Rudi kwenye NENO la Mungu.

Maandiko yanatuambia Mungu aliumba dunia kwa kutamka Neno lake lenye Imani na Nguvu, Mungu alitamka alichotamani kukifanya, kikatokea! lakini alikiamini kabla hakijatokea , akatamka nacho kikawa! Alipotaka kufanya uumbaji hakufikiri fikiri kwamba itakuwaje au hakutamka kwa mashaka kwamba je kisipotokea! Alitamka

Tunapohitaji kuona matarajiano yetu. Tutamke NENO la Mungu tukiamini itakua, tunaweza kuumba maisha yetu ya ushindi kama Mungu alivyoumba na kuitengeneza nchi kila kitu kakipanga mahali pake! sio kwamba uamini tu bali TAMKA Neno lake 2 Wakorintho 4:13 “Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena”

Ikiwa una uhitaji! Rudi kwenye NENO! Neno la Mungu linasema nini khs hitaji lako? Liamini hilo NENO, litamke, Liweke moyoni mwako, lijae kwa wingi moyoni mwako, kuliko hitaji lako, NENO la imani lifanyike kama dawa, kwa jicho la imani ona umepokea hitaji lako na endelea kuamini..NENO litafanya kazi kwako na utapokea kama ulivyoona.

Ikiwa u mgonjwa, una maumivu kwenye viungo vyako, angalia ugonjwa wako kupitia Neno la Mungu, mfano katika Isaya 53:4-5, Kwa kupigwa kwake (wewe) umepona! Sasa, amini hilo Neno, Litamke jiambie kwa kupigwa kwako Yesu amekuponya! Liweke moyoni mwako, lijae kwa wingi kuliko ugonjwa ulionao. Kwa jicho la imani jione umepona kabisa, Haijalishi ni hitaji la namna gani, ni vizuri kuombewa na watu lakini sio lazima uombewe, wewe mwenyewe ikiwa unaamini Nguvu za Mungu unaweza kutamka Neno juu ya hitaji lako ukapokea. Fanyia mazoezi utapokea majibu unayohitaji!

–MD–

Advertisements

8 thoughts on “Rudi kwenye NENO la Mungu.

 1. Shalom wapendwa,
  Hakika ni ujumbe mzuri sana maana Neno la Mungu ni kila kitu katika maisha yetu maana biblia inasema neno la Mungu ndio uzima wetu.Ndani ya neno kuna kila kitu-ujuzi wote,maarifa yote,uponyaji wa roho,nafsi na mwili n.k.Ndio sababu Yesu alisema katika Mathayo 7:24-25 kuwa “Kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba,mvua ikanyesha,mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”
  Kwa hiyo neno ndilo msingi au mwamba ambao kanisa linapaswa kusimama juu yake siku zote.
  Mbarikiwe.

 2. Mungu akubariki sana Aika kwa kulielewa NENO! @Blessed Luhinda, NENO la Mungu linasema ukiwa na Imani hata kidogo imani yako itafanya kazi, ndio maana Yesu aliwaambia aliowahudumia kwamba Imani yako imekuponya, maralia sio kitu kwa Mungu ikiwa mapepo yasiyoonekana yanatoka je UKIMWI unaoonekana kwanini usitoke?

  Anaponya magonjwa yote bure,kwa kuliamini NENO lake na kuishi sawasawa ya hilo Neno unapokea! Sio mapenzi ya Mungu tuumwe, tuishi kwa mateso na umasikini, tuishi kwa kutokujua HAKI zetu kutokana na NENO la Mungu, ndio maana kila hali unayopitia kuna NENO la kukusaidia…lakini kama umeliamini na umelifanya kuwa chakula chako, limejaa moyoni mwako. Unakua muumbaji wa maisha yako unapolitumia na kulifanyia kazi NENO la Mungu!

  Neno ka Mungu linatumika kama Silaha ya mashambulizi dhidi ya adui, tunaweza kujilinda wenyewe kwa NENO la Mungu! “Tena ipokeeni chapeo ya wokovu na upanga wa Roho ambao ni NENO la Mungu” Waefeso 6:17..lakini ili NENO lifanyike kama silaha inabidi kulisoma, kulitafakari, kulielewa, kulizungumza na KUMSIFU MUNGU kwa Neno lake, kila siku!

  Unapomsifu Mungu kwa Neno lake..kwamba Neno lake ni tamu, kwamba Neno lake ni kweli na amina, Neno lake halishindwi, kwamba linatupa HEKIMA na MAARIFA, ni taa ya miguu yetu,Neno lake ni njia ya kutupa utajiri na maisha yenye amani na furaha..KULISIFU Neno..Litaumbika ndani na kuchimba ndani zaidi kwenye kilindi cha moyo…Hakuna MLIMA utasimama mbele yako, ikiwa umejaa NENO la MUNGU!

 3. Sawa kabisa NENO NENO NENO la Mungu ndiye Mungu Mwenyewe Ukiwa kwenye Neno la Mungu upo salama. Nimeipenda meseji hii MUngu akubariki Mtumishi wa Mungu. “Tuliangalie Neno”

 4. Bwana Yesu asifiwe wapendwa! Maralia ni kitu gani mbele za Mungu? inategemeana tu na imani ya mtu mwenyewe kama anaamini kwamba kwa kupigwa kwake yesu nimepona toka moyoni mwake bila kusitasita wala asisikie mahubiri ya mtu mwingine wa pembeni basi hata maralia anapona. lakini kama haamini basi awahi hospitali kutibiwa.
  Kwani Yesu ameahidi kuponya magonjwa ya aina gani? naomba kujifunza hapa. maana nijuacho mimi magonjwa yote yanapona ili mradi ukitumia jina la Yesu.

 5. Nakubaliana na wewe, lakini kwa upande mwingine unaweza kuwapotosha wengine, ukisema mtu akiugua malaria aseme kwa kuteswa kwake mimi nimepona, akitazamia uponyaji wa malaria na kwa vyovyote hatoweza kupona, je hauoni kuwa unaweza kusababisha huyo mtu apoteze maisha kwa ugonjwa huo?

 6. Amen.Ahsante kwa mafundisho ya kututia moyo.Jana usiku Roho Mtakatifu aliniamsha kutokana na hitaji nililonalo akanipa ahadi kwenye Isaya 65:17-25.Baada ya kusoma huu ujumbe wako hapa nimejifunza kitu lile neno nililopewa likae ndani ya moyo wangu kuliko hitaji nililo nalo.Niliamini na kulitamka nalo litafanyika..hakika Mungu anasema neno lake halitamrudia bure pasipo kuyatimiza yale ambayo ameyakusudia yatimizwe.TURUDI KWENYE NENO LA MUNGU WAPENDWA!
  Ubarikiwe Da’Mary na umependeza sana!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s