Mtu mwenye wake wengi, anapookoka!

Mtu mwenye Wake wengi anapo mpokea Bwana Yesu. Je! Ni hatua gani anayo/anazotakiwa kuchukua dhidi ya hao wake zake?

Advertisements

28 thoughts on “Mtu mwenye wake wengi, anapookoka!

 1. Siyi “mwisraeli Feki”,
  Wewe unashika Amri kumi?
  Je,Torati iliruhusu wanawake kuhubiri?

 2. Pandael,
  Ni kweli unachokisema pengine kinaweza kuwa na mashiko. Hata mimi najua ndani ya makanisa yetu, kuna mafundisho ya dini(matangopori) na mafundisho ya Biblia!! Yapo kabisa.! Ukijadili mambo haya ya Biblia ukiwa na pre-conceived ideas fulani, unaweza kujikuta unapotoka kwelikweli!! Ni lazima ujiempty-headed kwanza!! Tofauti na hapo utaishia kuwa mbishi kama Sungura!! Lwembe naye ni mbishi kiaina tu ila huwa ni mwelewa kiasi chake!!
  Pamoja na insights zako hizi Pandael (na wengine kama akina Sungura, Lwembe, Seleli, Marry, n.k.), ni vyema mkautii ukweli wa maandiko ulio wazi sana kama vile Amri 10, na mafundisho mengine ya Biblia. Tofauti na hapo, kazi na uelewa wenu wa kiimani ni bure!!
  Aidha, ni dhahiri kuwa, NDOA ni muunganiko wa ke na me wenye imani/itikadi moja tu!! Ni vyema watu wakaepuka ndoa mseto!!
  Ubarikiwe.
  Siyi

 3. Ndg Lwembe,
  Nashukuru sana kwa kuweza kujibu majibu sahihi ya Kimaandiko.
  Hasa suala la ASKOFU awe mume wa MKE MMOJA na suala la SHEMASI awe mume wa MKE MMOJA.
  Mkazo ni MKE MMOJA, Mungu akijua hasa kuwa wapo wenye WAKE WENGI walioamuamini.
  Hayo ndiyo niliyotaka kuyazungumzia baada ya maswali niliyomuuliza Siyi.
  MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI.

 4. SIYI,
  Nimeamini alichokisema ndugu Lwembe kuwa mambo haya huyajui kabisa kama vile suala la TORATI na SABATO linavyokukanganya.
  Kama ni alama umepata 0/100.
  Kwa maneno mengine uko OP.

 5. Pandael
  Nakushukuru sana kwa maswali yako. Najua umeuliza lakini unafahamu vyema msingi wa Maandiko. Nami nakujibu kama ulivyouliza;

  1. “Mtu mwenye Wake wengi anapo mpokea Bwana Yesu. Je! Ni hatua gani anayo/anazotakiwa kuchukua dhidi ya hao wake zake?”
  Jibu
  Biblia imenyamaza kwa habari ya mwanaume mwenye wake wengi amapomwamini Kristo. Huenda aya hiyo ipo lakini mimi sijaiona!! Kilicho bayana ni kwamba, Biblia kwa mujibu wa mpango wa Mungu, ni mume mmoja, mke mmoja. Hakuna positivity kwa wanaume wenye wake wengi ndani ya Biblia, isipokuwa negativity tu.

  2. Hao wanawake wanaochwa, wako tayari kuolewa na wanaume wengine?
  Jibu
  Wawe tayari ama la, nijuacho ni hiki, ni heri kuacha vyote(siyo wanawake tu) kwa ajili ya Kristo. Wanawake wanaoachwa wanaweza kuolewa au kuridhia kukaa hivyohivyo ilmradi mumewe awe anawahudumia kimahitaji (not ngono) tu kama watakuwa hawajaolewa.

  3. Kwenye AGANO JIPYA, ni wapi MAANDIKO yanasema,mtu mwenye wake wengi anapomwamini BWANA YESU awafukuze wake wengine abaki na yule wa kwanza?
  Jibu
  Mfano upo kwa Ibrahimu alipomfukuza Hajiri. Mke wa kwanza, ndiye mke halali kwa mujibu wa Maandiko. Wengine ni uzinzi tu.

  4.Nini maana ya NDOA?
  Jibu maana ya ndoa ni muunganiko wa watu wakubwa wenye jinsia mbili tofauti wanaokubalina kuishi pamoja kama mume na mke -mume mmoja na mke mmoja. Hii ndiyo maana ya NDOA kwa mujibu wa Biblia. Tofauti na hapo ni uzinzi na tama mbaya tu.
  Ubarikiwe
  Siyi

 6. Lwembe
  Ha ha ha ha ha ha!!
  Ni kweli sina ujuvi mkubwa kwenye mambo ya wokovu. Ila ninao kidogo. Ukisema sijui chochote kabisa, hilo si kweli rafiki yangu. Labda wewe nifundishe sasa kuhusu hili la wanawake wengi na mume mmoja.
  Umesema, fundisho la mke mmoja na mume mmoja ni fundisho la dini. Unamaanisha nini? Kama ni man made creed, nani alilileta kwenye ukristo? Mwaka gani?
  Ubarikiwe sana. Nakungoja.
  Siyi

 7. Lwembe,

  Mimi nilichosema tu ni kwamba msingi wa ndoa ni mke mmoja- mume mmoja.Hata sijaingia ndani kujadili hii mada!

  Najua yako mambo ya askofu kuwa mme wa mke mmoja, na mambo ya kila mtu na akae kama alivyoitwa.
  Kwa hiyo anayetaka kujadili hii mada kwa undani lazima azingatie kuyachambua hayo!

 8. Lwembe,

  Mimi nilisema msingi wa ndoa ni mke mmoja – mume mmoja.
  Sijaingia hata kwenye kuchambua hii mada!

  Nayajua mambo ya askofu kuwa mume wa mke mmoja, najua habari za kila mtu kubaki kama alivyoitwa!

  Kwa hiyo mtu anayeingia deep kujadili hii mada lazima ayachambue hayo!

 9. @ Pendael,
  Huyo Siyi hajui chochote kuhusu hayo mambo ya wokovu; labda mumfundishe!

  @ Sungura,
  Unapompokea Kristo, unakuja na wake zako wote! Haya mambo yenu ya kubaki na mke mmoja ni mambo ya dini tu!

  Ukimuacha mke naye akaenda akaolewa na mtu mwingine hata akiwa ni mpagani, note wanahesabiwa UZINZI! kama hao Waisilamu ndo kabisa!!

  Ila huyo hawezi kuwa askofu wala mchungaji, wala deacon; yeye anabakia kuwa muumini wa kawaida akisubiri kunyakuliwa pamoja na wake zake wote!

 10. SIYI,
  Acha UPOTOSHAJI wa MAANDIKO.
  Wewe jibu swali kwa kutumia MAANDIKO kuliko Uzoefu.
  Swali lililoulizwa ni;
  “Mtu mwenye Wake wengi anapo mpokea Bwana Yesu. Je! Ni hatua gani anayo/anazotakiwa kuchukua dhidi ya hao wake zake?”
  Swali liko wazi,tafadhali umjibu muuliza.
  Nami nitakuuliza baadhi ya maswali kama ifuatavyo:
  1.Hao wanawake wanaochwa, wako tayari kuolewa na wanaume wengine?
  2.Kwenye AGANO JIPYA, ni wapi MAANDIKO yanasema,mtu mwenye wake wengi anapomwamini BWANA YESU awafukuze wake wengine abaki na yule wa kwanza?
  3.Nini maana ya NDOA?

 11. Mimi naona baadhi ya watu mnachanganya mambo. Biblia ina msingi mmoja wa ndoa kama alivyosema Sungura. Mtu akioa wake wengi wakati hajamwamini Kristo, siku akija kumwamini, inabidi azingatie huo msingi wa ndoa -mke mmoja, mme mmoja! Akiendelea kuwa na wake zake wote ilhali amemwamini Yesu (wengine mnasema kuokoka), mtu huyo bado ni mpagani! Tusichukue mifano mibaya ya baadhi ya matendo ya watu wa Mungu ndani ya Biblia, na kuihalalisha mifano hiyo kuwa mizuri kisa ilifanywa na watu wa Mungu. Tutatandikwa!!! Tuangalie sana!!
  Neema ya Bwana iwafunike.
  Siyi

 12. Wapendwa,
  Kama ambavyo huwezi kupata andiko la moja kwa moja linalosema kuwa ukiwa na wake wengi ukiokoka ubaki na mmoja, huwezi pia ukapata andiko la moja kwa moja linalosema kuwa ukiwa na wake wengi ukiokoka ubaki nao wote!

  Lakini msingi wa ndoa ni mume mmoja-mke mmoja!!

 13. Pandael
  Kwa hiyo wewe unataka mtu akioa wake wengi, na kisha akampokea Kristo, aendelee kuwa na wake zake hao wote? Kama ni hoja ya kuopgopa kuteseka kwa hao watakaotalakiwa, huoni kuwa, mila na desturi zetu, zinakuwa na sauti kubwa kuliko neno la Mungu?
  Anyway, nilikuwa napita tu!!
  Siyi

 14. Stephen Ngullo,
  Wakati mwingine kama hujui jambo unalozungumzia ni heri unyamaze kimya kuliko KUJIFANYA mwalimu wa Biblia.
  Ulisema ” Mtu aliyekuwa na wengi wengi AKISHAOKOKA anatakiwa kubaki na MKE MMOJA na kuawaacha wengine.”
  Hebu thibitisha KIMAANDIKO. Onesha ni wapi BWANA YESU alizungumzia jambo hili POTOFU unalong’ang’ania kufundisha bila kufiliria Madhara kwa wale watakaofukuza wake zao.
  ONYO.
  WAGALATIA 1:8-9
  ” 8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
  9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”
  UFUNUO 22:18-19
  “18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
  19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”

 15. Bwana Yesu asifiwe Ndugu David Msuya
  hii mada siyo ngumu kama unavyo fikilia kabra ya kusema mada ngumu jiulize Yusu alikuja kutafuta nini duniani wakati alikuwa mbinguni kwenye laa kisha ateswe ni kwa sababu gani ?
  naomba nikueleze kidogo kuhusu wokovu biblia inasema sisi wote tulikuwa tumepotea na kupungukiwa na utukufu wa Mungu
  Yesu alikuja kututafuta na kutuokoa kutoka kwenye dhambi ambazo adhabu yake ilikuwa ni kifo na kwennda jehanamu kwenye mateso ya milele kwa upendo mkubwa wa Yesu alikubali kubeba makosa,dhambi zetu zote msalabani ili sisi tusamehewe na kuingia mbinguni yohana 3:16
  unapookoka na kufanyika mwana wa Mungu yoh 1:12 sharti la kwanza ni kuishi maisha matakatifu na kuwa mtakatifu kama Mungu 1petro 1:15
  sasa kuoa zaidi ya mke mmoja ni kufanya uzinzi na wazinzi wote sehemu yao ni jehanamu
  Mungu alimuumbia mwanadamu mme mmoja na mke mmoja tu soma matahayo 19:4
  kwa hiyo ukitaka kwenda mbinguni na ulikuwa na wake zaidi ya mmoja ni kuwaacha wote na kubaki na mke wa kwanza mke wa ujanani tu

  balikiwa kwa hayo

 16. Bwana Yesu asifiwe wapendwa wote
  kwako Pendael Simoni
  nilitoa mchango wangu kwa mtu aliye na wake wengi anapomwamini Yesu au anapookoka katika talehe zifuatazo 13/5/2015/7/6/2015 Ndugu yangu Pendael umeniuliza badhi ya majibu umesema bado hajakidhi kuna maswali manne umeniuliza nami naomba kwa unyekevu wa ku Mungu nijibu kama ifuatavyo:-
  1.swali la kwanza umesema wanawake wanaochwa wako huru kuolewa na wanaume wengine(NASEMA WAKO HURU KUOLEWA NA WAUME WENGINE)naona hapa kuna utata ambao mimi sijui unatoka wapi naomba tunaotaka kujifunza tufuatane
  (a)kwanza tujue ziko ndoa za aina mbili hapa
  1.Ndoa za watu wasio amini na wanaoamini. yako mambo uwe unaamini au huamini lazima yatekelezwe
  mfano kuchumbia au kuchumbiwa na kukubaliwa na mwezi pia na wazazi wa pande zote kunakofutana na mahari kuashiria kukubaliwa,kuwaacha wazazi na kuishi pamoja na kujulika katika jamii kuwa ni mke na mme
  sasa mtu ambaye anaamini kabra hawajakalibiana lazima wapate baraka za Bwana kwa maombi
  Sasa tufuatane huyu mtu alio akiwa haamini haamini nini Neno la Bwana swala la Ndoa mwanzilishi wake ni Mungu mwenyewe tunaona alimuumbia Adamu mke mmoja na si wawili huyu kwa kutokuamini akaoa mke zaidi ya mmoja akaliasi Neno la Bwana anapoamini maana yake analudi katika mpango wa Mungu wa kuwa na mke mmoja na mme mmoja
  soma Mwanzo 1:26..27 na mtu unapoolewa na mme wa mtu mwingine au unaoa mke wa mtu mwingine unahesabika kuwa mzinzi soma Mathayo 19:3..6) mme ukioa mke zaidi ya mmoja wale wanao fuata baada ya yule wa kwanza unahesabika unazini
  2.swali la pili umeuliza baada ya ghalika kuna watu walioa zaidi ya mmoja wapo wengi ndiyo sababu ya kuchoma miji ya sodoma na gomora ni dhambi ya uzinzi,wafalume wengi walimkosea Mungu kwa dhambi hii ya uzinzi kama akina Daudi,sulemani na wengine wengi ndio maana katika matendo Biblia inasema zamani za ujinga alijifanya kuwa haoni lakini kupitia Yesu anaangalia anataka wote watubu kwa kumwamini Yesu yaani waokoke soma matendo 17:30)
  3.swali la tatu umesema ni wapi katika agano jipya biblia inaagiza mtu anapokuwa na mke zaidi ya mmoja awafukuze wengine mathayo 19:4.5/1wakolinto 7:2/waefeso 5:25..28 unaposoma neno la mungu unaambiwa mpango wa Mungu mme mmoja/mke mmoja sasa unapoludi kwenye mpango wa Mungu ni kuachana na wengine na kubaki katika mpango wa MUNGU KWA KULIFUATA NENO LA MUNGU TU
  4. Umeuliza nini maana ya ndoa maana ya ndoa nilishajibu kwenye majibu yangu ya mwanzo kwa leo naludia kwa ufupi
  yafuatayo yakitimia inakuwa ni Ndoa
  (a)mme na mke wawe hajawahii kuolewa au kuoa au wote wawe wamefiwa na mke au mme aliye halali(1wakolinto 7:8..9,38..39/warumi 7:2..3)
  (b)mke au binti kuwa tayali kuolewa na mme huyo (mwanzo 24:57..58)
  (c)mme lazima apate ruhusa ya wazazi katika vikao vya majadiliano ya mahari mwanzo 34:8,11-12/1wakolinto 7:36
  (d)mme na mke au kijana wa kiume na binti kuwaacha wazazi na kushi pamoja na kujulikana hivyo katika jamii

  nb.ni koso kubwa kwa vijana kujuana kabra ya ndoa kuishi pamoja kama mme na mke baadaye ndipo inafungwa ndoa makanisani badala ya baraka mtachuma raana
  Mungu awabaliki naomba tuendele kujifunza

 17. Stephen Ngullo;
  Nimekuuliza maswali MAWILI (2) na umefanikiwa kujibu swali MOJA TU kwa usahihi wa MAANDIKO.Swali ulilolijibu kwa usahihi,niliuliza ” Vipi kuhusu Mume/mke aliyefiwa na mwenza, ana haki ya kuwa na ndoa?”
  Hili swali lingine lililosema ” Mtu aliyekuwa na wengi wengi AKISHAOKOKA anatakiwa kubaki na MKE MMOJA na kuawaacha wengine. Hebu thibitisha KIMAANDIKO au Je, hivyo ndivyo BIBLIA inavyosema?” hujatoa majibu ya kimaandiko.
  Swali kwenye mada ni ” Mtu mwenye Wake wengi anapo mpokea Bwana Yesu. Je! Ni hatua gani anayo/anazotakiwa kuchukua dhidi ya hao wake zake?”
  Kwenye MAJIBU YA TAREHE 13/05/2015 at 11:05 PM, ULISEMA
  ” Nije kwenye hoja ya msingi mme mwenye wake wengi anapookoka inakuwaje ni kuwaacha na kubaki na yule wa kwanza ambaye alitangulia kukaa naye mwazo na kupata ruhusa ya wazazi wa Mwanamke na kwa ujumla Mungu tangu mwanzo mpango wake ni mme mmoja na mke mmoja.Mtu wa kwanza kuoa zaidi ya ni lameki kitu ambacho ni chukizo mbele za Mungu ndio maana hata wakati wa ghalika wote walio kuwa na mke zaidi ya mke mmoja wote walighalikishwa na maji kwa hiyo mtu anapo okoka ni kuachana na wote waliokuwa wampandilia Ndoa ya mwanzilishi”
  MASWALI KUHUSU MAJIBU YAKO YENYE MASHAKA;
  1.Hao wanawake wanaochwa, wako tayari kuolewa na wanaume wengine?
  2.Je, baada ya Gharika hakuna watumishi wengine wa Mungu walioa mke zaidi ya mmoja au wake wengi?
  3,Kwenye AGANO JIPYA, ni wapi MAANDIKO yanasema,mtu mwenye wake wengi anapomwamini BWANA YESU awafukuze wake wengine abaki na yule wa kwanza?
  4.Nini maana ya NDOA?

 18. Wapendwa Bwana Yesu apewe sifa
  mpendwa Pendael Simoni naomba nijibu maswali yako kama ifuatavyo:-
  1.umetaka uhakika pale niliposema mtu mwenye wake wengi kuwaacha wengine na kubaki na Mke wa ujanani sasa twende kwenye maandiko kwanza Ndoa lazima ujue ni ya Mme mmoja na mke mmoja na hao wanapooana hawi wawili tena ila wanakuwa mwili mmoja (mathayo 19:4.5/1wakolinto 7:2/ pia lazima ujue mtu wa kwanza kuoa mke zaidi ya mmoja alikuwa Lameki mtoto wa kaini Mwanzo 4:19,23 na wote walokuwa na wake zaidi ya mmoja wakati wa ghalika waliangamizwa kwa maji huo ni ushahidi tosha kuwa ni chukizo mbele za Mungu walioingia katika safina ni wale wenye mke na mme mmoja tu safina ni mfana wa Mbinguni soma mwanzo 7:13
  2.kuhusu mke aliyefiwa au mme aliyefiwa mimi nasema yuko huru kuolewa au kuoa mwingine kwani Biblia inasema mke au mme hufungwa kwa vile mwenzi wake yuko Hai soma 1wakolinto 7:..39 hivyo akifiwa yuko hulu kuolewa na yeyote katika Bwana soma pia malaki 2:13…16/warumi 7:2…3/luka 16:18
  mwisho niseme watu wengi wataenda motoni kwa uzembe wa kutofanyia kazi neno la Mungu
  kwa leo nishie hapo Balikiwa AMIIN

 19. Mpendwa wetu DAVID MSUYA

  Wachangiaji walio wengi WAMEELEZA VIZURI SANA suala la mume na
  mke mmoja.Ni suala la kimaandiko tena liko wazi sana.Kaka Msuya naomba tutafakari kwa pamoja maandiko yafuatayo; MATHAYO 19:1-8
  na MARKO 10:2-9.Tunahitaji UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU Katika
  mambo yote-1 YOHANA 2:20,27.

  Mungu awabariki nyote.

 20. Suala la ndoa ni suala nyeti ambalo linachangi a sana Maisha ya Kiroho ya mwandamu ndio maana MUNGU amezungumzia suala hili la ndoa katlka nyakati zote za Biblia. HIVYO SOTE TUNATAKIWA KUWA WAANGALIFU KWANI TUNAWEZA KUWAFANYA WATU KUWA WANA WA JEHANAMU kuliko Kuwafanya WANA WA MUNGU. Kwako, STEPHEN NGULLO. Maelezo yako ya Mwanzoni uliyoyatoa kuhusu ndoa kwa kiasi kikubwa yameenda vizuri.Nilipopata UTATA ni kuhusu uliposema yafuatayo; Mtu aliyekuwa na wengi wengi AKISHAOKOKA anatakiwa kubaki na MKE MMOJA na kuawaacha wengine. Hebu thibitisha KIMAANDIKO au Je, hivyo ndivyo BIBLIA inavyosema? Vipi kuhusu Mume/mke aliyefiwa na mwenza, ana haki ya kuwa na ndoa?

 21. Wapendwa ktk Yesu Bwana Yesu asifiwe
  mimi nafulahi leo nami kutoa Elimu kama ifuatavyo kwanza wengi hawaelewi yafutayo ya kitimia Mungu anakuwa anaitambua hiyo Ndoa
  1.Mume na Mke wawe hawajawahi kuoa au kuolewa au mmojawapo au wote wamefiwa na mke au mme aliye halali (1wakolinto 7:8..9,38..39/warumi 7:2..3)
  2.Ruhusa ya Mwanamke kwa kuwa radhi kuolewa na mme huyo (mwanzo 24:57..58)
  3.Mme lazima apate ruhusa ya wazazi wa mwanamke katika vikao vya majadiliano ya mahali ikiwa wazazi wa mwanamke wataluhusu waishi pamoja na mahali ifuate baadaye au vinginevyo la msingi ni ruhusa ya wazazi (mwanzo 34:8,11..12/1wakolinto 7:36)
  4Mme na Mwanamke baada ya ruhusa ya wazazi wa mwanamke wakiwaacha wazazi na kuambatana pamoja na kuishi pamoja na kutambulika hivyo katika jammi basi hao wamekuwa si wawili tena bali mmoja hawezi kutengenishwa wameunganishwa na Mungu (Mathyo 19:5..6)
  Nije kwenye hoja ya msingi mme mwenye wake wengi anapookoka inakuwaje ni kuwaacha na kubaki na yule wa kwanza ambaye alitangulia kukaa naye mwazo na kupata ruhusa ya wazazi wa Mwanamke na kwa ujumla Mungu tangu mwanzo mpango wake ni mme mmoja na mke mmoja. Mtu wa kwanza kuoa zaidi ya ni lameki kitu ambacho ni chukizo mbele za Mungu ndio maana hata wakati wa ghalika wote walio kuwa na mke zaidi ya mke mmoja wote walighalikishwa na maji kwa hiyo mtu anapo okoka ni kuachana na wote waliokuwa wampandilia Ndoa ya mwanzilishi

  nishie hapo mbalikiwe nyote

 22. Mimi nafikiri mwanaume anatakiwa mwenyewe achague mmoja kati ya hao wake zake na kuwaacha wengine huru.

 23. Apewe sifa mwokozi wetu Yesu Kristo,

  Aliye na wake wengi hana budi kuwaacha na kubakia na mmoja wa KWANZA hata kama amekongoroka na kuchoka maana ndie mke wake, hii ni kama mtu huyo anataka kuingia mbinguni kule tulipoandaliwa makao na Bwana wetu Yesu Kristo.

  Ila lazima kuwe na hekima katika kufanya haya, ndio maana siku za hivi leo swala hilo tunamwachia mchungaji tu, na sisi wengine tukizidi kumuombea mchungaji h\roho ya hekima na maarifa kama ya mfalme Suleman.

  Aman na iwe kwenu ndugu katika Bwana.

 24. Kila mume ni haki kuoa mke mmoja, ikitokea mme akaoa mke zaidi ya mmoja ni kwa sababu zake mwenyewe na kwakuongozwa na shetani. Lakini inapofika wakati akagundua kuwa ni makosa kwa kutubu na kuokoka basa mke wa kwanza ndiye atabaki kuwa mkewe na wale/yule wengine inatakiwa kuachana kwa amani. Kama kuna mtoto/watoto waliofikisha umri wa kuchukuliwa na baba atalazimika kuwachukua baba yao au itategemeana na makubaliano ya pande mbili lakini mambo yote hayo yafanyike kwa amani.

  Mungu akubariki sana!

 25. Sasa huu ni mjadala wa kiutu uzima,wenye kumfanya mtu achimbe vema Kitabu (biblia)na kuwassilisha dondoo zenye nguvu. Nimeupenda.
  Ngoja nami nijipange ili nichangie hoja makini.
  Mbarikiwe.

 26. Ndugu David Msuya,shallom.

  Nakuomba usome 1 Wakorintho sura yote ya saba, utaona mistari mingi sana kwenye sura hiyo inazungumzia mke au mume mmoja na wala sio wake zaidi ya mmoja. Kabla ya kuanza kusoma muombe kwanza Roho Mtakatifu akufunulie wazi wazi nini kipo kwenye mistari hiyo, maana Yeye ndiye Mwalimu wetu. Halafu kila mara unaposoma biblia jitahidi kuuliza au kujiuliza maswali, unapofanya hivyo utaona Roho Mtakatifu akikufundisha kutokana na hayo maswali. Kwa mfanao kwenye sura hiyo, mstari wa 3 unasema hivi;

  “Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe”

  Swali ni hili nini wajibu wa mume au mke kwenye ndoa? Je kuna aina moja tu ya wajibu au zipo aina nyingi za kuwajibika ndani ya ndoa? Nini madhara ya mmoja anapoacha kutimiza wajibu wake kwa mwenzake kwenye ndoa yake? n.k.

  Kupitia maswali kama hayo utapata mafunuo mengi sana juu ya wajibu wa wana ndoa kwenye ndoa yao na pia utapata mistari mingi sana ndani ya biblia inayozungumzia juu ya kuoa mke mmoja au mume mmoja.

  Ubarikiwe na Bwana Yesu.

 27. Wapendwa Bwana Yesu apewa sifa.
  Hii mada ni ngumu kidogo na inahitaji msaada wa Roho Mtakatifu.Maana kama wewe uliwaoa hao wanawake halafu kwa bahati nzuri ukawazalisha halafu wewe leo unasema umeokoka kwa huwataki tena nadhani huo sio wokovu.

  Pili naomba mnisaidie kitu kimoja. Hivi kuna mstari kwenye Biblia unaokataza kuoa wake wengi??

  Amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s