Upi ni wakati sahihi kuanzisha mahusiano?

Mimi ni kijana ambaye NAMJUA MUNGU, naomba leo nijitokeze kuuliza juu ya wakati upi ni sahihi wa kuanzisha uhusiano/ kutafuta mchumba?

Je, niangalie kigezo cha umri peke yake kwamba kuanzia miaka 25 kama  ni mvulana? kumbuka life expectancy ya Tanzania ni miaka 45 kama sijakosea. Niangalie economic status yangu kwa wakati huo?

Lutengano

Advertisements

16 thoughts on “Upi ni wakati sahihi kuanzisha mahusiano?

 1. yani nimebarikiwa sana kwa makala hii nimejifunza vingii sana.ubarikiweee sana kwa majibu mazuri

 2. kweli kabisa tunatakiwa kumtegemea mungu maana kwa akili zetu hatuwezi lolote yeye aliye nena na ezekiel juu ya mifupa mikavu atafanya njia

 3. MBARIKIWE SANA NIMEIPENDA BLOG HII, PENDEKEZO LANGU ZIWEPO HOJA NYINGI ZAIDI, ZIKIWEMO KUHUS VIJANA, MAANA ULIMWENGU HUU, PAMOJA NA UTANDAWAZI HUU VIJANA WENGI NDIO WANA KABILIWA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA, MIMI PIA NI KIJANA. AHSANTE.

 4. MIRADI MUHIMU KWA KILA MTU KUFANYA MAISHANI MWAKE

  Maelezo haya pia yanajibu swali lililoulizwa na ndugu anaitwa Lutengano akiuliza hivi:

  “Mimi ni kijana ambaye NAMJUA MUNGU, naomba leo nijitokeze kuuliza juu ya wakati upi ni sahihi wa kuanzisha uhusiano/ kutafuta mchumba?

  Je, niangalie kigezo cha umri peke yake kwamba kuanzia miaka 25 kama ni mvulana? kumbuka life expectancy ya Tanzania ni miaka 45 kama sijakosea. Niangalie economic status yangu kwa wakati huo?”

  Baada ya kusoma swali hili pamoja na majibu niliyoyatoa wali nimeona niwape wapendwa wote maelezo yanayohusu Miradi muhimu maishani ambayo mtu akijiepusha kuifanya maisha yake yote yanakuwa ya mashaka siyo kanisani tu hata katika jamii iliyomzunguka.

  1. MRADI WA KUOA AU KUOLEWA
  Huu ni mradi wa kwanza unaotakiwa kufanywa na vijana wenye umri kati ya miaka 25-35. Mradi huu ukiufanya nje ya umri huo ni dhahiri kuwa maisha yako ya mbele yatakuwa magumu. Kuoa na kuolewa ninaviita kuwa ni mradi kutokana na gharama zinazoambatana na shughuli yenyewe.

  Shughuli za kuoa na kuolewa ni Mradi uwezao kugharimu pesa nyingi au kidogo kutegemea na mazingira na wahusika. Siyo busara kukaa muda mrefu bila kufanya uamuzi wa kuoa au kuolewa ukingali na umri unaofaa.

  Kuchelewa kuoa au kuolewa ni dalili mbaya kwamba huenda na maisha yako ya uzeeni yakawa magumu. Kwa mfano kama utaoa au kuolewa una umri wa miaka 38 au 40 na kuanza kuzaa watoto baada ya umri huo, ni dhahiri kuwa watoto wako huenda ukawaweka katika maisha magumu baadaye na kusababisha kizazi chote kitakachokufuata kuishi maisha ya taabu kiuchumi na kijamii.

  Fanya uamuzi wa busara. Amua mapema kuoa au kuolewa. Jiandae na kuishi maisha ya raha na ya ufahari kwa kuoa au kuolewa kabla hujavuka umri wa miaka 30 .

  2 MIRADI YA KUSOMESHA WATOTO
  Baada ya kuoa au kuolewa kifuatacho ni kuzaa watoto. Kuzaa siyo kazi. Kazi kulea. Kila unapozaa mtoto unapaswa kuelewa kuwa huo ni mradi umeanzisha ambao utapaswa kuusimamia kwa zaidi ya miaka 20 kwa kuwekeza fedha nyingi tangu mimba ilipotungwa hadi mwaka wa 21 kwa kila mtoto.

  Kazi ya kusomesha watoto tuliowazaa huwa ndio mradi mkuu katika maisha unaotafuna wazazi wengi wenye uchungu na maisha ya watoto na kizazi chao kitakachoendelea. Kuzaa huenda ndiyo miradi inayohitaji fedha nyingi zaidi ya miradi yote katika maisha.

  Kama ilivyo katika miradi ya kawaida, miradi ya kusomesha watoto huleta faida au hasara kwa mwenye miradi kutegemeana na usimamizi alionao na sera za nchi kuhusu elimu kwa ujumla. Mtoto anapaswa kusoma hadi kiwango kitakachomwezesha kujitegemea kifedha na kiuchumi.

  Ukihesabu gharama ya kumsomesha mtoto kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu, huenda ukafikiria upya idadi ya watoto unaowataka. Na kama tayari unao watoto zaidi ya 4 huenda unasikitika au kuwaza kila mara ni jinsi gani watoto hao utawafikisha chuo kikuu. Huu ni mradi mkubwa unaohitaji fedha nyingi kuutekeleza.

  Mpendwa elewa kwamba Miradi ya kusomesha watoto unapaswa kuifanya uwapo kati ya umri wa miaka 25 na 40. Ukitimiza miaka umri wa 41 hupaswi kufikiria tena kuzaa watoto. Kwa mfano, Ukizaa mtoto ukiwa na umri wa miaka 42 uelewe kama wewe ni mfanyakazi wa kuajiriwa utastaafu ikitimiza miaka 60 mtoto akiwa na umri wa miaka 18. Huenda mtoto huyo akashindwa kuendelea na elimu ya juu kwani pato lako litashuka kutokana na kustaafu. Hata kama umejiajiri, ukitimiza miaka 60 hutaweza kufanya kazi za kipato kikubwa kama unavyofanya sasa.

  Usikubali mke wako kubeba mimba wewe ukiwa na umri zaidi ya miaka 40 au yeye akiwa na miaka zaidi ya 35..

  2. MRADI WA KUJENGA NYUMBA YA KUISHI

  Kumbuka kuwa maisha ni nyumba. Bila nyumba hujawa na maisha. Epuka kuishi nyumba za kupanga kwa muda mrefu bila kujenga nyumba yako. Kama wewe ni mtumishi wa serikali au kanisa na cheo chako kinakuruhusu kuishi nyumba ya kanisa au serikali, tumia fursa hiyo kujenga nyumba yako. Usibweteke. Usijisahau. Umri unakwenda na utajikuta huwezi tena na umri wa kustaafu unakaribia.

  Unashauriwa kuanza Ujenzi wa nyumba ukiwa kati ya umri wa miaka 30 na 50. Ukitimiza umri wa miaka 50 ukiwa hujajenga mpendwa maisha yako ya uzeeeni ni magumu.

  4. MRADI WA KUJENGA NYUMBA ZA BIASHARA

  Wapendwa miradi hii ni mizuri sana. Wengi siku hizi hasa wale wenye viwanja kandoni mwa barabara za mitaa yetu hujenga nyumba za kupangisha wafanya biashara. Ni miradi mizuri ya kibiashara na kiuchumi.

  Hata kama wewe ni Pastor Itakusaidia kuinua hali yako kifedha badala ya kutegemea waumini wako watoe sadaka ndipo mkono uende kinywani.

  Katika swala hili waweza kuanzisha Miradi kama vile: maduka ya kupangisha wafanyabiashara, nyumba za kupangisha makazi, nyumba za kulala wageni, zahanati, kituo cha afya, hospitali, shule ya awali, shule ya msingi, sekondari au chuo. Miradi mojawapo ya hiyo ukiifanya kwa utaratibu waweza kuimaliza ukiwa na umri wa miaka 55.

  Kwa mfano ukijenga nyumba tatu zenye za kupangisha zenye uwezo wa kuingiza Shs 150,000 kila moja kwa mwezi utakuwa na uhakika wa kupata Tshs 150,000 x 3 = 450,000 kila mwezi nje ya pensheni utakayopata toka mashirika ya pensheni kama NSSF, LAPF, PPF au PSPF baada ya kustaafu kwa wale ambao ni wafanyakazi wa serikali au wachangiaji wa mifuko hiyo waliojiajiri.

  5. MIRADI YA MASHAMBA YA MITI YA MATUNDA/MBAO/BIASHARA

  Upandaji wa miti ya mbao au biashara mbalimbali inaweza kuinua maisha ya mtu akiwa amestaafu au hata kabla. Usimamizi wa miradi hii siyo wa gharama kubwa. Gharama huwepo katika hatua za mwanzo tu.

  Wafanyakazi za kuajiriwa wanaweza kutumia fursa ya likizo ya kila mwaka kupanda miti katika mashamba yao. Ukipanda shamba la miti ipatayo 10,000 ukiwa na umri wa miaka 40 unatarajia kuwa utimizapo umri wa kustaafu miaka 60 miti hiyo itakuwa imekomaa na kuwa na uwezo wa kutoa mbao na matunda.

  Miti mingi ya matunda huanza kutoa matunda ndani ya miaka mitano (5) kwa mfano miti ya machungwa, parachichi, pasheni, nk. Miti ya mbao iko ya aina nyingi kama vile; greveria, karatusi, misonobali, nk. Kumbuka kuwa mti mmoja waweza kutoa mbao zipatazo 10 hadi 50 kutegemeana na ukomavu wa mti. Je, mbao zina bei gani kwenu au hapo mijini unapoishi?

  Je, Ukistaafu kazi uliyo nayo utakuwa maskini? Je utaishi maisha ya ombaomba kama una shamba lako la miti ya matunda na mbao au kuni? Ukiweka lengo la kupanda miti mbalimbli kwa miaka mitano au kumi kuanzia sasa unaweza kupanda ipatayo 10,000 kabla ya kufikisha umri wa miaka 55. Huu ndio uwekezaji ambao hautakuletea majuto ukistaafu.

  6. MIRADI YA MASHAMBA YA MAZAO YA KUDUMU

  Siasa ya Tanzania kwa sasa inakazia kauli mbiu ya KILIMO KWANZA. Kauli hiyo siyo kwamba haiwahusu wapendwa na wafanyakazi waliojiajiri katika biashara au kuajiriwa na serikali au sekta binafsi.

  Kama ukijiwekea utaratibu wa kununua mashamba na kufanya mipango ya kuyatunza kila mwaka au kila mwisho wa wiki, kwa kupanda miti ya matunda, mazao ya kudumu kama vile kahawa, migomba, katani, machungwa, limao, ndimu, stakaferi, pasheni, michikichi, minazi, maembe, nk. Nakuhakikishia kwamba hutaishi maisha ya kubahatisha kama ndege wa angani Mungu asipowapa chakula hawali na asipowapa mavazi wanatembea uchi.

  Watu wengi wakifikia umri wa uzeeni huwa hawapendi waondoke kazini walipokuwa wameajiriwa. Hii husababishwa na kuwa hawakujiandaa vya kutosha kabla ya kustaafu.

  Miradi ya Kilimo cha mazao ya kudumu yaweza kufanywa na mtu yeyote hata kama ana kipato au mshahara wa Tshs 200,000 kwa mwezi. Shamba linalotakiwa siyo lazima liwe la ekari mia moja.

  Hata ekari moja tu unaloweza kununua kwa mwanakijiji mmoja kwa Tshs 50,000 laweza kutosha kukupa maisha bora sasa hadi uzeeni. Fanya KILIMO KWANZA kiwe chaguo lako la kwanza kwa kulima na kupanda mazao yatakayoongeza pato lako kwanza kabla na baada ya kuzeeka.

  Hitimisho:
  Kutokana na kwamba watu wengi huwa hawaoni mbali hulazimika kuishi maisha yenye kubahatisha na kujikuta wakidhani wataokolewa kwa kucheza bahati na sibu za taifa au za kwenye simu zinazoendeshwa na makampuni ya simu.

  Ukweli ni kwamba hakuna mtu aliyetajirika kwa kucheza bahati nasibu.

  Kumbuka kama nilivyotangulia kufafanua awali, kila kipindi ni muhimu kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.

  Haifai kuanza kutafuta Mchumba wakati una miaka 15 hadi 22. Umri mzuri kama nilivyosema ni ule wa kuanzaia 25 ukiwa umeshaanza kupevuka kimawazo na umemaliza mihemuko yote ya ujana. Umri huu ndipo unakuwa umepita kipindi wanachosema wengine kuwa ni barehe ya pili kupita.

  Vijana wa kike na kiume wanashauriwa kuwa na urafiki usioelekea katika mahusiano ya ngono wa ndoa wawapo katika umri chini ya miaka 25. Pia wanashauriwa kujiepusha na utamaduni wa kudhani kwamba mwenza mwema ni yule anakubali mfanye ngono kabla ya ndo. Jiepushe kabisha kufanya ngono kabla ya kuingia katika ndoa. Naelewa kwamba Ulaya na Amerika swala hili lilishahalalishwa hata makanisani. Hapa Tanzania linakuja kwa kasi ya kutisha. Sijui tutapona au tutaangamia.

  Kikubwa cha kukumbuka unapomaliza kusoma mada yangu hii ni kwamba mahusiano ya kutaka kupata mwenza wa ndoa si jambo gumu sana wala lenye mitihani mikubwa sana kiasi cha kudhani kwamba lazima ufunge upande milimani kuomba na kufunga.

  Kumbuka kuwa Wanawake na wanaume wote wako sawa. Kinachotakiwa wewe ni kuoa au kuolewa na “UMPENDAYE” bila kijali hali yoyote aliyo nayo. “UMPENDE SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO” .

  Epuka kukaa zaidi ya miaka 3 eti unachumbia au unachunguza mwenendo wa mwenza wako mtarajiwa. Huo ni utoto. Kukaa kipindi kirefu bila kufunga ndoa eti mnachunguzana ni utoto unaowapeleka kutenda dhambi hatimaye.

  Mimi nashauri mara nyingi kuwa uchumba hadi ndoa visizidi miezi 24 baada ya hapo mchakato wa kufunga ndoa uanze. Mfano ukianza kuchumbiana na mtu ukiwa na umri wa miaka 25 nategemea kuwa utafunga ndoa ukiwa na miaka 27 mwanaume. Mwanamke anaweza kuanza kukubali kuchumbiwa akiwa na umri wa miaka 22 na kuoelewa akiwa na miaka 24 au 25.

  Kuanza kuchumbiana ukiwa na miaka 18 au 20 mkaendelea hadi mkatimiza 27 au 30 ndipo mkafunga ndoa itokee hivyo kwa bahati mbaya tu siyo kwa kupanga. Wote waliofanya hivyo waliacha ushuhuda mbovu mitaani au makanisani.

  UBARIKIWE SANA.

 5. VIPINDI MUHIMU VYA MAISHA AMBAVYO HUPASWI KUFANYA MAKOSA

  Mpendwa unayesoma maelezo yangu haya nakuomba usichoke kusoma hadi mwisho. Nakuhakikishia kuwa utakosa mengi endapo utashindwa kusoma maelezo yangu haya hadi mwisho yanayojaribu kutoa jibu kwa msomaji wa blog hii aliyeuliza; Nanukuu swali:

  “Mimi ni kijana ambaye NAMJUA MUNGU, naomba leo nijitokeze kuuliza juu ya wakati upi ni sahihi wa kuanzisha uhusiano/ kutafuta mchumba?
  Je, niangalie kigezo cha umri peke yake kwamba kuanzia miaka 25 kama ni mvulana? kumbuka life expectancy ya Tanzania ni miaka 45 kama sijakosea. Niangalie economic status yangu kwa wakati huo?”
  Wapendwa katika maisha haya kuna vipindi ambavyo kila mtanzania anapaswa kuwa makini asifanye makosa. Ukifanya kosa linakuwa chanzo cha maumivu makuu maisha yako yote kiroho na kimwili hadi utakapoondoka duniani. Fuatana nami katika ufafanuzi wa kujibu swali hilo la mpendwa wetu na wasomaji wengine pia wanaofuatilia majibu ya maswali kupitia blog yetu hii. Nimegawanya vipindi vya maisha ya mwanadamu kwa kufuatana na umri. Majibu ya swali utayapata kadri unavyosoma mada hii hadi mwisho. Karibu twende pamoja.

  UMRI WA MIAKA 00- 06 :

  Kila mtu anapaswa kupata malezi bora toka kwa wazazi/walezi wako, soma chekechea, Sunday school, kwaya za watoto kanisani, nk.

  UMRI WA MIAKA 07-14

  Kila mtu anapaswa kupata elimu ya msingi na wala usifanye uzembe wala asifanye visingizio vya kumfanya aikose. Kukosa elimu ya msingi ni kosa kubwa maishani mwako.

  UMRI WA MIAKA 15-20

  Kila mtu anapaswa asome sekondari kama hakubahatika kwenda sekondari basi ni muhimu sana kupata hata elimu ya kati kama vile VETA, Vyuo vya ufundi, utalii, kompyuta, biashara, udereva, nk).

  UMRI WA MIAKA 21- 25

  Unatakiwa upate elimu ya juu na usome kwa bidii, au jiajiri mwenyewe kama hauko chuoni, ukimaliza masomo tafuta ajira, pata kazi ya kufanya yenye kipato kisichopungua shs 3000 kwa siku. Tafuta nyumba ya kupanga angalau chumba cha Shs 500/ kwa siku au shs 1000 kwa siku.

  UMRI WA MIAKA 25-30:

  Huu ndio umri haswaa wa kuanza kujihusisha kutafuta marafiki au mke/mume mtarajiwa. Ukitafuta mke/mume katika umri chini ya hapa. Utakuwa unajipachika majukumu yasiyokuwa ya kwako. Unajihatarishia maisha yako ya baadaye.

  Katika umri huu anza kuwa na uhusiano na watu wa jinsi tofauti na yako ili kuweza kujipatia mweza wa maisha yako. Anza kutafuta Mchumba au mke/mume toka kokote utakakopendezwa moyo wako. Kuna njia nyingi za kupata mke au mume. Njia kubwa inayotumika kote ulimwenguni ni KUMPENDA MOYONI. Hata kama ukifunuliwa katika njozi au maono au unabii, KIPIMO SAHIHI NI KUMPENDA MOYONI MWAKO wala siyo kigezo kingine chochote. UPENDO WA KUELEKEA KATIKA NDOA, HUWA NI ULE UNAOTOKEA KUMPENDA MTU BILA KIGEZO CHOCHOTE AU KITU FULANI KUTANGULIA, Mfano pesa, mali, uzuri wa sura, sauti, maumbile ya mwili, kabila, ukoo, taifa, nk. Ukimpenda mtu kwa sababu ya kuona mojawapo ya vigezo hivyo, HUO SIYO UPENDO WA NDOA, NI TAMAA YA MWILI. Mfano ukimpenda mtu kisha ukaulizwa umempenda nini nawewe ukajibu nimempenda kwa jinsi anavyoimba sauti nzuri katika kwaya, au ninampenda jinsi anavyotembea, ongea yake, upole wake, macho yake meupe, umbo lake namba nane, kwao wana uwezo kiuchumi, nk, ELEWA KWAMBA HUO SIO UPENDO WA KIMUNGU WALA KI-NDOA.

  Ndani ya kipindi hicho hakikisha umepata mke au mume wa maisha yako. Usifanye makosa katika umri huu. Hii ni Amri. Utanielewa baadaye kwa nini nasema ni Amri. Wote waliokosea kuoa au kuolewa wakiwa katika kipindi hiki wana majuto ambayo nitayasema baadaye. Ukisha pata mwenza wako, anza kuzaa watoto. Anza kufanya utaratibu wa kupata kiwanja cha kujenga nyumba yako ya kudumu ili uondokane na maisha ya kupanga nyumba za watu.

  UMRI WA MIAKA 30- 40.

  Endelea na kuzaa watoto. Mimi huwa nashauri watu wasizidishe watoto wanne. Ukifikisha umri wa miaka 40 mimi nashauri wateja wangu na wapendwa wenzangu wafunge kuzaa kabisa. Najuma mada ya kufunga kuzaa inakuwa na malumbano makubwa makanisani lakini mimi huwa ndio msimamo wangu. Biashara ya kuzaa watoto achana nayo. Achia vijana waendelee kuzaa. Wewe ng’atuka katika huduma hiyo.

  Katika umri huu pia hakikisha kuwa hufikishi umri wa miaka 40 ukiwa bado hujajenga nyumba yako ya kuishi. Piga ua galagaza. Jenga nyumba yako. Ondoka nyumba za kupanga. Ishi na mwenza wako na watoto katika nyumba yenu binafsi.

  Katika umri huo pia anza kufikiria kufanya miradi ya kudumu kama vile mashamba ya mazao ya kudumu mfano, miti ya mbao, miti ya matunda maembe, chikichi, minazi, parachichi, michungwa, migomba, mikaratusi, nk. Kumbuka miradi hii unatakiwa kuwa nayo kama maandalizi ya kuelekea uzeeni ambako hutakuwa na nguvu tena za kufanya kazi. Miradi hiyo ndiyo itakuwa inakulipa pensheni uzeeni. Kumbuka utamaduni wa kudhani kuwa watoto wetu ndio watakaotulea uzeeni umepitwa na wakati. Kila mtu anahangaikia maisha yake. Umri huo ndio wa kutafuta mashamba na miradi ya maana ili kuiendeleza familia yako kiuchumi.

  Ndani ya kipindi hiki pia waweza kujiendeleza kielimu zaidi. Waweza kusoma digrii ya pili hadi ya tatu (Masters and Phd Degree courses) hii ni kwa wale waliofanikiwa kusoma hadi vyuo vya elimu ya juu na kupata shahada ya kwanza. Kwa wale ambao hawakupata shahada ya kwanza wanaweza kujiendeleza pia hadi wakapata shahada ya kwanza mpaka ya tatu(PhD) kama wana uwezo wa kiuchumi. Kutokujiendeleza kielimu ni kujiweka katika nafasi ya kuachwa nyuma kimaendeleo na wale wanaojiendeleza.

  UMRI WA MIAKA 40 – 50

  Funga kuzaa kabisa mara tu unapotimiza miaka 40. Wapendwa wengi huwa hawakubaliani na hoja hii lakini mara nyingi ni wale wasiokuwa na macho ya kuona mbali. Kisayansi na kiimani pia umri huu ndio mzuri wa kuacha kuzaa. Wanandoa wanapoacha kuzaa katika umri huu wanapata fursa nzuri ya kufanya au kusimamia miradi ya uchumi wa familia zao. Kwa wale wanaotaka kumtumikia Mungu ni wakati mwafaka. Kumtumikia Mungu kwa njia za Uinjilisti, kwaya, bendi, uchungaji, uaskofu, nk wakati huu ndio mzuri sana.

  Wanandoa katika kipindi hiki ndipo wako huru kufurahia penzi lao katika ndoa yao. Lakini pia kuzaa watoto ukiwa umepitiliza miaka 40 unajiweka katika wakati mgumu wa kuwatunza watoto wako utakao wazaa ukiwa na miaka labda 44 au 48 au 50.

  Kwa nini tusisitize watu waache kuzaa wakiwa katika umri zaidi ya 40. Ukiacha sababu za kibayolojia ambapo mwanamke anashauriwa kucha kuzaa akiwa na umri wa miaka 35 na mwanaume miaka 40, watoto wote utakaowazaa ukiwa na umri wa miaka kuanzia 41 watashindwa kupata uangalizi wako kiuchumi watakapokuwa ndipo kwanza wanapouhitaji hasa katika maswala ya elimu na mitaji ya kuanza kujitegemea. Hii hasa inawagusa wafanyakazi serikalini na katika makampuni binafsi ambapo kisheria lazima wang’atuke kazini kwa lazima wakitimiza miaka 60. Endapo utazaa watoto ukiwa na umri wa miaka 48 au 55 utastaafu kazi ukimwacha mtoto wako yupo chekechea au shule ya msingi. Kumbuka watu wakishastaafu kazi huwa hawana mshahara tena wa kutosha kusomesha watoto wao na wao wenyewe kujitegemea kiuchumi. Kwa hiyo nawashauri wale ambao ni wafanyakazi walioajiriwa hata waliojiajiri wajue kuwa ukishatimiza umri wa miaka 50 mtoto utakayemzaa utakujakustaafu akiwa hajavuka hatua yoyote ya kimaendeleo. Miaka 60 hata kama umejiari ni umri unaopaswa kupumzika uendelee kula pensheni uliyojiwekea katika miradi yako.

  Unapotimiza miaka 50 hakikisha una mradi hata mmoja umeshaanzisha ambao ni wa kudumu. Hapa sizungumzii miradi kama ya kuuza duka au vinywaji au vyakula. Hii siyo miradi ya kudumu. Miradi ya kudumu nimeifafanua hapo juu.

  Hata kama wewe ni mchungaji (Twety four hours full time God’s servant) unapaswa kuwa na miradi yako ya kudumu. Utamaduni wa kutegemea ruzuku za kutoka kwa waumini wanapotoa zaka au sadaka mimi sikubaliani nao kwani huo ulikuwa wa Agano lake kwa Makuhani ambao walizuiliwa hata kuwa na urithi wa ardhi au nyumba na mashamba. Lakini Agano Jipya lasema sisi sote tumekuwa makuhani wa Mungu.

  UMRI WA MIAKA 50 – 60

  Huu ni umri wa kuanza kutafakari ulikotoka na unakokwenda. Fanya tathmini ya miradi yako. Simamia kwa uangalifu mkubwa kwani hii ndiyo tegemeo lako la uzeeni. Kipindi hiki unapaswa kuhakikisha kuwa watoto wako wote wamemaliza elimu ya juu. Mtoto wa kwanza uliyemzaa ukiwa na miaka 30 hapa atakuwa anatimiza miaka 30 ya umri wake. Huyu atakuwa ameshaanza kujitegemea. Mtoto wako wa mwisho uliyemzaa ukiwa na umri wa miaka 40 atakuwa anamaliza elimu ya chuo kikuu akiwa na miaka 20.

  UMRI WA MIAKA 60 – 75

  Huu ni umri wa kufanya ziara za kwenda nje ya nchi, kutalii Isreali, Ujerumani, Korea, Marekani, mbuga za wanyama, visiwani, nk.

  Huu ni umri wa kupumzika na kufurahia uzee. Huu ni umri ambao hupaswi kuwaza kabisa nitakula nini leo au kesho.

  Huu ni umri ambao wewe unapaswa kuwa Mshauri wa vijana na watu wazima wanaoelekea uzeeni. Mimi nashauri hata kama ni Mchungaji au Askofu akitimiza umri wa miaka 65 ang’atuke uongozi wa kiroho awape wengine waendeleze kazi aliyoianzisha. Utamaduni wa kung’ang’ania hadi unafia madhabahuni kwa sababu za uzee ni utamaduni usio na tija. Rithisha kazi kwa wengine wewe ukae ukiwapa ushauri wa kiuzoefu na kitaalam.

  Kwa upande wa wanasiasa, nawashauri wakitimiza miaka 65 iwe kabisa ni mwisho wa kujishughulisha na kazi za siasa. Haifai kuona wazee wetu wakifanya kazi ambazo zingefanywa na vijana. Wazee wetu wengine hushangaza watu wawapo bungeni au katika majukwaa ya siasa huishia kusinzia kwenye viti wawapo katika vikao muhimu vya maamuzi. Kwa nini unajichosha hivyo katika taifa ambalo zaidi ya 50% ni vijana wenye umri chini ya miaka 40 ? Pumzika waachie wengine wafanye kazi.

  Kwa upande wa wasomi, hasa walimu wa vyuo vikuu, napendekeza wapumzike kazi za kufundisha wakishatimiza miaka 60 wabakie kuandika vitabu na machapisho na kushiriki makongamano ya kitaaluma na kitaalam. Tabia ya kung’ang’ania kufundisha haifai katika zama hizi.

  UMRI WA MIAKA 75-100

  Endelea kuishi kwa kula mema ya nchi. Upuka kazi zenye kukupa msongo wa mawazo. Jiuzulu kazi zote za kuongea na waandishi wa habari, acha kuhubiri mikutano midogo na mikubwa iwe ya Injili au kijamii. Pumzika masaa mengi bila kusahau kujifanyia mazoezi ya mwili.

  Endelea kula muda wa ziada toka kwa Mungu kwani Biblia imesema , kama tukiwa na nguvu miaka yetu ni themanini (80) vinginevyo mwisho ni 75.

  HITIMISHO NA MAONI

  Bila shaka mada hii imetoa mwanga na mwelekeo ambao walioajiriwa hata wasiokuwa waajiriwa wa serikali wanaweza kufuata ili kujipatia maisha bora kabla na baada ya kustaafu ajira.

  Kwa ufupi napenda kusisitiza mambo muhimu hapa kama ifuatavyo;
  • Hakikisha unafanya mambo yanayolingana na kipindi cha maisha ulichomo kama ilivyoelezwa katika kila kipengere cha mada hii kuhusu vipindi vya umri na mambo yakupasayo kufanya.

  • Usifanye makosa yatakayoleta majonzi yasiyokoma moyoni kwa kukosea kufanya yakupasayo kufanya kwa kipindi cha umri wako wa sasa.

  • Usibweteke na kiwango chochote cha mshahara au kipato chako cha sasa. Wala usijifariji kuwa kiinua mgongo cha mifuko ya pensheni hata kingekuwa kikubwa kivipi kwamba kitatosha maisha yako ya uzeeni kama umajiriwa. Hakikisha una mradi wa kiuchumi utakaochangia pato lako la uzeeni kutoteteleka hadi utakapoingia kaburini.

  • Pamoja na kwamba dini na tamaduni zetu zinafurahia kuzaa watoto wengi kwa hoja ya kuujaza ulimwengu, au kuoa wake wengi kwa misingi ya dini au utamaduni, kwa maoni yangu, na kwa kuzingatia sera ya serikali ya Tanzania inayotambua watoto wasiozidi wane(4) mtumishi wa umma hata mwananchi wa kawaida inafaa asizae watoto zaidi ya wanne (4) maishani mwake. Umri wa kuzaa usizidi miaka 40.

  • Kila mtumishi wa Mungu, watumishi wa serikali, waumini wa makanisa yote, kila mmoja awe na mradi wake ama kijijini/Mjini kwao, ili mradi uwe mradi ambao hausumbui kusimamia kama nilivyofafanua awali. Watumishi wa Mungu, wachungaji na maaskofu ni muhimu sana kuwa na miradi inayowaingizia kipato mbali kabisa na zaka na sadaka.

  • Kama una umri wa miaka kati ya 25 hadi 30 hakikisha umepata mwenza wa maisha yako. Achana na utamaduni wa kuishi peke yako. Hata kama una kipato cha kutosha(hasa wanawake) amua kuolewa. Achana na kudhania kuwa maisha ya ndoa ni mateso au karaha. Funga ndoa mapema. Anza kuzaa watoto mapema (endapo kizazi chako hakitakuwa na shida yoyote). Zaa watoto wanaolingana na uwezo wa kipato chako.

 6. BWANA YESU ASIFIWE!

  Watumishi wa MUNGU napenda kuwapa moyo juu ya utumishi wetu tulionao.Unajua tunayemtumikia ni mkuu nanimwenye mamlaka makubwa sana.
  Sasa naomba kila asomaye ujumbe huu atambue kuwa ipo nguvu kubwa ya MUNGU ndani yake na inatenda kazi kwani mamlaka aliyonayo YESU naya alitupatia sisi pia
  Hebu ona mamlaka tuliyo nayo sasa YOHANA 14:12-14 na MATHAYO 18:18.Jamani oneni raha.
  Pia kazi yetu (assignment) ni ndogo tu,hebu ione
  YOHANA14:15 na KUMBUKUMBU LA TORATI 28:1-2 na utabarikiwa zaidi ukisoma mlango wote wa 28.
  MUNGU AWABARIKI na tuelekee mbinguni

 7. BWANA YESU ASIFIWE!

  Watumishi wa MUNGU napenda kuwapa moyo juu ya utumishi wetu tulionao.Unajua tunayemtumikia ni mkuu nanimwenye mamlaka makubwa sana.
  Sasa naomba kila asomaye ujumbe huu atambue kuwa ipo nguvu kubwa ya MUNGU ndani yake na inatenda kazi kwani mamlaka aliyonayo YESU naya alitupatia sisi pia
  Hebu ona mamlaka tuliyo nayo sasa YOHANA 14:12-14 na MATHAYO 18:18.Jamani oneni raha

 8. Shalom mpendwa!!

  Nianze kwa kukupongeza kwa kuuliza swali kama hilo, maana ni jambo linalosumbua vijana wengi hivi leo.

  Kuhusu wakati au umri wa kuanza mahusiano inategemea uelewa wa mtu binafsi wa nini maana ya mke(ambaye huanzia kwenye uchumba) kutokana na elimu aliyoipata katika makuzi yake.Mana katika jamii nyingi mke anaonekana ni chombo cha sterehe,mtu mwingine anataka kuoa ili awe na familia kama jambo la kifahari na mengine mengi.Lakini kumbuka biblia katika kitabu cha mwanzo mungu alimpatia Adam msaidizi ambaye ni hawa.Hii inamaanisha mungu aliona si vema kumwacha Adam peke yake na majukumu aliyompa kwa hiyo akampa hawa awe msaidizi wake.Kwa mantinki hiyo kuna kipindi utafikia wakati kama kijana unahitaji mweza ambaye ni msaidizi wako kama biblia isemavyo ili muweza kutimiza majukumu uliyo nayo.Mke ni msaidizi,kwa kutambua hilo wakati kuanza mahusiano hufikia wenyewe, kwamba kwa hali uliyo nayo wakati huo unahitaji msaidizi(mke).Automatically utaanza chakato wa kutafuta mchumba kwa uongozi wa utatu mtakatifu.Mara nyingi hali huja baada ya mtu kuweza kujimudu yeye mwenyewe mfano kwa wanaosoma ni baada yakusoma na kuwa na career fulani.

  Kwa uelewa zaidi wa jambo hili, kama wewe ni mpenzi wa kusoma vitabu tafuta kitabu kiitwacho “Marriage & Family The missing Dimension” ..ubarikiwe!!

 9. SHALOM MPENDWA!
  imeandikwa MITHALI 24:27
  “Tengeneza kazi yako huko nje,Jifanyizie kazi yako tayari shambani,Ukiisha,jenga nyumba yako.”

  God bless you!

 10. Jina la Bwana libalikiwe!
  Napenda kuongelea kwa upande wa vijana wa kiume tu.
  kwa hali ya sasa hivi mara nyingi utatakiwa uwe na kipato au chanzo cha kipato pamoja na mazingira ya kuishi na mke uwe umeyaandaa. Vilevile unaweza kuwa na umri kuazia hata miaka 22.

 11. do,vijana!! nadhani Roho mtakatifu apewe nafasi katika hili. si jambo rahisi kuse ni hivi au ni vile. inategemea sana mtu, na Mungu. kunao walioanza mahusiano ya muda mrefu sana yakazaa ndoa nzuri na wengine mafupi na ndoa nzuri pia na vice versa. uchumba wangu ulienda miaka mitatu,ila nilimpenda miaka mitatu kabla sijamchumbia kwa ajili ya kumthibitisha Bwana. ndoa ni jambo jema na uchumba mzuri mara nyingi huzaa ndoa nzuri. nafikiri uchumi sio (factor) kigezo sana,ila afya ya kiroho,ki hisia na ki jamii(social). hivi vitatu ni muhimu ili kuweza kuibeba familia itakayozaliwa na uchumba wako. katika haya matatu, usipojiweza mwenyewe,utaweza kuwabeba wengine na kuwasaidia wa familia yako? jambo lingine,ujimudu katika u wewe mwenyewe(singleness).watu wengi walishindwa na kumudu hili wakidhani kuwa wakioa/kuolewa matatizo yao yote yatakwisha kumbe yakaongezeka. nadhani ni vyema vijana wakaanza kuomba mapema ila kwa kiasi cha kuongozwa na Roho,ila mtu asilazimishwe kama anaona taswira itaanza kum badilikia vibaya. vijana fulani zamani tulipokuwa vijana waliposikia tukisema mambo ya ndoa walitucheka na kusema,’nyinyi oeni,sisi tunamsubiri Yesu anarudi karibuni.’ baadae,iliwaletea shida sana na kuanza kuingia kwenye uchumba karibu mara nne na uchumba kuvunjika hadi wanaoa,wamepitia ‘skendo’ nyingi. kwa kuwa tayari umeanza kuuliza swali hili,labda ndio wakati wenyewe unafika.angalia watu mbali mbali katika Biblia walivyoingia kwenye uchumba au upate ushauri wa watu waliokutangulia ki imani walivyofanya. usipokuwa na uhakika, viongozi wako kanisani wanaweza kukusaidia maana, taratibu za kanisani kwako pia ni njia ambayo Mungu amekuwekea ili usijikwae katika hili. Mchungaji Willy Mshila.

 12. sahau wakati, the time wll tell acha tamaa, atakuja right person kwa muda muafaka, sahau life expectancy kwani kimaumbile/kimungu sio sahihi!

  tulia tu wakati ukifika utajikuta ndani ya uhusiano au vp?

 13. Bwana Yesu asifiwe!

  Kwanza kijana napenda kukupongeza kwamba unamjua Mungu (jambo ambalo ni la kwako zaidi na Mungu wako) na pia kwa kutushirikisha kutaka kujua WAKATI SAHIHI WA KUANZISHA UHUSIANO/KUTAFUTA MCHUMBA.

  Ninachojua mimi ni kuwa wakati sahihi wa kuanza uhusiano NI PALE UTAKAPOFIKA WAKATI WAKE WA KUANZA UHUSIANO, i.e “at right time to come, the relation will come”. Kumbuka katika kitabu cha MHUBIRI 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” Wakati nilipokuwa chuoni Mzumbe (2002-2005), mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi (KAWE LIVING WATER BIBLE FELLOSHIP), alinishangaza kwa kusema hakuna haja ya kuhangaika na maombi ya mchumba/mume/mke mapema hususan mnapokuwa bado masomoni, nilishangaa sana!! Tangu kuokoka kwangu ndivyo nilivyofundishwa kuwa ni muhimu kuanza mapema maombi ya mchumba, hakika mafundisho ya Apostle Ndegi yalikuwa mapya kwangu, nilishangaa haaa!

  Lakini hoja yake kuu ilikuwa ni kwamba, mara ukianza kufanya maombi ya mchumba unajikuta umeanza kujenga taswira ya ndoa akilini mwako, taswira ya kuwa na mume/mke unaanza kujenga taswira ya maisha ya ndani ya nyumba kama mwanandoa, inamaanisha nini? Hapa kinchofanyika ni kuanza kuwa katika mkao wa mwanandoa halisi, unaanza kupata taswira ya kuhudumiwa na mke nyumbani, unapata taswira ya watoto nyumbani, lakini pia inajengeka taswira ya TENDO LA NDOA(hapo bado haujaoa), taswira ya tendo la ndoa kukuingia itasababisha mental set up yako kuanza kuelekea kwenye mhemko (hivi ni mhemko au mhemuko au muhemuko?) wa tendo hilo ambalo kabla ya ndoa huitwa “zinaa”. Nachelea kusema kuwa hapo ndipo roho ya uzinzi inapoingia nafsini mwa kijana (simaanishi wewe, amani iwe nawe, haleluya!).

  Kitabu cha WIMBO ULIO BORA 3:1-5 pia ilinishangaza maneno yake, baada ya mahangaiko ya kumtafuta mpenzi wa nafsi yake pale mstari wa 5 anasema “NAWASIHI….. MSIYACHOCHEE MAPENZI, WALA KUYAAMSHA HATA YATAKAPOONA VEMA YENYEWE.

  Inawezekana nikashangaza kwamba ninajibu nisichoulizwa na ndugu yetu Lutengano, kwamba nimeanza kuzungumzia mapenzi/tendo la ndoa, japo yeye ameulizia UHUSIANO/UCHUMBA. Kwa kweli hivi vitu vinaendana watu wa Mungu, na si dhambi kuambiana mapema.

  Sasa nijibu swali la ndugu yetu Lutengano. Kwangu mimi kama mtu niliyeokoka SUALA LA KUOA HALITAKUWA NI KWA SABABU YA ECONOMIC STATUS WALA UMRI (japo age of majority ni lazima), KUOA KWANGU ITAKUWA NI KIIMANI ZAIDI, imeandikwa “mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye akisitasita moyo wangu hauna furaha nae”

  Napenda nikuhakikishie kuwa mara wakati utakapofika kila kitu kitafanyika chenyewe, hutatumia nguvu kubwa kumuomba Mungu akupe huyo mchumba, unaelewa ni kazi rahisi sana kumuomba Mungu mvua wakati wa masika (amini usiamini imeandikwa kwenye biblia), kasheshe kumuomba Mungu mvua kiangazi, mpendwaaaa! “Eti niliwahi kusikia ni mara chache wachumba wa muda mrefu kuoana (japo sijalifanyia utafiti)” labda kama kuna mmoja amelifanyia utafiti atuambie (au kama halina umuhimu tuliache tu).

  “NAWASIHI….. MSIYACHOCHEE MAPENZI, WALA KUYAAMSHA HATA YATAKAPOONA VEMA YENYEWE” Ukifika wakati wake, ukimwomba Mungu atakupa mke mwema (japokuwa neno mume mwema bado sijaliona kwenye biblia), ukimwambia mama/baba ninataka kuoa watakubariki, ndugu watakuunga mkono, jamaa na marafiki watakusapoti (niamini nisemalo), wooote watasema amina (isipokuwa shetani na jeshi lake, usiogope).

  Na upande wako dada halikadhalika, ukifika wakati wake, ukimwomba Mungu atakupa mume mwema (japokuwa neno mume mwema bado sijaliona kwenye biblia, japo niliwahi ambiwa binti mwema atapata mume kutoka kwa MUNGU).

  Mungu awabariki, na amani ya Kristo YESU iwe nanyi, amina!
  (Mr. Pelesi J. Majani)

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s