Unafahamu Nini kuhusu Nyota yako?

JINSI WACHAWI WANAVYOWEZA KUIBA NYOTA YAKO

Salam wapendwa katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Leo nipo hapa kuwaletea topic mpya kabisa ambayo wachungaji wengi hawaifundishi makanisani na yamkini baadhi yao hawaijui.kama kichawa cha habari kinavyosema, leo nataka kuzungumza juu ya wachawi.kunawatu wengi sana Duniani wanalia kila wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini? nataka nikuambie leo, wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! hapa ni kwamba shetani huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. Unajua kila mmoja wetu anakitu alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. ngoja nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani,soma mathayo 2:1-5.biblia inasema “Yesu alipozaliwa zamani za mfalme herode mamajusi wa mashariki walikwenda kumwona, na walipofika wakauliza yuko wapi aliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyita yake nasi tumekuja kumsujudia. Ukisikia mamajusi ujue si watu wema. kasome biblia ya kiingereza imesema ‘Astrologers’ yaani wabashiri au wanaanga. pia biblia ya NIV imesema Maggi, yaani washirikina, biblia nyinge imesema the Meggicians yaani wachawi.kwa tafsri hizi moja kwamoja tunatambua kwamba hawa mamajusi kuwa ni wachawi. Sasa rejea katika kauli yao walipofika kwa Yesu walisema “Yuko wapi waliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyota yake nasi tumekuja kumsujudia” mpendwa wangu sasa naomba ufungue akili yako ili Mungu akusaidie. watu hawa ni wachawi, lakini cha ajabu wanasema wameiona nyota ya Yesu wakajua ya kuwa aliyezaliwa ni mfalme. kwa hiyo tunajifunza kwamba kumbe wachawi wanauwezo wa kutazama katika ulimwengu wa roho na kutambua kwamba wewe unanyota gani katika maisha yako.

Si kwamba walikosea kwa Yesu kusema kwamba Yesu ni mfalme, walisema kweli kabisa rejea kauli za Bwana wetu alipokuwa kwa pilato aliulizwa wewe ndiye mfalme wa wayahudi hakukataa bali alijibu wewe wasema.pia akaongeza kusema kwamba ufalme wangu si dunia hii. kwa hiyo ni mfalme. pia ukirejea katika Isaya 9:6 biblia inasema na uweza wakifalme utakuwa mabegani mwake; Hivyo basi wachawi wakishatazama katika ulimwengu wa roho na kuona nyota yako kuwa ni ya kifalme kama ya Yesu au labda nyota yako ni Biashara, au Elimu, au Ajira,nk. wanachokifanya ni kwamba wanaiba ile nyota na kuiweka kwa mtu mwingine au wakaiacha tu.

Kuna dalili za kutambua nyota yako ni ipi hasa ni rahisi sana kutambua nyota ya mtoto mdogo. kwa mfano: mtoto akiwa na nyota ya uongozi,utambua hivi watafute wanapokuwa wanacheza watoto wengi kwa pamoja, kisha angalia vizuri kaa utulie usipige kelele kisha uangalie vizuri ni lazima atakuwepo mtoto atakayewadhibiti wenzake na kuwalazimisha kufanya anavyotaka yeye na lazima watafanya, kwamfano anawezakusema nyamazeni na wote kweli wakanyamaza, au twendeni na wote kweli wakamfuata.

Pia dalili za kutambua Nyota iliyoibiwa ni hizi, kwa mfano mtoto alikuwa anafanya vizuri kabisa darasani lakini sasa hivi anazidi kudidimia wala hapendi kusoma, ukiona hivyo ujue tayari wameshachukua wanjanja! pia kwa mtu mzima unaweza kukuta kwamba unaandaa mipango lakini haitimii mipango yako.unapanga mwaka huu lazima nitafungua Duka lakini utashangaa linazuka tatizo hutafungua hilo duka mpaka mwaka utaisha. au unaandaa mpango mzuri kabisa lakini utashangaa unamwona mwenzako tayari ameshaanzisha mpango uleule kama ulivyokuwa unapanga. au kama ni biashara utaona mwingine kaanzisha vilevile kama ulivyokuwa unafikilia hapo ujue Nyota yako inatumiwa na mwingine. Unajua nyota hizi huambatana na mawazo yako. jinsi mawazo yako yalivyo ndivyo na nyota yako ilivyo hawezi mtu akaitumia nyota yako pasipo mawazo yako.utajikuta kwamba wakati mwingine unapoteza fahamu kama hujielewi vizuri vile. hapo ujue kuna kitu.

SASA TUNAKWENDA KURUDISHA HIYO NYOTA YAKO KUTOKA KWA WACHAWI:

sali sala hii kwa bidii:
Baba katika Jina la Yesu kristo nimetambua kama kunawizi wa nyota uliyonipa katika maisha yangu sasa kwa Jina lako naiamuru Nyota yangu kokote iliko irudi.katika jina la Yesu ninakuja kinyume na kila nguvu za shetani nazikata kamba zashetani nilizofungwa katika jina la yesu.asante bwana kwa kurudisha nyota yangu.

SASA SHIKA MKONO WAKO KATIKA SCREEN YAKO NIKUOMBEE:
Baba katika Jina la Yesu asante Mungu kwa sababu wewe ni mkuu kuliko wote.kwa Jina lako Mungu ninaamuru Nyota iliyoibiwa ya mtoto huyu, mama huyu,kijana huyu, binti huyu irudi mara moja na taabu iwapate hao waliomwibia nyota yake mtu huyu katika jina la Yesu.

na baada ya hapo ni lazima utajiona tofauti katika mawazo yako, umekuwa na mawazo tofauti hii ni ishara kwamba nyota yakko imerudi,kama hutaona hizo dalili hizi ni ishara kwamba nyota yako haijarudi tafadhali rudia tena sala hii usichoke mpka uzione dalili hizi.
bwana akubariki.

Ev. Moses Mayila

Advertisements

44 thoughts on “Unafahamu Nini kuhusu Nyota yako?

 1. WATUMISHI…ACHENI MTAZAMO HASI JUU YA SOMO LA NYOTA…MAANA LAFAA KABISA KWA KANISA…MAARIFA YA NYOTS KTK BIBLIA NI TOFAUTI KABISA NA MAARIFA YA NYOTA ZA WAGANGA NA ASTRONOMERS…HIVYO WW PSTA MAARIFA YA NYOTA KTK BIBLIA MAANA MUNGU AMETUKATAZA KUFANYS HESABU ZA NYOTA LAKINI HAJATUKATAZA KUPATA MAARIFA JUU YA NYOTA KAMA ILIVYOANDIKWA WSTU WANGU WANAAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA…NAAM.. NA MAARIFA YA NYOTA PIA. MIMI NILIFUNDISHWA SOMO HILO KWS KUTUMIA MISTARI MINGI TUU KTK BIBLIA NA NIMEBARIKIWA SAANA NA NINAENDELEA KUBARIKIWA KTK KRISTO, AMINA. NAPENDA NIKUAMBIE WATUMISHI WENGI WALIOFANIKIWA KTK KILA JAMBO WANAELEWA VIZURI SANA MAMBO YA NYOTA. HIVYO WOTE MNAOPINGA SOMOA NYOTA KTK KANISA, HAMKO SAHIHI. LIFUATILIENI SANAAA SOMO HILO…HAKIKA MTAMSHUKURU ALIYELETA MAADA HII. amani ya BWANA iwe nanyi, amina.

 2. safi Sana orbi nimara yakwanza kuingia humu lakini nimebarikiwa na elimu yako Mkristo anaongozwa na roho sio nyota napia shetani hawezi kuiba nyota ya mtu anacho iba nimapando ya neno jinsi ulivyofundishwa kuhusu na roho yeye huja nakutengua fikra zako ili neno hilo lizitimie ndani mwako Mungu awabariki

 3. Naomba Roho wa Mungu atufunulie ukwel halic ni upi maana kwa upande wangu mpaka sasa cjaelewa kipi ni sahihi yan nimechanganyikiwa,leo hii nilikua kwenye ibada kanisa la kkkt kimara dar es salaam na mtumishi wa Bwana Msomali amejaribu kugusia kuhusiana na hili somo ila nachoomba ni Roho wa Mungu atupe ufahamu sahihi juu ya neno la Mungu

 4. Wote wanao pinga hilo somo la huyo mwl ninahakika kama ukikutana nao watakuw ni wale wa madhehebu ya mapokeo,wamefungwanamafundisho ya makanisani mwao
  Jaribuni kusoma tena na mfikirie na siyo kubisha tu..
  Na ndy maana mnakuw na tabia za kupiga magoti mbele ya sanamu huku mkisem hamuabudu sanamu

 5. naomba ntajie nyota yangu herufi ya kwanza ya jina langu ni G.nimezaliwa 27/02

 6. ‘maalifa ni chembe ya uhai’

  Nimebalikiwa kwa kila nilicho kisoma, na kupitia BWANA WANGU YESU KRISTO ufahamu wangu umeweza kuchuja ipi ni NGANO na yapi ni MAKAPI.

  Tujifunze kutafakari.
  Mwanafalsafa maarufu wa uingereza alisema kuwa; KUELEWA HARAKA NI KAMA KULEWA. Alimaanisha nini basi, Alishauri kujifunza kutafakari na si kupokea neno kama lilivyo.
  MAISHA huubwa na MANENO ambapo ndipo ilipo asili YA IMANI. Natambua pengine hujanielewa lakini namaanisha kuwa; Imani ya mtu asiye mkamilifu hubadirika badirika kulingana na jinsi anavyo pokea. Huyu akisema hili, yule akaleta lile ilimladi kukiwa na ufafanuzi wa kina mtu hukubaliana nikimaanisha kupokea au kuamini bila hata kutafakari. Kuandika ni njia moja wapo ya kuteta na mtu ambaye hauko naye, kwa hyo maneno ni sumu.

  Kuhusu nyota na mambo mengine ya uchawi na ushirikina hayo ni mambo ya ulimwengu maana hata huo ufafanuzi wa biblia unaotolewa ni upotoshaji yaani hauna mkazo unao toshereza. Kwa wachungaji au mtu yeyote ambaye anahitaji kuandaa somo, Mtangulize MUNGU kabla hujafikisha malengo yako kwa Hadhira, maana ni hatari kubwa sana kutenga chakula chenye sumu harusini au kulioni. Kama wasingekuwepo wafafanuzi katika jambo hili la NYOTA, Hebu jifikilie ni watu wangapi walikua wanakwenda kupotoka namaanisha wale wasio ipa nafasi akili yao kutafakari, HAKIKA NI WENGI, na wasingeishia hao tu wapo nawengine wangedokezwa na swala hili.

  Mungu atubariki.

 7. Enyi mlioibiwa “Nyota zenu”,
  Hivi, mlipookoka, ni kwamba mlitangaziwa kuwa “Sasa umekwisha kuokoka” baada ya kufuatisha ile sala aliyokuongoza mhubiri au ulimpokea kweli Kristo na sasa ni Bwana anayekuongoza? Au mambo haya ni ya kuyasoma tu na kuhadithiana?

  Kama ni mambo halisi, basi wachawi walipowaibia hizo nyota zenu na mali zenu, huyo Bwana mliyemkiri alikuwa wapi??

  Au kama mliibiwa hizo nyota zenu kabla hamjaokoka, Je alipowaokoa, hakuwarudishia hivyo mlivyoibiwa? Au hajui kuwa mliibiwa?

  Ninachokiona kwenu ni kwamba hamkijui mlichokikiri, vinginevyo mambo ya kumdai shetani alivyowaibia ni hadithi za Abunuwasi. Mungu anapokukomboa huvikomboa vyoooote vinavyokuhusu! Hebu tazama hapa:
  Mwa 14:14-16, “14-Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.”

  Sasa ninyi ndugu zangu mnaomdai Shetani nyota zenu, huyo aliyewakomboa alikuwa ni nani? Mchungaji wenu au muinjilisti au ni askofu mkuu wenu au ni yule nabii au mwalimu wenu? Kristo akikukomboa huvikomboa vyooote!

  Ni kweli ndg Orbi, kanisa liko jangwani!

  Ndg zangu, msipende njia za mkato, mtaishia kuzungushwa huko jangwani kama wale waliotoka Misri, hao wote kasoro watu wawili tu, walifia jangwani, “SUCKED IN”!!
  Lisikilizeni Neno linachowafundisha na mshikamane na hilo Neno tu!

 8. Wapendwa nawasalimu katika jina la bwana wetu Yesu Kristo. Hii mada kwa ujumla imenigusa sana. Kikubwa ninashangaa sana kwa nini watumishi wa Mungu wanapinga kwamba shetani ni mwizi. Biblia inatuambia wazi wazi kwenye yohana. 10:10 kwamba shetani ni mwizi. pamoja kati ya vitu anavyoweza kuiba ni nyota/ama Neema/Grace (Zawadi tuliyopatiwa na Mungu bila kustahili), Shetani pia anaweza kuiba ufahamu, sura, upendeleo, ndoa, biashara n.k. kwa ujumla anaweza kuiba hatima ya maisha yako. Ninaungana na mtumishi wa Mungu hapo juu. Wakristo Waliookoka yapasa tuenende kwa roho. na lazima tufahamu hila za shetani ili tuweze kumshinda, angalia 2 wakorintho 2:11 “ili shetani asije akatushinda. Kwa maana tunajua mipango yake”. Mtu yeyote ambaye hajampokea Kristo lazima shetani amwibie tena kwa sana tu. Wala si hivyo tu sisi pia tulioijua kweli ya Kristo tukianguka dhambini pia tunaweza kuibiwa. Sasa ni lazima tupigane na turudishe vyote shetani ambavyo alifanikiwa kuiba wakati wowote labda ambapo kabla hatujahesabiwa haki na mara baada kwani tumeanguka na kuinuka maranyingi. Hizi anguka anguka zinatupotezea utukufu tuliokuwa nao awali. Wakati tunatubu ama wakati mtu anampokea Kristo anafanyika kuhani na anapewa mamlaka ya kuamuru jambo lolote na likawa. Wapendwa katika Kristo kwenye maombi yetu tusisahau kuamuru kurudishiwa vyote ambavyo shetani ameviiba. Mambo haya ni roho. 1Wakoritho 2:14 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.” BARIKIWA!

 9. Lwembe na Mabinza,

  Asante kwa kutupa ufahamu…….labda ninukuu toka kwako Mabinza
  “Mtu akiamini mambo kama hayo ikiwemo mambo ya nyota, muumini hatoki humo kabisa na kwa hiari yake hutumia kila silaha kujilinda ili aendelee kuwa MTUMWA wa imani yake hiyo! Labda msemo mzuri ni huu “become willing slaves to victory … if you get sucked in, it can be extremely difficult to think your way clear again”.

  Waumini wengi wa Ukristo katika nchi zetu……bado wako katika utumwa wa dini za kienyeji…..uchawi…..unajimu na mambo kama hayo……Wanakiri kuokoka na kumpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wao, lakini imani hiyo huwa imegusa ngozi TU…! Haijabadili chochote ndani ya maisha yao……kimtazamo….. na Kifikra… Imani katika Kristo haijawakomboa Kifikra (Mind transformation)……Na wanapodai kuwa ndani ya Kristo watajaribu kutumia chochote walichokiamini toka zamani na “Kukivalisha” Ukristo ili waendelee kuwa katika Kongwa lile la zamani….!
  Ndio Maana Babu wa Loliondo alivuta waumini maelfu toka ndani ya makanisa…..kwa sababu ndani ya wengi mizizi na matambiko bado ina nguvu…na Wala sio Kristo (ingawa hasemi na kukiri mbele za watu)……..Na ndio maana kwa wengi kurudishwa kwa misukule ni kitu kikubwa mno kuliko kuokoka na kuja kwa Kristo….! Hebu angalia hofu ya Freemasons……! Usingelitegemea muumini aliye ndani ya Kristo kupagaishwa na hofu ya Freemasons kama tuonavyo leo….!

  Hivyo msishangae kuona mimbari ambazo usingetegemea kabisa kufundisha upotofu kama huu wa nyota….! Na waumini kuanza kuuliza niambie nyota yangu …….niambie nyote yangu……! Na wanaouliza hivi ni waumini ambao kila jumapili wanaingia makanisani….wanaimba mapambio…..wanasema Bwana Asifiwe…..na wanadai wanasoma na kuongozwa na Neno na Roho Mtakatifu….!

  Ilikuwa ni rahisi kuwakomboa wana wa Israel toka Misri……ilichukua siku moja tu…kufunga mizigo na kuondoka….Lakini ilichukua Miaka Arobaini kuwaondoa Umisri ndani ya maisha yao…..!

  Hivyo sishangai napokuta watu wanaodai kuitwa Wakristo wakivutwa na kupapatikia kama watu wasio na mchungaji mafundisho ya Nyota……Misukule…….Mzaliwa wa Kwanza……Mzaliwa wa Haki……Malango……! Unajua wazi Kanisa bado linazunguka jangwani…..! Bado kuna kazi kubwa ya kufanya katika shamba la Bwana.

  Mungu Atusaidie…

 10. Wapendwa SG,

  Kwa mjibu wa sayansi ya Anga; Nyota iliyokaribu sana na Dunia ni jua, inasemwa kuwa umbali kutoka Duniani hadi kwenye Jua ni kadri ya maili 93 milioni hivi. Wataalamu hao wa anga wanasema kuwa Jua ndiyo kisababishi kikuu au ndiyo chanzo cha Nguvu zote Nne za kiasiri, ambazo ni Nguvu ya Nyukilia, Nguvu ya uvutano, nguvu ya umeme na nguvu ya sumaku! Nyota hujiwasha yenewe kwa kutumia nguvu ya kinyukilia (Nuclier fission) kwa mchanganyiko wa hewa ya Nitrogen na Helium.
  Mawazo kuwa nyota ni kitu “Maalumu” hata kufikia kuzioanisha fikra hizo na Imani za kidini, zimeanza zamani sana kabla ya kuzaliwa kwa Yesu. Wataalamu wa nyota (Astrologists) wanamahusiano ya kutegemeana kati yao na Wataalamu wa Elimu ya Anga. Inaaminishwa Kiupotofu na wanajimu na washirikina wa kidini kuwa, yapo mahusiano ya moja kwa moja na matokeo ya kimaisha yahusuyo ubinadamu Duniani. (astronomical phenomena and events in the human world.) WAHINDI, WACHINA na MAYANS, ambao ni wataalamu wa mapema wa elimu hiyo, wanaamini kuwa, jua, Mwezi Nyota na viumbe vingine vya angani huathili kuzaliwa, bahati, mafanikio na maisha ya Mwanadamu. Fikra hizo ambazo zilihusianishwa na kutumika katika uuguzi na ushirikina wa kusoma Nyota pamoja na ubashiri wa kinyota (Horoscopes); fikra na falsafa za wauguzi, washirikina na waganga wa mapema kutoka india, uchina na Methopotamia viliingizwa katika Dini karibu zote za ki Ibrahimu (ukristo, uyahudi,na uislamu) kutokana na mwingiliano wa Kibiashara, kijamii na ustaarabu uliotokana na tawara na dini za Kipagani.

  Jambo hili la kuamini Nyota kuwa inaathili maisha ya mwanadamu, iliingizwa na Romani katoliki katika dini iliyoitwa Ukristo. Elimu hiyo inajurikana kuwa Siderism, ambayo falsafa yake inasema kuwa “is the belief that the stars influence human behavior or herald major changes in human history”. Imani hiyo ilijengeka kutoka na upotoshaji uliolenga kuioanisha Dini ya kipagani ya Kirumi ya kale na ukristo, tokana na simlizi la kuzaliwa kwa Yesu ambako kulijulikana kwa wale Mamajusi watatu ambao waliongonzwa na Nyota. Theory nyingine inatokana na Kutokea kwa Kimondo (comet) kilichozaniwa kuwa kiliashiria kufa kwa Julius Caesar, tukio jingine liloimalisha
  theory hizi ni pale kulipoonekana kwa Kimondo kingine kikubwa ambacho kinajulikana kama Hale-Bopp, wakati wa kiongozi mkuu wa kidini Octavian na baada ya kimondo hicho kukatokea Mauaji ya Kiharaki katika ile Heaven’s Gate! Mitazamo hii ya kiimani ya kipagani na falsafa mbali mbali ambazo kwa sababu ya mda siwezi kwa leo kuzieleza hapa, ndizo zilizofanya wanadini kuingia katika lango hili lisilo la kimaandiko kuwapotosha watu.

  Mwanafalsafa mmoja wa Kiingereza alitoa Kanuni yake katika Tabia za mtu katika Imani, hasa kwa mambo kama, homeopathy, psychic powers, alien abduction as “claptrap” ijulikanayo kuwa ni “STEPHEN’S Law” inasema kuwa, Mtu akiamini mambo kama hayo ikiwemo mambo ya nyota, muumini hatoki humo kabisa na kwa hiari yake hutumia kila siraha kujilinda ili aendelee kuwa MTUMWA wa himani yake hiyo! Labda msemo mzuri ni huu “become willing slaves to victory … if you get sucked in, it can be extremely difficult to think your way clear again”.

  Mwanafalsafa mwingine aitwaye, Jonathan Glover yeye anasema na kuilinganisha nguvu ya Imani katika mambo potofu kuwa, ni kama Mgonjwa akienda kwa daktari na kupewa dawa ambazo zikampa nafuu kubwa, kisha alipo rudi siku nyingine, Daktari yule akamwambia mgonjwa huyo kuwa, lo! ile dawa niliyokuwa nimekuandikia HAIKUFAI sasa nakubadirishia dawa, nikupe ikufaayo! Laki mgonjwa yule atajiuliza mbona nilipotumia ile dawa nikapata nafuu kubwa? Mgonjwa atawaza na kusema moyoni mwake kuwa, haikosi Daktari huyu hana ujuzi wa kutosha, hivyo atabaki katika tatizo lake muda wote hadi atakapo kufa!

  “Biblia katika Methali inasema, “Maarifa ni chembe ya uhai”.

 11. “ASIONEKANE KWAKO MTU AMPITISHAYE MWANAWE AU BINTI YAKE KATI YA MOTO, WALA ASIONEKANE MTU ATAZAMAYE BAO, WALA MWENYE KUBASHIRI, WALA MSIHIRI, WALA MTU ALOGAYE KWA KUPIGA MAFUNDO, WALA MTU APANDISHAYE PEPO, WALA MCHAWI, WALA MTU AWAOMBAYE WAFU.”
  KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10-11

 12. “UMECHOKA KWA WINGI WA MASHAURI YAKO; BASI, NA WASIMAME HAO WAJUAO FALAKI, WAZITAZAMAO NYOTA, WATABIRIO KILA MWEZI MAMBO YA MWEZI HUO, WAKAKUOKOE NA MAMBO YATAKAYOKUPATA.”
  ISAYA 47:13

 13. Hahahaha…! Polepole, kanisa linageuzwa njia! Yaani lina veer off ile NJIA na kuanza safari ya kuzirudia nyota na uaguzi, na kuibiana nyota, kupewa kinga, na kuzirudisha nyota na kuvunjiwa laana na …!!!

  Natamani kukaa chini ili nilieeeeeeee….! Baada ya Injili yooote mliyohubiriwa, leo hii mnataka kujua jinsi wachawi wanavyoziiba nyota za watu?? Mnataka kuanza kufundishwa mambo ya nyota, mpaka mfikishwe katika ibada yake!!!

  Ama kweli, sikio la kufa!!!

 14. mbona hili somo la nyota kila muhubili ninayemsikliza anatumia andiko moja tu katika kitabu cha mathayo, mimi nafikiri hermeneutic haitumiki vizuri kwa sababu somo limekosa maandiko yakutosha kuunga mkono kwa habali ya nyota, pili mwandishi haonyeshi watu walioibiwa nyota zao katika Biblia, tatu kule kwenye Agano la nani aliwahi kuibiwa nyota?

 15. Ev.mayila shukrani kwa topic yako nzuri na ya kusisimua,mimi cna uelewa wowote kuhusu nyota yangu je?unaweza kunisaidia kuhijua nyota yangu kama nimeporwa na wajanja naomba msaada wako

 16. naomba maombi katka maisha yangu maana sifanikiwi kwa lolote mpaka nakata tamaa

 17. namwomba Mungu anisaidie nijifungue salama, na mchumba wangu anitunze, na kumpenda mtoto. amina.

 18. AKSANTE NDUGU MCHUNGAJI KWA KUTUFUMBUA MACHO KUHUSU NYOTA, MIMI JINA LANGU LINAANZA NA HERUFI YA M, JE, KIPAJI CHANGU KINAASHIRIA KUWA NANI KATIKA SHUGHULI ZA DUMIANI?

 19. am pleased so much with this lesson, am so happy to knw somthing which i never knew about. Thanks alot ev. Moses

 20. Bwana Yesu asifiwe

  Ndugu Ev Moses Mayila kweli somo ilo ni ya kweli na ya muimo sana apa jini ya jua .kwa imani yangu nimeomba na kushika screen kama vile ulio andika na kuomba .kwa jina ya Bwana wangu YESU KRISTU.amina

 21. Kuna mambo ya kujiuliza kwanza na kuifuatilia historia.

  Kuna mtu mwingine aliwahi kuzaliwa kukawa na ishara ya nyota?
  Mamajusi waliona nyota halisi angani au ilikuwa ya kusomeana kama wajanja wa leo?
  Je mamajusi walikuwa wacha Mungu au wachawi kama wengine wanavyowaita?

  Kuna kitu cha ajabu kidogo kwamba hawa watu walimsujudia mwokozi. Lakini pia waliweza kumsikia Mungu na kumtii kwa habari ya kupeleka taarifa kwa Herode.
  Tukumbuke pia tukio la kuzaliwa kwa Yesu walijuzwa watu wengi kwa njia za ajabu,wakiwemo hao mamajusi, wachunga kondoo, n.k.

  Najua Mayila hamaanishi nyota kama za akina shehe Yahya, lakini katika biblia sioni kama kuna nabii au mtu yeyote alliyetumia hiyo lugha ya nyota kujaribu kumweleza mtu fulani mambo ambayo Mungu amemkusudia kuyatimiza hapa duniani

  Nyota (sayari) zamani kabala ya sayansi kuendelea sana zilitumika kuashiria mambo fulani,hasa majira, na ndio maana kukawa na wanasayansi wa nyota( mamajusi), tofauti kabisa na wanavyofanya wajanja wa leo, ambao mara unasikia nyota yako ni nge,mbuzi, ng’ombe n.k

  Sioni sababu ya kuwafundisha watu kuhusu mambo wanayotakiwa kutimiza katika maisha yao kwa kutumia lugha ya nyota, maana ni lugha inayotuniwa sana na waganga.

  Ni kuchanganya watu.

 22. kiukwel hili somo limenifundisha mengi sana napia nadhani siyo mm pekee bali ni kwa kila mmoja aliye husika kusoma nadhan amejua kuhusiana na nyota.

 23. mimi naitwa george robert lewis,naomba ni julishe nyota yangu ni ipi?kwani sijuwi ni mwaka mwezi gani nimezaliwa?

 24. MCHUNGAJI Mayila,

  Mafunuo yako ya Nyota ni kinyume kabisa na Mafundisho ya Biblia, hayana kabisa msingi wa Kusimama toka mafundisho ya Yesu katika Injili, Matendo ya Mitume na hata Nyaraka za Paulo.
  Kwa kifupi tu mafundisho yako yanaleta mkanganyiko katika mwili wa Kristo.

 25. Bwana yesu asifiwe mimi nimeokoka lakinio mume wangu ajaokoka ingawa namuombea bado wachawi wanamfuata sana

  mimim stellah

 26. salam katika Jina la bwa wetu Yesu kristo.

  wapendwa awali ya yote samahani sana kwa kutojibu mapenda comment zenu, hi kwa sababu ya majukumu mengi.kusema kweli sijatembelea hapa siku nyingi sana na dio maana hamjaona mada yoyote katika blog hiii.

  jamani kwanza naomba mnielewe, mimi sijasema kwamba sisi tuaongozwa na nyota, ila nimesema kila mtu anayo nyota ambayo kwa jina jingine kipaji,kipaji hiki humuwezesha mtu kufanya mambo mbali mbali katika jamii yake, kama: uogozi, msemaji wa hadharani,nk.

  naanza na dada yangu mwanaid rajabu.
  Nyota niliyofundisha hapa haihusiani na Nge,ng’mbe wala herufi za majina.kwani hayo ni mafundisho ya mashetani! ila nyota nilizofundisha hapa ni vipaji katika jamii inayokuzunguka ambavyo mtu huzaliwa navyo.
  mume anayefaa kukuoa dada yangu ni yule atokaye kwa mungu, biblia iasema mke mwema hutoka kwa bwana, ikiwa mke mwema hutoka kwa bwana basi, vivyo hivyo na mume mwema naye hutoka kwa bwana.Mungu amemuumbia kila mtu mwenzi wake special.angalia mambo yalivyokuwa kwa ibrahimu, kabla hajaitwa ibrahim alijukana kwa jina la Abram na mkewe aliitwa Sarai.lakini Mungu aliwabadilisha majina yao kwa sababu maalum badala ya kuitwa Abram alimwita Ibrahimu maana yake baba wa mataifa, na mkewe badala ya kuitwa Sarai alimwita Sara maana yake mama wa mataifa. ukitafakari kwa makini sana utajifunza kitu hapa kutoka na haya majina. Abram zimebadilishwa herufi chache tu katika jina lake bila kupoteza uhalisia wa wa matamshi wa jina lake lakini likaleta maana ya baba wa mataifa, mkewe naye imeondolewa herufi moja katika jina lake ambayo ni ‘i’ likaleta maana ya mama wa mataifa, ukiangalia wawili hawa walikuwa wanandoa na walioana bila ya kuambiwa na mungu kwamba nyinyi oaneni, lakini wanajikuta kwamba majina yao yao yanaleta maana ya kwamba wao ni wazazi wa mataifa, ni ajabu sana! hivyo basi nakuomba dada yangu uachane na na imani potofu za wabashirio nyota na majina kwa herufi. bali uamini kwamba mume mwema hutoka kwa Mungu.naamini mwanaidi wewe ni mwislamu, lakini nataka nikuambie ukweli kwamba huko uliko yuko mungu lakini si Mungu wa kweli! Qruan 47:15 inasema Allah ameandaa mito ya ulevi peponi, lakini hiyo hiyo qruan 5:90 inasema ulevi ni wa shetani, ikiwa ulevi ni wa shetani na tumeona Allah kaandaa ulevi, Je! Allah siye Shetani? jibu Allah ndiye Shetani, tafakari dada yangunaomba uhame huko mara moja nenda kanisani, tafuta makanisa ya Assemblies of God, Pentecoste, AIC,jiunge huko watakusaidia, au kama uko dar es salaam wasiliana na mimi nikupeleke kanisani. Bwana akusaidie katika jina Yesu.

  nakuja kwako Orbi:
  nyota ya mtu au kipaji cha mtu kinachoibiwa na wachawi ni cha yule ambaye hajampoke Yesu, kumbuka Biblia katika kitabu cha kutoka 33:33 inasema hakuna uchawi juu ya yakobo.unajua asilimia kubwa ya waumini wengi ni wale walio vuguvugu hawa ndo wako katika hatari kubwa ya kutekwa na shetani, na ndio maana utakuta kwamba mtu anakwenda kanisani kila leo lakini kila anachojaribu kuufanya kinaharibika akifanya biashara haifanikiwi,kwa nini? kwasababu hajakaa sawa katika direction ya Mungu hivyo washirikina wamepata nafasi ya kumteka, jamani Shetani ananguvu hata Yesu anajua alipokuwa akitoa pepo alisema hivi ‘hakuna mtu awezaye kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuvichukua vitu vyake pasipo kwanza kumfunga huyo mwenye nguvu’ unajua orbi kunawatu ambao kazi yao ni kuwafunga wenzao kichawi wasifanikiwe katika kila jambo, jamani hebu tuacheni ubishi tukubali kwamba wachawi wapo na moja ya kazi zao ni kumfunga mtu asifanikiwe katika kazi zake.mimi wachawi nimekaa nao najua wanavyofanya na ndio maana nitaendelea kupiga kelele katika hili.mchawi hagsi mtu wa Mungu ila yule ambaye ni vugu vugu ndiye humgusa, na ndio maana katika waraka wangu wa jana nimepinga kwamba tiba ya mchungaji Ambilikile Mwapasile wa Loliondi haikutoka kwa mungu baada ya wachawi kwenda kuchezea katika eneo lake la huduma hiyo.nadhani kidogo kaka umenielewa.

  kwako John Paul
  nadhani nimemjibu dada yetu na wewe kama unaswali niulize, lakini nakuomba uniulize kupitia email yangu ili nikujibu upesi maana sitembelei mara kwa mara blog hii kutokana na msongamano wa email katika email box yangu.

  na wote mnaotaka kuniuliza au kuwa siliana na mimi tumieni email yangu au hata hapa unaweza kuacha reply siku nikifungua nitakujibu.
  mbarikiwe wote na asanteni sana kwa changamoto.

 27. Wapendwa katika Kristo Yesu,
  Tusipovua utu wa kale na kuvaa utu upya tutaenenda kama wamataifa.
  Efeso 4;17….msienende kama mataifa,
  Efeso4:24…Mkavae utu mpya,
  2kolitho 5:17…Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya,ya kale yamepita.
  wakovu wengi hawauvui utu wao wa kale.Yatupasa kuua utu wa kale

 28. Kweli tunahitaji kuwa macho sana!

  Baada ya kuanza tu kusoma kichwa cha somo, sikusikia Amani kabisa juu ya somo hili, lkn namshukuru Mungu nilipoanza kuangalia response za watu nikakutana na mchango wa ndg. Orbi, ambao ninaamini utawasaidia wengi wanaotafuta kuijua Kweli inayotokana na Neno la Mungu na si vitu vigeni!

  Mungu atusaidie!

 29. Mpendwa Ndugu John Paul,

  Kweli Tuzidi kuomba neema ya Mungu kwa Watumishi, kwani kadri kuchapo ndivyo naona Shetani anajaribu mno kurarua kundi la wateule kwa kuwavamia watumishi, hasa kuleta ujumbe unaoleta mikanganyo kwa waumini au wale walio wachanga katika imani hii.

  Neno la Mungu liko wazi, kwani Paulo anasema ” MUNGU….AKATUFUFUA PAMOJA NAYE…..AKATUKETISHA PAMOJA NAYE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ” sasa kama tumeketishwa PAMOJA NA KRISTO, ni mchawi yupi atakayekuja kutunyang’anya nyota zetu tukiwa tumeketishwa na Kristo katika ulimwengu wa Roho hata kama kweli tuna nyota hizo! Maana angalau Biblia inaonyesha kuwa tunaweza kuwa na malaika anayefuatana nasi ( Matendo 12:15) Lakini hata tukiacha hilo sisi tuna Roho wa Mungu aliyemkuu kuliko malaika na nyota anayetuongoza! Yeye ndiye msaidizi wetu tunapotembea katika maisha haya! Hatuna Nyota ya Jaha!Wala ya mkosi! wala nyota ya laana! Sisi ni mzao mteule! Kwa kuyaruhusu Mafundisho kama haya taratibu, pasipo kuelewe yatavunja kabisa ule msingi wa kumwamini Yesu na Roho wake! Na kujikuta kabisa Tunakiri wokovu lakini si ule wokovu ulio katika maandiko! Na hiki ndicho nacho kinachoendelea katika kanisa la Tanzania, Na hatimaye kwa mafundisho kama haya ni kwa wengi kuupoteza uzima wa milele!

 30. Ndugu Orbi,

  Mimi namshukuru Mungu kwa ajili yako pia. Ninapata hamasa sana kwa jinsi ambavyo unachambua maandiko na unavyosimamia Neno la Mungu linavyosema.

  Mimi niliposoma article hii kwa mara ya kwanza nilipata maswali mengi sana. Pamoja na kuwa na maswali hayo na kuhitaji ufafanuzi wa mengi nilisita kwanza ili nione mada hii inavyoendelea.

  Wakati nasubiri nione kinachoendelea likaja swali la dada Mwanaidi Rajab ambaye alihitaji kufahamu aina ya mtu anayafaa kumuona kwa vigezo vya “nyota” na “herufi ya kwanza ya jina”. Hili lilinishtua kwa sababu aliyeuliza anahitaji kufahamu mambo kama “taurus”, na mengine yanayofanana na hayo ambayo hutolewa na wataalamu wa nyota za kimajini akiwemo sheikh Yahaya na kwenye magazeti mengi ya secular. Sijafahamu sana kwa nini dada Mwanaidi hajamuuliza sheikh Yahaya hilo tatizo lake, labda aliona “somo” hili linafanana na la sheik Yahaya!…

  Kwa Mwinjilist Moses Mayila:

  Kwa kuwa uliyeleta somo hili ni mtembeleaji mzuri sana hapa, nilitegemea utamsaidia dada huyu ili kama somo hili halihusiani na nyota za “kaa”, “nge”, nk dada huyu aweze kujua wapi pa kukimbilia. Lakini hadi sasa nashangaa tu kwa sababu dada huyo hujamsaidia. Mimi niliona mtu aliyeleta somo anastahili zaidi kumsaidia mtu ambaye atakuwa na swali kutoka katika somo hilo.

  Mimi binafsi nina maswali mengi na kuna mambo mengi sana ambayo nahitaji ufafanuzi kutoka katika mada hii. Na ninaamini “mwinjilisti” Moses Mayila unasoma hapa…..

  Ninachokuomba tu ni kuwa kama umeleta somo hili kwa ajili ya watu kujifunza na kusaidika ninatarajia utamsaidia dada Mwanaidi Rajabu katika tatizo lake la kutaka kufahamu nyota ya mtu wa kumuoa. Na kutoka katika jibu utakalompatia ndipo hapo nami nitaanzia kuuliza niliyonayo ambayo nahitaji “kujifunza”.

  Lakini kama hauko tayari kumsaidia dada huyu ambaye, kwa ukweli, anahitaji msaada mkubwa basi naona lengo la wewe kuleta “somo” halitakuwa ni JEMA.

  Wakati nasubiri kutoka kwako napenda tuendelee kutafakari maneno yafuatayo kutoka kwa ndg Orbi:

  “Sasa wapendwa tunakwenda wapi, huyo Roho Mtakatifu amebakia ni wa nadharia tu? Neno lake limekuwa halieleweki na ulinzi wake na malaika hawawezi mpaka wachawi wachukue nyota zetu!”

 31. Wapendwa,

  Hivi tumefikia mahali ambapo kila mafundisho yanaloletwa kwa kutumia Biblia au mtu anaitwa mchungaji basi tunameza pasipo kutafakari kama maneno ya Mungu? Na kwa nini tunatamani maajabu maajabu ya kila jambo na kuyafanya kuwa ya rohoni? Nadhani huu ni mtego ambao shetani anatumia sasa hivi kuwanasa wateule!

  Kanisa la leo (Nikiwa na maana waumini) tunaenda wapi? Haya mafundisho ya Nyota si mafundisho ya Biblia! Kwa ujasiri kabisa nasema ni mafundisho kutoka kuzimu! Paulo anasema katika 2COR10:5 “TUKIANGUSHA MAWAZO NA KILA KITU KILICHOINUKA,KIJIINUACHO JUU YA ELIMU YA MUNGU, NA KUTEKA NYARA KILA FIKRA IPATE KUMTII KRISTO”

  Hii ni elimu ngeni katika kanisa inayotaka kujiinua na kutufanya tusiongozwe na Neno la Mungu na Roho wake mtakatifu! Paulo anaendelea kusema ” IWENI NA NIA HIYO HIYO NDANI YENU AMBAYO ILIKUWA NDANI YA KRISTO” (Phil2:5) Yesu hakuongozwa na NYOTA, na hata alipokutana na wale watu wawili katika njia ya Emmaus, aliwaonyesha kwa kuwafunza NENO LAKE “AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE AKAWAELEZA KATIKA MAANDIKO YOTE YANAYOMHUSU YEYE MWENYEWE”(Luka 24:27)

  Mitume katika Agano jipya hawakuongozwa na Nyota! Amasivyo kitabu cha Matendo ya Mitume kingejaa shuhuda za kuongozwa na Nyota! Waumini wa kanisa la kwanza licha ya shida na mateso waliyopitia hakiuambiwa shetani ameeiba Nyota zao! Watu wa Mungu hebu tufunguke katika ufahamu wa Neno la Mungu.

  Na hata ukirudi Agano la kale, mwandishi wa Zaburi anasema ” NENO LAKO NI TAA YA MIGUU YANGU, NA MWANGA WA NJIA ZANGU”(Zab 119: 105)Hatumulikiwi na wala kuongozwa na Nyota tuliomwamini Yesu na Neno lake!

  Hebu tuangalie Isaya anasemaje; ” SIMAMA SASA NA UGANGA WAKO, NA WINGI WA UCHAWI WAKO, ULIOJITABISHA NAO TANGU UJANA WAKO, LABDA UTAWEZA KUPATA FAIDA,LABDA UTAWEZA KUSHINDA,UMECHOKA KWA WINGI WA MASHAURI YAKO, BASI WASIMAME WAJUAO FALAKI(astrologers, wanajimu, watazama nyota) WAZITAZATAMAO NYOTA,WATABIRIO KILA MWEZI MAMBO YA MWEZI HUO,WAKUOKOE NA MAMBO YATAKAYOKUPATA (Isaya 47:12-13)

  Sasa wapendwa tunakwenda wapi, huyo Roho Mtakatifu amebakia ni wa nadharia tu? Neno lake limekuwa halieleweki na ulinzi wake na malaika hawawezi mpaka wachawi wachukue nyota zetu!

  Hebu tuwe waangalifu, hasa kufahamu kondoo waliovaa mavazi ya mbwa mwitu ambao wanapanda mbegu ya uharibifu katika kanisa, Paulo anasema wazi ” BASI ROHO ANANENA WAZIWAZI YA KWAMBA NYAKATI ZA MWISHO WENGINE WATAJITENGA NA IMANI WAKISILIKIZA ROHO ZIDANGANYAZO NA MAFUNDISHO YA MASHETANI (1Tim 4:1) Naona kabisa kanisa la Tanzania linaelekea huko! Mimbarini kumekua ni kiini cha mafundisho ambayo kwa utaratibu yanawaondoa wateule kwenye IMANI KATIKA KRISTO YESU PASIPO KUJUA! Na kwa vile tumejaa wasikio ya utafiti, basi lolote lile linaloletwa na yoyote aitwae mtumishi linamezwa pasipo hata kutafakariwa! Hebu Bwana Atufungue macho ya Rohoni wapendwa!

 32. mie nyota yangu ni kaa na nimezaliwa 23/06,na herufi yangu ya kwanza ni “M” kinyota ninafaa kuolewa na mtu wa nyota gani ambaye tunaweza kudumu kwenye ndoa yetu, na huyo mtu jina lake la kwanza lianze na herufi gani?
  Aksante

 33. mimi ni mwanamke wa miaka 38 nina mtoto mmoja ila
  sijafanikiwa kupata mume wa kunioa huyu niliye naye
  nimekaa nae zaidi ya miaka 7 na sasa ameamua kuniacha
  bila sababu naomba uniombee nami nipate mume wa kuishi
  nae.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s