Waimbaji wa nyimbo za Injili imbeni nyimbo za kumuinua Kristo!

Kumekuwa na jambo linalokera kwa baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili, kuna nyimbo nyingine hata sisikilizi wala kuangalia, hata wewe mpendwa ikiwa umeokoka ukiziona hizo nyimbo utasikitika, hazina Utukufu hata kidogo, hazina tofauti na nyimbo za “Misri” wanavyoimba na kucheza kama vile hawako serious na uimbaji wa nyimbo za Injili. Kama vile wanajiimbia wao na kuwaburudisha wanaowasikiliza. 

Unaposema unaimba nyimbo za Injili, sio kwa sababu una pesa ya kuingia studio na una sauti nzuri. Watu wengi tunapenda kusikiliza nyimbo za Injili ili tuone mabadiliko kwenye maisha yetu sio kutuburudisha, angalia tungo zako zimekaaje, wengine wakisikia neno limeingia mitaani, tayari wamepata kichwa cha habari cha wimbo! Usafi wa moyo ndio unadhihirisha kazi yako. Mungu akubariki muimbaji wa Injili naomba unisamehe kwa makwazo yangu. Nawakilisha!

 —Jonas Malimbo

Advertisements

51 thoughts on “Waimbaji wa nyimbo za Injili imbeni nyimbo za kumuinua Kristo!

 1. Ooh,My Really Living God!!!!!!!!!!!!!,
  naona kama naota vile sijaamini,nafikiri ushauri huo wa kuuza mtandaoni utakusaidia,ila kweli waimbaji ni wa kuwaombea,tuna studio tunayoyapata huko ni Mungu atutie nguvu,kwani na wao ni binadamu,na wakti mwingine basi usiweke mpaka uhakikishe umeuza hizo nakala unazofikiria lakini,kweli itakusaidia siyo kweli kila mtu anaweza kukutendea hayo uanayofikiri,najua kweli ni gharama sana kuandaa kila kitu kwa studio ,lakini kama umefikia huko nafikiri muwe sasa na wanasheria watakaowasaidia,nimeumia si tu kuwa MCHIMBA MASHIMO ulirikodiwa na mume wangu,na ukahubiri vyema nafikiri hili suala la haki miliki,mfafanuliwe zaidi na athari za kuweka nyimbo zenu kama mnaona hamfaidiki nazo,kwanilengo ni Kumuhubiri Kristo na watu wangependa kusikia,muwe pia na wasambazaji wazuri ambao hawatawanyonya,kwani kupromote kitu si mchezo bali hata blog hii inasaidia kupromote kazi zenu.
  Mungu Akusaidie sana na wakati mwingine hebu zungumzeni na wahisika siyo kuwatisha
  nina ushuhuda wa mtumishi mmoja wa Radio ya injili Arusha,alimtishia mwimbaji mmoja tuliyemwezesha kurikodi bure kwa kurudia album yake yote kwani ilikuwa imeharibiwa,Mtumishi huyo alikuwa navurumisha ujumbe katika simu,hadi nikawa sina hamu ya kwenda kwenye maombi kule Olasiti,nilivunjika moyo nikasema khe!kumbe hata nyimbo za Injili zina hati miliki,mimi mkatoliki,ninavyojua katika utaratibu wa nyimbo za wakatoliki kama mtu katunga yeye halafu wimbo ukarudiwa basi tunaweka jina la mtunzi na hakuna malumbano wala malipo maana wote tupo kwenye kuujenga mwili wa Kristo,na ndiyo maana utakuta mtunzi yupo Kigoma Musoma wanaimba,na wanarikodi tunanunua kazi zao,inatia moyo,sasa huku kutishana kwa kutoelewa chanzo mbona shida ipo tena kubwa sana.
  Mungu awasaidie ila ni mengi sana ya Waimbaji wanahitaji ushauri,kutiwa moyo na kuombewa sana.
  Poleni mliovunjika moyo,naomba msamaha kwa niaba yake hata kama hataomba ili Mungu aendelee kumuhudumia katika huduma yake ametoka mbali na hajafika bado ni safari ndefu na kumwacha Yesu kwa kuangalia album moja tu kati ya zote alizo nazo.
  Sina Mengi Mungu Awabariki sana.

 2. Mungu awabariki wachangiaji wote;

  Kwako ndugu yetu ALBERT PAUL
  Blog hii ni INJILI! hivyo basi, tunazungumza na kuchangia yale ambayo hayatatuondoa kwenye lengo letu. HIi blog inatembelewa na watu wote…wa kijamii na wahusika wa INJILI, wakijamii wajapo kwetu wanauona msimamo wetu. Na hili ndilo lengo letu! SIo kwa kushindana bali tunajengana na kuonyana!

  Kwa vile nimeandika inatembelewa na wahusika wa Injili inamaanisha wachungaji, wainjilisti, waimbaji, mapadre na wote wahusika. Na pia wanaochangia mahali hapa wengi ni hao hao waimbaji, wachungaji, na wenye huduma mbalimbali za kiroho, sasa yale tunayoyaandika kuwahusu hao unaotamani wafikiwe au waone, ukweli ni kwamba yanawafikia na wanasoma. Na wale wanaohusishwa moja kwa moja tunawasiliana nao kuwajuza nini kinaendelea kuwahusu.

  Karibu tena, ikibidi karibu kwenye familia ya watu waliookoka (Wakristo)

  Ubarikiwe

 3. Kumjua Mungu na kuitambua nafasi yake kikamilifu kunatosha sana kumpa mtu utulivu wa ndani ambao ndio huleta matokeo mazuri ya huduma ya mtu. Kinyume na hapo ni kupapasa tu! zab 99

  Inapendeza sana kufanya huduma hii ya uimbaji baada ya kuvunjwa na kupondwa kabisa, baada ya ku’experience’ vizuri uwepo wa Mungu ktk maisha yako binafsi ya kiroho! Hii inamfanya mtu atoe dhabihu za midomo yake kwa unyenyekevu kwa kuwa anamjua vizuri anaye muabudu!

  Bwana awazidishe

 4. “maana huko sio kunitangazia biashara bali kuniharibia.”””Mwimbaji nyimbo za injili?????????????????? Duuuuuuuuuuuuuu I cant imagine!!! Ana ujasiri kweli kweli!!!!

 5. Bwana Yesu asifiwe!!!

  Hii noma sasa!!! Yaani noma kweli kweli!!! Shame on us dears. Kwa kweli naogopa kama imefikia hatua hii!!!! Hapa sasa naanza kuamini kabisaaaaaaaa baadhi ya watumishi wa Mungu wamekaa kibiashara zaidi. Nahisi kulia!!!!

  Tumwinue Yesu na si biashara zetu!!!!

 6. Wapendwa Shaloom!
  Angalieni niliyoyakuta kwenye blog ya nyimbo za dini.
  waimbaji tunakwenda wapi?

  UJUMBE WA DADA JENNIFER MGENDI.

  YAH: NYIMBO ZA JENNIFER MGENDI

  Nakusalimu katika jina la Bwana.

  Nakuandikia kukutaka uondoe video zangu zote nyimbo 12 za album yangu ya Yesu Nakupenda ulizoweka kwenye blog yako maana huko sio kunitangazia biashara bali kuniharibia. Angalau ungeweka wimbo mmoja ningesema unanitangazia sasa umeweka nyimbo 12 mtu ana sababu gani ya kununua album hiyo wakati anaiona yote kwenye blogu yako? Tafadhali fanya hivyo mapema kabla sijachukua hatua zaidi.

  JIBU LETU KWA DADA JENNIFER MGENDI

  Dada Mpendwa na Mtumishi wa Bwana;

  Jennifer Mgendi

  Asante kwa ujumbe wako ambao kusema kweli umenishangaza kwani umekuwa kinyume na nilivyotegemea. Tumezoea kupata maombi kutoka kwa waimbaji wa Injili (au wapambe wao) WAKITUOMBA tuweke nyimbo zao zilizoko katika Youtube katika blogu hii ili ziweze kuwafikia watu wengi zaidi. Kwako kumbe ni kinyume!

  Kama ilani yetu inavyosema katika blogu yetu (nyimbozadini.blogspot.com), video karibu zote unazoziona hapa zimetoka Youtube. Kwa vile tayari zimewekwa huko, sisi tuliona si vibaya tukiwarahisishia watu kwa kuziweka video hizo sehemu moja. Ni wazo hili ndilo lilipelekea kuanziswa kwa blogu hii.

  Ukienda youtube.com na kutafuta video za Jennifer Mgendi ukifuata njia hii http://www.youtube.com/results?search_query=jennifer+mgendi&aq=0, utazipata video zote ambazo tumeziweka katika blogu hii. Video hizi zimewekwa na watu mbalimbali huko (ukiwemo wewe mwenyewe!). Hata kama tukiziondoa nyimbo zako katika blogu hii, watu wanajua kwamba video hizi zinapatikana Youtube na watakwenda kuzitazama huko. Ili kufanya video zako zisitazamwe kokote kule duniani isipokuwa tu na watu watakaozinunua, itabidi kwanza uwasiliane na watu wa Youtube ili waziondoe video zako zote huko. Baada ya hapo itabidi pia uwasiliane na watu wa East African Tube pamoja na Bongo video na kwingineko ili waziondoe video zako katika mitandao yao. Pia ukienda google.com na kutafuta video za Jennifer Mgendi, utapata sehemu nyingi sana mtandaoni ambako video zako zinapatikana. Wasiliana na hao pia ili waziondoe huko.

  Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba, katika wakati huu wa utandawazi itakuwa vigumu sana kuwazuia watu kutazama video zako katika mtandao. Nitakupa mifano michache. Makampuni makubwa ya muziki hapa Marekani yamekuwa katika vita vikali sana kuhakikisha kwamba miziki yao (audio) haipatikani mtandaoni bure. Makampuni haya yamekuwa makali sana kiasi cha kuwapeleka watu mahakamani na kuwalipisha pesa. Juhudi zote hizi hata hivyo hazijasaidia lolote na leo hii ukitaka wimbo au video yo yote unaweza kuipata mtandaoni bure. Mpaka wamejaribu kutengeneza CD na Video ambazo zinajiharibu zenyewe baada ya muda. Hata hili nalo halijafanikiwa kwani watu walikataa kuzinunua. Matokeo yake wameamua kushirikiana na baadhi ya tovuti zinazoruhusu watu kupakua (download) nyimbo zao kwa kuwatoza kiasi fulani cha pesa.

  Makampuni ya kutengeneza picha za ngono pia yanakumbwa na msukosuko huu na mengi sasa yanafungwa. Waraibu wa picha hizo (Mungu Awasaidie kuachana na tabia hii) sasa hawaoni sababu ya kununua au kuzikodisha picha hizo chafu wakati wanaweza kuzipata mtandaoni (siyo Youtube).

  Maduka makubwa ya kukodisha video na miziki hapa Marekani (mf. Hollywood Video) pia yanafungwa kwa sababu wateja wamekuwa wakipungua mwaka hadi mwaka. Yote ni kwa sababu ya upatikanaji wa video hizi mtandaoni.

  Hata magazeti dhati pevu kama Los Angeles Times, Boston Herard na New York Times yamekumbwa na misukosuko ya aina hii kiasi cha kulazimika kupunguza wafanyakazi, kupunguza kurasa au kuhamia mtandaoni moja kwa moja. Dada, haya ni matokeo tata ya utandawazi na uhuru unaoletwa na teknolojia hii ya kupashana habari kwa kasi ya radi. Sidhani kama utafanikiwa katika azma yako ya kuhakikisha kwamba video zako zote hazipatikani mtandaoni. Wengi wamejaribu wameshindwa. Utachukulia hatua kali wangapi?

  Ni lazima pia izingatiwe kwamba kasi ya mtandao huko nyumbani bado si nzuri na ni watu wachache sana wanaoweza kutazama video nzima nzima katika Youtube. Kwingineko, Youtube kwa wengi wetu tulioko nje imegeuka kuwa ndiyo chanzo kikuu cha kufahamu nini kinaendelea nyumbani kuhusu muziki na mambo mengineyo. Watu wengi sana wamekuwa wakiniuliza wapi wanaweza kununua nyimbo (audio) za video wanazoziona hapa nami huwaambia wawasiliane na waimbaji na wamiliki wake (kama ambavyo nimeanza kuweka hapo juu kuhusu nyimbo za Adelina na Veronica Sanga (feat Med Medrick Sanga). Lengo la blogu hii SI kuharibu biashara yenu watumishi wa Bwana bali ni kufanya nyimbo zenu (ambazo tayari ziko kwenye Youtube) ziwe mahali pamoja ambako wakazi wa nchi za Afrika Mashariki na kwingineko kunakosemwa Kiswahili (na hasa ambao wako nje ya nchi zao) waweze kuzisikiliza/kuzitazama kwa urahisi ili wapate kuzifahamu na hatimaye kuzinunua. Tatizo ni kutopatikana kwa nyimbo hizi (hasa audio) mtandaoni. Nimefurahi sana kuona kwamba albamu yako ya Mchimba Mashimo inapatikana katika iTunes. Endelea kuweka nyimbo zako mtandaoni namna hii na hutakuwa na sababu ya kuiogopa Youtube tena!

  USHAURI WANGU

  Dada Jennifer, ushauri wangu ni kwamba, badala ya kupigana vita ambavyo inaonekana havishindiki, ni bora kama nyinyi wasanii wa injili mngeungana na kuanzisha tovuti ambayo ingeuza nyimbo zenu mtandaoni. Wenzenu wengi kutoka Kenya – akina Peace Mulu, Betty Bayo, Emmy Kosgei, Marion Shako, Emmy Gait na wengineo tayari wanauza nyimbo zao mtandaoni na hawana tatizo na nyimbo zao kuwekwa katika Youtube kwani Youtube ndiyo hasa tovuti mama ya video duniani kote . Kimsingi mtu akiuona wimbo katika Youtube na kuupenda, hatua inayofuata ni kuutafuta katika sauti (audio) ili aununue na kuwa anausikiliza katika gari lake au kichezeshi chake cha mp3. Kwa hivyo kwa watu wengi Youtube bado ni sehemu nzuri ya kutangazia nyimbo zao. Inabidi pia mjue kwamba watu wengi sasa hawataki kununua CD nzima nzima. La! Wanataka wimbo mmoja mmoja waupendao na ambao bei yake katika tovuti nyingi ni senti 99 za Kimarekani ($.99). Fanyeni hivyo na matunda yake mtayaona. Vinginevyo mtabakia tu kulalamika kwamba mnadhulumiwa.

  KAMA KWELI UNATAKA KUCHUKUA HATUA

  Kama kweli unataka kuichukulia hatua blogu hii basi ni kazi rahisi sana. Unachotakiwa kufanya ni kuwaandikia watu wa Google na kuwaambia kwamba blogu hii imekuharibia biashara kwa kuweka nyimbo zako za injili ZILIZOKO kwenye youtube (pia inamilikiwa na Google! Na nyimbo zingine umeziweka wewe mwenyewe!), na kwamba unataka blogu hii ifungwe. Kutokana na wingi wa kazi walizonazo, Google huwa hawana muda wa kufanya uchunguzi wa kina na blogu hii itafungwa mara moja! Kwa kukurahisishia kazi, anuani (na faksi) ya Google Blogger unakoweza kupeleka malalamiko yako ni hii:

  Google, Inc.
  Attn: Google Legal Support, Blogger DMCA Complaints
  1600 Amphitheatre Parkway
  Mountain View, CA 94043

  Au unaweza kuwapelekea faksi kwa kutumia namba ifuatayo:

  +1 (650) 618-2680 Attn: Blogger Legal Support, DMCA Complaints

  Pia tembelea tovuti yao na fuata maelekezo yao hapo na blogu hii itafungwa mara moja. Lengo letu halikuwa kujipatia pesa na ndiyo maana hatujaweka matangazo yo yote katika blogu hii. Lengo letu ni kutangaza injili ya Bwana kwa asilimia 100. Na kama blogu hii itafungwa, Mungu Mwenye Nguvu Anao uwezo na Atatafuta njia nyinginezo zitakazoifanya injili yake kwa njia ya nyimbo iweze kusonga mbele. Kazi ya Bwana DAIMA itasonga mbele na kamwe haitegemei blogu au Youtube. Imeandikwa kwamba Yeye Ana uwezo wa kuyafanya hata mawe (AMBAYO HAYAJUI BIASHARA!) yaweze kuimba na kumtukuza! (Luka 19:40).

  Asante sana dada na Mungu Aendelee kukusaidia na kukubariki katika utumishi wako

  Nyimbozadini.Blogspot.com

  Post a Comment On: NYIMBO ZA DINI
  “UJUMBE (NA “ANGALIZO”) KUTOKA KWA DADA JENIFER
  8 Comments – Show Original Post Collapse comments
  John Mwangoka – Ujerumani said…
  Wallahi pesa zitatumaliza. Blogu hii ikifungwa litakuwa pigo kwangu binafsi. Japo nyimbo hizi zapatikana Youtube pia, nshazoea kuja hapa na kuzikuta zote at one place. I will particularly miss the audios. Huku Ujerumani hakuna cha video wala nini. Tumwogopeni Mungu jamani. Kwani pesa ndiyo nini? Mnaimba ili kutajirika? Kama nyimbo zote ziko Youtube, huyu kuziweka hapa kuna ubaya gani?

  Vinginevyo tuambieni wapi tunaweza kuzipata hizi nyimbo KATIKA AUDIO ili tuzinunue na kuweza kuzisikiliza maofisini na kwenye magari yetu.
  July 23, 2010 2:07 PM
  Anonymous said…
  wewe mwanamke sisi tulijua dhumuni ni kulifikisha neno la mungu kwa watu wote kumbe una yako. Acha watu wanaomjali mungu wafanye kazi yao kwa uadilifu, sio wote wapenda pesa kama wewe huyu bwana alikuwa na uwezo wa kuwatoza watu pesa lakini amegundua umuhimu wa neno la mungu kwa kila mtu thats why ameweka watu wasiklize free, wewe unaleta mawenge yako ya kutaka pesa watumishi wa mungu huwa hawalipwi mama they receive whatever they get hakuna mishahara makanisani not to talk about music let people have funy for once wangapi umeona wamewekwa huku hawajaomba kutolewa cos hii ndio walikua wakiitaka neno litembee kwa watu wote na huyu bwana nyimboza dini ndio anawasaidia kutawanya neneo la mungu so plse keep cool AMEN
  July 23, 2010 6:02 PM
  Anonymous said…
  Umemjibu vema na tena umemueleza kwa ufahamu wa hali ya juu sana kiasi kwamba kama ana masikio ya kusikiliza basi ameyasikia uliyomwambia.

  Ujue kuwa Jeniffer hana ufahamu wowote wa hizi tovuti na google na yutubu kuwa zinafanya nini, ndiyo maana yeye anaangalia biashara yake tu bila kuangalia kuwa anaufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa akina nani.Fikra zake zimejikita palepale bongo alipozaliwa hajui kwamba ulimwengu umekuwa kijiji.

  nakupongeza sana bloger kwa ujuzi na upeo wako na hata kwa upendo wako wa kutufyatulia nyimbo zote za injili hadi tunaweza kuzipata hapa.Mimi mwenyewe niko USA na juzi nimeagiza DVD Za “Utumwa wa Israel, Yerusalem Mbeya, Na SDA na Shinyanga AIC baada ya kuziona na kuzisikilza kwenye tovuti yako.Kwa hiyo usijali wewe endelea tu kutuwekea, mwenye akili nzuri kama ulivyosema ataelewa kuwa hiyo ndiyo njia ya kumtangazia biashara yake.Uchoyo haufai, hizo pesa mtapata lakini hamtakujashiba, waache watu wapate neno la Mungu kwa njia hii kama hawa watumishi walivyosheheni nyimbo kwenye blog yao inatia moyo sana.
  July 23, 2010 10:52 PM
  Mama Getrude – Sweden said…
  Something is terribly wrong with Christianity. Hawa maaskofu na ma-prophet wanaozuka kila leo some of them they are just there for the money. Sijui tunakwenda wapi. Mungu Atusaidie jamani.

  Na pia mju kwamba baadhi ya waimbaji hawa hawajasoma na welewa wao wa mambo yanavyoenda duniani ni mdogo sana. Inasikitisha!
  July 24, 2010 2:04 AM

  Laiser said…
  wow!!thank you bloger kwa namna ambayo Mungu amekupa hekima ya kumemjibu dada Jennifer. Sikutegemea neno alilosema dada huyo litoke kwa mtumishi wa Mungu but well, nimetufikia, japo linasikitisha, kwa sababu tulitegemea kuwa hawa watumishi wako kazini kwa sababu wanafahamu kuwa “mavuno ni mengi watendaji ni wachache” ila sivyo kwa wengine. Mungu atusaidie. Mungu akubariki brother kwa kuziweka nyimbo hizi hapa zimekuwa faraja kwangu na wengine niliowaeleza juu ya kazi yako. Keep it up, kama ulivyomwambia Jennifer kuwa Mungu aweza kuinua mawe, twaamini pamoja nawe.
  July 24, 2010 3:12 AM
  Anonymous said…
  Dada Jennifer. Nakuomba uache kuimba nyimbo za Injili mara moja. Jaribu Bongo Fleva. Huko utatajirika haraka sana!!!

  Ila hata nyimbo za Bongo Fleva nazo Youtube zimejaa kwelikweli. Sijui utakimbilia wapi.

  Nilikuwa nasikia tu kwamba waimbaji wengine are there kujitajirisha lakini I never thought kwamba itakuwa this obvious. Sitanunua kazi yako yo yote tena!
  July 24, 2010 8:32 PM
  Anonymous said…
  Kweli Mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache nilitegemea mtumishi Jennifer uwe na furaha ujumbe wa Neno la Mungu unawafikia watu kote duniani. ila nimeshangazwa sana kuona unalalamika wanakuharibia biashara. kwa hiyo dada yangu kazi yako ni ya biashara na si kueneza neno la Mungu. kweli Mungu atuponye
  Neema
  July 25, 2010 5:00 AM
  Anonymous said…
  Asilalamike Rose Muhando, Christina Shusho au Bahati Bukuku uje ulalamike wewe? Nyimbo zenyewe zinazolalamikiwa utafikiri za Mazishi. Anyway. Solution ni rahisi tu. Kama huyu jamaa alivyokushushia pointi, zitoe hizo nyimbo huko Youtube na kila kitu kitakuwa salama.

  Umenishangaza sana dada Jennifer!!!

 7. Mimi nakuunga mkono dada Wema, Ni kweli kuna waimbaji wanajiona matawi ya juu sana, hata kuwapata kwa ajili ya huduma inakuwa ni kazi kweli. Unakuta mwimbaji kaalikwa kwenye mkutano wa injili anataja dau fulani kutokana na hali ya uchumi kuwa mdogo wanaamua kumlipa kidogo kwanza ili baada ya mkutano amaliziwe kilicho chake, anaimba siku mbili ya tatu anagoma kupanda jukwaani mpaka amaliziwe pesa yake… Mimi naomba kuuliza Je huduma yao ni kwaajili ya wenye pesa tu? Uko wapi ule wito wao waliokuwa nao walipoanza huduma? walipokuwa hawana majina makubwa walikuwa wanyenyekevu tayari kufanya huduma hata bila malipo nini kimewapata sasa?
  Kweli inaumiza sana na inasikitisha sana. Wapendwa maombi yanahitajika sana sana kwa watumishi hao, Wakumbuke kule Mungu aliwatoa, pesa ni nini?
  Jambo jingine nawaomba sana waimbaji waimbe nyimbo za kumsifu Mungu, Mungu hukaa katika sifa, waache mipasho na majigambo hvisaidii wala havijengi, watakaposifu katika roho na kweli Mungu atashuka haijalishi una jina kubwa au dogo, haijalishi kushangiliwa au la na Mungu akishuka atafanya mambo ya ajabu sana. Tusitafute kuburudisha watu na kushangiliwa angalia watu wanapata nini katika uimbaji wako, wanacheza na kushangilia tu halafu wanaondoka na shida zao? au wakati ukiimba Mungu anashuka na kuwaponya na kukutana na shida zao hata kabla ya maombezi?
  Angalia sana kile watu wanapata katika huduma yako, Najua wapo waliopewa ujumbe wa Faraja, wengine wa kuonya, wengine wa kukaripia nk, hakikisha kile umepewa ndicho kinachofikiwa na walengwa.
  Niishie hapo kwa leo. Mungu awabariki sana.

 8. Mimi nadhani yaliyopita si ndwele, na sasa hatuna budi kuganga yaliyopo.

  Hivi kuburudishwa na nyimbo za injili, si kwamba ni njia mojawapo wa kumuepusha mtu na kutenda dhambi (chanzo cha kutenda dhambi)? Hebu fikiria kwa mtu aliyekuwa na hasira iliyotokana na jambo fulani, halafu akasema, hebu nitazame video ya Ney Mwaipopo ya Raha Jipe mwenyewe, akaburudika na hasira zikamtoka. Hapa sio kwamba wimbo huu umetenda lilo jema?

  Binafsi naona wimbo ambao haufai ni ule ambao unawafundisha watu mambo mabaya, uwafundishao watu kutenda maovu, na sidhani kama kuna wimbo wa injili wa aina hii.
  Kama upo basi uwekwe bayana.

  Nashauri kitu kimoja. Kama inawezekana, waalikwe wahusika, waimbaji wa nyimbo za injili katika mjadala huu nao tuwasikie wanasema nini. Mimi nadhani hili litatuelimisha zaidi.

  Ndugu Moderator uniwie radhi, maamuzi yangu yaliambatana na ghadhabu ambayo sikuweza kuimudu.

 9. Bwana Yesu asifiwe

  Kweli Wema nyimbo za Late Sedekia hazina manjonjo ya kimwili, nyimbo nyingi wanaimba wamesimama na vinubi vyao, lakini katika Roho usipokaa sawa waweza hata kuzimia /kulia kucheka sana kwa kweli nyimbo zake zinamtukuza Mungu wetu.

  Tunajifunza

 10. mimi naona aliyeuliza swali ameliuliza kwa wakati muafaka maana tusipo angalia uimbaji wa nyimbo za injili unaelekea kwingine kabisa , nyimbo badala ya kumuinua mungu na kutia moyo wale walio katika safari ya kwenda mbinguni tunasutana wenyewe kwa wenyewe . kwanza kwenye uimbaji kuna matabaka; kuna wanaojiona wanaimba vizuri kuliko wengine (Matawi ya juu), utakuta muimbaji anapanga ratiba ya kuimba kwenye tamasha, yaani wale wanaoanza kuimba ni wale wasiojua kwa madai yao na ukisema mimi nitaimba baadaye wanasema utapoza tamasha maana wale waimbaji wazuri wanawasha moto sasa wewe ukiiimba mwishoni tamasha linapoa. mimi nilimpokea yesu kupitia uimbaji wakati niko shule nakumbuka marehemu Sedekia alikuwa akija mashuleni kuhudumu tulikuwa tunabarikiwa kweli alikuwa akiimba namna ambavyo mungu ni mwaminifu , utukufu wake yeye, na tulikwa tunatulia na kusikiliza. siku hizi yaani muimbaji asiposhangiliwa wanaona haimbi vizuri. ngoja niishie hapo maana naweza jaza kitabu. mbarikiwe

 11. Matatizo ninayoyaona mimi ambayo yanasababisha hali hii kwenye uimbaji wa nyimbo za injili siku hizi baadhi yake ni haya:

  Siku hizi kuna waimbaji ambao hawajaokoka kabisa. Yaani mtu anaamua kuimba nyimbo za injili, inaitwa ‘kuimba gospel’ ili tu akiuza apate pesa lakini yeye hahusiki kwa vyovyote na alivyoimba kwenye nyimbo hizo. Na kuna waimbaji wengine ambao huitwa wameokoka, lakini anaamua kushirikisha kipaji cha mtu ambaye hajaokoka ili nyimbo na album yake kwa ujumle itoke vizuri kwa kusudi la kukubalika sokoni.

  Pia wako waimbaji ambao sasa wanakodi wacheza shoo, ili wacheze vilivyo kwa lengo la kuvutia wateja wanunue album hiyo.

  Sijuwi tunawezaje kupata uimbaji wa kumuinua Kristo kwa namna hii.

  Ninavyoona mimi kuimba nyimbo za kumuinua Kristo ni matokeo ya mwisho ya hali ya kiroho ya mwimbaji pamoja na kusudi la kuimba nyimbo hizo. Pasipo waimbaji wacha Mungu sawa sawa na wenye kuimba nyimbo za injili kama utumishi wao kwa Mungu , sidhani kama ni rahisi kupata nyimbo za kumuinua Kristo.

  Changamoto ninayoiona ni uwepo wa waimbaji wenye nia thabiti ya utumishi na ambao maisha yao yatasema kile wanachokiimba kuliko kutegemea maneno ya kukariri ndiyo yafikishe ujumbe.

  Ninauliza kama kuna nafasi yoyote ya Kanisa kushiriki katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili la uimbaji unaopotosha lengo na kunakosababisha jina la Yesu litukanwe. Maana ninachoona ni kama waimbaji wa injili wanajiongoza wao wenyewe,[japo inaweza kuwa si wote].

  Mungu atusaidie.

 12. Shalom,
  Ndg Albert sikusema uimbaji hauna gharama wala matamasha hayana gharama ninacho kikataa mimi ni biashara ya uimbaji…. naomba uelewe sipingi vingilio kwenye matamsha maana kuna gharama imetumika kuandaa…kwa mfano tunamuita muimbaji kanisani sio kwenye tamasha halafu anasema bila laki 4 mi siwezi kuja kuimba je hii nini hebu tujibu ndg Albert…. Muimbaji mmoja kinara hapa nchini aliwai kuitwa kanisa moja muda kidogo umepita alisema hawezi kwenda bila laki 4 yeye na watoto wake wataishije? … .. nikajiuliza maswali je wahubiri wakifanya hivyo itakuwaje?….

  ndg Albert uelewe zipo nyimbo za rohoni ambazo ni matokeo ya mtu kuishi maisha ya kujawa na Roho mtakatifu (zaburi na tenzi za rohoni)… kuna nyimbo ambazo zinaanzia kwenye nafsi ya mtu…zingine zinatokana na majeraha ya mtu mfano raha jipe mwenyewe… aina za nyimbo ambazo zaweza gusa roho za watu ni aina hii nyimbo za rohoni hizi ukiimba nguvu za Mungu zinatembea na udhihirisho wa Roho mtakatifu waweza onekana, Hizo aina zingine zakujifurahisha..

  Leo niiishie hapo.

  Mungu awatunze Tunajifunza.

 13. Ndugu Albert Paul,shalom.
  Kwenye mchango wako wa tarehe 15/7/10 uliandika hivi;
  “Historia ya kuja kwa Yesu, kuteswa na kusulubiwa kwake kama ilivyoandikwa katika biblia haijahusisha dini nyingine kama uislamu, kwa hiyo sidhani kama itakuwa ni sahihi kusema kuwa wasiokuwa na imani ya kikristo basi wamepotea njia. Wakati huo huo tujiulize, mtume Mohamed naye alikuja duniani kufanya nini? Je,ni sahihi kwa wale wamwaminio kutumia ujio wake kuelezea hatma ya wale wasiomwamini?” Ukaendelea kusema “Binafsi naamini kuwa wapo wamwaminio Mungu huyu huyu wakristo WANAYEMWAMINI pamoja na kuwa hawaamini kuwa Yesu ndio njia ya pekee na uzima”

  Neno nililoliandika kwa herufi kubwa(wanayemwamini) linaonyesha wewe umejitoa katika kundi la wakristo, ina maana upo kwenye kundi jingine ambalo sio la wakristo. Lakini hili silo ambalo nataka tuliangalie kwa makini. Ninachotaka tukiangalie kwa makini ni hii dhana nzima kwamba mtu hata kama hampokei Yesu kama Bwana na Mwokozi wake, bado anaweza kuuona ufalme wa mbinguni, dhana ambayo ndg Albert Paul umekuwa ukisisitiza sana katika kila mchango wako.

  Hoja yako kwamba historia ya Yesu haipaswi kuhusianishwa na dini zingine ukatolea mfano wa uislamu, ni sahihi kabisa kwa sababu ukristo(ufuasi wa Kristo) umeanza tangu mwanzo mwa karne ya kwanza wakati uislamu umekuja zaidi ya miaka mia sita baadaye. Yesu Kristo ni mwanzo wa vyote(Methali 8:22-31), hata wana historia wamegawanya nyakati kwa kufuata kabla ya kuzaliwa kwa Kristo na baada ya kuzaliwa kwa Kristo(B.C and A.D). Kwa hiyo litakuwa jambo la ajabu sana ukristo kuhusishwa na dini zingine wakati dini hizo au waasisi wa dini hizo sio vyanzo vya uhai wao wenyewe wala wa wafuasi wao. Yesu Kristo ni mwanzo na mwisho wa vitu vyote(Alpha na Omega) vinavyoonekana na visivyoonekana(Yohana 1:1-3, Kolosai 1:16, Waebrania 1:2-4,10 Ufunuo 1:8).

  Kwa maana hiyo basi huyu (Yesu) ambaye ni mwanzo na mwisho wa kila kitu (hata huyo mtume Mohamed aliumbwa na Yesu) ndiye anayepaswa kufuatwa. Katika kitabu cha Waebrania 2:8b-10 neno la Mungu linasema hivi “Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hamjaona vitu vyote kutiwa chini yake, ila twamwona Yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya KILA MTU. Kwa kuwa ilimpasa Yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake VITU VYOTE VIMEKUWEPO….”. Kwa maana ya mistari hiyo utaona kwamba Yesu hakuja hapa duniani kwa ajili ya wakristo tu(kwanza ukristo haukuwepo kabla ya kuja kwake) au wale tu wanaomfuata Yeye, bali alikuja na kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu. Shida ipo kwa wanadamu wenyewe wanapomkataa na kuandamana na wanadamu wenzao(Mohamed) ambao sio Alpha wala Omega yaani sio Mungu.

  Kudhihirisha kuwa Yesu hakuja kwa ajili ya wakristo tu kama ambavyo unataka kutanabaisha ndg yetu Albert Paul, naomba tusome neno la Mungu toka Yohana 1:10-11 linalosema ‘Alikuwako ulimwenguni, hata kwa Yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.Alikuja kwake ,wala walio wake hawakumpokea’. Hebu ndugu yangu jiulize biblia inaposema ‘walio wake hawakumpokea’ ni akina nani hao? Ni wale wote wasioamini kuwa Yesu ni Mungu na njia pekee ya kufika kwenye ufalme wake, na wale wote wanaoamini kuwa Yesu ni Mungu lakini wanatenda kinyume na maagizo yake. Maagizo yake ni yapi? Yapo mengi sana lakini kati ya hayo ni haya hapa:

  -Yohana 3:18-Amwaminiye Yeye hahukumiwi, asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini Jina la mwana pekee wa Mungu.
  -Yohana 3:36-Amwaminiye mwana yu na uzima wa milele, asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
  -Yohana 4:42b-tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
  Je umeona kitu hapo Ndg Albert Paul kwamba Yesu sio Mwokozi wa wakristo tu bali ni mwokozi wa ulimwengu wote(watu wote, viumbe vyote). Soma pia Yohana 6:35, 40.

  Kuhusu Yesu kuwa njia pekee ya kufika kwa Mungu wa kweli imeandikwa hivi katika Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA na KWELI na UZIMA; mtu haji(hafiki) kwa Baba(Mungu) ila kwa njia ya Mimi(Yesu)” (maneno ya kwenye mabano ni yangu). Sasa hili halina ubishi kwamba Yesu ambaye ndiye Mungu anakuambia Yeye ndiye njia pekee ya kufika kwenye ufalme wake, kama wewe utaona hata yule anayemwabudu na kumuamini ng’ombe(wahindi) kuwa anaweza kumfikisha kwa Mungu wa kweli, basi hilo ni juu yako, lakini ukifuata hilo utapotea milele. Ndugu yetu Benard Mwenda amelieleza kwa kirefu pia katika mchango wake wa jana(19/7/10).

  Nina imani kuwa unajua kwamba kuna destinations mbili tu za watu baada ya maisha haya yaani uzima wa milele(paradiso) na moto wa milele(jehanamu). Hizi ni njia mbili tofauti, hakuna anayeweza kupita kwenye njia zote mbili kwa wakati mmoja na akafika kwenye moja ya destinations hizi. Kama mtu haamini kuwa Yesu ndiye njia pekee ya kwenda kwenye destination ya uzima wa milele, basi lazima mtu huyo anaifuata ile njia nyingine ya upotevuni itakayomfikisha jehanamu. Biblia imeziweka njia hizi mbili kwenye hali ya upana wake(Mathayo 7:13-14). Biblia inasema njia nyembamba iendayo uzima na njia pana iendayo upotevuni. Na Yesu anasema kuhusu uzima wa milele namna hii “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe,Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma”(Yohana 17:3)

  Inawezekana ndg Albert Paul unaliona jina Yesu kuwa sawa na jina kama Mohamed au manabii wengine kama akina Isaya, Yeremia ,Daniel,Hagai n.k. Jina Yesu ni jina la Mungu mwenyewe ndio sababu tunakuambia Yesu ni Mungu. Imeandikwa hivi kwenye injili ya Yohana 17:11b ‘Baba mtakatifu, kwa JINA LAKO ulilonipa , uwalinde hawa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo” Soma pia Waebrania 1:4, Wafilipi 2:9.

  Kuhusu hili la ujio wa Mohamed kwamba naye amekuja kufanya nini hapa duniani, naomba unionyeshe popote katika biblia mahali manabii wa kale(niliowataja hapo juu na ambao sikuwataja) waliotabiri au kueleza ujio wa Mohamed na kusudi la ujio wake. Yesu alitabiriwa na karibu manabii wote kuja kwake na kusudi la ujio wake. Nadhani ni sahihi zaidi kujiuliza wewe mwenyewe ujio wako hapa duniani una kusudi gani, kwa sababu Mungu hajakuleta hapa duniani bila kusudi lolote, it is not a coincident, there is a specific purpose and after that purpose usipotee milele bali umrudie Yeye aliyekuleta hapa. Sasa kama huijui njia sahihi, hata hilo kusudi hutalijua kamwe. Mwanadamu yeyote hajaletwa duniani kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu, bali anaweza kusadia kuonyesha njia sahihi ya wengine kukombolewa(kuhubiri injili ya wokovu). Aliyekuja kwa kusudi hilo ni Yesu peke yake (Mathayo 1:21).

  Mungu awabariki wote.

 14. Ndugu Moderator, wala sihitaji tena kuchangia chochote kwenye blog yako, nimechoka!
  Nashukuru kwa jitihada zako za kunifukuza. Umefanikiwa. Ila, ndugu zako wajiitao wameokoka, wanahitaji mtizamo mpya hasa wa namna ya kulitafakari neno la Mungu. Nawapa ushauri wa bureeeeeee! Nimepata masikitiko makubwa kwa namna wanavyoitafakari bibilia, ni jambo la kusikitisha hasa kwa watu ambao hawataki mabadiliko.

  Kila la heri mkuu.
  Lakini inakuwaje upublish comment ya mtu atofautishaye Mungu wa Wakristo na Waislam kwa namna hii? MUNGU(huyu ni wa Wakristo) na mungu(wa Waislam) halafu ushindwe kupublish comment yangu?

 15. Ndugu Albert Paul,

  Kutokana na majibu uliyonijibu kwa maswali niliyokuuliza, japo nimekuelewa vema kabisa kulingana na mawazo yako, lakini kukuelewa kwangu bado kumezaa maswali mengi juu ya majibu yako. Kutokana na namna unavyofahamu wewe kama ulivyonieleza, ninaingia katika fahamu zako na kujiuliza maswali yafuatayo:-

  1.Umeeleza kuwa Yesu Kristo alikuja kwa ajili ya kututoa katika utumwa wa dhambi, na pia umesema kuwa ujio wake haukuhusishwa na dini nyingine. Hapa ninajiuliza swali, iwapo hakuja kwa ajili ya dini nyingine, imekuwaje basi watu wengi duniani kuacha dini zao na kufuata mafundisho ya Yesu?. Kwa nini hawaridhiki na dini zao ambazo kwa mtazamo wako zinaweza bado kuwafikisha mbinguni?

  2.Umeeleza kuwa Mkristo ni yeyote ambaye imani yake anaihusisha na ujio wa Yesu Kristo na asiye Mkristo ni yule ambaye imani yake haimhitaji Kristo kuwa ndiye njia pekee. Ninavyofahamu mimi, mfumo wa utawala wa wanadamu hapa duniani ni mfano wa mfumo wa utawala wa Mungu. Katika Serikali mmoja, tuchukue mfano serikali ya Rais Kikwete, ninavyojua Kikwete hataweza kukubali kuwa, kila mtu au makundi mbalimbali katika nchi yake, yafuate mifumo yao yenyewe kadiri yanavyoona inafaa, bila kufuata taratibu za nchi. Haitawezekana kuwa na mifumo tofauti ya kiutawala katika nchi moja. Sasa Mungu ni mmoja na ufalme wake ni mmoja, yeye ndiye mtawala wa yote, ni kwa sababu gani sasa aweke mifumo tofauti ya kumfikia wakati yeye ndiye mtawala pekee?

  3.Umesema wanadamu wote wanayo nafasi sawa katika kumjua Mungu kwa sababu lengo lao ni moja labda tofauti ni namna ya kumjua huyo Mungu. Nionavyo mimi, wote kama wanakuwa na nafasi sawa katika kumjua Mungu, basi pia wote wangekuwa na nafasi sawa katika kumuishi huyo Mungu. Hivi, kuna uwezekano wa kuwa na lengo moja la kujenga maghorofa yanayofanana kwa hali zote, kisha wajenzi wakajenga kwa vipimo tofauti na hatimaye majengo hayo yakafanana kwa hali zote?

  4.Kama nilivyoandika hapo juu, taratibu za duniani ni mfano wa taratibu za Mungu, mahakama katika nchi huwa na hukumu zenye sheria sawa. Haiwezekani watu wawili tofauti waliofanya kosa moja mfano la kuiba; katika hukumu, moja akahukumiwa kuwa ni mkosa na akafungwa jela, na mwenziwe kwa kosa hilohilo akaambiwa kuwa hajatenda kosa japo naye ameiba! Ninavyofahamu, na Mungu wetu ndivyo alivyo. Kule mbinguni haitawezekana kabisa, mfano; aliye mwislamu ahukumiwe kwa kosa la kutofanya swala tano kila siku alipokuwa hapa duniani, na mimi nisihukumiwe kwa kosa hilo hilo eti kwa sababu sikuwa mwislamu hapa duniani! Huyo ninaona siye Mungu wa haki ninayemwamini mimi! Wewe unasemaje katika hilo?

  Ninafahamu kuwa, katika vipindi tofauti tofauti katika biblia, walikuja manabii mbalimbali. Kwanza kabisa Mungu aliwaumba na kuwaweka katika bustani ya Edeni, mababu zetu ambao ni Adamu na Hawa. Baada ya gharika, kilianza kizazi kingine cha akina Nuhu, akina Musa, Daudi, kikaja kizazi kingine cha manabii, kama akina Eliya, Yeremia, Ezekiel, Daniel, Isaya n.k. Pia kwa kipindi tofauti kabisa alikuja Yesu Kristo akiwa na mitume waliomwunga mkono baadaye, kama akina Paul, Petro, Yohana, Yakobo N.k.

  Mimi binafsi ninavyojaribu kuisoma biblia, ninagundua kuwa kila kundi la watu niliowataja hapo juu, lilikuwa na mafundisho yanayotofautiana kwa namna moja ama nyingine, mfano mdogo tunauona kwa nabii Musa ambaye aliambiwa na Mungu kuwa awape wana wa Israeli sheria mbali mbali za kuzifuata. Sheria mojawapo ilikuwa ni ile ya kuwapiga kwa mawe hadi wafe, wanawake wote waliokuwa wamepatikana na kosa la kufanya uzinzi/uasherati, Kumb. 21:18-21, Kumb. 22:23-24. Lakini tunaona kosa hilo hilo la kufanya uzinzi, lilipofanywa nyakati za Yesu, Mafarisayo walijaribu kumpelekea Yesu Kristo ili ahukumu, lakini Yesu katika hukumu yake hakuwa tayari kuwaamuru wale mafarisayo wampige yule mwanamke kwa mawe!. Ukisoma vivuri eneo hili, inaonesha kuwa Yesu hakukubaliana kabisa na hukumu zilizokuwa zikitumika kabla yake. Yohana 8:4-7. Swali kwako Albert, katika eneo kama hili, ili nijihakikishie kuwa nakuwa salama na ninaamua sheria za haki za kunifikisha mbinguni, nimfuate nani; Musa au Yesu? kama ni Musa ni kwa nini, na kama Yesu ni kwa nini? Au nimfuate yeyote ninayemtaka? Kwa nini?

  Kwa kumalizia ndugu yangu Albert ni kwamba, Neno la Mungu ni gumu kama hujampokea Bwana Yesu na kumfanya kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Ukimpokea kwa dhati na kuachana kabisa na mapokeo ya wazee kama alivyofanya mtume Paul,[Wagal 1:14] ninaamini kabisa moyo na nafsi yako itabadilika na utakuwa kiumbe kipya kweli kweli, siyo kinadharia, maana kuna wanaookoka siku hizi kinadharia. mimi ni Mkristo, ninamwamini Yesu Kristo kuwa ndiye pekee, ninaamini kuwa hakuna njia nyingine ya kumwona Mungu zaidi ya kumfuata Yesu, Yohana 14:6, “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”. Ninafahamu kabisa pia kuwa Yesu ni Mungu, kwa vile ni Mungu ninajua kabisa kuwa Mungu hawezi kusema uwongo, Hesabu 23:19, “Mungu si mtu, aseme uwongo….” Akisema kuwa yeye ni njia pekee, ndivyo ilivyo. Kama itakuwa Neno alilosema kuwa yeye ni njia, kweli na uzima, na kuwa mtu hatafika kwa Baba ila kwa njia ya yeye, liwe ni uwongo, basi u-Kristo wetu ni bure kwa sababu tumemwamini mwongo! Maandiko yanayofanana na kupotea kwa jinsi hiyo waweza kusoma katika, 1Wakorinto 15:12-19

  Njia ni nyembamba sana wanaopata neema ya kuiona ni wachache sana, Mathayo 7:14 “Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache”. Maneno haya hayawahusu wanaomwamini Kristo tu, bali ya kila anayetaka kumwona Mungu siku ya mwisho. Namshukuru Mungu kwa sababu mimi nami baada ya kupinga sana juu ya wokovu hatimaye kwa neema yake aliniokoa.

  Nd. Albert, Bwana akupe neema na kibali cha kuwa katika njia itakayokufanya siku moja umwone. Amani ya Kristo pia ionekane kwako na pia ikufunike unapokuwa unatafakari juu ya hili.

  Shalom!

 16. Ndg Albert,

  1.Nanukuu
  “Sasa ndugu yangu John Paul, unahakika gani kuwa mwimbaji ali-quote baadhi ya maneno ya Wagalatia 3, 1-6? Neno roho wakati unaandika baadhi ya maneno ya wimbo ulioutoa kama mfano, uliliandika kwa herufi ndogo,sijajua ni kwa nini unahusisha na roho ya herufi kubwa,na ungejuaje mwimbaji alimaanisha herufi kubwa au ndogo. Uliutafakari wimbo kwa makini ktk harakati za kupata kilichokusudiwa? Binafsi sijausikia huo wimbo,lakini napata picha ya kuwa mwinjilisti alikuwa anawakumbusha watu wasigombane, anawauliza, kwa nini mnaanza ktk hali ya uMungu(ktk roho) na mwaishia kugombana(ktk mwili)?, tafsiri hii ni kulingana na maneno ya wimbo uliouandika,inajionyesha wazi.”

  Maelezo niliyotoa kuhusu suala hilo yameshaeleweka kwa wasomaji wanaoifahamu Biblia na wanaotaka kufahamu Biblia.

  2. “Upendo wa kweli ni wa kumsaidia mtu ajiepushe na hatari ilimradi tu isiwe kwa masharti/vigezo fulani fulani.”
  Je,maneno yako hayo yanabaki hivyo hata kama masharti na vigezo vinavyotumika kumsaidia mtu huyo ni namna ambavyo neno la Mungu linaagiza?

  3. Jibu lako hili ni too general-
  “Soma kitabu kitakatifu,tafakari kwa kina maudhui ya maneno uliyoyasoma ili upate tafsiri sahihi isiyombagua mtu yeyote kwa misingi ya itikadi za kidini zenye kumwamini Mungu umwaminio wewe.”

  Hebu fafanua kidogo, Kitabu hicho kitakatifu ni kipi?

 17. Mh
  Ninamashaka na Ukristo wako Albert Paul, toka mwanzo kule unajibishana na John Paul, mtu unayeona hata Mtume Mohamed anaweza kukufikisha mbinguni! tena Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo ndiye huyo wa waislamu nadhani unamatatizo. Chagua moja maana hata huko unakojipeleka kwa Mungu wa waislamu we ni kafiri huendi kwenye pepo yao ukifa. Amua sasa kumfuata Yesu kikamilifu sio mguu ndani mguu nje utaangamia. Ubarikiwe

 18. Nd. Albert Paul ,
  Asante sana kwa kunijibu maswali yangu kadiri unavyoamini, bila shaka nimekuelewa vyema kabisa. Nami nimeweza kujifunza kitu kutoka kwako yale unayoyaamini. Tathmini yangu katika kujifunza kutoka kwako nimejifunza kuwa, kwako imani YEYOTE inayoamini kuwa kuna Mungu na pia kuna maisha baada ya kufa, watu wake wakiifuata imani hiyo kadiri inavyoelekeza au kufundisha, watamwona Mungu.

  Nimekuelewa kuwa, mtu akiwa ni muislamu na anauamini uislamu kwako ni sawa, anayeuamini ubudha katika mungu ni sawa, usabato pia sawa, akiamini uyehova sawa , akiamini ukatoliki sawa, akiamini u-protestant wote sawa, akiamini u-pentekoste pekee sawa!n.k…. Ili mradi tu anatajwa Mungu katika imani hiyo, ndivyo nilivyokuelewa! Kama nitakuwa nimekuelewa tofauti utanisahihisha.

  Kabla sijaweza kuchangia chochote ninawakaribisha wengine waweze kutoa mawazo yao juu ya hili, japo chanzo cha mada hii kimetoka kwenye uimbaji wa kwaya. Kwa vile mada hii ya dini iko tofauti na mada lengwa, tungeihamishia labda kwenye mada ya “tujadiliane”.

  Shalom.

 19. MHHHHHHHHHHHHi kaka Albert tena nawewe ,wanamwamini mungu gani wakati YESU ndiye MUNGU,kweli itabaki kuwa kweli Mwenye mbingu ni YESU. njia ni moja tu wote tunaotaka kwenda mbinguni ni lazima tupite hapa YESU.tofauti na yesu hakuna njia kabisa ni motoni motoni tu. YESU NDIYE MUNGU WA KWELI:ILE MBINGU hata ukaomba mara tano kama unaemuomba siyo YESU umechemsha ,mungu mwingine umuombaye anashimo liitwalo kuzimu hana mbingu ni uwongo wa SHETANI HUOOO00.

 20. Ndugu yangu Jonas Malimbo, katika maoni yako ya July 10, 2010 umeeleza / kujibu swali la Ndg Albert ukisema “…siwezi kutaja majina lakini ujumbe umefika kwa njia moja au nyingine naamini utaeleweka kwa baadhi ya watu. Zipo nyimbo nyingi kweli ambazo haziuoneshi ukristo wetu kama wewe ni mfuatiliji wa nyimbo za Injili unaweza kufanya uchunguzi…”

  Ni kweli waamini hii ni njia sahihi ya kusaidia?
  Kama watu wanafanya makosa, na unaona wanapotosha, ni kwanini usiwe muwazi? BINAFSI NAENDELEA KUONA TATIZO LA UNAFIKI KWENYE UKRISTO WA NYUMBANI.
  Ni tatizo la kimalezi kwani waTanzania wamefunzwa kutokuwa offensive hata pale wateteapo lililo sahihi. Tatizo ni kuwa UNAFIKI huu waingia hata kwenye dini.
  Kama kitu si sahihi, sema kuwa “WIMBO HUU / AMA MUIMBAJI HUYU SIDHANI KAMA ANAMTUKUZA MUNGU KWA SABABU HIZI NA HIZI NA HIZI. Na huu ni mtazamo wangu”
  Kila msomaji anaelewa kuwa una haki ya kutoa mtazamo wako na haki ya KUKOSEA NA KUKOSOLEWA. Nami katika majadiliano mengi hapa nimesema hilo na NIMEKOSOLEWA PIA.
  Kama ulivyosema, si lazima kila mtu akubaliane nawe (kama ambavyo si lazima ukubaliane na kila mtu). Sioni kwanini uje na hoja hapa kama hauko tayari kuiweka bayana

 21. Ndugu Haggai,kama wewe unavyoduwaa na mimi ndivyo hivyo, na ndio maana sichoki kutoa maoni yangu.
  Ni elimu mpya niipatayo kuhusu “R” na “r” ambayo pia nitaifuatilia zaidi nijue undani wake. Pengine elimu hii ndiyo iliyokuwa inanifanya nisielewe kifungu kile.
  Sasa ndugu yangu John Paul, unahakika gani kuwa mwimbaji ali-quote baadhi ya maneno ya Wagalatia 3, 1-6? Neno roho wakati unaandika baadhi ya maneno ya wimbo ulioutoa kama mfano, uliliandika kwa herufi ndogo,sijajua ni kwa nini unahusisha na roho ya herufi kubwa,na ungejuaje mwimbaji alimaanisha herufi kubwa au ndogo. Uliutafakari wimbo kwa makini ktk harakati za kupata kilichokusudiwa? Binafsi sijausikia huo wimbo,lakini napata picha ya kuwa mwinjilisti alikuwa anawakumbusha watu wasigombane, anawauliza, kwa nini mnaanza ktk hali ya uMungu(ktk roho) na mwaishia kugombana(ktk mwili)?, tafsiri hii ni kulingana na maneno ya wimbo uliouandika,inajionyesha wazi.

  Ndugu John Paul, kwenye comment yako ya July 14, uliniuliza maswali, swali la 1 na la 3, hebu pitia kwanza majibu niliyompatia ndugu Bernard,

  2. Upendo wa kweli ni wa kumsaidi mtu ajiepushe na hatari ilimradi tu isiwe kwa masharti/vigezo fulani fulani.
  Swali lako la 4, nalijibu kama ifuatavyo.
  Soma kitabu kitakatifu,tafakari kwa kina maudhui ya maneno uliyoyasoma ili upate tafsiri sahihi isiyombagua mtu yeyote kwa misingi ya itikadi za kidini zenye kumwamini Mungu umwaminio wewe.

  Amani iwe nanyi.

 22. Nianze kwa kujibu maswali ya ndugu Bernad.
  1. Kwa mujibu wa Biblia, Yesu alikuja kututoa katika utumwa wa dhambi kwa yeye kuteswa na kusulubiwa msalabani. Historia ya kuja kwa Yesu,kuteswa na kusulubiwa kwake kama ilivyoandikwa ktk bibilia haijahusisha dini nyingine kama uislamu,kwa hiyo sidhani kama itakuwa ni sahihi kusema kuwa wasiokuwa na imani ya kikristo basi wamepotea njia. Wakati huohuo,tujiulize, mtume Mohamad naye alikuja duniani kufanya nini? Je, ni sahihi kwa wale wamwaminio kutumia ujio wake kuelezea hatma ya wale wasiomwamini?

  2&3. Mkristo ni yeyote yule ambaye imani yake anaihusisha na ujio,kuteswa,maisha yake hapa duniani,kufa na kufufuka, yake kwa ujumla. Asiye mkristu ni yule ambaye kwa namna moja ama nyingine, imani yake haimhitaji yeye kuamini kuwa Yesu ndio njia pekee ya kuufikia ufalme wa Mungu. Binafsi naamini kuwa wapo wamwaminio Mungu huyu huyu wakristo wanayemwamini pamoja na kuwa hawaamini kuwa Yesu ndio njia ya pekee na uzima.

  4. Wote wana nafasi sawa katika kumjua Mungu kwa maana lengo lao ni moja labda utofauti ni kuwa namna ya kumjua Mungu huyohuyo ndio tofauti.

  6. Kama unamwamini Yesu (wote wa imani yenye msingi wa Kristo) basi huna budi kumfuata,kwa maana ya kufuata yote aliyokuwa anafundisha. Kama utamwamini halafu usienende kwa kadiri ya matendo yake hutaweza kuuona Ufalme wa Mungu.

  5&7. Mkristo yeyote yule anamwamini Yesu kwa kuwa yeye ndiye msingi wa imani ya ukristo. Kumfuata Yesu ni kuenenda kwa kadiri ya mafundisho na matendo yake.

  8. Kuokoka kama neno la kiswahili ni hali ya kuwa huru, kuepuka,kujinasua n.k kutoka katika jambo lolote ambalo si zuri,linaloleta usumbufu,linaloleta kutokuridhika.

  Kwa maana ya kidini.
  Kwa mujibu wa wakristo walokole, kuokoka ni hali ya mtu binafsi kumkiri Yesu kwa kinywa chake kuwa Yesu ni mwokozi na ni njia pekee ya kuweza kuufikia ufalme wa Mungu.

  Kwa Roman Catholic, kuokoka ni hali ya kuondolewa dhambi ya asili kupitia ubatizo ambao wazazi kumkiria mtoto mchanga kwa kukiri kuwa Yesu ni mwokozi wa Maisha yake na kukiri kuikubali imani katoliki pamoja na kumkataa shetani na mambo yake yote. Kwa upande wa waislam sijaona dhana hii ya kuokoka, hata kwa imani nyingine zenye kumwamini Mungu muumba wa vyote,yawezekana kuna namna yao ambayo pia lengo ni moja,la kuuona ufalme wa Mungu.
  Kwa ujumla kabisa,kuokoka kwa maana ya dini ambazo neno kuokoka hutumika ni hali ya kujiepusha na kutokutenda dhambi.

  9. Ndio. Kwa yeyote aaminiye kuhusu kuokoka kama nilivyoeleza hapo juu,hana budi kuokoka ili aweze kumwona Mungu.

  10. Yote uliyoyataja ndio namna ya maisha ya Yesu na Mtume Mohamad. Naamini ni hivi pia kwa manabii wote ambao watu(wamwaminio Mungu aliye hai, mwumba mbingu na nchi) huelekeza imani zao kwao kwa kuwa vitabu vyao vitakatifu vinaeleza hivyo. Watu hawa walitenda mazuri kulingana na imani zetu, hivyo tukitenda yale waliyotenda, tutamwona Mungu.

  Ndugu Bernard Mwenda, nimeyajibu maswali yako na naimani kuwa utakuwa umenielewa/umenifahamu vyema.
  Ubarikiwe sana.

 23. JINA LA YESU NI LA KUOGOPWA SANA SANA NA HAKUNA KAMA YESU,HILI TATIZO LA KUMTAJA YESU BILA KUMAANISHA NI HATALI SANA MAANA YESU NI MUNGU HUWEZI KUMCHEZEA WALA KUMFICHA CHOCHOTE,KAMA MTU UNATAKA KUPATA HELA SEMA NIA YAKO USIWAFUNGIE WASIOOKOKA NJE WAKATI NA WEWE MWENYEWE HUTAINGIA,WAIMBAJI NDUGU ZETU TULIOGOPE HILI JINA JINA HILI LIMESHINDA MAUTI JINA HILI LIMETULETEA UKOMBOZI JINA HILI NI JINA PEKEE WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO KUOKOLEWA KWALO,NI MAOMBI YANGU TULIPE JINA LA YESU HESHIMA NA UTUKUFU.ENDELEENI KUIMBA KWA KUMAANISHA MBWEMBWE NYINGI HAZINA HAJA TUNACHOHITAJI NI KUMUIMBIA YESU NA KWENDA MBINGUNI VILE VILE TUNAPOONA WALE WASIOMJUA YESU WANAMRUDIA KWA UJUMBE ULIOMO NDANI YA WIMBO,TUNAWAPENDA TUNATAKA KUMUONA YESU NA WAIMBAJI WETU .

 24. Ndugu Pablo,
  Ahsante kwa ushauri wako.Nadhani ndani ya blog hii hakuna mabishano isikuwa ni kufundishana na kuonyana kwa kufuata misingi ya neno la Mungu ambalo hilo ndilo ulilolisisitiza hapo juu.Maswali yanakuwa mengi kwa mchangiaji fulani pale tu anapochangia mchango wake usiokuwa na msimamo thabiti wa neno la Mungu.Najua wengine wanajikita zaidi kwenye dini au madhehebu yao, kitu amabacho si sahihi sana kuwa hivyo ndani ya blog hii kwa kuwa madhehebu ni taratibu za kibinadamu tu, si utaratibu wa Mungu.Ndiyo sababu basi watu wanasisitiza kuwa wokovu si dini wala dhehebu, ni mpango kamili wa Mungu mwenyewe wa kumtoa mtu katika anguko la dhambi kwa kumpokea Yesu Kristo ndani ya moyo wake.Sasa anapokuja mwingine akisema hata bila kumkubali Yesu kama Mwokozi wake, naye pia atamuona Mungu(atarithi ufalme wa Mungu),lazima tumuelimishe kuwa hilo sio sahihi (kwa kutumia neno la Mungu) ili sasa aione njia iliyosahihi ya kufika kwenye ufalme wa Mungu.Kwa kufanya hivyo sio kubishana bali ni kuelekezana na kuelimishana ili kwa pamoja tusonge mbele kwenye safari hii ya kwenda mbinguni.
  Mungu akubariki sana.

 25. tunashukuru wapendwa kwa maelekezo haya ila tudumu katika neno wala tusifanye hapa uwanja wa mabishano!

 26. Ndugu Albert,

  Kuanza kwa Roho na kuanza kiroho nimeelezea tafauti yake. Labda zaidi kidogo tena:

  ‘Kuanza kwa Roho’ herufi kubwa ‘R’ inamaanisha Roho mtakatifu. ‘Kuanza kiroho’ ni kuanza katika ulimwengu wa roho. Ulimwengu wa roho uko wa giza na wa nuru.

  Haya niliyoongeza yanatosha. Kama una nia ya kuelewa utakuwa umeelewa. Mimi siwezi kukulazimisha. Soma Biblia ufahamu jinsi ambavyo ‘R’ imetumika kwenye Roho mtakatifu na ‘r’ kwenye roho ya mtu au limwengu wa roho.

  Maana ya kukamilishwa katika mwili imeelezewa vizuri sana katika Biblia, hapo hapo katika maandiko hayo katika Galatia 3. Soma vizuri.

  Kwa kuwa kuna maswali yaliyoulizwa na ndugu Bernard mimi sitakuwa na maswali mengi kwa sasa. Lakini nitauliza machache tu.

  Umeandika hivi:

  “Kwa yeyote yule (mkristu na asiye mkristu) atakayebahatika kuishi maisha aliyoishi Bwana Yesu,akiweza kuzingatia matendo na mafundisho aliyokuwa akiyatoa, basi mtu huyu ni sharti atauona ufalme wa Mungu. Sasa,wapo wanaokuja na tafsiri za kusema kuwa asiyemwamini Yesu, basi ni wa mataifa na amepotea njia. Tafsiri hii ni ya hatari sana na inakwenda kinyume kabisa na amri iliyokuu, amri ya Mungu mapendo ya kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe.”

  1.Kutokana na maelezo hayo, mtu ambaye hatabahatika kuishi maisha aliyoyaishi Bwana Yesu, hatima yake itakuwaje?

  2. Unavyofahamu wewe upendo wa kweli ni upi kati ya haya: Kumsaidia umpendaye ajiepushe na hatari au kumwacha tu katika hali yake ya hatari ili aangamie?

  3.Je, itikadi zote za dini {kama ulivyoandika} hutumia Biblia?

  4. Wewe uliandika katika mchango wako wa tarehe 12 hivi:

  “Jamani, tufundishe kile ambacho Mungu anataka na si kufundisha vitu ambavyo madhehebu au dini zetu zinavyotaka….”

  Ndiyo maana nikauliza ni kwa namna gani tutafahamu kile ambacho Mungu anataka ili tuweze kufundisha?

  Wewe umesema tusifundishe kile ambacho madhehebu yanataka bali anachotaka Mungu. Najua yanachotaka madhehebu tunaweza kukipata kutoka katika mafunzo ya madhehebu. Swali ni wapi tunaweza kukipata kile anachotaka Mungu ili tukifundishe?
  Hivi ndicho ninachomaanisha kwa swali lile la pili.

 27. Albert Paul,
  Labda nisitishe kwanza kile ambacho nilitaka kukisema juu yako mpaka hapo utapokuwa umejibu maswali mazuri ya ndg yetu Bernard Mwenda.Lakini kwa kifupi kama mtu anajiita ni mkristo halafu anaona maneno Roho na kiroho ni kitu kimoja basi mtu huyo anaisoma biblia bila kuielewa.Mahali popote kwenye biblia palipo na neno Roho lililoanza kuandikwa kwa herufi kubwa ina maana ya Roho Mtakatifu na mahali popote palipoandikwa kwa herufi ndogo ina maana ya roho ya mtu au roho zingine zote za ufalme wa giza(angalia Mwanzo 1:2b).
  Halafu hili suala unalotaka kulihalalisha kuwa hata asiyemwamini Yesu alimradi anatenda matendo mema na anatimiza hiyo amri unayoiita ya mapendo,atauona ufalme wa Mungu,hilo si kweli.Hebu soma vizuri Yohana 3:18 na 36.Biblia inasema mtu hahukumiwi akimwamini Yesu,na kwa kumwamini Yesu ndiko kunakupelekea kutenda matendo mema ikiwa ni pamoja na upendo kwa sababu Mungu ni upendo(1Yohana 4:7-21).Asiyemwamini Yesu tayari amehukumiwa, sasa hebu niambie mtu anayeamini kuwa Yesu si Mungu lakini anatenda matendo mema,ni kweli atauona ufalme wake?
  Nimesema labda nitaandika mengi baada ya wewe kujibu maswali ya Mwenda ila kwa kweli michango yako inaniduwaza kidogo.
  Mungu akubariki.

 28. Albert Paul.
  Ninayo maswali,naomba nikuulize kutokana na mengi unayoyaandika hapo juu.
  1.Lengo la Yesu Kristo kuja hapa duniani lilikuwa ni nini?
  2.Mkristo ni nani?
  3.Asiye Mkristo ni nani?
  4.Mkristo na asiye Mkristo wote ni sawa katika kumjua Mungu?
  5.Je, kumwamini Yesu maana yake ni nini?
  6.Je, unaweza kumwamini Yesu Kristo huku usimfuate lakini bado siku ya mwisho ukamwona Mungu?
  7.Je, kumfuata Yesu maana yake nini?
  8. Unaposikia kuwa mtu fulani ameokoka huwa unaelewa nini?
  9.Je, kuokoka ni lazima kwa kila anayetaka kumwona Mungu?
  10.Matendo/tabia/mwenendo na yanayofanana na hayo yaliyo mazuri,ndiyo pekee yatakayomwezesha mwanadamu kumwona Mungu?

  Ninayo maswali mengi yanayofanana na hayo, lakini kwa leo naomba ukiweza unijibu haya niliyokuuliza. Nimeandika maswali haya kwa sababu; kutokana na maelezo yako katika maeneo mbalimbali kwenye blog hii nimekuwa siielewi imani yako, iwapo wewe ni Mkristo au vinginevyo. Maswali haya yanaweza kuwa kama ni ya kitoto, lakini kwa kweli nataka kujifunza kutoka kwako ili niweze kupanuka na kujua jinsi wengine wanavyouelewa-Kristo tofauti labda na mimi.

  Utakaponijibu maswali haya nitakuwa nimekuelewa na pia wengine watakaribishwa ili tuweze kuchangia kwa pamoja, kujua tofauti ya aliye Mkristo na asiye. Pia tutaweza kujua ni nani atakayeweza kumwona Mungu kati ya Mkristo na asiye, kutokana na maandiko katika biblia. Ninakupenda katika Kristo Yesu.

  Amani ya Kristo ikufunike!

 29. @LISA, Dokii ilisikika ameokoka, akatoa na album. Kwa kipindi anaishi South Africa kuhusu Flora Mbasha, anaimba nyimbo mchanganyiko! injili, jamii lakini kwa siku za hivi karibuni amekua mburudishaji zaidi hasa kwenye siasa na masuala ya jamii.

  @MARY,saa nyingine kuhukumu kunafaa 1Wakorintho 5:1-13 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa isiyokuwako hata katika mataifa….nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo…msari wa 12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje?

  Yohana 7:24 “Basi msihukumu hukumu kwa macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo haki”

  kama ni kweli kuna jambo halijakaa sawa na kuna uhakika kwamba lipo, nadhani tuseme tu! ili wengine wafundishike,wajirekebishe na mwili wa Kristo ujengwe! Hii ndio hukumu ya haki

  Pia samahani kwani kuvaa sare ya jeshi kuna tatizo? sio inaonesha alama ya mkristo kuwa vitani? ama!

 30. Ndugu John Paul,
  Kuanza kwa Roho na kuanza kiroho, hakuna tofauti, kwa maana na kwa kiswahili, yani ni sawa na mtu anaposema, human face na face of human,maana ni ile ile. Kwenye nukuu uliyoitoa hakuna kiashirio chochote cha kimaana ambacho kitakufanya uongeze Mtakatifu. Kukamilishwa katika mwili wasemaje ndugu John Paul? Hapa maneno haya ya biblia yanatwambia nini? Ikiwezekana toa tafsiri ya kifungu ulichokinukuu.

  Yesu alisema asiyemwamini yeye, amekwisha kuhukumiwa na pia alisema yeye ni njia ya kweli na uzima, yeye atakayemwamini, atauona ufalme wa Mungu.
  Ni maneno mazuri kwa hakina na yenye kuleta faraja. Tatizo linakuja kwenye Tafsiri ya maneno haya matamu yaburudishayo roho kwa namna ya pekee.

  Kwa maneno hayo aliyoyatamka Yesu, ninamwelewa hivi;
  maisha na matendo yake yalikuwa ni mfano wa kuigwa. Kwa yeyote yule (mkristu na asiye mkristu) atakayebahatika kuishi maisha aliyoishi Bwana Yesu,akiweza kuzingatia matendo na mafundisho aliyokuwa akiyatoa, basi mtu huyu ni sharti atauona ufalme wa Mungu. Sasa,wapo wanaokuja na tafsiri za kusema kuwa asiyemwamini Yesu, basi ni wa mataifa na amepotea njia. Tafsiri hii ni ya hatari sana na inakwenda kinyume kabisa na amri iliyokuu, amri ya Mungu mapendo ya kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe.

  Majibu ya maswali yako Bwana John Paul.

  Ninaamini Biblia ni neno la Mungu lenye kumgusa kila mmoja katika dunia hii bila kujali itikadi yake ya kidini ilimradi tu inamtambua Mungu muumba wa vyote,muumba wa mbingu na dunia. Tafsiri tofauti za maandiko katika biblia ndizo zitutengazo binadamu, pamoja na kuwa Mungu mwenyewe alishaweka bayana kuwa watu wa dunia yote ni kitu kimoja,twatoka kwake, na akatukumbusha kuwa yeye hataki kitu kingine,bali, upendo miongoni mwetu,ni amri ituunganishayo watu wa dunia hii.

  Swali lako la pili nduyu yangu sijalielewa. Liweke vizuri zaidi nipate kulielewa,then nitakujibu kama litakuwa ndani ya uwezo wangu.

 31. Naposema kuburudisha roho, namaanisha kuguswa kwa namna ya kukikubali kile ambacho mwimbaji kakusudia, kama si kizuri, ni dhahiri kuwa kitakugusa kwa hali ambayo hutafurahia na hivyo roho haitaburudika/furahika. Ni ukweli usiopingika kuwa ktk nyimbo za injili burudani huletwa na mambo mengi kuanzia kile asemacho mwinjilisti/mwimbaji, namna ya uwasilishaji yaani, aina ya muziki autumiao, Wakongo kwa mfano,huburudika sana pale muziki unapokuwa kwa ladha ya bolingo kwa mfano, ala za musiki n.k.
  Ni hayo tu.

 32. Nianze na bwana Paul Holella.
  Ndugu yangu, uandaaji wa nyimbo za injili si bure, inagharimu pesa nyingi. Kazi hizi zikiandaliwa vibaya vibaya si ajabu hata wewe ukazisusa bila hata kujali neno la Mungu lilokusudiwa!

  Hata kwenye nyumba za ibada,kuna wakati wa fungu la kumi, sadaka,matoleo n.k, hakuna nyumba ya ibada isiyokuwa na kipengele hiki. Tena sadaka zinapotokea kukusanywa ktk kiwango kidogo,wapo viongozi ambao hulizungumzia na kutumia mbinu ambazo huwahamasisha waumini ktk kutoa mafungu ya kumi, sadaka matoleo n.k. Sasa ndugu yangu Paul Holella, ni kipi kinachokushangaza kwenye huduma hii ya nyimbo za injili?bila pesa ungeweza kupata huduma hii? Labda nitoe ushauri, matamasha ya nyimbo za injili yawe yanafanyikia kwenye nyumba za ibada ili angalao basi watu waingie bure au watoe pesa kidogo za ukarabati wa nyumba hizo n.k kuliko kufanyia matamasha kwenye kumbi maalumu kwa kazi hizo lakini hukodishwa kwa gharama kubwa halafu kwa sababu ni nyimbo za dini basi watu wanataka kuingia bure!

  Maneno yasemwayo ktk nyimbo za dini,naamini yote huwa yanajenga,la si hivyo nyimbo tuzisikiazo zisingeruhusiwa kuuzwa na hata redioni na kwenye TV Stations, zisingekuwa zinaonyeshwa. Hivyo basi maneno mazuri yasemwayo, HUBURUDISHA Roho,na nafsi, na pia namna ya uwasilishaji wa maudhui HUBURUDISHA mwili pia kwa watu kucheza n.k. Sasa sijui ndugu John Holella unamaanisha nini unaposema nyimbo za injili zimekuwa zikiburudisha tu, tupe ufafanuzi zaidi.

 33. EEh ninaogopa kuhukumu , lakini jamani inabidi tuwaombee kwa mzigo, mpendwa mmoja ameuliza kuhusu mbasha, je wale waliovaa sare za jeshi tusemeje? yako mambo yanazidi kiasi, kweli hapo shetani anatupiga bao la kisigino.Niliwahi sikia mahali fulani walitangaza kumualika mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu (wa 2008/2009) katika uzinduzi wao, walipowasiliana jibu walilopewa ni kwamba kumleta mwimbaji huyo hadi mkoani wangemgharamia malazi na chakula kama kawaida , lakini bila kukosa milioni moja taslimu ,mbona walichoka wakaamua kufanya uzinduzi bila mwimbaji huyo, tulipouliza mbona mwimbaji waliyekuwa wametutangazia hayupo,ndipo walitujibu hayo.

  Ninachotaka kusema kwamba kweli kuna waimbaji sasa wapo sokoni na siyo shambani mwa Bwana tena, ni hatari, niliwahi kuandika wakati fulani kuwa utakuta wimbo mmoja una steps karibu kumi hivi unadhani hapo wasikilizaji watadaka maneno ? hakuna ” kama siyo kushangaa mitindo ya kucheza, ndiyo maana nikasema shetani anatupiga goli la kisigino.
  Tuwaombee waimbaji ili wajae Roho Mtakatifu ili wawe shambani mwa Bwana na kwa utukufu wake.

 34. hata namii nakubali unachokisema mtumishi watu haw nafikiria wameingia katia nafasi zisizokuwa zao ni sawa na uwe na doctor aliyepaswa kuwa askari tegemea sindano zisizo na dozi sahihi

 35. Ndugu Albert Paul,

  Nami nashukuru kwa kuwa tunaendelea kujadiliana hapa, kwa nia ya kujifunza.

  Umeandika kwamba majibu yangu yanakulazimisha ujiulize maswali mengi na unalazimika kuomba ufafanuzi tena. Ni sawa kabisa. Kwa kuwa ni katika kuuliza na kupata majibu ya yaliyoulizwa ndipo mtu anaweza kujifunza kitu. Kuna msemo usemao ‘asiyeuliza hana ajifunzalo’.

  Ninalokuomba ni kwamba yaandike hayo maswali mengi uliyolazimika kujiuliza ili tushirikiane pamoja. Waweza kuniuliza mimi mwenyewe, kwa kuwa ndiye naendelea ku-dialogue na wewe, au waweza yaweka tu hapa ili kila anayeweza kuwa na jibu aweze kuchangia. Lakini hata ukiniuliza mimi natumaini haimzuwii mtu mwingine kuchangia.

  Nasubiri maswalli hayo na maelezo ya wapi hasa unahitaji tena ufafanuzi.

  Labda tu mambo machache ya kuweka wazi ni kuwa si kwamba mimi nalalamika kwa sababu uislamu umehusishwa mahali pasipo stahili bali NASIKITIKA kwa sababu uimbaji wa nyimbo za injili kwa sasa unaelekea pabaya. Idadi kubwa sana ya watu wanaoimba nyimbo au muziki wa injili hawajui kama ni kiasi gani wako sahihi na kiasi gani wako wrong. Kwa kifupi ni kwamba kwa waimbaji wengi hakuna tathmini.

  Ndg Albert, Wimbo huo niliusikia tarehe 10/7/2010 kama saa 1 asubuhi hivi, kwa saa za Afrika mashariki. Na kama umeangalia vizuri niliandika mchango wangu saa 5:34 asubuhi hiyo hiyo. Sasa kama kuna muislam atalalamika atafanya hivyo kwa wakati wake. Hata hivyo sifahamu ni waislam wangapi wameshausikia wimbo huo na kutafakari ujumbe wake. [Tatizo pia si watu wengi husikiliza nyimbo kwa lengo la kupata ujumbe bali wengi husikiliza muziki kwa lengo la kuondoa ‘ukimya’. Wakati pakiwa kimya mtu anaona bora afungulie muziki pachangamke] Yawezekana walishalalamika, who knows! Mimi nalifahamu Neno la Mungu kwa kiasi ambacho Mungu amenijalia kufahamu. [Sifa na utukufu ni kwake]. Ninaufahamu habari za uislam kwa kiasi fulani pia. Kwa hiyo siwezi kusubiri hadi muislam alalamike wakati kuna jambo linaharibika. Nasimama katika zamu yangu. Natakiwa kutekeleza jukumu langu kama mkristo – Kuonya, kushauri na hata kukemea kama ikilazimika.

  Mahali pengine ambapo hujanielewa na ninataka kupafafanua ni pale ulipoandika “kuanza kiroho”. Maandiko niliyonukuu kutoka kitabu cha Wagalatia yanasema “kuanza kwa Roho”. Roho inayozungumziwa hapa ni Roho Mtakatifu aliyeahidiwa na Yesu siyo ‘kiroho’ (spirituality). Kama ingekuwa kiroho ya spituality ingewezekana reasoning yako kwa upande fulani ikawa sahihi. [Maana zipo aina nyingi za spiritualism]. Ndiyo maana nikaandika nilivyoandika kwa sababu nafahamu tofauti ya kiroho na Roho mtakatifu. Hakuna Roho mtakatifu kwa waisilam. Mtu hupokea Roho mtakatifu baada ya kumwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Na katika uislam hakuna jambo la namna hiyo!

  Waweza kurudia kusoma tena hapo juu kama unaona hujaelewa vizuri. Lakini kama kuna swali bado wala usisite kuuliza, uliza tu. Lakini tu tuzingatie tusijekwenda nje sana ya mada yetu hii iliyopo.

  Mambo ya Ukristo versus Uislam yana ukurasa wake. Kwa hiyo kama una dukuduku kuhusiana na Imani hizo mbili kwa ujumla unaweza kuingia ukurasa wa Ukristo/Uislam. Lakini kwa kifupi ni kwamba ni Yesu Kristo aliyesema asiyemwamini yeye amekwisha kuhukumiwa na pia akasema hakuna mtu atakayekwenda kwa Mungu, Bwana wa Majeshi, pasipo kupita kwake (Yesu). Maneno hayo yako katika Biblia. Kama kuna kinyume chake waweza kuonyesha kinapatikana katika kitabu gani.

  Naomba kumalizia kwa kukuuliza maswali yafuatayo:

  1. Je, unaamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu?

  2. Ni kwa namna gani mtu anaweza kufahamu namna ambavyo Mungu anataka kuhusiana na jambo fulani?

  Nasubiri kutoka kwako ndugu.

 36. Ndugu John Paul, nashukuru kwa ufafanuzi wako.Najisikia faraja sana kwa kuyajibu maswali yangu.

  Majibu yako ndugu John Paul yananilazimisha kuzidi kujiuliza maswali mengi na nalazimika kuomba ufafanuzi zaidi.

  Kwanza kabisa, naona umeamua kuchukua hisia ambazo mwislamu angetakiwa kuzihisi kwa kuwa uislamu umehusishwa sehemu ambayo siyo. Hapa namaana kuwa,kama mwislamu kahusishwa sehemu ambayo haikustahili, basi yeye ndiye aliyetakiwa kulalamika na si wewe. Kama mwislam halalamiki,iweje wewe ulalamike?

  Kwa yeyote atakayetafsiri, “kuanza kiroho” ni lazima tu ataishia na maana ya kuwa watu walianza kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu na mwisho wanatenda kinyume na mapenzi ya Mungu(hali ya mwili). Maneno haya yawezekana kabisa yanawasilishwa kwa namna nyingine miongoni mwa waumini wa kiislamu kwani nao pia kwa kadiri ya nijuavyo mimi,lengo lao pia ni kuishi kwa kadiri ya Mungu apendavyo. Wao kama hawasemi kuishi kiroho, basi wanasema kuishi kwa kadiri ya Alah(samahanini kama nitakuwa nimekosea spelling za Alah) anavyotaka.

  Kaka John Paul, Waislam hao wasimamao na vipaza sauti vyao kukashifu ukiristo, wanadhihirisha upungufu mkubwa walionao kiroho,wapo kimwili,kidunia zaidi, na naamini ni upungufu wao binafsi na si kwa waislam wote. Waislamu wa aina hii,kama kweli wapo, hawatofautiani na baadhi ya wakristu wanaowakashifu Waislamu kwa kuwaambia kuwa ni wa mataifa na wamepotea njia kwa kuwa tu hawamwamini na hawamfuati Yesu ambaye ni njia ya kweli na uzima (kwa kadiri ya imani ya kikristo). Hili nimelishuhudia kwa baadhi ya Wakristu niliopata kuzungumza nao.

  Jamani, tufundishe kile ambacho Mungu anataka na si kufundisha vitu ambavyo madhehebu au dini zetu zinavyotaka kwa maana dharau na kashfa zinazotupiwa dini, ni matokeo ya kuaminishwa yale ambayo dini/madhehebu yetu yanaona ni sahihi na kisha kutumwa kufundisha vile vilivyoaminishwa na ambavyo dini/madhehebu yanataka na si vile ambavyo Mungu anataka.

 37. Shalom,
  nionavyo mimi kwa waimbaji wetu kuna shida imeingia ndani yao si dhani kama bado wanaimba ili kumtukuza kristo……. wamehamia kuburudisha zaidi. Niliwahi sikia uzinduzi wa kikundi fulani cha uimbaji hapa Dar uzinduzi huo ulitangazwa sana na radio Wapo na walisema kila atayefika ATABURUDISHWA …niliwaza maswali mengi sana….. kwa hiyo hawamuimbii Kristo YESU ila wanaburidisha watu …..Nyimbo zao nyingi si za rohoni ingawa wanaweza taja maneno ya kwenye biblia…ukitizama kwa macho ya ndani utagundua sio za Kristo hazijatoka kwa Roho Mtakatifu…. wana sauti na uwezo wa kutunga nyimbo kama tu waimbaji wa kawaida…
  Kwenye mialiko yao ni Pesa tu.. ….kwa mfano mwimbaji mmoja maarufu siwezi mtaja jina ili kuimba mnanegotiate kama biashara la sivyo haimbi na mnakubaliana idadi ya nyimbo….
  Mungu awatunze…

 38. Bwana Yesu Asifiwe sana,Kaka paulo Ubarikiwe sana,sijui kama wafahamu wangapi twanyanyuka kwa kusoma shauri zako hapa SG .Jamani mimi binafsi najengeka sana kiroho na fafanuzi zako unazoziandika.Mungu akuzidishie kaka.

 39. Ndugu Albert Paul,

  Nashukuru kwa maswali yako uliyoniuliza kutokana na mchango wangu uliotangulia.

  1.Ufafanuzi zaidi kuhusu kwa nini ule wimbo wenye maneno ambayo baadhi yake nimeyaandika nimesema haufai kuwa ulivyo ni huu ufuatao:

  Tatizo kubwa lililoko kwenye wimbo huo ni kule kutumiwa maandiko ya Biblia mahali pasipostahili. Ule wimbo ungefaa sana kama angeimba tu kuwashauri kwamba watu wasigombane lakini asiweke yale maneno ya ‘asema Bwana wa majeshi’ na ‘mlianza katika roho kwa nini mwataka kumalizia katika mwili’. Kama ungekuwa hivyo ujumbe wake ungefaa tu jamii nzima kwa kuwaasa waache ugomvi kwa sababu ugomvi una madhara mengi kwa jamii. Hapo ndipo ungefaa kutoa ujumbe wa kisiasa na kijamii.

  Kutumia maneno ‘..asema Bwana wa majeshi’ na ‘mlianza katika roho kwa nini mnataka kumalizia katika mwili’ hakuna uhusiano wowote na waislamu misikitini. Maneno haya ni maneno katika Biblia, ambacho ni kitabu cha kikristo. ‘Asema Bwana wa majeshi’ ni neno ambalo lilikuwa likitumika/hutumika ku-seal ujumbe utokao kwa Mungu Jehovah, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambaye ndiye Bwana wa Majeshi. Ni jambo ambalo halipo kwamba Bwana wa Majeshi, Mungu wa Yesu Kriso awapelekee ujumbe waislamu ili wasigombane misikitini. Hakuna misikiti wala uislamu kwenye Biblia. Kuwaonya waislamu halafu uka-seal kwa muhuri wa Bwana wa Majeshi ni mkanganyiko wa ajabu sana! Mkristo wa kweli anaelewa ninachomaanisha.

  ‘Mlianza katika roho sasa mnataka kumalizia katika mwili’ ni maneno yanayopatikana katika kitabu cha Waraka wa Mtume Paul kwa Wagalatia sura ile ya 3.

  Kwa kuwa umeomba ufafanuzi maneno yenyewe yanasomeka hivi katika Gal 3:1-6 hivi:

  “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nali aliyewaloga, niyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je, Mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je, mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. Basi yeye awapaye Roho na kufanya miujiza katikati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.”

  Nadhani hadi hapo utakuwa umeona jinsi maneno hayo yalivyo katika Biblia. Maneno hayo ni kwa watu ambao walikuwa wameipokea Injli na Roho mtakatifu aliyeahidiwa na Yesu Kristo. Lakini katika mwenendo wa ukristo wao ikafika mahali wakaanza kukengeuka. Ndipo mtume Paul aliwaandikia hayo kuwaonya na kuwafundisha!

  Sasa kuwaambia waislamu kwamba walianza katika Roho na sasa wanataka kukamilishwa katika mwili, ni kama kuwakashifu maana wao kwanza hawakubali kwamba Paul ni mtume na kisha hawaamini kama Yesu ni mwokozi wa ulimwengu. Kwa hiyo maneno hayo hayawahusu kwa namna yoyote ile. Maneno yanayowafaa waislamu, kutoka kwa mkristo kuhusiana na masuala ya Mungu ni kuwaambia wamwamini Bwana Yesu Kristo ili waokoke.

  Biblia haina fundisho lolote kwa waislamu bali ni mahubiri kwanza. Wakishaokoka ndipo wanaweza kutumia mafundisho hayo kutoka Galatia 3.

  Kwa taarifa yako, hata sasa ninapoandika haya ninasikia kwa mbali kuna mhadhara wa waisilamu wamefunga vipaza sauti na volume kubwa wanakashifu ukristo. Wanasoma Biblia halafu wanaanza kuyafanyia mzaha maneno waliyosoma.

  Mungu wa Mbinguni mwenye rehema na huruma, asiye mwepesi wa hasira, na awasaidie!

  2. Yale maneno ya wimbo niliyoandika niliandika kwamba ni baadhi ya maneno yaliyokuwa katika wimbo ule. Hata hivyo kama wimbo ungeendelea hadi mwishoni pengine ningeandika mengi kuliko hayo. Kwa vipi? Soma yafuatayo:

  Mimi ninaposikiliza wimbo huwa nasikiliza ujumbe kwa kuwa ndicho kilicho muhimu kwangu. Halafu nikiamua kufungulia redio au kuangalia TV ni kwamba huwa ni muda wa kufanya hivyo kwa hiyo nachukulia kama ni wakati muhimu ili niweze kupokea kilichokusudiwa kwangu kwa njia ya redio au ya TV. Huwa sisikilizi radio au kuangaalia TV wakati nime-concentrate kwenye jambo jingine. Hiyo ndiyo sababu huwa natamani niupate ujumbe wote ulioko kwenye wimbo kuanzia neno la kwanza hadi la mwisho ili nifanyie kazi kinachonihusu. Ndiyo maana nilifanikiwa kuyakariri maneno yale. Ni kawaida yangu. Nikisikiliza wimbo fulani ni lazima niyapate sawa sawa maneno yake.

  Kwamba kwa nini nilishindwa kujua jina nadhani labda hukusoma vizuri. Niliandika kwamba mwendesha kipindi hicho aliingilia na kuuondoa wimbo ule pasipo kutaja jina la muimbaji kisha akaruhusu wimbo mwingine ambao nao hakutaja jina lake. Wakati wimbo huo mwingine unaendelea nikazima redio na kuendelea na shughuli zingine. Si wakati wote waendesha vipindi hutaja majina ya waimbaji wa nyimbo. Kwa hiyo kilichonifanya nishindwe kumjua laiyeimba ni kwa sababu mwendesha kipindi hakutaja jina la muimbaji huyo. Kama lingetajwa ni lazima ningelijua.

  Natumaini nimeeleweka.

 40. Bwana Yesu asifiwe!!!

  Naomba kuuliza Hivi Dokii ameokoka??? nimeona baadhi ya kanda zake lakini sijabahatika kununua bado.

  Na je Flora mbasha ni mwanamuziki wa aina gani ?? Injli?? Siasa?? Jamii??

  Waimbaji wa Injili kama hawaeleweki vile!!!!!!!!! (hii ni kwangu mimi)

  Tunajifunza

 41. Ndugu Jonas Malimbo, mtu anaweza kufanya jambo na akajiona yupo sahihi kabisa, bila ya kumwambia moja kwa moja hataweza kujitambua kuwa kuna mahali kakosea na wapi anatakiwa kujirekebisha. Hujaweza kuweka mazingira ya angalao mwimbaji aweze kutambua kuwa ni yeye anayeambiwa ajirekebishe. Ingekuwa vyema sana angalao ungeongelea hasa ni maneno gani ambayo yalikufanya ukasema baadhi ya nyimbo za injili hazimtukuzi Mungu.

  Ndugu John Paul ametoa mfano wa wimbo ambao kwake yeye ameona kuwa haumtukuzi Mungu. Binafsi nimeshindwa kabisa kuelewa tatizo la maneno uliyoyaandika ndugu John Paul, ningependa kupata ufafanuzi zaidi. Halafu inakuwaje ukariri maneno yote hayo halafu ushindwe kumjua aliyeuimba?

 42. Asante wapendwa, ni kweli nakubaliana na nyi hasa wanaosema sio vizuri kuwajadili watu. Ni kweli tunapaswa kuombeana hasa watumishi tatizo wengi wa waimbaji sio wasomaji neno, waombaji, wala watu wa kusikiliza mahubiri au kutulia kwenye ibada kila jumapili. Unakuta wanahudhuria makanisa zaidi ya 2 hadi 3 siku ya jumapili kuimba, akimaliza anaondoka hasubiri neno, anahamia kwingine anakuta neno limeisha anaimba, hasubiri hata kufunga ibada kwa maombi anawahi sherehe ameitwa MC….
  Halafu kuna suala la hawa apromota sijui au meneja ndio kabisa wanawaharibu na unakuta wala hawana wokovu, ndio wanowachagulia style na nadhani hata mavazi, lengo kubwa likiwa ni mapato matokeo yake video unakuta vitu vya ajabu kabisa, nadhani kuna mmoja alikuja kumsema mwimbaji hapa SG kuwa ndiye alimfundisha taarabu, oh anamdai na mambo kama hayo. Ombi langu waimbaji msitumikishwe na mtu, mashabiki, wapambe kwa ajili ya hela au faida fanyeni kazi ya Mungu kwa kujituma, kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu, na hii itawezekana tu kama mtajibidiisha kusoma na kusikiliza Neno na kuliishi.
  Tunajifunza.

 43. Ameni kaka JOHN PAUL shingo ngumu ni tatizo kama mwanadamu hawezi kuonyeka na neno la mungu hakuna tunaloweza kumsaidia nalo,basi waimbaji mnaosoma hapa jamani shikeni maonyo na badilikeni tumwabudu Yesu kwa kuwa yeye ni wakuheshimiwa na kuogopwa,

 44. Asante Albert, hayo ni maoni yangu binafsi sio lazima mtu akubali ni mtazamo tu! siwezi kutaja majina lakini ujumbe umefika kwa njia moja au nyingine naamini utaeleweka kwa baadhi ya watu. Zipo nyimbo nyingi kweli ambazo haziuoneshi ukristo wetu kama wewe ni mfuatiliji wa nyimbo za Injili unaweza kufanya uchunguzi. Binafsi nabagua sana nyimbo za muziki wa Injili

  Ndugu John umesema kweli, kuna wimbo mwingine wa mchiriku unaitwa wakinamama kwakweli Mungu anisaidie.

 45. Dada Leva, ni sawa kabisa; maombi yanaweza kubadilisha hali hii. Na ninaamini tunaendelea kuomba hata kabla ya mada hii kuwekwa hapa.

  Lakini pamoja na kuwaombea mimi nadhani nao kama watumishi wa Mungu wana hatua ya kuchukua ili kuwezesha mabadiliko hayo. Maombi ya kumuombea mtumishi yana ukomo wake. Hufanya kazi tu kama mtumishi mwenyewe anachukia na kujuta kwa tatizo alilonalo. Kuchukuia, kujuta, kutaka kuacha pamoja na maombi ya wanaomuombea ndivyo husababisha mabadiliko yatokee. Kuna wakati maombi hayawezi kusaidia kwa sababu ya kiburi, ukaidi na ugumu wa shingo ya anayeombewa. Ndivyo ilivyokuwa kwa Samwel alipoambiwa kwamba asiendelee kumuombea Sauli kwa maana Mungu ameshamkataa. [1Sam 15:24 – 16:1]

  Kwa hiyo, waimbaji kama watumishi, hawatakiwi kuwa vipofu bali wanatakiwa kuwa macho ili waweze kutathmini utumishi wao unavyoendelea. Isije ikafika mahali pa kukataliwa na Mungu. Mbaya sana!

  Kwa kuandika haya sina maana kwamba waimbaji wote wa injili wanaangukia kwenye kundi hilo alilolitaja ndugu Jonas Malimbo, hapana! Wapo ambao wanatambua na kuuheshimu wito wao na wanatumika kwenye eneo la uimbaji kwa kuongozwa na Mungu. Ninawaombea Mungu wa mbinguni azidi kuwapigania katika utumishi wao!

  Lakini kusema ukweli huduma ya uimbaji wa muziki wa injili kwa ujumla limekumbwa na matatizo mengi sana. Waimbaji wengi wanaimba tu ili kupata pesa. Hawajali ujumbe uliopo kwenye wimbo wala ubalozi wao kama wawakilishi wa kristo katika mwenendo wao wa maisha ya kila siku na wawapo kwenye uimbaji.

  Sidhani kama ni lazima kumnyooshea mkono muimbaji fulani ndipo mtu aamini kuwa kweli kuna tatizo kwenye uimbaji wa nyimbo za injili. Mtu anayetambua thamani ya uimbaji wa injili na miiko yake atakuwa ameelewa ninachokizungumzia na kinachozungumziwa na wachangiaji wengine katika mada hii.

  Lakini kuna mfano mmoja nalazimika kuutoa kuhusiana na kile nilichoeleza kwamba waimbaji wengi sasa hawajali ujumbe uliopo kwenye wimbo bali wanachojali watu watanunua nyimbo zao, wapate pesa, basi! Mfano wenyewe ni wimbo ambao nimeusikia kwenye radio moja ya kikristo. Ninakumbuka baadhi ya maneno yaliyokuwa katika wimbo huu, ambayo ni haya yafuatao:

  ‘Kwa nini mnagombana. Kwa nini mnatafunana na kumalizana. Kwa nini mnaumana. Tumechoshwa na kugombana kwenu.Tumechoshwa na migogoro.’

  halafu wimbo ukaendelea…..

  ‘Baada ya kuanza katika, roho kwa nini mnataka kumalizia katika mwili?

  Msigombane ee asema Bwana wa majeshi,
  Makanisani na misikitini msigombane, asema Bwana wa majeshi
  Wachungaji na washirika wenu msigombane, asema Bwana wa majeshi,
  Masheikh na maimamu na washirika wenu misikitini, msigombane, asema Bwana wa majeshi…’

  Wimbo ulipofika hapo mwendeshaji wa kipindi akaingilia na kusema kwamba tunaonywa na waimbaji tusigombane halafu akau-fade ule wimbo na akasema ‘tunaendelea kupata ujumbe kwa nyimbo kutoka waimbaji wengine hawa wanaofuata’, halafu akaruhusu wimbo mwingine hewani.

  Baada ya kusikia maneno ya wimbo huo nilichoka kabisa! Tangu lini waislamu walianza kwa roho halafu wanataka kumalizia katika mwili? Je,Je,je,je, ni nyingi mno katika ujumbe wa wimbo huo. Ingawa sikuusikia unavyoishia lakini hadi hapo tayari ilishadhirika wazi kwamba huo wimbo haufai kuitwa ni wimbo wa injili, labda kama ni wimbo wa siasa!

  Bahati mbaya hawakutaja jina la aliyeimba wimbo huo, lakini hata hivyo nisingeliweka hapa bali ningewasiliana naye moja kwa moja!

  Jamani waimbaji wa nyimbo za Injili ni vema tusome sana Biblia na tujifunza neno la Mungu ili hata mtu ukitunga wimbo uwe uko sawa na Neno.

  Wacha tu niishie hapa kwa sasa…!

 46. Watakuwa watakatifu tukikazana kuwaombea watabadilishwa ,tufunge tuombe kwa ajili ya waimbaji wetu,tunawapenda ila tutaondoa tatizo kwa kuomba na kuamuru roho za uharibifu zinazoharibu maana ya nyimbo ziwatoke tuanze kuomba wapendwa.

 47. Bwana Jonas Malimbo, hebu tupe mifano ya Nyimbo za injili ambazo unauhakika kuwa hazimtukuzi Mungu. Kutoka kwenye mifano halisi ya njimbo hizo, kama tumeshapata kuzishuhudia au kama bado tutajitahidi tuzione na kisha tutazijadili ili tupate kuwa na uhakika wa ulicho kiandika na ili mimi binafsi nikubaliane na ulichokiandika. Kinyume na hapo, sikubaliani nawe na wala sipingani nawe.
  Nashukuru.

 48. Bwana Yesu asifiwe Jonas, ni kweli kabisa, siku moja nilipokuwa nikitazama njimbo za injili kwenye TV, nilipigwa na butwaa, baada ya kuona wimbo mmoja waimbaji wamevaa suruali za kubana na hata cheza yao kwakweli haiko kabisa kwenye utukufu wa Mungu, mpaka nikafikiri kuwa labda ni mawakala wa shetani, sasa ninasema heshima kwa Mungu wetu tunaye muabudu na kumuogopa iko wapi? INAUMIZA SANA KWAKWELI ENYI WATU WA MUNGU, NAFIKIRI watakuwa hawana Roho mtakatifu anaye waongoza.

 49. Bwana Jonas hujakosea, maoni yako ni sawa kabisa. Tatizo kubwa liko kwa Wachungaji na walezi wa kwaya. Hawakemei mambo hayo. Utakuta kwaya ina viongozi ambao wana uwezo kidogo wa fedha wa kununua vyombo na vitu vingine vya Kanisani, wanapoanza kuingiza mambo yao Mchungaji anakuwa hakemei hali hiyo. Vilevile wanakwaya wengi vipindi vya neno, shule ya jumapili na mafundisho ya biblia hawatilii maanani, Wachungaji wengine hilo hawajali.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s