Nini tofauti kati ya KANISA na DHEHEBU

Je! Kuna waKristo wasio katika dhehebu lolote ama ni lazima kila mKristo awe katika dhehebu? Na kama wote wapo kasoro hao, hilo nalo si “dhehebu la wasio na dhehebu”? Kama sote tu-waKristo, twamwamini Mungu mmoja na tunatakiwa kuendesha ibada kwa mujibu wa Biblia (ambayo naamini inastahili kuwa moja)

(i):   Kwanini kuwepo tofauti ya uendeshaji ibada kwa kunukuu biblia moja?
(ii):  Kwanini baadhi ya madhehebu yaseme uendeshaji ibada wa wengine si wa Kikritso?
(iii): Ni kweli kuwa kuna baadhi ya madhehebu yanayomcha Mungu zaidi ya mengine?
 
Katika kutangaza Neno la Mungu ulimwenguni kote, baadhi ya madhehebu yametumia njia za kisasa kuwafikia watu ulimwenguni
(i): Je ni sahihi kwa madhehebu kubadilika kulingana na sayansi na teknolojia katika kuhubiri?
(ii): Ni kweli kuwa kuendana na mahitaji ya kuwafikia waKristo pote ulimwenguni, kanisa / dhehebu linastahili kubadili mtindo ama mfumo wa ibada kuwapata watu walio katika tamaduni nyingine (mfano nyimbo)?

Natanguliza shukrani

–Mubelwa T. Bandio–

Advertisements

11 thoughts on “Nini tofauti kati ya KANISA na DHEHEBU

 1. Namshukuru Mungu sana kwa sababu anatuwezesha kuwasiliana jinsi hii kwa mtandao huu.Ni vyema sana mtu kumheshimu Mungu kwa roho yake yote ili apokee uwezo wa kuamini kila kazi aifanyayo Mungu.Kwa mfano Mungu amefanya kazi ya uumbaji na kuna wale wanoiheshimu na wasioiheshimu.Neno lasema mtu atakaye kumwendea Mungu lazima aamini kwanza ya kwamba huyo Mungu yuko.Mungu huyo ni nani? Ni Yesu kristo aliyekuja katika mwili mfano wa mwanadamu (wafilipi 2:5-11),isaya7:14, isaya 9:6-7 1tim 3:16 n.k).Ikiwa ni vigumu kwa yeyote kuamini kuwa Yesu ndiye Mungu basi itakuwa vigumu kumfuata kwa sababu achukuliwa kama mwanadamu tu,hata wengine wamesema wanaanzisha makundi yao kwa mfano walile la Yesu na matokeo ni, wengi ambao wanataka kumwamini kristo wamepotezwa bila kufahamu.lakini nasema Yesu analo kanisa lake binafsi(mathew 16:18) nalo tangu mwanzo wake linadumisha imani moja,ubatizo mmoja, roho mmoja,Mungu mmoja (efeso 4:5-6) mafundisho na matendo hayabadilishwi kwa mfano wa mitindo ya maisha maana Bwana ni yeye yule jana, leo na hata milele.Ikiwa sisi tunajengwa katika msingi uliowekwa na mitume na manabii (efeso 2:19-22) basi yatupasa kuhubiri na kutenda kama wao maana wao ndio wanaotuhubiria sisi kupitia hayo maandiko(yuda1:3-4).Kanisa hilo linaenea tangu jerusalem hata mwisho wa nchi (matendo 1:8) na liko hai hata milele maana alisema halitashindwa na milango ya kuzimu(mathew 16:18).hata nami nimejaliwa kulifikia na kuzaliwa ndani kama inenavyo biblia katika waebrania 12:22-26. matendo 2:36-42, na msitari wa 47 unasema bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.maana yake ni kwamba kanisa haliongezeki kwa watu kujiunga bali kwa kuamini,kutubu,kubatizwa(kwa maji na kwa roho) kwa jina lake yesu kristo ili kupata msamaha wa dhambi na kupokea kipawa cha roho mtakatifu.(matendo 8:14-17, 26-39, matendo 10:44-48 n.k).kundi lingine lolote au dhehebu lolote haliwezi kumfanyia kristo kazi hizi au kumwokolea kristo watu maana yeye Yesu asema hayatambui hayo wala wanofanya kazi humo, (mathew 7.21-23 (7:13-28).hii ni kwa sababu kila kundi limejiwekea utaratibu wao , mafundisho yao matendo yao na hata katiba zao kama dunia kando na biblia na wanafuata hayo huku hawafahamu kuwa wanamtia wivu Yesu kristo aliyetupatia biblia na utaratibu wake.kwa hivyo makundi hayo ambayo yamejiwekea utaratibu wao na kuacha wote au kwa sehemu ule ulioanzishwa na Bwana ndio madhehebu hiyo mormons ikiwa ndani mengine ni kama katoliki,full gospel, lutheran, redeemed,pentecostal assemblies na kadhalika.lakini hayatalishinda kanisa la BWANA YESU.

  Barikiweni sana.

 2. Ndugu Hagai,Mwenda na wachangia mada wengine,

  Kanisa kwa lugha rahisi ni kwa wale waliokusanyika au “waliioitwa” kwa ajili ya Bwana, lakini hata watu ambao hawajaitwa na Bwana huwezi kujiingiza katika kundi la walioitwa na Bwana!Ambao Bwana mwenyewe atawachuja atakapokuja chukua walio wake,”VIACHENI VYOTE VIKUE HATA WAKATI WA MAVUNO, NA WAKATI WA MAVUNO NITAWAAMBIA WAVUNAO YAKUSANYENI KWANZA MAGUGU……MYACHOME…..BALI NGANO IKUSANYENI GHALANI MWANGU!” (Mathew 13: 24-43)
  Hivyo basi KANISA lililoko ulimwenguni huwa nyakati zote limechanganya walioamini na wale wasioamini!

  Kwa kifupi kanisa linaweza kuelezwa ifuatavyo,

  – Muunganiko wa waamini kuwa mwili mmoja katika Kristo (1Cor 12: 12-14)

  – Muunganiko na Kristo kwa kuondoa kiambaza cha (dhambi) kilichotutenga (Ephesians 2:19-22)Sisi ni jamii moja na watakatifu walioko mbinguni!

  – Muunganiko katika kifungo cha Roho Mtakatifu (Ephe 4:1-6)

  Kwa kifupi KANISA hilo ndio ule mkutano mkubwa unaoelezwa katika kitabu cha ufunuo (Ufunuo7: 9-12)ambao hakuna mtu awezae kuuhesabu!”watu wa kila taifa” na “kabila” na “jamaa” na “lugha” na “wamevikwa mavazi meupe” na wakisema kwa sauti kuu “WOKOVU UNA MUNGU WETU AKETIE KATIKA KITI CHA ENZI NA MWANAKONDOO”

  Kwa kuyajua hayo sasa unaweza kujiuliza Dhehebu ni nini” Kwanza kabisa kusanyiko linaoitwa na Mungu ni Kanisa la Mungu, Mungu hana kitu kinachoitwa “Dhehebu” lakini dhehebu kwa macho ya kibinadamu linaweza kabisa mbele za Mungu kuwa ni Kanisa! Yaani kusanyiko la watu waliopokea wokovu,kwani Dhehebu huwa ni tawi la Kanisa! yaani mkusanyiko wa Watu wa Mungu! Mkusanyiko wa watu wa Mungu duniani umeitwa ni kanisa! lakini w3amejitenga katika makundi mbali mbali “madhehebu” kutokana na “convictions” zao mbali mbali ambazo wameona ni sahihikabisa katika kusanyiko lao “KANISA” katika kumfuata Kristo!

  Kwa kifupi madhehebu yaani Wakristo wenye “convictions” tofauti na zile za mitume walijitokeza katika kanisa la Kwanza! Hebu angalia nukuu hii:

  ” Lakini baadhi ya MADHEHEBU ya MAFARISAYO WALIOAMINI wakasimama wakisema ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika ile torati ya Musa!” (ACT 15:1-5)

  Hawa ni Wayahudi waliomwamini Yesu! Walipokea Wokovu! lakini walisisitiza kuzifuata taratibu za sheria za Musa, kwa kifupi kwao ni Wokovu + Sheria za Musa= kukubaliwa na Mungu!

  Kwa kifupi watu hawa ingawa waliaamini na kuokoka lakini “walipotosha” kweli ya Injili! Act 15:24-29)

  Hivyo ndivo yalivyo “Madhehebu” si kwamba yanapotosha la hasha! Msisitizo wake wa mafundisho unaweza ukawa unapotosha au unasimama katika kweli ya Injili!Na tofauti za madhehebu na madhehebu zinaweza kuanzia kwenye vitu vidogo vidogo na hata kufikia vitu vikubwa vya kitheolojia! Wengine wanaweza kusema hakuna Wokovu duniani! mtu anaokoka Mbinguni! na wakaja na nukuu zao katika Biblia! Wengine wanaweza kusema ubatizo ni kwa Mtu aliyeaamini wengine wakasema la! Kwani hata mtoto pia naweza akabatizwa! Wengine wanaweza wakasema Ishara ya mtu aliyeokoka ni lazima anene kwa Lugha! wengine wanabisha na kusema la! hiyo ni mojawapo ya Ishara tu1 inaweza kutokea na isitokee! Wengine wanaweza kusema kanisa litakuwepo wakati wa dhiki kuu! wengine wakasisitiza la! kanisa litakuwa limetwaliwa!Wengine wanasema wokovu na kwa watu waioteuliwa toka misingi ya ulimwengu! na HAWAWEZI kuupoteza wokovu! wengine wanasema la! Hivyo madhehebu ni ukweli usiokimbilika!

  Lakini pia Madhehebu yanaweza kabisa kuzaliwa kwa baadhi ya watu katika kundi la wakristo kuanza kufundisha “MAPOTOFU” hebu angalia nukuu hii;

  “NAJUA BAADA YA KUONDOKA KWANGU MBWA MWITU WAKALI WATAINGIA KWENU WASILIHURUMIE KUNDI (KANISA,) TENA KATIKA NINYI WENYEWE ( YAANI KATIKA KANISA) WATAINUKA WATU WAKISEMA MAPOTOVU WAWAVUTE HAO WANAFUNZI WAANDAME WAO……HIVYO KESHENI! (ACT 20: 28- 31)

  Historia ya Ukristo imeonyesha jinsi Bwana alivyoyatumia “madhehebu” mbali mbali kuwa chachu ya kufundisha Kweli ya Mungu, wakati kweli hiyo iliposahaulika! na kuleta uamsho ulimwenguni! Tumeona kazi za akina Martin Luther, John na Charles Wesley,George Whitefield,William na Catherine Booth na wengineo, na pia uamsho wa kipentekoste uliotokea Azusa Street mwanzoni mwa Karne hii.

  Lakini pia tumeona mfumuko wa “madhehebu” mbali mbali ambayo kwa vipimo vya neno la Mungu wamekuwa chachu mbaya ya kuwavuta mbali na Kristo, madhehebu kama Mormons nk!

 3. Wapendwa wote,
  Nawashukuru kwa maelezo yenu ambayo yote ni mazuri sana. Kama alivyosema Orbi hapo juu kuwa Ekklesia ni kusanyiko ama wanaomfuata Mungu au kusanyiko lolote lile. Ni sawa na kingereza ukisema ‘Assembly’ bila kunyumbulisha kuwa ni assembly of what, itabaki kuwa ni kusanyiko tu lililobeba watu wa aina mbalimbali na wenye malengo tofauti tofauti.
  Lakini biblia iko wazi kabisa kuhusu kanisa ambalo Yesu aliliita ni bibi harusi na Yeye ni bwana harusi. Hapo ndipo ninapokuja kwenye mantiki ya ndg Mwenda kwamba kama mtu hajampokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yake, kwamba huyu hajawa bibi harusi wa bwana Yesu, hivyo watu wa namna hiyo wanapokutanika sidhani kama ni sahihi kuwaita kanisa kwa maana ya mabibi harusi wa Yesu.
  Alilosema Mwenda kwamba ili kanisa liitwe kanisa wokovu ni hatua ya kwanza kabisa.
  Baraka kwenu nyote.

 4. Ndugu Mwenda,

  Naona maelezo yako yanatakiwa ufafanunuzi, nikianza na nukuu hii;

  “Dhehebu ambalo limepata neema ya kuwa katika kweli yote, na lile ambao ni vuguvugu wote ni kanisa, Ufunuo 3:14-16.”

  Na pia nukuu hii:

  “Wale ambao hawapo katika Kristo, yaani wasioamini kuwa Yesu ni mwokozi wao na wakakubali kuokolewa, hao siyo kanisa; hao ni dhehebu lililo katika jitihada tu za kumtafuta Mungu.”

  Kwa kifupi tu na wengi wameeleza kuwa manaa ya “KANISA” au “EKKLESIA” kwa Kigiriki ikiwa na maana moja tu “Kusanyiko” Liwe kusanyiko lolote lile! Kama ukisoma kwa Kigiriki cha wa wakati huo neno hilo “EKKLESIA” yaani kusanyiko au “assembly” limetumika pia hata kwa makusanyiko mengine yasio kabisa na uhusiano na Wakristo au hata watu wa Mungu! Kama wale waliomshambulia Paulo kule Efeso au Philipi.

  Lakini inapokuja kwa Wakristo kanisa linakuwa ni kusanyiko la Watu wa Mungu! ambao wanatakiwa wawe wamemwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wao! Hivyo hata kama Yesu hajaaminiwa kama Bwana na Mwokozi wao, bado sifa au jina la kuwa KANISA AU KWA MAANA YA KUSANYIKO INAKUWA HAIJAPOTEA! NI KUSANYIKO LISILO HAI! LIMEKUFA, Na ndio maana Yohana katika ufunuo anasema unajina la kuwa HAI LAKINI UMEKUFA!

 5. wote waliotoa maoni nawapongeza kwa jitihada kubwa ya kutufundisha na sisi wengine.
  Asante

 6. Wana wa Mungu.

  Kwa kifupi, tofauti kati ya kanisa na dhehebu, ni kwamba, Kanisa ni kusanyiko la watu wooote wanaomwamini Yesu na ambao wamempokea kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao. Kusanyiko hilo kwa pamoja tunaliita kanisa.

  Dhahebu au madhehebu ni makundi mbalimbali ya watu ambao wapo kwa pamoja katika harakati za kumtafuta Mungu. Madhehebu hayo yanaweza kuwa katika kweli yote ya Neno la Mungu, mengine yakawa vuguvugu na mengine yanaweza kuwa nje kabisa ya Neno la Mungu.

  Dhehebu ambalo limepata neema ya kuwa katika kweli yote, na lile ambao ni vuguvugu wote ni kanisa, Ufunuo 3:14-16.

  Wale ambao hawapo katika Kristo, yaani wasioamini kuwa Yesu ni mwokozi wao na wakakubali kuokolewa, hao siyo kanisa; hao ni dhehebu lililo katika jitihada tu za kumtafuta Mungu.

  Ili mwanadamu awe miongoni mwa wanaokuwa katika kanisa, wokovu ni hatua ya mwanzo ya kumfanya kuwa kanisa; bila wokovu hawezi kuwa kanisa. Ndiyo maana pia, hata katika kanisa kuna walio vuguvugu na walio moto, kudhihirisha kuwa wokovu kwanza ni lazima.

  Kanisa ni halisi, na siyo nadharia.

  Nawapenda wote!

 7. Thanks Bandio,
  Lazima Watu wafundishwe kuwa Wakristo na Sio Walokole wama Wanadini.

  Nachukia Udini kupita maelezo, Kizazi chetu lazima Kisimame kitoke kwenye Kongwa waliloishi wazazi wetu. Dini inaleta ubaguzi, dini zinaleta magomvi, dini zinaleta issue kibao, huwezi hudumu eti sio dini yetu, huwezi kuoa eti dini yetu, huwezi fanya chochote.

  Biblia inasema Mwana waadamu atakpokuja ataikuta imani?which faith was he talking about?hahaha follow mu steps on http://www.samsasali.blogspot.com

 8. Ukisoma biblia Yesu alimwambi Petro….“Juu Ya Mwamba huu nitalijenga Kanisa Langu Wala Malango Ya Kuzima hayatalishinda”. Fuatana nami kati tofauti hizi.

  1. Uanzilishi Wake.
  Kanisa linaanzishwa na Yesu mwenyewe Mwenyewe na ndiye anaeleza, “Nami nitalijenga” it means up to that time Establishment ya “Kanisa” la maana ya Yesu lilikuwa halija exist ila madhehebu yalikuwepo. Madhehebu yote yana waanzilishi, hata lile la shetani lina mwanzilishi wake, hata hilo unalosali lina mwanzilishi, but content ya Kanisa! Kristo ndiye mwanzilishi.

  2. Ukubwa/Mtawanyiko/Spread
  Kanisa la Yesu lipo ulimwenguni mwote hata ambako hakuna madhehebu, kanisa la Kristo ambalo atakuja kulitwaa limeenea kote duniani. Madhehebu mengi sana yameenea mijini, na kuna madhehebu lipo sehemu moja tu duniani lakini sio Kanisa la Kristo Yesu hili lipo duniani kote.

  3. Ofisi za Usajiri
  Kanisa la Kristo lilifanyiwa usajiri wake pale Carvary na Makao yake Makuu yako mbinguni katika ulimwengu wa Roho, ndio maana Yesu anasema wala Malango Ya Kuzima hayatalishinda kwa maana ya “Spiritual Battle” Ofisi Kuu yaani mbinguni watakuwa tayari kuleta msaada. Madhehebu yote wamesajiriwa Wizara ya Mambo ya Ndani na Makao Makuu yake ni hapa hapa duniani.

  4. Gharama za Usajiri
  Gharama ya usajiri wa Kanisa la Kristo ni Damu ya Mwanakondoo aliyoimwaga pale msalabani, maana hakuna ondoleo la dhambi isipokuwa Damu ya Yesu Kristo. Madhehebu yote yamelipa ada ya Usajiri Serikali kwa ajili ya kuwepo kwake.

  5. Ukamilifua (Perfections)
  Kanisa la Kristo halina mapungufu na linakamilishwa na na Yesu Mwenyewe,maana Kanisa atakalolitwaa halina doa wala waa, madhehebu yote yana mapungufu kwa kuwa yanaongozwa na wanadamu na hakuna mwanadamu asiye kamili. Ndio sababu wapo watu wengi wanaohama kutoka dhehebu moja tu.

  More other points visit. http://www.samsasali.blogspot.com

 9. Kanisa La Kristo Sio Dhehebu – Toleo la 1

  Fedha tunazotumia zimegawanyika katika aina tofauti, 10,000/-, 5,000/-. Na taratibu za siasa zimegawanyika, CCM, TLP. Kwa hiyo tunaona kupitia mifano kwamba neno “dhehebu” ni magawanyiko au kundi fulani. Katika ulimwengu wa dini, “Dhehebu” ni jamii ya watu waliotengana na Kanisa lilianzishwa na Kristo. Ndiyo katika Agano Jipya Biblia inazugumza kuhusu makusanyiko (1 Kor. 1:2) au Kanisa zima (Efe. 1:22-23). Lakini wale watu kwenye makusanyiko walikuwa Wakristo katika Kanisa la Kristo. Hawakuwa Walutheri katika Kanisa la Moravian.
  I. Kanisa La Kristo Ndilo Kanisa la Karne ya Kwanza.
  A. Tuangalie yaliyo kweli.

  1. Kanisa la Kristo siyo Kanisa la Wayahudi.
  a. Agano la Kale, msingi wa Wayahudi ulitolewa, Rum. 7:1-4; Kol. 2:14-17; Ebr. 8:8-13.

  2. Kanisa la Kristo siyo “Protestant” kundi la watu waliochukia na mafundisho ya Katoliki kwa hiyo wakaacha kusali na wakaanzishwa makanisa yao.
  a. Madhehebu yote yalianzishwa baada ya karne ya kwanza na kama kuna kundi la watu walianzisha bada ya karne la kwanza na wanadamu, basi hawa watu hawawezi kuwa Kanisa lililojengwa na Kristo.
  b. Kanisa la Bwana wetu alilianzisha katika karne ya kwanza mwaka wa 33, Marko. 9:1; Mdo. 1:8; Mdo. 2:1-4, 47.

  3. Vitendo vya madhehebu havimo katika Kanisa.
  a. Madhabahu ya maombi.
  b. Kupiga kura kwa watu wanaotaka kujiunga.
  c. Vyombo vya muziki.

  4. Kanisa la Kristo sio Kanisa la Katoliki.
  a. Kanisa la Katoliki lilianzishwa katika mwaka wa 606 Bk, karibu na miaka 600 baada ya maisha ya Yesu.
  b. Na tukiangalia mafundisho ya Wakatoliki tutaona kwa ufupi hawapati mamlaka yao kutoka kwa Mungu.

  II. Fafanuzi ya Kanisa.
  A. Neno “Kanisa” limetoka kwenye neno ya Kiyunani “Ecclesia,” na maana yake ni “Walioitwa”.
  1. Kwa hiyo Kanisa ni mwili wa watu walioitwa kutoka ulimwenguni, 2 Thes. 2:14.
  a. Kwa kutii injili, 2 Thes. 1:7-9.
  2. Kanisa linaongozwa na Kristo, kichwa cha Kanisa lake, Kol. 1:18.
  3. Na Roho anakaa ndani ya Kanisa, Efe. 2:22-23.

  B. Kanisa ni moja katika hesabu.
  1. Yn. 10:16, Kuna kundi ngapi?________
  2. Na Kanisa ndiyo kundi lile, Mdo. 20:28.
  3. Tena kuna mwili moja, Efe. 4:4.
  4. Na mwili ni Kanisa, Efe. 1:22-23.
  5. Tunajua Yesu alifundisha kuhusu ndoa tunaweza kuwa na mke moja tu, Mat. 19:1-9; Rum. 7:1-4.
  6. Na Kanisa ni mke wa Yesu, Efe. 5:22-23.

  Hitimisho:
  Tutaendela kujifunza kuna Kanisa moja tu. Wazo la Kanisa moja naona tumeelewa. Lakini labda tumeelewa kwa maneno na siyo kwa matendo kwa sababu mara nyingi watu wanaanguka na wanajiunga na madhebu. Kwa maana hawakuelewa vizuri mafundisho ya Kristo ndiyo maana wanapotea.

  Somo hili na mengine, ni kutoka http://www.kanisalakristo.com

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s