Je! Kumiliki mali ni kizuizi cha kuolewa?

Bwana yesu asifiwe wapendwa!
Mimi ni dada wa miaka 32. Sijabahatika kupata mume wa kunioa hadi sasa. Ila Mungu amenijalia kupata vitu vingi ambavyo kwa maisha yetu ya kibinadamu tunaamini ni muhimu. Mungu amenijalia mtoto mzuri wa kike, amenipa kazi nzuri, elimu yenye kiwango kizuri, amenipa nyumba na gari pia. Swali linakuja kila ninapoongea na watu mbalimbali wananiambia kwa hali ya kawaida si rahisi kumpata mwenzi wa maisha kwa sababu ya vitu ambavyo Mungu amenijalia vitapelekea kila mwanaume ninayempata kuniogopa.

Je! Inawezekana nisiolewe kwa sababu hii tu? Ninapata wakati mgumu na ninashangaa kwanini iwe hivyo wakati vitu na mali vyote vyatoka kwa Mungu. Yeye ndiye aliyenijalia nikavipta nikiwa bado sijampata mume;  Je! Mali hizo ni sababu ya mimi kutompata mume?

Wapendwa naombeni mnishauri nipo kwenye kipindi kigumu sana. Namlilia Mungu usiku na mchana asikie ombi langu la kumpata mwenzangu.

Abella

Advertisements

16 thoughts on “Je! Kumiliki mali ni kizuizi cha kuolewa?

 1. Luke 12:3
  What you have said in the dark will be heard in the daylight, and what you have whispered in the ear in the inner rooms will be proclaimed from the roofs.

 2. Shalom wapendwa!
  Nashukuru kwa maoni ambayo nimeyapata kutoka kwenu. Kweli nimefarijika na nimepata ujasiri wa kuendelea kusimama katika IMANI ya kuomba kwa bidii. Maana nimegundua Mungu wetu hashindwi kwa lolote na ana jibu kwa wakati wake. Naamini baada ya muda nitarudi kutoa ushuhuda kupitia Strictly Gospel.
  Mbarikiwe.

 3. Pole dada Abella.Maandiko matakatifu yanasema kuwa utajiri na Heshima vyatoka kwa Bwana.Pia mahali pengine inasema nci na vyote vijazavyo nchi ni mali ya Bwana.
  Pia mke mwema hutoka kwa Bwana na kama ni hivyo hata mume mwema hutoka kwa Bwana.
  Ninaamini kuwa baraka za Bwana hazina majuto,kwa hiyo usiogope zidi kumuamini Mungu kwa habari ya mume mwema.
  Japo hujatuambia ukweli kuhusu huyo mtoto uliye naye.Mfano baba yake nk.
  Lakini pia kama umezaa mtoto nje ya ndoa na wewe ni mkristo ujue ni lazma kwanza utubu kwa ajili ya hilo ili damu ya Yesu ikutakase na kama ni mpango wa Mungu atamrudisha huyo mwanaume uliyezaa naye,la sivyo,atakupa wa kwako anayekufaa nyakati zote.
  Pole!

 4. Dear abella,

  Nikipongeze kwanza kwa kupata mtoto. Hiyo ni zawadi kutoka kwa mungu ipasayo kumshukuru.

  Kuhusu kupata mume,ndg kumbuka malezi ya kikabila na jamii yetu kwa ujumla wake imekuza kizazi kiaminicho ya kuwa mwanamke hana nafasi katika kumiliki mali.Huu ni ukweli usiopingika kwa wengi katika jamii yetu ya kupasa ufahamu.

  Lakini pia kumbuka jamii ya leo imeelimika kwa uchache wake na inazidi kuelimika juu ya umiliki wa mali kwa mwanamke.Hii ndiyo maana kuna misemo iliyoingia mitaa kwa wasomi wengi kama “nani anayetafuta mwanamke goalkeeper siku hizi??” ..huu ni mojawapo ya misemo iliyopo mitaa ukimaanisha ni nani siku hizi ambaye anatafuta mwanamke asiyejishughulisha??.

  Pia hata kwenye biblia ina eleza hayo kwamba mungu alimpa Adamu msaidizi, ikimaanisha mtu ambaye anaweza kufanyakazi kama yeye Adamu afanyavyo ambaye ni Hawa.Kwa hiyo kuna watu wanatafuta watu wa aina yako kuwa wenzi au wasaidizi kama biblia isemavyo ili msaidiane katika kazi au uwezo wa kutafuta kama ulio nao wewe.Kwa mantiki hiyo hiyo nikutie moyo, kumiliki mali au kuwa na uwezo wa kutafuta ni sifa nzuri ya mwanamke anayefaa kuolewa kwa kizazi cha leo kama msadizi wa mume katika familia.

  Ndg Abella pia umkumbuke mungu mana ndiye mpaji wa vyote kwa wakati wake na kwa kusudi lake.Mana anasema katika maneno yake ..nyenyekea kwenye mkono wa bwana ulio hodari ili akukweze kwa wakati wake pia kuna maneno mengine yanasema ..”Let us have confidence, then, and approach God’s throne, where there is grace. There we will receive mercy and find grace to help us just when we need it.” ..ndg Abella mume mwema atoka kwa bwana na mungu ni mwaminifu mana amasema ..”call me in times of trouble/sorrow.I will rescue you, and you will honor me” na kama ni mpenzi wa kusoma vitabu tafuta kitabu kiitwacho “Purpose driven life” kitakusaidia sana katika kipindi hichi ulicho nacho.

  Ni maombi na imani ya yangu mungu atakuina zaidi ya ufikivyo ..mana sikio lake si zito asisikie maombi yako

 5. Kumiliki mali NI kizuizi cha kuolewa vile vile SI kizuizi cha kuolewa. Mambo haya mawili, yaani KUWA na KUWA SI kizuizi cha kuolewa kunategemea yule anayemiliki mali hizo.

  1.Kumiliki mali kunaweza kuwa kizuizi cha kuolewa iwapo anayemiliki mali hizo:

  i)atatumia kuwa na mali kama kipimo cha utu wake.
  -Kuna watu wengi wenye mali na hutumia mali hizo wakizitegemea kuwa kama ndiyo kielelezo chao. Mfano, kama akiitwa kwenye kikao/mkutano au akikutana na watu yeye peke yake ndiye atataka awe msemaji. Yaani swali lolote likiulizwa yeye ndiye anataka ajibu kwanza. Sasa, kuwa na mali siyo kuwa na kila kitu maishani. Kuwa na mali haimaanishi mtu huyo ana hekima sana au ufahamu wa mambo yote. Msichana ambaye atatumia kuwa na mali kama kipimo cha utu wake NI VIGUMU SANA kupata mwanaume wa kumuoa maana moyo wake uko katika mali. Hali hiyo hujionyesha wazi kwa watu, hata kwa yule anayehitaji kuoa.

  ii).atakuwa anatumia mali hiyo kuishi maisha ya gharama.
  iii).atakuwa na dharau kwa wasio nazo
  iv).atakuwa anaangalia hali ya kipato cha anayetaka kumuoa
  v).hataweza kujishusha ili watu wanapomtazama wamuone yeye na wala si mali zake.

  2.Kumiliki mali kunaweza kusiwe kizuizi cha kuolewa iwapo mwenye kumiliki mali hizo:
  i).atajitambua hali yake na hivyo atafanya kila kitu katika nafasi yake.
  ii).hataishi maisha ya anasa bali kiwango kinachokubalika katika jamii inayo mzunguka
  iii).ataheshimu watu wote, hata wale wasio nacho kabisa.
  iv).hatabagua mtu wa kumuoa kwa kutazama kipato. [na hapa ni pagumu sana!]
  v).atajishusha na ili watu wanapomtazama wamuone yeye kwanza ndipo watambue kumbe ile ni mali yake.
  -Kuna tatizo kubwa lililopo ambapo watu wanaweza kuona mali kwanza ndipo waulize ni za nani. Inatakiwa watu wanaposema uhusu uhusiano wa binti na mali zake waseme kama hivi-

  “msimuone vile, yule ana mali nyingi.!” na wala siyo waseme,
  “si ndiyo yule mwenye gari/nyumba fulani, nani asiyemjua?..”

  Nimeandika kwa uchache na kufafanua kwa kifupi tu lakini natumaini niliyoandika yanaweza kuleta mawazo mapya na kutafakari kwa upana zaidi kuhusu jambo hili. Ninajua si dada huyu tu mwenye kutatizwa na tatizo hili. Wako akina dada wengi ambao wana kazi nzuri, elimu nzuri, pesa nyingi, lakini hawajapata mwenzi wa maisha.

  Ushauri: Kuna tabia au hali ambazo kwa hali ya kawaida ya kidunia, yaani kwa mtu ambaye hana Yesu moyoni ni vigumu sana kuziepuka. Tabia za namna hiyo kama vile kiburi, majivuno, dharau, na zinazofanana na hizo, nyingine husababishwa na mapepo au majini yaliyoweka makao ndani ya wadada wengi. Wadada wanaongoza zaidi ya wakaka kwa tabia kama nilizotaja hapo juu.

  Maana yangu ya kuandika haya ni kwamba kama dada Abella umeokoka utakuwa katika nafasi nzuri ya kujihoji kwa kuwa ume-narrow lile eneo la kujichunguza. Lakini kama bado hujaokoka ni vigumu mno na inawezekana kuna sababu nyingine [kama alivyoandika ndg Kamala Lutanisibwa] zaidi ya kuwa na mali inayoweza kuwa inasababisha hilo. Lakini wako pia watu waliookoka lakini kuna eneo fulani wanakuwa hawajafanikiwa kushinda. Kwa hiyo tafakari sana hapa ili uone wapi ulipo katika hali ya kiroho.

  Jambo jingine ni kuhusu “watu mbali mbali” unaoongea nao wanaokushauri kuwa ukiwa na mali ni vigumu kuolewa. Si kila mtu anaweza kuwa na ushauri mzuri kwako. Wako wengine ni kwa sababu ya kuwa na ufahamu mdogo, wengine kwa sababu ya hila, wengine kwa sababu wao wameshaolewa, wengine kwa sababu hawajaolewa, wengine kwa sababu wanazo, wengine kwa sababu hawanazo, wengine kwa sababu ya imani zao nk. Kuongea na watu siyo jambo baya lakini muhimu ni aina gani ya watu unaoongea nao. Sasa katika hali ya namna hii, SI KILE WANACHOKUSHAURI WATU kinacho-matter bali UKWELI wa jambo lenyewe. Katika mambo ambayo “wengi wape” haifanyi kazi ni pamoja na hili!

  Iko sababu nyingine ambayo inaweza kuwa ni tatizo. Wako akina dada wengi ambao walijikuta wakipata mtoto kabla ya ndoa. Tukio la kupata mtoto pasipo kuendelea kuishi na baba wa mtoto ni tatizo. Si wanaume wengi wako tayari kuoa mwanamke mwenye mtoto wa baba mwingine. Lakini hili ni tisa, kumi ni pale baba wa mtoto atakuwa anaendelea kutoa matunzo kwa mtoto. Mara katuma zawadi za krismas, birth day au anakuja kumsalimia mtoto wake. Yaani hata kama hakuna nia mbaya lakini kile kitendo tu cha watu kufahamu kwamba kuna jambo la namna hiyo, hiyo huwafanya wanaume wahitaji wa kuoa wakae mbali, mbali sana! Hata kama mtu ataonyeshwa badi kwenye maono ni atapambana sana!

  Naandika haya in vain tu kwa kuwa hakuna sana habari za kutosha kuhusu wewe zaidi ya hayo uliyoandika. Kwa hiyo naandika tu haya kama kurusha jiwe kwenye kundi la ndege, pengine I might hit one!

  Kwa kumalizia niseme hivi, angalia hali yako ya kiroho ukoje na Mungu. Kumlilia Mungu peke yake haitoshi bali kuwa katika harmony na Mungu. Unaweza kukuta pengine haihitaji kulia kwa Mungu bali kuishi maisha fulani tu ambayo Mungu atayaona na hivyo kumwelekeza muoaji kwako.

  Kama kuna swali kutokana na haya niliyoandika unaweza kuuliza tu ili tuendelee kubadilishana mawazo.

 6. Duh,wanaume na sisi jamani, mtu kuwa na elimu nzuri gari na nyumba basi magoti yanagongana. Huko ni kutokujiamini kwa sababu wanaume wengi wanapenda kuwatawala wanawake kwa vigezo hivyo vya kuwa na pesa ,elimu n.k kuliko wake zao.

  Dada Abella hiyo ya wanaume kukacha mwanamke akiwa na mafanikio kuliko wao ni ya kweli. Na inatokana na malezi katika makabila yetu kuwa mwanamke akiwa na mafanikio kukuzidi atakunyanyasa, ingawa kweli wanawake wengi wamekuwa wakifanya hivyo, cha kusikitisha hata wapendwa, naamini Abella hauko hivyo. Tena sio mwanamke akiwa na mali tu hata akiwa na mafanikio ya kawaida ila ni mrembo kwelikweli, oh wanaume ni waoga jama, nakwambia wengi huwa wanagwaya !!
  May God make u a path Abella.
  Jambo jingine,nakushauri ukae mahali ambapo wanaweza kupatikana wanaume wa kiwango chako, believe me utapata mume. Masikini kuoa kwa mfalme huo lazima uitwe muujiza maana huwa haitokei mara kwa mara.

 7. WASALAAM! Dada, Maisha ni mjumuiko wa mengi. Maisha ni muendelezo wa yaliyokuwepo, yaliyopo, na yajayo. simply Life is history.
  Kwa upande wangu naaminikuwa historia inajirudia na itaendelea kuwepo milele(Liberation can be part of the outcome of either education Men got, Society from which they come from etc.
  Uhalisia
  Kiuhalisia niajabu mwanaume kumwoa mwanamke aliyejaliwa mali bila kujali amezipata vipi. kama zawadi kwa wazazi, Kujichumia mwenyewe na vinginevyo.
  Asili yetu wanaume tumejijengea kuwa sisi ndio sisi Japo vitabu vitakatifu Vimeandika kuwa Mwaname ndie kiongozi wa familia. Sasa je, unategemea nije nikuoe kisha niwe kiongozi wa familia wakati mali kubwa karibia 80% ni yako?
  Mwanaume husifiwa kwa kutafuta kokote na wala si kwakuoa aliyenazo kwakuwa atadharaulika mbele ya akadamnasi. Kumbuka mtu kamwe huwezi wakwepa watu. (noone shall ever live out of interaction) Hivyo aidha watoto wenu baadae watasimangwa kuwa mamayao eitha alioa babayao au na mengineyo mengi.
  Mwalimu nyerere alisema kwenye mkutano wa wanawake wa ccm miaka ya 70 huko” Mwanaume ndiye kiongozi wa familia hivyo ndiye mtafutaji japo mwanamke anaweza kuwa na kipato wakati mumewe aidha hana kazi, kipato kile hakibadilishi mfumo wa baba.
  hapo tunapata picha kuwa Mali kiutaftaji yatakiwa iwe ni jukumu la baba sasa wewe unayo je baba unategemea awe nani? Labda ataekuzidi.
  ukirudi kwa hawa vijana wasiokuwa na uwezo labda upate anayetafuta mtaji kwa mwanamke atakuja ila siku ukimwachia kidogo alichokuwa anatafuta atakuacha.
  Kikubwa ni kujiweka sawa na wanawake wenginewa kawaida tu.
  Ninanamfano wa jirani yangu yeye alibahatika kuteka viwanja na kujenga mapango kwa faida ya kupangisha baadae ila kwakuwa ni mali isiyoonekana sana haikuwa ngumu kumpata mwenzie. licha ya yote alikuwa ni mtu wa kujimix na kila aina ya watu sio kwakuwa unamali unataka kukamiliasha kauli ya ”birds of the same feathers flocks together” Changamana na watu. Hakuna mume anayetoka Mbinguni akashuka kama Yesu alivyopaa mbiguni. wala hatakushukia kama embe au nazi lidondokavyo miguuni mwa mpanzi.
  Hivyo lazima ujumuike.
  Mwisho be simple. na wala karne hii tumekuwa na watu wengi wanajiita warokole kumbe sio hivyo wamepotosha maana kamili la urokole kwahiyo ukienda kama mrokole they might get you on a different perception.
  Mwisho ningeomba tukufahamu na wewe mwenyewe ni mtu wa aina gani siotunakupa mawazo aukukuonesha njia tukidhani tunamwelewesha anaeendana na malezo yetu kumbe weneed to use execptoinal ways yakusaidia kutatua linalokusibu.
  Mwanadamu yeyote dunianai aliumbwa na Mungu. WANADAMU WOTE TUNA MAPUNGUFU. hivyo hata ukutane na asieelewa siku akielewa utashangaa. Zakayo alichukiwa na kila mtu lakini cha ajabu Yesu ndiye aliyemtembelea badala ya wale waliomchukia lazaro.

 8. Shalom! Nashukuru kwa maoni na ushauri ninaondelea kuupata. kwa dada Sophia, mwanangu ana miaka mitano sasa.

 9. Dear Abella,
  Pole kwa hii hali inayokukabili.Huyu mwanao ana umri gani sasa?Pili,itakubidi unyenyekee kabisa na umsome sana mtu yeyote anayeonyesha nia ya kutaka kukuoa.Unajua kuna dada ambao wanachambua wachumba(they are selective.They look for some qualities from men that are hard to find).
  Kulingana na hali yako,naona kidogo inakuwa vigumu kukutana na watu wa kawaida ambao ndio wengi.Hawa wanaume wa kawaida itabidi wakuogope hata kukukaribia.
  Ukimpata mume ambaye hana ”qualities”unazozitarajia lakini ni wa Yesu,omba Mungu awaunganishe.
  Mimi nina elimu ya chuo kikuu cha Nairobi(B.Com)lakini mume wangu ni wa form four na hana kazi lakini tunaishi kwa amani.Sasa ni miaka 17.
  Jibu ni kutoweka viwango katika uchaguzi wako wa mchumba na kumwomba Mungu kwa imani.sophia-kenya

 10. Abella

  Katika jamii zetu za Kiafrika ambazo bado zimeathirika na tatizo la kuwa mwanaume ndiye juu ya kila kitu yaani “Male chauvism” au “male superiority” kwa lugha ya kigeni, au basi tuite mfumo dume unaweza kweli ukakabiliwa na kupata mwenzi wa maisha, lakini haitakiwi kuwa hivyo katika nyumba ya watu wa Mungu.

  Tumeona katika maisha ya kawaida kwa baadhi ya wanandoa, mwanamke anapopiga hatua za kimaendeleo zaidi ya mumewe imekuwa ni tatizo! Nafahamu baadhi ya ndoa ambayo wanandoa walioana wakiwa na elimu ya kidato cha nne, na kama waalimu wa shule za msingi, lakini mwanamke alijisukuma kielimu hadi kufikia kiwango cha Phd! Matokeo yake mumewe ilibidi angalau kwenda kusoma angalau diploma kutetea ndoa! lakini haikusaidia ndoa ilivunjika……..siwezi kusema ni nani alikuwa mkosaji……inawezekana ni mume kujiona kuwa amezidiwa kielimu na mkewe! au mwanamke kupata kiburi cha elimu! Ukweli unabakiwa kama nilivyosema kuwa kwa jamii ambayo mwanaume amelelewe na kufundishwa kwamba yeye ndiye kinara dhidi ya mwanaume basi utapata shida kupata mwenzi!

  Na lakusikitisha kabisa ni kuwa hata watu ambao wamemwamini Yesu bado utaona wanakuwa na mitazamo ile ile ya jadi, badala ya kufuata uongozi wa Mungu na kusukumwa na upendo ambao ndio msingi mkuu wa ndoa!

  Lakini na mimi nasema kama walivyokushauri wengine, tafuta kusudi la Mungu na ngoja wakati wa Mungu! Na pia usisikilize maneno ya watu! Una uhakika gani ni mafanikio ya mwili ndio yanayowakimbiza wanaume kwako? Hii itategemea wewe unavyoyaangalia hayo uliyo nayo! Endelea na maisha ya kumtumaini Mungu! Kama ndoa ni kusudi lake kwako itakuja tu!Ubarikiwe!

 11. Bwana Yesu Asifiwe Dada Abella,
  Napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yako kwa kufikisha umri huo na kuweza kuwa na vile Mungu alivyokujalia kabla ya kuolewa. Mimi kwa upande wangu naamini mpango wa Mungu ni kutupatia vitu vyema na vya thamani. Kuwa na mume ni mpango wa Mungu ambao anakupa kwa wakati sawasawa na mapenzi yake, wakati wake ukifika atakupatia mwenzi ambaye hatajali kuwa wewe una mali au vipi.
  Mimi ni mwanasheria nimekuwa nakutana na wanandoa wengi ambao wamekata tamaa na wanadhani suluhisho ni divorce, nimekuwa najaribu sana kutafakari ni kwa nini watu waachane kama ni mpango wa Mungu wao kuwa pamoja? lakini nikapata jibu kuwa mambo mengi huwa binadamu tunajiamulia bila kuwa na uhakika kuwa ni Mpango wa Mungu hivyo baada ya muda mfupi tunakuwa tunajutia.
  Hivyo basi kama neno la Mungu lisemavyo kuwa mapenzi ya Mungu yatimizwe katika maisha yetu ni matumaini yangu kuwa endelea kumwomba Mungu nae atakupa haja ya Moyo wako sawa sawa na mapenzi yake.
  Ubarikiwe

 12. unakubaliana nao wanaokwambia hivyo? jaribu basi kupoteza mali zako uone kama utampata huyo mwenza. hivi ndoa ina uhusiano na mali? kama jibu ni ndio basi hiyo sio ndoa bali ujasiriamali

  yawezekana una sababu nyingine za kutokumpata huyo mweza na labda muda bado!

  lakini ni lazima sote tuingie kwenye ndoa? kuna wanaotamani kutoka na bila shaka wanakuonea wewe wivu ambaye hujawai ingia mle!

  kuwa mpole tu na mwamini Mungu kama alivyokupa mali za dunia ni rahisi kukupa makubwa zaidi endapo hutakuwa na mitizamo finyu ya mali

 13. mmmm ngoja tusikilize maoni ya wanaume hapa, binafsi naona kama hazikupi kiburi hizo baraka zozote za mwili sio kikwazo kuolewa… Binti usahau nyumba ya baba yako.. Mithali,
  Yaani usivipe umuhimu kuwa ndio kigezo pekee ambacho mume mtarajiwa aone kwako, je una vigezo vingine vya kuwa mke mwema?
  Ubarikiwe

 14. Dear Abella,

  Napenda kukutia moyo,kwamba kuwa na mali kunaweza kusababisha wewe kukosa mwenzi wako, sio kweli,Upendo wa kweli hauangalii vitu,bali unaangalia upendo wa ndani,

  Kwanza toa maisha yako kwa YESU,na muombe MUNGU akupatie mume ambaye ni chaguo jema.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s