YESU ANAKUPENDA

Hapo mwanzo alikuwepo ROHO MTAKATIFU hata kabla ya uumbaji! Siku Mungu anaiumba dunia alitamka kwa NENO lake kila kitu kikatokea, Aliposema na iwe jua nalo likawa, Wawepo Samaki Watawale  bahari vyote vikawa!! Mwanzo 1:1-31

Kwa vile Mungu yupo pamoja nawe anaishi ndani yako. Usiogope maana tangu mwanzo hujazaliwa Mungu alikujua, roho yako ilikuwepo hata kabla ya mwili, Hivyo Basi, Roho yako iambatanishe na ROHO wa Mungu! uwe connected kwake ili afanye  njia kwako uwe halisi kwa hali ya mwilini kama Mungu alivyokukusudia. “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.’’ Yeremia 1:5

Ndugu, Bwana Yesu Hawezi Kukuacha, ANAKUPENDA kwa KINYWA chako umba baraka palipo na laana, amani pasipokuwa na amani uzima palipona ugonjwa shwari palipo na dhoruba.Utaona matokeo mazuri katika maisha yako.

Hauko Peke Yako, Mungu Yu Pamoja Nawe!

Advertisements

5 thoughts on “YESU ANAKUPENDA

 1. Mbarikiwe sana nashukuru ujumbe huu umekuja kwa ajili yangu kabisa kutokana na yale ninayoyapitia kwa sasa nashukuru kukumbuswa huwa Bwana hajaniacha yuko nami.

 2. Napenda kuwashukuru wote kwa kunitumia ujumbe kama huu ambo unatutia moyo kweli naamini Mungu anatupenda na hatotuachcha kamwe tukimwita kwa jina lake. jamani Mungu awabariki sana kwa mana mnafanya Kazi ya Kutuombea wengine na Mungu azidi kuwazidishia zaidi na zaidi. Bwana Yesu apewe sifa.

 3. Bwana asifiwe napenda kumshukuru mungu kwa jinsi anavyo tupigania tena napenda kuwatia moyo wale wote ambao wanajitoa kwa moyo wao wote kuomba usiku na mchana kwa ajili ya wngine mungu awabariki sana na awapiganie awafanyie njia hata pasipo na njia kadri wanavyoombea wengine mungu naye akapambane na magumu yao yakawe marahisi pia azidi kuwatia nguvu na uhodari ili kazi ya mungu isonge mbele.
  Rose

 4. Asante Kwa Ujumbe! kuwa Yesu Anatupenda!

  Naamini kila Mkristo inabidi akumbushwe kwa kwa hilo!

  Kwa baadhi yetu hasa tunapokuwa tukiendelea katika mapito ya Imani hii, huu Upendo we Yesu unaanza kupimwa kwa vile anavyotupatia, vya mwili na hata Rohoni pia,! Ni kweli Neno la Mungu limesema Bwana atatutendea na kutupatia hayo, pengine tumemwomba afya ya mwili, akatupatia! mahitaji, kwa wengine nyumba, magari, biashara, kazi nk vyote vikawa upande wetu! Lakini Upendo wa Yesu ni zaidi ya haya!

  Kwani hata wasiomwamini wengi wao wana hayo!Nyumba nzuri, biashara, kazi nk Kwa hiyo tunaona Bwana ni mtoaji tu kwa mwanadamu! Kipimo chetu cha kuuona uwepo wa Mungu kwetu ( upendo wa Yesu) lazima uwe ni wa tofauti kabisa na wale ambayo hawajaonja uzuri wa KALVARY!

  Kwa wale waliouonja upendo wa calvary kwahakika wanaweza kusema hakika kama Paulo “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo” Kwani Paulo aliweza kusema hakika katika “dhiki” ameuona upendo wa Kristo! katika “adha”ameuona upendo wa Kristo! Katika “uchi”ameuona upendo wa Kristo!

  Hivyo Mungu na atufunulie kuujua upendo huo! Tufike mahali tukaauone upendo huo si kwa magari tunayoendesha! Si kwa nyumba tulizojenga! Si kwa mume mzuri au mke mzuri niliyenaye! Si kwa paspoti iliyogongwa visa na kuwa na kibali cha kutembelea nchi mbali mbali! Si kwa mishahara mikubwa! wengine ni dola! Uero! Pound nk! Tukitumia vigezo tutakuwa tumeshindwa kuutambua upendo huo mkuu!

  Nashukuru kuwa YESU ananipenda! Amenihakikishia maisha ya milele! na si kwa sababu nimetenda mema! La hasha! Si kwa sababu nilikuwa nimemtafuta sana! LA HASHA! Aliyafungua macho yangu ya kujiona mimi ni mwenye dhambi! Na kwamba nastahili hukumu ya milele ambayo ni hakika! Na kwa kunipa uwezo wa kumwamini Yeye na kazi yake msalabani Hukumu hiyo ikafutwa! Huwa nashangaa kuwa mbele za Mungu sina mashtaka! Hofu baada ya kufa imeondoka! Siogopi napotembea kwa miguu kuwa ajali ikinikuta je! Siogopi napoendesha gari, na kila napoingia ndani ya gari au ndege huwa nafikiri pengine hii ndio safari yangu ya mwisho duniani! Hofu huwa kwa mke na watoto tu! lakini huwa naamini pia hata kama Bwana ataamua kunichukua kwa njia hii basi atawalinda wao pia! kwani itakuwa imempendeza! Kwani siku zangu ziliandikwa katika kiganja cha mikono yake! hata kama niiishi miaka 50,60, 90! Lipi jipya duniani! Lipi linaweza kunifurahisha ulimwenguni? Paulo akayaona yote kama “uchafu” kwa uzuri usio na kiasi kwa kumjua Kristo Yesu! Nasi Tuombe hivyo! Nyumba zetu nzuri ziwe mavi! mbele ya uzuri wake! magari yetu, flat screen za TV nusu ukuta! Nisipende hata kuziona ni BARAKA! ZISIJE ZIKANIPOFUSHA MACHO KUUONA UPENDO WA YESU! UBARIKIWE KWA UJUMBE HUU, UMEFANYA SIKU YANGU KUWA NJEMA.!

 5. BWANA Yesu asifiwe nina shukuru sana watu wa Mungu kwa kuungana nami ktkt shida iliyokuwa inanipashida nilikuwa na subuliwa na mgongo kwa kweli nishukuru kwa kuungana nami ktkt maombi yenu Mungu wa mbinguni awabariki nimepokea uzima ss hv hata maji nabeba namrudishia Mungu utukufu amina milele

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s