwa hiyo wakati mwingine watu waliokoka hupatwa na magonjwa kwa ajili ya kupima imani zao kwa Mungu, na wakati mwingine wasiokoka wanapatwa na magonjwa ili kuwaadabisha na hatimaye wamjue Mungu wa kweli kama ambavyo Paulo wakati huo akiitwa Sauli alipopata upofu ili awe chombo safi cha kazi ya Bwana.

  Kwa leo naomba niishie hapa na Mungu wa amani atubariki sisi sote.
  Amen.

 49. Mpendwa Eng Paul Holela,

  Ninakushukuru sana kwa ushauri wako kuhusu namna ifaayo kwa ajili ya kunisaidia kujifunza. Nitandelea kuifanyia kazi.

  Namshukuru Mungu leo nimepataka nafasi ya kuendelea kujibu yale maswali. Lakini mimi pia natazamia kujifunza toka kwa majibu ya mtu mwingine.

  5. Kabla sijajibu kwamba ni sawa/hali au si sawa/halali kwa mtu aliyeokoka kuwa na magonjwa ninaandika kwanza yafuatayo:

  Katika michango iliyotangulia limeshazungumzwa sana kwamba si kila ugonjwa husababishwa na nguvu za giza. Na ili kufahamu kwamba unatokana au hautokani na nguvu za giza ni lazima kuwe na signal ya Roho mtakatifu katika baadhi ya magonjwa na kwa mengine huwa wazi kutokana na ugonjwa ulivyoanza.

  Si kila ugonjwa ni kifungo. Kwa maana ninayofahamu mimi kifungo ni kitu kilichomfunga mtu, yaani ni mateka. Hawezi kutoka katika kilichokufunga hadi kimefunguliwa. Na kifungo kinapofunguka hakiwezi kurudi tena hadi hapo itokee sababu au uhalali wa kukifanya kifungo hicho kirudi. Kwa hiyo ugonjwa ambao umesababishwa na kifungo unapomtoka mtu hauwezi kumrudia tena kama mtu huyo atatambuwa kwamba ameshafunguliwa, yuko huru. Na katika uhuru alioupokea lazima atambuwe kanuni za kuenenda na kujilinda asije akauharibu uhuru huo na kujikuta amerudi tena katika makosa yatakayomsababishwa kufungwa.

  Mfungwa anapokuwa amefunguliwa kutoka magereza ni lazima aishi kama inavyotakiwa kuishi uraiani. Kama hatatambuwa hilo na kuanza kuishi pasipo kufuata mwenendo sahihi ni lazima atatiwa hatiani na kurudishwa gerezani tena, kwenye kifungo!

  Mtu anapokuwa amefunguliwa (delivered) kutoka katika ugonjwa uliokuwa umesababishwa na vifungo vya guvu za giza ni lazima sasa aishi jinsi inavyowapasa kuishi watu walio huru. Na namna bora zaidi ya kumfanya atambuwe ni kwa kujifunza na kulifuata Neno la Mungu. Bwana Yesu alisema kwamba pepo anapomtoka mtu, tunaweza kusema pepo aliyekuwa amemfunga mtu kwa ugonjwa, huzunguka zunguka na akikosa mahali pengine pa kwenda hurudi tena na kuangalia mahali alipokuwa. Akikuta pako safi na hakuna kizuizi huenda akakusanya pepo wengine saba ambao ni wabaya kuliko yeye (pepo) kisha huja kuingia ndani ya mtu huyo. Na hali yake yamwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Mathayo 12:43-45

  Wako watu wengi ambao wamekuwa wakifanyiwa maombezi ya ukombozi lakini kwa sababu hawakupata misingi ya Neno la Mungu deliverance kwao hudumu kwa muda mfupi tu na kisha yale matatizo hurudi tena, na mara nyingi kwa nguvu zaidi. Mtu akifanyiwa maombezi ya kufunguliwa ni muhimu kujifunza Neno la Mungu ambalo ndilo litakuwa ulinzi wake na pepo mwenye kutekeleza kile kifungo anaporudi hawezi kuingia kwa sababu Neno liko ndani.

  Tumeshakubaliana kwamba si kila ugonjwa husababishwa na nguvu za giza. Ninavyofahamu mimi Magonjwa husababishwa na vitu vingi:

  i). Yapo ambayo husababishwa na nguvu kutoka katika ulimwengu wa roho. Magonjwa haya huwa hayaonekani sababu yake hata kama mgonjwa atapimwa katika maabara bora kabisa duniani. Hapa ndipo yalipo magonjwa mengi ya kifungo ambako mtu anahitaji kufundishwa Neno la Mungu na/au kufanyiwa maombezi ya nguvu ili kupata uponyaji.Katika kundi hili yapo pia yanayoweza kupimwa maabara yakaonekana sababu yake lakini pamoja na kutumia dawa zinazofahamika kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo mgonjwa huwa hapati kupona.

  ii). Yapo ambayo husababishwa na hali ya kimazingira. Mtu anaweza kuugua ugonjwa fulani kwa sababu tu hajazingatia kanuni za afya bora au kwa sababu ametumia kitu fulani kinyume na matumizi halali ya kitu hicho. Natumaini kila mtu anafahamu kuhusu aina hii ya magonjwa. Magonjwa haya hutambulika na vipimo vya maabara na matibabu yake yako ndani ya uwezo wa kibinadamu kutokana na elimu na maarifa ambayo Mungu ametujalia kuwa nayo. Na hata kama hayatibiki lakini angalau basi mtu anaweza kupewa elimu au chanjo/kinga ili ambaye hajayapata asije akapata.

  Niliandika kwamba si kila ugonjwa ni kifungo. Kutokana na tafsiri ya ‘kifungo’ niliyoandika sidhani kama ni sahihi mfano mtu akiamka anaumwa na tumbo lakini ikifika jioni ameshapona tukisema alikuwa katika kifungo cha nguvu za giza!

  Magonjwa yako kwa kusudi mbali mbali:

  i).Yapo magonjwa mbayo ni mashambulizi toka kwa shetani, yaani vita. Zaburi 34:19

  ii).Yapo ambayo ni vifungo. Haya hukusudiwa kumfunga mtu kwa muda mrefu na kama hawezi kufunguka yawezekana hadi akafika mwisho wa uhai wake akiwa bado anasumbuliwa na ugonjwa huo. Luka 13:11

  iii).Yapo magonjwa ambayo ni majaribu, yaliyoruhusiwa na Mungu, ili kuwa mtihani. Ayubu 2:4-7

  iv).Yapo magonjwa ambayo ni adhabu toka kwa Mungu. Matendo 12:22-23.

  v).Yapo magonjwa ambayo ni speed governor, kwa ajili ya kumuadabisha mtu ili akae katika kusudi aliloitiwa na Mungu. 2Korintho 12:7,

  vi).Yapo magonjwa ambayo ni madhara tu ya makosa ya kibinaadamu. Muhubiri 7:29. Haya huwa hayana kusudi lolote. Ni mavuno tu ya kile alichopanda mtu. Mfano mtu anapopata cancer kwa sababu ya kuvuta tumbaku! Hapa yapo pia magonjwa ya kuzaliwa nayo kwa sababu, mfano, mama hakupata lishe sahihi wakati wa ujauzito.

  Kwa hiyo katika mchanganuo wa sababu na kusudi la magonjwa ambao nimeuandika hapo juu tunaweza kuona kwamba yapo magonjwa ambayo kwa kweli si haki na wala si sawa kumpata mtu ambaye ameokoka; mtu anayesema Yesu yuko ndani yake; mtu anayesema yeye ni mshindi na zaidi ya kushinda – na maneno mengine ambayo humaanisha mtu akimpata Yesu amekuwa salama. Lakini kwa upande mwingine tunaweza kuona kwamba ni haki/sawa kwa mtu aliyeokoka kupatwa na ugonjwa. Kinachotakiwa kufahamika hapa ni nini sababu na nini kusudi la ugonjwa huo.

  Kwa mtu aliyeokoka mimi naona ni sawa/haki kupata ugonjwa ikiwa tu ugonjwa huo una kusudi la Mungu ndani yake. Kama nilivyoandika kwamba kuna magonjwa ambayo ni majaribu/mtihani. Mtu wa Mungu akipatwa na ugonjwa wa namna hii na kisha akapambana na kuvuka ni lazima itakuwa imempa hatua katika kumjua Mungu. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Ayubu. Baada ya kuwa amevuka katika adhiki ile alijikuta akisema maneno haya:

  “Nilikuwa nimesikia habari zako kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu limekuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, nakutubu na kutubu katika mavumbi na majivu” Ayubu 42:5.

  Ingawa kabla ya kuugua huko Ayubu alikuwa anajiona ni mwenye haki na alikuwa amejitahidi kufaya kila linalotakiwa kwa mcha Mungu. Lakini baada ya kuvuka jaribu lake ndipo akamfahamu Mungu zaidi na zaidi. Na mwisho wa uchungu wote wa kuugua vikaishia katika toba na ujuzi mwingi wa Mungu.

  Vile vile ninaona ni sawa kwa mtu aliyeokoka kupata ugonjwa ikiwa kwa ugonjwa huo ndipo moyo wake utakavyokuwa karibu na Mungu. Mungu ni baba yetu na anatufahamu. Ikiwa alifaya jambo hilo kwa mtume Paulo ili asije akajisifu na kujitwalia utukufu ninaamini Mungu anaweza kufanya hivyo hata sasa ikiwa kuna mchana Mungu wake ambaye anamuona kama akibaki salama anaweza kuharibika kwa kiburi cha uzima.

  Pia yako magonjwa ambayo Mungu huyaleta ili kuwa kama karipio – bakora! Mtu wa Mungu akipatwa ugonjwa wa namna hiyo ndipo fahamu zake zaweza kumrudia na kumfanya atafakari na kuangalia ni wapi amekosea. Na anaporekebisha uzima humrudia na safari ya mbinguni huendelea. Mimi naona ugonjwa kwa ajili ya kusudi hili ni sawa tu.

  Ninayoona si sawa na haki kwa mtu aliyeokoka kuwa nayo ni magonjwa yanayosababishwa na nguvu za giza. Katika haya yamo magonjwa ya vifungo ambayo husababishwa na mapepo. Hapa naona si swa kabisa. Kama nilivyoandika hapo juu kwamba kule kuwa si haki/sawa haimaanishi haiwezekani. Kuna uwezekano wa mtu ambaye ameokoka akashambuliwa na magonjwa ambayo katika ufafanuzi nimeyaita magonjwa ya vita. Vita vya mkristo ni lazima kuvipigana. Ninavyofahamu ni kwamba inawezekana mtu aliyeokoka akapatwa na ugonjwa wenye kusudi la vita. Kama atapambana kama mkristo na kushinda vita hivyo hiyo pia huwa ni hatua muhimu. Hakuna ushindi pasipo kupigana. Na maisha ya mkristo ni maisha ya ushindi kwa sababu ndani yake kuna vita vya aina nyingi. Lakini katika vita hivyo kuna ushindi.

  Watumishi wengi na watu wengi wa Mungu huwa wanashuhudia hili. Kuna wakati ambapo mtu wa Mungu anaweza kukutana na ugonjwa fulani, lakini kwa kutambua kuwa ni hila/vita na kwa kusimama na ahadi za Neno la Mungu ugonjwa huo hutokomea.

  Jambo moja ninalofikiri ni kwamba yawezekana kukawa na tofauti kati ya kuugua na kuwa na ugonjwa. Ugonjwa unapokuja mwilini na kutoka nalichukulia kama jambo la kawaida. Kwa sababu yawezekana ni vita na ikisha kushindwa huisha. Lakini ugonjwa unapokuwa umeingia ndani ya mwili halafu ukakaa kwa muda mrefu na ukawa unaendelea kukaa hilo naliona ni jambo jingine. Lakini si lazima kwamba ugonjwa unapokaa muda mrefu utakuwa umetoka katika nguvu za giza. Nimeshaandika mfano wa mtume Paulo kwamba alipewa mwiba ili kumuadabisha. Kwa hiyo ni lazima kuwa na mawasiliano na Roho mtakatifu.

  Lakini pia kule kuwa si sawa/ki haimaanishi haiwezekani. Ni mambo mengi yanayotendeka duniani ambayo si haki na wala si sawa lakini yanatendeka tu kwa sababu anayetendewa hana uwezo wa kuyazuwia. Hali ni hiyo hiyo kwa mtu aliyeokoka. Mtu anaweza kuwa ameamua kuokoka lakini ni dhaifu ktk imani, yaani hajalifahamu vizuri Neno la Mungu na haki zake kama mkristo. Huyu anaweza kuvamiwa na magonjwa kutoka nguvu za giza kwa sababu uhalali wa yeye kuvamiwa ni kwa sababu hajasimama vizuri katika Mungu. Kusimama vizuri katika Mungu ni pamoja na kuwa na elimu ya kutosha kuhusu Mungu na haki za mkristo. Mtu ambaye hajasimama vizuri ni rahisi kutenda mambo ambayo hayampasi kama aliyeokoka na huko ndiko hufungua milango ya nguvu za giza kumvamia. Kumbe kinachotakiwa ni kwamba mtu kama mkristo anatakiwa kuwa na ujuzi wa kutosha wa Neno la Mungu

  Yako magonjwa ambayo husababishwa na ujinga, kukosena kwa maarifa ya namna sahihi ya kuishi kama binaadamu. Mambo haya ni kama vile kutokufuata kanuni za usafi na afya kwa ujumla. Japo hakuna ninayemfahamu lakini ninafikiri wapo watu ambao japo ameokoka lakini alishawahi kuugua kipindupindu kwa sababu ya kula chakula kwenye mazingira machafu. Mtu ukiwa unafahamu kwamba kula chakula kichafu au katika mazingira machafu kunaweza kusababisha kipindupindu halafu ukaendelea na tabia hiyo eti kwa sababu umeokoka mimi naona ni sawa na kumjaribu Mungu. Wakati mwingine tunapaswa kutumia vizuri akili tulizopewa na Mungu ili kukabilia na baadhi ya mambo ambayo tuna mamlaka nayo. Kwa hiyo hata kama mtu ameokoka ni lazima kufahamu kanuni za maisha ya binaadamu, vinginevyo anaweza kujikuta akiugua hovyo hovyo na kuanza kusingizia ‘shetani anajiinua’ kumbe ni kukosa kwake maarifa!

  Naona nimalizie kwa kuandika hivi kwamba NI sawa/haki kwa mtu aliyeokoka kupatwa na ugonjwa ikiwa kuna kusudi la Mungu ndani yake lakini SI sawa/haki kwa mtu aliyeokoka kupatwa na ugonjwa ambao hauna kusudi la Mungu na/au unaosababishwa na nguvu za giza kisha ugonjwa huo ukakaa mwilini mwake na kuwa sehemu ya maisha yake.

  Katika Yote Mawasiliano na Mungu ndilo jambo la muhimu.

  Hivi ndivyo nilivyoweza kujibu kwa sasa. Kama kuna mahali nimekosea nitafurahi kusahihishwa ili tuendelee kujifunza.

 50. Wonderful!

  Nafuatilia sana mada hii, namshukuru Mungu kwa ajili ya wachangiaji ambao kupitia wao nimepata vitu vingi vya kunisaidia.

  Mungu awabariki sana!

 51. Ndugu Paul,
  Jana nimekutana na rafiki yangu aliyekuwa amehudhuria mafundisho ya Neno kwa ajili ya kuukulia wokovu (mafundisho ya awali baada tu ya kuokoka)kwa muda wa miezi kadhaa, ushuhuda wake umenifanya nielewe zaidi hii mada ya kufunguliwa. Ni kweli kama Neno mtu hajalijua/halijamfungua ni rahisi kuendelea kukandamizwa na shetani. Hata mimi nimeelewa kuna sehemu nilichelewa kuelewa Neno nikakandamizwa na shetani ila sasa hanipati tena! glory to God.

  Mchango wangu uliopita nilieleza niliyoelewa, nadhani hukunielewa tu kuwa nilitaka kufahamishwa kama nilichoelewa ndicho au sicho.

  Mtu kuwa chini ya vifungo fulani ambazo pia shuhuda zake nyingi nimezikia mara nyingi pakiwa na maagano, au kuishi ktk dhambi fulani kwa muda hata shetani akaufanya kuwa ni mlango wake. Nilichokuwa nimeelewa mwanzo na ambacho nilikataa ni kila mtu kutenda dhambi fulani na kupata pepo!au kila tatizo la kimwili kuli-associate na Pepo, unless mtu amepata insight!

  Hainisumbui sana mtu kuokoka na kuwa mgonjwa(ugonjwa wa kawaida unaoeleweka eg. kuumwa tumbo kwa ajili ya chakula kibaya, malaria, kichwa kwa ajili ya uchovu nk) kwa sababu nilishaeleza hapo kabla kuwa siyo kila ugonjwa ni pepo/nguvu za giza nk mfano Timoth, mtume Paul, Epafrodito na sehemu nyingi agano la kale watu waliomwamini Mungu bado waliweza kuugua i.e hawakuwa 100% free from disease. Labda tujifunze zaidi hapo coz kuna watu wana imani ya kutokuugua na hawaugui, na wengine wanaamini na kukiri Neno but still wanaugua!

  Naendelea kujifunza kama nilivyokiri toka awali,
  Mbarikiwe!

  Glady

 52. Shalom,
  Ndugu yetu Glady aka Furaha katika majibu ya maswali yako tulikujibu vizuri kabisa ila naona wewe unashindwa kuelewa …..
  1. kwa kifupi tulisema unaweza kuomba msamaha/rehema/ kufutwa kwa uovu/makosa/dhambi za watu waliopo hata waliokufa lengo ni madhara ya uovu wao yasiwapate hiyo jamii husika au kizazi…pindi uovu ukisamehewa na shida zinazotokana na huo uovu zinaondolewa….sio maombi yote ya Toba ni ya kuwafanya watu waende mbinguni jaribu kuongeza ufahamu wako kwenye eneo hili….

  2. Ni kweli mtu aliyeokoka kuwa chini ya laana au vifungo ni kweli kuna mahali ambapo hapako sawa…ila kuokoka ameokoka….mafundisho ya deliverance ndo yanamuonyesha hapo mahali ambako hapako sawasawa ili pawe sawa sawa…… naona hapa umeanza kuelewa JINA LA BWANA YESU LIBARIKIWE……Dada Furaha labda nikuulize swali naomba unijibu Kwanini inakusumbua sana mtu aliyeokoka kuwa katika kifungo lakini mtu aliyeokoka kuwa mgonjwa haikusumbui??

  3. uovu wa hao watu ndo unaosamehewa….. haimaanishi wao wataenda mbingini kwa sababu uovu wao umesamehewa….pitia Daniel sura ya 9 na Neh sura ya kwanza utaona na yapo maandkiko mengi sina muda wa kutosha kuyatafuta…

  4 Huu mfano Dada Furaha ninukuu hivyo alivyo sema beny Hinn…. Mama huyo alikuwa hajui kinacho mtesa mpaka Benny Hinn alipomwambia na kumwombea kama niliandika wakati uliopita… Kwani Adama alipofanya dhambi si tulikuwepo? mbona madhara yake na sisi yametufika? Mbona ni rahisi kuelewa tu…..jaribu kupanua ujuzi wako dada kwenye hili eneo la maombi ya aina hii…

  …..3. Dada furaha imani Dhaifu ni ipi? kwani imani nini? imani inakujaje?…..Imani ni kuwa na uhakika wa mambo tunayoyatarajia- Ebr 11:1 ….. Imani huja kwa kusikia, kusikia kwa neno la Kristo. Nikusaidie unaposema imani dhaifu unamaanisha mtu aliyesikia neno la kristo lakini haweki kwenye matendo…imani isiyotenda kazi. Waathirika wa imani dhaifu ni wengi sana…. walokole wengi sana wapo hapa….. Toka mwanzoni tuliweka wazi unapopata shida kama umeokoka unaanza na kumuuliza Mungu hii inatokana na nini? ni natural au mishale ya yule mwovu. Niliwahi kuhojiana na jirani yangu mmoja ambaye ameokoka nilimuuliza swali we ukisikia unaumwa labda huwa unachukua hatua gani? alinijibu huwa anakwenda hospitali kwanza halafu ikishindikana ndo anaangalia rohoni….. sa sijui kama hii ni sahihi kama umeokoka nafikiri kwanza unauliza hii nini na imeotoka wapi ili ujue ni namna gani uishugulikie…. TUSUBIRI TUJIBIWE YALE MASWALI YALIYO BAKIA NAAMINI UTAELEWA VEMA TU……EFESO 6:16 usipokuwa na neno sahihi la Kristo juu ya Eneo fulani hiyo ngao ya imani huna….Imani huja kwa kusikia neno la kristo…. Ukisikia juu ya wokovu ukaamini utapata wokovu…ukisikia juu ya uponyaji ukaamini utapata uponyaji….ukisikia injili ya wokovu ukaamini utapata wokovu ila usiposikia uponyaji…. utakuwa umeokoka ila unaweza kufa na magonjwa kwa sababu huna imani ya kuponywa.

  Mtu aliyokoka kuwa na hofu juu ya pepo ni kitu cha ajabu sana maana mapepo ni viumbe dhaifu mno kama unajua ku-exercise mamlaka yaliyopo ndani ya kristo..ila usijesema mi siogopi pepo ili kufurahisha wasomaji hali ukiletewa mtu aliyepagawa pepo unabidi ukaite kikundi cha maombi kanisani …….kuwaza kuwa shida fulani juu yako au mtu mwingine kuwa chanzo ni mapepo si sawa … ni lazima ujifunze kusikiliza rohoni mwako ili ujue chanzo ninini? na namna ya kutatua. Kuna dada mmoja mtoto wake aliungua na maji ya moto alichomeka mkono kwenye maji yanayotokota akaungua… badala ya kuwahi kupaka asali kama tulivyozoea yeye alimuuliza Roho Mtakatifu….RMT akamwambia chomeka mkono wa mtoto kwenye maji ya baridi mpaka aache kulia … yule dada akafanya hivyo mkono wa mtoto ukapona saa hiyo hiyo…wala hakukuwa na alama yoyote. Jifunze kitu hapa Dada yangu na pia anaweza kukuongoza kwenda Hosp? nk….

  PIA imani ya namna hii kuwa ngao unaposhambuliwa unahitaji kujifunza kusikiliza kutoka kwa MUNGU spoken word (rhema) Siku moja niliwahi kuumwa ghafla usiku wa manane nikiwa sekondari macho yakapoteza kuona na tumbo liliuma sana nilikuwa siwezi kusimama wima kabisa…..NIKASIKIA SAUTI IKISEMA PAUL SHETANI LEO AMEKUJA KUKUUA SEMA MANENO YAFUATAYO HAKUNA SILAHA ZITAKAZOFANYIKA KINYUME NAWE ZITAFANIKIWA…….nilijua ni Mungu anasema na nikasema kama nilivyoelekezwa…ghafla nikaanza kuona…na maumivu ya tumbo yaliisha baada ya muda mfupi….hilo neno lilikuwa ngao kwangu siku hiyo… vp kama ningekimbilia hosp? au nisingesikia hilo neno?. Na pia niliwahi kupata shida nyingine niliomba sana kwa muda mrefu lakini ile shida iliendelea kunifuata baadaye Mungu aliniambia…VUNJA MAAGANO……
  Pia niliwakupata shida nyingine niliomba muda mrefu shida haikuondoka nikamuuliza Mungu Kwanini akaniambia NATAKA IMANI YAKO…. hapo ndipo nilipojifunza imani na shida ikaondoka……. Dada Yetu Furaha aka Glady elewa sio matatizo yote ni laana au vifungo au maagano tulishaongolea mwanzoni….. Niliwahi kumuombea Binti mmoja alikuwa na tatizo la mguu aliwahi kupata ajali mguu ukavunjika kwenye ankle akatibiwa hosp ila bado mguu ulikuwa na maumivu makali akikanyaga chini…. aliponieleza nikamfundisha imani…1Pet1:24b…kwa kupigwa kwake mmeponywa…..tukamshukuru Mungu kwa KUMPONYA nikamwambia kanyaga chini akakanyaga na maumivu yakaondoka kabisa GROLY TO GOD. Shida ya huyu haikuwa pepo………

  Kwa leo niishie hapa…. Kama yanawafaa wawezachukua kama hayafai yaache….

  Mungu awabariki wapendwa wote…

 53. Wapendwa wote Mungu awabariki kwa michango yenu mizuri ambayo nimeifuatilia na nimejifunza vitu vingi. Namshukuru ndugu Paul na dada Lisa pia kwa kunijbu maswali niliyouliza nilipochangia tar 1 June. Nimejifunza kuwa:
  1. Toba inayozungumziwa mfano kat Dan 9:4-5; siyo kutubu (ambayo naelewa kuwa ni kugeuka na kuacha njia mbaya)au niseme kuwatubia ili waliokufa wageuke/wageuzwe/wasamehewe ila ni kuomba Mungu aufute uovu walioutenda ili usitupate sisi tulio hai. Naomba kama nimeelewa tofauti au visivyo mnisahihishe.
  2. Nimejifunza kuwa makosa/uovu wa wazee unaweza kusababisha matatizo kwa watu ambao hawajamwamini Kristo. Sababu ninayoiona ni kuwa, tukitubu Mungu anasamehe maovu yetu na kutuponya magonjwa yetu yakiwemo hayo matatizo ambayo yangetokana na makosa ya wazee wetu.Kol 1:13; Zab 103: 3-4.Hivyo basi kwa mtu aliyeokoka kuendelea kuwa chini ya vifungo na laana then something must be wrong somewhere-labda hajaamini vizuri/hajaelewa vzr maana ya wokovu ambao ndio kufunguliwa kwenyewe, imani dhaifu i.e kutokuamini a,b,c ambazo Yesu anazifanya pale mtu anapomwamini . mimi ndivyo nionavyo hapo.
  3. Nimejifunza kuwa naweza kutubu kwa ajili ya watu wengine WALIO HAI na wakasamehewa-Hili ni sawa, lakini sio kama kutubu kwa ajili ya watu wasio hai ili WAO/WAFU wasamehewe.
  4. Katika michango ya mada hii ya deliverance, nimejifunza au nimeelewa au niseme pia ninaamini kuwa matatizo ya kurithi/vifungo/laana siyo lazima uende ukatambike ndo vikupate kama vinaweza kusababishwa na wazazi/wazee, mfano aliotoa ndugu Paul Holela wa Beny Hinn kuwa yule mama alipata mateso kwa sababu WAZAZI WAKE WALIABUDU MIUNGU (hakusema kama na yule mama neye aliabudu miungu pia!?)si ina maana kuwa hizo laana ni DIRECT haijalishi wao walienda kutambika wakakuacha nyumbani au mliambatana phyiscally lakini hayo waliyofanya yalikuhusu na wewe moja kwa moja! Hapa ndipo ninaamini kuwa Mtu akiisha kuokolewa, anasamehewa dhambi zake zote, anahamishwa kutoka ufalme wa giza kwenda ufalme wa nuru na vifungo vitamwachia na havitampata tena ispokuwa:
  1.Anaweza kujaribiwa kwa kurudisha nyuma fikra zake kuwa LABDA Mungu hajanisamehe kabisa -Hofu inampa shetani nafasi na anaweza kumtesa.
  2. Majaribu ya kurudia mambo ya kale kwa kushiriki desturi zilizo kinyume na Neno la Mungu
  3.Imani dhaifu. Mimi naona imani inatakiwa sana hapa. Inawezekana hata kama kweli mtu akawa anaona matatizo fulani au shida fulani fulani badala ya kuzama ktk kuwaza ni pepo, ni shetani, ni laana, akawaza/tafakari upande wa pili kuwa nimeokoka, Upendo wa Yesu unanifunika, shetani hana nafasi kwangu…Imani INAZIMA MISHALE YA YULE MWOVU (Efe 6:16).Mimi hapa nitakubaliana na ndugu Furaha kuwa, mawazo ya kuwa kila wakati pepo, shetani anaweza kuwa karibu kiasi cha kuleta hofu na shida ktk maisha ya mtu aliyeokoka inategemeana na Imani aliyo nayo muhusika. Imani ikiwa KUBWA kuwa Yesu yu upande wangu, then SINA HOFU juu pepo kuwa na nafasi kubwa/karibu kwangu kiasi hicho.
  Naendelea kujifunza.
  Mungu awabariki wote,
  Gladness

 54. Shalom,
  Kaka John Paul, nashukuru kwa majibu yako nimeyapenda sana na ninaamini wasomaji wsatajifunza mengi hapo hasa utakapomaalizia yale yaliyobakia Mungu akikujalia…Naamini wasomaji wenye nia ya kujifunza wamepata kitu kizuri Mungu akubariki sana……
  wewe ni mmoja wa watu ambao nimeona wanapojifunza kitu kibiblia unaweka neutral gear kwanza ( namaanisha unatoa msimamo ulinao kwanza) then unajifunza kama unaona maandikio kwa mara ya kwanza …Hiii itunze ndugu John Itakusaidia kufika mbali….
  Mungu awatunze wasomaji wote
  Eng Paul Holella

 55. Ndugu Paul
  Naomba unisamehe kwa kutokujibu maswali yako ingawa uliuliza ili mtu yeyote ajibu na ndugu John Paul ameshajibu baadhi, hata mimi kuna mahali hapo juu niliyapitia kidogo. Lakini pia naomba unisamehe kama umekwazika niliposema hatushindani ila ni kushirikishana kila mmoja na mwenzake, sikumaanisha kuwa kuna anayeshindana ila ni kama onyo tu kwa wote. Hata hivyo nashukuru kwa kunisahihisha kuwa ningesema kwa mtizamo wangu mimi yalionekana kuwa nje ya mada kidogo, lakini kwa wengine wataona ipo ndani ya mada. Asante, Hii ni kweli kwa sababu tunatofautiana kiuelewa na hata kiwango cha mafuta ni tofauti tofauti.Hii ndio maana ya kujifunza.

  Asante, Mungu awabariki wote.

 56. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,

  Nilichojifunza mwanzoni kabisa mwa mfululizo wa michango ya ndugu Paul Holela katika mada hii ni pamoja na haya aliyoandika hivi:

  “a. Kama umeokoka na unaona kuna dalili ya nguvu za giza kufuatilia au kushambulia sana maisha yako au kukandamiza baadhi ya maeneo chunguza unaweza kuta kuna uhalali fulani ambao mashetani wanaupata hapo na ni vema kuushughulikia hata we mwenyewe ila kama huna msuli wa kutosha tafuta msaada( majeshi ya Kukodi)

  b. Kuna kupitiliza kwingi kwa watu wengi wanaofundisha haya mafundisho ya ukombozi tuwe makini kidogo hapa,

  c. Mimi huwa siiti delivarence, naitaga maombi tu…. kwa wakati mtu akiwa anaona anashida na anahitaji maombi nitamuombea… tunatumia neno pamoja na maombi….

  d. Na kama hizo nguvu za giza ni uhalali kukaa kwa mtu ni lazima kuuondoa huo uhalali wake kwanza ndio umtoe maana wale viumbe hawana nguvu ila wanatumia kufanya siri ili kuwakandamiza watu”.

  Kutokana na hayo aliyoandika ndugu Paul pamoja na michango ya wachangiaji wengine, mimi nimeona kwamba sababu ya mtu aliyempokea Yesu lakini bado akawa katika vifungo, kama mada yetu ilivyo, ni pamoja na:

  i. Kutokuchunguza vizuri baadhi ya maeneo katika maisha ambapo mashetani wanaweza kupata uhalali wa kumsumbuwa mtu huyo. Mfano wa uhalali huo ni kama vile Kuwa na maagano ya damu yaliyofanyika katika ulimwengu wa roho kabla mtu huyo hajaokoka ambayo wakati mtu anampokea Yesu hayakushughulikiwa.

  ii. Kutokulifahamu Neno la Mungu linavyosema kuhusiana na eneo husika na hivyo kutokuzifahamu haki za mtu aliyempokea Yesu.

  iii. Kutokuwa na bidii katika kumtafuta Mungu.

  iv. Kupata mafundisho potofu ambayo yanaweza kumfanya mtu huyo awe tegemezi kwa watu wengine waende mbele za Mungu kwa ajili yake na si kujitegemea yeye mwenyewe kwenda mbele za Mungu.

  v. Kuendelea kushikilia mambo ya gizani ambayo si
  sahihi mbele za Mungu.

  Kuhusu kufanyiwa huduma ya deliverance ndipo mtu afunguliwe, nilichojifunza hadi sasa ni kwamba;

  i. Deliverance siyo huduma maalumu bali ni maombezi tu ya kumuomba Mungu ili mtu anayehusika aweze kupokea majibu ya mahitaji yake kama vile kupona ugonjwa. Deliverance ni neno tu la kiingereza lenye maana ya ukombozi/kufunguliwa na maneno mengine yanayofanana maana na hayo.

  ii. Siyo lazima mtu aende kwa mtu mwingine kumuombea maombi hayo lakini kama mtu anaona hana nguvu za kutosha ni vema kushirikisha mtu mwingine ili kuomba pamoja au kuombewa kabisa.

  iii. Deliverance yenye manufaa ni mtu anapofunguliwa kwa maombi afundishwe Neno sahihi la Mungu ili asijeingia katika tabu tena kwa kutokulifahamu Neno la Mungu. Maana Neno la Mungu ndiyo msingi wa maisha ya ushindi kwa mkristo.

  iv. Baadhi ya imani za kipentekoste, kama alivyoandika ndugu Benedicta, zinapinga huduma ya Deliverance kwa sababu ambazo ni pamoja na tuliyopata kwenye michango hapa kwamba kuna watu wanapitiliza wanapofundisha jambo hili. Kupitiliza huku kunamuondoa mtu mahali salama na kumuweka mahali pa hatari, na mafundisho mengine huwa ni tofauti kabisa na Neno la Mungu. Ninaamini pamoja na kupinga huduma hiyo huwa wanatoa njia mbadala ya kumfanya mtu aweze kutoka katika vifungo vya giza.

  Natumaini ndugu Benedicta unaendelea kufuatilia mjadala huu muhimu.

  Ninaomba kujibu maswali ya ndugu Paul, kiasi nitakachoweza kwa sasa. Lengo la kujibu ni kubadilishana ufahamu kwa lengo la kujifunza na kujengana. Kama kwa namna moja au nyingine nitakuwa nimejibu isivyo sahihi ni vema pakasahihishwa ili tuweze kwenda pamoja katika msingi wa Neno la Mungu!

  1. Bwana Yesu alipowaombea wanafunzi kutakaswa hata baada ya kuwa wameamini [Yohana 17:17] alikuwa anaomba ili katika maisha yao hapa duniani waendelee kutakaswa siku kwa siku. Si lazima kwamba ingawa walikuwa wameamini lakini walikuwa bado hawajatakaswa. Katika mstari wa 15 Bwana Yesu aliomba kwamba ..’bali uwalinde na yule mwovu’…hii haimaanishi kwamba kabla ya maombi hayo Mungu alikuwa hawalindi wale wanafunzi, bali ni maombi ambayo yalikuwa yanaombwa ili yaendelee kufanya kazi, KAMA AMBAVYO HATA SASA NASI TUNAYATUMIA.

  Katika kitabu cha Ufunuo 22:11 kuna maneno haya: “…..na mtakatifu azidi kutakaswa”. Kwa hiyo pamoja kuwa walikuwa wametakaswa kwa kumwamini Yesu, bado ni lazima kuendelea kutakaswa na kujitakasa. Anayehitaji kujitakasa/kutakaswa si yule tu ambaye hajatakasika bali hata aliyetakasika naye anatakiwa aendelee kujitakasa/kutakaswa.

  Lakini wakati anaomba maombi hayo katika Yohana 17:20 Bwana Yesu alisema kwamba si hao tu [wanafunzi] aliokuwa anawaombea bali na wote walioamini baada ya maombi hayo hadi sasa tunaposoma hapa na watakaoendelea kumwamini baada ya kuwa tumemaliza kusoma mchango huu. Sisi tuliomwamini Yesu pia tunatakiwa kuendelea kutakaswa kwa Neno na wote wanaondelea kumwamini wanatakiwa watakaswe kwa Neno, na kutakaswa kutaendelea hadi mtu anapofika mwisho wa safari au hadi siku ile ya unyakuo, kwa wale watakaokutwa wakiwa hai.

  Kwa hiyo maombi yale ya Bwana Yesu ni maombi hai na endelevu.

  2. Wakati akiwaandikia Warumi, mtume Paul alikuwa anawafundisha jinsi ipasavyo kwa mtu kuenenda baada ya kuwa amemwamini Kristo. Pamoja na mafundisho mengi tunayoyasoma katika kitabu hiki cha Waraka kwa Warumi ni pamoja na hilo ulilonukuu katika Sura ya 12:2 la kuwafundisha wageuzwe kwa kufanywa upya nia zao ili waweze kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema na ya kumpendeza na ukamilifu!

  Inawezekana kabisa mtu akawa amemwamini Yesu lakini nia yake ikawa haijamwelekea Kristo. Yuko mtu anayesema anamwamini Yesu na hata kujitangaza ameokoka lakini mtu huyo anaendelea katika mambo yasiyopasa kwa mtu anayemwamini Yesu. Mpendwa Furaha alitoa mfano huo kwamba utakuta mtu anajiita ameokoka lakini bado anaendelea kufanya mambo yaliyo kinyume na Neno la Mungu kama vile kusali ibada za wafu, kumuomba mama Maria amwombee kwa Mungu nk. Mtu wa namna hii huwezi sema nia yake inamwelekea Kristo. Nia ya mtu ikimwelekea Kristo ni lazima mtu huyo atafanya kile tu anachoelekeza Kristo na si vinginevyo.

  Wako wengi katika siku zetu ambao pamoja na kusema wanamwamini Kristo na mwengine kusema wameokoka lakini nia zao, kwa ukweli, hazijamwelekea Kristo. Kipimo kwamba nia hazijamwelekea Kristo ni kwa sababu wanafanya mambo yaliyo kinyume na maagizo ya Kristo. Sasa kwa sababu wao husema wanamwamini Yesu huwezi kuwabishia ila kwa sababu wanaendelea katika mambo ambayo yako kinyume na Kristo, kinachopatikana ni kwamba Kumbe mtu anaweza kumwamini Kristo lakini nia yake ikawa haijamwelekea Kristo. Lakini kwa hali ya kawaida kumwamini Kristo kwa namna hii ni hatari, si salama!

  Ndiyo maana mafundiso ya Neno la Mungu ni muhimu ili mtu anaposema anamwamini Kristo ajichunguze kweli kama anavyosema ndivyo alivyo! Na mtu akigundua hayuko sawa na anachosema kinachotakiwa ni kutubu na kuomba msamaha, kisha kazi ya kuutafuta utakatifu iendelee.

  Yako mambo mengi katika Sura hiyo ya 12, katika kitabu cha Warumi, ambayo mtume Paulo alikuwa anafundisha na ambayo yote yangefaa kukaa kwenye swali lako. Mfano wa hayo machache ni haya:

  12:2 – Msiifuatishe namna ya dunia hii; je, mtu anaweza kuamini halafu akaifuatisha namna ya dunia hii?

  12:9 – Pendo lisiwe na unafiki. je, mtu anaweza kuamini lakini akawa na pendo lenye unafiki?

  12:14 – Wabarikini wanaowaudhi. je, mtu anaweza kuamini lakini akawalaani wanaomuudhi?

  12:16 – Msiwe watu wa kujivunia akili. je, mtu anaweza kuamini lakini akawa anajivunia akili?

  12:17 – Msimlipe mtu ovu kwa ovu. je, mtu anaweza kuamini halafu bado akawa analipa ovu kwa ovu?

  Mafundisho yaliyopo katika Sura hii ya 12 ya kitabu cha Warumi ni moja ya mafundisho ya msingi kwa mtu anayesema amemwamini Yesu. Ni mafundisho ambayo yanamuongoza mtu kujitambuwa nafasi yake baada ya kuwa ametangaza kumpokea Yesu. Kushindwa kuenenda katika mambo hayo ya msingi husababisha mkristo huyo kudumaa kwa sababu ya kuchanganya mambo. Na katika kudumaa huko ni rahisi kuvamiwa na nguvu za giza, ingawa anasema ameokoka, kwa sababu nia yake haijamlingana Kristo ili aweze kufahamu hakika yaliyo mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu.

  3. Mtu anayesema ameokoka lakini anazini, mlevi, mwizi, nk mtu huyo nia yake haijamwelekea Kristo. Na wokovu wa namna hiyo ni wokovu ambao hauwezi kumfikisha mtu mbinguni. Kuokoka ni Maisha na wala si Maneno peke yake. Bwana Yesu alikufa msalabani ili mtu anayemwamini aweze kusamehewa dhambi na kupewa nguvu ya kuishi maisha matakatifu. HUU NDIO WOKOVU. Lakini pia si kila mtu anayesema ameokoka huwa ameokoka kweli. Kipimo cha mtu kwamba hajaokoka ingawa anasema ameokoka ni kama haishi sawa sawa na mwenendo uwapasao watu waliookoka. Kusema umeokoka lakini unaishi tofauti na inavyowapasa watu waliookoka maana yake ni kwamba hujaokoka. Ni sawa na mtu kusema yeye ni msafi wakati ukimwangalia anaonekana amejaa uchafu mwilini na ananuka harufu mbaya ya uchafu!

  Mtu anayesema ameokoka lakini bado anafanya yale yale wanayoyafanya ambao hawajaokoka, huyo anatakiwa akae chini atafakari upya. Kama ni kuokoka aokoke kweli au aache kusema kwamba ameokoka, hadi hapo atakapoamua kuokoka. Kwa sababu mtu hataingia mbinguni kwa sababu ya KUSEMA ameokoka bali kwa sababu ya KUISHI maisha matakatifu.

  4. Suala la ugonjwa kuwa unasabibishwa au hausabishwi na nguvu za giza ninatumaini kile ulichokiandika katika mchango wako wa tarehe 26, May 2010 kinaweza kuwa moja ya majibu ya swali hili. Uliandika hivi:

  “…..ili kujua shida chanzo chake ni nguvu za giza au natural ni lazima Roho Mtakatifu akupe signal…”

  Nyongeza yangu ni kwamba wakati mwingine mambo huwa dhahiri kabisa. Kwa mfano mtu anaweza kuja kwenye maombi akasema tumbo linamuuma na akiulizwa tangu lini halafu yeye akisema tangu jana maana juzi usiku alikula chakula kilichochacha!…. Sidhani kwa hali ya namna hii kama panahitajika signal kutoka kwa Roho mtakatifu. Au mwingine anaweza kuja akasema anasikia maumivu makali kichwani na ukimuuliza kulikoni halafu yeye akasema alikuwa anatembea njiani mara akajisikia kama amefunikwa na kitu kama nguo halafu kuanzia hapo kichwa kikaanza kuuma. Hii pia sidhani kama ni lazima kusubiri signal ili kutambua asili ya ugonjwa. Hii ni mifano tu!

  Hivi ndivyo nilivyoweza kujibu. Nitaishia hapa kwa sasa. Nitaendelea kujibu maswali mengine.

 57. Shalom,
  Nashukuru kwa wachangiaji na tunaendelea kujifunza….

  ndugu nashukuru kwa kunijibu swali nililo kuuliza moja kwa moja ufafanuzi wako…
  Dada Furaha, sijaona mchangiaji hata mmoja mpaka sasa anayeshindana na mwenzie humu ndani nadhani huo mtizamo wako si sahihi …. Tunapojadili humu ndani hatupigi kura kila mmoja anaelezea ukweli na namna anavyoielewa mada husika halafu wasomaji wanajifunza na kuchukua vitu vinavyowezawasaidia kwenye maisha yao …. Biblia inasema Mafuta yaliyo ndani yetu hutufundisha yote…… kwa hayo mafuta yaliyo ndani twaweza jua ulipochangia ni kutetea msimamo ulionao au la…
  Naomba nirudie Mtu yeyote akifunguliwa kutoka katika nguvu za giza ameokoka au hajaokoka hiyo deliverance …..
  Ningefurahi sana kama ungenijibu maswali niliyouliza kuliko ulivyosema yako nje ya mada….. ungetumia lugha hii …kwa mtizamo wako yako nje ya mada ila kwa mtizamo wa mtu mwingine yanaweza yakawa ndani ya mada……

  Naomba nijibiwe maswali ambayo sijajibiwa … ndugu yetu John Paul, Hagai, asheri, Bernad Mwenda, Furaha na wengine……

 58. Nazidi kuwashukuru wachangiaji wote tunapoendelea kujifunza. Kwa kweli napata kitu. Ndugu Haggai baraka za Bwana zikukalie umenifungua macho kuhusu Gal 5:17 siku zote nilikuwa najua inasema …mwili ukishindana na roho ie roho zetu kumbe ni Roho Mt, ooh glory to God.

  Nikirudi kwenye mada yetu, napenda nimshukuru ndugu yetu Paul kwa maelezo yake ktk kujibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa. Pamoja na majibu ya ndugu Paul (ambayo hajajitokeza mwingine wa kuyatolea majibu, bado kuna clearity ambayo sijaipata.Tukianza na swali la kwanza liliouliza:
  1.Ni wapi huduma ya deliverance inaonekana ktk Biblia hasa baada ya kifo na ufufuko wa Yesu Kristo, majibu yake siyo rasmi kwa sababu hakuweza kuonyesha maandiko husika hapo. Yule mgerasi alikuwa hajaokoka na pili Yesu alikuwa bado hajafa na kufufuka-ambapo hapa ndipo penye siri kuu ya ushindi wetu dhidi ya yule adui tunapomwamini Kristo aliyekufa na kufufuka! Pia wanafunzi wake/mitume/kanisa la kwanza hatujaona mahali walipowarudia waumini wakaanza kuwatoa laana, mapepo nk (kama yupo aliyepata maandiko atu/anisaidie hapa tafadhali).

  2. Katika swali la pili nimejifunza kuwa Wakishafunguliwa watu hawapati tena tatizo kama wakijifunza na kutumia mamlaka yaliyo ktk Kristo Yesu. Hapa napata kurudi tena kama tulivyokwisha jadili hapo juu kuwa mtu akiokoka na akaishi ktk Neno la Mungu basi mtu huyu hawezi tena kusumbuliwa na vifungo ila asijibweteke tu akaishi anavyotaka, ila akazane kujifunza Neno la kuliishi.

  3. Ktk swali la tatu nakubaliana na wewe kuhusu majini mahaba, lakini pia nimejifunza kuwa sio kila kufunguliwa kunamsaidia mtu aishi maisha matakatifu mfano ukifanikiwa biashara, shule, kupata kazi nk na pia sio quarantine kuwa mtu atafanikiwa forever (coz hapo juu umeeleza mtu anatakiwa ajifunze Neno, mamlaka ya Mkristo nk). Kama ni hivyo, naona pia deliverance ina faida za mwilini zaidi ya rohoni sijui kama nitakuwa sawa ila ni mtizamo wangu tu. Tuyatafakari zaidi yaliyo juu siyo ya hapa duniani ambayo ni ya kitambo tu Fil 2:1; Fil 4: 8. Mtume Paul anahesabu mambo yote kuwa kama mavi kwa ajili ya UZURI WA KUMPATA KRISTO (Fil 3: 7-8.Christ should be our satisfaction!

  Nimejifunza pia kuna watu wanafundisha/wanaamini/wanajifunza kuwa kila mtu aliyeokoka akitenda dhambi basi hapo NI LAZIMA pepo aje akuingie (mifano mingi imetolewa na ndugu Paul hapo juu eg mtu kamnunia mumewe, mtu hana imani mishale ya mashetani inampata, mtu amesengenya, amejivuna nk). Wapenzi tukienda hivyo itakuwa Kristo alikufa bure!! Tumeokolewa bure kwa neema wapenzi, Mungu akitujalia kuelewa kitabu cha Warumi, ambacho is a center for Biblical Christianity…tukisoma pia 1Yoh: 2: 1-2 na tena mahali pengine asema, tukiziungama dhambi zetu Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote. Na pia Ebr 4: 14-16 Tunaye kuhani anayeweza kuchukuliana nasi ktk udhaifu wetu. Kama kila tukikosea, au chance ya mtu kutenda dhambi na pepo kumvaa hapo hapo ingekuwa rahisi kiasi hicho, then ingekuwa issue kwa sababu watu wote waliookoka dunia nzima, watumishi na kila mtu yeyote tungekuwa tumejaa mapepo tele! Jamani wapenzi, naomba tupate muda wa kujifunza vizuri MAANA YA WOKOVU WETU, UPENDO WA YESU KRISTO TUNAPOMWAMINI, IMANI na Neno la Mungu kwa ujumla wake.

  Wapendwa naomba tujifunze kuwa tunaye Mungu ambaye ni BABA YETU, si katili wala jeuri kiasi hicho, ni Mungu wa Neema. na ndio maana tukijinyenyekesha tunapotubu anatuhurumia na kutusamehe kupitia mwanawe Yesu Kristo (Ebr 4:16). Hatuokolewi wala kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo ya sheria (Simaanishi tuishi ktk dhambi la hasha!) ila kama ktk 1Yoh 2: 1-tukitenda dhambi (kwa bahati mbaya) tunaye mwombezi. Ila kama mtu amekuwa jeuri na kuamua kuendelea KUISHI ktk dhambi aliyoifanya na ameishakujua kuwa amekosea, ameonywa iwe na R.Mt au mtumishi/mkristo mwanzake na hataki kutubu, basi hapo naweza kuamini kuwa Pepo aweza kumpata (Mitahli 29: 1;) (Na hapa ninao ushuhuda wa kijana mmoja aliyekuwa ameokoka na yupo ktk kanisa akiwa mzinzi, akianguka anasema wazi anatubu, anarudia, anatubu mara kadhaa, baadaye akajawa mapepo hadi akachanganyikiwa kabisa).

  Nachelea sana mafundisho ambayo (mimi nitayaita manyonge) yanayomfanya mtu awe na hofu/woga/ mawazo ya pepo pepo kila wakati. Haya yanamfanya Mkrsito kuwa mfungwa wa pepo baada ya kuokoka badala ya kuelewa kuwa Yesu Kristo yu karibu naye zaidi ya pepo (maana tumemvaa Kristo)na badala yake kila saa anawaza/anaona tu pepo yupo karibu na yeye. Ef 2: 13…ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza sasa mmekuwa karibu (karibu na nani? …na Mungu)kwa damu yake Kristo. Kuna watu akitembea akijikwa anakemea pepo, akiona nyoka pepo, tawi la mti likianguka juu ya paa la nyumba yake..pepo, akipata malaria..pepo, akiumwa tumbo amekula chakula kikamdhuru..pepo, gari ikipata pancha tairi zimechakaa…pepo, mtoto akilia usiku tumbo limejaa gesi..pepo..!! sasa jamani wapendwa, tumeokolewa tukaletwa kuwa karibu zaidi na pepoo,(laana, vifungo, mashetani nk )? au tumehamishwa na kuletwa ktk UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE yaani KRISTO?? Hapa nieleweke kuwa simaaninshi hakuna chance ya pepo au shetani kusababisha tatizo ktk ya mtu aliyeokoka, ila nachotaka kuonyesha ni kuwa SIYO RAHISI kiasi ambacho wapendwa wengine wanaweza kupata hofu kiasi hicho. Labda Imani inakuwa ndogo kuliko chembe ya haradali! Kanisa la kwanza ktk Mdo ya mitume ni mfano tu wa jinsi waamini walivyotembea kwa imani na Yesu Kristo, kuliko kuwa na hofu juu ya walipotoka i.e kwenye ufalme wa giza.

  Pia wapendwa nachelea kutoa maoni yangu juu ya huduma zinazoweza kuonekana kana kwamba ni njema, ili hali hazipo supported na Neno la Mungu-mfano mpaka sasa kuna mjadala juu ya huduma ya kurudisha misukule, deliverance baada ya kuokoka iwe kwa kutapisha, kuharisha, kuwekewa mikono nk nk, maji ya upako, mafuta ya upako, kuoshwa nuksi kwa kunawishwa mikono, miguu,.. na mambo mengine yanayoendelea nafikiri tunayafahamu. Nafikiri pia extremities/ kudadavua sana kunakopitiliza kwa Neno la Mungu (Bila Roho Mt)kunatuweka pabaya na hata wakati mwingine kunatutoa nje ya mstari-yaani nje ya Neno la Mungu.

  Mungu atujalie kumjifunza kupitia Roho wake Mtakatifu, na tukae salama rohoni kama mwimbaji wa tenzi za rohoni aliyesema …ni salama rohoni mwangu!

  Mbarikiwe till wakati mwingine, tunaendelea kujifunza.

  NB: Maswali ya ndugu Paul Holela ya tar 3 June, mengi naona yanatoka nje kidogo ya mada, ingawa kuna mahali nimeyapitia pitia. Pia kama ndugu Haggai alivyosema, hapa hatupo kuonyeshana nani anajua zaidi/mashindano na jazba, ila ni ku-share kila mtu na mwenzake kwa kadiri tuonavyo kuwa siku ile inakaribia.

  Amani ya Kristo iwakalie.

 59. Shalom wapendwa wote,
  Ndugu yangu Paul Holela katika kujibu moja ya maswali ya ndg Furaha hasa lile swali la kwanza alilotaka kujua ni wapi katika kanisa la kwanza au Agano Jipya tunaona huduma hii ya deliverance hasa baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu, umesema tunaiona huduma hiyo wakati Yesu alipotoa mapepo kwa yule mgerasi. Nijuavyo mimi hilo lilifanyika kabla ya Yesu kufa na tena huyo mgerasi hakuwa ameokoka kabla ya kuingiwa na hayo mapepo. Kwa vyote vyote vile lazima mtu huyo, maisha yake yalikuwa chini ya mtawala au mkuu wa anga yaani shetani ndio sababu mapepo yakapata uhalali wa kukaa ndani yake(ingawa biblia hailezi hayo kwenye hiyo Marko 5)

  Pia naona kama vile sasa tunatoka nje ya maswali ya msingi ya mada hii ambayo yaliuliza hivi;
  1.Inakuwaje mtu ameokoka na anaendelea kuwa ktk vifungo vya ibilisi?
  2. Ni mpaka ufanyiwe HUDUMA nyingine ya deliverance ndo ufunguliwe kwenye laana za mababu n.k? Haya ndo yalikuwa maswali ya msingi ya mada hii.

  Sasa ndg yangu Paul unaposema shida ipo kwa watu kuichukulia deliverance kama huduma kwa kuifananisha na uchungaji na uinjilisti, unataka kuniambia deliverance si huduma? Nilichoelewa ni kwamba umesema deliverance ni maombi au mafundisho ayapatayo mtu kwa ajili ya kukombolewa(ukombozi). Hapo nakubaliana na wewe kabisa kuwa deliverance ni ukombozi unaomkomboa mtu toka kwenye utawala mmoja(wa giza) na kumwingiza mtu huyo kwenye utawala mwingine(wa nuru) ambao kwa maneno mengine huitwa wokovu Wakolosai 1:13-14 ‘Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake, ambaye katika yeye tuna UKOMBOZI (au WOKOVU) yaani msamaha wa dhambi’ Kwa hiyo ukombozi maana yake ni msamaha wa dhambi ambayo adhabu yake ni mauti na adhabu ya mauti ni laana inayoonekana kwa jinsi ya mwili.

  Hivyo huyo mgerasi aliokolewa na Yesu toka kwenye nguvu za giza, alipokombolewa hakuwa ameokoka kabla! Je baada ya tendo hilo la ukombozi kwa huyo mgerasi aliendelea kuishi chini ya vifungo vya shetani? Biblia haijaweka wazi lakini ukisoma Marko 5:19b-20 kuna maneno haya ‘…kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana na jinsi alivyokurehemu(kusamehe). Akaenda zake,akaanza KUHUBIRI….’ Kuhubiri maana yake kutangaza habari njema au matendo makuu ya kukombolewa kwake. Haiwezekani akatangaza habari hiyo njema kama bado yupo chini ya vifungo vya shetani. Mtu huyo alianza kutangaza habari njema ya wokovu alioupata baada ya kukutana na Yesu Kristo.

  Kwa mujibu ya majibu yako kwa Furaha deliverance ni maombi ya aina fulani aombayo au ajiombeayo mtu ili kupona tatizo au laana au ugonjwa unaomsumbua mtu huyo. Lakini biblia kwenye waraka wa Yakobo 5:16b inasema ‘Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii’ Neno ‘mwenye haki’ mimi nalitafsiri kama mtu aliyeokoka, anayeamini na kukiri kwa kinywa chake kuwa Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yake. Kwa maana nyingine asiyeokoka, ambaye bado yupo kwenye utawala wa shetani hana ‘haki’ maana hana mahusiano na Mungu hivyo hawezi kufanya maombi haya mpaka atakapoamua kukabidhi maisha yake kwa Yesu, ndio sababu biblia inasema mwenye haki wangu ataishi kwa imani.

  Nakubaliana na wewe kuwa maombi ya kikuhani(kuhani) yanafanya Mungu asamehe maovu na dhambi za watu wengine bila ya hao watu kuokoka(Kutoka 32:11-14). Ndio sababu wokovu ni wa mtu binafsi kwa mtu huyo kufanya uamuzi wa kumpokea Yesu ktk maisha yake ili nguvu ya Mungu iingie ndani yake kwa lengo la kumsaidia kuishi maisha ya ushindi.
  Kuhani anapofanya maombi, yanabadilisha au yanasitisha adhabu ambayo Mungu alikuwa aishushe kwa watu hao(kama ilivyotekea kwa Musa kwenye hiyo Kutoka 32:11-14), lakini maombi hayo hayabadilishi mwenendo wa maisha ya wale watu wanaombewa msamaha wa adhabu ambayo ingewapata. Wanaendelea kuishi maisha hayohayo ya dhambi mpaka hapo wao binafsi watakapoamua kumpa Mungu maisha yao ndipo huuvua utu wao wa kale na kuuvaa utu mpya kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

  Ndugu yangu Paul Holela, sasa nije kwenye swali lako la mwisho uliloniuliza mimi moja kwa moja kwamba Je, ni kweli kwamba tunaunganishwa na Kristo katika mwili wa nyama na damu? Ninashukuru kwamba wote tunakubaliana kwamba mtu ni roho aliye na nafsi hai na anaishi katika mwili, maana yake ni kwamba ili mtu akamilike lazima hivi vitatu(roho,nafsi na mwili) viwepo. Huyu anayeitwa mtu mwanzo aliumbwa akiwa hana dhambi hivyo alikuwa mtakatifu(roho,nfsi na mwili) na kwa utakatifu huo aliweza kuishi katika ulimwengu zote mbili bila shida yoyote. Baada ya mtu huyo kutenda dhambi au mtu anapotenda dhambi hutengwa au hujitenga na uwepo wa Mungu kwa kuwa Mungu(Baba=Mwana=Roho Mt) ni mtakatifu hachangamani au hakai mahali pasipo na utakatifu. Utengano huo hauwi kwenye roho tu au nafsi tu au mwili tu wa huyo mtu, utengano huo huwa ni complete kwenye roho na nafsi na mwili pia. Ndio sababu biblia inasema kuipenda dunia(dhambi) ni kuwa adui wa Mungu.

  Ili mtu huyu(roho,nafsi na mwili) aweze kurudisha mahusiano au kuungwa tena na Mungu au Kristo lazima afanye toba au uamuzi wa kuacha kile kilichosababisha utengano na kuomba rehema kwa Mungu kumrudisha Roho wake Mtakatifu ndani ya huyo mtu ambaye tumesema hakamiliki bila kuwa na roho, nafsi na mwili. Biblia kwenye injili ya Yohana 14:23 inasema ‘Yesu akajibu akawaambia, MTU akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, NASI(Baba,Mwana na Roho Mt)tutakuja kwake na kufanya makao kwake’ Tena biblia kwenye 1Korintho 3:16-17 inasema ‘Je hamjui ya kwamba NINYI(kanisa au mtu) ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu(roho,nafsi na mwili) yeyote akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamwangamiza mtu (roho,nafsi na mwili) huyo, kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi(mtu au kanisa lililookoka-nukuu kutoka Biblia Mpya ya NENO iliyotafsiriwa toka biblia ya kiingereza New International Version). Ukiendelea kusoma mlango wa sita mstari wa 17 wa Wakorintho hiyo hiyo utakutana na maneno haya ‘Lakini MTU(roho,nafsi na mwili) aliyeungwa na Bwana(Kristo) anakuwa roho moja naye’ Mstari wa 19 unasema ‘Je hamjui ya kwamba miili (ambayo ndani yake kuna roho na nafsi) yenu ni hekalu la Roho Mt (ambaye ni Mungu kamili), akaaye ndani yenu ambaye mmepewa na Mungu?’

  Kwa mistari hii michache toka kwenye biblia naweza kusema bila tashwishwi yoyote kuwa mtu hawezi kuungwa na Kristo katika roho peke yake au katika nafsi peke yake au katika mwili peke yake, lazima muunganiko huo uwe a complete set ili uweze kuona mafanikio yake sawasawa. Wapendwa wengi wamediriki kusema kuwa utakatifu ni rohoni tu, hiyo sio kweli, Kristo hawezi kukaa rohoni mwako wakati huohuo mwili wa nyama uwe umembeba shetani kwa maana ya kutimiza tamaa zake na kufanya mambo yaliyo kinyume na matakwa ya huyo aliyeko rohoni mwako, hivyo muunganiko lazima uwe katika vyote vitatu vinavyokamilisha huyo anayeitwa mtu.

  Nimejibu kutokana na nilivyolielewa swali lako kama nimejibu sivyo wewe ulivyokuwa umekusudia katika kuuliza swali hilo, tafadhali naomba nipe ufafanuzi ili tuendelee kujadiliana kwa utukufu wa Kristo Yesu na wala si kwa mashindano kana kwamba nani anajua zaidi ya mwingine. Nina furahi sana kila siku jinsi ambavyo ninajifunza mengi sana toka kwa wachangiaji wote kwenye blog hii, kuna mambo mengi ambayo nilikuwa siyajui, kuna mistari au maeneo mengi sana ndani ya biblia ambayo nilikuwa sijayasoma, lakini kwa michango ya wapendwa mbalimbali imeniwezesha kupita katika maeneo hayo na kupata ufunuo mpya kabisa katika maisha yangu ya wokovu.

  Utukufu na heshima ziwe kwa Mungu wetu atupaye kila siku roho ya hekima na ya ufunuo wa kumjua Yeye, nami naomba aendelee kutia nuru macho yetu ya ndani.

  Amen.

 60. Shalom ndg yangu Paul Holela.
  Nimebanwa kidogo na kazi lakini naandaa baadhi ya majibu ya maswali yako, hasa lile la mwisho uliloelekeza kwangu moja kwa moja,naomba uwe na subira.
  Ubarikiwe na Bwana.

 61. Amen kaka Emmanuel,unajua wokovu wangu nimekulia katika huduma ya maombezi, nimewaona wengi, wengine anafuguka kwa ile imani tu ya kusogea kanisani yaani toka mlangoni kuleee anakwambia ghafla akasimama na kuweza kwenda mwenyewe bila hata mtu kumsalisha sala ya toba wala kumwombea ni ile imani yake. nimeona wengine wakija wakiwa hoi wakitubu wakikaa katika wokovu lakini wagonjwa kitandani au wanatembea (kansa, UKIMWI, kupooza) hadi wanakufa katika wokovu.
  Binafsi niliokoka nikiwa naishi mwenyewe bila mume wala kuwa na mwamnaume karibu miaka 5 lakini pamoja na kutubu na kumpokea Yesu na sala ya toba, kama mwezi niliendelea kuota ninalala na mtu, sikuwa na uwezo wala ufahamu wa kukataa nikiwa usingizini, lakini baada ya kama mwezi hivi nilishangaa alipooniinamia nikawana uwezo wa kwanza kumuona kama mtu, pili nilipata nguvu ya kumsukuma toka juu yangu, alisimama hewani juu ya kitanda kwa muda na kuondoka, nilikaa baada ya muda tena alinitokea na kunishika mkono nikamwambia unanipeleka wapi? akaniachia ghafla toka hapa sijawahi kuota hivyo ni zaidi ya miaka 5 sasa. ndio maana nakubaliana na Paul kwamba, ukiokoka na kuwa na Yesu nafsi inaweza kuwa katika vifungo (possesed) lakini sio chini ya (oppressed) kwasababu vitu kama roho za uchungu, hasira, wivu, tamaa vimo sana katika walokole na nadhani ni vitu vya kujibidiisha kwa maombi uvishinde au visikupate
  Nakubaliana na wote pia kuwa ni Jina la Yesu na damu ya Yesu tu ndivyo vitakavyotukomboa ila ukishindwa mwenyewe sio vibaya kuomba watu wakuweke kwenye maombi au wakuwekee mikono.Efeso 6: 10-19 ni ishara tosha kuwa ukristo ni vita na pia tunatakiwa kuombeana. Tunajifunza

 62. Sharom

  Asante dada Rose nimekua nikifuatilia mchango wako ktkt hii mada nikagundua kua hata mimi ni nge cha ngia kama wewe

  Ila mimi napenda kuongeza kwa kusema kama ulivyo sema hapo mwanzo kwamba kinacho okoka ni roho sio mwili ndio maana utaona watumishi wengi ktk Agano la kale kama akina Daudi walikua na Roho wa Mungu na walipakwa mafuta lakini miiili ilikua na vifungo vya tamaa
  Nahii inatokana na Maisha tulio kua tukimtumikia shetani na mikataba tulio ifanya pamoja na wazazi wetu kwa kujua au kuto kujua kwa miaka mingi tulio ishi kabla ya kuokoka kitucha msingi ni kwamba hata kama mtu ata fanya maombi ya ukombozi bado ni kwamba yesu ndio mhusika mkuu nijina la Yesu na damu ya Yesu ndivyovinavyo tumika kutukomboa si vinginevyo

 63. Amen dada Lisa hili la kutubu na kujifungua kutoka laana za mababu pia alishafundisha Mwl Mwakasege katika semina moja kama Malango, na kwakweli ukiangalia kuna wapendwa walioamini na wanajitahidi kila namna kuliishia neno ila utakuta vitu fulani vya kiukoo wao haviwaachii, ndio mimi naona kuna umuhimu mtu mwingine kukuombea au kukuwekea mikono kama Yakobo alivyosema (wawekewe mikono) ila havitakurudia iwapo utasimama ktk neno. Nimeishaiona hii kwa kijana aliokoka akitokea uganga wa kienyeji, vitabia fulani viliendelea kumsumbua hadi ilibidi aombewe ndipo aliacha(roho za mababu) Mbarikiwe

 64. Mwisho ni kwamba Agano la kale linatupa maarifa nini cha kufanya. Kwa mfano walipotubu walisafishwa kwa damu za wanyama lakini sisi tunayo Damu ya Yesu. tunaomba Mungu anatusafisha kwayo.

 65. BWANA BWANA YESU ASIFIWE SANA!!!

  Nanukuu kwa Glady
  Ndugu Lisa ktk mchango wake wa tarehe 26 May amesema kwamba mtu anatakiwa …..atubu kwa ajili ya dhambi ya mababu na vizazi vilivyopita (hata mm nadhani kuna mahali nimeshawahi kufanya hivyo)lakini napata wazo kuwa je hii si kama ibada ya wafu??

  Naomba nichangie kwa kusema hii si ibada ya wafu labda kwa jinsi msomaji atakavyotafsiri.

  Tukiangalia 2Samweli 21:1-3 Kulikuwa na njaa siku za Daudi kwa miaka mitatu. Daudi anamwuliza Mungu na kujibiwa ni kwa sababu ya nyumba ya Sauli yenye damu kwa kuwa aliwauwa Wagibeoni. Kuna mambo ilibidi daudi ayafanye ili kufuta ile njaa.
  Kama babu yako aliuwa, alitambika, aliua pacha mmoja, haiishii kwenye kuokoka peke yake soma neno la Mungu likupe maarifa nini cha kufanya. Zamani shida kama hizi zilitolewa kwa kutumia damu za wanyama (Walawi 16:1-…….) lakini sasa tunayo damu ya Yesu.

  Kuna somo lingine la kutoka Nehemia 1:5-9Nehemia anakiri kuwa yeye na nyumba ya baba yake wamefanya dhambi. Mimi naona hapa Biblia inaposema BABA ZENU HAIMAANISHI LAZIMA YULE ALIYEKUZAA HALAFU YUKO HAI. Ni mlolongo wa vizazi na vizazi. Baada ya maombi haya yaliyounganisha vizazi/ mababa wengi Nehemia alipata kibali cha kwenda kuujenga Yerusalemu. Kuna neno pia linasema BABA ZENU WALIKULA MANA JANGWANI WAKAFA LAKINI MIMI CHAKULA CHA UZIMA. Baba zenu wanaotajwa hapa si kwamba ni yule aliyekuzaa bali alishapita, hapa ni issue ya lugha.

  Kitabu cha Ezra 9:7 Wakati wana wa Israeli wanatoa dhabihu ya jioni baada ya kuijenga madhabahu ya Bwana Ezra anatubu kwa kunyenyekea mbele za Bwana na kudhihirisha kuwa tangu siku za baba zao wamefanya hatia hata leo. Nasisistiza baba anayetamkwa hapa si yule ambaye in real amekuzaa au yuko hai. Ezra anatubu si kwa kosa lake tu hata la zamani hizo za baba zake.

  Katika kitabu cha Yeremia 1:1-3 Neno lilimjia wakati Yerusalemu umetekwa may be walikuwa uhamishoni. Katika Yermia 2: 4- 5 Mungu anamkumbusha Israeli kupitia Yeremia kwamba baba zao walifarakana na Mungu. Kwa hiyo hali iliyowapata Israeli wakati ule ilitokana na dhambi ya baba zao. Mstari wa tisa Mungu anasema NITATETA NANYI NA WATOTO WA WATOTO WENU. Uovu unapatilizwa kwa baba hadi mjukuu.
  Yeremia 2 : 23 Wawezaje kusema sikutiwa unajisi …..itazame njia yako ya bondeni ujue uliyoyatenda.

  Neno pia linasema Nitawapatiliza wana uovu wa baba zao tangu kizazi cha tatu hadi cha nne.

  Pia kuna mstari usemao Mungu anatafuta atakayelijenga boma.

  Nashawishika kusema kuwa hata kama umeokoka lakini kuna mambo ya machukizo yanaweza kukuandama. Lakini utakapostuka na kulijenga boma kwa kutumia damu ya Yesu mambo hayo ya machukizo yataacha kukuandama nawe utakuwa umeng’oa ule mzizi.

  Kwa mtazamo wangu kuhusu huduma ya Ukombozi yawezekana ni matamshi tu yaliyobase kwenye Lugha zaidi. Wengine waweza kuiita maombi lakini wanafanya kitu kilekile.

  Bwana Yesu asifiwe!!

  Tunajifunza

 66. Shalom,

  Naomba niyajibu maswali ambayo John Paul ameyakumbusha kutoka kwa Mpendwa Furaha na Shoo GAP.

  Tuanze na ya mpendwa furaha…
  1. Bwana Yesu ktk huduma yake aliwafungua watu wengi waliofungwa na nguvu za giza… mfano ni yule mgerasi… na mitume pia walifanya hivyo …shida hapa ni kuichukulia deliverance kama huduma na unataka uifananishe na uchungaji au uinjlist na nk… ukimwombea au ukimfundisha mtu aliyefungwa akafunguliwa huo ndio ukombozi wenyewe…. Biblia imejaa historia tele za ukombozi… Yesu alisema Mungua amempaka mafuta kuwafungua waliofungwa……

  2. Mtu aliyefunguliwa na kufundishwa kwenye eneo fulani la maisha yake… akajue kuitumia nafasi aliyo nayo na mamlaka ktk Kristo kwenye eneo hilo hawezi pata shida…Ila nilishatungulia kusema mwanzoni si shida zote zinahihitaji aina hii ya maombi…

  3. Maombi ya deliverance yanaweza kumsaidia mtu kuishi maisha matakatifu… nitakupa mfano … mtu ambaye anatokewa na majini mahaba halafu anazini kwenye ndoto… je huyu akifunguliwa hutakuwa umemsaidia kuwa msafi?… Yuda 1:8…….. Uliza wakwambie walokole wanaotokewa na haya majambo ni wangapi? Nimeshaomba na kuwafundisha wengi wenye hili tatizo na ni walokole…

  Ndugu Shoo GAP,

  1. mtu anaweza kufunguliwa kwenye maeneo ya maisha yake kabla na hata baada ya kuokoka…. sawa na kuponywa unaweza kuponywa na Mungu ukiwa umeokoka na wengine hawajaokoka ila Mungu anawaponya…
  Cha msingi ni kuyashughulikia maeneo yote ambayo Mungu anakuonyesha yanaweza kukuletea shida au mwenyewe umeona ……
  2.Mtu yoyote mwenye imani na anayejua kuomba anaweza kuwaombea au kujiombea aina hii ya maombi..
  3. Vyote Neno na Maombi vinatumika
  4.Yeye mwenyewe atapoona anashuhudiwa ndani yake kuwa yupo sawa….

  Dada furaha naomba nijibu maswali uliyoyaelekeza kwa dada Lisa…

  Nikianza na huu utangulizi wako nimeupenda sana…… akiokoka na akaendelea kujifunza neno kwa usahihi…..
  vipi kama asipojifunza neno kwa usahihi?… maana yake laana vifungo vitamtesa…. je time inayo elapse wakati anajifunza neno inakuwaje?…jibu ni anakuwa katika shida … akipata neno sahihi anatoka kwenye hiyo shida thats deliverance kwa neno……

  Kauli yako ni nzuri sana HAKUNA LAANA WALA VIFUNGO VYA UKOO VINAWEZA KUKUPATA… kama hukuwahi kuwa umefungwa nakubaliana na wewe kuwa haviwezi kukupata labda uende ukatambike ili vikupate….

  1.Nafikiri inakupasa kuelewa maana halisi ya maombi ya Toba… ni maombi ya kuomba rehema kwa ajili ya uovu, dhambi na makosa ili kuleta ulinganifu/kumlingana Mungu kwenye hilo eneo ambalo limehasilika kutokana na uovu…. pata muda kama unapenda kujifunza fuatilia maombi ya kikuhani kuna vitu utavielewa hapa…

  Unaweza ukaomba rehema/ukatubu juu ya uovu, dhambi na makosa ya watu wengine unaposimama ktk nafasi ya Ukuhani…

  Angalia daniel 9:4-15 Neh 1:6
  Daniel anatubu ouvu na dhambi zake + wenzake+ baba zake waliokufa.. hawaombei waokoke ila Mungu aufute uovu waliofanya ukasababisha waende utumwani……
  Mungu akiwasamehe tu anaondoa shida inayotokana na huo uovu Zab 103:3…akusamehe uovu ….kuponya magonjwa yako…
  Panatofauti kati ya Dhambi, makosa na uovu angalia kutoka 34: 7……., uovu, na makosa, na dhambi… hii kauli kaiongea Mungu hajakosea kudadavua hapa na pia angalia Isaya 53:5 …..alijeruhiwa kwa makosa…. alichubuliwa…..maovu. . jiulize maswali kwanini wametofautisha uovu dhambi na makosa?….. uovu unasababisha shida inayotembea kwenye vizazi….
  Turudi kwenye swali lako …nawe jiulize je daniel aliabudu wafu? jibu utakuwa umepata..

  2.Jiulize haiwezekani kuwaombea msamaha/rehema watu wengine na Mungu akawasamehe? je anapowasamehe wanakuwa wameokoka? je unaujuzi wa maombi ya nafasi ya ukuhani?
  Huwa wanaomba Mungu aufute uovu ambao unasababisha madhara kwa wengine…

  3.Mungu hata muhukumu mwana kwa ajili ya uovu wa baba ila madhara ya uovu wa vizazi vilivyotangulia vinaweza kuwaathiri watoto kama wasipishughulikia….

  Siku moja nilikuwa naangalia Miracle highlight ya Pastor Benny Hinn zamani kidogo akaletwa mama mmoja alipofika kwa Benny Hinn, Benny akasema kwa ufunuo kwamba mababa zako waliabudu miungu…akaomba Baba tusamehe kwa uovu huo…akamwomea huyo ama akafunguka…

  4. Uovu usiposhugulikiwa kwa toba unaleta shida …..haijalishi agano lipi? uovu unaweza fanyika kwenye nchi ukadhuru hata walokole…angalia jirani zetu waliopigana wenyewe kwa wenyewe kama walokole walipona……

  Ili kuendelea kuijifunza kuna maswali nataka niyaulize humu anayeweza kujibu kwa mtazamo wakibiblia atusaidie…

  1.Kwanini Bwana Yesu aliwaombea Wanafunzi watakaswe kwa ile kweli yoh 17:3….wakati walisha amini tayari

  2.Mtume Paul alimaanisha nini alipowambia warumi waliokuwa wameamini tayari ktk War 12:2…..mgeuzwe nia zenu… je unaweza ukaamini na nia yako isimwelekee Kristo?

  3. Je wapendwa waliookoka…hawazini, sio waongo…hawanywi pombe….wala hawaibi….maisha yao ni ale nini? avae nini? akae wapi? Nia zao zimemwelekea Kristo? mtazamo wao ni(maisha ya kawaida- natural realm) Je wameokoka?

  4. Unajuaje ugonjwa huu ni nguvu za giza au sio?

  5. Ni sawa/haki kulingana na neno la Mungu wapendwa watu waliookoka kuwa na magonjwa? ( kwa chanzo chochote, demonic au natural)

  6. Je asili ya Magonjwa si nguvu za giza direct au indirect?

  7. Mtu ambaye anarekebishwa mfano kutoka kwenye tabia labda ya majivuno na anakubali anaiacha… kabla ya hapo alikuwa hakuokoka? maana majivuno ni kuwa nje ya upendo kwa mujibu wa 1kor13:4-7.

  8 Kama magonjwa ni haki yetu je kazi ya kupigwa Bwana Yesu ni Bure?

  9.Kama magonjwa si haki yetu ktk Kristo Yesu….Wanaoumwa hawajaokoka?

  10.Je Mtu ambaye anadai ameokoka halafu wanaweza gombana na mumewe wasiongee siku 3 wakiwa kitanda kimoja Je mtu kama huyu ameokoka? Je hawezi kuingiwa na mapepo?

  11.Je Mtu ambaye hajui TRUTH ya mamlaka na privileges ktk Kristo na kuzitumia (exercising authority) hawezi kukandamizwa na nguvu za giza?

  12.Mtu ambaye hajui kuitumia imani kama ngao dhidi ya mishale ya adui efeso 6:16… je mashetani wakipiga mishale haitampata kwa sababu ameokoka? na ikimpata tukamwombea akalipuka pepo atakuwa hajaokoka?

  13 Je Mtu ambaye ni mjivuni( hawezi ku-appreciate kazi, vitu , mafanikio ya wengine ila yeye tu ndio bora na vya kwake tu ndio bora) mfano labda umejipinda ukajenga nyumba ya 80 Million anakuja kwako anaongea hivi aaah sio mbaya kwa kuanzia yaani hawezi kusema hongera… wakati yeye hana hiyo nyumba…Je mtu wa tabia ya namna hii kaokoka? na kama ameokoka je kazi ya msalabani haikutosha kuondoa hii tabia maana yote yamekuwa mapya?

  14. Je wapendwa ambao ni wasengenyaji Wameokoka? je hawawezi kuingiwa na pepo wachafu kwa kuwa waliongozwa sala za kuokoka?

  15. Je ni sawa kibiblia mpendwa kuharibu mimba au mtoto kufia tumboni? je hizi sio kazi za mapepo? je watu ambao wamewahi kuharibu mimba au watoto kufia tumboni Wameokoka?

  16.naomba mnisaidie kuilewa warumi 7:14-25

  17.Ndugu hagai Je ni kweli tumeunganishwa na Kristo ktk Mwili wa nyama na Damu?

  Mungu awatunze wote wasomaji na wachangiaji

  Mungu akinipa neema kwa faida ya wasomaji nitaandika kwa undani ili wengi waelewe kuhusu roho, mwili na nafsi… wakati mwingine….

 67. Wapendwa,
  Ndugu yetu John Paul amekumbusha maswali muhimu sana yaliyoulizwa na wachangiaji wengine.Kitu ninachoomba maswali hayo yasionekane kuelekezwa kwa ndg yetu Paul Holela tu, bali yawe kwa kila anayeweza kujibu na kufafanua ili tuendelee kujifunza zaidi.Pia sio lazima mtu akajibu yote, kama anaweza kutueleza au kujibu mojawapo ya maswali hayo ni vema maana tutakuwa tumepata kitu cha kujifunza.
  Atukuzwe Yeye atupaye neema hii ya kumjifunza na kuona ukuu wake kila siku.
  Mbarikiwe sana.

 68. Mpendwa Paul,

  Ninashukuru kwa majibu ya maswali ambayo niliuliza katika mchango wangu uliopita. Maswali hayo niliyauliza ili kuweza kufahamu, kutoka kwako, kama KILA TATIZO NI KIFUNGO. Mfano umasikini, ugonjwa na matatizo mengine. Lakini kutokana na majibu yako nimeendelea kuelewa kwamba SI KILA TATIZO LINATOKANA NA NGUVU ZA GIZA. Matatizo mengine ni ya kibaiolojia,kifisikia na kikemikali na ambayo ufumbuzi wake uko ndani ya ujuzi wa kibinaadamu. Majibu yako yameweka balance ili tusije halalisha kila tatizo kwamba ni kifungo. Hicho kitakuwa ni kifungo cha kujifunga wenyewe! Hadi sasa tumeona kwamba si kila tatizo linalompata mtu aliyeokoka linasababishwa na nguvu za giza. Mengine yanatokana na ukosefu wa uelewa wa baadhi ya mambo katika maisha ya kila siku,[kama vile elimu, bidii] sawa tu na mtu ambaye hajaokoka.

  Kuna maswali ambayo yaliulizwa na wachangiaji ambayo hadi sasa hayajajibiwa. Mimi nimekuwa nikisubiri kwa hamu ili niweze kujifunza. Kama inawezekana naomba utusaidie kuyajibu kutokana na uzoefu ulio nao katika suala hili. Japo yapo huko juu ninaona ni vema nikayanukuu tena.

  Furaha ameuliza hivi:

  1. Ni wapi ktk kanisa la kwanza/ Agano jipya tunaona huduma ya deliverance hasa baada ya kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo?
  2.Na je wapendwa wanaofunguliwa huwa hawapati tatizo tena ktk maisha yao kimwili, biashara nk?
  3. Je deliverance/ maombi ya kuwafungua vifungo huwasaidia wanaoombewa kuishi maisha Matakatifu?

  Na ndugu Shoo GAP ameuliza hivi:

  (1) Kama maana ya Delivarence kwa kiswahili ni Ukombozi au kufunguliwa; Ni wakati gani inapaswa ifanyike delivarence? Kabla, wakati au baada ya kuokoka, inafanyika mara ngapi kwa taratibu gani?
  (2) Watu gani wafanye hiyo delivarence? Hao wanaofanya delivarence wao je wanahitaji wafanyiwe delivarence? au walishafunguliwa kabisa?
  (3) Kati ya Neno la Mungu na Maombi ni kipi muhimu kuliko jingine katika kufanya delivarence? Kumbuka tunaomba kwa sababu Mungu ametuambia tuombe katika Neno lake.
  (4) Kipimo gani kitumike kujua kuwa huyu tayari ameshafanyiwa delivarence?

  Tuendelee kujifunza!

 69. Shalom wapendwa,

  Ninamshukuru sana Mungu katika Jina la Yesu Kristo, kwa ajili ya mada hii nzuri ambayo kwa ujumla wake imekuwa changamoto kwetu tuliookolewa. Mada hii nimekuwa nikiifuatilia kwa makini sana tangu ilipoanza; karibu kila aliyechangia nimeweza kuusoma mchango wake. Kwa kweli nimejifunza mengi na nazidi kujifunza mengi katika mada hii. Kwa mtazamo wangu, mada hii nimeiona kuwa inaweza kuwa ni sehemu ya ufunguo wa yote ambayo tumekuwa tukiyajadili mahali hapa siku hadi siku, kuhusiana na maisha yetu ya wokovu.

  Baada ya hayo, nami pia nimeona nichangie kile ambacho hata hivyo hakitakuwa na tofauti kubwa ukilinganisha na yale ambayo tayari wengine wamekwisha changia.

  Nikianzia na swali la, kwa nini mtu aliyeokoka anaweza kuendelea kuwa katika vifungo vya Ibilisi:- Kwa mtazamo wangu ni kwamba, ni kweli mtu aliyemwamini Yesu Kristo anaweza kuwa bado katika vifungo vya Ibilisi au akawa bado katika matatizo ya kimwili na kiroho. Sababu kuu (ambayo wengi wameielezea) inayoweza kumfanya mtu kuendelea kuwa katika hali hii ya kukosa baraka za Mungu ni moja tu, nayo ni kukosa Neno la Mungu ndani ya mhusika.

  Mtu kama hana Neno la Mungu ndani yake, hata kama atafanyiwa hiyo ambayo tunaiita deliverance, bado mhusika ataendelea kuteseka japo kwa sehemu katika hatua za mwanzo baada ya kuombewa, ataweza kuona kama anapata nafuu, lakini nafuu hiyo haitadumu muda, atarudia tena katika hali yake ya mwanzo. Deliverance ni sawa na maombezi ya kawaida tu kwa mtu mwenye shida, ndivyo ninavyolitazama neno hili “deliverance”.

  Mtu mwenye mapepo kwa mfano, au mwenye shida yoyote ya kimwili au kiroho, akifanyiwa maombi kwa mamlaka ya Jina la Yesu Kristo, mapepo au matatizo ya mtu huyo iwapo ni magonjwa au vinginevyo huweza hutoka kwa wakati ule. Hii itafanyika kwa sababu tu ya imani ya muombaji, lakini mtu anayekuwa ameombewa, iwapo baada ya kuombewa hatafundishwa Neno la Mungu la kumsaidia kujua nini chanzo cha tatizo lake, na nini cha kufanya ili tatizo hilo lisijirudie tena, baada ya muda kidogo tu kuna uwezekano mkubwa wa lile tatizo kurudi tena.

  Yesu Kristo katika huduma yake, wakati fulani alimwombea mtu mmoja, na baada ya kumwombea alimwambia kuwa amekuwa mzima asitende dhambi tena. Maneno hayo “umekuwa mzima usitende dhambi tena” tunaweza kuyaona katika kitabu cha, Yohana 5:13-14, ambayo kimsingi yalikuwa ni fundisho kwa mgonjwa aliyeombewa ili kuufanya muujiza wake udumu. Maandiko hayo yanasema hivi,[Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale. Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, ANGALIA UMEKUWA MZIMA; USITENDE DHAMBI TENA, LISIJE LIKAKUPATA JAMBO LILILO BAYA ZAIDI]. Yesu anamwambia aliyekuwa mgonjwa usitende dhambi tena! Maneno haya ni mafundisho kwa aliyekuwa mgonjwa kwamba iwapo anataka muujiza wake udumu alitakiwa kuacha dhambi kabisa. Hapa mimi najifunza kuwa kumbe, kuna vifungo vingine vinaweza kuwapo kwetu kwa sababu tu ya dhambi au kutolijua Neno la Mungu.

  Kuhusu umasikini kwa watu tuliookolewa:- Kwa ujumla nijuavyo mimi, mtu aliyeokoka na kukaa katika kweli yote, anaweza kuwa masikini wa mali za hapa duniani, au pia anaweza kuwa tajiri wa mali za hapa duniani kama ambavyo mchangiaji moja ameelezea hapo juu. Hii ni kwa sababu hatuokolewi ili tuwe matajiri hapa duniani au pia hatuokolewi ili tuwe masikini hapa duniani japo maandiko mengine yanatufundisha hivyo, lakini lengo kuu hasa la wokovu wetu hapa duniani ni ili siku moja tuje kuurithi uzima wa milele kule mbinguni; hilo ndilo lengo kuu la wokovu wetu.

  Tunapokuwa hapa duniani tunaweza kuwa na utajiri au tusiwe nao, lakini pale tunapoukosa utajiri huku tukiwa katika Neno la Mungu, tusidhani kuwa tumeukosa utajiri au baraka kwa sababu labda tuna laana na tunahitaji deliverance, na wala tusidhani kuwa kukosa kwetu mali kumeletwa labda na dhambi, la hasha. Umasikini au utajiri kwa hapa duniani ni mambo ya kupita tu, ndiyo maana kwa neema ya Mungu tunapokuwa masikini, amani ya Kristo ambayo alituahidi hutufunika. Tunapougua magonjwa, amani ya Kristo aliyotuahidi hutufunika, tunapokuwa na kila hitaji la mwili hapa duniani, pale tunapolikosa hitaji hilo, bado amani ya kristo huendelea kutufunika. Magonjwa, shida, kukosa mahitaji tunayoyatamani siyo kigezo cha sisi kuwa tuna laana. Tukikosa yote haya, kipimo chetu kikuu kiwe ni amani ya Kristo ndani mwetu. Iwapo pamoja na mabaya hayo tunakuwa na amani, basi tujue kuwa hayo ni mapito tu, tuzidi kukaa katika Neno na mwishowe tutaziona baraka kama alivyoziona Ayubu.

  Yesu Kristo mwenyewe alituahidi amani, hakusema kuwa kila kitu kitakuwa mteremko, la hasha, ndiyo maana hata Yeye alikufa kifo cha msalaba huku akiwa na amani hadi mauti. Andiko moja wapo linalotuahidi amani tunaliona katika, Yohana 14:17 nalo linasema, [AMANI NAWAACHIENI; AMANI YANGU NAWAPA niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, WALA MSIWE NA WOGA!]. Wala msiwe na woga! Mtu aliye katika kweli, anayeijua kweli ya Neno la Mungu, hawezi kuwa na woga, wala hofu, wala mashaka. Iwapo atapatwa na lolote lililo baya kwa vipimo vya macho ya kibinadamu, hatababaika kwa sababu atafahamu kuwa dhiki aliyo nayo ni nyepesi na ni ya muda tu, na pia atafahamu kuwa hapaswi kuangalia vinavyoonekana, bali visivyoonekana, kama tunavyoweza pia kusoma katika maandiko, 2Wakorinto 4:17-18, ambapo tunasoma, [Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele].

  Hivyo mtu wa namna hii, yanapomtokea matatizo ya namna yoyote ya aina hii, atafarijiwa na Neno kama hilo, kwamba ni ya muda tu ili mradi yupo katika Kweli yote.

  Tofauti na mazingira ya umasikini au shida kwa watu wa Mungu, umasikini au shida ambazo zitatokana na Ibilisi hazina amani ndani yake, ndani ya mtu huyo ni woga, hofu, mashaka, wasiwasi kutokuamini n.k. Hii ni kwa sababu Neno la Mungu halipo ndani yake, na mtu mwenye shida za aina hiyo anahitaji Neno, na siyo deliverance au maombezi peke yake, japo yatasaidia lakini ni kwa muda tu. Mtu asiye na Neno ndani yake, kila tatizo linapomjia ataona suluhisho kubwa kwake ni kwenda kwa mtumishi wa Mungu.

  Kuhusu Majini kwa mtu aliyemwamini Yesu; ni kweli mtu aliyemwamini Yesu bado anaweza kuwa na majini ndani yake. Tatizo la kuendelea kuwa na majini japo mtu amemwamini Yesu, sababu zake ni hizo hizo nilizoziandika hapo juu; kutokuwa na Neno la Mungu. Anaweza kuombewa na watumishi wa Mungu wenye mamlaka ya Kristo na ikaonekana yale mapepo yametoka, lakini kama muhusika hajajua ni nini kiini cha tatizo alilonalo na anapaswa kufanya nini, baada ya muda mchache tu yale majini hurudi tena kwa yule mtu.

  Tunaweza kuona maandiko yanayohusiana na jambo hilo katika, Luka 11:24-26, ambapo tunasoma, [Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,NITARUDIA NYUMBA YANGU NILIYOTOKA. Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA, WALIO WAOVU KULIKO YEYE MWENYEWE, WAKAINGIA NA KUKAA HUMO; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza]. Unaona!, maandiko haya yanatuonesha jinsi ambavyo mapepo yanavyoweza kurudi tena kwa mtu ambaye tayari alishaombewa. Kumbe hapa mtu huyu baada ya kuombewa alipaswa kufundishwa namna ya kuiacha kabisa dunia na anasa zake. Angefundishwa hivyo mapepo hayo baada ya kutaka kumrudia yangekuta mlango umefungwa. Lakini yanaporudi na kukuta nyumba yake ipo safi na imepambwa na dhambi ni rahisi sana kuingia na kuendelea kumtesa mtu huyo.

  Mtu aliyeokoka na kulijua Neno na akawa mtendaji wa Neno, mapepo au majini yanamtambua, ndiyo maana wale wana wa Skewa Muyahudi, waliojaribu kulitaja jina la Yesu ili majini yaondoke kama tunavyosoma katika Matendo ya Mitume 19:13-16, kwa sababu majini wanawajua watu wa Mungu, Wale wana wa Skewa kwa vile walikuwa hawaishi sawasawa na Kristo, waliraruliwa na kuchaniwa nguo zao na waliondoka mbio huku wakiwa uchi na kujeruhiwa. Kwa nini waliraruliwa, ni kwa sababu majini yanawajua watu wa Mungu na wasio.

  Jambo la msingi pia katika yote haya, tunatakiwa kufahamu kwamba, wakati mwingine majini nayo yanaweza kutuonea na kutukosesha baraka bila sababu sisi tuliookolewa. Yanafanya hivyo ili tuiache imani, yaani tukate tamaa tuone kama Mungu tunayemwabudu hayupo au hawezi kutusaidia. Iwapo hatuzijui haki zetu, majini huchukua loophole hiyo na kutunyanyasa yapendavyo. Na haki hii hatuwezi kuifahamu kama hatujajifunza Neno la Mungu kwa ukamilifu. Matatizo mengi kwa watu tuliookolewa ambao tunakaa katika kweli yote, yanaweza kuondolewa kwa muhusika kwa kuomba kwa kuzitaja ahadi za Mungu ili shetani asikie; akisikia atakimbia kwa kuwa atafahamu kuwa tumemgundua kuwa hana kitu kwetu, lakini deliverance bila muhusika kumfundisha Neno la Mungu, atazidi kutaabika.

  Shalom wapendwa.

 70. Mpendwa ndg yangu Paul Holela,

  Ninakushukuru sana kwa ufafanuzi wako kuhusu roho,nafsi na mwili vinavyokamilisha kitu kinachoitwa mtu.Ninajua hakika kwamba ili mtu aitwe mtu lazima awe na vitu hivyo vitatu yaani roho, nafsi na mwili.

  Lakini nataka kukumbusha kwamba toka anguko la Adamu pale kwenye bustani ya Eden, mwili na roho vilikosa mawasiliano ya kufanana, hapo ndipo pakawa na kutokuelewana kati ya mwili na roho.Kazi kubwa ya nafsi ni kama mkalimani(translator) kati ya lugha ya mwili na roho ili mwili na roho viweze kufanya kazi kwa maelewano.Ndio maana mtume Paulo kwenye Efeso 2:1-3 anaeleza jinsi dhambi na maovu mengine yanavyotufanya tuwe watoto wa mfalme wa anga na kutenda matendo yanayomtukuza shetani.Lakini nataka tuuangalie kwa makini mstari wa 5 unaosema “hata tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu,ALITUHUISHA pamoja na Kristo…” Hapa tumehuishwa roho,nafsi na mwili. Kumbuka pia kuwa nafsi nayo ina milango ya fahamu ijulikanayo kama UAMUZI(willingness), HISIA(emotion) na MAWAZO.Kwa hiyo mtu anapookoka maana yake anamruhusu Yesu Kristo kwa njia ya Roho Mtakatifu kutawala hii milango mitatu ya nafsi ili pia atawale roho na mwili wa huyo mtu.Hilo linaelezwa vizuri sana na maneno ya mtume Paulo kwa Waefeso 2:10 anaposema ‘Maana tu kazi yake,TULIUMBWA katika Kristo Yesu, TUTENDE MATENDO mema,ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo’.Kwa mstari huu siamini kwamba mtu anapookoka kwa kumaanisha hasa kumpokea Yesu na Roho Mtakatifu kuwa ndani yake,basi wokovu huo utakuwa wa taratibu ukianza na roho,halafu ukae muda tena abadilishe nafsi yake kisha tena akae muda abadilishe mwili(matendo ya mwili).Kwa lugha nyingine unataka kuniambia kuwa mtu atakuwa amegeuzwa nia na kuwaza kwake kwa ndani(wokovu wa rohoni) halafu akaendelea kufanya zinaa, ulevi na uchafu mwingine wote wote(matendo ya mwili)kwa sababu process ya kuokoa mwili haijafika bado!! Hii ni ajabu.Ninachojua tunatoka imani hadi imani na utukufu hadi utukufu(2Korintho 3:18) kwa sababu kuna ngazi mbalimbali za imani na kiwango tofauti tofauti cha utukufu.Kila mtu aliyeokoka anaweza ku-experience kiwango tofauti cha utukufu wa Mungu kwa kadri ya kiu aliyonayo ya kumtafuta Mungu, maana yake ni kwamba utukufu wa Mungu unaweza kukufunika kweli kweli mahali na wakati fulani lakini wakati mwingine ukaona kama vile Mungu amenyamaza kimya unaona kiwango kidogo tu cha utukufu wake.

  Nilichotaka kukieleza ndg yangu Paul Holela ni kwamba pale mtu anapoamua kweli kweli kwamba Bwana Yesu akamate usukani wa maamuzi yako, hisia zako na mawazo yako(yaani anapookoka au anapoamua kutubu kwa kuongozwa sala ya toba au anapozaliwa mara ya pili) badiliko hili linakuwa ni complete set yaani rohoni, nafsini na mwili lazima utii maana mtu wa ndani anakuwa ametiwa nuru, huyu mtu wa nje(mwili) hana namna ya kumkatalia mtu wa ndani.

  Neno toka Galatia 5:17 linalosema ‘Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka’ linahusu Roho Mtakatifu na miili yetu kwa sababu neno ‘Roho’ limeandikwa kwa kuanza na herufi kubwa kinyume na ‘roho’ zetu ambalo huandikwa kwa kuanza na herufi ndogo(najua hujanukuu neno hili ila nataka wasomaji wengine waone wanaposoma mstari huu).

  Lakini ukiendelea kwenye chapter hiyo hiyo ule mstari wa 24 unasema hivi ‘Na hao walio wa Kristo Yesu(waliokoka, waliozaliwa mara pili)wameusulubisha mwili pamoja na MAWAZO yake mabaya na tamaa zake’ N.b maneno ya kwenye mabano ni yangu.Kwa mantinki hiyo pale tu mtu anapojitoa kuwa wa Kristo Yesu(kumbuka kuamua kuwa mali ya Kristo ni hiyari ya mtu) anakuwa ameutiisha mwili wake kufuata matakwa na mapenzi ya Kristo, sijui kama kitendo hiki kinafanyika taratibu kwa kuacha matendo mafu moja baada ya lingine yaani unaacha uzinzi leo unaendelea kulewa kwa miezi sita halafu ndipo unaacha.Zaburi ya 103:3 unaeleza wazi nini kinatokea pindi Mungu anaposamehe dhambi za mtu, hebu tusome ‘Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote’ Hapa neno magonjwa linaweza kutafsiriwa kuwa na maana ya shida au taabu au mahangaiko mbalimbali.

  Mungu ni mtakatifu kadhalika Roho wake, ndio sababu anaitwa Roho Mtakatifu.Kwa utakatifu huo kamwe hawezi kuchangamana au kukaa mahali ambapo sio patakatifu.Hapa nina maana kuwa Roho Mtakatifu hawezi kukaa kwenye roho ya mtu ambaye bado anatenda matendo ya giza yaani mwili wake na nafsi yake bado vimeshikiliwa na mfalme wa giza kamwe hawawezi kuchangamana,ndio maana biblia inasema kuna shirika gani kati ya nuru na giza? Pia biblia kwenye 1Kor 6:17 inasema ‘Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye’ Tunaungwaje na Bwana?, kwa kuzaliwa mara pili na sidhani kama tunaungwa roho tu bali biblia inasema ‘yeye’ yaani mtu=roho, nafsi na mwili.

  Nimesema hata kwenye mchango wangu wa kwanza kuwa ukiona mtu anasema ameokoka na bado anaandamwa na magonjwa yaletwayo na nguvu za giza au bado ana tabia na mwenendo wa ufalme wa giza(nasema hivyo kwa sababu sio magonjwa yote yanaletwa na mapepo wachafu au na vifungo vya shetani), jua tatizo halipo kwa mwenye kuokoa yaani Mungu bali tatizo lipo kwa anayesema ameokoka huku bado amemkumbatia mfalme wa hilo giza. Hao ndio Yesu aliita watu wanaomwabudu kwa midomo yao lakini mioyo yao ipo kwa mfalme wa anga(shetani). Umetumia sentensi hii kuwa ‘The fullness of God in our life doesn’t come at once’ , that is very true but the salvation of our Lord Jesus enters a person once, and that salvation is a complete package kama ambavyo pia umekubaliana kuwa wokovu hauwezi kugawanywa katika mwili,nafsi na roho. Hiyo fullness of God mimi nimeelewa kitu kama utukufu au uwepo wa Mungu, hata hivyo biblia inatuambia tunamjua Mungu kwa sehemu tu kwa hiyo sidhani kama kuna mwanadamu yeyote anayeweza kufikia ile fullness of God ndio maana hata wale wazee ishirini na nne wenye uhai wanne kila wakiangalia utukufu wa Mungu ulivyo wa ajabu wanaishia kusema ‘Mtakatifu,Mtakatifu…

  Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.

 71. Wapendwa mbarikiwe sana kwa mada nzuri ambayo nimekuwa nikiifuatilia. Napata kujifunza mitazamo tofauti tofauti na imani/ misingi ya watu juu ya Neno la MUngu. Nadhani kila mmoja anayefuatilia huu mjadala kuna kitu anajifunza. Mungu awabariki wachangiaji wote.
  Kwa kuanzia mimi nipo miongoni mwa wanaoamini kuwa mtu akiokoka na akaendelea kujifunza Neno la Mungu kwa usahihi, haya mambo ya laana, vifungo nk naamini havitamtesa kama ktk Kol 1:13. lakini kwa kuwa hapa ni mahali pa kujifunza naomba niulize maswali yaliyonijia wakati nafuatilia mjadala huu.
  1. ndugu Lisa ktk mchango wake wa tarehe 26 May amesema kwamba mtu anatakiwa …..atubu kwa ajili ya dhambi ya mababu na vizazi vilivyopita (hata mm nadhani kuna mahali nimeshawahi kufanya hivyo)lakini napata wazo kuwa je hii si kama ibada ya wafu??
  2. Kufanya hivyo si sawa na wanaoamini mtu akifa bado anaweza kuombewa na akapata msamaha/akaokoka baada ya kufa?
  3.Na je lile Neno kuwa baba hatauchukua uovu wa mwana wala mwana hatauchukua uovu wa baba inakuwaje linapokuja swala la kurithi matatizo ya wazee waliotangulia?
  4. Na je hilo Neno nililoandika hapo kwenye swali no 3(samahani nimeshindwa kunakili Kitabu na verse coz nimejikuta sina Biblia karibu) kwa nyakati za sasa/ Agano jipya tunalichukuliaje?
  naomba mchango wenu kwa maswali hayo ili tujifunze kwa pamoja. Najua kuna wanaofahamu sana na tunaofahamu kidogo hivyo mm nimependa nijifunze zaidi hapo kwa sababu inahusiana na maada hii ya vifungo pia.

  Wakati mwingine nitachangia kwa urefu zaidi nikiwa na muda wa utulivu.
  Mungu awabariki wote.

 72. Shalom,
  Ndugu John Paul,
  1.Umasikini ni kweli waweza kuwa kifungo, muhusika anajitihada za kufanya kazi na bado umasikini aka (hali ya uhitaji wakati huwezi kupata mahitaji yako) unamuandama anaanzisha biashara inakufa….
  ni kifungo hicho cha umasikini….. mfano niliwahi kuomba na dada mmoja wa kanisa la BCIC aka kwa Gwamanywa, huyu dada ameokoka nikimaanisha ameamini/amezaliwa mara ya pili, wakati na Deal na Shida yake Bibi yake wa kambo huko kabla huyu binti hajaokoka alimfunga kichawi asifanikiwe kiuchumi na hata kwenye elimu na pia asielewane na mdogo wake, wakati naomba nilikuta huyo bibi kaweka majini wengi kama 12 hivi na kila mmoja anakazi yake, nikavunja hivo vifungo vya uchawi… huyu alikuwa akifanya mitihani mitihani inapotea hapo shuleni baada na kurudi shuleni mitihani ikapatikana na amefaulu….utukufu kwa Yesu…. na pia akiingia ndani wanapokaa mdogo wake anatoka nje na akienda nje mdogo wake anaingia ndani…baada ya maombi hii hali ikaondoka mdogo akasema dada yake alipowakuwa akiingia ndani kichwa kilikuwa kinamuuma ndo maana alikuwa anamkimbia,
  tunajifunza nini hapa huyu dada mafanikio yake yalikuwa yamefungwa kwenye shule kichawi…. nimewahi kuomba na watu kama watatu hivi wa aina hiii na Mungu aliwafungua wote hao walikuwa wameokoka….
  2.inategemea na sababu inayomfanya kuwa masikini …. kama ni vifungo inabidi kuomba maombi ya kuvunja vifungo… na kama ni uvivu inabidi afanye kazi kwa bidiii..
  3. Deliverance haimfanyi mtu kuwa tajiri ndugu John Paul ila ni maombi yanyovunja nguvu za giza zilizofunga mtu kuafanikiwa, baada ya mtu kuwa huru bado anamaamuzi afanikiwe au lah…. Bila haya maombi anakata kufanikiwa ikawa ngumu kwa sababu ya vifungo hivyo umasikini…. ila sio umasikini wote ni vifungo vingine ni uvivu wa mtu….
  4.matajiri ambao hawajaokoka wananjia zao za kupata utajiri….wote tunajua hili na sio tuliokoka tunanjia za kibiblia za kufanikiwa….
  5.inaweza ikawa vifungo au upungufu wa elimu husika…nimewahi ku deal na kesi ya mama mmoja ambaye alikuwa anashida kazini… na ilikuwa ni nguvu za giza Thank God alimfungua….
  6.Inaweza ikawa vifungo au Elimu ya kiMUNGU ya ndoa na malezi ya watoto kikristo…. Ndugu John Paul je umewahi kukuta mtu aliyefungishwa ndoa na majini halafu ndoa yake ikadumu h????? asiposhughulia hiki kifungo ndoa lazima ipige mzinga….

  Huu ni mtizamo wangu Mungu awabariki Sana wachangajiaji wote na wasomaji tunaendelea kijifunza

 73. Shalom,
  Mjadala ni mzuri sana tunapata kujifunza vitu vingi, pia kujua ndugu wengine ktk kristo wanawaza nini juu ya hili tunalojadili,
  Ndugu Asheri,
  Nianze hapa ukisoma vizuri injili ya Yohana 5:24 …., Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele;
  Hawa wayahudi wa Yohana 8:31-
  kama walimwamini Yesu unawaitaje? Waliokuwa wakimwamini Yesu walikuwa wanapata uzima ndani yao… ndo maana alimwambia zakayo Wokovu umeingia nyumbani kwako……
  Sasa tujiulize huu wokovu ulioingia nyumba mwa Zakayo ulikuwa ni upi?…… aliyekuwa anamwamini Yesu alipata uzima wa milele aka wokovu….. Hawa walimwamini yeye atakayewalipia Deni ya dhambi zao….. na sisi tunamwamini yeye aliyetulipia deni ya dhambi zetu…….

  Ndugu Hagai, mi sijaugawa wokovu wala maandiko niliyotoa kwenye michango yangu yote hayajaugawa wokovu, yamemgawa mtu…. Mtu ni roho yenye nafsi na anaishi kwenye Mwili.. 1 Thes 5:23
  Mungu wa amani awatakase kabisa, nanyi nafsi zenu na roho zenu na mili yenu,
  Wokovu aka uzima wa milele aka kuzaliwa mara ya pili ni roho maandiko yote uliyoyataja yanasema hivyo na mi naungana nawewe,
  Angalia Warumi 12:2….mgeuzwe kwa kufanya upya nia zenu…. nia ni sehemu ya nafsi Hapa JOHN PAUL atusaidie maana najua anamasomo mazuri sana ya nafsi…. nafsi inataarifiwa kilichofanyika rohoni kwa kusoma neno la Mungu( inakuwa updated) … Mwili tunautoa dhabihu… sisi tunaitoa iwe dhabihu….. tunaisubmit under the control of our spirit… mpaka hapo sijaugawa wokovu…. Nilichotaka kuweka wazi ni kuwa roho, nafsi na mwili vinashughulikiwa tofauti….. si shida zote zilizoko kwenye mwili au nafsi ni maagano au vifungo zingine ni tamaa za mtu mwenyewe.
  Pamoja na kuwa huingia rohoni matunda yake huonekana katika mwenendo wake kama ataamua kuifuata nia ya roho…angalia Warumi 8:8–10, kwa hiyo unaweza ukaokoka usiiifuate nia ya roho, ukaufuata mwili na matunda ya mwilini yataonekana na hatimaye utakufa…
  mfano.. unaweza ukazalilishwa nia ya roho ikasema usijibu neno… nafsi na mwili vikasema haiwezekani lazima nimwonyeshe, sasa wewe unaamua uifuate nia ipi?
  Hili ni somo lingine la namna ya kuongozwa na Roho Mtakafu wakati mwingine tutajadili… mjadala wetu ni delivarence…..

  Mpendwa Furaha,
  Nashukuru kuwa umepata majibu ya maswali yako 6 kati ya 9 uliyouliza ingawa nilikujibu maswali yako yote 9, Nafikiri rudia kuyasoma unaweza ukaelewa…. ushauri wangu tuisome biblia tukiwa na mtizamo neutral itatusaidia kujifunza na kuelewa vitu sana…

  Mi nashindwa kuelewa hapa magonjwa, umasikini je si giza???????? Yesu alishughulia haya yote msalabani sasa mwili wako ukiumwa nawe umeokoka je giza halijachangamana na nuru….. au umasikini je giza halijachangama na nuru .. ila vifungo vikikutwa ndani ya mtu aliyeokoka cha kwanza kuwaza hajasimama na haiwezekani maana giza na nuru havichangamani! Tuielewe injili jamani wapendwa..
  Cha kwanza kabisa angalia kiwango cha nuru kinachoingia ndani mtu anapookoka, Roho mtakatifu anaingia ndani yake na nguvu kidogo na nuru kidogo, utukufu kidogo hivi vinaingia ndani ya roho ya mtu,
  unapobatizwa na Roho Mtakatifu nuru inaongezeka….ukiendelea sana kuwa na ushirika na Mungu utukufu mwingi unakufunika hapa ndipo mwili wako unakuwa hekalu la Roho Mtakatifu na hii ni process …. the FULLNESS OF GOD IN OUR LIFE DOESNT COME ALL AT ONCE…ni hatua, katika kiwango cha utukufu kidogo na ujuzi kidogo wa neno Pepo wanaweza kukaa kwenye mwili wa aliyeokoka…..sio rohoni kwenye mwili, hawawezi kumposes ila wanamkandamiza… hasa wakiwa na uhalali….
  Nitatafuta muda hapo mbele nielezee vizuri namna pepo wachafu wanavyoweza kukaa katika mwili wa Mtu hata aliyeokoka…..

  Dada furaha isikushangaze sana kuwakuta watu walioamini wanashika baadhi mapokeo… ni kwa sababu hawajujua kweli yote…. hawajafundishwa neno la Kristo kwenye hayo maeneo… ila kila dhehebu la kikristo lina mapokeo yanatofautiana percentage halipo ambalo ni neno la kristo 100%
  Hata mimi na wewe unaweza kukuta bado tunashika mapokeo… sidhani kama tumechunguza doctrine zote za kidhehebu kama ni agizo la Kristo…..

 74. Ninakubaliana na mpendwa Furaha katika yote unayoandika kuhusu mada hii, ikiwa ni pamoja na maswali uliyouliza mwanzo na haya ya nyongeza ambayo bado tunasubiri majibu yake. Mimi naona kwamba mtu ‘mwenye experience’ ya deliverance ndiye anaweza kujibu sahihi maswali hayo. Kwa sababu katika watu wanaochangia hapa kuna wachangiaji wengine wameandika kwamba wana – experience ya deliverance. Hivyo ninatumaini watajibu maswali haya kwa ufasaha zaidi ili tuendelee kujifunza.

  Pamoja na maswali yaliyoulizwa na Furaha, ambayo yakijibiwa ninaamini tutapata kitu cha kujifunza,
  katika michango ambayo imeshaandikwa hadi sasa kuna mambo mbali mbali yamejitokeza, ambayo yako kati ya vifungo ambavyo mtu anaweza kuwa kafungwa. Ninaona ni vema tukaendelea kuyajadili ili ndugu Benedicta pamoja na yeye yeyote ambaye anapata mafundisho katika mjadala huu, tuendelee kujifunza. Mambo yenyewe ni haya yafuatayo:

  i).Je, ni kweli kwamba umasikini ni kifungo?

  ii).Mtu akisema ameokoka halafu akawa bado ni masikini, ili kuwa tajiri mtu huyo anahitaji deliverance?

  iii) Je, inawezekana kufahamu kiwango cha utajiri ambacho mtu aliyeokoka akikifikia ndiyo isemekane amefikia kwa sababu alifanyiwa deliverance? [ikiwa mtu anaweza kuwa tajiri kwa sababu ya kufanyiwa deliverance]

  iv).Kwa kuwa kuna matajiri ambao hawajaokoka ina maana tayari wameshaanza kuonja matunda ya kufunguliwa/deliverance kama ni kweli kwamba umasikini ni moja ya vifungo na utajiri ni moja ya manufaa ya wokovu. Je, mtazamo huu ni kweli?

  v).Kukwama kwa biashara, kufukuzwa kazini nk, ni lazima viwe vinasababishwa na vifungo toka kwa shetani?

  vi).Mtu akiokoka halafu ndoa yake isiwe na amani au watoto wake wawe wakorofi, je ni lazima hali za namna hii ziwe zinasababishwa na vifungo?

  Ninatumaini katika kuyajadili haya tutapata mengi ya kujifunza.

 75. Wapendwa Mungu awabariki mno kwa michango yenu mizuri. Kaka Asheri, John Paul mmeeleza kwa undani sana wokovu ni nini na nn kinatarajiwa kwa mtu anayesema AMEOKOKA. Kaka Asheri umenigusa sana, baraka za Bwana zikukalie. Kweli Neno la Mungu ni tamu. Ndugu Haggai Kinyau, baraka za Mungu ziwe juu yako, umenigusa na kunifunza sana. Kwa upande wangu naona kuugawa wokovu kwamba NI ROHO TU NDIYO INAYOOKOKA wakati mwili nafsi na roho huwezi kuvitenganisha na mtu akaishi kwa kweli napata shida kidogo hapo na maelezo ya Ndugu Paul Holela.

  Kuna rafiki yangu mmoja hupenda kusema INJILI siyo ngumu ila watu hupenda kudadavua sana until inakuwa ngumu na kuwakosesha watu.

  Pia ktk mchango wangu wa tarehe 26 May 2010, niliuliza maswali ambayo Namshukuru ndugu Paul kwa mchango wake ktk kuyajibu baadhi, ila bado sijapata mchangiaji wa kujibu yaliyosalia. Naomba niyarudie tena ili kama kuna mtu anaweza kunisaidia nipate kujifunza zaidi, maswali yenyewe ni haya hapa:
  1. Ni wapi ktk kanisa la kwanza/ Agano jipya tunaona huduma ya deliverance hasa baada ya kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo?
  2.Na je wapendwa wanaofunguliwa huwa hawapati tatizo tena ktk maisha yao kimwili, biashara nk?
  3. Je deliverance/ maombi ya kuwafungua vifungo huwasaidia wanaoombewa kuishi maisha Matakatifu?

  Kuna kitu najifunza kwamba mtazamo wa baadhi ya wachangiaji ni kuwa wokovu ni KITU KIDOGO SANA, na kuwa bado hauna nguvu ya kutosha kumnasua mtu kutoka ktk shida zingine. Lakini mm naunga mkono mawazo ya ndugu Haggai, Asheri, John Paul na wengine ambao wanaona kuwa WOKOVU NI KAMILI provided mtu ameamua KUJIKANA, KUCHUKUA MSALABA WAKE NA KUMFUATA KRISTO KWELI KWELI. Kuna mtu unaweza kumkuta anakiri kuwa ameokoka lakini hataki kuachana na mapokeo ya dini yake yaliyo KINYUME NA NENO LA MUNGU, Bado wapo waliookoka na bado wanasali Misa za wafu, Sala za Bikira Maria, hawaamini kunena kwa lugha, hawaamini ubatizo wa Roho Mt, hawaamini ubatizo wa Maji ,hawaamini……… – list ni ndefu kwa kweli. Sasa mtu wa hivi hata ukimkuta na vifungo fulani ktk maisha yake, utasema kuwa wokovu/ sala ya toba haitoshi kumfungua mtu vifungo au utakubaliana na Ndg waliochangia hapo juu kuwa wokovu ni uamuzi wa mtu kutoka ndani yake, na juhudi ktkt kujifunza NENO (ambapo kujifunza ni pamoja na kulitenda/ kuliishi NENO)?

  Kwa kutumia mfano mmoja tu wa Zakayo alipokutana na Yesu akamwamini, ile decision/ determination yake kwa kweli tunaweza kujifunza kitu, pengine asingeamua kurudisha vitu vya watu i.e toba ya kweli; nasema pengine angeweza kusumbuliwa na vifungo fulani hapo baadae.
  Hivyo mm nazidi kujifunza kwamba tusiendekeze tu kama mtu mambo yake ya kiroho labda au ya kimwili hayaendi vizuri basi tu-conclude tu kuwa ana vifungo au laana, lakini tuchunguze au mtu mwenyewe achunguze maisha yake na kujipima ktk Neno la Mungu kabla ya kuwa na hofu kuwa laana za babu zinamfuata and the like. Kwangu mimi I strongly believe kuwa So long nimeokoka HAKUNA LAANA WALA VIFUNGO VYA UKOO VINAVYOWEZA KUNIPATA. Neno ninalosimamia ni hili Kolosai 1: 13…NAYE ALITUOKOA KTK NGUVU ZA GIZA..akatuhamisha na pia Nuru na Giza havichangamani!
  Naomba niishie hapa kwa sasa, ila natamani sana kujibiwa maswali yangu ili tuendelee kujifunza kwa pamoja

 76. Shalomu,

  Ndugu Paul

  Nakushukuru kwa mchango wako, ila napenda nifafanue kuwa katika mchango wangu nilisema kuwa sikuwa na nafasi ndiyo maana sikuweka maandiko na ndiyo maana nilisema kwa uzoefu wangu, hata hivyo naamini kile nilichokisema ni neno la Mungu, yaani yote niliyoyasema yako katika neno la Mungu ila sikusema yako wapi. Yale niliyoyasema yanapatikana Kolosai 1:13, 2Wakorintho 5:17, 1Petro 1:3, 5, 23 n.k.

  Ninapenda kuelezea kuwa nimeisoma Yohana 8:31, na ninakubaliana nawe neno ndilo linalotuweka huru, lakini ukiangalia kwa makini, hiyo 8:31 utagundua kuwa Yesu alikuwa akiongea na Wayahudi waliomwamini, lakini tujiulize swali moja la msingi, je walikuwa wameokoka? Nikisoma sehemu hiyo yote ninashawishika kuamini kuwa pamoja na kuwa walimwamini, lakini hawakuwa wameokoka na ndiyo maana baada ya mazungumzo ya muda mrefu, walitaka kumpiga Yesu kwa mawe. Lakini pia ndugu John Paul ameelezea hali waliyokuwa nayo wanafunzi wa Yesu kabla Yesu hajafa msalabani, hivyo nami naungana naye kuwa fully package ya wokovu ilianza kutenda kazi rasmi baada ya Yesu kufa na kufufuka katika wafu. Damu ya Yesu ndiyo inayotusafisha dhambi zote (1Yohana 1:7)

  Pamoja na niliyoyaeleza hapo juu, nirudie kusema kuwa ninakubaliana nawe kuwa neno la Mungu ni nyenzo muhimu sana kwa mtu kukua kiroho, na kama kuna delivarence basi mtu kumjua Mungu kwa njia ya neno ndiyo delivarance ya kweli, kama Yesu alivyosema mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru na Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli.

  Nikirudi kwenye mada, nadhani ninaomba niseme kuwa, KUOKOKA ni maisha au kwa lugha nyingine WOKOVU ni maisha ya mtu na si tukio la mara moja. Vilevile, naomba niseme kuwa kama kulivyo kuzaliwa, mwanadamu anapozaliwa anakuwa mtoto mdogo asiyejua mambo mengi na ndivyo inavyokuwa kwa mtu anapookoka ndiyo maana Yesu aliagiza watu wafanywe wanafunzi na wafundishwe kuyashika yote yaliyoagizwa (Mathayo 28:19-20).

  Ndugu Paul amesema katika mchango wake wa tarehe 26 May 2010 kuwa wokovu hufanyika rohoni, ni kweli, hata hivyo, mambo ya rohoni ndiyo yanayotawala mambo tunayoyaona ya mwilini na ndiyo maana Biblia inasema vita vyetu si vya mwilini bali vya rohoni, hivyo tutwae silaha zote za Mungu (Waefeso 6:10-18).

  Dhambi ilipoingia duniani pale Edeni iliingia pamoja na laana na mateso na Biblia inasema mwanadamu alikufa kiroho, na kifo hicho cha kiroho ndicho kilicholeta shida zote ikiwemo laana, magonjwa na takataka zingine zote (Mwanzo 3:17-19). Ni kutokana na dhambi ya pale Edeni, mwanadamu akajiweka chini ya utumwa wa dhambi na shetani na hivo tukawa tumepotea, hatuna Mungu duniani.

  Tunapozungumza kuzaliwa mara ya pili, ni kweli mtu anazaliwa katika ulimwengu wa roho, na ni katika ulimwengu huohuo mtu huyu anakuwa kiumbe kipya. Ni kweli hatubadiliki umbile wala rangi, lakini tunabadilishwa falme, kutoka ufalme wa shetani kwenda kwenye ufalme wa Mungu na ndipo tunakuwa wana wa Mungu, ndiyo maana nilisema kuwa wokovu ni mapinduzi kwa asilimia 100.

  Kama nilivyosema hapo juu, mtu anazaliwa akiwa mtoto mchanga, hivyo anahitaji kuukulia wokovu na anakuwa kwa kujifunza neno la Mungu na kuliishia neno. Mtu anapookoka anasamehewa dhambi na kupewa uwezo/nguvu ya kuishinda dhambi. Baada ya mtu kupewa uwezo, anakuwa na uhuru wa kuutumia uwezo huo au la. Ninachosema hapa ni kuwa, mtu ambaye hajaokoka ni mtumwa wa dhambi, hivyo hana uwezo wa kuishinda dhambi, bali dhambi inamtawala, lakini baada ya kuokoka, mtu anakuwa na uwezo wa kuishinda dhambi, lakini anaweza akaamua kuendelea kutenda dhambi na mwiho anakuwa kama mtu asiyeokoka. Lakini wapo wengine wanaweza kuendelea kufanya mambo yaliyo kinyume na neno bila kujua kuwa ni makosa kwa sababu ya kukosa mafundisho ya neno la Mungu, na pindi wakishajua basi wanakuwa wepesi kuacha.

  Ninaomba niseme kuwa ukisoma kwenye nyaraka za Paulo utaona kwa sehemu kubwa anawafundisha watakatifu juu ya kuuishia wokovu. Mfano katika Efeso 4:22-24 inazungumzia kuuvua mwenendo wa kwanza ambao unaendana na tamaa za mwili na kutuagiza kuuvaa utu mpya. Mstari wa 25 anazungumzia kuuvua uongo, mstari wa 27 anazungumzia kuwa tusimpe ibilisi nafasi, anaendelea kusema mwibaji asiibe tena , kisha neno ovu lisitoke kwetu n.k. Katika Efeso 5 Paulo anaendelea kusema namna ya kuendelea kuuishia wokovu akisema uasherati usitajwe kwetu kamwe, tusilewe kwa mvinyo bali tujazwe Roho na kuwa tuhakiki ni nini impendezayo Bwana.

  Maandiko hayo yote yanaonyesha kuwa baada ya kuokoka, inatupasa kuchukua hatua kuuishia wokovu, na hili linahitaji maamuzi ya mtu mwenyewe pamoja na bidii ya mtu huyo katika kumjua Mungu kwa kupitia neno la Mungu. Nimelazimika kusema haya kufafanua juu ya hoja kuwa tunapaswa kuokoka rohoni, nafsi na mwili. Yesu alisema kuwa Mtu akitaka kumfuata na ajikane mwenyewe aubebe msalaba wake amfuate. Hili linaonyesha kuwa wokovu hufanyika rohoni na hilo likishafanyika, basi tunapaswa kuishi maisha ya kujikana wenyewe (hapa ni kuiitiisha nafsi ili imtii Mungu). Vilevile, Paulo anasema basi enendeni kwa Roho wala hamtazitii kamwe tamaa za mwili kwa kuwa mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho vivyo hivyo (Galatia 5:16-26). Biblia imetutaka pia kuitoa miili yetu kuwa dhabihu iliyo hai ….. wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu …(Rumi 12:1,2). Tunachokiona hapa ni kuwa mwili unatiishwa na kufanywa dhabihu (sadaka) ili kumpendeza Mungu. Hili halifanyiki kwa maombi ya kuvunja bali ni kwa maamuzi ya kuishi maisha matakatifu, na mtu akishaamua, Roho yupo tayari kumsaidia na kumuwezesha kulifikia lengo. Naomba tusome pia Efeso 6:12-13, Rumi 8:2,9,14, Rumi 6:11, 12, Galatia 3:13,14; 5:1, 5, 13 Efeso 2:1,12 na Efeso 2:18-22; 3:17; 4:13.

  Hata hivyo, yapo matatizo ya msingi tunayokutana nayo siku za leo, au niseme kanisa la leo. Moja ya matatizo ya msingi ni kutompokea Roho Mtakatifu na pale tulipompokea hatuko tayari kumfuata, pamoja na kuwa Biblia inasema wazi kuwa wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu (Rumi 8:14). Ni kutokana na kutokuongozwa na Roho, wengi wetu tunaendelea kutenda dhambi na hapo biblia inasema kuwa tunakuwa siyo wana wa Mungu. Sasa tujiulizwe swali la Msingi, Je MTU ANAPOSEMA KUWA AMEOKOKA HALAFU ANA MAPEPO, JE HUYU MTU ANAONGOZWA NA ROHO WA MUNGU? na je akifa katika hali hiyo hiyo atakwenda MBINGUNI? Je mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu alafu akawa na pepo mchafu?

  Tatizo lingine kubwa limesemwa vizuri na Ndugu John Paul, kuwa wengi wa wanaosema kuwa wameokoka kiukweli hawajaokoka, na kwasababu hiyo bado mioyo yao ni michafu na hivyo shetani anaweza kuendelea kuwatesa na kuwatumia anavyotaka. Lakini niseme kuwa MTU AKIKUTANA NA YESU AKASAMEHEWA NA KUOSHWA DHAMBI ZAKE ANAKUWA MTU WA TOFAUTI SANA, ni sawa na mtu aliyepondwa na jiwe akawa teketeke. Mtu wa aina hii anakuwa tayari kwa lolote ili mradi tu awe na Kristo. Lakini wapo watu siku hizi wanaokoka huku wakiweka masharti (utakuta mtu unamshuhudia anasema niko tayari kuokoka lakini sitabatizwa, au siwezi kuhama dini, au siwezi kumwacha mchumba wangu n.k.) Lakini ukikutana na mtu aliyeamua kuokoka, utashangaa jinsi anavyokuwa na moyo mwororo.

  Siku moja tulikuwa mahali fulani tunaendesha mkutano wa Injili. Kukawa na dada fulani, toka siku ya kwanza anakuja kwenye Mkutano, ananyosha mkono kuokoka halafu anatolewa pepo. Hili liliendelea kwa siku tatu, ndipo siku ya nne nikaamua kuongea naye. Baada ya mazungumzo nikabaini kuwa yule dada anaishi kwenye nyumba ya mume wa mtu, yaani mume wa mtu kampangia nyumba, anampa chakula, nguo n.k. Nikamwambia kuwa kama anataka kuokoka basi anapaswa kumuacha huyo hawara yake, akasema yeye anataka kuokoka lakini aendelee na huyo hawara. Mpaka tunamaliza siku nane mahali pale tulimwacha katika hali yake ileile.

  Tukiwa sehemu nyingine tukifanya mkutano, alitokea mtoto mmoja akiwa na pepo. Tulikemea pepo yule mpaka saa nne usiku ndipo wakatoka. Baada ya hapo ikabidi tumpeleke mtoto yule kwao maana isingekuwa vema tumwache usiku ule aende peke yake. Tulipofika tuligundua kuwa wazazi wa mtoto yule ni watu waliookoka tangu wakiwa vijana, yaani hata kabla hawajaoana, tena walikuwa washirika wa dini moja na sisi na ni viongozi kanisani kwao. Wakati tunaendelea kuongea nao, mara pepo zikalipuka kwa mtoto mwingine. Baada ya kuongea nao kwa muda tukagundua kuwa watu wale wana matatizo makubwa ya ndoa yao, yaani ndoa ilikuwa inawaka moto. Ilibidi tupange muda wa kuongea nao ili wayamalize matatizo yao na ndoa. Hapa ni kuwa Ibilisi alipewa nafasi naye akaitumia kuwatesa watoto. Mimi nikikutana na mtu aliyeokoka mwenye pepo, huwa napenda kujua maisha yake ya kiroho yakoje kwanza.

  Tutaonana wakati mwingine

 77. Wapendwa,
  Hakika mada hii ni nzuri na michango ya watu wote waliotangulia ni mizuri mno na inaelimisha.Maswali yanayoulizwa yanaendelea kutoa changamoto mbalimbali kwa lengo au kusudi la kujifunza zaidi.Nami leo naomba nichangie mada hii kama ifuatavyo.
  1.Nianze kwa kueleza maana ya toba na sala au maombi ya toba.Kwangu mimi hivi ni vitu viwili tofauti kwa maana kwamba toba ni uamuzi wa ndani wa mtu kuona kwamba hali ya maisha ya dhambi aliyonayo haymsaidii na hivyo anaamua kubadilika.Kwa kuwa uwezo wa kujibadilisha yeye mwenyewe hana ndipo sasa anaomba msaada au nguvu ya kumbadilisha kwa kufanya sala au maombi ya toba kwa Mungu ili Mungu aingilie kati hali aliyonayo kwa kuweka nguvu ya Roho Mtakatifu ili mtu huyu aendelee kuukulia wokovu.Kwa kifupi toba ni uamuzi wa kubadilika na maombi ni kibebeo cha uamuzi huo kwenda kwa Mungu(repent means change your mindset).
  2.Kuna hatua kadhaa mtu anazotakiwa kupitia ili aweze kupata wokovu wa kweli, baadhi ya hatua hizo ni
  a) Lazima mtu huyo yeye mwenyewe ajue kuwa ana dhambi
  hivyo lazima atubu dhambi zake na kumanisha kuziacha
  kabisa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu si kwa nguvu au
  uwezo wake.Soma Rumi 3:23, Galatia 3:22, Rumi 3:9-12.
  b) Lazima mtu huyo amwamini Bwana Yesu moyoni mwake na
  kuyatoa maisha yake(mwenendo na tabia zake) yote ili
  Yesu awe Bwana na Mwokozi wake.Soma Rumi 10:9-10,
  Matendo 16:31, 2:21 Yohana 17:3 n.k.
  c) Lazima mtu huyo aishi maisha ya WOKOVU maana yake
  maisha ya kumpendeza na kuwa na hofu ya Mungu kila
  mahali na kila wakati ili hii hofu ya Mungu itamfanya
  asiwe na hofu ya wanadamu zaidi kuliko Mungu.Hofu ya
  Mungu ndiyo itamsaidia kuzishika amri zake kupitia
  neno lake. Soma 2Korintho 5:17(maisha mapya ndani ya
  Kristo), 1Yohana 2:1-6,Galatia 6:16-17 n.k.
  Baada ya hatua hizo pamoja na zingine ambazo sijazitaja hapo juu, ndipo mtu huhesabiwa au huonekana ameokoka kweli na baada ya kuokoka kuna vitu kadhaa vinavyofanyika kwa huyu ‘kiumbe kipya’-kumbuka habadiliki sura wala umbile lake bali utu wa ndani unabadilika hivyo unasukuma pia kuufanya utu wa nje(mwili wa nyama) kutii mabadiliko hayo, ndiyo sababu utakuta mtu alikuwa mlevi ghafla hamu ya kunywa pombe inaisha au alikuwa mwasherati mara hamu ya kuzini inakatika, alikuwa hana upendo tena kwa mke au familia yake anarudisha ule upendo wa kwanza.Yote hayo yanafanyika kwa kuwa amebadilishwa nia ya ndani ya kuwaza na kufikiri kwake, anarudishiwa ile nia ya kwanza aliyoumbiwa Adamu kabla ya kuanguka dhambini.Yafuatayo ni baadhi tu ya mambo yanayofanyika baada ya mtu kuokoka.
  1. Anafanyika kuwa mwana wa Mungu, Yohana 1:12, Isaya 56:5
  1Yoh 3:1-2 2Petro 1:4 n.k.
  2. Dhambi za mtu huyo zinaoshwa/zimeoshwa na kusafishwa kwa damu ya Yesu na Mungu anasamehe na hazikumbuki tena.Isaya 1.18. Ufunuo 1:5, Efeso 1:17 n.k
  3. Mtu huyo anavikwa vazi jipya la wokovu ili liwe kama ukuta wa kiroho wa kumlinda Isaya 61:10, 60:18.
  4. Roho Mtakatifu anakaa ndani yake na anakuwa naye kama mwalimu, kiongozi, mtoa uzima na msaidizi na atakujulisha yote(yaliyopita,yaliyopo na yajayo) tena anakuombea kwa kuugua sana.Yohana 14:15-17,1Kor 3:16-17 Rumi 8:26 n.k
  5.Anapewa nguvu na mamlaka YOTE dhidi ya shetani na nguvu zote za giza.Luka 10:19, Mark 16:17-18,Yer.1:10,Efeso 1:21, Math 16:19 n.k
  6. Amehamishwa toka mautini na kuingizwa uzimani.Labda hapa nielezee kidogo (kwa jinsi ninavyoelewa)maneno haya mawili ‘mautini’ na ‘uzimani’.Kwangu mimi mautini maana yake ni kuishi maisha ya uduni na kutokufanikiwa kwa kiwango kile Mungu alichotupangia na uzimani maana yake ni kuisha maisha ya mafanikio katika kila eneo la maisha yetu.Kumbukumbu la Torati 30:15-16 kisha 19-20.Yoh 5:24 n.k
  7. Mtu huyo analindwa kwa ulinzi wa mamlaka ya ufalme wa mbinguni.Zab 34:7, 91:11, Ufunuo 19:10,Zakaria 2:8-10.n.k
  8. Na mwisho mtu huyo anafanyika kuwa mtumishi au mtumwa mwaminifu wa Mungu katika Kristo Yesu.Efeso 1:20-23,1Kor 12:18-20, Yer 1:4-10, Math 28:18-20 n.k.
  Baada ya kusema yote hayo kabla na baada ya mtu kuokoka inaniwia vigumu sana kuugawa huu wokovu katika nafsi,mwili na roho(ingawa yametolewa maelezo mazuri sana na wachangiaji hasa ndugu yangu Paul Holela).Kwangu mimi wokovu is a complete package as said by John Paul ila sisi wanadamu au hawa wanaopokea huo wokovu wanakuwa bado VUGUVUGU yaani bado wameshikilia baadhi ya mambo ya shetani na kwa Mungu nako wanataka, hivyo watu hawa ndio wanaoonekana wanafanya sala za toba kila mkutano wa injili wanaohudhuria lakini hawafanyi maamuzi kwanza ya kubadilika toka mioyoni mwao kabla ya kufanya sala ya toba(naomba nisieleweke vibaya kwa sababu maisha ya toba ni ya kila siku kwa mtu aliyeokoka kwa sababu ni kuhani anatakiwa kutubu hata kama yeye hajatenda dhambi lakini anaishi kwenye jamii inayotenda dhambi kila siku hivyo wakati mwingine anadhambishwa hata kama yeye hajafanya hivyo, hivyo lazima atubu kila wakati).
  La msingi ambalo nataka kulisisistiza ni kwamba baada tu ya mtu kuokoka lazima aukulie wokovu kwa kujifunza na kufundishwa mafundisho sahihi ya wokovu.Wengi wanafikiri wokovu ni dini mpya, wokovu ni mfumo wa maisha ndani ya ufalme wa Mungu unaomwezesha mtu kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Kama mtu anaendelea na michanganyo ya kwa shetani kidogo na kwa Mungu kidogo basi mtu huyo hajaokoka maana yake hajawa converted.
  Mungu awabariki waote.

 78. Dada Rose,

  Namshukuru Mungu kwa kuwa umejifunza kitu kutoka katika mchango wangu. Ninatumaini tutaendelea kujifunza mengi kadri mada hii inavyoendelea.

 79. Shalom,
  Ndugu Benedicta,
  Sijajua Shida yako hasa ni nini? ili tujue namna ambavyo tunaweza kukusaidia, nilikuwa nawaza baada ya kuona mchango wako labda uandike tena shida inayokusumbua ili tumuulize Mungu tunakusaidiaje? njia za za kibiblia za kumsaidia mtu zinatofautiana mtu na mtu… mwingine utampa neno, mwingine inabidi uwatoe pepo…, mwingine nguvu za kichawi, na wengine maagano yavunjwe… mwingine afundishwe neno tu…..

  Usiteseke na shida yako na Bwana Yesu anaweza kukupumzisha Mathayo 11:28,
  Humu mtandaoni tunachangia mada kwa ujumla sana ukisema shida yako tutadeal nayo specifically.

  Kwa mawasiliano email yangu ni holela@ce.udsm.ac.tz au pholella@yahoo.com….

  Mungu akubariki sana…..

 80. Shalom kaka John Paul,
  asante sana kwa ufafanuzi wako, kwakweli ni sawa kila kitu ulichosema, nimejifunza mengi sana kwako na kwa Paul pia. Nimejua sasa kupitia ufafanuzi wako kuwa wokovu kamili ni pamoja na kuwa umejawa na neno na Roho mtakatifu na moyo wa kutubu kweli, sala ya toba haraka haraka sio tiketi ya kuhalalisha kuita wokovu. Nimejifunza kuwa wokovu ni namna unavyoishi SASA. Kweli nimefunguka macho kwa mengi hapa. Asante sana wapendwa kwa yote, tunapochangia ni kama tunatoa yale tuyajuayo ili wengine watuambia kama ni sahihi, nashukuru sana kwa mengi niliyojifunza hapa.
  Mbarikiwe,
  Rose

 81. Bwana Yesu asifiwe sana, mimi kwa maoni yangu ni kwamba unatakiwa kufanyiwa deliverence nawe pia kuwa na bidii ktk maombi na neno,utapata kufunguliwa.

 82. Dada Rose,

  Nashukuru kwa ufafanuzi wako, lakini utanisamehe kwa sababu bado naendelea kujifunza kutoka kwako.

  1. Kuna swali ambalo nililiuliza katika mchango wangu uliopita lakini sijapata jibu lake, naomba kulirudia tena:
  Je, ni sahihi nikisema kwamba binti huyo alichelewa kufunguliwa kwa sababu alikuwa hajaingia sawa sawa katika wokovu?

  2. Kutokana na Waefeso 3:20-21, ambayo umeitumia wewe, nadhani ni sahihi nikisema kwamba nguvu iliyoko ndani ya mtu inategemea ni kiasi gani mtu huyo analifahamu Neno la Mungu na kwa kiasi alichokabidhi maisha yake kwa Yesu. Mtu mwenye ufahamu mdogo wa Neno la Mungu na ambaye hajajikabidhi vizuri kwa Mungu ni dhahiri kwamba nguvu iliyoko ndani yake itakuwa kidogo. Na nguvu iliyoko ndani inapokuwa kidogo ndipo mtu huyo anakuwa katika hatari ya kushambuliwa na nguvu za giza. Kinyume chake ni kwamba mtu mwenye ufahamu mkubwa wa Neno la Mungu halafu amejikabidhi vizuri kwa Mungu nguvu iliyoko ndani yake itakuwa ni kubwa. Na nguvu inavyokuwa kubwa ndivyo mtu huyu anakuwa mbali na uwezekano wa kushambuliwa na nguvu za giza. Kwa hiyo UFAHAMU WA NENO LA MUNGU na KUJIKABIDHI KWA MUNGU KIKAMILIFU ni kanuni muhimu kwa mtu ili kumfanya mtu huyo awe mbali na mashambulizi na vifungo vya nguvu za giza. “Mtiini Mungu, mpingeni shetani naye anatawakimbia! [Yakobo 4:7].”

  Kama nilichoandika hapo juu si sahihi ninaomba masahihisho.

  3. Ikiwa kuna watu ambao wakiombewa sala ya toba husimama na kuendelea na wengine baada ya sala ya toba hurudi tena dhambini;
  Je, ni sahihi nikisema kwamba kinachofanya wengine warudi nyuma baada ya kuombewa sala ya toba ni kwa sababu zao binafsi [kama vile mazingira, kushikilia mambo ya kale kama yule binti uliyemtolea mfano] na si kwa sababu ya uwezo mdogo wa sala ya toba? [ikiwa kwa hiyo hiyo wengine wanasimama na kuendelea mbele!]

  4. Nilipoandika ‘ndumila kuwili’ sikumaanisha yeye tu. Nashukuru kwa kupanua wigo wa neno hili. Ndumilakuwili ni mtu ye yote anayesema ameokoka lakini bado akawa ana mambo mengine ya gizani ambayo anaendelea nayo. Hasara ya jambo hili ni kwamba mtu wa namna hii hawezi kuiona furaha ya wokovu kwa sababu yale mambo aliyoyashikilia, ambayo hayakubaliki katika wokovu yatamsababishia vifungo na mateso kutoka katika nguvu za giza. Kwa hiyo ili mtu aipate furaha ya wokovu na kuwa mbali na vifungo vya giza ni sharti ajitowe kikamilifu kwa Mungu.

  5. Kutokana na Neno la Mungu ni kwamba watakaoingia mbinguni ni watu waliookoka. Na watu kama wezi, wazinzi, waasherati, walevi na wote wasiojitakasa hawataingia mbinguni [Ufunuo 21:8; 1Kor 6:9-10]. Sasa mtu ambaye anajiita ‘ameokoka’ halafu ni mlevi, muongo, mwizi sidhani kama ni sahihi kumwita mtu huyu ameokoka [wakati huo anapoendelea na matendo hayo mabaya]. Ndiyo maana husemwa kwamba wokovu ni wa SASA. Si kwa sababu mwaka juzi mtu aliombewa Sala ya Toba, hapana… ni kwa sababu SASA anaishi maisha matakatifu. Kinachomfanya mtu awe ameokoka ni HALI YAKE YA SASA ANAYOISHI si kwa sababu hapo zamani za kale alisali sala ya toba. Ndiyo maana Yesu akasema si kila mtu asemaye Bwana, Bwana ataurithi ufalme wa Mungu. Kwa kuwa mtu aliyesali sala ya toba halafu akaendelea kuwa mwizi, muongo huyu hawezi kuurithi uzima wa milele. Au sivyo?

  6. Mtu anayesema ameokoka lakini anaendelea katika uovu hadi akafia huko huyo hakuwa na wokovu na wala hawezi kwenda mbinguni. Biblia inasema “heri wafu wafao katika Bwana maana watapumzishwa baada ya tabu zao.” [Ufunuo 14:13]. Mtu hawezi kuwa katika Bwana Yesu halafu anatenda maovu!

  Kujikwaa kidogo kwa Petro ninafikiri unamaanisha alipomkana Yesu? Lakini tukisoma maandiko tunaona kwamba Yesu alitambua kwamba Petro alikuwa hajaokoka kikamilifu. Aliuona moyo wa Petro. [Kwa ujumla ni kwamba alifahamu udhaifu waliokuwa nao wanafunzi wake.] Ndiyo maana alimwambia kwamba Petro katika Luka 22:32 hivi;

  ” ..lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike, nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako”. Kwenye kiingereza [KJV] neno lililotumika ni “…and when thou art converted..”

  Hii inaonyesha Petro [na mitume wenzake] walikuwa hawajaongoka [they were not converted yet..] hadi baada ya kifo na kufufuka kwa Yesu. Ndiyo maana pamoja na kuwa na Yesu lakini walikuwa wanakosea na kukwama katika mambo mengi, ambako wewe umeita kujikwaa kidogo. Ndiyo maana Yesu akawaahidi kupokea nguvu baada ya kujiliwa na Roho mtakatifu, katika Matendo 1:8 (ambayo pia umenukuu). Kwa maneno mengine ni kwamba kabla ya kupokea Roho mtakakatifu hawakuwa na nguvu. Baada ya kupokea Roho mtakatifu mitume walijawa na nguvu za ajabu na baada ya hapo mimi sifahamu andiko kuhusu tukio lolote linaloonyesha kwamba walijikwaa!

  Baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu, package ya Wokovu ilikamilika: Neno liko kamili na nguvu za Roho mtakatifu ziko kamili. Kwa hiyo kwa wakati wetu mtu anayetaka kuokoka, akimaanisha kuokoka huwa anaoongoka, yaani anakuwa-converted, anabadilishwa. Mtu akisema ameokoka halafu bado ana matendo maovu, huyo hajabadilishwa, hajawa converted. Wokovu kamili ni pale mtu anapokuwa converted.

  Simon yule mchawi, pamoja na kuamini na kubatizwa, moyo wake ulikuwa haujageuka. Ulikuwa bado umeshikilia heshima [self esteem], kwa sababu yeye alikuwa ni mtu aliyeheshimika. Na kitendo hicho hakikuwa chema mbele za Mungu, ndiyo maana Petro akamwambia ” Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu” [Mdo 8:21].

  Hapa nitafafanua kidogo…….

  Ukisoma vizuri maandiko unaweza kuona kwamba hata kuamini kwa Simon hadi kubatizwa kulikuwa ni kwa kufuata mkumbo na kutafuta maslahi binafsi. Katika kitabu cha Matendo Sura ya 8:

  i).Watu walikuwa wanamsikiliza kwa sababu aliwashangaza kwa uchawi wake na walimsifia sana. (8:10)

  ii).Watu aliowashangaza [wateja wake] wanamuamini Yesu kupitia Filipo baada ya kusikia habari njema za ufalme wa Mungu (8:12) na wanabatizwa

  iii).Baada ya kuona wateja wake wamekimbilia kwa Filipo na yeye akaona kilichopo ni kuamini na kubatizwa ili afuatane na Filipo aone mwisho wa mambo hayo ni nini (8:13)

  iv). Baada ya kuona watu walioamini wanawekewa mikono na kupokea Roho mtakatifu, yeye tayari akaona hiyo ni dili.
  Akapiga akili akaona cha kufanya ni kununua hiyo karama ili na yeye akiweka mikono kwa mtu apokee Roho mtakatifu. (8:18&19). Yeye alijua akipata kitu hicho heshima yake itarudi pale pale. Na wala maandiko hayaonyeshi kama na yeye aliwekewa mikono ili apokee Roho mtakatifu! Hii ni kwa sababu yeye hakuwa na haja hiyo, bali yeye alitaka kutimiza malengo ya kutunza heshima yake. Kama angekuwa amepokea Roho mtakatifu asingekuwa na mawazo tena ya kununua Karama hiyo.

  Tuendelee……

  Wako wakristo wengi kwa siku zetu ambao wameamini na kubatizwa lakini mioyo yao si minyofu mbele za Mungu. Na hata wengine wanaweza kuwa wanafuatana na watumishi wa Mungu katika huduma, kama Simon alivyoambatana na Filipo,lakini bado mioyoni mwao wameshikilia mawazo na kuendelea na tabia za kale kama vile wizi, tamaa mbaya nk. Kushikilia vitu hivyo, hata baada ya mtu kukiri wokovu {kama Simon}, ni kukosa unyofu wa moyo mbele za Mungu. Kinachotakiwa ni kutubu na kuacha kabisa ndipo mtu huyo atakuwa salama [Mdo 8:22]. Mtu anayeshikilia mambo maovu hata baada ya kukiri wokovu huyo yuko katika vifungo vya uovu kwa sababu hajauachilia wote.

  Wako wengi wanaokimbilia katika wokovu kwa sababu mbali mbali. Wengine kutangaza ‘kuokoka’ kumbe lengo lake ni kutaka kupata mke/mume aliyeokoka kwa kuwa anaamini mke/mume aliyeokoka siyo mhuni; Wako wanaoamua ‘kuokoka’ kwa sababu kasikia mtu ukiokoka unakuwa tajiri; wako wanaoamua ‘kuokoka’ kwa sababu kasikia mtu ukiokoka huwezi tena kusumbuliwa na wachawi nk, nk, nk. Hawa ndio watu ambao baada ya kuombewa sala ya toba na hata kubatizwa [kama Simon] utakuta wanaendelea na uzinzi, wizi, uongo na kila aina ya uovu! Wanaendelea hivyo kwa sababu wao hawakuokoka kwa ajili ya kwenda mbinguni bali waliokoka kwa sababu ya maslahi binafsi tofauti na kusudi halisi la Wokovu. Hawajawa converted! Hawa ndio baadhi yao huzunguka kila sehemu wakifanyiwa deliverence baada ya deliverence lakini utu wao wa kale hawataki kuuacha. Mimi nasema kwamba mtu wa namna hii ataendelea kufanyiwa deliverence hadi siku ya kufa kwake pasipo kuwa delivered. Kumbe deliverence kamili ni kuacha utu wa kale na kujifunza neno la Mungu ambalo ndilo lililojaa maelezo na hatua za ukombozi kwa watu kupitia imani katika Kristo Yesu!

  7. Yule mtumishi ambaye alikuwa anatumia leseni ya kughushi ni kwamba hakuwa amejifunza vizuri Neno la Mungu kwa maana kugushi ni Uongo. Lakini kiu yake ya kumtafuta Mungu ilimlipa kwa kuwa Mungu aliona kwamba huyo sasa kamaanisha ndiyo maana akamfunulia tatizo hilo. Kama hilo ni tatizo ambalo lingemkosesha mbingu mimi naona siyo sawa tukisema alikuwa ameokoka. Maana hakuwa salama kiroho. Kwa macho ya kibinadamu alikuwa anaonekana ameokoka lakini kwa Mungu alikuwa anaonekana bado kuna tatizo. Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Utumishi siyo tiketi ya kuingia mbinguni! Mungu wa mbingni na atusaidie ili tuweze kujichunguza maisha yetu kisha kuchukuwa hatua pale tunapobaini kuna tatizo!

  Kama mtumishi aliingia katika maombi ya kufunga hadi akapata ufumbuzi wa tatizo huu ni mfano kwamba kila mtu akidhamiria kumtafuta Mungu ni lazima atapata ufumbuzi wa tatizo lililoko mbele yake. Na kama kila mtu anaweza kupata ufumbuzi wa tatizo lake ina maana, kutokana na mada, atakuwa amejifanyia ‘deliverence’ yeye mwenyewe. Hivyo kinachokosekana kwetu watu ni ile dhamira halisi ya kutaka kukutana na Mungu kibinafsi ndiyo maana mtu anaona njia ya mkato ni kwenda kwa mtumishi akafanyiwe deliverence!

  Naomba kuishia hapa kwa sasa lakini nasubiri majibu ya maswali niliyokuuliza pamoja na masahihisho mahali ambapo nitakuwa nimeandika isivyo sahihi.

 83. wapendwa,Shalom naomba tu niwakumbushe kuwa strongholds are not neccesarily demonic or principality,inaweza kuwa mtu labda ameshikwa kwenye mambo mengine, kama kusengenya, hasira, wivu nk, labda tukubaliane kwamba hakuna walokole ambao bado wanasumbuliwa na mambo kama haya, and the list goes on and on. Biblia katika Rom 12:2 inasema Don’t be like the people of this world, but let God change the way you think. Then you will know how to do everything that is good and pleasing to him. In my opinion hatuwi super christian immediately tukimkiri bwana yesu kuwa mwokozi wetu,bali kuna mambo ambayo yanahitaji kuendelea kumuomba mungu atusaidie ili tuukulie wokovu wetu siku hata siku,Pia mtume paul alituonya kuwa tuna vita vya roho na mwili. Warumi 7:21-25 21The Law has shown me that something in me keeps me from doing what I know is right. 22With my whole heart I agree with the Law of God. 23But in every part of me I discover something fighting against my mind, and it makes me a prisoner of sin that controls everything I do. 24What a miserable person I am. Who will rescue me from this body that is doomed to die? 25Thank God! Jesus Christ will rescue me. Nionavyo mimi si vyema sana kujihesabu wenye haki mbele za mungu kwa kuwa tumezaliwa upya bali ni vyema kuendelea kukulia wokovu wetu siku hata siku.
  Bwana awabariki na tuendelee kujifunza na kusaidiana.

 84. Namtukuza BWANA kwa ajili ya kila mmoja anayeendelea kuchangia. katika kila mchango napata kitu,(naamini na wengine pia) hata ile inayo suggest kuwa ‘ukiona mambo hayo yanakufuatilia ujue hujaokoka kweli’, nao wamenisaidia, wananipa changamoto ya kuendelea kuchunguza maisha yangu ya wokovu. Imenifanya nirudie na kurudia somo la maana ya wokovu.Ninawaombea kuendelea kupokea toka kwa BWANA ili mzidi kutufundisha….Amen!

 85. Shalom,
  Asheri na wengine,
  ninachokiona Asheri unachanganya concept nzima ya kuzaliwa mara pili…. ni kweli kuzaliwa mara ya pili ni mapinduzi makubwa ndani ya mtu ila unasahau kwamba yanafanyaka kwenye eneo gani la mtu…rohoni,mwilini au nafsini… nilipookoka mimi sikuongezeka urefu wala kubadilika rangi ila kulikuwa kuna mabadiliko ndani yangu, kuwaza kwangu na kunia kwangu kumebadilishwa sana na neno la Mungu… Niliwahi kusoma Kitabu cha Mtumishi JOHN PAUL kinaitwa WEKA HURU UFAHAMU WAKO kilinisaidia kubadilika kwenye baadhi ya mitizamo ambayo siyo ya kibiblia….
  Uzuri ndugu Asheri hujaongelea Biblia inasemaje? ila uzoefu na uelewa wako … jaribu kuangalia Biblia inasemaje juu ya hilo….
  Angalia Hii Yohana 8:31-32
  8:31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;

  8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
  mstari 31 akawaambia wayahudi waliomwamini…..aka waliookoka/waliozaliwa mara ya pili…. pamoja na kumwamini Yesu kuna uhuru ambao hawakuwa nao bado…
  uhuru unapatikanaje? ni kwa kuifahamu kweli…..Kweli nini Yohana 17:17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli ….ok kweli ni neno la Mungu lugha nyingine ni Mafundisho sahihi ya Kristo kwenye eneo fulani la maisha ya mtu au ni neno la Mungu kwenye eneo fulani ya maisha ya mtu au maelekekezo yatakanayo na neno la Mungu kwenye eneo fulani ya Maisha ya mtu… ukijua kweli kwenye eneo fulani ukaamini ukatendea kazi kwenye hilo eneo unakuwa huru…. mtu ambaye hayuko huru kwa sababu hajui kweli fulani za Neno la Mungu utamwitaje?? Wapendwa tusaidaiane kujibu hapa……

  Mungu akubariki sana Asheri

 86. Bwana Yesu asifiwe sana!!

  Kuhusu kuokoka na kuacha maisha ya kale; kwa kweli wana wa Mungu ni wengi sana wanafanya hivyo na wako kwenye mstari kiroho. Lakini tukirudi kwenye maswala ya maendeleo kimwili kwa kweli hali inatisha sana. Ndio maana wengi wa Mataifa wanasema Watu wameokoka na bado ni maskini kwa kweli inatia huruma sana.
  Tumechoshwa na hali hizi za wana wa Mungu kuwa na maendeleo duni na huku imeandikwa tumiliki na kutawala, na Yesu alifanyika maskini ili sisi tuwe matajiri.
  Tusome pia vitabu vya watu waliopitia kwenye maagano na ulimwengu wa giza ili tujue jinsi ulimwengu wa roho unavyofanya kazi, japo kuna vingine sio vizuri. Kuna mambo madogo madogo ambayo wana wa Mungu wanapuuza kumbe yana effect kubwa sana kwenye ulimwengu wa roho.
  Juzi wakati nimemaliza tu kusoma mjadala huu akatokea dada mmoja from no where akasema ” basi jana tulikuwa tunafundishwa na mtumishi mbinu za kujinasua pale mtu unapobaki sehemu moja bila kusonga mbele, mara mama mmoja akalipukwa na mapepo yakilalamika ni kwa nini mtumishi anafundisha hizo mbinu za kujinasua na wakati wao(mapepo) wanataka wawatese na kuwakandamiza. Na mapepo yakadai kwamba yanamtafuta sana mtumishi. ”
  Kumbuka pale walikuwa ni wana wa Mungu wanafundishwa namna ya kujinasua.

  Hapa nilipata funzo kwamba shetani anaweza kukufungia pahala mpaka ujinasue hata kama umeokoka.

  Tunajifunza.

  Mugu atusaidie kwenye mjadala huu

 87. Bwana Yesu asifiwe!!

  Kaka Paul napata mafundisho mazuri kutoka kwako. Sifa na utukufu ni kwa Bwana Yesu. Issue kama leseni ya kughushi mtu waweza kuona ni jambo dogo kumbe ni kubwa sana kwenye ulimwengu wa roho, na moja kwamoja umekuwa mlango wa kuingilia mapepo. Mungu atusaidie sana. Hii inanikumbusha kijana mmoja alituonya ku- burn CD na kusema mabo madogo kama haya yatatukosesha ufalme wa Mungu. Nazidi kujifunza tusipuuzie mambo madogo.

  Unapompokea Yesu waweza kuwa na mambo yanayokufuatia mfano mzuri ni katika Luka 9: 54 Yakobo na Yohana wanakasirika na kutaka kuagiza moto, lakini walikuwa wamempokea YEsu na muda wote wako na Yesu si kimwili tu hata kiroho. Lakini Yesu aliwaambia hamjui ni roho gani mliyo nayo. Yakobo na mwenzake walikuwa wanawaza mauti tu lakini Yesu aliwaza uzima. Kwa hiyo kuna roho fulani walikuwa nayo ndiyo maana wakawaza kuagiza moto. Hata sisi roho hizo zaweza kufuatilia mtu aliyeokoka na kubaki kupiga marktime bila mafaniko kimwili na hata kiroho.

  Kwa utafiti mdogo ni kwamba kwa wale ambao wamezaliwa kwenye familia za wazazi waliookoka na maranyingi huwa hawasumbuliwi na vifungo kwani kwa vyovyote wazazi wao walishafuta maagano kwa hiyo watoto wanakuwa huru.

  Lakini kama mtu amezaliwa kwa familia zenye matambiko na kuabudu mizimu, mambo haya ya vifungo yanasumbua sana.

  Wenye uelewa mwingi wekeni hapa ili watu wa Mungu tujifunze wasiendelee kufungwa bali wamiliki na kutawala kimwili na kiroho bila kifungo.

  Tunajifunza

 88. Shalom kaka John Paul,
  ni kweli mtu ukisoma maelezo yangu unaweza usielewe, lakini lengo langu kuu ni kuuonyesha wokovu kama mchakato, wengi tunaitwa, tunatubu lakini wengi wanarudi nyuma, wenye juhudi binafsi wakisaidiwa na Roho mtakatifu wanasimama tena. Nahii process ndio ninayoilezea kuwa tuliahidiwa nguvu Matendo 1:8 na kila kitu kitachofanyika nasi kitategemea nguvu tuliyonayo Efeso3:20-21 zaidi hata kama kanisa/mtumishi ana nguvu kiasi gani iliyo ndani yetu ndiyo itakayofanya mchakato uendelee aidha mbele au kurudi nyuma ulikotoka.
  1. Sasa kwenye maswali yako kuwa binti angeweza kupona pale pale ni sawa kama wanavyosema wengine na kweli ni wengi tu wanapokea uponyaji hata wa mwili papo hapo, lakini pia wapo aina hii, mara nyingi sala ya toba watu wanasalishwa,kuna wengine wanatubu na kujutia maovu na kutoyarudia lakini kuna wengine kutokana na mazingira anaweza kuyarudia tena, kisha anavyoendelea kufundishwa neno ndivyo Imani yake inakua na baada ya kupokea Roho mtakatifu anakuwa amefikia hatua muhimu, sasa kipindi hiki ndicho unakuta wengi wanarudi nyuma, wengine kwa kujua au kwa kutojua,tuliwahi kuongelea hili kwa Mr Nice.
  2. Unaweza kumwita ndumilakuwili lakini inaweza kuwa sio ajabu kuwakuta watu wa namna hii hata ambao wamekaa muda mrefu ktk wokovu; je hakuna wachungaji wazinzi? (Kenya walimtembeza Askof mitaani)wezi? matapeli? wanaodanganya? hapa ndio ninasema suala zima la wokovu sio automatically unapona, unakuwa safi, unafunguliwa na kuanzia hapo hakuna uovu, kuna kukwama na kurudi nyuma lakini nguvu ya Roho Mt na Neno vitakurudisha ktk mstari,ni kitu kinachoendelea na juhudi ya mtu na kanisa binafsi vinahitajika.
  3. Kuhusu nani mwenye wokovu hiyo ni wazi ni yule aliyeomba toba, kujutia aliyokosa na kujitahidi kutoyarudia tena akisaidiwa na Neno kulishika na kulitenda, lakini kwavile wokovu ni mchakato kati yetu unaweza kutana na mwanafunzi mpya ambaye ndiyo anahangaika kuukulia wokovu na pia wazamani ambaye ndiyo hivyo anarudi nyuma. Ndiyo maana kulikuwa na Yuda Iskariot na Anania na Safira aliyeendelea nyuma hadi kifo, kuna kina Petro na Simon mchawi waliojikwaa kidogo na kuinuka kwa kujuta, je hawa hawakuwa na wokovu? labda nikuulize huyu mtumishi aliyekuwa anamwombea naye kwa kutumia leseni ya kughushi alikuwa ni nini? Isipokuw aRoho alimwongoza akajuta na kuacha.
  Nadhani hapa nimeeleweka.
  Asante, Rose.

 89. Shalomu,

  Nawashukuru wachangiaji wote kwa michango yao mizuri, hata hivyo, nadhani kuna haja ya kuangalia maana ya kuokoka au kuzaliwa mara ya pili. Hata hivyo, niombe radhi kuwa muda wangu ni mfupi hivyo sitaweza kuchangia sana na kuonyesha maandiko.

  Kwa uzoefu na uelewa wangu, mtu anapozaliwa mara ya pili anakuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo Yesu. Biblia inasema kuwa mtu huyu amehamishwa kutoka kwenye ufalme wa giza na kuingia katika ufalme wa Mungu. Mtu akishaokoka analindwa na nguvu za Mungu kwa imani yake katika Kristo Yesu.

  Ukweli ni kuwa wokovu ni mapinduzi halisi katika maisha ya mwanadamu, mabadiliko ya asilimia 100. Ndani ya wokovu kuna mambo mengi sana ikiwemo kuondokana na laana na kila aina ya vifungo.

  Lakini niseme kuwa, mtu akishaokoka anahitaji kufundishwa neno la Mungu na neno ndiyo litamfanya aweze kukuwa kiroho.

  Samahani ninatakiwa kuanza kazi, nitarudi baadaye nikipata fursa.

  Shalomu

 90. Dada Rose,

  Nashukuru sana kwa kujibu swali langu kwa kutokana na namna ulivyolielewa. Lakini nilichotaka kufahamu kutokana na nilivyouliza ni kile alichojibu ndugu Paul katika jibu lake namba 6 wakati akijibu maswali ya mpendwa Furaha. Ninashukuru sana mtumishi Paul kwa jibu hilo. Kwenye majibu yako kuna mafundisho muhimu ambayo nitayakumbushia tukifikia hapo kwa kadri mjadala huu unavyoendelea.

  Naomba kukuuliza dada Rose maswali kutokana na mfano wa binti aliyekuwa anaombewa halafu hakupona na kile ulichoongezea mwishoni:

  1.Kama binti huyo wakati anaokoka angefundishwa kwamba mtu ukiokoka inabidi uachane na aina yoyote ya maisha ya udanganyifu na pia kuondokana na mambo yote ya kale kama vile makaratasi ya waganga wa kienyeji

  i) Je, asingekuwa ameshafunguliwa hata kabla ya kuja kusumbuwa watu wanamuombea haponi kumbe bado ni ndumila kuwili?

  ii) Je, ni sahihi nikisema kwamba binti huyo alichelewa kufunguliwa kwa sababu alikuwa hajaingia sawa sawa katika wokovu?

  2.Umeandika hivi:

  “pia wengi wetu kubadilika ni vigumu sana. bado kuna wanaofanya uzinzi, kuna washirikina waaminio nyota, kuna wezi, wadanganyifu nk lakini tunajiita wenye wokovu mradi tumefanya sala ya toba!”

  i). Je, inawezekana mtu akawa ameokoka halafu akawa ni mtu mwenye tabia ulizozitaja hapo juu?

  ii) Je, mtu aliyeokoka ni yupi, au ni wote, kati ya hawa wawili?:

  a) Aliyeomba sala ya toba halafu akaendelea na maisha yake ya dhambi,[wizi, uzinzi nk] AU

  b) Aliyeomba sala ya toba halafu akabadili mwenendo wa maisha yake na kuanza kuishi maisha matakatifu?

  Natanguliza shukurani zangu kwa majibu ya maswali hayo niliyokuuliza.

 91. Bwana asifiwe,
  Dada Furaha naomba nikujibu maswali yako….
  1.Biblia imeweka wazi kabisa kinachozaliwa mara ya pili nini kati ya mwili, nafsi na roho soma Yoh 3:4-6….. Kinachozaliwa kwa Roho( imeanza Cap R maana yake Roho Mtakatifu) ni roho ( small r maana yake ni roho ya mwanadamu), Nasfi(mind) inabadilishwa kwa neno ili uweze kunia, kuwaza sawa sawa na kilichofanyika kwenye roho, Warumi 12:1-3, Mwili unaotoa kama dhabihu, jaribu kujifunza kwa makini man in three dimensions spirit, soul and body…Pamoja na hayo bado kushughulikia shida iliyopo kwenye Mwili au nafsi sio kwamba Yesu ametuachia tujiokoe wenyewe na unajua wanadamu ni natural with our natural ability we cant deal with supernatural…. Kuomba juu ya shida iliyopo kwenye mwili au vifungo bado nguvu inatokana na kazi ya Bwana yesu ya msalaba, Tunatumia neno, nguvu za Roho Mtakatifu, Damu ya Yesu na Jina la Yesu… mimi sijamuelewa dada furaha kama kuomba kwa ajili mtu mwenye shida za nguzu za giza kwa jina la Yesu au Damu ya Yesu hapo Yesu anakuwa ametuachia tujikomboe wenyewe…. ninachojua mimi mkibiblia tunaomba kwa jina La Yesu Nguvu za Roho Mtakatifu ndo nzinatenda kazi baada ya kulitatumia Jina Yesu…. Ushauri jifunze pia namna ya Kutumia Mamlaka ilyopo ndani ya Kristo….

  2 kuhamishwa kutoka katika ufalme wa giza kwenda katika ufalme wa nuru … ni kitu kinachotokea katika ulimwengu wa roho na ni roho zetu ndo zinazohamishwa maana yake tunakuwa citzen wa mbinguni katika ulimwengu wa roho na Wa jamhuri wa muungano wa Tanzania katika mwili. nguvu za giza hazifungi roho ya mtu aliyeokoka… vifungo vinakuwepo kwenye nafsi au Mwili… watu waliokoka hawawezi kuwa possesed na mapepo ila wanaweza wakawa oppressed na mapepo kama wasipojua namna ya kutumia mamlaka waliyonayo na nafasi tuliyonayo katika ulimwengu wa roho baada ya kumwamini Kristo au kuzaliwa mara ya pili….

  3. Issue ya Timetheo, si kila shida iliyopo ni nguvu za giza au vifungo, kuna magonjwa ambayo ni natural kabisa na unaweza ukanywa dawa ikaisha na mengine ni Demonic ili kutibu inabidi umtoe pepo… ili kujua shida chanzo chake ni nguvu za giza au natural ni lazima Roho Mtakatifu akupe signal…
  Hatujua kwanini Mtume Paul Hakumuombea Timotheo biblia haijaweka wazi mi na na amini kuwa angemuombea angepona haijalishi chanzo cha tatizo nini maana kwa jina la Yesu Magonjwa Yote yaweza kupona… Labda ndivyo Roho Mtakatifu alivyo muongoza kufanya…
  Pia usihusishe ukubwa wa huduma ya mtu na shida aliyonayo maana unaweza ukawaombea watu wakapona magonjwa yao ila wewe mwenyewe ukawa bado unaumwa…hapa siri yake nyingine tutaingolea Mungu akipenda…..

  4.Dada furaha nafikiri umeshindwa kuelewa huu mfano nilioutoa hapa katika mdo 8:5-14 Petro anamwambia Simoni aliyekuwa mchawi nakuona huu katika vifungo vya uovu…. Nilichotaka watu waone hapa ni kwamba Simoni aaliyeamini( akaokoka aka kuzaliwa mara ya pili, akabatizwa nadhani kwa maji mengi)… bado ameonekana kuwa na vifungo vya uovu… mikataba au sio mikataba mie sijaongelea hapo… huu ni mfano wa kwenye biblia kuna mtu ambaye aliokoka lakini bado alikuwa katika vifungo vya uovu…kwa nini Mtume Petro hakumfanyia maombi ya ili afunguliwe mimi sijui… ila nafikiri Petro alikuwa hajui historia ya simoni… sijui kama alikuwa anajua kudeal na case kama ya simoni naamini mpaka Hii sura ya Mdo 8 bado walikuwa hawajaua kweli yote… ndo maana walikuwa hawajui kama mataifa pia wanatakiwa kuhubiriwa neema ya wokovu mpaka ilipofika mdo 10 ndo petro akajua hiyo pia….

  5. Wakati wa Yesu Biblia imeonyesha wazi kabisa alikuwa akiwatoa watu kwenye vifungo vya nguvu za giza… mitume pia imeoneka waliwaombea watu wakatoka pepo wachafu na kuponywa magonjwa yao… Shida hapa kuiita Deliverance kama huduma inayojitegemea naona sio sawa ministrial gift ni tano Mitume. manabii, walimu, wainjilist na wachungaji na karama ni 9…. deliverance ni kama sehemu ya uponyaji kwa hiyo inaweza ikawa imebebwa ndani ya yeyote kati ya hizi huduma tano, Kama wewe ni mtume/mchungaji nk ukafanya maombezi watu wakafunguliwa katika nguvu za giza hiyo si ndo wanayoita deliverance…. ila kuna EXTREME TEACHING kwenye hili eneo kama ilivyo kwenye maeneo mengine kama prosperity nk
  kwa mfano ili mtu afunguliwe lazima atapike…….

  6. hatuoni hizo historia kwa sababu inawezekana waliokoka na kufunguliwa katika nguvu za giza moja kwa moja, mfano mtu anaweza kuokoka leo na kuponywa shida zake hapohapo na mwingine kaokoka leo ila akoponywa mwezi ujao….
  Nimewahi kudeal na watu aliokoka akafunguliwa hapohapo wakati namuongoza sara ya toba, nikamuongoza na kukataa kongwa zote za nguvu za giza… Wakalipuka pepo nikawafukuza kwa Jina La Yesu wakamwachia ….GlORY TO GOD .. ukiwa makini kumsikiliza Roho Mtakatifu wakati unamuongoza mtu kuokoka unaweza kushughulikia vifungo pia wakati huo huo… hapa JOHN PAUL nitakuwa nimejibu swali lako pia.

  8. labda nikuulize swali Mtu ambaye ameokoka halafu bado ni masikini au ni mgonjwa je kazi ya Yesu haijakalika kwake? maana Biblia inasema YESU alikichukua laana zetu, Umasikini na magonjwa yetu…. Kwa kupigwa kwake tuliponywa.. soma vizuri tuli…. wakati Yesu anatuokoa wakati huo huo alikuwa anatuponya, anatufanikisha, anatufungua na vifungo vya giza… sasa we hushangai aliyeokoka leo akaponywa mwezi hujao….aliyeokoka leo umasikini ukaisha baada ya miaka 10, ila kinachokusumbua ni wakati tofauti wa kushughulikia kuupoka wokovu yaani kuzaliwa mara ya pili na siku tofauti ya kufunguliwa na vifungo vya nguvu za giza….
  Biblia inasema warumi 8:17 imani huja kwa kusikia….. ukisikia injili ya kuokoka ukaiamini utakoka ila unaweza kuendelea na shida zingine kama kawaida… ukisikia injili ya uponyaji ukaamini utaponywa ila unaweza ukawa masikini bado aka huna hela…. na ukisikia injili ya kutoka katika vifungo vya giza ukaamini na kuitendea kazi vifungo vya giza vitakuachia….. na ukisikia injilin ya kufanikiwa nktk Kristo ukaamini utaanza kufanikiwa na kutoka kwenye umasikini…

  9. Sijajua unachukuliaje kuokoka au mtu aliyesimama … tukifanya evaluation kimaandiko unaweza humu mtandaoni wote hatujasimama… ila mtu ambaye amemkubalin YESU kama Mwokozi kwake na Hajamkana anaendelea ukiri huo wewe hutamwitaje? ameokoka au… mapungufu kila mtu anayo na kazi ya Roho Mtakatifu kutukamilisha mimi sijakamilika asilimia 100 sasa sijui utaniitaje? nimesimama au la?
  Mara nyingi zikisoma Neno nagundua mapungufu mengi kwenye maisha yangu… nakugundua upungufu mkubwa wa udhihirisho wa utukufu wa Mungu…..

  Pia Asilimia kama 90 hivi wamefunguliwa kabisa kwenye hizo shida walizo zitaja tukawaombea… Maisha ya mwanadamu yanamaeneo mengi sana unaweza ukashaghulia eneo moja na lingine bado ina bidi wajue kweli ya Mungu kwenye hayo maeneo wayashulikie, mfano unaweza ukapona ugonjwa lakini ndoa yako ikawa bado ICU, ukijua kweli ya Mungu kwenye Ndoa ndoa itapona…

  Niishie hapa kwa leo Mungu awatunze wasomaji wote …
  NEEMA YA BWANA YESU IWE PAMOJA NANYI NYOTE AMINA.

 92. Naomba tena niulize hili, Je hao wapendwa wanaofunguliwa huwa wanakuwa perfect hawana tatizo tena lolote ktk mwili? hawaugui tena? bishara zinakwenda barabara hadi Yesu atakaporudi? Na je deliverance inawasaidia kuishi maisha MATAKATIFU thereafter?

 93. Nafuatilia maada hii kwa karibu nikiendelea kujifunza.
  Kwa Ndugu John Paul mi naona hayo yakifanyika imetosha na mtu hana sababu ya kuwa na wasi wasi wa kufuatiliwa na laana ya vizazi na mambo kama hayo. Nadhani kinachofuata ni mtu kujitahidi na kutafuta kuishi kulingana na Neno la Mungu linavyoagiza kuhusu utakatifu. Mahali fulani ktk Mithali nadhani imeandikwa ‘Aogopacho mtu ndicho kimjiacho’!
  Ingawa sijapata muda mzuri wa utulivu wa kuchangia lakini kwa haraka napata maswali kadhaa ambayo mojawapo ni haya hapa
  1. Hivyo tuseme wokovu ni wa roho tu i.e Yesu alifanya kazi ya kuokoa roho akatuachia tujiokoe (tujifungue/tujikomboe?)miiili na nafsi zetu?
  2.Kuhamishwa kutoka ktk ufalme wa giza na kuletwa ktk ufalme wa nuru wa mwana wa pendo lake maana yake ni nini kama bado nguvu za giza zinamfunga mtu huyo huyo aliyemwamini Yesu hata akishakuwa ktk Ufalme wa NURU?
  3.Timotheo alikuwa ana matatizo ya tumbo na magonjwa ya mara kwa mara tena kwa nyakati hizi tungesema Paulo alimpa ‘an aukward’solution ya kutumia kileo, kwa nini hakumfanyia deliverance? Je huyu alibeba utumishi mkubwa kiasi kile still akiwa chini ya vifungo na mikataba ya kuzimu?
  4. Kuna mpendwa hapo juu ametoa mfano wa Simon mchawi alipookoka na Petro anamwambia anamwona ana vifungo vya uovu (ingawa uelewa wangu hapo ni tofauti na mchangiaji huyo kuwa sioni kama ana maanisha bado Simon ana mikataba ya mashetani), kwa nn hatuoni akimfanyia maombi ya ukombozi?? Badala yake Simon anapondeka na kunyenyekea akaomba Toba?.
  5. Ni wapi ktk Biblia tunaiona hiyo huduma ikifanya kazi hasa ktk Kanisa lla kwanza/ agano jipya?
  6. Watu wengi waliomwamini Yesu nyakati za Yesu na mitume na wengine waliofunguliwa mapepo wakaamini, mbona hatuoni historia ya wao kurudi tena ktk maombi ya deliverance?
  7. Wapendwa tunapotubu na kumpokea Kristo, hiyo toba haiwi kamili huwa kuna vitu vinabaki?
  8. Je tuseme kazi ya Yesu ya kumwokoa mwanadamu haikukamilika kuna mapungufu?
  9. Watu wengi wanatoa experience wakisema kuwa walikuwa ‘wameokoka vizuri tu’ lakini bado wakawa na hivyo vifungo, labda hili naliona kama too personal kwa sababu mtu huwa hajishuhidii mwenyewe huko kuokoka vizuri tu ni nani anayeweza kukudhibitisha? Je wanajipima ktk NENO la Mungu au kitu gani?
  Wapendwa bado nina maswali mengi kuhusu mada hii ila kwa sasa naomba niache haya kwanza yamkini nikisaidiwa majibu naweza kujifunza zaidi.

  Samahani sijaweza kunukuu maandiko moja kwa moja kwa sababu ya muda ila next time nitaweka vifungu vya maandiko husika.

  Natamani Sana kujifunza Kweli ya Neno la Mungu kuhusu hili na siyo Experience tu. Msingi wetu ni Neno la Mungu tu. Naomba uthibitisho wa maandiko.

  Bless you dears!

 94. Bwana Yesu asifiwe sana!!

  Kuna kufanya toba sahihi pia. Ndio maana tunaambiwa kwenye neno kwamba tuziangalie njia za kale na kujua wapi tulipoanguka ili tutubu.

  Kwa hiyo waweza kufanya toba lakini ikawa si sahihi. Kwa mfano unaweza kutubia utoaji mimba kwenye familia yako. Lakini ukaendelea kuona matukio kama hayo yanaendelea. Kumbe labda tatizo linatokana na mababu waliomtoa mtu mimba zamani hizo may be kama kafara n.k. Kwa hiyo utatubu kwa dhambi ile ya mababu na kung’oa kabisa ule mzizi.

  Kwa jinsi nilivyofundishwa kabla hatujafanya toba tuchunguze chanzo chake kwa kuuliza waliotangulia au unaweza kumwomba Mungu akupe mafunuo.
  Tunajifunza

 95. Naomba niwape mfano wa binti mmoja ambaye alikuwa akiombewa katika huduma yetu. Mtumishi alishangaa kwanini imemchukua huyu binti muda mrefu hivi kufunguliwa mapepo pamoja na kuwa ameokoka. Mtumishi akaingia katika kufunga na kuomba Mungu amwonyeshe nini kinatakiwa; kwanza alionyeshwa udhaifu wake (alikuwa anaendesha gari kwa leseni ya kughushi isisyo halali) pili alionyeshwa binti yule anapokaa nyumbani wanaendelea kutunza vitu ambavyo ndivyo vilimletea vifungo, anamakaratasi na vitu alipewa kwa waganga bado anavitunza (ina maana anaviamini bado).
  Kilichofuata ni kutubu kwa Mtumishi na kumweleza kwa utaratibu binti ili kwa ufahamu wake na si kushurutishwa aachane na hivyo vitu, binti yule alifunguliwa mara moja! Sasa unakuta mtu akienda akiombewa mara moja tu hajapona kahama, au kakata tamaa pia wengi wetu kubadilika ni vigumu sana. bado kuna wanaofanya uzinzi, kuna washirikina waaminio nyota, kuna wezi, wadanganyifu nk lakini tunajiita wenye wokovu mradi tumefanya sala ya toba! Na haya yapo hata katika watumishi pia, sia ajabu kama wale mitume na mtoto bubu nao inabidi warudi wajipange upya ndipo watu wanahoji oh mbona wanaombewa kila leo. Tunajifunza

 96. Shalom ndugu John Paul, naomba nikujibu swali lako ndiyo huyu mtu ataendelea kusumbuliwa kama hajafunguka wakati alipoombewa sala ya toba, na kuna wengine anaweza kuombewa hata zidi ya mara moja na ikamchukua muda kuona mabadiliko. Hapa ndiyo niliposema kuna nguvu inayotumika ina uwezo gani Efeso 3:20-21, naomba nikupe mfano huu:
  Katika kisa kile cha baba mwenye mtoto bubu;
  1. Uponyaji unategemea imani ya mtu anayeombewa, huyu mzazi hakuwa na imani na wale mitume hivyo kijana wake hakufunguliwa pamoja na maombi yao Marko 9: 17-24
  2. Uponyaji unategemea nguvu ya mtumishi, mara Yesu alipokuja alimkemea pepo akamtoka Marko 9: 25-29 hapa tunaona Yesu mwenyewe akiwaambia kuwa kuna namna ambayo haitoki isipokuwa kwa kufunga na kuomba.
  Hivyo mtu unaweza ombewa na watu wengi lakini ukaja kupona kwa mtumishi mwingine inategemeana imani yako umeweka wapi na nguvu inayotenda kazi katika mtumishi au kanisa husika.
  3. Uponyaji unategemea na nguvu au maombi ya mtu hii ndiyo kama Mtumishi anavyosema Mary, lakini hii ni muhimu kujua kila muamini aliahidiwa kupokea hii nguvu Matendo 1:8 na huyu Roho mtakatifu atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya Yesu, katika kufuatana na hayo ndiyo kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi vitakwisha Galatia 5: 16-25, Luka 22: 40-46. Kadri unavyoenenda kiroho na kuepuka maovu na kudumu katika maombi ndivyo unavyofunguliwa vifungo vya nafsi kwa kuombewa au kwa nguvu itakayokuwa ikitenda kazi ndani yako kupitia Roho mtakatifu.
  Napenda kurudia tena sala ya toba pekee haitoshi kumfungua mtu kama anavifungo, pili sio imani tu bali na juhudi binafsi ya mtu vitasaidia kumweka huru, nina mifano ya wengi walio katika wokovu na bado wamo katika vifungo vya nafsi na mwili wengine hata wanahudumu hivyo hivyo, kwanini aidha mtumishi hakuwaombea na kuwashauri ipasavyo kuukulia wokovu au wao ni wale wanaotaka kupokea tu miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote kiroho, bila kusoma na kuliishia Neno, bila kuomba. Tuendelee kujifunza

 97. Shalom,

  Dada Mary Sabihi nimeusoma vizuri mchango wako. Mwalimu alipofanya hivyo kama alivyoambiwa na Bwana Yesu akaponywa mara moja (hakuchanjwa tena)

  Kuna kitu mpaka sasa sijaelewa vizuri katika huduma hii ya ukombozi. Nimeshawahi hudhuria lkn sikuelewa vizuri

  1) Je watu hufanya bila kumuuliza Yesu au?
  Naona watu kila siku, miaka sasa wanatubia uovu ule ule, je mara moja haitoshi? au kuna tatizo la kuamini na kupokea?

  2) Kama tatizo hilo kwako halipo, unaamini limekwisha au haulijui, kwanini watu wanaendelea kukiri na kuomboleza sawa sawa na wengine?

  3)Labda ufunuo huu wa ukombozi haujaeleweka sawa sawa? Au inawezekana tafsiri ya neno hili linatuchanganya, kwamba inawezekana si kitu cha pekee sana ila ni maombi kama mengine cha msingi ni kujua jinsi gani na wapi pa kuyafanya kwa uongozi wa Roho Mtakatifu?

  Nami nasubiri kujifunza zaidi.

 98. Nikiwa ni mmoja wa wanaofuatilia mjadala huu, baadhi ya mambo niliyojifunza hadi sasa ni kwamba mtu anaweza kumpokea Yesu moyoni lakini akaendelea kusumbuliwa na nguvu za giza kutokana na kuendelea kwa mikataba na maagano ya damu yaliyofanyika kati yake na ulimwengu wa giza. Ili kuondokana na hayo inabidi afahamu suluhisho sahihi kama vile alivyoambiwa kufanya mwalimu aliyejitolea mfano maisha yake mwenyewe katika mchango wa dada Mary Sabihi ambako ni Kutubia uovu wote, kuvunja maagano yote na nguvu za giza na kuweka Agano kwa Damu ya Yesu.

  Kitu kingine ambacho nimekipata toka katika michango iliyotangulia ni kwamba mtu anaweza kuomba maombi ya ukombozi yeye mwenyewe, kama atakuwa na nguvu hizo,[kama mwalimu wa semina wa dada Mary Sabihi] lakini kama hana nguvu za kutosha ndipo inabidi aende kwa mtu mwingine mwenye nguvu zaidi ya kiroho.

  Jambo la tatu nililojifunza ni kwamba maagano ya damu katika ulimwengu wa roho hudumu hadi hapo yatakapovunjwa kwa agano la damu ya Yesu Kristo. Kwa hiyo mtu ambaye hakuwa na historia ya maagano katika familia au ukoo wake yawezekana asiwe na maagano ya nguvu za giza ya kuvunja.

  Kwa kuwa tunajifunza, ninauliza swali kwamba Je, mambo hayo, [yaani Kutubia uovu wote, Kuvunja maagano na nguvu za giza na Kuweka agano kwa Damu ya Yesu] yakifanyika wakati mtu anapoombewa au anapoomba Sala ya Toba, bado mtu huyo ataendelea kusumbuliwa?

  Nitajifunza vizuri sana kama swali langu litajibiwa.

 99. Juma lililoishia na tar 23/05/2010 tulikuwa na semina ya maombi , ambayo ilifundisha juu ya mahali sahihi pa kuombea .Ndani ya mada hiyo kukawepo na maswala ya madhabahu na jinsi yanavyosumbua hata kama umeokoka. Mwalimu alitoa mfano wake yeye mwenyewe, kwamba aliokoka mwaka 1993,na alimpenda Mungu sawa sawa kilichomshangaza ni kuona anaendelea kuchanjwa na wachawi,hii ilimumiza sana akijiuliza maswali mengi kuwa ni uovu gani bado hajaucha?.Ilipofika mwaka 1997, siku moja usiku wa saa nane aliamka akamwomba Mungu sana, na kumuuliza kwa nini anaendelea kuchanjwa na neno linasema yote yalikwisha pale msalabani? ndipo Yesu aliposema nae kwamba ni maagaano ya damu na mashetani, akamuliza kwa vipi? akamkumbusha matambiko na ibada za mizimu zilizokuwa zikifanyika kifamilia, na kwa waganga alikokuwa akienda kwa hiari yake mwenyewe n.k kwamba hakuzikataa na kuvunja maagano na wanganga, na mizimu, na madhabahu zilizokuwa zikifanyiwa ibada( na ibada hizo damu za wanyama au ndege zilitumika kuimarisha maagano hayo),ndipo alipomuliza Yesu sasa afanyeje? akamjibu, kwanza kutubia maovu yoote, pili kuvunja maagano na mikataba yoote kama alivyomwelekeza na tatu kusimamisha DAMU YA YESU kati yake ( DAMU iwe ukuta) na kuweka agano kwa DAMU ya Yesu.Alisema baada ya kumaliza maombi hayo, hakuchanjwa tena hadi leo hii(2010).
  Alisema kule kuvunjwa kwa mwili wa Yesu ndio alama ya ukombozi ,kwa kuwa ulikuwa mwili wa dhambi (asili)uliobeba dhambi, kwa sababu mwili kama mwili una majivuno, kiburi,tamaa mbaya na tabia zote za mwilini kupitia nafsi, hivyo ni lazima vishughulikiwe kwa sababu alisema hata kabla hatujazaliwa tulikuwa tukishiriki zile ibada kwa asilimia 100.
  Nitoe maandiko kwa uchache;
  Mwan 31:31yote na 35:16-17 ni habari inayomhusu Yakobo na Labani ambapo miungu ya Labani iliibiwa na Rahel binti yake, bila ya Yakobo kujua wakaapizana (waswahili wanasema)kwamba aliyechukua na lolote litokee, matokeo ni kifo cha Raheli wakati akijifungua mtoto Benjamin.
  2 Sam 11: na sura 12 habari yamfalme Daudi na Uria na jinsi Mungu alivyokasirika na kukusudia mabaya ktk uzao wake wote, na yule mtoto aliyezaliwa na mke wa Uria Mungu hakumwacha aishi,ule uovu uliondoka nyumbani mwa Daudi kupitia kifo cha yule mtoto, ndio maana Daudi aliacha kuomboleza akala chakula, bila tendo hilo kufanyika damu ya Uria ingelia siku zote kupitia mtoto yule.
  AMUZI 6:26-30 Gideon pamoja na kuchaguliwa ili awaamue waisrael, Mungu alimwembia avunje madhabahu na miungu ya baba yake kisha ajenge nyingine kwa maelekezo yake.
  EFE 2;2-11-16.
  Ufu 2:12-16 Kanisa la Pergamo lilimpemda Mungu sawasawa na kulishika jina lake Yesu lakini , wakati huo huo walikuwepo walioshika mafundisho ya Balamu, wengine ya Wanikolai, YESU aligiza kutubu .
  Hapo mimi naona, ili tusijikwae kama mtu anaona haamini ukombozi baada ya kuokoka basi na awe huru na yule ambaye anaamini ukombozi au kufunguliwa kwa ushuhuda wa matukio halisi katika maisha yake basi na aendelee kuamini hivyo .
  Ninahitimisha kwa kusema kuwa ni kweli wako watu hawajui mambo ya jadi, mila, matambiko (mambo ya ufalme wa giza), na ambao wamezaliwa na kukuta familia zao haziamini mambo hayo na hata historia zake hawanazo , kwa upande mwingine wako waliokutwa au kupitia mambo niliyoeleza hapo juu, na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu wakafanikiwa kutoka kwenye vifungo , maana hata duniani ipo methali isemayo aisifuye mvua imemnyeshea.
  Naomba niendelee kujua zaidi ya ninavyojua kupitia kwenu.

 100. Shalom Wapendwa,
  Hii mada ni nzuri na itakuwa na msaada sana kama tutaijadili kwa nia ya kujifunza na sio kwa kutetea misimamo ambayo tulikuwanayo au ya makanisa tuliyotoka au tunayosali……
  Nianze kusema kwamba kifo cha Bwana Yesu ndicho kilileta Wokovu( kuzaliwa mara ya pili), uponyaji, mafanikio, na kututoa kwenye laana zote kwa ujumla wote huu ndio ukombozi,
  1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;1:14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
  Tunapookoka Biblia inasema Taza ukiwa 2kor 5:17, Yoh 1:12, 3:4-6
  haya maandiko yanatuonyesha Tunapookoka nini kimefanyika, Tumefanyika kiumbe kipya, Tupefanyika watoto wa Mungu, Tumezaliwa mara ya pili,
  Tuangalie Mtu yupi anayezaliwa mara ya pili, Yohana anasema Kinachozaliwa Na Roho(Roho Mtakatifu) ni roho( ni mtu wa ndani- roho wa mwanadamu) Na Mambo yote yamekuwa mapya ya kale yamepita ni hapa katika roho ya mwanadamu, 1Thes 5:23 Paulo Mtume ametofautisha kati ya roho, nafsi na mwili, Tunapoamini injili ya wokovu tunazaliwa mara ya pili…. wapi roho zinafanywa upya … lakini nafsi na mwili bado…. Biblia inasema imani huja kwa kusikia, warumi 10:17, ukisikia injili ya wokovu ukiamini unaokoka lakini unaweza ukaendelea kuwa masikini, mgonjwa, na vifungo vingine… angalia hapa uponyaji na wokovu vyote ni package moja maana Biblia inasema 1 Petro 2:24…..Kwa kupigwa kwake mliponywa….. jiulize pzmoja na mimi… Wangapi wameokoka lakini magonjwa ni mzigo mkubwa sana kwao… wangapi wameokoka na umasikini ni mzigo mkubwa sana kwao…. Nasema hivi mtu anaweza akawa ana Vifungo vya nguvu za giza akazaliwa mara yapili na vifungo vikaendelea kuwepo kama asipo amini na kuitumia injili ya kuvunja vifungo vya nguvu za giza kwa mamlaka ambayo Bwana Yesu ametupa, sawa sawa tu na mtu ambaye ameokoka na bado anaumwa umwa kila siku……
  Angalia mfano huu hapa katika kitabu cha matendo ya mitume 8:4-13 Mchawi Kaamini injili ya Filipo kaokoka na kubatizwa, anangalia kitu ambacho Mtume Petro anamwambia Mdo8:23 anamuona yupo katika vifungo vya uovu, Tafakari kwa makini sana hiii mdo 8:4-23,
  Nimewahi kukutana na mama mmoja ameokoka miaka kama kumi hivi ila ila aendelei kiroho kabisa na kila alipokuwa akianzisha biashara lazima ife, akiwa kiongozi wa kikundi chochote lazima kife na ameokoka baada ya kuomba nguvu za giza zikalipuka alifungwa na mama yake wa kambo ambaye alikuwa mchawi, Mwingine naye ameokoka ila huwa anaota nyoka anamtembelea kitandani analala naye… tukafanya maombi pepo zikalipuka wote walifunguliwa…. Mwingine Binti alikuwa haelewani na bosi wake kabisa hata akimsalimia bosi haitiki maisha yake yalikuwa magumu sana hapo kazini Bibi yao alikuwa amewafunga..Nilipoomba Nguvu za giza zikamwachia na aliporudi kazini hiyo shida haikuwepo tena, wakawa na maelewano mazuri tu na bosi wake…
  Siku moja alikuja mama mmoja mlokole akaomba nimuombee anasumbuliwa na nguvu za giza Mizimu ya kifipa…. Wakati naomba mizimu ikalipuka ikasema huyu si tumepewa toka akiwa tumboni…. nikawauliza aliyewapa nani na wapi? mizimu ikasema wazazi wake walimkabidhi kwa mizimu akiwa tumboni na maagano yalifanyika kwenye milima huko ufipani….. Nikawaambia mimi kama kuhani wa Mungu aliye juu naomba rehema kwa ajili yake na wazazi wake akwa uovu waloofanya…halafu nasafiri mpaka kwenye hiyo milima na kuvunja hayo maagano mkwenye hiyo ardhi…. Nikawaamuru wamtoke wakatoka…

  Kama umeokoka na unaona kuna dalili ya nguvu za giza kufuatilia au kushambulia sana maisha yako au kukandamiza baadhi ya maeneo chunguza unaweza kuta kuna uhalali fulani ambao mashetani wanaupata hapo na ni vema kuushughulikia hata we mwenyewe ila kama huna msuli wa kutosha tafuta msaada( majeshi ya Kukodi)
  pia kuna kupitiliza kwingi kwa watu wengi wanaofundisha haya mafundisho ya ukombozi tuwe makini kidogo hapa,

  Mimi huwa siiti delivarence, naitaga maombi tu…. kwa wakati mtu akiwa anaona anashida na anahitaji maombi nitamuombea… tunatumia neno pamoja na maombi….
  Na kama hizo nguvu za giza ni uhalali kukaa kwa mtu ni lazima kuuondoa huo uhalali wake kwanza ndio umtoe maana wale viumbe hawana nguvu ila wanatumia kufanya siri ili kuwakandamiza watu….

  Mungu awabariki sana….
  Wakati mwingine nitachangia tena

 101. Asante Shoo GAP na Pastor Thobias, nitarudi hapa kujaribu kueleza kwa kutumia Neno (mistari) kama alivyosema John Paul.
  Ila tu napenda kusisitiza kwamba hata wakati wa Yesu alifanya delivarence (kufungua) isipokuwa inategemea kifungo kiko wapi rohoni, mwilini au katika nafsi.
  katika vyote Imani ni muhimu, kwani bila ya hiyo huwezi kumwendea Mungu, lakini kuna nguvu itakayohitajika kukutoa katika hicho kifungo:
  1. kutoka kwa Mungu kupitia kwa watumishi wake
  2. kutoka kwa Mungu kupitia Neno lake
  3. Kutoka kwa Mungu moja kwa moja kwako kwa maombi yako ukiongozwa na Roho wake mtakatifu
  So ukombozi kamili wa mtu ni mchakato(a process) ambao sio tu unamhusu Yesu msalabani, bali mtumishi anayehusika, imani na juhudi binafsi ya mtu husika.
  Lakini tu ninapenda kusema hivi vifungo vya roho ni mojamoja kwa ukimkiri na kumpokea Yesu unafunguliwa ila mwili na nafsi vitaendelea kupingana na roho ni wajibu wako kujitahidi ukisaidiwa na watumishi wa Mungu na waokovu wenzio (maana kila mwokovu ni mtumishi na ameokolewa kwa kusudi maalumu) kujifungua nafsi hii iliyofungwa ktk vifungo vya shetani.
  Sasa kuna hili la vifungo vya mwili, hili tunaona ndiyo linachanganya maana wengine wamefikia kuacha wokovu mradi tu haponi ugonjwa, ulemavu, nauliza je Timotheo alikuwa na ugonjwa, Paulo alikuwa na ugonjwa na hata kufikia kuambiw ktk udhaifu huu wa kimwili ( na si wa roho au nafsi) ndipo kusudi la Mungu kwake linatimia.
  Tunajifunza

 102. Friday, May 22, 2009 at 7:48 am nilituma maswali hayo hapo chini kwenye mjadala wa MASWALI wenye kichwa cha Deliverence.
  Ninaomba mni-fungue na mimi ili niondoe ujinga. Tarehe Monday, November 16, 2009 at 1:33 pm nikatuma changamoto au maswali haya haya kuhusu Delivarenc(Ukombozi) kwenye thread yenye kichwa UKOMBOZI NI NINI? Hadi sasa nasikitika sijapata majibu. NINAOMBA SANA SANA YEYOTE MWENYE MCHANGO ANISAIDIE.

  Ninajinukuu
  “Namshukuru Mungu kwa ajili yenu mliojaribu kujibu.
  Tunapoendelea kujifunza, tujaribu kujibu maswali haya pia.
  (1) Kama maana ya Delivarence kwa kiswahili ni Ukombozi au kufunguliwa; Ni wakati gani inapaswa ifanyike delivarence? Kabla, wakati au baada ya kuokoka, inafanyika mara ngapi kwa taratibu gani?
  (2) Watu gani wafanye hiyo delivarence? Hao wanaofanya delivarence wao je wanahitaji wafanyiwe delivarence? au walishafunguliwa kabisa?
  (3) Kati ya Neno la Mungu na Maombi ni kipi muhimu kuliko jingine katika kufanya delivarence? Kumbuka tunaomba kwa sababu Mungu ametuambia tuombe katika Neno lake.
  (4) Kipimo gani kitumike kujua kuwa huyu tayari ameshafanyiwa delivarence?
  MUNGU AWABARIKI TUNAPOENDELEA KUJIFUNZA.”

 103. mpendwa tatizo hapa sio imani bali mtu binafsi hajajitoa kwa mungu sawa na rumi 12-1 kwa hiyo kipindi hicho bado roho inatawala mwili na hapa sio swala la deliverance wala kuvunja laana bali mtu kujitoa kwa mungu kwani neno linasema
  niiteni nami nitaitika
  eleza haja yako nawe utapewa
  njoo na tuhojiane

  kushindwa kufuata kanuni ya neno katika kusimama na mungu ndio sababisho la watu kutobadilika na kubaki kama wamebadili dini

 104. Shalom wapendwa,
  Nijuavyo mie, unapookoka na kumkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni roho ndiyo inaokolewa Rumi 10:9.
  Lakini mtu ni nafsi, roho na mwili.
  Kifungo kinachokaa katika Roho ni hicho cha kuwa chini ya utawala wa shetani ambapo ukimkiri Yesu unakuwa huru (Roho)
  Nafsi ndio kiungo kati ya mwili na roho hivyo kuna bado vitu mwili utapenda kuvifanya ambavyo ni kinyume na ukiri wako, kwa hiyo vitu kama wizi, uzinzi ni mfano wa nafsi isiyofunguliwa bado ambapo ukimpokea Roho Mt akakaa ndani yako anakufungua unakuwa na matunda ya Roho na sio yale ya Mwili Galatia 5:17-24.
  Mwili pia una vifungo vyake mfano magonjwa, ulemavu nk, hivi nadhani ni vitu ambavyo vinaweza kuponywa na Mungu kutegemeana na mwenyewe anavyoona, mfano vitamletea utukufu utakaowavuta watu wengine waokoke, kama vinakufanya ushindwe kufanya makusudi yake, lakini pia hivi vifungo Mungu anaweza kukuacha navyo kama ilivyokuwa kwa mwiba wa Paul 2 Korintho 12: 9.
  Sasa nijuavyo kupokea Roho mt inabidi uwekewe mikono, kupokea uponyaji wa mwili pia, au kwa kuomba mwenyewe isipokuwa haviji automatically kama ilivyo kwa Roho yako unapomkiri Yesu, ili kukuwezesha hata kama uko ktk vifungo ukichukuliwa na mauti unanafasi ya kuingia mbinguni hata kama uliitwa mwizi jana (mf mwizi msalabani na Yesu), ni kiwete nk.

  Hivi ndivyo ninavyoelewa mie, mbarikiwe

 105. Shalomu,

  Naomba niseme kuwa kwa njia ya kumwamini Yesu, tunazaliwa mara ya pili. Tunazaliwa si kwa mapenzi ya mwanadamu, bali mapenzi ya Mungu. Kwa sababu hiyo, kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho (Yohana 1:12,13, 3:6).

  Kwa kuwa mtu anapookoka anazaliwa katika ufalme wa Mungu na hivyo anahamishwa kutoka katika ufalme wa giza, Biblia inasema kuwa tazama ya kale yamepita yote yamekuwa mapya. Kama hivi ndivo, basi kuokoka kunatuweka huru mbali na dhambi, mbali na shetani, mbali na laana na vifungo n.k.

  Ninavyoamini mimi, hakuna nguvu iliyokubwa zaidi ya nguvu ya kutuokoa na Mwana wa Adamu alikuja ili kutuokoa na kwa kufanya hivyo alizivunja kabisa kazi za Ibilisi (1Yohana 3:7). Sasa kama laana na hivyo vifungo ni kazi za Ibilisi, basi kwa njia ya wokovu vinavunjika vyote na mtu anakuwa kiumbe kipya, huru kabisa.

  Labda kwa leo nimalizie kwa kusema kuwa, ukiangalia maandiko kwa makini huwezi kuona kitu deliverance kama sehemu ya mtu kuokoka au kuwekwa huru, mtu anawekwa huru pale anapookoka (anapozaliwa mara ya pili).

  Mungu akinijalia nitarudi tena kuchangia mada hii, maana naamini wengi wanaangamia kwa kutokujua uweza wa Mungu ulioko katika wokovu.

  Shalomu

 106. Kama Deliverence ni Ukombozi na Yesu ndiyo mkombozi, je ina maana mtu anapompokea Yesu (mkombozi), kwa maana ya kuokoka, bado kuna ukombozi mwingine unaotakiwa kufanyika ambao ni tofauti na ule ukombozi wa Yesu Kristo?

  Mimi pia nahitaji mafundisho hapa. Lakini naona ingekuwa vizuri mtu anayeandika, kwa upande wowote, aambatanishe na maandiko anayosimamia, kama yapo!

 107. BWANA YESU ASIFIWE SANA!!!

  KWA KWELI JAMBO HILI LINAHITAJI MAFUNDISHO YA KIREFU KWANI HATA MIMI NASUMBULIWA NA VIFUNGO. NA TATIZO HILI PIA LIKO KWA WENGI WALIOOKOKA. MARA NYINGI UKIWA KATIKA VIFUNGO MAFANIKIO UTAKUWA NAYO KIROHO, LAKINI KIMWILI MTU ANAPATA SHIDA SANA, MFANO BIASHARA HAZIENDI, KAZI UKIPATA UNAACHISHWA, WATOTO WAKOROFI N.K

  NINALOJUA MIMI NI KUFANYA TOBA NA KUVUNJA MADHABAHU ZA SHETANI KATIKA UZAO(VIZAZI), ARDHI, MALANGO. HIZO NDO TOBA NAZOJUA MIMI KAMA NIKO RIGHT AU SIKO RIGHT TAFADHALI TUPENI MSAADA WA MAFUNDISHO.

  TUFANYEJE???.

  BWANA YESU ASIFIWE.

 108. My dear deliverance ni muhimu, kwa sababu tumepita katika mambo mengi mengine kwa kujua na mengine bila kujua. Kwa hiyo lazima ufunguliwe kwa deliverance, na katika hili wakati wa kufunguliwa kama kuna eneo bado umefungwa adui atakamatwa nawe utaombewa na utakuwa huru. Nasema kwa uzoefu ni bora kufunguliwa ama sivyo utajikuta unapiga tu kwata hupokei uponyaji au huoni mpenyo katika jambo unaloliombea.

  Ubarikiwe

 109. Mimi ninavyo fahamu, mtu akiokoka kikweli kweli, hapo anakuwa kiumbe kipya, yote yakale yanakuwa mapya, hakuna haja ya kuombewa tena,

  ukiona mtu ameokoka halafu anakuwa na mambo hayo hapo ujue bado hajaokoka bado.

 110. Nashukuru kaka isaac kwa mchango wako. labda nieleze kwa kifupi kuwa wakati naiona hii blog less than two weeks ago, i was so disparate! nilikuwa natafuta ni wapi naweza pata mawasiliano niombe msaada. Cha kwanza nilichokiangalia ni sehem ya maombi, na kabla ata ya kuendelea zaidi niliandika maombi yangu ambapo nilitaja direct kinachonisumbua.Naona km tatizo langu liko kiroho zaidi kuliko kimwili lakini kwa kuwa sielewi ndo maana nikaomba na ushauri huenda kuna anayejua sababu. Yamkini nasababisha mimi pasipo kujua.ndo maana nikataka nijue na habari za delivarence ambazo sizifaham kwa undani.Hata hivyo namshukuru Mungu kuwa toka nimeifaham blog hii nimekuwa nikifuatilia mada mbalimbali za nyuma ambazo ninaendelea kujifunza mengi, ila katika hili nahitaji msaada sana.

 111. Bwana Asifiwe wa pendwa wa Yesu
  I believe the solution to this problem
  isn’t just praying. I say this because i myself ‘ve been in that situation and i know exactly how it is
  I was born and raised in a christian family
  but after moving to Australia I changed and got caught into some disgusting and disturbing behaviors and still did go to church.
  I could feel the guilt in my heart and tried to pray and fast for up to 3 days but my behavior grew even worst and i couldn’t understand why.
  But a time arrived when i came to my senses and realized that It’s your DETERMINATION and or your WILLINGNESS combined together with prayers.
  coz even God cannot do a thing if we’re not willing to change. it’s up to us coz it’s us who give God permission to work throughout our lives.

  It’s very hard to break a habit but it’s not impossible.
  if your willing to do something, one thing i’ve learned is that the whole universe conspires you in doing so

  now I praise God coz I was able to break my habit. so determined and willing to see again, i’m free.
  full of light and unforgettable experience
  JESUS is LORD
  J4L

  DETERMINATION and WILLINGNESS + PRAYERS
  Nothing is impossible

 112. Bwana YESU apewe sifa wapendwa. Unajua mtu anapo zaliwa mara yapili kweli anaunganishwa na ufalme wa Mungu ni sawa lakini maombi ya ukombozi ni muhimu sana kuvunja mikataba na ulimwengu wa nguvu za giza.uwe HURU asilimia 100 kusamehe lakini ujasahau ni kifungo bado unahitajika kukombolewa uweze kufanya hivyo ubarikiwe sana

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s