Kuhubiri sawasawa

Ni jambo lililozoeleka kwa watumishi wa Mungu wakiwemo wahubiri na wainjilisti kwenda vyuo vya Theolojia/Biblia kusoma:

Je! Ni Lazima mtu kwenda chuoni kusoma ndipo aweze kuhubiri sawa sawa?

Advertisements

18 thoughts on “Kuhubiri sawasawa

 1. Pana hekima nyingi sana na mitazamo mingi sana, hakika kristo atakaporudi atatafunulia yote

 2. napenda kuwaomba wauliza maswali wawe wanatumia maneno fasaha ktk maswali ili mtu anayejibu ajibu sahihi mfano ni hapo juu ameuliza kuhubiri ni lazima uende chuo ilitakiwa aseme uchungaji ni lazima uende chuo? Kwa nini nasema hivi ni kwa sababu kazi ya kichungaji si kuhubiri tu ni kuliwakilisha kanisa ktk mambo mengine pia mfano ktk huduma zingine za kijamii nje ya kanisa ndio vitu hivyo pia ambavyo watumishi wanafundishwa wawapo vyuoni ni kama ktk kozi hata za mashuleni tunaona mtu ansoma engineering lakini bado kuna vikozi vidogo anafundishwa ili aje kuwa boss mzuri kama account na vingine vingi vya utawala
  Asanteni

 3. Nafikiri kitu cha kwanza ni shule ya Roho Mtakatifu, ambaye ndiye anayeweka huduma ndani ya Mtu iwe ni kufundisha au kuhubiri” akatoa wengine kuwa mitume, wengine kuwa walimu, wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji hata kazi ya huduma itendeke na mwili wa kristo ujengwe. Paulo kabla hajaitwa alikuwa na Elimu ya dini, alikuwa amesoma katika shule au ninaweza kusema chuo ambacho walimu wa dini, mafarisayo walikuwa wamepitia.
  Elimu ya dini ina doctrine nyingi ambazo nyingi hata watu waliokokoka tunazifahamu
  kama Theology is the doctrine of God, His being, His Nature, His triune(utatu)
  The way He reveal himself,
  Pheumatology is the doctrine of the holy spirit, His counselor, His Person hood, His function, His manifestation, His task, His work, His nature
  soriotology is the doctrine of salvation
  Antropology is the doctrine of man, his creation, reasons for his creation, the purpose of his existance, his fall
  There are many doctrine, nikizitaja zote sitamaliza hapa.
  Paulo anasema katika wakorintho wa kwanza, sura ya 2, nilikuja kwenu katika hali ya udhaifu, au nilikuwepo kwenu katika hali ya udhaifu, nami niliwahubiri katika dalili, na za nguvu na katika Roho mtakatifu, sikuja katika hekima ya maneno yenye kushawishi akili za watu katika kuhubiri,Imani yenu isije ikajengwa katika hekima za wanadamu bali imani yenu iwe katika nguvu na uwezo wa Mungu.
  kwahiyo si vibaya kusoma theology au tunaita christian doctrine, kule hufundishwi kuhubiri unafundishwa doctrine nilizozitaja hapo juu.
  itakupa uelewa katika elimu ya Mungu, lakini si ya kutegemea au kutengeneza msingi muhimu katika kuhubiri au kufundisha neno la Mungu.
  Utahubiri kwa kiwango cha juu, unapokuwa unaoperate katika nguvu na ukiwezeshwa na Roho mtakatifu, kwasababu hapo ndipo nguvu ya huduma ilipo

 4. jamani kwenda chuo siyo ishu maaana kuna watumishi wamekwenda bible college lakini ukiwashtukiza wafanye huduma hawawezi mpaka akasome kalenda ya biblia na huu ni udhaifu mojawapo ambao makanisa yanao ni kuwapangia watumishi wao kitu cha kusema na ninafikiri hii nayo tuifanye mada.unakuta mtumishi hasomi neno au hatafuti Mungu ili ampe cha kusema kwa sbabu anajua kalenda ina kila somo la kila siku kwa hiyo haombi maana amerahisishiwa kila kitu.tofauti na mtumishi ambae ana wito huyu atafunga ataomba Mungu ampe kitu cha kusema na watu wake. udhaifu mwingine ni kwamba watu wanakwenda bible college si kwa ajili ya kumtumikia Mungu bali wapate ajira so unakuta tua watu ambao hawajaitwa bali wamejiita wenyewe wapate ajira!!

 5. Ndugu Paul,

  Kwanza kabisa labda unielewe tu kuwa mimi ni muumini tu wa imani ya Bwana Wetu, ambaye sijaenda Bible College!Kwa hiyo inawezekana kabisa kwa sehemu najibu nadharia tu! Ningelikuwa nimekwenda Bible College angalau ningekuwa more practical! Lakini licha kutokwenda kwangu Bible College, nimekuwa nijibiidisha napopata Muda kuhudhuria mafunzo mbalimbali ambayo hutolewa kwa watu ambayo hawana nafasi ya Kwenda vyuo vya Biblia,na katika course hizo nimekutana na Watumishi wa Mungu ambao kwa sababu mbalimbali wamekosa muda wa kwenda vyuo vya Biblia na kuona wakisema wamenufaika na masomo hayo na kupanua ufahamu wa Neno la Mungu ambao hawakuwa nao kabla ya masomo hayo, na labda kwa upande mwingine nimekuwa na urafiki wa karibu mno na waalimu wanaofundisha vyuo vya Biblia labda wanaweza kuwa wameniathiri kufikiri kwangu!Kwa hiyo naomba unichukulie kwa hilo! Kwa hiyo kama yupo aliyekwenda Bible College anayefuatilizia maada hii anaweza kujibu vyema Maswali yako zaidi na kufafanua maoni yangu, yeye atatupa practical experience ya kuwa chuo cha biblia kuliko mimi.

  Na kwa upande wa kutofautisha Watumishi waliokwenda vyuo vya Biblia na wasiokwenda, naona nitakuwa subjective! Niwatofautishe kwa kwa mambo yapi hasa? Mahubiri yao? Mafundisho yao? Maisha yao ya Maombi? Hekima? Vigezo ni vingi mno!Na kumbuka kila Mtumishi ana karama yake binafsi awe amekwenda Chuo cha Biblia au la! Kila Mtumishi ni unique!kama ambavyo kila mtu ni tofauti!Na hata waliokwenda chuo cha Biblia huwezi kuwa generalize!na kuwalundika pamoja katika utendaji wao wa Huduma zao na hata wasiokwenda chuoni pia!

  Nimehubiriwa na watumishi wengi mno katika maisha yangu ya wokovu na kila mtumishi amekua na sehemu yake kunijenga Kiroho!Na baadhi wameniachia maswali ambayo mpaka leo sina majibu! Nimehubirwa na watumishi ambao ni darasa la saba hata kusoma Biblia ni shida! lakini nilielewa ujumbe waliotaka kuufikisha na ukanibariki! Nimehubiriwa na watu wenye PHD ya Theology wakanifanya nitamani nami kwenda Bible College kupanua ufahamu wa Neno la Mungu! Lakini pia nimehubiriwa na watumishi wenye nia na njaa ya kumtumikia Mungu, lakini ufahamu wao wa Neno unatamani kama wangalikwenda Chuoni! Na Nimehubiriwa na watumishi waliokwenda Bible College nikahangaika kujua wanasema nini hasa katika mahubiri yao! Kwani utangulizi wa Neno, mifano, kufanunua neno! kuliweka katika practical experience kukaniacha nitoke mtupu!

  Hivyo kusema nitawatafoutishaje ni swala pana sana, lakini tofauti yao iliyo wazi ni kuwa huyu amekwenda Bible College na huyu hajaenda!Kama ambavyo unaweza kumtofautisha mtu wa Darasa la saba na Mwenye shahada ya chuo kikuu!

  Lakini labda ndugu John labda njia ya kuwatofautisha iliyo wazi ambayo hata wewe ulipo unaweza ukaitumia, ni kuchukua syllabus ya Chuo cha Biblia hata cha kanisa lako unaloabudu, angalia ni nini wanafundisha huko, kinachofundishwa huko ndicho hicho anachokikosa yule ambaye hajaenda! Na labda kuiweka mada hii kwa vitendo, ni kuumuliza Mchungaji wako, kama alikwenda Chuoni ni kwa nini alifanya hivyo! na kama hajaenda chuoni kwa nini alifanya hivyo, kwa kufanya hivyo unaweza kujua tofauti!Na kama kanisa lako linapeleka wachungaji chuoni, ni kwa nini linafanya hivyo! na kama halina utaratibu huo, ni kwa nini!

  Kwa upande wangu mimi nimehubiriwa sana kwa kipindi kisichopungua miaka 10 na wachungaji waliokwenda Bible College na wamenibariki mno! Wachungaji wangu wote walikuwa na Digrii za kwanza katka elimu ya kawaida tu, mmoja ya Udaktari (Muhimbili, mwingine ya Uchumi, mwingine uchoraji, na halafu wote wakawa na Master’s of Divinity/Theology na mchungaji niliye naye sasa anajiandaa kuchukua PHD, kwangu wamekuwa ni baraka! lakini hii hainifanyi naporudi kijijini kwangu nisiabudu kwa mchungaji ambaye namfahamu miaka mingi aliyefika darasa la saba! akiihubiri injili kwa uaminifu mkubwa, na watu wakiokoka! Naamini kila aliyeokoka akiwa hai kiroho na ameamua kuingia katika utumishi hasa akitambua ameitwa na Mungu ana Ujumbe! Na ni kwa mtumishi huyo mwenyewe kuamua, kama anaona kwenda kusoma chuoni atafikisha Ujumbe aliopewa na Mungu vyema au LA! Na kwa mimi ambaye ni mpokeaji wa Neno la Mungu siangalii ujumbe umeletwa na chombo gani hasa! Maana Yeye ni Mfinyanzi mwenye Amri ya kuumba chombo kimoja kiwe hivi na kingine kiwe hivi! Kwangu ni kuufanyia kazi Ujumbe huo!

 6. Ndugu Orbi,

  Ninashukuru kwa majibu yako. Nami ninaomba nieleweke tu kuwa lengo la mimi kuuliza swali hilo si kupinga chochote, bali ninapanua tu mada ili tuweze kuliangalia jambo hili kwa mapana, marefu na kina.

  Pamoja na maelezo hayo uliyoandika, naona hukulipata vizuri swali langu. Kwa maneno mengine Niliuliza kama kuna uwezekano wa kutofautisha mtumishi aliyekwenda chuoni na yule ambaye hajakwenda, katika utendaji wao wa utumishi katika mwili wa Kristo. Yaani mchungaji au mwinjilisti fulani akifanya jambo fulani watu wanaweza wakafahamu KWA HAKIKA [siyo kudhani]kwamba ni kwa sababu hakwenda chuo cha Biblia kusoma!

  Nafahamu kabisa kwenye vyuo hawafundishi watumishi kuwa wakorofi, au kufundisha watu wakose hekima ya kutatua mambo mbali mbali au kuwa na tabia fulani ambayo inaonyesha mapungufu katika utumishi. Sasa kama haya hayafundishwi chuoni maana yake ni kwamba aliyekwenda na asiyekwenda chuoni anaweza kuwa na matatizo hayo; kama tu ulivyosema matatizo aliyoyataja dada Mary kuwa hayasabishwi na kwenda chuoni bali ni mtu mwenyewe.

  Sasa, kama aliyekwenda chuoni na asiyekwenda chuoni wanaweza kupata matatizo sawa, PENGINE na kinyume chake ni sawa kwamba Aliyekwenda chuoni na Asiyekwenda chuoni wanaweza kuwa na mambo mazuri yanayofanana. Kama hili ni kweli, NDIYO MAANA nimeuliza Je, inawezekana kutofautisha aliyekwenda chuoni na asiyekwenda chuoni katika utendaji wao kazi ya utumishi? Hili ndilo swali langu la msingi na ndilo ninatamani sana nipate jibu.

  Kuna jambo uliloandika ambalo nalifanyia homework na kama nitapata maelezo tofauti na ulivyoandika wewe nitayaleta hapa, kwa kadri ya Neema ya Mungu itakavyoturuhusu, ili tuweze kuendelea kujadiliana kwa lengo la kujifunza. NI hili uliloandika hivi: “”Kwangu mimi naona ni VIGUMU MTU MMOJA KUIBEBA KWELI YOTE YA MUNGU! Hata tusugue magoti kiasi gani! Ndio Maana tumefanyika mwili mmoja, kila kiungo kwa mwenzake!””

  Jambo jingine ambalo naomba tukubaliane ni kuwa kujifunza wanakojifunza watumishi katika vyuo siyo sawa na kujifunza wanakojifunza wanaofundishwa na watumishi hao. Kwa maneno mengine ni kwamba si kila mtu anayefundishwa Neno la Mungu anafundishwa ili kuwa katika utumishi unaotambulika kama mchungaji, mwinjilisti, nabii nk. Pia mtu anayefundishwa Neno la Mungu ili atoke dhambini hatuwezi kulinganisha na kujifunza anakojifunza mtu aliyekwenda kusomea uchungaji. Kwa hiyo kuhubiri Injili siyo kuwafundisha watu kuwa watumishi, bali kuwafundisha watoke dhambini waingie kwenye wokovu na wakifika humo ndipo wengine huamua kwenda vyuoni kusomea utumishi. Nimeyaandika haya kufafanua mfano ulioutoa wa Filipo na Mkushi.

  Kwa sasa nasubiri jibu la swali langu na pengine likishajibiwa ninaweza kuwa na mengine ya kuandika!

  Immanuel!

 7. Ndugu Mary,

  Nakubaliana na wewe, lakini kama Wachungaji waliokwendwa Chuoni wana Kiburi, tatizo nadhani sio Chuo, na kama wanawaona wachungaji/ watumishi wasiopita chuo sio watumishi au watenda kazi wa Bwana, huo sasa ni upofu wa kutojua Maandiko! Na unahitajika ufanyike msaada! Kwani kila Mkristo kwa kule kuokoka kwake tu, yaani kumpa maisha yake Yesu, ameisha fanyika Mtumishi Wa Mungu! Sisi ni Mzao wa Kikuhani!Tunaujasiri ule ule wa kumsogelea Mungu na kuingia patakatifu pake kwa njia aliyotuanzishia Yeye Mwenyewe! Haijalisha elimu ya Mungu niliyonayo Kichwani!Haijalishi ufahamu wangu mpana wa Maandiko!

  Hivyo dada yangu Mary sidhani tatizo linaletwa na kwenda Chuoni,bali ni la Mwanadamu, kwani hata watumishi ambao kabisa hawajauona mlango wa Chuo cha Biblia tumeona wakiwa na matatizo mengi, ambayo wengine tunadhani kama labda wangepata mahali kwa kujifunza ingewasaidia katika kupanua ufahamu wa Huduma zao.

  La msingi kama ulivyosema ni wewe uliyeitwa na Mungu umeitwa kufanya nini katika Ufalme wake! Wako wanaodai hawaitaji kufundishwa, watafundishwa na Roho Mtakatifu tu! Si mbaya ni vyema kabisa! Lakini siku ambayo Roho Mtakatifu atakapo amua kuwa kimya (maana kuna nyakati huwa kimya)Au ukachanganyikiwa kuisikia sauti yake, basi huwa huna hata ufahamu wa kushikilia ambao unatokana na kujifunza Neno lake! Na hata Kumsikiliza Roho Mtakatifu tu huwa kunafanya kazi katika wigo wa Neno lake!

  Na vile na wale ambao wanasema Watajifunza Neno pasipo Kumpa nafasi Roho Wake anayetufungulia mafumbo ya Mungu yaliyoko katika NENO, wana hatari kubwa pia ya kuifuata dini au imani baridi yenye ukavu na sheria kama mafarisayo na walimu wa sheria! UBARIKIWE!

 8. Bwana Yesu asifiwe;
  Mimi nashukuru kwa michango na somo hili zuri , ila nadhani ndg Orbi umeeleza vizuri sana , katika maelezo yako naona majibu yote na mifano uliyoitoa imeonyesha kuwa wote waliojifunza /kufundishwa kipindi kile walifundishwa moja kwa moja na Mungu mwenyewe kupitia mazingira k.m Daudi alipokuwa anamkimbia Sauli katika kutangatanga akimtegemea Mungu , ndiyo hiyo Zaburi uliyoitaja , kama sikosei Daudi hakwenda chuoni,n.k nadhani watumishi wengi wa agano la kale hawakuwa na vyuo walikuwa wanajikita sana na mambo ya Mungu (pamoja na utii) , kwa hiyo walipokea ujumbe moja kwa moja kutoka JUU ( ingawa kuna baadhi walikuwa na vyuo va manabii).Licha ya Daudi tunawasoma pia watu kama Ayubu, Ibrahim, Yusufu na wengine wengi , watu / jamii iliyowazunguka walijifunza kwao kupitia maisha yao.Kwa hiyo naona chuo sio lazima saaana, kwa sababu kuna watumishi wana kiburi cha uzima sababu ya kupitia chuo, tunawasikia wakiwa madhabahuni wanavyowaona wasiopitia chuoni kuwa si watumishi halisi wa Mungu , na tumeshawaona watumishi wasiopitia chuo chochote wakitumika vizuri zaidi. Nadhani la msingi ni; ukisimama vizuri na Mungu, anaweza kukutumia vizuri kwa nafasi aliyokupa .

 9. Mpendwa John,

  Mahali niliko muda huu yaani napo blog, hapaniruhu kufungua Biblia ili inisaidie kutoa nukuu katika kujibu maswali yako.

  Lakini ningependa kusema hivi Ndugu John, kitendo tu cha Mwenyezi Mungu kutupa maneno yake katika Maandishi, tayari kinafungua mlango wa KUJIFUNZA au Umuhimu wa KUJIFUNZA! Au KUFUNDISHWA! Hebu rudia kitabu cha Kumbukumbu la Torati! Ona ni Mara ngapi Israel waliambia WAJIFUNZE maneno ya TORATI! Na Pia WAFUNDISHE Watoto wao! Na Musa wakati anamaliza safari yake alimwambiaje Joshua! Kwa yoyote anayesoma Biblia anaposoma maneno aliyoaambia Yoshua natoa hamu ya kutaka kukaa na KUJIFUNZA maneno ya Mungu.

  Nikirudi nyuma kidogo tena utaona kuwa Mungu alizungumza na Musa moja kwa moja mara nyingi sana! Lakini kuna wakati Mungu alizungumza au alimfunza vitu Musa kwa kupitia watu! Angalia Musa alipokuwa anapata tabu kutatua matatizo ya Israel, Jethro Mkwewe alimfundisha kanuni ya delegation! na Israel waliifuata siku zote! Hivyo hata katika Agano la kale, ambapo Mungu aliweza kuzungumza na watu moja kwa moja, lakini njia ya KUJIFUNZA maneno yake, ni njia mojawapo aliyoichagua! Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Nehemia, Ezra na wengineo, na Hasa ukisoma Zaburi 119! Jaribu tu kupigia mistari neno NIMEJIFUNZA AMRI ZAKO! KUZIFUNDISHA AMRI ZAKO!

  Tukirudi kwenye Agano jipya ambacho wote tunakiri ni kipindi cha Roho Mtakatifu, Tumeona Roho Mtakatifu huyo huyo akiwatuma watu KUWAFUNDISHA waamini! Mfano mzuri ni Philipo! Yule Mkushi akiwa safarini aliyasoma Maandiko, lakini hayakumuelewa kabisa! Na Roho Mtakatifu aliona kabisa kuwa haelewi anachosoma! Na wala hakuamua kumfunulia maana ya MAANDIKO hayo! Bali aliamua kumtuma Philipo! Siwezi kumjibia Roho Mtakatifu kwa nini alifanya hivi! lakini labda ni kuwa aliiona njia rahisi kabisa Mkushi huyo kuujifunza na kuulewa ujumbe wa Mungu ilikuwa ni KUFUNDISHWA na Philipo, au labda Mkushi huyo asingeweza kubeba MAFUNUO ya Roho Mtakatifu! Au pengine Roho Mtakatifu alikuwa anatujengea kanuni ya kujifunza kuwa tunaweza kusoma Neno la Mungu tusilielewe, na inatubidi kukubali KUFUNDISHWA NA KUELEKEZWA NA WATUA AMBAO ROHO MTAKATIFU AMEAMUA KUWAFUNULIA!

  Kuna mifano mingi kama Hii katika kitabu cha Matendo ya Mitume! Angalia APOLLO ambaye anaonekana alikuwa anajua sana Kuhubiri, Lakini ilibidi Paulo amuweke sawa na KUMFUNDISHA NENO LA MUNGU KWA USAHIHI ZAIDI!

  Kwa kifupi kabisa naikubali hoja yako kuwa Mungu anaweza kabisa kumfundisha Mtu kila kitu kinachopaswa utumishi, na anaweza kwa kuwa yeye ni Mungu, Lakini kwa maneno yake katika Biblia ameonyesha kuwa hata watumishi aliowaita katika utumishi ilibidi KUWAFUNDISHA mambo mengine kupitia WATUMISHI WENGINE! alifanya kwa Musa! alifanya kwa Daudi! Alifanya hata kwa Paulo! Hata pia kwa Petro! Kwangu mimi naona ni VIGUMU MTU MMOJA KUIBEBA KWELI YOTE YA MUNGU! Hata tusugue magoti kiasi gani! Ndio Maana tumefanyika mwili mmoja, kila kiungo kwa mwenzake! na ndio maana Mungu katika Neno lake akaweka huduma ya WAFUNDISHAJI!
  WAFUNDISHAJI/WAALIMU wanaweza kufunuliwa na Mungu Kama Philipo na wakaja kutufundisha sisi! Kwa hiyo hata wale ambao Mungu hatawaita kwenda katika Chuo cha Biblia, itabidi wakae na kujifunza toka kwa wengine!Roho Mtakatifu atapenda kuwafunza KWELI HII siku kwa siku! Kitendo cha Mtumishi huyo wa Bwana kuingia tu kanisani na kumkuta Mtumishi mwingine anafundisha ujumbe wa Mungu, Kwake yeye ni chuo cha Biblia cha kutosha!Na inawezekana kwake ikawa ni njia nzurI AMBAYO BWANA ameamua kuitumia kuliko kujisajili chuoni rasmi! Ubarikiwe!

 10. Shalom,

  Binafsi ninajifunza ambayo nilikuwa siyajuwi kutokana na michango iliyoandikwa hadi sasa. Lakini pamoja na kujifunza huko nina swali:

  Je, kuna mpaka wa Roho Mtakatifu kumfundisha mtu ambapo zaidi ya hapo ni hadi mtu akajifunze chuoni? Yaani kama kuna mambo ambayo Mungu huwa hahusiki kumfundisha mtu moja kwa moja/privately hadi ajifunze chini ya mwingine?

  Ninauliza hivi ili kuweza kujua kama kuna mapungufu yoyote ambayo mtumishi aliyeamua “kusugua goti” ili Mungu amfundishe anaweza kuwa nayo ikilinganishwa na wale waliokwenda chuoni.

  Kama kuna mambo ambayo Mungu hawezi kumfundisha mtu hapo ndipo tunaweza kuona umuhimu wa kwenda chuoni kusoma. Lakini kama hakuna mambo ambayo Mungu hawezi kumfundisha mtu, yaani kama Mungu anaweza kumfundisha mtu kila kitu kinachompasa katika utumishi, basi kutakuwa hakuna umuhimu wa kwenda chuoni?

  Natanguliza shukurani zangu.

 11. bwana yesu asifiwe,wapendwa kwenda chuo kwa watumishi wa mungu, sio vibaya kwasababu wanajifunza mengi, ila inabidi wawe makini wasije wakaacha huduma zao,maana kuna mafundisho mengine yanapotosha.

 12. Wapendwa,

  Kama nilivyogusia kidogo hapo juu hatuendi chuo cha Biblia kupata ufundi wa kuhubiri tu la hasha! Ni kweli nina wito wa Mungu, nimemsikia Mungu akitaka nimtumikie, lakini pia katika huduma gani? Je ni Mchungaji?Je ni uinjilist! na kama ni Uinjilist je ni mashuleni? Vyuoni! Au kwa kuchapisha vitabu na Maandiko! Na kama ni Mchungaji Je nitumike katika kusanyiko gani/lipi? Kama ni hivyo lazima nipate kujifunza msisitizo/msimamo wa Kanisa langu ni upi, wanaamini nini,wana taratibu zipi katika mambo ya kuendesha ibada, ndoa, nk! Haya yote hata nikiwa na wito sitarajii kuamka asubuhi na kukuta nayafahamu.

  Mchungaji hafanyi kazi ya kuhubiri tu,anatakiwa kutatua matatizo ya waamimini,yaani matatizo ya kijamii, hivyo misingi ya saikolojia ya mwanadamu anabidi aifahamu, si lazima abobee,lakini atafanyaje counselling kwa watu mbali mbali walioumizwa maishani, ambao ni sehemu ya kondoo anao walea kiroho.Hivyo kwenda chuoni kunaweza kabisa kusiwe lazima lakini ni muhimu.

  Kwa kifupi mtenda kazi katika kizazi cha leo (Mtumishi wa Injili) Kwa upande wangu inabidi awe mwelewa wa vitu vya msingi, awe anaweza kuyatambua matukio ya kiuchumi na siasa yanayotokea ulimwenguni, anaujua ulimwengu unaomzunguka na kuhusianisha na Neno la Mungu, anajua ulimwengu uko wapi leo na unakwenda wapi kesho! (TRENDS) kama hazijui alama za nyakati katika kizazi chake ataweza kuhuubiri ujumbe ambao kila siku ni mpya kwa kila Kizazi!

  Na chuo cha Biblia huwa ni mahali pa kuwakutanisha watu wa Mungu pia, kujifunza toka kwa wengine, mawazo na uzoefu tofauti wa watu wengine walioisikia sauti ya Mungu kama wewe.

  Kwa kifupi kwenda Chuo cha Biblia hakikufanyi wewe kuwa wa Kiroho zaidi, la hasha, elimu ya kitu chochote inaweza kujenga kiburi! Kujifunza theology hakuwezi kunifanya nimjue Mungu moyoni, kunaweza kupanua ufahamu wangu kichwani lakini sio moyoni, naweza kujua historia ya Biblia na kujibu maswala magumu ya kitheolojia na ya imani, lakini moyoni nikabakia mtupu kabisa. Na kwa watu waliiokoka ni vyema toka awali wanatapotaka kwenda Chuoni kutambua ni chuo cha aina gani! Je Kina ukiri wokovu, kina mpya mtu nafasi ya kumruhusu Roho wa Mungu afanye kazi! Kina mpa mtu nafasi ya kuukulia wokovu! Kuishi maisha matakatifu, usipozingatia haya, wengi wamekwenda Bible College /Seminary na kurudi wameipoteza Imani!Wakavu na kubakia kufundisha hekima za wanadamu!

 13. Bwana Yesu asifiwe sana.
  Ninachoamini mimi ni kwamba, ili tuweze kuwa na mtumishi anayeweza kuhudumu vizuri msingi si kwenda chuoni bali ni kuwa na wito kwanza wa kumtumikia Mungu, kwani hata akienda chuoni kama hana wito atafanya huduma kama kazi nyingine yoyote. Mtu akiwa na wito wa kazi ya Mungu halafu akaongezea na elimu ya vyuoni atafanya kazi ya Mungu kwa ufanisi zaidi. Kwani katika vyuo vingine kuna theolojia zinazofundishwa ambazo kama huna msingi wa Neno la Mungu hata kiroho chako kinaweza kufa ukabakia fundi wa kuhubiri lakini ndani umekufa.

 14. Ili kuhubiri ni LAZIMA niende chuo cha biblia? Jibu ni Hapana, Kwani Mungu alitumia hata punda kufikisha ujumbe wake! Lakini Je MUHIMU kwenda kujifunza Biblia? Jibu ni ndio!

  Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66,na haikushushwa kama Quraan! Vitabu hivyo vimeandikwa na watu mbalimbali kwa lugha tofauti,mazingira tofauti, waandishi wakiwa na elimu tofauti wote wakiwa na ujumbe wa Mungu, ili kwanza kuziifikishia jamii zao (sio sisi) lakini Mungu akiwa na makusudi kila kizazi kuupate ujumbe huo.

  Sasa je si muhimu kukaa chini ukipata nafasi kujifunza kuhusu habari za kitabu hiki? Mpaka kuvipata hivyo vitabu 66 na kuviweka pamoja kuna watu walikaa chini kufanya kazi hiyo? Je hutapenda kujua ni akina nani? Lugha unayotumia wewe kuisoma Biblia yako sio ile ambayo iliandikwa toka awali! Je unahakika Biblia unayoisoma leo imebeba maana halisi kama yule aliyeandika mwanzo! Je ukipata nafasi ya kujifunza lugha zilizotumika awali? Je haitakufanya uhubiri ujumbe wako wa usahihi zaidi? Unapoisoma Biblia yako leo, imewekwa mistari, na sura kukusaidia kunukuu, Kumbuka kuna watu walikaa chini na kujifunza ili kukurahishia wewe!

  Biblia mpaka kukufikia mimi na wewe leo kama ilivyo imepitia safari ndefu mno!Mpaka kufikia kuitwa Neno la Mungu haikuwa kitu chepesi! Watu wamechomwa moto ili wasiitafsri na wala kuichapisha! Imeuzwa na kutengenezwa kama bidhaa ya magendo! Kuna vitabu vingi vilichujwa hadi kufikia unavyosoma leo! Je hupendi ukipata nafasi kujifunza juu ya Biblia!

  Na labda la msingi ni ujumbe wake! Tuna uhakika gani ujumbe tunaouhubiri ndio ule ule waandishi wa mwanzo wa Biblia walitaka tuujue! Ni ujumbe upi huo! Je kuna kanuni za kuutafsri ili tusiupoteshe? Hata mitume katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ilibidi wakae na wajadiliane kuona kama wanachohubiri na kufundisha ndicho hicho kweli?Inawezekanaje vitabu 66, kutoka kwa waandishi tofauti, ambao wengine baadhi yao hawafahamiani kabisa kuwa na ujumbe mmoja! Hii tu inakusukuma ukipata nafasi kukaa na kujifunza!au kwenda chuo cha Biblia!

  Na kwa muhubiri yoyote, ili afikishe ujumbe wake vyema, ni lazima kwanza aujue ujumbe vyema, ili asije akapeleka ujumbe mwingine ambalo ni MUHIMU SANA, lakini pia kuitambua jamii anayoipelekea Ujumbe! Kufikisha ujumbe tu ni somo linatotakiwa kufundishwa! Kuwahubiria vijana wa chuo kikuu wanielewe ni tofauti na wavua samaki wa ferry au wachimba kokoto kunduchi! hata kama ujumbe nao wapelekee ni ule ele! Ilimchukua Mungu miaka 1,500 akitumia watu wa kila aina, wasomi, wavuvi, wafalme, maskini, matajiri ili kuufikisha ujumbe kwetu wanadamu!

  Kwa kifupi ni MUHIMU kwenda kujifunza maneno ya Mungu, lakini si LAZIMA! kwani ujumbe wa Mungu ni yeye Mwenyewe anaupeleka! Sisi ni vyombo tu! Wengine ni vyombo vya udongo! Shaba! hata Dhahabu! Wengine wataitwa kuupeleka ujumbe huu kwa watu wanaostahili kuuelewe ukiwa katika vyombo vya udongo! Wengine watauulewa ujumbe huu ukiwa katika vyombo vya shaba! na wengine itabidi wapelekewe katika vyombo vya dhahabu!La msingi ujumbe umefika kama ulivyo na umetimiza KUSUDI LAKE!

 15. Naamini sio lazima. Kazi ya Chuo ni kuboresha huduma iliyo tayari ndani ya mtu. Hata hivyo,kama watu duniani wanasoma ili waweze zaidi kufanya kazi zao,ni muhimu kupata masomo ili kuifanya kazi ya Mungu ambayo ndio wito mkuu zaidi duniani. Lapili,ni muhimu kujua kuna shule rasmi na shule zisizo rasmi. Yesu aliwapa wanafunzi wake masomo ingawa haikuwa shule kama tunavyozifahamu leo; Eliya pia alimfundisha Elisha huduma nje ya darasa ingawa wakati wake kulikuwa na shule ya manabii,(2 wafalme 1 & 2)

 16. bw. asifiwe! kwenda kusoma siyo lazima ila inasaidia katika utumishi kujifunza zaidi lakini wako watumishi ambao hawajasoma theolojia na Mungu anawatumia kwa kiwango kikubwa kuliko hata waliosoma mpaka ngazi za juu za theolojia!

 17. Bwana Asifiwe!
  Ukweli ni kwamba sio lazima japokuwa ni vizuri kwenda kusoma ili kumjua vizuri Mungu unayetegemea kuhubiri habari zake. Hiyo ndiyo sababu kubwa inayofanya watumishi wa Mungu kwenda kusoma kwenye vyuo vya Theolojia

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s