Amani Itawale!!

Hakuna kitakachozuia amani yako…ruhusu shauku ya kukaa kwenye uwepo wa Mungu, wakati mwingine tafakari ukuu wa Mungu kwenye maisha yako, usitafakari yote yanayokukosesha amani..mtafakari BWANA, kumbuka matendo makuu aliyokutendea, kumbuka shuhuda na maajabu anayoyatenda kila siku kwa watu wake…Muda wako binafsi na Mungu hata kama ni dakika chache, unabadilisha maisha yako yote, AMANI INATAWALA moyoni, unafurikwa na ukuu wa Mungu, Unajaa sifa na kila utakalofanya ni shuhuda tu, utakuwa mwepesi…Hautakumbuka yale yote, utayadharau, na kuona ulipoteza muda wako bure…Ikiwa Mungu akiangalia mkono wake, analiona jina lako pale, ikiwa ameyatanda mawingu kama pazia, na mbinguni ni kiti chake cha enzi, anayo AMANI TELE anagawa bure… Ile milima, bahari, yale mawingu yalivyokaa kwa AMANI na utulivu yeye ndiyo ameviweka, na kwavile wewe u wa thamani kwake…..AMANI ITAWALE kwako kuanzia saa hii, nyumbani kwako na ndugu zako Natamka AMANI, kazini, shuleni na kila eneo utakanyaga ni AMANI tu. Ruhusu ile shauku ya kukaa na Mungu, ile kiu…itawale. Itakuwa AMANI DAIMA…Smile as you are going through your day!!

Wafilipi 4:7 “Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu

Advertisements

2 thoughts on “Amani Itawale!!

  1. Ameni Mtumishi Mary ubarikiwe na Bwana kwa somo lako limenifungua sana, na nimejifunza jambo jema sana maishani mwangu nitajisogeza sana kwa Bwana Yesu, Mungu anisaidie.

  2. Bwana Asifiwe da Mary..napokea hili Neno mchana huu, ni kwa ajili yangu.kweli nimekosa amani mengi yananisumbua nahisi kusuuzika moyo, niombeeni, Mungu akubariki

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s