Kuamsha Upya Uhusiano Wako Binafsi na Mungu

Mwanzoni mwa wokovu wako ulikuwa na hamu na kutamani sana kuwa na Mwokozi wako, ulikuwa kila ukipata muda unapitia kanisani au la unaingia chumbani uongee nae na kumwabudu na kumsifu. Kinywa chako kilijaa sifa, sifa za Mwokozi huyu aliyekutoa kule katika shimo la upotevu! aliyekupenda bila kuangalia mapungufu yako, ulimpenda nawe na kujitoa kwake kabisa na kumpa ahadi ya kuwa naye ukimtumikia milele.

Lakini sasa ni kinyume, taratibu umekuwa busy sana na kazi, familia, shule, miradi, ndugu, sherehe etc… “yaani mambo yamekuwa mengi sana sana na Mungu akusamehe kwani Yeye mwenyewe anaona….” Ghafla kinywa chako kimejaa maombi, mahitaji, shida, ni shida unampelekea huyu Mungu akusaidie!… inaonekana kama haziishi zinaongezeka kila siku… kila jumapili (ambayo ndio walau unapata muda wa kuwa karibu na Mungu) unakuja na shida mpya: unaumwa hapa, unataka kazi nzuri zaidi, unataka mwenza mzuri, nyumba kubwa, watoto… ila bado hatimizi kwa wakati wako…

Mzee Yakobo katika waraka wake: (Yakobo 4:5-10) anasema:

5 Au mwadhani kwamba maandiko yanasema bure kuwa, huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6Lakini Yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko husema: ‘‘Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema’’

7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili. 9Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuombeleza na furaha yenu kuwa huzuni. 10Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua. Ndugu zangu ni wakati wa kurudisha upya mahusiano yetu binafsi na Mungu, tumeambiwa:

1. Tukimkaribia nae atatukaribia, turudishe upendo, shauku na ukaribu kwa Mungu wetu kwa kutumia muda zaidi kadri tuwezavyo kumsifu, kumwabudu na kumtukuza

2. Tunapaswa kumtii Mungu, tuliokolewa kwa neema hivyo tunapaswa kumtii na kutenda yaliyo mapenzi yake, maana hatukustahili isipokuwa ni huruma yake tu, basi tusimtie wivu kwa kutomtii, bali tupinge maovu.

3. Tunyenyekee mbele za Mungu kama tunataka atuinue, tutubu kwa yote tuliyomkosea kabla hatujampelekea shida zetu.

Mungu akubariki.unaposoma Neno lake hili.

Advertisements

2 thoughts on “Kuamsha Upya Uhusiano Wako Binafsi na Mungu

  1. Amina Irene,
    hata chanzo cha uasi Lusifa hakuatak kunyenyekea, alitaka apewe sifa na ibada sawa na Mungu.
    Tunaambiwa tunyenyekee chini ya mkono wenye nguvu na hayo mengine tutashinda ila tatizo tunaenda kinyume na kujiletea matatizo mengi.
    Tunajifunza

  2. sifa na utukufu apewe yawe, Ni kweli kabisa bila unyenyekevu mbele za MUNGU hatuwezi kufika popote,maana penye unyenyekevu ndipo penye utii na kuuona ufalme wa Mungu.Adam na Eva walishindwa kuwa wanyenyekevu katika bustani ya Eden wakataka kuwa sawa Mungu nao wakaukosa uzima wa milele.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s