TANZANIA, Wake Up!

tanzaniapic

Dear All,

JEREMIAH  23:23-32 (KJV)

23 Am I a God at hand, saith the Lord, and not a God afar off? 24 Can any hide himself in secret places that I shall not see him? saith the Lord. Do not I fill heaven and earth? saith the Lord. 25 I have heard what the prophets said, that prophesy lies in my name, saying, I have dreamed, I have dreamed. 26 How long shall this be in the heart of the prophets that prophesy lies? yea, they are prophets of the deceit of their own heart; 27 Which think to cause my people to forget my name by their dreams which they tell every man to his neighbour, as their fathers have forgotten my name for Baal. 28 The prophet that hath a dream, let him tell a dream; and he that hath my word, let him speak my word faithfully. What is the chaff to the wheat? saith the Lord. 29 Is not my word like as a fire? saith the Lord; and like a hammer that breaketh the rock in pieces? 30 Therefore, behold, I am against the prophets, saith the Lord, that steal my words every one from his neighbour. 31 Behold, I am against the prophets, saith the Lord, that use their tongues, and say, He saith. 32 Behold, I am against them that prophesy false dreams, saith the Lord, and do tell them, and cause my people to err by their lies, and by their lightness; yet I sent them not, nor commanded them: therefore they shall not profit this people at all, saith the Lord.

JEREHEMIA 23:23-32 (KJV)

Advertisements

9 thoughts on “TANZANIA, Wake Up!

 1. iam so blessed just becoz of this ministry and i enjoy having more from it God bless it powerfully!!!!!!!!

 2. Wapendwa,

  Mzee Makunzo, Haule, Top na Wanablog,

  Kwa kifupi kabisa ili Kanisa letu la Tanzania liwe chachu njema kwa taifa letu inabidi watu wa Mungu tuolikiri jina Lake Tufanye kazi ya ziada! Na huwa naogopa kabisa napoona yanayoendelea ndani ya Kanisa la Bwana, Hasa kuhusu kile kinachofundishwa mimbarini leo!Hasa Waumini wanachopenda kukisikia na kukimbilia!

  Na huwa najiuliza, Je Hizi Biblia tunazozibeba kila Jumapili kwenda nazo makanisani na kurudi nazo majumbani mwetu huwa kweli tunazipa nafasi ya Kuzisoma na Kutambua kuwa Ni Maneno ya Mungu yaliyo hai? Maana kama Tungezipa nafasi ya Kweli katika maisha Yetu tusingeliona mengi tunayoyaona ndani ya kanisa leo! Mbio za kutafuta “baraka’! Huku tukisema kwa “YESU KUNA RAHA” Hasa mioyoni mwetu Tukiwa na maana ya “raha” ya kuwa na magari, nyumba, mavazi ya thamani! pesa nyingi nk! Je kweli “RAHA” tunayoitiwa na Yesu ni Hiyo? Ulimwengu wa leo ndio unayakimbilia haya! Na Sauti tunazozisikia Leo ni kuwafanya waumini wayakimbilie haya kwa kutumia JINA LA YESU!

  Si ile Injili iliyofanya Kanisa la Kwanza wakauza Nyumba na Mashamba! Na bila kutajaria Yesu atawapa nini! Vigezo vya kupimia “mafanikio” vimekuwa ndio vile vile vinavyotumika duniani! Maisha ya kujikana, kujitoa, kuwa tayari kufa hata kuabika kwa ajili ya Injili hayasikiki tena Mimbarini! Imekuwa ni Injili ngeni!Na ukihubiri unaweza poteza waumini!

  Ni kweli Mungu ameahidi BARAKA! lAKINI HATUMFUATI KWA KUZIFUATA BARAKA! Tunamfuata kwa sababu ametutoa Dhambini! Ametuma Uzima Wa milele! Ametufanya Watoto wake! Anatupa Nguvu za Kushinda Dhambi LEO! Amekwenda kutuandalia Makao ya Milele! AMEAHIDI HATATUACHA WALA KUTUPUNGUKIA!tuna uhakika wa maisha haya na yajayo pia! Na kwa kadri kila mmojawetu aliyepewa Talanta na yeye na jinsi tutakavyozitumia ATATUBARIKI! NA BARAKA ZITAKUWA KWA UTUKUFU WAKE ZAIDI KATIKA KUENDELEZA UFALME WAKE! Naona Tumesahau kabisa Tu wapitaji na Wasafiri! Siona baadhi ya manabii na mitume wa leo wakiwakumbusha waumini haya! Kuna makanisa mengi hata yanayoitwa ya Kiroho kuanzia January hadi December hayajawahi kuhubiriwa au Kukumbushwa Yesu atarudi mara ya pili!

  Kwa kifupi tunahitaji kuutambua wakati! Na kumuuliza Roho wake nini alichokusudia kwa Kanisa lake, nini anataka tusikie toka kwake, ili tuweze kuitambua sauti yake na Kuitii! Bwana asije akatuuliza Leo kama Alivyomuuliza Sauli “…..MAANA YAKE NINI, BASI, HIKI KILIO CHA KONDOO MASIKIONI MWANGU NA HUU MLIO WA NGO’MBE NAOUSIKIA….” Kwa kifupi leo kuna milio na sauti nyingi katika zizi la Mungu au niseme madhabahuni mwa nyumba ya Mungu, Je hii milio na sauti tunayoisikia leo katika mibari zetu ni ya kutoka Mungu? Sauti zisizofanya tuwe tofauti na Mataifa! Sauti zisizotukumbusha Kurudi kwa Bwana ku karibu! Sauti zisizotukumbusha kuishi maisha masafi na matakatifu! Sauti zisizotukumbusha tumtolee Bwana kwa moyo na wala si kupanda mbegu na kutajaria malipo! Sauti zisizotukumbusha sisi ni watumwa tu!WAUMINI WENZANGU NA TUAMKE!

 3. Mwanakwetu Orbi Salamu,

  Natamani sana ungekuwa na kipaza sauti au Radio au Tv ukatoa kilichoko moyoni mwako. Ujumbe mzito unaostahili mwamko wa kiroho kwa Watanzania na wengineo

  Wachache sana wanaliona hilo uliloliona, wengi aa mambo ya kawaida. Kwa hakika ni lazima kuamke toka usingizini. Jamani tunalala mpaka matongotongo ya kiroho yanatufanya tusione kitu,True this is a practical message kwetu.

  Ndiyo kukumbushane Tuamke. – Asante,

  Mzee Makunzo.

 4. Mpendwa ktk Bwana Orbi.Jumapili iliyopita nilikuwa kwenye Bible study EAGT Msasani,(Mada)usingizi wa kiroho na Kuamka toka usingizini. Maandiko yalikuwa Mathayo 25,Rumi13:11,Zab 106:39,Ulikuwa nasi ktk roho,Barikiwa.

 5. Haloo TZ watu wengi hiki kipindi tunapenda vitu rahisi hatupendi kujituma(kujidhabihu) ndio maana kama watoto wa JEHOVA tunashindwa kufahamu mawazo ya BABA yetu,maana tumeungana na kwaida za dunia hii na kutotaka kumwamini ROHO MTAKATIFU ktk matendo.MTU AKIIPENDA NAFSI YAKE ATAIANGAMIZA ITOENI MIILI YENU IWE DHABIHU ILIYO HAI TAKATIFU MAANA HII NDIO BWANA ANAPENDEZWA NAYO;

 6. Nathan,

  Asante kwa mchango wako,Kama utasoma post yangu katika “Umoja wa Waislamu, OIC na Kadhi” Nimejaribu angalau kutoa sehemu yangu ya Mchango kutaka tuamke kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yetu.

  Kwa kifupi, nikimnukuu Paulo ” NAAM TUKIJUA WAKATI, KWAMBA SAA YA KUAMKA USINGIZI IMEKWISHA WADIA, KWA MAANA SASA WOKOVU WETU U KARIBU KULIKO TULIPOANZA AMINI, USIKU UMEENDELEA SANA, MCHANA UMEKARIBIA, BASI NA TUYAVUE MATENDO YA GIZA NA KUZIVAA SILAHA ZA NURU”

  Kwa upande wangu nikiangalia hali yetu kama watu tuliomwamini Yesu, tumeshindwa KUJUA WAKATI! Wengi naona tumeshindwa kabisa kuangalia hali halisi ya Nchi, yaani hali ya kisiasa, hali ya kanisa kwa kuangalia yanayotendeka ndani na nje ya kanisa tukaweza KUJUA NI WAKATI GANI KANISA AU WATU WA MUNGU TUNAPITIA!

  Sauti zinazopata kibali kwa waumini leo si zile zinazotamka Neno la Mungu kwa uhalisia! bali…….Ndoto……..Maono……….Baraka……!Ngurumo……..!Sauti za “Manabii” pasipo unabii wowote……! Sauti za Mitume pasipo utume wowote! Waumini hatutaki kabisa Kukaa kwenye Maandiko! Tunataka waonaji!……. Sauti za Manabii na Mitume zimechukua nafasi katika mioyo ya waumini! Yale maneno “Yasemaje Maandiko” “Yanenaje Maandiko” “kwa maana imeandikwa” Leo kwa wengi ni Kama asemavyo Mtume…….! Kama asemavyo Nabii……..!Kama alivyooteshwa na Mungu…….! “Ukitaka kujua nyota yako……..”

  Kwa kifupi inabidi Tuamke!

 7. Shalom!

  Sometimes i wonder, when God looks at us anasikitika kwa kiasi gani. the bible has all kinds of warnings! considering what is happening in our days, either hatusomi biblia, na kama tunasoma basi hatuelewi kabisa kilichoandikwa, na kama tunaelewa basi hatuamini kabisa chochote kilichoandikwa kwenye biblia na hivyo hatumwamini Mungu kabisa. manake we do 100% the opposite.
  My prayer is, Mungu atusaidie, tufike mahali pa kuyachukua maneno yake na kuyaweka moyoni ukweli kwa kiasi ambacho yatatusaidia kuchambua mbivu na mbichi for it is written in hebrews 4:12 “the word of God is alive and active. Sharper than any double-edged sword, it penetrates even to dividing soul and spirit, joints and marrow; it judges the thoughts and attitudes of the heart.” I CRY FOR THE WORD OF GOD. REAL WORD OF GOD AND NOT PEOPLE’S DREAMS. I hunger for the WORD OF GOD, my soul longs for The WORD OF GOD, this world is now crazy, hakuna kinachoeleweka, my mind cant comprehend what is happening, I NEED TO HEAR WORDS OF THE WONDERFUL COUNSELLOR.
  I CALL UPON EVERYBODY WITH THIS DESIRE FOR THE WORD TO CRY OUT TO GOD ATUPE WATUMISHI WATAKAOTUAMBIA NENO LA MUNGU NA SI KUTUSIMULIA NDOTO ZAO KILA SIKU.

 8. Watch out for those who prophesy their own false dreams!Jihadharini na manabii wanaotabiri ndoto zao za uongo!
  Ulimwengu wetu unahitaji uangalifu wa kiroho.La sivyo,tutaangamia.Tuzijaribu kila roho na tuache kufuata miigizo ya kiroho.Sophia

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s