Mwingira amtangazia kifo Babu wa Loliondo

Adai siku zake za kuishi zinahesabika

Kiongozi mkuu wa huduma ya Efatha, Mtume na Nabii Josephat Mwingira amemtangazia kifo Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapila, maarufu kama Babu wa Loliondo, huku akisema siku za babu huyo kuishi sasa zinahesabika.

Akitoa tangazo hilo mbele ya waumini katika makao makuu ya huduma hiyo Mwenge, jijini Dar es salaam, Jumapili iliyopita, Mwingira alisema babu Mwasapila atakufa kwa kuwa amemtukana Mungu wa mwingira kwa kuzidi kutamka kuwa tiba anayoitoa imetoka kwa Mungu.

Mwingira ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu tangu atangaze rasmi vita dhidi ya Babu Mwasapila. Akitangaza vita  hiyo, Mwingira aliilaani tiba ya Babu huku akisema; “itoweke na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti”

Katika tukio la Jumapili iliyopita, mwingira alisoma andiko kutoka Waebrania 1:1-2, kisha akasema Mungu haongei na miti huongea na wanadamu ambao ni watumishi wake. Aliendelea kusema kuwa, babu wa Loliondo amemkasirisha sana kwa kuwa amemtukana Mungu kwa kusema kwamba Mungu ameongea na miti na badala ya watumishi wake.

“Mungu haongei na miti, anaongea na watumishi wake, hata katika kuponya Mungu ameagiza tuweke mikono kwa wagonjwa, Marko 16:15-18 inafafanua hili. Sasa kwa sababu babu wa Loliondo amemtukana Mungu, naye siku zake zinahesabika, kwani Biblia inasema usimwache mchawi kuishi” alisema Mwingira.

Wakati akiendelea na mahubiri yake huku akipita kuombea wenye shida mbalimbali, ghafla alifuatwa na mtumishi mmoja wa kanisa hilo na kumweleza kuwa, ndani ya kanisa hilo amekamatwa msichana ambaye ametumwa kuloga ili kuharibu kazi ya Mungu.

Hata hivyo, Mwingira hakuonesha kushtushwa na taarifa hiyo badala yake aliendelea kuombea watu huku akisema; “mimi sitishwi na wachawi” baadaye wakati akiendelea kuombea watu waliofika eneo ambalo msichana huyo alikuwa ameanguka na kuamuru ainuliwe ili amhoji.

Miongoni mwa maswali aliyoulizwa msichana huyo ni wapi alikotokea na alikuwa ametumwa na nani. Katika majibu yake msichana huy0 alieleza kuwa ametokea Ngorongoro na ametumwa na mtu aliyedai amechoshwa na maombi ya Mwingira yanayokwamisha kazi zake za kichawi. Msichana huyo alitaja jina la aliyemtuma ambaye hatuwezi kuandika jina lake.

Msichana huyo alikutwa na pete yenye picha ya mtu aliyetajwa na msichana huyo kuwa ndiye kamtuma, pamoja na chuma kilichochongwa mfano wa fuvu lililobebwa na ndege pamoja na bangili kubwa ya shaba.

Baadaye Mwingira alimuuliza; “sasa nikufanye nini”? yule msichana akajibu; “naomba unisamehe sitarudia tena ufanya uchawi na sitarudi kule nilikotoka” Mwingira akamuuliza tena; “Unakubali kumpokea Yesu”? yeye akajibu; “ndiyo” Baadaye msichana huyo aliongozwa sala ya toba.

Mwingira ni mmoja wa viongozi wa dini ya kipentekoste ambao walikuwa wa kwanza kabisa kutangaza kuipingatiba ya Babu wa Loliondo.

NYAKATI

Advertisements

64 thoughts on “Mwingira amtangazia kifo Babu wa Loliondo

 1. UNAMTABIRIA MTU KIFO HUO SI UFISADI WA IMANI; BABU ANASEMA NENO LA MUNGU NA LOLOTE LENYE PUMZI LAFAAA KWA MAFUNDISHO YA MUNGU

 2. MANENO YA JUU YANAKUWA NA UHALALI MBELE ZA MUNGU SASA
  TUMEINGIAO ULIMWENGU WA DIGITALY/DIJITALI RASMI KIIMANI NI 666;
  NINI MAANA YA 666: ZIPO SITA TATU MOJA KATIKA UWEPO MTATU MTAKATIFU FITINA YAKE INAKUWA JUU YA BINADAMU
  NAMBA SITA YENYEWE UKUMBUKE MUNGU ALIUMBA NA KUMWUUMBA BINADAMU SIKU YA SITA KWA SITA SI MAANA NYINGINE ZAIDI YA MWANADAMU : IKMAANINSHA MWANADAMU MWENYEWE
  UTAWALA WA TEKNOLOJIA NI SAYANSI YENYE UTAFITI NA WERESI WA MAPITIO NA MAJARIDA KATIKA KUWEKA AU KUGUNDUA JAMBOA AU MASHINE FULANI;
  TEKNOLOJIA NI MBINU AU UWEZO WA KUFANYIKA KITU KWA NAMAN YA HARAKA UFANISI BILA KUTUMIA NGUVU NYINGI BALI AKILI NA MAARAIFA
  TEKNOLIJIA YA MWAFRIKA AU MWEUSI NI UCHAWI: KWA HIYO WAWEZA SEMA UCHAWI WA WASOMI NA WATAFITI KATIKA UTAFITI WAO
  DIJITALI NI NAMNA YA KUASAFIRI MASAFA KWA 0/1 : HIZI NI NAMBA MUHIMI SANA MOJA INAWAKILISHA NATURAL NAMBA NYINIGNE WHOLE NAMBA : NI KUSAFIRI KWA SIGNAL SIYO MTIRIRIKO : KWA HIYO HAPA NAMBA INAHUSIKA :NA NAMBA HIZI NDIZO ZINATUFANYA TUSEME TAYARI TUPO KWENYE 666: TUNSABIRI MTAWALA SASA WA UKWELI BAADA YA USA KUTHIBITISHA MASHARIKI YA KATI LAZAIMA VIONGOZI WAKE WATIIFU WAQURANI WAFE : MFANO SADAM HUSSEIN; ASSAD; ILI DUNIA ITWALIWE SMOOTHLY

 3. YESU NI MUNGU: SASA INAWEZA IKAMAANISHA MTU ANAWEZA KUAGIZWA NA YESU KASEMA MUNGU;ILA TUOMBEANE NATUTAKIANE HERI:KWA AJILI YA MAPITO HAYA MAGUMU; ILA DUNIA IMESHATEKWA TUNASUBIRI 2013; TANGAZO RASMI LA KUTAWALIWA NA 666: NA SIO MWISHO DUNIA; ILA MWISHO UPO WATEULE: DUNIANI KWA KIPINDI HIKI HAKUNA NABII ILA WABASHIRI:WATABIRI NA WANAJIMU MFANO MAREHEMU SHEIKH YAHYA NI MNAJIMU SIO NABII NDIO ; AMEKUFA KARIBU NA MAY 21;FATHER’S DAY OF MASONIC OF GREAT GRAND; NA ALIJIKUBALI YEYE SI NABII AKAUNGANA NA WANADAMU WENYE MATATIZO KUWASAIDIA KWA FEDHA:HUKU AKIWATIBU KWA KUFITINISHA MAJINI KWA MAJINI NA UJANJA UJANJA WA QURAN ; WATU WASOGEZE SIKU ILA SIO WAPONE;

  TUMIENI NGUVU YA MAOMBI SIO KUTEMBEA NA BIBLIA HAKUTOSHI: BIBILIA NYINGI NI VIGANJA VYA WATOTO KWA AJILI YA KUSOMEA NYOTA: OMBA MWENYEWE WA KINYWA CHAKO; BIBLIA NI MANENO YA KUKUONGOZA WEWE UWE NA TOBA YA KWELI NA KUKUPA MWANGAZA NA YALE YA AWALI YALIYOTENDWA NA MANABII: NARUDIA TENA MUDA HUU TUNAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU TU;HAKUNA NABII ATAKAYE KUAMBIA YMUNGU,LABDA HAJUI NAMNA YAKUWAKILISHA, MTUMAINIENI MUNGU SASA

 4. BABU LOLIONDO ANAKULA MAISHA TU MPKA SASA DUH KWELI MUNGU MKUBWA YAAANI BADO HAJAAGA MAISHA KABISA

 5. SASA NINI KIMETOKE KILA MTU ABAKI NA IMANI YAKE KAMA NI MWINGIRA MTUME NA NABII WANAO MWAMINI WA MWAMINI KAMA NI WA KWABABU BASI NA IWE HIVYO ILA KILA MTU AANGALIE NJIA YAKE ILIYO SALAMA NI NINI? KAMA YEYE MTUME NA NABII MWINGILA ANAPOFUNDISHA KUA USIANGALIE MTU ANASEMA NINI ANGALIA NENO LINASEMA NINI…BASI

 6. BWANA ASIFIWE KWA WOTE

  WANDUGU WOTE NA SHUKURU KWA MUCHANGO WENU ZAIDI KWA YOTE MBELE YA MUNGU NA WANADAMU TUTUMIYE HEKIMA JUU NENO LAMUNGU YA YA UTARATIBU KWA MUKUBWA AMA MDOGO KWA NJIA ZOTE TUWE NA UTARATIBU. ATA WAKATI YA KALE WACHAWI WALIOPO ATA LEO KWETU SISI NI KUCHUNGUZA PAMOJA NA MAOMBI YA KWELI MBELE YA MUNGU SIO KWA NGUVU YETU MBALI UWEZO LA MUNGU

  KAMA VILE KUFA YA MUTU YA MUNGU IKO KUKINYA YA WATU NI SAWA LAKINI TUJUWE KAMA VILE NENO ILIPOSEMA KWA MWANZO BAADA YA ADAM NA EVA KUTENDA ZAMBI MUNGU ALISEMA NAO ADI LEO MUTAKULA KWA CHASHO LA USO WENU KISHA MUTAKUFA . KUFA NILAZIMA KUISHI NDIO BAHATI AMA KWA NEEMA YA MUNGU.

  KAMA VILE MTUMISHI MWINGILA ANAPOSEMA YA KAMA BABU IKO KARIBU YA KUFA NI SANA LAKINI KITU YA YEYE KUSEMA AOMBE MUNGU WAKE KAMA KWELI VILE ALIPOSEMA SIO NJIA YA KWELI MUNGU AMUSAIDIYE BABU ATUBU AMURUDILIYE MUNGU WA KWELI

  NA KAMA VILE ALIPOSEMA MWINGILA BABU ALISEMA MTI ILISEMA NA BABU KU NJIA GANI AMA ILIKUWA NDOTO NDIPO NILIPOSOMA

  SASA IKAKUWA JE SAMAKI ALIPOTAPIKA MTUMISHI YONA BAADA YA SIKU TATU ? MUNGU ALISEMA PIA NA SAMAKI ?

  kWA IMANI YANGU MUNGU IKO NA NJIA ZINGI YA KUZUNGUMUZA NA WATU KAMA VILE ALIPOMULIZA MUSA UKO NA NINI MKONONI ?

  WANDUGU TUSAIDIANE SANA KWA SAFARI YETU YA KWENDA MBINGUNI

  MUBARIWE WOTE

 7. Bwana Yesu asifiwe!!!
  watumishi wa mungu pamoja na koment zenu zote ukweli unabaki pale pale wewe unaye mwamini babu amini na yule anae amini mtumishi mwingira amini lakini ujue wewe mwenyewe hatuwezi kukuamini kwani sio mungu wala si mtu yeyote ambaye unajulikana siku ya mwisho utakua mavumbi kama sisi anasema waacheni watumishi nitajua mimi nitakavyo waathibu usisema mtumishi yeyote… wewe unae msema vibaya mtumishi mwingila angalia …..sana kuwa na wewe sikitu mbele za mungu kwani hatuoni unachokijua kuhusu mungu ………………wengi wanapenda kusema vibaya oh!! mwingira kakosea wewe umejuaje makosa kama si umetumia akili ya kibanadamu ok …..nacho weza sema mimi watumishi nikwamba kila mtu aangalie anacho kiamimi naweza kwenda kwa babu nikapona theni nikaendelea na ukahaba wangu ama unywaji pombe wangu pia naweza kwenda kwa mtumishi mwingira nikaombewa nikaokoka nikaacha ujinga wote nilio kua nafanya

  so watumishi wakike kwa wakiume usimdiskasi mtu wamungu waache wenyewe watumishi walio chaguliwa waambizane lakini sio wewe usiye chaguliwa wala usie jua kesho wapi utaamukia
  watumishi wapenzi naomba KILA MTU AAMINI KILE ANACHO WEZA KUAMINI

  AMINA KUBWA KWA WOTE WALIO CHANGIA MUNGU WANGU WA MBINGUNI AWABARIKI SANA….

 8. YESU NI MUNGU: SASA INAWEZA IKAMAANISHA MTU ANAWEZA KUAGIZWA NA YESU KASEMA MUNGU;
  ILA TUOMBEANE NATUTAKIANE HERI:KWA AJILI YA MAPITO HAYA
  MAGUMU;
  ILA DUNIA IMESHATEKWA TUNASUBIRI 2012; TANGAZO RASMI LA KUTAWALIWA NA 666: NA SIO MWISHO DUNIA; ILA MWISHO UPO WATEULE: DUNIANI KWA KIPINDI HIKI HAKUNA NABII ILA WABASHIRI:WATABIRI NA WANAJIMU MFANO MAREHEMU SHEIKH YAHYA NI MNAJIMU SIO NABII NDIO ; AMEKUFA KARIBU NA MAY 21;FATHER’S DAY OF MASONIC OF GREAT GRAND; NA ALIJIKUBALI YEYE SI NABII AKAUNGANA NA WANADAMU WENYE MATATIZO KUWASAIDIA KWA FEDHA:HUKU AKIWATIBU KWA KUFITINISHA MAJINI KWA MAJINI NA UJANJA UJANJA WA QURAN ; WATU WASOGEZE SIKU ILA SIO WAPONE;
  TUMIENI NGUVU YA MAOMBI SIO KUTEMBEA NA BIBLIA HAKUTOSHI: BIBILIA NYINGI NI VIGANJA VYA WATOTO KWA AJILI YA KUSOMEA NYOTA: OMBA MWENYEWE WA KINYWA CHAKO; BIBLIA NI MANENO YA KUKUONGOZA WEWE UWE NA TOBA YA KWELI NA KUKUPA MWANGAZA NA YALE YA AWALI YALIYOTENDWA NA MANABII: NARUDIA TENA MUDA HUU TUNAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU TU;HAKUNA NABII ATAKAYE KUAMBIA MUNGU ,LABDA HAJUI NAMNA YAKUWAKILISHA
  MTUMAINIENI MUNGU

 9. ANACHOFANYA MWINGIRA LABDA NI KWA AJILI YA KUSAIDIA WANADAMU ILA WENYE SHIDA KAMA SISI YA FEDHA ZA KAZI ILA KWA MAANA ZAIDI HAKUNA MUNGU KAMA YEYE AABUDIWE KWA SABABU MUNGU NI ROHO NA WAMWABUDUO IMEWAPASA KUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI, JE ROHO HIZO NI ZIPI? MWINGIRA ANAJUA WATU WANA SHIDA HASA SISI WATU WEUSI:

 10. Mwingira ni tajiri: na yote aliyosema Yesu ya kuwa tajiri kuingia katika mbingu ni afadhali na ni rahisi sana kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, jamaa ana BENKI;HII INAMAANISHA YEYE NI FREEMASON TAYARI;ANA HOSPITAL ZA KUTOSHA NA HII NI NYOKA IKIMAANISHA NDIYE YEYE FREEMASON: ILA CHA MAANA TAMBO ZA MANENO YA YESU ; SI HALISIA YA YALE NA YESU ANAYEZUNGUMZIWA

 11. dini siku hizi imekuwa biashara ndo maana mwingila ana muombea hadi kifo anaona atachukuliwa wateja wake.

 12. Mungu atusaidie sana..

  tunahitaji maombi na kuombeana sisi kwa sisi kumrudia Mungu bali siyo kutukia misanamu

 13. shalloom..

  issue hapa kila mtu kusimama katika imani na siyo kuangalia imani yako how strong you’r..otherwise mwisho wa siku utajikuta upo katika kundi ambalo huku tegemea kuwa ……angalia wapi Mungu anatenda kazi yake na je anawatumia watumishi wake ?je naweza pata msaada that cn have hope to you at last

  thank you all chments ..
  stayblessed in Jesus Name..i love you all.

 14. HALELUYA!

  Asante Melckzedeck kwa mchango wako.
  Kama ulivyosma ni kweli kwamba “TUNATAKIWA KUJUA MSINGI WA KUWA DAWA YA BABU IMETOKANA NA MUNGU AU SHETANI”. Nami kwa post yangu sijasema kama imetoka kwa Shetani bali nimeona sehemu ya matokeo ya dawa hiyo, ambayo ni tofauti na “wingu” tunalolisikia.

  Nilichotahadharisha ni, mtumishi yeyote wa Mungu akisema kitu, ni vyema kujihoji, na kutafuta sana kutoka kwa Mungu juu ya yale anayosema na si kumzungumzia vibaya kwa namna yoyote yule.
  Kwanini ninasema hivi? Ukiangalia kwa makini katika maoni yangu sijamlaumu kati ya hao wawili; Mtume na Nabii Mwingira wala Mchungaji mstaafu Mwasapile (Babu), kwakuwa wao kama watumishi wana kitu ambacho watu wa kawaida hawana, so wanaweza kuona au kujua vitu ambavyo wengine hawajui. Sasa tunawatambuaje kama wanachokisema ni sahihi? Kwa kumuuliza ajuaye siri zote, yaani Mungu. Kwakuwa kama mtu akisema ameambiwa / ameoteshwa na Mungu, wewe ni nani ubishe? Mpaka pale Mungu amnapokuwa amekuambia/kuonyesha/kujulisha/kukuhakikishia juu ya jambo hilo lililosemwa.

  Kwahiyo mtumishi yeyote wa Mungu, awe amelaumu/amelaani, ama amebariki huduma na dawa inayotolewa na babu HATUWEZI KUMUINGILIA KATIKA NAFASI YAKE YA UTUMISHI KWA KILE ANACHOSEMA.

  Kwa kifupi BAADA TU YA MUDA TUTAPATA MAJIBU, NAMI NAENDELEA KUJIFUNZA KUPITIA HILI.

 15. Maelezo mazuri sana ndugu yangu. Nimependa maelezo kuwa “watu watakufa hata kama tiba ni sahihi na muombeaji ni kutoka kwa Mungu kwani hakuna dawa ya kifo siku zikifika.”
  Hili linawasumbua baadhi ya watu kwani wapo wanaotetereka ama kupoteza imani wanapohisi “maombi yao hayajajibiwa” kwa kuwa tu walimuombea mtu wao na bado akafa. Utawasikia wakilalamika.
  MAELEZO MAZURI, BARAKA KWAKO

 16. Shalom!
  Mtumishi Iqualiptus hapa hakuna aliyesema kwamba kaambiwa na Mungu kwamba babu wa loliondo ametoka kwa Mungu lakini pia wale wanaosema kwamba katokana na hila ya ibilisi hakuna aliyesema kwamba kaambiwa na Mungu. Na pia issue siyo kupona tu kwani kuna watu wameombewa na wamekufa pia, ikiwa na maana kwamba mtu hapewi dawa ili asife au kuombewa ili asife watu watakufa hata kama tiba ni sahihi au muombeaji ni kutoka kwa Mungu kwani hakuna dawa ya kifo siku zikifika. Lakini pia kuna watumishi wengine wa Mungu wamekubali babu ni halali kutoa tiba ya kikombe. sasa wtu wanataka kueleweshwa basis ya babu kuwa ametokana na Mungu au na Ibilisi.

  Ubarikiwe mtumishi

 17. Iqualiptus,

  Pole na masaibu yaliyokupata kwa nduguzo walioenda kwa babu.La msingi tu upotofu wa Babu na kikombe chake haumfanyi naye Mwingira akaongeza upotofu mwingine juu yake! Kuna njia za kupambana na maadui zetu, ziko wazi katika Neno la Kristo! Tungelitegemea sana Nabii na Mtume huyu kulitambua hilo! Mpaka dakika ya mwisho msalabani alisema “WASEMEHE KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO”! Nabii wetu na mtume kasahau hilo? Au hajatumwa na Kristo! Mungu amsaidie na kumfungua!

  Ubarikiwe.

 18. Asifiwe Yesu!
  Wale wote wanaosema “Babu katumwa na Mungu” kwenye mjadala huu mbona hamsemi kama na nyie Mungu kawaonyesha hivyo? Mtumishi wa Mungu akisimama kuzungumzia jambo fulani si mpaka mbishane nae.

  MIMI NI MMOJA WA WALIOPOTEZA NDUGU WA KARIBU SANA. Kaka yangu alikwenda,akarudi, tukawa nae wiki kadhaa, HAKUPONA na alikufa. Ndugu wengine waliokwenda huko ni wengi wenye magonjwa tofauti tofauti lakini hakuna hata mmoja aliyepona (katika hawa ndugu zangu), JAPOKUWA MWANZONI WALILETA HABARI “NZURI” KUWA WANAENDELEA VIZURI TANGU WAPATE “KIKOMBE CHA BABU”. Nawazungumzia hawa kwakuwa ninawajua na nimezungumza nao ana kwa ana.

  Mwanzoni nilidhani pengine kwakuwa hawafuati “masharti ya babu” lakini baadae nikagundua sivyo kwakuwa nina-sample ya watu wa aina tofauti, kitabia, kiumri na ki-upendo kwa Mungu. Bamoja NA AINA ZOTE ZA HAO NDUGU ZANGU HAKUNA ALIYEPONA.

  Swali kwa wanaomsema mtumishi Mwingira kuwa “amekosea na ni muongo” JE NINYI MMETHIBITISHA UKWELI WA BABU KWA WATU WENU WA KARIBU KAMA MIMI?.

  Wapendwa, ili kujua siri za Mungu na utendaji wake pia utendaji wa adui, tunamuhitaji Mungu mwenyewe kwa Roho wake atusaidie. Hata kama uaijua Biblia yote utakuwa huielewi yote na SIRI ZA MUNGU ZINAGAWIWA NA ROHO WAKE KWA WALE ALIOWARIDHIA NA WANAOHITAJI TU.

  Yesu awabariki!

 19. Mtumishi Angel unaonekana una jazba sana. Pole sana mtumishi ni maongezi tu na watu kueleza hisia zao juu ya lile wanaloliona kwamba ni sahihi. Unajua hapa issue kubwa ni juu ya kusema babu wa loliondo ni mshirikina na siyo kwamba Mwingira ni mtumishi wa Mungu au la. Mimi ndiyo ninavyoiona mada imekaa. Issue ya Mtume imekuja baada ya kumtangazia kifo babu watu wakahoji kwa nini ametangaziwa kifo na wakati watu wakitazama wanaona siyo Roho wa Mungu amesema babu atangaziwe kufa?? Hapa ndiyo hata mimi naona kuna jambo la kuerekebisha kwamba ikiwa babu ni mshirikina basi kazi yake itavunjwa ila tusije tukawa tunashindana na Mungu. Kwani kuna shida gani kazi ikiwa ni ya kishirikina itavunjwa tu lakini ikiwa ni ya Mungu kweli itasimama kwani mwingira naye si amesema kwamba ametumwa na Mungu? je kuna mtu aliyekuwepo wakati wakiongea na Mungu? naona hakuna ila tunaona kazi inaendelea. na babu naye amesema kwamba ameonyeshwa na Mungu pia hatukuwepo hivyo tusubiri huku na maombi mengi naona itajulikana! Na ukweli utakapodhihirishwa kila mtu atajua lakini kwa sasa tusije tukawa tunaongea mambo ambayo hata nafsi zetu zitatuambia kwamba hatuna uhakika na tunayozungumza. Barikiwa in Jesus Name!!

 20. Ngugu Angel wasalaam!!
  Nimesoma maoni yako na ninaomba nikuulize haya yafuatayo
  Hapa ninaomba tujenge hoja zaidi kuliko kujibizana kwa jazba, na ni matumaini yangu utanisaidia sana kama kweli nimepotea.
  Je! kwa misingi ya Biblia Mtumishi Mwingira yupo sahihi wapi kulingana na hoja hii na Kwa misingi ya Biblia Babu wa Loliondo kakosea wapi! Ahsante!!!!

 21. Zepipo, umeongea saana but am sorry to tell you that what you have said did not make sense at all! Nyie ndo mnaotumiwa na Ibilisi kuharibu kazi za Mungu na kuwadhoofisha watumishi wa Bwana. Who are you to judge anyone! Umejitega kwa maneno ya kinywa chako, You are now in trouble and YOU NEED HELP!

  You should get this into your mind…you can not stop God’s purpose. Usishindane na Mungu, utaumia. Huyo Ibilisi mwenyewe anayekutumia alishindwa… na hata leo bado ni looser. Anawavuta wengi wamuasi Mungu kwa kuwatumia watu kama Babu Loliondo na kina nyie bila nyie kujijua (au pengine mnajitambua). Unahitaji hekima ya Mungu kuliona hilo tena unahitaji kuomba rehema kwa Mungu kwa kumuongolea vibaya mtumishi wake.
  Who are you to judge the servant of God!!!!

  Whatever you say, ukweli unabaki palepale…you Zepipo CAN NOT change the truth. NO ONE can!

  YOU NEED HELP!

 22. Mimi binafsi napenda kuwashukuru wote mliochangia mada hii vizuri na kwa hali na mali mkiwa na lengo moja la kumkumbusha mtumishi Mwingira kwa pale alipojikwaa kurejea upya, huku akijua yeye kama anavodai ni mtumishi wa Mungu basi watu wengi wanamtazama na kujifunza mengi kutoka kwake.

  Nimefurahiswa sana na hoja aliyoitoa ndugu yangu Hagai Kinyau maneno yake ya busara ni sawa kabisa nandio yamebeba dhima kuu ya mchango wangu, ninaomba kwa watu wote wenye akili timamu watilie maaanani haya yatawasaidia sana. Vilevle nimependa mchango wa wachangiaji wengine kama vile Orb,Bubelwa na John.

  Kabla ya kutoa kile nilichonacho naomba nichangie kidogo kwenye maoni ya Dada Angel anaposema watu wanamhukumu mtumishi bila kujua, ni kweli kabisa katika mengi aliyoyaandika dada Angel yanaelekea kwenye ukweli kwa njia moja ama nyingine, ila kama atasoma makala hii aelewe haya yafuatayo kwa msaada wake;
  -Mosi ni kwamba ktk michango yote iliyotolewa ni wachangiaji wachache sana wamenyoosha mkono moja kwa moja kwa muktadha wa kuhukumu ila wengi wamejaribu kutoa maoni na ushauri hasa wakirefer milango ya biblia, na zaidi ya hayo wengi wameonesha kusikitishwa na Mtumishi kuonekana kama yupo nje ya maaandiko na si vinginevyo, kitu ambacho ni sawa kama mtu ana dalili za kuwa nabii wa uongo kwann tusiambiane kwa tahadhari ili tusije tukapotea??? nayamkini kupoteza wengine kwa mambo ya uongo na uvumi.

  -Pili; dada yangu Angel naomba ufahamu kuwa si wote waitao bwana bwana ni wa Bwana wengi ni feki hasa kama wewe umejaliwa kupewa macho ya kiroho juu ya hili.

  -Tatu; ukweli nakwambia ukimpima Babu wa Loliondo na Mwingira ktk muktadha wa jambo hili ukifwata misingi ya Biblia utaona Mwingira amepunguiwa hekima ya mungu bali anatumia uwezo na maarifa yake mwenyewe akizingatia maslahi yake na si ya Biblia,hivyo nafikiri umeelewa angalau kidogo kwann nasema hivi.

  Mwisho ni kwamba Mwingira anaishi kwenye akili zake zaidi maaana Biblia hasa Bwana-Yesu Kristo amehimiza Upendo kama amri kuu na haya mengine kama kutabirtabir mara Utume,kufufua wafu mara kuponya na mengine mengi ni ya ziada tu. Bare in mind kwamba UPENDO ndio kitu cha msingi ktk Ukristo ambapo angekuwa nacho Mwingira asingesema haya hata kidogo.Ila kwa masikitiko makubwa kabisa walokole wengi watakosa mbingu kwa kulisahau hili na kuamini kuwa wamefika na kubaki kutoa hukumu kwa wengine kana kwamba wao wameshamaliza safari.

  I’M VERY SORRY FOR THAT,
  MAY GOD HELP US!!!!

 23. Hii sasa imekuwa tena sio mjadala wenye nia ya kujenga tu bali pia kuharibu.Hii ni vita ya kiroho kati ya falme mbili zenye imani tofauti…sasa mnaposema yeye anahukumu mbona nyie basi mnasomeka kumhukumu huyu mtumishi wa Mungu Mwingira! Imani yenu ipo wapi…Ofcourse, imani yenu ipo kwa babu.

  Laiti mngaliyajua maandiko vyema na kupata ufunuo wa Roho mtakatifu naamini msingemshambulia, msingemuhukumu, or question his actions the way you do…Eh Mungu uwasamehe kwamaana hawajui walitendalo.

  Kwanza kabisa chuki, hasira na jazba zilizopo juu ya mtumishi wa Mungu Apostle and Prophet Josephat Mwingira ziwekwe pembeni ili mpate kuipokea kweli nayo kweli iwaweke huru. We have no right to judge someone, only God does.

  Haters trying to destroy his reputation but that cant happen because whatever you say or question him it will not change the truth that he is indeed the annointed man of God and he is sent to preach the Gospel,speak the truth and set people free from lies. Believe it or not, Yeye ni mtumishi wa Mungu mpakwa mafuta APOSTLE AND PROPHET and no one can ever change this truth!
  Oh Yeaah, we all have the right to follow what we wanna believe and say what we think and feel BUT the truth will never change, God of Israel will always be God and whatever he shall say through his TRUE servants it shall be done whether you believe him or not whether we like it or not. Whosoever believe in the truth shall be set free indeed but you aint ready to hear the truth so how can you be set free! We are lost…but the good news is Jesus came to rescue the lost. FAITH in him and his true servants will set us free…

  Isaiah 54:16-17 says NO weapon forged against you will prevail, and you will refute every tongue that accuses you. This is the heritage of the servants of the LORD, and this is their vindication from me,” declares the LORD. Therefore guys we should all be careful what we say against servants of God, in other words you should stop pointing fingers….if you dont know what to trust anymore, if you aint believe in him or other church and servants then as much as you wanna know the truth why dont you ask God himself to show you the truth!!! OR why then dont you those who are against him shut your mouth and wait and see the manifestation of his words coming to pass! perhaps you will believe…TIME WILL TELL. Shalom

 24. Swali zuri sana ndugu yangu Melckzedeck.
  Kama kuna mtumishi aliyeenda kwa Babu, akaona utoaji dawa na kukiri kuwa ni wa kishirikina, na atueleze kilichomfanya aamini hivyo.
  Blessss

 25. Shalom wapendwa!
  Nami nichangie kwa kifupi hoja iliyopo kwenye jukwaa hili la KIMungu. Yaliyozungumzwa ni maoni mazuri ila tunatakiwa kuomba zaidi kuliko kunena maneno matupu ya habari za kusikia ambazo zinafanya watu wa Mungu tunaonekana kama watu wa maneno ya kuzua tu. Mambo ambayo kwa maoni yangu nilitarajia kuyasikia ni haya yafuatyo; 1) Mtumishi asimame aseme aliomba na Mungu akamwambia kwamba tiba ya babu ni ya ushirikina na siyo maneno ya kusikia kwa watu wengine ndiyo yawe mahubiri yaani third party information. Watu wa Mungu hatutakiwi kwenda hivyo.
  2) Kama kuna mhubiri ameenda kwa babu kudhibitisha habari ya tiba hii anayotoa babu akaona mambo ya kishirikina yakitendeka kuliko kusikiliza toka kwa watu kwa sababu unajua watu ni wapotoshaji wanaweza wakatunga jambo lisilokuwepo kabisa likawa kama lipo na kwa sura wanayoitaka wao.
  Ni maoni yangu hayo Watumishi mubarikwe sana!!!

 26. Ndugu zangu wapendwa,
  Wengi wameandika mengi kuhusu mada hii, ila wakati napitia wachangiaji mada, nilikutana na ndugu AMINI,
  Ambaye alisema
  TUNATUMIKIA TORATI, NA WAKATI HUO NEEMA YA KRISTO.
  Ni ukweli usipingika kuwa tunahitaji waalimu wa kufundisha Neno.
  Utakumbuka wakati wa Yesu, alipita mahali watu hawakumpokea vizuri, wanafunzi wake mmoja wao akasema BWANA TUITE MOTO???
  Yesu akasema Hamjui ni Roho gani mliyo nayo, hakuwaruhusu waite moto,
  Tena walisema TUITE MOTO KAMA ELIYA ALIVYO FANYA?? Nadhani mnajua Eliya alivyofanya.
  Leo Kanisa linaita MOTO.
  Math 5;
  Ijulikanayo kama Hotuba ya mlimani, inatufundisha namna ya kuwafanya adui zetu, nadhani watu wengi, wakiwemo watumishi wa Mungu hawasomi maelezo haya, wengi wangali kwenye TORATI.
  Ebr 8;13-
  Kwa kule kusema Agano la Jipya,amelifanya lile la Kwanza kuwa kukuu,
  Lakini kitu kianzacho kuwa kikuu kuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.
  (Kwa kusema hivyo kuna vitu ambavyo viliishatoweka, katika Agano la Kale vilitumika, lakini Agano jipya ukivitumia unaonekana wa ajabu)
  Ndio maana nimesema tunahitaji waalimu, na kwa sababu hiyo waalimu wa uongo wamepata nafasi kuingiza mafundisho ya uongo, na watu kwa kutojua Kweli wengi wametumbukia tayari.
  Nitoe mfano mdogo-
  Efeso 2;20-
  Mmejengwa juu ya msingi wa Mitume na Manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
  Efeso 4;11-
  Naye alitoa wengine kuwa MITUME, na wengine kuwa MANABII, na wengine kuwa WAINJILISTI, na wengine kuwa WACHUNGAJI, na WAALIMU.
  Biblia imesema tumejengwa katika msingi wa huduma mbili hizi kubwa, yaani MTUME, na NABII.
  Ebu tuangalie katika Biblia, watu waliotembea na Bwana Yesu live, hakuna aliyekuwa MTUME na NABII kama yupo mtu najua huyo atusaidie,
  Paulo alikuwa Mtume,
  Alichukua Barnaba, Sila Hao ndio walikuwa MANABII.
  Petro alikuwa MTUME.

  Sasa leo mtu anakwambia kuwa yeye ni
  MTUME na tena ni NABII.
  Yaani ni sawa na kusema kuwa KANISA LIMEJENGWA JUU YAKE, MTU MMOJA TU,
  Siku hizi za mwisho mambo mengi yanatokea, na yataendelea kutokea,tuwe macho,tuwe makini,
  Kwanza tuone Mitume na Manabii wa siku hizi wanapatikanaje?
  Mtu anaamka asubuhi anatangaza kuwa mimi ni Mtume, au mimi ni Nabii-
  Mdo 13;1-
  Na huko Antokia katika Kanisa lililokuwako, palikuwa na Manabii na Waalimu,nao ni Barnaba, na Smioni aitwae Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Mfame Herode,na Sauli, basi hawa wlipokuwa wakimfanyia Bwana Ibada na kufunga, Roho Mt akasema, nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile iliyowaitia, ndipo wakiisha funga na kuomba wakaweka mikono juu yao wakawaacha waende zao.
  LEO NI MTU ANAAMKA TU MRADI ANA HELA, TAYARI NI MTUME,TAYARI NI NABII.
  Wapime Mitume hao.
  Mdo 14;8–18.
  Mst 14-
  Lakini Mitume Barnaba na Paulo walipopata habari,wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika mkutano,wakipiga kelele, wakisema akina Bwana mbona mnafanya haya? SISI NASI TU WANADAMU HALI MOJA NA NINYI,TWAWAHUBIRI HABARI NJEMA, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili, na kumwelekea Mungu aliye hai, aliye umba Mbingu na Nchi na Bahari na vitu vyote vilivyomo,ambaye zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote yaende katika njia zao wenyewe, lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema,
  Akiwapeni mvua kutoka Mbinguni,na nyakati za mavuno,akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha.
  NA KWA MANENO HAYO WAKAWAZUIA MAKUTANO WASIWATOLEE DHABIHU.
  (Linganisha na mitume wa leo)
  YESU ANASEMAJE HAPA CHINI??
  Math 12;7-
  Lakini kama mgalijua maana yake maneno haya,NATAKA REHEMA WALA SI SADAKA, msingaliwalaumu wasio na hatia.
  Math 9;13-
  Lakini nendeni mkajifunze maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA WALA SI SADAKA, kwa maana sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi.
  (Linganisha na wa siku tulizo nazo, Bwana anasema alikuja kuwaita wenye dhambi)
  Akiishawaita wakaja kwake, basi waziache,sio waje kwake na bado wakae nazo)
  Nikihitimisha mchango wangu ni kuwa watumishi wasio wa kweli watatuchanganya tu, wala si ajabu.

 27. Bwana yesu asifiwe wapendwa narudi kwa mara nyingine nadhani wote tupo hapa kwa kuelimishana ili siku moja tukakutane katika ufalme wa milele.

  Mi sijasema mwingila yuko right kotekote ndio sababu nikasema mwingira nae pia ni mwanadamu amevaa mwili wa nyama kukosea kunawezekana kwa kuwa yeye si malaika na ndio maana hata biblia imesema tukisema hatuna dhambi tunajidanganya.

  Tunaishi kwa rehema za Mungu wetu, nilitarajia kwamba kwa kumkosoa Mwingira kwa makosa yake pia na babu nae hafanyi right , ni kweli babu hastahili kuombewa kifo, na pia babu hawezi kufa kwa laana ya Mwingira kwa sababau hatujui Mungu ana mpango gani na maisha ya babu.

  tunachotakiwa ni kuwaombea wote kama Mwingila anakosea katika kauli basi Mungu amponye na Babu pia kama dawa zake hazijatoka kwa Mungu basi Mungu ayafunue haya kwa watumishi wake ili wasiende huko.

  Mubarikiwe

 28. Ndugu yangu Marthawilly.
  Katika maoni yako umesema “kuna baadhi ya watu waliotoka kwa babu wa loliondo ukiwaambia sasa umepata uponyaji basi mpokeee Yesu anakujibu babu ajanishauri hivyo.” na kisha ukaongeza kuwa “Mi nashuhudia watu wanaoponywa kwa maombi wanampokea Yesu na kufanya kazi yake kwa utiiifu, sisi sote tumewaona watu wengi wenye vyeo viongozi na hata mataifa mengine wameenda kwa babu lakni hakuna aliyerudi na kulisifu jina la bwana badala yake jina la babu ndilo linalozidi kupanda chati”
  Ningependa kujua kama hizi ni TAKWIMU RASMI ama unazungumza kulingana na wale waliokuzunguka?
  Ni kweli wale wanaoponywa kwa maombi wote huendelea kufanya kazi nzuri ya Bwana? Nina mashaka na hili kwani nawajua waliotangaza kuokoka kwa hofu ya kufa na wakishapona wanarejea walikokuwa. Na baadhi yao walishaandikwa hapa (wanamuziki maarufu) ambao walitangaza kuokoka walipokuwa na matatizo, wakashuhudia kuwa wameombewa na baada ya kuponya tunaona walipo.
  Ni kweli kuwa “HAKUNA ALIYERUDI NA KULISIFU JINA LA BWANA”? Mimi nawajua wachache.
  Tuwe makini na maoni yetu ili kuhakikisha kuwa FACTS zinabaki kuwa FACTS na mawazo binafsi yanakuwa hivyo.
  BARAKA KWENU NYOTE

 29. Martha willy;

  Nakubaliana na wewe kabisa juu ya hilo lakini mashaka yangu yapo kwenye kauli anazotoa Mwingira juu ya babu. Yeye kama mtumishi wa Mungu hakupaswa kutoa kauli hizo hata kama huduma ya babu si ya Ki- Mungu. Kwanini amuombee kufa? Kwanini aseme waumini wake watakaoenda kwa babu watakufa. Mi nafikiri angepaswa kuwahubiria kweli waumini wake instead of kuwatisha kuwa wakienda kwa babu watakufa na pia amuombee babu na kumfundisha ili aange kuwadanganya watu na amtumikie Mungu wa kweli kwani ni kusudi la Mungu kuwa kila mmoja aifikilie toba na si kufa katika dhambi. Sasa Mwingira anavyomuombea babu kifo anamsaidia au anamuangamiza? Na kwanini amuhukumu babu kiasi hicho ilihali yeye ni mtumishi wa Mungu na anayajua maandiko. Pamoja na kuwa tiba ya babu haitokani na Mungu vile vile Mwingira kakosea sana.

  Eee Mungu utuhurumie wanao………..

 30. Bwana yesu asifiwe unajua mwingila ni mtumishi wa Mungu pia ni mwanadamu amevaa mwili wa nyama, tusichukulie upande mmoja tu wa mwingila je nani alishuhudia babu alipokuwa anahojiwa na TBC,mi nadhani mtumishiwa Mungu anapomwombea mtu na kupona mtu huyo anamkili Yesu na kumpa maisha yake lakini sijasikia mtu aliyetoka kwa babau baada ya kuponan ameamua kutoa maisha yake kumpa Mungu,nilimsikia babu kwa masikio yamngu akihojiwa na tbc akisenmma kwamba mtu akinywa ile dawa kama ni mlevi basi asitumie pombe hadi baada ya siku kadhaa ndipo atumie pombe,hivi ni biblia gani ambayo inasema mtu anywe pombe.

  kuna baadhi ya watu waliotoka kwa babu wa loliondo ukiwaambia sasa umepata uponyaji basi mpokeee Yesu anakujibu babu ajanishauri hivyo.

  Mi nashuhudia watu wanaoponywa kwa maombi wanampokea Yesu na kufanya kazi yake kwa utiiifu, sisi sote tumewaona watu wengi wenye vyeo viongozi na hata mataifa mengine wameenda kwa babu lakni hakuna aliyerudi na kulisifu jina la bwana badala yake jina la babu ndilo linalozidi kupanda chati

  Jamani Mungu atusaidie wapendwa atupe macho ya rohoni ili tuongee vitu tulivyo na uhakika navyo.

  MUBARIKIWE

 31. Kaka yangu Haggai Kinyau, kwanza nakupa pongezi sana kwa comments zako ulizotoa,najua ni Roho mtakatifu ametenda kazi ndani yako.Ni kweli kabisa ulichosema kuwa WATUMISHI WA SASA WANAFANYA “adui” ZETU KULIDHARAU JINA LA BW. WETU YESU KRISTU.Hii ni kwa sababu ya matendo yao na maneno yao,yasiyokuwa na mwelekeo wa yale aliyotufundisha Bw. wetu.
  Pia namuomba huyo dada Anne Muhumula atusaidie kupeleka ujumbe kwa mtumishi kaka Mwingira,amuombe Mungu amsaidie maana ameanza kutoka kwenye mstali,ameanza kuwa na kiburi,mpaka anajiona ni zaidi ya watu wote,eti yeye ni BABA hata Bw.wetu Yesu kristu alisema tunaye BABA mmoja ambaye ni YEHOVA yaani Mungu aliyeumba mbingu na dunia.jamani watu wa Mungu tusaidiane kuwaombea watu wa Efatha Mungu awafungue macho,waijue kweli nayo kweli iwaweke huru.
  Mungu wetu aliyemwingi wa rehema awabariki woooooooooote!

 32. Wapendwa shalom
  Ninawapongeza watumishi wote wa Mungu ambao mmechangia mada hii mkiwa wazi kwa pamoja kwa umoja kwa roho moja ijengwayo na kweli ya Kristo Yesu Mungu mkuu.
  Naweza kusema kuwa mtumishi wa Mungu Nabii na Mtume Mwingira amekosea kutoa matamko yale kama mwakilishi wa Mungu hata kama huduma ya babu ni kutoka kwa shetani.
  Kwa bahati mbaya sana watumishi wengi wa Mungu leo wanapenda kutumia maandiko kutoka agano la kale jinsi yalivyo kujipatia mamlaka ya kutoa hukumu na maamuzi na wakati huo huo wakijinasibu kusimamia neema ya Yesu. Huu ni mchanganyo ambao umelifanya kanisa leo lipoteze sura halisi ya mwili wa Yesu. Tupo kati kati ya utekelezaji wa Torati na wakati huo huo tunaitumikia injili ya Yesu. Matokeo ya maisha haya ni kuwa na wakristo vugu vugu ambao kwao maneno ya wachungaji wao.
  Ni wakati ambao tunatakiwa kuamka na kupiga kelele kuweka wazi uhalifu huu wa neema ya Kristo Yesu kwani yeye yu malangoni kulichukua kanisa lake.
  Mungu awabariki sana

 33. napata mashaka sana kwanza kwa majina wanayojipa hawa ‘the so called watumishi wa mungu’ wanaojipa majina kama mitume manabii nk. pili hii kauli ya mwingira n si ya kwanza kusikia toka kwa aina ya watu kama mwingira nadhani ni MGONGANO WA KIMASLAHI 2. naamini kwa tiba hii ya babu samunge loliondo si wote watapona ila wapo watakaopona. iliandikwa imani yako itakuponyesha.

 34. Mtawatambua kwa matendo yao, Mpendwa wangu tambua kuwa linaloanzishwa na mwanadamu

 35. Mungu haendi kwa namna hiyo, wakati mwingine ni heri mtumishi wa Mungu kunyamaza na kufanya aliloitiwa, kama ni kweli alitamka hayo.. Mambo mengine ni ya kumwendea Mungu moja kwa moja ili yeye ndio afanye kitu kitakacho ziokoa roho za watu wake!

  Suala babu halikupaswa kuleta hasira au chuki dhidi yake, maana haiwezi kusaidia, na hata kufa kwake sio usalama wa roho za watu wanaoenda huko. Ninaona badala yake lingetumika kama changamoto kwa ajili ya kulisaidia kanisa na kuongeza nguvu ya kulijenga ktk misingi mizuri ya Neno la Mungu ili wasiyumbishwe tena hata baadae hali inayofanana na hii ikitokea!

  Mungu azidi sana kuwasaidia watumishi wake!

 36. Ndg yangu ANNE MUHUMULA (EFATHA).
  Huyo MTUMISHI unayemsema (naamini ni Mwingira) ndiye anayestahili kujua kuwa yeye ni binadamu na sio malaika wala Mungu. Kujivika kazi na wajibu wa Mungu kunamfanya ajiondoe kwenye kundi la wanadamu. Nadhani ni yeye anayestahili kuelezwa kuwa ni binadamu na sio Mungu na sio sisi. Sababu hasa ya sisi kumsema ni kwa kuwa amejifanya Mungu na si mwanadamu. Anatenda anayopinga na anashangaza.
  Watu husema Mungu atadhihirisha na naamini ameanza kudhihirisha lile ambalo tumekuwa tukiliwaza na kulitilia shaka.
  Anatoa kauli mbele ya umati ambao TUNAFAHAMU BAADHI YAO ambao alishawafanyia huduma na hawakupona, na sasa wameenda kwa “Babu” wamepona. Unadhani wanamuelewaje?
  Labda kama unaweza unisaidie maswali yangu hapo juu kwamba “Huyu NABII NA MTUME ni nani? Alifika vipi hapo alipo? AMEUPATA WAPI UNABII NA UTUME. NI NJIA GANI ZINAZOTUMIKA KUMPATA NABII NA MTUME?”

 37. naona sasa watumishi wa Mungu na dini nayo imekuwa ya kisiasa zaidi. Badala ya wewe mtumishi wa Mungu kupiga magoti na kuomba unaanza kuhukumu who are you by the way? wewe unajijua upo sahihi hapo ulipo? Tumwombe sana Roho wa Mungu katika hili

 38. Mwingira napingana nawe kabisa, u nani wewe hata uhukumu, nilikujua kwa mara ya kwanza kupitia gazeti moja la dini huku kukuwa na picha yako(mbele ya gazeti) na watumishi (nafikiri kutoka Efatha kilimanjaro) wakiwa wameinama miguuni kwako kukuabudu na hukuwaamuru wasikuabudu? ngali unajua imetupasa kumuabudu Mungu peke yake?Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako. Sipo pamoja nawe Mwingira kama kweli huyo babu si mtumishi wa Mungu, simama katika nafasi yako na Mungu aliye hali atamdhihirisha wazi wazi.

 39. Anne Muhumula(EFATHA).
  Naomba utueleze una maana gani, tusimseme mtumishi gani Mwingira au nani? Na kama Mwingira hatakiwi kusemwa, je yeye amepata wapi ruhusa ya kumsema na kumtamkia kifo mch. mstaafu Ambilikile? Au yeye ni ruhusa kuwasema na kuwalaani wenzake lakini yeye kusemwa ni mwiko!!

  Kama unasoma biblia yako vizuri kwenye 2 Samweli 12:1-14, Daudi aliyekuwa mfalme na mpakwa mafuta wa Bwana alionywa na kukemewa na Nathani kwa kitendo chake cha kumchukua mke wa Uria aliyeitwa Bath-Sheba na kuzini naye. Kama Daudi mpakwa mafuta wa Bwana wa kiwango kile alionywa na kukemewa na Nathani sembuse Mwingira!! Kitu kizuri ni kwamba Daudi alikiri na kutubu dhambi hiyo, ukisoma 2 Samweli 12:13-14 inasema hivi;

  “Ndipo Daudi akamjibu Nathani ‘nimefanya dhambi dhidi ya BWANA’ Nathani akamjibu ‘BWANA amekuondolea dhambi yako. Hutakufa. Lakini kwa sababu kwa kufanya hili umefanya adui za BWANA kuonyesha dharau kabisa, mwana atakayezaliwa kwako atakufa”

  Nadhani umeweza kuona jinsi ambavyo watumishi wengi wa sasa wanavyofanya ‘adui’ zetu kulidharau jina la Bwana Yesu kama amabavyo Daudi alifanya Bwana adharauliwe na adui zao. Swali la kujiuliza ni hili je watumishi wa leo wako tayari kukiri makosa na kutubu kama alivyofanya Daudi? Nina uhakika wengi hawawezi kufanya hivyo, la sivyo Mwingira angekuwa tayari amejitokeza hadharani na kusema kuwa hayo yalikuwa ni maneno yake mwenyewe wala sio kutoka kwa Mungu maana Mungu wetu ni mwenye huruma na rehema nyingi, hapendi watu wake wafe katika dhambi na kupotea milele.

  Tuzidi kuwaombea watumishi wetu ili waweze kusimama kwenye utumishi wao, wakati huo huo tukiombeana sisi kwa sisi kwa sababu maombi ni silaha kali sana ya kuubomoa ufalme wa shetani ambao kwa sasa umejipenyeza sana hata kwa watumishi wakubwa wa Bwana. Pia Maombi ya watakatifu yana harufu nzuri ya manukato kwa Mungu wetu, tusichoke kuombeana na kuwaombea watumishi wetu ili wasimame katika kweli ya neno la Mungu.

  Baraka nyingi kwako Anne na Wana SG wote.
  Pasaka Njema.

 40. Msimseme mtumishi wa Mungu vibaya, mtapata laana.Wao ni binadamu kama nyie sio malaika.

 41. Ndugu Orbi.
  Umenena vema.
  Swali la kwanza ni kuwa WATU WANAMSIKILIZA NANI? Huyu NABII NA MTUME ni nani? Alifika vipi hapo alipo?
  LABDA HANA VIGEZO VYA KUWA ALIVYO hivyo watu wanamu-overate.
  Niliwahi kuuliza AMEUPATA WAPI UNABII NA UTUME. NI NJIA GANI ZINAZOTUMIKA KUMPATA NABII NA MTUME? Maoni yangu hayakubandikwa.
  Pengine kwa kujua alikotoka, watu watajua tunakoelekea naye.
  Nina wasiwasi kuwa HAJAKOSEA, BALI HUYU NI YEYE. Yeye asiyejua alipo wala aendako.
  Bado NAOMBA KUJUA HISTORIA NA ASILI YA UTUME NA UNABII WAKE.
  I hope sio wa “kuoteshwa” na ambao unapinga “ndoto” za wengine zanye maslahi.

 42. NATHAN,

  Asante kwa ujumbe wako, somo kubwa hapa la kujifunza ni kuwa Watumishi ni watu wa kawaida tu walioitwa na Mungu, wanaweza kukosea, wanaweza kutoa mawazo yao, lakini kitu ambacho naona kimejengwa kweti sisi waumini wengi ni pale msingi wetu wa Imani unapoanza kujengwa juu wa Watumishi na wala SIO MANENO YA MUNGU! Hii kwangu mimi naona imekua ni tatizo kwa KANISA LA TANZANIA! Waumini wengi ni rahisi kuamini maneno yanatoka Kwa NABII, MTUME kuliko Kweli iliyodhahiri ndani ya Neno!

  Labda kwa matamko kama haya toka Kwa Mwingira mwenyewe yanaweza kufungua macho kwa baadhi ya waumini, kuwa NABII naye anahitaji maombi!Nabii anahitaji msaada! na NABII pia anaweza kuzungumza yale yamjazayo moyo na wala sio yaliyoletwa na ROHO MTAKATIFU!

  Na kwa hili watu wakajifunza kukaa kwenye NENO LA MUNGU LISILOTETEREKA!

 43. Wakati wa siku za mwisho ukifika basi kutakuwa na manabii wa uongo!! Mimi sina shaka kabisa huyu Mwingira ni mmoja wao! Iweje awe na jazba namna hii badala ya kutumia muda wake kumuombea babu?? Dini yangu ya kikristo ni dini ya upendo… imekuwaje kuhusu yale maagizo ya “MSIHUKUMU”????

 44. Shalom wapendwa!

  it is written”Dear children, let us not love with words or speech but with actions and in truth.” 1John 3:18 Jesus once said that we should love our enemies. (Mathayo 5:44 – Lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. Mathayo 5:39 – 40) because he knew that at some point in our lives tutakuja kupata taabu sana katika kutofautisha kati ya adui wetu wa kweli na wale tunaowadhani ni adui zetu. Mtumishi mmoja aliwahi kufundisha mahali fulani juu ya vita vya kiroho akasema, “kama adui yako unamuona kwa macho ya damu na nyama basi ujue bado hujamjua adui yako”
  Ninachojiuliza mimi hapa ni kwamba, Hivi adui tunayeshindana naye ni nani? anaonekana?
  jambo la pili ninalojiuliza ni kwamba, Pamoja na ukweli kwamba binafsi na watumishi wengi hatukubaliani na hili linaloendelea kule loliondo, Je hii ni sababu ya kutamka laana juu ya mtendaji na wale wote waliokwenda loliondo? ni sababu tosha ya kuwatamkia mauti?
  Does this constitute kile yohana anachotufundisha hapo juu, “Kupenda kwa tendo na kweli”
  Biblia ninayosoma mimi inaniambia “Mungu hapendi mtu yeyote apotee bali wote waifikilie toba” (2Pet. 3:9).
  Nini maana ya upendo wa kweli? kama Mungu, aliye mtakatifuna anayechukia dhambi huvumilia ili tu mtu afikilie toba, sisi tulio waovu tunapaswa kuvumiliana kwa kiwango gani?
  Wakati fulani niliwahi ku comment na kuonesha huzuni yangu juu ya huu ukristo wa kishabiki nikinukuu maneno ya mtu mmoja aliyesema “commitment without reflection is fanaticism in action, but reflection without commitment is the paralysis of all action”
  Huu si wakati wa kufanya ushabiki, ni wakati wa kukaa chini na kujifunza maneno ya Mungu tukijua kuwa watumishi nao ni wanadamu na kuna wakati madhaifu yao yanaonekana, tunahitaji kuwaombea na si kushangilia tu kila kitu wanachosema, kwa kuwa kuna wakati wao pia hutoa yale yaijazayo mioyo yao yasiyo na uhusiano wowote na makusudi ya Mungu.
  Ninasikitishwa sana nakile kinachoendelea kule loliondo, hasa baada ya kufuatilia documentary inayooneshwa mlimani TV, lugha wanazotumia wale wasaidizi wa babu pamoja na maneno ya babu mwenyewe. vimenithibitishia na kunipa uhakika wa kile nilichokiamini toka mwanzo kuwa tiba hii haina uhusiano na uponyaji wa Mungu.
  Mungu awabariki.

 45. Kwa kuwa ni imani yetu kuwa MUNGU NI MMOJA, NA ROHO MTAKATIFU NI MMOJA, NA NDIYE AWAONGOZAYE WATUMISHI WA MUNGU, yatokeapo haya maana yake ni rahisi… Si wote wasemao huongozwa na ROHO humaanisha ROHO MTAKATIFU, maana WASINGEHITILAFIANA WALA KUOMBEANA MABAYA… Hivyo basi, aidha mmoja au wote mzushi, maana hawawezi wote kuwa wa kweli. Waumini tutafakari upya imani zetu kwa hawa ‘WATUMISHI, MITUME, MANABII, WACHUNGAJI, MAPADRE, MAASKOFU…” na mafundisho YAO, na IMANI ZETU KWA MUNGU!

 46. Mi nadhani kwa uelewa wangu mdogo wa biblia nabii wa Mungu humuonyesha mambo yatakayotokea (soma habari za manabii wote hata yule wa Nigeria TB Joshua anatabiri mambo yatakayotokea)who is Mwingira? Prophet, Pastor,Apostle or what? DEUTRONOMY 18:22

 47. Hatimaye amedhihirisha MAKUCHA ya u-uungu wake.
  Leo anajiunga na Mch Gwajima kujitangazia nafasi za Mungu.
  Kama nilivyofanya kwa Mch Gwajima, nasubiri kuona

 48. Mwingira.
  maandiko yanasema tusiwanenee vibaya watumishi wa Mungu,lakini mimi nina mashaka na utumishi wako.Kwani wewe unasema ni nabii,unayeyajua vzuri maandiko ya Mungu,inakuwaje unaenda kinyume? Nasema ivyo kwani kuna siku pia niliona unawaombea viongozi (mafisadi)wafe na kansa. Bw,wetu Yesu Kristu pamoja na makosa yetu yote hajawahi kutuombea kifo kwa Mungu,we ni nani hata uwaombee watu kifo? Ebu muogope Mungu na uache kujifanya Mungu mtu. Kufa kwa mwanadamu ni siri ya Mungu na wala siyo ya mwanadamu,kama ni ivyo basi wote tungekuwa hatupo,kwani kila mtu ana adui zake. wafundishe watu mambo ya kiroho kwa ajili ya ufalme wa Mungu ujao na wala siyo mambo ya kidunia yanayopita yaani utajiri,kazi nzuri,kuoa,kuolewa,kufaulu n.k yote hayo yanapita. Hivyo Bwana atakubariki

 49. Waumini wanataka kusikia kama hatutaenda kwa babu alternative ni nini? Je tungewafundisha maandiko vyakutosha wangeenda? Kwa nini wagonjwa ni wengi? Watu hawaitaji vitisho wanahitaji fact.

 50. Mwingira Mwingira Mwingira
  Wewe ni nani hado umtangazie binadamu mwenzio KIFO? Nina mashaka na utumishi wako? Badala ya kusimama mbele ya madhabahu na kuropoka maneno makali hivyo ungeingia kwenye maombi umuombee babu ili aache kuwadanganya watu(kama ni kweli) na pia amuombe Mungu awafu gue macho ya kiroho watu ili waone ukweli wa mambo. Pamoja na hayo alipaswa awafundishe watu kweli ili iwaweke huru. Kuongea ongea tu bila kufanya lolote hakumsaidii yeye mwenyewew Mwingira, babu wala watu wanaoenda huko. Zaidi sana watu wanamwona Mwingira kama ana chuki na Babu tu.

  Mwingira kwakweli hapo amechemsha kabisa; anafanya mambo kama mtaifa asiyejua maandiko? Watu wanamshangaa kabisa! Mbona alivyosema muumini wa kanisa lake atakayeenda kwa babu atakufa watu wameenda na hawajafa na kwanini awatishe watu badala ya kuwafundisha kweli. Kwa sababu mtu ataogopa kwenda kwa babu kwa sababu askofu wake kasema akienda atakufa; kitu ambacho si sahihi. Watu wanatakiwa wasiende kwa sababu wanaijua kweli juu ya tiba hiyo.

  Mwingira funguka!

 51. …mimi nafikiri kama ni tu suala la MCHAWI KUTOKUISHI, basi, yule msichana aliyekamatwa kanisani hapo akiwa ameingia humo kwa lengo la kuloga alitakiwa AFE kwanza. Maana mtu hawezi kuloga kama yeye si mchawi. Huyu dada ndiye alitakiwa afe kwanza maana amekamatwa live [kutokana na habari hii] akitaka kuloga.

  Sijuwi ni kwa nini wamwachie huyo AISHI kisha wakamuombea na sala ya toba, halafu yule aliye mbali ndiye atakiwe KUFA?. Sasa atafanyaje ili atimize andiko lisemalo USIMWACHE MCHAWI AISHI? Jibu linabaki kwenye mabano: {……….}!

  Hivi mzee Mwasapila ndiye adui mkubwa zaidi wa roho za watu kwa sasa? Mbona naona kama vile mtumishi Mwingira amekuwa too offensive kwake?

  Mungu atabaki kuwa Mungu tu!

  Kuna habari ambazo msomaji hapa anaweza kuzikosoa au kuzithibitisha kuwa: “Mwingira alishawahi kutangaza kanisani kwake kuwa mtu atakayekwenda Loliondo kwa ajili ya kunywa dawa ATAKUFA. Lakini watu walikwenda na bado wapo hapo hapo kanisani wala hakuna aliyekufa kwa sababu ya kwenda Loliondo”

  Naona sasa kuna hatari ya “watumishi” kuanza kuagiza moto kutoka mbinguni kwa ajili ya kuangamiza wale wanaoonekana kuwa kinyume, kama walivyofanya Yakobo na Yohana katika Luka 9:54. Lakini Yesu aliwajibu:

  “…Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa”

 52. Kinachotakiwa kwa watumishi wa Mungu ni kuwafundisha watu kwamba ni kwa nini wanafikiri huduma ya babu haitokani Mungu,wakithibitishatisha kibiblia.
  Kuliko kuinuka na matamko ya jazba ambayo yanawafanya watu waone kama hawa watu lao moja isipokuwa wanahofia kuchukuliana kondoo,
  binafsi kilichonitisha katila jambo hili wepesi wa watu kukimbia mambo kabla ya kufanya tathimii kujua msingi wa jambo lenyewe,ama kweli siku zimesogea.

 53. Mchungaji Mwingira. Mi nafikiri hili swala la babu linahitaji mafundisho ya kina ili sisi wakristo wa kawaida ambao hatujaenda vyuo vya Biblia tuelewe vizuri. Tukielewa vizuri tutakua huru, hatutashawishika kwenda kwa babu. Lakini mkitumia mahubiri ya kulazimisha kwamba huduma ya babu si ya kweli na mnaiponda itawachanganya wengi kwa sababu kumbuka kuna watu WENGI wanashuhudia kwammba wamepona na hao ndo wanaowashawishi wengi kwenda kwa babu. Kummbuka watu wanapokusikiliza hapo kanisani wanalinganisha na uhalisia wa mambo yanayoripotiwa na walio wengi wanavutwa sana na miujiza ndio maana hapa mjini ikianzishwa huduma yeyote yenye miujiza wengi wataenda kama ilivyo kwa babu. Watu wanateswa sana na maradhi ndicho kinachowakimbiza loliondo na kwa vile hawakufundishwa VYEMA kuzipambanua roho wanaenda. Kwa uelewa wao mdogo wanaona huyu ni mchungaji na anaombea hiyo dawa na anaeleza alivyooneshwa na mungu.
  Hili jambo tusilichukulie kimzaha tu. linatufungua macho tuone jinsi ambavyo uelewa wa maandiko wa watu wengi ulivyo mdogo na hili ni kwa pande zote mbili; kwa wafundishaji na kwa wanaofundishwa. wafundishaji wa neno ( wachungaji, waalimu, mitume,) nafikiri walipaswa kufundisha kuhusu hili jambo kwa kujenga msingi kwenye maandiko YA KUTOSHA kuonesha ni kwa jinsi gani huduma ya babu haitoki kwa Mungu. Kwa maneno mengine nilitarjia kuona/kusikia vichwa vya masomo kwenye vyombo vya habari kutoka kwa watumishi wa Mungu vinavyoeleza kwa kina kuhusu uponyaji wa kiMUNGU. kwa bahati mbaya nimekua nikisikia na kuona watumishi wakitoa matamko makali ya kumponda babu. kwa mtu wa kawaida anaona hawa watumishi wanamwonea babu wivu kwa sababu anapata watu wengi hawafundishi mtu wa kawaida aelewe ni kwa nini wanaipinga. nimemsikia mtumishi mmoja jumapili iliyopita akihubiri mahubiri yanayoashiria kuwapiga marufuku waumini wake kwenda kwa babu.Mahubiri ya vitisho hayasaidii sana. FUNDISHA, mtu akielewa utakuwa umemsaidia kupevuka upeo wake ataweza kupambanua roho yeyote itakayotokea.

 54. hapa Mtumishi wa mungu umekwenda mbali,ni Mungu pekee ndiye ajuaye uhai wa mtu kwamba amebakiza muda gani kabla hajatoweka,tunajua dhahiri kwamba kazi ya Babu si kazi ya Mungu Aliye Hai,na ni jukumu la Watumishi wa Mungu Aliye Hai kuwajuza watu wa Mungu juu ya mafundisho potofu ili kuwasaidia kiroho(hasa wale walio wachanga katika imani)

  Pia ningependa kumpongeza Mtumishi Mwingira pamoja na watumishi wengine waliothubutu kunena juu ya mafundisho haya ya KIKOMBE,kwamba si mafundisho sahihi ya ki-Biblia na wala si njia sahihi ya uponyaji wa ki-Mungu.

  Hivi ndivyo inavyopasa kwa Mtumishi yeyote aliyetumwa na Mungu,anapaswa kuinena KWELI YOTE.na kuitetea injili,kunyamaza kimya ilihali INJILI inageuzwa huu ni usaliti kwa Mungu na mtumishi wa namna hii hafai katika ulimwengu huu wa sasa uliojaa kila namna ya upotofu.

  Lakini katika hili naona Mwingira ametumia lugha kali,kwa sababu hata Yesu anampenda Babu na anapenda Babu huyu aache uongo wake na kumgeukia Mungu wa Kweli na si kuangamia kama maandiko yanavyonena
  Kanisa linahitaji kuomba sana kwa ajili ya jambo hili ili watu wasiangamie kwa kukosa maarifa.Watanzania tumtafute Mungu wa kweli,sio kuanza kuabudu sanamu na kuzitegemea hizo(kikombe)
  MUNGU NA ATUSAIDIE

 55. Kwako Mtume Mwingira,

  Ni siku za nani aliye hai ambazo hazihesabiki? Mbona hata wewe siku zako zinahesabika? Au umesahau Maandiko? “WAMRUDISHA MTU MAVUMBINI USEMAPO,RUDINI, ENYI WANADAMU”(Psalm 90:3) Na Mtunga Zaburi huyo huyo anaendelea kusema “BASI, UTUJULISHE KUZIHESABU SIKU ZETU, TUJIPATIE MOYO WA HEKIMA” Alisema hivyo kwa sababu zinahesabika!ni Chache mno!Ni Mvuke upitao na Kesho haupo!

  Huduma yako kama Imetoka kwa Aliye Hai haitavunjwa na KIKOMBE! Ni yeye aliyesema hata alipokuwa Ametundikwa Msalabani; “BABA UWASAMEHE KWA MAANA HAWAJUI WALITENDALO” Huu ndio ujumbe kwa maadui zetu!

  UBARIKIWE!

 56. Mungu wa mbinguni ni Mungu wa wote wenye mwili hana ubaguzi kwa yeyote na ana weza kumtumia kama apendavyo yeye mwenyewe. Watumishi wa Mungu na omba kujua hivi tu mwamini nani kati Mwingira na Mwaisapile kwani kila mmoja anadai anatumiwa na Mungu. kama na kwenda kinyume basi naomba mniombee ili Mungun anipe rehema zake kwani na mimi nina mpango wa kwenda mbinguni kumwona Bwana wetu Yesu kristo aliye juu

 57. Nadhani Mtume amesahau kuwa tuko katika agano la Neema na si la kale(jino kwa jino).
  kipindi hiki ni cha neema na si cha kukurupuka na kutoa hukumu, kwa kuquote maandiko ya agano la mwilini.
  nb:tutofautishe unabii na hisia za mtumishi.

 58. Mimi sidhan kama kristo alikuja ili kuua bali kumfanya kila mwenye dhambi kufikia toba ya kweli kwa njia kuamini injili.babu mwenyewe kazeeka hiv akifa kesho Mwingira atajisifia? ? Viongoz wa dini acheni kuropoka kwa kuongozwa na hisia na si roho.Mtu anayeongozwa na roho hawez kuropoka hovyo bali hutumia hekima na maombi ktk mambo km haya.JE kafunuliwa na roho yupi kwamba babu ni mshirikina ? Huyo roho mbona hakuwafunulia watumishì wengine?

 59. Kwa kweli Mungu aingilie kati kwenye hili kwani Mwingira wewe ni mtumishi wa Mungu lakini isije kuwa unachosema sijui kwa wengine kwani unavyosema Mungu haongei na miti,maana huyo Babu hakusema mti umemwambia hivi.
  Mungua anisaidie sitaki kuhukumu kabisa hapa,ila Mwingira kama Mtumishi wa Mungu kwako ni jazba imetawala sana toka habari za Semunge Loliondo zimekuwapublished

 60. Wapendwa Bwana Yesu Asifiwe. Mimi Nadhani watumishi wa Mungu inabidi turejee kwenye maandiko imeandikwa Vita vyetu sio juu ya Damu na nyama bali ni juu ya ufalme wa giza (Waefeso 6:12). Sasa kuombea mtu afe kimwili je na mapepo yatakuwa ndio yameshindwa(2Wakorintho 10:3-6)

  Mbarikiwe

 61. Hakika ipo kazi kwenye mwili wa Kristo(Kanisa).

  Hivi huyu mzee asipokufa itakuwaje kwa Mwingira? Na je akifa baada ya miaka 10 ijayo itakuwa bado ni tamko au maombi ya Mwingira yanafanya kazi tu? Au akifa sasa hivi, kwa sababu ya umri wake, kumbuka ana miaka 76, kwa hiyo yupo kwenye ile zone iliyoandikwa kwenye Zaburi kwamba miaka yetu ni 70 na mtu akiwa na nguvu miaka 80, je akifa sasa hivi kwa uzee wake tu Mwingira atatuhakikishiaje kuwa amekufa kwa neno lake?

  Nabii Eliya alipofunga mvua isinyeshe aliweka na muda (miaka 3 na Nusu-Yakobo 5:17), ninamuomba Mwingira aweke pia muda wa kufa kwa huyu babu ili watu wawe na uhakika pasi na shaka kwamba amekufa kwa maombi ya Mwingira.

  Mawazo yangu ni kwamba nadhani imefika wakati watu Mungu wasipende sana hili jambo la mtu akikosa au kutenda dhambi afe, badala yake ni kumuombea ili aifikilie toba asije akafa katika dhambi akapotea milele. Hiyo ndio kazi au huduma walioitiwa akina Mwingira, kuponya roho za watenda dhambi sio kuziombea zife zipotee milele (Yakobo 5:20).

  Mungu awabariki.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s