Rose Muhando Autambulisha UTAMU WA YESU

 

Muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania, ametambulisha nyimbo zake mpya ambazo zitapatikana kwenye album yake ya nne. Nyimbo hizo ni UTAMU YA YESU na RAHA YA AJABU ambazo zinapendwa na kufanya vyema kwenye vituo vya redio za injili Tanzania. Hakika kwa Yesu ni Kutamu kama anavyosema Rose, “Nimeonja utamu wa Yesu, Ukitaka gari nzuri, majumba mazuri onja utamu wa Yesu”. Baadhi ya maneno yaliyomo kwa wimbo mpya wa Mtumishi wa Mungu Rose Muhando, tunasubiri video ya album yake mpya!

Advertisements

49 thoughts on “Rose Muhando Autambulisha UTAMU WA YESU

 1. MNAVYOSEMA SIVYO MTU YEYOTE AKIFANIKIWA WANADAMU HUFIKIRIA MAMBO MABAYA NAFIKIRI DADA HUYU ASINGE ENDELEA WANADAMU WANGE TOWA MANENO , HAWEZI KUENDELEA LAKINI KAFANIKIWA MUNGU KAMUINUWA SASA NIMAMBO MAKUBWA JE? KAMA WEWE KWELI UNAWEZA EBU JARIBU KWANZA TUONE. KILA KITU HUDUMA KIIMBA KUHUBIRI NIKIPAJIKUTOKA KWA MUNGU MNAPWASWA KUWA WASHAURI KAMA MMEONA KITU KISICHOENDEKA SAWA KWASABABU SIYO MUNGU NIMWANADAMU NIVIZURI KUSHAURI SIY KUSHUTUMU. MUNGU AWABARIKI.

 2. Mtu anapokuwa ndani ya Yesu ya kale yote yanapita, hata kama alikuwa mwizi, jambazi, mwasherati nakadhalika. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. na kila mtoto Mungu ana makusudi naye hata kabla hajazaliwa. Usihukumu nawe utahukumiwa

 3. Yesu kasema mnahubiri maji hali mwakunywa mvinyo,tena twaambiwa tuijaribu kila roho kwani sio zote zatoka kwa Mungu,watoto hupatikana kwa ndoa na wanao patikana nje ya ndoa tendo hilo laitwa uasherati ambayo ni moja ya kinyume cha zile amri kumi za Mungu!

 4. michael kwani watoto wanapatikana wapi? baba yao unamuulizia wa nini? angalia kama umesimama vyema usianguke.

 5. inasemekana huyu dada ana watoto watatu,je yeye kawapata vipi na baba yao ni nani?

 6. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI WA MUNGU. KWA KWELI WIMBO WA ROZI MUHANDO UMENIVUSHA HATUA FULANI MUNGU AZIDI KUMBARIKI.

 7. Kusema Kweli kanda yote ya Dada Rose Bint Mhando, nimeisikiliza na kuitazama mara tatu kwa kuirudia tena na tena.

  Hata hivi ninavyoandika maoni yangu niko nayo tena nimenunua santuri halisi (Original CD) kama anavyosisitiza dada Rose mwenyewe.

  Kwa upande wa ujumbe Da Rose anajitahidi sana. Ujumbe wake unaeleweka vizuri kimantiki na kimuundo na kiushairi. Anajua kupangilia vina na mizani.

  Kwa upande wa burudani inayokamata hadhira na kuifanya isichoke kumtazama au kumsikiliza, napo pia Rose anaelewa vyema kucheza na akili za watu (Audiences psychology). Rose anaelewa wateja na wapenzi wake wanachohitaji ili waendelee kuwepo uwanjani. Mitindo anayoitumia (Dancing styles) zinaendana na nyakati za sasa. Mitindo yote ya kuruka mbele kwenda nyuma, upande kwenda kushoto kulia juu china, Rose ameweza kutawala jukwaa. Msanii wa kweli wa Injili (Gospel Music Artist) lazima ajue kutawala jukwaa kama ilivyo kwa Mwinjilisti yeyote wa kawaida (Gospel Evangelist) lazima ajue kutawala kipaza sauti na jukwaa (Microphone and Platform) vinginevyo hatapata wasikilizaji uwanjani. Hii ndiyo siri ya mafanikio ya Rose bint Mhando.

  Kwa upande wa ubora wa Video (Picture quality and production) Da Rose amejitahidi kuwapata watengenezaji wazuri wa Video. Ubora wa picha ni muhimu sana katika kazi yoyote ya sanaa.

  Kwa upande wa waimbaji wenza (Singers Showers or partners) wengine huwaita wacheza shoo, amejitahidi kuwapata vijana wanaojituma kwa bidii. Inaoenekana labda anawalipa vizuri au anawatunza vizuri (hii ni siri yake). Lakini mimi ninavyowasoma naona kwamba wanajituma na wanaipenda kazi hii ya kumsaidia Rose kuimba kwenye majukwaa na video zake.

  Kwa upande wa MAVAZI:

  Rose Mhando amejitahidi kuwa “neutral” katika kuchagua mavazi ya kuvaa akiwa jukwaani au akiwa anachukuliwa picha zake kulingana na mahali pa kuchukulia picha (Video shooting).

  Swala la mavazi limeendelea kuleta minong’ono mingi kwa watu ingawa wananung’unika huku wakiendelea kununua kaseti zake kwamba Rose anavaa nguo fupi ikilinganishwa na huduma yake. Mimi baada ya kutazama CD yake nimeona kwamba yeye mwenyewe anavaa nguo zote zinazopita kwenye magoti.

  Hakuna nguo hata moja niliyoona amevaa ikiwa haivuki kwenye magoti. Wale wacheza “Show” wamo waliovaa nguo au skirt zinazoishia kwenye magoti. Sasa kutokana na aina ya “dances” anazozifanya Rose na timu yake ndipo hapo inapofika sasa mpaka “skin tight dress” za wacheza show zinaonekana. Mapaja yote huwa yanaonekana wawapo katika kuimba na kucheza. Hata Rose mwenyewe kuna Suti moja ya rangi ya Pink na nyingine ya rangi ya kama bluu hivi zote hizo anaporuka au kunyanyua mguu huwa zinamfanya mtazamaji amwone mapaja yake au nguo aliyovaa kwa ndani. Kwa mfano ukitazama wimbo wake usemao, “IMBENI NA KUSIFU” utaona kwamba wale wasaidizi wake kusemaa ukweli zile sketi zao zinawaacha wakiwa wazi kwenye sehemu za mapajani. Kuna wakati wanaimba wakiwa wamesimama kwenye jiwe kubwa na mpiga picha yupo chini yao. Hapa naona haikuwa sawa.

  Ukimtazama yule dada wa pili kutoka kushoto kati ya wale wacheza show wa kike utaona aibu kuendelea kumtazama kwani yeye kusema ukweli mapaja yote yanabaki wazi kabisa awapo katika kuimba na kuruka juuu kwa style ya “Leggae” iliyotumika.

  Tatizo lililopo ni kwamba huenda Rose na timu yake wawapo katika kuimba huwa wako rohoni sana kiasi kwamba maswala ya unaonekanaje mbele ya hadhira siyo hoja. Waimbaji wa Rose labda wanajaa Roho Mtakatifu kiasi kwamba Sketi wanazovaa wawapo kwenye jukwaa siyo “issue” kwao. Kwa upande wa wacheza show wa kiume hakuna tatizo mimi ninaloona katika uvaaji. Wamejitahidi wamevaa vizuri na kwa unadhifu (smartness).

  Ukiatazama mavazi ya Rose na hawa wadogo zake wa kike utagundua kwamba upande wa mashati au blauzi zao kwa kila wimbo walioimba hawakuvaa blauzi zinazoacha vifua vyao wazi. Hapa wapendwa wengi hapawakwazi kabisa. Kinachowakwaza wengi nilioongea nao ni zile sketi zilizoshonwa (sijui kwa ushauri wa mlezi wao) kwa mtindo wa “skirt solo”. Zimeshonwa kwa mtindo ambao unamruhusu mwimbaji kurukaruka juu bila kuzuiliwa na sketi hiyo. Labda ndiyo maana Rose akaona ashone sketi za wacheza show wake zenye muundo huo.

  Ukitazama wimbo wake pia usemao, “RAHA TUPU” utaona kuwa sketi aliyovaa Rose hasa ile ya suti nyeupe na wale wadogo zake wanaomsaidia utaona kwamba hawakuvaa sketi zinazowasitiri mapaja yao.

  Inawezekana kwamba Rose Mhando hajasoma somo la mavazi na Saikolojia yake mbele ya watu. Ieleweke kwamba hata kama unamsifu Mungu hasa uwapo mbele ya Hadhira yako kama hautajitahidi kuzuia sehemu nyeti za maungo yako (Sensitive body parts) zisionekane kabisa kuna mambo mawili yatajitokeza wewe bila kujua:

  La kwanza utashangiliwa sana na hadhira yako kwa vigeregere na vifijo. Wewe kwa kutojua utadhania kwamba watu wako wanafurahia nyimbo zako au kwamba wamebarikiwa sana, kumbe wanashangilia kuona nguo zako za ndani au sehemu ya mapaja yako. Kumbuka unapokuwa uwanjani (acha kanisani) wanakuwepo watu wenye sura mbili. Sura ya kutafuta kubarikiwa kutokana na nyimbo zako na wenye sura ya kutaka kuburudisha nafsi zao kwa kukutazama unavyoruka na wanatamani uruke juu sana hadi waone nguo yako hasa ya ndani (chupi ikiwezekana). Haya ndiyo makundi yaliyopo katika viwanja vya Injili. Kumbuka kwamba dunia nzima ya mziki kwa sasa inatukuza watu wanaoimba wakiwa wamevaa chupi na sidiria tu. Dunia hiyo hiyo ndiyo inayotaka hata waimbaji wa Nyimbo za Injili (Gospel Music Artists) waige kila kitu kilichopo duniani hata kama ujumbe utabakia ule ule wa Biblia ili mradi tu wewe unaimba kuwaburudisha kimwili kuliko kiimani na kiroho.

  Kwa swala la Mvuto mbele ya wakristo, bado Rose anao mvuto sana hata kama nayo mapungufu katika maeneo kadhaa likiwamo swala la mavazi na ndoa yake. Kwa mfano, Wiki iliyopita (tarehe 4-11 March 2012) jana Rose Mhando alikuwa viwanja vya FURAHISHA Jijini Mwanza. Kwa mujibu wa taarifa za kutoka eneo la tukio inasemekana kwamba umati uliojitokeza kuhudhuria mkutano ule wa Injili haujawahi kutokea Mwanza. Msururu wa magari uliokuwepo haujawahi kuwapo hasa siku ya Mwisho ya Mkutano kwani msururu wa magari ulitoka maeneo ya kanisa la AIC – Makongoro hadi Benki ya Posta au Kituo cha Igombe (kwa wale wanaojua Mwanza wanaelewa). Inasemekana pia kwamba Rose Mhando akimaliza kuimba tu umati uliokuwepo ulikuwa unatawanyika bila hata kusubiri mahubiri ya Muhubiri wa siku hiyo. Mkutano wote aliyevuma sana ni Rose Mhando kuliko Mhubiri aliyekuwa amepangwa hata waandaaji wa Mkutano hawakujulikana ni akina nani bali ilijulikana tu ni Rose Mhando.

  Pamoja na malalamiko mengi yanayosemwa juu ya Rose, nahitimisha kwa kusema kwamba Rose Mhando na timu ameweza kuendelea mbele pamoja na yote yanayosemwa juu yake. Inawezekana kabisa kwamba (hata kama yeye siyo mtakatifu kama watu wanavyotamani awe) ameweza kuwafikia watu mamilioni sana kwa Neno la Mungu kuliko hata sisi tunaomchambua na au kumhukumu kwamba hana lolote mbele za Mungu. Ni vyema kila mmoja kuangalia ni jinsi gani kazi yake ilivyo mbele za Mungu badala ya kuzama kulaumu Rose Mhando.

  Ushauri wangu kwa Rosse na wadogo zake ni kwamba kama wanaweza warekebishe aina za sketi zao zisiwe nyepesi wala zisiwe za SOLO kwani zinawaacha mapaja wazi na kuleta lawama zisizokuwa na sababu katika umma wa wakristo. Kama ikiwezekana wacheza show wako wa kike wavae “track suits” au sketi za kawaida ambazo haziruki na kuacha mapaja nje.

  Mwisho kabisa, Dada Rose nimesikia kwamba baadhi ya wachungaji wa makanisa ya DODOMA wanakutafuta bila kufanikiwa. Wiki iliyoishia tarehe 11 Machi 2012 nilikuwa Dodoma na kufanikiwa kuulizia habari zako hapo mjini Dom. Baadhi ya watumishi wa Mungu nilioongea nao wanasema kwamba wewe hupatikani (You are unreachable all the time) hata kama mtu akikutafuta vipi eti huwa hupatikani. Nakushauri ujitahidi kuwa unapatikana ili watu wenye mawazo mazuri wakupe siyo lazima uyakubali yote wanayokwambia kama hayajakuingia au hayaendani na wito na maono yako.

  Nakutakia kila la kheri.

 8. Hakika kwa nguvu,akili na uwezo wakibinadam dada Rose usingefanikiwa ila kwakua Roho Mtakatifu yupo ndani yako hakika umebarikiwa sana dada.Mungu aendelee kukutia nguvu milele na milele kwani nyimbo zako zimekua faraja kwangu.

 9. Nimeona kwamba chuki ndio inayotawala kwenye kutoa ushauri na siyo upendo. ushauri wangu tafadhali tutoe ushauri wa kweli na tuongee yaliyo kweli mfano kama viingilio na kutoza fedha kubwa. MBARIKIWE WOTE KATIKA BWANA

 10. Jamani msimlalamikie Rose Muhando si alibadili dini tu kutoka ktk uislamu na akawa muanglikana ila hajaokoka,mpaka atakapofika mahali pakutubu dhambi nakudhamiria kabisa kwa dhati,ila hastahili kulaumiwa.

 11. Hata mimi nimeonja na bado nazidi kuonja utamu wa Yesu. kweli kwa Yesu kuna utamu sana.

 12. na kuhusu nyimbo za kimwili na kiroho ni zipi kumbuka kwamba tumeambiwa ikiwa tunamkiri Masihi basi ni lazima tuzaliwe kimwili na kiroho

  asante.

  Aiyalon.

 13. sidhani kwamba wachangiaji au mimi tumesema waimbaji wanaringa,inawezekana ni mtazamo wako hata hivyo kila mtu ana uhuru wa kutoa mtazamo wa mawazo yake. ninaposema kwamba waimbaji wa injili wanacheza sana haimaanishi wanaringa lakini watu wanaomtangaza Mungu lazima wawe tofauti maana hata kuzungumza kwao wanatofauti na ndio maana Petro alipomkana Yesu aliposema hamjui akaambiwa si kweli maana hata usemi wako wafanana naye ni kwa nini? inawezekana mimi sina sauti ya kuimba kama Rose na wengine,lakini kutoa mtazamo wangu kwa kile nikionacho si kosa nadhani.kwa nini nasifia uimbaji wake? na kwa nini nikoseo uchezaji na mavazi? ina maana ni mambo ambayo hayapendezi watu na sio mimi haya yamekuwa yakiongelewa,hivi kuimba makwapa wazi ni sawa kweli? sidhani kama hata kwa mila na desturi zetu mtoto wa kike anakuwa huru kunyanyua makwapa yake wazi kwa wazee wake.na hili ndio linaturejesha nyuma wakristo wengi kwa kujiona kwamba tuko kamili kwa kila jambo hatutaki kukosolewa inawezekana wewe ni mshabiki wa hawa waimbaji lakini wakati huohuo hutaki kusema kasoro unazoziona kwa maana unayoijua wewe.lakini Mungu pia anatutaka turekebishane kwa maana ya kukumbushana na ndio maana Mungu anasema ni vyema kukusanyana kwa maana hapo mtapata kukumbushana,kwani kwa nini watu wanaenda kanisani? si kila mmoja anayo Biblia kwake na anajua kusoma? lakini bado haitoshi ndio maana watu wanakusanyika.unaposema kama tyunaona waimbaji hawatendi sawa basi tufanye yanayopasa nadhani huko sahihi maana kila mtu amepewa kipaji chake na mwenyezi mungu lakini kupewa kipaji hicho ni dhamana kubwa na tunapaswa kutumia vyema vipaji vyetu maana kuna siku tutaulizwa! kuna watu wanaokosoa watangazaji kwenye Radio na Luninga wanaotangaza je na wao waambiwe wakatangaze kama wanona hawafanyi sawa? jibu ni kwamba watangazaji hao wanapaswa kusikiliza kile kinachosema na kukipima na sio kurishika kwamba wanajua kila kitu.kuhusu mavazi,ni kweli akina mama wengi wanavaa mavazi ambayo hayasitahiki lakini naona umesahau kwamba hapa wanaozungumzwa si akina mama kwa ujumla bali ni waimbaji.

  kwa hiyo siwezi kuzungumzia ujumla wa kina mama wakati mada yangu ni nyingine. KIza NA NURU HAVITANGAMANI KAMWE!

  Aiyalon.

 14. Jamani wapendwa,
  Penye kutoa hongera tutoe hongera na kwenye kurekebishana turekebishane.

  Awali ya yote mimi ni miongoni mwa wale walio wachaguzi sana wa aina za nyimbo za kusikiliza na kununua but dada Rose nampa hongera kwa kazi zake za uinjilishaji kuitia nyimbo, najua kupitia yeye wengi wamemjua Yesu na wengi wamejengwa na wengine wamekuwa watumishi katika kumuimbia Mungu n.k,

  Nyimbo kuwa za kiroho au kimwili; Ninashukuru kwa wapendwa kulisemea hili but mimi nina mtazamo tofauti. Je ni nyimbo zipi ni za kiroho na zipi ni za kimwili? Ukweli ni kwamba zile nyimbo zote ni za kiroho hata circular music. Ila tunapozungumzia za Mungu katika Kristo ndio zinazaliwa kwa mwanadamu wa asili akishirikiana na Roho wa Mungu kuziandaa (kutunga n.k.).

  Wale tunaoona kama hawa waimbaji wanaringa, hawastahili au wangeimba/wangecheza hivi na hivi maana yake ni “tunaweza kufanya kuliko wao katika huduma hiyo”, hivyo kwa ushauri wangu “TUFANYE BASI KILICHO BORA NA CHA KIMUNGU KULIKO WAO”!
  Nashauri tukumbuke kuna kuitwa, kuchaguliwa kutengwa na…

  SUALA LA MAVAZI; Hili si la Rose peke yake, wadada na wamama kwa sasa “wana ugonjwa” unaoonekana kama vile ni sugu. Mtu yeyote hapa aseme kama hawaoni kuanzia majumbani kwetu, makanisani, maofisini, biasharani na hata kwenye maeneo yote ya jumuia. Kwa wale wanaozungumzia mavazi natamani wangewasema au kuwaonya na kuwafundisha wote na si Rose peke yake.

  Mbarikiwe!

 15. WASANII WA INJILI NA KUCHEZA (KUDANSI}

  hapo awali wakati nakua ki akili nilikuwa nikihudhuria sana kanisani mpaka hivi leo.lakini kuna mambo ambayo yananitatiza hasa kwa mwenendo wa uimbaji na uchezaji wa makanisa unavyoendelea hususani kwa waimbaji wa sasa maana nasikia hata waimbaji wa injili wa sasa wanaitwa wanamusiki wa kizazi kipya cha injili.
  1. uchezaji wakati wa kuimba unazidi mno hakuna tofauti na wasanii wa mataifa,nikisema mataifa nina maana wale ambao wanaimba nyimbo ambazo hazimtukuzi mungu,nadhani kama ni kucheza basi kusipitilize unajuwa kuna wakati mpaka hata ukiangalia video ya mwimbaji wa injili unakosa umakini wa kuzingatia massaje.. ujumbe bali unabaki kuangalia ile staili anayocheza! Mungu anasisitiza wanadamu kuwa na kiasi,ni kweli hata Mbinguni biblia inasema tutaimba na kuruka ruka ! lakini mambo ya Mungu kawaida ni tofauti sana na ya mwanadamu japo alituumba kwa mfano wake.nadhani waimbaji wanasahau sana katika uchezaji wengi wao ukiwauliza wanasema wanatumia kucheza kwani inakuwa rahisi kumvuta mtu ambaye hajaokoka! aone ni sawa yuko kwenye miziki ile aloizoea ya kidunia lakini kamwe Yesu hakuwaokoa watu huku akiwadanganya na mifano ambayo haiwasaidii ,mifano mingi aliyowapa ilikuwa hai.na kingine waimbaji wa injili kwenye mavazi pia kwakweli haifurahishi nyumba ya Mungu si masihara wala Mungu hataniwi,sio kwamba eti ukiwa umevaa mavazi ya kimasikini ndio unakuwa na credit kubwa ya kuwa karibu na Mungu hapana! lakini mavazi ya mtu wa Mungu lazima yamtangaza bwana pia.

  2. sielewi kwa nini waimbaji wa nyimbo za injili wanaweka viingilio vikubwa pindi wanapoitwa kutoa huduma! huwezi kumchukua mtu kama Rose Muhando kwa shilingi laki tano kumleta Zanzibar ninapoishi.haiwezekani sijui kwa nini hawajali na wameweka masilahi mbele.

  kamanimekosema nisamehewe saba mara sabini

  Aiyalon
  Asante,

 16. mimi naomba niseme kwamba hata mavazi nayo yanatosha kumtambulisha mtu,kama ni mtu anayemtukuza Mungu kwa ajili aonekane na wanadamu wenziwe ataonekana!mavazi Mungu ameyaweka kwa maana kubwa sana nadhani watu waliomkiri Bwana kama Mwokozi wa maisha yao ni lazima wavae mavazi yanayomtangaza yeye wala wasivae mavazi ambayo yanaleta utata. Mimi nawaona waimbaji wengi wa injili wakivaa mavazi ambayo kwa kweli hayastahili pamoja na kuimba kwa sauti nzuri.lakini siingilii sana Mungu mwenyewe atachagua kondoo na mbuzi.mimi nafikiri kuna kila sababu kwa watu wa Mungu kuangalia kivazi.

  asante Aiyalon

 17. Wapendwa,

  Pamoja na kuzipenda sana nyimbo za dada Rose, kinachonikwaza sana ni mavazi yake. Mavazi yake hayaendani na waraka wa Paulo kwa Timotheo wala Ule waraka wa Petro Mtume kwa watu wote kuhusu mavazi. Kanuni kuu ya vazi lolote kwa Mkristo bila kujali madoido yake yaliyowekwa na mafundi wa kushona ni KUSTIRI MWILI AU MAUNGO YETU.

  Kama Rose anaimba amevaa mavazi yasiyofunika makwapa na miguuni au magoti yake kwa jinsi hali ilivyo kwa watanzania wengi, huu ni utovu wa nidhamu katika uvaaji wa Kikristo.

  Nyimbo za Rose utazipenda ukiwa unazisikiliza kutoka kwenye Radio tu siyo kwenye Video au TV. Mavazi hasa ndilo tatizo.

  Wakati nikiwapongeza wale madada wajiitao J-SISTERS nilisema kwamba bora kuvaa SURUALI wakati wa kuimba kuliko kuvaa Sketi fupi ambayo huacha magoti nje au nguo za ndani kuonekana wakati wa kurukaruka ukiwa unaimba kwa style zako za kufa PEPO.

  Somo la mavazi bado halijaeleweka kwa waimbaji wengi Tanzania. Rose Mhando mimi nakushauri ujaribu kuvaa mavazi yenye mbwembwe kibao lakini yasiwe yale yanayoacha sehemu yoyote ya mwili kuonekana ukiacha nyayo za miguu tu. Nguo za kuonesha Kifua, Sehemu ya Matiti, Makwapa wazi, magoti wazi nakushauri uachane nayo utakapokuwa unaandaa Albam Ya Video “UTAMU WA YESU”. Hata wale wacheza Show wako wa Kike hakikisha unawanunulia sketi ndefu ambazo haziwaruki juu ya magoti. Kama hili ni gumu bora wavae Track Suits kama wavaavyo wale madada wa J-SISTERS.

  Kumbuka nyimbo zako siyo tu kwamba zinalitangaza taifa la Tanzania na utamaduni wake, bali pia zinalitangaza NENO la Mungu aliye hai mwenye kushika maadili ya Neno lake alilolisema.

  Rose nyimbo zako ni nzuri kwa maana ya kufuata taratibu za mashairi ya Kisasa hasa katika tasinia ya nyimbo za Injili. Aidha zinaendana na wakati. Zinapendwa sana kwa sababu ya Mirindimo yake ya haraka na hupendwa zaidi na vijana. Hii inatokana na utafiti mdogo nilioufanya katika kuzungumza na watu wasiokuwa vijana kuhusu nyimbo zako. Wengi wa waliohojiwa wanaona kwamba huna utaratibu mzuri hasa katika kuvaa nguo zenye staha na stara. Jitahidi kurekebisha kasoro hiyo na Mungu atakujalia kwenda mbali zaidi siyo kwa baraka za vitu vya mwili bali UZIMA WA MILELE.

  Nakuomba ujitahidi kusoma makala zangu nilizowahi kuandika katika blog hii kuhusu Mavazi ya Mkristo. Ukitaka kupata Mada zangu zote fungua Google Machine, kisha andika: Obed Venerando Milinga; ukishaandika hivyo ukaamuru Google itakuletea mada zangu zote ikiwemo ya kuhusu Mavazi. Hata kama kanisa unalosali halichukulii uzito mkubwa Jinsi Uvaavyo, kwa kuwa unaimba nyimbo zinazopendwa na wengi nje ya madhehebu yako UMEKUWA MTU WA KITAIFA NA KIMATAIFA. Hivyo unapaswa kuwa mtu wa Kimataifa bila kuacha Utaifa wako.

  Nakutakia Uimbaji wenye Tija siyo wenye Shida.

  By Obed Venerando Milinga- Kigoma.

 18. Thank you very much for your new song /album Utamu wa Yesu. It’s indeed very inspiring cabable of building some one spiritually.Please I wish to request you to send me Utamu wa Hesitate ringtone to my phone No. 0718069140 so that I may continue listening to as I wait for your new album. Otherwise thank you in advance and be blessed abundantly.
  Yours in Christ,
  ERNEST W. SIMIYU.
  [ONE OF YOUR KENYAN FANS]

 19. Kaka Orbi ahsante sana kwa neno nimegusika sana na mtazamo wako wa Biblia. Naomba kujuana nawe zaidi ikiwa uko Facebook tafadhali nitafute kwa: (Paul Joseph Badia ,email badiapaul@yahoo.com)

 20. Hey Rose, Bwana asifiwe.mimi naingoja sana hiyo video ya utamu wa YESU.

 21. hakika huyu ni mwimbaji wa kimataifa na wimbo huu unaburudisha pia unaelimisha

 22. MUNGU akubariki mtumishi mwa mungu kazi yako ni njema nyimbo zako karibu zote zinanibarik sana.ila napenda kukushauri kuwa mavazi uliyovaa yanaharibu ushuhuda wa neno la mungu ukizingatia kuwa sisi tuliookoka ni barua inayosomwa.hivyo nakushauri uvae mavazi ya heshima yanayompa MUNGU UTUKUFU.

 23. Amani, Heshima na Upendo.
  Nimekuwa mbali kwa sababu za kimaisha tu. Lakini nikingali nanyi kila nipatapo nafasi kama sasa.
  Leo ndio nimesikiliza wimbo huu kwa mara ya kwanza. Na ninawaza kama sote tunasikiliza wimbo mmoja. Nikisoma maoni ya baadhi ya watu, siamini kama ni wimbo mmoja tuusikilizao.
  Naamini wimbo huu ni mzuri na baraka kwako Rose

 24. Wapendwa Paul John na Haggai Kinyau,

  Nashukuru kwa mjadala wenu hasa kuhusu baraka na mafanikio ya mwilini, kwa kifupi wengi wanatatizika na hilo.Katika majadiliano yenu Mmetoa mafundisho ambayo yatasaidia wengi, baraka na mafanikio ya Rohoni ndio ya msingi na Bwana kama atakavyo au apendevyo yeye mwenyewe atatubariki kwa wingi wa Baraka za mwilini kwa Makusudi yake,ili kila atupacho katika mwili katika maisha haya ya kitambo kifupi kiweze kumletea utukufu Yeye.

  Naamini mmesaidia wengi wanaotatizika na somo hili.

  MBARIKIWE.

 25. Ndg Haggai,

  Ninashukuru kwa maelezo yako ambayo nami nakubaliana nayo. Cha masingi ambacho naona umekubaliana nami ni kuwa SI LAZIMA kila mcha Mungu awe na mafanikio ya kimwili. Bali kilicho muhimu ni mafanikio ya kirohokwa kuwa mtu hataenda mbinguni kwa sababu ya umasikini wake au utajiri wake kimwili bali uhusiano wake kiroho na Mungu.

  Na ninaamini pia huo ushuhuda uliousikia kutoka kwa Rose Muhando,japo mimi sikuusikia, ulikuwa unasisitiza juu ya badiliko la kiroho. Amani ya kweli, furaha moyoni, kuwa na uwezo wa kusamehe na kuachilia nk. Kama ni hivyo basi ni vema. Lakini kama ushuhuda huo ulijengwa juu ya msingi wa magari, nyumba na pesa, hiyo si sawa.

  Maelezo yako yamejitosheleza. Nisije nikavuruga ujumbe huo mzuri.

  Asante sana na Mungu akubariki.

 26. Ndugu John Paul.

  Ahsante kwa yote uliyoandika, nimekusoma na kukuelewa vizuri sana. Ni kweli na nadhani ni vizuri kutumia neno hilo la SI LAZIMA kwa maana kuna sehemu nyingi ndani ya biblia zinazoonyesha wacha Mungu waliokuwa na mafanikio ya kimwili pia na vile vile kuna sehemu zingine nyingi pia zinazoonyesha wacha Mungu wengine waliokuwa hawana mafanikio ya kimwili, LAKINI wote hawa walikuwa na mafanikio sana ya kiroho kwa kumcha Mungu!

  Mfano mzuri ni wa yule Lazaro maskini kwenye Luka 16:19-31; hapa pamoja na Lazaro kuwa maskini sana na kuwa na uhitaji mkubwa wa mahitaji ya kimwili LAKINI alikuwa na mafanikio makubwa sana ya kiroho ambayo tumeonyeshwa au tumeyaona baada ya yeye kufa. Kwa maana hiyo basi ndio sababu Biblia inasisitiza kwanza kumcha Mungu kabla ya kitu kingine chochote. Naomba wapendwa wengi wasichukulie kuwa umaskini wa Lazaro ndio ulikuwa kigezo cha yeye kukaa kifuani mwa Ibrahimu, mwenye mtazamo huo, namuomba aisome biblia yake kwa upya. Hilo ni kweli pia kwa upande wa tajiri kwamba hakuwa kwenye mateso hayo au sehemu ile aliyokuwa kwa sababu ya utajiri wake, alikuwa huko kwa sababu ya kuufanya utajiri wake kuwa ndiye mungu wake, mwisho wake ukawa ni kuangamia milele.

  Neno la Mungu na mabadiliko ya rohoni anayoyapata mtu baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake, ndiyo yatabaki kuwa kigezo pekee cha kuwavuta watu waje kwa Yesu. Nadhani hii ndio ilikuwa point yangu toka mwanzo pale niliposema badiliko la dhati(kama lipo) ndani ya maisha ya kiroho ya Rose Muhando baada ya kuachana na uislamu na kuingia kwenye ukristo, kitu ambacho nadhani ndicho alichokuwa anataka watu waone pale aliposimama na kuueleza umati ule kwenye lile tamasha juu ya maisha yake kabla na baada ya kumpokea Yesu. Sijui kama dhana yangu hii ilikuwa potofu niliyoipata baada ya kusoma lile gazeti la Nyakati.

  Ndugu yangu John Paul, kuhusu kuwaalika waimbaji kama hao na jinsi ulivyonishauri nifanye hivyo, mimi nilishaweka msimamo wangu juu ya jambo hilo kwenye ile post yangu ya tarehe 8/05/2011 kuwa siwezi kumlipa mwimbaji hela zote hizo hata kama napenda sana aje aimbe au atoe huduma kwenye shughuli yoyote niliyoiratibu. Huo ndio ulikuwa msimamo wangu na utabaki hivyo siku zote. Hivyo sina hata sababu ya kujaribu kufanya hivyo ili kwamba niweze kuchangia mada kwa uthibitisho au uzoefu juu ya jambo hilo. Kimsingi inasikitisha sana pale Mungu anapowanyanyua waimbaji wetu halafu wao wanaanza kutoza viingilio au ada ya mialiko kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo! Ninaweza kuelewa mwimbaji akihitaji angalau nauli na vitu vingine vidogo vidogo kwa ajili ya kumfikisha mahali hapo alipoalikwa(kama kunahitajika gharama ya nauli), lakini utashangaa mwimbaji labda yupo Arusha, akialikwa kwenda labda Monduli adai fedha nyingi kiasi hicho?!

  Nadhani tukiliangalia jambo hili kwa mapana yake tunaona kanisa ndilo limewafikisha waimbaji hawa hapo walipo(money minded) kwa sbabu limewakumbatia mno waimbaji binafsi kuliko vikundi vya kwaya vinavyoimba makanisani mwao siku za ibada. Muumini anapoalikwa kuzindua album ya mwimbaji binafsi yupo tayari kutoa maelfu kama sio mamilioni ya hela kwa album hiyo moja lakini muumini huyo huyo ukimwambia achangie kikundi cha kwaya ya kanisani kwake anatoa hela kidogo sana na kwa shingo upande mno. Vikundi vingi vya kwaya vikialikwa mahali havilipwi fedha yoyote na nauli wanajichangisha wenyewe, lakini mwimbaji binafsi ni tofauti kabisa. Kwa kweli inasikitisha na kuumiza sana kwamba iliyotarajiwa kuwa HUDUMA imegeuka kuwa BIASHARA tena biashara inayogharimu sana!

  Mungu wetu aturehemu!

 27. Ndugu Haggai,

  Nashukuru kwa majibu ya maswali yangu kwako. Nilikuwa bz kwa namna fulani hivyo nikachelewa ku-resond.

  Nimeridhika na majibu ya maswali yote isipokuwa lile la kwanza linalouliza kama ni lazima kila mtu anayemcha Mungu kuwa na mafanikio ya kimwili. Japo umeonyesha mifano ya kwenye Bible kuhusu wacha Mungu waliobarikiwa kwa sababu ya kumcha Mungu lakini natumaini nawe pia unawafahamu katika Bible wacha Mungu waliomcha Mungu hasa na wengine wakatumiwa katika matukio makubwa, kama vile Yohana mbatizaji, lakini maisha yao kimwili yalikuwa duni kabisa. Hata katika Ebrania 11:37-38 imeandikwa kuwaelezea watu hao kuwa ni watu ambao:

  “…..walizunguka zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi, walikuwa wahitaji, …..(watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao),walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi”.

  Na nyakati za watu hao, wakati wakizunguka kwenye mapango, tayari matajiri walikuwepo. Hatuwezi kusema hayo ndiyo yalikuwa maisha ya wakati ule. Kwangu mimi, kutokana na ninavyoisoma Biblia, jibu langu ni kuwa SI LAZIMA kila mcha Mungu kuwa na mafanikio ya kimwili. Sababu ziko nyingi sana na nyingine zikiwa ni mapenzi ya Mungu wala si ya binadamu.

  Kwa sababu hiyo UTAMU WA YESU si tu kwa magari, nyumba, mashamba nk. Kuna zaidi na pengine TOFAUTI ya hapo. Hivyo UTAMU WA YESU haustahili kulinganishwa na mambo ambayo hata kama mtu hana Yesu anaweza kuwa nayo tu. Kuwaambia watu waje kwa Yesu kwa sababu kuna magari mazuri maana yake ni kuwa walio nao tayari hawawezi kuja kabisa!

  Ninanukuu sehemu ya maoni yako halafu niendelee:

  “Sijawahi kukutana na hali hiyo, labda kwa sababu sijawahi kumwalika mwimbaji ‘mkubwa’ wa calibre ya Rose Muhando, hata kama ningefanya hivyo kwa kweli nisingetoa hizi hela.
  Kwa msingi huo basi, mwimbaji wa namna hii akinunua gari na kujenga nyumba, hayo mimi nayaita mafanikio ya mpumbavu ambayo mwisho wake ni kuangamia milele, na mwimbaji wa namna hiyo hana mafanikio ya rohoni”.

  Waimbaji wetu ndio wanaishi maisha hayo na vitu wanavyomiliki vinatokana na vipato hivyo vya pesa kwanza kabla ya huduma [kama kweli ni huduma]. Kwa kuwa hujaalika mwimbaji wa aina ya Rose Muhando, ninakushauri FANYA HIVYO halafu ujionee mwenyewe ili siku nyingine ukichangia mada uchangie ukiwa na uthibitisho wewe mwenyewe.

  Dada Eunice alishathibitisha hilo ndiyo maana akaandika hivi:

  “..siku moja nilimchagua muimbaji anayeimba kwa mguso wa kiroho, kwa upole anayeheshimika kwamba nyimbo zake zinagusa uwepo wa Mungu LAKINI Alinitajia bei kumbwa nilimuomba anipunguzie iwe laki 5 akaniambia hailipi!!!Hivyo si vizuri kumsemea vibaya muimbaji mmoja,hata usiowategemea hawashikiki”

  ..ni kweli hawashikiki kwa sababu ya ‘bei’ zao ni kubwa mno. Hivyo, kwangu mimi, wanaponunua magari na kujenga nyumba kwa sababu ya bei hizo kubwa SIAMINI kama ni SAHIHI kuyanadi mafanikio yao hayo kuwa YAMETOKANA NA UTAMU WA YESU na hivyo iwe sababu ya kuwaita watu waje kuokoka. That is not what the ALTAR CALL is about! Huo si mwaliko wa Injili ya Yesu, Mitume na hata Biblia kwa ujumla. Mwaliko wa Yesu ni kwa ajili ya UZIMA WA MILELE. Na ndani ya uzima huo ndimo kuna mengine ambayo ni nyongeza. Na nyongeza si kitu cha lazima. Hutolewa mahali kinapohitajika na pengine huzuiwa mahali ambapo inaonekana kinaweza kuleta madhara!

  Ndiyo maana akasema, “…na hayo mengine mtazidishiwa/shall be added unto you”.

  Ninatafuta muda mzuri ili niandike kwa kirefu pamoja na mifano kueleza hoja yangu kuwa SI LAZIMA kila mcha Mungu awe na mafanikio ya kimwili. Lakini kama una neno juu ya haya niliyoandika unaweza kuandika tu na hata kama ni swali nitalibu [kwa kadri litakavyokuja] ili tuendelee kupanua ufahamu juu ya jambo hili.

  Asante.

 28. Kaka Orbi nakushukuru sana ,nimependezwa nawe kwa ukiri wako.Ukisikiliza ule wimbo unagundua mwimbaji huyu alitafuta maneno ya kuelezea uzuri wa Yesu akashindwa ndo maana akaona ni vema atumie neno hili,”hahisi hivyo”anasema utamu wa Yesu haufanani hata na Asali!anakumbuka enzi zake alipokuwa kibarua cha kulima Mpunga.

  Kuna waimbaji wengi tu hata wale tunaodhani ni wa rohoni kuliko wengine wamezungumzia raha ya kuwa ndani ya Yesu kwa namna tofauti.Esther Wahome ana wimbo mmoja unaitwa Asali,anazungumzia utamu wa Yesu pia.wengine wameimba Yesu ni mpenzi,wemgine yesu ni rafiki, mwokozi, mtetezi,inategemea na feelings za mtu na aliyotendewa !

  Kuhusu viingilio ,kwa kweli hapa ni tatizo kwa sababu waimbaji wengi au wote wanataja viingilio.huwezi ukambeza mmoja. siku moja nilimchagua muimbaji anayeimba kwa mguso wa kiroho, kwa upole anayeheshimika kwamba nyimbo zake zinagusa uwepo wa Mungu LAKINI Alinitajia bei kumbwa nilimuomba anipunguzie iwe laki 5 akaniambia hailipi!!!Hivyo si vizuri kumsemea vibaya muimbaji mmoja,hata usiowategemea hawashikiki.mimi siwalaumu na wenyewe wanatumia Gharama nyingi pia.si Vibaya wakaishi maisha mazuri kama wanampendeza Mungu.

  Mimi sio siri Huyu Rose ananibariki sana yaani mpaka naona ndio muhubiri wangu,kiufupi ni muinjilisti!natamani siku moja anitembelee kwangu nimuandalie chakula. Sauti yake ni tamu inanipa raha moyoni,maneno ya ujasiri anayotamka bila kuogopa ni uinjilisti tosha.speed anayokwenda nayo anapoimba nahisi napaa.nikimsikia anaimba nasimama na kununua soda ili nimsikie vizuri hata kama CD Yake ninayo nyumbani.
  Lakini si yeye tu,bali hata Christina Shusho,Bahati Bukuku, Martha Mwaipaja ,Miriam Lukindo wananiletea raha na kunikumbusha habari za Yesu wangu.Mungu Awabariki waimbaji wote wanaolitukuza jina lake!

 29. Ndugu John Paul, Bwana Yesu asifiwe.

  Awali ya yote naomba nichukue nafasi hii kukutaka radhi kwamba nilikuwa nje kidogo ya mtandao huu wa internet hivyo sikuweza kuyajibu mapema maswali yako matatu kama ambavyo uliyauliza kutokana na mada hii.

  Swali lako la kwanza lenye vipengere viwili vya a na b liliuliza hivi:
  a). “Hivi ni lazima mcha Mungu awe na mafanikio ya kimwili pia?”
  Jibu: Kwa jinsi ninavyoelewa neno MCHA Mungu lina maana ya mtu anayemhofu Mungu na kumtegemea Yeye kwa kila kitu kwa kipindi chote cha maisha yake hapa duniani. Mcha Mungu yeyote ni mtu aliyefunikwa na HOFU ya Mungu, na hofu hii humtengenezea mtu huyo tabia (character) ya kutokufanya chochote kilicho kinyume na mapenzi ya Mungu hata kama mazingira yanamlazimisha kufanya kilicho tofauti na mapenzi ya Mungu. Kwa mfano mcha Mungu yeyote hatapokea rushwa hata kama mazingira yanayomzunguka yamemtengezea nafasi ya kufanya hivyo; na mazingira hayo yanaweza kuwa yale ya yeye kukosa mahitaji muhimu kwa mwanadamu kama chakula,mavazi n.k. Kwa hiyo kwangu mimi MCHA Mungu kwa maana ya niliyoieleza hapo juu ni lazima awe na mafanikio ya kiroho na kimwili pia kwa sababu kumcha Bwana ni kukataa uovu na ubaya wote na kumtii Mungu ambaye Yeye mwenyewe amesema tukimtii baraka au mafanikio yataambatana nasi. Ibrahimu alikuwa mcha Mungu na alibarikiwa sana, Ayubu alikuwa mcha Mungu na alibarikiwa sana pia. Yakobo alikuwa mcha Mungu ilisababisha baba mkwe wake abarikiwe sana kwa sababu ya uwepo wa Yakobo (Mwanzo 30:25 na kuendelea; lakini pia Yusufu alikuwa mcha Mungu na hiyo ilisababisha nyumba ya Farao na Misri kwa ujumla kubarikiwa.

  Labda swala la kuzingitia hapa ni hayo mafanikio ameyapata kabla au baada ya kuanza kumcha Mungu. Swali hili linanipeleka kwenye dhana potofu ya shetani aliyokuwa nayo juu ya MCHA Mungu aliyeitwa Ayubu. Dhana hii potofu ya shetani ilikuwa ni kwamba Ayubu alianza kumcha Mungu baada ya Mungu kumbariki na kupata mali nyingi na kumwekea ulinzi pande zote, huu ni mtizamo finyu sana. Na dhana hii ndiyo waliyonayo wapendwa wengi wa kanisa la leo, kwamba wanataka waone kwanza mafanikio ya kimwili ndipo waanze kumcha au kumtumikia Mungu. Mtizamo sahihi ni kwamba mtu anamcha Mungu kwanza ndipo baraka zinafuata, sio kinyume chake.

  Mathayo 6:33 inasema “Lakini utafuteni KWANZA ufalme wa Mungu na haki yake na HAYO YOTE MTAONGEZEWA” (Biblia NENO). Lakini msingi wa mstari huu unaanzia kwenye maelezo ya kuanzia mstari wa 25-32 na kwa kifupi ni kwamba ndani ya ufalme wa Mungu kuna kila kitu kwa ajili ya maisha yetu hapa duniani na maisha yale ya milele. Kwa maana hiyo haki amani na furaha katika Roho Mtakatifu itakuwepo tu pale tutakapokuwa pia tumepata mahitaji yetu ya kila siku. Mtu aliyeokoka sijui atakuwaje na furaha na amani wakati atakapokuwa analala njaa kila siku na hana hata nguo ya kuvaa. Ndio sababu biblia inatuhimiza kuitunza pia miili yetu kwa chakula na mavazi!

  b). Kipengere cha pili cha swali lako kinasema:
  “Ni kipi kinatangulia kuwakilisha hali ya kingine: Mafanikio ya kimwili yanawakilsha yale ya kiroho au mafanikio ya kiroho yanawakilisha yale ya kimwili?”

  Kabla sijaendelea kujibu swali hili nakuomba urejee kwenye post zangu za tar.2 na 4/5. Kwenye ile ya tarehe mbili nilinukuu neno toka 3 Yohana 1:2 inaoonyesha mafanikio kwanza ya kiroho kabla ya kimwili; na ile post ya tarehe 4 nilinukuu andiko toka Kumbukumbu la Torati 28:1-14 ambalo pia linaoonyesha kuwa baraka mbali mbali zitaandamana na mwanadamu pale tu atakapo mtii Mungu, kwa lugha rahisi nikasema kama mtu huyo atakuwa ameokoka kweli na nikaenda mbali zaidi kwa kusema Mungu anaangalia Nia iliyoko ndani ya moyo wa huyo mtu inayompelekea aseme kuwa anamtii Mungu. Kama nia hiyo ni kinyume na mapenzi ya Mungu, kwamba kama mtu huyo ana agenda yake ya siri ndani ya moyo wake, ina maana mtu huyo hana mafanikio ya rohoni na hivyo hata ya kimwili hana, HATA kama kwa muonekano wa kibinadamu anaonekana kufanikiwa; na ndipo nikasema kufanikiwa kwa mpumbavu kutamwangamiza. Nini maana ya kufanikiwa kwa mpumbavu? Ni mafanikio nje ya mpango wa Mungu.

  Ili wapendwa tujue kwamba mafanikio yaliyo kwenye mpango wa Mungu ndani ya Yesu Kristo yanaanzia rohoni kwanza hebu tusome toka Waefeso 1:3 inayosema hivi;
  “Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ALIYETUBARIKI sisi kwa baraka ZOTE za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo”
  Kwa maana ya mstari huo baraka zote za watu waliookoka zinatakiwa zianzie rohoni, maana zipo tayari katika ulimwengu wa roho na hiziwezi kuonekana katika ulimwengu wa kimwili kwa sababu hali ya kiroho ya wapendwa wengi haiko sawa. Ili baraka hizi zipate kuonekana ni lazima tuingie kwanza kwenye ulimengu wa kiroho na kujiweka sawa huko maana vita kubwa na ngumu ipo kwenye kuumiliki ulimwengu wa kiroho.

  Kwa hiyo mafanikio ya kiroho ndiyo hutakiwa kuwakilisha mafanikio ya kimwili kama ilivyoelezwa kwenye hiyo 3 Yohana 1:2. Homework kubwa ninayoiacha kwa wasomaji wa blog hii ni namna gani utajua mafanikio ya mtu kiroho? Kazi kwenu!

  Swali lako la pili tumelijadili sana kwenye blog hii juu ya waimbaji kukodisha kumbi na kutoza viingilio kwa ajili ya uzinduzi wa album zao n.k. Nadhani watu wengi sana walichangia na kutoa mawazo yao, na naona mwelekeo wa swali hili ni huo huo. Lakini kwa kifupi mimi sipendi wala sikubaliana na mwimbaji yeyote anapoalikwa mahali kwenda kutoa huduma ya uimbaji halafu adai malipo ya kiasi kikubwa kama hicho ulichokitaja. Sijawahi kukutana na hali hiyo, labda kwa sababu sijawahi kumwalika mwimbaji ‘mkubwa’ wa calibre ya Rose Muhando, hata kama ningefanya hivyo kwa kweli nisingetoa hizi hela.
  Kwa msingi huo basi, mwimbaji wa namna hii akinunua gari na kujenga nyumba, hayo mimi nayaita mafanikio ya mpumbavu ambayo mwisho wake ni kuangamia milele, na mwimbaji wa namna hiyo hana mafanikio ya rohoni.

  Swali lako la tatu lilisema hivi;
  ‘Kwa kuwa dunia nayo huwabarikia watu wake, je ni sahihi kuwaalika watu kuja kwa Yesu kwa kutumia vivutio hivyo hivyo ambavyo dunia inawavutia watu, yaani vivutio vya kimwili?’

  Jibu la swali hili ni simple and clear kwamba HAPANA sio sahihi kufanya hivyo. Kwanza nashukuru umeliweka swali hili vizuri sana pale uliposema “kwa kuwa dunia nayo huwabarikia WATU WAKE’, hapo ina maana kwamba kuna ‘watu’ wa dunia na ‘watu’ wa Mungu, hii tofauti lazima ionekane wazi kati ya makundi haya mawili. Maana yake kuna watu wanaobarikiwa kwa sababu ya kufuata au kutekeleza matakwa ya dunia hii, nadhani naeleweka ninaposema matakwa ya dunia hii!! Watu wa namna hiyo wanapotaka kutumia mafanikio au baraka hizo kuwaambia watu kuwa ni Yesu kawabariki wakati inajulikana wazi kuwa ni wezi wa mali za umma, waenda kwa waganga wa kienyeji na wauaji wa maalbino n.k, hakika huo ni udanganyifu na wanajipalia mkaa vichwani mwao.

  Mafanikio au baraka kama hizo ndizo zilizomfanya yule kijana tajiri aliyeenda kumuuliza Yesu afanye nini ili apate kuokoka (uzima wa milele), alipoambiwa auze zile mali zote alizozipata nje ya Yesu, alisikitika sana na kuondoka bila kuaga (Mathayo 19:16-22). Kwa hiyo tuwavute watu kwenda kwa Yesu kwa mafanikio yetu ya kiroho ambayo yameonekana kwenye ulimengu wa kimwili. Faida kubwa ipo katika kufanikiwa kiroho kwanza na yatakayojitokeza kwenye ulimwengu wa kimwili yatadumu na kumpa Mungu utukufu. Lakini baraka zitokanazo na mahangaiko na msukumo wa kidunia hazidumu na siku zote zinampeleka mtu kwenye maangamizi.

  Labda nimalizie sasa kwa kusema kidogo kuhusu mada hii ya Rose Muhando. Msingi wa post zangu ulikuwa juu ya maisha ya mwimbaji huyu kabla na baada ya kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake, haziku-base sana kwenye utambulisho wa wimbo wake ambao tangu mwanzo nimekiri kuwa sijawahi kuusikia na wala sijui maneno yaliyopo ndani ya wimbo huo. Lakini nilichokisema ni kwamba Rose anastahili kupongezwa(kwa mtazamo wowote ule mtu anavyoweza kuelewa) kwa kitendo chake cha kusimama kwenye tamasha la watu wengi na kusema wazi kuwa maisha nje ya Kristo ni ubatili mtupu kwa wale wote ambao hawajampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao, hata kama wapo ndani ya ukristo kwa miaka mingi.

  Baraka kwenu nyote.

 30. Dah.. mimi mnisamehe tu wapendwa, kusema kweli hivyo alivyo vaa sijapendezwa kabisa..

  Nampenda sana na kazi yake ni njema sana, lkn wakati mwingine naona ni vizuri zaidi kuwa sensitive sana hata ktk uvaaji hasa ukizingatia utawafikia watu wa aina nyingi sana. Mambo madogo kama hayo yanayoweza kurekebishika yasiharibu ladha ya kazi nzuri unayoifanya!

  Mungu akubariki sana dada kwa kujitoa ktk kumtumikia!

 31. Amani, Heshima na Upendo kwenu
  Ndugu IRENE. Umesema “nyimbo za sasa hivi kweli hazina uwepo wa Mungu kabisa, wengi tunauza albamu tu.”
  NAOMBA UNISAIDIE KUTAJA NYIMBO ZA INJILI ZISIZO ZA SASA AMBAZO UNAAMINI ZINA UWEPO WA MUNGU KABISA.

  Asante

 32. kazi kweli kweli, mimi ni msikilizaji tu, hiyo tunaita friendly fire, ambayo ipo miongoni mwa wapendwa hasa Tanzania, hebu tuone

 33. Shalom wapendwa,
  najifunza mengi hapa, naunga mkono comments za John Paul, Orbi na Mary Joshua. Nionavyo ni kuwa kimtokacho mtu ndicho kilicho moyoni mwake. Kama uliokoka kupata pesa na unazipata hata ikibidi kwa njia zisizosahihi ni lazima na mahubiri yako yataonyesha hayo tu maana ktk wokovu huoni la zaidi. Mavzi yako pia yatakutambulisha wewe ni nani. sorry if I sound too harsh but… kweli tunakoenda tunawakwaza watu wasiingie badala ya kuwahubiri waingie ktk wokovu. Barikiweni

 34. Ndugu Haggai,

  Kwa Lengo tu la kuendelea kujadiliana kuhusu UTAMU WA YESU ninaomba kukuuliza kidogo kutokana na maneno haya uliyoandika hivi:

  “Ndio sababu biblia inasema wazi kuwa tunatakiwa kufanikiwa katika mambo yote na kuwa na afya kama vile roho zetu zifanikiwavyo (3 Yohana 1:2). Kwa maana nyingine mtu aliyeokoka, mafanikio yake ya kimwili yanatakiwa yafanane na mafanikio yake ya kiroho, ukiona kinyume chake jua kuna tatizo mahali.”

  Siku hizi kuna mahubiri hayo kuwa kama umeokoka na bado unaishi maisha ya uhitaji basi ujue kuna tatizo mahali. Na kwa sababu hiyo wale ambao ni wahitaji katika maisha ya kimwili wamekuwa wakitazamwa kama ni wa-dhambi na/au wanahitaji kufanyiwa deliverance na kuvunjiwa laana za umasikini…..!

  Ndiyo maana katika makanisa mengi viongozi katika idara mbali mbali wamekuwa wakichaguliwa kwa kuangaliwa hali yao ya KIPATO maana kipato cha mtu sasa ndicho kinachoashiria UCHA MUNGU wake kwa sababu ni vigumu, kama binadamu, kuamua moja kwa moja juu ya hali ya kiroho ya mtu. Kwa hiyo tunachokiona sisi ni magari, kazi nzuri, nyumba nzuri, degree, kwenda ulaya, na hivi ndivyo tunatumia kuamua kuwa kwa kuwa huyu mtu KAFANIKIWA kwa kiasi fulani KIMWILI, maana yake na roho yake imefanikiwa kwa kiasi hicho hicho!

  Maswali yangu machache ni haya yafuatayo:

  1. a)Hivi ni LAZIMA mcha Mungu awe na mafanikio ya kimwili pia?
  b)Ni kipi kinatakiwa kiwakilishe hali ya kingine: mafanikio ya kimwili yawakilishe yale ya kiroho au mafaniko ya kiroho yawakilishe yale ya kimwili?

  2. Muimbaji anayefanya huduma yake kwa viingilio vya juu na kudai pesa kwanza kwenye akaunti yake ndipo aje kuhudumu, mfano kuimba kwenye mkutano kwa siku 3 tena kwa kufuatisha CD, akadai milioni 2 kwanza kwenye akaunti yake, ANAPONUNUA GARI, KUJENGA NYUMBA, KUBADILISHA AINA YA MAVAZI YAKE nk……

  Je! Twatakiwa kusema kuwa mtu huyo kavipata vitu hivyo kwa sababu ya YESU AU kwa sababu ya PESA anazozipata kama MALIPO ya uimbaji wake?

  3.Kwa kuwa dunia nayo huwabarikia watu wake,
  Je! Ni sahihi kuwaalika watu kuja kwa Yesu kwa kutumia vivutio hivyo hivyo ambavyo dunia inawavutia watu, yaani vivutio vya kimwili?

  Nimeandika haya nikiwa katika kutafakari maana ya maneno:

  UFALME WA MUNGU SI KULA WALA KUNYWA, BALI NI HAKI, AMANI NA FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU. [Rum 14:17]

  Asante.

 35. Mungu awabariki watumishi, na pia ambariki Roze kwa huduma mzuri ya uimbaji maana ndiyo huduma pekee itakayodumu hata milele mbinguni, ila sikufurahishwa sana na uvaaji ktk picha hiyo.Mnisamehe kwa hilo, huo ni mtazamo wangu.

 36. Ndugu Orbi,
  Ulichosema kwenye post yako ya tarehe 3/5/2011 hakuna anayeweza kupingana nacho, lakini biblia ninayoisoma inaniambia kwenye Kumbukumbu la Torati (sehemu zingine) 28:1-14 kuwa pale tu nitakapomtii Mungu(najua neno utii lina maana pana na mojawapo ni kuokoka kwa lugha rahisi) baraka mbalimbali zitaambatana nami, tena biblia inasema ni baraka hizi zote, sio kidogo kidogo, zote!!. Najua baraka ya kwanza na kubwa ni kujua uzuri wa Yesu katika kila eneo la maisha yetu na kutuwezesha kuishi maisha ya utakatifu hata kama hatuna mali na vitu hivi vinavyoonekana.

  Lakini itanishangaza sana kama kweli umekuwa mali ya Yesu aliye na utajiri wote halafu wewe uwe maskini wa kutupwa. 2 Kor 8:9 inasema wazi kuwa Yesu Kristo ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yetu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini wake sisi tupate kuwa matajiri(wa kiroho na kimwili pia).

  Kama ilivyo kwako Orbi kwamba hujausikia wimbo huo, hata mimi sijausikia, lakini angalau nina ABCD ya maisha ya Rose Muhando huko nyuma kabla hajampokea Yesu na kubadili dini toka uislamu na kuwa mkristo. Kwa maana hiyo niliposoma kuwa ametoa ushuhuda wake kwenye lile tamasha nilijua alichokuwa anakisema toka moyoni mwake kutokana na hali aliyokuwa nayo huko nyuma na badiliko lililotokea kwenye moyo wake baada ya kumpokea Yesu na kisha kuonekana kwenye ulimwengu wa kimwili.
  Cha muhimu hapa ni kwamba Mungu wetu tunayemtumikia si maskini, kwa nini sisi watumishi wake wa kweli tuwe maskini? Nakumbuka wanafunzi wa Yesu walimuuliza swali Yesu kuwa wao wameacha vitu mbali mbali, wake na watoto na wamemfuata, je watapata nini? Jibu la Yesu lilikuwa rahisi na straight forward kwamba watapata hapa hapa duniani mara mia ya vile walivyoviacha na kisha UZIMA WA MILELE. Huo ndio utamu wa kuwa ndani ya Yesu naye kuwa ndani yetu!!

  Onyo! Usikimbilie kwa Yesu kwa NIA ya kupata mara mia ya vile ulivyoviacha! Hutapata hata kimoja kwa sababu Yeye anaona NIA au Kusudi lililojificha ndani ya moyo wako, na kama kusudi hilo ni kinyume na mapenzi yake, hata uimbe mpaka mwisho wa dunia hii kamwe hutauona utamu wake. Ndio sababu watu wengi wanasema wameokoka lakini maisha yao hayalingani na wokovu huo(kiroho hata kimwili pia) kwa sababu wameokoka kwa kusudi fulani ambalo ni kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu, ndio sababu biblia inasema moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu kuliko kitu chochote , tena una ugonjwa wa kufisha (Yeremia 17:9-10), neno linasema hivi;

  “Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi. Ni nani awezaye kuujua? Mimi BWANA huchunguza moyo na kuzijaribu NIA, kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake, kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili”

  EMANUELI!!

 37. kaka orbi! japo sijausikiliza huo wimbo lakini msg yako imenigusa sana kwani hiyo ndio injili ya kweli, nyimbo za sasa hivi kweli hazina uwepo wa Mungu kabisa, wengi tunauza albamu tu. tukae ktk neno la Mungu na kutembea katika Roho mtakatifu na kumtafakari yeye aliye stahimili mapingamizi makuu kristo Yesu, tukiwa na macho ya rohoni tutajua mambo mengi kwani Roho asema nasi waziwazi, tunatakiwa kuwa makini sana na uimbaji wa sasa hivi tumekuwa mwilini sana na kuenenda kidunia sana kinachotutofautisha ni maneno ya muhusuyo Mungu lakini hayana uhai ndani yake. asanteni

 38. Dada Eunice,

  Mimi sijausikiliza wimbo huo nimetumia tu nukuu iliyoko kwenye post, hivyo maoni yangu yanaweza kuwa yanakosea kabisa, kwa hilo naomba msamahama. Mungu akubariki.

 39. Kaka Orbi! mimi nimeusikiliza huo wimbo kweny praise power radio,dada rose anazungumzia tofauti kati ya mali utakazozipata wakati hauna yesu na mali ambazo utazipata kwa njia sahii wakati ukiwa ndani ya Yesu.anasema utamu wa yesu utakuweka mbali na dhambi.vya nje ya yeu ni vizuri lakini ni vichungu na vinawasha kama upupu.ni heri kuwa ndani ya Yesu na kuonja utamu uliomo katika yeye badala ya kuhangaika na mali za dunia ambazo zaweza kukuletea madhara.ukitaka magari mazuri onjeni utamu wa Yesu,ya nje yana upupu.ukionja utamu wa Yesu utakuweka mbali na dhambi,ina maana utatii Neno lake na mito ya baraka itatiririka kwako,anasema Dada Rose Muhando!Mungu Ambarika Rose na waimbaji wengine wote.Amen

 40. Wapendwa,

  Naamini kwa dhati kuwa kuna utamu ndani ya Yesu, ingawa kwangu neno utamu linakuwa zaidi kwa kitu ambacho unakigusa au kuleta hisia za mwilini, lakini hili si hoja Inawezekana ni lugha ya Uimbaji tu iliyotumika.

  Kwangu mimi ninatazika na hayo maneno “UKITAKA GARI NZURI MAJUMBA MAZURI ONJA UTAMU WA YESU”

  Mimi naamini Msukumo unaotusukuma kwenda kwa Yesu si MAGARI NA MAJUMBA MAZURI! Haikuwa hivyo kwa Kanisa la Kwanza, kwani kwa waumini wa KANISA LA KWANZA Utamu wa Kumjua Yesu uliwasukuma WAUZE VIWANJA NA MAJUMBA! Na Paulo anasema kuwa anayaona mambo yote kama UCHAFU….NALIYAHESABU KUWA HASARA…..KWA AJILI YA UZURI USIO NA KIASI WA KUMJUA KRISTO YESU!

  Kwa kifupi kabisa hata tusipoendesha Magari na kuwa na majumba mazuri bado tutaona utamu wa Kukaa ndani ya Yesu Kristo! Tulikuwa na magari na majumba mazuri kabla hatujamjua Yesu Kristo, lakini hayakutuletea Utamu wowote!Na Furaha ya Kweli ni pae tulipomruhusu aingie moyoni Mwetu na Kutupanisha na Mungu kwa msamaha wake na kuwa NA AMANI NA MUNGU!

  Sio lengo langu kumvunja moyo dadangu Mhando, kwani natambua waimbaji wanaiimba kile ambacho wakristo wengi wanakiamini leo au wanapenda wasikie! Na watu wanapenda kusikia mafanikio ya mwilini! Lakini kwa baadhi yetu Kuuonja Utamu wa Yesu kutatufanya tuache magari yetu mazuri yenye viyoyozi, majumba mazuri, na vitu kadha wa kadha ili kumtumikia Yeye popote pale atakapotuamuru Twende! utamu wa kuwa ndani ya Yesu ni KUMTII! Kwani tunatarajia Mji wenye msingi ambao mwenye Kuubuni na kuujenga ni Mungu!

 41. naona kama anachelewa kuitoa hiyo album.afanye haraka tumesubiri mpakaaa.jamani Rose fanya haraka

 42. Wapendwa,

  Hakika kwa Yesu kuna utamu na raha ya ajabu. Wengi ambao maisha yetu huko nyuma hayakumtukuza Mungu tumeuona utamu na raha hiyo baada ya kukabidhi maisha yetu kwa Yesu, mimi nikiwa mmoja wao.

  Cha kufurahisha ni kwamba nilisoma kwenye gazeti moja nadhani ni Nyakati pale Rose Muhando aliposimama bila woga wala aibu kwenye tamasha la Pasaka na kueleza maisha yake kabla ya kumpokea Yesu yalivyokuwa mabaya na baada ya kumpokea Yesu yalivyo badilika sasa. Huu ni ushuhuda muhimu sana ambao ukiendelezwa kwenye matamasha ya namna hii unaweza kuwavuta watu wengi kukabidhi maisha yao kwa Yesu. Ndio sababu biblia inasema wazi kuwa tunatakiwa kufanikiwa katika mambo yote na kuwa na afya kama vile roho zetu zifanikiwavyo (3 Yohana 1:2). Kwa maana nyingine mtu aliyeokoka, mafanikio yake ya kimwili yanatakiwa yafanane na mafanikio yake ya kiroho, ukiona kinyume chake jua kuna tatizo mahali. Kumbuka pia biblia inaonya juu ya kufanikiwa kwa mpumbavu kuwa mafanikio hayo yatamwangamiza. Heri tufanikiwe ndani ya Yesu ili tusiangamie.

  Mungu awabariki wote.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s